Tarjama Ya Maana Ya AL-QUR-AAN AL-'ADHWIYM (Alhidaaya)

Share

000-Tarjama Ya Maana Ya AL-QUR-AAN AL-'ADHWIYM (Alhidaaya): Utangulizi

 

بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

 

 

UTANGULIZI

 

Himdi Anastahiki Allaah (سبحانه وتعالى) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba wake(رضي الله عنهم)  na wote waliowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Mwisho.

 

Qur-aan ni Maneno matukufu ya Allaah Aliyoteremshiwa Nabiy wa mwisho Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) yenye kusadikisha yale yaliyokuja kabla yake katika Vitabu vilivyotangulia na ni Maneno yasiyoweza kufikiwa na upotofu mbele yake wala nyuma yake kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):

لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴿٤٢﴾

Hakitofikiwa kitabu hicho na ubatilifu mbele yake, wala nyuma yake; ni uteremsho kutoka kwa Allaah Mwenye hikmah wa yote, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.[1]

 

 

Pia Qur-aan ni Kitabu cha mwisho chenye ujumbe kwa viumbe wote kutoka kwa Rabb wa walimwengu, kwa lengo la kuwaongoza viumbe kwenye njia iliyonyooka; na ni mwongozo, rahmah na shifaa kwa Waumini.

 

Pia Qur-aan ni muujiza wa pekee, na wakati huo huo ni changamoto kwa viumbe wote. Hata kama viumbe vyote hivyo vitashirikiana ili vilete mfano wa Qur-aan basi havitoweza kuleta mfano wake; katika ufasaha wake, hukumu zake, elimu zake, mwongozo wake na yote iliyoyaelezea.[2]

 

Qur-aan imekusanya yale yote yenye kuhitajiwa na viumbe; yawe ya dunia au Aakhirah yao, zikiwemo khabari za kabla yao na khabari za baada yao, na ni muamuzi na hakimu kwa Waumini wake; na ni Kitabu Alichohitimishia Allaah shariy’ah Zake.

 

Ni katika desturi Zake Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa kila Rasuli akitumwa huwa anapelekwa kwa lugha ya watu wake ili aweze kuwafikishia ujumbe, Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ

Na Hatukutuma Rasuli yeyote isipokuwa kwa lugha ya kaumu yake ili awabainishie (ujumbe).[3]

 

Ni jambo lenye kujulikana kuwa lugha ya Ma-Quraysh na ndio lugha ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ilikuwa ya Kiarabu bayana; hivyo ujumbe uliokuja ndani ya Qur-aan ulikuja katika lugha ya Kiarabu, ambayo ndiyo lugha fasaha kuliko lugha zote.[4]

 

Usomaji wa Qur-aan katika lugha yake, kwa walengwa wake wengi wasiokuwa Waarabu ambao hawakuafikishwa kuisoma lugha ya Kiarabu na kuifahamu vizuri, haswa Qur-aan na elimu zake, haukuweza kuwafikisha kufahamu misingi ya Dini yao, hivyo basi, ndio pakawa na haja na umuhimu mkubwa wa kuweko Tarjama itakayoweza kumsaidia Muislamu kuweza kufikia kufahamu anachosemeshwa na Rabb wake; iwe maamrisho au makatazo apate kutekeleza.

 

Elimu ya Tarjama ilibuniwa na kupelekea kuweko Tarjama nyingi sana katika kila zama na kila pahala na kwa lugha maarufu za walimwengu, jambo lililopelekea kumfikisha mlengwa kuweza kufahamu mengi katika aliyotakiwa ayafahamu kulikomfikisha kutekeleza na upande mwengine kuitakidi kama alivyofikishiwa na hizo Tarjama.

 

Tarjama nyingi huenda zikawa zimefanikiwa kumfikisha mlengwa kufahamu maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kiasi fulani na kufahamu baadhi ya makusudio ya Ayaat katika upande wa shariy’ah. Ama kwenye upande wa itikadi, Tarjama nyingi miongoni mwa hizo, kwa masikitiko makubwa, hazikufanikiwa kumfikisha Muislamu pale alipotakiwa afike kiitikadi kwa sababu moja au nyingine; kwa kuwa kwenye Tarjama hizo kuna mchanganyiko wa itikadi zisizo sahihi na fikra za kifalsafa mbalimbali au fikra za wale wenye upotofu ndani ya nyoyo zao wenye kufuata hawaa za nafsi zao.

 

Baada ya kuzipitia Tarjama zote za Kiswahili zenye kujulikana kuwa ni za watu wenye kunasibishwa na Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah tumeweza kugundua kuwa kuna upungufu huo wa kumfikisha Muislamu mwenye kuzungumza Kiswahili pale alipotakiwa kufika kiitikadi; itikadi iliyobalighishwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Hivyo, hakujapatikana Tarjama inayorandana na itikadi ya Salafus-Swaalih (Wema waliotangulia) miongoni mwa Maswahaba, Taabi’iyn na Atbaa'Taabi’iyn na waliowafuata kwa wema.[5]

 

Kwa minajili hiyo, tukaona kuna umuhimu wa kuweko kwa Tarjama itayokwenda sambamba na Manhaj ya Salaf haswa katika kuibalighisha na kuidhihirisha ile itikadi iliyobalighishwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambayo iko wazi kwenye Qur-aan kwa atakaye kushikamana nayo.[6]

 

Ni vyema ifahamike kuwa, Tarjama hii au nyingine yoyote ile, lengo lake kuu ni kuwasaidia walengwa kuweza kufikia kuifahamu Qur-aan, kutakowafikisha kuwaidhika na kuitendea kazi, haswa katika Aayah zenye kuhusiana na ‘Aqiydah yao ili wapate kuitakidi vile wanavyotarajiwa waitakidi kama walivyokuwa wakiitakidi Salaf (Maswahaba na wale waliowafuata kiitikadi na mwenendo).

 

Tarjama ni jaribio la kuuweka wazi ujumbe na kufikisha makusudio yake kwa walengwa kwa kiasi cha uwezo wa mwana Aadam, na Tarjama ni fani miongoni mwa fani za sayansi ya Qur-aan; sayansi ambayo inazungumzia kila lenye kufungamana na Qur-aan kuanzia kuteremka kwake, Suwrah zake, Aayah zake (za mwanzo na za mwisho kuteremka), sababu za kuteremka kwa Aayah au Suwrah, ukusanyaji wake, mpangilio wa Aayah na Suwrah zake, visa vyake, mifano yake, kujibu tuhuma dhidi yake na kadhalika.

 

Mkusanyiko wa hayo yote na mengineyo ndani ya sayansi hiyo unadhihirisha kuwa kunahitajika uangalifu mkubwa katika kukata shauri na kutoa hukumu kuhusu maana ya Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى). Ndio ikawa njia pekee sahihi na ya salama ya kufanikisha hilo, ni kwa kushikamana na kutegemea yale yaliyopokelewa na kuthibiti kutoka kwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba (رضي الله عنهم) na wala si kutokana na rai.

 

La msingi na lililo muhimu katika kazi ya Tarjama ambalo ni sharti katika masharti ya anayefanya hiyo Tarjama awe mtu mwenye kushikamana na msingi madhubuti wa kufuata manhaj ya Salaf na wala si msingi wa kuzusha au ubunifu na wala asiwe mtu wa hawaa. Atakapokuwa ameshikamana na manhaj sahihi ya Salaf, basi hivyo ndivyo kutampeleka na kumlazimisha kama ni sehemu ya itikadi yake kushikamana na zile Tarjama zenye kwenda sambamba na mafundisho ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), zenye kunukuu kauli za Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), au kauli za Maswahaba (رضي الله عنهم) au kauli za Taabi’iyn na Atbaa’ Taabi’iyn.

 

Kutokana na hali hii basi, Mufassiriyna wameweka Manhaj maalumu ya Tafsiyr ya kufuatwa na kushikiliwa na ambayo kwayo kwa kuipitia vizuri, ndipo tutaweza kufikia kupata Tarjama iliyo sahihi.

 

1.      Tafsiyr ya Qur-aan kwa Qur-aan

 

Kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan ndio njia ya kwanza inayopasa kufuatwa; kwani Qur-aan inajifasiri yenyewe kwa yenyewe. Utakuta pahala inaeleza jambo kwa kifupi na pahala pengine inalieleza jambo hilo hilo kwa ufafanuzi na kwa uchambuzi. Jambo inalolieleza kwa ujumla katika sehemu moja hulieleza kwa kuliwekea ima mipaka au kulihusisha kwa watu makhsusi katika sehemu nyingine. Hivyo, njia iliyo sahihi kabisa katika kufasiri Qur-aan, ni kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan.[7]

Ibn Al-Qayyim (رحمه الله) amesema:

“Kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan ni njia bora kabisa inayofikisha ujumbe na kuufafanua. Na si ajabu kwani Allaah (سبحانه وتعالى) ni Mjuzi wa malengo na makusudio Yake. Anafafanua Aayah Zake kwa Aayah nyinginezo. Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿١٠٥﴾

Na hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat (ishara, dalili) na wao (makafiri) waseme: “Umedurusu” (kutoka Ahlil-Kitaab) na ili Tuibainishe kwa watu wenye kujua.[8]

 

Ni jambo lisilopingika kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifahamu kikamilifu kila kilichoelezwa ndani ya Qur-aan; na ndio akawa wa kwanza kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan kama ilivyopokewa kuwa alifasiri baadhi ya Aayah kwa Aayah nyinginezo.[9]

 

Maswahaba (رضي الله عنهم) walishuhudia na kumsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akifasiri Qur-aan kwa Qur-aan; hivyo nao kama ilivyo desturi yao walimuiga katika hilo pia kama walivyokuwa wakimuiga katika mengineyo; na kwa kufahamu kuwa ni jukumu lao kufikisha kila walichochukua kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuwafikishia wataokuja baada yao. Maswahaba (رضي الله عنهم) waliwafunza wanafunzi wao Taabi’iyn kila walichopokea kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) tena kwa muradi wake Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Taabi’iyn nao waliwafunza wanafunzi wao Atbaa’ Taabi’iyn kila walichopokea na kuchukua kutoka kwa waalimu wao ambao ni Maswahaba (رضي الله عنهم), nao kwa upande wao walinukuu na kufikisha kwa waliokuja baada yao tena kwa muradi ule ule walioupokea na kuuchukua kutoka kwa Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na katika waliyoyapokea ni aina hii ya kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan.

 

Hivyo, haijuzu wala si sahihi kuiacha aina hii ya Tafsiyr na kuiendea nyingine ikiwa Aayah husika ina Aayah nyingine iliyoifasiri kama ilivyo katika mifano ifuatayo:

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٥٩﴾

Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua, na wala punje katika viza vya ardhi, na wala kilichorutubika na wala kikavu isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha wazi.[10]

 

Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwabainishia na kuwawekea wazi kuwa funguo za ghayb ni tano; kwa kuwasomea kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ifuatayo:

 إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾

Hakika Allaah Ana elimu ya Saa, na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika tumbo la uzazi na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.[11]

 

Mfano mwengine ni pale Allaah (سبحانه وتعالى) Anaposema:

الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢﴾

Wale walioamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma; hao ndio watakaopata amani nao ndio walioongoka.[12]

 

Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwabainishia na kuwawekea wazi kuwa dhulma ni shirki; kwa kuwasomea Aayah ifuatayo:

وَإِذْ قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ وَهُوَ يَعِظُهُ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ﴿١٣﴾

Na Luqmaan alipomwambia mwanawe huku akimuwaidhi: “Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah, hakika shirki ni dhulma kubwa mno!”[13]

 

 

2.      Kufasiri Qur-aan kwa Sunnah za Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)[14]

 

Sunnah ni tafsiyr, kishereheshaji na kibainifu cha Qur-aan kwa kudhihirisha yasiyokuwa dhahiri. Sunnah inaisherehesha Qur-aan kwa kuyachambua, kuyapambanua na kwa kuyaainisha yale ambayo Qur-aan imeyaelezea kwa ujumla. Sunnah inaweka mipaka kwa yale yasiyokuwa yamewekewa mipaka na Qur-aan. Sunnah inayachambua yaliyotolewa hukumu kwa pamoja, ikifafanua yaliyoachwa wazi hukumu zake; yote kwa kuwa katika Qur-aan kuna yasiyoweza kufahamika isipokuwa kwa kupata ufafanuzi na kuwekwa wazi na Sunnah za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); kama vile uchambuzi wake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika namna za amri na makatazo, idadi za Rakaa za Swalaah, viwango vya yale Aliyofaradhisha Allaah (سبحانه وتعالى) katika hukumu.[15]

 

 

Ufafanuzi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kitu kisichoweza kuepukika; na ndio akaweka wazi kwa kusema kuwa hakupewa Qur-aan pekee, bali alipewa pamoja na Qur-aan kinachofanana nayo.[16]

 

Umahiri katika lugha ya Kiarabu pekee haukuwa wenye kutosheleza wala hautatosheleza katika kufahamu kusudio la Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) bila ya kutafuta msaada kutoka kwenye Sunnah. Kama ilivyokuwa hali kwa Maswahaba (رضي الله عنهم) japokuwa walikuwa wenye ufasaha na umiliki kamili wa lugha ya Kiarabu, lakini walikuwa wakitatanishwa au wakati mwengine wakifahamu baadhi za Aayah kinyume na inavyotakiwa ifahamike, jambo lililowapelekea kurejea kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kutafuta ufafanuzi.

 

Kuna mifano mingi tu ya Aayah za Qur-aan ambapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amezifasiri na kuzifafanua. Tafsiyr au ufafanuzi wake (صلى الله عليه وآله وسلم) uko wa namna mbili; hufasiri Aayah au neno ambalo Maswahaba (رضي الله عنهم) hawakuweza kuifahamu tafsiyr yake au walipofahamu kinyume na inavyotakiwa ifahamike.

 

Mfano neno قُوَّةٍ (nguvu):

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifasiri neno قُوَّةٍ katika Aayah ya Al-Anfaal kuwa ni Ar-Ramyu:

 وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ

“Na waandalieni nguvu zozote mziwezazo.”[17]

Tafsiyr ya neno قُوَّةٍ kuwa ni Ar-Ramyu limepatikana katika usimulizi ufuatao:

عَنْ عُقْبَةَ بْن عَامِر يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ عَلَى الْمِنْبَرِ يَقُولُ: ((وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ... أَلَا إِنَّ الْقُوَّةَ الرَّمْيُ، أَلَا إِنَّ الْقُوَّةَ الرَّمْيُ، أَلَا إِنَّ الْقُوَّةَ الرَّمْيُ))

‘Uqbah bin ‘Aamir (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hali akiwa yu juu ya minbar akisema: “Na waandalieni nguvu kama muwezavyo…” Tanabahi! Hakika Al-Quwwah ni Ar-Ramyu (kutupa mshale, kulenga kwa kutumia silaha), hakika Al-Quwwah ni Ar-Ramyu, hakika Al-Quwwah ni Ar-Ramyu.”[18]

 

Mfano mwengine ni neno الْكَوْثَرَ

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alilifasiri nenoالْكَوْثَرَ katika Suwrah Al-Kawthar:

إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ ﴿١﴾

Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar (Mto katika Jannah)[19]

 

kuwa ni Mto katika Jannnah, maana ambayo haikufahamika isipokuwa kwa njia ya kufafanuliwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:

عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) : ((إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ)) أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: ((هُوَ نَهْرٌ فِي الْجَنَّةِ))

Anas (رضي الله عنه) amehadithia (kuhusu kauli yake Allaah): Hakika Sisi Tumekupa Al-Kawthar”; kuwaNabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Huo ni Mto katika Jannah.”[20]

 

Mfano mwengine ni neno زِيَادَةٌ

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifasiri kwa kubainisha kuwa neno زِيَادَةٌ katikaAayah ya Suwrah Yuwnus,

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ

Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (jazaa) nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah Jannah).[21]

 

 

Kuwa ni kumuona Allaah Ta’aalaa; maana ambayo haikufahamika isipokuwa kwa njia ya ufafanuzi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ صُهَيْبٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِذَا دَخَلَ أَهْلُ الْجَنَّةِ الْجَنَّةَ نُودُوا: يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ، إِنَّ لَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ مَوْعِدًا لَمْ تَرَوْهُ، فَقَالُوا: وَمَا هُوَ؟ أَلَمْ تُبَيِّضْ وُجُوهَنَا وَتُزَحْزِحْنَا عَنِ النَّارِ، وَتُدْخِلْنَا الْجَنَّةَ؟)) قَالَ: ((فَيُكْشَفُ الْحِجَابُ، فَيَنْظُرُونَ إِلَيْهِ، فَوَاللَّهِ مَا أَعْطَاهُمْ اللَّهُ شَيْئًا أَحَبَّ إِلَيْهِمْ مِنْهُ)) ثُمَّ تَلاَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَى وَزِيَادَةٌ))

Swuhayb (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watakapoingia Ahlul-Jannah katika Jannah; wataitwa: Ee Ahlal-Jannah! Hakika nyinyi mna ahadi kwa Rabb wenu bado hamjaiona; watauliza: ‘Ni (ahadi) ipi hiyo? Kwani Hukuzing’arisha nyuso zetu, na Hukutuokoa na moto, na Hukutuingiza Jannah?’” Akasema: “Litaondoshwa pazia, na watamtazama Allaah; Naapa kwa Jina la Allaah Hakuwahi Allaah kuwapa kitu wanachokipenda zaidi kuliko huko (kumuona Allaah).” Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasoma Aayah hii: Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (jazaa) nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah Jannah).[22]

 

Hii inathibitisha kuwa ufafanuzi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni wenye umuhimu mkubwa katika kufasiri Qur-aan kwani ni ufafanuzi wa aina yake pekee na wenye thamani isiyoweza kununulika wala kukadirika ndio ikawa Qur-aan inaihitaji Sunnah (Hadiyth); na ndio ikawa hakuna kitabu katika vitabu vya Hadiyth isipokuwa kutakuwepo mlango wa Tafsiyr Maathuwr.[23]

 

  

3.      Kufasiri Qur-aan kwa kauli za Maswahaba (رضي الله عنهم) 

 

Kauli (tafsiyr) za Maswahaba  (رضي الله عنهم)ni chanzo cha tatu cha kutafuta ufafanuzi pale inapokuwa haujapatikana ufafanuzi kutoka vyanzo viwili vilivyotangulia, kama alivyosema Al-Haafidhw Ibn Kathiyr katika utangulizi wa Tafsiyr yake kuwa: “Tutakapokuwa hatukufanikiwa kupata Tafsiyr katika Qur-aan au Sunnah, tutarejea katika kauli za Maswahaba (رضي الله عنهم) kwani wao waliifahamu Qur-aan vilivyo kwa ufasaha na sarufi zake, na kwa kuwa walishuhudia matukio yaliyosababisha kuteremshwa kwa Aayah au Suwrah husika, hakuna aliyeyashuhudia isipokuwa wao, na pia kutokana na kuwa na na elimu sahihi na ‘amali njema haswa haswa Wanachuoni miongoni mwao.”[24]

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alibainisha na kufafanua kwa kufasiri maana za Aayah za Qur-aan kwa Maswahaba zake (رضي الله عنهم) kama inavyoashiria kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ

“…ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao...”[25]

 

Maswahaba (رضي الله عنهم) walijifunza Qur-aan na elimu yake kwa kina kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).[26]

 

Hata hivyo, ufahamu wa Maswahaba (رضي الله عنهم) wa Qur-aan na ufahamu wao haukuwa wa daraja moja; kwani miongoni mwao (رضي الله عنهم) wako waliojulikana kuwa ni wafasiri wa Qur-aan; kama vile Makhalifa wanne (رضي الله عنهم), Ibn Mas’uwd[27] ambaye alikuwa akijulikana miongoni mwa Maswahaba kuwa ni mjuzi wao wa Qur-aan (kuisoma na kuifasiri). Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما),[28] pia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) na wengineo ambao walikuwa na ufahamu uliokamilika kwa vile ulijengeka juu ya elimu iliyo sahihi iliyopambika kwa ‘amali swaalih. Hivyo, tafsiyr zao zina thamani, uzito na umuhimu mkubwa mpaka ikawa tafsiyr ya Maswahaba inachukua hukumu ya Al-Marfuw’[29] haswa inapojulikana kuwa Swahaba huyo hakuwahi kupokea Israaiyliyyaat katika hilo.

 

Kilichojitokeza ni kuwa hakuna tafsiyr iliyoandikwa katika wakati wao, kwani ilikuwa ni sehemu katika Hadiyth.

Mfano wa Tafsiyr ya neno  لَامَسْتُمُ (mmewagusa) kuwa ni kujimai katika kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ

“au mmewagusa wanawake.”[30]

Ibn ‘Abbaas alilitafsiri kwa kusema kuwa: “Ni kujimai.”[31]

 

Mfano mwengine ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا ۚ

Na miongoni mwa watu yuko ambaye hununua maneno ya upuuzi ili apoteze (watu) njia ya Allaah bila elimu, na huichukulia mzaha. Hao watapata adhabu ya kudhalilisha.[32]

 

Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) amesema kuhusu Aayah hii: “Naapa kwa Jina la Allaah hii inamaanisha ni muziki.”[33]

 

Mfano mwengine ni kuhusu kufanya sa’y baina ya majabali mawili ya Swafaa na Marwah kulikotajwa kwenye kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ

Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika alama za Allaah. Basi yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah basi hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo[34] 

Baadhi ya Maswahaba (رضي الله عنهم) walifahamu kinyume na vile inavyotakiwa ifahamike Aayah hiyo. Mmojawao ni baba wa Hishaam bin ‘Urwah Akamuuliza Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) ambaye alimfahamisha kwa kutumia ‘sabab an-nuzuwl’ (sababu iliyopelekea kuteremka Aayah) ili aweze kufahamu usahihi wa maana ya Aayah kama ilivyothibiti katika kauli ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) katika usimulizi ufuatao:

عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّهُ قَالَ: قُلْتُ لِعَائِشَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَأَنَا يَوْمَئِذٍ حَدِيثُ السِّنِّ: "أَرَأَيْتِ قَوْلَ اللَّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: ((إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ يَطَّوَّفَ بِهِمَا))  فَمَا أُرَى عَلَى أَحَدٍ شَيْئًا أَنْ لَا يَطَّوَّفَ بِهِمَا، فَقَالَتْ عَائِشَةُ: "كَلَّا، لَوْ كَانَتْ كَمَا تَقُولُ، كَانَتْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ لَا يَطَّوَّفَ بِهِمَا، إِنَّمَا أُنْزِلَتْ هَذِهِ الْآيَةُ فِي الْأَنْصَارِ كَانُوا يُهِلُّونَ لِمَنَاةَ، وَكَانَتْ مَنَاةُ حَذْوَ قُدَيْدٍ، وَكَانُوا يَتَحَرَّجُونَ أَنْ يَطُوفُوا بَيْنَ الصَّفَا وَالْمَرْوَةِ، فَلَمَّا جَاءَ الْإِسْلَامُ سَأَلُوا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ ذَلِكَ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ يَطَّوَّفَ بِهِمَا))

Kutoka kwa Hishaam bin ‘Urwah kutoka kwa baba yake kwamba alisema: Nilimwambia ‘Aaishah (رضي الله عنها) mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na mimi wakati huo ni kijana mdogo: “Unaionaje kauli ya Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa: Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika alama za Allaah. Basi yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah basi hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo”[35] Sioni kama kutakuwa na kitu (dhambi) juu ya yeyote ikiwa hatofanya sa’y baina ya majabali mawili haya.” Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) alisema: “Si hivyo; lau ingelikuwa kama unavyosema basi ingekuwa (hivi): “Hakutokuwa na dhambi juu yake kama hatotufu baina ya (vilima) viwili hivyo.” Kwa hakika Aayah hii imeteremshwa kuhusiana na Answaar walikuwa wakihiji kwa Manaat (wakiliabudu sanamu hilo na wakilifanyia Hijjah na wakilitufu), lakini walikuwa hawatufu (sa’y baina ya Swafaa na Marwah) na lilikuwa hilo sanamu la Manaat likielekea (kijiji cha) Qadiyd, hivyo walikuwa wakiona tabu kulitufu. Ulipokuja Uislamu walimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hivyo (kwenda sa’y baina ya Swafaa na Marwah), ndio Allaah Akateremsha: Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika alama za Allaah. Basi yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah basi hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo.”[36]

 

 

4.      Kufasiri Qur-aan kwa kauli za Taabi’iyn

 

Kutakaposhindwa kupatikana Tafsiyr ya Aayah husika kwenye Qur-aan, au kwenye Sunnah, au kwenye kauli za Maswahaba (رضي الله عنهم); ‘Ulamaa hurejea kwenye kauli za Taabi’iyn;[37] kwani kama walivyotajika baadhi ya Maswahaba (رضي الله عنهم) kwa Tafsiyr, wametajika pia baadhi ya Taabi’iyn kwa Tafsiyr.[38]

 

Taabi’iyn walitegemea katika Tafsiyr zao, ufahamu wao wa Qur-aan kutokana na yaliyokuja ndani ya Qur-aan yenyewe, na yale waliyoyapokea kutokana na Maswahaba (رضي الله عنهم), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na yale Aliyowafungulia Allaah kupitia njia ya ijtihaad na utafiti wao katika Qur-aan na wala hawakuwa tayari kutumia rai zao.[39]

 

Kinachofahamika ni kuwa Tafsiyr zilizopokelewa kutokana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na pia kutokana na Maswahaba (رضي الله عنهم) hazikuwa za Qur-aan yote, bali zilikuwa ni zenye kuhusiana na baadhi ya Aayah za Qur-aan au baadhi ya maneno ya Aayah ambayo yaliyoonekana kuwa ni miongoni mwa yale yenye kuhitaji ufafanuzi kwa wale waliokuwa katika zama hizo.  Kutofahamika huku, huwa kunazidi kila pale wanapobaidika watu na zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba (رضي الله عنهم); hivyo wale wenye kujishughulisha na fani ya Tafsiyr miongoni mwa Taabi’iyn, wakaongeza katika Tafsiyr kadiri ya kule kuongezeka kutofahamika; kisha baada yao wakaja wale waliokamilisha Tafsiyr ya Qur-aan huku wakitegemea juu ya yale waliyoyafahamu katika lugha na lahaja za Waarabu, na juu ya yale yaliyothibiti kuwa ni sahihi kwao katika matukio yaliyotokea wakati wa kushuka kwa Qur-aan na mengineo.

 

Taabi’iyn wametunukiwa daraja ya kuwa miongoni mwa watu bora kabisa[40]kwa kuwa walichukua na kuchota elimu zao kutoka vyanzo sahihi na vilivyoasisiwa kwa misingi sahihi.

 

Mfano wa Tafsiyr ya neno قَانِتُونَ katika Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾

...vyote vinamtii.[41]

Kuhusiana na neno قَانِتُونَ, Mujaahid alilifasiri kwa kusema kuwa: “Ni kutii: na kuwa utiifu wa kafiri hupatikana pale kivuli chake kinaposujudu, wakati ambapo yeye mwenyewe (kafiri) ni mwenye kuchukia hilo.”[42]

 

Mfano mwengine ni kuhusiana na Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ ﴿٢٥٨﴾

“... akasema: “Mimi (pia) nahuisha na nafisha...[43]

Kuhusiana na ibara hii: ‘Mimi (pia) nahuisha na nafisha,’ Qataadah amesema kuwa yule mfalme aliyemuhoji Nabiy Ibraahiym (عليه السلام) alimaanisha kuwa: Watu wawili waliostahiki kuuawa, wangeletwa mbele yake, na angeliamrisha mmoja wao auawe na angeliuawa; na angeliamrisha kuwa mtu wa pili asamehewe na angesamehewa; hivi ndivyo ninavyoleta uhai na kifo.”[44]

Hivyo Tafsiyr ya Taabi’iyn ni chanzo chengine cha kutafuta ufafanuzi pale inapokuwa haujapatikana ufafanuzi kutoka kwenye vyanzo vilivyotangulia.  Hata hivyo baadhi ya Wanachuoni wanaonelea kuwa Tafsiyr za Taabi’iyn na wanafunzi wao hazitoki moja kwa moja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na wala si kama Tafsiyr za Maswahaba (رضي الله عنهم), yote kwa kuwa Taabi’iyn na wanafunzi wao hawajamuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na wala hawakushuhudia Wahy pale zinapoteremshwa Aayah; na vilevile si wote wanakubalika uaminifu wao, kwa kuwa wao si kama Maswahaba (رضي الله عنهم) ambao uaminifu na uadilifu wao umeshuhudiwa na kuthibitishwa na Qur-aan. Ama wao Taabi’iyn na wanafunzi wao wamesifiwa kama ni ‘kizazi’ na si mmoja mmoja.

 

 

Hata hivyo, maelezo mazuri na ya salama ni yale ya Shu’bah bin Al-Hajjaaj na wengineo ambayo ameyanukuu Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: “Kauli za Taabi’iyn katika furuw’ (matawi ya Shariy’ah) si hoja, basi vipi zitakuwa hoja katika Tafsiyr. Kwa maana kuwa haziwi hoja juu ya wengineo wasiokuwa wao miongoni mwa wale waliowakhalifu; na hii ndio sahihi. Ama pale watakapokubaliana juu ya kitu, basi bila shaka yoyote ile ni hoja, na endapo watakhitalifiana basi haitokuwa kauli ya baadhi yao hoja juu ya wengine, na wala juu ya watakaokuja baada yao, bali kutafuatwa na kutazamwa lugha ya Qur-aan, au Sunnah, au kauli za Maswahaba (رضي الله عنهم).“[45]

 

Hakuna shaka yoyote ile kwamba ujuzi wa lugha ya Kiarabu, na matawi yake una mchango mkubwa na ni ufunguo katika kuifahamu Qur-aan na kuweza kupata Tafsiyr yenye kukubalika. Hivyo basi, ufahamu sahihi wa Tafsiyr ya Qur-aan, makusudio yake na yote yenye kufungamana nayo, unafungamana pia na ufahamu sahihi wa lugha ya Kiarabu na matawi yake.

 

Kadhaalika, kuna elimu na fani nyingi ambazo zimefungamana na kushikamana na Qur-aan zenye kuweza kusaidia katika kufikia kufahamu Tafsiyr ya Aayah; kama vile elimu ya Uswuwl ya Tafsiyr pamoja na kutabahari (kubobea) katika fani zote zile ambazo hakuna njia ya kufahamika Tafsiyr wala kuwa sahihi isipokuwa kwayo, kama vile kufahamu sababu za kuteremka kwa Aayah (Asbaab An-Nuzuwl), Naasikh wa Mansuwkh (kinachofuta na kilichofutwa), na kadhalika. Hivyo, Tafsiyr inayokubalika ni ile yenye kufuata Manhaj iliyoelezwa juu inayotegemea zaidi nukuu badala ya mawazo au rai ya Mfasiri.

 

Tarjama hii kwa lugha ya Kiswahili si Tarjama mpya, bali ni katika yale yanayohitajika kufanywa kwa Tarjama zilizopo kama ni huduma muhimu ya kujaribu kuzifikisha daraja ya kukubalika kiitikadi kutakozipelekea kuwa sahihi kiitikadi kwa kuthibitisha yale yote yaliyothibiti tena bila ya kuleta Ta'twiyl[46] wala kuleta Tamthiyl[47] wala kuleta Takyiyf[48] na wala kuleta Tahriyf[49], kisha kushikamana na hiyo itikadi kama vile walivyokuwa wameshikamana nayo Salaf.

 

Haitarajiwi Tarjama hii kuja na kipya kisichowahi kuthibiti au kusikiwa au kuandikwa, bali ni Tarjama inayotarajiwa kujaribu kuhuisha kwa kuyathibitisha yale yote yaliyothibiti kwa kusahihisha na kurekebisha pale palipokwenda kombo katika Tarjama za Kiswahili haswa haswa katika uwanja wa ‘Aqiydah na zaidi kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) katika Majina Yake na Sifa Zake na kumsifia kama Alivyojisifu Yeye Mwenyewe (سبحانه وتعالى) au alivyomsifu Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) bila ya kuzibadilisha sifa hizo, wala kuzigeuza wala kuzifananisha wala kuzipindua maana yake. Hivyo tumemthibitishia Allaah (سبحانه وتعالى) yale yote Aliyojithibitishia Mwenyewe (سبحانه وتعالى) kuanzia neno ‘mkono’, ‘uso’, ‘kuja’, ‘kuteremka’, na kadhalika.  Na jambo hili huenda likaonekana kuwa ni jipya na si la kawaida kwa baadhi yetu, na hali ni kuithibitisha itikadi ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah (Salaf), itikadi ambayo imepokelewa kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na ni itikadi ya Maswahaba zake (رضي الله عنهم) na ni itikadi ya kila aliyewafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Qiyaamah.

 

Tarjama itathibitisha maneno hayo na mengine kama hayo kama yalivyothibitishwa na Qur-aan na Sunnah sahihi za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) bila ya kumithilisha au kushabihisha au kuawilisha au kukanusha na kukataa, kwa visingizio kuwa yakithibitishwa kama yalivyothibitibasi kuna khofu kuwa atashabihishwa Muumba na viumbe Vyake! Hiyo si hoja muwafaka, kwani iymaan thabiti ya Muislamu kuhusiana na Allaah (سبحانه وتعالى) ni kuwa: Hapana anayefanana Naye (Muumba) hata mmoja wala hakuna kitu chochote mfano Wake kama inavyothibitishwa na Allaah (سبحانه وتعالى) Mwenyewe.[50]

 

Kwa hiyo, lengo kubwa la kuifanya kazi hii, ni kujaribu kuifanya iwe karibu kabisa na Tafsiyr za Salaf kwa kuchunga mas-alah yote ya ‘AQIYDAH na mengine muhimu kwa kuleta maana za karibu na sahihi zilizopokelewa na kuthibiti.

 

Tumeona ni vyema na ndio sahihi ndani ya kazi hii pia, kulithibitisha Jina ‘Allaah’ badala ya kulifasiri kwa kuligeuza na kutumia neno ‘Mwenyezi Mungu’, kama linavyotumika katika karibu Tarjama zote za lugha ya Kiswahili. Ni iymaan yetu kuwa kulithibitisha jina Lake ‘Allaah’, kama lilivyothibiti, ni kumuadhimisha Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) na kulipa haki Jina Lake Tukufu; na kubwa na la muhimu zaidi ni kuwa kuna thawabu kwa kuwa ndivyo lilivyothibiti. Hivyo, tutalitumia na kulithibitisha Jina la ‘Allaah’ pote katika Tarjama hii kama lilivyothibitishwa na Qur-aan na Sunnah za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa lengo la kuwarejesha Waumini katika kutumia Majina ya Allaah kama yalivyothibiti.

 

Hali kadhaalika, tumethibitisha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya “Rabb” kwa kuibakisha kama ilivyo katika asli yake bila kuipa maana; kwa sababu neno “Rabb” linatumika Kiswahili kama “Rabi” na linafahamika, vilevile kulipa maana ya “Mola” tumeona ni maana finyu isiyokidhi taarifu kamili ya “Rabb”. “Ar-Rabb” Ina maana nyingi na pana. Inaweza kumaanisha; Mfalme, Bwana, Mlezi, Mwendeshaji na Mpangaji, Mola, Msimamiaji, Mwenye Kuneemesha n.k. Hivyo, tumeonelea litumike kwenye Tarjama hii hivyo hivyo lilivyo.

 

Na katika Tarjama hii tumeona muhimu kutaja Asbaab An-Nuzuwl zilizo sahihi ili msomaji afahamu sababu ya kuteremshwa Aayah na apate ladha ya kufahamu sababu mbalimbali zilizosababisha kuteremshwa Aayah au Suwrah fulani, na hivyo kuongeza faida ya elimu yake ya Qur-aan.

 

Vilevile, tumeongezea baadhi ya faida za ziada ili nazo zimpanulie ufahamu msomaji na kumuongezea elimu na ufahamu wa Qur-aan kwa kina.

 

 

Tumetegemea zaidi katika kuikamilisha kazi hii Tafsiyr zifuatazo:

 

·       تفسير القرآن العظيم للإمام الحافظ ابن كثير

Tafsiyr Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym ya Al-Haafidhw ‘Imaad Ad-Diyn Abi Al-Fidaa Ismaa’iyl bin Kathiyr.

 

au maarufu kama ‘Tafsiyr Ibn Kathiyr

·       تفسير ابن كثير

 

·       تيسير الكريم الرحمن في تفسير كلام المنان

Taysiyr Al-Kariym Ar-Rahmaan Fiy Tafsiyr Kalaam Al-Manaan ya Al-‘Allaamah Ash-Shaykh ‘Abdur-Rahmaan bin Naaswir As-Sa’diy.

au maarufu kama ‘Tafsiyr As-Sa’diy.

تفسير السعدي

 

·       التفسير الميسر - نخبة من العلماء

At-Tafsiyr Al-Muyassar – Nukhbat Minal ‘Ulamaa

 

Na Tarjama (Tarjama) ifuatayo ya Kiingereza:

·        Interpretation of The Meanings of THE NOBLE QUR’AN IN THE ENGLISH LANGUAGE (a Summarized Version of At-Tabari, Al-Qurtubi and Ibn Kathir with Comments from Sahih Al-Bukhari – Dr. Muhammad Taqi-ud-Diyn Al-Hilaaliy, Dr Muhammad Muhsin Khan.

 

Mwisho tunamshukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutuwafikisha kuweza kuikamilisha kazi hii tukufu, kazi ambayo ni jukumu kubwa mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) na wala hatusemi kuwa Tarjama hii itakuwa haina kasoro, kwani hakuna mkamilifu isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى).

 

Tunawaomba ndugu zetu watuarifu kwa kosa lolote lile watakaloligundua au kasoro yoyote ile watakayoiona.

 

Tunamuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Atughufurie kwa makosa yetu na Aijaalie kazi hii iwe ni kwa ajili ya kuzipata radhi Zake Pekee na Atutakabalie.

Na Allaah Anajua zaidi

 

الحمد لله رب العالمين وصلى الله على محمد وعلى آله واصحابه وسلم

 

 

 

Imeandaliwa Na:  Alhidaaya.com

 

 

 

[1] Fusw-swilat (41: 42).

[2] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ﴿٨٨

Sema: “Ikiwa watajumuika wana Aadam na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan; hawatoweza kuleta mfano wake, japokuwa watasaidiana wao kwa wao.” [Al-Israa 17:88].

[3] Ibraahiym (14: 4).

[4] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ ﴿١٠٣﴾

Na kwa yakini Tunajua kwamba wao wanasema: “Hakika hapana isipokuwa mtu anamfundisha (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم Qur-aan).” Lisani wanayomnasibishia nao ni ya kigeni, na hii ni lisani ya Kiarabu bayana. [An-Nahl 16:103].

 

[5] Mfano wa haraka ni kama neno ‘Istawaa’ katika Aayah ya 5 ya Suwrah ya 20 (Twaahaa), Tarjuma za Kiswahili zilizoko hivi sasa, karibu zote zinaeleza ‘istiwaa’ (kulingana, kuwa juu) kuwa maana yake ‘istawlaa’ ni ‘kutawala’, kinyume na ufahamu na tafsiyr ya Salaf ya neno hilo. Msimamo wa Salaf katika tafsiyr ya Aayah hiyo ni kama huu uliopokelewa kuwa, Ja’far bin ‘Abdillaah na wengine miongoni mwao walisema: “Tulikuwa kwa Imaam Maalik bin Anas basi akatokea mtu akamuuliza? Ee Abaa ‘Abdillaah! Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥

“Ar-Rahmaan; Yuko juu (Istawaa) ya Arsh.” [Twaahaa 20: 5]. 

Je, ni vipi Istawaa? Basi Imaam Maalik hakuwahi kughadhibika kutokana na kitu chochote kile kama alivyoghadhibika kutokana na swali la mtu huyo, kisha (Imaam Maalik) akatazama chini na huku akikwaruza kwaruza kwa kijiti kilichokuwa kwenye mkono wake mpaka akarowa jasho, kisha akanyanyua kichwa chake na kukirembea kile kijiti kisha akasema: ‘Vipi’ ni ghayr-ma’quwl (hakutambuliki), na al-Istiwaa ghayr-maj-huwl (si jambo lisilojulikana), na kuamini hilo ni waajib (lazima), na kuuliza (au kuhoji hilo) ni bid’ah (uzushi); na nina khofu kuwa wewe ni mzushi.” Akaamrisha mtu huyo atolewe; basi akatolewa.” 

Imesimuliwa kwenye Al-Hilyah (6/325-326) na pia imesimuliwa na Abu ‘Uthmaan Asw-Swaabuniy katika ‘Aqiydatus Salaf Asw-haab Al-Hadiyth (uk. 17-18), kutoka kwa Ja’far bin ‘Abdillaah kutoka kwa Maalik na Ibn ‘Abdil-Barr katika At-Tamhiyd (7/151) kutoka kwa ‘Abdullaah bin Naafi’ kutoka kwa Maalik na Al-Bayhaqiyy katika Al-Asmaa wasw-Swifaat (uk. 408) kutoka kwa ‘Abdullaah bin Wahb kutoka kwa Maalik; Ibn Hajr amesema katika Al-Fat-h (13/406-407) mlolongo wake ni mzuri na imesahihishwa na Adh-Dhahabiy katika Al-‘Uluww (uk. 103). Shaykh Al-Albaaniy amesema Hadiyth hii ni Swahiyh Mukhthaswar Al-‘Uluww - Imaam Adh-Dhahabiy iliyopitiwa na Shaykh Muhammad Naaswirud-Diyn Al-Albaaniy (uk. 131).

[6]Salaf ni Maswahaba (رضي الله عنهم) na wanafunzi wao -Taabi’iyn- na wanafunzi wa wanafunzi wao -Atbaa’ Taabi’iyn-. Hawa ni wale aliowataja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa ni watu bora kabisa wa karne zote.

 

[7] Tazama Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr - Ibn Taymiyyah.

[8] Al-An’aam (6: 105).

[9] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ ﴿١٧﴾ فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ ﴿١٨﴾ ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ ﴿١٩﴾

Hakika ni juu Yetu kuikusanya na kukuwezesha kuisoma kwake. Basi Tunapoisoma (kupitia Jibriyl), fuata kusomwa kwake. Kisha ni juu Yetu kuibainisha (kwako).” [Al-Qiyaamah 75: 17-19].

 

[10] Al-An’aam (6: 59).

[11] Luqmaan (31: 13).

[12] Al-An‘aam (6:  82).

[13] Luqmaan (31: 13).

[14] Sunnah (Hadiyth) ni kila kilichonasibishwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kauli au kitendo au yale aliyoyakubali au sifa za kimaumbile au tabia au mwenendo.

[15]Hakika kila kile alichohukumu kwacho Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni katika yale aliyoyaelewa (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na Qur-aan; kama alivyosema Imaam Ash-Shaafi’y; taz. Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr. Allaah (سبحانه وتعالى)Anasema:

إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ بِمَا أَرَاكَ اللَّـهُ ۚ وَلَا تَكُن لِّلْخَائِنِينَ خَصِيمًا ﴿١٠٥﴾

Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki ili uhukumu baina ya watu kwa Aliyokuonyesha Allaah. Wala usiwe mtetezi kwa makhaini. [An Nisaa 4: 105]; pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

وَمَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي اخْتَلَفُوا فِيهِ ۙ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٦٤﴾

Na Hatukukuteremshia Kitabu isipokuwa uwabainishie yale waliyokhitilafiana kwayo, na ni mwongozo na rahmah kwa watu wanaoamini.” [An Nahl 16: 64].

[16] Kama ilivyothibiti kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema

((أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ، أَلَا يُوشِكُ رَجُلٌ يَنْثَنِي شَبْعَانًا عَلَى أَرِيكَتِهِ يَقُولُ: "عَلَيْكُمْ بِالْقُرْآنِ فَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِ مِنْ حَلَال فَأَحِلُّوهُ وَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِمِنْ حَرَامٍ فَحَرِّمُوهُ... ((رواه أبو داود والترمذي والحاكم وصححه وأحمد بسند صحيح

“Tanabahi! Hakika nimepewa Qur-aan na inayofanana nayo (Sunnah) Tanabahi! Utafika wakati mtu aliyeshiba mno ataegemea kwenye kochi na kusema: “Shikamaneni na Qur-aan, mtakayokuta humo ya halali halalisheni, na mtakayokuta ya haramu haramisheni.” [Imepokewa na Abu Daawuwd, na At-Tirmidhiy, na Al-Haakim na ameisahihisha Ahmad kwa isnaad Swahiyh].

 

[17] Al-Anfaal (8: 60).

[18] Muslim, katika Kitabu cha Al-Imaarah, mlango wa fadhila za Ar-Ramyu na ushajiishaji wake; na At-Tirmidhiy, katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, mlango na katika Suwrah Al-Anfaal.

[19] Al-Kawthar (108: 1).

[20] Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, Tafsiyr Suwrat Al-Kawthar, At-Tirmidhiy, katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, mlango na katika Suwrah Al-Kawthar.

[21] Yuwnus (10: 26).

[22] Ahmad, katika Musnad Kumi waliobashiriwa Jannah, Ukamilisho wa Musnad ya Kuufiyyiyn; na At-Tirmidhiy, katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, mlango na katika Suwrah Yuwnus.

[23]Ni Tafsiyr yenye kutegemea yaliyo sahihi katika yaliyopokelewa kulingana na mpangilio huu; Tafsiyr ya Qur-aan kwa Qur-aan; Tafsiyr ya Qur-aan kwa Sunnah, Tafsiyr ya Qur-aan kwa kauli za Maswahaba (رضي الله عنهم), Tafsiyr ya Qur-aan kwa kauli za Taabi’iyn kwa kuwa wao walichukua tafsiyr zao kutokana na Maswahaba (رضي الله عنهم). Vitabu vinavyotajika katika fani hii ya Tafsiyr ni kama:

i. Jaami’ul Bayaan Fiy Tafsiyril Qur-aan ya Ibn Jariyr Atw-Twabariy.

ii. Tafsiyrul Qur-aanil ‘Adhwiym ya Ibn Kathiyr.

iii. Fat-hul Qadiyr ya Ash-Shawkaaniy.

[24] Utangulizi wa Tafsiyr Ibn Kathiyr; vyanzo vya Tafsiyr.

[25] [An-Nahl 16: 44]. Kadhalika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ ﴿١٩

“Kisha ni juu Yetu kuibainisha (kwako).” [Al-Qiyaamah 75:19] inawarudi kwa uwazi kabisa wale wenye kudai kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakubainisha maana ya Majina na Sifa za Allaah, na kwa kauli yao hii; ima wanakusudia kuwa: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa hajui maana ya Majina na Sifa za Allaah; au ima Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alificha kile alichokifahamu. Taz. Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr.

[26]Amesema Abuu ‘Abdir-Rahmaan As-Sulamy: “Wametuhadithia wale waliokuwa wakitusomesha Qur-aan kama ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رضي الله عنه) na ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) na wengineo kuwa wao walikuwa pale wanapojifunza kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Aayah kumi huwa hawaongezi nyingine mpaka pale watakapojifunza (na kutekeleza) yale yaliyomo ya elimu na ‘amali katika hizo Aayah kumi walizojifunza, basi wakasema: Tulijifunza Qur-aan na elimu na ‘amali kwa pamoja, na kwa sababu hiyo ndio walikuwa wakichukua muda kati kuhifadhi Suwrah.” Taz. Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr.

[27]Aliyepokelewa akisema: “Naapa kwa Yule Ambaye hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakuna katika Kitabu cha Allaah Suwrah isipokuwa mimi najua ilivyoteremka, na hakuna Aayah isipokuwa najua imeteremshwa kwa ajili gani (sababu) na lau ningelimjua yeyote kuwa yeye ni mjuzi zaidi yangu kwa Kitabu cha Allaah, na ngamia anaweza kufika, basi ningepanda kwenda kwake.” [Imepokelewa na Muslim, katika Kitabu cha Fadhila za Maswahaba, mlango wa fadhila za ‘Abdullaah bin Mas’uwd na mama yake (رضي الله عنهما)].

[28]Ibn ‘Abbaas aliyetambulikana kama ni ‘Tur-jumanil Qur-aan’ na aliyeombewa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kama ilivyothibiti kwa kusema:

((اللَّهُمَّ عَلِّمْهُ الْحِكْمَةَ وَتَأْوِيلَ الْكِتَابِ))

“Ee Allaah, Mfunze Hikmah na Ta-awiyl (ufasiri, utambuzi) wa Kitabu (Qur-aan).” [Imepokelewa na At-Tirmidhiyy, katika Kitabu cha Ad-Da’waat, milango ya Manaaqiyb; na Sunan Ibn Maajah, katika Kitabu cha Ibn Maajah, milango ya fadhila za Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)].

[29]Ni kila kilichotegemezwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kauli au kitendo au kuthibitisha jambo au sifa katika tabia zake au umbo lake.

[30]An-Nisaa (4: 43).

[31]Tafsiyr Ibn Kathiyr.

[32] Luqmaan (31: 6).

[33] Atw-Twabariy (20: 127).

[34] Al-Baqarah (2: 158).

[35] Al-Baqarah (2: 158).

[36] Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, Suwrat Al-Baqarah, mlango wa aliyekuwa adui wa Jibriyl.

[37] Tazama Ibn Taymiyyah, Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl at-Tafsiyr.

[38] Kama vile Mujaahid, Sa’iyd bin Jubayr, ‘Ikrimah, Twaawuws, ‘Atwaa, Zayd bin Aslam, Abul ‘Aaliyah na Muhammad bin Ka’b, ‘Alqamah bin Qays, Masruwq, ‘Aamir Ash-Sha’biy na Hasan Al-Baswriy na Qataadah.

[39] Imaam At-Tirmidhiy amesema: “Ama yale yaliyopokelewa kutokana na Mujaahid na Qataadah na wengineo miongoni mwa Ahlul-‘Ilmi kwamba walifasiri Qur-aan,  basi hakuna haja ya kuwadhania kuwa walifasiri Qur-aan bila ya elimu –kwa rai zao- au kutokana na nafsi zao, na kumekwishapokewa kutokana na wao yale tuliyoyasema yenye kuthibitisha kwamba wao hawakuifasiri Qur-aan kutokana na nafsi zao bila ya elimu; kama ilivyothibiti kutokana na Al-Hassan bin Al-Mahdiy Al-Baswriyy amesema: Ametupa khabari ‘Abdur-Razzaaq kutokana na Ma’mar kutoka kwa Qataadah kuwa amesema: “Katika Qur-aan hakuna Aayah yoyote ile isipokuwa nimesikia kitu kuhusiana nayo.” [At-Tirmidhiyy katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, mlango wa katika yale yaliyokuja kwa yule anayefasiri Qur-aan kwa rai yake]

[40] Kutoka kwa Ibn Mas’uwd(رضي الله عنه)  amesema kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

((خَيْرُ النَّاسِ قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ)) صحيح البخاري ومسلم

“Watu bora kabisa ni karne yangu, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Kitabu Al-Manaaqib, mlango wa Fadhila za Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); na Muslim Kitabu cha Fadhila za Maswahaba, mlango wa Fadhila za Maswahaba (رضي الله عنهم)].

[41] Al-Baqarah (2: 116).

[42] Tafsiyr Ibn Kathiyr.

[43] Al-Baqarah (2: 258).

[44] Tafsiyr Ibn Kathiyr.

[45] Tazama Ibn Taymiyyah, Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr.

[46] Kukanusha maana.

[47] Mithilisha; linganisha, kufananisha.

[48] Kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo kuchunguza ni kwa namna “gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah.

[49] Kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah kwa kutoa maana isiyo sahihi.

[50] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١١﴾

“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye Mwenye kusikia yote daima, Mwenye kuona yote daima.[Ash-Shuwraa 42: 11].

 

Share

001 - Al-Faatihah

 

 الْفَأتِحَة

Al-Faatihah[1]: 1

 

 

 

Imeteremka Makkah kwa kauli iliyokuwa Sahihi, na ndiyo kauli ya Jumhuri ya ‘Ulamaa (Wanachuoni wengi)

 

 

 

 

 بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿١﴾

1. Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.

 

 

 الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾

2. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah) Rabb wa walimwengu.

 

 

الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣﴾

3. Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.

 

 

 مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٤﴾

4. Mfalme wa siku ya malipo.

 

 

 إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

5. Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.

 

 

اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿٦﴾

6. Tuongoze njia iliyonyooka.[2]

 

 

صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ ﴿٧﴾

7. Njia ya wale Uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.[3]

 

[1] Faida: Hii ni Suwrah iliyokuwa Adhimu na bora, kuliko Suwrah zote za Qur-aan, nayo ni miongoni mwa Suwrah zenye majina mengi na miongoni mwa majina yake ni: Al-Faatihah, Ummul-Qur-aan, AlhamduliLLaah, Asw-Swalaah, Ash-Shifaa, Ar-Ruqyahh, Sab‘ul-Mathaaniy, Ummul-Kitaab. Haijateremka katika Tawraat wala katika Injiyl wala katika Zaburi mfano wake.

Utukufu na Fadhila za Suwratul-Faatihah unaelezewa katika Hadiyth nyingi, baadhi yake ni hizi zifuatazo:

 

Hadiyth Ya Kwanza:

 

Abuu Sa’iyd bin Al-Mu’allaa (رضي الله عنه) amehadithia kwamba:  Nilikuwa nikiswali, akaniita Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikawa sikumuitikia mpaka nilipomaliza kuswali. Kisha nikamwendea akaniambia: “Kimekuzuia nini usinijie?”  Nikasema:  Ee Rasuli wa Allaah, nilikuwa naswali. Akasema: “Kwani Allaah Hakusema: “Enyi walioamini! Muitikieni Allaah na Rasuli Anapokuiteni kwenye yale yenye kukuhuisheni.” [Al-Anfaal (8: 24)]. Kisha akasema: “Nitakufundisha Suwrah tukufu kabisa katika Qur-aan kabla hukutoka Msikitini.” Akanikamata mkono, alipotaka kutoka Msikitini, nikamwambia: ee Rasuli wa Allaah, ulisema utanifundisha Suwrah tukufu kabisa katika Qur-aan. Akasema: “Naam, AlhamduliLLaahi Rabbil-‘Alaamiyn, hiyo ni (Aayaat) Saba zinazokaririwa (kusomwa) na Qur-aan Adhimu niliyopewa.” [Al-Hijr (15: 87) Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth Ya Pili:

 

Abuu Sa’iyd Al-Khudhriyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Baadhi ya Swahaaba (wakiwa safarini) walifika karibu na kabila fulani la Waarabu, wakakataa kuwapokea. Walipobakia katika hali hiyo, huku mkuu wao alitafunwa na nyoka (au nge). Wakasema: Je, mna dawa yoyote au tabibu? Wakajibu: Nyinyi mmekataa kutupokea kwa hiyo hatutamtibu mgonjwa wenu hadi mtulipe! Wakakubali kuwapa kundi la kondoo. Mmoja wa Swahaba akaanza kumsomea Suwratul-Faatihah huku akikusanya mate na kumtemea (mahali alipotafunwa). Mgonjwa akapona kisha watu wake wakawaletea kondoo lakini wakasema. Tusiwachukue mpaka tumuulize Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Walipomuuliza alicheka akasema: “Mmejuaje kuwa Suwratul-Faatihah ni ruqyah? Chukueni na nigaieni sehemu yangu.” [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth Ya Tatu:

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: Jibriyl (عليه السلام) alipokuwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisikia sauti kutoka juu. Jibriyl (عليه السلام) akatazama juu akasema: “Huu mlango wa mbinguni umefunguliwa na haujapatapo kufunguliwa isipokuwa leo.” Malaika akateremka humo akasema: “Huyu Malaika ameteremka ardhini, hajapatapo kuteremka kamwe isipokuwa leo.” Akasalimia kisha   akasema: “Pokea bishara ya nuru mbili ulizopewa ambazo hakuna Nabiy aliyepewa kabla yako; Ufunguo wa Kitabu (Al-Faatihah), na Aayah (mbili) za mwisho wa Suwratul-Baqarah.  Hutosoma herufi humo ila utapewa barakah zake zilizomo.” [Muslim]

 

Hadiyth Ya Nne:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayeswali Swalaah bila ya kusoma humo mama wa Qur-aan (Suwratul-Faatihah) huwa haikutimia (ina kasoro).” Alikariri mara tatu: “Haikutimia.” Mtu mmoja alimwambia Abuu Hurayrah: (Hata) tukiwa nyuma ya Imaam? Akasema: Isome mwenyewe (kimya kimya) kwani nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Allaah (تعالى) Amesema: Nimeigawa Swalaah baina Yangu na mja Wangu nusu mbili, mja Wangu atapata yale aliyoyaomba. Mja anaposema: AlhamduliLLaah; Rabb wa walimwengu, Allaah (تعالى) Husema: Mja Wangu kanihimidi.  Na anaposema: Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu, Allaah (تعالى) Husema: Mja wangu kanisifu na kunitukuza kwa wingi, na anaposema: Mfalme wa siku ya malipo, Allaah (تعالى) Husema: Mja wangu kaniadhimisha. Na mara moja alisema: Mja wangu ameniaminisha. Na anaposema: Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada, Husema: Hii ni baina Yangu na mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba. Na anaposema: Tuongoze njia iliyonyooka, njia ya wale Uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea, Husema: Hii ni ya mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba.” [Muslim, Maalik, At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]  

 

Hadiyth Ya Tano:

 

‘Ubaadah bin Swaamitw (رضي الله عنه) amehadithia kwamba  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna Swalaah kwa asiyesoma (ndani yake) Ufunguo wa Kitabu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

  

 

[2] Faida: Kuhusu njia iliyonyooka:

 Hadiyth Ya Kwanza:

 

 An-Nawaas bin Sam’aan  (رضي الله عنه)amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (تعالى) Amepiga mfano; Swiraatw (njia) iliyonyooka, imezungukwa pande zote na kuta mbili na kila ukuta una milango iliyo wazi na imefunikwa na mapazia. Na katika lango la swiraatw kuna mlinganiaji akiita: “Enyi watu! Ingieni nyote katika swiraatw na msipite pembeni.” Na juu ya swiraatw, mlinganiaji mwengine anamuonya mtu yeyote anayetaka kufungua hiyo milango akiwaambia: Masikitiko kwenu! Msiufungue! Kwani  mkifungua mtapita ndani! Kwani Asw-Swiraatw ni Uislaam, na kuta mbili ni mipaka Aliyoiweka Allaah. Na milango iliyofunguliwa ni yaliyoharamishwa na Allaah. Na huyo Daa’iy (mlinganiaji) juu ya lango la Swiraatw ni Kitaabu cha Allaah, na Daa’iy juu ya swiraatw ni maonyo ya Allaah yaliyo ndani ya kila nafsi ya Muislaam.”  [Ahmad, ameisahihisha Al-Albaaniy; Swahiyh Al-Jaami’ (3887)]

 

Hadiyth Ya Pili:

 

Jaabir (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Tulikuwa tumekaa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akachora mstari mbele yake, akachora mistari miwili kuliani, na mistari miwili kushotoni kisha akaweka mkono wake katika njia ya katikati akasema: “Hii njia ya Allaah” Kisha akasoma: “Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni, na wala msifuate njia (nyinginezo) zitakufarikisheni na njia Yake.” [Ahmad, Swahiyh Ibn Maajah (11)] 

[3] Faida: ‘Adiy bin Haatim (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Walioghadhibikiwa ni Mayahudi, na waliopotea ni Manaswara.” [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Ghariyb na taz. Silsilah Asw-Swahiyhah (363)]

 

Share

002 - Al-Baqarah

 

الْبَقَرَة

Al-Baqarah: 2 [1]

 

Imeteremka Madiynah, hakuna khilafu katika kauli hii.

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

 الم ﴿١﴾

1. Alif Laam Miym.[2]

 

 

ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾

2. Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wenye taqwa.[3]

 

 

 

الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾

3. Ambao huamini ya ghayb na husimamisha Swalaah na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.[4]

 

 

وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿٤﴾

4. Na ambao huamini yaliyoteremshwa kwako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenye yakini na Aakhirah.

 

 

 أُولَـٰئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥﴾

5. Hao wako juu ya mwongozo kutoka kwa Rabb wao, na hao ndio wenye kufaulu.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٦﴾

6. Hakika wale waliokufuru ni sawa kwao, ukiwaonya au usiwaonye wao hawatoamini.

 

 

خَتَمَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ ۖ وَعَلَىٰ أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٧﴾

7. Allaah Amepiga mhuri juu ya nyoyo zao, na juu ya masikio yao; na juu ya macho yao pana kifuniko; na watapata adhabu kuu.

 

 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾ 

8. Na miongoni mwa watu wako wasemao: ”Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho” hali ya kuwa si wenye kuamini.

 

 

يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾

9. (Wanadhani) Wanamhadaa Allaah na wale walioamini lakini hawahadai ila nafsi zao na wala hawahisi.

 

 

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ ﴿١٠﴾

10. Ndani ya nyoyo zao mna maradhi na Allaah Akawazidishia maradhi, na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha.

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ ﴿١١﴾

11. Na wanapoambiwa: “Msifanye ufisadi katika ardhi.” Husema: “Hakika sisi ni watengenezaji.”

 

 أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ ﴿١٢﴾

12. Tanabahi! Hakika wao ndio mafisadi lakini hawahisi.

 

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا كَمَا آمَنَ النَّاسُ قَالُوا أَنُؤْمِنُ كَمَا آمَنَ السُّفَهَاءُ ۗ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهَاءُ وَلَـٰكِن لَّا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾

13. Na wanapoambiwa: “Aminini kama walivyoamini watu.” Husema: “Je, tuamini kama walivyoamini wapumbavu.” Tanabahi! Hakika wao ndio wapumbavu lakini hawajui.

 

 

 وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا إِلَىٰ شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِئُونَ ﴿١٤﴾

14. Na wanapokutana na wale walioamini husema: “Tumeamini.” Na wanapokuwa peke yao pamoja na mashaytwaan wao, husema: “Hakika sisi tuko pamoja nanyi, hakika sisi ni wenye kuwadhihaki tu.”

 

 

 اللَّـهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١٥﴾

15. Allaah Anawadhihaki wao na Atawaendeleza katika hali yao ya upindukiaji mipaka wa kuasi, wakitangatanga kwa upofu.

 

 

 أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَارَتُهُمْ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٦﴾

16. Hao ndio wale waliobadilisha upotofu badala ya uongofu, basi haikupata faida  biashara yao na wala hawakuwa wenye kuongoka.

 

 

مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ ﴿١٧﴾

17. Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, ulipoyaangaza yaliyopo pembezoni mwake Allaah Akawaondoshea nuru yao na Akawaacha katika viza; hawaoni.

 

صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿١٨﴾

18. Viziwi, mabubu, vipofu basi hawatorejea.

 

 

 أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾

19. Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni, ndani yake mna viza na radi na umeme, wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakikhofu mauti, na Allaah ni Mwenye kuwazunguka makafiri.  

 

 

يَكَادُ الْبَرْقُ يَخْطَفُ أَبْصَارَهُمْ ۖ كُلَّمَا أَضَاءَ لَهُم مَّشَوْا فِيهِ وَإِذَا أَظْلَمَ عَلَيْهِمْ قَامُوا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَذَهَبَ بِسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٠﴾

20. Unakaribia umeme kunyakua macho yao, kila unapowaangazia (njia) hutembea humo, na unapowafanyia kiza husimama; na lau Allaah Angelitaka basi Angeliwaondoshea kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 

 يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٢١﴾

21. Enyi watu! Mwabuduni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa.

 

 

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾

22. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.

 

 

 وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾

23. Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake, na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli. 

 

 

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا وَلَن تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿٢٤﴾

24. Msipofanya, na wala hamtoweza kufanya, basi ogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa kwa makafiri.

 

 

وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ كُلَّمَا رُزِقُوا مِنْهَا مِن ثَمَرَةٍ رِّزْقًا ۙ قَالُوا هَـٰذَا الَّذِي رُزِقْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَأُتُوا بِهِ مُتَشَابِهًا ۖ وَلَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥﴾

25. Na wabashirie wale walioamini na wakatenda mema kwamba watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, kila watakaporuzukiwa humo katika matunda kuwa ni riziki husema: “Haya ndiyo yale tuliyoruzukiwa kabla.” Na wataletewa hali ya kuwa yanashabihiana, na watapata humo wake waliotakaswa, nao humo ni wenye kudumu.

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾

26. Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na ulio zaidi yake (kwa udogo). Basi wale walioamini wanajua kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wao; ama wale waliokufuru husema: “Anataka nini Allaah kwa mfano huu?” Kwa (mfano) huo, Huwapoteza wengi na Huwaongoza kwayo wengi na wala Hawapotezi kwavyo ila mafasiki.

 

 

الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٢٧﴾

27. Wale wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata Aliyoyaamrisha Allaah kuungwa, na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye khasara.

 

 

 كَيْفَ تَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَكُنتُمْ أَمْوَاتًا فَأَحْيَاكُمْ ۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٨﴾

28. Vipi mnamkufuru Allaah na hali mlikuwa wafu Akakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakuhuisheni, kisha Kwake mtarejeshwa?

 

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٩﴾ 

29. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini Kisha Akazielekea (Istawaa[5]) mbingu na Akazifanya timilifu mbingu saba, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

 

 وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾

30. Na pindi Rabb wako Alipowaambia Malaika: “Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi khalifa.” Wakasema: “Utaweka humo atakayefanya ufisadi humo na kumwaga damu, na hali sisi tunakusabihi kwa Himidi Zako na tunakutukuza kwa Utakatifu Wako?” (Allaah) Akasema: “Hakika Mimi Nayajua zaidi msiyoyajua.”

 

 

وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣١﴾

31. Na Akamfunza Aadam majina yote (ya kila kitu), kisha Akavionesha mbele ya Malaika; Akasema: “Niambieni majina ya hivi mkiwa ni wakweli.”

 

 

قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٣٢﴾

32. Wakasema: Utakasifu ni Wako hatuna elimu isipokuwa Uliyotufunza; hakika Wewe Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

 قَالَ يَا آدَمُ أَنبِئْهُم بِأَسْمَائِهِمْ ۖ فَلَمَّا أَنبَأَهُم بِأَسْمَائِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٣٣﴾

33. Akasema: “Ee Aadam, wajulishe kwa majina yao.” Basi alipowatajia majina yao; (Allaah) Akasema: “Je, Sikuwaambieni kuwa hakika Mimi Najua ghayb ya mbingu na ardhi na Najua mnayoyadhihirisha na mliyokuwa mkiyaficha.

 

 

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٣٤﴾

34. Na pale Tulipowaambia Malaika: “Msujudieni Aadam.” Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari na akawa miongoni mwa makafiri.

 

 

 وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٣٥﴾

35. Na Tukasema: “Ee Aadam, kaa wewe na mkeo (Hawaa) Jannah na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na wala msiukaribie mti huu; mtakuwa miongoni mwa madhalimu.”

 

 

فَأَزَلَّهُمَا الشَّيْطَانُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ ۖ وَقُلْنَا اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٣٦﴾

36. Shaytwaan akawatelezesha wote wawili kwayo, Akawatoa kutoka katika hali waliyokuwa nayo. Tukasema: “Shukeni mkiwa maadui nyinyi kwa nyinyi, na mtapata katika ardhi makazi na starehe hadi muda maalum.”

 

 

 فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِن رَّبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٣٧﴾

37. Kisha Aadam akapokea maneno kutoka kwa Rabb wake; na (Rabb wake) Akapokea tawbah yake, hakika Yeye Ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.

 

 

قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٨﴾

38. Tukasema: “Shukeni kutoka humo nyote. Utakapokufikieni kutoka Kwangu mwongozo basi yeyote atakayefuata mwongozo Wangu hakutokuwa na khofu juu yao wala hawatohuzunika.”

 

 

وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (ishara, dalili) Zetu hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَوْفُوا بِعَهْدِي أُوفِ بِعَهْدِكُمْ وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ ﴿٤٠﴾

40. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na timizeni ahadi Yangu Nikutimizieni ahadi yenu na Mimi Pekee niogopeni.

 

 

وَآمِنُوا بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ ۖ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّايَ فَاتَّقُونِ ﴿٤١﴾

41. Na aminini yale Niliyoyateremsha yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nanyi, na wala msiwe wa kwanza wenye kuzikanusha; na wala msibadilishe Aayaat Zangu kwa thamani ndogo na muwe na taqwa kunikhofu Mimi tu.

 

 

وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na wala msichanganye haki kwa batili na mkaficha haki; na hali mnajua.

 

 

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾

43. Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah na rukuuni pamoja na wanaorukuu (katika utiifu).

 

 

أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٤٤﴾ 

44. Je, mnaamrisha watu watende mema na mnajisahu nafsi zenu na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu; je hamtii akilini? 

 

 

وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na tafuteni msaada kupitia subira na Swalaah; na hakika hilo ni kubwa isipokuwa kwa wanyenyekevu.

 

 

الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ وَأَنَّهُمْ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ﴿٤٦﴾

46. Ambao wana yakini kwamba hakika wao ni wenye kukutana na Rabb wao na hakika wao Kwake ni wenye kurejea.

 

 

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾

47. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya walimwengu wote.[6]

 

 

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٤٨﴾ 

48. Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitoifaa nafsi nyingine kwa kitu chochote kile, na wala haitokubaliwa kutoka kwake uombezi wowote na wala hakitochukuliwa kutoka kwake kikomboleo, na wala hawatonusuriwa.

 

 

وَإِذْ نَجَّيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿٤٩﴾

49. Na pindi Tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Fir’awn walipokusibuni adhabu mbaya, wakiwachinja watoto wenu wa kiume na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo kwenu ulikuwa ni mtihani mkuu kutoka kwa Rabb wenu. 

 

 

وَإِذْ فَرَقْنَا بِكُمُ الْبَحْرَ فَأَنجَيْنَاكُمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٠﴾ 

50. Na pindi Tulipoitenganisha bahari kwa ajili yenu; Tukakuokoeni na Tukawagharikisha watu wa Fir’awn na huku nyinyi mnatazama.

 

 

وَإِذْ وَاعَدْنَا مُوسَىٰ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٥١﴾

51. Na pindi Tulipomuahidi Muwsaa siku arubaini kisha mkamwabudu ndama baada yake na mkawa madhalimu.

 

 

ثُمَّ عَفَوْنَا عَنكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٢﴾ 

52. Kisha Tukawasameheni baada ya hapo ili mpate kushukuru.

 

 

وَإِذْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَالْفُرْقَانَ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿٥٣﴾

 53. Na pindi Tulipompa Muwsaa Kitabu na Furqaan (upambanuo) ili mpate kuongoka.

 

 

 وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ عِندَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٥٤﴾

54. Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu yake: “Enyi kaumu yangu! Hakika nyinyi mmedhulumu nafsi zenu kwa kuabudu kwenu ndama, basi tubuni kwa Muumbaji wenu;  na ziueni nafsi zenu, hivyo ni bora kwenu mbele ya Muumbaji wenu.” Akapokea tawbah yenu; hakika Yeye Ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.

 

 

وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْكُمُ الصَّاعِقَةُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٥﴾

55. Na pindi mliposema: “Ewe Muwsaa! Hatutokuamini mpaka tumuone Allaah wazi wazi”; ikakuchukueni radi na umeme angamizi nanyi mnatazama.

 

 

ثُمَّ بَعَثْنَاكُم مِّن بَعْدِ مَوْتِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٦﴾

56. Kisha Tukakufufueni baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru.

 

 

وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۖ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٥٧﴾ 

57. Na Tukakufunikeni kwa mawingu na Tukakuteremshieni Al-Manna na As-Salwaa. (Tukakwambieni): “Kuleni katika vizuri Tulivyokuruzukuni.” Hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.

 

 

 

وَإِذْ قُلْنَا ادْخُلُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ فَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا حِطَّةٌ نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطَايَاكُمْ ۚ وَسَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٨﴾

58. Na pindi Tuliposema: “Ingieni mji huu (Quds) na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, na ingieni katika mlango wake huku mmeinama kunyenyekea na semeni “Hittwah” (Tuondolee uzito wa madhambi); Tutakughufurieni makosa yenu na Tutawazidishia (thawabu) wafanyao ihsaan.

 

فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٥٩﴾ 

59. “Basi wale waliodhulumu walibadilisha kauli kinyume na ile waliyoambiwa, Tukateremsha juu ya waliodhulumu adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa yale waliyokuwa wakifanya ya ufasiki.”

 

 

وَإِذِ اسْتَسْقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ فَقُلْنَا اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ ۖ فَانفَجَرَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۖ كُلُوا وَاشْرَبُوا مِن رِّزْقِ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٦٠﴾

60. Na pindi Muwsaa alipoomba maji kwa ajili ya kaumu yake. Tukasema: “Piga kwa fimbo yako jiwe.” Zikachimbuka na kububujika kutoka kwalo chemchem kumi na mbili. Kila kabila likajua kinywaji chao. Kuleni na kunyweni kutokana na riziki ya Allaah na wala msieneze uovu katika ardhi hali ya kuwa ni wenye kufanya ufisadi.

 

 

وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نَّصْبِرَ عَلَىٰ طَعَامٍ وَاحِدٍ فَادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُخْرِجْ لَنَا مِمَّا تُنبِتُ الْأَرْضُ مِن بَقْلِهَا وَقِثَّائِهَا وَفُومِهَا وَعَدَسِهَا وَبَصَلِهَا ۖ قَالَ أَتَسْتَبْدِلُونَ الَّذِي هُوَ أَدْنَىٰ بِالَّذِي هُوَ خَيْرٌ ۚ اهْبِطُوا مِصْرًا فَإِنَّ لَكُم مَّا سَأَلْتُمْ ۗ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ وَالْمَسْكَنَةُ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٦١﴾

61. Na pindi mliposema: “Ee Muwsaa! Hatuwezi kusubiri kwa chakula cha aina moja tu, tuombee kwa Rabb wako Atutolee katika inavyoviotesha ardhi; kati ya mboga zake, matango yake, thomu (au ngano) yake, adesi zake na vitunguu vyake.” (Muwsaa) Akasema: “Je mnataka kubadilisha yaliyo duni kwa yaliyo bora? Shukeni mjini, hakika huko mtapata mnayoyauliza.” Na ikapigwa juu yao dhila na umaskini na wakastahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah, hayo ni kwa kuwa wao walikuwa wakikanusha Aayaat (ishara) za Allaah; na wakiwaua Manabii bila ya haki; hayo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالنَّصَارَىٰ وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٢﴾

62. Hakika wale walioamini, na wale ambao (kabla ya Uislamu) ni Mayahudi, na Manaswara na Masabai (waabudu nyota); yeyote atakayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na akatenda mema, basi watapata ujira wao kutoka kwa Rabb wao, na hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٦٣﴾

63. Na pindi Tulipochukua ahadi yenu na Tukaunyanyua juu yenu mlima (Tukasema): “Shikilieni Tuliyokupeni kwa nguvu na kumbukeni yaliyomo humo mpate kuwa na taqwa.”

 

 

ثُمَّ تَوَلَّيْتُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۖ فَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَكُنتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٦٤﴾

64. Kisha mkakengeuka baada ya hayo, na lau si fadhila za Allaah juu yenu na rahmah Yake mngekuwa miongoni mwa wenye kukhasirika.

 

 

وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ الَّذِينَ اعْتَدَوْا مِنكُمْ فِي السَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴿٦٥﴾

65. Na kwa yakini mlikwishawajua  wale miongoni mwenu waliotaadi mipaka ya As-Sabt Tukawaambia: “Kuweni manyani waliobezwa.”[7]

 

 

 

فَجَعَلْنَاهَا نَكَالًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهَا وَمَا خَلْفَهَا وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٦٦﴾

66. Tukaifanya kuwa ni adhabu ya kuonya kwa waliokuweko zama zao na wataokuja baada yao na ni mawaidha kwa wenye taqwa.

 

 

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا بَقَرَةً ۖ قَالُوا أَتَتَّخِذُنَا هُزُوًا ۖ قَالَ أَعُوذُ بِاللَّـهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٦٧﴾

67. Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu wake:  “Hakika Allaah Anakuamuruni mchinje ng’ombe.” Wakasema: “Unatufanyia mzaha?” Akasema: “Najikinga kwa Allaah kuwa  miongoni mwa wajinga.”

 

 

قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا فَارِضٌ وَلَا بِكْرٌ عَوَانٌ بَيْنَ ذَٰلِكَ ۖ فَافْعَلُوا مَا تُؤْمَرُونَ ﴿٦٨﴾

68. Wakasema: “Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo?” (Muwsaa) Akasema: “Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ng’ombe mwenyewe si mpevu wala si mchanga, bali ni wa katikati baina ya hao, basi fanyeni mnavyoamrishwa.”

 

 

قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا لَوْنُهَا ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ صَفْرَاءُ فَاقِعٌ لَّوْنُهَا تَسُرُّ النَّاظِرِينَ ﴿٦٩﴾

69. Wakasema: “Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie rangi yake?” (Muwsaa) Akasema: “Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe wa rangi ya njano iliyoiva mno, rangi yake huwapendeza wanaotazama.”

 

 

 قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ الْبَقَرَ تَشَابَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّا إِن شَاءَ اللَّـهُ لَمُهْتَدُونَ ﴿٧٠﴾

70. Wakasema: “Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo? Kwa hakika ng’ombe wametutatiza na hakika sisi In-Shaa-Allaah  tutakuwa wenye kuongoka.”

 

 

قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا ذَلُولٌ تُثِيرُ الْأَرْضَ وَلَا تَسْقِي الْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌ لَّا شِيَةَ فِيهَا ۚ قَالُوا الْآنَ جِئْتَ بِالْحَقِّ ۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧١﴾

71. (Muwsaa) Akasema: ”Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe ambaye hakutiishwa; kwa kulima ardhi wala kwa kumwagilia maji shamba; ni kamilifu hana dosari.” Wakasema: “Sasa umekuja na haki.” Basi wakamchinja na hawakuwa wenye kukaribia kufanya hivyo. 

 

 

وَإِذْ قَتَلْتُمْ نَفْسًا فَادَّارَأْتُمْ فِيهَا ۖ وَاللَّـهُ مُخْرِجٌ مَّا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٧٢﴾

72. Na pindi mlipoiua nafsi, kisha mkakhitilafiana kwayo, na Allaah ni Mwenye kutoa hayo mliyokuwa mkiyaficha.

 

 

فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا ۚ كَذَٰلِكَ يُحْيِي اللَّـهُ الْمَوْتَىٰ وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٧٣﴾

73. Tukasema: “Mpigeni (huyo maiti) kwa kipande chake (huyo ng’ombe).” Hivyo ndivyo Allaah Anavyohuisha wafu na Anakuonyesheni Aayaat (miujiza, dalili) Zake huenda mkatia akilini.

 

 

 ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً ۚ وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاءُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٧٤﴾

74. Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, zikawa kama mawe au ngumu zaidi. Na kwa hakika katika mawe kuna yanayobubujika humo mito. Na hakika katika hayo kuna yanayopasuka yakatoka humo maji. Na hakika katika hayo kuna mengine yanayoporomoka kutokana na khofu ya Allaah. Na Allaah si Mwenye kughafilika kuhusu myatendayo.

 

 

أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾

75. Je, mnatumai kwamba watakuaminini na hali lilikuwa kundi miongoni mwao linasikia maneno ya Allaah kisha linayageuza baada ya kuyaelewa na hali wanajua?

 

 

وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ قَالُوا أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَاجُّوكُم بِهِ عِندَ رَبِّكُمْ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٧٦﴾

76. Na wanapokutana na wale walioamini husema: “Tumeamini.” Na wanapokuwa peke yao; wao kwa wao; husema: “Hivi mnawasimulia yale Aliyokufungulieni Allaah ili wapate kukuhojini kwayo mbele ya Rabb wenu; hamtii akilini?”

 

 

 أَوَلَا يَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٧﴾

77. Je, hawajui kwamba Allaah Anajua wanayoyaficha na wanayoyatangaza?

 

 

وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴿٧٨﴾ 

78. Na miongoni mwao wako wasiojua kusoma wala kuandika; hawakijui Kitabu ila matamanio ya kuwaza tu, nao hawana ila kudhania tu.

 

 

فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ ﴿٧٩﴾

79. Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa mikono yao; kisha wakasema: ”Hiki ni kutoka kwa Allaah” ili wabadilishe kwa thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma.[8]

 

 

وَقَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَةً ۚ قُلْ أَتَّخَذْتُمْ عِندَ اللَّـهِ عَهْدًا فَلَن يُخْلِفَ اللَّـهُ عَهْدَهُ ۖ أَمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٨٠﴾

80. Na walisema: “Hautotugusa moto ila siku chache tu.” Sema: “Je, mmechukua ahadi kwa Allaah?” Basi Allaah Hakhalifu ahadi Yake, au mnasema kuhusu Allaah msiyoyajua?

 

 

بَلَىٰ مَن كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَاطَتْ بِهِ خَطِيئَتُهُ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨١﴾

81. Ndio! Yeyote aliyechuma uovu na yakamzunguka kwayo makosa yake; basi hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨٢﴾

82. Na wale walioamini na wakatenda mema; hao ni watu wa Jannah, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنكُمْ وَأَنتُم مُّعْرِضُونَ ﴿٨٣﴾ 

83. Na pindi Tulipochukua fungamano ya wana wa Israaiyl (Tukawaambia): “Msiabudu isipokuwa Allaah; na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini; na semeni na watu kwa uzuri na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah;” kisha mkakengeuka ila wachache miongoni mwenu na hali nyinyi mnapuuza.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ لَا تَسْفِكُونَ دِمَاءَكُمْ وَلَا تُخْرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَارِكُمْ ثُمَّ أَقْرَرْتُمْ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ ﴿٨٤﴾

84. Na pindi Tulipochukua fungamano lenu (Tukawaambia): “Msimwage damu zenu, wala msitoe nafsi zenu kutoka miji yenu;” kisha mkakubali nanyi mnashuhudia.

 

 

ثُمَّ أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ تَقْتُلُونَ أَنفُسَكُمْ وَتُخْرِجُونَ فَرِيقًا مِّنكُم مِّن دِيَارِهِمْ تَظَاهَرُونَ عَلَيْهِم بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَإِن يَأْتُوكُمْ أُسَارَىٰ تُفَادُوهُمْ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيْكُمْ إِخْرَاجُهُمْ ۚ أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ ۚ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰ أَشَدِّ الْعَذَابِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٨٥﴾

85. Kisha nyinyi ndio hao mnaua nafsi zenu na mnalitoa kundi miongoni mwenu kutoka majumbani mwao mnasaidiana dhidi yao kwa dhambi na uadui; na wanapokujieni mateka mnawakomboa na hali hilo limeharamishwa kwenu kuwatoa. Je, mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakanusha baadhi yake? Basi hapana jazaa ya anayefanya hayo miongoni mwenu isipokuwa hizaya katika dunia, na Siku ya Qiyaamah watapelekwa kwenye adhabu kali zaidi, na Allaah si Mwenye kughafilika kuhusu myatendayo.

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ ۖ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٨٦﴾

86. Hao ndio wale waliobadilisha uhai wa dunia badala ya Aakhirah, basi haitopunguzwa kwao adhabu wala hawatonusuriwa.

 

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ ۖ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ ﴿٨٧﴾

87. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu na Tukafuatisha Rusuli baada yake. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام. Je, basi kila anapokujieni Rasuli kwa yale yasiyoyapenda nafsi zenu, mlitakabari; hivyo kundi mlilikadhibisha na kundi mnaliua.[9]

 

 

وَقَالُوا قُلُوبُنَا غُلْفٌ ۚ بَل لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَقَلِيلًا مَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾

88. Na wakasema: “Nyoyo zetu zimefunikwa.” Bali Allaah Amewalaani kwa kufuru zao; basi machache tu wanayoyaamini.

 

 

وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُم مَّا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ ۚ فَلَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾

89. Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao, na japokuwa kabla ya hapo walikuwa wakiomba ushindi dhidi ya wale waliokufuru; basi yalipowajia yale waliyokuwa wakiyatambua waliyakanusha, basi laana ya Allaah iwe juu ya makafiri.[10]

 

 

بِئْسَمَا اشْتَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ أَن يَكْفُرُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ بَغْيًا أَن يُنَزِّلَ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ فَبَاءُوا بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٍ ۚ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٩٠﴾

90. Ubaya ulioje walichojibadilishia nafsi zao, kwamba wakufuru yale Aliyoyateremsha Allaah wakichukizwa na uhasidi kwa kuwa Allaah Kateremsha katika fadhila Zake juu ya Amtakae katika waja Wake. Basi wakarudi kwa kustahiki ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata adhabu ya kudhalilisha.

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا نُؤْمِنُ بِمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَيَكْفُرُونَ بِمَا وَرَاءَهُ وَهُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَهُمْ ۗ قُلْ فَلِمَ تَقْتُلُونَ أَنبِيَاءَ اللَّـهِ مِن قَبْلُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩١﴾

91. Na wanapoambiwa: “Aminini yale Aliyoyateremsha Allaah”, husema: “Tunaamini yale yaliyoteremshwa kwetu” na wanayakanusha yale yaliyokuja baada yake, na hali ya kuwa hayo ni haki yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao. Sema: “Kwa nini basi mnawaua Manabii wa Allaah toka hapo kabla kama kweli mlikuwa waumini?

 

 

وَلَقَدْ جَاءَكُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٩٢﴾

92. Na kwa yakini alikujieni Muwsaa kwa hoja bayana kisha mkamwabudu ndama baada yake na hali ya kuwa nyinyi ni madhalimu.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاسْمَعُوا ۖ قَالُوا سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَأُشْرِبُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْعِجْلَ بِكُفْرِهِمْ ۚ قُلْ بِئْسَمَا يَأْمُرُكُم بِهِ إِيمَانُكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩٣﴾

93. Na Tulipochukua fungamano lenu na Tukaunyanyua juu yenu mlima; (Tukasema): “Shikilieni Tuliyokupeni kwa nguvu na sikilizeni.” Wakasema: ”Tumesikia na tumeasi.” Wakanyweshwa katika nyoyo zao (kumwabudu)  ndama kwa kufuru yao. Sema: “Ubaya ulioje inakuamrisheni kwayo imani yenu mkiwa ni waumini.”

 

 

 

قُلْ إِن كَانَتْ لَكُمُ الدَّارُ الْآخِرَةُ عِندَ اللَّـهِ خَالِصَةً مِّن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٤﴾

94. Sema: ”Ikiwa nyumba ya Aakhirah iliyoko kwa Allaah ni makhsusi kwenu pekee pasi na watu wengine; basi tamanini mauti mkiwa ni wakweli.

 

 

وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٩٥﴾

95. Na hawatoyatamani abadani kutokana na iliyoyatanguliza mikono yao. Na Allaah ni Mjuzi wa madhalimu.

 

 

 

وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَىٰ حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا ۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَن يُعَمَّرَ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿٩٦﴾

96. Na kwa yakini utawakuta wao (Mayahudi) ni watu wenye pupa mno kuliko yeyote juu ya uhai na kuliko wale walioshirikisha. Anapenda mmoja wao lau angelipewa umri mrefu wa miaka elfu. Na wala huko hakutamuondoshea adhabu kwa kupewa umri mrefu. Na Allaah ni Mwenye kuona wanayoyatenda. 

 

 

قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٩٧﴾

97. Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) kwa idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na mwongozo na bishara kwa Waumini.[11]

 

 مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ ﴿٩٨﴾

98. Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rusuli Wake, na Jibriyl, na Miykaala, basi hakika Allaah ni adui kwa makafiri.

 

 

وَلَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ وَمَا يَكْفُرُ بِهَا إِلَّا الْفَاسِقُونَ ﴿٩٩﴾

99. Na kwa yakini Tumeteremsha kwako Aayaat bayana, na hawazikanushi isipokuwa mafasiki.

 

 

أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْدًا نَّبَذَهُ فَرِيقٌ مِّنْهُم ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Je, ndio kila wanapochukua ahadi kundi miongoni mwao huivunja? Bali wengi wao hawaamini.

 

 

 

وَلَمَّا جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ نَبَذَ فَرِيقٌ مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ كِتَابَ اللَّـهِ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ كَأَنَّهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٠١﴾ 

101. Na alipowajia Rasuli kutoka kwa Allaah mwenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao kundi miongoni mwa wale waliopewa Kitabu walikitupa Kitabu cha Allaah nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui.

 

 

 

وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٢﴾

102. Na wakafuata yale waliyoyasoma mashaytwaan juu ya ufalme wa Sulaymaan; na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili katika (mji wa) Baabil; Haaruwt na Maaruwt. Nao wawili hawamfundishi yeyote mpaka waseme: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru.” Kisha wakajifunza kutoka kwa hao wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao hawawezi kamwe kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah; na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi; na kwa yakini walijua kwamba atakayechuma haya hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni ubaya ulioje walichojiuzia nafsi zao, lau wangelikuwa wanajua.

 

 

وَلَوْ أَنَّهُمْ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَمَثُوبَةٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ خَيْرٌ ۖ لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٣﴾

103. Na lau wangeliamini na wakawa na taqwa, basi malipo kutoka kwa Allaah yangekuwa ni khayr lau wangekuwa wanajua.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا وَقُولُوا انظُرْنَا وَاسْمَعُوا ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٠٤﴾

104. Enyi walioamini! Msiseme (kumwambia Nabiy)raa’inaa” lakini semeni “undhwurnaa” na sikilizeni. Na makafiri watapata adhabu iumizayo.

 

 

مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿١٠٥﴾

105. Hawapendi wale waliokufuru miongoni mwa Ahlil-Kitaab, wala washirikina kwamba iteremshwe kwenu khayr yoyote ile kutoka kwa Rabb wenu. Na Allaah Humkhusisha kwa rahmah Yake Amtakaye. Na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.

 

 

مَا نَنسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِّنْهَا أَوْ مِثْلِهَا ۗ أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٦﴾

106. Hatufuti Aayah yoyote au Tunayoisahaulisha ila Tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au mfano wake. Je, hujui kwamba Allaah juu ya kila kitu ni Muweza?

 

 

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٠٧﴾

107. Je, hujui kwamba Allaah Ana ufalme wa mbingu na ardhi. Nanyi hamna pasi na Allaah mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.

 

 

أَمْ تُرِيدُونَ أَن تَسْأَلُوا رَسُولَكُمْ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۗ وَمَن يَتَبَدَّلِ الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿١٠٨﴾

108. Au mnataka kumuuliza Rasuli wenu kama alivyoulizwa Muwsaa hapo kabla? Na yeyote atakayebadilisha iymaan kwa kufru, basi kwa yakini amepotea njia iliyo sawa.

 

 

وَدَّ كَثِيرٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُم مِّن بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِّنْ عِندِ أَنفُسِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْحَقُّ ۖ فَاعْفُوا وَاصْفَحُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٩﴾

109. Wengi katika Ahlil-Kitaab wametamani kama wangelikurudisheni baada ya kuamini kwenu mkawa makafiri kwa husuda iliyomo katika nafsi zao; baada ya kuwabainikia kwao haki. Basi sameheni na puuzeni; mpaka Allaah Alete amri Yake. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.[12]

 

 

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١١٠﴾

110. Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah, na lolote mnalolitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu katika khayr mtalikuta kwa Allaah, hakika Allaah kwa yale myafanyao ni Mwenye kuona.

 

 

وَقَالُوا لَن يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ تِلْكَ أَمَانِيُّهُمْ ۗ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١١١﴾

111. Na walisema: “Hatoingia Jannah isipokuwa aliyekuwa Yahudi au Naswaara.” Hilo ni tamanio lao.  Sema: “Leteni ushahidi wenu wa wazi mkiwa ni wakweli.”

 

 

بَلَىٰ مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُ أَجْرُهُ عِندَ رَبِّهِ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١١٢﴾

112. Ndio! Bali yeyote aliyeusalimisha uso wake kwa Allaah, na ilhali yeye ni mwenye kufanya ihsaan basi atapata ujira wake kwa Rabb wake, na wala haitokuwa khofu juu yao wala hawatohuzunika.

 

 

وَقَالَتِ الْيَهُودُ لَيْسَتِ النَّصَارَىٰ عَلَىٰ شَيْءٍ وَقَالَتِ النَّصَارَىٰ لَيْسَتِ الْيَهُودُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُمْ يَتْلُونَ الْكِتَابَ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ مِثْلَ قَوْلِهِمْ ۚ فَاللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿١١٣﴾

113. Na Mayahudi wakasema: “Manaswara hawana lao jambo.” Na Manaswara wakasema: “Mayahudi hawana lao jambo,” na hali wao wanasoma Kitabu. Hivyo hivyo ndivyo walivyosema wale ambao hawajui mfano wa kauli yao. Basi Allaah Atawahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wakikhitilafiana.

 

 

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّـهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١١٤﴾

114. Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayezuia Misikiti ya Allaah kutajwa ndani yake Jina Lake na akajitahidi katika kuiharibu? Hao haitokuwa kuingia kwako humo isipokuwa wakiwa ni wenye khofu; watapata duniani hizaya na Aakhirah watapata adhabu kuu.

 

 

وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿١١٥﴾

115. Na Mashariki na Magharibi ni ya Allaah; basi popote mnapogeuka kuna Wajihi wa Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.[13]

 

 

وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾

116. Na wakasema: “Allaah Amejichukulia mwana.” Utakasifu ni Wake. Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii.

 

 

 بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿١١٧﴾

117. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Anapokidhia jambo basi huliambia “Kun!” Basi nalo huwa.

 

 

وَقَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ لَوْلَا يُكَلِّمُنَا اللَّـهُ أَوْ تَأْتِينَا آيَةٌ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّثْلَ قَوْلِهِمْ ۘ تَشَابَهَتْ قُلُوبُهُمْ ۗ قَدْ بَيَّنَّا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿١١٨﴾ 

118. Na wakasema wale ambao hawajui: “Lau Angetusemesha Allaah au ingetujia Aayah (muujiza);” kadhalika walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hiyo. Zimeshabihiana nyoyo zao. Kwa yakini Tumekwishabainisha Aayaat (ishara, dalili) kwa watu wenye yakini. 

 

 

 إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا ۖ وَلَا تُسْأَلُ عَنْ أَصْحَابِ الْجَحِيمِ ﴿١١٩﴾

119. Hakika Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki ukiwa mwenye kutoa bishara njema na mwonyaji wala hutoulizwa kuhusu watu wa moto uwakao vikali.

 

 

وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٢٠﴾

120. Na hawatoridhika nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila zao. Sema: “Hakika mwongozo wa Allaah ndio mwongozo (pekee).” Na ukifuata hawaa zao baada ya yale ambayo yaliyokujia katika elimu, basi hutopata kutoka kwa Allaah mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.

 

 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٢١﴾

121. Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ipasavyo ya kusomwa kwake; hao ndio wanaokiamini, na atakayekikanusha basi hao ndio waliokhasirika.

 

 

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿١٢٢﴾

122. Enyi wana wa Israaiyl, kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya walimwengu.

 

 

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا تَنفَعُهَا شَفَاعَةٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿١٢٣﴾

123. Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitoifaa nafsi nyingine kwa lolote, wala haitokubaliwa kutoka kwake kikomboleo wala hautomfaa uombezi wowote wala hawatonusuriwa.

 

 وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ ۖ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾

124. Na pindi Alipojaribiwa Ibraahiym na Rabb wake kwa amri nyingi, naye akazitimiza. Akasema: “Hakika Mimi Nakufanya uwe Imaam kwa watu.” (Ibraahiym) Akasema: “Na katika kizazi changu?” (Allaah) Akasema: “Haiwafikii ahadi Yangu madhalimu.”

 

 

وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿١٢٥﴾ 

125. Na Tulipoifanya Nyumba (Al-Ka’bah) kuwa ni mahali pa kurejewa na watu na pa amani, na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia. Na Tulichukua ahadi kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl kwamba: “Itakaseni Nyumba Yangu kwa wanaotufu na wanaokaa i’tikaaf, na wanaorukuu na kusujudu.”[14]

 

 

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُقْ أَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُم بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُ قَلِيلًا ثُمَّ أَضْطَرُّهُ إِلَىٰ عَذَابِ النَّارِ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٢٦﴾

126. Na pindi aliposema Ibraahiym: “Rabb wangu Ufanye mji huu (Makkah) kuwa wa amani na Waruzuku watu wake katika matunda atakayemwamini Allaah miongoni mwao na Siku ya Mwisho.” (Allaah) Akasema: “Na atakayekufuru Nitamstarehesha kidogo kisha Nitamsukumiza katika adhabu ya moto, na ubaya ulioje mahali pa kuishia.”

 

 

وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٢٧﴾

127. Na aliponyanyua Ibraahiym na Ismaa’iyl msingi wa Nyumba (Al-Ka’bah): “Rabb wetu, Tutakabalie, hakika Wewe ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

 رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٢٨﴾

128. “Rabb wetu, Tujaalie tuwe wenye kujisalimisha Kwako pamoja na kizazi chetu wawe ummah wenye kujisalimisha Kwako na Tuonyeshe taratibu za ‘ibaadah zetu na Pokea tawbah zetu, hakika Wewe ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu. 

 

 

رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٢٩﴾

129. “Rabb wetu, wapelekee Rasuli miongoni mwao atakayewasomea Aayaat Zako na atakayewafunza Kitabu na Hikmah na atakayewatakasa. Hakika Wewe ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.”

 

 

وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُ ۚ وَلَقَدِ اصْطَفَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٣٠﴾

130. Na ni nani atakayejitenga na mila ya Ibraahiym isipokuwa anayeitia nafsi yake upumbavu? Na kwa yakini Tumemkhitari duniani, naye Aakhirah ni miongoni mwa Swalihina.

 

 

إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ ۖ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٣١﴾

131. Rabb wake Alipomwambia: “Jisalimishe na utii” (Ibraahiym) Akasema: “Nimejisalimisha na kutii kwa Rabb wa walimwengu.”

 

 

وَوَصَّىٰ بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَا بَنِيَّ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٣٢﴾

132. Na Ibraahiym akawausia hayo wanawe na (kadhalika) Ya’quwb (akawaambia): “Enyi wanangu! Hakika Allaah Amekukhitarini nyinyi Dini; basi msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.”

 

 

 أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِن بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٣﴾

133. Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfikia Ya’quwb alipowaambia wanawe: “Mtaabudu nini baada yangu?” Wakasema: “Tutamwabudu Ilaaha wako (Allaah) na Ilaaha wa baba zako, Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq; Ilaah Mmoja, nasi ni Waislamu (tunajisalimisha) Kwake.”

 

 

تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٤﴾

134. Huo ni ummah kwa yakini umeshapita, utapata uliyoyachuma nanyi mtapata mliyoyachuma; na wala hamtoulizwa kuhusu waliyokuwa wakitenda.

 

 

 وَقَالُوا كُونُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ تَهْتَدُوا ۗ قُلْ بَلْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٣٥﴾

135. Na wakasema: “Kuweni Mayahudi au Manaswara mtaongoka.” Sema:  “Bali (tunafuata) mila ya Ibraahiym aliyeelemea haki na wala hakuwa katika washirikina.”

 

 

قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٦﴾

136. Semeni: “Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw na aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Rabb wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni nasi ni Waislamu (tunajisalimisha) Kwake. [15]

 

 

فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنتُم بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ ۖ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣٧﴾

137. Watakapoamini kama vile mlivyoamini nyinyi, basi kwa yakini watakuwa wameongoka; na wakikengeuka basi hakika wao wamo katika upinzani, na Allaah Atakutosheleza nao, Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

صِبْغَةَ اللَّـهِ ۖ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ صِبْغَةً ۖ وَنَحْنُ لَهُ عَابِدُونَ ﴿١٣٨﴾

138. (Dini yetu ni) Dini ya Allaah na dini gani yaweza kuwa bora zaidi kuliko Dini ya Allaah? Na sisi ni wenye kumwabudu Yeye Pekee.

 

 

قُلْ أَتُحَاجُّونَنَا فِي اللَّـهِ وَهُوَ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ وَلَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُخْلِصُونَ ﴿١٣٩﴾

139. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Je, mnahojiana nasi kuhusu Allaah na hali Yeye ni Rabb wetu na Rabb wenu; nasi tuna ‘amali zetu nanyi mna ‘amali zenu, na sisi Kwake ni wenye ikhlasi.“

 

 

أَمْ تَقُولُونَ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطَ كَانُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ قُلْ أَأَنتُمْ أَعْلَمُ أَمِ اللَّـهُ ۗ وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَتَمَ شَهَادَةً عِندَهُ مِنَ اللَّـهِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٤٠﴾

140. Je, mnasema kwamba Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw (dhuriya) walikuwa Mayahudi au Manaswara? Sema: “Je, nyinyi mnajua zaidi au Allaah?” Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi alionao kutoka kwa Allaah? Na Allaah si Mwenye kughafilika kuhusu myatendayo.

 

 

تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٤١﴾

141. Huo ni ummah kwa yakini umeshapita, utapata uliyoyachuma nanyi mtapata  mliyoyachuma, na wala hamtoulizwa waliyokuwa wakitenda.

 

 

سَيَقُولُ السُّفَهَاءُ مِنَ النَّاسِ مَا وَلَّاهُمْ عَن قِبْلَتِهِمُ الَّتِي كَانُوا عَلَيْهَا ۚ قُل لِّلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٤٢﴾

142. Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: “Nini kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea!” Sema: “Mashariki na Magharibi ni ya Allaah, Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.”[16]

 

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ ۚ وَإِن كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٣﴾

143. Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. Na Hatukukifanya Qiblah ambacho ulikuwa ukikielekea (Baytul-Maqdis) isipokuwa Tupate kumpambanulisha yule anayemfuata Rasuli miongoni mwa mwenye kugeuka akarudi nyuma. Na hakika ilikuwa ni jambo gumu isipokuwa kwa wale ambao Allaah Amewaongoza. Na Allaah Hakuwa Mwenye kupoteza iymaan yenu (Swalaah), hakika Allaah kwa watu, bila shaka ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.[17]

 

 

قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ ۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا ۚ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٤﴾

144. Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. Na popote mtakapokuwepo (mkataka kuswali), basi elekezeni nyuso zenu upande wake. Na hakika wale waliopewa Kitabu bila shaka wanajua kwamba hivyo ni haki kutoka kwa Rabb wao. Na Allaah si Mwenye kughafilika kuhusu wayatendayo.[18]

 

 

وَلَئِنْ أَتَيْتَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ بِكُلِّ آيَةٍ مَّا تَبِعُوا قِبْلَتَكَ ۚ وَمَا أَنتَ بِتَابِعٍ قِبْلَتَهُمْ ۚ وَمَا بَعْضُهُم بِتَابِعٍ قِبْلَةَ بَعْضٍ ۚ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ إِنَّكَ إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٥﴾

145. Na hata ukiwaletea wale waliopewa Kitabu kila Aayah (ishara, ushahidi) basi hawatofuata Qiblah chako. Na wewe hutofuata Qiblah chao. Na wala baadhi yao hawatofuata Qiblah cha wengineo. Na kama ukiyafuata matamanio yao baada ya kukufikia elimu; hakika hapo utakuwa miongoni mwa madhalimu.

 

 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ ۖ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنْهُمْ لَيَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٤٦﴾ 

146. Wale Tuliowapa Kitabu wanamtambua (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama wanavyotambua watoto wao; na hakika kundi miongoni mwao wanaficha haki na hali wao wanajua.

 

 

الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿١٤٧﴾

147. Haki kutoka kwa Rabb wako basi kamwe usiwe miongoni mwa wenye shaka.

 

 

وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ أَيْنَ مَا تَكُونُوا يَأْتِ بِكُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٤٨﴾

148. Na kila mmoja ana upande wa kuuelekea. Basi shindaneni kwenye mambo ya khayr. Popote mtakapokuwa Allaah Atakuleteni nyote pamoja (Qiyaamah). Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 

وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۖ وَإِنَّهُ لَلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٤٩﴾ 

149. Na popote utokako (ili kuswali) basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. Na hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wako. Na Allaah si Mwenye kughafilika kuhusu myatendayo.

 

 

وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيْكُمْ حُجَّةٌ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي وَلِأُتِمَّ نِعْمَتِي عَلَيْكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٥٠﴾

150. Na popote utokako (ili kuswali) basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. Na popote mtakapokuwa basi elekezeni nyuso zenu upande wake, ili watu wasiwe na hoja juu yenu isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope bali Niogopeni na ili Nitimize neema Yangu juu yenu na ili mpate mwongoke.

 

 

كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿١٥١﴾

151. Kama Tulivyomtuma kwenu Rasuli anayetokana na nyinyi, anawasomea Aayaat Zetu na anakutakaseni na anakufunzeni Kitabu na Hikmah (Sunnah), na anakufundisheni mambo ambayo hamkuwa mkiyajua.

 

 

فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ﴿١٥٢﴾

152. Basi nidhukuruni na Mimi Nitakukumbukeni; na nishukuruni wala msinikufuru.

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٣﴾

153. Enyi walioamini! Tafuteni msaada kwa subira na Swalaah; hakika Allaah Yu pamoja na wanaosubiri.

 

 

وَلَا تَقُولُوا لِمَن يُقْتَلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتٌ ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ وَلَـٰكِن لَّا تَشْعُرُونَ ﴿١٥٤﴾ 

154. Wala msiseme kwa waliouawa katika njia ya Allaah kuwa ni wafu, bali wakohai lakini hamhisi.

 

 

وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾

155. Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri.

 

 

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿١٥٦﴾

156. Wale ambao unapowafika msiba husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.”

 

 

أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ﴿١٥٧﴾

157. Hao zitakuwa juu yao Barakah kutoka kwa Rabb wao na rahmah, na hao ndio wenye kuongoka.

 

 

إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٥٨﴾

158. Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika alama za Allaah. Basi yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah basi hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya khayr basi hakika Allaah ni Mwenye kupokea shukurani, Mjuzi wa yote.[19]

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ ﴿١٥٩﴾

159. Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja bayana na mwongozo baada ya kuwa Tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu, hao Anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.

 

 

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَبَيَّنُوا فَأُولَـٰئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٠﴾ 

160. Isipokuwa wale waliotubu na wakatengenea na wakabainisha (haki); basi hao Napokea tawbah zao, Na Mimi ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ لَعْنَةُ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿١٦١﴾

161. Hakika wale waliokufuru na wakafa hali ya kuwa ni makafiri; hao iko juu yao laana ya Allaah na Malaika na watu wote.

 

 

 خَالِدِينَ فِيهَا ۖ لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿١٦٢﴾

162. Wenye kudumu humo, hawatopunguziwa adhabu na wala wao hawatopewa muhula wa kupumzika.

 

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

163.  Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.

 

 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن مَّاءٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿١٦٤﴾

164. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na mabadiliko ya usiku na mchana na merikebu zipitazo katika bahari kwa vile viwafaavyo watu na Aliyoyateremsha Allaah kutoka mbinguni katika maji Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake na Akaeneza humo kila aina ya mnyama na mgeuko wa upepo na mawingu yanayotiishwa baina ya mbingu na ardhi ni Aayaat (dalili, zingatio) kwa watu wenye akili.

 

 

 وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ ﴿١٦٥﴾

165. Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. Na lau wangelitambua wale waliodhulumu watakapoona adhabu kwamba nguvu zote ni za Allaah; na kwamba hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu.

 

 

إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ﴿١٦٦﴾

166. Wale waliofuatwa watakapowakana wale waliowafuata wakiwa wameshaiona adhabu; na yatawakatikia mafungamano yao.

 

 

وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا ۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ اللَّـهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ ۖ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ ﴿١٦٧﴾

167. Na watasema wale waliofuata: “Lau tungelipata fursa ya kurudi (duniani) tungewakana kama walivyotukana.” Hivyo ndivyo Allaah Atakavyowaonyesha ‘amali zao kuwa ni majuto juu yao. Na wala hawatokuwa wenye kutoka motoni.

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٦٨﴾

168. Enyi watu! Kuleni katika vilivyomo ardhini vya halali, vizuri; na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.

 

 

إِنَّمَا يَأْمُرُكُم بِالسُّوءِ وَالْفَحْشَاءِ وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٦٩﴾ 

169. Hakika hakuna isipokuwa anakuamrisheni maovu na machafu (na ubakhili) na mseme dhidi ya Allaah msiyoyajua.

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۗ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٧٠﴾

170. Na wanapoambiwa: “Fuateni Aliyoyateremsha Allaah” Husema: “Bali tunafuata tuliyowakuta nayo baba zetu.” Je, japokuwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu chochote na wala hawakuongoka?

 

 

 وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٧١﴾

171. Na mfano wa wale waliokufuru ni kama mfano wa yule ambaye anapiga kelele kwa ambaye hasikii ila sauti na mwito. Viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawatii akilini.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ ﴿١٧٢﴾

172. Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni na mshukuruni Allaah mkiwa mnamwabudu Yeye Pekee.

 

 

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٧٣﴾

173. Hakika Allaah Amekuharamishieni mzoga na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Lakini aliyefikwa na dharura bila ya kutamani wala kupindukia mipaka; basi si dhambi juu yake. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ الْكِتَابِ وَيَشْتَرُونَ بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۙ أُولَـٰئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ إِلَّا النَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٤﴾

174. Hakika wale wanaoficha yale Aliyoyateremsha Allaah katika Kitabu na wakakibadilisha kwa thamani ndogo; hao hawali katika matumbo yao isipokuwa moto, na wala Allaah Hatowasemesha Siku ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa nao watapata adhabu iumizayo.

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ وَالْعَذَابَ بِالْمَغْفِرَةِ ۚ فَمَا أَصْبَرَهُمْ عَلَى النَّارِ ﴿١٧٥﴾

175. Hao ndio wale waliobadilisha upotofu badala ya uongofu na adhabu kwa maghfirah. Basi kuvumilia gani huko kwao ndani ya moto?

 

 

 ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ نَزَّلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِي الْكِتَابِ لَفِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ ﴿١٧٦﴾

176. Hayo ni kwa sababu Allaah Amekiteremsha Kitabu kwa haki. Na hakika wale waliokhitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani wa mbali.

 

 

لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا ۖ وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ ﴿١٧٧﴾ 

177. Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi lakini wema ni mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na akawapa mali juu ya kuipenda kwake jamaa wa karibu na mayatima na masikini na msafiri na waombao na katika kukomboa watumwa na akasimamisha Swalaah, na akatoa Zakaah na watimizao ahadi zao wanapoahidi, na wanaosubiri katika dhiki za ufukara na maafa ya magonjwa na njaa na katika vita. Hao ndio waliosadikisha na hao ndio wenye taqwa.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى ۖ الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالْأُنثَىٰ بِالْأُنثَىٰ ۚ فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ ۗ ذَٰلِكَ تَخْفِيفٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَرَحْمَةٌ ۗ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٨﴾

178. Enyi walioamini! Mmeandikiwa shariy’ah ya kisasi kwa waliouawa; Muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke, na anayesamehewa na nduguye kwa lolote basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema na kumlipa kwake iwe kwa ihsaan. Hiyo ni takhafifu kutoka kwa Rabb wenu na rahmah. Na atakayevuka mipaka baada ya hapo basi atapata adhabu iumizayo.

 

 

وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٧٩﴾

179. Na mtapata katika kisasi (kuokoa) uhai enyi wenye akili ili mpate kuwa na taqwa.

 

 

كُتِبَ عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ إِن تَرَكَ خَيْرًا الْوَصِيَّةُ لِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ ﴿١٨٠﴾

180. Mmeandikiwa shariy’ah kuwa anapofikiwa mmoja wenu na mauti kama ameacha mali, kufanya wasia kwa wazazi wawili, na jamaa wa karibu kwa namna inayoeleweka katika shariy’ah. Wajibu kwa wenye taqwa.[20]

 

 

فَمَن بَدَّلَهُ بَعْدَ مَا سَمِعَهُ فَإِنَّمَا إِثْمُهُ عَلَى الَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٨١﴾ 

181. Atakayeubadilisha (wasia) baada ya kuusikia; basi hakika dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha. Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

فَمَنْ خَافَ مِن مُّوصٍ جَنَفًا أَوْ إِثْمًا فَأَصْلَحَ بَيْنَهُمْ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٨٢﴾

182. Basi mwenye kukhofu kwamba muusiaji kenda kombo bila kukusudia au kakusudia dhambi kisha akasuluhisha baina yao; basi haitokuwa dhambi juu yake. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾

183. Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa.

 

أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ ۚ وَأَن تَصُومُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٨٤﴾

184. (Swiyaam ni) Siku za kuhesabika. Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini, basi akamilishe idadi katika masiku mengineyo. Na kwa wale wanaoiweza lakini kwa mashaka watoe fidia; kulisha masikini. Na atakayefanya kwa khiari yake jema lolote, basi hilo ni bora kwake. Na mkifunga Swiyaam ni bora kwenu mkiwa mnajua.

 

 

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٨٥﴾

185. Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na Furqaan (upambanuo). Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi atimize idadi katika siku nyinginezo. Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu; na ili mkamilishe idadi na ili mumkabbir Allaah kwa kuwa Amekuongozeni na ili mpate kushukuru.

 

 

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾

186. Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka.

 

 

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٨٧﴾

187. Mmehalalishiwa usiku wa kufunga Swiyaam kujamiiana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Allaah Anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkijifanyia khiyana nafsi zenu, hivyo Akapokea tawbah yenu na Akakusameheni. Basi sasa waingilieni na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). Kisha timizeni Swiyaam mpaka usiku. Na wala msiwaingilie hali ya kuwa nyinyi wenye kukaa i’tikaaf Misikitini. Hiyo ni mipaka ya Allaah basi msiikaribie. Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (na hukmu) Zake kwa watu wapate kuwa na taqwa.[21]

 

 

 وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا فَرِيقًا مِّنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٨٨﴾

188. Na wala msiliane mali zenu kwa ubatilifu na mkazipeleka (rushwa) kwa mahakimu ili mle sehemu katika mali ya watu kwa dhambi na hali mnajua.

 

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَن تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٨٩﴾

189. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu miandamo ya mwezi. Sema: “Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa watu na Hajj.” Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake, lakini wema ni kuwa na taqwa. Na ingieni majumbani kupitia milango yake. Na mcheni Allaah mpate kufaulu.[22]

 

 

وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿١٩٠﴾

190. Na piganeni katika njia ya Allaah na wale wanaokupigeni, wala msitaadi. Hakika Allaah Hapendi wenye kutaadi.

 

 

وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ ۚ وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ ۖ فَإِن قَاتَلُوكُمْ فَاقْتُلُوهُمْ ۗ كَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ ﴿١٩١﴾

191. Na wauweni popote muwakutapo, na watoeni popote walipokutoeni. Na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na wala msipigane nao kwenye Al-Masjidil-Haraam mpaka wakupigeni humo, watakapokupigeni basi wauweni. Namna hivi ndivyo jazaa ya makafiri.

 

 

فَإِنِ انتَهَوْا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٢﴾ 

192. Wakikoma, basi Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّـهِ ۖ فَإِنِ انتَهَوْا فَلَا عُدْوَانَ إِلَّا عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿١٩٣﴾

193. Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah (shirki, kufru); na Dini iwe kwa ajili ya Allaah Pekee, wakikoma basi kusiweko na uadui ila kwa madhalimu.

 

 

الشَّهْرُ الْحَرَامُ بِالشَّهْرِ الْحَرَامِ وَالْحُرُمَاتُ قِصَاصٌ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ ﴿١٩٤﴾

194. Mwezi mtukufu kwa mwezi mtukufu na vitukufu vimewekewa kisasi. Basi anayekushambulieni nanyi mshambulieni kwa kadiri ya alivyokushambulieni. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.

 

 

  وَأَنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٩٥﴾

195. Na toeni katika njia ya Allaah wala msijitupe katika maangamizi kwa (kuzuia) mikono yenu isitoe. Na fanyeni ihsaan Hakika Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.[23]

 

 

 

وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ ۚ فَإِنْ أُحْصِرْتُمْ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۖ وَلَا تَحْلِقُوا رُءُوسَكُمْ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِّن رَّأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِّن صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ ۚ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَمَن تَمَتَّعَ بِالْعُمْرَةِ إِلَى الْحَجِّ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۚ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ فِي الْحَجِّ وَسَبْعَةٍ إِذَا رَجَعْتُمْ ۗ تِلْكَ عَشَرَةٌ كَامِلَةٌ ۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمْ يَكُنْ أَهْلُهُ حَاضِرِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١٩٦﴾

196. Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah.  Na kama mkizuilika basi chinjeni wanyama walio wepesi kupatikana. Na wala msinyoe vichwa vyenu mpaka mnyama afikie machinjoni pake. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake (ikambidi anyoe); basi atoe fidia kwa kufunga Swiyaam au kutoa swadaqah au kuchinja mnyama. Na mtakapopata amani, basi mwenye kujistarehesha kwa kutekeleza ‘Umrah kwanza kisha Hajj, achinje mnyama aliye mwepesi. Na asiyepata afunge Swiyaam siku tatu katika Hajj na saba mtakaporejea. Hizo ni kumi kamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawaishi karibu na Al-Masjidil-Haraam. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Allaah ni Mkali wa kuakibu.[24]

 

 

 الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٧﴾

197. Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji (akahirimia), basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote mlifanyalo katika ya khayr Allaah Analijua. Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili![25]

 

 

لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ ۚ فَإِذَا أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ عِندَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ ۖ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّينَ ﴿١٩٨﴾ 

198. Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wenu. Basi mtakapomiminika kutoka ‘Arafaat mdhukuruni Allaah kwenye Mash’aril-Haraam (Muzdalifah) na mdhukuruni Yeye kama Alivyokuongozeni kwani hakika mlikuwa kabla ya hapo ni miongoni mwa waliopotea.[26]

 

 

 ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٩﴾

199. Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu; na ombeni maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.[27]

 

 

فَإِذَا قَضَيْتُم مَّنَاسِكَكُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَذِكْرِكُمْ آبَاءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا ۗ فَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ﴿٢٠٠﴾

200. Mtakapomaliza kutekeleza ‘ibaadah zenu za Hajj, basi mdhukuruni Allaah kama mnavyowadhukuru baba zenu au kumdhukuru zaidi. Kwani kuna baadhi ya watu wasemao: “Rabb wetu Tupe katika dunia;” naye katika Aakhirah hana sehemu yoyote.

 

 

  وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿٢٠١﴾

201. Na miongoni mwao kuna wasemao: “Rabb wetu Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na Tukinge na adhabu ya moto.”

 

 

 أُولَـٰئِكَ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّمَّا كَسَبُوا ۚ وَاللَّـهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٢٠٢﴾

202. Hao watapata pato lao kutokana na waliyoyachuma, na Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.

 

 

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٢٠٣﴾

203. Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika. Atakayeharakisha kuondoka katika siku mbili, basi hakuna dhambi juu yake; na atakayetaakhari basi hakuna dhambi juu yake; kwa mwenye kuwa na taqwa. Na mcheni Allaah na jueni kwamba Kwake mtakusanywa.

 

 

 وَمِنَ النَّاسِ مَن يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللَّـهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ ﴿٢٠٤﴾

204. Na miongoni mwa watu yupo anayekuvutia kauli yake katika uhai wa dunia na humshuhudisha Allaah kwa yale yaliyomo katika moyo wake na hali yeye ndiye khasimu mbaya zaidi.

 

 

وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ ﴿٢٠٥﴾ 

205. Na anapoondoka hufanya bidii katika ardhi ili afisidi humo na aangamize mimea na vizazi.  Na Allaah Hapendi ufisadi.

 

 

 وَإِذَا قِيلَ لَهُ اتَّقِ اللَّـهَ أَخَذَتْهُ الْعِزَّةُ بِالْإِثْمِ ۚ فَحَسْبُهُ جَهَنَّمُ ۚ وَلَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿٢٠٦﴾

206. Na anapoambiwa: “Mche Allaah!” Hupandwa kiburi kinachompeleka kutenda madhambi. Basi Jahannam inamtosheleza na mahali pabaya palioje pa kupumzikia.

 

 

  وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠٧﴾

207. Na miongoni mwa watu yupo anayeiuza nafsi yake kutafuta radhi za Allaah. Na Allaah ni Mwenye huruma mno kwa waja.[28]

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٠٨﴾

208. Enyi walioamini! Ingieni katika Uislamu kikamilifu, na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.

 

 

فَإِن زَلَلْتُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْكُمُ الْبَيِّنَاتُ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٠٩﴾

209. Lakini mkiteleza baada ya kukujieni hoja bayana, jueni kwamba hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٢١٠﴾

210. Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah Awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika, na limehukumiwa jambo. Na kwa Allaah ndipo hurudishwa mambo.

 

 

 سَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَمْ آتَيْنَاهُم مِّنْ آيَةٍ بَيِّنَةٍ ۗ وَمَن يُبَدِّلْ نِعْمَةَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢١١﴾

211. Waulize wana wa Israaiyl, Aayah (miujiza, ishara) ngapi Tumewapa zilizo bayana? Na atakayebadilisha neema ya Allaah (kwa kufru) baada ya kumjia, basi hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu.

 

 

زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا ۘ وَالَّذِينَ اتَّقَوْا فَوْقَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَاللَّـهُ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢١٢﴾

212. Wamepambiwa wale waliokufuru uhai wa dunia na wanawakejeli wale walioamini. Na wale walio na taqwa watakuwa juu yao Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Humruzuku Amtakaye bila ya hesabu.

 

 

 كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۖ فَهَدَى اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ ۗ وَاللَّـهُ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢١٣﴾

213. Watu walikuwa ummah mmoja kisha Allaah Akatuma Nabiy wabashiriaji na waonyaji na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu baina ya watu katika ambayo wamekhitilafiana kwayo. Na hawakukhitilafiana katika hayo isipokuwa wale waliopewa hicho (Kitabu) baada ya kuwajia hoja bayana kwa kufanyiana baghi na uhusuda baina yao. Allaah Akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa idhini Yake. Na Allaah Humwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.

 

 

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّـهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّـهِ قَرِيبٌ ﴿٢١٤﴾

214. Je, mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali bado haijakufikieni (mitihani) kama ya wale waliopita kabla yenu? Iliwagusa dhiki za umasikini na maafa ya magonjwa na njaa na wakatetemeshwa mpaka Rasuli na wale walioamini pamoja naye wanasema: “Lini itafika nusura ya Allaah?” Tanabahi! Hakika nusura ya Allaah iko karibu.

 

 

يَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ ۖ قُلْ مَا أَنفَقْتُم مِّنْ خَيْرٍ فَلِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢١٥﴾

215. Wanakuuliza nini watoe?  Sema: “Mnachotoa chochote katika khayr basi ni kwa ajili ya wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini, na msafiri.”  Na lolote mlifanyalo katika khayr basi hakika Allaah kwa hilo ni Mjuzi.

 

 

 كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢١٦﴾

216. Mmeandikiwa shariy’ah kupigana vita nako kunachukiza mno kwenu. Na asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni khayr kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.

 

 

 يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ ۖ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ ۖ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَكُفْرٌ بِهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَإِخْرَاجُ أَهْلِهِ مِنْهُ أَكْبَرُ عِندَ اللَّـهِ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَكْبَرُ مِنَ الْقَتْلِ ۗ وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا ۚ وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢١٧﴾

217. Wanakuuliza kuhusu mwezi mtukufu kupigana humo. Sema: “Kupigana humo ni dhambi kubwa, lakini kuzuia njia ya Allaah na kumkufuru Yeye na (kuzuia) Al-Masjidil-Haraam na kuwatoa watu wake humo ni (dhambi) kubwa zaidi mbele ya Allaah. Na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua.” Na wala hawatoacha kukupigeni vita mpaka wakutoeni katika Dini yenu wakiweza. Na atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, akafariki hali ya kuwa ni kafiri, basi hao zimeporomoka ‘amali zao katika dunia na Aakhirah. Na hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢١٨﴾

218. Hakika wale walioamini na wale waliohajiri na wakapigana jihaad katika njia ya Allaah, hao wanataraji rahmah ya Allaah, na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾

219. Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.” Na wanakuuliza nini watoe. Sema: “Yaliyokuzidieni.” Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na shariy’ah) ili mpate kutafakari.[29]

 

 

 

 فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۗ وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ ۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَأَعْنَتَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٠﴾

220. Katika dunia na Aakhirah. Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengeneza ni khayr.  Na Allaah Anamjua fisadi na mtengenezaji. Na lau Angetaka Allaah Angelikutieni katika shida.” Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.[30]

 

 

 

 وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٢١﴾

221. Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Na wala msiwaozeshe (wanawake wa Kiislamu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Hao wanaitia katika moto na Allaah Anaitia katika Al-Jannah na maghfirah kwa idhini Yake. Na Anabainisha Aayaat (na shariy’ah) Zake ili wapate kukumbuka.

 

 

 وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ ﴿٢٢٢﴾ 

222. Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara; basi waepukeni wanawake katika hedhi. Wala msiwakaribie kujimai nao mpaka watwaharike. Watakapotwaharika basi waendeeni kupitia pale Alipokuamrisheni Allaah.”  Hakika Allaah Anapenda wenye kutubia na Anapenda wenye kujitwaharisha.[31]

 

 

 نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُم مُّلَاقُوهُ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٢٣﴾

223. Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. Na kadimisheni (mema) kwa ajili ya nafsi zenu. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika nyinyi ni wenye kukutana Naye. Na wabashirie Waumini.[32]

 

 

 وَلَا تَجْعَلُوا اللَّـهَ عُرْضَةً لِّأَيْمَانِكُمْ أَن تَبَرُّوا وَتَتَّقُوا وَتُصْلِحُوا بَيْنَ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٢٤﴾

224. Na wala msifanye (Jina la) Allaah kuwa ni nyudhuru ya viapo vyenu kukuzuieni katika kutenda wema na kuwa na taqwa na kusuluhisha baina ya watu. Na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٢٥﴾

225. Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi lakini Atakuchukulieni kwa yaliyochuma nyoyo zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mpole, Mvumilivu.[33]

 

 

 لِّلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِن نِّسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ ۖ فَإِن فَاءُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٢٦﴾

226. Kwa wale walioapa kujitenga na wake zao (kutokujamiiana) wangojee miezi minne. Wakirejea; basi hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 وَإِنْ عَزَمُوا الطَّلَاقَ فَإِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٢٢٧﴾

227. Na wakiazimia talaka, basi hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا ۚ وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٨﴾

228. Na wanawake waliotalikiwa wabakie kungojea zipite hedhi (na twahara) tatu. Na wala si halali kwao kuficha Aliyoumba Allaah katika matumbo yao ikiwa wao ni wenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na waume zao wana haki kuwarejea katika muda huo ikiwa wakitaka suluhu. Nao wake wana haki kama ambayo (ya waume zao) iliyo juu yao kwa mujibu wa shariy’ah. Na wanaume wana daraja zaidi juu yao. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ ۗ وَلَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَأْخُذُوا مِمَّا آتَيْتُمُوهُنَّ شَيْئًا إِلَّا أَن يَخَافَا أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا افْتَدَتْ بِهِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٢٩﴾

229. Talaka ni mara mbili. Hivyo kuzuia kwa mujibu wa shariy’ah au kuachia kwa ihsaan. Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika mlivyowapa wanawake, isipokuwa wote wawili wakikhofu kuwa hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah. Mtakapokhofu kuwa wote wawili hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah; basi hakuna lawama juu yao katika ambacho amejikombolea kwacho. Hiyo ni mipaka ya Allaah basi msitaadi. Na atakayetaadi mipaka ya Allaah basi hao ndio madhalimu.

 

 

 فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ مِن بَعْدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ ۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يَتَرَاجَعَا إِن ظَنَّا أَن يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۗ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٢٣٠﴾

230. Na akimtaliki (mara ya tatu) basi hatokuwa halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwengine. Akimtaliki (au akifariki) hapatokuwa dhambi juu yao wawili kurejeana wakidhani kwamba watasimamisha mipaka ya Allaah. Na hiyo ni mipaka ya Allaah Anaibainisha kwa watu wanaojua.

 

 

وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ ۚ وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِّتَعْتَدُوا ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ وَلَا تَتَّخِذُوا آيَاتِ اللَّـهِ هُزُوًا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمَا أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّنَ الْكِتَابِ وَالْحِكْمَةِ يَعِظُكُم بِهِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٣١﴾

231. Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao; basi wazuieni kwa wema au waachilieni kwa wema. Na wala msiwazuie kuwakusudia dhara mkafanya uonevu. Na atakayefanya hivyo basi kwa yakini amejidhulumu nafsi yake. Na wala msizifanyie mzaha Aayaat (na shariy’ah) za Allaah. Na kumbukeni neema za Allaah juu yenu na Aliyokuteremshieni katika Kitabu na Hikmah (Sunnah) Anakuwaidhini kwayo. Na mcheni Allaah na jueni kwamba Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

 

 وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَن يَنكِحْنَ أَزْوَاجَهُنَّ إِذَا تَرَاضَوْا بَيْنَهُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ ذَٰلِكَ يُوعَظُ بِهِ مَن كَانَ مِنكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗ ذَٰلِكُمْ أَزْكَىٰ لَكُمْ وَأَطْهَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢٣٢﴾

232. Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao; basi msiwazuie kuolewa na waume zao (wa awali) ikiwa wameridhiana baina yao kwa mujibu wa ada. Hayo anawaidhiwa kwayo yeyote miongoni mwenu mwenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo kwenu ni wema zaidi na safi kabisa. Na Allaah Anajua nanyi hamjui.[34]

 

وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ ۖ لِمَنْ أَرَادَ أَن يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ ۚ وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ لَا تُكَلَّفُ نَفْسٌ إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَا تُضَارَّ وَالِدَةٌ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوْلُودٌ لَّهُ بِوَلَدِهِ ۚ وَعَلَى الْوَارِثِ مِثْلُ ذَٰلِكَ ۗ فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٍ مِّنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا ۗ وَإِنْ أَرَدتُّمْ أَن تَسْتَرْضِعُوا أَوْلَادَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِذَا سَلَّمْتُم مَّا آتَيْتُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٣﴾ 

233. Na wazazi wa kike wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa mwenye kutaka kutimiza kunyonyesha. Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa ada. Hailazimishwi nafsi ila kwa iliwezalo. Asidhuriwe mzazi wa kike kwa ajili ya mwanawe, na wala mzazi wa kiume kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi (wa baba) mfano wa hivyo. Watakapotaka kumwachisha kunyonya kwa maridhiano baina yao wawili na mashauriano basi hapana dhambi juu ya wawili hao. Na mtakapotaka kutafuta wa kuwayonyesha watoto wenu, basi si dhambi kwenu ikiwa mtalipa mlichoahidi kwa mujibu wa shariy’ah. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye kuona.

 

 

 وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا ۖ فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٣٤﴾

234. Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao (eda) miezi minne na siku kumi. Watakapofikia muda wao, si dhambi kwao katika yale waliyoyafanya katika nafsi zao kwa ada ya shariy’ah. Na Allaah kwa yale myatendayo, ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

 

 

وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ أَوْ أَكْنَنتُمْ فِي أَنفُسِكُمْ ۚ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ سَتَذْكُرُونَهُنَّ وَلَـٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّا أَن تَقُولُوا قَوْلًا مَّعْرُوفًا ۚ وَلَا تَعْزِمُوا عُقْدَةَ النِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْكِتَابُ أَجَلَهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي أَنفُسِكُمْ فَاحْذَرُوهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٣٥﴾

235. Wala si dhambi juu yenu katika ambayo mmedokezea ya kuposa wanawake hao au mliyoficha katika nafsi zenu. Allaah Anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka lakini msifunge nao ahadi kisiri isipokuwa mseme kauli inayoeleweka kawaida. Na wala msiazimie kufunga ndoa mpaka muda ulioandikwa shariy’ah (katika eda) ufike mwisho wake. Na jueni kwamba Allaah Anajua yaliyomo katika nafsi zenu basi jihadharini Naye. Na jueni kwamba hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mvumilivu.

 

 

لَّا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ مَا لَمْ تَمَسُّوهُنَّ أَوْ تَفْرِضُوا لَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى الْمُوسِعِ قَدَرُهُ وَعَلَى الْمُقْتِرِ قَدَرُهُ مَتَاعًا بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُحْسِنِينَ ﴿٢٣٦﴾

236. Hakuna dhambi kwenu mkiwataliki wanawake ambao hamkuwagusa au kuwabainishia kwao mahari. Wapeni kiliwazo kwa mwenye wasaa kadiri ya uwezo wake na mwenye dhiki kadiri ya uwezo wake. Maliwaza kwa mujibu wa ada, ni haki kwa wafanya ihsaan.

 

 

وَإِن طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّا أَن يَعْفُونَ أَوْ يَعْفُوَ الَّذِي بِيَدِهِ عُقْدَةُ النِّكَاحِ ۚ وَأَن تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۚ وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٧﴾ 

237. Na mkiwataliki kabla ya kuwagusa na mkawa mmeshawabainishia kwao mahari, basi (wapeni) nusu ya hayo mliyobainisha isipokuwa wakisamehe au asamehe yule ambaye fungamano ya ndoa liko mikononi mwake. Na mkisamehe ni ukaribu zaidi ya taqwa. Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye kuona.

 

 

حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ﴿٢٣٨﴾

238. Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.[35]

 

 

 فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا ۖ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿٢٣٩﴾

239. Mkikhofu (swalini) huku mnatembea au mmepanda kipando. Mtakapokuwa katika amani mdhukuruni Allaah kama Alivyokufunzeni yale mliyokuwa hamuyajui.

 

 

وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا وَصِيَّةً لِّأَزْوَاجِهِم مَّتَاعًا إِلَى الْحَوْلِ غَيْرَ إِخْرَاجٍ ۚ فَإِنْ خَرَجْنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِي مَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعْرُوفٍ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٤٠﴾

240. Na wale waliofishwa miongoni mwenu wakaacha wake, wausie kwa ajili ya wake zao masurufu kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa. Watakapotoka wenyewe basi hakuna dhambi juu yenu katika yale waliyofanya katika nafsi zao katika yanayokubalika na shariy’ah. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.[36]

 

 

 وَلِلْمُطَلَّقَاتِ مَتَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ ﴿٢٤١﴾

241. Na wanawake waliotalikiwa wapewe kiliwazo (kitoka nyumba) kwa mujibu wa shariy’ah, ni haki juu ya wenye taqwa.

 

 

كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴿٢٤٢﴾

242. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na shariy’ah) Zake mpate kutia akilini.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ الْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ اللَّـهُ مُوتُوا ثُمَّ أَحْيَاهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٢٤٣﴾

243. Je, hukuwaona wale walitoka majumbani mwao nao wakiwa ni maelfu wakikhofu mauti, Allaah Akawaambia: “Kufeni” kisha Akawahuisha? Hakika Allaah ni Mwenye fadhila juu ya watu lakini watu wengi hawashukuru.

 

 

وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٢٤٤﴾

244. Na piganeni katika njia ya Allaah, na jueni kwamba Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ وَاللَّـهُ يَقْبِضُ وَيَبْسُطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٤٥﴾

245. Ni nani atakayemkopesha Allaah mkopo mzuri kisha (Allaah) Amzidishie mzidisho mwingi. Na Allaah Anakunja na Anakunjua, na Kwake mtarejeshwa.

 

 

 أَلَمْ تَرَ إِلَى الْمَلَإِ مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ إِذْ قَالُوا لِنَبِيٍّ لَّهُمُ ابْعَثْ لَنَا مَلِكًا نُّقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ قَالَ هَلْ عَسَيْتُمْ إِن كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ أَلَّا تُقَاتِلُوا ۖ قَالُوا وَمَا لَنَا أَلَّا نُقَاتِلَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَقَدْ أُخْرِجْنَا مِن دِيَارِنَا وَأَبْنَائِنَا ۖ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ تَوَلَّوْا إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٢٤٦﴾

246. Je, hukuwazingatia wakuu katika wana wa Israaiyl baada ya Muwsaa walipomwambia Nabiy wao: “Tutumie mfalme tupigane katika njia ya Allaah.” (Nabiy) Akasema: “Huenda kuwa hamtopigana ikiwa mtaandikiwa shariy’ah kupigana?” Wakasema: “Tuna nini hata tusipigane katika njia ya Allaah na hali tumekwishatolewa kutoka majumbani mwetu na watoto wetu?” Walipoandikiwa shariy’ah kupigana walikengeuka isipokuwa wachache miongoni mwao. Na Allaah ni Mjuzi wa madhalimu.

 

 

 

وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ اللَّـهَ قَدْ بَعَثَ لَكُمْ طَالُوتَ مَلِكًا ۚ قَالُوا أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ الْمُلْكُ عَلَيْنَا وَنَحْنُ أَحَقُّ بِالْمُلْكِ مِنْهُ وَلَمْ يُؤْتَ سَعَةً مِّنَ الْمَالِ ۚ قَالَ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاهُ عَلَيْكُمْ وَزَادَهُ بَسْطَةً فِي الْعِلْمِ وَالْجِسْمِ ۖ وَاللَّـهُ يُؤْتِي مُلْكَهُ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٤٧﴾ 

247. Na Nabiy wao akawaambia: “Hakika Allaah Amekutumieni Twaaluwt kuwa ni mfalme.” Wakasema: “Vipi yeye atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi tunastahiki zaidi ufalme kuliko yeye, na wala hakupewa wasaa katika mali?” (Nabiy) Akasema: “Hakika Allaah Amemkhitari juu yenu na Akamuongezea ukunjufu katika elimu na kiwiliwili, na Allaah Humpa Amtakaye ufalme Wake.” Na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.

 

 

 وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ آيَةَ مُلْكِهِ أَن يَأْتِيَكُمُ التَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَبَقِيَّةٌ مِّمَّا تَرَكَ آلُ مُوسَىٰ وَآلُ هَارُونَ تَحْمِلُهُ الْمَلَائِكَةُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٤٨﴾

248. Na Nabiy wao akawaambia: “Hakika ishara ya ufalme wake ni kwamba litakujieni kasha ndani yake mna kituliza nyoyo kutoka kwa Rabb wenu na mabaki katika yale waliyoacha watu wa Muwsaa na watu wa Haaruwn, watalibeba Malaika.” Hakika katika hayo mna Aayah (ishara, dalili) kwenu mkiwa ni Waumini.

 

 

فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِالْجُنُودِ قَالَ إِنَّ اللَّـهَ مُبْتَلِيكُم بِنَهَرٍ فَمَن شَرِبَ مِنْهُ فَلَيْسَ مِنِّي وَمَن لَّمْ يَطْعَمْهُ فَإِنَّهُ مِنِّي إِلَّا مَنِ اغْتَرَفَ غُرْفَةً بِيَدِهِ ۚ فَشَرِبُوا مِنْهُ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُ هُوَ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ قَالُوا لَا طَاقَةَ لَنَا الْيَوْمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ ۚ قَالَ الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو اللَّـهِ كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿٢٤٩﴾

249. Alipoondoka Twaaluwt na jeshi akasema: “Hakika Allaah Atakujaribuni kwa mto; atakayekunywa humo, hatokuwa pamoja nami; na ambaye hakuonja hakika huyu yu pamoja nami, isipokuwa atakayeteka teko mmoja kwa mkono wake.” Basi wakanywa kutoka humo isipokuwa wachache miongoni mwao. Alipouvuka yeye na wale walioamini pamoja naye; wakasema: “Leo hatuna nguvu kabisa dhidi ya Jaaluwt na jeshi lake.” Wakasema wale walio na yakini kwamba wao ni wenye kukutana na Allaah: “Makundi mangapi machache yameshinda makundi mengi kwa idhini ya Allaah? Na Allaah Yu pamoja na wenye kusubiri.”

 

 

وَلَمَّا بَرَزُوا لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ قَالُوا رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ﴿٢٥٠﴾

250. Na walipojitokeza kupambana na Jaaluwt na jeshi lake wakasema: “Rabb wetu Tumiminie subira na ithibitishe miguu yetu na Tunusuru dhidi ya watu makafiri.

 

 

 

 فَهَزَمُوهُم بِإِذْنِ اللَّـهِ وَقَتَلَ دَاوُودُ جَالُوتَ وَآتَاهُ اللَّـهُ الْمُلْكَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَهُ مِمَّا يَشَاءُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّفَسَدَتِ الْأَرْضُ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ ذُو فَضْلٍ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٢٥١﴾

 251. Wakawashinda kwa idhini ya Allaah na Daawuwd akamuua Jaaluwt; na Allaah Akampa ufalme na hikmah, na Akamfunza katika Aliyoyataka. Na lau Allaah Asingelizuia watu baadhi yao kwa wengine, basi ingelifisidika ardhi lakini Allaah ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu.

 

 

تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٢٥٢﴾

252. Hizo ni Aayaat za Allaah Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Rusuli.

 

 

تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۘ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّـهُ ۖ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ ۚ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِن بَعْدِهِم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَلَـٰكِنِ اخْتَلَفُوا فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ ﴿٢٥٣﴾

253. Hao ni Rusuli, Tumewafadhilisha baadhi yao juu ya baadhi. Miongoni mwao kuna aliyesemeshwa na Allaah, na Akawapandisha baadhi yao vyeo. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام. Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana wale wa baada yao, baada ya kuwajia hoja bayana. Lakini walikhitalifiana, basi miongoni mwao ambao walioamini na miongoni mwao waliokufuru. Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana lakini Allaah Anafanya Ayatakayo.

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ ۗ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٥٤﴾

254. Enyi walioamini! Toeni katika Tulivyokuruzukuni kabla haijafika Siku ambayo hakutokuweko mapatano humo wala urafiki wala uombezi. Na makafiri wao ndio madhalimu.

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

255. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye Uluwa, Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa.[37]

 

 

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٥٦﴾

256. Hapana kulazimisha katika Dini, kwani imekwishabainika kati ya uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaghuti na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.[38]

 

 

 اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥٧﴾

257. Allaah ni Mlinzi Msaidizi wa wale walioamini, Anawatoa kutoka katika viza na kuwaingiza katika nuru. Na wale waliokufuru marafiki wao wandani ni twaghuti, huwatoa kutoka katika nuru na kuwaingiza katika viza. Hao ni watu wa motoni wao humo ni wenye kudumu.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِي حَاجَّ إِبْرَاهِيمَ فِي رَبِّهِ أَنْ آتَاهُ اللَّـهُ الْمُلْكَ إِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّيَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ ۖ قَالَ إِبْرَاهِيمُ فَإِنَّ اللَّـهَ يَأْتِي بِالشَّمْسِ مِنَ الْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ الْمَغْرِبِ فَبُهِتَ الَّذِي كَفَرَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥٨﴾

258. Je, hukumzingatia yule ambaye alimuhoji Ibraahiym kuhusu Rabb wake kwa vile Allaah Alimpa ufalme; aliposema Ibraahiym: “Rabb wangu ni Ambaye Anahuisha na Anafisha.” Akasema: “Mimi pia nahuisha na nafisha.” Ibraahiym akasema: “Hakika Allaah Analileta jua kutoka Mashariki basi wewe lilete kutoka Magharibi.” Akapigwa na butwaa na kushindwa yule aliyekufuru. Na Allaah Haongoi watu madhalimu.

 

 

أَوْ كَالَّذِي مَرَّ عَلَىٰ قَرْيَةٍ وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحْيِي هَـٰذِهِ اللَّـهُ بَعْدَ مَوْتِهَا ۖ فَأَمَاتَهُ اللَّـهُ مِائَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ ۖ قَالَ كَمْ لَبِثْتَ ۖ قَالَ لَبِثْتُ يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۖ قَالَ بَل لَّبِثْتَ مِائَةَ عَامٍ فَانظُرْ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمْ يَتَسَنَّهْ ۖ وَانظُرْ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجْعَلَكَ آيَةً لِّلنَّاسِ ۖ وَانظُرْ إِلَى الْعِظَامِ كَيْفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكْسُوهَا لَحْمًا ۚ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ قَالَ أَعْلَمُ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٥٩﴾

259. Au kama yule aliyepita katika kijiji nacho ni kilichoporomoka kabisa juu ya mapaa yake; akasema: “Vipi Allaah Atahuisha hiki (kijiji) baada ya kufa kwake?” Basi Allaah Alimfisha miaka mia; kisha Akamfufua. Akasema: “Umekaa muda gani?” Akasema: “Nimekaa siku moja au sehemu ya siku.” (Allaah) Akasema: “Bali umekaa miaka mia; basi kitazame chakula chako na kinywaji chako hakikuharibika. Na mtazame punda wako; na Tutakufanya uwe Aayah (dalili, ishara) kwa watu. Na itazame mifupa jinsi Tunavyoinyanyua, kisha Tunaivisha nyama.” Basi ilipombainikia alisema: “Najua kwamba hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.”

 

 

 

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ أَرِنِي كَيْفَ تُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِن ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَـٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِي ۖ قَالَ فَخُذْ أَرْبَعَةً مِّنَ الطَّيْرِ فَصُرْهُنَّ إِلَيْكَ ثُمَّ اجْعَلْ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٍ مِّنْهُنَّ جُزْءًا ثُمَّ ادْعُهُنَّ يَأْتِينَكَ سَعْيًا ۚ وَاعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٦٠﴾ 

260. Na pindi aliposema Ibraahiym: “Rabb wangu nionyeshe vipi Unahuisha wafu?” (Allaah) Akasema: “Je, kwani huamini?” Akasema: “Hasha!  Lakini ili moyo wangu utumainike.” (Allaah) Akasema: “Basi chukua ndege wanne wazoeshe kwako, (uwachinje), kisha weka juu ya kila jabali sehemu ya hao (ndege); kisha waite watakujia mbio; na jua kwamba hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

مَّثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّائَةُ حَبَّةٍ ۗ وَاللَّـهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦١﴾ 

261. Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja ya mbegu iliyotoa mashuke saba, katika kila shuke kuna punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye; na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.

 

 

 

الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَا أَنفَقُوا مَنًّا وَلَا أَذًى ۙ لَّهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٦٢﴾

262. Wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allaah kisha hawafuatishii kwa waliyoyatoa masimbulizi wala udhia watapa ujira wao kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.

 

 

قَوْلٌ مَّعْرُوفٌ وَمَغْفِرَةٌ خَيْرٌ مِّن صَدَقَةٍ يَتْبَعُهَا أَذًى ۗ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَلِيمٌ ﴿٢٦٣﴾

263. Kauli njema na msamaha ni bora kuliko swadaqah inayoifuata udhia. Na Allaah ni Mkwasi, Mvumilivu.

 

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾

264. Enyi walioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa kujionyesha kwa watu wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri.

 

 

 وَمَثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ وَتَثْبِيتًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِن لَّمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٦٥﴾

265. Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kutafuta radhi za Allaah na kujithibitisha nafsi zao ni kama mfano wa bustani iliyoko pahala paliponyanyuka; ikafikiwa hiyo bustani na mvua kubwa, ikatoa mazao yake maradufu, na hata kama haikufikiwa na mvua kubwa basi mvua ndogo huitosheleza. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye kuona.

 

 

 أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَن تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ لَهُ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَأَصَابَهُ الْكِبَرُ وَلَهُ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفَاءُ فَأَصَابَهَا إِعْصَارٌ فِيهِ نَارٌ فَاحْتَرَقَتْ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢٦٦﴾

266. Je! Anapenda mmoja wenu awe ana bustani ya mitende na mizabibu ipitayo chini yake mito; anayo humo kila aina ya mazao; ukamfikia uzee, naye ana kizazi dhaifu; kisha ikapigwa na kimbunga cha moto kikaiteketeza? Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (ishara, zingatio) kwenu mpate kutafakari.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٢٦٧﴾

267. Enyi walioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma na katika ambavyo Tumekutoleeni kutoka katika ardhi. Na wala msikusudie vibaya kutoka humo mkavitoa na hali nyinyi wenyewe si wenye kuvichukuwa isipokuwa kuvifumbia macho. Na jueni kwamba hakika Allaah ni Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa.[39]

 

 

 الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاءِ ۖ وَاللَّـهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦٨﴾

268. Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni machafu, (ubakhili), na Allaah Anakuahidini maghfirah kutoka Kwake na fadhila. Na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.

 

 

 

يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٦٩﴾

269. Humpa hikmah Amtakaye. Na anayepewa hikmah basi kwa yakini huwa amepewa khayr nyingi. Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili.

 

 

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ ۗ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿٢٧٠﴾

270. Na chochote mtoacho au mkiwekacho nadhiri, basi Allaah Anakijua. Na madhalimu hawana wa kuwanusuru.

 

 

 إِن تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ ۖ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّئَاتِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٧١﴾

 271. Mkidhihirisha swadaqah basi ni vizuri hivyo, na mkizificha na kuwapa mafakiri, basi hilo ni khayr kwenu. Na Atakufutieni katika maovu yenu. Na Allaah kwa yale myatendayo, ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

 

 

لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾

272. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwahidi, lakini Allaah Humhidi Amtakaye. Na chochote cha khayr mtoacho basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika khayr mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa.[40]

 

 

 لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِي الْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢٧٣﴾

273. (Swadaqah ni) Kwa ajili ya mafakiri waliozuilika katika njia ya Allaah hawawezi kwenda huku na kule katika ardhi (kutafuta rizki); asiyewajua huwadhania kuwa ni matajiri kutokana na staha ya kujizua kwao, unawatambua kwa alama zao, hawaombi watu kwa ung’ang’anizi. Na chochote mtoacho katika khayr basi Allaah kwacho ni Mjuzi.

 

 

الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ سِرًّا وَعَلَانِيَةً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٢٧٤﴾

274. Wale wanaotoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri; watapata ujira wao kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.

 

 

 

الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا ۗ وَأَحَلَّ اللَّـهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا ۚ فَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَنْ عَادَ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧٥﴾

275. Wale wanaokula ribaa hawatosimama (Siku ya Qiyaamah) ila kama anavyosimama yule aliyezugwa na shaytwaan kwa kuguswa na kupatwa. Hivyo kwa sababu wao wamesema: “Hakika biashara ni kama ribaa.” Na Allaah Amehalalisha biashara na Ameharamisha ribaa. Basi atakayefikiwa na mawaidha kutoka kwa Rabb wake akakoma; basi ni yake yale yaliyopita, na hukumu yake iko kwa Allaah. Na atakayerudia basi hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

يَمْحَقُ اللَّـهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ ﴿٢٧٦﴾

276. Allaah Huifuta baraka (mali ya) ribaa na Huzibariki swadaqah. Na Allaah Hapendi kila kafiri apapiae madhambi.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٢٧٧﴾

 277. Hakika wale walioamini na wakatenda mema na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah; watapata ujira kutoka kwa Rabb wao na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿٢٧٨﴾

278. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika ribaa ikiwa nyinyi ni Waumini.

 

 

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٩﴾

279. Na msipofanya basi tangazeni vita kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake. Na mkitubu basi mtapata rasilimali zenu msidhulumu na wala msidhulumiwe.[41]

 

 

 

 وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ ۚ وَأَن تَصَدَّقُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٨٠﴾

280. Na ikiwa (mdaiwa) ni mwenye hali ngumu, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkifanya deni kuwa ni swadaqah basi ni khayr kwenu mkiwa mnajua.

 

 

 

 وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٨١﴾

281. Na iogopeni Siku mtakayorejeshwa ndani yake kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa.[42]

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ ۚ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ ۚ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَن يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّـهُ ۚ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا ۚ فَإِن كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ ۚ وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ ۚ وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا ۚ وَلَا تَسْأَمُوا أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَىٰ أَجَلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَىٰ أَلَّا تَرْتَابُوا ۖ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا ۗ وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ ۚ وَلَا يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ ۚ وَإِن تَفْعَلُوا فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّـهُ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٨٢﴾ 

282. Enyi walioamini! Mtakapokopeshana deni mpaka muda maalumu uliopangwa, basi liandikeni. Na aandike baina yenu mwandishi kwa uadilifu. Na wala asikatae mwandishi kuandika kama Allaah Alivyomfunza. Basi aandikishe kwa imla yule ambaye ana haki (mdai) na amuogope Allaah, Rabb wake, na wala asipunguze humo kitu chochote. Basi ikiwa yule ambaye ana haki amepumbaa kiakili au mnyonge, au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe msimamizi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili wanaume miongoni mwenu. Na ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamme mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi, ili kama mmoja wao hao wanawake wawili akikosea (akasahau), basi mmoja wao atamkumbusha mwengine. Na mashahidi wasikatae watapoitwa. Na wala msichukie kuliandika (deni) dogo au kubwa mpaka muda wake. Hivyo kwenu ndiyo uadilifu upasavyo mbele ya Allaah na ndio unyoofu zaidi kwa ushahidi; na ni karibu zaidi ili msiwe na shaka; isipokuwa itakapokuwa biashara taslimu mnayoiendesha baina yenu, basi si dhambi kwenu msipoiandika. Na shuhudisheni mnapouziana. Na wala asidhuriwe mwandishi wala shahidi; na mkifanya basi hakika huo ni ufasiki kwenu. Na mcheni Allaah, na Allaah Anakufunzeni, na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

 

وَإِن كُنتُمْ عَلَىٰ سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَّقْبُوضَةٌ ۖ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ ۗ وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ ۚ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٢٨٣﴾

283. Na mkiwa safarini na hamkumpata mwandishi, basi (mdai) akabidhiwe rahani. Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah, Rabb wake; na wala msifiche ushahidi; na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allaah kwa yale mnayoyatenda ni Mjuzi.

 

 

لِّلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَإِن تُبْدُوا مَا فِي أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ اللَّـهُ ۖ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٨٤﴾

 284. Ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha; basi Allaah Atakuhesabuni kwayo. Humghufuria Amtakaye na Humuadhibu Amtakaye. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.[43]

 

 

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾

 285. Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rusuli Wake. (Nao husema): “Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rusuli Wake.” Na wakasema: “Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia.[44]

 

 

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾  

286. Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata (thawabu) iliyoyachuma, na ni dhidi yake (kwa maovu) iliyojichumia. “Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabb wetu, Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu. Rabb wetu, Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mola Mlinzi wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri.[45]

 

 

 

 

[1] Faida: Fadhila za Suwrah Al-Baqarah kama zilivyopokelewa katika Ahaadiyth mbalimbali:

 

Hadiyth Ya Kwanza:

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Msifanye nyumba zenu makaburi. Kwa hakika shaytwaan haingii nyumba ambayo husomwa humo Suwratul-Baqarah.” [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh] na katika Riwaayah ya Muslim, Hadiyth (780): “Shaytwaan anakimbia nyumba inayosomwa ndani yake Suwratul-Baqarah.”

 

Hadiyth Ya Pili:

Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kila kitu kina kipeo cha kudhibiti (na kuangaza yaliyo chini) na Al-Baqarah ndio kipeo cha Qur-aan. Atakayesoma Al-Baqarah usiku nyumbani kwake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba yake nyusiku tatu. Na atakayesoma mchana ndani ya nyumba yake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba hiyo kwa siku tatu.” [Atw-Twabaraaniy (6/163), Ibn Hibbaan (2/78) na Ibn Mardawayh, Swahiyh At-Targhiyb (2/314)]

 

Hadiyth Ya Tatu:

An-Nawwaas bin Samm’aan (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Siku ya kufufuliwa, Qur-aan, na watu waliokuwa wakiisoma na kutekeleza mafunzo yake wataletwa mbele wakitangulizwa na Suwratul-Baqarah na Aal-‘Imraan.”  Akasema An-Nawwaas: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoa mifano mitatu kwa Suwrah mbili hizi na sikusahau mifano hiyo tokea wakati huo. Alisema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Watakuja kama mawingu mawili, vivuli vyeusi viwili, au njia mbili za ndege watawatetea watu wao.” [Muslim]

 

Hadiyth Ya Nne:

Abuu Umaamah Al-Baahiliy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Someni Qur-aan kwani itakuja Siku ya Qiyaamah ikiwa ni shafaa’ah (kiombezi) kwa watu wake wanaoisoma na kutekeleza. Someni taa mbili; Al-Baqarah na Aal-‘Imraan kwani zitakuja Siku ya Qiyaamah kama kwamba ni maumbile ya mawingu, au sehemu mbili za mawingu, au safu za makundi mawili ya ndege na zitatoa hoja kwa niaba ya watu wake siku hiyo. Someni Suwratul-Baqarah, kwani ukiwa nayo utapata baraka, na ukiaacha ni khasara na majuto, na wachawi hawawezi kuihifadhi kwa moyo.” [Muslim (804)] 

 

[2] Faida: Herufi hizi na nyenginezo kama hizo zinazoanza mwanzoni wa baadhi ya Suwrah, ni katika ‘ilmu ya ghayb ambayo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Imehadithiwa kutoka kwa Abuu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan, ‘Aliy na Ibn Mas‘uwd  (رضي الله عنهم). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

[3] Faida: Hudaa, Hidaayah ziko aina mbili; (1) Hidaayatut-Tawfiyq: Ni iymaan ambayo mahali pake ni moyoni na ni Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee Awezaye kuiweka katika nyoyo za waja. Dalili ni kauli yake Allaah (سبحانه وتعالى) Alipomwambia Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye alipendelea kumuongoza ‘Ammi yake Abuu Twaalib katika Uislamu alipokuwa anakaribia kuaga dunia. Allaah Akasema: “Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye.” [Al-Qaswasw (28: 56)]. (2) Hidaayatul-Irshaad (hidaaya ya kuongoza): ni kuelekeza, kubainisha, kuongoza njia, kumwongoza mtu katika kutekeleza mema n.k. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى): “Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka.” [Ash-Shuwraa (42 :52)].

 

[4] Faida: Maana ya kusimamisha Swalaah:  Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Ni kuswali kwa kuzingatia nguzo na sharti zake.”  Adhw-Dhwahaak amesema kuwa Ibn ‘Abbaas alisema: “Iqamaat Asw-Swalaah maana yake ni kukamilisha rukuu, sujuwd, kusoma Qur-aan, khushuu (unyenyekevu), na kuhudhurisha moyo katika Swalaah.” Qataadah alisema: “Iqamaat Asw-Swalaah maana yake ni kuchunga wakati, wudhuu, rukuu na sujuwd za Swalaah.” Muqaatil bin Hayyaan alisema: “Iqaamat Asw-Swalaah ina maana: Kuchunga wakati, kujitwaharisha kwa ajili yake, kukamilisha rukuu, sujuwd na kusoma Qur-aan, tashahhud na kumwombea rahmah Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hiyo ndiyo Iqaamat Asw-Swalaah.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

[5] Faida: Istawaa: Inamaanisha Yuko juu kabisa kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى).  Na msimamo wa Salaf katika tafsiyr ya Aayah hiyo ni kama uliopokelewa kuwa, Ja’far bin ‘Abdillaah na wengine miongoni mwao walisema: “Tulikuwa kwa Imaam Maalik bin Anas basi akatokea mtu akamuuliza? Ee Abaa ‘Abdillaah! Allaah (تعالى) Anasema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥

Mwingi wa rahmah Yuko juu (Istawaa) ya ‘Arshi. [Twaaha  (20: 5)]. 

Je, ni vipi Istawaa? Basi Imaam Maalik hakuwahi kughadhibika kutokana na kitu chochote kile kama alivyoghadhibika kutokana na swali la mtu huyo, kisha [Imaam Maalik] akatazama chini na huku akikwaruzakwaruza kwa kijiti kilichokuwa kwenye mkono wake mpaka akarowa jasho, kisha akanyanyua kichwa chake na kukirembea kile kijiti kisha akasema: ‘Vipi’ ni ghayr ma’quwl (hakutambuliki), na Al-Istiwaa ghayr maj-huwl (si jambo lisilojulikana), na kuamini hilo ni waajib (lazima), na kuuliza (au kuhoji hilo) ni bid’ah (uzushi); na nina khofu kuwa wewe ni mzushi! Akaamrisha mtu huyo atolewe, basi akatolewa. [Imesimuliwa kwenye Al-Hilyah (6/325-326) na pia imesimuliwa na Abuu ‘Uthmaan Asw-Swaabuniy katika ‘Aqiydatu As-Salaf Asw-haab Al-Hadiyth uk. (17-18), kutoka kwa Ja’far bin ‘Abdillaah]

 

[6] Faida: Kufadhilishwa kwa hao Baniy Israaiyl juu ya walimwengu wote; makusudio yake ni walimwengu wa zama zao kwani inafahamika kuwa ummah uliokuwa bora kuliko ummah zote ni ummah wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa dalili ya kauli ya Allaah (تعالى): Mmekuwa ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki.” [Aal-‘Imraan (3: 110)].

[7] Faida: As-Sabt maana yake asili, ni mapumziko na hivyo Siku hiyo yao ya mapumziko (Jumamosi), Mayahudi waliwekewa shariy’ah wasivue samaki lakini walikhalifu amri kwa kutumia njama na ujanja wakavua samaki kumuasi Allaah, basi Allaah Akawaghadhibikia na kuwageuza manyani.

[8] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka ikiwazungumzia Mayahudi na Manaswara [Al-Bukhaary katika: Khalqu Af-’aal Al-‘Ibaad kutoka kwa Swahaba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)]

 

[9] Faida: Uthibitisho kwamba Jibriyl ((عليه السلام ni Ruwh Al-Qudus: Ibn Mas‘uwd  (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ruwh Al-Qudus alinifahamisha kuwa hakuna roho itakayokufa mpaka imalizike rizki yake na muda wake, kwa hiyo mcheni Allaah na mtakeni rizki katika hali iliyo bora.” [As-Sunnah: (14/304), ameisahihisha Al-Albaaniy katika Mushkilat Al-Faqar (15), Swahiyh Al-Jaami’ (2085) Hadiyth kutoka Abuu Umaamah Al-Baahiliy (رضي الله عنه)].

 

[10] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kuhusu Mayahudi kama alivyohadithia ‘Aaswim bin ‘Umar bin Qataadah kuhusu watu katika kaumu yake walisema: Katika ambayo yaliyotuitia katika Uislaam kwa rahmah ya Allaah (تعالى),  na Akaiongoza kwetu, ni pale tulipokuwa tukisikia kutoka Mayahudi, wakati sisi tulikuwa washirikina waabudu masanamu, na Ahlul-Kitaab walikuwa ndio wenye ‘ilmu tusiyokuwa nayo sisi. Na ikawa inaendelea shari baina yetu na wao, basi ilikuwa pale tunapopata (matatizo) kutoka kwao kwa baadhi ya waliyoyachukia, walituambia: Hivi karibuni anakaribia kutumwa Nabiy, basi sasa tutawaua mauwaji ya ‘Aad na Iram, na yeye atakuwa pamoja nasi.   Ikawa tunasikia sana hilo. Kisha Allaah Alipomtuma Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وىله وسلم) tukamuitikia alipotuitia kwa Allaah  (تعالى)na tukatambua waliyokuwa wakituahidi. Tukawakimbilia na tukamwamini, lakini wao wakamkanusha basi ikateremshwa kwao Aayaat za Al-Baqarah: Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao, na japokuwa kabla ya hapo walikuwa wakiomba ushindi dhidi ya wale waliokufuru; basi yalipowajia yale waliyokuwa wakiyatambua waliyakanusha, basi laana ya Allaah iwe juu ya makafiri” (2: 89). [Amepokea Ibn Is-haaq katika Siyrah].

 

Sababun-Nuzuwl: Pia, Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: Mayahudi walikuwa wakimuomba Allaah (kuletwa kwa Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili wapate ushindi juu ya (Qabila la) Aws na Khazraj kabla ya kutumwa kwake Nabiy. Kisha Allaah Alipomtuma kwa Waarabu, wakamkanusha na kukataa kwamba walikuwa wakimzungumza. Basi Mu’aadh bin Jabal na Bishr bin Al-Baraa bin Ma’ruwr kutoka Bani Salamah waliwaambia: Enyi Mayahudi! Mcheni Allaah na ingieni katika Uislamu, kwani mlikuwa mkimuomba Allaah kuja kwa Muhammad wakati sisi tulikuwa bado makafiri na nyinyi mlikuwa mkituambia kwamba atatumwa na mkatuelezea sifa zake kwetu. Salaam bin Mushkim kutoka Bani An-Nadhwiyr akajibu: Hakuleta lolote tunalolitambua, wala si yeye ambaye tulikuwa tukikutajieni. Hapo Allaah Akateremsha Aayah kuhusu kauli yako: Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao… (2: 89) [Ameipokea Ibn Ishaaq- Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

[11] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka hali ya kuwa ni jawabu kwa Mayahudi miongoni mwa wana wa Israaiyl, pale walipodai kuwa Jibriyl ((عليه السلام ni adui yao. [Imaam Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)] na pia kama alivyohadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba: Kundi miongoni mwa Mayahudi lilihudhuria kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakasema: Yaa Abaa Qaasim! Tuelezee kuhusu tunayokuuliza kwani hayajui isipokuwa Nabiy. Akasema: “Niulizeni mnayotaka lakini niwekeeni ahadi kwa Allaah (kama ahadi) aliyofungamana Ya’quwb kwa wanawe, kuwa nikikuhadithieni jambo mkalijua, mtanifuata katika Uislamu.” Wakasema: Umelipata hilo! (tumekubali). Akasema: “Niulizeni mtakacho.” Wakasema: Tuelezee mambo manne tutakayokuuliza; Tueleze ni chakula gani alichojiharamishia Ya’quwb kabla ya kuteremshwa Tawraat? Na tueleze vipi yanakuwa maji (manii) ya mwanamme na mwanamke, na vipi anakuwa (mtoto) wa kiume anayetokana na maji hayo? Na tueleze vipi anakuwa usingizini huyu Nabiy ambaye hajui kusoma? Na nani anakuwa kipenzi chake katika Malaika? Akasema: “Je mnanipa ahadi kwa Allaah kuwa nikikuelezeni mtanifuata?” Ibn ‘Abbaas akasema: Mayahudi wakampa ahadi. Akasema: “Nakuapieni kwa Ambaye Ameteremsha Tawraat kwa Muwsaa ((عليه السلام hivi mnajua kuwa Ya’quwb aliugua maradhi makali, yakakaa muda mrefu maradhi yake, akaweka nadhiri kwa Allaah kuwa, endapo atapona maradhi yake, atajiharamishia vinywaji avipendavyo sana na vyakula avipendavyo sana na kilikuwa chakula akipendacho zaidi nyama ya ngamia na kinywaji akipendacho zaidi ni maziwa yake?” Wakasema: Allaahumma na’am! Akasema: “Yaa Allaah Washuhudie!  Na nakuapieni kwa Allaah Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, na Ambaye Amteremsha Tawraat kwa Muwsaa ((عليه السلام, hivi mnajua kuwa maji ya mwanamme ni meupe mazito, na maji ya mwanamke ni ya njano mepesi, basi moja ya maji hayo yakiwa juu ya mengine anakuwa jinsia yake huyo mtoto na kufanana naye kwa idhini ya Allaah.  Na endapo yakiwa maji ya mwanaume juu ya maji ya mwanamke, anakuwa (mtoto) wa kiume, na yakiwa maji ya mwanamke juu ya mwanamme, anakuwa wa kike kwa idhini ya (Allaah سبحانه وتعالى)?” Wakasema: Allaahumaa na’am! Akasema: “Yaa Allaah Washuhudie! Na nakuapieni kwa Allaah Ambaye Ameteremsha Tawraat kwa Muwsaa, hivi mnajua kuwa huyu Nabiy asiyejua kusoma (kuwa) yanalala macho yake wala haulali moyo wake?” Wakasema: Allaahumma na’am! Akasema: “Yaa Allaah Shuhudia!” Wakasema: Basi sasa wewe tuelezee ni nani kipenzi chako katika Malaika? Hapo ndio tutakuwa na wewe au tutafarikiana. Akasema: “Hakika kipenzi changu ni Jibriyl na wala Allaah Hakutuma Nabiy yeyote ila anakuwa kipenzi chake.” Wakasema: Hapo ndio tunafarikiana! Lau angekuwa kipenzi chako mwengine katika Malaika tungekufuata na tungekusadikisha. Akasema: “Kipi kinachokuzuieni kumsadikisha?” Wakasema: Hakika yeye ni adui yetu. Ibn ‘Abbaas akasema: Hapo ndipo Alipoteremsha Allaah Ta’aala: Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako...”  mpaka kauli ya Allaah [Aayah (2: 101)]  “...Kitabu cha Allaah nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui.” na hapo wakastahiki ghadhabu juu ya ghadhabu (2: 90) Suwrah Al-Baqarah) [Musnad Ahmad (2384). Ni Hadiyth Swahiyh kwa mkusanyiko wa njia zake na imenukuliwa Ijmaa’ juu usahihi wake].

 

[12] Sababun-Nuzuwl: Kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Basi sameheni na puuzeni; mpaka Allaah Alete Amri Yake…” (2: 109). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipanda punda akamwambia Sa’d: “Je hukusikia alivyosema Abuu Hubaab?” (akikusudia ‘Abdullaah bin Ubayy. “Amesema kadhaa wa kadhaa.” Sa’d bin ‘Ubaadah akasema: “Msamehe na puuza, basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamsamehe. Na alikuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake wakiwasamehe Ahlul-Kitaab na Washirikina, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:Basi sameheni na puuzeni; mpaka Allaah Alete Amri Yake…”   [Amehadithia ‘Urwah kutoka kwa Usaamah bin Zayd, amepokea Abuu Ash-Shaykh katika Al-Akhlaaq].

 

An-Naasikh Wal-Mansuwkh: Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Basi sameheni na puuzeni; mpaka Allaah Alete amri Yake” imefutwa hukmu yake kwa kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “basi waueni washirikina popote muwakutapo” (9: 5) na “Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho” (9: 29).

[13] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka pale Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa akiswali akiwa juu ya mnyama wake, alipokuwa akirudi kutoka Makkah kuelekea Madiynah, basi hapo ikateremshwa: “basi popote mnapogeuka kuna Wajihi wa Allaah.” [Amehadithia Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) amepokea At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ahmad na Ibn Jariyj. Na amesema At-Tirmidhiy ni Hadiyth Hasan Swahiyh].

 

[14] Sababun-Nuzuwl: Imeteremka Aayah hii kuhusu kauli yake Allaah (سبحانه وتعالى) “Na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia”; ni pale ‘Umar (رضي الله عنه) alipomwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Lau tungelifanya sehemu aliyosimama Ibraahiym kuwa ni sehemu ya kuswalia”, kisha baada ya hapo ikateremka hii Aayah. [Al-Bukhaariy kwa ufupi kutoka kwa ‘Umar] na sehemu aliyosimama Ibraahiym ndiyo iitwayo Hijri.

 

 

[15] Al-Asbaatw: Ni makabila kumi na mbili ya wana wa Ya’quwb ((عليه السلام waliotoka Manabii.

[16] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii na zinazofuatia zimeteremka kama alivyohadithia Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anaposwali akielekeza uso wake Baytul-Maqadis lakini kila mara alikuwa anatazama mbinguni akingojea amri ya Allaah. Kisha Allaah Akateremsha: Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam…” (2: 144) Kisha tukatamani kujua kuhusu hukmu ya waliofariki kabla ya kugeuzwa Qiblah. Hapo Allaah Akateremsha: “Na Allaah Hakuwa Mwenye kupoteza iymaan yenu (Swalaah), hakika Allaah kwa watu, bila shaka ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.” (2: 143) Kisha Mayahudi wakasema: Ni jambo lipi limewageuza na kuwatoa kwenye Qiblah chao? Hapo Allaah Akateremsha: Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: “Nini kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea…”  mpaka mwisho wa Aayah (2: 142) [Hadiyth ameipokea Imaam Ibn Is-haaq katika Siyrah].

 

[17] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kama ilivyohadithiwa na Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali Swalaah zake akielekeza uso wake Baytul-Maqdis (Palestina) kwa muda wa miezi kumi na sita au miezi kumi na saba, lakini alipendezewa kuwa Qibla chake kiwe ni Al-Ka’bah (Makkah).  [Ikateremshwa Aayah: Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam…” (2: 144)]. Akaswali pamoja na watu (akielekea Al-Ka’bah). Kisha mmoja wa aliyekuwa akiswali naye alitoka nje akapitia watu Msikitini wakiwa wako katika rukuu’ (wakielekea Baytul-Maqdis). Akasema kuwaambia: “Nashuhudia kwa Allaah, nimetoka (sasa hivi) kuswali pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa ameelekea Makkah (Al-Ka’bah).” Waliposikia hivo, hapo hapo waligeuka kuelekea Al-Ka’bah wakati wakiwa katika hali hiyo hiyo ya rukuu’. Baadhi ya Waislaam waliokuwa wakiswali kuelekea Qibla (cha Baytul-Maqdis) kabla ya kubadilishwa kuelekea Nyumba (Al-Ka’bah Makkah) walifariki au walikufa shahidi nasi hatukujua tuseme nini kuhusu wao (na kuelekeza Swalaah zao Baytul-Maqdis). Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: Na Allaah Hakuwa Mwenye kupoteza iymaan yenu (Swalaah), hakika Allaah kwa watu, bila shaka ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.” (2: 143) [Al-Bukhaariy].

 

Faida:  Masjid hiyo waliyoswali Maswahaba wakageuza Qiblah chao kuelekeza Al-Ka’bah, ndio inayojulikana kama Masjd Al-Qiblatayni (Msikiti wa Qiblah mbili) Yaani; kuelekea kwao ndani ya Swalaah moja, kwanza Baytul-Maqdis (Palestina) kisha kuelekea kwao Al-Ka’bah.

 

 

 

[18] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kama alivohadithia Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali kwa kuelekeza uso wake Baytul-Maqdis (Palestina) lakini alikuwa akitazamatazama mbinguni akitegemea amri ya Allaah (Ambadilishie Qiblah) ndipo ikateremka hii Aayah: Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia…” (2: 144) [Al-Bukhaariy na wengineo kwa riwayaah nyenginezo].

 

[19] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kuhusu baadhi ya Maswahaba (رضي الله عنهم) walihisi uzito kutufu baina Swafaa na Marwah, kwa sababu ilikuwa ni katika ‘ibaadah za enzi ya jaahiliyyah, na washirikina waliweka sanama lao linaloitwa Manaat, wakiliabudu sanamu hilo na wakilifanyia Hijjah na wakilizunguka. Ulipokuja Uislamu walimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hivyo ndio Allaah Akateremsha Aayah hii (2: 158) [Al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها)].  Rejea Utangulizi wa Tarjama, tanbihi katika: Kufasiri Qur-aan kwa kauli za Maswahaba  (رضي الله عنهم).

Sababun-Nuzuwl: Pia, sababu nyingine ni pale iliposhuka Aayah inayoamrisha kutufu Al-Ka’bah, ilikuwa haikutajwa katika Qur-aan kutufu Swafaa na Marwah. Maswahaba wakasema: Ee Rasuli wa Allaah, tulikuwa tunatufu Swafaa na Marwah na Allaah Ameteremsha kuhusu kutufu Nyumba (Al-K’bah) je itakuwa dhambi kwetu kutufu Swafaa na Marwah? Hapo Allaah Akateremsha Aayah hii: Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika alama za Allaah…” (2: 158) [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Sababun-Nuzuwl: Pia ‘Aaswim bin Sulaymaan (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nilimuuliza Anas bin Maalik (رضي الله عنه) kuhusu Swafaa na Marwah, akasema: Tulikuwa tunaona kuwa hilo ni jambo la ujhaaliyyah. Kisha ulipokuja Uislamu tukazuia kutufu (vilima viwili hivo) ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika alama za Allaah…” (2: 158) [Al-Bukhaariy].

 

[20] An-Naasikh Wal-Mansuwkh: Aayah hii wamekhitalifiana wanachuoni kuhusu kufutwa kwake na kutofutwa na kuteremshwa baada yake Aayah ya miyraath ya Suwrah An-Nisaa (4: 11-12), na wengine wamesema kuwa hiyo ni Aayah ya hukmu na haijafutwa, na wengine wameona ni makhsusi na nyingine ni ya jumla. Na wengine wameona imefutwa na Hadiyth ya Abuu Umaamah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah amekwishampatia kila mwenye haki haki yake, basi hakuna wasiyyah kwa mwenye kurithi.” Kwa kifupi, kuna ikhtilaaf ya wanachuoni kuhusu Aayah hiyo katika kauli nne.

 

[21] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه)   kwamba: Maswahaba wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) walipokuwa wakifunga swawm kisha ikatokea kuwa walale bila ya kufuturu (Magharibi), walikuwa huendelea kufunga swawm (usiku wote na mchana) mpaka kufike jioni tena (Magharibi). Siku moja Swahaba Qays Ibn Swirmah alikuwa amefunga swawm. Ulipofika wakati wa kufuturu alimwendea mkewe akamuuliza: Je una chakula? Akajibu: Hapana! Lakini nitajaribu kukupatia. Na na alikuwa akifanya kazi ngumu. Akaghilibiwa na usingizi na alipokuja mkewe (na chakula) alimkuta ameshalala. Akasema: Ole wako, umelala! Ilipofika mchana wa siku ya pili, alzimia. Yakatajwa hao kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), hapo Aayaah hii ikateremshwa: Mmehalalishiwa usiku wa kufunga Swiyaam kujamiiana na wake zenu…” wakafurahi mno! Na ikateremka: “Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). Kisha timizeni Swiyaam mpaka usiku” [Al-Bukhaariy kutoka kwa Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه)].  Na pia hukmu ya kufunga Swawm ilipotolewa Waislamu walijizuia kujamiana na wake zao mwezi mzima, lakini baadhi ya watu walikuwa wakifanya khiyana (kuvunja shariy’ah) basi Allaah Akateremsha: Allaah Anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkijifanyia khiyana nafsi zenu, hivyo Akapokea tawbah yenu na Akakusameheni. Basi sasa waingilieni na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu…”

 

Sababun-Nuzuwl: Kuhusu kauli ya Allaah: Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe…. ni kwa sababu walikuwa baadhi ya Maswahaba wanaendelea tu kula huku wakiwa wamefunga nyuzi (kamba) mbili mguuni; mmoja mweusi na mmoja mweupe mpaka ibainike kuzitofautisha kwake nyuzi hizo. Allaah Akateremsha: (Ufafanuzi wa): mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku)”. [Al-Bukhaariy na Muslim; Hadiyth ya Sahl bin Sa’d  (رضي الله عنه)].

 

Faida: Maswahaba walitatanishwa na kushindwa kuelewa maana ya neno uzi mweupe kutokana na uzi mweusi”.  ‘Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Ilipoteremshwa Aayah: mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku)”, Nilichukua nyuzi moja nyeupe na moja nyeusi nikaweka chini ya mto wangu lakini haikunibainikia. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) asubuhi nikamwelezea. Akasema: “Hakika hiyo (imekusudiwa) ni kiza cha usiku na weupe wa Alfajiri” [Al-Bukhaariy Na Muslim].

 

[22] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka pale walipokuwa Answaar wa Madiynah wakienda Hajj na wakirejea wanapitia kwa nyuma ya majumba yao na hawakuwa wakiingia majumbani mwao kwa kupitia milangoni ya mbele ya majumba yao. Siku moja alikuja mtu mmoja akiwa ametoka Hajj akaingia kupitia mlango wa mbele wa nyumba yake akaaibishwa kwa ajili ya kitendo chake hicho. Hapo basi ikateremka hii Aayah: Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake, lakini wema ni kuwa na taqwa. Na ingieni majumbani kupitia milango yake…”  [Al-Bukhaariy, Muslim, Hadiyth ya Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه)].

 

[23] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kuhusu baadhi ya Maswahaba ambao walikusudia kurudi ili kutengeneza mashamba yao na mali zao na waache jihaad [At-Tirmidhiy kutoka kwa Abuu Ayyuwb (رضي الله عنه)].

Pia, imeteremka kwa wale ambao walikuwa wakijitolea swadaqah wanatoa vile ambavyo Ametaka Allaah (سبحانه وتعالى). Pindi walipopatwa na ukame, wakajizuia kutoa [Atw-Twabaraaniy kutoka kwa Abuu Jubayrah (رضي الله عنه)].

Pia, walikuwa baadhi yao akifanya madhambi husema: “Allaah Hatonisamehe mimi” [Atw-Twabaraaniy kutoka kwa Nu’maan (رضي الله عنه)].

 

[24] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka hali ya kuwa ni jawabu la swali aliloliuliza mtu mmoja: “Nini nitafanya katika ‘Umrah yangu?” Ikateremka kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah. Na kama mkizuilika…).” [Atw-Twabaraaniy kutoka kwa Ya’laa ibn Umayyah (رضي الله عنه)].

 

Sababun-Nuzuwl: Kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake (ikambidi anyoe); basi atoe fidia” mpaka mwisho wake, imeteremka kuhusu Swahaba Ka’ab Ibn ‘Ujrah kama alivyohadithia kwamba:  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama karibu yangu, na chawa walikuwa wakianguka kutoka kichwani mwangu. Akasema: “Je chawa wanakutatiza?” Nikasema Ndio. Akaniamrisha kichwa kinyolewe. Ka’ab Akasema: Aayah hii imeteremshwa kunihusu mimi. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniamrisha nifunge swawm siku tatu au kulisha masikini sita kwa faraq (Nusu ya pishi za tende au chakula kinginecho kwa kila maskini mmoja; jumla ni pishi tatu kwa maskini sita) au kuchinja kafara, kondoo au kilichopatikana wepesi.  [Al-Bukhaariy, Muslim kutoka kwa Ka’b (رضي الله عنه)].

 

[25] Sababun-Nuzuwl: Sababu ya kuteremka kauli ya Allaah: “Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa.”; Walikuwa watu wa Yemen wakienda Hajj hawachukui matumizi ya njiani na khatimae wanasema: “Sisi ni wenye kutawakali kwa Allaah.” Na wakiingia Makkah wakawa wanaanza kuombaomba watu. Hapo ikateremka Aayah. [Al-Bukhaariy kutoka kwa ‘Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)].

 

Faida: Kuhusu miezi ya Hajj; Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) alisema: Ni Shawwaal, Dhul-Qa’dah na siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah. [Fat-hul-Baariy (3/491)].

 

 

[26] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wenu”, imeteremka kuhusu Maswahaba kuwa waliona uzito kufanya biashara kwenye masoko yaliyokuwa yakitumika zama za Jaahiliyyah. Ndipo ikateremka hii Aayah. [Al-Bukhaariy kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)].

 

[27] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: “Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu;” imeteremka kuhusu Maquraysh kwa vile wao walikuwa wakimiminika kutokea Muzdalifah na hali ya kuwa watu wengineo wanamiminika kutokea ‘Arafah. Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaamrisha nao Maquraysh wamiminike kutokea ‘Arafah kama wafanyavyo wengineo. [Al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها)].

 

[28] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: Na miongoni mwa watu yuko anayeiuza nafsi yake kutafuta radhi za Allaah”, imeteremka kuhusu Suhayb (رضي الله عنه) pale alipotoka Makkah akiwa ni mwenye kuhamia Madiynah wakamfuata watu wa Makkah ili wamrejeshe. Alikuwa amewaacha vijakazi wawili Makkah, basi ili aachiwe kuhajiri kutoka Makkah kwenda Madiynah, aliwapatia hao waliomfuata vijakazi wawili hao. Hapo wakamuachia. [Imaam Al-Haakim kutoka kwa Anas (رضي الله عنه)].

 

 

 

 

[29] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremshwa pale 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) ambaye alikuwa mmoja wa Maswahaba aliyekuwa akilewa, siku moja alisema: Ee Rasuli wa Allaah, tupe hukmu kuhusu Al-khamr (pombe), hapo ikateremka Aayah: Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari…” (2: 291). Kisha ikafuatia Aayah (4: 43). Kisha ikaharamishwa kabisa katika Suwratul-Maaidah (5: 90). Rejea huko kupata maelezo bayana.

 

[30] Sababun-Nuzuwl: Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: Ilipoteremka Aayah: Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya ihsaan” na pia: “Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma… (4: 10), watu wakajiepusha na mali na chakula cha yatima. Ikawa ni ngumu kwao wakalalamika kwa Nabiy hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: “Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengeneza ni khayr…” (2: 220) [Swahiyh An-Nasaaiy (3671), Fathul-Baariy (5/463)].

 

[31] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara; basi waepukeni wanawake katika hedhi.” imeteremka kuhusu Mayahudi ambao walikuwa mwanamke akipatwa hedhi, walikuwa hawali nae chakula wala hawajumuiki nae katika majumba. Maswahaba wakamuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu jambo hilo, hapo ikateremka Aayah hii kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Fanyeni kila kitu isipokuwa jimai.”  [Muslim Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه)].

 

[32] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo.imeteremka kuhusu Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo ikateremka hii Aayah [Al-Bukhaariy, Muslim kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه)].

 

Pia, Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alisema kuwa kauli hiyo; Wanawake zenu ni konde kwenu iliteremshwa kuhusu baadhi ya watu wa Answaar ambao walikuja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamuuliza (kuhusu kumuingilia mwanamke kutokea upande wa nyuma) akawajibu: Muingilie vyovyote upendavyo madhali ni ukeni.” [Ahmad].

 

[33]  Sababun-Nuzuwl: Aayah hii “Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi…” (2: 225)  Imeteremshwa kutokana na vile mtu kuapa: “Hapana wa-Allaahi, Ndio wa-Allaah.” (Yaani kuapa apa kila mara) [Amehadithia Aaishah (رضي الله عنها) ameipokea Al-Bukhaariy].

 

[34] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao; basi msiwazuie kuolewa na waume zao (wa awali)…”imeteremka kuhusu Ma’aqil bin Yasaar (رضي الله عنه) kuwa alimuozesha dada yake kwa mwanaume kisha yule mwanaume akamtaliki, akakaa mpaka eda yake ikamalizika. Baada ya kumalizika eda, yule mwanaume akamchumbia tena huyo dada yake kwa Ma’aqil, lakini Ma’aqil alikataa ndio hapo ikateremka hii Aayah [Al-Bukhaariy kutoka kwa Ma’aqil (رضي الله عنه)].

 

[35] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri)... imeteremka kuhusu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali Swalaah ya Adhuhuri nusu ya mchana wakati jua linaposhtadi na ilikuwa ni Swalaah ngumu zaidi kwa Maswahaba (رضي الله عنهم). Mara nyingine ilikuwa haipatikani nyuma yake ispokuwa swaffu moja au mbili. Baada ya hali hiyo, ikateremka hii Aayah. [Ahmad kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه)].

 

Sababun-Nuzuwl: Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu” ni kwamba; walikuwa Maswahaba wakizungumza ndani ya Swalaah; mtu anamsemesha ndugu yake katika haja zake akiwa ndani ya Swalaah. Basi hapo ikateremka hii Aayah. [Al-Bukhaariy, Muslim kutoka kwa Zayd bin Arqam (رضي الله عنه)].

 

[36] An-Naasikh Wal-Mansuwkh: Wanachuoni wengi wamesema kuwa Aayah (2: 240) ilifutwa na Aayah (2: 234) kwa lile Alilosema Allaah. Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao (eda) miezi minne na siku kumi.” (2: 234) Mathalan Al-Bukhaariy alisimulia kuwa Ibn Az-Zubayr alisema: “Nilimwambia ‘Uthmaan bin ‘Affaan Aayah: “Na wale waliofishwa miongoni mwenu wakaacha wake, wawausie kwa ajili ya wake zao masurufu kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa” (2: 240) Ilifutwa na Aayah (2: 234), kwa hiyo kwanini basi uliikusanya (ndani ya Qur-aan)?  ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رضي الله عنه) akajibu:  Ee mpwa wangu! Sitobadili sehemu yoyote ya Qur-aan kutoka mahala pake.” [Fat-h Al-Baariy (8/48)].

 

[37] Faida: Aayah hii ndiyo Aayah adhimu kabisa katika Qur-aan kwa dalili ya Hadiyth ya Muslim (810) kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Rabaah Al-Answaariy kutoka kwa ‘Ubayy bin Ka’ab ambaye amehadithia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yaa Abal-Mundhir! Hivi unajua ni Aayah gani ndani ya Kitabu cha Allaah kuwa ni adhimu kabisa?” Akasema: Nikasema: Allaah na Rasuli Wake ni wajuzi zaidi. “Yaa Abal-Mundhir! Hivi unajua ni Aayah gani ndani ya Kitabu cha Allaah kuwa ni adhimu kabisa?” Akasema: Nikasema: Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu” (mpaka mwisho wa Aayah). Akasema Ubayy: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanipiga kifuani kisha akasema: “Wa-Allaahi upongezwe kwa ‘ilmu yako yaa Abal-Mundir.” [Muslim] na katika mapokezi ya Ahmad imeendelea: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, Aayah hii ina ulimi na midomo miwili ambao inamtukuza Mfalme (Allaah) katika mguu wa Arshi.” [Swahiyh Targhiyb (1471)].

 

Pia, Aayah hii ina Jina tukufu kabisa la Allaah katika kauli Yake (تعالى): ”Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu” na  dalili ni: Abuu Umaamah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  Jina Tukufu  kabisa la Allaah  Ambalo likiombewa kwalo Anaitikia limo katika Suwrah tatu; Al-Baqarah, Aal-‘Imraan, na Twaahaa’. [At-Tirmdhiy, Silsilah Asw-Swahiyhah (746)] Na mapokezi mengineyo yaliyothibitisha kuhusu Ismul-A’dhwam (Jina tukufu kabisa).

 

Kuhusu kauli ya Allaah (تعالى): ((Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi)) Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Iwapo mbingu saba na ardhi saba zingekunjuliwa na kulazwa sambamba, basi zingefikia kipimo cha (udogo wa) pete katika jangwa, kulinganisha na ‘Arsh.” [Ibn Abiy Haatim (3/981)].

 

[38] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: “Hapana kulazimisha katika Dini…” imeteremka kuhusu mwanamke ambaye alikuwa kila anapozaa mtoto wake hufariki. Basi mwanamke huyo akaweka nadhiri katika nafsi yake kwamba pindi akizaa na akaishi mtoto wake asife, atamfanya kuwa Yahudi. Na walipotolewa Mayahudi wa Baniy An-Nadhwiyr, kulikuwa katika wao kuna watoto wa Answaar. Kisha wakasema: “Hatuwaachi watoto wetu!” (Wakikusudia na mtoto huyo?)  Hapo ikateremeka Aayah hii [Ibn Jariyr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)].   

 

[39] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: “Enyi walioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma…” mpaka mwisho, imeteremka  kuhusu baadhi ya Maswahaba  ambao walikuwa wakileta chane au shada la tende kisha wanalitundika Msikitini. Pindi Swahaba yeyote katika Ahlus-Swufaa anapohitajia chakula anatungua tende iliyoiva na mbichi. Na hao Maswahaba waliokuwa wakileta tende Msikitini, walikuwa ni wale ambao wasiopenda kujitolea katika njia ya  khayr. Basi wakileta chane au shada la tende ambalo lina mchanganyiko wa tende ambazo hazikuiva kutokana na matatizo ya ulimaji  wa tende, na nyinginezo zilikuwa mbovu. Na wengine huleta chane au shada ambalo limekatika katika. Hapo ndipo ikateremka hii Aayah. [At-Tirmidhiy kutoka kwa Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه), na Taz. Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

Sababun-Nuzuwl pia: Ibn Jariyr alinukuu kuwa Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) alisema kuhusu sababu ya kuteremshwa hiyo Aayah: “Iliteremeshwa kuwahusu Answaar. Msimu wa kuvuna tende kila ulipowadia, Answaar walikusanya tende mbivu katika bustani zao na kuzitundika kwenye kamba iliyofungwa kati ya nguzo mbili ndani ya Masjid ya Rasuli wa Allaah. Masikini katika Muhaajiruwn walikuwa wakila tende hizo. Hata hivyo, baadhi ya Answaar waliweka tende duni katika tende mbivu zilizokomaa, walidhani kwamba iliruhusiwa kufanya hivyo, ndipo Allaah Alipoteremsha Aayah hii juu ya wale waliofanya hivyo. [Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

[40] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: “Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa…” imeteremka kuhusu Maswahaba walikuwa hawawapi hata kidogo ndugu zao wa karibu katika Washirikina, basi hapo ikateremka: Wale wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata Aliyoyaamrisha Allaah kuungwa...” (2: 27). [Ibn Jariyr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)].

 

[41] Faida: Ilipoteremka Aayah Namba (2: 275) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema; “Yeyote asiyejizuia kufanya mukhaabarah (kukodisha shamba kwa malipo ya kugawana sehemu ya mazao) basi apokee tangazo la vita kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

[42] Faida: Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنه) amesema kuwa hii ni Aayah ya mwisho kuteremshwa ndani ya Qur-aan [An-Nasaaiy – Tafsiyr Ibn Kathiyr].

[43] An-Naasikh Wal-Mansuwkh: Aayah hii imefutwa hukmu yake, kwa Aayah iliyoifuata ambayo ni Aayah ya mwishoni mwa hii Suwrah.

 

[44] Sababun-Nuzuwl: Aayah hii na inayofuatia imeteremka kwa sababu, pale ilipotoremka Aayah iliyotangulia;  “…Na mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha; basi Allaah Atakuhesabuni kwayo… (2: 284), ilikuwa ngumu mno kwa Maswahaba, wakaogopa mno kuhusu kuhesabiwa vinavyofichika moyoni Basi hukmu hii ilikuwa ngumu mno kwa Maswahaba. Wakakaa kitako wakiwa wameegemea magoti yao wakasema: Ee Rasuli wa Allaah!  Tumeamrishwa ‘amali tunazoziweza kama Swalaah, Swiyaam, jihaad, swadaqah, lakini imeteremka kwako Aayah hii wala hatuiwezi! Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Je mnataka kusema kama walivyosema Ahlul-Kitaab walio kabla yenu waliosema: Tumesikia na tumeasi? Bali semeni: “Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia.” Basi walipoizoea katika ndimi zao, hapo Allaah Akateremsha: Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia)…. Mpaka mwisho. Kisha walipofanya hivyo, Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha: “Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake…” mpaka mwisho (2: 286) [Muslim kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) na mfano wake kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)].

 

[45] Faida: Abuu Mas‘uwd Al-Answaariyy ‘Uqbah bin ‘Amr bin Tha’labah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesoma usiku Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah zitamtosheleza.” Yaani: zinamtosheleza kumkinga na kila baya na lenye kumdhuru. [Al-Bukhaariy na  Muslim].

 

Imaam Muslim amenukuu katika Swahiyh yake kuwa Aayah hizi mbili alipewa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika kikomo mbingu ya saba katika Safari ya Al-Israa Wal-Mi’raaj pamoja na kupewa Swalaah tano na msamaha kwa mtu asiyemshirkisha Allaah na yeyote au chochote.

 

Share

003 - Aal-'Imraan

 

آل عِمْران

Aal-‘Imraan: 3[1]

Imeteremka Madiynah Kwa Ijmaa’

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

الم ﴿١﴾

1. Alif Laam Miym.

 

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﴿٢﴾

2. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliye hai daima, Msimamia kila kitu.

 

 

 

 نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٣﴾

3. Amekuteremshia Kitabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki kinachosadikisha yaliyo kabla yake na AkateremshaTawraat na Injiyl.

 

 

 

 

مِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ الْفُرْقَانَ ۗ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤﴾

4. Kabla (ya kuteremshwa Qur-aan), iwe ni mwongozo kwa watu na Akateremsha Furqaan (upambanuo). Hakika wale waliokufuru Aayaat za Allaah watapata adhabu kali. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kuangamiza.

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ﴿٥﴾

5. Hakika Allaah Hakifichiki Kwake chochote katika ardhi wala katika mbingu. 

 

 

 هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦﴾

6. Yeye Ndiye Aliyekusawirini umbo katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.[2]

 

 

 

 

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٧

7. Yeye Ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu humo mna Aayaat zenye maana wazi, hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo zisizokuwa wazi maana zake. Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu hufuata zile zisizokuwa wazi maana zake kutafuta fitnah (upotofu) na kutafuta maana zake zilofichika, na hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah. Na wenye msingi madhubuti katika elimu husema: “Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Rabb wetu.” Na hawakumbuki ila wenye akili.[3]

 

 

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٨﴾

8. (Husema): “Rabb wetu, Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kuwa Umetuhidi na Tutunukie kutoka kwako rahmah. Hakika Wewe ni Mwingi wa kutunuku na kuneemesha.”

 

 

رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿٩﴾ 

9. “Rabb wetu! Hakika Wewe ni Mkusanyaji watu Siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika Allaah Havunji miadi.”

 

 

 

 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمْ وَقُودُ النَّارِ ﴿١٠﴾

10. Hakika wale waliokufuru hazitowafaa kitu mali zao na wala watoto wao mbele ya Allaah, na hao ndio kuni za moto.

 

 

كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١١﴾

11. Kama mwenendo wa watu wa Fir’awn na wale waliokuwa kabla yao. Wamekadhibisha Aayaat Zetu basi Allaah Aliwaadhibu kwa madhambi yao, na Allaah ni Mkali wa kuakibu.

 

 

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا سَتُغْلَبُونَ وَتُحْشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ ۚ وَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿١٢

12. Waambie waliokufuru: “Mtashindwa na mtakusanywa katika Jahannam, na ni pabaya mno mahala hapo pa kupumzika.”

 

 

 

 قَدْ كَانَ لَكُمْ آيَةٌ فِي فِئَتَيْنِ الْتَقَتَا ۖ فِئَةٌ تُقَاتِلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَأُخْرَىٰ كَافِرَةٌ يَرَوْنَهُم مِّثْلَيْهِمْ رَأْيَ الْعَيْنِ ۚ وَاللَّـهُ يُؤَيِّدُ بِنَصْرِهِ مَن يَشَاءُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّأُولِي الْأَبْصَارِ ﴿١٣﴾

13. Kwa hakika ilikuwa ni Aayah (ishara) kwenu katika makundi mawili; yalipokutana (vita vya Badr). Kundi linapigana katika njia ya Allaah na jingine ni makafiri ambao wanawaona (Waislamu) mara mbili yao kwa mtazamo wa macho. Na Allaah Humsaidia kwa nusura Yake Amtakaye. Hakika katika hayo bila shaka ni zingatio kwa wenye utambuzi.

 

 

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ ﴿١٤﴾

14. Watu wamepambiwa huba ya matamanio miongoni mwa wanawake, na watoto, na mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa ya aina bora na wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni starehe za uhai wa dunia, na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri.

 

 

 قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ ۚ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿١٥﴾

15. Sema: “Je, nikujulisheni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wale waliokuwa na taqwa kwa Rabb wao watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo na wake waliotakasika na radhi kutoka kwa Allaah. Na Allaah ni Mwenye kuwaona waja.”

 

 

الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ﴿١٦﴾ 

16. Wale wasemao: “Rabb wetu, hakika sisi tumeamini, basi Tughufurie madhambi yetu na Tukinge na adhabu ya moto.”

 

 

 الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ﴿١٧﴾

17. Wenye kusubiri na wasemao kweli, na watiifu, na watoaji mali katika njia ya Allaah na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri.

 

 

 

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

18. Allaah Ameshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye; na (pia) Malaika na wenye elimu (kwamba Allaah) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

 

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ۗ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللَّـهِ فَإِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩﴾

19. Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu. Na hawakukhitilafiana wale waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia elimu kwa kufanyiana baghi na uhusuda baina yao. Na atakayekanusha Aayaat za Allaah basi hakika Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu.

 

 

 فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّـهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ ۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْأُمِّيِّينَ أَأَسْلَمْتُمْ ۚ فَإِنْ أَسْلَمُوا فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠﴾

20. Na wakikuhoji, basi sema: “Nimejisalimisha kwa Allaah na ambao walionifuata” Na waambie waliopewa Kitabu na wasiojua kusoma na kuandika: “Je, mmesilimu?” Wakisilimu basi wameongoka, na wakikengeuka basi hakika juu yako ni kubalighisha. Na Allaah ni Mwenye kuwaona waja.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ الَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِالْقِسْطِ مِنَ النَّاسِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢١﴾ 

21. Hakika waliokanusha Aayaat za Allaah na wakaua Manabii bila ya haki, na wakaua wale wanaoamrisha haki miongoni mwa watu, basi wabashirie adhabu iumizayo.

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٢٢﴾

22. Hao ni wale ambao zimeporomoka ‘amali zao katika dunia na Aakhirah na hawatopata yeyote mwenye kuwanusuru.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُدْعَوْنَ إِلَىٰ كِتَابِ اللَّـهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ وَهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٢٣﴾ 

23. Je, hukuzingatia wale waliopewa sehemu katika Kitabu wanaitwa katika Kitabu cha Allaah ili kiwahukumu baina yao; kisha kundi miongoni mwao linageuka na huku wanapuuza.

 

 

 ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۖ وَغَرَّهُمْ فِي دِينِهِم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤﴾

24. Hivyo ni kwa sababu wamesema: “Hautotugusa moto isipokuwa siku chache za kuhesabika.” Na yakawadanganya katika dini yao yale waliyokuwa wakiyazua.

 

 

فَكَيْفَ إِذَا جَمَعْنَاهُمْ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ وَوُفِّيَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٥﴾

25. Basi itakuwa vipi Tutakapowakusanya katika Siku ambayo haina shaka ndani yake, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyochuma; nao hawatodhulumiwa.

 

 

قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٦﴾

26. Sema: “Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, khayr imo Mkononi Mwako.  Hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 

 تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۖ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ ۖ وَتَرْزُقُ مَن تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢٧﴾

27. Unauingiza usiku katika mchana na Unauingiza mchana katika usiku; na Unatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu na Unatoa kilicho mfu kutokana na kilicho hai na Unamruzuku Umtakaye bila ya hesabu.

 

 

لَّا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّـهِ فِي شَيْءٍ إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ الْمَصِيرُ ﴿٢٨﴾ 

28. Waumini hawawafanyi makafiri kuwa marafiki wandani badala ya Waumini. Na atakayefanya hivyo, basi hatokua na chochote mbele ya Allaah, isipokuwa mkiwa mnaogopa khatari kutoka kwao. Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi yake. Na kwa Allaah ni mahali pa kuishia.

 

 

 قُلْ إِن تُخْفُوا مَا فِي صُدُورِكُمْ أَوْ تُبْدُوهُ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَيَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٩﴾

29. Sema: “Mkificha yale yaliyomo katika vifua vyenu au mkiyafichua, Allaah Anayajua. Na Anajua yale yaliyomo katika mbingu na yale yaliyomo katika ardhi. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 

يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُّحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِن سُوءٍ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ أَمَدًا بَعِيدًا ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٣٠﴾

30. Siku itayokuta kila nafsi yale iliyoyatenda katika khayr yamehudhurishwa, na yale iliyoyatenda katika maovu, itatamani nafsi lau kama ingelikuwa baina yake na baina hayo (maovu) masafa ya mbali. Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi yake. Na Allaah ni Raufu mno kwa waja.

 

 

 قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.”[4]

 

 

قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴿٣٢﴾

32. Sema: “Mtiini Allaah na Rasuli, lakini mkikengeuka basi hakika Allaah Hapendi makafiri.”

 

 

إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٣٣﴾

33. Hakika Allaah Amemkhitari Aadam na Nuwh na kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha ‘Imraan juu ya walimwengu.

 

 

 ذُرِّيَّةً بَعْضُهَا مِن بَعْضٍ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٣٤﴾

34. Kizazi cha wao kwa wao na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

 

إِذْ قَالَتِ امْرَأَتُ عِمْرَانَ رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٣٥﴾ 

35. Pale aliposema mke wa ‘Imraan: “Rabb wangu, hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kilichomo katika tumbo langu kuwa ni wakfu kukutumikia, basi nitakabalie. Hakika wewe ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

 فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنثَىٰ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ ۖ وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ ﴿٣٦﴾

36. Basi alipomzaa akasema: “Rabb wangu, hakika mimi nimezaa mwanamke,” na Allaah Anajua zaidi alichokizaa. “Na mwanamme si kama mwanamke. Nami nimemwita Mayram nami namkinga Kwako na dhuria wake kutokana na shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.

 

 

فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا ۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا ۖ قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا ۖ قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٧﴾ 

37. Basi Rabb wake Akampokea kwa kabuli njema na Akamkuza mkuzo mzuri na Akamfanya Zakariyyaa kuwa mlezi wake. Kila Zakariyyaa alipoingia kwake katika chumba cha kuswalia alikuta kwake kuna riziki Akasema: “Ee Maryam! Umepata wapi hivi? ”Akasema: “Hivi ni kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah Anamruzuku Amtakaye bila ya hesabu.”

 

 

 هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٨﴾

38. Hapo hapo Zakariyyaa akamwomba Rabb wake, akasema: “Rabb wangu Nitunukie kutoka Kwako kizazi chema hakika Wewe ni Mwenye kusikia du’aa yangu.”

 

فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًا بِكَلِمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٣٩﴾

39. Basi mara Malaika akamwita (Zakariyyaa) naye akiwa amesimama anaswali katika chumba kwamba: “Hakika Allaah Anakubashiria Yahyaa mwenye kusadikisha Neno (la Kun!) kutoka kwa Allaah na ni mwenye sharaf, busara na taqwa, na anayejitenga mbali na matamanio na Nabiy miongoni mwa Swalihina.”[5]

 

 

قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَقَدْ بَلَغَنِيَ الْكِبَرُ وَامْرَأَتِي عَاقِرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكَ اللَّـهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ﴿٤٠﴾

40. (Zakariyyaa) Akasema: “Nitapataje ghulamu na hali uzee umeshanifikia na mke wangu ni tasa?!” Akasema: “Hivyo ndivyo Allaah Anafanya Atakavyo”

 

 

قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً ۖ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمْزًا ۗ وَاذْكُر رَّبَّكَ كَثِيرًا وَسَبِّحْ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ ﴿٤١﴾ 

41. (Zakariyyaa) Akasema: “Rabb wangu niwekee Aayah (ishara)” Akasema: Ishara yako ni kwamba hutoweza kuwasemesha watu siku tatu ila kwa kuashiria tu. Na mdhukuru Rabb wako kwa wingi na msabihi jioni na asubuhi.”

 

 

وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَاكِ عَلَىٰ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ ﴿٤٢

42. Na pale Malaika waliposema: “Ee Maryam! Hakika Allaah Amekuteua na Amekutakasa na Amekukhitari juu ya wanawake wa walimwengu.”

 

 

 يَا مَرْيَمُ اقْنُتِي لِرَبِّكِ وَاسْجُدِي وَارْكَعِي مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾

43. “Ee Maryam!  Kuwa mtiifu kwa Rabb wako, na sujudu, na rukuu pamoja na wanaorukuu.”

 

 

ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۚ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يُلْقُونَ أَقْلَامَهُمْ أَيُّهُمْ يَكْفُلُ مَرْيَمَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يَخْتَصِمُونَ ﴿٤٤﴾ 

44. Hizo ni khabari za ghayb Tunakufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).  Na hukuwa pamoja nao walipotupa kalamu zao, ili nani kati yao amlee Maryam. Na hukuwa pamoja nao walipokhasimiana.

 

 

 

 إِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na pale Malaika waliposema: “Ee Maryam! Hakika Allaah Anakubashiria Neno (la Kun!) kutoka Kwake (umzae mtoto), jina lake ni Al-Masiyhu ‘Iysaa mwana wa Maryam, mwenye taadhima katika dunia na Aakhirah na ni miongoni mwa waliokurubishwa (kwa Allaah).

 

 

وَيُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا وَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٤٦﴾

46. Na Atawasemesha watu katika utoto wake na utu uzima wake na ni miongoni mwa Swalihina.

 

 

قَالَتْ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكِ اللَّـهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٤٧﴾

47. (Maryam) Akasema: “Itakuwaje nipate mtoto na hali hakunigusa mtu?” (Malaika) Akasema: “Hivyo ndivyo Allaah Huumba Akitakacho. Anapokidhia jambo basi huliambia: "Kun!" (Kuwa!) Basi nalo huwa.

 

 

 وَيُعَلِّمُهُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٤٨﴾

48. Na Atamfunza Kitabu na Hikmah na Tawraat na Injiyl.

 

 

 وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنِّي قَدْ جِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ أَنِّي أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٤٩﴾

49. Na ni Rasuli kwa wana wa Israaiyl (akisema): “Hakika mimi nimekujieni na Aayah (ishara, dalili) kutoka kwa Rabb wenu, kwamba mimi nakuundieni kutokana na udongo kama umbo la ndege, kisha napuliza humo basi huwa ndege kwa idhini ya Allaah. Na naponyesha vipofu na wenye ubarasi na nahuisha wafu kwa idhini ya Allaah. Na nakujulisheni mtakavyokula na mtakavyoweka akiba majumbani mwenu. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayah kwenu mkiwa Waumini.

 

 

 وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعْضَ الَّذِي حُرِّمَ عَلَيْكُمْ ۚ وَجِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿٥٠﴾

50. Na mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale yaliyoharamishwa kwenu. Na nimekujieni na Aayah (ishara, hoja) kutoka kwa Rabb wenu. Basi mcheni Allaah na nitiini.

 

 إِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۗ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٥١﴾

51. Hakika Allaah ni Rabb wangu na Rabb wenu basi mwabuduni. Hii ndio njia iliyonyooka.”

 

 

 فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٥٢﴾

52. Basi alipohisi ‘Iysaa ukafiri kutoka kwao; alisema: “Nani wanusuruji wangu kwa ajili ya Allaah? Wakasema wafuasi watiifu:  “Sisi ni wasaidizi wa Allaah. Tumemwamini Allaah na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu (tunajisalimisha Kwake).”

 

 

رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلْتَ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٥٣﴾

53. “Rabb wetu, tumeamini Uliyoyateremsha na tumemfuata Rasuli basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (haki).”

 

 

وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ ﴿٥٤﴾

54.  Wakapanga makri lakini Allaah Akapanga kulipiza makri. Na Allaah ni Mbora wa kulipiza mipango ya makri.[6]

 

 

إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا وَجَاعِلُ الَّذِينَ اتَّبَعُوكَ فَوْقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۖ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأَحْكُمُ بَيْنَكُمْ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٥٥﴾ 

55.  Pale Allaah Aliposema: “Ee ‘Iysaa, hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua usingizini na Mwenye kukupandisha Kwangu na Mwenye kukutakasa kutokana na wale waliokufuru na Nitawafanya wale waliokufuata (kujisalimisha kwa Allaah) kuwa juu ya wale waliokufuru mpaka Siku ya Qiyaamah, kisha Kwangu ndio marejeo yenu Nitahukumu baina yenu katika yale mliyokuwa kwayo mkikhitilafiana.”[7]

 

 

فَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَأُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٥٦﴾

56. Basi wale waliokufuru, Nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Aakhirah, na hawatopata yeyote mwenye kunusuru.

 

 

وَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ ﴿٥٧﴾

57. Ama wale waliomini na wakatenda mema, basi Atawalipa ujira wao kikamilifu. Na Allaah Hapendi madhalimu.

 

 

ذَٰلِكَ نَتْلُوهُ عَلَيْكَ مِنَ الْآيَاتِ وَالذِّكْرِ الْحَكِيمِ ﴿٥٨﴾

58. Hizo Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika Aayaat na ukumbusho wenye hikmah.

 

 

 

إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّـهِ كَمَثَلِ آدَمَ ۖ خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٥٩﴾

59. Hakika mfano wa ‘Iysaa kwa Allaah ni kama mfano wa Aadam. Amemuumba kutokana na udongo kisha Akamwambia: “Kun!”, basi akawa.

 

 

الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُن مِّنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿٦٠﴾

60. Haki kutoka kwa Rabb wako, basi usiwe miongoni mwa wanaotia shaka.

 

 

 

 

فَمَنْ حَاجَّكَ فِيهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ فَقُلْ تَعَالَوْا نَدْعُ أَبْنَاءَنَا وَأَبْنَاءَكُمْ وَنِسَاءَنَا وَنِسَاءَكُمْ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَتَ اللَّـهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ ﴿٦١﴾

61. Basi yeyote atakayekuhoji kwayo baada ya kukujia elimu, basi sema: “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu, na nafsi zenu, kisha tuombe mubaahalah, tuifanye laana ya Allaah iwe juu ya waongo.[8]

 

 

 إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْقَصَصُ الْحَقُّ ۚ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦٢﴾

62. Hakika haya ni masimulizi ya haki. Na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah. Na hakika Allaah Yeye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

 

فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِالْمُفْسِدِينَ ﴿٦٣﴾

63. Wakikengeuka, basi hakika Allaah ni Mjuzi wa mafisadi.

 

 

 قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾

64. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine kuwa miola badala ya Allaah.” Wakikengeuka; basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu.”

 

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تُحَاجُّونَ فِي إِبْرَاهِيمَ وَمَا أُنزِلَتِ التَّوْرَاةُ وَالْإِنجِيلُ إِلَّا مِن بَعْدِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٥﴾

65. Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwanini mnahojiana kuhusu Ibraahiym na hali haikuteremshwa Tawraat na Injiyl isipokuwa baada yake? Je, hamtii akilini?

 

 

هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ حَاجَجْتُمْ فِيمَا لَكُم بِهِ عِلْمٌ فَلِمَ تُحَاجُّونَ فِيمَا لَيْسَ لَكُم بِهِ عِلْمٌ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٦﴾

66. Ha! Nyinyi ndio hawa mliohojiana katika yale ambayo mnayo elimu nayo, basi kwa nini mnahojiana katika yale msiyokuwa na elimu nayo? Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.

 

 

 

مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٦٧﴾

67. Hakuwa Ibraahiym Yahudi wala Naswara; lakini alikuwa mwenye kujiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki, Muislamu na hakuwa miongoni mwa washirikna.

 

 

إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٦٨﴾

68. Hakika watu walio karibu zaidi kwa Ibraahiym ni wale waliomfuata na huyu Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini. Na Allaah ni Mlinzi na Msaidizi wa Waumini.

 

 

 

 

وَدَّت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يُضِلُّونَكُمْ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٦٩﴾ 

69. Linatamani kundi katika Ahlil-Kitaabi kama wangelikupotezeni, lakini hawapotezi ila nafsi zao na hawahisi.

 

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ ﴿٧٠﴾

70. Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwanini mnakanusha Aayaat za Allaah na hali nyinyi mnashuhudia?

 

 

 يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَلْبِسُونَ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٧١﴾

71. Enyi Ahlal-Kitaabi!  Kwanini mnachanganya haki na batili na mnaficha haki na hali nyinyi mnajua?

 

 

وَقَالَت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ آمِنُوا بِالَّذِي أُنزِلَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَجْهَ النَّهَارِ وَاكْفُرُوا آخِرَهُ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٧٢﴾

72. Na kundi miongoni mwa Ahlil-Kitaabi likasema (kuambiana): “Aminini yale ambayo yameteremshwa kwa wale walioamini mwanzo wa mchana na kanusheni mwisho wake, wapate kurejea (waache dini yao).”

 

 

وَلَا تُؤْمِنُوا إِلَّا لِمَن تَبِعَ دِينَكُمْ قُلْ إِنَّ الْهُدَىٰ هُدَى اللَّـهِ أَن يُؤْتَىٰ أَحَدٌ مِّثْلَ مَا أُوتِيتُمْ أَوْ يُحَاجُّوكُمْ عِندَ رَبِّكُمْ ۗ قُلْ إِنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٧٣﴾ 

73. “Na wala msimwamini isipokuwa yule anayefuata dini yenu.” Sema: “Hakika mwongozo wa kweli ni mwongozo wa Allaah, (mnakhofu) kwamba atapewa mmoja (elimu) mfano wa yale mliyopewa au wakuhojini mbele ya Rabb wenu” Sema: “Hakika fadhila zi Mkononi mwa Allaah; Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.

 

 

يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٧٤﴾

74. Humchagua kwa rahmah Yake Amtakaye; na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.

 

 

وَمِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مَنْ إِن تَأْمَنْهُ بِقِنطَارٍ يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ وَمِنْهُم مَّنْ إِن تَأْمَنْهُ بِدِينَارٍ لَّا يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ إِلَّا مَا دُمْتَ عَلَيْهِ قَائِمًا ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَيْسَ عَلَيْنَا فِي الْأُمِّيِّينَ سَبِيلٌ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾

75. Na katika Ahlil-Kitaab yuko ambaye ukimpa amana ya mrundi wa mali atakurejeshea, na katika wao yuko ambaye ukimpa amana ya dinari moja tu hatoirudisha kwako isipokuwa utakapodumisha kumsimamia (kumdai). Hilo ni kwa sababu wao wamesema: “Hakuna juu yetu lawama kwa wasiojua kusoma na kuandika” na wanamsingizia uongo Allaah, na hali wao wanajua.

 

بَلَىٰ مَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ وَاتَّقَىٰ فَإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ ﴿٧٦﴾

76. Bali ndio! Atakayetimiza ahadi yake akawa na taqwa, basi hakika Allaah Anapenda wamchao Allaah.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٧﴾

77. Hakika wale wanaobadilisha ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo; hao hawana sehemu yoyote katika Aakhirah na wala Allaah Hatowasemesha na wala Hatowatazama Siku Ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa na watapata adhabu iumizayo.[9]

 

 

 وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًا يَلْوُونَ أَلْسِنَتَهُم بِالْكِتَابِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ الْكِتَابِ وَمَا هُوَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٨﴾

78. Na hakika miongoni mwao kuna kundi wanaopotosha Kitabu kwa ndimi zao (wanaposoma) ili mdhanie kuwa hayo ni yanayotoka katika Kitabu, na hali hayo si yenye kutoka katika Kitabu, na wanasema: “Hayo ni kutoka kwa Allaah”; na hali hayo si kutoka kwa Allaah na wanamsingizia uongo Allaah na wao wanajua.

 

 

مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤْتِيَهُ اللَّـهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِّي مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ ﴿٧٩﴾

79. Ni mustahili kwa mtu kwamba Allaah Amempa Kitabu na Al-Hukma na Unabii kisha awaambie watu: “Kuweni wenye kuniabudu mimi badala ya Allaah” Bali (atawaambia): “Kuweni Wanachuoni waswalihina kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyadurusu.”[10]

 

وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُم بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨٠﴾ 

80. Na wala hakuamuruni kuwachukua Malaika na Manabii kuwafanya miola. Je, anakuamrisheni ukafiri baada ya nyinyi kuwa mmejisalimisha kwa Allaah?

 

 

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨١﴾

81. Na pindi Alipochukua Allaah fungamano kwa Manabii (akawaambia) “Kwa yale niliyokupeni kutoka kitabu na hikmah, kisha akakujieni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi; ni juu yenu kumwamini na kumnusuru.” (Kisha Allaah): Akasema “Je, mmekiri na mmekubali kuchukua juu ya hayo fungamano zito Langu?” Wakasema: “Tumekiri.” (Allaah) Akasema: “Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia.[11]

 

 

فَمَن تَوَلَّىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٨٢﴾

82. Basi atakayekengeuka baada ya hayo, basi hao ni mafasiki.

 

 

أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾

83. Je, wanataka dini isiyokuwa ya Allaah, na hali amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi akipenda asipende na Kwake watarejeshwa.

 

 

قُلْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَالنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿٨٤﴾

84. Sema: “Tumemwamini Allaah, na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym, na Ismaa’iyl na Is-haaq, na Ya’quwb na Al-Asbaatw na yale aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na Manabii kutoka kwa Rabb wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao, nasi ni Waislamu (tunajisalimisha) Kwake.”[12]

 

 

 وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

85. Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.[13]

 

 

 

 

كَيْفَ يَهْدِي اللَّـهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٦﴾ 

86. Vipi Allaah Atawaongoza watu waliokufuru baada ya kuamini kwao na wakashuhudia kwamba Rasuli ni haki na zikawajia hoja bayana? Na Allaah Hawaongozi watu madhalimu.[14]

 

 

 أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُمْ أَنَّ عَلَيْهِمْ لَعْنَةَ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿٨٧﴾

87. Hao jazaa yao ni kwamba juu yao ipo laana ya Allaah na ya Malaika na ya watu wote.

 

 

خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٨٨﴾

88. Wenye kudumu humo hawatopunguziwa adhabu wala hawatopewa muda wa kuakhirishwa adhabu.

 

 

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٨٩﴾

89. Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengenea, basi hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ ﴿٩٠﴾ 

90. Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru; haitokubaliwa tawbah yao, na hao ndio waliopotoka.[15]

 

 

 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾

91. Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao dhahabu ya ujazo wa dunia nzima lau wakitaka kujifidia nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru.

 

 

 لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٩٢﴾

92. Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachotoa basi hakika Allaah kwacho ni Mjuzi.

 

 

 كُلُّ الطَّعَامِ كَانَ حِلًّا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ إِلَّا مَا حَرَّمَ إِسْرَائِيلُ عَلَىٰ نَفْسِهِ مِن قَبْلِ أَن تُنَزَّلَ التَّوْرَاةُ ۗ قُلْ فَأْتُوا بِالتَّوْرَاةِ فَاتْلُوهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٣﴾

93. Kila chakula kilikuwa halali kwa wana wa Israaiyl, isipokuwa kile alichojiharamishia Israaiyl (Ya’quwb) mwenyewe kabla ya kuteremshwa Tawraat. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Basi leteni Tawraat kisha muisome mkiwa wakweli.”

 

 

 

فَمَنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٩٤﴾

94. Na yeyote atakayemtungia Allaah uongo baada ya hayo; basi hao ndio madhalimu.

 

 

قُلْ صَدَقَ اللَّـهُ ۗ فَاتَّبِعُوا مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٩٥﴾

95. Sema: “Allaah Amesema kweli.” Basi fuateni millah (Dini) ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.

 

 

إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾ 

96. Hakika nyumba ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ‘ibaadah) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah), yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu.

 

 

فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا ۗ وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾ 

97. Ndani yake kuna Aayaat (ishara, dalili) zilizo wazi; mahali pa kisimamo cha Ibraahiym. Na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah ni Mkwasi kwa walimwengu.

 

 

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَاللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعْمَلُونَ ﴿٩٨﴾ 

98. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwa nini mnakanusha Aayaat za Allaah; na hali Allaah ni Shahiyd juu ya myatendayo?”

 

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ تَبْغُونَهَا عِوَجًا وَأَنتُمْ شُهَدَاءُ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٩٩﴾ 

99. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Kwanini mnamzuilia aliyeamini njia ya Allaah mnaitafutia ionekane kombo na hali nyinyi mashahidi (juu ya haki)? Na Allaah si Mwenye kughafilika kuhusu myatendayo.”

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تُطِيعُوا فَرِيقًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ يَرُدُّوكُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ كَافِرِينَ ﴿١٠٠﴾

100. Enyi walioamini! Mkilitii kundi la waliopewa Kitabu watakurudisheni baada ya kuamini kwenu muwe makafiri.

 

 

وَكَيْفَ تَكْفُرُونَ وَأَنتُمْ تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ آيَاتُ اللَّـهِ وَفِيكُمْ رَسُولُهُ ۗ وَمَن يَعْتَصِم بِاللَّـهِ فَقَدْ هُدِيَ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٠١﴾

101. Na vipi mkufuru na hali mnasomewa Aayaat za Allaah na Rasuli yuko kati yenu? Na atakayeshikamana na Allaah basi kwa yakini ameongozwa kuelekea njia iliyonyooka.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٠٢﴾

102. Enyi walioamini! Mcheni Allaah kama ipasavyo kumcha na wala msife isipokuwa nyinyi (mmeshakuwa) ni Waislamu.[16]

 

 

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٠٣﴾ 

103. Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Allaah juu yenu, pale mlipokuwa maadui (kati yenu); kisha Akaunganisha nyoyo zenu, mkawa kwa neema Yake ndugu; na mlikuwa ukingoni mwa shimo la moto Akakuokoeni humo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat Zake mpate kuongoka.

 

 

 

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفلِحُونَ ﴿١٠٤﴾

104. Na watokeze kutoka kwenu umati wa watu unaolingania khayr na unaoamrisha mema na unaokataza munkari. Na hao ndio waliofaulu.

 

 

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٠٥﴾

105. Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na wakakhitilafiana baada ya kuwajia hoja bayana. Na hao watapata adhabu kuu.

 

 

 

يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ اسْوَدَّتْ وُجُوهُهُمْ أَكَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿١٠٦﴾ 

106. Siku nyuso zitakuwa nyeupe na nyuso (nyingine) zitakuwa nyeusi. Basi wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi (wataambiwa): “Je, mlikufuru baada ya kuamini kwenu?!  Basi onjeni adhabu kwa yale mliyokuwa mkikufuru.”

 

 

 وَأَمَّا الَّذِينَ ابْيَضَّتْ وُجُوهُهُمْ فَفِي رَحْمَةِ اللَّـهِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١٠٧﴾

107. Na wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe; basi watakuwa katika rahmah ya Allaah. Wao humo ni wenye kudumu.

 

 

تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۗ وَمَا اللَّـهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٨﴾

108. Hizi ni Aayaat za Allaah Tunakusomea kwa haki (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na Allaah Hataki dhulma kwa walimwengu.

 

 

 

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿١٠٩﴾

109. Na ni vya Allaah vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na kwa Allaah Pekee mambo (yote) yatarejeshwa.

 

 

 كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾

110. Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki.[17]

 

 

لَن يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى ۖ وَإِن يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ ﴿١١١﴾

111. Hawatokudhuruni isipokuwa udhia tu, na wakikupigeni vita watakupeni migongo, kisha hawatonusuriwa.

 

 

ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِّنَ اللَّـهِ وَحَبْلٍ مِّنَ النَّاسِ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الْمَسْكَنَةُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿١١٢﴾ 

112. Wamepigwa na udhalili, popote wanapopatikana isipokuwa kwa ahadi ya (hifadhi ya) Allaah na ya watu, na wakastahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah, na wakapigwa na umasikini. Hivyo kwa kuwa walikuwa wakikanusha Aayaat (ishara) za Allaah; na wakiua Manabii pasi na haki. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wanataadi.

 

 

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾

113. Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).[18]

 

 

يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٤﴾

114. Wanamwamini Allaah na Siku ya Mwisho na wanaamrisha mema na wanakataza munkari na wanakimbilia katika mambo ya khayr, na hao ni miongoni mwa Swalihina.

 

 

وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَن يُكْفَرُوهُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ ﴿١١٥﴾

115. Na khayr yoyote waifanyayo hawatokanushiwa (thawabu zake).  Na Allaah ni Mjuzi wa wenye taqwa.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۚ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١١٦﴾

116.  Hakika wale waliokufuru hazitowafaa kitu mali zao na wala watoto  wao mbele ya Allaah; na hao ni watu wa motoni wao humo ni wenye kudumu.

 

 

 

مَثَلُ مَا يُنفِقُونَ فِي هَـٰذِهِ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَثَلِ رِيحٍ فِيهَا صِرٌّ أَصَابَتْ حَرْثَ قَوْمٍ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ فَأَهْلَكَتْهُ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ اللَّـهُ وَلَـٰكِنْ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿١١٧﴾ 

117. Mfano wa vile wanavyovitoa katika uhai (wao) huu wa duniani ni kama mfano wa upepo ndani yake mna baridi ya barafu, ukasibu shamba lilolimwa la watu waliojidhulumu nafsi zao ukaliangamiza. Na Allaah Hakuwadhulumu lakini wamejidhulumu nafsi zao.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١١٨﴾

118. Enyi walioamini! Msifanye rafiki wandani na msiri (wenu) wasiokuwa nyinyi. Hawatoacha kukuharibieni. Wanatamani kama mngetaabika. Imekwishajitokeza bughudha kutoka midomoni mwao. Na yale yanayoficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Aayaat, (ishara, hoja, dalili) mkiwa mtatia akilini.

 

 

هَا أَنتُمْ أُولَاءِ تُحِبُّونَهُمْ وَلَا يُحِبُّونَكُمْ وَتُؤْمِنُونَ بِالْكِتَابِ كُلِّهِ وَإِذَا لَقُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا عَضُّوا عَلَيْكُمُ الْأَنَامِلَ مِنَ الْغَيْظِ ۚ قُلْ مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١١٩﴾ 

119. Ha! Nyinyi ndio wale mnaowapenda na wala wao hawakupendeni, na mnaamini Kitabu chote; na wanapokukuteni husema: “Tumeamini” na wanapokuwa peke yao wanakutafunieni ncha za vidole kutokana na chuki. Sema: “Kufeni kwa chuki zenu.” Hakika Allaah ni Mjuzi kwa yaliyomo vifuani.

 

 

إِن تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا بِهَا ۖ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ ﴿١٢٠﴾

120. Ikikuguseni hasanah (nusura, ushindi) inawachukiza, na likikusibuni baya hulifurahia; na mkisubiri na mkawa na taqwa haitokudhuruni chochote katika hila zao. Hakika Allaah ni Mwenye kuyazunguka wayatendayo. 

 

 

وَإِذْ غَدَوْتَ مِنْ أَهْلِكَ تُبَوِّئُ الْمُؤْمِنِينَ مَقَاعِدَ لِلْقِتَالِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٢١﴾ 

121. Na pindi ulipotoka asubuhi mapema (ee