Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

 

Imekusanywa Na:

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

 

Share

00-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Utangulizi

 

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

00-Utangulizi:

 

 

بِسْمِ الله الرَّحْمنِ الرَّحِيم

الْحمْدُ لِلَّه وَالصَّلاةُ وَالسِّلامُ عَلى خَاتم الأنْبِيَاء وَالْمُرْسَلِين، الْمَبْعُوثُ رَحْمَةً لِلْعَالَمِين، مُحَمَّد وَعَلى آلِه وَأصْحابِه أجْمَعِين وَمَنْ تَبِعَهُمْ بِإِحْسَانٍ إِلَى يَوْمِ الدِّينِ.

Himdi Anastahiki Allaah, Swalaah na salaam zimfike Nabiy na Rasuli wa mwisho, aliyetumwa awe rahmah kwa walimwengu, Muhammad, pamoja na ahli zake na Maswahaba zake wote, na wanaowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Malipo.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ

 Basi jua kwamba: laa ilaaha illa Allaah (hapana muabudiwa wa haki ila Allaah)  [Muhammad: 19]

 

 

Maana ya Tawhiyd kama alivyosema ‘Allaamah ‘Abdir-Rahmaan Naaswir As-Sa’dy katika Al-Qawlus-Sadiyd Fiy Maqaaswidit-Tawhiyd - Sharh Kitaab At-Tawhiyd: “Tambua kwamba maana ya Tawhiyd haina mipaka. Ni maarifa na kukiri kumpwekesha Ar-Rabb (Mola) kwa Sifa za ukamilifu, na kuthibitisha kwamba Anapwekeshwa katika Sifa Zake Adhimu na Tukufu, na kumpwekesha katika ‘ibaadah zote”.  

 

Kinyume cha Tawhiyd ni shirk ambayo ni kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika hayo yaliyotajwa yote yanayomuhusu Yeye Pekee.

 

‘Ulamaa wameigawanywa Tawhiyd katika sehemu tatu:

 

1-Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah

 

Nayo ni kumpwekesha Allaah katika Uumbaji, Uendeshaji wa mambo yote katika Ulimwengu, Utoaji rizki, Uletaji uhai na Ufishaji, kwa kuamini kwamba Yeye Ndiye Aliyeumba kila kitu, Anayeruzuku na kuendesha mambo yote ni Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Hana mshirika, na kuamini kwamba Ufalme wote ni wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّـهُ ۚ

Sema: “Ni nani Rabb wa mbingu na ardhi?” Sema: “Ni Allaah.” [Ar-Ra’d:16]

 

Na Anasema:

 

 قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ

Sema: “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini. Au nani anayemiliki kusikia na kuona; na nani anayemtoa aliye hai kutoka mfu, na anayemtoa mfu kutoka aliye uhai; na nani anayeendesha mambo (yote)?”  Watasema: “Ni Allaah”; basi sema: “Je basi hamuwi na taqwa?” [Yuwnus: 31]

 

 

2-Tawhiyd Al-Uluwhiyyah

 

Maana yake ni kumwepekesha Allaah katika 'ibaadah na kuzielekeza ‘ibaadah zote kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) bila ya kumshirikisha na chochote kama Anavyosema:

 

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾

Sema: “Hakika Swalaah yangu, na kuchinja kafara na ‘ibaadah zangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu.”

 

لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٦٣﴾

 “Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza.”   [Al-An’aam: 162-163]

 

 

3-Tawhiyd Asmaa wasw-Swifaat

 

Kumpwekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa Sifa Zake Tukufu, na Majina Yake mazuri, bila kuzigeuza Sifa hizo maana zake, au kuzipinga, au kuzifananisha na viumbe au kuzipa unamna. Yeye Amejipa Majina mazuri mazuri na Sifa nzuri nzuri na Akawataka waja Wake wamuombe na kumtukuza kwa Majina na Sifa hizo. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

 وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanamili katika kukadhibisha Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A’raaf: 180]

 

 

Qur-aan nzima imedhihirisha Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa); mfano Suwratul-Faatihah ambayo tunaisoma kila siku mara kumi na saba katika Swalaah zetu za fardhi na pia katika Swalaah zote nyinginezo, imejumuisha aina tatu zote za Tawhiyd.

 

 بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿١﴾

Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.

 

 الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾

AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah) Rabb wa walimwengu.

 

الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣﴾

Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.

 

 مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٤﴾

Mfalme wa siku ya malipo.

 

 إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.  [Al-Faatihah: 1-5]

 

Na pia kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 

 رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾

 Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake; basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika ‘ibaadah Yake. Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)?  [Maryam: 65]

 

 

 

 

Share

01-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Tawhiyd Ni Elimu Tukufu Na Bora Kabisa

 

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

01-Tawhiyd Ni Elimu Tukufu Na Bora Kabisa

 

 

Binaadamu anahitaji kujifunza atambue maana, fadhila na umuhimu wa Tawhiyd, kisha afanyie kazi kuithibitisha.

 

 

Elimu ya Tawhiyd ni tukufu na bora kwa kuwa ni elimu anayoihitaji mja kila wakati, kwa sababu inahusiana na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ambaye Anapasa kupwekeshwa katika ‘ibaadah bila ya kumshirikisha. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ

Basi jua kwamba: laa ilaaha illa-Allaah (hapana muabudiwa wa haki ila Allaah) na omba maghfirah kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. [Muhammad: 19]

 

Aayah hiyo imetanguliza elimu ya asasi ya Dini nayo ni maarifa ya Tawhiyd,

 

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ

Basi jua kwamba: laa ilaaha illa-Allaah (hapana muabudiwa wa haki ila Allaah)

 

kisha ikafuatia na maarifa ya elimu ya matawi ambayo ni kuomba maghfirah,

 

وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ

 na omba maghfirah kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike

 

Kwa hiyo imethibitisha ubora wa elimu ya Tawhiyd kabla ya ‘amali za mwana Aadam, sababu ‘ibaadah na ‘amali za mwana Aadam bila ya kumpwekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hazikubaliwi na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

Juu ya kuwa Aayah hiyo imeteremshwa kumkusudia Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), lakini haimaanishi kwamba hiyo ni amri kwake kwamba amjue Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), kwani ujuzi wa kumjua Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) umeshafunuliwa Wahyi kwake kabla ya hapo. Aayah hiyo imeteremshwa akiwa Madiynah na kabla yake imepita miaka 13 akiwa ni Rasuli mjini Makkah akiwalingania watu wake neno hilo la laa ilaaha illa Allaah. Lilokusudiwa ni kule kutajwa mwanzo elimu ya kumjua Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kabla ya elimu ya ‘amali kama hivyo kuomba maghfirah, au ‘amali nyinginezo kama Swalaah, Zakaah, Swawm, Hajj na kadhaalika.

 

Akathibitisha Rasuli  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu ujuzi wake kuhusiana na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) akasema:

 

 فَوَاللَّهِ إنِّي لَأَعْلَمُكُمْ بِاَللَّهِ وَأَشَدُّكُمْ لَهُ خَشْيَة  رواه البخاري

Wa-Allaahi, (Naapa kwa Allaah) kwamba hakika mimi namjua zaidi Allaah na ni mwenye kumkhofu zaidi kuliko nyinyi. [Al-Bukhaariy]

 

Na ‘amali hazikubaliwi isipokuwa baada ya kumwamini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Imethibiti kutoka kwa Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba aliulizwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

أَيُّ الْعَمَلِ أَفْضَلُ؟ فَقَالَ: ((إِيمَانٌ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ))

‘Amali ipi bora kabisa? Akajibu: ((Kumwamini Allaah na Rasuli Wake)) [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  katika Al-Bukhaariy]

 

Share

02-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Tawhiyd Inahusiana Na Majina Mazuri Ya Allaah Na Sifa Zake

 

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

02-Tawhiyd Inahusiana Na Majina Mazuri Ya Allaah Na Sifa Zake

 

 

 

 

Tawhiyd inahusiana na Majina Mazuri ya Allaah na Sifa Zake.  Ndio maana Aayatul Kursiyy ikawa ni Aayah bora kabisa katika Qur-aan na Suwratul-Ikhlaasw ikawa thawabu zake kuisoma ni sawa na thuluthi ya Qur-aan kwa sababu ndani yake zinaelezea Majina na Sifa za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye Uluwa, Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa. [Al-Baqarah: 255]

 

 بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾

Sema: “Yeye ni Allaahu Mmoja Pekee.

 

اللَّـهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾

 “Allaah ni Aliyekamilika sifa za utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote. 

 

 

لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾

 “Hakuzaa na wala Hakuzaliwa.

 

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾

 “Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye.”  [Ikhlaasw: 112]

 

 

Share

03-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Tawhiyd Ni Fitwrah (Maumbile Asili Ya Mwana Aadam)

 

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

03-Tawhiyd Ni Fitwrah (Maumbile Asili Ya Mwana Aadam)

 

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾

Basi elekeza uso wako kwenye Dini yenye kujiengua na upotofu inayoelemea haki. Umbile la asili la kumpwekesha Allaah Aliyowaumbia watu. Hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah. Hivyo ndio Dini iliyonyooka sawasawa, lakini watu wengi hawajui.  [Ar-Ruwm: 30]

 

Na Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا مِنْ مَوْلُودٍ إِلَّا يُولَدُ عَلَى الْفِطْرَةِ  فَأَبَوَاهُ يُهَوِّدَانِهِ ، وَيُنَصِّرَانِهِ  وَيُمَجِّسَانِهِ  كَمَا تُنْتَجُ  الْبَهِيمَةُ بَهِيمَةً جَمْعَاءَ ، هَلْ تُحِسُّونَ فِيهَا مِنْ جَدْعَاءَ؟)) ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ:  وَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: ((فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ))  

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba alikuwa akisema: Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema; ((Hakuna kizazi kinachozaliwa (mtoto mchanga) isipokuwa anazaliwa katika 'fitwrah' kisha wazazi wake (humbadilisha na) humuingiza katika dini ya Uyahudi, au Unaswaara au Umajusi, kama mfano mnyama mwenye pembe  anavyomzaa mnyama mwenye pembe kama yeye, je, mtahisi kuwa hana pembe?   Kisha Abuu Hurayrah akasema: Someni mkipenda: (kauli ya Allaah):  ((Umbile la asili la kumpwekesha Allaah Aliyowaumbia watu. Hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah))  [Al-Bukhaariy na Muslim]     

 

 

 

Share

04-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Tawhiyd Ni Ahadi Waliyofungamana Viumbe Wote Na Allaah Kabla Ya Kuzaliwa Kwao

 

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

04-Tawhiyd Ni Ahadi Waliyofungamana Viumbe Wote Na Allaah Kabla Ya Kuzaliwa Kwao

 

 

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alikusanya roho za wana Aadam wote kabla ya kuumbwa kwao, zikafungamana ahadi Naye ya kukiri kwamba Yeye Ndiye Rabb wao na kwamba watampwekesha bila ya kumshirikisha na zikaahidi pia kumtii:

 

وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ﴿١٧٢﴾

Na pindi Rabb wako Alipochukua katika wana wa Aadam kutoka migongoni mwao, kizazi chao, na Akawashuhudisha juu ya nafsi zao, “Je, Mimi siye Rabb wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka, tumeshuhudia!” (Allaah Akawaambia): “Msije kusema Siku ya Qiyaamah: hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya.”

 

أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِن قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِّن بَعْدِهِمْ ۖ

Au mkasema: “Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. [Al-A’raaf: 172-173]

 

Roho hizo ni za wana Aadam wote tokea Nabiy Aadam (‘Alayhis-Salaam) mpaka siku ya Qiyamaah. Kwa maana: wana Aadam wote wanaozaliwa au watakaozaliwa leo au kesho au mwakani na kuendelea mpaka Siku ya Qiyaamah, roho zao zimeshaumbwa. Dalili ni Hadiyth ifuatayo ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kuhusu roho kupulizwa tumboni mwa mama anaposhika mimba inayofikia muda wa miezi minne (siku 120):    

 

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم -وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ: ((إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَمْ سَعِيدٍ؛ فَوَاَللَّهِ الَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا. وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا)) رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: “Ametusimulia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake).  Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. Wa-Allaahi naapa kwa Yule Ambaye hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye ‘amali za watu wa Jannah hadi ikawa baina yake na Jannah ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja wenu hufanya ‘amali za watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share

05-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Mwenyewe Ameshuhudia Tawhiyd

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

05-Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Mwenyewe Ameshuhudia Tawhiyd

 

 

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amethibitisha Tawhiyd Mwenyewe katika Aayah kadhaa; baadhi yake zifuatazo:  

 

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

Allaah Ameshuhudia kwamba hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye; na (pia) Malaika na wenye elimu (kwamba Allaah) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.  [Aal-‘Imraan: 18]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa):  

 

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

 Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.  [Al-Baqarah: 163]

 

 

Alipompa Nabiy Muwsaa Ujumbe Alisema:

 

 

إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي﴿١٤﴾

  “Hakika mimi ni Allaah hapana Muabudiwa wa haki ila Mimi; basi niabudu, na simamisha Swalaah kwa ajili ya kunidhukuru.”  [Twaahaa: 14]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ ﴿٩٢﴾

“Hakika huu ummah wenu ni ummah mmoja; Nami ni Rabb wenu, basi niabuduni.”    [Al-Anbiyaa: 92]

 

 هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ﴿٢٢﴾

Yeye ni Allaah, Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri, Yeye Ndiye Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.

 

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٢٣﴾

Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye kusalimisha na Amesalimika na kasoro zote, Mwenye kusadikisha ahadi na kuaminisha, Mwenye kudhibiti, kushuhudia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Jabari, Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye ukubwa na uadhama, Subhaana Allaah! Utakasifu ni wa Allaah kutokana na ambayo wanamshirikisha.

 

هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٢٤﴾

Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabbih Pekee kila kilichokuweko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.   [Al-Hashr: 22-24]

 

 

Share

06-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Tawhiyd Imethibitika Mwanzoni na Mwishoni Wa Uhai Wa Binaadamu

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

06-Tawhiyd Imethibitika Mwanzoni na Mwishoni Wa Uhai Wa Binaadamu

 

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

وَهُوَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْحَمْدُ فِي الْأُولَىٰ وَالْآخِرَةِ ۖ وَلَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٧٠﴾

Naye ni Allaah, Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye. Ni Zake Pekee Himidi za mwanzoni (duniani) na za Aakhirah. Na hukumu ni Yake Pekee, na Kwake Pekee mtarejeshwa.  [Al-Qaswasw: 70]

 

 

Mwanzoni kabla ya uhai:

 

هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦﴾

Yeye Ndiye Aliyekusawirini umbo katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo. Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Aal-‘Imraan: 6]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ الْأَنْعَامِ ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۚ يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِّن بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ﴿٦﴾

Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, kisha Akamfanya humo mkewe na Akakuteremshieni katika wanyama wa mifugo jozi nane. Anakuumbeni matumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyo Ndiye Rabb wenu Ana ufalme, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, basi vipi mnageuzwa?  [Az-Zumar: 6]

 

Mwishoni:

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۗ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا ﴿٨٧﴾

Allaah; hapana muabudiwa wa haki ila Yeye. Bila ya shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah haina shaka ndani yake. Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?   [An-Nisaa: 87]

 

Share

07-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Nguzo Tano Za Kiislamu Zimeanzia Na Neno La Tawhiyd:

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

07-Nguzo Tano Za Kiislamu Zimeanzia Za Neno La Tawhiyd

 

 

 

Nguzo tano za Kiislamu zimeanzia na Neno la Tawhiyd:

 

عن أبي عَبْدِ الرَّحْمنِ عَبْدِ اللهِ بنِ عُمَرَ بنِ الخَطابِ رَضيَ اللهُ عنهُما قال: سَمِعْتُ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ: ((بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ : شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ ))

 

Kutoka kwa Abuu ‘Abdir-Rahmaan ‘Abdillaah bin 'Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Uislamu umejengwa kwa nguzo tano: Kushuhudia na kukiri kwamba kuwa hakuna muabudiwa wa haki  isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli wa Allaah, na kusimamisha Swalaah, na Kutoa Zakaah, na kuhiji katika Nyumba (Makkah) na Swawm Ramadhwaan)).[Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share

08-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Tawhiyd Ni Lengo Kuu La Kuumbwa Wana Aadam Na Majini

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

08-Tawhiyd Ni Lengo Kuu La Kuumbwa Wana Aadam na Majini

 

 

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ﴿٥٦﴾

Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu. [Adh-Dhaariyaat: 56]

 

Anatujulisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwamba Ametuumba kwa hikmah nayo ni kumpwekesha katika ‘ibaadah wala hakutuumba kwa kuwa Ana haja nasi kwani yeye ni Al-Ghaniyy (Mkwasi Asiyehitaji kitu) kama Anavyosema:

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَنتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَاللَّـهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ﴿١٥﴾

Enyi watu!  Nyinyi ni mafakiri kwa Allaah! Na Allaah Ndiye Mkwasi,  Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote. [Faatwir: 15]

 

Akathibitisha hayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anapoendelea kusema baada ya Aayah iliyotangulia ya Suwrah Adh-Dhaariyaat:

 

مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ﴿٥٧﴾

Sitaki kutoka kwao riziki yoyote, na wala Sitaki wanilishe. [Adh-Dhaariyaat: 57]

 

Akatujulisha kwamba Hahitaji lolote kutoka kwa waja Wake, bali waja ndio wanaomhitaji Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwani Yeye Ndiye Anayewaruzuku na Anawaendeshea maisha yao na Ndiye Anayewapangia na kuwatengeneza mambo yao. Yeye ni Allaah, Anayestahiki kuabudiwa kwa haki Naye Ndiye Muumba wa kila kitu:

 

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢﴾

Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb wenu. Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.  [Al-An’aam: 102]

 

Na Anasema pia:

 

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٦٢﴾

  Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu, Muumba wa kila kitu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye; basi vipi mnaghilibiwa?   [Ghaafir: 62]

 

Viumbe hao, wanajumuika Malaika, majini na wana Aadam. Wote hao wanastahiki kumwambudu kwa kuwa ni haki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kutoka kwao na lau kama watamshirikisha, basi Atawaadhibu hata ikiwa Malaika watamshirikisha, kama Anavyosema:

 

وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٢٩﴾

Na yeyote yule miongoni mwao atakayesema: “Mimi ni mwabudiwa badala Yake,” basi huyo Tutamlipa Jahannam. Hivyo ndivyo Tunavyolipa madhalimu.   [Al-Anbiyaa: 29]

 

Na atakayemshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hatoweza kufidia kuepuka na adhabu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hata akiwa na dhahabu inayojaa ardhini! Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

  إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾

Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao dhahabu ya ujazo wa dunia nzima lau wakitaka kujifidia nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru. [Aal-‘Imraan: 91]

 

Share

09-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Aina Zote Tatu za Tawhiyd Zinaafikiana, Haiwezekani Kukosekana mojawapo

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

09-Aina Zote Tatu za Tawhiyd Zinaafikiana, Haiwezwkani Kukosekana Mojawapo

 

 

 

Aina zote Tatu za Tawhiyd zinaafikiana. Kutokuamini mojawapo humtoa mtu nje ya Uislamu kwa sababu makafiri Quraysh waliamini Tawhiydur-Rubuwbiyyah wakakanusha ya Uluwhiyyah. Waliamini kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Muumba wao, na Ndiye Muumba wa mbingu na ardhi, Ndiye Anayendesha mambo yote, Ndiye Anayewaruzku, Na Ndiye Anayeteremsha mvua n.k. Dalili kadhaa katika Qur-aan:

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٨٧﴾

Na ukiwauliza: Ni nani kawaumba? Bila shaka watasema: “Allaah.”  Basi vipi wanaghilibiwa?  [Az-Zukhruf: 87]

 

Na pia:

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٥﴾

Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” bila shaka watasema: “Allaah.” Sema: “AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah).” Bali wengi wao hawajui.   [Luqmaan: 25]

 

Na pia:

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلْ أَفَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّـهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ أَوْ أَرَادَنِي بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ ۚ قُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ ۖ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ﴿٣٨﴾

Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” Bila shaka watasema: “Allaah.” Sema: “Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah; ikiwa Allaah Atanikusudia dhara; je, wao wataweza kuondosha dhara Yake? Au Akinikusudia rahmah; je wao wataweza kuizuia rahmah Yake?” Sema: “Ananitosheleza Allaah”, Kwake watawakali wenye kutawakali. [Az-Zumar: 38]

 

Na pia:

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٦١﴾

Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi, na akatiisha jua na mwezi?” Bila shaka watasema: “Allaah.” Basi vipi wanavyoghilibiwa?

 

اللَّـهُ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ لَهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٦٢﴾

Allaah Humkunjulia na Humdhikishia riziki Amtakaye katika waja Wake. Hakika Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّن نَّزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ مَوْتِهَا لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿٦٣﴾

Na ukiwauliza: “Ni nani Ateremshaye maji kutoka mbinguni, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake?” Bila shaka watasema: “Allaah”.  Sema: “AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah.” Bali wengi wao hawatii akilini.   [Al-‘Ankabuwt: 61 -63]

 

Na pia:

 

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ﴿٣١﴾

Sema: “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini. Au nani anayemiliki kusikia na kuona; na nani anayemtoa aliye hai kutoka mfu, na anayemtoa mfu kutoka aliye uhai; na nani anayeendesha mambo (yote)?”  Watasema: “Ni Allaah”; basi sema: “Je basi hamuwi na taqwa?”   [Yuwnus: 31]

 

Lakini walimshirikisha katika ‘ibaadah zao wakidai kuwa walivyokuwa wakiviabudu vinawakaribisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِي مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ ﴿٣﴾

na wale waliojichukulia badala Yake walinzi (wakisema): “Hatuwaabudu isipokuwa ili wapate kutukurubisha kwa Allaah tumkaribie” Hakika Allaah Atahukumu baina yao katika yale waliyokhitilafiana nayo. Hakika Allaah Hamwongoi aliye muongo, kafiri.  [Az-Zumar: 3]

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akathibitisha tena kwamba Yeye Ndiye wa kuabudiwa katika Rubuwbiyyah Yake (Uola, umiliki, uendeshaji wa ulimwengu, uumbaji, utoaji rizki, uhuishaji na ufishaji, n.k.)  na Uluwhiyyah Yake (‘ibaadah): 

 

اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ قَرَارًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴿٦٤﴾

Allaah Ambaye Amekufanyieni ardhi kuwa mahali pa makazi, na mbingu kama ni paa na Akakutieni sura, Akazifanya nzuri zaidi sura zenu, na Akakuruzukuni katika vizuri. Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu. Basi Tabaaraka-Allaah, Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu.

 

هُوَ الْحَيُّ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۗ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٦٥﴾

Yeye Ndiye Aliye hai daima hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye; basi muombeni Yeye wenye kumtakasia Dini. AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu.   [Ghaafir: 64- 65]

 

 Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٠١﴾

Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje kuwa Yeye Ana mwana na hali hana mke! Naye Ameumba kila kitu, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

 

 

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢﴾

Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb wenu. Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.  [Al-An’aam: 101-102]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٦٢﴾

Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu, Muumba wa kila kitu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye; basi vipi mnaghilibiwa?  [Ghaafir: 62]

 

 Na pia:

 

خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ يُكَوِّرُ اللَّيْلَ عَلَى النَّهَارِ وَيُكَوِّرُ النَّهَارَ عَلَى اللَّيْلِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ أَلَا هُوَ الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ ﴿٥﴾

Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, Anaufunika usiku juu ya mchana, na Anafunika mchana juu ya usiku, na Anatiisha jua na mwezi; kila kimoja kinakwenda mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Tanabahi! Yeye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa kughufuria.

 

 

خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ الْأَنْعَامِ ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۚ يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِّن بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ﴿٦﴾

Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, kisha Akamfanya humo mkewe na Akakuteremshieni katika wanyama wa mifugo jozi nane. Anakuumbeni matumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyo Ndiye Rabb wenu Ana ufalme, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, basi vipi mnageuzwa?   [Az-Zmuar 5 – 6]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ هَلْ مِنْ خَالِقٍ غَيْرُ اللَّـهِ يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٣﴾

Enyi watu! Kumbukeni neema za Allaah kwenu. Je, kuna muumbaji yeyote badala ya Allaah Anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhi? Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, basi wapi mnapogeuzwa? [Faatwir: 3]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ ﴿١١٥﴾

 “Je, mlidhania kwamba Sisi Tulikuumbeni bila kusudio mcheze tu na kwamba nyinyi Kwetu hamtorejeshwa?”

 

 

فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ ﴿١١٦﴾

Basi Ametukuka Allaah Mfalme wa hak). Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye. Rabb wa ‘Arsh tukufu.

 

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿١١٧﴾

Na yeyote yule anayeomba du’aa (au kuabudu) pamoja na Allaah muabudiwa mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Rabb wake. Hakika hawafaulu makafiri.   [Al-Muuminuwn: 115-117]

 

Na pia Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ﴿٧﴾

Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, mkiwa ni wenye yakini.

 

لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ﴿٨﴾

Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye, Anahuisha na Anafisha; Rabb wenu na Rabb wa baba zenu wa awali. [Ad-Dukhaan: 7- 8]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٣﴾

  Hakika Rabb wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh. Anaendesha mambo yote. Hakuna mwombezi yeyote ila baada ya idhini Yake. Huyu Ndiye Allaah Rabb Wenu, basi mwabuduni. Je, hamkumbuki?   [Yuwnus: 3]

 

Anathibitisha pia kuhusu Tawhiyd Yake ya Asmaa na Swifaat kwamba inaafikiana na Tawhiyd ya Rubuwbiyyah na Uluwhiyyah:

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ﴿٨﴾

Allaah, hapana hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye. Anayo Majina Mazuri kabisa.  [Twaahaa: 8]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.  [Al-Baqarah: 163]

 

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa)

 

إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْقَصَصُ الْحَقُّ ۚ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦٢﴾

Hakika haya ni masimulizi ya haki. Na hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah. Na hakika Allaah Yeye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Aal-‘Imraan: 62]

 

Kuwa na ujuzi wa Tawhiyd ya Asmaa wasw-Swifaat (Majina na Sifa za Allaah) utamtambua Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) vizuri kabisa na hutokuwa mwenye kukanusha, na itakuepusha na kupotoa maana ya Majina na Sifa Zake na kuzibadilisha maana au kumfananisha na viumbe vyenginevyo. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ

  Sema; “Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa.    [Al-Israa: 110]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ الرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا ﴿٥٩﴾

Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh Ar-Rahmaan, basi ulizia kuhusu Yeye; kwani ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اسْجُدُوا لِلرَّحْمَـٰنِ قَالُوا وَمَا الرَّحْمَـٰنُ أَنَسْجُدُ لِمَا تَأْمُرُنَا وَزَادَهُمْ نُفُورًا ۩﴿٦٠﴾

Na wanapoambiwa: “Msujudieni Ar-Rahmaan” husema: “Ni nani huyo Ar-Rahmaan? Tumsujudie unayetuamrisha, na inawazidishia kukengeuka kwa chuki.  [Al-Furqaan: 59 – 60]

 

Na pia:

 

كَذَٰلِكَ أَرْسَلْنَاكَ فِي أُمَّةٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهَا أُمَمٌ لِّتَتْلُوَ عَلَيْهِمُ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَـٰنِ ۚ قُلْ هُوَ رَبِّي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ مَتَابِ ﴿٣٠﴾

Hivyo ndivyo Tumekutuma katika Ummah uliokwishapita kabla yake umati nyingine ili uwasomee yale Tuliyokufunulia Wahy; nao wanamkufuru Ar-Rahmaan. Sema: “Yeye Ndiye Rabb wangu, hapana muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake natawakali na Kwake ni mahali pangu pa kurejea kutubu.”   [Ar-Ra’d: 30]

 

Share

10-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Tawhiyd Ni Haki Yake Allaah (Subhaanahu Wa Ta'alaa)

 

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

10-Tawhiyd Ni Haki Yake Allaah (Subhaanahu Wa Ta’aalaa)

 

 

 

 

 

Ameamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuabudiwa bila ya kumshirikisha na kitu au kumlinganisha na yeyote au chochote kile:

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٢١﴾

Enyi watu! Mwabuduni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa.

 

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾

Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.   [Al-Baqarah: 21-22]

 

Na Anaamrisha pia:

 وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ

Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. [An-Nisaa: 36]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا  

Na Rabb wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia ihsaan wazazi wawili.   [Al-Israa: 23]

 

Na pia kila Rasuli aliamrishwa kuwalingania watu wake kumwabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) bila ya kumshirikisha na chochote:

 

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ  

Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (alinganie) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaghuti.”   [An-Nahl: 36]

 

Na katika miongoni mwa wasia kumi wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa Rasuli Wake Anasema:

 

 قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ  

  Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Rabb wenu kwenu. Kwamba msimshirikishe na chochote,   [Al-An’aam: 151]

 

Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akausia kwa Swahaba zake:

 

عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: كُنْتُ رَدِيفَ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) عَلَى حِمَارٍ فَقَالَ لِي: ((يَا مُعَاذُ؟ أَتَدْرِي مَا حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ, وَمَا حَقُّ الْعِبَادِ عَلَى اَللَّهِ؟)) قُلْتُ اَللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ, قَالَ: ((حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ أَنْ يَعْبُدُوهُ, وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا, وَحَقُّ الْعِبَادِ عَلَى اَللَّهِ أَنْ لاَ يُعَذِّبَ مَنْ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا)) قُلْتُ يَارَسُولَ اَللَّهِ أَفَلاَ أُبَشِّرُ اَلنَّاسَ؟ قَالَ: ((لاَ تُبَشِّرْهُمْ فَيَتَّكِلُوا)) أَخْرَجَاهُ فِي اَلصَّحِيحَيْنِ

Imepokelewa kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu ‘anhu)   amesema: Nilikuwa nyuma ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nimepanda punda akasema: ((Ee Mu’aadh! Unajua nini haki ya Allaah juu wa waja Wake na haki ya waja juu ya Allaah?)) Nikajibu: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi: Akasema: ((Haki ya Allaah kwa waja wake ni kwamba wamwabudu na wasimshirikishe na chochote. Na haki ya waja kwa Allaah ni kwamba Hatomwadhibu yeyote ambaye hamshirikishi na kitu)). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Nibashirie watu? Akasema: ((Usiwabashirie wasije kuitegemea)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share

11-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Neno La Tawhiyd Ni Miongoni Mwa Maneno Ayapendao Allaah Na Rasuli

 

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

11-Neno La Tawhiyd Ni Miongoni Mwa Maneno Ayapendayo Allaah

Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

 

 

 

 

 

Kutoka kwa Samurah bin Jundub (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) ambaye amesema:

 

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((أَحًبُّ الْكَلامِ إِلَى اللَّهِ أَرْبَعٌ: سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلا إِلَهَ إِلا اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، لا يَضُرُّكَ بِأَيِّهِنَّ بَدَأْتَ))

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Bora ya maneno kwa Allaah ni manne: Subhaana-Allaah, walhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar, wa laa hawla wa laa quwwata illaa biLLaah - Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahikii Allaah, na  hapana muabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa.… si vibaya kuanza kwa lolote katika hayo))  [Muslim]

 

Na Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya-Allaahu ‘anhu):

 

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((لأَنْ أَقُولَ: سُبْحَانَ اللهِ، والحَمْدُ للهِ، وَ لاَ إَلَهَ إلاَّ اللهُ، واللهُ أَكْبَرُ، أَحَبُّ إَلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ))

Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kusema kwangu: Subhaana-Allaah, WalhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar- Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana muabudiwa wa haki  ila ni Allaah, na Allaah ni Mkubwa.… ni bora kwangu kuliko kila kilichoangaziwa na jua))   [Muslim]

 

Na Hadiyth ya ya Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya-Allaahu ‘anhu):

 

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((إِنَّ أَفْضَلَ الدُّعَاءِ: الْحَمْدُ لِلَّه، وَأَفْضَلُ الذِّكْرِ: لاَ إلَهَ إِلاَّ الله))

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Bora ya du’aa ni mtu kusema: AlhamduliLLaah- Himdi Anstahiki Allaah, na dhikri bora ni: laa ilaaha illa-Allaah - hapana muabudiwa wa haki ila Allaah)) [At-Tirmidhiy, ibn Maajah. Al-Haakim na ameisahihisha na ameiwafiki Adh-Dhahaby na angalia: Swahiyh Al-Jaami (1/362) [1104]

 

Na maneno hayo yana thawabu nzito, mbele ya Allaah na ndiyo ’amali zinazotangulia na kubakia Aakhirah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ﴿٤٦﴾

Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia. Na mema yanayobakia ni bora mbele ya Rabb wako, kwa thawabu na matumaini.  [Al-Kahf: 46]

 

Akataja Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuhusu Aayah hiyo kuwa miongoni mwa 'amali zilokusudiwa ni kusema pia: Subhaana Allaah, wal-HamduliLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar[Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

 

Share

12-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Vitabu Vya Mbinguni Vimeteremshwa Kuamrisha Tawhiyd

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

12-Vitabu Vya Mbinguni Vimeteremshwa Kuamrisha Tawhiyd

 

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿١﴾

Hawakuwa wale waliokufuru miongoni mwa Ahlil-Kitaabi na washirikina wenye kujitenga na hali waliyonayo mpaka iwafikie hoja bayana.

 

رَسُولٌ مِّنَ اللَّـهِ يَتْلُو صُحُفًا مُّطَهَّرَةً ﴿٢﴾

Rasuli kutoka kwa Allaah anawasomea Sahifa zenye kutakaswa.

 

فِيهَا كُتُبٌ قَيِّمَةٌ ﴿٣﴾

Ndani yake humo mna maandiko yaliyonyooka sawasawa.

 

 

وَمَا تَفَرَّقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿٤﴾

Na hawakufarikiana wale waliopewa kitabu isipokuwa baada ya kuwajia hoja bayana.

 

 

 

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾

Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara. [Al-Bayyinah: 1-5]

 

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾

Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Manabii baada yake. Na Tumemfunulia Wahy Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na dhuriya, na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, Na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zabuwr. [An-Nisaa: 163]

 

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 الم ﴿١﴾

Alif Laam Miym.

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﴿٢﴾

Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliye hai daima, Msimamia kila kitu.

 

 

 نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٣﴾

Amekuteremshia Kitabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki kinachosadikisha yaliyo kabla yake na AkateremshaTawraat na Injiyl.

 

 

مِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ الْفُرْقَانَ ۗ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤﴾

Kabla (ya kuteremshwa Qur-aan), iwe ni mwongozo kwa watu na Akateremsha pambanuo (la haki na batili). Hakika wale waliokufuru Aayaat za Allaah watapata adhabu kali. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kuangamiza. [Aal-‘Imraan: 1-4]

  

Na Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

الر ۚ كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ﴿١﴾

Alif Laam Raa. Kitabu ambacho Aayaat Zake zimetimizwa barabara, kisha zikafasiliwa waziwazi kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

 

أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ﴿٢﴾

Kwamba: “Msiabudu isipokuwa Allaah. Hakika mimi (Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mwonyaji kwenu na mbashiriaji.”  [Huwd: 1-2]

 

Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kutokana na Hadiyth ya Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

 

((الْأَنْبِيَاءُ إِخْوَةٌ مِنْ عَلَّاتٍ، وَأُمَّهَاتُهُمْ شَتَّى، وَدِينُهُمْ وَاحِد))

((Manabii ni ndugu kwa baba na mama zao ni mbalimbali, na Dini yao ni moja)) [Muslim]

 

Wanasema ‘Ulamaa kutokana na Hadiyth hii kuwa, asli ya iymaan ya Manabii wote ni moja, na Shariy’ah zao ni tofauti, lakini wote wanaungana na kuafikiana wote kwa Tawhiyd yao ambayo ni moja.

 

Share

13-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Kauli Ya Tawhiyd Ndio Bora Kabisa Waliyotamka Rusuli Wote

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

13-Kauli Ya Tawhiyd Ndio Bora Kabisa Waliyotamka Rusuli Wote

 

 

Imepokelewa kutoka kwa babu yake ‘Amru bin Shu’ayb (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema:

 

((خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ, وَخَيْرُ مَا قُلْتُ أَنَا وَالنَّبِيُّونَ مِنْ قَبْلِي: لَا إِلَهَ إِلَّااللَّهُوَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ))

((Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni:  “Laa Ilaaha Illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr” [Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Peke Yake, Hana mshirika. Yeye Ndiye Mwenye Ufalme na Ndiye Mwenye kuhimidiwa, Naye ni Muweza wa kila kitu])). [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy 3585]

 

 

Neno la Tawhiyd ni dhikri (utajo) bora kabisa:

 

 عن جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ يَقُولُ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "أَفْضَلُ الذّكْر لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَأَفْضَلُ الدُّعَاءِ الْحَمْدُ لِلَّهِ"

Kutoka kwa Jaabir bin ‘AbdiLLaah amesema: “Nimesmikia Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Dhikri bora kabisa ni “laa ilaaha illa Allaah”, na du’aa bora kabisa ni “AlhamduliLLaah”)). [At-Tirmdhiy na Ibn Maajah].

 

 

Na ndio maana Aayah tukufu kabisa ikawa ni Aayatul-Kursiyy (Al-Baqarah 2: 255) na Suwratul-Ikhlaasw (112) ikawa ni sawa na thuluthi ya Qur-aan, japokuwa ni Suwrah ndogo kabisa.

 

 

 

Share

14-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Tawhiyd Ni jambo La Kwanza Walolingania Rusuli Wote

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

14-Tawhiyd Ni jambo La Kwanza Walolingania Rusuli Wote

 

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

 وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾

Na Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi; basi Niabuduni.” [Al-Anbiyaa: 25]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (alinganie) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaghuti.” [An-Nahl: 36]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

 وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ آلِهَةً يُعْبَدُونَ﴿٤٥﴾

 “Na waulize wale Tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Rusuli Wetu; je, Tulifanya badala ya Ar-Rahmaan  waabudiwa wengine ili waabudiwe?” [Az-Zukhruf: 45]

 

 

 ‘Allaamah Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema katika mhadhara wake: “At-Tawhiyd Yaa Ibaada Allaah”: “Manabii wote kuanzia wa mwanzo wao hadi wa mwisho wao, walianza kulingania kwao watu kwa Tawhiyd, kwa kuwa Tawhiyd ndio msingi ambao Dini imejengeka. Tawhiyd ikiwa imara, nyumba itasimama vizuri na kuwa imara. Na huu ni mfano wa misingi ya majumba na majengo; kwanza huanza kwa kujenga msingi ukawa imara kisha ndio kukajengwa nyumba na kupandishwa. Nyumba haiwezi kusimama bila ya msingi imara. Lau utajenga nyumba bila ya msingi imara wenye nguvu, basi nyumba itaporomoka na kuangamia waliomo humo ndani. Hali kadhalika Dini ikiwa haikujengeka katika  ‘Aqiydah swahiyh, inakuwa ni dini isiyomfaa mtu na wala haimnufaishi chochote, hata kama atajitaabisha vipi kufanya juhudi. Dini yake haitomfaa kitu, kwa kuwa haikujengeka juu ya msingi swahiyh, nao ni Tawhiyd. Kwa ajili hio, kitu cha kwanza walichoanza Rusuli (‘Alayhimus-Salaam) kuwalingania watu wao, ilikuwa ni Tawhiyd, nayo ni kabla ya kuwaamrisha Swalaah, Zakaah, Swawm n.k. Na ilikuwa ni kabla ya kuwakataza zinaa, wizi, kunywa pombe na maasi mengine, walianza kwanza kwa msingi ambao ni Tawhiyd. Na kila Nabiy alimwambia kaumu yake:

 

 يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ

“Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. 

 [Mwisho wa kunukuu maneno ya ‘Allaamah Al-Fawzaan].

 

 

Dalili hizo zimo katika kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu Rusuli Wake Wafuatao:

 

 

Nabiy Nuwh (‘Alayhis-Salaam):

 

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٢٣﴾

Kwa yakini Tulimpeleka Nuwh kwa kaumu yake, akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Je, basi hamtokuwa na taqwa?” [Al-Muuminuwn: 23]

 

 

 

Nabiy Huwd (‘Alayhis-Salaam):

 

وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٦٥﴾

Na kwa ‘Aad (Tuliwapelekea) kaka yao Huwd.  Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Je basi hamtokuwa na taqwa?”  [Al-A’raaf: 65]

 

 

Nabiy Swaalih ('Alayhis-Salaam):

 

وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ

 

Na kwa Thamuwd (Tuliwapelekea) kaka yao Swaalih. Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. [Al-A’raaf: 73]

 

 

Nabiy Shu’ayb ('Alayhis-Salaam):

 

وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ

Na kwa (watu wa) Madyan (Tuliwapelekea) kaka yao Shu’ayb.  Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake.  [Al-A’raaf: 85]

 

 

 Nabiy Ibraahiym ('Alayhis-Salaam):

 

وَإِبْرَاهِيمَ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ ۖ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٦﴾

Na Ibraahiym pale alipowaambia kaumu yake: “Mwabuduni Allaah na mcheni. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua. [Al-‘Ankabuwt: 16]

 

 

Nabiy Muwsaa ('Alayhis-Salaam):

 

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ

 

Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu yake: “Enyi kaumu yangu! Hakika nyinyi mmedhulumu nafsi zenu kwa kuabudu kwenu ndama, basi tubuni kwa Muumbaji wenu.  [Al-Baqarah: 54]

 

Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam):

 

 لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾

 

Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam.” Na Al-Masiyh alisema: “Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.” [Al-Maaidah: 72]

 

Na Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye aliwalingalia watu wake waliokuwa wakiabudu masanamu, miaka kumi na tatu alipokuwa Makkah kwa Tawhiyd kabla ya kufaridhishwa Swalaah, Zakaah, Swawm au Hajj. Akaamrishwa apigane na watu mpaka watu washuhudie kuwa laa ilaaha illa Allaah kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:

 

عن ابنِ عُمَرَ رضي الله عنهما أنَّ رسُوَل الله صلى الله عليه وسلم قال: ((أُمِرْتُ أَنْ أُقاتِلَ النَّاسَ حتَّى يَشْهَدُوا أنْ لا إلَهَ إلاَّ اللهُ وأنَّ محمداً رسوُل اللهِ، ويُقِيمُوا الصَّلاَةَ، ويُؤتُوا الزَّكاةَ، فإذا فَعَلوا ذَلِكَ عَصَموا منِّي دِماءَهُمْ وأمْوَالَهُمْ إلا بِحَقِّ الإِسْلامِ، وحِسابُهُم على اللهِ تعالى)

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiyaa Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washahadie: “laa ilaaha illa Allaah” (hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), na kwamba Muhammad ni Rasuli  wa Allaah mpaka watakaposwali, na wakatoa Zakaah na wakifanya hivyo, watakuwa wamepata himaya kwangu ya damu yao na mali yao isipokuwa kwa haki ya Uislamu. Na hesabu yao itakuwa kwa Allaah Ta’aalaa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share

15-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Rasuli (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Alitilia Umuhimu Mkubwa Kuhusu Tawhiyd

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

15-Rasuli (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

Alitilia Umuhimu Mkubwa Kuhusu Tawhiyd

 

 

 

 

Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alithibitisha Tawhiyd akatoa mafunzo kwa Maswahaba tokea kutumwa kwake kama Rasuli mpaka kufariki kwake. Ikawa Tawhiyd ni jambo kuu akilingania na kupigana vita kwa ajili yake. Alipomtuma Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa gavana wa Yemen na Qaadhwiy wao alimwambia: 

 

 

((إِنَّكَ تَأْتِي قَوْمًا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ, فَلْيَكُنْ أَوَّلَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ شَهَادَةَ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ))

((Unakwenda katika nchi ya watu wa Ahlul-Kitaab, kwa hiyo, jambo la kwanza walinganie katika shahada ya laa ilaaha illa Allaah)). [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 

 

Akawafundisha Maswahaba wengineo:

 

عن أبي عَمْرو، وَقِيلَ: أبي عَمْرَةَ، سُفْيَانَ بْنِ عَبْدِ اللهِ  رَضيَ اللهُ عَنْهُ قَال: قُلْتُ: يا رَسُولَ الله، قُلْ لي في الإِسْلاَمِ قَوْلاً، لاَ أَسْأَلُ عَنْهُ أَحَداً غَيْرَكَ. قَال: ((قُلْ: آمَنْتُ باللهِ ثُمَّ اسْتَقِمْ)).  

Kutoka kwa Abu 'Amru vile vile (anajulikana kama) Abu 'Amrah Sufyaan bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah, niambie kitu kuhusu Uislamu ambacho siwezi kumuuliza mtu yeyote isipokuwa wewe.  Akasema: ((Sema; Namuamini Allaah, kisha kuwa mwenye msimamo)) [Muslim]

 

Watoto pia aliwafundishwa Tawhiyd:

 

عَنْ أبي العَبَّاس عَبْدِ اللهِ بنِ عَبَّاسٍ رَضي اللهُ عنهما قال: كُنْتُ خَلْفَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يًوْماً، فقال: ((يا غُلامُ، إنِّي أُعَلِّمُكَ كلِماتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجاهَك، إذا سأَلْتَ فاسْأَلِ اللهَ، وإذا اسْتَعنْتَ فاسْتَعِنْ باللهِ، واعْلَمْ أنَّ الأُمَّة  لَوِ اجْتَمَعَتْ على أَنْ يَنْفَعُـوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيْءٍ قدْ كَتَبَهُ اللهُ لَكَ، وإن اجْتَمَعُوا على أن يَضُرَّوكَ بِشيءٍ لَمْ يَضُروكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأقْلامُ وَجَفَّتِ الصُّحُفُ))

Kutoka kwa Abul ‘Abbaas ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: “Siku moja nilikuwa nyuma ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: ((Ee kijana! Nitakufundisha maneno (yenye manufaa); Mhifadhi Allaah Atakuhifadhi. Muhifadhi Allaah na utamkuta mbele yako. Ukiomba, muombe Allaah, ukitafuta msaada tafuta kwa Allaah. Tambua kwamba, ikiwa ummah mzima utaungana kukunufaisha wewe kwa kitu, basi hutonufaika ila tu kwa kile Alichokwishakuandikia Allaah, na wakikusanyika kukudhuru kwa chochote, hotodhurika ila tu kwa kile Allaah Alichokwishakuandikia (kuwa kitakudhuru), kwani Kalamu zimeshanyanyuliwa na sahifa zimeshakauka (Majaaliwa yasiyobadilikika) [At-Tirmidhiy akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]   

 

 

Mpaka katika hali ya kufariki kwake alitilia umuhimu mkubwa Tawhiyd:

 

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي مَرَضِهِ الَّذِي لَمْ يَقُمْ مِنْهُ: ((لَعَنَ اللَّهُ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى اتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ))

Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema alipokuwa katika maradhi ambayo hakuinuka tena [alipokaribia kufariki]: ((Allaah Amewalaani Mayahudi na Manaswara wamegeuza makaburi ya Manabii wao kuwa Misikiti))  [Al-Bukhaariy na Muslim na wengineo]

 

Nabiy Ya’quwb (‘Alayhis-Salaam) naye pia aliwausia wanawe alipokuwa karibu na kufariki kwake:

 

 أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِن بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٣﴾

Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfikia Ya’quwb alipowaambia wanawe: “Mtaabudu nini baada yangu?” Wakasema: “Tutamwabudu Ilaaha wako (Allaah) na Ilaaha wa baba zako, Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq; Ilaah Mmoja, nasi ni Waislamu (tunajisalimisha) Kwake.” [Al-Baqarah: 133]

 

 

 

Share

16-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Ukilala Ukiamka Utamke Neno La Tawhiyd

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

16-Ukilala Ukiamka Utamke Neno La Tawhiyd

 

 

Mafundisho ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yanatujulisha kuwa jambo la kwanza la kufanya unapoamka ni kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa Tawhiyd (kumpwekesha), na kwamba fadhila zake ni kutakabaliwa mtu haja zake:

 

عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ تَعَارَّ مِنْ اللَّيْلِ فَقَالَ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ  وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ. ثُمَّ قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي  أَوْ دَعَا اسْتُجِيبَ لَهُ, فَإِنْ عَزَمَ فَتَوَضَّأَ ثُمَّ صَلَّى قُبِلَتْ صَلَاتُهُ))

Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeamka usiku akasema: “Laa ilaaha illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa-Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, wa Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah walaa ilaaha illa-Allaah wa-Allaahu Akbar walaa hawla walaa quwwata illa biLLaah” (Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Pekee Hana mshirika, Ufalme ni Wake na Himdi ni Zake Naye ni Mweza wa kila kitu. Ametakasika Allaah, na Himdi ni za Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Allaah ni Mkubwa kabisa, hapana uwezo wala nguvu ila za Allaah), kisha akasema: “Rabbigh-fir-liy” [ee Allaah, nighufurie] au akaomba, ataitikiwa. Na akiazimia kutawadha na kuswali atatakabaliwa Swalah yake)). [Al-Bukhaariy na wengineo]

 

 

Na katika Swalaah ya Sunnah ya Alfajiri ambayo ni rakaa mbili unatakiwa usome, Suwratul-Kaafiruwn (109) na Suwratul-Ikhlaasw (112) na [Suwratul-Baqarah 2: 136], [Suwratul-‘Imraan 3: 84].

 

 

Adhkaaar na Nyiradi za asubuhi zote zimetaja Tawhiyd (Rejea Kitabu cha Hiswnul Muslim kinapatikana ndani ya alhidaaya.com), vilevile ndani ya Swalaah tunatamka Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Kadhaalika unapotaka kulala ni Sunnah usome, Suwratul-Ikhlaasw (112), Al-Mu’awidhataan (113, 114) ambazo zinasomwa pia katika Swalaah ya Witr pamoja na Suwratul-Kaafiruwn (109), Aayatul-Kursiyy 2: 255), na Aayah mbili za mwisho za [Suwratul-Baqarah 2: 285- 286], Suwratul-Mulk (67) Suwratus-Sajdah (32) na pia adhkaar mbali mbali za wakati wa kulala. Baadhi ya hizo adhkaar ni kama zifuatazo:

 

 

Hadiyth ya Al-Baraaa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

((إِذَا أَتَيْتَ مَضْجَعَكَ فَتَوَضَّأْ وُضُوءَكَ لِلصَّلَاةِ، ثُمَّ اضْطَجِعْ عَلَى شِقِّكَ الْأَيْمَنِ، ثُمَّ قُلْ: اللّهُـمَّ أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت. ((فَإِنْ مُتَّ مِنْ لَيْلَتِكَ فَأَنْتَ عَلَى الْفِطْرَةِ، وَاجْعَلْهُنَّ آخِرَ مَا تَتَكَلَّمُ بِهِ))

((Utakapofika kitandani mwako [kutaka kulala] tawadha wudhuu kama wa Swalaah kisha lalia ubavu wako wa kulia kisha sema: 

 

Allaahumma aslamtu nafsiy Ilayka, wa fawwadhwtu amriy Ilayka, wa wajjahtu waj-hiya Ilayka, wa alja-tu dhwahriy Ilayka, raghbatan warahbatan Ilayka. Laa malja-a walaa manjaa Minka illaa Ilayka. Aamantu Bikitaabikal-ladhiy Anzalta wabi Nabiyyikal-lladhiy Arsalta.

Ee Allaah, nimeisalimisha nafsi yangu Kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe na nimeuelekeza uso wangu Kwako na nimeutegemeza mgongo wangu Kwako, kwa matajarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila Kwako. Nimekiamini Kitabu Chako Ulichokiteremsha na Nabii Wako uliyemtuma.  

 

((Ukifariki usiku huo utafariki katika fitwrah [maumbile ya asli ya Tawhiyd], na ifanyeni iwe ya [dhikri] ya mwisho kuisoma)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Kadhaalika adhkaar ya kulala iliyotajwa katika Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ni:

 

اللّهُـمَّ رَبَّ السّمـواتِ السَّبْـعِ وَرَبَّ العَـرْشِ العَظـيم، رَبَّنـا وَرَبَّ كُـلِّ شَـيءٍ، فالِـقَ الحَـبِّ وَالنَّـوى، وَمُـنَزِّلَ التَّـوْراةِ وَالإنْجـيلِ والفُـرْقانِ. أَعُـوذُ بِـكَ مِن شَـرِّ كُـلِّ شَـيءٍ أَنْـتَ آخِـذٌ بِنـاصِـيَتِهِ. اللّهُـمَّ أَنْـتَ الأوَّلُ فَلَـيسَ قَبْـلَكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الآخِـرُ فَلَـيسَ بَعْـدَكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الظّـاهِـرُ فَلَـيْسَ فَـوْقَـكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الْبـاطِـنُ فَلَـيْسَ دونَـكَ شَيءٌ، اقـْضِ عَنّـا الـدَّيْـنَ وَأَغْـنِنـا مِنَ الفَـقْرِ

((Allaahumma Rabbas-samawaatis-sab’-i wa Rabbal-’Arshil-’Adhwiym. Rabbanaa wa Rabba kulli shay-in. Faaliqal-habbi wan-nnawaa, wa munzilat-Tawraati wal-Injiyli wal-Furqaan. A’uwdhu Bika minsharri kulli shay-in Anta Aakhidhun binaaswiyatihi. Allaahumma Antal-Awwalu falaysa Qablaka shay-un. Wa Antal-Aakhiru falaysa Ba’-daka shay-un. Wa Antadh-Dhwaahiru falaysa Fawqaka shay-un. Wa Antal-Baatwinu falaysa Duwnaka shay-un. Iqdhwi ‘annad-dayna waghninaa minal-faqri.

Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba na Rabb wa ’Arshi Tukufu. Rabb wetu na Rabb wa kila kitu. Mpasuaji wa mbegu na kokwa (zikawa miche) na Aliyeteremsha Tawraati na Injiyl  na Qur-aan. Najikinga Kwako kutokana na shari ya kila kitu. Wewe Ndiye Mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah Wewe Ndiye wa Mwanzo hakuna kitu kabla Yako. Nawe Ndiye wa Mwisho hakuna kitu chochote baada Yako. Nawe Ndiye Uliye juu hakuna kitu chochote juu Yako. Nawe Ndiye Uliye karibu hakuna kitu chochote kilicho karibu kuliko Wewe, Tulipie madeni yetu na Utuepushe na ufakiri)) [Muslim]

 

Na pindi unapokosa usingizi ukawa unajigeuzageuza kitandani, utasoma yaliyomo katika Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa):

 

لا إِلـهَ إِلاّ اللهُ الـواحِدُ القَهّـار، رَبُّ السَّـمواتِ وَالأرْضِ وَما بَيْـنَهـما، العَزيـزُ الغَـفّار

Laa ilaaha illa-Allaahul-Waahidul-Qahhaar. Rabbus-samawaati wal-ardhwi wamaa baynahuma, Al-’Aziyzul-Ghaffaar.

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah  Al-Waahid (Mmoja Pekee) Al-Qahhaar (Mshindi Mwenye kudhibiti na kudhalilisha). Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake, Al-’Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima) Al-Ghaffaar (Mwingi wa kughufuria). [Al-Haakim na ameisahihisha Adh-Dhahabiy (1/540), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [864] na Ibn As-Sunniy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [757]. Na tazama Swahiyh Al-Jaami’ (4/213) [4693].

 

 

Unapoamka kuswali Tahajjud ni Sunnah kusoma Suwratul-’Imraan (3:190-200). Pia adhkaaar zifuatazo:

 

Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) imetajwa adhkaar ifuatayo:

 

اللّهُـمَّ رَبَّ جِـبْرائيل، وَميكـائيل، وَإِسْـرافيل، فاطِـرَ السَّمواتِ وَالأَرْض، عالـِمَ الغَيْـبِ وَالشَّهـادَةِ أَنْـتَ تَحْـكمُ بَيْـنَ عِبـادِكَ فيـما كانوا فيهِ يَخْتَلِفـون. اهدِنـي لِمـا اخْتُـلِفَ فيـهِ مِنَ الْحَـقِّ بِإِذْنِك، إِنَّـكَ تَهْـدي مَنْ تَشـاءُ إِلى صِراطٍ مُسْتَقـيم

Allaahumma Rabba Jibraaiyla wa Mikaaiyla wa Israafiyla, faatwiras-samaawaati wal ardhw, ’Aalimal ghaybi wash-shahaadah, Anta Tahkmu bayna ’ibaadika fiymaa kaanuw fiyhi yakhtalifuwn. Ihdiniy limakhtulifa fiyhi minal haqqi bi-idhnika Innaka Tahdiy man Tashaau ilaa swiraatwil-mustaqiym.

 

Ee Allaah, Rabb wa Jibiriyl na Mikaaiyl na Israafiyl, Mwanzishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa mambo ya ghayb na yaliyo wazi, Wewe Unahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitofautiana. Niongoze mimi kwenye haki katika yale ambayo (watu) wametofautiana kwa idhini Yako.  Hakika Wewe unamuongoza Umtakae kwenye njia ilionyoka. [Muslim]

 

Kadhaalika Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) imetajwa adhkaar ifuatayo:

 

 

اللّهُـمَّ لَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ  نـورُ السَّمـواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِنَّ، وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ قَـيِّمُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ  وَمَنْ فيـهِنَّ، (وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ رَبُّ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ  وَمَنْ فيـهِنَّ) (وَلَكَ الْحَمْدُ لَكَ مُلْـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ  وَمَنْ فيـهِنَّ) (وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ مَلِـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ) (وَلَكَ الْحَمْدُ) (أَنْتَ الْحَـقُّ وَوَعْـدُكَ الْحَـقُّ،  وَقَوْلُـكَ الْحَـقُّ، وَلِقـاؤُكَ الْحَـقُّ،  وَالْجَـنَّةُحَـقُّ، وَالنّـارُ حَقُّ، وَالنَّبِـيّونَ حَـقُّ، وَمـحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم حقُّ، والسَّاعَةُ حَـقُّ)  (اللّهُـمَّ لَكَ أَسْلَمتُ، وَعَلَـيْكَ تَوَكَّلْـت، وَبِكَ آمَنْـت، وَإِلَـيْكَ أَنَبْـتُ، وَبِـكَ خاصَمْتُ، وَإِلَـيْكَ حاكَمْـتُ، فاغْفِـرْ لي مـا قَدَّمْتُ، وَما أَخَّـرْتُ، وَما أَسْـرَرْتُ، وَما أَعْلَـنْتُ) (أَنْتَ المُقَـدِّمُ وَأَنْتَ المُـؤَخِّر، لاَ إلَهَ إِلاّ أَنْـت) (أَنْـتَ إِلـهي لا  إلَهَ  إِلاّ أَنْـت)

Allaahumma Lakal-Hamdu Anta Nuwrus-samaawati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Anta Qayyimus-samaawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Anta Rabbus-samawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Laka Mulkus-samaawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Antal-Haqqu, wawa’dukal-haqqu, waqawlukal-haqqu, waliqaaukal-haqqu, wal-Jannata haqqun, wannaaru haqqun, wannabiyyuwna haqqun, wa Muhammadun  SwallaAllaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam haqqun, was-saa’atu haqqun. Allaahumma Laka aslamtu, wa ’Alayka tawakkaltu, wabika aamantu, wa Ilayka anabtu, wabika khaaswamtu, wa Ilayka haakamtu, faghfir liy maa qaddamtu wamaa akh-khartu, wamaa asrartu, wamaa a’lantu, Antal-Muqaddimu wa Antal-Muakh-khiru laa ilaaha illa Anta. Anta Ilaahiy laa ilaaha illa Anta.

 

Ee Allaah, Himdi ni Zako, Wewe Ndiye Nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Himdi ni Zako, Wewe Ndiye sababu ya kusimama kwa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Himdi ni Zako, Wewe Ndiye  Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake; na Himdi ni Zako, Wewe Ndiye  Mfalme wa mbingu na ardhi, na Himdi ni Zako, Wewe ni haki [kweli] na ahadi Yako ni ya kweli, na neno Lako ni la kweli, na kukutana na Wewe ni kweli, na Jannah ni kweli, na Moto ni kweli, na Manabii ni kweli, na Muhammad SwallaAllaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam ni kweli, na Qiyaamah ni kweli. Ee Allaah, Kwako nimejisalimisha, na kwako nimetawakali, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimerejea kutubia.

Na kwa ajili Yako (au kwa hoja na dalili Zako) nimetetea (maadui Wako). Na nimeelekea Kwako kukufanya Wewe ni Hakimu Wangu (kuhukumu baina yetu). Basi  nighufurie niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza; Wewe Ndiye Al-Muqaddimu (Mwenye kutanguliza) na Al-Muakh-khiru (Mwenye kuchelewesha), hapana  mwabudiwa wa haki ila Wewe; Wewe Ndiye Mwabudiwa wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe. [Al-Bukhaariy]

 

 

Share

17-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Tawhiyd Ndiyo Inayotenganisha Baina Ya Uislamu Na Ukafiri Au Baina Ya Muislamu Na Kafiri

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

17-Tawhiyd Ndiyo Inayotenganisha Baina Ya Uislamu Na Ukafiri

Au Baina Ya Muislamu Na Kafiri

 

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾

Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine kuwa waabudiwa badala ya Allaah.” Wakikengeuka; basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu.” [Aal-‘Imraan: 64]

 

 

Na pia Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾

Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.” Na hali hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Ilaah Mmoja Pekee. Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo. [Al-Maaidah: 73]

 

Neno la Tawhiyd “Laa ilaaha illa Allaah” ndio neno ambalo atakapolitamka mtu akiwa anakiri moyoni kwamba hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, na kumalizia kuamini kwamba Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mja na Rasuli wa Allaah, humuingiza katika Uislamu. Lakini Uislamu wake utatimia kikamilifu pale atakapoamini kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa Hana mshirika na atakapofuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake. Vilevile kumwamini Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kuamini kwamba hakuna ‘ibaadah au mafunzo yoyote yale isipokuwa aliyokuja nayo yeye Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Muislamu atakapothibitika nalo neno la Tawhiyd, huwa ni ufunguo wake wa Jannah kwa dalili ifuatayo:

 

عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ :((مَنْ قَالَ: "أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللَّهِ وَابْنُ أَمَتِهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ وَأَنَّ الْجَنَّةَ حَقٌّ وَأَنَّ النَّارَ حَقٌّ" أَدْخَلَهُ اللَّهُ مِنْ أَيِّ أَبْوَابِ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةِ شَاءَ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit ambaye amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) amesema: ((Atakayesema: “Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laashariyka lahu, wa anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu – Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Peke Yake, Hana mshirika na kwamba Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake, na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah, na ni mwana wa mja wake na Neno Lake Alimtupia Maryam na Ruwh kutoka Kwake, na kwamba Jannah ni haki, na Moto ni haki” Allaah Atamuingiza Jannah kupitia mlango wowote autakao miongoni mwa milango minane ya Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Abuu Twaalib ambaye ni ‘ammi yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataa kutamka neno la Tawhiyd wakati alipokuwa anafariki, na hivyo juu ya kuwa ni ‘ammi yake ambaye alimhami na maudhi ya makafiri Quraysh wa Makkah, lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amemhukumia Moto kwa dalili:

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أَهْوَنُ أَهْلِ النَّارِ عَذَابًا أَبُو طَالِبٍ وَهُوَ مُنْتَعِلٌ بِنَعْلَيْنِ يَغْلِي مِنْهُمَا دِمَاغُهُ))‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wasallam) amesema: ((Adhabu nyepesi kabisa ya watu Motoni ni adhabu ya Abuu Twaalib, atakuwa amevaa viatu [vya moto] vitakavyomsababisha bongo lake kuchemka)).[Muslim]

 

 

Na kisa katika Hadiyth ifuatayo cha kijana wa kiyahudi aliyesilimu:

 

فعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: كَانَ غُلَامٌ يَهُودِيٌّ يَخْدُمُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَمَرِضَ، فَأَتَاهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَعُودُهُ، فَقَعَدَ عِنْدَ رَأْسِهِ فَقَالَ لَهُ: أَسْلِمْ! فَنَظَرَ إِلَى أَبِيهِ وَهُوَ عِنْدَهُ، فَقَالَ لَهُ أَطِعْ أَبَا الْقَاسِمِ، صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ . فَأَسْلَمَ ، فَخَرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يَقُولُ : ((الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنْقَذَهُ مِنْ النَّارِ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba kulikuweko na mtoto (kijana mdogo) wa kiyahudi akimhudumia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alipoumwa, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikwenda kumtembelea, akaketi pembeni ya kichwa chake akamwambia: ((Silimu!)). Mtoto akamtazama baba yake aliyekuweko hapo. Akamwambia: “Mtii Abal-Qaasim Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam”.  Akasilimu. Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatoka huku akisema: ((AlhamduliLLaah – Himdi ni za Allaah Ambaye Amemuokoa na Moto)). [Al-Bukhaariy (1356), Ahmad (13565) na Abu Daawuwd (3095)]

 

 

Na Tawhiyd ndio sababu ya Al-Walaa wal-Baraa (Kupendana na kuandamana kwa ajili ya Allaah (Dini) na kuchukiana au kutengana kwa ajili ya Allaah)

 

Na ndio maana Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na usuhuba na mapenzi na Bilaal na Maswahaba wengineo waliokuwa watumwa ambao waliingia katika Uislamu kwa sababu ya Dini, na akatengana na Abuu Twaalib na Abuu Lahab kwa sababu ya wao kuikana Dini ya Kiislamu. Hali kadhaalika Maswahaba walitengana na baadhi ya ahli zao kwa sababu ya ukafiri wao. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٢٢﴾

Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanafanya urafiki na kuwapenda wanaompinga Allaah na Rasuli Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao (Allaah) Amewaandikia katika nyoyo zao iymaan, na Akawatia nguvu kwa Ruwh (Wahyi) kutoka Kwake, na Atawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allaah. Tanabahi! Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufaulu.   [Al-Mujaadalah: 22]

 

 

Share

18-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Kunyooka Katika Tawhiyd Ni Sababu Ya Kupata Husnul-Khaatimah

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

18-Kunyooka Katika Tawhiyd Ni Sababu Ya Kupata Husnul-Khaatimah

 

 

 

Muislamu anapothibitika katika iymaan na taqwa, hubashiriwa Jannah wakati anapofikwa na mauti:  Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

 

 إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْتُوعَدُونَ﴿٣٠﴾

 

Hakika wale waliosema: “Rabb wetu ni Allaah.” Kisha wakathibitika imara; Malaika huwateremkia: (kuwaambia): “Msikhofu, na wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa.”

 

 

نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ﴿٣١﴾

 

“Sisi ni rafiki zenu walinzi katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mtakayoomba.

 

نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ﴿٣٢﴾

“Ni mapokezi ya takrima kutoka kwa Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu.” [Fusw-Swilat: 30-32]

 

Kadhaalika, Muislamu anahitaji kuthibitika katika neno la Tawhiyd ili asalimike kaburini na aweze kujibu maswali matatu atakayoulizwa na Malaika wawili; Munkar na Nakiyr.

 

عَنْ الْبَرَاء بْن عَازِب رَضِيَ اللَّه عَنْهُ أَنَّ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((الْمُسْلِم إِذَا سُئِلَ فِي الْقَبْر شَهِدَ أَنْ لاَ إِلَه إِلاَّ اللَّه وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُول اللَّه فَذَلِكَ قَوْله (يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ))) البخاري  وَرَوَاهُ مُسْلِم أَيْضًا وَبَقِيَّة الْجَمَاعَة

Imetoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Muislamu akiulizwa katika kaburi, atashuhudia kwamba: "Laa ilaaha Illa-Allaah wa Anna Muhammadar-Rasuulu-Allaah" [Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli wa Allaah] hiyo ndiyo maana ya kauli ya Allaah: “Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah.”)) [Ibraahiym: 27 - Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 

Neno hilo limepigiwa mfano na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni kama mti mzuri:

 

عَنْ ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) قَال: كُنَّا عِنْد رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: ((أَخْبِرُونِي عَنْ شَجَرَة تُشْبِه - أَوْ - كَالرَّجُلِ الْمُسْلِم لاَ يَتَحَاتّ وَرَقهَا صَيْفًا وَلاَ شِتَاء وَتُؤْتِي أُكُلَهَا كُلّ حِين بِإِذْنِ رَبّهَا)) قَالَ اِبْن عُمَر: فَوَقَعَ فِي نَفْسِي أَنَّهَا النَّخْلَة وَرَأَيْت أَبَا بَكْر وَعُمَر لاَ يَتَكَلَّمَانِ فَكَرِهْت أَنْ أَتَكَلَّمَ فَلَمَّا لَمْ يَقُولُوا شَيْئًا. قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ: ((هِيَ النَّخْلَة)). فَلَمَّا قُمْنَا قُلْت لِعُمَرَ: يَا أَبَتَاهُ وَاَللَّه لَقَدْ كَانَ وَقَعَ فِي نَفْسِي أَنَّهَا النَّخْلَة. قَالَ: مَا مَنَعَك أَنْ تَتَكَلَّم؟ قُلْت: لَمْ أَرَكُمْ تَتَكَلَّمُونَ فَكَرِهْت أَنْ أَتَكَلَّم أَوْ أَقُول شَيْئًا.  قَالَ عُمَر: لَأَنْ تَكُون قُلْتهَا أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ كَذَا وَكَذَا - البخاري

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: "Tulikuwa na Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi  wa sallam) akauliza: ((Niambieni kuhusu mti unaofanana na au kama Muislamu, ambao majani yake hayaanguki wakati wa majira ya joto, wala wakati wa majira ya baridi, na hutoa matunda yake kila mara kwa idhini ya Rabb wake)). Ibn ‘Umar akasema: “Niliufikiria kuwa ni mtende, lakini niliona vibaya kujibu nilipoona Abuu Bakr na ‘Umar hawakujibu”. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Ni mtende)). Tulipoondoka, nilimwambia ‘Umar: “Ee baba yangu! Wa-Allaahi nilihisi kuwa ni mtende”. Akasema: “Kwa nini basi hukutaja?” Nikasema: “Nilikuoneni kimya, nikaona vibaya kusema kitu”. Akasema ‘Umar: "Ungelisema, ingelikuwa bora kwangu kuliko kadhaa na kadhaa” (Yaani ningelikuwa na fakhari zaidi kuwa wewe mwanangu ndiye uliyeweza kujibu pekee). [Al-Bukhaariy]

 

 Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) imethibitisha hayo Anaposema:

 

 أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ ﴿٢٤﴾

Je, huoni vipi Allaah Amepiga mfano wa neno zuri kama mti mzuri mizizi yake imethibitika imara na matawi yake yanafika mbinguni? (marefu mno).

 

 

تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا ۗ وَيَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٥﴾

Unatoa mazao yake kila wakati kwa idhini ya Rabb wake. Na Allaah Anapiga mifano kwa watu ili wapate kukumbuka.

 

 

وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِن فَوْقِ الْأَرْضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٍ ﴿٢٦﴾

Na mfano wa neno baya ni kama mti mbaya uliong’olewa juu ya ardhi hauna imara.

 

 

يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّـهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ﴿٢٧﴾

Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotoka madhalimu. Na Allaah Anafanya Atakavyo.  [Ibraahiym: 24-27]

 

 

 

 

Share

19-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Tawhiyd Ni Bora kuliko Mali Na Starehe Za Dunia, Neno La Tawhiyd Ni Zito Siku ya Qiyaamah

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

19-Tawhiyd Ni Bora kuliko Mali Na Starehe Za Dunia,

Neno La Tawhiyd Ni Zito Siku ya Qiyaamah

 

 

 

Makafiri Quraysh wa Makkah walitaka kumpa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mali na starehe za dunia, walitaka kumpa cheo  ili aache kulingania Tawhiyd, lakini Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakufadhilisha hayo, bali alijikita katika da’wah yake kwa kuwa aliamini kulingania Tawhiyd ndio haki na ndio itakayomfaa bin Aadam Siku ya Qiyaamah, Siku ambayo mtu atatamani kufidia kwa mali yake yote aliyokuwa nayo duniani ili aepukane na adhabu ya Moto kwa kukanusha Tawhiyd kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾

Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao dhahabu ya ujazo wa dunia nzima lau wakitaka kujifidia nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru. [Aal-‘Imraan: 91]

 

Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hadiyth iliyosimuliwa na Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

 

((يَقُولُ اللهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى لِأَهْوَنِ أَهْلِ النَّارِ عَذَابًا: لَوْ كَانَتْ لَكَ الدُّنْيَا وَمَا فِيهَا، أَكُنْتَ مُفْتَدِيًا بِهَا؟ فَيَقُولُ: نَعَمْ ، فَيَقُولُ: قَدْ أَرَدْتُ مِنْكَ أَهْوَنَ مِنْ هَذَا وَأَنْتَ فِي صُلْبِ آدَمَ: أَنْ لَا تُشْرِكَ - أَحْسِبُهُ قَالَ: وَلَا أُدْخِلَكَ النَّارَ - فَأَبَيْتَ إِلَّا الشِّرْك))

((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Atamwambia mtu atakayekuwa na adhabu nyepesi kabisa Motoni: “Je, ungekuwa una dunia nzima na yaliyomo ndani yake [mali n.k.] ungeitolea fidia?” Atajibu: “Ndio.” Atasema Allaah: “Nilikutaka kwa jambo jepesi zaidi kuliko hayo, ulipokuwa katika uti wa mgongo wa Aadam kwamba usinishirikishe.” Nadhani Akasema: “Na sitokuingiza motoni lakini umekataa isipokuwa kunishirikisha”)). [Muslim]

 

Ni dhahiri kwamba neno la Tawhiyd ambalo ni jambo jepesi kabisa kulitamka litakuwa na thamani zaidi kuliko dunia na yaliyomo duniani, bali neno la Tawhiyd; laa ilaa illa Allaah litakuwa zito kabisa katika Miyzaan ya ‘amali Siku ya Qiyaamah:

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرَيِّ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ الله (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ ((قَالَ مُوسَى عَلَيْهِ السَّلامُ يَا رَبِّ! عَلِّمْنِي شَيْئًا أَذْكُرُكَ وَأَدْعُوكَ بِهِ. قَالَ: قُلْ يَا مُوسَى: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ.  قَالَ يَا رَبِّ! كُلُّ عِبَادِكَ يَقُولُونَ هَذَا. قَالَ: يَا مُوسَى،  لَوْ أَنَّ السَّمَوَاتِ السَّبْعَ وَعَامِرَهُنَّ غَيْرِي وَالأَرَضِينَ السَّبْعَ فِي كِفَّةٍ،  وَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ فِي كِفَّةٍ، مَالَتْ بِهِنَّ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ))  رَوَاهُ ابْنُ حِبَّانَ وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ.

Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muwsaa alisema: Ee Rabb wangu! Nifundishe kitu mahsusi kwangu ambacho kwacho nitakudhukuru na kukuomba duaa. (Allaah) Akasema: Ee Muwsaa!    Sema:

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ 

Laa ilaaha illa-Allaah.  

 

Muwsaa akasema: Ee Rabb wangu! Waja Wako wote wanasema hivi. (Allaah) Akasema: Ee Muwsaa, lau kama mbingu saba na kila kilichokuwemo isipokuwa Mimi, na ardhi saba zikiwekwa katika kiganja cha mizani, na laa ilaaha illa-Allaah ikawekwa katika kiganja kingine cha mizani, basi laa ilaaha illa-Allaah itazishinda hizo.” [Ibn Hibaan, na Al-Haakim ameikiri kuwa ni Swahiyh]

 

 

 

 

 

 

Share

20-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Tawhiyd Inamuepushia Mtu Majanga Na Balaa

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

20-Tawhiyd Inamuepushia Mtu Majanga Na Balaa

 

 

 

 

Majanga na balaa yanaondoshwa kwa Tawhiyd, na ndio maana du’aa za kuepushwa na hayo zimekuwa ni kwa Tawhiyd, na du’aa ya Nabiy Yuwnus (‘Alayhis-Salaam) alipokuwa katika kiza na dhiki ndani ya tumbo la samaki (nyangumi) ilikuwa ni ya Tawhiyd na kwayo akaokolewa na kupata faraja. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa): 

 

وَذَا النُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾

Na Dhan-Nuwn (Yuwnus) alipoondoka akiwa ameghadhibika, akadhani kwamba Hatutamdhikisha; akaita katika kiza kwamba: “Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Subhaanak! Utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.”

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamuitikia:

 

فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُنجِي الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨٨﴾

Basi Tukamuitikia na Tukamuokoa kutokana na ghamu. Na hivyo ndivyo Tuwaokowavyo Waumini. [Al-Anbiyaa: 87-88]

 

 

Du’aa hiyo ya Nabiy Yuwnus (‘Alayhis-Salaam) pia ni sababu ya Muislamu kutakabaliwa haja zake kama ilivyokuja dalili katika Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ سَعْدٍ عَنْ أَبِيهِ عَنْ سَعْدٍ  (رضي الله عنه)  قَالَ:  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم): ((دَعْوَةُ ذِي النُّونِ إِذْ دَعَا وَهُوَ فِي بَطْنِ الْحُوتِ:  لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ  .فَإِنَّهُ لَمْ يَدْعُ بِهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ فِي شَيْءٍ قَطُّ إِلاَّ اسْتَجَابَ اللَّهُ لَهُ))

Kutoka kwa Ibraahiym bin Muhammad bin Sa’d kutoka kwa baba yake kutoka kwa Sa’d (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Du’aa ya Dhan-Nuwn alipoomba alipokuwa katika tumbo la nyangumi, “Laa ilaaha illa Anta Subhaanaka inniy kuntu minadhw-dhwaalimiyn.” Basi hakika hakuna mtu Muislamu aombaye kwayo kitu chochote kile ila Allaah Atamuitikia)). [Swahiyh At-Tirmidhy] 

 

Na Hadiyth zifuatazo zimetaja baadhi ya adhkaar ambazo zinamuondoshea mtu kila aina ya dhiki, janga na balaa.  

 

Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa):

 

لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ الْعَظـيمُ الْحَلِـيمْ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُرَبُّ العَـرْشِ العَظِيـمِ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُرَبُّ السَّمَـوّاتِ ورّبُّ الأَرْضِ ورَبُّ العَرْشِ الكَـريم 

Laa ilaaha illa-Allaahul-‘Adhwiymul-Haliym. Laa ilaaha illa-Allaahu Rabbul-‘Arshil-‘Adhwiym. Laa ilaaha illa-Allaahu Rabbus-samawaati wa Rabbul-Ardhwi wa Rabbul-‘Arshil-Kariym. 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Aliye Mtukufu Mpole. Hapana mwabudiwa wa haki  ila Allaah Rabb wa ‘Arshi Tukufu. Hapana mwabudiwa wa haki  ila Allaah Rabb wa mbingu na Rabb wa ardhi na Rabb wa ‘Arshi tukufu. [Al-Bukhaariy (7/154) [6346], Muslim (4/2092) [2730] na Ahmad] 

 

 

Hadiyth ya Abu Bakr Nafiy’ bin Haarith Ath-Thaqafiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu): 

 

اللّهُـمَّ رَحْمَتَـكَ أَرْجـو فَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـيْن، وَأَصْلِـحْ لي شَأْنـي كُلَّـه لَا إِلَهَ إِلَّا أنْـت 

Allaahumma Rahmataka arjuw falaa takilniy ilaa nafsiy twarfata ‘ayni, wa aswlih liy sha-niy kullahu, laa ilaaha illaa Anta. 

Ee Allaah, Rehma Zako nataraji,usinitegemeze kwenye nafsi yangu japo kwa muda wa upepeso wa jicho, na Unitengenezee mambo yangu yote, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe. [Abu Daawuwd (4/324) [5090], Ahmad (5/42), ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Abiy Daawuwd (3/959)]  

 

 

Hadiyth ya Asmaa bint ‘Umays (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:   

    

((أَلَا أُعَلِّمُكِ كَلِمَاتٍ تَقُولِينَهُنَّ عِنْدَ الْكَرْبِ اللهُ اللهُ رَبِّي لا أُشْـرِكُ بِهِ شَيْـئاً))

 

((Je, nikufunidshe maneno uyaseme wakati wa janga: Allaah, Allaah, Rabb wangu, simshirikishi na chochote)). [Abu Daawuwd (2/87) [1525] na taz. Swahiyh Ibn Maajah (2/335)] 

 

Hata makafiri waliondoshewa janga pale walipokuwa wakimuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa ikhlaasw. Mfano pale walipopanda jahazi dhoruba kali ikawafikia iliyokaribia kuwazamisha, walimkabili Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee bila ya kumshirikisha mtu kumuomba Awaokoe kama ilivyo dalili katika kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):  

 

هُوَ الَّذِي يُسَيِّرُكُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا كُنتُمْ فِي الْفُلْكِ وَجَرَيْنَ بِهِم بِرِيحٍ طَيِّبَةٍ وَفَرِحُوا بِهَا جَاءَتْهَا رِيحٌ عَاصِفٌ وَجَاءَهُمُ الْمَوْجُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ أُحِيطَ بِهِمْ ۙ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ لَئِنْ أَنجَيْتَنَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ﴿٢٢﴾

Yeye Ndiye Anayekuendesheni katika bara na bahari. Mpaka mnapokuwa katika majahazi na yanakwenda nao kwa upepo mzuri, na wakafurahia; mara ukawajia upepo wa dhoruba, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakayakinisha kwamba wameshazungukwa. Hapo humwomba Allaah wenye kumtakasia Yeye Dini (wakisema): “Ukituokoa katika haya, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.” [Yuwnus: 22] 

 

Lakini baada ya kuwaokoa wanarudi kumshirikisha: 

 

فَلَمَّا أَنجَاهُمْ إِذَا هُمْ يَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا بَغْيُكُمْ عَلَىٰ أَنفُسِكُم ۖ مَّتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُكُمْ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٣﴾

 

Lakini Anapowaokoa, tahamaki wao wanafanya baghi katika ardhi bila ya haki. Enyi watu! Hakika baghi yenu ni dhidi ya nafsi zenu. Ni starehe ya uhai wa dunia. Kisha Kwetu marejeo yenu; Tutakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda. [Yuwnus: 23] 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

فَإِذَا رَكِبُوا فِي الْفُلْكِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ ﴿٦٥﴾

Wanapopanda merikebu humwomba Allaah wakiwa wenye kumtakasia Yeye Dini, lakini Anapowaokoa katika nchi kavu, tahamaki hao wanamshirikisha. [Al-‘Ankabuwt: 65]

 

Share

21-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Tawhiyd Ni Sharti Ya Kupata Shafaa’ah Ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

21-Tawhiyd Ni Sharti Ya Kupata Shafaa’ah Ya

Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

 

 

 

 

Sharti la kwanza kuweza kupata Shafaa’ah Siku ya Qiyaamah ni kuthibitisha Tawhiyd. Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema:

 

قُلْتُ يَا رَسُولَ اللهِ مَنْ أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِكَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ؟ قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلى اللهُ عليهِ وَسَلَّمَ: ((لَقَدْ ظَنَنْتُ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ أَنْ لا يَسْأَلَني عَنْ هذَا الْحَدِيِثِ أَحَدٌ أَوَّلَ مِنْكَ لِما رَأَيْتُ مِنْ حِرْصِكَ عَلَى الْحَدِيثِ أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَنْ قَالَ: لا إِلهَ إِلاَّ اللهُ خَالِصَاً مِنْ قَلْبِهِ أَوْ نَفْسِهِ))

“Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Nani atakayefurahika kabisa kwa Shafaa’ah (uombezi) wako Siku ya Qiyaamah: Akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): ((Nilidhani ee Abaa Hurayrayh kwamba hakuna yeyote asiyekuwa wewe atakayeniuliza maelezo haya kwa vile jinsi nilivyoona himma yako juu ya jambo hili. Atakayefurahika zaidi kati ya watu kwa Shafaa’ah yangu Siku ya Qiyaamah ni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah – hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, kwa niyyah safi moyoni mwake au nafsi yake)). [Al-Bukhaariy]

 

Na Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa):

 

قال النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: ((إِنَّ الشَّمْسَ تَدْنُو يَوْمَ القِيَامَةِ حَتَّى يَبْلُغَ العَرَقُ نِصْفَ الأُذُنِ، فَبَيْنَمَا هُمْ كَذَلِكَ اسْتَغَاثُوا بِآدَمَ، ثُمَّ بِمُوسَى، ثُمَّ بِمُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم فَيَشْفَعُ لِيُقْضَى بَيْنَ الخَلْقِ، فَيَمْشِي حَتَّى يَأْخُذَ بِحَلقَةِ البَابِ، فَيَوْمَئِذٍ يَبْعَثُهُ اللهُ مَقَامًا مَحْمُودًا، يَحْمَدُهُ أَهْلُ الجَمْعِ كُلُّهُمْ))

Amesema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika jua litakaribia Siku ya Qiyaamah mpaka majasho ya watu yatafikia karibu na masikio. Watakapokuwa katika hali hiyo, wataomba msaada kwa Aadam, kisha kwa Muwsaa kisha kwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Ataomba Shafaa’ah kwa Allaah ili Ahukumu baina ya viumbe Vyake. Ataendelea mpaka atakamata kikamatio cha mlango. Siku hiyo basi Allaah Atamuinua Maqaaman Mahmuwdaa [cheo cha kusifika] na watu wote wa mkusanyiko watamsifu)). [Al-Bukhaariy]

 

Shafaa’ah hiyo ndiyo Maqaaman Mahmuwdaa ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾

Na katika usiku, amka uswali (tahajjud) kuisoma (Qur-aan); ni ziada ya Sunnah kwako Asaa Rabb wako Akakuinua cheo kinachosifika. [Al-Israa: 79]

 

Ama makafiri ambao duniani waliwaelekea wengine kuwaomba na kutaka uombezi kwao wakakanusha Tahwiyd ya Uluwhiyyah (Kumpwekesha Allaah katika ‘ibaadah):

 

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّـهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١٨﴾

Na wanaabudu pasi na Allaah ambavyo haviwadhuru wala haviwanufaishi na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” Sema: “Je, mnamjulisha Allaah kwa yale Asiyoyajua katika mbingu na ardhini?” Subhaanah! (Utakasifu ni Wake) na Ametukuka kwa ‘Uluwa kwa yale yote wanayomshirikisha. [Yuwnus: 18]

 

 

Huko Aakhirah, hawatopata Shafaa’ah ya yeyote yule kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ﴿٤٨﴾

Basi haitowafaa uombezi wowote wa waombezi. [Al-Muddath-thir: 48]

 

 

Juu ya hivyo hao wanaowaabudu watakanusha kuabudiwa kwao:

 

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ ﴿١٣﴾

Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende.

 

 

إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ ﴿١٤﴾

 

Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawatakuitikieni.  Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu, na wala hakuna atakayekujulisha vilivyo kama Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Faatwir: 13-14]

 

 

 

 

Share

22-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Tawhyd Ni Sharti Ya Kuingia Jannah

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

22-Tawhyd Ni Sharti Ya Kuingia Jannah

 

 

 

Dalili zifuatazo zimetaja kuwa: Laa ilaaha illa Allaah ni sharti ya kuingia Jannah:

 

Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

((لاَيَدْخُلُ الْجَنَّةَ إِلا نَفْسٌ مُؤْمِنَةٌ))

((Hatoingia Jannah isipokuwa nafsi iliyoamini))

 

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anathibitisha kwamba kutenda mema pekee hamitoshi mtu kuingia Jannah, bali mpaka mtu awe mwenye kuamini. Na Tawhiyd ni msingi wa iymaan:

 

 وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ يُرْزَقُونَ فِيهَا بِغَيْرِ حِسَابٍ﴿٤٠﴾

Na yeyote atakayetenda mema kati ya mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Jannah wataruzukiwa humo bila ya hesabu. [Ghaafir: 40]

 

Pia Hadiyth ya ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((مَنْ شَهِدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ وَالْجَنَّةُ حَقٌّ وَالنَّارُ حَقٌّ أَدْخَلَهُ اللَّهُ الْجَنَّةَ عَلَى مَا كَانَ مِنْ الْعَمَلِ))

((Atakayeshuhudia moyoni na kukiri kwamba: laa ilaaha illa Allaah  (hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah na Rasuli Wake, na neno Lake Alilompelekea Maryam na Ruwh kutoka Kwake, na kwamba Jannah ni haki, na Moto ni haki, Allaah Atamuingiza Jannah kwa ‘amali zozote alizonazo)). [Al-Bukhaariy (3/1267) (3252), Muslim (1/57) (28) Ahmad (5/313) (22727), Ibn Hibbaan (1/431) (202), An-Nasaaiy (6/331) (11132)]

 

Na Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisema:

 

((يَا أَبَا هُرَيْرَةَ (وَأَعْطَانِي نَعْلَيْهِ) قَالَ: اذْهَبْ بِنَعْلَيّ هَاتَينِ فَمَنْ لَقِيتَ مِنْ وَرَاء هَذَا الْحَائِطِ يَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاّ اللّهُ مُسْتَيْقِنا بِهَا قَلُبُهُ فَبَشّرْهُ بِالْجَنّةِ))

((Ee Abaa Hurayrah (akanipa viatu vyake) Nenda na viatu vyangu hivi, utakayemkuta nyuma ya ukuta huu akiwa anakiri moyoni na anashuhudia kwamba: laa ilaaha illa Allaah (hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah) akiwa amethibitika nayo moyoni, mbashirie Jannah)). [Muslim]

 

 

Na Hadiyth ya ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّة))

((Atakayefariki akiwa anajua kwamba: laa ilaaha illa Allaah (hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah) ataingia Jannah)). [Muslim]

 

 

Share

23-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Anayethibitisha Tawhiyd Ataepushwa Na An-Naar (Moto) Siku ya Qiyaamah

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

23-Anayethibitisha Tawhiyd Ataepushwa Na An-Naar (Moto) Siku ya Qiyaamah

 

 

 

 

Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

مَا مِنْ أَحَدٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ صِدْقًا مِنْ قَلْبِهِ إِلَّا حَرَّمَهُ اللَّهُ عَلَى النَّارِ

((Hakuna mtu atakayekiri moyoni na kushuhudia kwa kusadikisha moyoni mwake kwamba: laa ilaaha illa Allaah (hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, isipokuwa Allaah Atamharamisha na An-Naar (Moto). [Al-Bukhaariy (128) Muslim (32)]

 

 

Akapokea tena tena Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

  يَخْرُجُ مِنْ النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ شَعِيرَةٍ مِنْ خَيْرٍ وَيَخْرُجُ مِنْ النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ بُرَّةٍ مِنْ خَيْرٍ وَيَخْرُجُ مِنْ النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ ذَرَّةٍ مِنْ خَيْر .

((Atatoka Motoni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah (hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), akiwa moyoni mwake kuna kheri (iymaan) kiasi cha uzani wa shairi. Na Atatoka Motoni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah akiwa moyoni mwake kuna kheri (iymaan) kiasi cha mbegu moja. Na atatoka Motoni anayesema: laa ilaaha illa Allaah akiwa moyoni mwake kuna kheri (iymaan) kiasi cha uzani wa punje). [Al-Bukhaariy (44) Muslim (193)]

 

Hadiyth ya ‘Ithbaan bin Maalik Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

  إِنَّ اللَّهَ قَدْ حَرَّمَ عَلَى النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ يَبْتَغِي بِذَلِكَ وَجْهَ اللَّهِ

((Hakika Allaah Ameharamisha An-Naar kwa anayesema: laa ilaaha illa Allaah akitafuta Wajihi wa Allaah)). [Al-Bukhaariy (425), Muslim (33)]

 

Hadiyth ya ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba:

 

سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: (مَنْ شَهِدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ النَّارَ

Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayekiri moyoni na kushuhudia kwamba: laa ilaaha illa Allaah (hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), basi Allaah Atamharamisha na An-Naar [Moto])). [Muslim (29)]

 

Hadiyth ya Abuu Hurayrah na Abuu Sa’iyd (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba wameshuhudia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

 ((إِذَا قَالَ الْعَبْدُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ. يَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَأَنَا أَكْبَرُ. وَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ . قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا وَحْدِي .وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ لَا شَرِيكَ لَهُ. قَالَ : صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَلَا شَرِيكَ لِي .وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ  قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، لِي الْمُلْكُ، وَلِيَ الْحَمْدُ . وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ . قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِي. ثم قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:  مَنْ رُزِقَهُنَّ عِنْدَ مَوْتِهِ لَمْ تَمَسَّهُ النَّارُ))

((Mja akisema: “Laa ilaaha illa Allaah wa Allaahu Akbar.” (Hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Allaah ni Mkubwa).  Allaah ‘Azza wa Jalla Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi Nami ni Mkubwa.” Akisema mja: “Laa ilaaha illa Allaah Wahdahu.” (Hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Pekee). Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi Pekee.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaahu laa shariyka Lahu.” (Hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah hana mshirika) Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi sina mshirika.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaah, Lahul-Mulku walahul-Hamdu.” (Hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, ufalme na Himdi ni Zake). Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi, Ufalme na Himdi ni Zangu.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaah, walaa hawla walaa quwwata illa biLLaah.” (Hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Allaah) Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka Kwangu.” Kisha Rasuli wa Allaah akasema: Atakayeruzukiwa [kauli] hiyo wakati wa mauti yake, An-Naar [Moto] haitomgusa)). [Ibn Maajah (3794) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (713).

 

 

Share

24-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Wanyama Na Alivyoumba Allaah Vinathibitisha Tawhiyd

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

24-Wanyama Na Alivyoumba Allaah Vinathibitisha Tawhiyd

 

 Alhidaaya.com

 

 

Hud-hud (ndege) alikuwa miongoni mwa jeshi la Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis-Salaam). Aliporuka na kufikia mji wa Sabaa alikuta watu huko wanaabudu jua, akarudi kumpa taarifa Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis-Salaam) huku akidhihirisha kuikanusha ‘ibaadah hiyo batili. Uzuri ulioje ndege huyo kuikanusha ‘ibaadah ya kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na badala yake kuithibitisha Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)! Kisa chake kinaanza katika Qur-aan pale alipokosekana katika jeshi la Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis-Salaam). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَتَفَقَّدَ الطَّيْرَ فَقَالَ مَا لِيَ لَا أَرَى الْهُدْهُدَ أَمْ كَانَ مِنَ الْغَائِبِينَ ﴿٢٠﴾

Akakagua ndege, akasema: “Imekuwaje, mbona simuoni Al-Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walioghibu? 

 

 

لَأُعَذِّبَنَّهُ عَذَابًا شَدِيدًا أَوْ لَأَذْبَحَنَّهُ أَوْ لَيَأْتِيَنِّي بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٢١﴾

Bila shaka nitamuadhibu adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja bayana.”

 

 

فَمَكَثَ غَيْرَ بَعِيدٍ فَقَالَ أَحَطتُ بِمَا لَمْ تُحِطْ بِهِ وَجِئْتُكَ مِن سَبَإٍ بِنَبَإٍ يَقِينٍ ﴿٢٢﴾

Basi (Hud-hud) hakukaa mbali akasema: “Nimegundua ambayo wewe hukuyagundua na nimekujia kutoka Sabaa na habari za yakini.

 

 

إِنِّي وَجَدتُّ امْرَأَةً تَمْلِكُهُمْ وَأُوتِيَتْ مِن كُلِّ شَيْءٍ وَلَهَا عَرْشٌ عَظِيمٌ ﴿٢٣﴾

Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawamiliki, na amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa mno.

 

 

وَجَدتُّهَا وَقَوْمَهَا يَسْجُدُونَ لِلشَّمْسِ مِن دُونِ اللَّـهِ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ فَهُمْ لَا يَهْتَدُونَ ﴿٢٤﴾

Nimemkuta na watu wake wanalisujudia jua badala ya Allaah, na shaytwaan amewapambia ‘amali zao basi akawazuia na njia, kwa hiyo hawakuongoka.

 

 

أَلَّا يَسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي يُخْرِجُ الْخَبْءَ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُخْفُونَ وَمَا تُعْلِنُونَ ﴿٢٥﴾

Kwamba hawamsujudii Allaah Ambaye Anatoa yenye kufichika katika mbingu na ardhi na Anayajua yale mnayoyaficha na yale mnayoyadhihirisha.

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ۩﴿٢٦﴾

Allaah; hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Rabb wa Al-‘Arsh adhimu”. [An-Naml: 20-26]

 

 

Tumepata mafunzo yafuatayo kutokana na ndege huyo Al-Hud-hud:

 

  1. Alikuwa mwenye ‘Aqiydah swahiyh.

 

  1. Aikuwa ni mwenye kumwamini Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

  1. Alikuwa mwerevu kuweza kuchungua na kutambua wanayoyaabudu watu katika safari yake hiyo ya haraka kabisa.

 

  1. Aliungulika moyoni kuona watu wanakanusha Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Taa’alaa).

 

  1. Amefanya kazi ya Rasuli kulingania katika Dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

  1. Jambo kuu alolingania ni la kukanusha shirki na kuthibitisha Tawhiyd.

 

  1. Ameonya kuhusu udanganyifu, uchochezi wa shaytwaan kuwa anawapambia watu ‘amali zao.

 

  1. Ametafakari Utukufu wa Muumba wake, neema Zake na uwezo Wake wa kuyajua yaliyo dhahiri na yaliyofichika.

 

  1. Amefadhilisha Aakhirah kuliko dunia kwani hakujali mali na starehe alizojaaliwa nazo Malkia wa Sabaa.    

 

  1. Akathibitisha tena baada yote hayo Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

    

    11.  Ndege huyu Hud-hud amekuwa ni sababu ya Malkia wa Saba-a kusilimu katika Uislamu.

 

 

 

Basi tujiulize yafuatayo:

 

  • Je, ingekuwaje kama Hud-hud angepitia watu katika zama zetu hizi ambazo watu wanamshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aa’aa) kwa kila aina ya shirki? 

 

  • Je, ni wangapi wenye mfano wa Hud-hud?  

 

Ni dhahiri kwamba Hud-hud alikuwa mbora kuliko baadhi yetu juu ya kuwa yeye ni mnyama dhaifu anayeruka angani. Bali viumbe wote walioko mbinguni na wanyama ardhini, na vitu vyote Alivyoumba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) vinashuhudia Tawhiyd kwani vyote vinamsujudia na kumsabbih Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa) kama Anavyosema:

 

أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ يَتَفَيَّأُ ظِلَالُهُ عَنِ الْيَمِينِ وَالشَّمَائِلِ سُجَّدًا لِّلَّـهِ وَهُمْ دَاخِرُونَ﴿٤٨﴾

Je, hawaoni vile vitu Alivyoumba Allaah ambavyo vivuli vyake vinasogea huku na kule, kuliani na kushotoni vikimsujudia Allaah na huku vinanyenyekea?  

 

 

وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ﴿٤٩﴾

Na ni kwa Allaah pekee vinasujudia vyote vilivyomo mbinguni na ardhini katika viumbe vitembeavyo, na Malaika, nao hawatakabari.

 

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ۩﴿٥٠﴾

Wanamkhofu Rabb wao Aliye juu yao, na wanafanya yale wanayoamrishwa. [An-Nahl: 48-50]

 

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَسْجُدُ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ وَالنُّجُومُ وَالْجِبَالُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ النَّاسِ ۖ وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ الْعَذَابُ ۗ وَمَن يُهِنِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن مُّكْرِمٍ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ۩﴿١٨﴾

Je, huoni kwamba wanamsujudia Allaah walioko mbinguni na ardhini, na jua, na mwezi na nyota, na majabali na miti na viumbe vinavyotembea, na wengi miongoni mwa watu? Na wengi imewastahiki adhabu. Na ambaye Allaah Amemdhalilisha, basi hatopata wa kumkirimu. Hakika Allaah Anafanya Atakavyo. [Al-Hajj: 18]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ﴿٤٤﴾

Zinamsabbih mbingu saba na ardhi na waliyomo humo. Na hakuna kitu chochote isipokuwa kinasabbih kwa Himidi Zake, lakini hamzifahamu tasbiyh zao. Hakika Yeye ni Mvumilivu, Mwingi wa kughufuria. [Al-Israa: 44]

 

 

 

Share

25-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Ukitaka Mapenzi Ya Allaah, Thibitika Katika Tawhiyd

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

25-Ukitaka Mapenzi Ya Allaah, Thibitika Katika Tawhiyd

 

 

 

Kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kutekeleza amri Zake na kumpwekesha bila ya kumshirikisha ni katika dalili za kumpenda Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kupata mapenzi Yake pia.

 

Waumini wa kikweli humpenda Allaah Pekee bila ya kumshirikisha yeyote katika mapenzi Yake. Kinyume chake ni kuelemeza mapenzi kwa wasiokuwa Allaah kama Anavyosema (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  

 

 وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ

Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. [Al-Baqarah: 165]

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akaonya Waumini kwamba ikiwa watamkanusha na kuikanusha Dini Yake basi Anaweza kuwaleta wengineo ambao Atawapenda nao watampenda kikweli, Anasema hivyo katika kauli Yake:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ

Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda; wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri; wanafanya jihaad katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama za mwenye kulaumu. [Al-Maaidah: 54]

 

 

Anayempenda Allaah kikweli hupenda yale Anayoyapenda Allaah kama humpwekesha kwa aina zote za Tawhiyd, na huchukia yale Anayochukia Allaah kama kumshirikisha, na hapo ndipo iymaan ya mtu inapothibitika. Na ndipo sharti mojawapo ya “laa ilaaha illa Allaah” ikawa ni: “Kupenda ambako kunaondowa kinyume chake”; yaani kutokupenda au kuchukia.” Ndio pia maana ya “Al-Walaa Wal-Baraa” (Kupenda na kuandamana na kuchukia na kutengana kwa ajili ya Allaah).

  

Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja hayo katika Hadiyth zifuatazo:

 

Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa):  

 

  ((أَوْثقُ عُرَى الإِيمان: الموالاَةُ في الله والمعاداةُ في الله، والحب في الله، والبغضُ في اللَّه عز وجل))   

Shikizo thabiti kabisa la iymaan ni kuwa na urafiki wa karibu kwa ajili ya Allaah na kujitenga kwa ajili ya Allaah, na kupenda kwa ajili ya Allaah, na kuchukia kwa ajili ya Allaah ‘Azza wa Jalla)) [Atw-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr na ameisahihisha Al-Abaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (2539))]

 

Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

 

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((ثَلاَثٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ وَجَدَ حَلاَوَةَ الإِيمَانِ: أَنْ يَكُونَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِمَّا سِوَاهُمَا، وَأَنْ يُحِبَّ الْمَرْءَ لاَ يُحِبُّهُ إِلاَّ لِلَّهِ, وَأَنْ يَكْرَهَ أَنْ يَعُودَ فِي الْكُفْرِ كَمَا يَكْرَهُ أَنْ يُقْذَفَ فِي النَّارِ)) متفق عليه

Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mambo matatu atakayekuwa nayo, atapata utamu wa imaan: Allaah na Rasuli Wake wawe vipenzi zaidi kwake kuliko wengineo, ampende mtu na wala asimpende isipokuwa kwa ajili ya Allaah, na achukie kurudi katika ukafiri baada ya Allaah kumwokoa kutoka huko kama anavyochukia kuingizwa motoni. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ ، قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ :  ((مَنْ أَحَبَّ فِي اللَّهِ وَأَبْغَضَ فِي اللَّهِ وَأَعْطَى لِلَّهِ وَمَنَعَ لِلَّهِ فَقَدِ اسْتَكْمَلَ الإِيمَانَ))  

Amesimulia Abuu Umaamah  (رضي الله عنه):  “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Atakayependa kwa ajili ya Allaah, akachukia kwa ajili ya Allaah, akatoa kwa ajili ya Allaah, na akazuia kwa ajili ya Allaah, basi atakuwa amekamilisha imaan.”  [Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy (4681)]

 

 

عَنْ أَنَسٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَلَدِهِ وَوَالِدِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ)) أَخْرَجَاهُ

 

Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mmoja wenu hawi Muumini mpaka anipende mimi kuliko watoto wake na baba yake na watu wote.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Mafanikio ya duniani na ya Aakhirah hayapatikani isipokuwa pale Muislamu atakapopenda kwa ajili ya Allaah na akachukia kwa ajili ya Allaah na akafuata maamrisho ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hapo atakuwa miongoni mwa vipenzi vya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na watakuwa ni waliofadhilishwa kwa vyeo vya juu kabisa na kupewa nuru Siku ya Qiyaamah kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifautayo inaelezea:

 

عَنْ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ:قَالَ النَّبِىُّ صلى الله عليه وسلم: ((إِنَّ مِنْ عِبَادِ اللَّهِ لأُنَاسًا مَا هُمْ بِأَنْبِيَاءَ وَلاَ شُهَدَاءَ يَغْبِطُهُمُ الأَنْبِيَاءُ وَالشُّهَدَاءُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِمَكَانِهِمْ مِنَ اللَّهِ تَعَالَى)) قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ تُخْبِرُنَا مَنْ هُمْ. قَالَ:  ((هُمْ قَوْمٌ تَحَابُّوا بِرُوحِ اللَّهِ عَلَى غَيْرِ أَرْحَامٍ بَيْنَهُمْ وَلاَ أَمْوَالٍ يَتَعَاطَوْنَهَا, فَوَاللَّهِ إِنَّ وُجُوهَهُمْ لَنُورٌ وَإِنَّهُمْ عَلَى نُورٍ, لاَ يَخَافُونَ إِذَا خَافَ النَّاسُ وَلاَ يَحْزَنُونَ إِذَا حَزِنَ النَّاس)) وَقَرَأَ هَذِهِ الآيَةَ: ((أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ))   

Kutoka kwa 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Hakika miongoni mwa waja wa Allaah ni watu ambao si Manabii wala si mashahidi. Manabii na mashahidi watawaonea wivu kutokana na vyeo vyao vya juu mbele ya Allaah Ta’aalaa Siku ya Qiyaamah)) Wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Tujulishe nani hao?” Akasema: ((Hao ni watu waliopendana kwa ajili ya Allaah bila ya kuwa na uhusiano wa damu, walahawakuungana kwa ajili ya mali. Naapa kwa Allaah! Nyuso zao zina nuru nao wako katika nuru. Hawaogopi wanapoogopa watu, wala hawahuzuniki wanapohuzunika watu)) Kisha akasoma Aayah hii: ((Tanabahi!  Hakika vipenzi wa Allaah hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.)) [Abu Daawuwd (3527) na ameisahihisha Al-Albaaniy (Aayah: Suwrat Yuwnus: 62)]

 

Tambua pia kwamba mapenzi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) hayakamiliki bila ya kumfuata Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:  

 

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah  [Aal-‘Imraan: 31]

 

Kwa maana; kufuata Sunnah zake bila ya kuwenda kinyume na mafundisho yake na bila ya kuzusha mambo katika Dini.

 

 

Share