Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (رحمه الله) Mwanachuoni Wa Wanachuoni

 

 

 

Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah – Mwanachuoni Wa Wanachuoni

 

 

 

Mujaahid, Mufassir, Muhaddith, Faqiyh, Mujaddid (Muhuishaji Wa Diyn) ‘Aalim Al-‘Allaamah, Bahari Ya Elimu, Aliyebobea Katika Elimu Zote, Mwanachuoni Aliyepigana Jihaad, Baba Wa Wanachuoni, Hazina Ya Elimu Ya Nadra Kutokea, Ensaiklopidia (Encyclopedia) Ya Aina Yake

 

 

Abu ‘Abdillaah Muhammad Baawaziyr

 

 

 

 

 

 

 

Share

01-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Shukurani

 

01-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Shukrani

 

Alhidaaya.com

 

Natoa shukurani zangu nyingi kwa kila aliyechangia kazi hii kwa njia moja au nyingine.

 

Namuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Awamiminie wote khayr nyingi na baraka katika maisha yao na Awaruzuku wao na sisi Husnul-Khaatimah.

 

Share

02-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Faharisi: Yaliyomo: - Mwanachuoni Wa Wanachuoni

 

Alhidaaya.com

YALIYOMO

 

 

SURA YA 1: UTANGULIZI

 

 

 

 

 

SURA YA 2: MAISHA YA AWALI

 

Kuzaliwa Kwake na Utotoni Mwake

Malezi yake

Ibn Taymiyyah: Mtoto Mwenye Kipaji cha Akili

Kipaji cha Kumbukumbu cha Hali ya Juu

 

 

 

 

SURA YA 3: MAISHA YAKE YA UCHAJI ALLAAH

 

'Ibaadah Zake

Zuhd Yake

 

 

 

 

SURA YA 4: ELIMU YA KITABU CHA MAARIFA YOTE

 

 

Elimu Yake Na Kumbukumbu Nzuri Kabisa

Al-’Aqiydah Al-Waasitwiyyah

Mchango Wake Kwenye Fiqh Na Uswuwl Yake

 

 

 

 

SURA YA 5: ELIMU

 

 

Waalimu Wake

Wanafunzi Wake

Maandiko Yake

 

 

 

 

SURA YA 6: ‘AQIYDAH, MANHAJ NA UPINZANI

 

 

‘Aqiydah Na Manhaj Yake

Jibu kwa Wale Wanaodai Kwamba Alikuwa ni Mwenye Elimu Ya Diyn Isiyostaarabika 

 

 

 

 

SURA YA 7: JIHAAD, MITIHANI NA KIFO

 

 

Jihaad Yake

Jihaad Yake Katika Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu

Jihaad yake dhidi ya Wazushi na Madhehebu Potofu

Jihaada yake dhidi ya Wakiristo na Maraafidhah

a.       Al-Jawaab Asw-Swahiyh

b.       Minhaaj As-Sunnah

Jihaad yake dhidi ya Matartar

Mitihani na Kufungwa kwa Ibn Taymiyyah

Kifo chake, Allaah Amshushie Rahmah Zake juu yake

 

 

 

 

SURA YA 8: HADHI NA CHEO

 

 

Mhuishaji

Allaah Alimfanya Yeye Kuwa ni Mtu wa Darja ya Juu na Mpambanuzi wa Ukweli na Uongo 

Hadhi Yake Miongoni mwa Wanachuoni wa Enzi Zake

Namna Wanachuoni Walivyomsifu

 

 

 

 

HITIMISHO

 

 

 

 

MAREJEO

 

Vyanzo Vikuu

Vyanzo Vidogo

 

 

Share

03-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya 1: Utangulizi

 

03-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya 1: Utangulizi

 

Alhidaaya.com

 

 

Sura Ya 1: Utangulizi

 

Hakuna shaka yoyote kwamba, hakika shukrani zote zinamstahikia Allaah. Tunamhimidi, tunaomba msaada Kwake, na tunaomba maghfirah. Tunaomba hifadhi kwake Allaah kutokana na maovu ya nafsi zetu, na makosa ya matendo yetu. Yeyote Allaah Anayemuongoza, hakuna wa kumpotosha, na yeyote Allaah Anayempotosha, hakuna wa kumuongoa. Ninashuhudia pia kwamba hakuna yeyote anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allaah, na ninashuhudia kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mjumbe na Nabiy Wake.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) anasema:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٠٢﴾

Enyi mlioamini! Mcheni Allaah kama ipasavyo kumcha; wala msife isipokuwa mmekwishakuwa Waislamu kamili[Aal 'Imraan: 102]

 

Pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) anasema:

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا ﴿١﴾

Enyi watu! Mcheni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Aadam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawwaa) na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume na wanawake wengi. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana (haki zenu kwa kuunga) undugu. Hakika Allaah ni Mwenye kuwachunga daima. [ An-Nisaa: 1]

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٧٠﴾ يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا ﴿٧١﴾

Enyi walioamini! Mcheni Allaah na semeni kauli nyofu ya haki.Atakutengenezeeni ‘amali zenu, na Atakughufurieni madhambi yenu; na anayemtii Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amefanikiwa mafaniko adhimu. [Al-Ahzaab: 70-71]

 

Kwa hakika, maneno bora ya kweli ni Maneno ya Allaah, na uongofu bora ni uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Mambo maovu kabisa ni yale ya kuzusha, na kwa kila jambo jipya lililoanzishwa ni uzushi, na kwa kila uzushi ni upotofu, na upotofu unapelekea Motoni.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Kwa hakika, Wanachuoni ni warithi wa Rusuli, na Manabiy hawakuacha nyuma dinaar wala dirham kurithiwa. Isipokuwa, wameacha nyuma elimu ili kuweza kurithiwa, na yeyote anayechukua kutoka humo amepata fungu kubwa mno.” [1]

 

"Ilmu hii (Diyn) itabebwa na watu wenye kuaminika katika kila kizazi. Wakizikataa tahriyf (madai ya kizushi) ya wale wanaovuka mipaka, madai ya uongo ya waongo, na ta-awiyl (upinduaji tafsiri) za wajinga." [2]

 

"Allaah Atamuinua katika jamii hii mwishoni mwa kila miaka mia moja mtu ambaye ataihuisha Diyn yake." [3]

 

Historia ya Uislamu inasimama kama ni shahidi wa Wanachuoni wengi wakubwa wakubwa, watengenezaji na waitaji wa njia ya Allaah; wale ambao wamefuata nyayo za Salafus-Swaalih (wema waliotangulia) katika iymaan na matendo, katika kumuitikia Allaah na kuweka vipaumbele kwenye maisha; katika ushujaa na ujasiri, katika hatari na jitihada na katika kujitoa muhanga wa maisha yao yote kwa moyo wote kwa ajili ya shughuli ambazo ni faida kwa ajili ya siku ya Qiyaamah. Miongoni mwa wenye sifa hizi bora na walio juu ni al-Allaamah, Al-Imaam, Shaykh Al-Islam Taqiyud-Diyn Ahmad Ibn Taymiyyah – ambaye kumbukumbu za maisha yake zinaweza kufikia kurasa nyingi za historia ya Kiislamu zikiwa na mafanikio ya milele na hamasa zisizo na mpaka.

 

Ibn Taymiyyah alikuwa ni Mwanachuoni mkubwa ambaye alikuwa mweledi kwenye nyanja nyingi za elimu ya Kiislamu na aliyeishi ndani ya kipindi kiovu cha kisiasa, kijamii na kidini. Ndani ya kipindi chake, taifa la Waislamu lilikabiliana na vitisho vingi; vikiwemo vya ndani na nje – vitisho vilivyo vibaya zaidi ni:

 

·

·    Uvamizi wa jeshi la msalaba kutoka magharibi.

 

·   Uhaini wa Fwaatimiyah (Mashia) katika kusuhubiana na jeshi la msalaba dhidi ya taifa la Kiislamu.

 

·    Unyanyasaji wa Tartar kutoka mashariki, na mauaji yao na ufisadi usio na hisia yoyote.

 

·    Ufisadi wa wafalme na watawala, na kujiweka mbali kwao na Uislamu.

 

·    Ueneaji wa upofu katika kufuata Madh-hab uliosababisha ugawaji wa matabaka makubwa.

 

·   Ueneaji wa imani za kishirikina miongoni mwa Waislamu uliotokana na jitihada za wazushi na wanaojinufaisha nafsi zao kutoka miongoni mwa Mashia (Raafidhwah), Masufi na Mabaatwini.

 

Ilikuwa ndani ya kipindi hichi cha mashaka mengi ambapo Allaah alimpeleka Ibn Taymiyyah (Allaah Amrehemu) kusuguana na changamoto hizi na kwa ajili ya kuihami Diyn safi dhidi ya mawimbi makubwa ya makosa yasiyoeleweka, ukafiri, uzushi na mafundisho yasiyopatikana ndani ya Diyn.

 

Jumuiya nyingi zinazotaka mabadiliko na wale wenye fikra njema waliathiriwa na Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah, na walimshukuru na kwa wazi wazi walieleza hisia zao za shukrani kwa kazi zake. Wengi wao kwa namna moja ama nyengine wamechangia elimu zao au misimamo ya mienendo yao kwa hoja za mabadiliko zilizotolewa na Ibn Taymiyyah. Hata hivyo, hawawezi kuwa sahihi kudai kwamba walikuwa sawa sawa na Shaykh al-Islaam kwa sababu hata kwamba, mienendo hii ama wafikiriaji hawa wataona sababu ya msingi pamoja na Shaykh al-Islaam ndani ya baadhi ya mwenendo wa maisha na tabia zake, wataenda nae kinyume katika njia zake za msingi.

 

Lengo la Da’wah na jitihada za Ibn Taymiyyah lilielekezwa kwa kuanzisha Tawhiyd na kukana 'ibaadah yoyote isiyokuwa ya Allaah. Ingawa aliandika kwa mapana kwenye mada kubwa mbali mbali, zote hizi zilikuwa ni ndogo tu katika kuanzisha 'ibaadah ya Allaah. Hivyo, jumuiya za kisiasa za leo ambazo zinafanya kwamba uanzishwaji wa dhana ya ‘Taifa la Kiislamu’ kama kwamba ndio fanikio lao kuu, hali ya kuwa wanaamini kwamba wito wa kuanzisha 'ibaadah safi kwa ajili ya Allaah kuwa ni kikwazo, hawawezi abadan kuwa na usulubu wa mwenendo wa Ibn Taymiyyah.

 

Ibn Taymiyyah kwa hakika aliwaita watu kwa uwazi katika kupitia nafasi za Madhaahib mbali mbali na usahihi wa kutegemea Ijtihaad inapohitajiwa. Hili lilikuwa na lengo kwamba ufuataji upofu wa Madhahebu hautakuwa ndio kikwazo cha kurejea nyuma katika hali ya awali na ufuataji ambao utakuwa karibu na ushahidi. Da’wah yake ilipigana kurejea nyuma katika elimu ya Salaf, Waislamu waongofu siku ambazo Uislamu ulikuwa huru na ushirikina na uzushi.

 

Iwapo mfikiriaji mpya wa enzi za leo ataona sababu kuu za Ibn Taymiyyah kukana maamuzi ya upofu dhidi ya Madhehebu mbali mbali, lakini tu akaamua kulirudisha hili kwa kitu kiovu zaidi kama vile tafsiri zake binafsi au dhana za kisasa au mfano wa hizo; basi hatoweza kudai usulubu katika mwenendo wa Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah ambaye wito wake mkuu ulikuwa ni kuwarudisha watu nyuma kuelewa (misimamo ya) Salaf.

 

Vivyo hivyo, Shaykh al-Islaam alifuata njia ya Salaf katika kuwalingania viongozi Waislamu hata kama ni watendaji dhambi. Pale Wa-Tartar walipovamia Shaam,[4] Ibn Taymiyyah aliwaita watawala wa enzi zake na Waislamu kwa ujumla kusimama dhidi ya tukio hilo na kupigana nao. Ingawa hata hivyo Wa-Tartar ki-nje nje walitamka shahada, Ibn Taymiyyah aliwatambua kama ni watu wasioamini kwa sababu ya ufuataji wao wa moja kwa moja kwenye sheria za Genghis Khan Al-Yasiq, na pia kutoipa thamani kwa vyote – Shari’ah na heshima ya maisha ya Kiislamu.

 

Iwapo mtu hivi leo ataunganisha miambaano (mapengo) baina ya Wa-Tartar na baadhi ya watawala Waislamu wa wakati wa leo bila ya kutilia maanani sababu kuu, masharti na kutenda matendo ambayo yanasababisha ufisadi ndani ya ardhi na kumwagika damu; basi mtu huyo anatenda kinyume na mafundisho ya Shaykh Al-Islaam wala hawezi kujifakharisha mwenendo wake katika njia ya Ibn Taymiyyah.

 

Shaykh al-Islaam aliisimamisha bendera ya imani na elimu ya Ahlus-Sunnah ndani ya maisha yake, kipindi ambacho ndani yake kilikuwa kimejaa uzushi, upotofu, ufisadi uliotapakaa na bado alikuwa na hamasa. Jitihada zake mbele ya uso wa mashaka, msimamo wake mbele ya ukweli, subra zake chini ya mitihani na matumaini yake kwa mwisho mwema; kuna mafunzo mengi ndani yake kwa mwanafunzi wa maarifa ya uswuwl (jurisprudence) na mlinganiaji katika njia ya Allaah.

 


[1] Kipande cha sehemu refu ya Hadiyth iliyosimuliwa na Abu Daawuwd (3641 & 3642), at-Tirmidhiy (2682), Ibn Maajah (223), na Ibn Hibbaan (88), na al-Albaaniy akaithibitisha kwamba ni sahihi ndani ya kitabu chake cha Sahihy at-Targhiyb wa-Tarhiyb (70).

[2] Imesimuliwa na al-Bayhaqiy na kusahihishwa na Shaykh al-Albaaniy ndani ya Mishkaati, namba 248.

[3] Abu Daawuwd (3/4278), al-Haakim, at-Twabaraaniy ndani ya al-Awsatw. Imesahihishwa na al-Albaaniy ndani ya as-Swahiyhah (2/150)] 

[4] Jina la kale linalowakilisha maeneo ya Syria, Jordan, Palestina na Lebanon.

 

Share

04-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya 2: Maisha Ya Awali

 

 

04- Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya 2: Maisha Ya Awali

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Sura Ya 2: Maisha Ya Awali

 

 

Kuzaliwa Kwake Na Utotoni Mwake

 

 

Shaykh al-Islaam, Taqiyud-Diyn Abu al-‘Abbaas Ahmad bin Shihaab ad-Diyn Abu al-Mahaasin ‘Abdul-Haliym bin Majdud-Diyn Abi al-Barakaat ‘Abdus-Salaam bin ‘Abdillaah bin Abi al-Qaasim Muhammad bin al-Khidhwr bin Muhammad bin al-Khidhwr bin ‘Aliyy bin ‘Abdillaah bin Taymiyyah, alizaliwa mnamo siku ya Jumatatu ya mwezi 10 ya Rabiy’ al-Awwal mwaka 661 Hijriyyah sawa na tarehe 22/Januari/1263 Miylaadiyyah sehemu za Harraan[1] kwenye familia maarufu ya watu wa Diyn.

 

 

Babu yake, aitwaye Abu al-Barakaat Majdud-Diyn Ibn Taymiyyah (amefariki mwaka 653 H/1255 M) alikuwa ni mwalimu maarufu wa madhehebu ya Kihanbali na mwenendo wake wa Muntaqaa al-Akhbaar (yaani uchaguzi wa misemo ya Kitume) ambao unazipa sifa Ahaadiyth ambazo zimeegemezwa na Shari’ah za Kiislamu, hadi hii leo unatambulika kwamba ni kazi muhimu mno. Vivyo hiyo, mafanikio ya kiuanachuoni ya baba wa Ibn Taymiyyah, Shihaabud-Diyn ‘Abdul-Haliym Ibn Taymiyyah (amefariki mwaka 682 H/1284 M) yalienea kwa mapana.

 

 

Huu ulikuwa ni wakati ambapo magenge ya Wa-Tartar chini ya Hulagu Khaan walikuwa wakisumbua ulimwengu wa Uislamu kwa mateso yao maovu yanayoendelea katika uuaji. Ibn Taymiyyah alikuwa na umri wa miaka saba pale Wa-Tartar walipoanzisha uvamizi wao Harraan. Hapo hapo, wakazi waliiacha Harraan kwa kutafuta makazi sehemu nyengine. Familia ya Ibn Taymiyyah ilielekea Damascus mnamo mwaka 667 H/1268 M; ambayo kipindi hicho ilitawaliwa na Mamluki wa Misri. Ilikuwa ni hapa ambapo baba yake alikhutubia kutoka mimbari ya Msikiti wa Umayyah na alialikwa kusomesha Hadiyth ndani ya Msikiti (huo) na pia kwenye Daarul-Hadiyth ‘As-Sukuriyyah huko Damascus. Mihadhara hii ilihudhuriwa na wanafunzi walio na idadi kubwa na halikadhalika kwa Wanachuoni. Ibn Taymiyyah alifuata nyayo za baba yake ambaye alikuwa ni Mwanachuoni wa masomo ya Kiislamu kwa kujifunza kutoka kwa Wanachuoni wakubwa wa wakati huo, ambao miongoni mwao alikuwa ni mwanamke aliyeitwa kwa jina la Zaynab bint Makkiy akimfundisha (somo la) Hadiyth.

 

 

 

Malezi yake

 

Shaykh al-Islaam, Ibn Taymiyyah alilelewa, kuthaminiwa na kusimamiwa na baba yake. Alipata elimu kutoka kwake na Mashaykh wengine wa enzi zake. Hakujifunga tu mwenyewe na elimu ya wale waliomzunguka, lakini alitilia mkazo kwenye kazi za Wanachuoni waliokuwepo kabla ya wakati wake kwa njia ya kuchunguza na kuhifadhi. Alikuwa na kipaji cha akili na hodari wa kukamata elimu.[2]  Umakini wake wa muda kutoka umri wake wa awali,[3] ambao ulimsaidia kumuongoza maisha yake yote yaliyobakia kujazwa na matendo ya Jihaad, ualimu, uamrishaji mema, ukatazaji maovu, uandishi wa vitabu na barua na kuwajibu wapinzani. Upana na nguvu za athari zake na hoja zake (zilimuathiri) Myahudi kuukubali Uislamu mikononi mwake hali ya kuwa akiwa ni kijana mdogo.

 

 

Alianza kutoa fatwa akiwa na umri wa miaka kumi na tisa[4]  na kuanza kusomesha ndani ya Daar al-Hadiyth as-Sukuriyyah akiwa na umri wa miaka takriban 22 ya umri wake.[5]   Vyanzo vikuu vya elimu vilizunguka kwenye masuala ya sayansi kama vile: Tafsiyr; Sayansi ya Qur-aan; Sunnah; Vitabu sita; Musnad Imaam Ahmad; Sunan ad-Daarimiy; Mu’jam at-Twabaraaniy; Sayansi ya Hadiyth na wasimuliaji; Fiqh na Uswuwl yake; Uswuwl ad-Diyn na vigawanyo vyake; lugha; maandiko; hesabati; historia na mada nyengine kama vile elimu ya nyota, utabibu na ufundi. Ushahidi wa haya unapatikana kwa kuzisoma kazi zake ambazo baadae aliziandika; mada yoyote aliyoichunguza na kuiandika inamuacha msomaji kufikiria kwamba Ibn Taymiyyah alikuwa ni mweledi ndani ya nyanja hiyo.

 

 

 

Ibn Taymiyyah: Mtoto Mwenye Kipaji cha Akili

 

Siku moja, baba yake na familia yake walimwambia ajiunge nao kwenda mapumzikoni lakini ghafla akatokomea asionekane alipokwendea, hivyo ilibidi waende bila yeye. Waliporejea mwishoni mwa siku hiyo, walimlaumu kwa kutokwenda pamoja nao. Akasema, akiashiria kitabu kwenye mkono wake: "Hamjafaidika chochote kutokana na safari yenu, isipokuwa mimi nimehifadhi kitabu chote hichi kipindi mlipoondoka."

 

Alitambulikana kwa sura yake, kipaji chake cha kuhifadhi mambo na uhodari wake ambao uliwashangaza watu wa Damascus na kuwafanya kumstaajabia zaidi na zaidi. Ingawa alikuwa ni mdogo kiumri, umaarufu wake ulifikia maeneo ya jirani. Mara moja, mmoja wa Wanachuoni wa Halab alimtembelea Damascus. Wanachuoni na watu maarufu wa mji huo walikwenda kumlaki. Aliwaambia: "Nimesikia katika baadhi ya vitongoji kwamba kuna mtoto ambaye ni mwepesi wa kuhifadhi kila kitu. Nimekuja hapa ili kumuona."

 

Wakamuongoza huyo mtu kwenda chuo kimoja kidogo ambacho mtoto huyo akienda kuhifadhi Qur-aan. Mwanachuoni wa ki-Halabi akakaa kwa muda hadi huyo mtoto akapita na bao lake kubwa mkononi. Mwanachuoni huyo akamwita, hivyo akaenda kwake. Mwanachuoni akalichukua bao kutoka kwake na kumwambia: “Kaa hapa ewe kijana, na nitakuhadithia baadhi ya simulizi za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili uandike.” Akamsimulia baadhi yake, kisha akamwambia azisome.

 

Kijana akaanza kuzisoma kutoka baoni. Kisha Shaykh akamwambia: “Acha nikusikilize kutoka kwako.” Akaanza kuzirudia simulizi hizo kutoka kichwani mwake namna sawa sawa kama vile anasoma kutoka kwenye bao. Mwanachuoni akamwambia: “Futa hii, ewe kijana.” Akanukuu simulizi zaidi za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia azirudie. Kijana akafanya vile vile kama mwanzo; akazisoma kutoka baoni na kutoka kichwani mwake. Mwanachuoni akasimama na kusema: "Iwapo kijana huyu ataishi zaidi, atakuwa na hadhi kubwa [kuwa ni Mwanachuoni mkubwa]. Hatujapatapo kuona mtu kama huyu hapo kabla." 

 

 

Kipaji cha Kumbukumbu cha Hali ya Juu

 

Imaam Al-Bazzaar[6] alisema: “Rafiki mmoja aliyekuwa muaminifu akimjua aliniambia kwamba pale Shaykh (Rahimahu Allaah) akiwa yungali katikati ya umri wake wa ujana na akitembea kwenda maktaba, huwa anasimamishwa njiani mwake na Yahudi mmoja aliyekuwa akiishi pembezoni mwa barabara ikielekea maktaba. Yahudi huyo huwa anamuuliza masuala ya mambo tofauti, na huwa na uhakika wa masuala yake (kujibiwa vyema) kutokana na uhodari na ushupavu wa akili ya Ibn Taymiyyah. Ibn Taymiyyah humjibu harakaharaka hadi kwamba Yahudi huwa na shauku naye. Mwishowe, pindipo Ibn Taymiyyah akimpita yeye, basi humpatia vipande vya taarifa ambazo zinahakikisha uongo ambao upo dhidi yake (huyo Yahudi). Hili liliendelea hadi akaukubali Uislamu na akawa ni Muislamu mwenye kuufuata Uislamu kwa ukamilifu, na hili ni kutokana na baraka aliyopewa Shaykh tangu katika umri wa ujana.

 

Na tokea kuingia kwenye ujana, aliutumikia muda wake wote akishughulika na jitihada na utendaji, na akiihifadhi Qur-aan yote akiwa mdogo, na kuendelea kwa kusoma na kuhifadhi Hadiyth, Fiqh, na lugha ya Kiarabu hadi akawa mweledi wa masomo yote hayo. Hili lilikuwa linaenda sambamba na umakini wake wa hali ya juu katika kuhudhuria darsa za duara za elimu na kusikiliza simulizi za Hadiyth na Athar. Amesikia vitabu vingi kutoka kwa Wanachuoni tofauti wenye vipaji vya juu.[7] Ama kwa vitabu vikuu vya Uislamu kama vile ‘Musnad’ cha Ahmad, Swahiyh za al-Bukhaariy na Muslim, ‘Jaami’ cha at-Tirmidhiy, 'Sunan' cha Abu Daawuwd as-Sijistaaniy, an-Nasaaiy, Ibn Maajah, na ad-Daaraqutniy (Rahimahumu Allaah); kila kimoja katika hivi vimesimuliwa kwake kwa ukamilifu wake mara kadhaa. Kitabu cha mwanzo alichokihifadhi kwa ghayb katika Hadiyth kilikuwa ni cha al-Humaydi ‘al-Jam’ Bayn asw-Swahiyhayn.’

 

Ni nadra kuwepo kitabu katika nyanja za sayansi ya Uislamu [akawa hajakisoma] isipokuwa kwamba yeye ameshakutana nacho, na Allaah Akambariki kwa uwezo wa kukihifadhi upesi, na kukisahau ni nadra kwake. Mara chache [kuona kwamba] atakutana au kusikia kitu isipokuwa kwamba kimebakia kwenye akili yake, aidha kwa maneno au maana. Ilikuwa kana kwamba vile taaluma kwake imeganda ndani ya nyama yake, damu yake na mwili wake wote. Hakuchukua tu kibubusa vipande vya taaluma kutoka hapa na pale. Isipokuwa, alikuwa na uelewa na maarifa kamili, na alikuwa ni miongoni mwa watu wa juu wenye hadhi ya juu na ubora. Allaah Alimpatia kazi ambayo kikawaida huwa ndio sababu ya kumuharibu mtu mwengine yeyote, [lakini Allaah Akamjaalia] kumuongoza katika utukufu na furaha katika nyanja zote za maisha yake, na kutia athari ya uongozi wake kwa alama zilizo wazi kwa watu wote, hadi kufikia kwamba kila mtu mwenye uelewa mdogo tu kukubali kwamba yeye ni wale ambao kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwakusudia pale aliposema: "Kwa hakika, Allaah humleta katika kila mwanzo wa karne [mtu ambaye] atahuisha masuala ya Diyn kwa Ummah huu."[8]  Kwa vile Allaah Ameihuisha kupitia kwake Shari'ah za Diyn hii ambazo hapo zama za kale zilisahaulika kabisa, na kumfanya kuwa ni ithibati juu ya watu wote wa enzi hizi, na shukrani zote ni za Allaah, Bwana wa ulimwengu wote.[9]

 

 

 

 

 

 

 

 

[1] Imepakana na mpaka wa baina ya Syria ya leo, Uturuki na Iraaq (ambayo sasa ni sehemu ya Uturuki ya kusini-mashariki).

 

[2] Al-'Uquwd ad-Duriyyah, uk. 4, na al-Kawaakib ad-Durriyyah Fiy Manaaqib al-Mujtahid Ibn Taymiyyah cha al-Karmiy al-Hanbaliy, uk.80.

 

[3] Ar-Radd al-Waafir 'alaa man za'ama bi anna man sammaa Ibn Taymiyyah Shaykhul- Islaam Kaafir cha Ibn Naasir ad-Diyn ad-Dimashqiy, uk. 218, na A'yaan al-'Asr 'an Shaykhul-lslaam Ibn Taymiyyah, Siyratuh wa Akhbaaruh 'inda al-Mu'arrikhiyn cha Muhammad bin Swaalih, uk. 49.

 

[4] Sharafud-Diyn al-Maqdasiy (amefariki mwaka 694 H) amempa ruhusa ya kutoa hukumu za kishari'ah. Baadaye akatumia nafasi hii kujisifia, akisema “Nimempatia mimi ruhusa ya kutoa hukumu za kishari'a.” Al-Bidaayah wan-Nihaayah cha Ibn Kathiyr, 13/341, na al-'Uquud ad-Durriyyah, uk. 4

 

[5] Al-'Uquud ad-Durriyyah, uk. 5; al-Bidaayah wan-Nihaayah, 13/303; ar-Radd al-Waafir, uk. 146 na adh-Dhayl 'alaa Twabaqaat al-Hanaabilah cha Ibn Rajab, 2/388.

 

[6] Abu Hafsw ‘Umar bin ‘Aliy al-Bazzaar ambaye alikuwa ni rafiki yake binafsi na swahiba wake, ameandika maisha yake marefu na ya mwanzo kuhusu Ibn Taymiyyah katika kitabu kiitwacho ‘al-A’laam al-’Aliyyah fi Manaaqib Ibn Taymiyyah,’

 

[7] Amesoma kwa zaidi ya Wanachuoni 200. Angalia ‘al-Kawaakib ad-Durriyyah’ (uk. 52)

 

[8] ‘Swahiyh al-Jaami’’ (1874) na ‘as-Silsilah asw-Swahiyhah’ (599)

 

[9] Manaaqib Ibn Taymiyyah, ukurasa wa 7.

Share

05-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya 3: Maisha Yake Ya Taqwa

 

 

05 – Shaykh Al- Islaam Ibn Taymiyyah:  Sura Ya 3: Maisha Yake Ya  Taqwan Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

‘Ibaadah Zake

 

Ibn Taymiyyah alikuwa na ukaribu mno kwa Rabb wake ambao ulidhihiri ndani ya ‘ibaadah zake na utegemezi wake wa hali ya juu Kwake, hivi ndivyo tunavyomsadiki kuwa na hatuziweki sifa za yeyote mbele ya Allaah. Wale ambao wameandika wasifu wake wamejadili umaarufu wake katika ‘ibaadah, utawa, haya, mwenye kujitolea, unyenyekevu na ukarimu.[1]

 

Ibn al-Qayyim anasema kuhusu dhikri za Ibn Taymiyyah kwa Rabb wake: “Nilimsikia Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah, Allaah Amrehemu roho yake, akisema ‘Dhikri kwa moyo ni kama vile maji kwa samaki. Itakuwaje hali ya samaki iwapo itatengana kutokana na maji? …Mara moja nilihudhuria Swalaah ya Alfajr pamoja na Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah, kisha akaketi na kumkumbuka Allaah hadi kukaribia mchana. Kisha akageuka na kuniambia, ‘Hichi ndicho chakula changu cha asubuhi ya mapema, iwapo sitopata kifungua kinywa hichi, nguvu zangu zitaanguka.”[2]

 

Kinachodhihiri zaidi katika ‘ibaadah zake ilikuwa ni utegemezi wake halisi juu ya Rabb wake na imani zake ndani ya amri za Allaah. Mara nyingi pale anapokumbana na aina ngumu za mitihani, alikuwa na uegemezi mkuu mbele ya Rabb wake. Pale habari za kufukuzwa kwake kwenda Alexandria zilipomfikia na alipoambiwa: “Wanapanga kukuua, kukufukuza au kukufunga.” Alijibu: Iwapo wataniua itakuwa ni shahaadah kwangu. Iwapo watanifukuza, itakuwa ni hijrah kwangu; iwapo watanifukuza kwenda Cyprus, nitawalingania watu wake kwa Allaah ili wanisikilize. Iwapo watanifunga, hiyo itakuwa ni sehemu yangu ya kufanya ‘ibaadah zangu.”[3]

 

Ibn al-Qayyim (Rahimahu Allaah) pia anasema: “Alikuwa akisema mara kwa mara kwa unyenyekevu pale anapofungwa, ‘Ee Allaah, nisaidie ili nikukumbuke wewe, niwe mwenye kukushukuru wewe na kukuabudu wewe kisawasawa.’ Na alisema mara moja kuniambia mimi, ‘Yule ambaye amefungwa (kikweli kweli) ni yule ambaye moyo wake umefungwa kwa ajili ya Allaah na aliyependezeshwa mno ni yule ambaye matamanio yake yamemtia utumwani.’ "[4]

 

Al-Imaam al-Bazzaar (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wakati wa usiku, alikuwa akijitenga kutokana na kila mtu, akijifunga pamoja na Rabb wake, akiwa na uendelevu thabiti wa kuisoma Qur-aan tukufu, na kuzirudia ‘ibaadah tofauti za kila siku na za usiku.

 

Pale usiku unapokwisha, atakusanyika na watu kwenye Swalah ya Alfajr, akiswali Swalaah ya Sunnah kabla ya kukutana nao. Pale anapoanza Swalaah, moyo wako utataka kuruka kutoka sehemu yake kwa namna tu anavyoileta Takbiyraatul-Ihraam. Pale anaposoma, atakirefusha kisomo chake, kama ilivyopokewa kwa usahihi namna ya usomaji wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Rukuu yake na utulivu wake, na halikadhalika namna yake ya kuja juu, ni namna kamilifu za namna ilivyopokelewa kwa taratibu za Swalaah ya fardhi. Na hujiachia nafasi vizuri katika kikao chake cha mwanzo cha tashahhud, na huitamka tasliym ya mwanzo kwa sauti ya juu, hadi kufikia kwamba kila mtu aliyehudhuria kuisikia...

...Nikaja kutambua kwamba ni tabia yake kwamba hakuna yeyote atakayezungumza naye baada ya Swalaah ya Alfajr isipokuwa pale kunapokuwepo haja maalumu. Atabakia katika mtindo wa dhikri za Allaah, akijisikiza mwenyewe. Ataendelea kubakia hivyo hivyo hadi jua linapochomoza, na ambapo muda wa kuharamishwa kuswali umekwisha kuondoka.

Wakati wa kukaa kwangu pamoja naye Damascus, huwa natumia baadhi ya siku yangu na muda mwingi wa usiku wangu pamoja naye. Ataniita kuwa pamoja naye, nikikaa pembezoni mwake. Nikisikia yale anayosoma na kuyarudia, na huona akiirudia al-Faatihah’ mara kwa mara nyingine tena, na hutumia muda wake wote baina ya Fajr na jua kuchomoza akifanya hivi. Hivyo, hukaa nikijifikiria, nikiwaza: ni kwanini akisoma Suwraah makhsusi ya Qur-aan akiziacha nyingine? Ghafla, ikaja wazi kwangu – na Allaah ndiye Ajuaye zaidi – kwamba lengo lake katika kufanya hivyo ilikuwa ni kuunganisha pamoja kwa yale anayosoma baina ya yale yaliyopokelewa ndani ya Ahaadiyth na yale ambayo yaliyojadiliwa na Wanachuoni, kwa namna ambayo adhkaar iliyopokelewa ichukue hatamu dhidi ya Qur-aan, ama kinyume chake. Hivyo, aliona kwamba kuirudia ‘al-Faatihah’, huweza kuunganisha baina ya maoni yote, na kuvuna faida za matendo yote, na hili ni kutokana na hoja zake muhimu na uoni wake wa ndani.

 

Baada ya hili, huswali Dhwuhaa, na iwapo anataka kusikiliza Hadiyth kwenye sehemu nyingine, atakimbilia sehemu ile pamoja na yeyote aliyekuwa naye kipindi kile.

 

Ilikuwa ni nadra kwamba kwa mtu yeyote mwenye akili zake timamu anapomuona yeye kutokwenda na kuibusu mikono yake. Hata wafanyabiashara waliokuwa na shughuli nyingi walikuwa na kawaida ya kuacha yale wanayofanya ili kwenda kumsalimia.[5]

 

Iwapo ataona jambo ovu lolote mtaani, atafanya bidii ya kuliondoa, na iwapo atasikia kuna maziko yanafanyika sehemu fulani, atakimbilia kuswalia au kuomba msamaha kwa kuyakosa. Baadhi ya nyakati, huenda baada ya kumaliza kusikiliza Hadiyth kwenye kaburi la aliyefariki na kuliswalia.

 

Mara moja, yeye na swahiba zake walitoka kwenda kuharibu baadhi ya vilabu vya pombe. Wakavunja vyombo vyao, kumwaga ulevi wao, na kuvunja idadi kadhaa ya vinjwaji hivyo. Vilevile, kuna wakati alivunja nguzo kwenye Msikiti hapo Damascus ambayo watu walikuwa wakiiomba baraka kutokana nayo.[6]

 

Baadae, hurejea Msikitini mwake, ambapo hubaki aidha akitoa fataawa kwa watu au akitimiza mahitaji yao hadi inapofika wakati wa kuswali Adhuhr kwa Jamaa’ah. Hutumia baki ya siku yake kwa namna kama hiyo.

 

Darasa zale zilikuwa wazi kwa jamii: kwa wazee, vijana, matajiri, masikini, walio huru, wafungwa, wanaume na wanawake. Alikuwa na mvuto kwa kila mtu anayempita, na kila mtu alikuwa akijisikia kwamba yeye Ibn Taymiyyah anamtumikia zaidi kuliko anavyowatumikia watu wengine waliohudhuria.

 

Kisha huswali Swalaah ya Maghrib na kufuatiliza kwa Swalah za Sunnah kama ambavyo Allaah Anavyomuwezesha. Baadaye, mimi au mtu mwengine yeyote humsomea maandiko yake, na hutufaidisha sisi kwa nukta na maelezo mbali mbali. Hufanya hivi hadi tunaposwali ‘Ishaa, baada ya hapo huendelea kama tulivyokuwa kabla, tukichunguza kwenye nyanja tofauti za elimu. Huwa tunafanya hivi hadi muda mwingi wa usiku unapopita. Wakati wote huu – usiku na mchana – Ibn Taymiyyah mara kwa mara humdhukuru Allaah, akitaja Upweke Wake, na kuomba msamaha Wake.

 

Na kila mara huinua macho yake mbinguni na hatoacha kufanya hivi, kama vile kuna kitu amekiona huko juu kinachoyafanya macho yake yagande huko. Hufanya hivi kwa muda wote ninapokaa pamoja naye.

 

Hivyo, Subhaana-Allaah! Ni kwa namna gani siku hizi zilikuwa ni fupi! Yareti zingelikuwa ni refu! Naapa kwa Allaah, hadi hii leo, hakuna wakati uliotokea ukawa ni wenye kupendezesha zaidi kwangu kuliko muda ninaokaa pamoja naye, na hakuna kipindi nilichoonekana kwenye nafasi bora kama kipindi hicho, na hili halikuwa kwa sababu nyingine isipokuwa ni kheri alizotunikiwa Shaykh (Rahimahu Allaah).

 

Kila wiki, alikuwa akitembelea wagonjwa, haswa wale waliopo hospitalini, na nimearifiwa na zaidi ya mtu mmoja ambaye ukweli wake siutilii shaka kwamba maisha yake yote ya Shaykh yalitumika kwenye mtindo ambao nimeushuhudia na niliouleza hapo juu. Hivyo, ni ‘ibaadah gani, na jihaad gani, iliyo bora kuliko hii?[7]

 

Hivyo, angalia ni kwa namna gani Allaah Amemuongoza Imaam huyu kuepukana na yote isipokuwa yale anayohitajia ndani ya maisha yake. Alizidiwa na mapenzi yake kwa Allaah, na matokeo yake alitunikiwa sifa zote na ubora kinyume na Wanachuoni wa kidunia ambao wanauchagua, kuutafuta, na kuukimbilia. Wanapochagua mazuri yake, wanajifungia mbali kutokana na njia yake ya uongofu, na matokeo yake wanaangukia kinyume chake. Wanaenda kwenye mtindo wa kuchanganyikiwa, kama ambavyo mtu anayetembea kwenye giza, asijue kipi wanachokula wala wanachovaa. Wala hawaelewi lipi wanategemea kufanikiwa kutokana na malengo yao maovu na ya udhalilifu. Wanashindana kwayo, wakifanyia uadui kwa sababu zake, wakiijaza miili yao pamoja nazo, na wakisukuma kila kitu nje ya mioyo yao. Wanategemea zaidi muonekano wao wa nje hali yakuwa mioyo yao imepiga weusi na iliyojaa ufisadi. Wala hawatosheki hadi pale wanapokuwa maadui kwa wale wanaokana na wanaochukizwa na aina hiyo ya maisha.

 

Pale walipomuona Imaam huyu kama ni Mwanachuoni wa Aakhirah – akiachana na tabia zao za kukusanya mazuri ya dunia hii, akijiepusha na yenye kutia shaka, na kukana yale mambo ambayo hayana umuhimu kuruhusiwa – wakaja kuona kwamba mwenendo wake unawaweka wazi na kuwatia aibu. Hivyo, wakazidi choyo kwamba yeye ameonesha sifa za kiroho hali ya kuwa wao walikuwa hawana kitu zaidi ya yale maovu, na wakakusanyika kumvuruga kwa namna itakayokuwa, wakisahau kwamba wao walikuwa ni mbwa mwitu wakati yeye ni simba. Hivyo, Allaah Amemlinda yeye kutokana nao ndani ya matokeo zaidi ya moja, kama ambavyo Anafanya kwa waja Wake wapenzi. Amemlinda yeye kwa kipindi chote cha maisha yake, na kusambaza elimu yake baada ya kifo chake hadi hatamu za Ardhi.

 

 

Zuhd Yake

 

Imaam al-Bazzaar amesema kuhusiana na zuhd ya Shaykh al-Islaam:

 

“Ama kwa zuhd yake kutokana na dunia na marembo yake, Allaah Amefanya hili kuwa ni somo endelevu ndani ya maisha yake tokea wakati wa ujana wake. Rafiki mmoja muaminifu alinisimulia kwamba mwalimu wake aliyemsomesha Qur-aan Ibn Taymiyyah akisema:

 

 “Baba yake ameniambia wakati bado akiwa ni mtoto mdogo: “Nitapendelea kwako wewe kumuhakikishia kwamba iwapo hatoacha kusoma na kuifanyia kazi Qur-aan, nitampatia dirham arobaini kila mwezi.” Hivyo, akanipatia zile dirham arobaini, na kuniambia: “Mpatie yeye. Bado ni kijana, na huwnda akafurahikia na kuongeza hamu yake katika kuhifadhi na kuisoma Qur-aan, na mwambie kwamba atakuwa na kiwango kama hicho cha fedha kila mwezi.” [Hata] Hivyo, Ibn Taymiyyah akakataa kuzikubali, akisema:

 

 “Ee mwalimu wangu, nimemuahidi Allaah kwamba sitokubali aina yoyote ya malipo kwa ajili ya Qur-aan,” na wala hakuzikubali daima. Nikajisemeza kwamba hili haliwezi kutokea isipokuwa kwa kijana ambaye ametengwa na Allaah.

 

Mwalimu huyu amezungumza ukweli, kwani hifadhi na ulinzi wa Allaah ndio uliomkuza yeye kwenye mazuri yote ndani ya maisha yake kutoka mwanzo hadi mwisho. Kila mtu aliyekutana naye – haswa wale waliosuhubiana naye kwa vipindi virefu vya wakati – wanakubali kwamba hawakupata kuona mtu sawa na yeye kwenye zuhd yake ya dunia, hadi kufikia kiwango kwamba alikuwa ni maarufu kwa hili, na hili lilikuja kuwa wazi ndani ya kila moyo wa mtu asikiaye sifa zake, wa mbali na wa karibu. Ukweli kwamba, iwapo utakuwa ni mwenye kumuuliza mtu ambaye akiishi hapa kila siku ambaye hakuwa karibu mno na Shaykh: ‘Ni nani ambaye ameonesha zuhd ya juu ndani ya enzi zetu, na alikuwa ni mwenye ukakamavu wa kukana mambo yasiyo na muhimu ya dunia, na mwenye hamu kubwa ya kuitafuta Aakhirah?’ basi atasema: ‘Sijasikiapo mtu yeyote kama Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah)!’[8]

 

Hakuwa maarufu kwa hili isipokuwa kwa sababu ya kujitolea kwake katika kufanya hivyo. Ni Wanachuoni wangapi tunawashuhudia ambao wameridhika na kiwango kidogo cha dunia walichonacho kuliko alivyokuwa yeye? Hakupatapo kusikilikana akiulizia kuhusu mke mzuri, ama mtumwa wa kike aliye mchangamfu, ama nyumba iliyojengwa vyema, au watumwa watiifu, au bustani za kifakhari, au mnyama mwenye nguvu kwa ajili ya kutembelea, au nguo laini na za kisasa, au nafasi ya uongozi, wala hakupatapo kuzuia dinaar au dirham, wala hakupatapo kuonekana kukimbilia kupata kitu chenye kuruhusika na kisicho na umuhimu. Hili lilikuwa, ingawa kwamba, ukweli upo kuwa wafalme, watawala na wafanya biashara maarufu walikuwa chini ya amri yake, wenye kuyakubali maneno yake, wakiwa tayari kuja karibu naye kadiri wanavyoweza, wakimsifu wazi wazi, na kila mmoja akiwa tayari kushughulikia mahitaji yake ya kifedha.

 

Hivyo, je alikuwa ni sawa na wale ambao wanajihimilishia wenyewe elimu hali ya kuwa hawakuwa ni wenye kutokana na watu wake – wale ambao wanababaishwa na Shaytwaan kwenye kumtumikia yeye katika neno na kitendo? Je huoni kwamba wanaziangalia sifa zao na zake, tabia zao na zake, uchoyo wao katika kushindana dunia na kuachana kabisa kwake na mapambo yake, makimbilio yao katika kukusanya [dunia] kwa kadiri wawezavyo na kimbilio lake yeye kuiepuka, utumilikivu wao kwa watawala na kuendelea kubakia milangoni mwao kinyume na kujitumilikisha watawala kwake yeye, ukosefu wake wa vitisho kutoka kwenye mamlaka na nguvu zao, uwepesi wake wa kuzungumza kwake ukweli mbele yao, na nguvu ambayo atawahutubia wao? Kwa hakika, naapa kwa Allaah! Hata hivyo, wamejinyoa wenyewe – kwa dini yao, sio nywele zao, na mapenzi yao ya dunia yamechukua ndoto zao, na wameibiwa kwa nguvu – kwa elimu zao, sio kwa miliki zao, hadi kufikia kwamba watakimbilia mbali kutokana na wale ambao wamekuja kukiuliza kutokana nao, na hufanya urafiki kwa wale tu ambao watawasaidia kupata zaidi.

 

 

 

 

[1] Al-A'laam al-'Aliyyah, uk. 36-41, 42, 48 & 63 na al-Kawaakib ad-Durriyyah, uk. 83-88.

 

[2] Al-Waabil as-Sayyib cha Ibn al-Qayyim, uk. 60.

 

[3] Naahiyah min Hayaat Shaykhul-Islaam, uk. 30.

 

[4] Al-Waabil as-Sayyib, uk. 61.

 

[5] Hii ni kwa namna ya kwamba walikuwa wakikimbilia kupata barka za kuwa naye karibu na elimu yake, sio kwa sababu alikuwa ni mrithi wa chanzo cha barka.

 

[6] Al-Bidaayah wan-Nihaayah (13/34 na 14/122-123).

 

[7] The Lofty Virtues of Ibn Taymiyyah, ukurasas 15.

 

[8] The Lofty Virtues of Ibn Taymiyyah, ukurasa, 18.

 

 

Share

06-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya 4: Mwenye Elimu Ya Ki-Ensaiklopidia

 

06- Shakhy Al-Islam Ibn Taymiyyah: Sura 4: Mwenye Elimu Ya Ki-Ensaiklopidia

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sura Ya 4: Mwenye Elimu Ya Ki-Ensaikopidia

 

Elimu Yake Na Kumbukumbu Zake Za Ajabu

 

Shaykh al-Islaam alikuwa na elimu kubwa kabisa, hii inajumuisha elimu yake katika sayansi ya Qur-aan Tukufu, uwezo wake wa kuelewa manufaa yake yote katika nyanja zote, na nukta zake muhimu, elimu yake ya kuyaelezea matamko ya Wanachuoni, namna yake ya kuyatumia matamko haya kama ni ushahidi, na hali kadhalika uwezo aliopatiwa na Allaah umemuwezesha kuelezea maajabu yake, uzuri wa Shari’ah Zake, hazina zake zilizo adimu na za kushangaza, miujiza yake ya kilugha, na rehema zake zilizo wazi.

 

Iwapo mtu atakuwa ni mwenye kuzisoma baadhi ya Aayah za Qur-aan Tukufu ndani ya mojawapo ya darsa zake, ataendelea kuzielezea, na darsa yake itamalizia kwa hili. Darsa yake itamalizia kwa kipande kizuri cha siku, na wala hakuwa na mtu maalumu aliyetengwa kwa ajili ya kumsomea Aayah zinazotegemewa kwamba atakuja kujitayarisha [kuzisomesha] nazo. Isipokuwa, mtu yeyote ambaye alikuwa anahudhuria darsa zake atasoma kile kilicho chepesi kwake, na Ibn Taymiyyah baadaye atakuja kukielezea kile kilichosomwa. Kawaida yake huwa hasimami isipokuwa kwa wale waliohudhuria wanapoelewa kwamba yareti isingekuwa kwa uhafifu wa muda, angelipiga mbizi kuelezea katika kila pembe zaidi na zaidi. Hata hivyo, husimama kwa ajili ya kuruhusu wasikilizaji kupumzika. Kwa mfano, ametoa tafsiyr ya:

 

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾

"Sema: "Yeye ni Allaah, Mmoja. [Al-Ikhlaasw: 1]

 

Ambayo ufafanuzi alioutoa umechukua kitabu kizima kikubwa.

 

Pia, tafsiyr yake ya:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

"Ar-Rahmaan; Yuko juu (Istawaa) ya ‘Arsh." [Twaahaa: 5]

 

Iliyojaza taqriban vitabu 35, na imeelezwa kwamba alianza kukusanya tafsiyr ambayo ingelichukua vitabu hamsini kama angeliikamilisha.

 

Ama kwa elimu yake na uoni wake kuhusiana na Sunnah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), matamko yake, matendo, matukio ya maisha, vita, majeshi, miujiza ambayo Allaah Amemtunukia, elimu yake ya kipi kilicho sahihi kilichopokelewa kutoka kwake dhidi ya kile ambacho sio sahihi, hali kadhalika na matamko, matendo, matokeo, na hukumu za kishari’ah za Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum), bidii yao kwa ajili ya Diyn hii, na sifa zao walizotunukiwa kinyume na watu wengine ndani ya Ummah huu – ndani ya yote haya, alikuwa ni mwenye makini zaidi na alikuwa na uzoefu wa hali ya juu, na alikuwa ni mwenye kutumia muda mchache katika kurudia taarifa yoyote anayohitajia katika hili. Katu hatoitaja Hadiyth au fatwa ambayo ataitumia kama ni ushahidi wa kitu isipokuwa kwamba ataifanyia marejeo kwa chanzo chake sahihi ndani ya maandiko ya Kiislamu, au kuonesha iwapo ni Swahiyh au Hasan, n.k., au kutaja jina la Swahaba aliyeisimulia, na ni kwa nadra sana ataulizwa kuhusiana na simulizi isipokuwa tu ataithibitishia usahihi wake.

 

Imaam al-Bazzaar amesema:

"Na yaliyo maajabu zaidi kuhusiana na hili ni kwamba mnamo siku zake za mwanzo za kushitakiwa mjini Misri, alikamatwa na kufungwa jela, hadi kufikia kwamba alikuwa hawezi kuviingia vitabu vyake. Ndani ya kipindi hichi, aliandika vitabu vingi – vidogo na vikubwa – na akaeleza ndani ya vitabu hivyo ni ipi Ahaadiyth, simulizi, matamko ya Swahaba, majina ya Wanachuoni wa Hadiyth, waandishi na kazi zao – na akazielezea kila moja ya hizi kwa kurejea vyanzo vyake sahihi, haswa kwa majina.

 

Pia ametaja majina ya vitabu ndani ya kila simulizi gani imepatikana, hali kadhalika na wapi ndani ya vitabu utavipata. Yote haya yalikuwa safi kabisa moja kwa moja kutoka kwenye kumbukumbu zake, kwani katika wakati huo hakuwa na kitabu hata kimoja pamoja naye kwa ajili ya kutumia kama ni rejeo. Vitabu hivi baadaye vilichapishwa na kuangaliwa tena, na – Shukrani zote ni za Allaah – hakuna hata kosa moja lililoonekana ndani ya kitabu chochote katika hivyo, wala hakukuwa na haja ya kubadili chochote ndani ya vitabu hivyo. Na miongoni mwa vitabu hivi ni ‘as-Swaarim al-Masluul ‘ala Shaatim ar-Rasuul,’[1] na hili ni kutokana na sifa ambazo Allaah – Mtukufu – Amemtunukia mahsusi kwa ajili yake.[2]

 

Na Allaah Amembariki kwa uwezo wa kuelewa tofauti ya mawazo miongoni mwa Wanachuoni, matamko yao, ijtihaad zao ndani ya masuala tofauti, na kipi kimewekewa kumbukumbu (kimerikodiwa) kutokana na maoni yaliyo na nguvu, hafifu, yaliyokubaliwa na yaliyokataliwa kwa kila Mwanachuoni wa kila enzi. Alikuwa na uoni wa ndani kuhusiana na mawazo yao yepi yalikuwa ni sahihi sana karibu na ukweli, na alikuwa pia na uwezo wa kueleza kwa kila Mwanachuoni ni eneo gani alikuja nalo kwa kila wazo. Hali hii ilifikia hadi kwamba iwapo ataulizwa kuhusiana na lolote katika hili, ilikuwa ni kana kwamba kila tamko la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Swahaba wake, na Wanachuoni – kutoka wa mwanzo hadi wa mwisho wao – kulikuwa na sura iliyoganda ndani ya ubongo wake, pamoja naye akichagua anachotaka na kuacha anachotaka. Hili ni jambo ambalo kwa kila aliyekuwa anamuona au akipita kwenye elimu yake na wasiochukuliwa na ujinga au utashi wanakubaliana nalo.

 

Ama kwa vitabu vyake na maandiko yake, ni zaidi ya ninazoweza kutaja au kufikiria mada zake. Ukweli ni kwamba, nina wasiwasi kwamba mtu yeyote anaweza kuzitaja zote, kwani zipo katika nambari, vyenye ukubwa tofauti, na vimetandawaa duniani kote. Ukweli kwamba, hakuna nchi niliyotembelea isipokuwa nimeona moja ya vitabu vyake nchini humo.

 

Baadhi yake vilifikia vitabu kumi na mbili kwa ukubwa, kama vile ‘Talkhiys at-Talbiys ‘ala Asas at-Taqdiys,’ n.k. Baadhi yake vilikuwa na ukubwa wa vitabu saba, kama vile ‘al-Jam’ Bayn al-‘Aql wan-Naql.’[3]  Baadhi yake vina urefu wa vitabu vitano, kama vile ‘Minhaaj al-Istiqaamah wal-I’tidaal.’ Baadhi yake ni vitabu vitatu, kama vile ‘ar-Radd ‘ala an-Naswaara.’ Baadhi yake ni vitabu viwili, kama vile ‘Nikaah al -Muhallal’ na ‘Ibtwaal al-Hayl’ and ‘Sharh al-‘Aqiydah al-Asbahaaniyyah.’ Baadhi yake ni kitabu kimoja tu au chini ya hapo, na hivi ni vingi mno kuweza kuviorodhesha.”[4]

 

 

Al-’Aqiydah Al-Waasitwiyyah

 

Tokeo jengine ambalo linaonesha uwezo wake mkubwa na mpana wa elimu aliyokuwa nayo, yeye mwenyewe, Ibn Taymiyyah amesema:

 

"Jaji mmoja wa Kishafi’i kutoka Waasit (nchini Iraaq) kwa jina la Radhiyud-Diyn al-Waasitwiy, alinitembelea akiwa njiani kuelekea Hajj. Shaykh huyu alikuwa ni mtu mzuri na mwenye imani. Alinielezea hali za watu nchini huko (yaani Iraaq), chini ya Tartar (Wamongoli) waliokuwa na utawala wa kijinga, usio na haki, na upotefu wa imani na elimu.

 

Aliniomba nimwandikie ‘Aqiydah (Elimu ya Imani) kama ni rejeo kwake yeye na familia yake. Lakini nikakataa na kusema:  masuala mengi kuhusiana na ‘Aqiydah yameandikwa. Rejea kwa Wanachuoni wa Sunnah. Hata hivyo, alisisitiza katika ombi lake, akisema: Sitaki ‘Aqiydah yoyote isipokuwa ile utakayoandika. Hivyo nikaandika hii moja kwa ajili yake nikiwa nimeketi mchana mmoja.[5]

 

Kwa mchana mmoja tu aliweza kuandika kitabu kizima cha ‘Aqiydah kutoka kichwani mwake kwa dalili tele ndani yake. Haya ni maajabu ya Mwanachuoni huyu adhimu.

 

Mchango Wake Kwenye Fiqh Na Uswuul Yake

 

Ibn Taymiyyah tokea enzi za utotoni mwake, alikuwa ni mwanafunzi chipukizi na, kama wanaomsifia wakisema, hakuchukua hamu yoyote kwenye michezo na mazoezi [isiyokuwa na maana]. Baadaye, pia, alipokuwa mkubwa, hakurudi nyuma, sio dhihaka wala tamasha iliyochukua akili zake. Hata hivyo, kazi zake zinashuhudia ukweli kwamba alikuwa na elimu kisawasawa kwa aina tofauti za jamii yake ndani ya kipindi chake, tabia zao na mila, ustaarabu wao na hulka na hata starehe zao na ubunifu. Inaonesha kwamba sio tu kwamba alitumia muda wake kama ni Mwanachuoni aliyezikwa na vitabu, lakini pia alizisoma kwa mapana alama za matatizo na jamii ya kisasa [ya wakati huo].

 

Ibn Taymiyyah alikusanya [kwa shida] elimu ya kisekula na sayansi ya Dini ndani ya kipindi chake. Aliweka mkazo mahsusi kwenye lugha ya Kiarabu na akapata uweledi wa sarufi na maneno (lexicology). Sio tu alikielewa vyema kitabu cha Al-Kitaab cha Sibawayh, mamluki mkuu wa sarufi na elimu ya lugha (syntax), lakini aliweza kubainisha makosa yaliyomo ndani ya kitabu hicho pia; aliweza kumkosoa bingwa wa lugha ya Kiarabu maarufu.[6] Uwezo wake kwenye nyanja hii ulithibitisha kwa mapana kuwa na faida kwake baadaye katika kutengeneza kazi zake mwenyewe.

 

Alama safi ya kielimu ilimzunguka Ibn Taymiyyah ambaye, ukiachilia mbali uwezo wa kuhakiki elimu iliyokuwepo wakati wa enzi zake, aliiwasilisha upya ikiwa na dhamana zote na ufasaha inayomfaa mfikiriaji mbunifu. Akiwa na elimu yake ya ndani kwenye Qur-aan na uoni wake wa chini kwenye malengo na azma za ndani katika Shari’ah na kanuni za maarifa ya Shari’ah, Ibn Taymiyyah aliweza kuwasilisha somo lolote analotaka kulielezea, kwa kutumia vyanzo vya kishari’ah na uwezo wake wa kufahamu mambo mengi.

 

Hakuna hata kazi yake moja aliyoitengeneza ambayo mpangilio wake haupo mpana kwamba haiwezi kuridhiwa kama ni rejeo kuu (encyclopaedia) kwenye somo hilo. Majmu’ al-Fataawa inatuonesha sisi kwamba elimu kubwa mno ya uelewa wake katika Shari’ah kwa ujumla wake, na Fiqh kwa mahsusi. Kazi zake zinaunganisha ufahamu wa vitu vingi pamoja na ustadi wa kufikiri kama pia ni chakula cha kuwafikirisha kwa wasomaji.

 

Fasili za kishari’ah na ubunifu wa mawazo ya kishari’ah zilikuwa ni bidii nyengine ambazo nguvu zake Ibn Taymiyyah katika elimu ziliikamata vyema. Akiwa na uelewa makini mzuri katika hili pia, maandiko yake kwenye somo hili unahusisha mijadala kwenye masuala tata ya kishari’ah. Utengenezaji wa maarifa ya kishari’ah wa Ibn Taymiyyah unahusisha Iqtidha’ as-Swiraat al-Mustaqiym kikiwa na mjumuiko wa vitabu vingi vya mawazo ya kishari’ah na idadi kadhaa ya makala ndogo ndogo kama vile Al-Qiyaas na Minhaaj al-Wusuul ilaa ‘Ilm al-Usuul.

 

Kazi zinazohusiana na ukusanyaji wa misingi ya kishari’ah ya madhehebu tofauti ya kishari’ah yalikaribia kukamilika wakati wa Ibn Taymiyyah. Hata hivyo, alipitia hoja tofauti akiwa na fikra kamili na ustadi wa hali ya juu na ambayo yalikuwa na athari ya kutoa nguvu mpya kabisa kwenye mfumo wa kishari’ah. Katika kuelezea mawazo yake ya kishari’ah, bidii yenye kuendelea ya Ibn Taymiyyah ilikuwa ni kutoa muongozo wa mahitajio ya mabadiliko kwa kuegemea Sunnah. Mawazo ya kishari’ah na hali kadhalika kanuni zinazozitawala zilizoelezewa na Ibn Taymiyyah zimehifadhiwa kwenye vitabu chini ya jina la Fataawa Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah (Majmu’ al-Fataawa li Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah).[7]

 

  

 


 

[1] Inatafsirika kama ni 'Upanga Usio na Ukali katika Kumtusi Nabiy(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)'

[2] Kitabu ambacho kina zaidi ya Ahaadiyth 250, Athar 100, utajo wa zaidi ya wasifu wa watu maarufu 600 kutoka historia ya Ahlus-Sunnah wal-Jama’ah, na mkusanyo wa taarifa kutoka kwenye rejeo zaidi ya arobaini – zote kutoka kwenye kumbukumbu zake, na kitabu chote kimeandikwa katika kujibu tukio moja tu la ambalo Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah (Allaah Amrehemu) alimsikia Mkiristo akimtukana Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)!

[3] Maarufu kinajulikana kama ni ‘Dar’ Ta’arudh al-‘Aql wan-Naql’ na ‘Muwafaqat Swahiyh al-Manquul li Swariyh al-Ma’quul,’ na kinajadili uhusiano baina ya hoja na Wahyi.

[4] The Lofty Virtues of Ibn Taymiyyah, ukurasa, 9.

[5] Majmu’ Fatawa Ibn Taymiyyah, Kitabu cha 8, ukurasa 164

[6] Al-Kawaakib ad-Duriyyah, uk.2

[7] Vitabu hivi ambavyo vinafikia 37, kwa hakika ni rejeo kuu (encyclopaedia) katika Maarifa ya Shari’ah za Kiislamu.

 

Share

07-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya 5: Elimu

 

07-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya 5: Elimu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sura Ya 5: Elimu

 

 

 

Walimu Wake

 

Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah amesoma chini ya idadi kubwa ya Wanachuoni wakuu na yeye mwenyewe ametaja idadi yao kama ilivyopokelewa na Imaam adh-Dhahabiy moja moja kutoka kwake.[1] Mtungo huu wa walimu unajumuisha Wanachuoni wakiume arobaini na Wanachuoni wakike wanne.

 

Jumla ya idadi ya Wanachuoni ambao amepata elimu kutoka kwao inazidi mia mbili.

 

Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya walimu wake:[2]

 

-Abu al-'Abbaas Ahmad Ibn 'Abdid-Daa'im al-Maqdasiy

 

 

-Abu Muhammad ‘Abdur-Rahmaan Ibn Muhammad Ibn Ahmad Ibn Qudaamah Al-Maqdasiy

 

 

-Abu al-‘Abbaas Ahmad Ibn Ahmad Ibn Ni’mah Al-Maqdasiy

 

 

-Baba yake, Abu al-Mahaasin ‘Abdul-Haliym Ibn ‘Abdis-Salaam Ibn Taymiyyah

 

 

-Shangazi yake kwa upande wa baba, Sitt ad-Daar bint 'Abdis-Salaam Ibn Taymiyyah

 

 

-Abu al-Barakaat al-Munajjiy Ibn ‘Uthmaan at-Tanuukhiy ad-Dimashqiy

 

 

-Abu ‘Abdillaah Muhammad Ibn ‘Abdil-Qawiy Ibn Badraan al-Maqdasiy al-Mardawiy

 

 

-Ahmad Ibn Ibraahiym Ibn ‘Abdil-Ghaniy as-Saruujiy al-Hanafiy

 

 

-Abu al-Hasan ‘Aliy Ibn Ahmad Ibn as-Sa’adiy al-Maqdasiy as-Swaalihiy

 

 

-Abu Zakariya Yahya Ibn ‘Abdir-Rahmaan Ibn Najm al-Hanbaliy al-Ansaariy

 

 

-Abu Zakariya Yahya Ibn Abi Mansuur Ibn Raafi’ Ibn ‘Aliy al-Haraaniy Ibn as-Sayrafiy

 

 

 

-Abu Bakr Ibn Muhammad Ibn Abi Bakr Ibn al-Wasi’ al-Harawiy ad-Dimashqiy

 

 

-Abu al-‘Abbaas Ahmad Ibn Abi al-Khayr Salaamah Ibn Ibraahiym Ibn al-Haddaad ad-Dimashqiy

 

 

-Abu Muhammad al-Qaasim Ibn ‘Aliy Ibn Abi Bakr Ibn Qaasim Ibn Ghaniymah al-Irbily

 

 

-Abu al-Ghanaaim al-Muslim Ibn Muhammad Ibn al-Muslim Ibn ‘Alaan al-Qays ad-Dimashqiy

 

 

-Abu al-‘Abbaas Ahmad Ibn Shaybaan Ibn Haydar ash-Shaybaaniy

 

 

-Abu Hafsw ‘Umar Ibn ‘Abdil-Mun’im  Ibn al-Qawaas ad-Dimashqiy

 

 

-Abu Nasr 'Abdul-'Aziyz Ibn 'Abdil-Mun'im Ibn al-Khudhr Ibn Shibl Ibn ‘Abdil-Haarithy

 

 

-As-Swaalih al-Musnid Ibn Muhammad Ibn Badr Ibn Muhammad Ibn Ya’iysh al-Jazariy

 

 

-Abu Yahya Ismaa’iyl Ibn Abi ‘Abdillaah Ibn Hammaad Ibn ‘Abdil-Kariym al-‘Asqalaaniy

 

 

 

-Abu Is-haaq Ibn Ibraahiym Ibn Ahmad Ibn Abi al-Faraj Ibn Abi Taahir Ibn Muhammad Ibn Nasr

 

 

-Abu Is-haaq Ibraahiym Ibn Ahmad Ibn Ismaa’iyl Ibn Faaris at-Tamiymiy as-Sa’adiy

 

 

-Ahmad Ibn Abi Bakr Ibn Sulaymaan al-Waa’idh Ibn al-Hamawiy Abu al-‘Abbaas ad-Dimashqiy

 

 

-Abu ‘Abdillaah Muhammad Ibn Ismaa’iyl Ibn ‘Uthmaan Ibn al-Mudhafar Ibn ‘Asaakir ad-Dimashqiy ash-Shaafi’iy

 

 

-Abu Muhammad ‘Abdur-Rahmaan Ibn Abi as-Sa’r  Ibn as-Sayyid Ibn As-Saani’ al-Ansaariy

 

 

 

-Abu al-‘Izz Yuusuf Ibn Ya’aquub Ibn Muhammad Ibn ‘Aliy al-Mujaawir ash-Shaybaaniy

 

 

-Abu Is-haaq Ibraahiym Ibn Ismaa’iyl Ibn Ibraahiym Ibn Yahya Ibn ‘Alawiy Ibn al-Husayn al-Qurashiy al-Hanafiy

 

 

-Abu Muhammad Ismaa'iyl Ibn Ibraahiym at-Tanuukhiy 

 

 

-Abu al-'Abbaas al-Mu'ammil Ibn Muhammad al-Baalisiy

 

 

-Abu 'Abdillaah Muhammad Ibn Abi Bakr Ibn Sulaymaan al-'Aamiriy

 

 

-Abu al-Faraj 'Abdur-Rahmaan Ibn Sulaymaan al-Baghdaadiy

 

 

- Sharafud-Diyn al-Maqdasiy, Ahmad Ibn Ahmad ash-Shaafi'iy

 

 

-Muhammad Ibn 'Abdil-Qawiy al-Maqdasiy

 

 

-Taqiyud-Diyn al-Waasitiy, Ibraahiym Ibn 'Aliy as-Swaalihiy al-Hanbaliy

 

 

 

Wanafunzi Wake

 

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah alikuwa na wanafunzi wengi na ambao waliathirika naye kielimu, miongoni mwa wanafunzi wake walikuwa ni[3]:

 

 

 

-Ibn Qayyim al-Jawziyyah, Muhammad Ibn Abi Bakr Ibn Ayyuub az-Zar’iy

 

-Adh-Dhahabi, Muhammad Ibn Ahmad Ibn ‘Uthmaan at-Turkimaniy

 

-Ibn Qudaamah al-Maqdasiy, Muhammad Ibn Ahmad Ibn al-Haadiy

 

-Al-Mizzi, Yuusuf Ibn ‘Abdir-Rahmaan

 

-Ibn Kathiyr, Abu al-Fidaa ‘Imaadud-Diyn Isma’iyl Ibn ‘Umar

 

-Al-Bazzaar, ‘Umar Ibn ‘Aliy

 

-Ibn Muflih, Shamsud-Diyn Abu ‘Abdillaah Muhammad al-Maqdasiy ar-Raaminiy ad-Dimashqiy

 

-Al-Qaasim Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Yuusuf al-Barzaliy al-Ishbiyliy

 

-Abu al-Fat-h Muhammad Ibn Abi ‘Umar Muhammad Ibn Abi Bakr Ibn al-Ya’amariy al-Andalusiy al-Ishbiyliy al-Masry ash-Shafi’iy

 

-Ibn Qudaamah al-Hanbaliy, Ahmad Ibn al-Hasan Ibn ‘Abdillaah Ibn Muhammad Ibn Ahmad

 

-Ibn Abdid-Daaim, Abu ‘Abdillaah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abi Bakr Ibn Ahmad

 

-Ibn al-Waaniy, Muhammad Ibn ash-Shaykh al-Musnid Abi Is-haaq Ibraahiym Ibn Muhammad Ibn Ahmad

 

-Ibn Imaam as-Sakhrah al-Baysaaniy ad-Dimashqiy al-Maqdasiy, Muhammad Ibn Ibraahiym Ibn Muhammad Ibn Abi Bakr Ibn Ibraahiym al-Khazrajiy

 

-Ibn an-Najiyh, Abu ‘Abdillaah Muhammad Ibn ash-Shaykh Sa’d ad-Diyn Abi Muhammad Sa’d-Allaah Ibn ‘Abdil-Ahad Ibn ‘Abdil-Waahid al-Haraaniy

 

-Ibn as-Sayrafiy, Abul-Ma’aliy Muhammad Ibn Taghriyl Ibn Abdillaah al-Khawaarizmiy

 

-As-Saamit, Shamsud-Diyn Abu Bakr Ibn Muhammad Ibn ‘Abdillaah Ibn Ahmad Ibn al-Muhib ‘Abdullaah as-Sa’diy al-Maqdasiy

 

-Ibn Qaadhi al-Jabal, Ahmad Ibn Husayn

 

-Ibn FadhliLlaah al-‘Amri, Ahmad Ibn Yahya

 

-Muhammad Ibn al-Manj, Ibn ‘Uthmaan at-Tanuukhi

 

-Yuusuf Ibn ‘Abdi Mahmuud Ibn ‘Abdis-Salaam al-Batti

 

- Ibn al-Wardi, Zaynud-Diyn ‘Umar

 

-‘Umar al-Harraaniy, Zaynud-Diyn Abu Hafs

 

 

Ibn Hajr al-Asqalaaniy amesema:

 

Kama ingelikuwa hakuna sifa za Shaykh Taqiyud-Diyn isipokuwa kwa mwanafunzi wake Shaykh Shamsud-Diyn Ibn Qayyim al-Jawziyyah, mwandishi wa kazi nyingi, ambazo kote kote kutoka kwa wapinzani na wafuasi wake wamenufaika nazo, hii itakuwa ni angalizo tosha la nafasi yake kubwa (Ibn Taymiyyah). Hii ndio kwa sababu tunaona kujali kwake kwa hali ya juu kwa Ibn Taymiyyah mbele ya mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim ndani ya wasifu wa Ibn al-Qayyim:[4]

 

Mara moja aligundua hamu na shauku kubwa ya elimu kwa wanafunzi wake na hamu yake ya kujitolea kuipata na kuieneza (elimu), akaanza kumlea kwenye nasaha na miongozo ambayo itamsaidia kuzinyanyua akili zake na kuziongeza usimamizi wake madhubuti kama ni Mwanachuoni.

 

Hazina hizi zinatajwa na Ibn al-Qayyim katika sehemu tofauti katika pande mbali mbali za vitabu vyake. Ifuatayo ni baadhi ya mifano:

 

1. Ndani ya Miftaah daar as-sa’adah amesema, “Shaykh al-Islaam (Rahimahu Allaah), ameniambia baada ya kuanza kumtajia utata mmoja kufuatia mwengine, ‘Usiache moyo wake kuwa kama sponji kwa kila utata ambao utakupita, hadi kwamba unainywa yote na unaloweka nayo. Isipokuwa, kuwa kama gilasi gumu; mashaka yanaipita lakini hayakai ndani yake. Hivyo itayaona kwa unadhifu wake na kuyafukuza kwa ugumu wake. Kwa namna nyengine, iwapo utauacha moyo wako kunywa kila utata ambao utakupita wewe, itakuwa ni sehemu ya mapumziko kwa mashaka,’ Au alisema kitu chenye athari sawa na hiyo. Sikuona ushauri wowote ambao umeniletea manufaa makubwa katika kufukuza mashaka kuliko huu.”

 

 

2. Ndani ya Madaarij as-Saalikiyn, amesema, “Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah), ameniambia mara moja, ‘Pale mmoja anaposimama kwenye mitihani na ukosefu wa fedha ukawa hauepukiki, hatokuwa na hamaki inapotokezea hali hiyo, wala hatokuwa na majonzi au kuwa na huzuni kutokana nayo.’[5] Hivyo pale mtu anapokuwa mgonjwa kwa mitihani hiyo na haiachii kumvuruga, inatarajiwa kwamba atanyanyuka kwenye kiwango cha kufikia (utumwa halisi mbele ya Allaah). Roho yake itakuwa na adabu na itakuwa na tegemezi kwa Allaah, na itakuwa mbali na tabia mbovu, hadi mapenzi ya Allaah na moyo wake utalowana na roho yake na miguu yake vyote vitakuwa adilifu mbele ya amri (za Allaah). Katika hali hii, moyo wake utaona hisia kwamba Allaah Yu pamoja naye na Anamsaidia. Kila pigo lake na kila hatua yake itakuwa ni yenye kumfikiria Allaah, sio kwake mwenyewe. Moyo wake utapokea miono ya kiroho iliyo mingi, hadi kufikia kwamba atafurahikia Utukufu wa Allaah, Umiliki wake wa kila kitu, na Upweke wake. Ni katika ufahamu wa sifa hizi tatu kwamba elimu yote na misingi yote inategemezwa.”

 

 

3. Na Ibn Taymiyyah alikuwa akiwanasihi wanafunzi wake kutojihusisha kupita mpaka kwenye mambo yanayoruhusiwa. Ibn al-Qayyim amesema kuhusiana naye, “Siku moja, Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah), aliniambia kuhusiana na mambo yanayoruhusiwa, ‘hii ni kinyume cha (mafanikio ya) nafasi ya juu, hata iwapo kuachana nalo sio sharti la kufikia uokovu,’ au kitu kinachofanana na hicho.” Hivyo mwenye kumtambua (Allaah) ataachana na kila aliwezalo kwenye mambo yanayoruhusiwa, kwa lengo la kujilinda yeye mwenyewe, haswa iwapo hilo linaloruhusiwa ni kikwazo baina ya kinachoruhusiwa na kisichoruhusiwa kishari’ah.

 

 

Maandiko Yake

 

Kazi zake zilizopo sasa za Ibn Taymiyyah ni nyingi kwa idadi, ingawaje ukweli kwamba sehemu ya kazi zake zimeyayuka.

 

Alikuwa ni mwandishi aliye na kasi. Ndugu yake ‘Abdullaah amesema: “Allaah amemtunukia uwezo wa kuandika haraka na alikuwa akiandika kutoka kwenye akili yake bila ya kunukuu (kukopia).” [6] Ibn Taymiyyah alikuwa na karani ambaye alikuwa akinukuu (akitoa kopi) kazi zake kwa sababu ya ukweli kwamba alikuwa akiandika kwa kasi ya ajabu. Kulikuwa na mtu akijulikana kwa jina la ‘Abdullaah Ibn Rashiyq al-Maghrabiy ambaye alikuwa akiandika kazi za Shaykh, Ibn Kathiyr amesema kuhusiana naye: “Alikuwa akiweza kuzitengeneza hati za Shaykh kuliko za Shaykh mwenyewe.” [7] Alikuwa akichukua muda mwingi kupitia kazi zake kama alivyofanya baada ya yeye kutoka jela katika masuala ya talaka – ndani ya mwaka 721H.[8] Baada ya kurejea kwake Shaam ndani ya mwaka 712H, alijitolea muda wake mwingi kuandika kazi refu.[9] Alikuwa akiweka mkazo kwenye maandiko ambayo yametengwa kumsifu yeye;[10] Inaonesha kwamba uharibifu wenye kuendelea kuhusiana na yeye kutoka kwa maadui zake na ubadilishaji wa maneno yake ilikuwa ndio sababu ya hili.

 

Hakuchelewesha kujibu masuala ambayo yalifika kwake na alikuwa mbunifu (wa kuandika vitabu) na aliandika kutoka kwenye akili yake akiwa kifungoni.[11]

 

Baadhi ya kazi (vitabu na maandiko mengine) zake zilikuwa ni[12]:

 

 

-Ibtwaal al-Hiyal

 

-Ikhtiyaraat Shaykh al-Islaam

 

 

-Al-Istighaathah

 

-Al-Istiqaamah

 

-Iqaamat ad-Daliyl ‘alaa Ibtwaal at-Tahliyl

 

-Iqtidhwaa' as-Swiraat al-Mustaqiym Li Mukhaalafah Asw-haab al-Jahiym

 

-Aqsaam al-Qur-aan

 

-Al-Ikliyl fiy at-Tashaabuh wat-Taawiyl

 

-Amthaal al-Qur-aan

 

-Al-Amr bil Ma’ruuf wa an-Nahy ‘anil-Munkar

 

-Al-Iymaan

 

-Baghiyat al-Murtaad

 

-Bayaan Talbiys al-Jahmiyah fiy Taasiys Bida’ihim al-Kalaamiyah

 

-Tahriym as-Simaa’

 

-At-Tuhfah al-‘Iraaqiyah fiy al-A’maal al-Qalbiyah

 

-At-Tadmuriyyah

 

-Ta’arudh al-Hasanaat was Sayi-aat

 

-Ta’liyquh ‘alaa Futuuh al-Ghayb li-‘Abdil-Qaadir al-Kiylaaniy

 

-Tafsiyr Suurah al-Ikhlaas

 

-Tafsiyr Suuratay al-Maw’idhatayn

 

-Tafsiyr Suurah an-Nuur

 

-Tanbiyh ar-Rajul al-‘Aaqil ‘alaa Tamwiyh al-Jadal al-Baatil'

 

-Jawaab Ahl al-‘Ilm wal Iymaan bit-Tahqiyq maa Akhbar bihi Rasuul ar-Rahmaan Min Anna (Qul Huwa Allaahu Ahad Ta’dil Thuluth al-Qur-aan)

 

-Al-Jawaab al-Baahir fiy Zuwaar al-Maqaaabir

 

-Al-Jawaab as-Swahiyh liman baddala Diyn al-Masiyh

 

-Hijaab al-Mar-at wa Libaasuha fiy as-Salaah

 

-Al-Hisbah fiy al-Islaam

 

-Al-Hasanah was Sayi-ah

 

-Haqiyqah as-Swiyaam

 

-Al-Hamaawiyyah al-Kubraa

 

-Ad-Durah al-Mudhiy-ah fiy Fataawa Ibn Taymiyyah (al-Fataawaa al-Masriyah)

 

-Daqaaiq at-Tafsiyr 1-6 mijalada iliyokusanywa na Muhammad as-Sayyid al-Jaliynd

 

-Ar-Radd ‘alaa al-Akhnaaiy fiy Mas-alah az-Ziyaarah

 

-Ar-Radd ‘alaa Taasiys at-Taqdiys lir-Raaziy

 

-Risaalah ilaa Malik Qubrus – ar-Risaalah al-Qubrusiyyah

 

-Risaalah fiy Amraadhw al-Quluub wa Shifaa' uhaa

 

-Suaal fiy Mu’aawiyah Ibn Abi Sufyaan

 

-As-Siyaasah ash-Shar'iyyah li Islaah ar-Ra’iy war Ra’iyah

 

-Sharh Hadiyth Abi Dharr Radhiya Allaahu ‘anhu (Yaa ‘Ibaadiy Ini Haramtu adh-Dhulma ‘alaa Nafsiy)

 

-Sharh Hadiyth ( Innama al-A’maal bin Niyyaat)

 

-Sharh Hadiyth an-Nuzuul

 

-Sharh ‘Aqiydah al-Asfahaniyyah

 

-Sharh al-Muharrir – Ta’aliyquhu ‘alaa Kitaab al-Muharrir fiy al-Fiqh

 

-As-Swaarim al-Masluul 'alaa Shaatim ar-Rasuul

 

-As-Safadiyyah

 

-Al-Furqaan bayna Awliyaa' ar-Rahmaan wa Awliyaa' ash-Shaytaan

 

-Al-Furqaan bayna al-Haqq wa al-Baatil

 

-Fiy Mihnatih bi Misr (Vitabu viwili)

 

-Qaa'idah Jaliylah fiy at-Tawassul wa al-Wasiylah

 

-Qaa’idah Shariyfah fiy al-Mu’jizaat wal Karamaat

 

-Qaa’dah fiy al-Ijma’

 

-Qaa’idah fiy al-Isti’aadhah

 

-Qaa’idah fiy ar-Radd ‘alaa Man Qaala bi Fanaai al-Jannah wan Naar

 

-Qaa’idah fiy al-Mahabah

 

-Qaa'idah fiy Tawhiyd al-Uluuhiyyah

 

-Al-Qaa’dah al-Maraakishiyyah

 

-Al-Maaridiyyah – al-Masaail al-Maaridiyyah

 

-Ma’arij al-Uswuul ‘alaa Anna Uswuul ad-Diyn wa Fur’uahu qad Bayyanaha ar-Rasuul

 

-Muqaddimah fiy Uswuul at-Tafsiyr

 

-Mansak Shaykh al-Islaam

 

-Mandhuumah fiy al-Qadar

 

-Minhaaj us-Sunnah an-Nabawiyyah fiy Naqdh Kalaam ash-Shiy’ah wal Qadariyyah

 

-Muaakhadhah li Ibn Hazm fiy Ijma’

 

-An-Nubuwaat

 

-Ar-Radd 'alaa al-Mantiqiyyiyn

 

-Al-Waasitwah bayna al-Haqq wa al-Khalq

 

-Ar-Radd al-Aqwan 'alaa maa fiy Fusuus al-Hikam

 

-Al-'Aqiydah al-Waasitwiyyah

 

-Al-Wasiyyah as-Sughraa

 

-Al-Wasiyyah al-Kubraa

 

-Daar Ta'aarudh al-'Aql wa an-Naql

 

-Al-Madhwaalim al-Mushtarakah.

 

-Naqd Maraatib al-ljmaa'

 

 

Baadhi ya kazi zake zilizopo hapo juu zimeingizwa ndani ya Majmu’ al-Fataawa, ambacho ni mjumuisho wa maandiko na maamuzi yake yaliyowekwa pamoja na Ibn Qaasim na mwanawe.

 

[1] Majmu’’ al-Fatawa (18/76-121)

[2] Shaykh al-Islaam Ahmad Ibn Taymiyyah Rajul al-Islaah wa ad-Da’wah, uk. 113-124

[3] Shaykh al-Islaam Ahmad Ibn Taymiyyah Rajul al-Islaah wa ad-Da’wah, uk. 139-143

[4] ‘Wasifu wa Imaam Ibn al-Qayyim’ kilichoandikwa na Swalaahud-Diyn ‘Aliy Abdul-Mawjuud, kikafasiriwa na Abdul-Rafi Adewale Imaam na kuchapishwa kwenye mtandao na ‘Abdul-Haq ‘Abdul-Khaaliq

[5] Kilichobaki kinaonekana kuwa ni maneno ya Ibn al-Qayyim mwenyewe akieleza matamko ya Shaykh.

[6] Al-'Uquud ad-Durriyyah, uk. 64.

[7] Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/229.

[8] Al-'Uquud ad-Durriyyah, uk. 327

[9]  Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/67.

[10]  Al-A'laam al-'Aliyyah, uk. 36-41, 42, 4   8 & 63 na al-Kawaakib ad-Durriyyah, uk. 83-88

[11]  Al-Waabil as-Sayyib of Ibn al-Qayyim, uk. 60

 

[12]  Shaykh al-Islaam Ahmad Ibn Taymiyyah Rajul al-Islaah wa ad-Da’wah, uk. 377-380

Share

08-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya 6: 'Aqiydah, Manhaj Na Upinzani

 


Sura Ya 6: ‘Aqiydah, Manhaj Na Upinzani

 

Alhidaaya.com

 

 

 

‘Aqiydah Na Manhaj Yake

 

Ibn Taymiyyah alikana utumiaji wa akili kwa ufahamu wa Asmaa Wa Swifaat (Majina Matukufu na Sifa za Allaah) kwani hiyo haikuwa ni mwenendo bora ulioafanywa na Salaf. Alitoa hoja kwamba Swahaba na vizazi vya mwanzo havikukimbilia hifadhi ya maelezo ya kifilosofia katika ufahamu wa Majina Matukufu na Sifa zake. Aliendelea kutoa hoja kwamba iwapo Salaf wangeliona manufaa yoyote katika kupata hifadhi katika kalaam (hoja za maneno matupu ya kiakili na falsafa) wangelifanya hivyo na wangelihimiza. Hivyo, Ibn Taymiyyah alituhumiwa na wapinzani wake kwamba ni mtu aliyekuwa na elimu ya Dini isiyostaarabika kutokana na msimamo wake katika Majina na Sifa za Allaah.

 

Ukweli ni kwamba, ndani ya kitabu chake ‘Aqiydatul Waasitwiyyah, Ibn Taymiyyah amekana msimamo wa Mushabbihah (wale wanaofananisha uumbaji wa Allaah: wenye elimu ya Dini isiyostaarabika) na wale wanaokaidi, kukana, na kukimbilia hifadhi ya tafsiri za kilahaja na kimaana kwenye Majina na Sifa tukufu. Ametoa hoja kwamba mtindo wa Salaf ni kuchukua njia ya kati na kati baina ya mipaka iliyochupa mpaka katika elimu ya Dini isiyostaarabika na ile ya kukana. Akaendelea kueleza kwamba Salaf wamekubali kwamba Majina yote na Sifa za Allaah bila ya tashbiyh (kuanzisha ufananisho), takyiyf (kuchunguza ni kwa namna “gani” zimegandana na utukufu), ta’twiyl (kukana/kukaidi maana za juu), na bila ya ta-awiyl (kuipa maana ndogo, kugeuza maana halisi).

 

Mara nyingi husimuliwa tokeo maarufu la Maalik Ibn Anas ambaye alimjibu mtu moja kwa moja na kwa maneno machache kabisa ambaye aliuliza: Ni namna gani Allaah alivyo/kuwepo (istiwa) juu ya ‘Arshi? Alijibu kwamba “uibukaji/uwepo” (istiwa) unajulikana, “kivipi” hakutambulikani, “kuwa na imani juu ya hilo” ni lazima, na “kufanya uchunguzi na kuulizia kuhusiana na masuala hayo” ni uzushi wenye kulaumiwa (bid’ah). Hivyo Imaam Malik anakubali maana bora lakini bila ya kulinganisha, wenye kuanzisha unamna gani, na bila ya kutafuta hifadhi ya maana za kitashbihi.

 

Shaykh al-Islaam Ahmad Ibn ‘Abdil-Haliym Ibn Taymiyyah anatambulikana kama ni mmoja katika Mujaddid (waliouhuisha/walioboresha Dini upya baada ya kuingia uharibifu) muhimu sana katika Uislamu. Iwapo jitihada za Mujaddid zinazalisha matunda ndani ya enzi zake na kizazi chake, jitihada za Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah zimeanza kutoa matunda ndani ya enzi zake na zinaendelea kufanya hivyo hadi hii leo na hadi Qiyaamah, Wanachuoni walioathirika na watafutaji wa elimu na makundi ya Kiislamu yenye kutokana na Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah. Wanachuoni wangali wanarejea vitabu vyake katika kuwakana maadui wa Uislamu miongoni mwa Mayahudi na Wakiristo na Madhehebu yanayodai kuwa yanatokana na Uislamu kama vile Maraafidhah (Shia), Khawaarij, Mu’utazilah Huluuliyyah na Jahamiyyah, na madhehebu ya uzushi kama vile Ash’ari’ah (Masufi) na Murji-iah.

 

 

Mafanikio yake ndani ya Nyanja za Fiqh, Hadiyth, tafsiyr na suluuk (njia za kujikurubisha karibu kwa Allaah) zinajulikana vyema kwetu hadi kutohitajia kutoa mifano yoyote hapa. Vitabu vyake na maandiko yake yanashuhudia ushahidi katika hilo na wala hahitajii yeyote miongoni mwetu kumsifia, isipokuwa elimu na Fiqh yake ni yenye kubaki na inashuhudia kwamba hakuna anayeiikana isipokuwa kwa yule aliyekuwa mjinga na mkaidi na hasidi mwenye chuki.

 

 

Viapo vya Maimamu wa enzi zake na enzi zilizofuata zinaonesha dhahiri kwa mtu mwenye akili iliyo wazi uongo wa madai uliobuniwa na maadui wa Uislamu na maadui wa Sunnah dhidi ya Imaam huyu muhimu, na kuweka wazi elimu yake, ufahamu wake na umakini wa hoja. Hivyo, tunaelewa sababu kwanini watu wa kufr na uzushi wanampiga vita dhidi yake, ni kwa sababu kwamba aliivuruga misingi yao na

 

قَدْ مَكَرَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَى اللَّـهُ بُنْيَانَهُم مِّنَ الْقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيْهِمُ السَّقْفُ مِن فَوْقِهِمْ وَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ﴿٢٦﴾

Walikwishafanya makri wale wa kabla yao, basi Allaah Aliyasukua majengo yao kwenye misingi, sakafu zikawaporomokea juu yao, na ikawajia adhabu kutoka pande wasizozitambua.   (An-Nahl 16:26)

 

 

Shaykh al-Islaam anaelezea ‘Aqiydah yake ya kisalafi[1]  ndani ya fataawa:

“Vizazi vya mwanzo vya Ummah huu na Maimamu wao wote kwa pamoja wanakubaliana kwamba hakuna chochote chenye kufanana na Allaah, si katika asili Yake wala sifa Zake au matendo Yake. Mmoja katika Maimaam alisema: Yeyote anayemlinganisha Allaah na uumbaji Wake ni kaafir, na yeyote anayekana kwa kile Allaah Alichojisifia Mwenyewe ni kaafir; hakuna chochote ambacho Allaah Amejifananisha Mwenyewe au Rasuli wake alichomlinganisha na Yeye.”[2]

 

 

Yeye (Rahimahu Allaah) pia amesema:

 

“Tamko ambalo ni madhubuti kuhusiana na masuala yote haya ni kwamba Allaah Afananishwe kama vile Alivyojifananisha Mwenyewe au kama alivyofananishwa na Rasuli Wake, na kama vizazi vya mwanzo vilivyomfananisha, na sisi hatuhitajiki kuvuka mpaka kwa yale yaliyosemwa na Qur-aan na Hadiyth.”

 

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema: “Allaah asifananishwe isipokuwa kwa namna Aliyojifananisha Mwenyewe au kama alivyomfananisha Rasuli wake, na mtu asichupe mpaka dhidi ya Qur-aan na Hadiyth.”

 

Mwenendo wa Salaf ulikuwa ni kumfananisha Allaah kama vile Alivyojifananisha Mwenyewe na kama Alivyomfananisha Rasuli Wake, bila ya kuharibu au kukana, na bila ya kuuliza ni namna gani au ulinganisho Wake na viumbe Vyake. Tunafahamu kwamba yale ambayo Allaah Amejifananisha nayo Mwenyewe ni kweli, na wala hakuna maajabu au kitu chenye kubabaisha katika hilo, isipokuwa maana zake zieleweke kwa yule Mmoja Aliyesema hayo yaeleweke hivyo, haswa pale aliyesema hayo ni mwenye elimu zaidi kwa yale anayosema kuliko watu wengine wote na mwenye kufahamika na mwenye kuweza kueleza kile anachokitaka kueleza, na mwenye ufasaha katika kueleza, kutafsiri na kuongoza.

 

Kwa kuongezea na yote haya, hakuna chochote kinachofanana na Allaah, aidha kwa hali ya utukufu Wake au majina Yake na sifa au matendo. Tunaamini kisawasawa kwamba Yeye ana hali ya kweli na kwamba Ana matendo ya kweli, na sifa za kweli. Hakuna chochote chenye kufanana na Yeye, hali Yake, sifa au matendo. Iwapo kuna chochote kinachomaanisha upungufu au kwamba Yeye ana mwanzo, Yupo mbali kabisa na hilo kwa ukweli haswa, na Yeye afikiriwe kuwa ni mkamilifu katika namna ambayo hakuna ukamilifu juu yake. Yeye hana mwanzo na hakuna uwezekano wa kwamba Yeye ameumbwa, kwa sababu hakuna wakati ambao yeye hakuwepo. Kwa kitu chochote kuweza kuumbwa kinamaanisha kwamba kulikuwa na wakati ambao hakukuwepo, na kwamba uumbaji huo unahitaji muumbaji, lakini Yeye Ameendelea kuwepo tokea enzi zote.

 

 

Muono wa Salaf ni ule wa usasa, sio kwa kukana sifa tukufu wala kumlinganisha Allaah na viumbe Vyake. Hawazilinganishi sifa za Allaah katika sifa za viumbe Vyake, kama ambavyo hawailinganishi hali Yake na hali ya viumbe Vyake. Hawakaidi kwamba yale ambayo Amejisifia Mwenyewe au yale ambayo Rasuli Wake Amemsifia, inayopelekea kukana majina Yake matukufu na sifa zinazovuta hisia, na kuyatoa maneno kutoka sehemu (yake) sahihi (rudia An-Nisaa 4:46) na kuyakimbia majina na alama za Allaah (Fusswilat 41: 40).

 

 

 

Wote wanaokana sifa za Allaah na wale wanaomlinganisha Yeye kwa viumbe Vyake ni wenye hatia ya makosa yote. Wale wanaokaidi Sifa zake na kushindwa kuelewa majina yake na sifa za Allaah isipokuwa kwa namna ambayo inanufaisha viumbe hai, kwa hiyo wanakana dhana hizi na hivyo kuunganisha makosa yote; awali ya yote wamemlinganisha Yeye na viumbe Vyake, kisha wakakana sifa Zake kutokana na hilo. Kwamba ulinganisho wa majina hayo na sifa ni kwa kuweza kueleweka kutokana na majina na sifa za viumbe Vyake, kisha wakakana sifa ambazo Anastahiki kuwa nazo ambazo ni zake Allaah, Mwenye kushukuriwa na kusifwa.[3]

 

Jibu kwa Wale Wanaodai Kwamba Alikuwa ni Mwenye Elimu Ya Diyn Isiyostaarabika

 

Ibn Hajar al-Haythamiy (ni mmoja wa Fuqahaa mkubwa wa ki Shaafi’iy, aliyekufa mwaka 974 H na ni mtu ambaye ni mwengine kinyume na Ibn Hajar al-’Asqalaaniy, mwandishi wa Fat-h al-Baariy aliyefariki mwaka 852 H) amewatolea hoja Mashaykh wawili wa Uislamu, Ibn Taymiyyah na mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim, kwa mapana sana na kuwatuhumu kwamba ni wenye kumuelezea Allaah katika maelezo ya kimaumbo, wakimlinganisha yeye na viumbe Vyake, na imani nyengine zisizo na mashiko. Lakini alijibiwa na wengi, ambao walieleza uongo wa yale aliyoyaeleza na kufafanua kwamba Maimaam hao wawili walikuwa safi na mbali na imani yoyote inayokwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Mmoja wa Wanachuoni waliyemjibu vizuri alikuwa ni:

 

 

-Al-Mulla ‘Aliy Qaariy (Rahimahu Allaah), ambaye amesema, baada ya kunukuu tuhuma za Ibn Hajar al-Haythamiy dhidi yao na hoja zake dhidi ya Aqiydah zao:

 

 

Ninasema: Allaah Awalinde wao – yaani Ibn al-Qayyim na Shaykh wake Ibn Taymiyyah – kutokana na tuhuma kubwa kabisa. Yule ambaye anasoma Sharh Manaazil as-Saa’iriyn cha Nadiym al-Baariy al-Shaykh al-Ansaariy, ambaye ni Shaykh wa Uislamu kwa mujibu wa Masufi, ataona kwa uwazi kwamba walikuwa ni miongoni mwa Ahlus Sunnah wal Jamaa’ah na kwa hakika ni miongoni mwa awliyaa (marafiki wa karibu wa Allaah) wa Ummah huu. Miongoni mwa aliyosema ndani ya kitabu kilichotajwa ni yafuatayo:

 

 

“Maneno haya ya Shaykh al-Islaam yanadhihirisha nafasi yake kama ni Mwanachuoni mkubwa wa Ahlus-Sunnah, na nafasi yake miongoni mwa Wanachuoni, na inaonesha kwamba yeye ni msafi kwa wale maadui wake wa ki-Jahami wanayomtuhumu nao, kwamba amemlinganisha Allaah na viumbe Vyake, kama vile Raafidhah wanavyowatuhumu wao kuwa ni ma Naasibi, na Naasibi wanawatuhumu wao kuwa ni Raafidhah, na Mu’tazilah wanawatuhumu wao kuwa ni wenye elimu ya Diyn isiyostaarabika. Huo ndio urithi wa maadui wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao wanamtuhumu yeye na wafuasi wake kwa kubuni dini mpya. Na huu ni urithi ambao Wanachuoni wa Hadiyth na Sunnah kutoka kwa Nabiy wao na kwamba watu wa uongo wanawapa wao anwani za kijinai.

 

Allaah Amrehemu ash-Shaafi’iy, Ambaye Amesema Pale Alipotuhumiwa Kuwa Ni Raafidhi:

 

Iwapo kuwa ni Raafidhi inamaanisha kuwa na mapenzi na familia ya Muhammad, basi waache makabila mawili (ya binaadamu na majini) kushuhudia kwamba mimi ni Raafidhi.

 

 

Allaah Amrehemu Shaykh wetu Abul-‘Abbaas Ibn Taymiyyah pale aliposema:

Iwapo kuwa ni Naasibi inamaanisha kuwa na mapenzi na familia ya Muhammad, basi waache makabila mawili (ya binaadamu na majini) kushuhudia kwamba mimi ni Naasibi.

 

 

Allaah Amrehemu Wa Tatu – Ibn al-Qayyim – Pale Aliposema:

 

Iwapo kuwa ni mwenye elimu ya Diyn isiyostaarabika inamaanisha kuwa na msimamo thabiti wa sifa tukufu na kuzinasibisha hizo kuwa juu ya maana ya muongo, Basi shukrani zote ni za Allaah, mimi ni mwenye elimu ya Diyn isiyostaarabika, walete mashahidi wako.”[4]

 

 

-Wanachuoni Wa Kamati Ya Juu Ya Fatwa Waliulizwa:

Watu wanasema kwamba Ibn Taymiyyah alikuwa si mmoja katika Ahlus Sunnah wal Jama’ah, na kwamba alipotea na kuwapotosha wengine, na kwamba hili ni kwa maoni ya Ibn Hajar na wengineo. Je, kwa hayo wanayoeleza ni kweli au la?

 

 

Wakajibu:

 

 

Shaykh Ahmad Ibn ‘Abdil-Haliym Ibn Taymiyyah ni mmoja wa Imaam wa Ahlus Sunnah wal Jama’ah, ambaye aliwaita watu katika ukweli na katika njia sahihi. Allaah aliisimamisha Sunnah kwa kumtumia yeye na kuwavunja nguvu wafuasi wa uzushi na uzushi na ukafiri. Yule ambaye anamtambua kama ni mwengine zaidi ya hivyo ni yule ambaye ni mzushi na amepotea na anawapotosha wengine. Wamesikia mambo ya uongo kuhusiana naye, na wanafikiria kwamba ukweli ulikuwa ni uongo na uongo ulikuwa ni ukweli. Hayo yanatambuliwa na yule ambaye Allaah Anamuongoza na yule anayesoma kitabu chake na vitabu vya wapinzani wake, na kulinganisha wasifu wake na wao. Hii ni bora na ushahidi thabiti baina ya pande hizo mbili.[5]

 

Hivyo, iwapo tunatambua hapa kwamba yale yaliyoelezwa na watu kwamba alikuwa ni mwenye elimu ya Diyn isiyostaarabika na alikufuru Aqiydah sahihi na kumlinganisha Allaah, Allaah Atukuzwe, na sifa za viumbe Vyake, ni uongo uzushi ulio wazi na uongo ulio dhahiri dhidi ya Shaykh al-Islaam na mtindo wake na Aqiydah. Yeyote anayesoma aina ya vitabu vyake vikubwa ama vidogo atalitambua hilo.

 

 

 

 

[1] Vizazi vitatu ambavyo vimesifiwa na Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “Viumbe bora ni katika vizazi vyangu (au karne zangu), kisha wanaowafuata wao, kisha wale wanaokuja baada yao. Kisha watakuja watu ambao hawatojali iwapo matamshi yao yanakuja baada ya kiapo au kinyume chake (yaani, hawatochukulia umuhimu wa masuala kiuzito wake).” (Imepokewa na al-Bukhaariy, Muslim na at-Tirmidhiy).

[2] Fataawa ya Shaykh al-Islaam (2/126).

[3] Fataawa Shaykh al-Islaam (5/26-27) 

[4] Mirqaah al-Mafaatiyh, al-Mulla ‘Aliy Qaari (8/146, 147). Maneno yaliyo baina ya alama za nukuu “” zilinukuliwa na al-Mulla ‘Aliy Qaari kutoka kwa Imaam Ibn al-Qayyim, kutoka katika kitabu chake cha Madaarij al-Saalikiyn bayna Manaazil Iyyaaka Na’budu wa Iyyaaka Nasta’iyn (2/87, 88).

[5] Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz Ibn Baaz, Shaykh ‘Abdur-Razzaaq ‘Afiyfiy, Shaykh ‘Abdullaah Ibn Ghadyaan, Shaykh ‘Abdullaah Ibn Qa’uud. Fataawa al-Lajnah al-Daa’imah (2/451, 254).

Share

09-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya 7: Jihaad, Mitihani Na Kifo Chake

 

Sura Ya 7: Jihaad, Mitihani Na Kifo

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Jihaad Yake

 

Maisha ya Ibn Taymiyyah yalitengana (na maisha ya watu wengine) kwa kuwa na sifa kubwa kubwa za kuamrisha mema, kukataza maovu na kufanya Jihaad kwa ajili ya Allaah. Alichanganyisha nafasi yake ya kusomesha, utoaji wa fatwa za kishari’ah na uandishi pamoja na matendo yenye nafasi ya juu kabisa. Ukweli ni kwamba, maisha yake yote yalizungukwa na Jihaad. Pamoja na maelezo mafupi mno ya kuangalia maisha yake ndani ya nyanja hii, tunaweza kuona idadi kadhaa ya matukio:

 

 

Jihaad Yake Katika Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu

 

 

-Uharibifu wake wa masanamu na maeneo, kama vile uharibifu wa nguzo, ndani ya Masjid at-Taariykh huko Damascus, ambao watu walikuwa wakiiombea kutokana na nguzo hiyo baraka,[1] na vitu vyote ambavyo vilikuwa vikitumika kwa kuviabudia kinyume na Allaah na ambavyo kuwazuia watu kuzuru sehemu kama hizo. Tendo hili kakamavu lilitanguliwa na hatua mbili: kwanza, kwa kueleza ukweli wa sehemu hizi (zinazodhaniwa kuwa ni tukufu) ambazo nyingi zao zilisimuliwa kwa uharibifu na kwamba makaburi mengi ambayo yakitukuzwa na kufanyiwa ziara kwayo, ukweli ni kwamba yalikuwa hayana mnasaba wowote kwa wale wanaowasifia nao.[2] Pili, kwa njia ya mijadala ya kitaalamu kupitia mahojiano ya moja kwa moja, vitabu na barua, na kuelezea shirki hiyo na uzushi unaoungama katika matendo kama hayo na pia kupitia uwasilishaji wa maoni ya wapinzani na kuzikana hoja zao.

 

 

 

-Aliandika barua kwa aliyekuwa Mfalme wa Ukiristo nchini Cyprus akimualika katika Uislamu na kuweka wazi uongo na ufisadi unaofanywa na mapadri na watawa hali ya kuwa wakielewa vyema kwamba walikuwa juu ya upotovu. Baada ya kutaja uchaji Allaah wa Mfalme, mapenzi yake ya elimu na tabia zake nzuri kwa watu, Ibn Taymiyyah baadaye akamualika kuingia katika Uislamu na kufuata imani sahihi. Alifanya hivi katika mtindo laini na wenye maelezo yanayoelezea utaalamu wake, na akimuhimiza kuwa na ukarimu mbele ya Waislamu waliopo nchini Cyprus, wala asithubutu kubadili dini ya hata mmoja miongoni mwao.[3] Pia aliingia kwenye mijadala pamoja na Wakiristo, baadhi yake yeye mwenyewe aliinukuu ndani ya kitabu chake cha al-Jawaab as-Swahiyh.[4]

 

 

-Alifanya vikao vingi dhidi ya Masufi. Moja ya kikao chake maarufu kilikuwa dhidi ya Bataa'ihiyyah.[5] Aliwakana na kuweka wazi tabia zao za ki-Shaytwaan kama vile kuingia ndani ya moto na kutoka bila ya jeraha na madai yao kwamba hilo ni kuonesha miujiza yao ya kiasili. Alieleza kwamba hata kama wakifanya hivi au kuruka angani, haitokuwa ni ushahidi kwamba yanaweza kutumika kutangaza ukiukwaji wao wa Shari’ah kuwa ni sahihi.[6] Aliwapa changamoto kwa kuwataka kuingia kwenye moto pamoja nae kwa masharti kwamba awali ya yote wajikoshe kwa siki na maji ya moto. Hatimaye, waliwekwa wazi na kushindwa na wakakubali utiifu wa moja kwa moja katika Qur-aan na Sunnah.[7]

 

 

Ndani ya mwaka 699H, yeye na idadi kadhaa ya swahibu zake walipambana na wauzaji walevi; wakavunja vyombo vyao, kumwaga ulevi wao na kuwatwiisha kwa adhabu idadi yao kadhaa, (tendo ambalo) liliwafanya watu kutoka nje na kushangilia jambo hili.[8]

 

 

-Ama kwa vikao vyake dhidi ya watawala na nasaha zake kwao, vilikuwa ni maarufu. Moja kati ya kikao chake maarufu mno kilikuwa dhidi ya Ghaazaan, mtawala wa Tartar. Katika kipindi ambacho Tartar waliamuru vitisho na utawala (wa kidhalimu), alizungumza kwa mtawala akiwa na maneno makali kuhusiana na vitendo vyao, wakitandaza ufisadi na kwenda kinyume na vikwazo vya Waislamu hali ya kuwa wao wenyewe wakidai kuwa ni Waislamu. Vivyo hivyo, maneno yake mazito kwa Sultaan an-Naaswir, yalimlazimu Sultaan huyo kuacha kutekeleza matendo yasiyofaa kishari’ah.[9]

 

 

-Ibn Taymiyyah pia alikuwa anawaathiri watawala kurudia kwenye jukumu lao la kuamrisha mema na kukataza maovu. Mfano wa hili ni pale rushwa ilipotanda mno na ikaja kutambulika kama ni zana ya kuwezesha kupata nafasi za kiofisi na pia katika kukimbia adhabu ya kifo mnamo mwaka 712H, amri rasmi ikapelekwa Damascus, kutoka kwa Sultaan, ikieleza kwamba hakuna mtu yeyote atakayeruhusika kupatiwa nafasi au ofisi kupitia njia za pesa au rushwa na kwamba muuaji ahukumiwe kwa mujibu wa Shari’ah; amri hii ilitokana na ushauri wa Ibn Taymiyyah.[10]

 

 

Kuna mifano mengine inayofafanua jitihada za Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah), katika kuamrisha mema na kukataza maovu. Nitaeleza baadhi ya matukio hayo hapa chini kwa upana:

 

 

Jihaad Yake Dhidi Ya Wazushi na Madhehebu Potofu

 

Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah alijitolea jitihada zake kubwa katika kuyakana madhehebu tofauti mbalimbali. Yeye binafsi aliwahi kwa mwili wake kuwapa changamoto baadhi ya watu kutoka dhehebu la kizawa la Kisufi, ambalo likitambulikana kama ni Bataa’ihiyyah ambalo lilijihusisha kwenye michezo kama vile kutembea juu ya moto ili kuwashangaza jamii kubwa ya watu. Aliwaomba kutembea pamoja naye juu ya moto kwa sharti kwamba wajioshe wenyewe kwanza kwa siki na maji ya moto. Ukataaji wao uliziweka wazi ujinga wao, na hivyo Ibn Taymiyyah akauweka wazi uongo wa dhehebu la Bataa’ihiyyah.[11]  Hali kadhalika, alimkana Muhiyyud-Dyin Ibn ‘Arabiy na upotofu wa Wahdat al-Wujuud.

 

 

Ibn Hajar alisema, ‘... Kutokana na sifa za ajabu za mtu huyu (yaani Ibn Taymiyyah) ni kwamba alikuwa ni mtu mwenye nguvu sana miongoni mwa watu dhidi ya watu wa uzushi, Marawaafidhah, Mahuluuliyyah, na Waittihaadiyyah, na kazi zake katika hili ni nyingi na maarufu, na fataawa katika hayo hazina idadi... Ni wajibu wa mtu, ambaye ni mtaalamu wa elimu na amepata ufahamu kwamba atilie maanani maneno ya mtu ambaye imeegemea (elimu yake) katika vitabu vyake maarufu au kutokana na ndimi za wale watu waaminifu wanaofikisha maneno yake kwa usahihi – kisha kujitenga na yale yote yaliyokanwa na kujiamuru kutokana nayo kwa lengo la kutoa ushauri sahihi na kumshukuru kwa sifa zake nzuri kabisa na kwa yale aliyokuwa sahihi kama ilivyo njia ya Wanachuoni.

 

 

Iwapo hakuna sifa zozote za Shaykh Taqiyud-Diyn (Ibn Taymiyyah) isipokuwa kwa mwanafunzi wake maarufu Shaykh Shamsud-Diyn Ibn Qayyim al-Jawziyyah, mwandishi wa kazi nyingi, ambazo kutokana nazo wapinzani na wafuasi wake walinufaika nazo, basi hii itakuwa ni ushahidi tosha wa nafasi yake adhimu (Ibn Taymiyyah). Na kwanini iwe vyenginevyo pale ambapo Maimaam wa Kishaafi’iy na wengine, wala usizungumzie Mahanbali, katika kipindi chake kuthibitisha sayansi yake (ya Kiislamu) muhimu.[12]

 

Ama kwa mnasaba wa kuwakana watu wa uzushi na hatari waliyonayo kwa Waislamu, Ibn Taymiyyah amesema, ‘Pindipo baadhi ya watu walipomuuliza Imaam Ahmad Ibn Hanbal kwamba hawajisikii vizuri katika kuwapinga watu, aliwajibu, ‘Iwapo mimi ni wa kukaa kimya, ni namna gani watu wajinga walio wengi watauelewa ukweli kutokana na uongo?’ Wale walioanzisha maandiko ya kipotofu ambayo yanapingana na Qur-aan na Sunnah na wale waliozua mambo ya ‘ibaadah, basi ni wajibu juu yao kwamba waelezewe na kwamba Waislamu watahadharishwe dhidi yao – kwa makubaliano ya Wanachuoni Waislamu walio wengi. Ukweli ni kwamba, pale Imaam Ahmad bin Hanbal alipoulizwa kuhusiana na mtu anayefunga, kuswali na kujitenga pekee ndani ya Msikiti kwa ‘ibaadah; iwapo atakuwa ni mtu muhimu kwake kuliko mtu anayezungumza dhidi ya wazushi? Alisema, ‘Pale anapofunga na kuswali na kujitenga pekee, basi anafanya kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe. Hata hivyo, pale anapozungumza dhidi ya wazushi (watu wa bid’ah), anafanza hivyo kwa manufaa ya Waislamu kwa ujumla wake, na hili ni bora zaidi.’

 

 

Hivyo ilikuwa wazi kwamba kuwakana wazushi wazi wazi ni ya manufaa ya jumla kwa Waislamu na inatambulikana kama ni aina mojawapo ya mapambano katika njia ya Allaah. Kwani kuisafisha Diyn ya Allaah na kuitetea kutokana na mavamizi ni wajibu wa kiujumla – kama ilivyokubaliwa na Wanachuoni. Kwani, iwapo Allaah Asingeliwanyanyua baadhi ya watu kuwapinga wazushi, basi Diyn hii ingelishtadi kwa madhara, ufisadi na upotofu. Kwa hakika, aina hii ya ufisadi ni kubwa zaidi kuliko ufisadi unaotokana na wasioamini wanapowateka Waislamu. Kwani pale wasioamini wanapowateka nyara Waislamu, hawaharibu mioyo yao, au Diyn yao, isipokuwa baada ya muda. Ingawa, wazushi wanaziharibu nyoyo tokea hapo mwanzo.’ [13]

 

 

Jihaad yake dhidi ya Wakiristo na Raafidhah (Mashia)

 

a.     Al-Jawaab as-Swahiyh

 

Ibn Taymiyyah ameandika Al-Jawaab as-Swahiyh Liman Baddala Diyn al-Masiyh katika vitabu (mijalada) vinne ambavyo ndani yake aliweza kuzielezea pingamizi zote zilizotolewa dhidi ya Uislamu, aliweka bayana hoja kamili mpya na zenye kuridhisha kwa kuegemea Sunnah ya Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Moja kati ya waliomuandikia wasifu wake Shaykh al-Islaam, ni Shaykh Abu Zahrah, aliyesema: “Kitabu hichi peke yake kinatosha kutoa nafasi kwa ajili yake miongoni mwa wataalamu na madukturi wasomi ambao walitia bidii ya kuisafisha imani.”[14]

 

 

b.    Minhaaj as-Sunnah

 

Kama kilivyo Al-Jawaab as-Swahiyh, Minhaaj as-Sunnah ni kazi nyengine ya kipekee ya Ibn Taymiyyah ya juu kabisa ambayo ameandika kukana matabaka ya Kishia hapo zamani (na leo) yanayohatarisha ukakamavu wa imani sahihi ya kiasili. Kitabu hicho, chenye vijitabu (mijalada) vinne hadi nane na chenye kurasa zaidi ya 1,600; kimeandikwa kukijibu kitabu cha Minhaaj al-Karaaman cha Ibn al-Muttahir al-Hilliy ambaye, katika hamu yake iliyochupa mpaka, akataka kuthibitisha Utukufu uliopo kwa nafasi ya Kiiimamu (Imamu 12 wa Kishia), akajaribu kuwafanya Makhalifa waongofu watatu wa mwanzo kuwa ni wanafiki na walioritadi na pia kama ni viumbe viovu kabisa vilivyojiingiza kwenye unyanyasaji. Hili, kwa mujibu wa Ibn Taymiyyah, iliushushia hadhi Uislamu na kuifanya dhana ya Utume kuwa ni dhaifu. Hata kwa msingi wa ubishano wake, Minhaaj as-Sunnah ni kitabu muhimu kutokana na mtindo wake ulio wazi na hoja kali kali na maelezo yake ya kuridhisha na usahihi wake.

 

Nukuu nyingi hazielezi nafasi ya Ibn Taymiyyah kwenye Jihaad dhidi ya Wakiristo kabla ya kufukuzwa kwao nchini Shaam. Hata hivyo Imaam Al-Bazzaar, anataja yafuatayo pale anapojadili ukakamavu na moyo uliopigwa konde wa Ibn Taymiyyah: “Wananasibisha kwamba walimuona katika utekaji wa ‘Akkah, katika muonekano wa kishujaa ambao hauwezi kuelezeka. Wanasema kwamba alikuwa ndio chanzo ya sababu ya kutekwa (‘Akkah) na Waislamu kwa sababu ya matendo yake (mema), na ushauri na muono wake mkali.”[15]

 

Ama kwa Maraafidhah, walijijengea ngome yao wenyewe katika milima ya al-Jard na al-Kasrawaaniy. Ibn Taymiyyah akawafuata huko ndani ya mwaka 704H akiwa pamoja na kundi la wafuasi wake na kuwataka idadi yao kadhaa kuomba toba na (hivyo) wakasimamisha Shari’ah ya Uislamu juu yao (Maraafidhah). Mwanzoni mwa mwaka 705H, Ibn Taymiyyah alikwenda vitani akiwa pamoja na kundi la kivita na naibu Sultaan wa Shaam na Allaah Akawasaidia wao dhidi ya Maraafidhah.[16]

 

 

Jihaad Yake Dhidi Ya Ma-Tartar

 

Ibn Taymiyyah alikuwa na nafasi kubwa katika kuanzisha Jihaad dhidi ya ma-Tartar. Aliweka wazi ukweli wa masharti yao na kuonesha kwamba ilikuwa ni wajibu kupigana nao, kwanza, kwa sababu ya makubaliano ya Wanachuoni katika wajibu wa kupigana vita na kundi lolote ambalo linakana waziwazi na kukataa Shari’ah za Uislamu na pili, akieleza kwamba kanuni hii inafanya kazi kwa Tartar kwa sababu ya masharti yao.

 

Aliweka wazi sababu za ushindi na kueleza kwamba sio jambo lisilowezekana au lenye ugumu kupata ushindi dhidi yao iwapo Waislamu watafuata sababu za kupata ushindi kama vile kusimamisha Shari’ah, kuondosha unyanyasaji, kueneza haki na kuwa wakweli kwa niyah zao pale wanaposimamisha Jihaad katika njia ya Allaah.

 

Ibn Taymiyyah alichukua jukumu la kuyafunza majeshi na kuanzisha makundi ya Mujaahidiyn. Alihusika pia katika mavamizi ya kushtukiza dhidi ya kambi za kijeshi za Tartar. Pia alizamia jimbo ambalo watu wa Baatwiniyah (wenye itikadi ya Kishia) wakiishi katika milima ya Shaam, kwa sababu waliwasaliti Waislamu na kwa siri walishirikiana na maadui wa Uislamu, Matartar na Makrusedi. Ingawa dhehebu la Kibatini lilifanikiwa kumlaghai Ibn Taymiyyah pale walipojifanya kutubia na kuzikataa imani na mila zao mbovu. Lakini alitambua kwamba walimcheza kwa kutumia taqqiyah,[17] na kwamba walibakia kwenye uadui wao kwa Uislamu na Waislamu. Hakuacha kuwapiga vita na kuwasaka, na alitoa fatwa akiweka wazi imani zao zilizojificha na vitendo vyao viovu na akaamrisha haja ya kupigana vita nao.

 

Kwa upande mwengine, hakupatapo kuridhia ukweli pale anapojadiliana na watoto wa kifalme na wafalme kutokana na dharau zao katika kuihami ardhi ya Uislamu dhidi ya maadui wa ndani na nje. Hili linaonesha dhahiri kupitia barua yake kwa Sultaan an-Naaswir Muhammad Ibn Qalawuun. Ndani ya barua hiyo, alitishia kuendeleza taifa litakalojitenga kutoka katika utawala wa Kisultani, na kuutoa uaminifu wake kwa kiongozi mwengine ambaye hatoacha kuhami na kusimama dhidi ya uvamizi wa Matartar.

 

Pale mji wa Damascus ulipoanguka kwa mara nyengine ya pili kwa Matartar, Ibn Taymiyyah alikataa kusimama kwa kujishushuia hadhi, kwani alikubaliana pamoja na viongozi wa nchi hiyo kuchukua hatua muhimu kwa ajili ya ustawi wa Waislamu kwa kukutana na kiongozi wa Matartar. Ingawa walikuwa hawana nguvu kujihami wenyewe, hata hivyo alichukua hatua ya dharura katika kuhamasisha kuonana na Sultaan wa Matartar aitwaye Ghaazaan, akimuomba usalama wa watu wa Damascus bila ya kuisalimisha ngome yao. Hakuwa na moyo wenye kukubali na ulio na ujinga kama walivyo mashaykh wengine waliokutana na Ghaazaan wakimuomba msamaha na kuwakubali kwao. Lakini alikabiliana nae Ghaazaan uso kwa uso na kumuelezea kwamba uvamizi wa Damascus hautakuwa mrefu kwani Waislamu wanaendelea kupindua. Usalama ukapatikana kwa Waislamu wa Damascus kutokana na juhudi ya ukakamavu na ushujaa wa Ibn Taymiyyah.

 

Ibn Taymiyyah pia alishirikiana na Sultan an-Naaswir Ibn Qalawuun katika vita vyake dhidi ya Ghaazaan aliyedai kuwa ni Muislamu na kujipachika jina lake la Mahmuud. Ilithibitika kwa Ibn Taymiyyah kuwa vyenginevyo, kwa sababu Ghaazaan alikataa moja kwa moja kusimamisha Shar’iah za Kiislamu na hakuwa mwenye kuzithamini Shar’iah za Allaah. Alitawala nchi kwa kutumia kitabu cha al-Yaasiq ambacho kilikuwa na mchanganyiko wa shari’ah kutoka Ukiristo, Uyahudi, Uislamu na sheria za Genghis Khan mwenyewe. Alizikataa Shar’iah zilizoshushwa kwa Waislamu ndani ya Qur-aan na Sunnah.

 

Katika mwaka 702H, habari kuhusiana na kurejea kwa Matartar mjini Shaam zikaenea. Ibn Taymiyyah akafanya haraka kwenda kwa Sultaan wa Misri kuomba msaada dhidi ya hatari za Matartar na ubepari wao uliokuwa maarufu sana, haswa pale watawala wa Allepo na Hama walipoitupa miji yao na kukimbilia Damascus. Pale Matartar walipofikia Homs na Ba’lbek, Ibn Taymiyyah akaajiri mabaki ya jeshi ambalo liliondoka Hama na miji mengine. Aliliunganisha jeshi na kuanza kuandamana kwenda Damascus ili kuwa mbele katika daraja, hadi majeshi ya Khaliyfah al-Mustakfi na Sultaan an-Naaswir Ibn Qalawuun yalipofikia Damascus. Siku ya Jumamosi, Ramadhwaan ya pili, jeshi la Waislamu likawa limekamilika, na mashirikiano kwa ajili ya vita yalikuwa yameshaanza nje ya Damascus ili kuulinda mji huo kutokana na madhara yoyote. Eneo la vita lilikuwa ni Marj as-Safar.

 

Pale Matartar waliposikia kwamba jeshi kubwa linakuja, wakafanya haraka kukutana nao nje ya Damascus. Hivyo, mpango wa mwanzo wa Ibn Taymiyyah ukawa umefanikiwa kwani aliwazuia Matartar kufanya uharibifu zaidi wa mji. Kwani umuhimu wa mwanzo wa Matartar ulikuwa ni kuliharibu jeshi la Waislamu, (lakini walishindwa kufanya hivyo) wakauacha mji (wa Damascus) bila ya uchokozi.

 

Majeshi hayo mawili baadaye yakakutana, kila moja likiwa na mawazo kichwani mwake ya kuliharibu jeshi la mwengine, na vita vikaanza mara moja. Ilikuwa ni wakati wa adhuhuri na Waislamu ndani ya vita hivyo walikuwa wamefunga siku hiyo katika vita vya Shaqhab, vilivyopiganwa ndani ya mwezi wa Ramadhwaan. Ibn Taymiyyah akawaamuru kufungua Swawm kwa kufuata muongozo wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kila mmoja wao aliomba kutoka kwa Allaah aidha Shahaadah au ushindi. Ndani ya fikra zao ni Swahaba wa Nabiy (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na warithi wao waongofu (Mataabi’iyn). Wasiwasi wao wa mwanzo ulikuwa ni kuuhami Uislamu na kuuharibu uadui wa Matartar kwa namna yoyote, wakihakikisha kwamba hawatojaribu kurudi tena katika ardhi ya Uislamu kwa ufisadi wao, tofauti na ilivyokuwa mara ya mwanzo pale Matartar walipojitengenezea makundi mapya, yao wenyewe, baada ya kushindwa katika vita vya A’in Jaluut na kurudi katika uvamizi wa ardhi za Waislamu.

 

Shaykh al-Islaam alikuwa ni kiongozi wa jeshi, akiyatengeneza vyema malengo ya Waislamu, ingawa kwa upande mwengine hupigana na adui kwa ushujaa, akiwasukuma nyuma kurudi majumbani kwa kutambaa, wakawavunja Matartar, wakiizuia hatari yao na kuwaondoa Waislamu mbali na matishio yao. Hatimaye, wakaliacha jeshi la adui likiwa halina matarajio yoyote daima kurejea katika ardhi ya Uislamu. Mapigano ya Shaqhab yalikuwa ni mapigano ya mwisho kabisa baina ya Matartar na Waislamu.

 

Baada ya kufanya Jihaad dhidi ya Matartar na kuwashinda, tunamuona Ibn Taymiyyah akithamini vita hivyo, akichambua mafunzo ya kimanufaa ambayo yanaweza kufikiwa kutokana na mapigano hayo na kuelezea maeneo ya ulinganishi baina ya mapigano hayo dhidi ya Matartar na mapigano mengine ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).[18]

 

Mapigano yalikuwa na nafasi kuu katika majibu ya Ibn Taymiyyah kwa wale waliojaribu kumzuia na kuvunja nguvu makubaliano ya Waislamu. Walikuwa wakijaribu aidha kuwatisha Waislamu kwa kukithirisha mno uwezo na nguvu za adui, au wakidai kwamba Matartar ni Waislamu, na hivyo, kuwa ni udhuru wa kutopigana nao. Majibu ya Ibn Taymiyyah kwa Waislamu, ambao waliweza kurubuniwa na yale yaliyosemwa kuhusiana na kutowajibika kupigana na Matartar, yalikuwa ni maneno yake: “Iwapo mutanikuta mimi katika hadhi ya Matartar basi niueni!”

 

Jibu lake katika uwanja wa vita lilikuwa wazi na kwamba alianza kuwapiga vita Matartar, hivyo kutoacha nafasi ya Waislamu waliorubuniwa au waliokuwa na mawazo mengine kuhusiana na maamuzi muafaka katika kumpiga vita adui.

 

Hizo ni baadhi ya mifano ya Jihaad ya Ibn Taymiyyah, Allaah Amshushie rehema Zake, na uunganishi wake wa elimu pamoja na vitendo.

 

 

Mitihani na Kufungwa kwa Ibn Taymiyyah[19]

 

Ibn Taymiyyah alipitia mitihani mingi katika maisha yake na ni kazi ngumu kuipitia na kuielezea kwa namna nzuri ndani ya utafiti huu mfupi kuhusiana na yeye. Hivyo, nitataja tu orodha ya ile mitihani maarufu.

 

-Mtihani alioupata kwa sababu ya maandiko yake ya al-Hamawiyyah katika mwaka 698H.

 

-Mtihani alioupata kwa majadiliano yake kwa sababu ya maandiko ya al-Waasitwiyyah katika mwaka 705H.

 

-Mtihani alioupata kwa kuitwa kwake Misri na kufungwa katika mwaka 705H kwa miezi 18.

 

-Mtihani alioupata pamoja na Suufiyyah (Masufi waliomchongea kwa Kiongozi wa nchi) nchini Misri baada ya kuachiwa huru.

 

-Kufukuzwa kwake kwenda Alexandria katika mwaka 709H na kufungwa huko kwa miezi 8.

 

-Mtihani alioupata kwa sababu ya maamuzi mahsusi kuhusiana na talaka na kufuatiwa na kifungo katika mwaka 720H, kwa miezi mitano.

 

-Mtihani alioupata kwa sababu ya maamuzi yake ya Kishari’ah kuzuia kufanyika misafara mahsusi kuyazuru makaburi na kufuatiwa na kifungo katika mwaka 726H hadi kufa kwake katika mwaka 728H, Allaah amshushie rehema zake.

 

Majibu ya Ibn Taymiyyah kuhusiana na mitihani yote hii aliyokabiliana nayo yalikuwa daima ni majibu ya uhakika ambayo yaliyageuza mithani hii na madhara – kwa msaada wa Allaah – kuwa ni nafasi kuu ya kuiongeza Iymaan na kufikia pasipo na shaka katika maarifa na matendo.

 

Uitwaji wake nchini Misri, kwa mfano, ulimfanya kujadiliana na kuendelea na kuwaelezea wazushi ambao walieneza imani zao katika kila pembe ya nchi. Kutupwa kwake katika kifungo (jela) ilikuwa ni alama nyengine ya Baraka hii, kwani jitihada zake katika kuelimisha wafungwa na kuwalainisha hadi kufikia hatua ya kwamba utoaji wa elimu na Diyn ndani ya jela ulizidi baadhi ya taasisi zilizo nje ya jela. Hili lilitokezea kote; Misri (Cairo) na Alexandria. Uamuzi wake wa kubakia Misri baada ya kuachiwa ilikuwa kama alivyoelezea ndani ya barua[20] kwa mama yake, kwa sababu ya mambo muhimu kwa Diyn na dunia. Hili lilileta uzuri zaidi katika kusaidia Sunnah na kuwadidimiza wazushi. Moja kati ya matokeo ya uhakika ilikuwa ni vitabu na nyaraka alizoandika na alizotunga ndani ya jela. Pia aliwaomba radhi wale waliomdumaza, hata pale Ibn Taymiyyah alipopata nafasi ya kulipiza kisasi haswa. Mmoja miongoni mwa maadui zake, Ibn al-Makhluuf, Jaji wa ki-Maalikiy aliyesema: “Hatujaona mfano wa Ibn Taymiyyah; tulimlaghai lakini hatukuwa na uwezo kumzidi nguvu, pale alipokuwa na uwezo wa kutuzidi sisi nguvu, badala yake alituombea msamaha na kutuhami kwa niaba yetu.” [21]

 

Matokeo yake mengine ya uhakika ni kwamba mitihani hii ndani yake wenyewe yalikuwa ni sababu ya kuenea kwa kasi mno kazi za Ibn Taymiyyah.[22]

 

 

 

Kifo chake, Allaah Amshushie Rehema Zake juu yake

 

Hatimaye pale alipopigwa marufuku kuwa na kitabu chochote, karatasi au kalamu akiwa katika kipindi chake cha mwisho cha jela, Ibn Taymiyyah akajitolea muda wake wote katika kufanya ‘Ibaadah na kusoma Qur-aan. Alibakia katika hali hii kwa kipindi kifupi hadi alipoaga dunia mnamo tarehe ishirini Dhul-Qa’dah mwaka wa 728H. Aliugua kwa siku chache ambazo zilipelekea kifo chake.

Hili lilikuja kuwa ni mshituko mkubwa kwa watu na walitoka nje kwa idadi kubwa.

 

 

Wanahistoria wanakadiria kwamba kifo hichi ni moja kati ya mazishi machache na walilinganisha na mazishi ya Imaam Ahmad Ibn Hanbal, Allaah Awe radhi naye.

 

 

Ibn Taymiyyah alifariki kipindi alichokuwa kifungoni, kwa chuki na fitna alizotiwa Sultaan kutoka kwa wale maulamaa waliokuwa nwakimshindwa kielimu na wenye husda na mafanikio yake makubwa ya kielimu, kiucha Mungu, kiutendaji, kiufuasi na kukubalika kwake. Vilevile fitna tele za Masufi waliokuwa wakitaja mambo mengi kuhusiana naye kutokana nay eye kuwapinga uzushi na upotofu wao wa Diyn.

 

Hata hivyo, ukiachilia mbali hayo, mazishi yake yalishuhudiwa na wengi na yalikuwa ni maarufu na makubwa sana.

 

 

Imaam Al-Bazzaar amesema:

 

 “Mara tu watu waliposikia kifo chake, hakuna mtu hata mmoja aliyetaka kuwepo Damascus ambaye alikuwa na uwezo wa kuhudhuria Swalah na alitaka kubakia hadi alipohudhuria na kutoa muda kwa ajili hiyo. Matokea yake, masoko ya Damascus zikafungwa na shughuli zote za kimaisha zikasimama. Magavana, wakuu, Wanachuoni (Maulamaa) walitoka nje. Walisema kwamba hakuna wingi wa watu ulioacha kufika, kwa mujibu wa ufahamu wangu – isipokuwa watu watatu tu ndio hawakuhudhuria; hao watatu walikuwa wakitambulika kwa uadui wao dhidi ya Ibn Taymiyyah, walijificha wasionekane na watu kutokana na hofu ya maisha yao.” [23]

 

Ibn Kathiyr ametaja kwamba naibu Sultaan hakuwepo na Taifa likajiinamia kwa lipi la kufanya. Kisha naibu wa jela akaja kutoa rambirambi zake na kukaa karibu na Ibn Taymiyyah. Aliwafungulia njia wale Maswahibu wa karibu na watu wapenzi kuingia kumuona. Wakakaa pamoja naye, wakilia na kumshukuru.[24] “Kisha wakaanza kumuosha Shaykh… wakawaruhusu wale tu ambao waliosaidia katika kuosha kubakia pamoja naye. Miongoni mwao alikuwa ni Shaykh al-Haafidh al-Mizziy na kundi la waongofu wakuu na watu wema; watu wa elimu na Iymaan… kisha wakatangulia pamoja naye kwenye Jaami’ al-Umawiy. Kulikuwa na watu wengi mbele ya janaazah, nyuma yake, kwa upande wa kulia na kwa upande wa kushoto. Hakuna isipokuwa Allaah Aliyeweza kuwahesabu, kisha mtu mmoja akapiga ukulele “Hivi ndivyo yanavyotakiwa majeneza ya Maimamu wa Kisunnah!” Kwa hilo, watu, wakaanza kulia… pale adhana ya adhuhuri ilipoadhiniwa wakaswali hapo hapo kisunnah na kinyume na namna ya mila zilizozoeleka. Pale walipomaliza kuswali, naibu Khatwiyb akatoka – kwani khatwiyb mkuu alikuwa hayupo alikuwa Misri – na akaongoza Swalah juu ya Ibn Taymiyyah… Kisha watu wakamiminika kutoka kila pembe na milango yote ya Jaam’i… na wakakusanyika katika soko la al-Khayl.” [25]

 

Katika ardhi iliyo wazi, jeneza lake likaingizwa chini na ndugu yake, ‘Abdur-Rahmaan, akaongoza Swalah yake. Kisha jeneza lake likachukuliwa kaburini mwake na kuzikwa kwenye sehemu ya makaburi karibu na ndugu yake wa kiume, ‘Abdullaah, Allaah Awashushie rehema zake wote hao.

 

Imaam Al-Bazzaar amesema:

 

Kundi la watu waliokuwepo siku hiyo wamekubaliana kwamba walipoona idadi ya watu waliomswalia siku hiyo, hakuna wasiwasi wote kwamba walikuwa zaidi ya 500,000. Wataalamu wa historia wanasema kwamba hawakupata kusikia Swalah ya mazishi kuwa ni kubwa kama hivi isipokuwa ili Swalah ya jeneza al-Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaahu).[26] Hatimaye Shamsud-Diyn al-Waziyr akatokezea na kupelekwa pale liliopo kaburi lake, kwa kuwa hakuwepo hapo kabla, hivyo yeye na magavana pamoja naye wakamswalia Ibn Taymiyyah.

 

Hakuna jeneza ambalo limeonekana kuathiri hisia za watu katika heshima, ustahifu, ufakhari, uthamini, na shukrani kutoka kwa watu, na yote haya ni kutokana na elimu yake, matendo, zuhd, ‘ibaadah, ukataaji wa dunia, kushughulishwa na Akhera, umasikini wake, kujali, ukarimu, ujanadume, ustahamilivu, msimamo, ushujaa, uoni wa mbali, kuwa muwazi katika kuzungumzia ukweli, kuwa mkali dhidi ya maadui wa Allaah na Nabiy Wake na Diyn Yake, ubinaadamu wake, taadhima, na heshima mbele ya awliya’ wa Allaah, kutotilia maanani mazuri ya dunia, hamu yake ya kupindukia kwa ajili ya Akhera, na utafutaji wake wa hiyo Akhera usiochoka. Na utayasikia mambo haya na zaidi kutoka kwa wanaume, wanawake, na watoto, na wote humsifu kutokana na vile walivyokuwa wakimjua.

 

Alizikwa siku hiyo (Allaah Awe radhi naye). Kisha watu wakaanza kujikusanya kutoka vijiji na miji mbalimbali wakiwa wengine kwenye vipando wengine kwa miguu kumswalia kwa zamu juu ya kaburi lake, na kila habari za kifo chake zinapoifikia ardhi fulani, humswalia ndani ya Misikiti yake yote, haswa ndani ya miji na vijiji vya Misri, Shaam, Iraaq, Tabriz, al-Basrah, n.k.

 

Haya yote ni kutokana na namna walivyohisi kuwa na deni mbele ya Shaykh (Allaah Amshushie rehema zake) kwa kuwaongoza  kwenye ukweli na taratibu sahihi pamoja na ushahidi wa wazi, ushahidi wa maandiko na elimu, haswa kwa mnasaba wa kanuni za Diyn. Allaah Aliwabariki Qawm hii ambapo uzushi uliibuka ambao uliuuwa Sunnah, na idadi kubwa ya watu walizama kwenye uzushi na haraam katika hali ambayo hawakubutika kabisa! Na Allaah Akawabariki kwa kuwa naye kudhihirisha kanuni za Diyn na ukweli na imani sahihi kwao, na halikadhalika namna yake mahsusi ya kuwapinga wazushi ambayo haijaonekana kwa zaidi yake. Yote haya yalifanywa kwa mdomo wake, kalamu yake, vitabu vyake, na kanuni alizojifunga nazo kuzifuata ambazo zilikubaliana na ukweli na maana halisi, na pia uwazi, maandiko mepesi na ushahidi wa kielimu aliowasilisha ambao hakuna filosofa hata mmoja au wahoji waliomweza au kumkaribia kwa hoja. Yote haya aliyafanya hadi alipokuwa na uwezo wa kuingiza uwezo wake wote na kumtawala kila mzushi, na alikuwa na uwezo wa kuweka wazi na kufuta kila dhana ambazo zilisimamishwa na wakiomba kuzieneza.[27]

 

Tunamuomba Allaah Amlipe yeye kwa malipo bora kwa niaba ya Uislamu na Waislamu, Ametukuka Yule ambaye Amempa yale aliyokuwa nayo, akampatia uongofu bora kwa yale aliyoongoka nayo, na kumpatia yeye subira nzuri kabisa hadi kufariki kwake, na tunamuomba Allaah Awe Radhi naye, na Atupatie sisi na Waislamu wote maisha na kifo kinachoendana pamoja na Qur-aan na Yeye, na atujaalie sisi kushikamana vilivyo na wote hao kwenye yote waliyokuwa nayo, na tunamuomba Allaah Atujaalie sisi na wale wa baada yake kunufaika na elimu yake.

 

 

 

[1] Nahiyyah min Shaykhul-lslaam Ibn Taymiyyah, uk. 10-11; al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 13/34; as-Suluuk li Ma'rifah Duwal al-Muluuk cha al-Miqriyziyna Badaa'i' az-Zuhuur fiy Waqaa'i' ad-Duhuur cha Muhammad Ibn Ahmad Ibn 'Iyaas al-Hanafiy

[2] Rudia katika Ra-s al-Husayn cha Ibn Taymiyyah kilichoandikwa kwenye Majmu’ 'al-Fataawaa, Sura ya 27 na pia 17/500, 27/173 na 27/61 katika mada ya kaburi la Nuuh.

[3] Risaalah al-Qubrussiyah ya Ibn Taymiyyah, ndani ya Majmu’ al-Fataawaa, Sura ya 28. Hii inapatikana ikiwa na tafsiri pamoja na barua kadhaa za Ibn Taymiyyah: Barua za Ibn Taymiyyah kutoka Jela, kimechapishwa na Ujumbe wa Uislamu (Message of Islam), U.K.

[4] Al-Jawaab as-Swahiyh li man Baddala Diyn al-Masiyh cha Ibn Taymiyyah, 2/172.

[5] Wanatambulika kama ni al-Ahmadiyyah na ar-Rufaa’iyyah kutokana na kujisifia kwao kwa muanzilishi wao Ahmad ar-Rufaa’iy, mzaliwa kutoka kijiji kimoja cha al-Bataa’ih.

[6] Imaam ash-Shaafi’iy (Rahimahu Allaahu), amesema: “Iwapo umeona mtu anatembea juu ya maji au akiruka ndani ya anga, basi usimuamini hadi uhakikishe kisawasawa ukweli na kujinasibu kwake mbele ya Sunnah.”

[7] Majmu’ al-Fataawaa, 11/456-457, al-'Uquud ad-Durriyyah, uk.194 na al-Bidaayah wa an-Nihaayah 14/36.

[8] Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/122-123. Baadhi ya matokeo ambayo Shaykh alishiriki yalikuwa bila ya shaka yakifanyika kwa muongozo wa misingi iliyoshikamana na uamrishaji mema na ukatazaji maovu. Yeye mwenyewe Ibn Taymiyyah amejadili miongozo hiyo katika kijitabu chake cha al-Amr bil-Ma'ruuf wan-Nahy 'anil-Munkar.

[9] Al-Uquud ad-Durriyyah, pg. 281al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/54; al-Kawaakib ad-Durriyyah, uk. 138.

[10] Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/66.

[11] Majmu’ al-Fataawaa, (11/456-457), na al-Bidayah wan-Nihayah (14/36)

[12] Imetokana na ridhaa ya Ibn Hajr iliyopo mwisho mwa kitabu cha 'Radd al-Waafir'.

[13] Majmu’ al-Fataawaa (28/231-232) Imenukuliwa kutoka kwenye jarida la al-Istiqaamah Magazine, iliyonukuliwa kutoka Jarida la As-Sunnah Newsletter – http://www.qsep.com

[14] Ibn Taymiyyah, Hayaatuhu wa ‘Aswruhu wa Araauhu wa Fiqhuhu, uk. 519.

[15] Al'-Alaam al-'Aliyyah, uk. 68.

[16] Al-'Uquud ad-Durriyyah, uk. 179-194, al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/35 na as-Suluuk, 12/2.

[17] Taqiyyah (التقية) inatafsirikia kilugha kama “kuzungumza kinyume na imani ya ndani ya mtu.” Historia yote (inaonesha kwamba), Mashia wameitumia Taqiyyah kwa ajili ya kuepuka uchunguzi na kuepuka kukamatwa. Tendo la Taqiyyah linawaruhusu makundi ya Mashia kuenea na kukua. Kwa mujibu wa Mwanachuoni wa Kishia: “Ushia usingelienea iwapo kusingelikuwepo Taqiyyah.” (“Taaarikhush Shi’ah” cha Muhammad Husain Ja’far Sahiwal, uk.230). Imamu wa Kishia amesema kwamba Taqiyyah ni: “Kujichanganya pamoja nao (yaani wasiokuwa Mashia) kinjenje lakini kuwapinga kindanindani.” (Al-Kaafi, sura 9, uk.116).

[18] Al-'Uquud ad-Durriyyah, uk. 121.

[19] Imechukuliwa kupitia mtandao

 http://www.sunnahonline.com/ilm/seerah/0047.ht iliyoandaliwa na Abu Safwaan Fariyd

[20] Barua, Ibn Taymiyyah’s letters kutoka Jela.

[21] Al-Bidaayah wan-Nihaayah, 14/54.

[22] Al-'Uquud ad-Durriyyah, uk. 283.

[23] Al-A'laam al-'Aliyyah, uk. 82-83

[24] Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/138.

[25] Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/138.

[26] Katika ‘al-Bidaayah wan-Nihaayah’ (14/130), Ibn Kathiyr amesema: “Ahmad bin Hanbal amesema: “Waambie wazushi kwamba baina yetu na yao ni mazishi,” na hakuna shaka yoyote kwamba mazishi ya al-Imaam Ahmad yalikuwa na watu wengi na makubwa kwa namna na wingi wa watu wa mji huo ulivyokuwa, na namna ya watu walivyojikusanya kwa ajili yake na kumuheshimu, na serikali ikimpenda. Shaykh Taqiyud-Diyn amefariki ndani ya ardhi ya Damascus, na idadi ya watu wake haikufikia karibu na ile ya Baghdad kwa ukubwa. Hata hivyo, walijikusanya kwa idadi kuwa kwa mazishi yake hadi kufikia kwamba iwapo mtawala angeliwalazimisha watu wote kutoka nje, wasingelifikia kutoka nje katika idadi kubwa kama ilivyoonekana siku hiyo, na haya yote ni kwa mtu aliyefariki ndani ya ngome ya jela kwa amri ya mtawala.”

[27] The Lofty Virtues of Ibn Taymiyyah, ukurasa wa 7.

Share

10-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya Nane: Hadhi Na Cheo Chake

 

10- Shaykh Al-Islam Ibn Taymiyyah: SURA YA Nane: Hadhi Na Cheo Chake

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Mhuishaji[1]

 

Shaykh al-Islaam alikuwa ni katika mstari wa mbele miongoni mwa wahuishaji (Dini) wa kipindi hichi. Kwa sababu changamoto zake kwa wakati ule, watu waliokuwa wakimchukia katika zama zake walimtuhumu kuwa ni murtadi na watawala wakamtupa jela mara kadhaa.

 

Hata hivyo, Ibn Taymiyyah alikuwa ni Mwanachuoni mkubwa kwa wakati wake. Kiundani ni kwamba amesoma Fiqh kwa mujibu wa madhehebu ya Hanbali lakini hakujifunga nayo.

 

Alisoma vyanzo vya Shar’iah ya Kiislamu kwa undani wake na kuwa mtaalamu wa sayansi ya Kiislamu ambayo ikijulikana kwa enzi zile. Zaidi ya hayo, alipitia maandiko ya madhehebu mbalimbali ambayo yamepotea kutoka kwenye Uislamu, alisoma vitabu vya dini ya Kikiristo, Kiyahudi na madhehebu mbalimbali na aliandika kwa upana uchambuzi wake katika hayo yote.

 

Ibn Taymiyyah pia alichukua nafasi yake katika Jihaad dhidi ya Wamongoli ambao waliiteka sehemu za mashariki na kaskazini mwa dola la Abbasiyyah na kwa wakati ule walikuwa ni tishio kwa Misri na Afrika Kaskazini.

 

Wanafunzi wa Ibn Taymiyyah walikuwa miongoni mwa Wanachuoni wakubwa wa Kiislamu kwa wakati wao na walibeba kwa kizazi kinachofuata mabango (elimu) ya Ijtihaad na kuwarudisha katika vyanzo safi vya Uislamu alivyovinyanyua yeye. Miongoni mwao ni Ibn al-Qayyim, Mwanachuoni mkubwa katika nyanja za Fiqh na Hadiyth, adh-Dhahabiy, mtaalamu katika uchambuzi wa Hadiyth na Ibn Kathiyr, mtaalamu wa Tafsiyr, Taariykh na Hadiyth.

 

Allaah Alimfanya Yeye Kuwa Ni Mtu Wa Daraja Ya Juu Na Mpambanuzi Wa Ukweli Na Uongo[2]

 

Hili ni jambo ambalo pia likijulikana. Yeye (Allaah Amrehemu) hakuwa na kitabu hata kimoja au fatwa isipokuwa kwamba alichagua ndani yake maandiko mazito na ushahidi yakinifu juu ya yote, na akaingiza pia neno la ukweli pamoja na ushahidi mwingi wa wazi na ushahidi ambao yeyote atakayezipitia akiwa na dhana safi, moyo wake utakuwa ubaridi kwa hoja na dalili hizo na hatimaye utafungika kwamba ni ukweli usio na shaka. Katika maandiko yake yote unaona kwamba iwapo Hadiyth ni sahihi, moja kwa moja anaichukua na anaifanyia kazi, na kuiweka mbele juu ya maoni ya Mwanachuoni au Mujtahid yeyote.

 

Mfuatiliaji asiyefungamana na upande wowote atagundua kwamba maneno yake yalikuwa yanaenda kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah, na wala haendi kinyume na maneno yake kwa maneno ya mtu mwengine, hata ikiwa kwamba mtu huyo awe vipi, na wala hakuwa na hofu ya mtawala, mamlaka, mijeledi, au upanga kwa kufanya hivi, na wala hatayatupa (maneno yake) kwa maoni ya mtu mwengine yeyote. Alikamatana vyema kabisa kwa mshiko wa kisawasawa, akiifanyia kazi Maneno Yake Mtukufu:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾

 

Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi. [An-Nisaa: 59]

 

Na: 

 

وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ ۚ ﴿١٠﴾

 Na katika lolote lile mlilokhitilafiana, basi hukumu yake ni kwa Allaah. [Ash-Shuwraa: 10]

 

Sikupatapo kusikia mtu yeyote aliyejulikana kama alivyo yeye katika umakini wa hali ya juu wa kufuata Qur-aan na Sunnah, jitihada zake katika kuzichambua maana zake, na matendo yake yaliegemea katika amri zake. Hakupatapo kupitia jambo ambalo Wanachuoni hapo kabla wametoa hukumu isipokuwa yeye akichagua iliyo na nguvu na iliyo karibu na Qur-aan na Sunnah kutokana nazo. Allaah Alimbariki kwa sifa hii, na Akamfanya kuwa ni mtu mwenye amri kwa watu wa enzi zake.

 

Hii ilifikia hali hadi kwamba watu wanaotoka sehemu za mbali kumtumia kwake yeye kwa fataawa kuhusiana na hali zao, na huwa wakimuuliza awasaidie kuondosha utata wao waliokuwa nao kuhusiana na hili na lile. Hivyo, huwatuliza nyoyo zao kwa majibu yenye kutosheleza, yanayoshikika, na mara zote huegemeza msimamo wake kwa uthibitisho ulio wazi kutoka kwa maelezo halali ya Wanachuoni, hadi kwamba mtu yeyote mwenye uoni, elimu, na hayaa aliyeacha utashi wake na kukutana nazo huzikubali, na ukweli huwa wazi kwao.

 

Iwapo mtu atasikika kumpinga au kuvamia heshima yake, mara zote hutokezea kuwa hao ni watu wanaotambulikana na watu wengi kuwa ni watendaji maovu, na yeyote anayependa kuthibitisha haya ninayosema, mwache aangalie kwa jicho la uoni, kwani hatoona Mwanachuoni kutoka ardhi yoyote anayemfuata Imaam huyu na kutambua sifa na uongozi aliotunukiwa na Allaah, na humsifu kwa kila mkusanyiko isipokuwa kwamba katika nyuma ya kila Mwanachuoni wao ni wafuasi wakorofi wa Qur-aan na Sunnah, na wenye kushughulishwa (na dunia) katika kuitafuta Akhera na (ingawa) ni wenye kuitaka, na wao ni wenye kuwepo mbali kutokana na ukwepaji au kuwa na ujinga nayo.

 

Vivyo hivyo, hutopata kuona Mwanachuoni hata mmoja akimpinga yeye na kuchukuliwa kwa uadui isipokuwa kwamba ni mwenye bidii miongoni mwao katika kuzitafuta lahwa za dunia, na ni wa juu wao katika kujionesha na kutafuta sifa, na ni wa mwisho wa ustaarabu katika tabia njema, mwenye kushirikiana na wanyanyasaji katika majaribio yao, na mwenye pupa miongoni mwao kusema uongo. Ukiangalia wale waliokuwa wakimpenda na wale wasiompenda kuanzia kwa asiyejua (hata) kusoma, utaona wao kwamba kuwa ni waadilifu kama vile nilivyoyaelezea hayo makundi mawili ya Wanachuoni hapo juu. Nimejaribu kuonesha na kufikiria kwa yale niliyosema hapo juu, na nimegundua kwamba ni haswa kabisa kama nilivyoeleza.

 

Naapa kwa Allaah, sitoacha mbele ya yeyote kuzungumza haya, na yeyote mwenye shaka kwa ninayosema, basi na ajifikirie yeye mwenyewe na ataona kwamba yale ninayosema iwapo atajiondolea ufuniko wa shahawa zake. Hii si kesi isipokuwa kwa sababu Allaah Ametambua usafi makini wa Imaam huyu, na ukweli na kujitolea kwake katika kutafuta Ridhaa za Rabb wake na kuifuata Sunnah ya Nabiy Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).[3]

 

 

Hadhi Yake Miongoni mwa Wanachuoni wa Enzi Zake

 

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (Allaah Amrehemu) alikuwa na hadhi bora miongoni mwa Wanachuoni wa enzi zake. Hii ni kutokana na sababu nyingi, kama vile uwezo wake wa kusawazisha mambo ambayo yenye utata kwa Wanachuoni wengine wa enzi zake, kama vile suala la kuwapiga vita Matartar na suala la upotofu uliotoka kwa kundi la Maraafidhah.[4] Ibn Taymiyyah aliyapigia mbizi masuala haya na kuyatolea ufafanuzi kwa watu.

 

Mnamo mwaka 701H, Myahudi mmoja kutoka Khaybar akidai kwamba alikuwa na barua kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ambayo ikipinga (hukumu sahihi ya) Jizyah[5] ambayo Mayahudi (na wengine wasio Waislamu) walilazimika kuilipa kwa Waislamu. Ibn Taymiyyah aliweka bayana uongo wake na kuipitia mapungufu yake na kuitoa thamani barua hiyo ya uongo kutokana na maelekezo ya Hadiyth na pia kwa kuegemezea elimu ya historia.[6]

 

Wakati huo huo, Ibn Taymiyyah akiwa jela mjini Cairo, Ibn Kathiyr anasema: “Masuala ya kishari’ah yaliyo magumu yalikuwa yakiletwa kwake kutoka kwa magavana na watu mahsusi, ambayo ‘Ulamaa walikuwa hawawezi kuyafanyia kazi, na yeye huyajibu kutoka kwa Kitabu na Sunnah katika namna ambayo akili huwekwa wazi.”[7]

 

Sababu nyengine ni nafasi yake katika Jihaad; alikuwa si tu kwamba ni askari mwenye nguvu lakini pia mueleweshaji na muongozaji. Alifuatwa baadaye kutoa ushauri na mikakati ya kivita.

 

La muhimu zaidi, moja kati ya sababu kuu zilizokuwa ni msukuwa wa kuhodhi nafasi bora kabisa miongoni mwa Wanachuoni na watu wanaofanana naye ni uwezo wake wa kuelezea elimu. Pale anapotoa mhadhara; anapofikisha mazungumzo; anapotoa hukumu ya kishari’ah; anapoandika barua au kuandika kitabu katika nyanja yoyote, huzalisha kiwango cha elimu ambacho kipo mbali kabisa na kuwashinda Wanachuoni wengine wa wakati wake. Hii ndio sababu ya Ibn Taymiyyah kuwa ni sehemu ya rejeo miongoni mwa watu. Popote watu wawili wanapokutana na mgogoro kuhusiana na suala – na huenda wakawa ni watu wenye elimu na wanafunzi mfano wa hao kama ilivyoonekana kwenye baadhi ya masuala – mawazo yake huwa ndio sababu ya masawazisho baina yao.

 

 

[1] Evolution of Fiqh uk. 144 cha Dr. Bilal Philips.

[2] The Lofty Virtues of Ibn Taymiyyah, uk. 30.

[3] Kama ilivyotajwa na al-Haafidh al-Bazzaar ndani ya kitabu cha ‘The Lofty Virtues of Ibn Taymiyyah’, uk. 30.

[4] Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/78.

[5] Ni kodi ya kichwa wanayolipa wasiokuwa Waislamu waliobaleghe katika dola ya Kiislamu kwa misingi maalum na wao kupata hifadhi na uhuru wa kuabudu na kuwasaidia wao na mafakiri wao na wasiojiweza. Hii ni kutokana na Qur-aan, Suwraah Tawbah, 29:

قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ﴿٢٩﴾

Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho, na wala hawaharamishi Aliyoyaharamisha Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafuati Dini ya haki miongoni mwa wale waliopewa Kitabu, (piganeni nao) mpaka watoe jizyah (kodi) kwa khiyari, wakiwa hali ya kurudi chini kutii. [At-Tawbah: 29]

[6] Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/19.

[7] Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/46.

 

 

Share

11-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya Tisa: Wanachuoni Walivyomsifu

 

11- Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya Tisa: Wanachuoni Walivyomsifu

 

Alhidaaya.com

 

 

Wanachuoni Walivyomsifu[1]

 

Wanachuoni wengi wa wakati wake na baada ya wakati wake walikuwa wakimsifu Shaykh al-Islaam kwa elimu yake, ikhlaasw yake, hayaa, ucha Mungu wake, na kufuata kwa ukaribu mwendo wa Salaf. Matamko mengi katika haya ya kumsifia yamekusanywa ndani ya kitabu kilichoandikwa na al-Haafidh Ibn Naaswir ad-Diyn kilichopewa jina la ‘Radd al-Waafir’ kikikana dai lililochupa mpaka, lile ambalo linadai kusema kwamba Ibn Taymiyyah, ‘Shaykh al-Islaam’, hakuwa na imani.

 

Baadhi ya maneno haya ya kumsifia na matamko ya kumkubali Imaam huyu hayakuja tu kutoka kwa wanafunzi wake na wafuasi wake, lakini pia kutoka kwa maadui zake waliotoa uhibitisho kwamba amevuka kiwango cha elimu na ufahamu, na halikadhalika wametoa ushuhuda wa jitihada yake, ukarimu na Jihaad yake kwa ajili ya Allaah na kwa ajili ya kuutetea Uislamu. Yanafuatia baadhi ya maneno haya ya kumsifia na kumtamkia:

 

 

-Shaykh Ibn Naaswir ad-Diyn ad-Dimashqiy ameandika kitabu kiitwacho ar-Radd al-Waafir ‘ala man za’ama anna man sammaa Ibna Taymiyyah Shaykh al-Islaam kaafir, ambacho ndani yake amekana Mahanafi waliokithirisha na waliodai kwamba hairuhusiki kumuita Ibn Taymiyyah “Shaykh al-Islaam”, na kwamba yule ambaye atafanya hivyo atakuwa ni kafiri! Ndani yake (kitabu hichi) anataja Imamu themanini na tano (85), wote ambao wamemtaja Ibn Taymiyyah kama ni Shaykh al-Islaam, na kunukuu maneno yao kutoka kwenye vitabu vyao kwa athari hiyo. Pale al-Haafidh Ibn Hajar (Allaah Amshushie rehema zake) aliposoma kitabu hichi – ar-Radd al-Waafir – alikiandikia utangulizi, ambao alisema:

 

Shukrani zote ni za Allaah, amani iwe juu ya waja Wake na ambao Amewachagua.

 

 

Nimekutana na kitabu hichi chenye manufaa na kugundua namna elimu ya ndani ya Imaam (Ibn Taymiyyah) aliyoandika, na namna alivyo mahiri katika matawi mengi ya elimu, hadi kufikia kuwa ni Mwanachuoni mkubwa mwenye kuheshimika na kusifika kwa Wanachuoni. Nafasi yake maarufu aliyokuwa nayo Shaykh Taqiyud-Diyn (Ibn Taymiyyah) kama ni Imaam, ni yenye kuangaza kuliko jua, na jina lake kama ni Shaykh al-Islaam kwa wakati wake limeendelea kubakia hadi leo na litaendelea kubakia hadi kesho. Hakuna anayekataa hilo isipokuwa yule aliyekuwa ni mjinga wa nafasi yake mwenyewe, au asiyekuwa muadilifu. Ni namna gani atakuwa mkosefu yule anayefikiria hivyo na kwa namna gani atakuwa amekwenda mrama. Allaah ni Mmoja Ambaye tunamuomba kutulinda sisi kutokana na maovu ya nafsi zetu na ndimi zetu kwa baraka Zake na uongofu. Iwapo kungelikuwa hakuna ushahidi mwengine wa hadhi kuu ya mtu huyu isipokuwa kutoka kwa yale yaliyoelezewa na al-Haafidh ash-Shahiyr ‘Ilm ad-Diyn al-Barzaaliy ndani ya kitabu chake Taariykh, (pale aliposema):

 

 

 

“Kulikuwa hakuna mtu ndani ya historia ya Uislamu ambaye maziko yake watu walikusanyika kama walivyofanya kwa maziko ya Shaykh Taqiyud-Diyn (Ibn Taymiyyah). Ameweka bayana kwamba maziko ya Imaam Ahmad yalihudhuriwa na mamia kwa maelfu (laki kadhaa), lakini idadi ya Damascus ingalikuwa inalingana na ya Baghdad, au zaidi, basi hakuna mtu ambaye angejaribu kukaa mbali ya maziko yake. Zaidi ya hivyo, wote ambao walikuwepo Baghdad, isipokuwa kwa wachache, wakiamini katika uongozi wa Imaam Ahmad. Mtawala na Khaliyfah wa Baghdad kwa kipindi hicho alikuwa na nafasi kubwa ya mapenzi na heshima kwake. Hii ni tofauti na kesi ya Ibn Taymiyyah, kwa mtawala wa mji kutokuwepo wakati wa kifo chake, na Mafuqahaa walio wengi ndani ya mji huo walijitengea kikundi dhidi yake, na alikufa akiwa kifungoni ndani ya ngome. Lakini juu ya yote, hakuna aliyekaa mbali ya maziko yake au kushindwa kumtakia rehema yeye na kuomboleza, isipokuwa watu watatu tu (waliokuwa na chuki naye) waliokaa mbali kwa hofu ya hamaki za watu wengi.

 

Ingawa idadi hizi kubwa zilifika mazikoni, kulikuwa hakuna msukumo kwa hilo isipokuwa kwamba alikuwa ni mtu mkubwa na hamu yao ya kutaka malipo kwa kuhudhuria maziko yake. Hawakujikusanya kwa amri za watawala au kwa sababu nyengine yoyote. Imesimuliwa kutoka kwenye simulizi sahihi kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Nyinyi ndio mashahidi wa Allaah juu ya ardhi”[2]

 

Idadi kadhaa ya Wanachuoni wakimpinga Shaykh Taqiyud-Diyn kwa mara nyingi, kwa sababu ya hoja za kupingana naye ambazo ziliendana na masuala mbalimbali ya msingi na yale madogo. Kesi nyingi zilifunguliwa dhidi yake mjini Cairo na Damascus, lakini hakuna ripoti inayosema kwamba alikuwa ni kafiri na kulikuwa hakuna hukumu inayosema kwamba auawe, ingawa kulikuwa na watu wengi ndani ya serikali kwa wakati huo waliokuwa wakimpinga kwa nguvu zao zote, na alifungwa jena mjini Cairo, kisha baadaye Alexandria. Juu ya yote hayo, wote waliikubali elimu yake pana na hayaa zake za ndani kabisa na ikhlaasw yake, na wakimtambua kama ni mkarimu na mwenye juhudi, halikadhalika kwa kuutetea kwake Uislamu na kuwaita watu kwa Allaah kwa siri na dhahiri. Ni kwanini tusimdumaze yule anayesema kwamba alikuwa ni kafiri au yule anayemuita Shaykh al-Islaam ni kafiri, wakati hakuna kitu chochote kinachoonesha ukafiri wake?

 

Hapana shaka yoyote kwamba alikuwa ni Shaykh wa Uislamu, na masuala aliyoyapinga yalikuwa si vitu ambavyo amesema kutegemeana na matakwa na mapenzi yake, na wala hakusisitiza kuvizungumzia baada ya ushahidi uliofafanuliwa dhidi ya wakorofi. Vitabu vyake vimejazwa na hoja za kuwakana wale waliohamasisha elimu isiyoyastaarabika na yeye kuwakataa. Lakini hata hivyo, yeye alikuwa ni mwanaadamu ambaye aliweza kupata na kukosea. Yale ambayo alikuwa ni sahihi – ambayo ni mengi, yanaweza kuwa na manufaa, na tunaweza kumuombea rehma kwake kutokana na hayo, na yale ambayo amekosea basi yasifuatwe, lakini anaweza kutolewa udhuru kwa hilo, kwa sababu Imaam wa wakati wake wameshuhudia kwamba alikuwa na kila sifa ya Ijtihaad; hata yule ambaye anampinga kwa nguvu zote na kujitahidi kumsababishia madhara, akiitwa Shaykh Kamaalud-Diyn al-Zamalkaaniy, ameshuhudia juu ya hilo, kama alivyofanya Shaykh Sadrud-Diyn Ibn al-Wakiyl, ambaye alikuwa peke yake aliyeweza kufanya mjadala pamoja na Ibn Taymiyyah.

 

Wala haishangazi kwamba mtu huyu alikuwa mpinzani aliyeaminiwa na wazushi kama vile Raafidhah, Huluuliyyah na Ittihaadiyyah, ambao maandiko juu ya hilo ni mengi na maarufu, ambayo fatwa zao kuhusiana nao ni mengi kuweza kuyahesabu. Ni namna gani wangelikuwa na furaha kutambua kwamba kuna watu wanaomtuhumu kwa kufuru na kusema kwamba yule asiyemtambua kuwa ni kafiri basi ni kafiri. Yule aliyedai kuwa na elimu, iwapo ana sababu ama hisia, basi na apigie mbizi maneno ya mtu huyo ndani ya vitabu vyake, au kusikia kutoka kwa wasimulizi waaminifu na wakweli, ili kwamba aweke mbali yale anayoyaona kuwa ni pingamizi na kuwaonya wengine kwa njia ya ukweli, na kumsifia kwa masuala aliyokuwa sahihi, kama vile tabia ya Wanachuoni wengine walivyokuwa.

 

Iwapo hakuna sifa yoyote nzuri ndani yake yeye isipokuwa kwa ukweli kwamba alikuwa ni mwalimu wa Shaykh Shamsud-Diyn Ibn Qayyim al-Jawziyyah, mwandishi wa vitabu vingi vyenye manufaa, ambavyo kila mtu amenufaika navyo, basi hilo linatosha kuonesha nafasi yake ya juu. Je, ni kwa namna gani pale uweledi wake ndani ya nyanja tofauti za elimu na usomaji wake wa kipekee wa maandiko ulivyothibitishwa na Mashaafi’iy wakubwa wa enzi zake na wengineo, na zaidi kwa Mahanbali?

 

Hakuna haja ya kutilia maanani kwa yule anayemuita kuwa yeye ni kafiri juu ya mafanikio yote, au yule anayemtambua kuwa anayemuita “Shaykh al-Islaam” kuwa ni kafiri, bali atakayedai hivyo adharauliwe kwa mnasaba wa jambo hili; kwa hakika ajibiwe kwa namna ya kumkana kutokana na kusema hivyo, hadi pale atakaporudi katika ukweli. Allaah Anazungumza ukweli na Anawaongoa watu katika njia sahihi; Allaah Anatutoa sisi na Yeye Ndiye bora wa kuyaharibu mambo.[3]

 

Al-Haafidh Ibn Hajar[4] ametoa maelezo mbalimbali katika sehemu tofauti kuhusiana na Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah, ambaye amethibitisha kwamba alikuwa ni mtu wa elimu na mwema aliyeihami Sunnah. Nukta ambazo al-Haafidh Ibn Hajar (Rahimahu Allaahu) amempinga Shaykh al-Islaam zinaweza kutohesabiwa, na kuna wale ambao wamempinga Ibn Hajar yeye mwenyewe katika baadhi ya mambo ya Aqiydah. Isipokuwa tutanukuu yale ambayo yeye amesema kumsifia Shaykh al-Islaam, kwa minaajili ya kuweka bayana makosa ya wale wanaosema kwamba al-Haafidh (Rahimahu Allaahu) hakuwa ni mwenye kumuheshimu Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah.

 

Kinachofuatia ni kuangalia kwa juu juu yale aliyosema al-Haafidh Ibn Hajar (Rahimahu Allaahu) kuhusiana na Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaahu).

 

-Al-Haafidh Ibn Hajar ameandika wasifu mrefu wa Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaahu) ndani ya kitabu chake cha ad-Durar al-Kaaminah, mwanzoni amesema:

 

 

“Baba yake amemchukua kutoka Harraan ndani ya mwaka 667H, na akajifunza kutoka kwa ‘Abdud-Daa’im, al-Qaasim al-Arbiliy, Muslim Ibn ‘Allaan Ibn Abi ‘Umar na al-Fakhr, miongoni mwa baadhi tu. Amesoma mwenyewe na kunukuu Sunan Abi Dawuud, na kusoma ar-Rijaal (wasimulizi wa Hadiyth) na al-ilal (makosa ndani ya Hadiyth). Amepata elimu ya ndani kabisa, na akajitofautisha na kwenda mbele zaidi ya wengine. Ameandika vitabu, kusomesha na kutoa fatwa, na amewashinda wenziwe. Alikuwa na uwezo wa ajabu wa kukusanya tena mara moja; alikuwa ni Mujtahid; alikuwa na elimu ya ndani katika masuala ya maandiko na hoja; na alikuwa na uwezo wa kujadili masuala kwa undani kwa kuegemea maoni ya Wanachuoni wa mwanzo wa baadaye.”[5]

 

- Ibn Hajar amenukuu ndani ya wasifu wake maandiko mengi ya Maimaam waliomsifia Shaykh al-Islaam (Rahimahu Allaahu) na kuuthibitsha usomi wake katika hoja na nyanja za maandiko ya elimu. Kwa mfano, amesema:

 

 

“Nimesoma katika maandishi ya al-Haafidh Swalaahud-Diyn al-‘Alaa’iy pale alipoandika kuhusu wasifu wa Shaykh wa ma-Shaykh, al-Haafidh Bahaaud-Diyn ‘Abdullaah Ibn Muhammad Ibn Khalily, yafuatayo: Bahaaud-Diyn huyu amejifunza kutoka kwa Mashaykh wawili, Shaykh wetu, na mtaalamu na kiongozi wa njia ya Allaah, Shaykh mkubwa, yule anayeongoza wafuasi wake katika njia bora, yule ambaye alikuwa na sifa karimu nyingi na ushahidi wa nguvu, ambao mataifa yote wanathibitisha kwamba hawataweza kuorodhesha ushahidi wote huu; Rabb Atujaalie na sisi kusoma kutoka kwenye elimu yake kubwa na kunufaika nayo sisi kwa njia za elimu yake ndani ya dunia hii na Akhera. Huyo ni Shaykh, Imaam, Mwanachuoni, mwalimu, nyota inayong’ara, Imaam wa Imaam, Baraka ya Ummah, kiongozi wa Wanachuoni, mfano wa watu kuufuata, mwangaza wa wasomi, mnyanyasaji wa wazushi, bahri ya elimu, hazina ya wale wanaotafuta manufaa, Mfasiri wa Qur-aan, maajabu ya wakati wetu, asiyeshindwa (kwa hoja sahihi) kwa wakati wetu, Taqiyud-Diyn, Imaam wa Waislamu, ushahidi wa Allaah dhidi ya dunia, ni mmoja wa watu wanaojumuika na watu wa kweli, mfuataji wa waliopita kabla yake, mwenye kuukubali ukweli, alama ya uongofu, muhifadhi wa juu, mwenye hadhi ya juu ya kuzungumza kwa ufasaha, nguzo ya Shari’ah, mwenye kuhodhi elimu bora kabisa, Abul-‘Abbaas Ibn Taymiyyah.”[6]

 

Ingawa hayo maandiko niliyoyanukuu au kuyarejea, yana maneno ya al-Haafidh Ibn Hajar (Rahimahu Allaahu) au ambayo yamenukuliwa na al-Haafidh kutoka kwa wengine, kuzungumzia heshima ya Shaykh al-Islaam na kuweka bayana hadhi yake ndani ya nyanja ya elimu za Diyn, kwamba haimaanishi kuwa al-Haafidh hakupingana na Shaykh al-Islaam hata kidogo ndani ya baadhi ya maeneo ya elimu, au kwamba hakupatapo kumpinga (kielimu), kwa sababu kikawaida inatokezea kwamba Mwanachuoni mmoja hupingana na mwengine, bila ya ulazima wa kumaanisha kwamba yule anayepingana na mwengine hamuheshimu au hakubaliana na hadhi ya huyo mwengine, achilia mbali kumtuhumu kwa uzushi au upotofu. Hapo zamani, Imaam Maalik (Rahimahu Allaahu) alizungumza maneno yake maarufu: “Maoni ya mtu yeyote yanaweza kukubaliwa au kukataliwa, isipokuwa kwa yule aliomo ndani ya kaburi hili” au maneno yenye maana kama hiyo – kwa maana ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Bila ya kujali nani alikuwa sahihi katika suala fulani, iwapo alikuwa ni Shaykh al-Islaam au yule ambaye anayetofautiana naye au amejaribu kupingana naye, al-Haafidh Ibn Hajar au mtu mwengine yeyote, itakuwaje iwapo yule aliyekuwa sahihi katika masuala mengi ambayo wanapingana naye, ni Shaykh al-Islaam? (Rahimahu Allaahu)[7]

 

- Imaam adh-Dhahabiy (Rahimahu Allaahu) amesema, akiorodhesha mashaykh wake:

 

 

“Ni Shaykh wetu, Shaykh wa Uislamu, asiyeshindwa (na mtu) kwa wakati wetu katika masuala ya kielimu, juhudi, ufahamu, umahiri wa kiroho, ukarimu, ukweli mbele ya Ummah, uamrishaji mema na ukatazaji mabaya, na usomaji wa Hadiyth – ametumia jitihada zake kubwa katika kuitafuta na kuiweka katika maandishi, na amepitia aina ya wasimulizi tofauti na kuipata elimu ambayo hakuna mtu mwengine aliyeipata.

 

Amekithirisha katika kuifasiri Qur-aan (tafsiyr) na amechungua kwa ndani katika upambanuzi wake wa maana. Amefikia tafsiri kutokana nayo ambayo hakuna mwengine yeyote aliyeweza kufanya hivyo kabla yake. Pia amekithirisha katika Hadiyth na uhifadhiji wake; ni wachache mno wamehifadhi Hadiyth nyingi kama alivyofanya yeye. Amezifanyia marejeo Ahaadiyth kwa vyanzo vyake muafaka na wasimuliaji wake, na alikuwa na uwezo mwepesi wa kunukuu chochote anachotaka kuthibitishia ushahidi. Amewapita watu wote katika elimu ya Fiqh na maoni tofauti ya madhehebu mbalimbali, na fatwa za Swahaba na Taabi’iyn, hadi kufikia kwamba pale suala la fatwa linapokuwa haliendani sambamba na maoni ya madhehebu, basi yeye anaegemeza fatwa yake katika maoni ambayo yanakubaliwa kwa ushahidi ulio mzito. Amekithirisha elimu ya lugha ya Kiarabu, na kusoma masuala katika kiwango cha fikra na hoja. Amesoma maoni ya wanafilosofa na kuzipinga hoja zao na kuweka bayana makosa yao na kuwaonya dhidi yao. Ameichukua Sunnah kwa ushahidhi na uthibiti ulio na nguvu. Alidhuriwa kwa ajili ya Allaah na wapinzani wake na kuchunguzwa kwa kukubali kwake Sunnah iliyo safi, hadi pale Allaah Alipomsababishia kuwa bora na kuwafanya waongofu kuungana katika kumpenda yeye na kumuombea du’aa, na kuwakomesha maadui zake na kuwaongoa watu wa makundi na madhehebu mengine kupitia kwake yeye. Allaah Amewafanya wafalme na makamanda kumganda katika kumfuata yeye na kumtii, na ameihuisha Syria – na bila ya shaka Uislamu – kupitia juhudi zake, pale ilipokaribia kushindwa, kwa kujadiliana na watawala kuwakataa Matartar, pale watu walipokaribisha tashwishi kuhusiana na Allaah na Waumini wakajaribiwa na kutikisika kwa mtikisiko mkubwa (rudia al-Ahzaab 33: 10-11) na wanafiki wakawa na nguvu.

 

Sifa zake nzuri ni nyingi, na yeye ni mtu mkubwa kwa mtu kama mimi kuzungumzia maisha yake. Iwapo mimi nitaahidi kula kiapo baina ya Pembe na Maqaam nitaapa kwamba sijapata kuona mtu mfano wake yeye, na kwamba yeye hajaona mtu mfano wake yeye mwenyewe.”[8]

 

-Al-Haafidh ‘Imaadud-Diyn al-Waasitwiy (Rahimahu Allaahu) amesema:

“Naapa kwa Allaah, hakujapatapo kuonekana chini ya kipaa cha juu cha mbingu mtu yeyote mfano wa Shaykh wenu Ibn Taymiyyah kwa elimu, matendo mema, tabia, mambo yake, kushikana kwake na Sunnah, ukaribu, kujizuia na kutenda majukumu ya Allaah pale mipaka Yake mitukufu inapovunjwa; alikuwa ni mtu muaminifu kuliko mtu yeyote, mwenye ufahamu mkubwa zaidi wa elimu, mwenye athari zaidi, mwenye umakini zaidi katika kuutetea ukweli, mwenye ukarimu zaidi, mbora zaidi katika kufuata Sunnah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hatujapatapo kuona yeyote ndani ya wakati wetu anayefafanua mfano wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Sunnah zake katika maneno na matendo kuliko mtu huyu; mwenye moyo wenye kuelewa atashuhudia kwamba hii ni kufuata Sunnah katika namna sahihi ya neno.”[9]

 

-Al-Haafidh Jalaalud-Diyn as-Suyuutwiy (Rahimahu Allaahu) amesema:

“Ibn Taymiyyah, Shaykh, Imaam, ‘Allaamah (Mwanachuoni mkubwa), muhifadhiaji, mpinganiaji, Faqiyh, Mujtahid, Mfasiri bora kabisa, Shaykh wa Uislamu, kiongozi wa ikhlaasw, asiyeshindwa katika wakati wetu, Taqiyud-Diyn Abul-‘Abbaas Ahmad al-Mufti Shihaabud-Diyn ‘Abdul-Haliym, mtoto wa Imaam na Mujtahid Shaykh al-Islaam Majdud-Diyn ‘Abdus-Salaam Ibn ‘Abdillaah Ibn Abil-Qaasim al-Haraaniy.

 

 

Mmoja miongoni mwa alama za watu wakubwa, alizaliwa Rabiy’ al-Awwak 661 AH, na kujifunza kutoka kwa Ibn Abil-Yasaar, Ibn ‘Abdil-Daaim, na baadhi ya wengine.

 

 

Amechukua hamu ya kujifunza Hadiyth, na kusimulia na kuchagua (Ahaadiyth za maana); amekithirisha katika kusoma wasifu wa wasimuliaji, mapungufu katika Ahaadiyth, Fiqh, sayansi ya Uislamu, ‘Ilm al-kalaam na nyanja nyenginezo. Alikuwa ni mtu mwenye kasi ya kusoma, moja kati ya Wanachuoni wahodari wachache, mwenye ikhlaasw na mtu pekee. Ameandika vitabu mia tatu, na alijaribiwa na kuchunguzwa mara chungu nzima. Amekufa mwishoni mwa mwezi wa Dhu’l-Qa’dah mwaka 628 AH. “[10]

 

-Al-Haafidh al-Bazzaar amesema, akiwaandikia wapinzani wa Ibn Taymiyyah:

 

“Hamtapata kuona Mwanachuoni akimpinga yeye (Ibn Taymiyyah), akimzuia yeye, akiwa na hamaki kwake, isipokuwa kwamba alikuwa na uchu zaidi wa hayo katika kuyakusanya mazuri ya dunia, wenye hila na ujanja zaidi katika kuyapata hayo, mwenye shauku zaidi kuliko wote, mwenye hamu ya sifa… na mwenye kufanya mengi kuliko mwengine katika uongo kwenye ulimi wake.”[11]

 

-Al-Haafidh adh-Dhahabiy amesema:

“Ilikuwa inashangaza pale alipotaja juu ya suala ambalo kuna tofauti ya mawazo, na pale alipotoa ushahidi na kuamua wazo lililo na nguvu – na alikuwa na uwezo wa kuitekeleza Ijtihaad kwa sababu ya yeye kutimiza masharti yake. Sijapata kuona mtu aliyekuwa na kasi kuliko yeye ya kurudia Aayah ambayo imegusa lile suala analolifikia maamuzi, wala mtu aliyekuwa na nguvu katika kurudia maandiko na kutaja vyanzo vyake. Sunnah ilikuwa ipo mbele ya macho yake na katika ncha ya ulimi wake kuna misamiati safi na jicho lililo wazi.

Alikuwa ni alama miongoni mwa alama za Allaah katika tafsiyr na kuielezea. Kwa mnasaba wa msingi wa Diyn na elimu ya hitilafu - ya mawazo (katika suala fulani) basi yeye alikuwa hana mpinzani – hii ni pamoja na ukarimu, juhudi na kutotilia maanani matashi ya nafsi.

 

Na labda kanuni zake za kishari’ah katika aina mbalimbali za sayansi zilifikia vitabu (mijalada) mia tatu (300), au zaidi na mara zote alikuwa akizungumzia ukweli kwa ajili ya Allaah, bila ya kujali malalamiko yaliyomfikia.

Yeyote anayeshirikiana naye na kumtambua vyema  atanituhumu kwa kutokuwa na uaminifu kwa upande wake. Yeyoye anayempinga na kupingana naye atanituhumu kwa kupitilisha mambo, na nimekuwa mkosa kwa pande zote – wafuasi wake na wapinzani wake.

 

Alikuwa na ngozi ya rangi nyeupe na nywele nyeusi na ndevu nyeusi pamoja na nywele za jivujivu. Nywele zake zilifikia ndewe za sikio. Macho yake yalikuwa fasaha (kama) ulimi, na alikuwa na kifua kipana na chenye sauti safi pamoja na usomaji wa haraka. Alikuwa ni mwenye kuhamaki mara moja lakini mwenye kuibatilisha kwa subra na kujizuia.

 

Sijaona mfano wake yeye kwa kumuomba (yeye Allaah) na kutaka msaada Kwake Yeye, na kuwa na hisia sana kwa wenziwe. Hata hivyo, siamini kwamba yeye alikuwa ni mkamilifu, isipokuwa ninapingana naye; msimamo mkali na masuala madogo, kwani yeye – ingawa ana elimu pana, juhudi kubwa, na akili nyingi, na kwa mnasaba wa kuisafisha Diyn – alikuwa ni mtu miongoni mwa watu. Anaweza kupitikiwa na umakini na hamaki ndani ya mjadala, na kuwavamia wapinzani wake (kimaneno) hivyo kuotesha uadui ndani ya nyoyo zao dhidi yake.

 

Kama tu angelikuwa mlaini kwa wapinzani wake basi kungelikuwa na makubaliano kwa ajili yake (angekubalika na wote) – kwani hakika Wanachuoni wakubwa wameikubali elimu yake, wamekubali uwezo wake na ukosefu wa makosa, na kukiri kwamba alikuwa ni bahri isiyokuwa na mipaka na hazina isiyokuwa na mfano. Hata hivyo, wamefikia nafasi ya kujisikia na homa dhidi yake… na kila maneno ya mtu yanaweza kuchukuliwa ama kuachwa.

 

Alikuwa akisimamisha Swalaah na kufunga, kuzitukuza Shar’iah kinje na kindani. Alikuwa hatoi fatwa katika namna ya ufahamu mdogo kwani alikuwa na ufahamu mzuri kabisa, wala kwa namna ya ukosefu wa elimu kwani alikuwa ni bahri inayoelea. Wala hakuwa akiichezea Diyn lakini (akiitumia) kufikia katika ushahidi kutoka kwenye Qur-aan, Sunnah na Qiyaas na kuthibitisha na kujadiliana kwa kufuata nyayo za Maimaam waliomtangulia, hivyo alikuwa na malipo iwapo amekosea na malipo mara mbili iwapo amepatia.

 

Aliwahi kuumwa ndani ya Qasri (ambalo amefungiwa humo) akiwa na maradhi mabaya mno hadi alipokufa mnamo usiku wa Jumatatu ya 20 ya mwezi wa Dhul Qa’dah, na wakamswalia katika Msikiti wa Damascus. Na baadaye wengi wakamzungumzia kuhusiana na idadi iliyohudhuria mazishi yake, na idadi ya chini iliyotolewa ni alfu hamsini.”[12]

 

-Adh-Dhahabiy pia amesema:

 “Yeye ni zaidi wa ubora kuliko mfano wangu kuelezea sifa zake. Iwapo nitalazimishwa kuapa (kwa Allaah) katika pembe (ya Ka’bah) na sehemu ya (Maqaam Ibraahiym), nitaapa kwamba sijapata kuona kwa macho yangu mawili mfano wake yeye na kwa Allaah, yeye mwenyewe hajaona mfano wake yeye katika elimu.”[13]

 

- Ibn Hajr al-Asqalaaniy amesema:

“Shaykh wa Mashaykh wetu, al-Haafidh Abu al-Yu’mariy (Ibn Sayyid an-Naas) amesema ndani ya wasifu wake wa Ibn Taymiyyah: ‘Al-Mizzi amenisisitiza kuelezea mawazo yangu kuhusiana na Shaykh al-Islaam Taqiyud-Diyn. Nimemuona kuwa anatokana na wale watu walioipata elimu kubwa ndani ya sayansi kama alivyoipata. Alikuwa akikamilisha kuihifadhi na kuifanyia kazi Sunan na Aathaar. Iwapo atazungumzia kuhusiana na tafsiyr basi ataibeba bendera yake, na iwapo atazungumzia fatwa ndani ya Fiqh basi yeye alielewa mipaka yake. Iwapo atazungumzia kuhusiana na Hadiyth basi alikuwa ni Swahaba wa hiyo elimu na utambuzi wa wasimulizi wake. Iwapo atatoa mhadhara wa Diyn na Madhehebu basi hakuna mwengine anayeonekana kuwa na ufahamu au uangalifu kuliko alivyokuwa yeye, amewapita waliopita kabla yake katika kila sayansi, na wewe hutaona mtu yeyote mfano wake yeye, na macho yake mwenye hayajapata kuona mtu mfano wake yeye mwenyewe.

 

Alikuwa akizungumzia kuhusiana na tafsiyr na idadi kubwa ya watu wakihudhuria mikusanyiko yake, na idadi inayokubalika hurudi (wakiwa wamelewa) kwa utamu wake, bahri iliyojaa hazina. Iliendelea namna hii hadi ugonjwa wa uadui ukaingia (ndani ya nyoyo) za watu wa mji wake. Watu wa kutafuta makosa wakajikusanya pamoja na kutoa mambo ambayo hatokubaliana nayo kwa imani yake, na wakayahifadhi baadhi ya matamko yake kwa mnasaba wa hili. Wakamdumaza kwa sababu ya hili na kumuwekea mitego ambayo wangeliweza kumtangazia kuwa yeye ni mzushi. Walifikiria kwamba ameacha njia yao, na kujitoa kwenye dhehebu lao. Hivyo wakajadiliana naye, na yeye kwa wao, na baadhi yao wakakata mahusiano naye, na yeye (akakata mahusiano) pamoja nao.

 

Kisha akajadiliana na kundi jengine ambao lilikuwa likisifika kama ni Fuqaraa (kundi la Kisufi) ambao walidhani kwamba walikuwa na kila chembe ya maelezo ya ukweli wa ndani na juu ya ukweli wake. Na akawawekea wazi Kanuni hizi…

 

Basi hili likawafikia kundi la mwanzo na wakatafuta msaada kutoka kwa wale waliokata mahusiana naye na kumuwekea uovu dhidi yake. Hivyo wakalichukua suala hili kwa watawala, kila mmoja wao akiwa na maamuzi kwamba alikuwa si Muumini. Na kisha wakatayarisha kikao na kuwahamasisha wajinga kueneza neno hilo miongoni mwa Wanachuoni wakubwa. Na wakachukua hatua za kupeleka suala hilo kwa Mfalme wa Misri na hatimaye yeye (Ibn Taymiyyah) akakamatwa na kuwekwa jela. Na mikusanyiko ikaanzishwa kujadili umwagaji wa damu yake, wakiwaita kwa mnasaba wa hili watu kutoka kwenye Misikiti midogo na wanafunzi – wale watu ambao hujadiliana kwa lengo la kuwafanya wengine kuwa na furaha, na wapo wale wengine wenye kujadiliana kuonesha uwerevu wao, na wapo wengine waliotangaza takfiyr na kutangaza kutojumuika (naye). Na Rabb Wako Anajua nini kipo ndani ya vifua vyao na yale waliyoyazusha. Na yule ambaye ametangazia kufr alikuwa sio bora kuliko yule anayejadiliana kuwafurahisha wengine.

 

Na mwiba wa hila zao ukampata, na Allaah Akastawisha kila hila, na kumuokoa katika mikono ya wale Aliowachagua…

 

Basi akaendelea kuhama kutoka mtihani mmoja kwenye mtihani mwengine na katika maisha yake yote hakuondokana na tatizo moja isipokuwa kwenda kwenye tatizo jengine. Kisha ikafuatia lile lililofuatia katika suala la kukamatwa kwake na akabakia kifungoni hadi kifo chake, na kwa Allaah ni marejeo ya masuala yote. Katika siku ya maziko yake mitaa ilifurika watu, na Waislamu wakaja kutoka kila njia ya barabara…”[14]

 

-Ibn Hajr al-Asqalaaniy pia amesema:

“Nimesoma katika maandishi ya al-Haafidh Salaahud-Diyn al-Balaa’iy kwa kukubaliana na Shaykh wa Mashaykh wetu al-Haafidh Bahaaud-Diyn ‘Abdullaah bin Muhammad bin Khaliyl: ‘Shaykh wetu na mtaalamu na Imaam katika masuala ambayo ni baina ya Allaah na sisi, Shaykh wa utafiti (tahqiyq), mkanushaji (wa uzushi), pamoja na wale wanaomfuata yeye, katika njia bora. Mwenye sifa bora na thabati bora ambazo mataifa yote yaliyoridhia ni zaidi ya kuweza kuhesabika. Tunamuomba Allaah Atunufaishe sisi kutokana na yeye ndani ya maisha haya na Akhera. Huyo ndiye Shaykh, Imaam, ‘Aalim anayeelewa mambo, mwenye kujitolea sana, bahri (ya elimu), kiungo cha mwangaza, Imaam wa Maimaam, Baraka kwa taifa la Waislamu, alama kwa Wanachuoni, mrithi wa Rusuli, Mujtahid wa mwisho, ana sifa pekee miongoni mwa Wanachuoni wa Diyn – Shaykh al-Islaam, ushahidi wa Wanachuoni, mfano wa viumbe, ushahidi wa wasomi, mfutaji wa Wanachuoni, panga la wazozaji, bahri ya elimu, hazina yenye manufaa, mfasiri wa Qur-aan, maajabu kwa wakati wetu, mwenye sifa pekee katika enzi hizi na nyenginezo. Hakika Taqiyud-Diyn (Ibn Taymiyyah) ni Imaam wa Waislamu, ushahidi wa Allaah dhidi ya uumbwaji, muunganishi wa mema, ni mtu ambaye ni mfano wa waliomtangulia, mufti wa dhehebu, msaidizi wa ukweli, alama ya uongofu, nguzo ya Huffaadh, Bwana wa maana ya maneno, pembe ya Shari’ah, muanzilishi wa sayansi mpya, Abu al-Abbaas Ibn Taymiyyah.”[15]

 

Ibn Hajr pia amesema:

“... Ile misimamo yake ambayo imekataliwa kutokana naye haikusemwa kwa sababu ya matakwa yake na utashi wake tu na wala hakuwa ni mwenye kuendelea nayo na kung’ang’ania nayo baada ya kupatiwa ushahidi unaoonesha dhidi yake. Zifuatazo ni kazi zake zikiwa zimejaa na pingamizi kutoka kwa wale wanaosimamia tajsiyim ingawa yeye ni mtu mwenye kufanya makosa na pia ni mwenye kupata. Hivyo, kwa yale ambayo amepatia – na hayo ndio mengi – yapatiwe manufaa na Rehma za Allaah ziombwe kwa ajili yake kwa sababu ya hilo, na kwa yale ambayo hakuwa sahihi yafuatwe kwa upofu. Kwa hakika, amesamehewa kwa makosa yake kwa sababu yeye ni moja wa Maimaam wa wakati wake na imeshuhudiwa kwamba amekamilisha masharti ya Ijtihaad...

 

Miongoni mwa sifa za kustaajabisha za mtu huyu ni kwamba alikuwa miongoni mwa mtu mwenye nguvu kabisa dhidi ya Watu wa Uzushi, Rawaafidhah, na Huluuliyyah, na Ittihaadiyyah, na kazi zake katika hili ni nyingi na ni maarufu, na fataawaa zake katika hayo hazina hesabu, je namna gani yale macho ya wazushi yalivyokuwa na furaha pale yaliposikia wale walipomtangazia kuwa yeye ni kafiri! Na ni kwa shangwe gani wamekuwa walipoona wale wasiomtambua yeye kuwa ni kafiri wao wenyewe wakabandikwa jina la ukafiri! Ni wajibu kwa yule ambaye amejivalisha joho la elimu na kuwa na ufahamu kwamba, ayakadirie maneno ya mtu yaliyoegemezwa na vitabu vyake maarufu au kutoka kwa ndimi za wale waliomuamini kufikisha maneno yake kwa usahihi – kisha kujitenga nayo yote haya kwa yale yaliyokanwa na kuwatahadharisha wao kwa lengo la kutoa ushauri wa ukweli na kumsifia kutokana na sifa zake bora na kwa yale aliyokuwa sahihi kama ilivyo njia ya Wanachuoni.

 

Iwapo hakuna sifa zozote za Shaykh Taqiyud-Diyn isipokuwa kwa mwanafunzi wake maarufu Shaykh Shams ad-Diyn Ibn al-Qayyim al-Jawziyyah, mwandishi wa kazi nyingi, ambazo kutoka kwa pande zote za wapinzani wake na wafuasi wake wamenufaika nazo, basi inatosha hili kuonesha nafasi yake (Ibn Taymiyyah) kubwa kabisa. Na kwa nini iwe vyenginevyo kwa kuwa Maimaam wa Kishaafi’y na wengineo, bila ya kuwazungumzima Mahanbaliy, kwa wakati wake kuthibitisha kutokana na umashuhuri katika sayansi (za Kiislamu)...”[16]

 

-Ibn Kathiyr amesema:

 

 “Jambo dogo ambalo anaweza kulifanya pale anaposikia kitu ni kukihifadhi na kisha kuwa na mshughuliko wa kukisoma. Alikuwa na ufahamu na alijifunga kuhifadhi sana na hivyo, akawa ni Imaam katika tafsiyr na kilichofungamana nayo. Alikuwa na elimu (kubwa) katika Fiqh; ilisemwa kwamba alikuwa na elimu zaidi ya Fiqh katika madh-hab kuliko wafuasi wake wa yale madh-hab wanayoyafuata katika wakati wake na wakati mwengine. Alikuwa na fahamu tosha ya mawazo tofauti ya Wanachuoni. Alikuwa ni Mwanachuoni wa Uswuul, matawi ya Diyn, sarufi, lugha na sayansi nyengine za maandiko na ufahamu. Hakupatapo kuchukuliwa katika kikao na hakuna Mwanachuoni maarufu kuzungumza naye katika sayansi fulani isipokuwa kwamba kuona kwamba sayansi hii ilikuwa ni elimu maalumu (takhasus) ya Ibn Taymiyyah na humuona yeye kama ni mwenye maarifa ya kutosha katika hilo na kuipambisha... Ama kwa Hadiyth basi alikuwa ni mbebaji wa bendera yake, muhifadhi wa Hadiyth, na mwenye uwezo wa kupambanua jepesi kutokana na zito, akiwa na maelezo kamili ya wapokezi na kuwa ni mtaalamu katika hili...”[17]

Pia amesema,

“Alikuwa, Rehema za Allaah ziwe juu yake, kutoka katika Wanachuoni wakubwa kabisa, pia kutoka kwa wale wenye kufanya makosa na kupatia. Hata hivyo, makosa yake kwa mnasaba wa zile hukumu zilizo sahihi ilikuwa ni kama vile tone katika bahari kubwa na hayo (makosa) yanasamehewa kama ilivyosimuliwa kwa usahihi na [al-Bukhaariy], “pale Kiongozi anapotoa hukumu, na yupo sahihi basi anapatiwa malipo mara mbili, na iwapo atakosea basi analipwa moja.’”

 

Pia ameelezea kwamba pale Wanachuoni wa wakati wake wanapokusanyika kwa kikao pamoja na Ibn Taymiyyah kwa ajili ya kujadili kazi yake Aqiydah al-Hamawiyyah’ kwamba majibu yake kwa madai yao hayawezi kukanushwa.[18]

Vivyo hivyo ametaja kwamba pale Wanachuoni wanapokaa kujadiliana naye kwa mnasaba wa ‘Aqiydah al-Waasitiyyah yake, mjadala humalizikia kwa wao kukubaliana na yote yaliyokuwemo ndani ya kitabu hicho kama ilivyo ndani ya kitabu cha (Mjalada) 14 cha al-Bidaayah’ chini ya mada ya ‘Aqd al-Majaalis ath-Thalaathah.’

 

-Al-Haafidh al-Mizzi amesema:

“Sijaona mfano wake yeye, na jicho lake mwenyewe halijapata kuona mfano wake yeye. Na sijapata kuona mtu mwenye ufahamu zaidi yake yeye katika Kitabu na Sunnah ya Rasuli Wake, au yule mwenye kuzifuata hizo kwa ukaribu zaidi.”[19]

 

-Al-Haafidh Ibn Daqiyq al-‘Iyd amesema:

“Pale nilipokutana na Ibn Taymiyyah, niliona mtu akiwa na sayansi zote mbele ya macho yake, alichukua kutokana na sayansi hizo chochote anachopenda na kuacha chochote akipendacho.” [20] Baada ya hili akasema, “Naapa kwa Allaah sijafikiria kama yupo aliyebakia mfano wako wewe.” [21]

 

- Qaadhiy wa Qaadiys Ibn al-Huriyriy amesema:

“Iwapo Ibn Taymiyyah alikuwa si Shaykh al-Islaam basi yeye ni nani?”[22]

 

-Al-Haafidh al-Bazzaar amesema:

“Sikupatapo kumuona akitaja anasa na vivutio vya dunia hii, hakujichimbia katika mijadala ya kidunia na wala hakupatapo kuulizia aina yoyote ya makaazi yake. Isipokuwa aliipeleka akili na mijadala yake katika kuitafuta Aakhirah na lile ambalo litamuweka karibu na Allaah.”[23]

 

-Al-Shaykh Mullaa ‘Aliy al-Qaariy amesema:

 “Itaonekana wazi kwa yule anayesoma ‘Madaarij as-Saalikiyn’ (cha Ibn al-Qayyim) kwamba hawa wawili (Ibn Taymiyyah na Ibn al-Qayyimj) ni wakubwa katika Ahlus Sunnah wal Jamaa`ah, na ni Awliyaa wa taifa hili.” [24]

 

-Muhammad bin ‘Abdil-Barr as-Subkiy amesema:

“Naapa kwa Allaah, hakuna mtu anayemchukia Ibn Taymiyyah isipokuwa kwa mtu mjinga au mwenye kubeba matamanio ambayo yamemgeuza kutoka katika ukweli baada ya kuutambua (ukweli).”[25]

 

-Abu Hayyan al-Andalusiy amesema:

“Naapa kwa Allaah, macho yangu mawili hayajapata kuona mfano wa Ibn Taymiyyah.”[26]

 

-Al-Haafidh ‘Abdur-Rahmaan Ibn Rajab al-Hanbaliy amesema:

“Yeye ni Imaam, Mwanashari’ah, Mujtahid, Mwanachuoni wa Hadiyth, Haafidh, Mfafanuzi wa Qur-aan, Mpwekeshaji, Taqiyud-Diyn Abu al-‘Abbaas Shaykh al-Islaam, mwenye ufahamu bora katika wenye ufahamu bora, haiwezekani kukithirisha umaarufu wake pale anapotajwa... yeye, Rehma za Allaah ziwe juu yake, alikuwa na sifa pekee katika wakati wake kwa mnasaba wa ufahamu wa Qur-aan na elimu ya ukweli wa imani.”[27]

 

-Imaam wa Hanafi, Badrud-Diyn (Mahmuud bin Ahmad) al-‘Ainiy amesema:

 

“Yeyote anayesema kwamba Ibn Taymiyyah ni kafiri basi ukweli ni kwamba yeye mwenyewe ni kafiri, na yule anayemtuhumu kwa upotofu basi yeye mwenyewe ni mpotofu. Itawezekanaje kuwa hili (ni ukweli) wakati kazi zake zinapatikana kwa mapana na hakuna alama ya kuonesha upotofu wala fitnah zilizokuwemo ndani ya kazi hizo.”[28]

 

Pia amesema:

"Yeye ni Imaam, muongofu, mtaalamu, mcha Mungu, msafi, mwenye kujitolea, mtaalamu katika sayansi ya Hadiyth na tafsiyr, Fiqh na misingi miwili (yaani Kitabu na Sunnah) pamoja na ukali wa akili na umakini. Yeye ni upanga ulio mkali dhidi ya wazushi, mtawala, aliyeanzisha mambo ya Diyn na kamanda mkuu wa mema na mkatazaji wa maovu. Alikuwa na (ustaarabu wa) hisia, ushupavu na kuendeleza lile ambalo linatisha na kukatisha tamaa. Alikuwa ni mwenye kufanya dhikr sana, kufunga, kuswali na kuabudu.” [29]

 

-Shaykh Kamaal ad-Diyn Ibn az-Zamlakaaniy, ambaye alihojiana naye Ibn Taymiyyah, katika kikao zaidi ya kimoja, amesema:

“Popote anapoulizwa kuhusiana na nyanja fulani ya elimu, yule anayeshuhudia na kusikia (jibu hilo) huhitimisha kwamba hakuwa na elimu nyengine yoyote katika nyanja nyengine na kwamba hakuna mwengine mwenye kuwa na elimu kama hiyo. Wanachuoni wa makundi yote, popote wanapokaa pamoja naye, hunufaika naye kwa mnasaba wa fikra za madhehebu yao katika maeneo ambayo hapo kabla hawakuwa ni wenye kuyafahamu. Haifahamiki kwamba alikuwa ni mwenye kujadiliana na yeyote ambapo mjadala hufikia kusimama au kwamba chochote anachozungumzia katika eneo fulani ya elimu – iwapo inahusiana na sayansi ya Shar’iah au nyengineyo – basi kwa hapo hawatong’ara kwa wataalamu wa eneo hilo na wale wanaoungana nayo.”[30]

 

Pia amesema: “Masharti ya Ijtihaad yalijumuika ndani yake katika namna ambayo ilitakiwa, alikuwa na uwezo mkubwa wa kuandika vizuri kabisa na kufanya vyema kabisa katika kutamka, kupanga, kugawanya na kuelezea.”[31]

 

-As-Suyuutwiy ananukuu kutoka kwa az-Zamlakaaniy ambaye amesema:

“Mtaalamu wetu, Shaykh wetu, Imaam, Mwanachuoni, Mpekee (wa aina yake), Haafidh, Mujtahid, Mwenye Ikhlaasw, Mwenye kuabudu (‘Aabid), Mfano, Imaam wa Imaam, mfano wa Taifa, alama ya Wanachuoni, mrithi wa Mitume, Mujtahid wa Mwisho, Mwanachuoni pekee wa Diyn, Barka kwa Uislamu, Hoja ya Wanachuoni, Hoja ya Mutakallimiyn, muharibifu wa wazushi, mwenye kuikamata na kuing’arisha sayansi ya maajabu kabisa, mwenye Kuihuisha Sunnah. Ni yule ambaye Allaah Amemfadhilisha juu yetu, na kujenga ushahidi dhidi ya maadui Zake... naye ni Taqiyud-Diyn Ibn Taymiyyah...”

 

-Kisha as-Suyuutwiy anafuatizishia hili kwa kusema:

“Nimenukuu wasifu huu kutoka kwa maandiko ya ‘Allaamah, mtu aliyekuwa na sifa za kipekee katika enzi zake, Shaykh Kamaal ad-Diyn az-Zamlakaaniy, Rehma za Allaah ziwe juu yake, ambaye alikuwa ni mwenye kusema, ‘yule ambaye amehifadhi zaidi kuliko yeye hakupata kuonekana katika miaka mia tano iliyopita.” [32]

 

-As-Suyuutwiy amesema katika hali ya kuujadili wasifu wake:

“Shaykh al-Islaam, Haafidh, Faqiyh, Mujtahid, Mufassir wa kipekee, adimu kwa wakati wake, Mwanachuoni mwenye Ikhlaasw” [33] 

 

Tuna uwezo wa kutaja Wanachuoni wengi zaidi ambao walimsifu, lakini in shaa Allaah kwa yale tuliyoweza kunukuu hapo juu yanatosha kuipaka rangi picha ya Imaam huyu kwa uadilifu na ukweli. Ama kwa wale Wanachuoni ambao wametumia jina la ‘Shaykh al-Islaam’ kwake yeye, basi wapo wengi na inahitaji vitabu vingine kuwaorodhesha. [34]

 

 

 

 

 

 

 

 

 

[2] Al-Bukhaariy na Muslim

[3] (Imesemwa na kuandikwa na Ahmad Ibn ‘Aliy Ibn Muhammad Ibn Hajar ash-Shafi’iy, Allaah Amsamehe, siku ya Ijumaa ya mwezi 9 wa Rabiy’ al-Awwal, mwaka 835H. Shukrani zote ni za Allaah, na tunamuomba Allaah amtumie Swala na salamu juu ya Rasuli wake Muhammad na familia yake.) Al-Radd al-Waafir cha Imaam Ibn Naaswirid-Diyn ad-Dimashqiy (uk. 145, 146), al-Haafidh al-Sakhaawiy – mwanafunzi wa Ibn Hajar – amenukuu maneno ya Shaykh wake ndani ya kitabu chake cha al-Jawaahir wad-Durar (2/734-736). 

[4] Al-Haafidh Ibn Hajar al-‘Asqalaaniy ni Imaamu maarufu aliyefariki mnamo mwaka 852H; ambaye ni mwandishi wa vitabu vyenye manufaa kama vile Fat-h al-Baariy Sharh Swahiyh al-Bukhaariy, al-Talkhiys al-Habiyr, Tahdhiyb at-Tahdhiyb na vinginevyo.

[5] Ad-Durar al-Kaaminah fi A’yaan al-Mi’ah al-Thaaminah (1/168). 

[6] Ad-Durar al-Kaaminah (186-187).

[7] Masuala mengi ambayo Shaykh al-Islaam amekuwa akipingwa, haswa na Ibn Hajar al-Haythamiy, ambaye tumemtaja hapo juu, zinaweza kuelezewa kwamba ni zile ambazo zimeandikwa na Shaykh Nu’maan Khayr ad-Diyn Ibn al-Aluusiy (Rahimahu Allaahu) ndani ya kitabu chake chenye manufaa cha Jala’ al-‘Aynayn fi Muhaakamah al-Ahmadayn, kwa maana ya Ahmad Ibn Taymiyyah na Ahmad Ibn Hajar al-Haythamiy (Rahimahu Allaahu). 

Hili linaweza pia kupatikana ndani ya kitabu cha Da’awa al-Munaawi’iyn li Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah, ambacho ni utafiti wa kisomi uliofanywa na Dr. ‘Abdullaah Ibn Swaalih al-Ghusuun. Angalia pia: Islaam Q&A ya Shaykh Muhammad bin Swaalih al-Munajjid.

 

[8] Dhayl Tabaqaat al-Hanaabilah cha Ibn Rajab al-Hanbaliy (4/390).

[9] Al-‘Uquud al-Durriyyah, uk. 311.

[10] Twabaqaat al-Huffaadh, uk. 516, 517.

[11] Al-A`laam al-‘Aliyyah, uk. 82

[12] Ad-Durar al-Kaaminah’ cha Ibn Hajr al-Asqalaaniy chini ya wasifu wa Ibn Taymiyyah

[13] Ar-Radd al-Waafir, uk. 59 (katika matoleo mengine ipo ukurasa wa 35).

[14] Ad-Durar al-Kaaminah’ cha Ibn Hajr al-Asqalaaniy chini ya wasifu wa Ibn Taymiyyah

[15] Ad-Durar al-Kaaminah’ cha Ibn Hajr al-Asqalaaniy chini ya wasifu wa Ibn Taymiyyah. Kwa kitabu hichi kuchukuliwa kama kilivyo, ni vigumu kufahamu maoni ya Ibn Hajr kuhusiana na Ibn Taymiyyah. Kwani kikubwa alichokifanya ni kukusanya vitu vyote anavyoweza kupata kuhusiana na Shaykh na kisha kuanza kupambanua kwa Wanachuoni wote walioandika dhidi yake, na kumalizia na Wanachuoni wote waliomkubali. Inaonesha kwamba msimamo wa Ibn Hajr unaendana na wale aliomaliza nao katika wasifu wake, kwa sababu ya wao kuwa ni Mashaykh wake. Hoja hii inakubaliwa na nukuu inayofuatia kutoka kwa Ibn Hajr. Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.

[16] Kutoka ridhaa ya Ibn Hajr katika ‘Radd al-Waafir’ iliyopo mwisho wa kitabu.

[17] Al-Bidaayah wan Nihaayah, Ibn Kathiyr (14/118-119)

[18] Al-Bidaayah wan Nihaayah, Ibn Kathiyr (14/5)

[19]  Hayaat Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah, Shaykh Bahjah al-Baytaar, uk. 21, na ar-Radd al-Waafir, uk. 59.

[20] Min Mashaahiyr al-Mujaddidayn, Shaykh Swaalih al-Fawzaan, uk. 26.

[21] Al-Bidaayah wan Nihaayah, Ibn Kathiyr (14/27), na Dhail `alaa Twabaqaat al-Hanaabilah, Ibn Rajab (2/392).

[22] Hayaat Shaykh al-Islaam, (uk. 26)

[23] Al-A`laam al-Aliyyah fiy Manaaqib Ibn Taymiyyah, al-Bazzaar, (uk. 52).

[24] Mirqaat al-Mafaatiyh, (8/251-252) ufafanuzi wake kwa Mishkaat al-Maswaabiyh, kama ilivyonukuliwa ndani ya Shubuhaat Ahl al-Fitnah, (uk. 442) cha ‘Abdur-Rahmaan Dimishqiyyah.

[25] Ar-Radd al-Waafir (uk. 95) cha Ibn Naaswirid-Diyn

[26] Ar-Radd al-Waafir, uk. 63.

[27]  Adh-Dhail `alaa Twabaqaat al-Hanaabilah, Ibn Rajab (2/387-392).

[28] Ar-Radd al-Waafir, (uk. 245).

[29] Ar-Radd al-Waafir, uk. 159.

[30] Ar-Radd al-Waafir, uk. 58.

[31] Ar-Radd al-Waafir, uk. 58.

[32] Al-Ashbaah wa an-Nadwhaair an-Nahwiyyah, (3/681), angalia pia ‘Dhail alaa Twabaqaat al-Hanaabilah’ (2/392-393)

[33] Tabaqaat al-Huffaadh, (uk. 516 nam. 1144), na al-Asbaah wa al-Nadhaa’ir, as-Suyuutiy (3/683).

[34] Kama ilivyofanywa na baadhi ya Wanachuoni, miongoni mwao ni Ibn Naasir ad-Diyn ndani ya kitabu kilichotajwa cha ar-Radd al-Waafir.

Share

12-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Hitimisho

 

12- Shaykh Al-Islaam Ibn Tamiyyah: Hitimisho

 

Alhidaaya.com

 

 

Hitimisho

 

Miongoni mwa wachache, ambao dunia imewapata, kama ni mtu mwenye ubongo wenye kufahamu sana, hadhi na sifa, Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah alikuwa ni mmoja wao. Sifa zake bora na hadhi yake pekee kama ni Mwanachuoni wa Kiislamu ni zaidi ya utangulizi wowote. Wanachuoni wengi wakubwa kwa wakati wetu wanaonekana kuwa ni wenye kuikusanya elimu yake. Amechangia mengi taqriban katika misingi na matawi yote na vitovu vya elimu ya Kiislamu.

 

Mawazo yake, fikra na maamuzi yameathiri kwa mapana nyanja tofauti za maisha ya Kiislamu.

 

Shaykh al-Islaam alikuwa ni mwenye kuzikamata vyema dhana na imani za madhehebu tofauti ya Kiislamu na halikadhalika Ukiristo. Ndani ya kazi zake, amechukua ilani makini katika imani zote hizi na kunyofoa kutokana nazo Imani sahihi na bora na kuufundisha Uislamu.

 

Ibn Taymiyyah amejenga mazingira ya kimapinduzi ya kifikra kupitia mapote yote mawili; fikra zake na jitihada zake za uhuishaji ambayo athari yake zinahisiwa si tu kwa wakati wake lakini tokea enzi hizo hadi leo. Katika wakati wake, watu walikuwa wamegawika aidha katika wale ambao walikuwa ni wapinzani wenye nguvu au wafuasi wenye nguvu ambao kwa ukamilifu wamemkubali, au wasiojikubalisha, ambao walikubali baadhi ya mawazo na kukataa baadhi. Ibn Taymiyyah ameacha nyuma idadi kubwa kabisa ya vitabu na ustaarabu. Wapinzani wake ghafla wakazama kwenye kutojulikana, hali ya kuwa hadhi na kukubalika kwa kazi zake kumeongezeka.

 

Katika maisha yake, umaarufu wa Ibn Taymiyyah na taathira zake, ulienea zaidi ya mipaka ya Misri na Syria. Alipofungwa kwa mara ya mwisho ndani ya jela ya Damascus, barua nyingi zilikuja kutoka kwa wakaazi wa Baghdad wakipinga kukamatwa kwake na kutaka aachiwe huru. Alipokufa, Swalah ya maziko ilifanyika katika kila ardhi waliosikia kifo chake.

 

Ilikuwa ni muhimu kuandika kuhusiana na mtu huyu mkubwa; Mwanachuoni mkubwa aliyeishi baada ya vizazi vitatu bora, kizazi cha warithi wa waongofu (Salaf as-Swaalih).

 

 

 

Share

13-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Marejeo

 

13- Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Marejeo

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Marejeo

 

 

Vyanzo Vikuu

 

 

Qur-aan

 

Hadiyth

 

Muhammad Taqiyud-Diyn al-Hilali na Dr. Muhsin Khan, Qur-aan Tukufu – Tafsiri Kwa Kiingerea ‘The Noble Qur-aan’, English Translation of the Meanings and Commentary, (King Fahd Complex For The Printing Of The Holy Qur-aan, Madinah, K.S.A.)

 

Al-Bazzaar, al-Haafidh Abu Hafs ‘Umar Ibn ‘Aliy. Al-A'laam al-'Aliyyah Fiy Manaaqib Shaykh al-lslaam Ibn Taymiyyah, tahqiyq ya Zuhayr ash-Shaawiysh, toleo la tatu, 1400H, al-Maktab al-Islaamiy, Beirut.

 

Al-Bazzaar, al-Haafidh Abu Hafs ‘Umar Ibn ‘Aliy: Sifa Bora za Ibn Taymiyyah ‘The Lofty Virtues of Ibn Taymiyyah’, kilichofasiriwa na Abu Sabaaya.

 

Al-Miqriyziy, As-Suluuk li Ma'rifah Duwal al-Muluuk, tahqiyq ya Musfafaa Ziyaadah, chapa ya pili ya 1957, Chapa ya Lajnah at-Ta-liif wa at-Tarjamah, Cairo.

 

Ibn ‘Abdil-Haadiy, Al-‘Uquud ad-Duriyyah, Chapa ya Hijazi, Cairo

 

Ibraahiym Muhammad al-‘Aliy, Shaykh al-Islaam Ahmad Ibn Taymiyyah Rajul al-Islaah wa ad-Da’wah, 2000, Daar al-Qalam, Damascus

 

Ibn Kathiyr, al-Haafidh Abi Fidaa Ismaa’iyl, al-Bidaayah wan-Nihaayah, toleo la mwanzo 1421H, Daar al-Manaaar, Cairo.

 

Ibn Naasir ad-Diyn ad-Dimashqiy, Ar-Radd al-Waafir 'alaa man za'ama bi anna man sammaa Ibn Taymiyyah Shaykhul- Islaam Kaafir, tahqiyq ya Zuhayr ash-Shaawiysh, toleo la mwanzo, 1400H, al-Maktab al-Islaamiy, Beirut.

 

Ibn al-Qayyim, Al-Waabil as-Swayyib, Daar al-Bayaan.

 

Ibn Taymiyyah, Al-Jawaab as-Swahiyh liman Baddala Diyn al-Masiyh, kilichochapwa chini ya usimamizi wa 'Aliy as-Subh al-Madaniy, Chapa ya al-Madaniy, Cairo.

 

Barua ya Ibn Taymiyyah kutoka Jela ‘Ibn Taymeeyah’ Letter from the Prison’, iliyochaguliwa na kutolewa utangulizi na Muhammad al-’Abdah na kufasiriwa na Abu Ammar, toleo la mwanzo 1998, kimechapishwa na kusambazwa na Message of Islam, UK.

 

Ibn Taymiyyah, Majmu’ al-Fataawaa, toleo la mwanzo 1421H, Daar al-Kutub al-‘Ilmiyyah, Beirut.

 

Muhammad bin Ahmad bin 'Iyaas al-Hanafiy, Badaa'i' az-Zuhuur fiy Waqaa'i' ad-Duhuur, tahqiyq Muhammad Mustafaa, chapa ya pili 1402H, al-Hay'ah al Misriyyah al-'Aamah lil-Kitaab, Cairo.

 

 

Vyanzo Vidogo

 

 

Abu Ameenah Bilal Philips, Mabadiliko na Maendeleo ya Fiqhi ‘Evolution of Fiqh’, International Islamic Publishing House, 2006

 

Abu Rumaysah, Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (RahimahuLlaah), URL

http://www.allaahuakbar.net/scholars/Ibn_taymiyyah/Shaykh_al-islaam.htm

 

Abu Safwaan, Shaykh ul-Islâm ibn Taymiyyah, URL

http://www.Sunnahonline.com/ilm/seerah/0047.htm  

 

Abu Zahra, Muhammad: Ibn Taymiyyah, Hayaatuhu wa ‘Aswruhu wa Araauhu wa Fiquhuhu, Cairo (1952).

 

 

 

 

 

Share