Uswuwl Al-Fiqhi

 

Uswuwl Al-Fiqh

 

Imetafsiriwa na: Naaswir Haamid

 

Utangulizi Wa Alhidaaya.com

 

 

BismiLLaah wasw-swalaatu was-salaamu 'alaa RasuuliLLaah wa aalihi wa-aswhaabihi wa ba'ad,

 

Tumeona umuhimu mkubwa wa kukitafsiri kitabu hichi kutoka somo la Uswuul Al-Fiqhi kwani wasomi wengi, Mashaykh na wanafunzi wa Dini wamekuwa hawanufaiki vilivyo na kitabu hichi kwa kukosekana elimu hii kwa lugha ya kiswahili. Hivyo, tunatarajia kwamba kitabu hichi In shaa Allaah kiwe na manufaa makubwa haswa kwa wenye uchu wa kutafuta elimu pamoja na Mashaykh kwani ni somo muhimu linalosakwa sana na watafutaji elimu.

 

Hali kadhalika maelezo yaliyomo ndani ya kitabu hichi ni mepesi kuyasoma na kuyaelewa kwani yapo kwa utangulizi na kitabu hichi hakijaenda ndani sana kuhusiana na somo hilo la Uswuul.

 

Ni materejeo yetu kwamba kutokana na tafsiri hii, itapatikana faraja kwa wasomi pamoja na kupatikana usomaji uliotanuka kwa wanafunzi wa Uswuul.

 

Na bila shaka hiki ndicho kitabu cha kwanza cha somo la Uswuul al-Fiqhi kufasiriwa kwa lugha ya kiswahili. Tunaamini In shaa Allaah Waislam wengi watanufaika kwa kazi hii na yaliyomo ndani yake.

 

Allaah Amlipe ndugu yetu mfasiri wa kitabu hiki kwa Kiswahili, Al-Akh Naaswir Haamid. Tusiwasahau kwa du'aa In shaa Allaah wahusika wa ALHIDAAYA ambao wameisimamia kazi hii.

 

Alhidaaya.com

 

 

Share

01-Uswuul Al-Fiqhi: Kuhusu Kitabu Hichi

   

Uswuul al-Fiqh ni sayansi ambayo, hoja na ufunuo (wahy) unakaa pamoja kwa kushirikisha rai yakinifu na shari'ah iliyopokewa. Lakini bado, al-Uswuul haitegemei sana katika hoja hadi kufikia sehemu ya kukataliwa na shari'ah iliyopokewa, pia haiegemezwi kiurahisi katika kukubali kwa upofu utakaopelekea kutounganishwa na hoja.

 

Kitabu hichi ni hatua ya kurahisisha Uswuul al-Fiqh na utangulizi wake kwa wataalamu katika sayansi ya jamii na wale ambao hawana nafasi ya kusoma kwa ndani maelezo ya sayansi hiyo.

 

 

    

 

 

 

 

Share

02-Uswuul Al-Fiqhi: Yaliyomo

 

Uswuul Al-Fiqhi

 

Yaliyomo

 

Utangulizi

 

Sura ya Kwanza

 

Uswuul al-Fiqh: Taratibu za Uchunguzi na Elimu ndani ya Fiqhi ya Kiislamu.

 

Maana

Kiini cha hoja

Manufaa

Sayansi ambayo Uswuul al-Fiqh imepata msingi wa Elimu

Asili na Maendeleo ya Uswuul al-Fiqh.

Taratibu za kupata hoja Kutoka kwenye Vyanzo.

 

 

Sura ya Pili

 

Maswahaba ambao walitoa Fatwa kipindi cha maisha ya Mtume.

Kipindi cha Maswahaba wakuu.

Wakati wa Abu Bakr as-Swiddiyq

Sifa maalum za Fiqhi wakati huo

Wakati wa ‘Umar Ibn al-Khattwaab

Wakati wa ‘Uthmaan Ibn ‘Affaan

Wakati wa ‘Aliy Ibn Abi Twaalib

Fuqahaa miongoni mwa Swahaaba na Taabi’uun

 

 

Sura ya Tatu

 

Utungaji Sheria Baada ya Kipindi cha Maswahaba

Baada ya Taabi’uun: Kipindi cha Maimamu Mujtahidiyn

Watu wa Rai na Watu wa Hadiyth: Ahl al Hadiyth na Ahl al-Ra-ay

 

 

Sura ya Nne

 

Al-Imam ash-Shaafi’iy

Taratibu za al-Imaam ash-Shaafi’iy kwenye Kitabu chake: Ar-Risaalah

 

 

Sura ya Tano

 

Uswuul al-Fiqh Baada ya al-Imaam ash-Shaafi’iy

Maendeleo ya Uswuul al-Fiqh Baada ya al-Imaam al Shaafi’iy

Majukumu ya Wafuasi wa Abu Haniyfah katika Uandishi wa al-Uswuul

Mtindo wa wafuasi wa al-Imaam ash-Shaafi’iy, au Mutakallimuun, na wale wa Hanafiyah.

Mtindo wa wanazuoni wa Hanafi wa al-Uswuul.

Sayansi ya Uswuul al-Fiqh kipindi cha Karne ya sita Hijriyah na kipindi kinachofuata.

 

 

Sura ya Sita

 

Mada zinazohusiana na Ijtihaad

 

Share

03-Uswuul Al-Fiqhi: Utangulizi

Sayansi ya Usuul al-Fiqh, hakika inaeleweka kuwa ni njia muhimu sana ya uchunguzi ambayo imepata kuvumbuliwa na mawazo ya Waislamu. Hakika, kwa vile ni msingi madhubuti ambao juu yake nidhamu za Kiislamu zimeegemezwa, Uswuul al-Fiqh sio tu imenufaisha ustaarabu wa Kiislamu, lakini umechangia kuwa ni maandiko mazuri kabisa kwa ustaarabu wa dunia kwa jumla. Haitokuwa sehemu ya nje kueleza hapa namna utaratibu wa kufananisha ulivyoendelezwa ndani ya kuta za Fiqhi ya Kiislamu.

 

Tunaiwasilisha kazi hii fupi, kwa wote walio na hamu ya kuongeza elimu fulani kwenye sayansi hii. Na tunamuomba Allaah Ta’ala Atusaidie sisi na kutunufaisha kwa tuliyoelimika na kuelimika kwa yale tuliyonufaika, na kutulinda sisi kutokana na elimu isiyo na manufaa, na kutokana na vitendo ambavyo havikubaliki Kwake. Wa Akhiru Da’wana an al Hamdu Lillah Rabb al ‘Alamiyn (Sifa zote na shukrani zote ni zake Allaah, Bwana na mlinzi wa viumbe vyote).

 

 

 

Share

04-Uswuul Al-Fiqhi: Sura Ya Kwanza- Taratibu Za Uchunguzi Na Elimu Ndani Ya Fikhi Ya Kiislamu.

 

 

Maana:

 

Sayansi ya chanzo cha utaratibu wa Fiqhi ya Kiislamu Uswuul al-Fiqh imetafsiriwa kama ni mkusanyiko ulio pekee na maana maalum, wa uthibiti wa kisheria na ushahidi ambao, utakaposomwa kwa makini, utapelekea aidha kwenye elimu mahsusi ya uamuzi wa Shari’ah ama kwa uchache kwenye dhana yenye kueleweka inayohusisha hayo hayo. Utaratibu ambao kwa thibati hizo umechukuliwa na hali ya mthibitshaji.[1]

 

Kiini cha Hoja:

 

Kama ambavyo ni kiini cha hoja. Sayansi hii, pamoja na thibati zilizomo ndani ya vyanzo vya maandiko ya Shari’ah. Huziangalia kupitia mtazamo wa namna yake kwa maana ya Ijtihaad. Hukumu za kisheria zinatolewa kutokana na kipengele kimoja baada ya kimoja. Ingawa baadaye, kwenye kesi ambapo maandiko inatokea kwa pamoja kukhalifiana. Hiari ya uchaguzi imewekwa bayana[2].

 

Manufaa:

 

Sayansi ya Uswuul al-Fiqh inafanya uwezekano wa kuwa na elimu ya maamuzi ya Shariah kama ni somo, kwa upande wa wale wenye sifa za kufanya Ijtihaad na ambao wamefaulu masharti yake ya thibati za kisheria zilizotolewa na Mtoaji wa Sheria (Allaah).

 

Faida zinazopatikana kutokana na sayansi hii kwa wale wasiofaa kufanya Ijtihaad ni kwamba; kupitia masomo yao ya skuli bora za dhana za kisheria madhaahib za mujtahiduun (wale ambao wanatumia Ijtihaad) na hoja chini ya maamuzi yao. Wanafunzi wa somo la utaratibu wa uchunguzi ndani ya Fiqhi ya Kiislamu hawawezi kuelewa matawi tofauti ya dhana, kuzichambua na kuchagua kutoka miongoni mwa tafsiri na kufanya uchaguzi (wa hoja iliyo bora), na kuthibitisha mijadala ya kisheria kwa mnasaba wa kanuni zilizotolewa na mujtahiduun walio bora.

 



[1] Angalia Fakhrud-Diyn ar-Raazi; Al Mahswuul Fi ‘ilm Uswuul al-Fiqh, iliyohakikiwa na Dkt. Twaah Jaabir al-‘Alwaaniy; Riyaadh; Imamu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Ibn Sa’ud, toleo la mwanzo; 1399/1979; sehemu ya 1, uk. 94.

[2] Angalia maelezo juu ya Uswuul al-Fiqh yaliyoanzishwa na Maprofesa wa kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Al-Azhar, mwaka wa masomo 1382/1963 uk.22

Share

05-Uswuul Al-Fiqhi: Sayansi Ambayo Uswuul Al-Fiqh Imepata Msingi Wa Elimu.

 

Sayansi ya Uswuul al-Fiqh hakika ni somo huru na la kiaina yake. Hata hivyo, limeegemea kwenye misingi mahsusi ya kutoa hoja fulani juu ya hoja fulani. Elimu ambayo wanazuoni wa Sheria za Kiislamu hawawezi kufanya kitu bila yake. Njia hizi za kutoa hoja juu ya hoja nyengine, zimetolewa kutoka katika adabu tofauti:

 

a)    Nyengine zimetolewa kutokana na sayansi ya dhana ya Aristotelia ambapo mwanafalsafa wa maandiko ya dhana mutakallimuun wamefikiria kuwa na desturi ya kujadiliana wanapoanza kazi zao. Majadiliano haya ya kielimu yanajinasibisha, kwa mfano, kwa taratibu ambazo ndani yake maneno yanatoa maana, mgawanyiko wa masomo kwenda wakati wa leo na kutabiri, haja ya, na aina za, maongezi ambayo yanaelemea kwenye kanuni za dhana zilizotolewa kutokana na tafsiri na maana. Usahihi na khitimisho zilizoegemezwa kwenye hoja ya kuongeza maarifa, na majadiliano kuhusiana na ushahidi na namna utakavyotumika kuthibitisha madai ya mmoja ambaye anathibitisha hilo, au kukanusha migongano na mengineo zaidi.

b)    Nyengine zimetolewa kutoka Ilm al-Kalaam Elimu ya akili na hoja, na inahusisha majadiliano ya masuala kama hayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu al-Haakim. Kwa namna ambayo ama ni Shari’ah hiyo hiyo au sababu zinazoamua lipi sahihi au lisilo sahihi, au ya kwamba ama mmoja anaweza kuwa na elimu ya zuri na baya kabla ya uteremsho (wahyi) au ama kutekeleza shukrani kwa Muumbaji Mwenye wingi wa ukarimu. Ni wajibu uliopatikana kwenye Shari’ah au sababu za mwanaadamu.

c)     Nyengine ni jumla ya kanuni za elimu ya lugha ambazo wanazuoni wa al-Usuul wameendeleza kupitia elimu na uchunguzi wa lugha na kuwasilisha kwa namna ya mfumo wa kudhihirisha. Kama vile uchunguzi unaohusisha lugha na asili zake, mgawanyo wa maneno kwenda kwenye kimafumbo na herufi halisi, majadiliano ya elimu ya asili, maneno mawili tofauti yenye maana sawa (utata), mkazo, ushauri wa juu juu, kuonesha uhalisia, maana ya vipande vya sarufi na mengineo zaidi.

d)    Njia nyengine zimetolewa kutoka sayansi bora ya Qur-aan na Sunnah. Kama vile mijadala kuhusiana na kupokewa Hadiyth kwa msimuliaji mmoja Ahaad, au kwa wasimuliaji wengi wasioweza kusimulia uongo Tawaatur, njia zisizokuwa rasmi za kuitafsiri Qur-aan na kanuni zake, utaratibu wa kuikubali Ta’diyl ama kuikataa Jarh ya wasimuliaji, kutangua sheria al-Naasikh wa al-Mansuukh[1], shuruti za maandiko ya Hadiyth na mfuatano wa wasimulizi, na mengineyo zaidi.

e)    Mwisho, mifano iliyotumika na wanazuoni wa al Uswuul kwenye ufafanuzi wa hoja zao. Ambazo zimetolewa kutoka kwenye Fiqhi maalum, na kutoka kwenye ushahidi wa kina kwa sababu hiyo hiyo kama ilivyochukuliwa kutoka kwenye Qur-aan na Sunnah.

 

Mambo ambayo wanachuoni wa al Usuul wanajishughulisha zaidi nayo, yanahusisha yafuatayo:

§         Elimu ya kuwaza kwa makini na kutoa habari fulani juu ya kitu fulani.

§         Elimu ya lugha.

§         Amri na Makatazo.

§         Maarifa ya kufahamu al-‘Aam na misamiati mahsusi al-Khaasw.

§         Mambo yasiyothibitika al-Mujmal na dhana zinazotambulika al-Mubayyan.

§         Kutangua an-Naskh.

§         Tabia (kwa uwazi, zile za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na maana zake).

§         Makubaliano.

§         Simulizi kuhusiana na Sunnah.

§         Kufatanisha hoja al-Qiyaas.

§         Kuelekeza hoja iliyo bora inapotokezea kesi zenye migongano zilio dhahiri.

§         Kutumia uwerevu wa akili na elimu Ijtihaad.

§         Kufuata madhehebu maalum ya kisheria Taqliyd.

§         Vyanzo vyenye mgogoro (ambavyo ni nje ya vile vyanzo vinne “vilivyokubaliwa”).

 

 

 

 



[1] An-Naasikh wa al-Mansuukh: Ni somo la aya ambazo Qur-aan kwa maudhui yake zimetangua maana ya kisheria kwa aya nyengine, kwa hivyo inaitwa al-Mansuukh.Tawi hili la al-Uswuul pia linahusisha na somo la maudhui ya Hadiyth, aidha maudhui hayo yanaweza kutangua maana za kisheria ndani ya Qur-aan au kwenye Hadiyth nyengine.

Share

06-Uswuul Al-Fiqhi: Asili Na Maendeleo Ya Uswuul Al-Fiqh

 

Sio rahisi kulisoma somo la Uswuul al-Fiqh na maendeleo yake bila ya kupitia kumbukumbu za Fiqhi. Mafundisho ya vitendo kwa Shariah ambazo yamekusanywa kusanywa kutokana na vyanzo mahsusi vya sheria.

 

Kubuni maana ya Uswuul  ni: shina, au asili Aswl, wingi Uswuul au kile chengine ambacho kinajengwa juu yake. Kwa mfumo wa kisheria za Kiislamu (ndipo) Fiqhi inapojengwa hapo, na mizizi kutoka kwenye mashina ya Uswuul  ambayo yanakuwa na chanzo chake cha ushahidi. Matokeo yake, ili kufahamu asili ya Uswuul al-Fiqh, tunahitaji kuwa na uoni wa jumla juu ya historia ya Sheria za Kiislamu. Tashri’iy

 

Kuanzisha vifungu vya Shariah, kuamuru sheria kufuatwa, kuweka kanuni na amri, na kufafanua miundo ni kazi ambayo ni maalumu kwa Allaah pekee. Yeyote anayejipa na kuandikia kazi hizi zaidi ya Allaah, ametenda dhambi ya Shirk. Kwani, kufanya hivyo amekwenda kinyume kabisa na imani ya Upweke wa Allaah. Tawhiyd.

 

Allaah Ameweka na kugawa thibati na vyanzo vilizo wazi za ushahidi kwa ajili ya kwamba; waumini wasiwe na matatizo kutafuta muongozo wao kwenda kwenye vipengele vya Sheria Zake. Au Ahkaam kwa kutumia baadhi ya vyanzo hivi vya ushahidi. Ummah wa Kiislamu umekubaliana juu ya usahihi na uhusiano wake kwa Ahkaam, na wameukubali hivyo hivyo. Hata hivyo, kuna tofauti nyingi kwa mnasaba wa vyanzo vyengine vya ushahidi.

 

Vyanzo vya ushahidi ambavyo Ummah wote wamekubali, na juu ya usahihi wa ambao kuna makubaliano ya jumla, inajumuisha vyanzo viwili, ambavyo vinafanya msingi wa sheria kipindi cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Vyanzo hivi viwili vya sheria ni:

 

1)    Qur-aan: Hii inaweza kutafsiriwa kama ni maneno yaliyoteremshwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kuisoma pekee ni miongoni mwa tendo la ibada, Surah fupi ambayo ni changamoto kwa binaadamu kutoa chochote chenye kufanana nayo. Kila herufi ambayo imefikishwa kwetu ni kupitia kwa waandishi madhubuti wasio na pingamizi Tawaatur ambayo imeandikwa baina ya magamba mawili ya Kitabu Kitakatifu Msahafu kuanzia na Surat al-Faatihah “Sura ya ufunguzi” na kumalizia kwa Surat an-Naas.

2)    Sunnah: Inajumuisha kila kitu, nje ya Qur-aan. Ambayo imefikishwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), alilolisema, kutenda au kukubaliana nalo.

 

Hivyo, kila tamko la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), zaidi ya Qur-aan, na kila kitendo chake. Kuanzia mwanzo wa kazi yake mpaka mwisho wa siku zake, zinahusisha Sunnah yake. Kwa maneno ya jumla kila neno aidha linaanzisha uamuzi ambao unatumika kwa wafuasi wa Ummah wote, au uamuzi ambao unamhusisha Mtume mwenyewe peke yake au kwa Swahaaba zake wengine.

 

Bila ya kuangalia kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni tabia nzuri au vyenginevyo, kila neno lake, tabia na idhini. Inaweza kuchukuliwa kama ni chanzo cha ushahidi kwenye uamuzi wa kisheria. Hivi ndivyo ilivyo, bila ya kuangalia kwamba lafudhi zake au vitendo vina mnasaba wa dini au mwenendo. Au ama zimejihusisha na kutoa amri au kutoa maoni, kuzuia, kukataa, au kukubali. Na bila ya kuangalia ikiwa ama lafudhi zake au kitendo, kiliegemezwa kwenye uamuzi uliotolewa kabla kwenye Qur-aan, au ama inasimama kufanya kazi pekee (bila ya tegemezi) kuanzisha sheria.

 

Kipindi cha maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), maamuzi yote ya kisheria Ahkaam za Shariah, ukiunganisha na migawanyo yote, kama vile maamuzi makuu au yaliyopokelewa, elimu juu ya misingi ya imani, na mwenendo wa kanuni kuhusiana na matendo maalum na usahihi wake, yalitolewa kutokana na vyanzo viwili vya Qur-aan na Sunnah.

 

3)    Ijtihaad: Ilikuwa ikifanyiwa kazi na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wale Maswahaba zake ikiwa na mwelekeo wa kisheria ujulikanao kama Ahl an-Nadhwar. Ijtihaad ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilithibitishwa na Qur-aan na mara nyengine haithibitishwi. Ambapo kwa kesi hiyo, ilielezwa kwamba suluhisho lililo bora ni lile ambalo hakulifanyia kazi.

 

Ijtihaad iliyofanywa na Maswahaba, daima ilikuwa ni kujibu mazingira ambayo yametokea kwao. Baadaye, walipokutana na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), wataeleza kilichotokezea na kumwambia walichotolea uamuzi. Mara nyengine, yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anazikubali Ijtihaad zao, na uamuzi kama huo wa kwao (uliopata ruhusa ya Mtume) ulifanya sehemu ya Sunnah. Kama yeye Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) atazikataa Ijtihaad zao. Maelezo yake kuhusiana na mwenendo sahihi utakuwa ni Sunnah.

 

Hivyo, tunaweza kusema kwamba; kwa hatua hiyo sheria ilitegemea kwenye mifumo miwili ya Uteremsho Mtukufu. Wahyi:

 

  1. Uteremsho uliosomwa, Wahy Matlu, au Qur-aan yenye ukamilifu isiyoigika I’jaaz.

  2. Uteremsho usiosomwa. Wahy Ghayr Matlu, au Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Hakika, Ijtihaad iliyofanywa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) itakuwa ni yenye kufuatwa (precedent) kwa Swahaaba zake na baadaye Waislamu. Ambazo kwa uwazi inathibitisha uhalali wa Ijtihaad, ili kwamba pale watakaposhindwa kupata uamuzi ulioamuliwa kwa kisheria ndani ya Qur-aan au Sunnah, walihitajika kufanya kazi ya Ijtihaad ili kufikia kwenye hukumu peke yao.

 

Juu ya hivyo, labda ili kuipa nguvu na kuianzisha dhana hii, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwaamrisha baadhi ya Maswahaba zake kufanya Ijtihaad kuhusiana na mambo fulani akiwepo yeye mwenyewe. Kisha atawaambia nani alikuwa sahihi na nani alikosea.

 

 

Share

07-Uswuul Al-Fiqhi: Taratibu Za Kupata Hoja Kutoka Kwenye Vyanzo

 

Ama kwa Quraan…

 

Qur-aan ilisomwa na kueleweka kwa Swahaaba bila ya wao kuhitaji msaada wa kuhitaji kukimbilia katika kanuni rasmi za sarufi. Vile vile, wamejaaliwa kuwa na muoni ulio msafi, akili za uwerevu na zilizo makini. Walikuwa na uwepesi wa kufahamu malengo ya Mtoa Sheria (Allaah) na hekima zilizomo ndani ya Sheria Zake.

 

Hakika ni mara chache Maswahaba walikuwa wakimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na jambo lolote isipokuwa yeye mwenyewe alitaje kwanza.

 

Imesimuliwa kwamba Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) alisema “Sijapata kuona watu bora kuliko Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kupitia kipindi cha kazi yake, mpaka alipofariki. Wamemuuliza kuhusiana na mambo kumi na tatu, yote ambayo yametajwa ndani ya Qur-aan. Kwa mfano [maana ya]:

“Wanakuuliza (hukumu ya) kupigana vita katika miezi mitakatifu…” [2:217)

na “Wanakuuliza juu ya hedhi….” (2:222)”

 

Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) alisema, “Walikuwa wakimuuliza yeye kwa mambo ambayo yalikuwa na azma ya uhakika kwao[1].”

 

Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwa hili alisema: “Usiulize kwa jambo ambalo halikutokezea, kwani mimi nimemsikia baba yangu ‘Umar Ibn al-Khattwaab akisema: Mlaani yule aliyeuliza jambo ambalo halikutokezea.[2]

 

Qaasim (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema (kukiambia kizazi cha tatu cha Waislamu): “Munauliza kuhusu vitu tusivyowahi kuuliza, na kugombana kuhusu vitu ambavyo hatujawahi kugombana navyo. Hata munauliza kuhusu vitu ambavyo mimi sina maarifa navyo. Lakini kama tutajua, haitoruhusiwa kwetu kubakia kimya kuhusiana navyo[3].”

 

Ibn Is-haaq (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema: “Nimekutana na zaidi ya Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuliko mtu mwengine yeyote, na sijapata kuwaona watu walioishi maisha ya kawaida au ambao ni wachache wa kudai juu yao wenyewe[4].”

 

‘Ubaadah bin Nusay al-Kindi (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema: “Nimejuana na watu ambao ugumu wao haukuwa imara kama wa kwenu, na masuala yao yalikuwa kimya tofauti na yale munayouliza nyinyi[5].”

 

Abu ‘Ubaydah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema ndani ya kitabu chake cha Majaaz al Qur-aan: “Haikuwahi kusimuliwa kwamba Swahaabah yeyote alikwenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa elimu yoyote ambayo inawezekana kupatikana ndani ya Qur-aan[6].”

 

 

Ama kuhusu Sunnah…

 

Sehemu ya Sunnah ambazo zina lafudhi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zilikuwa ndani ya lugha za Maswahaba, hivyo walitambua maana zake na kuelewa maneno yaliyomo ndani ya aya (phrase) na yale maneno mengineo ambayo hudhihirisha maana yake (context).

 

Namna ulivyo mwenendo wa Mtume, waliweza kushuhudia (huo mwenendo), baadaye kuwaambia wengine vile vile kama walivyoona. Kwa mfano, mamia ya watu walimuona Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akifanya wudhuu na wao kufuata mwenendo wake bila ya kumuuliza kutaka maelezo. Kama baadhi ya vitendo kwenye wudhuu yalikuwa ni lazima na vyengine kupendekezwa, ambavyo kwa uwazi vimeruhusiwa na vyengine havikutajwa. Vivyo hivyo, walishuhudia (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akifanya Hijjah na Swalah, na vitendo vyengine vya ibada.

 

Watu walisikika wakimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutoa Fataawa kuhusiana na masuala tofauti, na alifanya hivyo. Kesi zilipelekwa kwake, na yeye alitamka hukumu. Matatizo yatatokea miongoni mwa Maswahaba, na yeye alitoa jibu la hakika. Aidha matatizo hayo yalihusiana na mahusiano ya pamoja, tabia binafsi, au masuala tofauti ya kisiasa. Walishuhudia mazingira yote haya na walifahamu maana (ya mazingira yaliyotokea). Ili kwamba hekima na malengo ya hukumu za Mtume zisifichwe mbali nao.

 

Watu walimuona namna Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa akiona tabia za Maswahaba wake na wengineo. Hivyo, kama yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimsifu yeyote, walitambua ya kwamba tendo la huyo mtu lilikuwa ni zuri, na kama atamlaumu yeyote, walitambua kwamba kuna kosa fulani kwa namna huyo mtu alivyofanya.

 

Juu ya hivyo, simulizi zote kuhusiana na Fataawa za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), maamuzi na kukubali au kutokubali baadhi ya masuala inaonesha kwamba yalitokea mbele ya watu wengi. Ni kama mfano wa anavyotambua daktari na wenziwe, kutokana na mjumuiko wa muda mrefu na kutambua wenyewe mazoea[7] sababu za yeye kuelekeza dawa fulani. Hivyo, hata Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walitambua hakika sababu na hekima zilizomo ndani ya maamuzi yake.

 

 

Ama kwa Ijtihaad…

 

Maelekezo ya kwamba Ijtihaad inaruhusika na inafaa kwa matumizi ya misamiati ya leo ni mengi. Kwa mfano, Mu’adh bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu) anaeleza kwamba wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipompeleka Yemen, aliuliza:

 

“Utafanya nini kama suala limeletwa mbele yako kwa hukumu?” Mu’adh akasema: “Nitahukumu kwa mujibu wa Kitabu cha Allaah” Mtume akauliza: “Kama hukupata suluhisho ndani ya Kitabu cha Allaah?” Mu’adh akasema: “Basi nitahukumu kwa Sunnah ya Mtume.” Mtume akauliza: “Na kama hukupata kitu ndani ya Sunnah ya Mtume?” Mu’adh akasema: “Basi nitafanya Ijtihaad kutengeneza hukumu yangu mwenyewe.” Mtume alikipiga piga kifua cha Mu’adh na akasema: “Sifa zote ni za Allaah Ambaye Amemuongoza mjumbe wake kwa lile ambalo linamfurahisha Yeye na Mtume Wake[8].”

 

Ijtihaad hii na kutumia hukumu yake mtu mwenyewe kama ilivyotajwa na Mu’adh, pia inaelezwa katika ushauri wa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliompa Abu Muusa (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipomteua kama ni Jaji: “Hukumu itolewe kwa mujibu wa maelezo ya shurti za Qur-aan au mwenendo uliowekwa na Sunnah…” Kisha akaongeza:

 

“Hakikisha unaelewa vizuri kila kesi ambayo imeletwa kwako ambayo hamna maandiko yanayohusiana nayo kutoka kwenye Qur-aan au Sunnah. Kwako, baadaye, ni jukumu la kuoanisha na kufananisha, ili kutofautisha mifano kwa lengo la kufikia hukumu ambayo ipo karibu na uadilifu na bora mbele ya Allaah[9].”

 

Hapo hapo, al-Imaam ash-Shafi’iy ameeleza “rai” kama ni maana ya Ijtihaad na Ijtihaad kama ni al-Qiyaas. Amesema “Hayo ni majina mawili kwa kitu kimoja[10].”

 

Abu Bakr asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ‘anhu), Khaliyfat Rasuul Allaah, amesema: “Namna Mtume alivyo, rai zake daima zilikuwa ni sahihi kwa sababu Allaah daima Akimuongoza. Ama katika kesi yetu, tunadhania na tunakisia.[11]

 

Hivyo, tunaweza kusema kwamba dhana ya Ijtihaad au “rai”, kwenye kipindi hicho, haikwenda mbali zaidi ya moja zifuatazo:

 

a)    Kutumia maana moja au nyingine zinazowezekana katika kesi ambapo hukumu inaweza kujikubali yenyewe katika tafsiri zaidi ya moja. Mfano, pale Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipowaamrisha Waislamu kuswali sehemu ya Banu Quraydhwah[12].

b)   Mlinganyo, Qiyaas, ambayo inahusu suala kwa kulifananisha na jengine, pia suala hilo linazungumzwa ndani ya Qur-aan au Sunnah. Kwa mfano Qiyaas ya ‘Ammaar aliyepambanisha kesi ya Tayammum akiwa katika hali ya Janaabah kwa Ghusl, na hivyo kupangusa (kujisiriba) mwili wake wote kwa vumbi[13].

c)     Ijtihaad ya kutia maanani kitu ambacho kinawezekana kuwa na manufaa au kuzuia kitu ambacho kinaweza kupelekea kwenye ubaya, au kuchukua uamuzi fulani kutoka kwenye matamko ya jumla, au kutumia tafsiri maalum, na mengineyo zaidi.

 

Bidii ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwahamasisha Maswahaba kufanya Ijtihaad na kuwafundisha katika matumizi yake inaweza kuonekana kwenye maneno ya Hadiyth hii:

“Hakimu anapofanya Ijtihaad na kufikia kwenye hukumu sahihi, anapata ujira mara mbili, na kama hitimisho lake si sahihi, pia anapata ujira mmoja.[14]

 

Ijtihaad ya Maswahaba wengi ilikuwa ni makini na kwamba kwenye kesi nyingi, uteremsho wa Qur-aan ulihakikisha huo umakini. Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliikubali. Bila ya shaka, ukaribu wao na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ulitosheleza wepesi wa kutambua malengo ya Mwingi wa Busara na Mtunga sheria, madhumuni makuu yaliyo ndani ya Sheria za Qur-aan, na maana ya maandiko. Nafasi ambayo waliokuja baada yao hawakufaidi moja kwa moja.



[1] Angalia ‘Abdullaah Ibn ‘Abdur-Rahmaan ad-Daarimiy, Sunan, I, uk. 51.

[2] Ad-Daarimiy, Sunan, I, uk. 50.

[3] Ad-Daarimiy, Sunan, I, uk. 49.

[4] Ad-Daarimiy, Sunan, I, uk. 51

[5] Ad-Daarimiy, Sunan, I, uk. 51

[6] Imenukuliwa na Shaykh ‘Aliy Abdur-Razzaq ndani ya Tamhiyd li Taariykh al-Falsafah, Cairo, uk. 152.

[7] Ad-Dahlawiy: HujajatuLlaah al-Baalighah, (Misri), I, uk. 289.

[8] Kwa maelezo kuhusiana na usahihi wa kunukuu Hadiyth kama ushahidi, angalia waandishi, Al-Ijtihaad wa at-Taqliyd, (Cairo, Dar al Ansar), uk. 23-24, na sura kuhusiana na Ijtihaad kitabu cha Al-Mahswuul.

[9] Angalia Ibn Qayyim, I’laam al-Muwaqqi’iyn

[10] Angalia al Imam ash-Shaafi’iy, Ar-Risaalah, (Cairo), uk. 476

[11] Ibn Qayyim, I’laam al-Muwaqqi’iyn, I, uk. 54, Ibn ‘Abd al-Basr, Jami’ Bayaan al ‘ilm, II, uk. 134.

[12] Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaamrisha kundi la Waislamu pamoja na maelekezo: “Simamisheni Swalah ya Laasiri sehemu ya Banu Quraydhwah.” Wakitoa tafsiri yao kuhusiana na hili, kundi moja la Waislamu ndani ya kundi wakaendelea na safari yao mpaka jua lilipozama (machweo), bila ya kusimama kwa ajili ya Swalah ya Laasiri kwa wakati wake. Hata hivyo, kundi la pili waligandia kufuata nafsi zao kuliko maagizo ya Mtume, walisimama mbali kidogo kabla ya sehemu ya Banu Quraydhwah ili kuweza kutekeleza Swalah katika wakati wake. Alipofahamishwa walivyofanya kuhusu kila kundi, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kwamba wote walikuwa sahihi.

[13] Hadiyth ni maarufu na ni sahihi, na iliingizwa ndani ya vitabu vya Imaam al-Bukhaariy, Abu Dawud, al-Nasaaiy, Ibn Maajah, na Ahmad katika mkusanyiko wa Hadiyth.

[14] Hadiyth hii ni ya maana na ilipokewa na al-Bukhaariy, Muslim, na wengineo katika mkusanyiko wao wa Hadiyth sahihi.

Share

08-Uswuul Al-Fiqhi: Maswahaba Ambao Walitoa Fatwa Kipindi Cha Maisha Ya Mtume

 

Maswahaba ambao walitoa Fatwa kipindi cha maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni: Abu Bakr, ‘Uthmaan, ‘Aliyy, ‘Abdur- Rahmaan bin ‘Awf, ‘Abdullaah bin Mas’uud, ‘Ubayd bin Ka’ab, Mu’aadh bin Jabal, ‘Ammaar bin Yaasir, Hudhayfah bin al-Yamaaniy, Zayd bin Thaabit, Abu ad-Dardaa, Abu Muusa al-‘Ash’ariy na Salmaan al-Faarisiy, Allaah Awe Radhi nao wote.

 

Maswahaba wengine walitoa Fatwa nyingi kuliko wengine. Wale ambao walitoa Fatwa nyingi ni: ‘Aaishah Ummul Mu’miniyn, ‘Umar bin al-Khattwaab, na mwanawe ‘Abdullaah, ‘Aliyy bin Abi Twaalib, ‘Abdullaah bin ‘Abbaas na Zayd bin Thaabit. Fatwa ambazo zilitolewa na yeyote kati ya hawa sita zinaweza kujaza kitabu kikubwa. Kwa mfano, Abu Bakr Muhammad bin Muussa bin Ya’quub bin al-Khalyfah Ma’muun alikusanya Fatwa za Ibn ‘Abbaas kwa vitabu ishirini.

 

Wale ambao wana idadi ya chini za Fatwa wamepokewa kuwa ni: Ummu Salamah Ummul Mu’uminiyn, Anas ibn Maalik, Abu Sa’iyd al-Khudriyy, Abu Hurayrah, ‘Uthman bin ‘Affaan, ‘Abdullaah bin Amr bin al-‘Aasw, ‘Abdullaah bin Zubayr, Abu Muusa al-Ash’ariy, Sa’iyd bin Abi Waqqaas, Salmaan al- Faarisiy, Jaabir bin ‘Abdullaah, Mu’aadh bin Jabal na Abu Bakr asw-Swiddiyq. Fatwa za mmoja kati ya hawa kumi na tatu zinajaza sehemu ndogo tu ya kitabu.

 

Orodha hii inaweza kuongezwa kwa Twalhah, az-Zubayr, ‘Abdur-Rahmaan bin Awf, ‘Imraan bin Huswayn, Abu Bakr, ‘Ubaydah bin asw-Swaamit na Mu’awiyah bin Abi Sufyaan. Waliobaki wametoa idadi chache za Fatwa, na mmoja au wawili tu kwenye matukio mengine zimesimuliwa kutoka kwa yeyote kati yao. Fatwa zao zinaweza kukusanywa kwenye kitabu kidogo, lakini baada tu ya kufanya uchunguzi na kuunganisha vipande vipande kwa hali ya juu[1].

 

Katika kutayarisha Fatwa zao, Maswahaba walikuwa wakipambanisha tukio moja moja lililowahi kuwatokea na suala linalofanana ambalo hukumu imetolewa katika maandiko ya Qur-aan na Sunnah. Hivyo, kulirudisha kuangalia maana na uhalisia wa kisheria kwa kujaribu na maandiko kwenye maana halisi ya neno, makusudio yake, na maelezo mengine yoyote yenye kunasibiana.

Baada ya kufikia maamuzi, watawaeleza wengine namna walivochambua mijadala yaliyowapelekea kwenye maamuzi, aidha kama ikiwa zimefikiwa kutoka kwenye herufi za maandiko au kutoka kwenye chanzo chake na watu watawafuata wao. Hakika, wanachuoni hawa wa Kiislamu wa mwanzo hawakusita kuchunguza suala mpaka kufikia katika uamuzi utakaojitesheleza nao, na mpaka wawe hakika wametosheka kwamba wamefanya jitihada zao za juu na hawawezi tena kuendelea.

 



 

[1] Angalia Ibn Hazm, Al-Ihkaam, Mj. uk. 92-93.

 

 

 

 

Share

09-Uswuul Al-Fiqhi: Kipindi Cha Maswahaba Wakuu

 

Baada ya kipindi cha Mbora wa Mitume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ukaingia wakati wa Maswahaba wakuu na viongozi walioongoka vyema Khulafau’ ar-Raashiduun. Kipindi hichi kilidumu kutoka mwaka 11 hadi 40 A.H. Wasomaji Qurra’ ni neno lililokuwa linatumika wakati huu kumaanisha wale Swaababah wenye utambuzi mzuri wa Fiqhi na waliokuwa wakitoa Fatawa.

 

 

 

Share

10-Uswuul Al-Fiqhi: Wakati Wa Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ‘anhu)

 

 

 

Maymuun bin Mahraan alifupisha utaratibu wa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliokuwa akiutumia kwenye kufikia maamuzi kama ifuatavyo:

 

Mgogoro unapofikishwa kwake, Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliangalia ndani ya Qur-aan, kama atapata chochote kwa mujibu wa hilo na ataweza kutoa hukumu, alifanya hivyo. Kama hatopata kuona suluhisho ndani ya Qur-aan, lakini akakumbuka kipengele fulani cha mwenendo wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), atatoa hukumu kwa mujibu wa hiyo (Sunnah). Kama hatopata kuona kitu chochote ndani ya Sunnah, atakwenda na kuwaambia Waislamu: “Mgogoro fulani na fulani umefikishwa kwangu. Yupo yeyote kati yenu anayetambua chochote katika mwenendo wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kwa huo (mwenendo) hukumu inaweza kutolewa?Kama yeyote ataweza kujibu suala lake na kutoa maelezo yenye kufanana, Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) husema: “Shukrani ni za Allaah Ambaye Amemuwezesha miongoni mwetu kukumbuka walichojifunza kutoka kwa Mtume wetu.” Kama hatopata kuona suluhisho lolote ndani ya Sunnah, basi atawakusanya viongozi na watu walio bora kabisa na kushauriana nao. Kama watakubalina kwenye suala, basi atatoa hukumu kwa msingi huo[1].

 

Kama taratibu zote hapo juu zitashindwa kufikia mwisho wowote, basi atafanya Ijtihaad na kutengeneza mawazo yake mwenyewe, aidha kwa kutolea maana ya andiko katika namna ambayo maana halisi itakuwa wazi, au kwa kufanyia kazi uwerevu wa akili yake ya kisheria.

 

Mfano wa Ijtihaad ya aina ya mwanzo ni pale alipoulizwa kuhusu Kalaalah Akijibu, Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema: “Mawazo yangu, kama ni sahihi, basi ni kutoka kwa Allaah, na kama si sahihi, basi ni kutoka kwangu na Shaytwaan. Kalaalah ni yule asiye na mrithi kuendea juu wala mrithi kuendea chini”[2].

Mfano mwengine kama huo ni pale ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipotamka kwake Hadiyth ifuatayo ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Nimeamrishwa kupigana vita dhidi ya watu hadi waseme kwamba Hapana mungu isipokuwa Allaah…[3] na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema, “Zakaah ni sehemu ya hiyo.[4]

 

Pale Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipotaka kupigana vita dhidi ya wale wanaozuia kutoa Zakaah, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alinukuu Hadiyth hii kuonesha kwamba kupigana nao hakuruhusiwi kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema “…hadi waseme kwamba Hapana mungu isipokuwa Allaah. Kisha, kama watasema hivi, damu zao na mali yao haitosumbuliwa na mimi, isipokuwa kwa haki thaabit (yaani mpaka wafanye vitendo ambavyo vinaadhibiwa kwa mujibu wa Shariah ya Kiislamu.)

 

Kwa mujibu wa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu), vitendo hivi vilikuwa ni: uzinifu, mauaji, na kuritadi, kwa vile kuzuia kutoa Zakaah haikutamkwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Lakini Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimwambia: “Zakaah ni sehemu ya hiyo, kwa ajili ya Allaah, nitapigana na yeyote aliyetekeleza Swalaah lakini hakulipa Zakaah! Kama yeyote atajaribu kuzuia kutokana na mimi, hata kiwango kidogo walichokuwa wakilipa kwa Mtume, nitakwenda nao vitani juu yake (Zakaah).

 

Mfano wa pili wa Ijtihaad ni pale alipoamua kwamba mama yake mama anaweza kurithi, lakini baba yake mama hawezi kurithi.

 

Baadhi ya Answaar walimwambia: “Unamruhusu mwanamke kurithi kutoka kwa aliyefariki, wakati yeye (mwanamme) hatorithi kutoka kwake (mwanamke) kama huyo (mwanamke) atakuwa na aliyefariki. Na unaacha bila ya chochote kwa mwanamke kutoka kwa yule (mwanamme) ambaye anaweza kurithi pale hali inapogeuka.” Baadaye Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliamua kwamba wote kuukeni na mabibi wa kuumeni watagawana moja ya sita ya urithi.

 

Mfano mwengine ni hukumu yake kwamba kila mmoja apokee mgao ulio sawa kutoka nyumba ya hazina baytul maal. ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimuuliza: “Utamuweka nafasi gani yule aliyeingia kwenye Uislamu akiwa na mashaka ya kuwa sawa na yule ambaye ameacha nyuma; nyumba yake na mali yake, na kuhama ili kuwa pamoja na Mtume?

 

Hata hivyo, Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu), alitilia mkazo kwamba: “Wote wameingia kwenye Uislamu kwa ajili ya Allaah, na malipo yao yapo Kwake Yeye; dunia hii si chochote.” Hata hivyo, pale ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokuwa Khaliyfah, alitofautisha baina ya watu na kulipa “ujira” kwa mujibu wa kila mmoja alivoanza kuingia kwenye Uislamu, kama wamehama, na kiwango gani wameumia kwa ajili ya Uislamu.

 

Mfano mwengine wa namna Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alivoifanya kazi ya Ijtihaad ni pale alipotofautisha uteuzi wa Khaliyfah kwa (kumuweka) mrithi wake, (tofauti) na ule uteuzi kwa njia ya Bay’ah. Hivyo, alimteua ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa ni Khaliyfah baada yake, na Maswahaba walikubaliana nae.

Khaalid bin al-Waliyd (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimuandikia Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu), kumwambia kwamba katika baadhi ya sehemu za Mkono wa Nchi za Kiarabu amekuta watu wakifanya vitendo vya liwaatw. Abu Bakr aliamua kushauriana na Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili kuchukua hatua ipi kuhusiana na hilo. Mmoja miongoni mwa Swahaabah alikuwa ni ‘Aliyy (Radhiya Allaahu ‘anhu), na hukumu yake ilikuwa ni kali kuliko zote.

 

Alisema: “Ovu lake lilitambulika kwa taifa moja tu, na unajua nini Allaah Aliwafanyia. Ninashauri kwamba watu hawa wachomwe hadi kufa.

 

Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimjibu Khaalid kumwambia kwamba wachomwe hadi kifo; na hili lilifanyika.[5]

 

 

[1] Ad-Dahlaawiy, HujajatuLlaah Al-Baalighah, (Misri), I, uk. 315.

[2] Kuna khitilafu kuhusu maana ya neno Kalaalah. Kwa mujibu wa baadhi, lina maana ya wale waliokufa bila ya kuacha nasaba ya mrithi, wala kizazi, wala baba au babu. Wengine, hata hivyo wanaona lina maana ya wale wanaokufa bila ya kizazi, bila ya kujali kama amefuatiwa na baba au babu. Aya inayoelezea ndani ya Qur-aan inapatikana Surat an-Nisaai, 4:176. Na ilikuwa ni kutokana na msingi huu wa aya kwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliamrisha kama alivyofanya. Sababu ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) ilikuwa kwamba aya hiyo inaelekeza kwamba ndugu wa kike wa Kalaalah apatiwe nusu ya urithi, na kama huyo baba angelikuwa hai, huyo ndugu wa kike asingerithi chochote kutoka kwa Kalaalah. Hivyo, ijapokuwa Qur-aan haielezi suala hilo, ni uadilifu ulio wazi kwamba maana iliyokusudiwa ni kwamba huyo Kalaalah ni yule anayekufa bila ya kuacha nasaba ya mrithi pande yoyote.

[3] Hadiyth hii ni sahihi na imepokewa kutoka kwa Maimamu al-Bukhaariy, Muslim, at-Tirmidhiy, Ibnu Maajah, Ahmad, At-Twayaalisii, na wengineo.

[4] Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa na maana ya kusema kwamba maana hiyo aliyoitoa kwa maneno ya Hadiyth hayakuwa na maana halisi. Isipokuwa, Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alihisi kwamba mfumo wa shahaadah: “Hapana mungu isipokuwa Allaah.” Hakika ifahamike kwa mzunguko, kama lenye maana ya imani, ambapo imani inajumuisha vifungu vingi, kikiwemo Zakaah, na kuongezea kwa ahadi ya shahaadah.

[5] Ibn Qayyim, I’laam al-Muwaqqi’iyn.

Share

11-Uswuul Al-Fiqhi: Sifa Mahsusi Za Fiqhi Wakati Huo

 

 

a.      Matumizi ya al-Qiyaas yalienea kwenye kesi ambapo hamna andiko linalofanana ndani ya Qur-aan au Sunnah na hakuna Swahaabah aliyekataa hili.

b.      Al-Ijma’ pia ilikuwa ikitumika kwa mapana kama ni msingi wa hukumu. Hii ilishajiishwa na ukweli kwamba Maswahaba walikuwa ni wachache, na ilikuwa kwao ni rahisi kukubaliana baina yao. Walitumia al-Ijma’ kwenye kesi nyingi. Kwa mfano; makubaliano yao kwamba Khaliyfah au Imaam ateuliwe, kwamba wanaoritadi wapigwe vita na wauawe, kwamba anayeritadi hawezi kuchukuliwa kama ni mahabusu wa vita, na kwamba hiyo Qur-aan ikusanywe na kuandikwa kuwa ni Kitabu kimoja.

 

 

Share

12-Uswuul Al-Fiqhi: Wakati Wa ‘Umar Ibn Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu)

 

Maoni ya ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kwa jaji Shurayh, kama ilivyotajwa hapo juu, inaeleza utaratibu wake wa kufikia maamuzi kutokana na ushahidi utakaopatikana. Sifa moja muhimu ya utaratibu wa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) ulikuwa, hata hivyo, ni ukweli kwamba alikutana kwa ushauri na Swahaabah na kujadiliana na masuala kwa pamoja ili kufikia kuelewa kuliko bora na kutafuta njia mnasaba ya kutoa hukumu. Kufikia kwake kwenye masuala ya kisheria, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikuwa kama vile ni daktari mwerevu aliye makini mwenye nia ya kutoa dawa kwa ajili ya kutibu maradhi bila ya kusababisha athari mbaya.

 

Matokeo yake, Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) ametuacha na utajiri mkubwa wa misingi ya sheria. Ibraahiym al Kakha’s (amefariki mwaka 97 Hijriyyah) alisema kwamba pale ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alipouawa kwa ajili ya Dini: “tisa ya kumi ya elimu yote iliondoka pamoja naye.” [1]

 

Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alisema kuhusiana naye, “njia yoyote ‘Umar anayoichagua, tumeikuta ni rahisi kuifuata.” [2]

 

Ufahamu wa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) ulikuwa ni wa hali ya juu na alijaaliwa kuwa na akili timamu ya kufikiria. Hivyo, alikuwa mara moja analinganisha moja kwa mengine, na kuweza kuchunguza maeneo ya suala kurudi kwenye misingi mikuu ili kuweza kuona maana yake kwa upana. Hivi ndivyo alivokuwa kipindi cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘Anhu), na wala hakubadilika pale alipokuwa yeye mwenyewe ni Khaliyfah.

 

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alisoma mengi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Ni kawaida kwake kutambua kwamba Mtume atajizuia kutokana na kuianzisha amri kwa watu kufanya jambo zuri, ijapokuwa alitaka kufanya hivyo, kwa sababu hakutaka kuwapeleka kwenye ugumu. Yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mara alikuwa akisema: “Kama mimi nisingekuwa nakhofia kulazimisha magumu kwa Ummah wangu, ningeliwaamrisha kufanya jambo……fulani na fulani.” [3]

 

Mara nyengine atawazuia kufanya jambo fulani, na baadaye, pale atakapoona kwamba sababu ya kuwazuia haina mashaka tena, ataondosha kizuizi hichi. Katika matokeo mengine, anafikia kuzuia kitu, na watamuambia kuhusu ugumu wake, na taabu itakayopatikana kutokana na kuzuiliwa huko, hivyo atajizuia kutokana na kuzuia ili kuwalinda kutokana na magumu.

 

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alimuona namna Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), pale anapokutana na uchaguzi baina ya vitu viwili, atachagua kile kilicho rahisi baina ya viwili; na hili lilikuwa na athari kubwa kwa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu). Hakika, yeye vyema alielewa kwamba Shari’ah ina malengo na matarajio ambayo ni lazima yafahamike na kutiliwa maanani; na kwamba kuna sababu muwafaka za, na nyuma yake kama sababu za hukumu hizi; ambazo nyengine zinafanywa kwa uwazi ndani ya maandiko makuu, wakati nyengine zinatajwa juu juu tu. Aliona ni wajibu wa mwanachuoni kuchunguza sababu hizo ambazo hazikutajwa ndani ya maandiko, ili kwamba maamuzi yaweze kutumika kwenye masuala mepya na maendeleo, na kila kitu kilicholetwa chini ya uamuzi wa Allaah ili kwamba watu wasiwe na mazoea ya kutafuta kitulizo na maamuzi ya kisheria kwenye matatizo yao nje ya Sheria ya Allaah.

 

Hivyo, tunapoangalia mwenendo wa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) katika Ijtihaad, tunakuta taratibu zilizo wazi za kufikia maamuzi, hoja zilizokuwepo nyuma yake zimeegemezwa kwa manufaa ya jamii, kwa ajili ya kuwa na hadhari ili kuzuia kufikia kutenda baya au kupinga uharibifu, na kutumia njia rahisi na ya manufaa chini ya sheria.

 

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kwa mfano, alitangaza baadhi ya hukumu kuwa ni batili kwa sababu ya hoja za kutumika kwake kipindi kirefu haitumiki tena, au kwa sababu ya baadhi ya vipengele vya kuufuata havipo tena. Miongoni mwa hukumu hizi: maombi yake kwa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba mateka wa vita vya Badr wauawe, maoni yake kuhusu Hijjah, na kwamba Mtume aliwaambia watu kwamba yeyote atakayesema: “Hapana Mola isipokuwa Allaah.” Ataingia Peponi, kwani wataegemea bila ya kufanya jitihada zaidi, maoni yake kwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kwamba asitoe tena mgao wa ziada kutoka kwenye hazina ya taifa kwa wale wepya walioingia kwenye Uislamu, na maamuzi yake ya kutoitumia pamoja na wengine ardhi iliotolewa.

 



[1] Ad-Dahlaawiy, HujjatuLlaah al-Baalighah, (Misri), I, uk. 278

[2] Ad-Dahlaawiy, HujjatuLlaah al-Baalighah, (Misri), I,  uk. 278

[3] Labda Hadiyth iliyokuwa maarufu kutumika katika mtindo huu ni ile kuhusiana na kusugua meno kabla ya Swalaah (as-siwaak).

Share

13-Uswuul Al-Fiqhi: Wakati Wa ‘Uthmaan Ibn ‘Affaan (Radhiya Allaahu ‘anhu)

 

‘Uthmaan alipopatiwa utii, alifanya kwa misingi wa kwamba anafanya kazi kwa mujibu wa Kitabu cha Allaah, Sunnah ya Mtume Wake, na kufuata maamuzi yaliowahi kutolewa na Makhalifa wawili. Hili, aliweka ahadi kulitimiza. Hata hivyo, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alionesha kwamba atakapokuwa Khaliyfah, atajitayarisha kufanya kazi kwa mujibu wa Kitabu cha Allaah na Sunnah ya Mtume Wake, na kisha kutumia jitihada zake za mwisho na nguvu atakayoweza katika elimu yake. Kwa sababu ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alionesha kwamba alikuwa tayari kuichukua kazi kulingana na sheria zilizowekwa na Makhalifa wawili wa mwanzo, aliungwa mkono na ‘Abdur- Rahmaan, ambaye alikuwa na maamuzi ya mwisho. Hivyo, chanzo cha tatu cha sheria, maamuzi yaliyotolewa na Makhalifa wawili wa mwanzo ilijumuishwa wakati wa Khaliyfah wa tatu, na yeye alikubali.

 

Kwa kuwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikuwa na nafasi yake kuhusiana na hili, pale yeye mwenyewe alipokuwa Khaliyfah alifanya kazi kwa mujibu wa Ijtihaad yake mwenyewe katika masuala ambayo Khulafaa’ waliopita tayari walikuwa washatoa Ijtihaad. Kwa mfano, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alifanyia kazi kwa mara nyengine suala la aidha mtumwa wa kike aliyepata watoto kwa bwana wao anaweza kuuzwa.

 

‘Uthmaan ibn ‘Affaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikuwa mmoja kati ya Swahaabah ambaye hakutoa idadi nyingi za Fatawa, labda kwa sababu masuala ya msingi aliyokutana nayo, yalikuwa tayari yameshafanyiwa kazi na Abu Bakr na ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhum), na alipendelea kutumia maoni yao. Lakini kwa kesi nyingine, alilazimika kufanya Ijtihaad, kama walivofanya waliomtangulia. Mara moja, kabla ya ‘Uthmaan kuwa ni Khaliyfah, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alimuuliza kuhusiana na suala la kisheria. Akijibu, ‘Uthmaan alisema: Kama utafuata maoni yako mwenyewe, hivyo itakuwa ni sahihi. Lakini, kama utafuata moni ya Khaliyfah kabla yake (yaani Abu Bakr), ni bora, kwa sababu alikuwa ni mzuri sana katika kutoa maamuzi.”

 

Pia alitekeleza Ijtihaad yake mwenyewe, wakati wa Hajj, hakupunguza Swalaah sehemu ya Minaa ingawa inaruhusika kufanya hivyo. Kuna ufafanuzi wa aina mbili kuhusiana na hili: ya mwanzo ni kwamba ameoa Makkah, na akafikiri kwamba watu wa Makkah hawaruhusiki kupunguza Swalaah hapo Minaa, ufafanuzi wa pili ni kwamba alikhofu kwamba Mabedui wataingiwa na wasiwasi pale watakapomuangalia yeye akifanya hivyo, na hivyo hakufanya.

 

‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu) pia alitengeneza Ijtihaad kwamba watu wote wasome Qur-aan kwa mujibu wa mtindo wa kisomo cha Zayd (Radhiya Allaahu ‘Anhu), kwasababu aliona kwamba hii ilikuwa ni sauti iliyo bora, na inayowezekana kuwa ni bora katika kuzuia kutokezea kwa migongano.

 

 

Share

14-Uswuul Al-Fiqhi: Wakati Wa ‘Aliy Ibn Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘Anhu)

 

Wakati Wa ‘Aliy Ibn Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu)

 

 

‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikuwa kama ‘Umar ibn al Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu), kwa maana ya kwamba alielewa na kutumia maandiko ya Qur-aan na akijali sana kuunganisha masuala fulani kwa misingi ya jumla. Kabla ya kushikilia ofisi ya Khaliyfah, alitambulika kuwa jaji bora Madiynah.

 

Pale (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomteua ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa ni jaji nchini Yemen. Yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuombea dua, akisema: “Ewe Mola, Uongoze moyo wake na mfanye atamke ukweli.” Hakika, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alithibitisha kuwa ni jaji bora, na alitatua kesi ngumu kwa wingi.

 

‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alielezea elimu yake kwa kusema: “Kwa Allaah, hakuna aya ya Qur-aan iliyowahi kuteremshwa isipokuwa nilijua nini ilishushwa, wapi na kwanini ilishushwa. Mola wangu Ameniwekea juu yangu moyo ambao unafahamu na ulimi wenye kutamka vyema.”

 

Wakati wowote linapopelekwa jambo kwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kwa maamuzi atalikubali bila ya kusita. Na kama ataulizwa kutoa Fatwa, atafanya hivyo kwa kuisoma kutoka Kitabu cha Allaah, na baadae Sunnah ya (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hakika, undani wa elimu ya Qur-aan na Sunnah ulijulikana vizuri sana.

 

‘Aishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) alisema: “Kwa mnasaba wa Sunnah ya (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), alikuwa ni mbora na maarufu kuliko watu wote.”

 

‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikuwa akitengeneza maana yake mwenyewe kwa njia ya Ijtihaad ikiegemezwa katika al Qiyaas, al Istis-haab[1], al Istihsaan[2], na al Istislaah[3], mara zote akiegemeza mawazo yake kwenye madhumuni mapana ya Shari’ah pindi anaposhauriwa kuhusu uwezekano wa kuengezeka Hadd-adhabu inayopatikana kwa yule aliyepatikana na hatia ya kunywa ulevi, alipambanisha ulewaji wa msingi usiokuwa sahihi kwamba ulewaji unaweza kumpelekea mtu kufanya tuhuma kama hizo.

 

Wakati wa Khilaafah yake, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alimtaka ushauri ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuhusiana na adhabu ya kundi la watu walioafikiana kwa pamoja kukusudia kufanya mauaji. ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alisema, “Ewe Kiongozi wa Wakweli! Kama kundi la watu watakusanyika pamoja katika kuiba, je, hutokata mkono mmoja wa kila mmoja?” Pale ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alipojibu kwa kukubali, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alisema, “Ndivyo, hivyo inavokuwa kwa kesi hii.” Kwa sababu hiyo, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alitamka msemo wake maarufu: Kama raia wote wa Swan’aa watakubalina kwa pamoja kumuua mtu mmoja, nitawaadhibu kifo wengi kati yao.”

 

Mfanano baina ya mauaji na wizi ulifanywa kwa sababu katika kila kesi kuna msukumo wa kijinai uliogaiwa baina yao wote waliotenda matendo hayo, na ni hili linalofanya adhabu kuwa yenye kutisha.

 

Juu ya hivyo, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alipendelea kuwachoma moto wakiwa hai wale walioritadi kwa nguvu na wazushi waliomzulia, ijapokuwa alikuwa anaelewa vyema kwamba maamuzi ya Sunnah yapo laini kumuweka asiyeamini kama huyo na walioritadi kwenye adhabu ya kifo. Katika maamuzi haya, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alionesha yeye mwenyewe kuwa na bidii kuanzisha adhabu kali na yenye kuzuia kuliko adhabu nyengine yoyote ya murtaddi, kwa sababu alitambua kuwa suala hili ni nyeti sana. Hivyo, alianzisha adhabu kali mno kwa tendo kama hilo, ili kuwaogopesha watu kulitenda. Juu ya hivyo, ili kusisistiza hili, hapo hapo alinukuu ubeti ufuatao wa shairi:

 

“Nilipotambua namna jambo lilivyo zito,

Nikawasha moto mkubwa na kusimama kwa ajili ya Qanbar.”

 

Pale ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alipomsikia mwanamke ambaye mumewe alikuwa nje kwa safari za kijeshi na ambaye nyumbani kwake watu asiowajua walikuwa wakimjia. Hivyo, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) akampelekea ujumbe kwamba asipokee wageni pale mumewe anapokuwa hayupo. Pale huyo mwanamke aliposikia kwamba Khaliyfah anataka kuzungumza naye, alifikwa na woga, na kwa vile alikuwa mjamzito, aliharibu mimba akiwa njiani kumuona ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu).

 

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikereka sana kwa lile lililotokea, aliwataka ushauri Swahaabah kuhusiana na jambo hilo. Miongoni mwao, alikuwa ‘Uthmaan ibn ‘Affaan, na ‘Abdur-Rahmaan ibn ‘Awf, walimuhakikishia: “Hukufanya jambo isipokuwa ukijaribu kumuelimisha, hukufanya jambo baya.”

 

Baadaye ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alimgeukia ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu), akimtaka mawazo yake. ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alijibu, “Watu hawa wamezungumza, na kama hili ni wazo bora walilokuja nalo juu, basi ni la uadilifu tosha. Lakini, kama wamezungumza tu kukuridhisha wewe, basi wamekulaghai. Nategemea kwamba Allaah Atakusamehe kwa kosa hilo, kwani Yeye Anatambua nia yako ilikuwa njema. Lakini, kwa Allaah, ulipe fidia kwa mtoto.”

 

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alisema, “Kwa Allaah, umezungumza nami kwa utiifu. Naapa kwamba usikae chini hadi ugawe pesa hii miongoni mwa watu wako.”

 

 



[1] Al-Istishaab: Kutambua mazingira katika utaratibu wa kutoa hoja ya kisheria.

[2] Al Istihsaan: Kuikubali Qiyaas-kufananisha ambayo inaonekana kuwa juu kisheria kwa kulinganisha na mfananisho ulio dhahiri. Ni katika maelezo hayo ambapo al Istihsaan inakuja kwa mara kadhaa kutafsiriwa kama ni “Hiari ya Mwanachuoni”.

[3] Al-Isislaah: Kutambua kisheria ustawi na hali njema za wote, mmoja mmoja na jamii kwa pamoja.

Share

15-Uswuul Al-Fiqhi: Fuqahaa Miongoni Mwa Swahaabah Na Taabi’uun

 

Fuqahaa Miongoni Mwa Swahaabah Na Taabi’uun

 

 

 

Kipindi hichi kinaaminika kuwa kimeanza kwa kupita kipindi kilichoitangulia, mwaka 40 Hijriyyah, pale kipindi cha Maswahaba wakuu walioongoka vyema kilipomalizika. Hivyo, ikaanza tarehe mpya, ile ya Fuqaaha kutoka miongoni mwa Swahaabah na wazee wa Taabi’uun. Sheria katika wakati huu bado sana ilikuwa kama wakati uliopita, kwani vyanzo vya sheria hiyo, yaani Qur-aan, Sunnah, IIjmaa’ na Qiyaas, vilibaki kama vilivyo. Hata hivyo, sheria kwa wakati huo ilitofautiana kwenye nyanja nyingi kulingana na ule uliopita kabla.

 

Miongoni mwa mabadiliko yenye maana yalikuwa yafuatayo:

 

1.       Wanachuoni wamekuwa wanapendelea zaidi kuchimbua kupita kiasi maana za maandiko kwa uwazi.

 

2.       Njia zao za kujadili Sunnah zilipatwa na mabadiliko makubwa. Hakika, tofauti hii ni tokeo la tofauti za kisiasa zenye kushikamana na kuibuka kwa madhehebu tofauti na walio na fitna thaabit, kama vile Shi’ah na Khawaarij, ambao nia zao kwa Sunnah zilikuwa ni tofauti. Hao Shi’ah walikaidi kukubali Hadiyth zilizokuwa hazijapokelewa na wafuasi wao wenyewe; na Khawaarij walikaidi kukubali Hadiyth kama, popote kwenye mfululizo wa wapokezi wa Hadiyth hakuna hata upokezi mmoja[1]. Khawaarij pia walizikataa Hadiyth zote zisizokuwa na uthibiti wa aya kutoka kwenye Qur-aan.

 

3.       Kosa la kutofautiana lililokuja juu, al-Ijmaa’ haikuwa tena yenye kuwezekana katika kipindi hichi. Kimsingi, hii ni kwa sababu kila kundi lilikosa imani ya wanazuoni wa kila kundi jengine, na hawatokubaliana na maoni yao tena, ama wakikubali au walikataa nao. Kwa kuongezea, Fuqahaa miongoni mwa Swahaabah wameanza kutawanyika sehemu zote za dunia ya Kiislamu, hivyo ilikuwa haiwezekani kwao kukutana kwa lengo la kujadili masuala.

 

4.       Pia katika dunia hii, mapokezi ya Hadiyth na Sunnah zimekuja kuwa maarufu, ambapo kesi hii huko nyuma haikuwahi kuwa kama hivi.

 

5.       Uwongo uliobuniwa wa Hadiyth, kwa sababu nyingi za kutambulika ambazo hatuhitaji kuzijadili hapa zilianza kuenea sana. Kwa mnasaba huu, Waislamu walipokea kwamba Ibn Abbaas alisema: “Tulikuwa tukipokea Hadiyth nyingi kutoka kwa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya watu kuwa na woga na ubunifu. Lakini pale watu walipoanza kuwa wazembe katika kusimulia sifa za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), tulisimamisha kusimulia Hadiyth.”



[1] Mfano wa Hadiyth zinaitwa mapokezi ya mtu mmoja “Khabar al Waahid” au, kwa wingi, Aahaad. Suala la nafasi ya Hadiyth kama hiyo unajadilwa baadaye kwenye andiko hili.

Share

16-Uswuul Al-Fiqhi: Sura Ya Tatu - Utungaji Sheria Baada Ya Kipindi Cha Maswahaba

 

UTUNGAJI SHERIA BAADA YA KIPINDI CHA MASWAHABA

 

Kipindi cha Swahaabah kilifikia hatamu baina ya mwaka 90-100 H, na kufuatiwa na kipindi cha Taabi’uun ambapo wanazuoni wake walianza kuwa na majukumu kwenye Fiqhi na kutoa Fataawa. Swahaabah wa mwisho wa Kuufah alifariki mwaka 86 au 87 H. Wa mwisho kwa Madiynah, ni Sahl bin Saa’d as-Saa’di, alifariki mwaka 91 H. Wa mwisho kwa Baswrah, ni Aanas bin Maalik, alifariki mwaka 91 H (wengine wanasema mwaka 93 H). Wa mwisho kwa Damascus, ‘Abdullaah bin Yusr, alifariki mwaka 88 H. Wa mwisho katika Swahaabah wote ni ‘Aamir bin Wathillah bin ‘Abdillaah (Abuu Twufayl), alifariki mwaka 100 H.

 

Hapo tena, wale waliokuja kuwa na jukumu la kutoa Fataawa walikuwa ni watu huru Mawaalii, wengi miongoni mwao wamewahi kuishi pamoja na Fuqaaha miongoni mwa Swahaabah, kama vile: Naafi’i, aliyeachwa huru na Ibn ‘Umar, ‘Ikrimah aliyeachiwa huru na Ibn ‘Abbaas, ‘Atwaa bin Rabbaah, Faqiyh (mwanachuoni wa sheria) wa Makkah; Twaawuus, Faqiyh wa Yamaamah. Ibraahiym an-Nakha’iy, Faqiyh wa Kuufah; Hasan al-Baswriy Faqiyh wa Baswrah na Ibn Siyriyn ambaye pia ni Faqiyh wa Baswrah; ‘Atwaa al-Khurasaaniy wa Khurasaan, na wengineo. Hakika, Madiynah ilikuwa ni ya aina yake kwa kuwa na Faqiyh wa ki-Quraysh, Sai’yd bin al-Musayyab.

 

Taabi’uun hawa, kwa uchache sana walibadili Fataawa za Swahaabah ambao kutokana nao wamepata elimu yao, hivyo ni vigumu kupata tofauti baina ya taratibu zao za kufikia maamuzi na za mababu zao. Hata hivyo, taratibu za kufikia maamuzi zilikuwa, kwa kipindi hichi, zinaanza kukua na, katika kuendelea kwake, zimekuwa wazi kuliko hapo kabla.

 

Imesimuliwa kwamba Hasan bin ‘Ubaydullaah an-Nakha’iy alisema: Nilimuuliza Ibraahiym an-Nakha’iy: “Umesikia kutoka wengine Fataawa zote ambazo nimesikia wewe ukitoa?” Alisema: “Hapana” Nilimuuliza “Hivyo wewe unatoa Fataawa ambazo hujazisikia?” Alisema: “Nimesikia nilichofanikiwa kusikia; lakini nilipokutana na masuala kuhusiana na yale nisiyowahi kuyasikia kitu, nilitofautisha, kwa kufananisha, pamoja na masuala niliyowahi kusikia[1].”

 

Miongoni mwa sifa zenye maana kwa kipindi hichi ni kuibuka kwa tofauti za maoni baina ya wanazuoni Wakishia kwenye masuala tofauti. Hili linaweza kuwekwa wazi kwa maamuzi mawili yaliyochukuliwa na Khaliyfah wa wakati huu, ‘Umar bin Abdil-‘Aziyz.

 

1.      Aliamrisha kwamba mwenendo uliosifiwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ukusanywe na kuwekwa kwenye maandishi. Kwa sababu hiyo, watu wa kila jimbo waliandika vitabu wanavyotambua kuwa ni sehemu ya Sunnah[2].

2.      Alizuia mamlaka ya kutoa Fataawa, kwenye wilaya nyingi; kwa watu wachache waliotajwa kwa majina, kama alivyofanya nchini Misri, pale alipotaja majina matatu tu kwa lengo hili. Cha kushangaza, wawili miongoni mwao walikuwa huru, Yaziyd bin Abi Habiyb na Abdullaah bin Abi Ja’afar, na wa tatu alikuwa ni Mwarabu, Ja’afar bin Rabi’ah. Khalifyah alipoulizwa kuhusu uteuzi wa watu wawili walio huru na Mwarabu mmoja tu, alijibu: “Ni kosa gani la kwangu kama watu hao walio huru wanajiendeleza wao wenyewe na nyinyi hamfanyi hivyo[3].”

 

Katika barua yake kwa Abuu Bakr, Muhammad bin ‘Aam bin Hazm al-Ansaarii, Khaliyfah huyo alieleza sababu zake za kuamrisha kwamba mwenendo uliosifiwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) uwekwe kwenye maandishi. Aliandika: “Angalia kwa Hadiyth yoyote ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), au Sunnah au mwenendo unaoweza kutafuta. Baadaye weka kwenye maandishi kwa ajili yangu; kwani nakhofia kwamba elimu hii itapotea kutokana na kufariki kwa wanachuoni[4].”

 

 

BAADA YA TAABI’UUN:

 

KIPINDI CHA MAIMAMU MUJTAHIDIYN

 

Kipindi hichi kilitambuliwa na Shah WaliyuLlaah ad-Dahlawiy kama ifuatavyo:

 

Fuqaaha wa kipindi hichi walichukua Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), maamuzi ya majaji wa mwanzo, na utambuzi wa kisheria wa Swahaabah, Taabi’uun na kizazi cha tatu, baadaye walitoa Ijtihaad zao wenywe.”

 

Huo ndio mtindo wa wanazuoni wa kisheria wa wakati huo walivyofanya kazi. Kimsingi, wote wao walikubali vyote, Hadiyth za Musnad[5] na pia Mursal[6].

Juu ya yote hayo, imekuwa ni tabia yao kutaja mawazo ya Swahaabah na Taabi’uun kama ni ushahidi. Kimsingi, kulikuwa na sababu mbili kwa hili:

 

1.     Mawazo kama hayo, yalikuwa hakika ni Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo imesimuliwa na mmoja wa Swahaabah au Taabi’uun ambaye kwa kukhofia kugeuza maneno, hawakuthubutu kuinasibisha Hadiyth kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

2.     Yawezekana sababu nyengine ni kwamba mawazo kama hayo yalitolewa na Swahaabah kutoka katika maandiko ya Hadiyth na kuwasilisha ufahamu wao wa Sunnah.

 

Bila ya shaka, kwa mfumo huu, hao Swahaabah walikuwa ni bora kuliko wale waliofuatia baadaye, kwa sababu walimfahamu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kwa hivyo walikuwa na uwezo zaidi wa kuyatolea maana kila alichozungumza. Hivyo, maamuzi na mawazo yao yalikubaliwa kama ni yenye nguvu, isipokuwa kwenye kesi ambapo wao wenyewe walitofautiana, au pale ambapo matamko yao yalikuwa na mgongano ulio wazi kwa Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iliyothabiti.

 

Kwa upande mwengine, kwenye masuala ambapo Hadiyth mbili au zaidi ziligongana, wanazuoni watarudi kwenye maoni ya Swahaabah ili kutambua ipi miongoni mwa hizo Hadiyth mbili zilikuwa ni sahihi. Hivyo, kama Swahaabah alisema kwamba Hadiyth imebatilishwa, au haikuwa yenye kufahamika kimaana; au kama hawakutamka kwa uwazi kitu chochote kuhusiana na Hadiyth, lakini wameidharau, na haikuendana sambamba na ulinganifu wake, hivyo kuonesha kwamba Hadiyth hiyo ilikuwa kwa upande fulani ina kasoro, na kwamba ilikuwa haiendani na hali halisi, au kwamba tafsiri yake ilikuwa ni nyingine isiyokuwa ya maana hiyo, basi Maimamu Mujtahidiyn wataridhika na maoni yao.

 

Pale matamko ya Swahaabah na Taabi’uun yalipotofautiana kwenye suala lolote, basi kila Faqiyh atafuata maamuzi ya wale wanaotoka wilaya hiyo hiyo kama alivyo yeye, na walimu wake, kwa sababu atakuwa na uwezo zaidi wa kupambanua usahihi wake, kutegemeana na ukaribu wake na wasimulizi, wa mawazo na maelezo yaliyomfikia yeye katika mamlaka yao. Vivyo hivyo, Faqiyh huyo atakuwa amejengeka vizuri na utaratibu wao wa kisheria.

 

Elimu ya dhana ya sheria iliegemezwa kwenye mawazo ya ‘Umar, ‘Uthmaan, Ibn ‘Umar, ‘Aishah, Ibn ‘Abbaas na Zayd bin Thaabit, na wafuasi wao kutoka miongoni mwa Taabi’uun, kama az-Zubayr (amefariki mwaka 94), Saalim (amefariki mwaka 106), Atwaa’ bin Yassaar (amefariki mwaka 103), Qaassim bin Muhammad (amefariki mwaka 103), ‘Ubaydullaah bin ‘Abdullaah(amefariki mwaka 99), al Zuhri (amefariki mwaka 124), Yahya bin Sa’ad (amefariki mwaka 143), Zayd bin Aslam (amefariki mwaka 136) na Rabi’at ar-Ra’i (amefariki mwaka 136), ilikuwa ni elimu inayokubalika zaidi kwa watu wa Madiynah. Ilikuwa kwa sababu hii ambapo Imaam Maalik aliegemeza hoja zake za kisheria kwenye mafundisho yao.

 

Namna hiyo, mawazo ya ‘Abdullaah bin Mas’uud na wafuasi wake, maamuzi ya Khaliyfah ‘Aliy, Shurayh (amefariki mwaka 77 H), na ash-Sha’abiy (amefariki mwaka 104 H), na Fataawa za Ibraahiym an-Nakha’iy (amefariki mwaka 96H), yalikuwa ni yenye kukubalika kwa watu wa Kuufah.

 

Akifafanua jambo hili, Shaah WaliyuLlaah ad-Dahlaawiy ameandika: Pale Masruuq (amefariki mwaka 63H) alipofuata mawazo ya Zayd bin Thaabit kuhusiana na mgawano wa mirathi baina ya babu na ndugu (wa merehemu), ‘Alqamah (amefariki mwaka 62 H) alimuuliza, “Jee yupo miongoni mwenu aliye mjuzi zaidi kuliko ‘Abdullaah bin Mas’uud?

 

Masruuq alijibu, “Hapana, lakini Zayd bin Thaabit na watu wa Madiynah wanagawa mirathi baina ya babu na ndugu…

 

Hivyo, kama watu wa Madiynah walikubaliana na jambo, wanazuoni wa kizazi wanaofuata, hao Taabi’uun walikubali kwa uthabiti. Hivyo ndivyo Maalik alivyoaamrisha pale aliposema: “Sunnah ambayo sisi, watu wa Madiynah, hatukutofautiana ni kadhaa na kadhaa.”

 

Ama ikiwa wanazuoni hao wa mwanzo kutoka Madiynah watakhitalifiana kuhusu jambo lolote, wanazuoni waliofuata watafuata mawazo yao ambayo yalikuwa na nguvu na yanaweza kutegemewa zaidi; aidha kwa mnasaba wa kwamba yanatumika na idadi kubwa ya wanazuoni wa mwanzo, au kwa kuwa ni toleo la mfanano wa kisheria wenye kuleta maana, al-Qiyaas, au ambayo imefikiwa kutoka maandiko fulani ndani ya Qur-aan au Sunnah. Ni mtindo huu ambapo Maalik anamaanisha pale anaposema: “Hili ni zuri zaidi kwa nilichosikia.” Baadaye, kama wanazuoni wanaofuata hawatopata suluhisho lolote kwenye tatizo ndani ya kazi ya mababu zao, wao wenyewe wataelekea kwenye maandiko yenye kufaa ili kutengeneza mawazo yao ya kisheria.

 

Kwa wakati huu, wanazuoni walishajiika kuanza kuweka vitu katika kumbukumbu kwa maandishi. Hivyo Maalik (amefariki mwaka 179)

Madiynah, Ibn Abi Dhi’ib (amefariki mwaka 158), Bin Jurayj (amefariki mwaka 150?) na Bin ‘Uyaynah (amefariki mwaka 196) Makkah, ath-Thawriy (amefariki mwaka 161) Kuufah, na Rabi’i bin Subayh (amefariki mwaka 160) Baswrah, walioanza kuandika vitu, na wote walifuata utaratibu huo.

 

Pale Khaliyfah, Mansuur, alipotekeleza Hajj na kukutana na al Imaam Maalik, alisema: “Nimeamua kuamuru kwamba nakala zitengenezwe za vitabu hivi ulivyoandika. Nitakutumia nakala kwa kila mkoa wa ulimwengu wa Waislamu na ili wanazuoni waendane kwa mujibu wa hivyo na sio kurudia kwenye kazi nyengine zozote.

 

Maalik alisema: “Ewe Amiyrul Muuminiyn, usifanye hivyo! Watu tayari wamekwishasikia mawazo tofauti ya kisheria na kusikiliza Hadiyth na masimulizi; na wameridhika na chochote kilichowafikia mwanzo, kwa hivyo hili limechangia kwa khitilafu katika mtindo wa desturi zao miongoni mwa watu. Achilia mbali wale watu wa kila mtaa kwa kuwa na chaguzi ambazo wamekwishafanya.

 

Simulizi hiyo hiyo inatolewa kwa kumrudia Khaliyfah, Haaruun ar-Raashiyd, kwamba alitaka kuwalazimisha watu kuwafuata Muwattwaa’.

 

Lakini Maalik alimwambia: “Usifanye hivyo, kwa sababu Swahaabah wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walitofautiana kwenye Sunnah. Baadaye walitawanyika na kuketi sehemu tofauti za Ulimwengu wa Waislamu; na sasa njia zao za khitilafu zimesimamishwa madhubuti kabisa.

 

…Maalik alikuwa ni mwenye elimu bora kuhusu Hadiyth zilizosimuliwa na watu wa Madiynah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na mfuatano wa wasimulizi wa Maalik ulikuwa wenye kutegemewa zaidi. Alikuwa pia ni mwenye elimu bora kuhusu maamuzi ya ‘Umar na matamko ya kisheria ya ‘Abdullaah bin ‘Umar na ‘Aishah (Radhiya Allaahu ‘anhum) na wafuasi wao kutoka miongoni mwa Fuqaaha saba. Sayansi ya usimulizi wa Hadiyth na Fataawa ziliegemezwa kwenye elimu ya Maalik na mfano wake yeye.

 

Abuu Haniyfah alikuwa ni mbora wa kujitolea katika kutoa maana za kisheria za Ibraahiym an-Nakha’iy na, kwa mara chache watakhalifu hoja zao. Alikuwa ni mzuri mno katika kutoa maamuzi kwa kutumia mtindo wa Ibraahiym, vile vile katika kutumia utaratibu huo ili kufanyia kazi maelezo ya kesi za sheria.

 

Kama utapendelea kuelewa ukweli kuhusu tulichokieleza, basi fupisha mafundisho ya Ibraahiym na majeshi yake kama yalivyoandikwa kwenye kazi zifuatazo: Al-Aathaar “Desturi” cha Muhammad ash-Shaybaniy, Jaami’ “Muhtasari Uliokamilika” cha ‘Abdur-Razzaaq na Muswannaf “Mtungo wa maandiko” cha Ibn Abi Shaybah, na zilinganishe pamoja na maoni rasmi ya Abuu Haniyfah. Hakika, utakuta kwamba Abuu Haniyfah yupo mbali kidogo na njia zao, na hata hvyo maoni yake hayakutofautiana na maoni ya wanazuoni kutoka Kuufah[7].”

 

Hakika, maoni ya ad-Dahlawi yanahitaji kuangaliwa kwa makini. Alikuwa ni mwenye pupa kueleza kwamba al-Imaam Maalik na Abuu Haniyfah, na wafuasi wao, walikuwa wapo juu au chini zaidi kukubaliana na maoni ya Taabi’uun na Swahaabah kabla yao (kinyume na kufikia Ijtihaad yao), na hawakuruka mipaka ya misingi ya sheria za mababu zao. Hili, hata hivyo, ni hitimisho ambalo si rahisi kukubaliana.

 

Ni uwazi unaotambulika kwamba kuna njia tofauti za kuiendea Fiqh; na kila mmoja wa Maimamu alibuni njia tofauti kwa somo hilo. Sio jambo lililo rahisi kudai kwamba hizi zilichukuliwa kutoka kwa Swahaabah na Taabi’uun. Angalia, kwa mfano, utaratibu wa Maalik katika kutumia desturi na mila za watu wa Madiynah kama ni chanzo (kidogo) cha kutunga sheria; au matumizi ya Abuu Haniyfah katika Istihsaan na ‘Urf[8].

 

Juu ya hivyo, hamna hata mmoja wao aliyeegemeza hoja zake kwenye Fataawa za Taabi’uun, lakini badala yake walishindana nao, wakisema “Walikuwa ni watu (wa elimu) na sisi pia.”

 

Kwa kuongezea, tofauti na yeyote kabla yao, kila mmoja ameweka wazi kifungu cha masharti ya kukubaliana na Hadiyth kuwa sahihi.

 

Juu ya hivyo, tokeo la kuongezeka usambazaji wa Hadiyth wakati huo, kwa kuongezea na kutokea kwa Hadiyth ambazo hazijapata kusambazwa hata siku moja, zimepelekea, kwa upande mwengine wa maamuzi ya kisheria na nafasi ambayo ni tofuati kabisa na zile zilizokamatwa na Swahaabah.

 



[1] Ibn Hajar, Al-Iswaabah, IV, 112; na Ibn ‘Abdul Barr, Al-Isti’aab (juu ya mstari wa Al-Iswaabah) uk. 145.

[2] Ibn Abdul Barr, Jaami’ Bayaan al ‘iIlm, I, uk. 33.

[3] Al-Maqriizi, Khuttat, IV, uk. 143.

[4] Barua hii ilisimuliwa na al-Imaam al-Bukhaariy ndani ya Swahiyh yake bila ya mfuatano wa wasimulizi ulio rasmi (yaani Ta’liqa kama ni Mu’allaq Hadiyth). Pia, iliingizwa na al-Imaam Maalik ndani ya Muwattwaa yake; Angalia maoni ya Zarqaani, I, uk. 10.

[5] Al-Musnad: Ni Hadiyth yenye mfuatano uliokatika wa wasimulizi kwendea nyuma hadi kumfikia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

[6] Al-Mursal: Ni Hadiyth ambayo mfuatano wake wa wasimulizi mwishoni umekatika, yaani ni ile inayoelezwa na Tabi’i kama imetoka moja kwa moja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hakika, kama upo uwezekana wa Tabi’i kutoisikia Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), basi Hadiyth aliyoisimulia kwa mtindo huu, hakika imesimuliwa kwake aidha na Tabi’i mwengine, au kutoka kwa mmoja miongoni mwa Swahaabah. Lakini kwa vile mwanachuoni Tabi’i hana mashaka kuhusiana na uadilifu wa mmoja kutoka kwa yule aliyemsimulia Hadiyth ameona haina haja ya kumtaja jina. Kwa vizazi vinavyofuata vya wanazuoni wa Fiqh na Hadiyth. Hata liwe suala la ama Hadiyth Mursal kuweza kukubalika lilikuwa ni jambo gumu. Sababu ya umakini wao ni kwamba; mfuatano wa Hadiyth hiyo ni, kubwa lao, mfuatano uliokatika; na hakuna shaka kwamba, kama msimulizi wa Tabi’i amepokea Hadiyth kutoka kwa kizazi chake chengine, kwamba huyo Tabi’i ni msimuliaji anayetegemewa. Hata hivyo, kwa hao wanazuoni wa Fiqh na Hadiyth wa kizazi cha mwanzo, halikuwa ni tatizo kubwa sana, kwani walikuwa wamewazoea wasimuliaji wa Tabi’i na Shuyuukh kutokana na yule waliyemsikia na kuipokea Hadiyth. Hivyo, ma-Imaam wawili Abuu Haniyfah na Maalik wanaikubali Hadiyth ya Mursal; ilhali Maimamu wawili waliofuata, yaani ash-Shafi’i na Ahmad, wanaikataa hiyo Mursal.

[7] Imefupishwa kwa ruhusa kutoka kwenye kitabu cha ad-Dahlawiy, HujjatuLlaah al Baalighah, (Egypt), I, uk. 205-308.

[8] Anachoeleza hapa mwandishi ni kwamba hizi njia zilizozuka ni zana za mtindo usiojulikana kwa Swahaabah, lakini bado zilitumika kwa mapana na kufungiwa kazi na Maimamu hawa wawili.

Share

17-Uswuul Al-Fiqhi: Watu Wa Rai Na Watu Wa Hadiyth: Ahl Al-Hadiyth Na Ahl Ar-Ra-ay

 

WATU WA RAI NA WATU WA HADIYTH:

AHL AL-HADIYTH NA AHL AR-RA-AY

 

Huenda ukweli huu ukaja kuwa makini zaidi pale tutakapotaja chimbuko la fikra mbili za kisheria yasiyokuwa rasmi; watu wa Rai au Ahl ar-Ra-ay, na wale wa Hadiyth au Ahl al-Hadiyth, na kutokea kwa tofauti baina yao kuhusiana na vyanzo vyote vya utaratibu, na masuala ya kesi za sheria. Ijapokuwa ni kweli kwamba fikra zote hizi zilikuwa na mizizi yake katika kuvifuata vizazi viwili vilivyopita, ilikuwa ni katika wakati huu kwamba, tofauti zao kwenye masuala ya Fiqhi yalikuja kuwa wazi, na ilikuwa ni wakati huu kwamba watu walianza kujigawa makundi kwa msingi wa tofauti zao katika kupata dalili za kisheria kutokana na vyanzo.

 

Waandishi wa Historia ya Sheria ya Kiislamu, wanasisitiza kwamba watu wa fikra za Rai, wa Ahl ar-Ra-ay ilikuwa ni kupanuka kwa elimu iliyotolewa na ‘Umar na ‘Abdullaah bin Mas’uud ambao miongoni mwao Swahaabah, walikuwa na upana wa kupanga katika matumizi yao ya Ra-ay (yaani mawazo). Badala yake, ‘Alqamah an-Nakha’iy (amefariki mwaka 60 au 70 H), ami na mwalimu wa Ibraahiym an-Nakha’iy, Ibraahiym alishajiishwa nao, baadaye alimsomesha Hammaad bin Abi Sulaymaan (amefariki mwaka 120 H), ambaye, baadaye alikuwa ni mwalimu wa Abuu Haniyfah.

 

Wanahistoria hao hao wanafafanua kwamba, hao watu wa Hadiyth wa Ahl al-Hadiyth ilikuwa ni mfululizo wa elimu za hao Swahaabah ambao khofu zao za kuchanganya barua za vyanzo vya maandiko (Nuswuus) ziliwafanya kuwa na hadhari kwa kila upande, hadi kufikia ambapo walikuwa hawawezi kwenda mbali zaidi ya maandiko. Hili lilikuwa ni, na kwa urefu, kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar bin al-Khattwaab, ‘Abdullaah bin ‘Amr bin al-‘Aas, az-Zubayr, na ‘Abdullaah bin ‘Abbaas.

 

Fikra za Ahl al-Hadiyth zilikuja kuenea zaidi sehemu za Hijaaz kwa sababu zilizo nyingi, na iliyo muhimu mno ilikuwa ni idadi kubwa ya Hadiyth na simulizi nyengine zilizojulikana na watu wa eneo hilo, na ukweli ni kwamba, Wilaya hiyo ilikuwa ni imara zaidi baada ya kiti cha Khilaafah kilipoondoshwa na shughuli nyingi za kisiasa zilipohamishwa, kwanza ni Damascus, baadaye Baghdaad. Imaam wa Madiynah, Sa’iyd bin al-Musayyab (amefariki mwaka 94 H), aliwahi kusimulia kwamba watu wa Makkah na Madiynah hawakupoteza Hadiyth na Fiqh nyingi, kwa sababu walikuwa wazoefu katika Fataawa na masimulizi ya Abuu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan, ‘Aliy (kabla ya kuwa Khaliyfah), ‘Aaishah, Ibn ‘Abbaas, Ibn ‘Umar, Zayd bin Thaabit na Abuu Hurayrah, na hivyo hawakuona haja ya kutumia Ra-ay kwa lengo la kupata sheria.

 

Fikra za Ahl ar-Ra-ay, kwa upande mwengine, zilipata sifa nchini Iraq. Wanazuoni wa kundi hili walifikiria kwamba tafsiri za kisheria za Shari’ah ziwe na msingi wa hoja, waangalie vizuri mapenzi ya watu, na kurejeza pamoja na upambanuzi wenye hekima. Hakika, wanachuoni hawa waliamini kuwa ni jukumu lao kuweka bayana maana hizi na hekima zilizomo ndani ya sheria, na kuzitenganisha baina yao; ili kwamba, kama hoja za sheria yoyote zitakosa mnasaba kwa kupita wakati au kubadilika mazingira; sheria haitokuwa tena yenye nguvu. Kama wataona hoja ndani ya sheria, mara nyengine wataonelea bora kutoa hoja kwa kutumia msingi wa matumizi ya kufananisha kwa hoja hizo. Hivyo, kwa kesi nyingi, hoja zitaafikiana pamoja na sheria bora pale hoja hizo zitakapogongana na ushahidi wa makundi tofauti ya Hadiyth.

 

Kuenea kwa utaratibu huu nchini Iraq, ulisaidiwa na idadi ya Swahaabah waliosukumwa na utaratibu wa ‘Umar. Miongoni mwao alikuwa ni Ibn Mas’uud, Abuu Muusa al-Ash’ariy, ‘Imraan bin Huswayn, Anas bin Maalik, Ibn ‘Abbaas na wengineo. Kuenea huku pia kulisababishwa sana na kupelekwa Khilaafah nchini Iraq, na kukaa kimakaazi kwa ‘Aliy na wafuasi wake.

 

Pale mapote, kama Shi’ah na Khawaarij, yalipotokea nchini Iraq, mgongano ukaibuka na utengenezaji wa Hadiyth za kubuni ukaenea sana[1]. Matokeo yake, wanazuoni wa kisheria wa Iraq walilazimishwa kuweka vigezo vya kukubali Hadiyth. Kutokana na ulazima huo, ni simulizi chache zilizotolewa na Swahaabah waishio Iraq zilikubalika. Juu ya hivyo, idadi kubwa ya matatizo ya kisheria na ongezeko la kuendelea kwenye masuala ya kisheria mapya ambayo hayakuwa na mfano wake nyuma kwenye eneo hilo, zilikuwa zaidi ya kujadiliwa kwa mnasaba wa Hadiyth zenye kutegemewa.

 

Kwa hivyo, ilikuwa kwa njia hii ambapo ‘Ummah uligawika, kwa wale wasiojihusisha na aidha Shi’ah au Khawaarij, kwenye makundi mawili, Ahl al-Hadiyth na Ahl ar-Ra-ay, na mgongano baina yao ukawa mkali.

 

Hivyo, Ahl ar-Ra-ay kawaida wakiwatoa makosa Ahl al-Hadiyth kwa kuwa na kiwango kidogo cha umakini na uchache wa ufahamu wa Fiqhi, ingawa Ahl al-Hadiyth walidai kwamba mawazo ya Ahl ar-Ra-ay hayakuegemezwa zaidi ila kwenye kubahatisha tu; na kwamba wamejitenga wenyewe kwa kutokuwa na hadhari inayohitajika katika masuala ya Dini yenye umuhimu, ambayo yanaweza tu kuhakikishwa kupitia msaada wa vyanzo vya maandiko.

 

Hakika, Ahl ar-Ra-ay walikubaliana na Waislamu wote kwamba pale mtu atakapofahamu Sunnah, hatoikataa. Kwa sababu si zaidi ila ni mawazo ya mtu fulani. Udhuru wao kwenye kesi zote hizo ambazo wamelaumiwa kwa kuchanganya Sunnah, si chochote ila kwamba hawakutambua Hadiyth yoyote kuhusiana na suala linalobishaniwa, au kwamba walitambua Hadiyth lakini hawakuikubali kuwa ni yenye maana kwa sifa ya udhaifu kwa wasimuliaji au kasoro nyengine waliyoiona (kasoro ambayo pengine wengine hawakuiona kuwa yenye kuharibu), au kwamba walitambua Hadiyth nyengine ambayo wao waliitambua kuwa yenye maana na ambayo ilipingana na kusudio la sheria ya Hadiyth inayokubalika na wengine.

 

Juu ya yote hayo, Ahl al-Hadiyth walikubaliana na Ahl ar-Ra-ay katika dharura ya kuwa na msaada wa hoja wakati wowote suala linapotokezea ambapo hakuna maamuzi maalum kwenye vyanzo vya maandiko. Lakini bado, juu ya sehemu hizi za makubaliano, mgogoro na mvutano baina ya makundi haya ulibaki kuwa mkali.



[1] Kwa vile kila dhehebu lilipigana kumzidi mwengine, na kupata wartadi kutoka katika Uislamu, waliamua kuziharibu maana za maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyowekwa kumbukumbu kwenye Hadiyth, na kuzizalisha na kuzinasibisha kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), maneno na maana zilizotengenezwa kunufaisha malengo yao wenyewe.

 

 

 

Share

18-Uswuul Al-Fiqhi: Sura Ya Nne - Al-Imaam Ash-Shaafi'iy

 

SURA YA NNE

 

AL-IMAAM ASH-SHAAFI’IY

Al-Imaam ash-Shaafi’y alizaliwa mwaka 150 H, mwaka ambao Imaam Abuu Haniyfah alifariki. Alijifunza Fiqhi, kwanza Makkah pamoja na baadhi ya wanazuoni wa Ahl al-Hadiyth, kama vile Muslim bin Khaalid al-Zinji (amefariki mwaka 179) na Sufyaan bin ‘Uyaynah (amefariki mwaka 198). Baadaye alikwenda kwa Imaam wa Madiynah na kiongozi wa Ahl al-Hadiyth, Maalik bin Anas, na kujifunza pamoja naye, na alijifunza kuhifadhi (ili baadaye kulinganisha) mkusanyo wake pamoja na Hadiyth na mawazo ya kisheria, hiyo ni Muwattwaa. Hakika, al-Imaam ash-Shaafi’iy maisha yote alijiona yeye mwenyewe kuwa ana deni kwa Imaam Maalik.

 

Imesimuliwa kwamba Yuunus bin ‘Abd al-A’mla alimsikia Imaam ash-Shaafi’iy akisema: “Wakati wowote wanapotajwa ‘Ulamaa (kazi na elimu zao kulinganishwa). Maalik aliwamurika wote hao. Hakuna yeyote aliyenifanyia ihsani kubwa kuliko Maalik bin Anas”.[1] Hivi ndivyo alivyosema Imaam ash-Shaafi’iy baada ya kujifunza lugha, mashairi, fasihi, baadhi ya sayansi ya asili na sayansi ya hesabu na historia.

 

Al-Imaam ash-Shaafiy hakuvutika kwa kila kitu alichojifunza kutoka kwa katika kazi ya Ahl al-Hadiyth. Kwa mfano, aliwakosoa kwa kukubali Hadiyth ambayo ni Munqati’[2] akisema: “Hiyo Munqati’ si chochote.”

 

Al-Imaam ash-Shaafi’iy pia hakukubaliana na aina ya Hadiyth ya Mursal, [3](ingawa yeye mwenyewe alitumia kwa dharura Hadiyth Mursal kwa kesi ya iliyosimuliwa na Sai’iyd bin al-Musayyab), na kuamuru juu yake masharti makali kwa kukubaliana na wasimulizi kama wenye kutegemewa (na ikiwa Hadiyth walioisimulia kuwa ni sahihi).

 

Pale Imaam ash-Shaafi’iy alipokwenda Iraq, alitambua kutoka ngome kali ya Ahl ar-Ra-aykwamba; walikuwa tayari zaidi kutafuta kosa kwa taratibu za kisheria na mawazo ya watu wa Madiynah, hususan mwalimu wake al-Imaam Maalik. Hivyo, al-Imaam ash-Shaafi’iy alisimama kwa kumhami mwalimu wake, elimu yake ya fikra na utaratibu wake. Imesimuliwa kwamba aliwahi kusema:

 

Muhammad bin al-Hassan aliniambia: “Mwalimu wetu (yaani Abuu Haniyfah) alikuwa na ujuzi zaidi kuliko wako. Mwalimu wako alitakiwa kutozungumza, lakini mwalimu wetu angelikuwa ni mkosa kwa kubaki kimya.” Nilighadhibika na kumwambia: “Nakuuliza kwa jina la Allaah, ni nani alikuwa na ujuzi zaidi katika Sunnah ya Mtume; Maalik au Abuu Haniyfah?” Alisema: “Maalik. Lakini mwalimu wetu alikuwa mahiri zaidi kwenye Qiyaas. Nikamjibu, “Ndio, na Maalik alikuwa na ujuzi zaidi kuliko Abuu Haniyfah kuhusu Qur-aan, kuhusu utenguzi wake, na kuhusu Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Yeyote aliye mjuzi zaidi katika Qur-aan na Sunnah, anayo haki zaidi ya kuzungumza!”[4]

 

Al-Imaam ash-Shaafi’iy alijifunza vitabu vya Muhammad bin al-Hassan na wanazuoni wengine wa Iraq.[5]Hakika, alikuja kuwa mwanafunzi wa Muhammad bin al-Hassan, na kujadiliana naye mawazo yake, wakati wote huo akikubali Sunnah na Ahl al-Hadiyth.

 

Al-Imaam ash-Shaafi’iy aliondoka Baghdaad kwa kipindi fulani, na aliporejea; mwaka 195 H, kulikuwa na darsa za duara arobaini au hamsini ambazo zilikutana kwa kawaida msikiti mtukufu. Al-Imaam ash-Shaafi’iy alianza kuhama kuanzia darsa moja ya duara kwenda nyengine, akielezea nini “Allaah na Mtume wakisema”, wakati walimu wengine walizungumza yale tu ambayo walimu wao walisema. Hatimaye, kukawa hakuna darsa ya kujifunza ndani ya msikiti isipokuwa kwa darsa ya kujifunza kwa Imaam ash-Shaafi’iy.

 

Baadhi ya wanazuoni wakubwa wa Ahl ar-Ra-ay kama Abuu Thawr, az-Za’farani’, al-Karaabiisi na wengine (ni miongoni mwa) waliohudhuria darsa za duara ya al-Imaam ash-Shaafi’iy. Wengi walitupilia mbali utaratibu wa Ahl ar-Ra-ayna kuanza kumfuata al-Imaam ash-Shaafi’iy. Al-Imaam Ahmad bin Hanbal pia alihudhuria darsa hii, na inasimuliwa kwamba alisema: “Msimuliaji yeyote ambaye amebeba kijidau cha wino, amefaidika kwa njia yoyote kutoka kwa al-Imaam ash-Shaafi’iy.” Pale al-Imaam Ahmad alipoulizwa kuelezea, alisema: “Hao Ahl ar-Ra-ay walikuwa wakiwacheka Ahl al-Hadiyth hadi pale al-Imaam ash-Shaafi’iy alipowafundisha vyenginevyo, na akathibitisha nafasi ya watu wa Hadiyth kwa hoja zilizo wazi.[6]

 

Juu ya hivyo, ilikuwa ni kujibu maombi ya Ahl al-Hadiyth, kwamba al-Imaam ash-Shaafi’iy aliandika kitabu chake, al-Hujjah (Mjadala) nchini Baghdaad. Kwa lengo la kufuta hoja ambazo Ahl ar-Ra-ay walizozileta dhidi yake.[7]

 

Baada ya hayo, al-Imaam ash-Shaafi’iy alitembelea Misri ambapo alikuta kwamba, watu walio wengi walijifunza somo na bila ya kuulizia kwa maoni ya Maalik. Kutokana na hayo, al-Imaam ash-Shaafi’iy alianza uchunguzi wa kina wa maoni ya kisheria ya Maalik, na kuona kwamba kwenye baadhi ya kesi “…yeye (Maalik) anatengeneza mawazo kwa kuegemea kanuni ya jumla (‘Aam), wakati akiacha masuala mahsusi (Khaasw); ilhali katika nyakati nyengine anatoa maamuzi kwenye suala mahsusi na akiacha kanuni ya jumla.”

 

Al-Imaam ash-Shaafi’iy pia aliona kwamba mara nyengine Maalik alikataa Hadiyth ya maana kwa kuegemeza tamko lililofanywa na mmoja wa Swahaabah au Taabi’uun, au kwa hoja yake mwenyewe iliyo bora. Mara nyengine, al-Imaam ash-Shaafi’iy aligundua kwamba; Maalik alikataa tamko la mmoja wa Swahaabah kwa kupendelea maoni ya Taabi’i, au mawazo yake binafsi; na kwamba angelifanya hivi kwenye kesi moja moja, na akirudia maelezo ya sheria yasiyojulikana ukweli wake. Bila ya kuangalia kanuni za jumla. Juu ya hivyo, Maalik alidai kwenye kesi nyingi kwamba kulikuwepo na Ijma’a kuhusiana na jambo hilo, pale panapotokezea, hasa, kutokubaliana kuhusiana nayo.

 

Al-Imaam ahs-Shaafi’iy pia alitambua mawazo ya Maalik; kuhusu Ijma’a ya watu wa Madiynah kwamba inaweza kutumika kama ni chanzo cha ushahidi, ilikuwa, ukweli hasa, sio yenye nguvu. Aliandika kitabu kwa jina la Al-Ikhtilaaf Ma’a Maalik ‘Kutokubaliana pamoja na Maalik’, ambamo alijadili mambo yote yaliyotajwa hapo juu.[8]

 

Kwa mujibu wa al-Imaam ash-Shaafi’iy, al-Imaam Maalik alipindukia mipaka iliyowekwa kwenye kutumia kanuni zake za al-Maswaalih al-Mursalah (uchaguzi wa iliyo bora zaidi), bila ya kuhitaji msaada wa kukuwepo taabu ya kutafuta chanzo cha ushahidi. Mawazo yake kwa mnasaba wa Abuu Haniyfah yalikuwa kwamba; kwenye kadhia nyingi alitilia mkazo jambo moja moja, katika masuala madogo na maelezo, bila ya kuangalia kanuni za msingi na masharti.[9]

 

Kwa kuyaweka akilini masuala haya, baadaye al-Imaam ash-Shaafi’iy alifikia hitimisho kwamba linalostahiki kuangaliwa zaidi ni mkusanyo wa masharti ya utungaji sheria, usimamizi wa kanuni za msingi kuhusu matumizi yake, na maendeleo ya utaratibu wa vyanzo kwa njia ambayo masuala ya Fiqh yanaweza kuamuliwa kupitia msaada wa usahihi na aina mnasaba za ushahidi. Hivyo, Fiqh inaweza kuwa ni matumizi ya vitendo kwa utaratibu huu, ili kwamba Fiqh iliyo mpya kuwezekana kuibuka kama ni mbadala wa fikra mbili zilizoanzishwa za mawazo ya kisheria.

 

Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba al-Imaam ash-Shaafi’iy alitunga ar-Risaalah, na kujenga Fiqh yake na mafunzo ya kisheria kwenye msingi wa masharti na utaratibu aliouelezea kwa kina ndani ya kitabu chake.

 

Al-Imaam Ahmad bin Hanbal alisema: “Hadi pale al-Imaam ash-Shaafi’iy alipokuja, hatukupata kuwaza vitu kama vya jumla na mahsusi al-‘Umuum wa al-Khuswuus[10]

 

Al-Imaam ash-Shaafi’iy alikuwa akisema kwa Imaam Ahmad: “Wewe una ujuzi zaidi kuhusu Hadiyth na wasimulizi kuliko mimi. Hivyo, kama Hadiyth ni sahihi, basi niambie. Kama ni sahihi, mimi nitaikubali hata kama (imesimuliwa na wasimulizi) kutoka Kuufah, Baswrah au Damascus.”[11] Tamko hili linaonesha wazi kwamba al-Imaam ash-Shaafi’iy alitilia mkazo zaidi kwa kuanzisha masharti kuliko kujihusisha na masuala madogo na maelezo.

 

Wanazuoni wanaoandika kwenye somo la historia ya Uswuulul al-Fiqh wote kwa pamoja wamekubaliana kwamba mwandishi wa kwanza kwenye somo hilo alikuwa ni al-Imaam ash-Shaafi’iy, na kwamba kitabu cha mwanzo kilichowahi kuandikwa kwenye somo hilo kilikuwa ni ar-Risaalah.[12]

 

Ndani ya kitabu chake, al-Bahr al-Muhiytw, az-Zarkashi (alifariki mwaka 794 H) ametenga sura kwa hili, ambamo amesema:

 

“Al-Imaam ash-Shaafi’iy alikuwa ni wa mwanzo kuandika kitabu kuhusu Uswuulul al-Fiqh. Ameandika ar-Risaalah, Ahkaam al-Qur-aan (Tafsiri ya Kisheria za Qur-aan), Ikhtilaaf al-Hadiyth (Mgongano wa Hadiyth), Ibtilaal al-Istihsaan (Kutofaa kwa Msaada wa Wanazuoni), Jima’a al-’Ilm (Ulinganifu wa ujuzi), na al-Qiyaas (Hoja kwa Kufananisha) – Kitabu ambacho amejadili makosa ya kundi la Mu’tazillah, na alibadili fikra zake kuhusu kukubali tamko lao. Baadaye, wanazuoni wengine walimuiga katika kuandika vitabu vya al-Uswuul.”

 

Katika kuisifu ar-Risaalah, al-Juwayni ameandika:-

 

“Hakuna yeyote kabla ya al-Imaam ash-Shaafi’iy aliyeandika vitabu kwenye somo la al-Uswuul, au aliyekuwa na ujuzi zaidi kama wake kuhusiana nayo. Imesimuliwa kwamba Ibn ‘Abbaas alitamka kitu kuhusu kuweka vitu vilivyo jumla kwa kuchambua kimoja kimoja, na kwamba baadhi ya wengine miongoni mwa wanazuoni wa mwanzo walitamka maneno yaliyoonesha kwamba walifahamu masharti haya. Lakini bado, wale waliokuja baada yao hawakusema chochote kuhusu al-Uswuul, na hawakuchangia chochote katika hilo. Tumeona vitabu vya Taabi’un na vya kizazi cha tatu, na tumeona kwamba hamna yeyote kati yao aliyeandika vitabu kuhusu al-Uswuul.”[13]

 



[1] Ibn ‘Abdul-Barr, Al-Intiqa’, uk. 23.

[2] Inaitwa Munqati’ kwa sababu ni Hadiyth iliyokatika sehemu yoyote ndani ya mnyororo wa wasimulizi. Kwani hata hivyo, haitohitaji kuthibitishwa kwa kudhani kwamba Hadiyth hiyo imepitishwa kutokea kizazi cha kale, na wala sio kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Hadiyth kama hiyo ilikataliwa na Fuqahaa wote waliofuatia.

[3] Ufafanuzi kuhusiana na Hadiyth Mursal, na mzozo unaoizunguka, umetolewa ndani ya Surah ya tatu. Angalia ‘rejeo chini ya ukurasa’ nambari 36.

[4] Ibn ‘Abdul-Barr, Al-Intiqa’, uk. 24.

[5] Ni vyema itajwe hapa kwamba Muhammad bin Hassan pia alijifunza chini ya al-Imaam Maalik, na kwamba toleo lake la Muwattwaa ya Maalik inatambulika na wengi kuwa iliyo sahihi zaidi. Al-Imaam Muhammad ndani ya kitabu chake cha Kitaab ar-Radd ‘Alaa Ahl al-Madiynah ni yenye uwezo wa kushawishi matamshi juu ya tofauti zinazopatikana kwa kuziendea taratibu zilizotumiwa na fikra mbili za mawazo ya kisheria; Maalik na Hanafiy, na hasa kwa Ahl ar-Ra-ay na Ahl al-Hadiyth, kwa ujumla.

[6] Ibn ‘Abdul-Barr, Al-Intiqa’, uk. 86.

[7] Ibn ‘Abdul-Barr, Al-Intiqa’, uk. 86.

[8] Angalia Fakhr ar-Raazi, Manaaqib ash-Shaafi’iy, uk. 26

[9] Imaam al-Haramayn, ‘Abd al-Maalik Juwayni, Mughiyth al-Khalq.

[10] Az-Zarkashi, Al-Bahr al-Muhiytw, MS.

[11] Ibn ‘Abdul-Barr, Al-Intiqa’, uk. 25.

[12] Kumekuwa na uchache wa kutopatana kutokana na makubaliano kwenye suala hili. Achilia mbali, kutoka kwa wafuasi kadhaa wa fikra za mwanzo za mawazo ya sheria ambao wametoa ushahidi. Hata hivyo, lakini sio mwepesi kukubali madai yao juu ya wanazuoni kabla ya al-Imaam ash-Shaafi’iy, kama ilivyo kwa al-Imaam Abuu Yuusuf wa fikra za Hanafiy, kwamba waliandika kuhusu matawi haya muhimu ya sayansi ya Sharia’h.

[13] Angalia ‘Abd ar-Razzaaq, Tamhiyd li Taariykh al-Falsafah, Cairo, uk. 152.

Share

19-Uswuul Al-Fiqhi: Taratibu Za Imaam Ash-Shaafi'iy Kwenye Kitabu Chake 'Ar-Risaalah'

  

TARATIBU ZA IMAAM ASH-SHAAFI'IY KWENYE KITABU CHAKE: AR-RISAALAH

Al-Imaam ash-Shaafi’iy alianza kitabu chake kwa kutanabahisha hali ya binaadamu kabla tu ya ujumbe wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa kufanya hivyo, aliwagawa kwenye makundi mawili:-

 

 

  1. Ahl al-Kitaab “Watu wa Kitabu”; au, wafuasi wa uteremsho wa mwanzo ambao wamebadili maandiko yao na kuharibu pamoja na baadhi ya amri za kisheria. Kiuhalisia, watu hawa wameingia kwenye ukafiri na wengi wao baadaye kujaribu kuchanganya na Ukweli Aliouteremsha Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).

  2. Washirikina na Makafiri walioabudia masanamu badala ya Allaah.

 

Baadaye al-Imaam ash-Shaafi’iy alisema kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Amewaokoa wanaadamu wote kwa kumleta wa Mwisho katika Mitume, na kumshushia Kitabu Chake, ili kwamba huenda wakapokea kupitia kwake, njia ya kuondokana na upofu wa ukafiri kwenda nuru ya uongofu:

 

{{Kwa hakika wale wanaoyakanusha mawaidha yanapowajia (Tutawaadhibu). Bila shaka hicho ni Kitabu kihishimiwacho.

 

Haitofikia batili (Kitabu hichi) toka mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye hikima, Ahimidiwaye}} [41:41-42]

 

Baadaye al-Imaam ash-Shaafi’iy aliendelea kujadili kwa undani hadhi ya

Qur-aan ndani ya Uislamu na matamko yake mengi kuhusu nini Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ameruhusu na kuzuia, vipi mwanaadamu amuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), malipo ya wale wenye kumtii Yeye; adhabu kwa wale Wanaomtii Yeye na namna Alivyowaangamiza kwa kuwapa habari za waliotangulia.

 

Baadaye, al-Imaam ash-Shaafi’iy alieleza kwamba wanafunzi wanaotafuta elimu ya Kiislamu wajifunze mengi ndani ya Qur-aan na sayansi zake, kadri watakavyoweza; na kwamba pale nia zao zitakapokuwa safi, kwa pamoja wanaweza kunukuu aya zake na kufahamu maana yake kutokana nazo.

 

Mwisho wa utangulizi wake wa ar-Risaalah, al-Imaam ash-Shaafi’iy alisema: “Hakuna tatizo litakalomshambulia miongoni mwa wafuasi wa Dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) isipokuwa kwamba kutakuwa na muongozo ndani ya Kitabu cha Allaah kuonesha njia sahihi. Kwani, Allaah, Mtukufu Aliye Bora, Amesema:

 

{{Kitabu Tulichokiteremsha kwako ili uwatoe watu katika giza uwapeleke katika nuru, kwa idhini ya Mola wao, uwafikirishe katika njia ya yule Mwenye kushinda (na) Mwenye kusifika (Naye ni Mwenyezi Mungu)}} [14:1]

 

Na pia Amesema:

 

{{(Tuliwaleta) Kwa Ishara zilizo wazi na kwa Vitabu. Na Tumekuteremshia mauidha ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao, na ili wapate kufikiri}} [16:44]

 

Na pia Amesema:

 

{{Kwa hakika Mwenyezi Mungu Anaamrisha uadilifu, na kufanya ihsani, na kuwapa jamaa (na wengineo); na Anakataza uchafu na uovu, na dhulma. Anakunasihini ili mupate kufahamu (mfuate).}} [16:90]

 

Na:

 

{{Na namna hivi Tumekufunulia Wahyi kwa amri Yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini wala imani; lakini Tumefanya Kitabu hiki (Qur-aan) ni nuru, ambayo kwa (nuru) hiyo Tunamwongoza Tumtakaye katika waja Wetu. Na kwa yakini wewe unaongoza katika njia iliyonyooka.}} [42:52]

 

Baadaye inafuatia Sura kuhusu al-Bayaan[53] ambapo neno hili linatafsiriwa kama ni neno la kisheria, na baadaye likagaiwa kwenye mafungu, kwenye kueleza katika njia ambazo uteremsho wa Qur-aan linamaanisha masuala yenye mnasaba wa kisheria. Mafungu hayo yapo matano:

 

1)     Yale ambayo Allaah Ametolea maamuzi kama ni kifungu cha sheria mahsusi kisichohitaji maana nyengine zaidi ya tafsiri yake halisi (literal). Fungu hili la al-Bayaan halihitaji ufafanuzi mwengine zaidi ya Qur-aan wenyewe.

2)     Yale ambayo inayataja Qur-aan ambayo yanaweza kutolewa maana katika njia tofauti, na yale ambayo Sunnah imetoa maelezo ya kuweka wazi, ipi iliyokusudiwa.

3)     Yale ambayo yameelezwa bayana kuwa yana ulazima, na yale Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ameeleza kwa matamshi ya vipi, kwanini, ni juu ya nani, na wapi kutumika na wapi kutotumika.

4)     Yale ambayo yameelezwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), lakini hayakutajwa ndani ya Qur-aan. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ameamrisha ndani ya Qur-aan kwamba atiiwe Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na amri zake zikubaliwe. Hivyo yanayotamkwa kutoka mamlaka ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), yanatambulika kuwa ni mamlaka ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).

5)     Yale ambayo yanahitaji viumbe Wake kutafuta kupitia Ijtihaad. Hii ni Qiyaas. Kwa mujibu wa al-Imaam ash-Shaafi’iy, Qiyaas ni utaratibu wa kufikia ufumbuzi wa kisheria kwa msingi wa ushahidi (hukumu zilizowahi kutolewa kabla na kukubaliwa) ambapo hutumika hoja maarufu au sababu inayofaa.

 

Al-Imaam ash-Shaafi’iy kisha aliendelea kuelezea mafungu haya matano kwenye sura tano tofauti, akitoa mifano na ushahidi wa kila moja. Hivyo, ar-Risaalah hiyo ilikuwa na sura zifuatazo:-

 

  • Aya za Jumla zilizoteremshwa ndani ya Qur-aan zinakusudiwa kuwa na mambo ya ujumla ‘Aam, lakini yamo pia Mahsusi Khaasw.

  • Aya za Jumla zilizo Wazi za Qur-aan ambazo zinaonesha kuwa ni Jumla lakini zinadhamiriwa kuwa Mahsusi moja kwa moja.

  • Fungu la al-Bayaan ndani ya Qur-aan kwa utaratibu ambao maana inadhihirishwa kwa kutumia maneno au aya nyengine.

  • Fungu la al-Bayaan ndani ya Qur-aan kwa utaratibu wa maneno, ambao unaonesha zaidi maana iliyofichikana al-Baatwin kuliko maana iliyo wazi adh-Dhwaahir.

  • Yale, ambayo Qur-aan yaliteremshwa kama ni Jumla lakini Sunnah ikatanabahisha kuwa yana maana Mahsusi.

 

Katika Sura iliyotajwa hapo juu, al-Imaam ash-Shaafi’iy alieleza uhalali wa Sunnah kama ni ushahidi na hadhi yake ndani ya dini. Kwa sababu hii, baadaye alihitimisha sura zifuatazo:-

 

  • Wajibu uliowekwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ndani ya Qur-aan kufuata Sunnah ya Mtume Wake.

  • Amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Akiamrisha utiifu kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), yote yanajumuisha kuwa ni utiifu Kwake na amri zilizotolewa zenye kujitegemea.

  • Masuala ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ameamrisha utiifu kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

  • Namna Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) Alivyoweka wazi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amelazimika kufuata yale yaliyoteremshwa kwake na kutii chochote atakachoamrishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), na kwamba Allaah Atamuongoza yeyote anayemfuata Yeye.

 

Ndani ya Sura hii, al-Imaam ash-Shaafi’iy amethibitisha kwamba sehemu ya Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zimejadiliwa na kuhusishwa na Qur-aan, wakati sehemu nyengine zimeeleza masuala yaliyohusika, ambayo hakuna maandiko yanayonasibiana nayo ndani ya Kitabu. Al-Imaam ash-Shaafi’iy pia ameonesha kwamba Sunnah ipo huru na Qur-aan, na kunukuu ushahidi ili kuwakosoa wale ambao hawakubaliani naye kwenye suala hilo. Kisha akasema: “Nitafafanua yale ambayo nimekwisha yaeleza kuhusu Sunnah, (kama) ni sehemu ya Qur-aan au sheria nyengine kwa mambo ambayo hayakubainishwa humu, pia hili litapambanua yale niliyojadili hapo juu, Allaah Akipenda. Kwanza, nitazungumzia Sunnah kwa mujibu wa Kitabu cha Allaah, kwa kutumia, njia ya kurasa za Qur-aan zenye kutengua al-Naasikh na kutenguliwa al-Mansuukh. Baada ya hapo, nitabainisha Fardh-wajibu (ndani ya Qur-aan) na kwa mnasaba wake Sunnah; Fardh-wajibu zilizotolewa kwa maneno ya Jumla ambayo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amefanya Mahsusi kupitia kwake kufafanua maelezo kuhusiana na vipi na wapi; maandiko ya Jumla ambayo yalikusudiwa kueleweka kama ni Jumla, na maandiko ya Jumla ambayo yalikusudiwa kueleweka kama ni Mahsusi, na mwisho; Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo hakuna maandiko ya juu kutoka Kitabu cha Allaah.”

 

Baadaye inafuata sura iliyoitwa, “Asili ya Kutengua na Kutenguliwa”; ambayo inaeleza kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ametumia utenguzi kuifanya (Shariah) nyepesi na yenye kubadilika zaidi. Sura hii pia inabainisha kwamba aya ya Qur-aan inaweza tu kutenguliwa kwa aya nyengine ya Qur-aan; na kwamba Sunnah inaweza tu kutenguliwa kwa Sunnah nyengine.

 

Kisha akajadili kwa pamoja; kutengua na kutenguliwa. Ambazo zinabainishwa ndani ya sehemu ya Qur-aan, na ndani ya sehemu ya Sunnah.

 

Baada ya hapo inabainishwa kuhusu Fardh-wajibu wa Swalaah na maelezo ndani ya Qur-aan na Sunnah kuhusiana na wale ambao wanaweza kuwa na udhuru wa kutoiswali, na wale ambao Swalaah haikubaliki kwa sababu ya kitendo kiovu ambacho huenda wamekitenda.

 

Kisha, al-Imaam ash-Shaafi’iy ameandika Kutengua na Kutenguliwa ambazo zinatajwa ndani ya Sunnah na al-Ijmaa’,

 

  • Zile za Fardh-wajibu ambazo Allaah Ameziweka ndani ya maandiko ya Qur-aan.

  • Zile za Fardh-wajibu zilizowekwa ndani ya maandiko ya Qur-aan ambapo pia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amezijadili ndani ya Sunnah.

  • Zile Fardh-wajibu zilizowekwa ndani ya maandiko ya Qur-aan ambapo Sunnah imebainishwa kuwa zilikusudiwa kutumika Mahsusi.

  • Zile Fardh-Wajibu kwa jumla zilizo wazi na kukusudiwa kuwa ni lazima, na ambapo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametoa maelezo ya namna ya kuzitekeleza, mfano Swalaah, Hajj, Zakaah, idadi ya wake, mwanamke ambaye haruhusiki kuolewa, na kizuizi cha mlo wa siku (dietary).

 

Kwenye sura inayofuata, amejadili kuhusu dosari ndani ya Hadiyth, na kueleza kwamba mgongano baina ya Hadiyth unaweza kutokea kwa sababu zilizo nyingi. Ameendelea kueleza baadhi ya sababu hizi. Kwa mfano, mgongano unaweza kutokea kwa sababu Hadiyth moja imetenguliwa na nyengine, au kwa sababu ya makosa yaliyotokea ndani ya upokezi wa Hadiyth hiyo. Ameelezea makosa ambayo huenda yamesababisha migongano ndani ya Hadiyth, na sababu nyenginezo nyingi zilizopelekea migongano kama hiyo. Kisha amezungumzia aina tofauti za uzuiaji, na kueleza kwamba baadhi ya Hadiyth zinabainisha nyengine.

 

Al-Imaam ash-Shaafi’iy pia ameweka sura kuhusu elimu, na kueleza kwamba kuna aina mbili za elimu. Ya kwanza; ni aina ya elimu maarufu ambayo hakuna uwezekano wa kutoifahamu kwa mtu mzima na mwenye akili timamu. Elimu yote ya aina hii inawezekana kupatikana na kutajwa ndani ya maandiko ya Qur-aan, na kila Muislamu anaelewa yote hayo kwa sababu imeteremshwa kwake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kila kizazi kilchotangulia. Hakuna (mjadala) kuhusiana na usahihi wa elimu hii, na wote wanakubali kwamba ni lazima. Hakika, asili ya elimu hii ni kwamba, hakuna uwezekanao wa kuwepo makosa katika kufika kwake au kutafsiri.

 

Aina ya pili ya elimu ni ya maelezo yanayotokana na mzizi wa ulazima, na sheria mahsusi zinazotokana nazo. Hizi hazijatajwa ndani ya maandiko ya Qur-aan, na nyingi katika hizo hazitajwi ndani ya maandiko ya Sunnah achilia mbali kutokana na mapokezi ya mmoja-pekee, Ahad.

 

Hivyo, al-Imaam ash-Shaafi’iy ametoa utangulizi wa somo jipya, upokezi wa mmoja-pekee, Khabar al-Waahid. Al-Imaam ash-Shaafi’iy baadaye akaeleza nini kinachokusudiwa kwa neno hili, na masharti ambayo yataitambua kama ni upokezi au sio upokezi wa aina ya mmoja-pekee. Tofauti baina ya kiapo na habari, Shahaadah na Riwaayah, imeelezwa. Ama kwa masuala ambayo yanaweza kukubalika kupitia upokezi wa mmoja-pekee, na kwa zile ambazo Khabar al-Waahid haitoshi peke yake.

 

Baadaye, al-Imaam ash-Shaafi’iy amejadili hadhi ya Khabar al-Waahid, na kama habari hizo zinaweza kutumika kama ni ushahidi. Hitimisho lake, linakubalika kwa hoja zilizo nzuri na makini, ni kwamba; hakika zinaweza kutumika. Hivyo, al-Imaam ash-Shaafi’iy ametangulia katika kufuta mashaka yote yaliyokuzwa na wanaompinga kwenye suala hili.

 

Sura zifuatazo zinafuatia:-

 

  • Kuhusu al-Ijmaa’. Maana yake, na nafasi yake kisheria.

  • Kuhusu al-Qiyaas. Maana yake na asili, kuhitajia kwake, aina ya Qiyaas, na nani mwenye na asiye na uwezo wa kuitumia.

  • Kuhusu Ijtihaad: Kwanza namna ilivyoegemezwa kwenye Qur-aan, na baadaye kwenye Sunnah, (sura) inahusisha Ijtihaad sahihi na isiyo sahihi.

  • Kuhusu Istihsaan; Hiari ya Mwanachuoni: ash-Shaafi’iy alikuwa ni mwangalifu kueleza kwamba Muislamu yeyote haruhusiwi kuitumia al-Istihsaan kwa lengo la kuingilia/kukosoa Hadiyth, wala hakujaribu kutamka hukumu yeyote ya kisheria isiyoegemezwa kwenye Qur-aan, Sunnah, al-Ijmaa’ na al-Qiyaas. Pia alielezea tofauti baina ya al-Qiyaas na al-Istihsaan.

  • Kuhusu kutokubaliana miongoni mwa Wanazuoni: al-Imaam ash-Shaafi’iy ameeleza kwamba, kutokubaliana huku ni katika aina mbili; aina ambayo zinazuiwa na zile zisizozuiwa.

 

Aina ya kutokubaliana ambazo haziruhusiwi na zile kuhusiana na masuala ambayo Allaah Ametoa ushahidi ulio wazi ndani ya maandiko ya Qur-aan au Sunnah. Kutokubalina kwa aina ambazo zinaruhusiwa, inahusiana na masuala ambayo yanaweza kutafsiriwa kwa kutumia njia tofauti na zile ambazo kila mwanazuoni anatumia aina yake ya kutoa hoja. Al-Imaam ash-Shaafi’iy kisha akatoa mfano wa aina zote, ametoa mifano ya masuala ambayo Maswahaba hawakukubaliana, kama vile ‘Iddah, viapo na mirathi. Ndani ya sura hii, al-Imaam ash-Shaafi’iy ametaja kitu kuhusiana na utaratibu wa kutumika hiari kwa maoni ya Maswahaba pale wanapohitalifiana.

 

Ar-Risaalah inahitimishwa kwa ufafanuzi wa mawazo ya ash-Shaafi’iy kwenye “mafungu ya ushahidi” yaliyoelezwa hapo juu.

 

“Tunaegemeza hukumu zetu kimsingi kwenye Qur-aan na Sunnah iliyokubaliwa kuhusiana na yale ambayo hayana mgogoro, nasema: “Hii ndio hukumu yetu baada ya kusoma kwa pamoja maana zilizo wazi na zilizofichikana ndani ya maandiko.” Baadyae, kama inatubidi tunukuu kwenye Sunnah ambayo imesimuliwa na baadhi tu ya watu wachache na kuhusiana na ile ambayo hakuna makubaliano, tunasema: “Tunaikubali Hadiyth kama ilivyo, lakini tupo makini kwamba yawezekana kuwepo makosa yaliyofichikana ndani ya wasimuliaji.” Baadaye, tutanukuu kwenye al-Ijmaa’ kisha kwenye al-Qiyaas. Qiyaas ni dhaifu kuliko Ijmaa’ na inatumika pale tu inapohitajika, kwasababu sio halali kuitumia al-Qiyaas wakati kuna mapokezi kuhusiana na suala linalojadiliwa.”

 

Kutoka kwenye maandiko ya al-Imaam ash-Shaafi’iy, tunatambua vyanzo vya Maarifa ya Sheria za Kiislamu yalivyokubaliwa, na vile ambavyo vilisababisha kutokubaliana kwa wakati huo.

 

Vyanzo ambavyo vilikubaliwa vilikuwa ni: Kwa ujumla ni Qur-aan na Sunnah.

 

Vyanzo ambavyo vilihusiana na kutokubaliana vinajumuisha Sunnah yote kwa pamoja, na baadhi ya mapokezi Khabar al-Waahid (ambayo al-Imaam ash-Shaafi’iy ameitaja kama ni al-Khaaswah) mahsusi. Lakini mchango wa al-Imaam ash-Shaafi’iy ulikuwa kwamba, alichunguza masuala haya mawili kwa pamoja ndani ya ar-Risaalah na ndani ya Jima’ al-‘Ilm.

 

Masuala mengine ambayo yalihusiana na kutokubaliana yalikuwa ni:-

 

1.     Al-Ijmaa’: Kulikuwepo kutokubaliana kuhusiana na uhalali wa matumizi yake kama ni ushahidi kuhusiana na aina tofauti za al-Ijmaa’. Ijmaa’ ya nani ikubalike kama ushahidi, masuala ambayo al-Ijmaa’ inaweza kutambulika kama ni ushahidi; na namna jamii inavyoweza kutanabahishwa kwamba kuna Ijmaa’ kwenye suala mahsusi.

2.     Al-Qiyaas na al-Istihsaan: Kulikuwa na mgogoro kuhusiana na maana ya tafsiri hizo, asili yake, uhalali wa matumizi yake kama ni sheria, uwezekano na utaratibu wa kuzitumia, na ama vitendo vya Maswahaba vinaweza kutambulika kama ni Qiyaas au Istihsaan.

3.     Pia kulikuwa na kutokubaliana kulikokuwa bayana kuhusiana na uhalisi wa amri za Qur-aan na uzuiaji, maana zake na athari zake kwenye kanuni nyengine, hukumu za Fiqh. Tunaweza kutambua kwamba katika kipindi hichi, Maimamu Wanne wa Sunni hawakutumia maana ya maneno yaliyojifunga kama vile Tahriym “uzuiaji”, al-Ijaab “uwajibu”, n.k. Kwani maneno haya hayakutumika kwenye misamiati yao. Isipokuwa aina hii ya maneno ya kisheria yalijitokeza baadaye, kama Ibn Qayyim alivyoeleza.[54]

4.     Vyanzo vyengine vya Maarifa ya Sheria za Kiislamu ambavyo vina tofauti, (ilikuwa) ni mara chache kujadiliwa kwenye kipindi cha wanazuoni wa mwanzo. Kwa mfano, kama maneno ya al-‘Urf, al-‘Aadah na al-Istis-haab yalikuwa sio sehemu ya misamiati yao.

 

 



[53] Ndani ya utangulizi wa tafsiri ya ar-Risaalah, Profesa Maajid Khadduuri anajadili maana ya al-Bayaan, na kunukuu tafsiri zilizotolewa na wanazuoni wa kuheshimika. Profesa Khadduuri ameandika:-

 

“Wengine wanasema, ina maana tu ya uteremsho unaojumuisha vifungu vya kisheria: Wengine wanajadili kwamba sio tu ni uteremsho, lakini pia kuwaweka wazi. Ash-Shaafi’iy, hata hivyo, anaonekana kutilia mkazo maudhui ya kisheria ya vifungu kwa hoja za kwamba mawasiliano yote ya Qur-aan yapo wazi, ‘ingawa baadhi yake yapo kwa ukali kuliko mengine’ na kwa wale tu wasiojua lugha ya Kiarabu yanakuwa baadhi ya mawasiliano yanaonekana kuwa hayapo wazi kuliko mengine.”

 

Kiuhakika, neno al-Bayaan linatafsiriwa na Profesa Khadduuri kama “uteremsho ulio bayana”. Angalia, Khadduuri, Islamic Jurisprudence (Maarifa ya Sheria za Kiislamu), Iliyochapishwa na Johns Hopkins Press, uk. 32-33.

[54] Ibn Qayyim, I’laam al-Muwaqqiy’in, I, uk.32.

Share

20-Uswuul Al-Fiqhi Baada Ya Al-Imaam Ash-Shaafi’iy

Sura Ya Tano

 

Uswuul Al-Fiqhi Baada Ya Al-Imaam Ash-Shaafi’iy

 

Ar-Risaalah ya Al-Imaam ash-Shaafi’iy ilihodhi masomo ya Maarifa ya Sheria za Kiislamu pale tu ilipoanza kutoka. Hakika matokeo yake ni kwamba; wanazuoni walijigawa kwenye makundi mawili. Kundi la kwanza ambalo ni wengi wao ni Ahl al-Hadiyth, waliikubali, na waliitumia kwa kuitetea elimu ya Shaafi’iy katika Maarifa ya kisheria. Kundi jengine, ambalo hata hivyo, walikataa mengi yaliyokuwemo humo, na walijaribu kubadilisha chochote ambacho kazi ya al-Imaam ash-Shaafi’iy iligongana na taratibu zao na mwendo wao, kabla haijapata nafasi (ar-Risaalah) ya kuwashajiisha watu. Wajumbe wa kundi hili wengi wao hakika walitokana na Ahl ar-Rai’iy, ambao wote hao walikuwa hawakubaliani na chochote, takriban mambo yote aliyoandika al-Imaam ash-Shaafi’iy.

 

Ibn al-Nadiym ametaja vitabu ambavyo vimeandikwa kwenye somo la Uswuul al-Fiqh baada ya ar-Risaalah, vikiwemo an-Naasikh wa al-Mansuukh na as-Sunnah cha al-Imaam Ahmad bin Hanbal (Amefariki mwaka 233 H). As-Sunnah, hata hivyo, ni kitabu kilichojikita zaidi kwenye Tawhiyd na itikadi za msingi za Uislamu “’Aqaaid” kuliko maarifa ya Sheria za Kiislamu. Kuna matoleo mawili ya kazi hii katika kuchapishwa, toleo kubwa ni lile lililochapishwa Makkah mwaka 1349 H; ambalo lina nakala za kurasa huko Dar-al-Kutub na Maktaba ya Dhwaahiriyyah - Egypt na Damascus zilizo halisi. Toleo dogo iliyochapishwa Cairo bila ya tarehe, inahusiana na itikadi za msingi za imani halisi za Sunni (Sunni Orthodoxy), au “Ahl as-Sunnah”.

 

Al-Imaam Ahmad pia ameandika kitabu cha Twa’at ar-Rasuul “Utiifu kwa Mtume”. Ibn al-Qayyim amenukuu kutoka kitabu hicho ndani ya kitabu chake cha I’laam al-Muwaqqi’iyn, na inaonekana kwamba amehodhi nakala yake. Juu ya hivyo, nimekitafuta kitabu hichi sehemu nyingi, lakini nimeshindwa kukiona. Kutoka kurasa zilizonukuliwa za kitabu cha Ibn al-Qayyim, ni uwazi kwamba kitabu hicho hakika kilikuwa ni kitabu muhimu kwenye somo la Maarifa ya Sheria za Kiislamu, na utaratibu wa kushughulika na Sunnah. Inawezekana kuwa kimepotea baada ya wakati wa Ibn al-Qayyim, au kimetiwa jalada ndani ya kitabu chengine, au kurasa zake zimepotea hadi kuweza kupatikana baada ya kutafuta sana.

 

Vyanzo pia vimetaja kwamba Daawuud adh-Dhwaahiriy (Amefariki Mwaka 270 H.) ameandika kuhusu al-Ijmaa’ “Makubaliano” Ibtwaal at-Taqliyd “Katika Kuondosha Kunukuu Kusiko Halisi”, Khabar al-Waahid “Katika Usimuliaji wa mmoja-pekee”, al-Khuswuus wa al-‘Umuum “Katika Mahsusi na iliyo Jumla”, al-Mufassar wa al-Mujmal “Maneno Machache (lakini dhahiri) na ya Maelezo”, al-Kaafi fiy Muqabbalaat al-Muttalibi, yaani al-Imaam ash-Shaafi’iy, “Katika kushindana na ash-Shaafi’iy”, Mas-alatun Khalafa Fihima ash-Shaafi’iy “Masuala Mawili Aliyotofautiana nayo pamoja na al-Imaam ash-Shaafi’iy”.

 

Wakati wa kipindi hichi “’Ulamaa” waliokubaliana na mafunzo ya fikra za al-Imaam Abuu Haniyfah walijitolea umakini wao katika kusoma ar-Risaalah ya ash-Shaafi’iy, vyote vyote; kwa lengo la kuziharibu yale wasiyokubaliana, na kutoa aina yao ya vyanzo-utaratibu na Misingi ya Maarifa ya Sheria za Kiislamu kutoka kwenye kesi za kisheria Fataawa ya al-Imaam Abuu Haniyfah.

 

Kwa dalili hizi, wanazuoni wa Hanafi walitoa vitabu (vingi) tofauti. ‘Iysa bin Abbaan (Amefariki Mwaka 220 H.) ameandika Khabar al-Waahid, Ithbaat al-Qiyaas, “Kuthibitisha Mfanano al-Qiyaas”, na Ijtihaad ar-Rai’, “Matumizi ya Hoja za Kisheria”.

 

Al-Barzai (Amefariki Mwaka 317 H.) ameandika Masaa’il al-Khilaaf “Masuala ya Kutokubaliana”, ambacho kina nakala za kurasa 236 ndani ya Maktaba ya Zaytuunah huko Tunisia, nambari 1619.

 

Abuu Ja’far at-Twahaawiy (Amefariki Mwaka 321 H.) ameandika Ikhtilaaf al-Fuqaaha “Kutokubaliana kwa Wanazuoni”, ambacho kilifanyiwa ufupisho na Abuu Bakr al-Jassaas (Amefariki Mwaka 370 H.). Kuna nakala ya kitabu huko Cairo. Kwa maelezo zaidi, rudia Fahrisi ya Ma’had al-Makhtuutat (1/329).[55]

 

Al-Karabiysi an-Najafi (Amefariki Mwaka 322) ameandika al-Faruuq “Tofauti”, ambacho kina nakala za kurasa za Ahmad III na Fayd Allaah, Maktaba ya Istanbul.

 

Baadhi ya kazi zisizo na majina kwenye Maarifa ya Sheria za Kiislamu pia zilihusishwa kwa Ibn Sama’ah (Amefariki Mwaka 233).[56]

 

Al-Kannani (Amefariki Mwaka 289) ameandika al-Hujjah fi ar-Radd Ala ash-Shaafi’iy, “Ushahidi wa Kutokubaliana na Imaam ash-Shaafi’iy”.

 

‘Aliy bin Muussa al-Qurumi, dhehebu la Hanafi (Amefariki mwaka 305) ameandika Maa Khalafa Fiyhi ash-Shaafi’iy al-‘Iraaqiyiin Fii Ahkaam al-Qur-aan” “Namna Ambazo ash-Shaafi’iy Alipingana na Wairaqi Kuhusu Tafsiri ya Kisheria ya Qur-aan”, Ithbaat al-Qiyaas, al-Ijtihaad na Khabar al-Waahid.

 

Abuu al-Hassan al-Karkhi (Amefariki Mwaka 340) ameandika kitabu chake maarufu cha al-Uswuul “Vyanzo”, ambacho kilichapishwa pamoja na majumuisho ya vitabu vyengine nchini Cairo (hamna tarehe).

 

Abuu Sahl al-Nawbakhtiy (Amefariki mnamo mwaka 93 H.) akitokana na Imaamiyyah, ameandika Naqd Risaalat ash-Shaafi’iy “Ukosoaji wa ar-Risaalah ya Shaafi’iy”, Ibtwaal al-Qiyaas “Kuzikataa al-Qiyaas”, na ar-Radd ‘Ala Ibn ar-Rawandi Fi Ba’d Ara’ihi al-Uswuuliyyah “Kuziharibu Baadhi ya Mawazo ya Kisheria ya Ibn ar-Rawandi”. Ibn Junayn (Amefariki Mwaka 347), anayetoka kundi la Zaydiyyah, ameandika al-Faskh ‘Alaa Man Ajaza al-Nasakh lima Tamma Shar’uhu wa Jalla Naf’uhu “Ubatilishaji wa Utenguzi ulioruhusiwa katika Sheria ambazo Zimekwishatenguliwa na Kuthibitishwa kuwa na Manufaa”, na al-Ifhaam li Uswuul al-Ahkaam “Kuelewa Misingi ya Maarifa ya Sheria za Kiislamu.”

 

Wafuasi waliobobea Mafunzo ya al-Imaam ash-Shaafi’iy kwenye fikra za kisheria walitoa kazi zifuatazo:-

 

  • Abuu Thawr (Amefariki mwaka 240) ameandika Ikhtilaaf al-Fuqaaha “Kutokubaliana kwa Wanazuoni”.

  • Abuu ‘Abd Allaah Muhammad bin Nasr al-Marwazi (Amefariki mwaka 294) pia ameandika kitabu katika somo hilo hilo.

  • Abuu Abbaas bin Surayj (Amefariki mwaka 305) ameandika kitabu akiwakataa wote wawili ‘Iysa bin Abbaan na Muhammad bin Daawuud adh-Dhwaahiriy kwenye masuala ambayo walipingana na al-Imaam ash-Shaafi’iy.

  • Ibraahiym bin Ahmad al-Marwazi (Amefariki mwaka 340) ameandika Al-Umuum wa al-Khuswuus “Jumla na Mahsusi” na Al-Fuswuul fi Ma’rifat al-Uswuul.[57] Sura kuhusiana na Elimu ya Chanzo-Utaratibu wa Kisheria.

 

Baadhi ya wanazuoni hawa, walijitolea fikra zao katika kutoa ufafanuzi wa ar-Risaalah ya ash-Shaafi’iy kama kwa Abuu Bakr as-Sayraafi (Amefariki mwaka 330). Abuu al-Waliyd an-Nisaburi (Amefariki mwaka 365 au 363), Abuu Bakr al-Jawzaqi (Amefariki mwaka 388) na Abuu Muhammad al-Juwayni, baba wa (anayejulikana na wengi) Imaam al-Haramayn, mwalimu kwa al-Imaam al-Ghazzaali.

 

Ufafanuzi kwenye ar-Risaalah pia umedhaniwa kuwa ni kazi ya wanazuoni wengine watano, kwa majina ni: Abuu Zayd al-Jazuuli, Yuusuf bin ‘Umar, Jamaal ad-Diyn al-Afqahsi, Ibn Fakiham na Abuu al-Qaassim ‘Iysa bin Naji. Hakuna kutokana na fafanuzi hizi, ambapo wanazuoni wamekuwa wakinukuu hadi baada ya karne ya saba, ndio wamepata nuru nyakati za leo.

 

Shaykh Mustwafa ‘Abdur-Razzaq,[58] ametaja kwamba maktaba ya wazi nchini Paris inashikilia nakala ya fafanuzi kutoka kwa al-Juwayni kuhusiana na ar-Risaalah, na kunukuu baadhi ya sehemu hizo. Mimi, mwenyewe, nimejaribu kuzipata kurasa hizi nchini Paris, lakini nimeshindwa. Labda, zimewekwa pamoja na vitabu vyengine chini ya mada au jina tofauti. Huenda, njia pekee ya kuipata ni kuitafuta kwenye kurasa zote tofauti. Kwamba, hata hivyo, hiyo ni kazi inayotisha, kwani mchunguzi atahitaji kutumia muda wake mkubwa mno katika kukifanya kibarua hichi.

 

 

MAENDELEO YA USWUUL AL FIQH
BAADA YA AL-IMAAM ASH-SHAAFI’IY

 

Yale tuliyoyataja hadi kufikia hapa yanaweza kutambulika kama ni maendelo. Kwani kimsingi ni mzunguko wa kukanusha, kukubali au kutoa maoni kuhusiana na ar-Risaalah na ukweli hauendelei mbali zaidi ya hapo. Pale tu taratibu zinaposimamishwa, basi taratibu hizi zilizopatikana hadi mnamo mwa mwanzo wa karne ya tano H, ndipo inaweza kutambulika kuwa ni maendeleo yalio muwafaka kuanza kuchukua hatamu kwenye uwanja huo.

 

Wakati wa kipindi hichi, al-Qaadhi al-Baqillaani (Amefariki mwaka 402 H.) na al-Qaadhi ‘Abdul-Jabbaar al-Hamadan (Amefariki mwaka 415 H.) ameibeba kazi ya kuandika upya somo lote la mafunzo na misingi ya Maarifa ya Sheria ya Kiislamu – Chanzo na Utaratibu, au al-Uswuul.

 

Ndani ya kitabu chake cha al-Bahr, az-Zarkhasi ameandika “…majaji wawili, Qaadhi wa Ahl as-Sunnah, Abuu Bakr Twayyib al-Baqillani, na Qaadhi wa Mu’tazilah, ‘Abdul-Jabbaar, alikuja na kupanua kuhusiana na yale yaliyoandikwa, kutolea maelezo kwa yaliyokuwa huko kale ni kidogo kuliko na yanayoonekana, akatoa maelezo kwa yale yaliyotajwa kwa njia ya jumla, na kuondosha utata.”

 

Al-Qaadhi al-Baqillani alitunikiwa cheo cha Shaykh al-Uswuuliyyiin[59] “Shahada ya Pili ya Wanazuoni wa al-Uswuul”, baada ya kuandika at-Taqriyb wa al-Irshaad “Ubainifu na Muongozo”. Kitabu hicho kimepotea kwa karne (zaidi ya moja), ingawa inawezekana kikatokea kwenye maandiko ya mjumuisho mmoja au mwengine. Katika kesi yeyote, wanazuoni wa al-Uswuul waliendelea kunukuu ndani (ya hicho kitabu) hadi karne ya tisa AH.

 

Kwa sehemu yake, al-Qaadhi ‘Abdul-Jabbaar ameandika kitabu chenye jina la ama al-’Ahd “Maagano” au al-‘Amad “Nguzo” na kuandika ufafanuzi wake kuhusiana na hicho kitabu.

 

Imaam al-Haramayn (Amefariki mwaka 478 H) amefupisha kitabu cha al-Baqillaani cha at-Taqriyb wa al-Irshaad, ndani ya kitabu chenye jina la at-Talkhiys “Iliyofupishwa” au al-Mulakhkhas “Ufupisho”, ambacho baadhi ya kurasa zake zimehifadhiwa ndani ya mjumuisho wa baadhi ya maandiko. Baadaye, wanazuoni wa Maarifa ya Sheria za Kiislamu walitumia fikra nyingi za al-Baqillaani kutoka kwenye kitabu chake.

 

Imaam al-Haramayn alitoa kelelezo cha kazi yake kwenye al-Uswuul, al-Burhaan “Ushahidi”, kwenye kitabu cha al-Baqillaani cha at-Taqriib, ambapo humo imejumuisha matawi ya Uswuul, kilikuwa kipo huru na taratibu zake, na kikafuata ushahidi wowote uliopatikana.[60] Imaam al-Haramayn hakukubaliana na walimu wake (yaani al-Imaam al-Ash’ari na al-Imaam ash-Shaafi’iy) katika makala nyingi. Na kwamba wengi wa wanazuoni wake wa karibu kutoka kwenye mafunzo ya fikra za kisheria za ash-Shaafi’iy, walikataa ufafanuzi wake na wala hawakuitambua namna ilivyohitaji, ingawa sehemu kubwa wamekitumia ndani ya vitabu vyao.

 

Wanazuoni wawili wa Maliki, al-Imaam Abuu ‘Abdillaah al-Maziri (Amefariki mwaka 536 H.) na Abuu al-Hassan al-Abyari (Amefariki mwaka 616 H.) waliandika ufafanuzi kwenye al-Burhaan, na mwanazuoni wa tatu wa ki-Maliki, Abuu Yahya, ameunganisha fafanuzi mbili hizo lakini bado, wanazuoni wote hawa watatu walichambua kwa pupa, kama sio kusikokuwa na haki, kwa Imaam al-Haramayn. Kwa sababu wa yale waliyoyatambua kuwa ni ujasiri katika kumkana al-Imaam al-Ash’ari kwenye mambo asiyokubaliana pamoja nao na katika kumkana al-Imaam Maliki kwenye suala la al-Maswaalih al-Mursalah. Imaam al-Haramayn aliongezea utangulizi kwa kitabu cha al-Imaam ash-Shaafi’iy ambacho kilizungumzia masuala yasiyopatikana ndani ya ar-Risaalah. Alianza kwa kujadili elimu ya vyanzo hivyo na dhana ambazo yeyote aliyependa kusoma sayansi yoyote kwa ndani, ni lazima asome. Alieleza kwamba vyanzo vya Uswuul al-Fiqh vilikuwa ni ‘Ilm al-Kalaam, lugha ya Kiarabu na Fiqh. Baadaye, alijadili kuhusu hukumu ya kisheria, wajibu na uwezo. Akijadili kwa undani, masuala yanayohusiana na sayansi tofauti, na kueleza yale ambayo yanaweza kueleweka kwa hoja. Na ambayo kwa dini, masuala yote hapo juu yanafanya utangulizi wa mjadala wa neno la al-Bayaan “Tamko lililo dhahiri”, mada ambayo al-Imaam ash-Shaafi’iy alianza nayo kwenye ar-Risaalah.

 

Hata hivyo, ni uwazi ulio dhahiri, pale tunapoona namna Imaam al-Haramayn alivyojadili mada ya al-Bayaan na kwa mada nyengine, ametaja ndani ya ar-Risaalah, kwamba al-Imaam al-Haramayn ametafsiri misamiati ya maneno; ikiwemo al-Bayaan kwa vizuri zaidi kuliko al-Imaam ash-Shaafi’iy alivyofanya. Alilitafsiri, akaelezea sifa zake, akataja kutokubaliana kuhusiana nayo, na akaweka mafungu yake tofauti. Pia alijadili jambo jengine ambalo al-Imaam ash-Shaafi’iy hakulijadili, Taakhiyr al-Bayaan ilaa Waqt al-Hajah “Kuiakhirisha al-Bayaan hadi muda utakaotakiwa”, na kuhusu kutokubaliana nayo. Baadaye katika kujadili mafungu tofauti ya al-Bayaan, alikariri kwa mara nyengine mafungu matano ambayo aliyataja al-Imaam ash-Shaafi’iy, akawakilisha maoni ya Abuu Bakr Daawuud adh-Dhwaahiriy kwenye mada hiyo, na baadaye akataja mafungu mengine ya al-Bayaan ambayo wanazuoni wengine walishauri.

 

Imaam al-Haramayn alishikilia ushauri wa kwamba al-Bayaan ina maana ya ‘ushahidi’, ambayo ina aina mbili: ‘Aqli “akili” na Sami’i “kupokea”. Msingi wa ushahidi wa “kupokea” ni Qur-aan iliyo na miujiza na kwamba; namna ukaribu wa ushahidi ulivyo kwa Qur-aan, ndivyo inavyotengeneza sheria/hukumu ya kufuatwa. Matokeo yake ni kwamba; mfuatano wa protokoli katika ushahidi wa “kupokea” ni: Qur-aan, Sunnah, al-Ijmaa’, Khabar al-Waahid na al-Qiyaas.

 

Baadaye alijadili kuhusu lugha, na kueleza kwamba, wanazuoni wa Maarifa ya Sheria za Kiislamu wamejadili kuhusu elimu ya lugha, kitu ambacho wanazuoni wa Kiarabu wamekiacha, kama vile Awaamir “Amri”; Nawaahi “Makatazo”, na al-‘Umuum wa al-Khuswuus “Jumla na Mahsusi” ambayo al-Imaam ash-Shaafi’iy amejadili.

 

Kwenye mjadala wa mada ya elimu ya lugha, ametaja baadhi ya mawazo ya al-Baqillaani ambayo yanaonesha wazi kwamba al-Baqillaani tayari amekwishaunganisha mambo haya, kwa taratibu za al-Imaam ash-Shaafi’iy.

 

Pale al-Imaam al-Ghazzaali alipokuwa mwanafunzi wa al-Haramayn, ilikuwa ni asili tu kwamba, amesukumwa na yeye. Ukweli ni kwamba, al-Imaam al-Ghazzaali ameandika vitabu vinne kwenye somo la al-Uswuul. Kazi ya mwanzo kati ya hizi ilikuwa al-Mankhuul “Mchakato”, toleo la ukubwa na wa wastani, iliyoandikwa kwa (ajili ya) wanaoanza na wanaonyanyukia kwenye kusoma al-Uswuul. Cha pili katika kitabu, hakuna kinachojulikana isipokuwa kwamba ilinukuliwa kwenye al-Mustwasfaa,[61]na kwamba mada yake ilikuwa Tahdhiyb al-Uswuul “Ustaarabu wa al-Uswuul”. Kitabu cha tatu kina jina la Shifa’ al-Ghaliyl fiy Bayaan ash-Shibh wa al-Mukhayyal wa Masaalik at-Taliyl, na kilifanyiwa uhariri na kuchapishwa nchini Baghdad mwaka 1390/1971. Mkusanyiko wake (encyclopedia) wa Shari’ah Chanzo-Utaratibu. Kitabu chake cha nne kwenye mada hiyo, na neno lake la mwisho, kilikuwa ni al-Mustwasfaa, ambacho kilichapishwa mara kadhaa nchini Misr na kwengineko. Hakika, hii ni kazi aliyoiandika baada ya kukaa mafichoni akifanya uchunguzi.[62]

 

Al-Imaam alianza kitabu chake kwa utangulizi ambapo aligusa takriban dhana zote za Aristotle, somo ambalo daima alikuwa akilipenda. Baadaye aliandika kuhusu ‘Hadd’ “Adhabu zilizotajwa”, kuhusu masharti ambayo ni lazima yatimizwe kabla ya kutendewa kazi, na kuhusu aina tofauti za Huduud. Baadaye alijadili kuhusu Daliyl “Ushahidi” na aina zake tofauti.

 

Kwa nukta hii ndani ya kitabu chake, al-Imaam al-Ghazzaali aliendelea kujadili pembe nne za kazi yake, mada ambazo zimekamata kila kitu ndani ya uwanja wa al-Uswuul, na ambazo mwalimu wake, Imaam al-Haramayn na waliomtangulia, kama vile al-Baqillaani, walijishughulisha nazo zaidi. Kwa vile mwalimu wake, alikuwa na maoni yake ambayo yalitofautiana na yale ya al-Imaam al-Ghazzaali alishikilia mawazo ambayo yapo tofauti. Kama ya waliomtangulia na kama ilivyo kawaida, wakati wa al-Imaam al-Ghazzaali kulikuwepo na wale waliokubaliana na mawazo yake na wale wasiokubaliana.

 

Haya ndio yalikuwa ni maendeleo muhimu yaliofanywa na wafuasi wa al-Imaam ash-Shaafi’iy ndani ya uwanja wa Uswuul.

 

Kundi la pili lililochangia kwenye maendeleo ya somo ni Mu’tazilah. Baada ya Qaadhi ‘Abdul-Jabbaar kuandika kitabu chake al-‘Amad au al-‘Ahd, na kuandika ufafanuzi wake uliokamilika kwenye kitabu hicho, alihifadhi baadhi ya mawazo ya al-Uswuul ndani ya mjumuiko wa kitabu kikuu (encyclopedia), baadhi ya sehemu zake ambazo zimepatikana na kuchapishwa chini ya mada ya al-Mughni “Maandiko” (volume) kumi na saba ya ‘encyclopedia’ hii yalitunukiwa kwenye masomo la al-Uswuul.

 

Kama alivyojihusisha Imaam al-Haramayn kwenye kitabu cha al-Baqillaani, ndivyo Abuu al-Husayn al-Basri al-Mu’tazili (Amefariki mwaka 435 H.) alivyojihusisha na vitabu vya al-Qaadhi ‘Abdul-Jabbaar, na kuandika ufafanuzi kwenye al-‘Amad/al-‘Ahd. Pale alipohisi kwamba ufafanuzi huu ulikuwa mkubwa, alikifupisha ndani ya kitabu chake maarufu cha al-Mu’tamad “Chenye Kutegemewa”, ambacho kimechapishwa na kinapatikana sehemu nyingi mno.

 

Wakati wa kipindi hichi, ash-Shaykh Abuu Ishaaq ash-Shiraazi (Amefariki mwaka 476 H.), ameandika vitabu vyake viwili al-Lam “Nuru yenye Kung’aa” na at-Tabswiyrah “Uwongofu”, vyote ambavyo vimechapishwa.

 

Al-Qaadhi Abuu Yahya al-Farra’ al-Hanbali ameandika kitabu kwenye Uswuul chenye jina la al-‘Uddah fi Uswuul al-Fiqhi “Zana za Uswuul al-Fiqhi”, ambacho kilifanyiwa uhariri na kuchapishwa nchini Saudi Arabia 1400/1980.

 

Ibn ‘Aqil al-Baghdadiy, ambaye ni mwanazuoni mwengine wa ki-Hanbali, ameandika al-Waadhwih Fiy al-Uswuul “Yaliyo Wazi Kwenye Uswuul”.

 

Abuu al-Khattaab ameandika kitabu chake maarufu, at-Tamhiyd “Dibaji”, ambayo ilifanyiwa uhariri hivi karibuni na kuchapishwa Makkah.

 

Miongoni mwa vitabu walivyoandika wanazuoni wa mafunzo ya mawazo ya kisheria ya Maliki kwa wakati huu ni ‘Uyuun al-Adillah Fiy Masaa’il al-Khilaaf Bayna Fuqaaha al-Amswaar “Wingi wa Ushahidi katika Masuala yenye Mgongano Miongoni mwa Wanazuoni wa Fiqh wa miji”, kilichoandikwa na Ibn al-Qasswaar al-Baghdaadiy (Amefariki mwaka 398 H.), ambacho kina nakala mpya huko Chuo Kikuu cha al-Qarawiyyiin nchini Fez.[63] Mwanazuoni ash-Shiraazi anakitaja kuwa ni kitabu bora kilichowahi kuandikwa miongoni mwa wanazuoni wa Maliki kwenye mada ya tofauti za wanazuoni. Ibn al-Qasswaar pia aliandika Muqaddimah fiy Uswuul al-Fiqh “Utangulizi kwa Uswuul al-Fiqh”, ambacho kina makala yake katika Maktaba ya Chuo Kikuu cha al-Azhar.

 

Vitabu vya Shaafi’yyah, Hanaabila, Maalikiyyah na Mu’tazilah, vyote vilifuata mtindo kama huu, katika mtiririko wa sura zao na ufumbuzi wa masuala yao muhimu. Hatimaye mtindo uliokuja kugundulikana kwa jina la “Taratibu za Mutakallimuun”.



[55] Toleo la sehemu ya ufupisho wa Jassas wa kitabu hichi ulichapishwa nchini Pakistan na Islamic Research Institute-Taasisi ya Uchunguzi wa Kiislamu-Mhariri wa toleo hiyo, hata hivyo amefanya makosa kuihusisha kazi hiyo moja kwa moja kwa Abuu Ja’far at-Twahaawiy.

[56] Angalia, Ibn al-Nadiym, Al-Fihrisi, uk. 284.

[57] Ibn al-Nadiym, Al-Fihrist, uk. 299.

[58] Angalia, ‘Abdur-Razzaaq, Tamhiyd li Taariykh al-Falsafah, Cairo.

[59] Angalia, al-Quraffi, Nafaa’ii, I, uk. 149.

[60] Toleo safi la Al-Burhaan limechapishwa hivi karibuni huko Qatar.

[61] Angalia al-Ghazzaali, al-Mustwasfaa, I, uk. 187. Tafsiri iliyo nzuri kabisa kwa lugha ya Kiingereza ya al-Mustwasfaa ya al-Ghazzaali ilifanywa na Dr. Ahmad Zaki Hammaad.

[62] Angalia rejeo chini ya ukurasa’ nambari 61.

[63] Angalia Brockermann, Hati, II, uk. 963, no. 49.

Share

21-Uswuul Al-Fiqhi: Majukumu Ya Wafuasi Wa Abuu Haniyfah Katika Uandishi Wa Al-Uswuul

 

MAJUKUMU YA WAFUASI WA ABUU HANIYFAH KATIKA UANDISHI WA AL-USWUUL.

 

Baadhi ya Wanahistoria wa Uswuul al-Fiqhi wametoa maoni kwamba al-Qaadhi Abuu Yuusuf na Muhammad bin al-Hassan wameandika kuhusu Maarifa ya Sheria za Kiislamu,[64]lakini dai hili halijathibitishwa.

 

Mwandishi wa Kashf adh-Dhwunuun[65] amenukuu ‘Ala’ pamoja na misemo ya ‘Ala’ ad-Diyn kutoka Mizaan al-Uswuul “Mizani ya Uswuul.”

 

Tambua ya kwamba Uswuul al-Fiqhi ni tawi la Uswuul ad-Diyn na kwamba utungaji wa kitabu chochote ni lazima uwe umeathirika na imani za mwandishi. Hivyo, kwa vile wengi wa waandishi wa Uswuul al-Fiqhi wametokana na Mu’tazilah wenye kutofautiana na sisi kwenye kanuni kuu, au kwa Ahl al-Hadiyth wenye kutofautiana na sisi kwenye masuala ya kina, hatuwezi kutegemea vitabu vyao.

 

Vitabu vya Wanazuoni wetu (wa Hanafi), hata hivyo, ni vya aina mbili. Aina ya mwanzo ni vile vitabu vilivyoandikwa kwa mtindo makini kabisa, kwa sababu waandishi wao walijua vyote viwili; kanuni na matumizi yake. Mifano ya aina hii, ni: Ma’khaadh ash-Shar’iy “Kuiendea Sharia’h” na al-Jidaal “Mjadala”” vilivyoandikwa na Abuu Mansuur al-Maturidi (Amefariki mwaka 333 H.).

 

“Aina ya pili ni ya kitabu kilichojadili kwa umakini kabisa pamoja na maana ya maneno na yaliyopangwa vizuri, kwa kuegemea mantiki za waandishi wao kwa kufikia suluhisho zenye maelezo kutokana na maana dhahiri za usimulizi. Hata hivyo, hawakuwa mahiri katika kushughulikia na nukta nzuri za al-Uswuul au masuala ya hoja safi. Matokeo ni kwamba waandishi wa aina ya pili walitoa mawazo kwenye kesi ambazo walikubaliana na wale waliopingana. Juu ya hivyo, vitabu vya aina ya mwanzo vilipoteza hadhi, ama kwa sababu vilikuwa ni vigumu kuvielewa au kwa sababu wanazuoni walikosa taratibu muafaka za kufanya kazi hii.”

 

Kuna mengi ambayo yanaweza kusemwa kuhusu usahihi wa tamko hili unavyofafanua maendeleo ya masomo ya Hanafi kwenye al-Uswuul, hata kama ilifanywa na mwanazuoni wa Kihanafi. Tamko hili, halifanyi lolote, kufikia karibu na ukweli wa kuelezea jukumu la Hanafiyyah kwenye maendeleo ya Uswuul al-Fiqhi. Kwenye kipindi cha mwanzo, wanazuoni hawa walijishughulisha zaidi kwenye kujadili masuala yaliyoletwa juu na al-Imaam ash-Shaafi’iy ndani ya ar-Risaalah yake kuliko kabla ya al-Imaam al-Maturdi, kama alivyofanya ‘Iysa bin Abbaan na wengine.

 

Wakati wa kipindi kinachofuata, mmoja miongoni mwao (ambaye) ni mwandishi mkubwa wa al-Uswuul alikuwa ni Abuu al-Hassan al-Karkhi (Amefariki mwaka 340 H). Kitabu chake kwenye al-Uswuul kinahusisha idadi maalum ya kurasa ambazo zilichapishwa na kitabu cha Abuu Zayd ad-Dabuzi, Ta’siys an-Nadhwar “Kuanzisha Maoni”, ambacho kimechapishwa ndani ya matoleo kadhaa nchini Cairo.

 

Baadaye, Abuu Bakr al-Jassaas (Amefariki mwaka 370 H.) aliandika kitabu chake, Al-Fuswuul Fiy al-Uswuul kama ni utangulizi wa kitabu chake Ahkaam al-Qur-aan “Tafsiri za Kisheria za Qur-aan”.[66]Al-Fuswuul kimechunguzwa na kufanyiwa uhariri kwa ajili ya uchunguzi wa shahada ya tatu (doctoral thesis), na kilichapishwa hivi karibuni nchini Kuwait.

 

Maendeleo ya kweli ya maandiko ya ki-Hanafi kwenye somo la al-Uswuul, inawezekana kutambulika kuanza kwa al-Imaam Abuu Zayd ad-Dabuuzi (Amefariki mwaka 340) ambaye aliandika vitabu viwili muhimu kwenye mada. Taqwiym al-Adillah “Thamani ya Ushahidi”, vyote au baadhi yake ambavyo vimechunguzwa na kuhaririwa, lakini bado havijachapishwa, na Ta’siys an-Nadhwar[67]Abuu Zayd aliifanyia kazi vyema al-Uswuul (kama) walivyofanya waliomtangulia, haswa kwa Al-Karkhi na Al-Jassaas, lakini kwa tofauti ambazo aliupanua uwanja na kuuelezea kwenye maelezo ya kina zaidi, pia alifanya nukuu fupi fupi kwenye nukta ambazo Hanafiyyah (Mahanafi) walikubalina na kutokubaliana na wengine, kwenye masuala ya Uswuul.

 

Abuu Zayd alifuatwa na Fakhr al-Islaam al-Baydaan (Amefariki mwaka 482 H.) ambaye ameandika kitabu maarufu cha Kanz al-Wuswuul Ilaa Ma’rifat al-Uswuul “Hazina ya Kuifikia Elimu ya Uswuul”, ambacho alijadili kuhusu Uswuul kwa jumla. Baadaye wanazuoni wa Hanafiyyah waliangalia kwa faida kubwa kwenye kitabu hicho na kuandika fafanuzi nyingi kwenye hicho kitabu, kilicho bora na muhimu zaidi, kilikuwa Kashf al-Asraar “Siri Zimefichuliwa” na ‘Abd al-Aziyz al-Bukhaariy (Amefariki mwaka 830). Fafanuzi hii imechapishwa kwenye matoleo kadhaa yaliyofanyiwa uhariri kote kuwili, huko nchini Uturuki na Misr.

 

Vivyo hivyo, Shams al-Aimmah as-Sarkhaasiy (Amefariki mwaka 423 H) ameandika Uswuul as-Sarkhaasiy, ambacho kimechapishwa ndani ya juzuu mbili nchini Misr. Kitabu hichi kinatambulika kuwa; kwa njia zote (kama ni) kitabu mbadala kwa kusoma kitabu cha Daabusi Taqwiym al-‘Adillah. Wanazuoni wa Hanafiyyah wa al-Uswuul wamechukua juhudi kubwa binafsi kwenye vitabu vya al-Bazdaawiy na as-Sarkhaasiy na wakajihusisha wenyewe kwenye kuvisomesha na kuvifafanua kwa muda mrefu.

 

Kutokana na hapo juu, ieleweke wazi kwamba maendeleo ya Uswuul al-Fiqhi, kama ni somo linalojitegemea, limekamilika, na kwamba hoja zake na mipaka ya elimu (parameter) zimetolewa tafsiri kwenye Karne ya tano AH. Hakika, kwa karne hiyo wanazuoni wa kila mafunzo ya fikra za kisheria wamerikodi tafsiri zao wenyewe na ufahamu wa Uswuul al-Fiqhi.

 

 

MTINDO WA WAFUASI WA AL-IMAAM ASH-SHAAFI’IY AU “MUTAKALLIMUUN”, NA WALE WA HANAFIYYAH (KI-HANAFI).

 

Uandishi wa somo la al-Uswuul, kiujumla unafuatiwa moja kati ya mitindo ifuatayo. Wa kwanza ulikuwa ni mtindo wa ash-Shaafi’iy au mtindo wa Mutakallimuun. Huu ulikuwa mtindo uliofuatwa na Shafi’iyyah, Malikiyyah, Hanaabilah na Mu’tazilah,[68]na ilitambuliwa kama ni “Mtindo wa Mutakallimuun” kwa sababu waandishi wa vitabu vilivyoandikwa kwa mujibu wa mtindo huu, walizoea kuzitolea utangulizi pamoja na mijadala ya elimu ya sifa za Uislamu na masuala thabiti, kama vile al-Hasan na al-Qabiyh “Nzuri na mbaya”, Hukm al-Ashyaa Qabl ash-Shar’iy “Hukmu Ya Masuala Kabla Ya Kuteremshwa Shari’ah”, Shukr al-Mun’im “Haja ya Shukrani Mtoaji”, na al-Haakim “Mmiliki wa Mamlaka” Sababu nyengine ya kubandikiwa “Mtindo wa Mutakallimuun” ni kwa matumizi ya mtindo wa kudhihirisha kwenye kutafsiri misingi ya utaratibu wa chanzo, kwenye kuangalia uhalali wa misingi hiyo, na katika kuzibatilisha kwa wale wenye mawazo yaliyotofautiana bila ya kutilia mkazo kwenye masuala na maelezo yenye kutokana na mzizi wa matumizi ya misingi hii.

 

 

MTINDO WA WANAZUONI WA KI-HANAFI WA AL-USWUUL.

 

Mtindo wa Hanafi katika uandishi wa al-Uswuul ulihusisha katika kutafsiri misingi ya Uswuul kutoka kwenye maelezo ya masuala ya kisheria ambayo waliowatangulia wao kabla wamekwisha kuyajadili. Hivyo, msingi wa masomo yao ya al-Uswuul ni yale yaliyotolewa kutoka kwenye maelezo ya masuala ya kisheria yaliyokwishatatuliwa huko nyuma, na sio kwa njia nyengine ya mzunguko. Hivyo kwa mujibu wa mtindo huu, yule ambaye anasoma Uswuul al-Fiqhi, atakusanya maelezo ya masuala kuhusiana na yale ambayo Maimamu wa Kihanafi wamekwishatolea Fataawa, na baadae kuyapambanua. Kwa kupitia upambanuzi wake, ataamua msingi ambao Fataawa hizi zitatolewa.

 

Shah Waliyu Allaah ametoa mawazo:-

 

“Nimeona kwamba, baadhi yao wamedai tofauti za baina ya Abuu Haniyfah na ash-Shaafi’iy zilizopatikana kwenye Uswuul zimetaja kitabu cha al-Bazdaawiy na kwengineko. Lakini, ukweli ni kwamba; Uswuul nyingi katika hizi zilikuwa zenyewe zimetolewa kutokana na matamshi tofauti ya kisheria ya Maimamu. Mawazo yangu kwenye suala hili ni kwamba, misingi hii ya al-Uswuul kama ni amri inayosema kwamba hiyo mahsusi “al-Khaasw” ni “Mubayyan”, na wala haihitaji kufuatwa kwa tamko la “Bayaan”, kwamba maelezo yaliyoongezwa kwa andiko linalohusisha kutengua “Naskh”, kwamba maarifa ya mambo mengi “al-‘Aam” ni kukataa maneno “Qatw’iy kama ilivyo mahsusi “al-Khaasw”; ya kwamba nambari halisi za wasimulizi haziwezi kuchukuliwa kama ni hoja kwa mujibu wa hiari Tarjiyh ya wazo la mmoja au mwengine na kwamba Hadiyth za yule ambae sio Faqiyh haihitaji kujipa tabu kuitumia kwenye kesi ambapo hakuna muafaka kwa hoja; kwamba hakuna uhalali wa fikra ya kuendelea kutoka sharti ya kabla “Shart” au wasifu “Wasf” kwenda kwenye toleo la kisheria; kwamba amri “al-Amr” kwenye maandiko, daima inaonesha wajibu wa kisheria “Wujuub”; na kuendelea mbele, zote hizi ni mifano kwa misingi iliyotumika kutoa hukumu za Maimamu. Hakika, hakuna usimulizi wenye maana wa kushauri kwamba Abuu Haniyfah au wafuasi wake wawili, Muhammad na Abuu Yussuf, walijifunga na chochote miongoni mwa misingi hii ya chanzo cha utaratibu. Kama ni hivyo, basi, misingi hii haina haja tena ya kuhifadhiwa na kutetewa kama walivyofanza al-Bazdaawiy na wengineo, kuliko wanavyofanza misingi ya upinzani”.[69]

 

 

SAYANSI YA USWUUL AL-FIQHI KIPINDI CHA KARNE YA SITA HIJRIYAH NA KIPINDI KINACHOFUATA.

 

Kutokana na kukusanywa pamoja mada kuu za somo hili, kwa mujibu wa mtindo wa Mutakallimuun, katika kazi kuu nne: Al-Ahd, Al-Mu’tamad, al-Burhaan na al-Mustaswfa, wanazuoni wakuu wawili katika miongoni mwa Mutakallimuun walifupisha vitabu hivi vinne kwenye kazi yao wenyewe.

 

Wa mwanzo alikuwa ni al-Imaam al-Fakhr ad-Diyn ar-Raazi (Amefariki mwaka 606 H.), ambaye alifupisha kwenye kitabu chake cha al-Mahswuul “Kinachofikiwa na Kupatikana”, ambacho nilipata heshima ya kukichungua na kukifanyia uhariri. Kazi hii imechapishwa kwenye juzuu sita na Chuo Kikuu cha Imaam Muhammad bin Sa’ud, na hivi sasa kinachapishwa.

 

Wa pili alikuwa ni al-Imaam Swafiy ad-Diyn al-Amidiy (Amefariki mwaka 635 H.), ambaye alifupisha vitabu hivi vinne ndani ya kitabu chake al-Ihkaam Fiy Uswuul al-Ahkaam “Umakini kwenye Chanzo-Utaratibu wa Sheria” ambacho kimechapishwa huko Riyaadh, Cairo na kwengineko.

 

Vitabu hivi viwili ni vikubwa na uhakika ni rahisi kuvisoma na kuvielewa kuliko vyengine. Kati ya viwili, al-Mahswuul kimeandikwa kwa lugha nyepesi, na kina maelezo na ufafanuzi zaidi. Masahihisho na fafanuzi nyingi zimeandikwa ndani ya vitabu hivi viwili. Taaj ad-Diyn al-Armaawi (Amefariki mwaka 656) amefupisha al-Mahswuul ndani ya kitabu chake cha al-Haaswil “Toleo” ambacho kimefanyiwa uchunguzi na kuhaririwa kwa ajili ya uchunguzi wa shahada ya tatu (doctoral thesis) huko Chuo Kikuu cha Al-Azhar, lakini bado hakijachapishwa.

 

Al-Imaam ar-Raazi yeye mwenyewe pia amekifupisha ndani ya kitabu chenye jina la al-Muntakhab “Mateuzi” ambacho mwanazuoni mmoja anakifanyia uchunguzi na uhariri.

 

Al-Qaadhi al-Baydhwaawiy (Amefariki mwaka 685) amefupisha al-Haaswil ndani ya kitabu chake Minhaaj al-Wuswuul Ilaa ‘Ilm al-Uswuul “Namna ya Kuimudu Sayansi ya Chanzo-Utaratibu”; lakini ufupisho wake ulikuwa na vifupisho vingi mpaka kuwa kama fumbo, ni vigumu mno kuuelewa. Hivyo, wanazuoni wengi walichukua hatua ya kutoa fafanuzi kwenye kitabu hicho. Miongoni mwa fafanuzi hizo, kizuri chao ni kile cha al-Isnawi (Amefariki mwaka 772) ambacho kina jina la Nihaayat as-Su’l “Mwisho wa Maulizo”. Kitabu kilichokuwa macho ya wanazuoni ndani ya uwanja huu kwa muda mrefu, na bado wanazuoni wa Shafi’yah wanakitumilia.

 

Kitabu cha Al-Amidiy al-Ihkaam “Umakini” kilifupishwa na Ibn al-Haajib (Amefariki mwaka 645) wa fikra za kisheria za Maliki ndani ya kitabu chake cha Muntaha as-Su’l wa al-Amal Fiy ‘Ilmay al-Uswuul wa al-Jidaal “Mwisho wa Sanyansi ya Maarifa ya Sheria za Kiislamu na Hoja”, ambacho ni maarufu miongoni mwa wafuasi wa al-Imaam Maalik.

 

Fafanuzi bora inayoweza kupatikana kwa kazi hii ni ile ya ‘Udad ad-Diyn (Amefariki mwaka 756), ambacho masahihisho na fafanuzi kadhaa zimeandikwa.

 

Vitabu vyote hivi vimeandikwa kwa kufuata mtindo wa Mutakallimuun, vikitoa tafsiri ya kanuni, kuelemea ushahidi juu yake, na kutafuta kuweza kubatilisha kwa njia hizi kwa wale wenye fikra pinzani, hadi kundi moja kati ya mawili yalikubali kushindwa.


Wanazuoni wa Hanafiyyah wa Uswuul nao halkadhalika walijituma kwenye kusoma vitabu vya al-Baydhwaawiy na as-Sarkhasi. Hali hii iliendelea kama ilivyo hadi mwisho wa karne ya sita na mwanzoni mwa karne ya saba H. Pale wanazuoni wa al-Uswuul walipoanza kutumia mtindo mpya. Mtindo huu ulihusisha kuichangaya pamoja mitindo ya Mutakallimuun na wanazuoni wa Hanafiyyah ili kutoa vitabu vyenye mchanganyiko wa Uswuul kwa makundi mawili.

 

Kufuatia mtindo huu, Mudhwaffar ad-Diyn as-Sa’ati (Amefariki mwaka 694) aliandika Badi’i al-Nidhwaam al-Jami’i Bayna Kitabay al-Bazdaawi wa al-Ihkaam. Kitabu hichi ni kimoja miongoni mwa vinavyopatikana kwa kuchapishwa.

 

Sadi ash-Shari’ah (Amefariki mwaka 747) ameandika Tanq’iyh al-Uswuul “Kuisafisha al-Uswuul”, ambacho alifupisha al-Mahswuul, Uswuul al-Bazdaawi na Mukhtasar bin al-Hajiyb. Baadaye aliandika fafanuzi kwenye kitabu chake mwenyewe chenye jina la at-Tawdhwiyh “Mbayana”, ambacho at-Taftazaani (Amefariki mwaka 792) amejumlisha fafanuzi nyembamba yenye jina la at-Talwiyh. Vitabu vyote vitatu; at-Tanqiyh, at-Tawdhwiyh na at-Talwyih vinapatikana katika chapa.

 

Taj ad-Diyn as-Subkiy ni miongoni mwa wanazuoni wa Shafi’iiyyah ambaye ameandika kitabu chake maarufu, Jam’al al-Jawaam “Mkusanyo wa Maarifa”. Kwenye utangulizi, ametaja kwamba amekusanya kazi yake kutokana na vitabu mia moja tofauti kwenye al-Uswuul. Wanazuoni wengi wameandika fafanuzi na kuweka rejeo (footnotes) kwa kitabu cha as-Subkiy. Kati ya hizi, labda fafanuzi iliyo muhimu zaidi na yenye kupatikana kwa mapana ni Sharh al-Jalaal al-Muhalliy, ambayo inabaki hadi leo kuwa ni msingi wa masomo ya al-Uswuul, haswa kwa wanazuoni wa Shafi’iiyyah (Ki-Shafi’iy).

 

Badr ad-Diyn az-Zarkhaasiy (Amefariki mwaka 794) pia ameandika ufafanuzi kwa jina la Tashriyf al-Masami’iy “Kuyaridhisha Masikio”, sehemu miongoni mwa hiyo ilichapishwa nchini Cairo ikiwa na rejeo za ash-Shaykh al-Muti’i (Amefariki mwaka 1354). Mmoja miongoni mwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Imaam Muhammad bin Sa’ud amechunguza na kufanyia uhariri sehemu ya kitabu hichi hivi karibuni kwa ajili ya kutunukiwa uchunguzi kwa shahada ya tatu (doctoral thesis).

 

Az-Zarkhaasiy pia ameandika al-Bahr al-Muhiytw “Bahari Iliyo Kubwa Mno”, ambacho amekusanya maoni ya wanazuoni wa al-Uswuul kutoka zaidi ya vitabu mia moja. Mwanafunzi hakuacha kuchunguza na kukifanyia uhariri kitabu hicho, chini ya usimamizi wetu, kwa ajili ya kutunukiwa uchunguzi kwa shahada ya tatu (doctoral thesis), na tayari amekwishakamilisha juzuu moja na kukichapisha.

 

Miongoni mwa Hanaabilah, Ibn Qudaamah (Amefariki mwaka 620) ameandika Rawdhwat an-Naadhwir wa Jannat al-Manaadhir, ambacho amefupisha Mustaswfa ya al-Ghazzaaliy, na kukiongezea maelezo mengine tofauti kwenye masuala ambayo Hanaabilah hawajakubaliana na wengine. Kitabu hichi, kimechapishwa mara kadhaa, na Hanaabilah wameona manufaa ndani yake, hadi hatua ya kufikia kuvikataa takriban vitabu vyengine vyote.

 

Sulaymaan at-Tufi (Amefariki mwaka 716) amefupisha kazi hii, na kutoa fafanuzi kwenye ufupisho wa juzuu mbili.

 

Miongoni mwa Maalikiyyah, al-Qarraafiy (Amefariki mwaka 684) ameandika Tanqiyh al-Fuswuul Fiy Ikhitiswaa al-Mahswuul “Kuisafisha Sura kwa Ufupisho wa Mahswuul” Al-Qarraafiy pia ameandika fafanuzi kwenye al-Mahswuul katika juzuu kubwa yenye jina la Nafaa’is al-Uswuul “Hazina za Uswuul”, sehemu miongoni mwake imefanyiwa uchunguzi na kufanyiwa uhariri chini ya usimamizi wetu mjini Riyaadh.

 



[64] Angalia al-Makki, Manaaqib al-Imaam Abuu Haniyfah, II, uk. 245, Utangulizi wa Uswuul as-Sarkhasiy, 1, 3, Qutubzadeh, Miftaah, as-Sa’adah, II, uk. 37, na Ibn an-Nadiym, Al-Fihrist, Watu wote waliofanya madai haya waliegemeza maelezo yao juu ya mawazo ya Ibn an-Nadiym ndani ya maandiko ya habari za maisha ya Muhammad bin al-Hasan. “Anacho kitabu cha Uswuul chenye sura kwenye Swalaah, Zakkah na Hajj.” Hili, hata hivyo, linaonesha kuturudisha kwenye kazi ya Uswuul ad-Diyn (Ukweli ni kwamba, kinachoonesha hapa, ni kwamba kumbukumbu ni kwa kazi ya al-Imaam Muhammad bin al-Hasan kwenye Fiqh, Kitaab al-Aswl, ambacho kimechapishwa hivi punde nchini Pakistan. Na zaidi ya hapo, mawazo ya kwamba Abuu Yuusuf ameandika kwanza kuhusu Uswuul imetokana na usimuliaji uliojumuishwa na Khaatib wa Baghdad ndani ya kitabu chake cha Taariykh Baghdad).

[65] Angalia Vol. 1, u. 110-111.

[66] Kazi kuu ya al-Jassaas, Ahkaam al-Qur-aan, ilikuwa ndio mada ya Mhariri wa kazi hii ya uchunguzi, na hivi sasa kimeshatafsiriwa kwenye lugha ya Kiingereza, pamoja na kutolewa maelezo,.

[67]Taqwiym al-Adillah, kimehaririwa kwenye juzuu kumi na hivi karibuni kitachapishwa, Allaah Akipenda.

[68] Kila kundi hili la wanazuoni wameongeza kitu cha kwao kwenye vitabu vyao, ingawa walitumia mtindo mmoja wa uandishi na mtindo mmoja wa kuwasilisha ushahidi na hoja.

[69] Angalia ad-Daalawi, Hujjatullah al-Baalighah, (Misr), I, uk. 336-341; pia ad-Dahlaawi, Al-Inswaaf Fiy Bayaan Asbaab al-Ikhtilaaf, (Salafiyya, Cairo), uk. 38-40.

Share

22-Uswuul Al-Fiqhi: Sura Ya Sita Na Ya Mwisho - Mada Zinazohusiana Na Ijtihaad

 

SURA YA SITA

 

MADA ZINAZOHUSIANA NA IJTIHAAD

 

Kiuhalisi, mada ya Ijtihaad ilichukua sura nzima ya kitabu cha al-Uswuul. Ndani ya sura hiyo, mwandishi (anatakiwa) aanze kwa kujadilii kuhusu Ijtihaad kwa kuitolea tafsiri, kuelezea masharti ya kutumika, na kuitofautisha baina ya aina tofauti za Ijtihaad. Hivyo, atajadili kama ndio au sivyo namna Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyoitumia Ijtihaad kuwa ni muundo wa kuabudu ‘Ibaadah, kama ikiwa ilitumika au haikutumika na Swahaabah kuwa ni muundo wa ‘Ibaadah wakati wa maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kama ikiwa jibu moja tu linalotokana na Ijtihaad kwenye suala lolote linaweza kuwa sahihi, au kama inawezekana kuwepo majibu tofauti yaliyo sahihi, na pale Ijtihaad iliporuhusiwa na isiporuhusiwa. Baadaye, wanazuoni walijadili kuhusiana na mada ya Taqliyd kwa mtindo huo huo.

 

Mnamo karne ya nane Hijriyah, Ibraahiym bin Muusa ash-Shaatwibiy (Amefariki mwaka 790 H) aliandika al-Muwaafaqaat “Upatano”, ambacho alizungumzia kuhusu Ijtihaad kwa mnasaba wa kuwa ni zoezi la kitaalamu katika nguzo mbili. Nguzo ya kwanza ilikuwa ni elimu iliyokamilika ya sarufi na elimu ya kupanga maneno kwa sarufi ya lugha ya Kiarabu. Aliacha somo hili kwa wanazuoni wa lugha ya Kiarabu na waandishi wengine wa al-Uswuul. Nguzo ya pili ya Ijtihaad, kwa mawazo ya ash-Shaatwibiy, ilikuwa ni elimu ya malengo ya Sheria ya Aliyekuwa Mbora wa Hekima na Mtungasheria.

 

Waliomtangulia ash-Shwaatibiy kwenye uwanja wa al-Uswuul hawakupata kuweka maanani sana kwenye malengo haya. Isipokuwa, kikubwa walichokifanya kwenye mwelekeo huu ulikuwa ni kutafuta sababu kuu ‘Illah. Kwa upande mwengine, ash-Shaatwibiy, aliandika kitabu chake kwa lengo la kujadili kuhusiana na jambo hili muhimu. Hakika, elimu ya malengo Maqaaswid ya Shari’ah ni muhimu kwa ajili ya kuelewa Sheria ya Mtungasheria. Hata hivyo, wanazuoni wa al-Uswuul hawakupatapo kukipa kitabu hicho hadhi yake inayotakikana. Hili linawezekana kuelezwa kwa dhana iliyojengeka ndani ya akili za wanazuoni wengi kwamba hairuhusu (kuchunguza) sababu za sheria ya Mtukufu, sababu ambayo ni kwamba kuchunguza huko, hakuwezi kufanywa au kupatikana umakini.[70]Inapokuwa kesi hii, au kuendelea mbele kwa hoja za wanazuoni wengi wakubwa, somo la masuala hayo ni madogo mno kuliko mahitaji ya faragha asiyohitaji mwanazuoni.

 

Hata hivyo, kitabu cha ash-Shaatwibiy kipo kwenye chapa na kinapatikana sehemu kadhaa, na tunaweza tu kutaraji kwamba walimu wa al-Uswuul na wale wenye jukumu la kuweka mtaala watawaongoza wanafunzi wao kwa kuwaweka kitako kwenye kazi hii muhimu, haswa kwa wale wanaosoma al-Qiyaas, at-Ta’lil na Ijtihaad. Wakati wetu, wanazuoni wakuu wawili, Ibn ‘Ashuur na ‘Allaal al-Fasi wameandika kwenye somo la malengo ya Shari’ah.

 

Ibn Hammaam (Amefariki mwaka 861 H), ameandika at-Tahriyr “Uhariri” na mwanafunzi wake, Ibn ‘Aamir al-Hajj (Amefariki mwaka 879 H) ameiandikia ufafanuzi yenye jina la at-Taqriyr wa at-Tahbiyr. Vyote vipo kwenye chapa. At-Tahriyr ni, moja kati ya vitabu vilivyoandikwa kwa kuchanganya mtindo wa Hanafiyyah na Mutakallimuun. Kuna fafanuzi nyengine, iliyoandikwa na Amr Badshah, yenye jina la Taysiyr at-Tahriyr “Kuwepesisha Uhariri”

 

Al-Qaadhi ‘Ala’ ad-Diyn al-Mardaawi (Amefariki mwaka 885 H) ameandika fafanuzi ya Uswuul bin Muflih[71] (Amefariki mwaka 763 H) yenye jina la Tahriyr al-Manquul wa Tahdhiyb ‘Ilm al-Uswuul. Kazi hii imefanyiwa uchunguzi na kufanyiwa uhariri, na ipo tayari kuchapishwa hivi karibuni. Mchunguzi huyo huyo, pia amejihusisha na Uswuul bin Muflih.

 

Baadaye, Ibn an-Najjaar al-Futuuhi wa fikra za kisheria za mafunzo ya Hanbali aliandikia ufupisho wa Tahriyr al-Mardaawi, na aliandika fafanuzi iliyokuwa nzuri kabisa. Fafanuzi hii inatambulika kuwa ni moja kati ya iliyo bora na yenye mambo mengi ya vitabu vilivyopita kuhusu al-Uswuul. Toleo ambalo halijakamilika la kitabu hicho, lilichapishwa nchini Misr kabla ya kuchungzwa na kufanyiwa uhariri na Maprofesa wawili muhimu, Dr. Nazih Hamaad na Dr. Muhammad az-Zuhayli. Kazi yao ilichapishwa na Kituo cha Elimu ya Uchunguzi kwenye Kitivo cha Shari’ah huko mjini Makkah. Sehemu kubwa ya kitabu hicho kimeshachapishwa, na kilichobaki sasa ni kazi ya wapigaji chapa.

 

Kwenye karne ya kumi na mbili AH, Muhiyb Allaah bin Abdush-Shakuur al-Bihaariy, wa mafunzo ya Hanafi (Amefariki mwaka 1119 AH) aliandika kitabu chake maarufu kwenye Uswuul, Musallaam ath-Thubuut. Hichi ni kimoja kati ya kitabu kilicho makini na chenye mambo mengi kilichoandikwa na kizazi cha baadaye cha wanazuoni wa Hanafi. Kitabu kimechapishwa pamoja na fafanuzi nchini India, na halikadhalika kimechapishwa pamoja na fafanuzi yake maarufu ya Fawaatih ar-Rahamuut, kwa kuegemeza mara kadhaa kitabu cha al-Mustaswfa cha Imaam al-Ghazaaliy.

 

Vitabu vyote hivi viliandikwa kufuatana na mtindo uliotajwa hapo juu, na wote hao walikuwa makini kwenye kutetea Madh hab ya mwandishi na kukataa yale ya wapinzani wake. Kutoka karne ya sita hadi sasa, hakuna Uswuul al-Fiqh yenye sifa ya kuwa ni nyenzo ya kufanyia uchunguzi, ambacho kitawalinda Wanazuoni wa Kiislamu kutokana na kufanya makosa kwenye Ijtihaad; isipokuwa kutokana na kitabu kimoja maarufu kilichoandikwa katika kupasisha kitabu cha ash-Shaykh Mustafa ‘Abd ar-Razzaaq Tamhiyd li at-Taariykh al-Falsafa al-Islaamiyyah “Dibaji ya Historia ya Falsafa ya Kiislamu”. Mwanafunzi wake, alijaribu kueleza kitabu hichi maarufu ndani ya kitabu chake Manaahij al-Bahth “Mitindo ya Uchunguzi.”

 

Mnamo karne ya kumi na tatu Hijriyah, Al-Qaadhi ash-Shawkaani’ (Amefariki mwaka 1255 H) aliandika kitabu chake maarufu kwenye Uswuul, Irshaad al-Fuhuul “Muongozo wa Wakuu”. Ijapokuwa juzuu zake ni ndogo, kitabu hichi kinawakilisha mawazo tofauti kwenye uwanja wa al-Uswuul, na ushahidi uliotumika na wasomi wa kila mmoja ni kwa njia ya ufupi lakini kwa mtindo safi kabisa, mwandishi pia anaeleza mawazo gani yeye anapendelea. Kitabu hichi, ambacho kimeshachapishwa mara kadhaa, ni chenye manufaa kwa mwanafunzi wa Uswuul al-Fiqh na kwa masomo ya kupambanisha (comparative) kwenye maarifia ya Sheria. Hata hivyo, kwa muono wetu wa elimu, hakijaingizwa kwenye mtaala wa taasisi yoyote, ingawa ni kitabu muafaka.

 

Muhammad Swiddiyq Khaan (Amefariki mwaka 1307 H), ameifupisha kazi hii kwenye kitabu chenye jina la Huswuul al-Ma’muul min ‘Ilm al-Uswuul “Kuyafikiria kwa Yale Yaliyotegemewa Kwenye Sayansi ya al-Uswuul” ambacho kipo katika chapa.

 

Hakika, Irshaad al-Fuhuul kinakadiriwa kuwa ni ufupisho mwanana kabisa wa al-Bahr al-Muhiytw ya az-Zarkhaasi. na Tas-hiyl al-Uswuul ya al-Mahallaawi inakadiriwa kuwa ni ufupisho wa Irshaad al-Fuhuul.

 

Baada ya kipindi hichi, tunaona kwamba, somo la al-Uswuul limefuata moja kati ya mielekeo mikuu ifuatayo:

 

1)    Kuandika miongozo ya masomo, ufupisho na hati (notes). Hili limefanywa na Maprofesa wa vitivo tofauti vya Shari’ah na Sheria, ili kulifanya somo la Uswuul al-Fiqh kuwa ni jepesi kwa wanafunzi wao; baada ya kutambua kwamba wanafunzi wao hawakuweza au hawakuwa tayari kulisoma somo hili. Matokeo yake, hati hizi haziwakilishi aina yoyote ya elimu ya juu kwenye uwanja huu; na kwenye kesi nyingine ni kule kujaribu tu kubadilisha masuala ya al-Uswuul al-Fiqh katika njia nyepesi na ya kisasa. Wanazuoni wafuatao: Marsafi; al-Mahallaami; al-Khudari, ‘Abdul-Wahhaab Khallaaf, ash-Shinqiti, as-Sayis, Mustafa ‘Abdul-Khaaliq, ‘Abdul-Ghani, ‘Abuu Zahrah, Abuu Nuur Zuhayr, Ma’ruuf ad-Dawaalibi, ‘Abdul-Kariym az-Zaydah, Zaki ad-Diyn Sha’baan, Muhammad Salaam Madhkuur, na wengineo wote, wameandika vitabu ambavyo kiuhalisi ni mihadhara ambayo wameitoa ndani ya vitivo walivyosomesha vya Shari’ah na Sheria.

2)    Muelekeo wa pili ulikuwa ni uandishi wa chunguzi (researches) za Vyuo Vikuu kwenye aina tofauti za sayansi hii, na uchunguzi na uhariri wa maandiko yasiyochapishwa. Bila ya shaka, aina zote mbili za mielekeo ni yenye manufaa makubwa, na hakika mimi sitokuwa na nia ya kuzibeza nguvu za yeyote. Lakini mielekeo hii inaangukia kuwa si chochote katika kufanikisha maendeleo ya ndani ya uwanja huu, na sanyansi ya Uswuul al-Fiqh inabaki kuwepo sehemu ile ile ambayo waliotutangulia wameiacha ndani ya Karne ya Sita Hijriyah.

 

Kutokana na maelezo ya hapo juu, tunaweza kupata hitimisho zifuatazo:

 

1.     Hakuna somo, ambalo sasa linajulikana kama Uswuul al-Fiqh, lililopata kuibuka likiwa na misamiati yake wakati wa enzi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au Swahaabah (Radhiya Allaahu ‘Anhum) zake.

 

Hata hivyo, takriiban mienendo ya Ijtihaad za aina tofauti zilizotumika wakati wa vipindi hivi viwili, ziiliweza kuwekwa chini ya misingi inayozunguka sayansi hii. Sababu za hili, ni kwamba walikuwa wakifikia maelezo ya kina ya hukumu zao kisheria kwenye suala maalum kutokana na vyanzo vya Sheria kama ni aina isiyokuwa na kanuni maalum, kama vile wanavyozungumza Kiarabu bila ya kanuni, au bila ya kuelewa kanuni za sarufi ambazo bado zilikuwa hazitambuliki wakati huo.

 

2.     Mwanazuoni wa mwanzo kukusanya kitabu kuhusu kanuni za sayansi ya Uswuul al-Fiqh alikuwa ni al-Imaam Muhammad bin Idriys ash-Shaafi’iy (150-204 H).

 

Kitabu cha mwanzo chenye maarifa ya kina kwenye somo hili kilikuwa ni Risaalah, ambacho ameandika kwa kuitikia ombi kutoka kwa al-Imaam ‘Abdur-Rahmaan bin al-Mahdi (135-198 H). Hii ilikuwa baada ya mafunzo maarufu ya Fiqh, mafunzo ya Ahl al-Hadiyth, yakiongozwa na al-Imaam Maalik bin Anas (93-179 H), na mafunzo ya Ahl ar-Ra-ay yakiongozwa na al-Imaam Abuu Haniyfah (70-150 H), yamepata kuanzishwa na kuenea mno.

 

Kutokana na kuenea sehemu tofauti kwa mafunzo haya mawili ya fikra za sheria, kukaibuka baina ya wafuasi wa mafunzo haya mawili, kwa kuongezea migongano ya kisiasa, kifikra na kinadharia iliyokuja juu wakati huu, ambayo yalikuja kutambulika kama ni “Mabishano ya Fiqh”.[72]

 

3.     Uswuul al-Fiqh ni nyenzo ya kufanyia uchunguzi kwa wanazuoni[73] na sehemu yake ya Fiqh inafanana na ile ya Dhana ndani ya Filosofia[74] (Logic in Philosophy). Hivyo, ilitolewa tafsiri kama ni “Mkusanyiko unaotambulika wenyewe, kuwa ni thibati za Shari’ah na ushahidi, kwamba, inaposomwa kisawasawa, utapelekea ama kwenye elimu maalum ya hukumu za Shari’ah au kwa uchache fikra za dhana zenye hoja kuhusiana na hilo hilo, tabia ambazo thibati hizo zinapatikana, na hadhi ya mthibitishaji.”[75]

 

Hivyo, Uswuul al-Fiqh inatoa muongozo wa kina unaomlinda Mujtahid kufanya makosa kwenye mitindo tofauti inayotumia chanzo halisi kwa lengo la kufikia hukumu za kisheria.[76] Juu ya hivyo, haikutumika kwa njia hii hadi al-Imaam ash-Shaafi’iy alipoiweka kwenye matumizi ndani ya Fiqh yake “Mpya”.[77]

 

4.     Ukweli muhimu ambao unaweza kuwekwa akilini ni kwamba wanazuoni wamesoma Fiqh na kutolea matamko kuhusiana nayo, kabla ya yeyote kuanza kuzungumzia kuhusiana nayo hiyo Uswuul (achilia mbali kazi ya Fiqh “Mpya” ya al-Imaam ash-Shaafi’iy).

 

Hivyo, majukumu waliyopewa na wengine kwa Uswuul al-Fiqh yalikuwa ni kidogo, kuliko yale ya kuthibitisha matamko ya kisheria Fataawa, ambazo walizitoa kwenye masuala maalum, na uzito wa hoja na mjadala baina yao. Hawakuangalia Uswuul al-Fiqh kama ni muongozo wenye maarifa ya kina ya Sheria au kama ni mtindo unaoweza kutumika katika muundo wote wa sheria. Wanazuoni Fuqaaha, walipoendewa na masuala pamoja na migogoro, walikuwa wakirudi nyuma moja kwa moja kwenye ushahidi ulio mnasaba, bila ya kuona haja ya kutumia kanuni za jumla zinazotumika ndani ya Uswuul al-Fiqh.

 

Hivyo, al-Imaam Abuu Haniyfah alitoa Fataawa zinazokaribia kufikia nusu milioni,[78]ambazo wanafunzi wake walisoma na kufaulu. Lakini, kanuni za kisheria ambazo al-Imaam Abuu Haniyfah aliegemezea Fataawa hizi, hazikuonekana chochote kama ni mstari usioingiliwa na mamlaka yake,[79] ukiacha simulizi chache ambazo alielezea kwa baadhi ya vyanzo vyake vya Ijtihaad. Alisema, ndani ya simulizi zake:

 

“Ninafuata Kitabu cha Allaah, na kama sikupata suluhisho humo, ninafuata Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kama sikupata suluhisho ndani ya Qur-aan au Sunnah, ninafuata matamko yoyote ya Swahaabah ninayopendelea mimi, na kuachana na yeyote ninayetaka. Kama kuna tamko kwenye suala maalum na Swahaabah yeyote, sitotumia mawazo mengine yoyote yaliyotumika na mwanazuoni yeyote. Lakini, kama nitapata suluhisho pekee kwenye mawazo ya Ibraahiym, ash-Sha’bi, Ibn Siyriyn, Hasan al-Baswriy, Atwa’a Sai’iyd bin al-Musayyab, nitafanya Ijtihaad kama walivyofanya wao.”[80]

 

Pale watu walipojaribu kumfanyia uadui Abuu Haniyfah dhidi ya Khaliyfah, al-Mansuur, aliandika kumpelekea Khaliyfah:

 

“Hali ilivyo sivyo kama ulivyoisikia, Ewe Amiyr al-Mu’miniyn! Nimefanya kazi kwa mujibu wa Kitabu cha Allaah, kisha kwa mujibu wa Sunnah ya Mtume, kisha kwa mujibu wa hukumu za Abuu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan na ‘Aliy, kisha kwa mujibu wa hukumu za Swahaabah waliobaki. Kisha, kama kutakuwa na mgongano baina ya matamshi yao, ninayatuliza kwa al-Qiyaas. Hakuna kiumbe wa Allaah aliye na urithi wa karibu Kwake Yeye kuliko mwengine.”[81]

 

Pale alipotuhumiwa kupendelea zaidi matumizi ya al-Qiyaas kuliko maandiko yaliyo wazi Nass ndani ya Qur-aan, alijibu: “Naapa kwa Allaah, wale wanaosema kwamba tunapendelea al-Qiyaas kuliko Nassw wamesema uongo na wametusengenya. Je, kuna haja yoyote ya al-Qiyaas baada (kupata iliyo dhahiri) ya Nassw?”[82]

 

5.     Ni uwazi ulio dhahiri kwamba tokea hapo awali mwa kipindi cha Umaawi hadi kuporomoshwa kwa Khaliyfah wa Kiislamu, mamlaka na uongozi ndani ya Ummah ulikuwa ndani ya mikono ya wale wasio na sifa za kuifanyia kazi Ijtihaad, wakati huo huo, majukumu ya Ijtihaad yalipelekwa kwa ‘Ulaama’ wasio na mamlaka. Na si rahisi kupata mbadala wa jambo hili, isipokuwa kwa Khaliyfah ‘Umar bin ‘Abdul-‘Aziyz, ambaye kutokana naye, hukumu nyingi zinahusiana na masuala ya maarifa ya sheria za Kiislamu zimesimuliwa. Hali hii ilikuwa na athari kubwa sana ya kuigwa Fiqh na Uswuul yake kutoka katika mandhari ya matendo ya maisha ya Muislamu, ili kwamba, kwenye kesi zilizo nyingi, masomo haya yalikuja kuwa ni ya kinadharia na kifikra.[83] Kimsingi, masomo yote yalikuja kuwa ni maelezo ya namna maisha ya Muislamu yanavyotakiwa yawe; sio namna ilivyokuwa, au namna itakavyokuwa baadaye.

 

6.     Waandishi na wanahistoria wa sayansi waliweka miongoni mwa sayansi za Shari’ah ambazo zimeegemezwa kwenye ushahidi uliotoka sehemu moja kwenda nyengine,[84]ijapokuwa baadhi ya waandishi walisema kwamba kanuni zake zimechukuliwa kutoka kwenye lugha ya Kiarabu, sayansi ya mawazo, na taratibu nyengine za Kiislamu.[85]Mmoja miongoni mwa waandishi waliobobea kwenye uwanja huu, ni al-Imaam al-Ghazzaaliy, ameandika:-

 

“Sayansi za kusifiwa ni zile ambazo sababu ‘Aql na ushahidi uliopokewa Sama’ zinashikana pamoja, na ambazo hitimisho linaegemezwa katika hoja zikiambatana na zile zilizoegemezwa kwenye uteremsho. Sayansi ya Fiqh na Uswuul yake ni moja miongoni mwa sayansi hizi. Inachukua sawa sawa kutoka uhalisi wa uteremsho na hoja bora. Hata hivyo, haitegemei kiuhalisi kwenye hoja hadi kufikia kwamba haitokubaliwa mbele ya sheria ya uteremsho, na wala haiegemezwi kiurahisi kwenye aina ya kukubali kwa upofu ambapo haitoshikana na hoja.[86]

 

Matamko ya al-Imaam al-Ghazaaliy na waandishi wengine kwenye somo la al-Uswuul linatuwezesha sisi kuwaza kwamba kuna vyanzo vitatu vya Fiqh:

 

i)                   Wahy uteremsho ulio Mtukufu: hii inahusisha vyote viwili, iliyokusanya Qur-aan isiyoigika, na wahyi usiyokusanywa, au Sunnah.

ii)                  ‘Aql au hoja: kuelezea maandiko, kutafuta njia ambazo zinaweza kutumika na njia ambazo sehemu tofauti zinaweza kuunganishwa kama kitu kimoja, kutafuta hoja zilizo kwenye sheria ambazo zinaonesha kuwa hazina hoja, kupata sheria kwenye mambo ambayo Mtungasheria hakuweka hukumu zilizo wazi ndani ya maandiko, na mambo mengine yanayofanana ambayo yanaweza kutafsiriwa na kuelezewa.

iii)                Uzoefu, mila na manufaa ya jamii.

 

Uswuul zote, ambazo zile wanazuoni walizokubaliana na zile zinazohusiana na kutokubaliana, zinaweza kugaiwa chini ya mada tatu kama ifuatavyo; Qur-aan, Sunnah, al-Ijma’, al-Qiyaas, fikra ambayo kimsingi ni kuhusiana na yenye manufaa yanaruhusiwa na yaliyo na madhara. Kimsingi yanayozuiwa, al-Istis-haab na al-Istihsaan. Kwa kuongezea, matamshi ya Swahaabah yalikuwa ni maarufu miongoni mwao na hakuna yeyote miongoni mwao aliyeyakataa, kanuni za daima (zilikuwa ni) kutumia mbadala wa isiyokuwa tata japo kwa hali ya chini; kusoma kesi kidogo zinazoweza kupatikana na zenye mnasaba kwa lengo la kupambanisha, manufaa ya umma na mila ambazo wala hazikuamrishwa au kuzuiwa ndani ya vyanzo vya Kiislamu; hitimisho kwamba hakuna sheria ambapo hakuna kitu cha kuonesha sheria yoyote, sheria za mataifa kabla ya Uislamu, na kuufunga mlango kuhusiana na hoja zilizo thibati.

 

  1. Kulikuwa na sababu fulani ndani ya historia yetu, baadhi yake, zimetajwa juu, kwamba, vyote vilipelekea kuwekwa vikwazo vingi juu yetu. Hivyo, lengo la akili zetu za Kiislamu na fikra na mantiki yalipelekwa kwenye masuala madogo, na kwamba tulikuwa tumezuiliwa kufikiri kwenye mambo mengi sifa zilizoonekana kuwa ni sura za mawazo ya Kiislamu. Hili lilikuwa na athari ya mbali kwenye namna tunavyojihusisha na Fiqh na suluhisho tunazotoa, na hizi nazo pia zimezaa sifa na sura hizo hizo.

 

  1. Ni jambo linalojulikana kwamba kwenye kila sayansi na maisha ya dunia, kuna mambo ambayo kiuhalisi yanakubali maendeleo, kwamba mara nyingine inahitaji kuwepo mpangilio ili kutambua uwezekano wake kamili. Hata hivyo, kuna baadhi ya mambo ambayo yameganda na hayakubali mabadiliko. Kwa mujibu wa nadharia za Kiislamu, hayo mambo mawili ni lazima yaunganishwe. Hivyo, Uswuul al-Fiqh zina sheria imara zisizobadilika, ambazo haziwezi kubadilishwa, na nyengine zinategemea kwenye maendeleo yenye kuendelea na kuzifanya mpya. Hili lipo wazi kutokana na mjadala wetu tulioenda nao kwenye Ijtihaad.

 

Hivyo, wakati tunapohimiza wanazuoni wote wa Kiislamu kutoanza kwa kukumba ila waanze kwenye kufaidika na hoja na Ijtihaad za wanazuoni ambao walizipitia kabla yao. Tunathibitisha kwamba, hakuna aliyedai kwamba hili ni jambo la lazima kulifuata kwa kila Mujtahid kwenye mambo ambayo matamshi yake yaliegemea tu kwenye hoja zake binafsi. Kubwa tunaloweza kusema kwenye jambo hili kwamba matamko yake ni: “ushauri, na ushauri unaweza kutumiwa”.[87]

 

  1. Kutokana na kusoma mitindo ya Waislamu wa kale, ni uwazi kwetu kwamba lengo kuu halikuwa rahisi katika kuichambua sheria na baadaye kutoa Fataawa. Hapo hapo, kwa upande mwengine dhumuni lao daima lilikuwa ni kusimamisha Mamlaka ya Allaah kupitia matumizi ya sheria Zake. Hili maana yake, kimsingi ni kwamba mazingira yaliyozunguka matumizi ya sheria hayawezi kutenganishwa na masharti yaliyoambatanishwa nayo.

 

Kama, kwa kuelewa hayo juu, tunahitaji kurudisha sayansi hii katika sehemu yake iliyo sahihi miongoni mwa sayansi za Kiislamu na kuibadilisha kwenye mtindo wa uchunguzi kwenye chanzo cha ushahidi wa Shari’ah ambapo huko tunaweza kupata hukumu, na masuluhisho, ya matatizo yetu ya kisasa, (hivyo kuendeleza kisawasawa Mamlaka ya Shari’ah), ni lazima tufanye yafuatayo:-

 

i)                   Kupitia upya mada zilizohusishwa ndani ya sayansi hii na kuzuia zile ambazo zisizo na uhusiano na wanazuoni wa kisasa au mwanachuoni. Hizi zinaweza kuwa Hukm al-Ashyaa Qabl ash-Shar’ “Hukumu kabla ya Shari’ah” Shukr al-Muniym “Namna mtu anavyotakiwa Kumshukuru Mwenye Nguvu Mwingi wa Rehema”. Mabaahith Hakimiyyatul ash-Shar’ “Masomo Kuhusiana na Mamlaka ya Shari’ah”, na kujihusisha sana na tafsiri. Ni lazima pia tutolee maamuzi migogoro kuhusiana na yasiyo kawaida Qira-aat Shadhdhah “Usomaji ulio Mbadala” wa Qur-aan, na asili ya Kiarabu ya Qur-aan nzima. Vivyo hivyo, ni lazima sasa tumalize msururu mrefu wa kutokubaliana kuhusu Hadiyth ya msimulizi-mmoja kwa kusema kwamba, kama simulizi hiyo itathibitishwa kwamba inaendana pamoja na masharti ya kuwa Swahiyh, itakubaliwa, na sheria zinaweza kupatikana humu.

 

Juu ya hivyo, ni lazima tupitie tena masharti yote, yaliyowekwa na baadhi ya wanazuoni wa kale, ambao wanaonekana kuathiriwa na mazingira. Kwa mfano, sharti ya kwamba Hadiyth isigongane na kanuni za jumla walizoweka, kwamba isisimuliwe na asiyekuwa mwengine ila ni Faqiyh, kwamba isigongane na al-Qiyaas, au utamaduni wa watu wa Madiynah, na maana zilizo wazi Dhwaahir za Qur-aan. Au sharti ya kwamba Hadiyth, kama inahusiana na suala la kawaida au gumu au lililo na taabu, ni lazima lijulikane na walio wengi. Masharti yote haya yatupiliwe mbali, na mtindo huu huu ufanyike kwa sharti nyengine. Kwa sababu yalikuwa na yataendelea kuwa ni mkanganyo na chanzo cha kutokubaliana baina ya Waislamu, na ambayo bado yanakula muda wa wanazuoni.

 

ii)                  Kuchukua somo la lugha kuhusiana na Fiqh ambalo litaangalia mitindo ya misamiati iliyotumika na Waarabu wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuangalia hatua za maendeleo, ambapo mitindo hii baadae ilipitia, na maana tofauti zilizonasibishwa kwenye maneno katika matumizi ya wakati huo. Hili, linatuwezesha kuelewa maandiko kama yanavyotakiwa kueleweka.

iii)                Kuwa makini na mitindo na kanuni zilizomo katika kuitekeleza Ijtihaad, kama vile al-Qiyaas, al-Istihsaan, al-Maswlahah, na nyenginezo, na kuzisoma kwa uoni wa historia, na kuweka akilini mazingira yaliyowapelekea kutamka matamko kutoka kwa Mujtahiduun. Ni lazima pia tujaribu kuingiza mhimili wa akili za wanazuoni kwa wale ambao wanafanya uchunguzi ndani ya mwanga wa al-Faqiyh na al-Uswuul.

iv)               Kuelewa kwamba kwa wakati huu, haiwezekani kuwepo Mujtahid Mutwlaq, na mwenye mamlaka ya kisheria (kwenye kutoa tafsiri ya vyanzo) katika haki yake mwenyewe, kutoa hukumu kwenye masuala. Kwa umbali wa tutakapofika kuhusu hili, labda ilio karibu na mbadala ni Mabaraza ya Kitaalamu.

 

Ili kuweza Mabaraza haya kutatua mahitaji ya Ummah kwenye masuala ya sheria, ni lazima yawe na jopo la wataalamu ambao uzoefu wao umo kwenye vitengo tofauti vya maisha, na ambao wataweza kwa uwazi kuona tatizo lolote lililopelekwa kwao. Kwa kuongezea hili, itawabidi kuwa na maarifa kamili ya maamuzi ya msingi na kanuni za Shari’ah ya Kiislamu. Mabaraza kama hayo ni lazima pia yawe na wanazuoni wengi wenye hadhi iliyo juu kabisa inayoweza kuwa, katika maarifa ya vyote viwili, sayansi ya Shari’ah na chanzo cha ushahidi kilicho na maelezo ya kina. Labda, mmoja miongoni mwa wanazuoni alikuwa akimaanisha fikra hii pale alipokutana na mtu aliyetaka kufungua Swawm yake ndani ya mwezi wa Ramadhaan na mwanazuoni alimwambia mtu huyo kutafuta mawazo ya daktari Muislamu aliye muaminifu, na kwa kuongezea kwamba; kama daktari huyo atatambua kuwa Swawm hiyo ni yenye dhara kwa afya yake, basi itaruhusiwa kwake yeye kujizuia kufunga Swawm.

 

v)                Ni lazima tufanye urahisi kwa wataalamu kwenye nyanja nyengine kusoma yale wanayohitajia katika sayansi ya Shari’ah.

vi)               Ni lazima tuwe wazoefu na Fiqh ya Swahaabah na Taabi’un, na zaidi ni kanuni ambazo walitumia kutolea maamuzi yao. Kwa uhalisi, Fiqh ya Khulafaa ar-Raashiduun na wafuasi wao inahitaji kusomwa kwa undani. Baadaye, elimu hii inaweza kuwakilishwa kwa wale ambao kazi yao ni kutengeneza sheria na kutoa hukumu ili kujibu mahitaji ya jamii ya Waislamu ya kisasa.

vii)             Ni lazima kuwa na mapenzi ya kuelewa malengo na madhumuni ya Shari’ah, na kuliendeleza somo hili kwenye masuala haya, kwa kuweka kanuni na miongozo.

 

 

Na Allaah Ndie Mtoaji wa Tawfiyq (ya Mafanikio na Khayr).



[70] Sababu nyingine ni ule uonekano kwamba mwanazuoni anajaribu Kumuaguwa Mtukufu “kwa mara ya pili”.

[71] Sehemu ya kazi hii imehaririwa na mwanafunzi kwa kutunikiwa uchunguzi wa shahada ya pili (Master’s thesis); na anakifanyia uhariri sehemu iliyobaki kwa kutunikiwa shahada ya tatu (Doctoral).

[72] Angalia Ibn Khalduun, Al-Muqaddimah, III, uk. 1163-64.

[73] An-Nashshar, Manaahij al-Bahth, uk. 55.

[74] Angalia Musallam ath-Thubuut na fafanuzi zake zikiambatana na kitabu cha al-Ghazzaaliy al-Mustaswfa, I, uk. 9-10. Mwandishi alikana kwamba dhana zilikuwa kama hizi, na kudai kwamba nafasi ya dhana kwenye uhusiano wa yote, hiyo Uswuul al-Fiqhi na filosofia ulikuwa sawa. Inawezekana ameathiriwa na mawazo kwamba dhana ni kiwango cha sayansi zote.

[75] Angalia Sura ya Kwanza ya kazi hii.

[76] Angalia ar-Raazi, Manaaqib ash-Shaafi’iy, uk. 98, na an-Nashshaar, Manaahij al-Bahth, uk. 55.

[77] Jina la Fiqh “Mpya” la kazi ya al-Imaam ash-Shaafi’y kwenye kazi yake kisheria limetolewa baada ya kuishi Misr. Hakika, kazi hii inawakilisha fikra zake zilizobobea kutokana na kipindi kirefu cha masomo yake chini ya mafunzo yote ya fikra za sheria za madhehebu ya ki-Maalik na ki-Hanafi.

[78] Angalia Mustafa ‘Abd ar-Razzaaq, al-Imaam ash-Shaafi’iy, uk. 45

[79] Angalia ad-Dahlaawi, Al-Insaaf na Abuu Zahrah, Abuu Haniyfah, uk. 223.

[80] Angalia Taariykh Baghdaad, Juzuu ya XXXI, uk. 368, al-Intiqa’, uk. 142, na Mashaayikh Balkh al-Hanafiyyah, uk. 190.

[81] Angalia as-Samarqandi, Miizaan al-Uswuul, I, uk. 52; Taaqi’ ad-Diyn al-Ghazzi, at-Twabaqaat as-Saniyah, I, uk. 43 na Mashaayikh Balkh, uk. 193.

[82] Rudia rejeo (footnotes) nambari 81.

[83] Angalia Muhammad Yuusuf Muusa, Taarikh al-Fiqh, uk. 160.

[84] Angalia al-Khawarizmi, Mafaatih al-‘Uluum, Juzuu ya VI, VIII; na Ibn Khalduun, Al-Muqaddimah, III, uk. 1125-1128, 1161-1166.

[85] Angalia Miftaah as-Sa’adah.

[86] Angalia al-Ghazzaaliy; al-Mustaswfa, Juzuu ya Kwanza, uk. 3 na al-Mankhuul, pia Shifa’ al-Ghaliyl fiy Bayaan ash-Shibk wa al-Malkhiyl, Maswaalih at-Ta’liyl, na Tahdhiyb al-Uswuul, vyote ni vitabu muhimu kwenye Uswuul.

[87] Msemo maarufu unaonasibishwa na Khalifyah ‘Umar bin al-Khatwwaab.

Share