002 - Al-Baqarah

 

الْبَقَرَة

 

002-Al-Baqarah

 

002-Al-Baqarah: Utangulizi Wa Suwrah

 

 

 Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 الم ﴿١﴾

1. Alif Laam Miym.[1]

 

 

ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾

2. Hiki[2] ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo[3] kwa wenye taqwa.[4]

 

 

 

الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾

3. Ambao huamini ya ghaibu[5] na husimamisha Swalaah[6] na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.

 

 

وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿٤﴾

4. Na ambao huamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenye yakini na Aakhirah.

 

 

 أُولَـٰئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥﴾

5. Hao wako juu ya mwongozo kutoka kwa Rabb wao, na hao ndio wenye kufaulu.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٦﴾

6. Hakika wale waliokufuru ni sawa kwao, ukiwaonya au usiwaonye wao hawatoamini.

 

 

خَتَمَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ ۖ وَعَلَىٰ أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٧﴾

7. Allaah Amepiga mhuri juu ya nyoyo zao, na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko, na watapata adhabu kuu kabisa.

 

 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾ 

8. Na miongoni mwa watu wako wasemao: Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho hali ya kuwa si wenye kuamini.

 

 

يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾

9. (Wanadhani) wanamhadaa Allaah, na wale walioamini, lakini hawahadai ila nafsi zao, wala hawahisi.

 

 

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ ﴿١٠﴾

10. Ndani ya nyoyo zao mna maradhi[7] na Allaah Akawazidishia maradhi, na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha.

 

 

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ ﴿١١﴾

11. Na wanapoambiwa: Msifanye ufisadi katika ardhi husema: Hakika sisi ni watengenezaji.

 

 

 أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ ﴿١٢﴾

12. Tanabahi! Hakika wao ndio mafisadi lakini hawahisi.

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا كَمَا آمَنَ النَّاسُ قَالُوا أَنُؤْمِنُ كَمَا آمَنَ السُّفَهَاءُ ۗ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهَاءُ وَلَـٰكِن لَّا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾

13. Na wanapoambiwa: Aminini kama walivyoamini watu husema:  Je, tuamini kama walivyoamini wapumbavu? Tanabahi! Hakika wao ndio wapumbavu lakini hawajui.

 

 

 وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا إِلَىٰ شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِئُونَ ﴿١٤﴾

14. Na wanapokutana na wale walioamini husema: Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao pamoja na mashaytwaan wao, husema: Hakika sisi tuko pamoja nanyi, hakika sisi ni wenye kuwadhihaki tu.

 

 

 اللَّـهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١٥﴾

15. Allaah Anawadhihaki[8] wao na Atawaendeleza katika hali yao ya upindukiaji mipaka wa kuasi, wakitangatanga kwa upofu.

 

 

 

 أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَارَتُهُمْ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٦﴾

16. Hao ndio wale waliobadilisha upotofu badala ya uongofu, basi haikupata faida  biashara yao na wala hawakuwa wenye kuhidika.

 

 

 

 

مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ ﴿١٧﴾

17. Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, ulipoyaangaza yaliyopo pembezoni mwake, Allaah Akawaondoshea nuru yao na Akawaacha katika viza, hawaoni.

 

صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿١٨﴾

18. Viziwi, mabubu, vipofu basi hawatorejea.

 

 

 أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾

19. Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni, ndani yake mna viza na radi na umeme, wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakikhofu mauti, na Allaah Ni Mwenye Kuwazunguka makafiri.

 

 

يَكَادُ الْبَرْقُ يَخْطَفُ أَبْصَارَهُمْ ۖ كُلَّمَا أَضَاءَ لَهُم مَّشَوْا فِيهِ وَإِذَا أَظْلَمَ عَلَيْهِمْ قَامُوا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَذَهَبَ بِسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٠﴾

20. Unakaribia umeme kunyakua macho yao, kila unapowaangazia (njia) hutembea humo, na unapowafanyia kiza husimama. Na lau Allaah Angelitaka, basi Angeliwaondoshea kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

 يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٢١﴾

21. Enyi watu! Mwabuduni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni, na wale wa kabla yenu, mpate kuwa na taqwa.

 

 

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾

22. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.

 

 

 وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾

23. Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya Mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake,[9] na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli.

 

 

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا وَلَن تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿٢٤﴾

24. Msipofanya, na wala hamtoweza kufanya, basi ogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa kwa makafiri.

 

 

وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ كُلَّمَا رُزِقُوا مِنْهَا مِن ثَمَرَةٍ رِّزْقًا ۙ قَالُوا هَـٰذَا الَّذِي رُزِقْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَأُتُوا بِهِ مُتَشَابِهًا ۖ وَلَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥﴾

25. Na wabashirie wale walioamini na wakatenda mema, kwamba watapata Jannaat (bustani) zipitazo chini yake mito, kila watakaporuzukiwa humo katika matunda kuwa ni riziki husema: Haya ndiyo yale tuliyoruzukiwa kabla. Na wataletewa hali ya kuwa yanashabihiana, na watapata humo wake waliotakaswa, nao humo watadumu.

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾

26. Hakika Allaah Haoni haya kupiga mfano wa mbu[10] na ulio zaidi yake (kwa udogo). Basi wale walioamini wanajua kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wao. Ama wale waliokufuru husema: Anataka nini Allaah kwa mfano huu? Kwa (mfano) huo, Huwapoteza wengi na Huwaongoza kwao wengi na wala Hawapotezi kwao ila mafasiki.[11]

 

 

الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٢٧﴾

27. Wale wanaovunja Ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata Aliyoyaamrisha Allaah kuungwa,[12] na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye khasara.

 

 

كَيْفَ تَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَكُنتُمْ أَمْوَاتًا فَأَحْيَاكُمْ ۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٨﴾

28. Vipi mnamkufuru Allaah na hali mlikuwa wafu Akakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakuhuisheni, kisha Kwake mtarejeshwa?[13]

 

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٩﴾ 

29. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini kisha Kisha Akazikusudia mbingu (Kuziumba)[14] na Akazifanya timilifu mbingu saba, Naye kwa kila kitu Ni Mjuzi.

 

 

 

 وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾

30. Na pindi Rabb wako Alipowaambia Malaika: Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi khalifa.[15] Wakasema: Utaweka humo atakayefanya ufisadi humo na kumwaga damu, na hali sisi tunakusabihi kwa Himdi Zako na tunakutukuza kwa Utakatifu Wako? (Allaah) Akasema: Hakika Mimi Nayajua zaidi msiyoyajua.

 

 

 

وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣١﴾

31. Na Akamfunza Aadam majina yote (ya kila kitu), kisha Akavionyesha mbele ya Malaika Akasema: Niambieni majina ya hivi mkiwa ni wakweli.

 

 

قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٣٢﴾

32. Wakasema: Utakasifu ni Wako! Hatuna ilimu isipokuwa Uliyotufunza, hakika Wewe Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 قَالَ يَا آدَمُ أَنبِئْهُم بِأَسْمَائِهِمْ ۖ فَلَمَّا أَنبَأَهُم بِأَسْمَائِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٣٣﴾

33. Akasema: Ee Aadam, wajulishe kwa majina yao. Basi alipowatajia majina yao, (Allaah) Akasema: Je, Sikuwaambieni kuwa hakika Mimi Najua ghaibu ya mbingu na ardhi na Najua mnayoyadhihirisha na mliyokuwa mkiyaficha?

 

 

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٣٤﴾

34. Na pale Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari,[16] akawa miongoni mwa makafiri.

 

 

 وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٣٥﴾

35. Na Tukasema: Ee Aadam, kaa wewe na mkeo (Hawaa) Jannah na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na wala msiukaribie mti huu, mtakuwa miongoni mwa madhalimu.

 

 

فَأَزَلَّهُمَا الشَّيْطَانُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ ۖ وَقُلْنَا اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٣٦﴾

36. Shaytwaan akawatelezesha wote wawili kwayo, Akawatoa kutoka katika hali waliyokuwa nayo. Tukasema: Shukeni mkiwa maadui nyinyi kwa nyinyi, na mtapata katika ardhi makazi na starehe hadi muda maalumu.

 

 

 فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِن رَّبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٣٧﴾

37. Kisha Aadam akapokea maneno kutoka kwa Rabb wake, na (Rabb wake) Akapokea tawbah yake. Hakika Yeye Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.

 

 

قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٨﴾

38. Tukasema: Shukeni kutoka humo nyote! Utakapokufikieni kutoka Kwangu mwongozo, basi yeyote atakayefuata Mwongozo Wangu hakutokuwa na khofu juu yao wala hawatohuzunika.

 

 

وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu, hao ni watu wa motoni, wao humo watadumu.

 

 

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَوْفُوا بِعَهْدِي أُوفِ بِعَهْدِكُمْ وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ ﴿٤٠﴾

40. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni Neema Yangu Niliyokuneemesheni, na timizeni Ahadi Yangu Nikutimizieni ahadi yenu, na Mimi Pekee niogopeni.

 

 

وَآمِنُوا بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ ۖ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّايَ فَاتَّقُونِ ﴿٤١﴾

41. Na aminini yale Niliyoyateremsha yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nanyi, na wala msiwe wa kwanza wenye kuyakanusha, na wala msibadilishe Aayaat Zangu kwa thamani ndogo, na muwe na taqwa kunikhofu Mimi tu.

 

 

وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na wala msichanganye haki kwa baatwil na mkaficha haki na hali mnajua.

 

 

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾

43. Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah na rukuuni pamoja na wanaorukuu (katika utiifu).

 

 

أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٤٤﴾ 

44. Je, mnaamrisha watu watende mema na mnajisahu nafsi zenu na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu, je hamtii akilini?[17]

 

 

وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na tafuteni msaada kupitia subira na Swalaah, na hakika hilo ni kubwa isipokuwa kwa wanyenyekevu.

 

 

الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ وَأَنَّهُمْ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ﴿٤٦﴾

46. Ambao wana yakini kwamba hakika wao watakutana na Rabb wao na hakika wao Kwake watarejea.

 

 

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾

47. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni Neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya walimwengu wote.[18]

 

 

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٤٨﴾ 

48. Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitoifaa nafsi nyingine kwa kitu chochote kile, na wala haitokubaliwa kutoka kwake uombezi wowote, na wala hakitochukuliwa kutoka kwake kikomboleo, na wala hawatonusuriwa.

 

 

وَإِذْ نَجَّيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿٤٩﴾

49. Na pindi Tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Firawni walipokusibuni adhabu mbaya, wakiwachinja watoto wenu wa kiume na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo kwenu, ulikuwa ni mtihani mkuu kabisa kutoka kwa Rabb wenu. 

 

 

وَإِذْ فَرَقْنَا بِكُمُ الْبَحْرَ فَأَنجَيْنَاكُمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٠﴾ 

50. Na pindi Tulipoitenganisha bahari kwa ajili yenu, Tukakuokoeni na Tukawagharikisha watu wa Firawni na huku nyinyi mnatazama.

 

 

وَإِذْ وَاعَدْنَا مُوسَىٰ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٥١﴾

51. Na pindi Tulipomuahidi Muwsaa siku arubaini kisha mkamwabudu ndama baada yake na mkawa madhalimu.

 

 

ثُمَّ عَفَوْنَا عَنكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٢﴾ 

52. Kisha Tukawasameheni baada ya hapo ili mpate kushukuru.

 

 

وَإِذْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَالْفُرْقَانَ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿٥٣﴾

 53. Na pindi Tulipompa Muwsaa Kitabu na pambanuo[19] (la haki na baatwil) ili mpate kuongoka.

 

 

 وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ عِندَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٥٤﴾

54. Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Hakika nyinyi mmedhulumu nafsi zenu kwa kuabudu kwenu ndama, basi tubuni kwa Muumbaji wenu,  na ziueni nafsi zenu, hivyo ni bora kwenu mbele ya Muumbaji wenu. Akapokea tawbah yenu, hakika Yeye Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.

 

 

وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْكُمُ الصَّاعِقَةُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٥﴾

55. Na pindi mliposema: Ee Muwsaa! Hatutokuamini mpaka tumuone Allaah wazi wazi, ikakuchukueni radi na umeme angamizi nanyi mnatazama.

 

 

ثُمَّ بَعَثْنَاكُم مِّن بَعْدِ مَوْتِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٦﴾

56. Kisha Tukakufufueni baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru.

 

 

وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۖ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٥٧﴾ 

57. Na Tukakufunikeni kwa mawingu na Tukakuteremshieni al-manna na as-salwaa[20]. (Tukakwambieni): Kuleni katika vizuri Tulivyokuruzukuni. Hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.

 

 

 

وَإِذْ قُلْنَا ادْخُلُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ فَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا حِطَّةٌ نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطَايَاكُمْ ۚ وَسَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٨﴾

58. Na pindi Tuliposema: Ingieni mji huu (Quds) na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, na ingieni katika mlango wake huku mmeinama kunyenyekea na semeni Hittwah[21] (Tuondolee uzito wa madhambi),Tutakughufurieni makosa yenu na Tutawazidishia (thawabu) wafanyao ihsaan.

 

 

 

فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٥٩﴾ 

59. Basi wale waliodhulumu walibadilisha kauli kinyume na ile waliyoambiwa, Tukateremsha juu ya waliodhulumu adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa yale waliyokuwa wakifanya ya ufasiki.

 

 

وَإِذِ اسْتَسْقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ فَقُلْنَا اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ ۖ فَانفَجَرَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۖ كُلُوا وَاشْرَبُوا مِن رِّزْقِ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٦٠﴾

60. Na pindi Muwsaa alipoomba maji kwa ajili ya kaumu yake. Tukasema: Piga kwa fimbo yako jiwe. Zikachimbuka na kububujika kutoka kwalo chemchemu kumi na mbili. Kila kabila likajua mahala pake pa kunywea. Kuleni na kunyweni kutokana na Riziki ya Allaah, wala msieneze uovu katika ardhi hali ya kuwa ni wenye kufanya ufisadi.

 

 

وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نَّصْبِرَ عَلَىٰ طَعَامٍ وَاحِدٍ فَادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُخْرِجْ لَنَا مِمَّا تُنبِتُ الْأَرْضُ مِن بَقْلِهَا وَقِثَّائِهَا وَفُومِهَا وَعَدَسِهَا وَبَصَلِهَا ۖ قَالَ أَتَسْتَبْدِلُونَ الَّذِي هُوَ أَدْنَىٰ بِالَّذِي هُوَ خَيْرٌ ۚ اهْبِطُوا مِصْرًا فَإِنَّ لَكُم مَّا سَأَلْتُمْ ۗ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ وَالْمَسْكَنَةُ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٦١﴾

61. Na pindi mliposema: Ee Muwsaa! Hatuwezi kusubiri kwa chakula cha aina moja tu, basi tuombee kwa Rabb wako Atutolee katika inavyoviotesha ardhi; kati ya mboga zake, matango yake, thomu (au ngano) yake, adesi zake na vitunguu vyake. (Muwsaa) akasema: Je mnataka kubadilisha yaliyo duni kwa yaliyo bora? Shukeni mjini, hakika huko mtapata mnayoyauliza. Na ikapigwa juu yao dhila na umaskini na wakastahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah! Hayo ni kwa kuwa wao walikuwa wakikanusha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah  na wakiwaua Manabii bila ya haki. Hayo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالنَّصَارَىٰ وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٢﴾

62. Hakika wale walioamini, na wale ambao (kabla ya Uislamu) ni Mayahudi, na Manaswara na Wasabai[22]; yeyote atakayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na akatenda mema, basi watapata ujira wao kutoka kwa Rabb wao, na hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٦٣﴾

63. Na pindi Tulipochukua ahadi yenu na Tukaunyanyua juu yenu mlima (Tukasema): Shikilieni Tuliyokupeni kwa nguvu na kumbukeni yaliyomo humo mpate kuwa na taqwa.

 

 

ثُمَّ تَوَلَّيْتُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۖ فَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَكُنتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٦٤﴾

64. Kisha mkakengeuka baada ya hayo, na lau si Fadhila za Allaah juu yenu na Rehma Yake mngekuwa miongoni mwa wenye kukhasirika.

 

 

وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ الَّذِينَ اعْتَدَوْا مِنكُمْ فِي السَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴿٦٥﴾

65. Na kwa yakini mlikwishawajua  wale miongoni mwenu waliotaadi mipaka ya As-Sabt[23]  Tukawaambia: Kuweni manyani waliobezwa.

 

 

 

فَجَعَلْنَاهَا نَكَالًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهَا وَمَا خَلْفَهَا وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٦٦﴾

66. Tukaifanya kuwa ni adhabu ya tahadharisho na fundisho kwa waliokuweko zama zao na wataokuja baada yao, na ni mawaidha kwa wenye taqwa.

 

 

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا بَقَرَةً ۖ قَالُوا أَتَتَّخِذُنَا هُزُوًا ۖ قَالَ أَعُوذُ بِاللَّـهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٦٧﴾

67. Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu wake:  Hakika Allaah Anakuamuruni mchinje ng’ombe.[24] Wakasema: Unatufanyia mzaha? Akasema: Najikinga kwa Allaah kuwa  miongoni mwa wajinga.

 

 

قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا فَارِضٌ وَلَا بِكْرٌ عَوَانٌ بَيْنَ ذَٰلِكَ ۖ فَافْعَلُوا مَا تُؤْمَرُونَ ﴿٦٨﴾

68. Wakasema: Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo? (Muwsaa) akasema: Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ng’ombe mwenyewe si mpevu wala si mchanga, bali ni wa katikati baina ya hao, basi fanyeni mnavyoamrishwa.

 

 

قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا لَوْنُهَا ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ صَفْرَاءُ فَاقِعٌ لَّوْنُهَا تَسُرُّ النَّاظِرِينَ ﴿٦٩﴾

69. Wakasema: Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie rangi yake. (Muwsaa) akasema: Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe wa rangi ya njano iliyoiva mno, rangi yake huwapendeza wanaotazama.

 

 

 قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ الْبَقَرَ تَشَابَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّا إِن شَاءَ اللَّـهُ لَمُهْتَدُونَ ﴿٧٠﴾

70. Wakasema: Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo? Kwa hakika ng’ombe wametutatiza na hakika sisi In-Shaa-Allaah  tutakuwa wenye kuhidika.

 

 

قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا ذَلُولٌ تُثِيرُ الْأَرْضَ وَلَا تَسْقِي الْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌ لَّا شِيَةَ فِيهَا ۚ قَالُوا الْآنَ جِئْتَ بِالْحَقِّ ۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧١﴾

71. (Muwsaa) akasema: Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe ambaye hakutiishwa wa kulima ardhi wala kwa kumwagilia maji shamba, ni mkamilifu hana dosari. Wakasema: Sasa umekuja na haki. Basi wakamchinja na hawakuwa wenye kukaribia kufanya hivyo. 

 

 

وَإِذْ قَتَلْتُمْ نَفْسًا فَادَّارَأْتُمْ فِيهَا ۖ وَاللَّـهُ مُخْرِجٌ مَّا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٧٢﴾

72. Na pindi mlipoiua nafsi, kisha mkakhitilafiana kwayo, na Allaah Ni Mwenye Kutoa hayo mliyokuwa mkiyaficha.

 

 

فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا ۚ كَذَٰلِكَ يُحْيِي اللَّـهُ الْمَوْتَىٰ وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٧٣﴾

73. Tukasema: Mpigeni (huyo maiti) kwa kipande chake (huyo ng’ombe). Hivyo ndivyo Allaah Anavyohuisha wafu na Anakuonyesheni Aayaat (Miujiza na Dalili) Zake huenda mkatia akilini.

 

 

 ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً ۚ وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاءُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٧٤﴾

74. Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, zikawa kama mawe au ngumu zaidi. Na kwa hakika katika mawe kuna yanayobubujika humo mito. Na hakika katika hayo kuna yanayopasuka yakatoka humo maji. Na hakika katika hayo kuna mengine yanayoporomoka kutokana na khofu ya Allaah. Na Allaah Si Mwenye Kughafilika kuhusu myatendayo.

 

 

أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾

75. Je, mnatumai kwamba watakuaminini na hali lilikuwa kundi miongoni mwao linasikia Maneno ya Allaah kisha linayageuza baada ya kuyaelewa na hali wanajua?

 

 

وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ قَالُوا أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَاجُّوكُم بِهِ عِندَ رَبِّكُمْ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٧٦﴾

76. Na wanapokutana na wale walioamini husema: Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao, wao kwa wao, husema: Hivi mnawasimulia yale Aliyokufungulieni Allaah ili wapate kukuhojini kwayo mbele ya Rabb wenu? Hamtii akilini?

 

 

 أَوَلَا يَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٧﴾

77. Je, hawajui kwamba Allaah Anajua wanayoyaficha na wanayoyatangaza?

 

 

وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴿٧٨﴾ 

78. Na miongoni mwao wako wasiojua kusoma wala kuandika, hawakijui Kitabu ila matamanio ya kuwaza tu, nao hawana ila kudhania tu.

 

 

فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ ﴿٧٩﴾

79. Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa mikono yao kisha wakasema: Hiki ni kutoka kwa Allaah ili wabadilishe kwa thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma![25]

 

 

وَقَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَةً ۚ قُلْ أَتَّخَذْتُمْ عِندَ اللَّـهِ عَهْدًا فَلَن يُخْلِفَ اللَّـهُ عَهْدَهُ ۖ أَمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٨٠﴾

80. Na walisema: Hautotugusa moto ila siku chache tu. Sema: Je, mmechukua ahadi kwa Allaah? Basi Allaah Hakhalifu Ahadi Yake, au mnasema kuhusu Allaah msiyoyajua?

 

 

بَلَىٰ مَن كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَاطَتْ بِهِ خَطِيئَتُهُ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨١﴾

81. Naam! Yeyote aliyechuma uovu na yakamzunguka makosa yake, basi hao ni watu wa motoni, wao humo watadumu.

 

 

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨٢﴾

82. Na wale walioamini na wakatenda mema, hao ni watu wa Jannah, wao humo watadumu.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنكُمْ وَأَنتُم مُّعْرِضُونَ ﴿٨٣﴾ 

83. Na pindi Tulipochukua fungamano la wana wa Israaiyl (Tukawaambia): Msiabudu isipokuwa Allaah, na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini, na semeni na watu kwa uzuri na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, kisha mkakengeuka ila wachache miongoni mwenu na huku nyinyi mnapuuza.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ لَا تَسْفِكُونَ دِمَاءَكُمْ وَلَا تُخْرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَارِكُمْ ثُمَّ أَقْرَرْتُمْ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ ﴿٨٤﴾

84. Na pindi Tulipochukua fungamano lenu (Tukawaambia): Msimwage damu zenu, wala msijitoe majumbani mwenu, kisha mkakubali nanyi mnashuhudia.

 

 

ثُمَّ أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ تَقْتُلُونَ أَنفُسَكُمْ وَتُخْرِجُونَ فَرِيقًا مِّنكُم مِّن دِيَارِهِمْ تَظَاهَرُونَ عَلَيْهِم بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَإِن يَأْتُوكُمْ أُسَارَىٰ تُفَادُوهُمْ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيْكُمْ إِخْرَاجُهُمْ ۚ أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ ۚ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰ أَشَدِّ الْعَذَابِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٨٥﴾

85. Kisha nyinyi ndio hao mnauana na mnawatoa kundi miongoni mwenu kutoka majumbani mwao, mnasaidiana dhidi yao kwa dhambi na uadui, na wanapokujieni mateka mnawakomboa na hali hilo la kuwatoa limeharamishwa kwenu. Je, mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakanusha baadhi yake? Basi hapana jazaa ya anayefanya hayo miongoni mwenu isipokuwa hizaya katika dunia, na Siku ya Qiyaamah watapelekwa kwenye adhabu kali zaidi. Na Allaah Si Mwenye Kughafilika kuhusu myatendayo.

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ ۖ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٨٦﴾

86. Hao ndio wale waliobadilisha uhai wa dunia badala ya Aakhirah, basi hawatapunguziwa adhabu wala hawatonusuriwa.

 

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ ۖ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ ﴿٨٧﴾

87. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu na Tukafuatisha Rusuli baada yake. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwh[26] Al-Qudus (Jibriyl (عليه السلام. Je, basi kila alipokujieni Rasuli kwa yale ambayo nafsi zenu haziyapendi, mlitakabari, kundi mkalikadhibisha na jingine mnaliua.

 

 

وَقَالُوا قُلُوبُنَا غُلْفٌ ۚ بَل لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَقَلِيلًا مَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾

88. Na wakasema: Nyoyo zetu zimefunikwa. Bali Allaah Amewalaani kwa kufuru zao, kwa hivyo ni kidogo tu wanayoyaamini.

 

 

وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُم مَّا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ ۚ فَلَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾

89. Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao - japokuwa kabla ya hapo walikuwa wakiomba ushindi dhidi ya wale waliokufuru – lakini (kisha) yalipowajia yale waliyokuwa wakiyatambua waliyakanusha, basi Laana ya Allaah iwe juu ya makafiri.[27]

 

 

 

بِئْسَمَا اشْتَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ أَن يَكْفُرُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ بَغْيًا أَن يُنَزِّلَ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ فَبَاءُوا بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٍ ۚ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٩٠﴾

90. Ubaya ulioje walichojibadilishia nafsi zao, kwamba wakufuru yale Aliyoyateremsha Allaah kwa baghi[28] (chuki na uhasidi) kwa kuwa Allaah Kateremsha katika Fadhila Zake juu ya Amtakae katika Waja Wake. Basi wakarudi kustahiki ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata adhabu ya kudhalilisha.

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا نُؤْمِنُ بِمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَيَكْفُرُونَ بِمَا وَرَاءَهُ وَهُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَهُمْ ۗ قُلْ فَلِمَ تَقْتُلُونَ أَنبِيَاءَ اللَّـهِ مِن قَبْلُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩١﴾

91. Na wanapoambiwa: Aminini yale Aliyoyateremsha Allaah, husema: Tunaamini yale yaliyoteremshwa kwetu na wanayakanusha yale yaliyokuja baada yake, na hali ya kuwa hayo ni haki yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao. Sema: Kwa nini basi mnawaua Manabii wa Allaah hapo zamani kama kweli mlikuwa waumini?

 

 

وَلَقَدْ جَاءَكُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٩٢﴾

92. Na kwa yakini alikujieni Muwsaa kwa hoja bayana kisha mkamwabudu ndama baada yake na mkawa  madhalimu.

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاسْمَعُوا ۖ قَالُوا سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَأُشْرِبُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْعِجْلَ بِكُفْرِهِمْ ۚ قُلْ بِئْسَمَا يَأْمُرُكُم بِهِ إِيمَانُكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩٣﴾

93. Na Tulipochukua fungamano lenu na Tukaunyanyua juu yenu mlima (Tukasema): Shikilieni Tuliyokupeni kwa nguvu na sikilizeni. Wakasema: Tumesikia na tumeasi. Wakanyweshwa katika nyoyo zao (kumwabudu)  ndama kwa kufuru yao. Sema: Ubaya ulioje inakuamrisheni kwayo imaan yenu mkiwa ni waumini!  

 

 

 

قُلْ إِن كَانَتْ لَكُمُ الدَّارُ الْآخِرَةُ عِندَ اللَّـهِ خَالِصَةً مِّن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٤﴾

94. Sema: Ikiwa nyumba ya Aakhirah iliyoko kwa Allaah ni makhsusi kwenu pekee pasi na watu wengine, basi tamanini mauti mkiwa ni wakweli.

 

 

وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٩٥﴾

95. Na hawatoyatamani abadani kwa sababu ya iliyoyatanguliza mikono yao. Na Allaah Ni Mjuzi wa madhalimu.

 

 

 

وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَىٰ حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا ۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَن يُعَمَّرَ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿٩٦﴾

96. Na kwa yakini utawakuta wao (Mayahudi) ni watu wenye pupa zaidi ya kuishi na kuliko washirikina. Kila mmoja wao anapenda lau angelipewa umri wa miaka elfu. Wala huko kuzidishiwa umri hakutamuondoshea adhabu. Na Allaah Ni Mwenye Kuona wanayoyatenda. 

 

 

قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٩٧﴾

97. Sema: Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na mwongozo na bishara kwa Waumini.[29]

 

 

 

 مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ ﴿٩٨﴾

98. Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rusuli Wake, na Jibriyl, na Miykaaiyl,[30] basi hakika Allaah Ni adui wa makafiri.

 

 

وَلَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ وَمَا يَكْفُرُ بِهَا إِلَّا الْفَاسِقُونَ ﴿٩٩﴾

99. Na kwa yakini Tumeteremsha kwako Aayaat bayana, na hawazikanushi isipokuwa mafasiki.

 

 

أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْدًا نَّبَذَهُ فَرِيقٌ مِّنْهُم ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Je! Eti ndio kila wanapochukua ahadi kundi miongoni mwao huivunja? Bali wengi wao hawaamini.

 

 

 

وَلَمَّا جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ نَبَذَ فَرِيقٌ مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ كِتَابَ اللَّـهِ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ كَأَنَّهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٠١﴾ 

101. Na alipowajia Rasuli kutoka kwa Allaah mwenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao, kundi miongoni mwa wale waliopewa Kitabu walikitupa Kitabu cha Allaah nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui.

 

 

 

وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٢﴾

102. Na wakafuata yale (ya uchawi) waliyoyatoa mashaytwaan (kuuzulia) ufalme wa Sulaymaan. Na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru, wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili katika (mji wa) Baabil; Haaruwt na Maaruwt.[31] Wala hao wawili hawamfundishi yeyote mpaka waseme: Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru. Kisha wakajifunza kutoka kwa hao wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao hawawezi kamwe kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa Idhini ya Allaah, na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi. Na kwa yakini walijua kwamba atakayechuma haya hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni ubaya ulioje walichojiuzia nafsi zao, lau wangelikuwa wanajua.

 

 

وَلَوْ أَنَّهُمْ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَمَثُوبَةٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ خَيْرٌ ۖ لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٣﴾

103. Na lau wangeliamini na wakawa na taqwa, basi malipo kutoka kwa Allaah yangekuwa ni kheri lau wangekuwa wanajua.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا وَقُولُوا انظُرْنَا وَاسْمَعُوا ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٠٤﴾

104. Enyi walioamini! Msiseme (kumwambia Nabiy) “raa’inaa”[32] lakini semeni “undhwurnaa” na sikilizeni. Na makafiri watapata adhabu iumizayo.  

 

 

مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿١٠٥﴾

105. Hawapendi wale waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu, wala washirikina kwamba iteremshwe kwenu kheri yoyote ile kutoka kwa Rabb wenu. Na Allaah Anamkhusisha kwa Rehma Yake Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye Fadhila kuu kabisa.

 

 

مَا نَنسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِّنْهَا أَوْ مِثْلِهَا ۗ أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٦﴾

106. Hatufuti Aayah yoyote au Tunayoisahaulisha ila Tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au mfano wake.[33] Je, hujui kwamba Allaah Ni Mweza wa kila kitu?

 

 

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٠٧﴾

107. Je, hujui kwamba Allaah Ana ufalme wa mbingu na ardhi. Nanyi hamna pasi na Allaah rafiki mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.

 

 

أَمْ تُرِيدُونَ أَن تَسْأَلُوا رَسُولَكُمْ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۗ وَمَن يَتَبَدَّلِ الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿١٠٨﴾

108. Au mnataka kumuuliza Rasuli wenu kama alivyoulizwa Muwsaa hapo kabla? Na yeyote atakayebadilisha imaan kwa kufru, basi kwa yakini amepotea njia iliyo sawa.

 

 

وَدَّ كَثِيرٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُم مِّن بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِّنْ عِندِ أَنفُسِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْحَقُّ ۖ فَاعْفُوا وَاصْفَحُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٩﴾

109. Wengi katika Watu wa Kitabu wametamani kama wangelikurudisheni baada ya kuamini kwenu mkawa makafiri kwa husuda iliyomo katika nafsi zao baada ya kuwabainikia kwao haki. Basi sameheni na puuzeni mpaka Allaah Alete Amri Yake. Hakika Allaah Ni Muweza wa kila kitu.[34]

 

 

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١١٠﴾

110. Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah, na lolote la kheri mnalolitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtalikuta kwa Allaah, hakika Allaah kwa yale myafanyayo Ni Mwenye Kuona.

 

 

وَقَالُوا لَن يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ تِلْكَ أَمَانِيُّهُمْ ۗ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١١١﴾

111. Na walisema: Hatoingia Jannah isipokuwa aliyekuwa Yahudi au Naswaara. Hilo ni tamanio lao.  Sema: Leteni ushahidi wenu wa wazi mkiwa ni wakweli.

 

 

بَلَىٰ مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُ أَجْرُهُ عِندَ رَبِّهِ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١١٢﴾

112. Sivyo hivyo! Bali yeyote aliyeusalimisha uso wake kwa Allaah, na ilhali yeye ni mwenye kufanya ihsaan, basi atapata ujira wake kwa Rabb wake, na wala haitokuwa khofu juu yao wala hawatohuzunika.

 

 

وَقَالَتِ الْيَهُودُ لَيْسَتِ النَّصَارَىٰ عَلَىٰ شَيْءٍ وَقَالَتِ النَّصَارَىٰ لَيْسَتِ الْيَهُودُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُمْ يَتْلُونَ الْكِتَابَ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ مِثْلَ قَوْلِهِمْ ۚ فَاللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿١١٣﴾

113. Na Mayahudi wakasema: Manaswara hawana lao jambo. Na Manaswara wakasema: Mayahudi hawana lao jambo, na hali wao wanasoma Kitabu (Tawraat na Injiyl). Hivyo hivyo ndivyo walivyosema wale wasiojua mfano wa kauli yao (hii). Basi Allaah Atawahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wakikhitilafiana.

 

 

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّـهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١١٤﴾

114. Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayezuia Misikiti ya Allaah kutajwa ndani yake Jina Lake na akajitahidi katika kuiharibu? Hao haitawafaa kuingia humo isipokuwa wakiwa ni wenye khofu. Watapata duniani hizaya na Aakhirah watapata adhabu kuu kabisa.

 

 

وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿١١٥﴾

115. Na Mashariki na Magharibi ni ya Allaah. Basi popote mnapogeuka kuna Wajihi wa Allaah.[35] Hakika Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote.[36]

 

 

وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾

116. Na wakasema: Allaah Amejichukulia mwana. Utakasifu Ni Wake! Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii.[37]

 

 

 بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿١١٧﴾

117. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Anapohukumu jambo huliambia Kun![38] (Kuwa!) Basi nalo huwa.  

 

 

وَقَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ لَوْلَا يُكَلِّمُنَا اللَّـهُ أَوْ تَأْتِينَا آيَةٌ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّثْلَ قَوْلِهِمْ ۘ تَشَابَهَتْ قُلُوبُهُمْ ۗ قَدْ بَيَّنَّا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿١١٨﴾ 

118. Na wakasema wale (majahili) wasiojua kitu: Lau Angetusemesha Allaah au ingetujia Aayah (Ishara)! Kadhalika walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hiyo. Zimeshabihiana nyoyo zao. Kwa yakini Tumekwishabainisha Aayaat (Ishara, Dalili za wazi) kwa watu wenye yakini. 

 

 

 إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا ۖ وَلَا تُسْأَلُ عَنْ أَصْحَابِ الْجَحِيمِ ﴿١١٩﴾

119. Hakika Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki ukiwa mwenye kutoa bishara njema na mwonyaji wala hutoulizwa kuhusu watu wa moto uwakao vikali.

 

 

وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٢٠﴾

120. Na hawatoridhika nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila zao. Sema: Hakika Mwongozo wa Allaah ndio Mwongozo (pekee). Na ukifuata hawaa zao baada ya yale ambayo yamekujia katika ilimu, basi hutopata kutoka kwa Allaah rafiki mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.

 

 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٢١﴾

121. Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ipasavyo ya kusomwa kwake. Hao ndio wanaokiamini, na atakayekikanusha basi hao ndio waliokhasirika.[39]

 

 

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿١٢٢﴾

122. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni Neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya walimwengu.

 

 

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا تَنفَعُهَا شَفَاعَةٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿١٢٣﴾

123. Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitoifaa nafsi nyingine kwa lolote, wala haitokubaliwa kutoka kwake kikomboleo wala haitoifalia uombezi wowote, na wala wao hawatonusuriwa.

 

 وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ ۖ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾

124. Na pindi Alipojaribiwa Ibraahiym na Rabb wake kwa amri nyingi, naye akazitimiza. Akasema: Hakika Mimi Nakufanya uwe Imaam[40] kwa watu. (Ibraahiym) akasema: Na katika kizazi changu? (Allaah) Akasema: Haiwafikii Ahadi Yangu madhalimu.

 

 

وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿١٢٥﴾ 

125. Na Tulipoifanya Nyumba (Al-Ka’bah) kuwa ni mahali pa kurejewa na watu na pa amani, na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym[41] kuwa ni pahala pa kuswalia. Na Tulichukua ahadi kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl kwamba: Itakaseni Nyumba Yangu kwa wanaotufu na wanaokaa i’tikaaf, na wanaorukuu na kusujudu.[42]

 

 

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُقْ أَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُم بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُ قَلِيلًا ثُمَّ أَضْطَرُّهُ إِلَىٰ عَذَابِ النَّارِ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٢٦﴾

126. Na pindi aliposema Ibraahiym: Rabb wangu Ufanye mji huu (Makkah) kuwa wa amani na Waruzuku watu wake katika matunda, atakayemwamini Allaah miongoni mwao na Siku ya Mwisho. (Allaah) Akasema: Na atakayekufuru Nitamstarehesha kidogo kisha Nitamsukumiza katika adhabu ya moto, na ubaya ulioje mahali pa kuishia.

 

 

وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٢٧﴾

127. Na aliponyanyua Ibraahiym na Ismaa’iyl msingi wa Nyumba (Al-Ka’bah): Rabb wetu, Tutakabalie, hakika Wewe Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

 رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٢٨﴾

128. Rabb wetu, Tujaalie tuwe wenye kujisalimisha Kwako pamoja na kizazi chetu wawe ummah wenye kujisalimisha Kwako, na Tuonyeshe taratibu za ibaada zetu na Pokea tawbah zetu, hakika Wewe Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu. 

 

 

رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٢٩﴾

129. Rabb wetu, Wapelekee Rasuli miongoni mwao atakayewasomea Aayaat Zako na atakayewafunza Kitabu na Hikmah na atakayewatakasa. Hakika Wewe Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[43]

 

 

وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُ ۚ وَلَقَدِ اصْطَفَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٣٠﴾

130. Na ni nani atakayejitenga na mila ya Ibraahiym isipokuwa anayeitia nafsi yake upumbavu? Na kwa yakini Tumemkhitari duniani, naye Aakhirah ni miongoni mwa Swalihina.[44]  

 

 

إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ ۖ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٣١﴾

131. Rabb wake Alipomwambia: Jisalimishe na utii. Akasema (Ibraahiym): Nimejisalimisha na kutii kwa Rabb wa walimwengu.

 

 

وَوَصَّىٰ بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَا بَنِيَّ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٣٢﴾

132. Na Ibraahiym akawausia hayo wanawe na Ya’quwb (akawausia wanawe pia):  Enyi wanangu! Hakika Allaah Amekukhitarieni nyinyi Dini, basi chungeni sana, angalieni msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.      

 

 

 أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِن بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٣﴾

133. Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfikia Ya’quwb pale alipowaambia wanawe: Mtaabudu nini baada yangu? Wakasema: Tutamwabudu Ilaaha wako (Allaah) na Ilaaha wa baba zako Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq; Ilaaha Mmoja, nasi ni Waislamu (Wenye kujisalimisha) Kwake.

 

 

تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٤﴾

134. Huo ni ummah uliokwishapita, utapata uliyoyachuma nanyi mtapata mliyoyachuma, na wala hamtoulizwa kuhusu waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

 

 وَقَالُوا كُونُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ تَهْتَدُوا ۗ قُلْ بَلْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٣٥﴾

135. Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Manaswara mtaongoka. Sema:  Bali (tunafuata) mila ya Ibraahiym aliyeelemea haki na wala hakuwa katika washirikina.[45]

 

 

 

 

قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٦﴾

136. Semeni: Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw[46], na aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Rabb wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao, nasi ni Waislamu (wenye kujisalimisha) Kwake.

 

 

فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنتُم بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ ۖ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣٧﴾

137. Watakapoamini kama vile mlivyoamini nyinyi, basi kwa yakini watakuwa wameongoka. Na wakikengeuka, basi hakika wao wamo katika upinzani, na Allaah Atakutosheleza nao, Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

صِبْغَةَ اللَّـهِ ۖ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ صِبْغَةً ۖ وَنَحْنُ لَهُ عَابِدُونَ ﴿١٣٨﴾

138. (Swibghah [Dini] yetu ni) Swibghah[47] (Dini) ya Allaah. Na  Swibghah (dini) gani yaweza kuwa bora zaidi kuliko Swibghah (Dini) ya Allaah? Na sisi ni wenye kumwabudu Yeye Pekee.

 

 

 

 

قُلْ أَتُحَاجُّونَنَا فِي اللَّـهِ وَهُوَ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ وَلَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُخْلِصُونَ ﴿١٣٩﴾

139. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, mnahojiana nasi kuhusu Allaah na hali Yeye ni Rabb wetu na Rabb wenu? Nasi tuna amali zetu nanyi mna amali zenu, na sisi tunamtakasia Yeye tu ibaada?

 

 

أَمْ تَقُولُونَ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطَ كَانُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ قُلْ أَأَنتُمْ أَعْلَمُ أَمِ اللَّـهُ ۗ وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَتَمَ شَهَادَةً عِندَهُ مِنَ اللَّـهِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٤٠﴾

140. Je, mnasema kwamba Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw (kizazi chake) walikuwa Mayahudi au Manaswara? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Allaah? Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi alionao kutoka kwa Allaah? Na Allaah Si Mwenye Kughafilika na yale myatendayo.

 

 

تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٤١﴾

141. Huo ni ummah uliokwishapita, utapata uliyoyachuma nanyi mtapata  mliyoyachuma, na wala hamtoulizwa waliyokuwa wakitenda.

 

 

سَيَقُولُ السُّفَهَاءُ مِنَ النَّاسِ مَا وَلَّاهُمْ عَن قِبْلَتِهِمُ الَّتِي كَانُوا عَلَيْهَا ۚ قُل لِّلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٤٢﴾

142. Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: Nini kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea! Sema: Mashariki na Magharibi ni ya Allaah, Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.[48]

 

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ ۚ وَإِن كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٣﴾

143. Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu.[49] Na Hatukukifanya Qiblah[50] ambacho ulikuwa ukikielekea (Baytul-Maqdis) isipokuwa Tupate kupambanua nani anayemfuata Rasuli kikweli, na nani atakayegeuka arudi nyuma. Na hakika ilikuwa ni jambo gumu isipokuwa kwa wale ambao Allaah Amewaongoza. Na Allaah Hakuwa Mwenye Kupoteza imaan yenu. Hakika Allaah Ni Mwenye Huruma mno kwa tu na Mwenye Kurehemu.[51]

 

 

 

قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ ۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا ۚ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٤﴾

144. Kwa yakini Tunaona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Sisi bila shaka Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Kwa hiyo, elekeza uso wako upande wa Masjid Al-Haraam (Ka’bah; Makkah). Na popote mtakapokuwepo (mkataka kuswali), basi elekezeni nyuso zenu upande wake. Na hakika wale waliopewa Kitabu bila shaka wanajua kwamba hivyo ni haki kutoka kwa Rabb wao. Na Allaah Si Mwenye Kughafilika na yale wayatendayo.[52]

 

 

وَلَئِنْ أَتَيْتَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ بِكُلِّ آيَةٍ مَّا تَبِعُوا قِبْلَتَكَ ۚ وَمَا أَنتَ بِتَابِعٍ قِبْلَتَهُمْ ۚ وَمَا بَعْضُهُم بِتَابِعٍ قِبْلَةَ بَعْضٍ ۚ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ إِنَّكَ إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٥﴾

145. Na hata ukiwaletea wale waliopewa Kitabu Aayah (Ishara, Dalili) za kila aina, hawatofuata Qiblah chako. Na wewe hutofuata Qiblah chao. Na wala baadhi yao hawatofuata Qiblah cha wengineo. Na kama ukiyafuata matamanio yao baada ya kukufikia ilimu, hakika hapo utakuwa miongoni mwa madhalimu.

 

 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ ۖ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنْهُمْ لَيَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٤٦﴾ 

146. Wale Tuliowapa Kitabu wanamtambua (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama wanavyotambua watoto wao, na hakika kundi miongoni mwao wanaficha haki na hali wao wanajua. 

 

 

الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿١٤٧﴾

147. (Ni) Haki kutoka kwa Rabb wako, basi kamwe usiwe miongoni mwa wenye kufanya shaka.

 

وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ أَيْنَ مَا تَكُونُوا يَأْتِ بِكُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٤٨﴾

148. Na kila mmoja ana upande wa kuuelekea. Basi shindaneni mambo ya kheri. Popote mtakapokuwa Allaah Atakuleteni nyote pamoja (Qiyaamah). Hakika Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۖ وَإِنَّهُ لَلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٤٩﴾ 

149. Na popote utokako (ili kuswali), basi elekeza uso wako upande wa Masjid Al-Haraam. Na hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wako. Na Allaah Si Mwenye Kughafilika na yale myatendayo.

 

 

وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيْكُمْ حُجَّةٌ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي وَلِأُتِمَّ نِعْمَتِي عَلَيْكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٥٠﴾

150. Na popote utokako (ili kuswali), elekeza uso wako upande wa Masjid Al-Haraam. Na popote mtakapokuwa, elekezeni nyuso zenu upande wake, ili watu wasiwe na hoja juu yenu isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope bali Niogopeni Mimi, na ili Nitimize Neema Yangu juu yenu na ili mpate kuhidika.

 

 

كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿١٥١﴾

151. Kama Tulivyomtuma kwenu Rasuli anayetokana na nyinyi, anawasomea Aayaat Zetu na anakutakaseni na anakufunzeni Kitabu na Hikmah (Sunnah), na anakufundisheni mambo ambayo hamkuwa mkiyajua.

 

 

فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ﴿١٥٢﴾

152. Basi nidhukuruni na Mimi Nitakukumbukeni, na nishukuruni wala msinikufuru.

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٣﴾

153. Enyi walioamini! Tafuteni msaada kwa subira na Swalaah, hakika Allaah Yu pamoja na wenye subira.

 

 

وَلَا تَقُولُوا لِمَن يُقْتَلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتٌ ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ وَلَـٰكِن لَّا تَشْعُرُونَ ﴿١٥٤﴾ 

154. Wala msiseme kuwa (Shuhadaa) waliouawa katika Njia ya Allaah ni wafu, bali wako hai lakini hamhisi.

 

 

وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾

155. Na bila shaka Tutakujaribuni kwa jambo katika khofu, njaa, upungufu wa mali, nafsi na mazao. Na wabashirie wenye subira.

 

 

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿١٥٦﴾

156. Wale ambao unapowafika msiba husema: Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.[53]

 

 

أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ﴿١٥٧﴾

157. Hao zitakuwa juu yao Barakah kutoka kwa Rabb wao na Rehma, na hao ndio wenye kuhidika.

 

 

إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٥٨﴾

158. Hakika Swafaa na Marwah ni katika Alama za Allaah. Kwa hiyo yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah, hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya kheri, basi hakika Allaah Ni Mwenye Kupokea Shukurani, Mjuzi wa yote.[54]

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ ﴿١٥٩﴾

159. Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja bayana na mwongozo baada ya kuwa Tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu, hao ndio Allaah Anawalaani na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.

 

 

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَبَيَّنُوا فَأُولَـٰئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٠﴾ 

160. Isipokuwa wale waliotubu na wakatengeneza (waliyoharibu) na wakabainisha (haki), basi hao Napokea tawbah zao. Na Mimi Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ لَعْنَةُ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿١٦١﴾

161. Hakika wale waliokufuru na wakafa hali ya kuwa ni makafiri, hao iko juu yao Laana ya Allaah na ya Malaika na ya watu wote.

 

 

 خَالِدِينَ فِيهَا ۖ لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿١٦٢﴾

162. Watadumu humo (ndani ya moto), hawatopunguziwa adhabu na wala hawatopewa muhula wa kupumzika.

 

 

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

163.  Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Mwingi wa Rehma, Mwenye Kurehemu.[55]

 

 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن مَّاءٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿١٦٤﴾

164. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya usiku na mchana, na merikebu zipitazo katika bahari kwa vile viwafaavyo watu, na maji ambayo Allaah Ameyateremsha toka mbinguni Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake, na Akaeneza humo kila aina ya mnyama, na mgeuko wa upepo wa rehma, na mawingu yanayotiishwa baina ya mbingu na ardhi, ni Aayaat (Dalili, Mazingatio) kwa watu wenye akili.

 

 

 وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ ﴿١٦٥﴾

165. Na miongoni mwa watu wako wenye kuwafanya viumbe miungu badala ya Allaah, wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. Na lau wale waliodhulumu wangelitambua watakapoona adhabu, kwamba nguvu zote ni za Allaah, na kwamba hakika Allaah ni Mkali wa Kuadhibu, (basi wasingelimfanyia Allaah washirika).

 

 

إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ﴿١٦٦﴾

166. Waliofuatwa watakapowakana wale waliowafuata na hali ya kuwa wamekwishaiona adhabu, na yatawakatikia mafungamano yao.

 

 

وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا ۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ اللَّـهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ ۖ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ ﴿١٦٧﴾

167. Na watasema wale waliofuata: Lau tungelipata fursa ya kurudi (duniani) tungewakana kama walivyotukana. Hivyo ndivyo Allaah Atakavyowaonyesha amali zao kuwa ni majuto yao. Na wala hawatokuwa wenye kutoka motoni.

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٦٨﴾

168. Enyi watu! Kuleni katika vilivyomo ardhini vya halali, vizuri na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.

 

 

إِنَّمَا يَأْمُرُكُم بِالسُّوءِ وَالْفَحْشَاءِ وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٦٩﴾ 

169. Hakika hakuna isipokuwa anakuamrisheni maovu na machafu (na ubakhili) na mseme dhidi ya Allaah msiyoyajua.

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۗ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٧٠﴾

170. Na wanapoambiwa: Fuateni Aliyoyateremsha Allaah husema: Bali tunafuata tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, japokuwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu chochote na wala hawakuongoka?

 

 

 وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٧١﴾

171. Na mfano wa wale waliokufuru ni kama mfano wa yule ambaye anapiga kelele kwa ambaye hasikii ila sauti na mwito. Viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawatii akilini.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ ﴿١٧٢﴾

172. Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni[56] na mshukuruni Allaah mkiwa mnamwabudu Yeye Pekee.

 

 

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٧٣﴾

173. Hakika Allaah Amekuharamishieni mzoga na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa asiyekuwa Allaah wakati wa kuchinjwa. Lakini aliyefikwa na dharura (akala) bila ya kutamani wala kupindukia mipaka, basi si dhambi juu yake. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ الْكِتَابِ وَيَشْتَرُونَ بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۙ أُولَـٰئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ إِلَّا النَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٤﴾

174. Hakika wale wanaoficha yale Aliyoyateremsha Allaah katika Kitabu na wakakibadilisha kwa thamani ndogo, hao hawali katika matumbo yao isipokuwa moto, na wala Allaah Hatowasemesha Siku ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa, nao watapata adhabu iumizayo.

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ وَالْعَذَابَ بِالْمَغْفِرَةِ ۚ فَمَا أَصْبَرَهُمْ عَلَى النَّارِ ﴿١٧٥﴾

175. Hao ndio wale waliobadilisha upotofu badala ya hidaaya, na adhabu kwa maghfirah. Basi kuvumilia gani huko kwao ndani ya moto?

 

 

 ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ نَزَّلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِي الْكِتَابِ لَفِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ ﴿١٧٦﴾

176. Hayo ni kwa sababu Allaah Amekiteremsha Kitabu kwa haki. Na hakika wale waliokhitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani wa mbali.

 

 

لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا ۖ وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ ﴿١٧٧﴾ 

177. Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi, lakini wema ni mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na akawapa mali juu ya kuipenda kwake jamaa wa karibu na mayatima na masikini na msafiri na waombao na katika kukomboa watumwa, na akasimamisha Swalaah na akatoa Zakaah, na watimizao ahadi zao wanapoahidi, na wenye subira katika dhiki za ufukara na maafa ya magonjwa na njaa na katika vita. Hao ndio waliosadikisha na hao ndio wenye taqwa.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى ۖ الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالْأُنثَىٰ بِالْأُنثَىٰ ۚ فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ ۗ ذَٰلِكَ تَخْفِيفٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَرَحْمَةٌ ۗ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٨﴾

178. Enyi walioamini! Mmeandikiwa sharia ya kisasi kwa waliouawa. Muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke, na anayesamehewa na nduguye kwa lolote basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema na kumlipa kwake iwe kwa ihsaan. Hiyo ni takhafifu kutoka kwa Rabb wenu na Rehma. Na atakayevuka mipaka baada ya hapo basi atapata adhabu iumizayo.

 

وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٧٩﴾

179. Na mtapata katika kisasi (kuokoa) uhai enyi wenye akili ili mpate kuwa na taqwa.

 

 

كُتِبَ عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ إِن تَرَكَ خَيْرًا الْوَصِيَّةُ لِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ ﴿١٨٠﴾

180. Mmeandikiwa sharia kuwa anapofikiwa mmoja wenu na mauti kama ameacha mali, kufanya wasia kwa wazazi wawili, na jamaa wa karibu kwa namna inayoeleweka katika sharia. (Haya) ni wajibu kwa wenye taqwa.

 

 

فَمَن بَدَّلَهُ بَعْدَ مَا سَمِعَهُ فَإِنَّمَا إِثْمُهُ عَلَى الَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٨١﴾ 

181. Atakayeubadilisha (wasia) baada ya kuusikia, basi hakika dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha. Hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

فَمَنْ خَافَ مِن مُّوصٍ جَنَفًا أَوْ إِثْمًا فَأَصْلَحَ بَيْنَهُمْ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٨٢﴾

182. Na mwenye kumkhofia muusiaji kwamba kaenda kombo bila kukusudia, au kakusudia dhambi kisha akasuluhisha baina yao, basi hana dhambi juu yake.  Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾

183. Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa.

 

أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ ۚ وَأَن تَصُومُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٨٤﴾

184. (Swiyaam ni) siku za kuhesabika. Lakini atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. Na kwa wale wanaoiweza lakini kwa mashaka na kutaabika watoe fidia kulisha masikini. Na atakayefanya wema kwa hiari yake, basi hivyo ni bora kwake. Na mkifunga (Swiyaam) ni bora kwenu mkiwa mnajua.

 

 

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٨٥﴾

185. Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo[57] (la haki na baatwil). Kwa hiyo atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi (inampasa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu ili mkamilishe idadi na ili mumtukuze Allaah kwa kuwa Amekuongozeni, na ili mpate kushukuru.

 

 

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾

186. Na watakapokuuliza Waja Wangu kuhusu Mimi, basi (waambie) hakika Mimi Niko Karibu (kwa ujuzi). Naitikia duaa ya muombaji anaponiomba. Hivyo basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka.[58]

 

 

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٨٧﴾

187. Mmehalalishiwa usiku wa Swiyaam kujamiiana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Allaah Anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkijifanyia khiyana nafsi zenu, hivyo Akapokea tawbah yenu na Akakusameheni. Basi sasa waingilieni na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). Kisha timizeni Swiyaam mpaka usiku. Na wala msiwaingilie hali ya kuwa nyinyi mko katika i’tikaaf misikitini. Hiyo ni Mipaka ya Allaah basi msiikaribie. Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (na Hukmu) Zake kwa watu wapate kuwa na taqwa.[59]

 

 

 وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا فَرِيقًا مِّنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٨٨﴾

188. Na wala msiliane mali zenu kwa ubatwilifu na mkazipeleka (rushwa) kwa mahakimu ili mle sehemu katika mali ya watu kwa dhambi na hali mnajua.

 

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَن تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٨٩﴾

189. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu miandamo ya mwezi. Sema: Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa watu na Hajj. Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake, lakini wema ni kuwa na taqwa. Na ingieni majumbani kupitia milango yake. Na mcheni Allaah mpate kufaulu.[60]

 

 

وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿١٩٠﴾

190. Na piganeni katika Njia ya Allaah na wale wanaokupigeni, wala msitaadi. Hakika Allaah Hapendi wenye kutaadi.

 

 

 

وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ ۚ وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ ۖ فَإِن قَاتَلُوكُمْ فَاقْتُلُوهُمْ ۗ كَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ ﴿١٩١﴾

191. Na wauweni popote muwakutapo, na watoeni popote walipokutoeni. Na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na wala msipigane nao kwenye Masjid Al-Haraam mpaka wakupigeni humo, watakapokupigeni basi wauweni. Namna hivi ndivyo jazaa ya makafiri.

 

 

فَإِنِ انتَهَوْا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٢﴾ 

192. Wakikoma, basi Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.

 

 

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّـهِ ۖ فَإِنِ انتَهَوْا فَلَا عُدْوَانَ إِلَّا عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿١٩٣﴾

193. Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah (shirki, kufru) na Dini iwe kwa ajili ya Allaah Pekee, wakikoma basi kusiweko na uadui ila kwa madhalimu.

 

 

الشَّهْرُ الْحَرَامُ بِالشَّهْرِ الْحَرَامِ وَالْحُرُمَاتُ قِصَاصٌ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ ﴿١٩٤﴾

194. Mwezi mtukufu kwa mwezi mtukufu na vitukufu vimewekewa kisasi. Basi anayekushambulieni nanyi mshambulieni kwa kadiri ya alivyokushambulieni. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.

 

 

 

  وَأَنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٩٥﴾

195. Na toeni katika Njia ya Allaah wala msijitupe katika maangamizi kwa (kuzuia) mikono yenu (isitoe). Na fanyeni ihsaan, hakika Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.[61]

 

 

 

وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ ۚ فَإِنْ أُحْصِرْتُمْ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۖ وَلَا تَحْلِقُوا رُءُوسَكُمْ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِّن رَّأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِّن صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ ۚ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَمَن تَمَتَّعَ بِالْعُمْرَةِ إِلَى الْحَجِّ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۚ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ فِي الْحَجِّ وَسَبْعَةٍ إِذَا رَجَعْتُمْ ۗ تِلْكَ عَشَرَةٌ كَامِلَةٌ ۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمْ يَكُنْ أَهْلُهُ حَاضِرِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١٩٦﴾

196. Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah.  Na kama mkizuilika basi chinjeni wanyama walio wepesi kupatikana. Na wala msinyoe vichwa vyenu mpaka mnyama afikie machinjoni pake. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake (ikambidi anyoe), basi atoe fidia kwa kufunga (Swiyaam) au kutoa swadaqa au kuchinja mnyama. Na mtakapopata amani, basi mwenye kufanya Tamattu’u[62] kwa kutekeleza ‘Umrah kwanza kisha Hajj, achinje mnyama aliye mwepesi. Na asiyepata afunge Swiyaam siku tatu katika Hajj na saba mtakaporejea. Hizo ni kumi kamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawaishi karibu na Masjid Al-Haraam. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.[63]   

 

 

 

 

 الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٧﴾

197. Hajj ni miezi maalumu.[64] Na atakayekusudia kuhiji ndani ya miezi hiyo (akahirimia), basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote la kheri mlifanyalo Allaah Analijua. Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili![65]

 

 

 

لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ ۚ فَإِذَا أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ عِندَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ ۖ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّينَ ﴿١٩٨﴾ 

198. Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wenu. Basi mtakapomiminika kutoka ‘Arafaat mdhukuruni Allaah kwenye Mash’aril-Haraam (Muzdalifah) na mdhukuruni Yeye kama Alivyokuongozeni, kwani hakika mlikuwa kabla ya hapo ni miongoni mwa waliopotea.[66]

 

 

 

 ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٩﴾

199. Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu na ombeni maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.[67]

 

 

 

فَإِذَا قَضَيْتُم مَّنَاسِكَكُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَذِكْرِكُمْ آبَاءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا ۗ فَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ﴿٢٠٠﴾

200. Mtakapomaliza kutekeleza ibaada zenu za Hajj, basi mdhukuruni Allaah kama mnavyowadhukuru baba zenu bali mdhukuruni (Yeye) zaidi. Kwani kuna baadhi ya watu wasemao: Rabb wetu Tupe katika dunia (mazuri yake lakini wanasahau Aakhirah), naye katika Aakhirah hana sehemu yoyote.

 

 

 

  وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿٢٠١﴾

201. Na miongoni mwao kuna wasemao: Rabb wetu Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na Tukinge na adhabu ya moto.[68]

 

 

 

 أُولَـٰئِكَ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّمَّا كَسَبُوا ۚ وَاللَّـهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٢٠٢﴾

202. Hao watapata pato lao kutokana na waliyoyachuma, na Allaah Ni Mwepesi wa Kuhesabu.

 

 

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٢٠٣﴾

203. Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika.[69] Atakayeharakisha kuondoka katika siku mbili basi hakuna dhambi juu yake, na atakayeakhirisha, basi hakuna dhambi juu yake, kwa mwenye taqwa. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Kwake mtakusanywa.

 

 

 وَمِنَ النَّاسِ مَن يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللَّـهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ ﴿٢٠٤﴾

204. Na miongoni mwa watu yupo anayekuvutia kauli yake katika uhai wa dunia na humshuhudisha Allaah kwa yale yaliyomo katika moyo wake na hali yeye ndiye khasimu mbaya zaidi.

 

 

وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ ﴿٢٠٥﴾ 

205. Na anapoondoka hufanya bidii katika ardhi ili afisidi humo na aangamize mimea na vizazi.  Na Allaah Hapendi ufisadi.

 

 

 

 وَإِذَا قِيلَ لَهُ اتَّقِ اللَّـهَ أَخَذَتْهُ الْعِزَّةُ بِالْإِثْمِ ۚ فَحَسْبُهُ جَهَنَّمُ ۚ وَلَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿٢٠٦﴾

206. Na anapoambiwa: Mche Allaah! Hupandwa kiburi kinachompeleka kutenda madhambi. Basi Jahannam inamtosheleza, na mahali pabaya palioje pa kupumzikia.

 

 

  وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠٧﴾

207. Na miongoni mwa watu yupo anayeiuza nafsi yake kutafuta Radhi za Allaah. Na Allaah Ni Mwenye Huruma mno kwa waja.[70]

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٠٨﴾

208. Enyi walioamini! Ingieni katika Uislamu kikamilifu, na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.

 

 

 

فَإِن زَلَلْتُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْكُمُ الْبَيِّنَاتُ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٠٩﴾

209. Lakini mkiteleza baada ya kukujieni hoja bayana, basi jueni kwamba hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٢١٠﴾

210. Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah Awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika (Siku ya Qiyaamah),[71] na jambo lihukumiwe. Na kwa Allaah ndipo hurudishwa mambo.

 

 

 سَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَمْ آتَيْنَاهُم مِّنْ آيَةٍ بَيِّنَةٍ ۗ وَمَن يُبَدِّلْ نِعْمَةَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢١١﴾

211. Waulize wana wa Israaiyl, ni Aayah (Ishara, Dalili) ngapi Tumewapa zilizo bayana? Na atakayebadilisha Neema ya Allaah (kwa kufru) baada ya kumjia, basi hakika Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.[72]

 

 

 

زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا ۘ وَالَّذِينَ اتَّقَوْا فَوْقَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَاللَّـهُ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢١٢﴾

212. Wamepambiwa wale waliokufuru uhai wa dunia na wanawakejeli wale walioamini. Na wale walio na taqwa watakuwa juu yao Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Humruzuku Amtakaye bila ya hesabu.

 

 

 

 كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۖ فَهَدَى اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ ۗ وَاللَّـهُ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢١٣﴾

213. Watu walikuwa ummah mmoja, kisha Allaah Akatuma Manabii wabashiriaji na waonyaji, na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu baina ya watu katika ambayo wamekhitilafiana kwayo. Na hawakukhitilafiana katika hayo isipokuwa wale waliopewa hicho (Kitabu) baada ya kuwajia hoja bayana kwa kufanyiana baghi[73] (chuki na husuda) baina yao. Allaah Akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa Idhini Yake. Na Allaah Humwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.

 

 

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّـهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّـهِ قَرِيبٌ ﴿٢١٤﴾

214. Je, mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali bado haijakufikieni (mitihani) kama ya wale waliopita kabla yenu? Ziliwagusa dhiki za umasikini na maafa ya magonjwa na njaa, na wakatetemeshwa mpaka Rasuli na wale walioamini pamoja naye wakasema: Lini itafika Nusura ya Allaah? Tanabahi! Hakika Nusura ya Allaah iko karibu.

 

 

يَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ ۖ قُلْ مَا أَنفَقْتُم مِّنْ خَيْرٍ فَلِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢١٥﴾

215. Wanakuuliza nini watoe?  Sema: Mnachotoa chochote katika kheri basi ni kwa ajili ya wazazi wawili, jamaa wa karibu, mayatima, masikini, na msafiri.  Na lolote mlifanyalo katika kheri basi hakika Allaah kwa hilo Ni Mjuzi.

 

 

 كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢١٦﴾

216. Mmeandikiwa sharia kupigana vita nako kunachukiza mno kwenu. Lakini asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni la kheri kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.

 

 

 يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ ۖ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ ۖ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَكُفْرٌ بِهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَإِخْرَاجُ أَهْلِهِ مِنْهُ أَكْبَرُ عِندَ اللَّـهِ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَكْبَرُ مِنَ الْقَتْلِ ۗ وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا ۚ وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢١٧﴾

217. Wanakuuliza kuhusu mwezi mtukufu na (swala la) kupigana humo. Sema: Kupigana humo ni dhambi kubwa, lakini kuzuia Njia ya Allaah na kumkufuru Yeye na (kuzuia) Masjid Al-Haraam na kuwatoa watu wake humo, ni (dhambi) kubwa zaidi mbele ya Allaah. Na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na wala hawatoacha kukupigeni vita mpaka wakutoeni katika Dini yenu wakiweza. Na atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, akafariki hali ya kuwa ni kafiri, basi hao zimeporomoka amali zao katika dunia na Aakhirah. Na hao ni watu wa motoni, wao humo watadumu.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢١٨﴾

218. Hakika wale walioamini na wale waliohajiri na wakapigana Jihaad katika Njia ya Allaah, hao wanataraji Rehma ya Allaah, na Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.

 

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾

219. Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza nini watoe. Sema: Yaliyokuzidieni. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na Sharia) ili mpate kutafakari.[74]

 

 

 

 فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۗ وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ ۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَأَعْنَتَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٠﴾

220. Katika dunia na Aakhirah. Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: Kuwatengenezea (ya kuwafaa) ni kheri zaidi. Na mkichanganya mambo yenu na yao basi hao ni ndugu zenu. Na Allaah Anamjua fisadi na mtengenezaji. Na lau Angetaka Allaah Angelikutieni katika shida. Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[75]

 

 

 وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٢١﴾

221. Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Na wala msiwaozeshe (wanawake wa Kiislamu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Hao wanaitia katika moto na Allaah Anaitia katika Jannah (Pepo) na maghfirah kwa Idhini Yake. Na Anabainisha Aayaat (na Sharia) Zake ili wapate kukumbuka.

 

 

 وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ ﴿٢٢٢﴾ 

222. Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: Hiyo ni dhara, hivyo basi waepukeni wanawake katika hedhi. Wala msiwakaribie kujimai nao mpaka watwaharike. Watakapotwaharika basi waendeeni kupitia pale Alipokuamrisheni Allaah.  Hakika Allaah Anapenda wenye kutubia na Anapenda wenye kujitwaharisha.[76]

 

 

 نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُم مُّلَاقُوهُ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٢٣﴾

223. Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi)[77] vyovyote mpendavyo. Na kadimisheni (mema) kwa ajili ya nafsi zenu. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wabashirie Waumini.[78]

 

 

 

 وَلَا تَجْعَلُوا اللَّـهَ عُرْضَةً لِّأَيْمَانِكُمْ أَن تَبَرُّوا وَتَتَّقُوا وَتُصْلِحُوا بَيْنَ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٢٤﴾

224. Na wala msifanye (Jina la) Allaah kuwa ni nyudhuru ya viapo vyenu[79] kukuzuieni katika kutenda wema na kuwa na taqwa na kusuluhisha baina ya watu. Na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٢٥﴾

225. Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi[80] lakini Atakuchukulieni kwa yaliyochuma nyoyo zenu. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mvumilivu.[81]

 

 

 لِّلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِن نِّسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ ۖ فَإِن فَاءُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٢٦﴾

226. Kwa wale walioapa kujitenga na wake zao (kutokujamiiana) wangojee miezi minne. Wakirejea, basi hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.

 

 وَإِنْ عَزَمُوا الطَّلَاقَ فَإِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٢٢٧﴾

227. Na wakiazimia talaka, basi hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا ۚ وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٨﴾

228. Na wanawake waliotalikiwa wabakie kungojea zipite hedhi (na twahara) tatu. Na wala si halali kwao kuficha Aliyoumba Allaah katika matumbo yao ikiwa wao ni wenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na waume zao wana haki kuwarejea katika muda huo ikiwa watataka suluhu. Nao wake wana haki kama ambayo (ya waume zao) iliyo juu yao kwa mujibu wa sharia. Na wanaume wana daraja zaidi juu yao. Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ ۗ وَلَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَأْخُذُوا مِمَّا آتَيْتُمُوهُنَّ شَيْئًا إِلَّا أَن يَخَافَا أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا افْتَدَتْ بِهِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٢٩﴾

229. Talaka ni mara mbili. Hivyo kuzuia kwa mujibu wa sharia au kuachia kwa ihsaan. Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika mlivyowapa wanawake, isipokuwa wote wawili wakikhofu kuwa hawatoweza kusimamisha Mipaka ya Allaah. Mtakapokhofu kuwa wote wawili hawatoweza kusimamisha mipaka Mipaka ya Allaah, basi hakuna lawama juu yao katika ambacho (mke) amejikombolea kwacho (khul’u)[82]. Hiyo ni Mipaka ya Allaah basi msitaadi. Na atakayetaadi Mipaka ya Allaah basi hao ndio madhalimu.

 

 

 فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ مِن بَعْدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ ۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يَتَرَاجَعَا إِن ظَنَّا أَن يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۗ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٢٣٠﴾

230. Na akimtaliki (mara ya tatu), basi hatokuwa halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwengine.[83] Akimtaliki (au akifariki) hapatokuwa dhambi juu yao wawili kurejeana wakidhani kwamba watasimamisha Mipaka ya Allaah. Na hiyo ni Mipaka ya Allaah Anaibainisha kwa watu wanaojua.

 

 

وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ ۚ وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِّتَعْتَدُوا ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ وَلَا تَتَّخِذُوا آيَاتِ اللَّـهِ هُزُوًا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمَا أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّنَ الْكِتَابِ وَالْحِكْمَةِ يَعِظُكُم بِهِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٣١﴾

231. Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao, basi wazuieni kwa wema au waachilieni kwa wema. Na wala msiwazuie kuwakusudia dhara mkafanya uonevu. Na atakayefanya hivyo basi kwa yakini amejidhulumu nafsi yake. Na wala msizifanyie mzaha Aayaat (na Sharia) za Allaah. Na kumbukeni Neema za Allaah juu yenu na Aliyokuteremshieni katika Kitabu na Hikmah (Sunnah) Anakuwaidhini kwacho. Na mcheni Allaah na jueni kwamba Allaah Ni Mjuzi wa kila kitu.

 

 

 وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَن يَنكِحْنَ أَزْوَاجَهُنَّ إِذَا تَرَاضَوْا بَيْنَهُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ ذَٰلِكَ يُوعَظُ بِهِ مَن كَانَ مِنكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗ ذَٰلِكُمْ أَزْكَىٰ لَكُمْ وَأَطْهَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢٣٢﴾

232. Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao, msiwazuie kuolewa na waume zao (wa awali) ikiwa wameridhiana baina yao kwa mujibu wa ada. Hayo anawaidhiwa kwayo, yeyote miongoni mwenu, mwenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo kwenu ni wema zaidi na safi kabisa. Na Allaah Anajua nanyi hamjui.[84]

 

 

وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ ۖ لِمَنْ أَرَادَ أَن يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ ۚ وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ لَا تُكَلَّفُ نَفْسٌ إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَا تُضَارَّ وَالِدَةٌ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوْلُودٌ لَّهُ بِوَلَدِهِ ۚ وَعَلَى الْوَارِثِ مِثْلُ ذَٰلِكَ ۗ فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٍ مِّنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا ۗ وَإِنْ أَرَدتُّمْ أَن تَسْتَرْضِعُوا أَوْلَادَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِذَا سَلَّمْتُم مَّا آتَيْتُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٣﴾ 

233. Na wazazi wa kike wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa mwenye kutaka kutimiza kunyonyesha. Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa ada. Hailazimishwi nafsi ila kwa iliwezalo. Asidhuriwe mzazi wa kike kwa ajili ya mwanawe, na wala mzazi wa kiume kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi (wa baba) mfano wa hivyo. Watakapotaka kumwachisha kunyonya kwa maridhiano baina yao wawili na mashauriano, basi hapana dhambi juu ya wawili hao. Na mtakapotaka kutafuta wa kuwayonyesha watoto wenu, basi si dhambi kwenu ikiwa mtalipa mlichoahidi kwa mujibu wa sharia. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika Allaah Ni Mwenye Kuona yale myatendayo.

 

 

 وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا ۖ فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٣٤﴾

234. Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wajisubirishe wenyewe (kwa kukaa eda) miezi minne na siku kumi.[85] Watakapofikia muda wao, si dhambi kwenu katika yale waliyoyafanya katika nafsi zao kwa ada ya kisharia. Na Allaah kwa yale myatendayo, Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ أَوْ أَكْنَنتُمْ فِي أَنفُسِكُمْ ۚ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ سَتَذْكُرُونَهُنَّ وَلَـٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّا أَن تَقُولُوا قَوْلًا مَّعْرُوفًا ۚ وَلَا تَعْزِمُوا عُقْدَةَ النِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْكِتَابُ أَجَلَهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي أَنفُسِكُمْ فَاحْذَرُوهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٣٥﴾

235. Wala si dhambi juu yenu katika ambayo mmedokezea ya kuposa wanawake hao au mliyoficha katika nafsi zenu. Allaah Anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka lakini msifunge nao ahadi kisiri isipokuwa mseme kauli inayoeleweka kawaida. Na wala msiazimie kufunga ndoa mpaka muda ulioandikwa kisharia (katika eda) ufike mwisho wake. Na jueni kwamba Allaah Anajua yaliyomo katika nafsi zenu basi jihadharini Naye. Na jueni kwamba hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mvumilivu.

 

 

لَّا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ مَا لَمْ تَمَسُّوهُنَّ أَوْ تَفْرِضُوا لَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى الْمُوسِعِ قَدَرُهُ وَعَلَى الْمُقْتِرِ قَدَرُهُ مَتَاعًا بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُحْسِنِينَ ﴿٢٣٦﴾

236. Hakuna dhambi kwenu mkiwataliki wanawake ambao hamkuwagusa au kuwabainishia mahari yao. Wapeni kiliwazo kwa mwenye wasaa kadiri ya uwezo wake, na mwenye dhiki kadiri ya uwezo wake. Maliwaza kwa mujibu wa ada, ni haki kwa wafanya ihsaan.

 

 

وَإِن طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّا أَن يَعْفُونَ أَوْ يَعْفُوَ الَّذِي بِيَدِهِ عُقْدَةُ النِّكَاحِ ۚ وَأَن تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۚ وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٧﴾ 

237. Na mkiwataliki kabla ya kuwagusa na mkawa mmeshawabainishia mahari yao, basi (wapeni) nusu ya hayo mliyobainisha, isipokuwa wakisamehe au asamehe yule ambaye fungamano la ndoa liko mikononi mwake. Na kusamehe kuko karibu zaidi na taqwa. Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah Ni Mwenye Kuona myatendayo.

 

 

حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ﴿٢٣٨﴾

238. Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.[86]

 

 

 فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا ۖ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿٢٣٩﴾

239. Mkikhofu, basi (swalini) huku mnatembea au mmepanda kipando. Mtakapokuwa katika amani, mdhukuruni Allaah kama Alivyokufunzeni yale mliyokuwa hamuyajui.

 

 

وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا وَصِيَّةً لِّأَزْوَاجِهِم مَّتَاعًا إِلَى الْحَوْلِ غَيْرَ إِخْرَاجٍ ۚ فَإِنْ خَرَجْنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِي مَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعْرُوفٍ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٤٠﴾

240. Na wale waliofishwa miongoni mwenu wakaacha wake, wausie kwa ajili ya wake zao masurufu kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa. Watakapotoka wenyewe basi hakuna dhambi juu yenu katika yale waliyojifanyia wenyewe katika yanayokubalika na sharia.[87] Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 وَلِلْمُطَلَّقَاتِ مَتَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ ﴿٢٤١﴾

241. Na wanawake waliotalikiwa wapewe kiliwazo (kitoka nyumba) kwa mujibu wa sharia, ni haki juu ya wenye taqwa.

 

 

كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴿٢٤٢﴾

242. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na Sharia) Zake mpate kutia akilini.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ الْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ اللَّـهُ مُوتُوا ثُمَّ أَحْيَاهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٢٤٣﴾

243. Je, hukuwaona wale waliotoka majumbani mwao nao wakiwa ni maelfu wakikhofu mauti, Allaah Akawaambia: Kufeni kisha Akawahuisha? Hakika Allaah Ni Mwenye Fadhila kwa watu lakini watu wengi hawashukuru.

 

 

وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٢٤٤﴾

244. Na piganeni katika Njia ya Allaah, na jueni kwamba Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ وَاللَّـهُ يَقْبِضُ وَيَبْسُطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٤٥﴾

245. Ni nani atakayemkopesha Allaah karadha nzuri kisha (Allaah) Amzidishie mzidisho mwingi. Na Allaah Anakunja na Anakunjua, na Kwake mtarejeshwa.

 

 

 أَلَمْ تَرَ إِلَى الْمَلَإِ مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ إِذْ قَالُوا لِنَبِيٍّ لَّهُمُ ابْعَثْ لَنَا مَلِكًا نُّقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ قَالَ هَلْ عَسَيْتُمْ إِن كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ أَلَّا تُقَاتِلُوا ۖ قَالُوا وَمَا لَنَا أَلَّا نُقَاتِلَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَقَدْ أُخْرِجْنَا مِن دِيَارِنَا وَأَبْنَائِنَا ۖ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ تَوَلَّوْا إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٢٤٦﴾

246. Je, hukuwazingatia wakuu katika wana wa Israaiyl baada ya Muwsaa walipomwambia Nabiy wao: Tutumie mfalme tupigane katika Njia ya Allaah. (Nabiy) akasema: Je, haiyumkiniki kuwa hamtopigana ikiwa mtaandikiwa kupigana vita? Wakasema: Tuna nini hata tusipigane katika Njia ya Allaah na hali tumekwishatolewa kutoka majumbani mwetu pamoja na watoto wetu? Walipoandikiwa wapigane vita, walikengeuka isipokuwa wachache miongoni mwao. Na Allaah Ni Mjuzi wa madhalimu.

 

 

 

وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ اللَّـهَ قَدْ بَعَثَ لَكُمْ طَالُوتَ مَلِكًا ۚ قَالُوا أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ الْمُلْكُ عَلَيْنَا وَنَحْنُ أَحَقُّ بِالْمُلْكِ مِنْهُ وَلَمْ يُؤْتَ سَعَةً مِّنَ الْمَالِ ۚ قَالَ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاهُ عَلَيْكُمْ وَزَادَهُ بَسْطَةً فِي الْعِلْمِ وَالْجِسْمِ ۖ وَاللَّـهُ يُؤْتِي مُلْكَهُ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٤٧﴾ 

247. Nabiy wao akawaambia: Hakika Allaah Amekutumieni Twaaluwt kuwa ni mfalme. Wakasema: Vipi yeye atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi tunastahiki zaidi ufalme kuliko yeye, na wala hakupewa wasaa katika mali? (Nabiy) akasema: Hakika Allaah Amemkhitari juu yenu na Akamuongezea ukunjufu katika ilimu na kiwiliwili, na Allaah Humpa Amtakaye Ufalme Wake. Na Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote.

 

 

 وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ آيَةَ مُلْكِهِ أَن يَأْتِيَكُمُ التَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَبَقِيَّةٌ مِّمَّا تَرَكَ آلُ مُوسَىٰ وَآلُ هَارُونَ تَحْمِلُهُ الْمَلَائِكَةُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٤٨﴾

248. Nabiy wao akawaambia: Hakika Aayah (Ishara, Dalili) ya ufalme wake ni kwamba litakujieni kasha ndani yake mna kituliza nyoyo kutoka kwa Rabb wenu na mabaki katika yale waliyoacha watu wa Muwsaa na watu wa Haaruwn, watalibeba Malaika. Hakika katika hayo mna Aayah (Ishara, Dalili, Hoja) kwenu mkiwa ni Waumini.

 

 

فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِالْجُنُودِ قَالَ إِنَّ اللَّـهَ مُبْتَلِيكُم بِنَهَرٍ فَمَن شَرِبَ مِنْهُ فَلَيْسَ مِنِّي وَمَن لَّمْ يَطْعَمْهُ فَإِنَّهُ مِنِّي إِلَّا مَنِ اغْتَرَفَ غُرْفَةً بِيَدِهِ ۚ فَشَرِبُوا مِنْهُ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُ هُوَ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ قَالُوا لَا طَاقَةَ لَنَا الْيَوْمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ ۚ قَالَ الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو اللَّـهِ كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿٢٤٩﴾

249. Alipoondoka Twaaluwt na jeshi alisema: Hakika Allaah Atakujaribuni kwa mto. Hivyo basi atakayekunywa humo, hatokuwa pamoja nami, na ambaye hatoyaonja (hatoyagusa kabisa) hakika huyu yu pamoja nami, isipokuwa atakayeteka teko moja kwa mkono wake. Basi wakanywa kutoka humo isipokuwa wachache miongoni mwao. Alipouvuka yeye na wale walioamini pamoja naye, walisema: Leo hatuna nguvu kabisa kukabiliana na Jaaluwt na jeshi lake. Wakasema wale walio na yakini kwamba wao watakutana na Allaah: Makundi mangapi machache yameyashinda makundi mengi kwa Idhini ya Allaah? Na Allaah Yu pamoja na wenye subira.

 

 

وَلَمَّا بَرَزُوا لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ قَالُوا رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ﴿٢٥٠﴾

250.  Na walipokabiliana uso kwa uso na Jaaluwt na jeshi lake walisema (wakiomba): Rabb wetu! Tumiminie subira na Ithibitishe miguu yetu isimame imara na Tusaidie tuwashinde watu makafiri.

 

 

 فَهَزَمُوهُم بِإِذْنِ اللَّـهِ وَقَتَلَ دَاوُودُ جَالُوتَ وَآتَاهُ اللَّـهُ الْمُلْكَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَهُ مِمَّا يَشَاءُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّفَسَدَتِ الْأَرْضُ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ ذُو فَضْلٍ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٢٥١﴾

 251. Wakawashinda kwa Idhini ya Allaah na Daawuwd akamuua Jaaluwt, na Allaah Akampa ufalme na hikmah, na Akamfunza Aliyoyataka. Na lau Allaah Asingelikinga baadhi ya watu kwa wengine, basi ingelifisidika ardhi. Lakini Allaah Ni Mwenye Fadhila juu ya walimwengu.

 

 

تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٢٥٢﴾

252. Hizo ni Aayaat za Allaah Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Rusuli.

 

 

تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۘ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّـهُ ۖ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ ۚ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِن بَعْدِهِم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَلَـٰكِنِ اخْتَلَفُوا فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ ﴿٢٥٣﴾

253. Rusuli hao, Tumewafadhilisha baadhi yao juu ya wengine. Miongoni mwao kuna aliyesemeshwa na Allaah, na Akawapandisha baadhi yao vyeo. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwh[88] Al-Qudus (Jibriyl (عليه السلام. Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana waliokuwa baada yao, baada ya kuwajia hoja bayana. Lakini walikhitalifiana. Basi wapo miongoni mwao ambao waliamini na wengine ambao walikufuru. Na lau kuwa Allaah Angelitaka, wasingelipigana lakini Allaah Anafanya Atakavyo.

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ ۗ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٥٤﴾

254. Enyi walioamini! Toeni katika Tulivyokuruzukuni kabla haijafika Siku ambayo hakutokuweko mapatano humo wala urafiki wala uombezi. Na makafiri ndio madhalimu.

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

255. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Al-Hayyu (Aliye Hai daima) Al-Qayyuwm (Msimamia kila kitu).[89] Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya Idhini Yake?[90] Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu Ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy[91] Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye ‘Uluwa, Mwenye Taadhima[92],[93].

 

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٥٦﴾

256. Hapana kulazimisha katika Dini, kwani imekwishabainika kati ya uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaghuti[94] na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.[95]

 

 

 اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥٧﴾

257. Allaah Ni Rafiki Mlinzi wa wale walioamini, Anawatoa kutoka katika viza na kuwaingiza katika nuru. Na wale waliokufuru marafiki wao wandani na walinzi ni twaghuti, huwatoa kutoka katika nuru na kuwaingiza katika viza. Hao ni watu wa motoni wao humo watadumu.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِي حَاجَّ إِبْرَاهِيمَ فِي رَبِّهِ أَنْ آتَاهُ اللَّـهُ الْمُلْكَ إِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّيَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ ۖ قَالَ إِبْرَاهِيمُ فَإِنَّ اللَّـهَ يَأْتِي بِالشَّمْسِ مِنَ الْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ الْمَغْرِبِ فَبُهِتَ الَّذِي كَفَرَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥٨﴾

258. Je, hukumzingatia yule[96] ambaye alimuhoji Ibraahiym kuhusu Rabb wake kwa vile Allaah Alimpa ufalme aliposema Ibraahiym: Rabb wangu ni Yule Ambaye Anahuisha na Kufisha. Akasema: Mimi (pia) nahuisha na kufisha. Ibraahiym akasema: Hakika Allaah Analileta jua kutoka Mashariki basi wewe lilete kutoka Magharibi. Aliyekufuru akabaki kinywa wazi bila jibu, akataghayuri rangi. Na Allaah Haongoi watu madhalimu.

 

 

 

أَوْ كَالَّذِي مَرَّ عَلَىٰ قَرْيَةٍ وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحْيِي هَـٰذِهِ اللَّـهُ بَعْدَ مَوْتِهَا ۖ فَأَمَاتَهُ اللَّـهُ مِائَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ ۖ قَالَ كَمْ لَبِثْتَ ۖ قَالَ لَبِثْتُ يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۖ قَالَ بَل لَّبِثْتَ مِائَةَ عَامٍ فَانظُرْ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمْ يَتَسَنَّهْ ۖ وَانظُرْ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجْعَلَكَ آيَةً لِّلنَّاسِ ۖ وَانظُرْ إِلَى الْعِظَامِ كَيْفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكْسُوهَا لَحْمًا ۚ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ قَالَ أَعْلَمُ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٥٩﴾

259. Au kama yule[97] aliyepita katika kijiji kilichoporomoka kabisa juu ya mapaa yake na kuwa magofu akasema: Vipi Allaah Atakihuisha hiki (kijiji) baada ya kufa kwake? Allaah Akamfisha miaka mia, kisha Akamfufua. (Allaah) Akamuuliza: Umekaa muda gani? Akasema: Nimekaa siku moja au sehemu ya siku. Akasema: Bali umekaa miaka mia. Hebu kitazame chakula chako na kinywaji chako, havikuharibika. Halafu mtazame punda wako. Na ili Tukufanye wewe uwe ni Aayah (Ishara, Dalili) kwa watu (za Uwezo wa Allaah), basi itazame mifupa jinsi Tunavyoinyanyua, kisha Tunaivisha nyama. Yalipombainikia hayo alisema: Najua kwamba hakika Allaah Ni Muweza wa kila kitu.

 

 

 

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ أَرِنِي كَيْفَ تُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِن ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَـٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِي ۖ قَالَ فَخُذْ أَرْبَعَةً مِّنَ الطَّيْرِ فَصُرْهُنَّ إِلَيْكَ ثُمَّ اجْعَلْ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٍ مِّنْهُنَّ جُزْءًا ثُمَّ ادْعُهُنَّ يَأْتِينَكَ سَعْيًا ۚ وَاعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٦٠﴾ 

260. Na pindi aliposema Ibraahiym: Rabb wangu! Nionyeshe vipi Unahuisha wafu? (Allaah) Akasema: Je, kwani huamini? Akasema: Sivyo hivyo! Bali Naam (naamini)! Lakini ili moyo wangu utumainike. (Allaah) Akasema: Basi chukua ndege wanne wazoeshe kwako, (uwachinje), kisha weka juu ya kila jabali sehemu ya hao (ndege), kisha waite watakujia mbio (wakiumbika upya), na jua kwamba hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

مَّثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّائَةُ حَبَّةٍ ۗ وَاللَّـهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦١﴾ 

261. Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika Njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja ya mbegu iliyotoa mashuke saba, katika kila shuke kuna punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye, na Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote.

 

 

الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَا أَنفَقُوا مَنًّا وَلَا أَذًى ۙ لَّهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٦٢﴾

262. Wale wanaotoa mali zao katika Njia ya Allaah kisha hawafuatishii kwa waliyoyatoa masimbulizi wala udhia watapa ujira wao kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.  

 

 

قَوْلٌ مَّعْرُوفٌ وَمَغْفِرَةٌ خَيْرٌ مِّن صَدَقَةٍ يَتْبَعُهَا أَذًى ۗ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَلِيمٌ ﴿٢٦٣﴾

263. Kauli njema na msamaha ni bora kuliko swadaqa inayofuatiwa na udhia. Na Allaah Ni Mkwasi, Mvumilivu.

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾

264. Enyi walioamini! Msibatwilishe swadaqa zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake riyaa-a[98] (kujionyesha) kwa watu wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri.

 

 

 وَمَثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ وَتَثْبِيتًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِن لَّمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٦٥﴾

265. Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kutafuta Radhi za Allaah na kujithibitisha nafsi zao, ni kama mfano wa bustani iliyoko pahala paliponyanyuka, ikapigwa na mvua kubwa, kisha ikatoa mazao yake maradufu, na hata kama haikupigwa na mvua kubwa basi mvua ndogo huitosheleza. Na Allaah Ni Mwenye Kuona yale myatendayo.

 

 

 أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَن تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ لَهُ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَأَصَابَهُ الْكِبَرُ وَلَهُ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفَاءُ فَأَصَابَهَا إِعْصَارٌ فِيهِ نَارٌ فَاحْتَرَقَتْ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢٦٦﴾

266. Je! Anapenda mmoja wenu awe ana bustani ya mitende na mizabibu ipitayo chini yake mito, anayo humo kila aina ya mazao, ukamfikia uzee, naye ana kizazi dhaifu, kisha ikapigwa na kimbunga cha moto kikaiteketeza? Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (Ishara na Mazingatio) kwenu mpate kutafakari.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٢٦٧﴾

267. Enyi walioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma na katika ambavyo Tumekutoleeni kutoka katika ardhi. Na wala msikusudie kutoa vibaya humo, mkavitoa ilhali nyinyi wenyewe msingevipokea isipokuwa kwa kuvifumbia macho. Na jueni kwamba hakika Allaah Ni Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa.[99]

 

 

 الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاءِ ۖ وَاللَّـهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦٨﴾

268. Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni machafu, (ubakhili), na Allaah Anakuahidini Maghfirah kutoka Kwake na Fadhila. Na Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote.

 

 

يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٦٩﴾

269. Humpa hikmah Amtakaye. Na anayepewa hikmah basi kwa yakini huwa amepewa kheri nyingi. Lakini hawakumbuki isipokuwa wenye akili.

 

 

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ ۗ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿٢٧٠﴾

270. Na chochote mtoacho au mkiwekacho nadhiri, basi hakika Allaah Anakijua. Na madhalimu hawana wa kuwanusuru.

 

 

 إِن تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ ۖ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّئَاتِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٧١﴾

 271. Mkidhihirisha swadaqa basi ni vizuri hivyo, na mkizificha na kuwapa mafakiri, basi hilo ni kheri kwenu. Na Atakufutieni katika maovu yenu. Na Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾

272. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwahidi, lakini Allaah Humhidi Amtakaye. Na chochote cha kheri mtoacho basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika kheri mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa.[100]

 

 

 لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِي الْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢٧٣﴾

273. (Swadaqa ni) kwa ajili ya mafakiri waliozuilika katika Njia ya Allaah, hawawezi kwenda huku na kule katika ardhi (kutafuta rizki). Asiyewajua huwadhania kuwa ni matajiri kutokana na staha ya kujizua kwao, unawatambua kwa alama zao, hawaombi watu kwa ung’ang’anizi. Na chochote mtoacho katika kheri, basi hakika Allaah Anakijua vyema.

 

 

الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ سِرًّا وَعَلَانِيَةً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٢٧٤﴾

274. Wale wanaotoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri, watapata ujira wao kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.

 

 

 

الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا ۗ وَأَحَلَّ اللَّـهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا ۚ فَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَنْ عَادَ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧٥﴾

275. Wale wanaokula riba hawatosimama (Siku ya Qiyaamah) ila kama anavyosimama aliyezugwa na shaytwaan kwa kuguswa na kupatwa. Hivyo kwa sababu wao wamesema: Hakika biashara ni kama riba. Na Allaah Amehalalisha biashara na Ameharamisha riba. Na atakayefikiwa na mawaidha kutoka kwa Rabb wake akakoma, basi yake ni yaliyokwishapita, na hukumu yake iko kwa Allaah. Na atakayerudia basi hao ni watu wa motoni, wao humo watadumu.

 

 

يَمْحَقُ اللَّـهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ ﴿٢٧٦﴾

276. Allaah Huifuta baraka (mali ya) riba na Huzibariki swadaqa. Na Allaah Hampendi kila aliye mwingi wa kukufuru apapiae madhambi.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٢٧٧﴾

 277. Hakika wale walioamini na wakatenda mema na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, (hao) watapata ujira wao kutoka kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿٢٧٨﴾

 278. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika riba[101] ikiwa nyinyi ni Waumini.

 

 

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٩﴾

279. Na msipofanya, basi tangazeni vita[102] kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake. Na mkitubu, mtapata rasilimali zenu, msidhulumu na wala msidhulumiwe.

 

 

 وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ ۚ وَأَن تَصَدَّقُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٨٠﴾

280. Na ikiwa (mdaiwa) ni mwenye hali ngumu, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkifanya deni kuwa ni swadaqa, basi ni kheri kwenu mkiwa mnajua.

 

 

 وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٨١﴾

281. Na iogopeni Siku mtakayorejeshwa ndani yake kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma, nao hawatodhulumiwa.[103]

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ ۚ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ ۚ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَن يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّـهُ ۚ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا ۚ فَإِن كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ ۚ وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ ۚ وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا ۚ وَلَا تَسْأَمُوا أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَىٰ أَجَلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَىٰ أَلَّا تَرْتَابُوا ۖ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا ۗ وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ ۚ وَلَا يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ ۚ وَإِن تَفْعَلُوا فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّـهُ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٨٢﴾ 

282. Enyi walioamini! Mtakapokopeshana deni mpaka muda maalumu uliopangwa, liandikeni. Na aandike baina yenu mwandishi kwa uadilifu. Na wala asikatae mwandishi kuandika kama Allaah Alivyomfunza. Na aandikishe kwa imla yule ambaye ana haki (mdai) na amuogope Allaah, Rabb wake, na wala asipunguze humo kitu chochote. Na ikiwa yule ambaye ana haki amepumbaa kiakili au mnyonge, au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe msimamizi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili wanaume miongoni mwenu. Na ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamme mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi, ili kama mmoja wao hao wanawake wawili akikosea (akasahau), basi mmoja wao atamkumbusha mwengine. Na mashahidi wasikatae watapoitwa. Na wala msichukie kuliandika (deni) dogo au kubwa mpaka muda wake. Hivyo kwenu ndiyo uadilifu upasavyo mbele ya Allaah na ndio unyoofu zaidi kwa Ushahidi, na ni karibu zaidi ili msiwe na shaka, isipokuwa itakapokuwa biashara taslimu mnayoiendesha baina yenu, basi si dhambi kwenu msipoiandika. Lakini shuhudisheni mnapouziana. Wala asidhuriwe mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hivyo, basi hakika huo ni ufasiki kwenu. Na mcheni Allaah, na Allaah Anakufunzeni, na Allaah ni Mjuzi wa kila kitu. 

 

 

وَإِن كُنتُمْ عَلَىٰ سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَّقْبُوضَةٌ ۖ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ ۗ وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ ۚ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٢٨٣﴾

283. Na mkiwa safarini na hamkumpata mwandishi, (mdai) akabidhiwe rahani. Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake, na amche Allaah, Rabb wake, wala msifiche ushahidi, na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allaah Ni Mjuzi wa mnayoyatenda.

 

 

لِّلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَإِن تُبْدُوا مَا فِي أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ اللَّـهُ ۖ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٨٤﴾

 284. Ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha, Allaah Atakuhesabuni kwayo. Humghufuria Amtakaye na Humuadhibu Amtakaye. Na Allaah Ni Mweza wa kila kitu.[104]

 

 

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾

 285. Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rusuli Wake. (Nao husema): Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rusuli Wake. Na wakasema: Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu, na Kwako ndio mahali pa kuishia.[105]

 

 

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾  

286. Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata malipo ya (mema) iliyoyachuma, na itabeba (matokeo ya maovu) iliyojichumia. Rabb wetu! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabb wetu! Usitubebeshe mzigo kama Uliowabebesha waliokuwa kabla yetu. Rabb wetu! Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe Ni Mawlaa[106] wetu, basi Tusaidie tuwashinde watu makafiri.[107]

 

[1]  الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):

 

Herufi hizi zinajulikana kuwa ni Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah. Herufi hizo zimetokea katika mwanzoni mwa baadhi ya Suwrah. Na idadi ya Suwrah hizo ni ishirini na tisa katika Qur-aan. Wafasiri wa Qur-aan wamekhitilafiana kuhusu maana zake, wakataja maana mbili tatu ila wote wamekubaliana kuwa rai iliyo ya nguvu na sahihi kabisa ni: Maana zake hazijulikani kwa sababu ni katika ilimu ya ghaibu ambayo hakuna ajuaye isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rai hiyo imetajwa na Abu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan, ‘Aliy na Ibn Mas‘uwd (رضي الله عنهم). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

[2] “Hiki Ni Kitabu” Badala Ya “Hicho Ni Kitabu”

 

Tarjama hii na nyenginezo za kuaminika zimefasiri: “Hiki ni Kitabu” badala ya “Hicho ni Kitabu” ilhali katika Aayah limetajwa neno ذَٰلِكَ   ambalo katika uhalisia wa lugha ya Kiarabu ni: Ismul-Ishaarah lil-ba’iyd (Kiashirio Cha Mbali). Hivyo ni kwa sababu: 

 

(i) Kitabu Hicho ذَٰلِكَ الْكِتَابُ  kimekusudiwa Kitabu kilichokuweko mbinguni katika Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):

إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ ﴿٧٧﴾ فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ ﴿٧٨﴾

“Hakika hii bila shaka ni Qur-aan tukufu. Katika Kitabu kilichohifadhiwa.” [Al-Waaqi’ah (56: 77-78)]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٤﴾

“Na hakika hii (Qur-aan) iko Kwetu katika Mama wa Kitabu, Imetukuka kwa hakika, imejaa Hikmah.” [Az-Zukhruf (43:4)]

 

(ii) ذَٰلِكَ  Ambayo ni Ismul-Ishaarah lil-ba’iyd (Kiashirio Cha Mbali) hutumika pia kwa ajili ya kuadhimisha (kukitukuza) kitu.  Na kiashirio cha mbali kinginecho ni  تلك kama ilivyotajwa katika mwanzo wa Aayah kadhaa kama Yuwnus (10:1), Yuwsuf (12:1), Al-Hijr (15:1), An-Naml (27:1), Al-Qaswasw (28:2), Luqmaan (31:2) na nyenginezo.

 

[3] Hudaa, Hidaaya Ni Aina Mbili:

 

(i) Hidaayatut-Tawfiyq (Hidaaya ya tawfiyq): Ni imaan ambayo mahali pake ni moyoni na ni Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee Awezaye kuiweka katika nyoyo za waja. Dalili ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) Alipomwambia Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye alipendelea kumuongoza ammi yake Abuu Twaalib katika Uislamu alipokuwa anakaribia kuaga dunia. Allaah Akasema:

 

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾

“Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye, lakini Allaah Humhidi Amtakaye, Naye Anawajua zaidi wenye kuongoka.” [Al-Qaswasw (28:56)]

 

(ii) Hidaayatul-Irshaad (Hidaaya ya kuongoza): Ni kuelekeza, kubainisha, kuongoza njia, kumwongoza mtu katika Uislamu kama vile Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomwongoza ammi yake Abuu Twaalib aingie Uislamu akamtaka atamke Shahaada (laa ilaaha illa-Allaah) lakini akakataa ikawa hakupata Hidaaya ya tawfiyq.  Hali kadhaalika Hidaaya hii ya irshaad ni kama vile kumwongoza mtu kutekeleza mema, kuelekea katika njia iliyonyooka n.k. Na hii ni sawa na Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ ﴿١٠﴾

“Na Tukambainishia njia mbili (ya haki na upotofu)?” [Al-Balad (90:10)]

 

وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ

“Na ama kina Thamuwd, wao Tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko hidaaya.” [Fusw-Sswilat (41:17)]

 

إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا﴿٣﴾

“Hakika Sisi Tumemuongoza njia; ima (awe) ni mwenye kushukuru au mwingi wa kukufuru.” [Al-Insaan (76:3)]

 

وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾

Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka.” [Ash-Shuwraa (42:52)]

 

[4]  Maana Ya Taqwa:

 

Taqwa ni mojawapo ya maneno ya kipekee katika lugha ya Kiarabu ambayo hayawezi kutafsiriwa kwa neno moja au mawili. Kwa hiyo maana yake kilugha ni kinga, kujilinda, himaya, hifadhi, kutahadhari  na kukhofu. 

 

Katika istilahi, Salaf wametaja mengi kuhusu taqwa, miongoni mwayo ni kumwabudu Allaah ipasavyo, kutekeleza yaliyoamrishwa na Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), kujiepusha makatazo Yao  na kubakia katika mipaka ya sharia ya Dini, kumkhofu Allaah na kukhofu Adhabu na Ghadhabu Zake, kuwa na raghba (utashi) na kutaraji Thawabu Zake, kumuadhimisha Allaah (سبحانه وتعالى)  na kumpenda mapenzi ya kikweli  pamoja  na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

Taqwa haihitajii kuhakikishwa mtu kuwa mahali fulani au wakati fulani, bali taqwa ya hakika  ni pale mtu anapokua yuko peke yake, akajiepusha na yaliyo haramu japokuwa hakuna mtu anayemuona. Na ndipo aliposema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa “Taqwa ipo hapa!” Akiashiria kwenye kifua chake palipo na moyo na kusema mara tatu.

 

Umar (رضي الله عنه)  alimuuliza Ubayy bin Ka’b (رضي الله عنه): “Taqwa ni nini?” Akajibu:    “Ee Amiri Wa Waumini! Je, hukuwahi kupita njia yenye miiba?” Akasema: “Naam!” Akasema: “Ulifanya nini?”   Akasema: “Niliinua miguu yangu huku nikiitazama  na kuinua  mguu mmoja na mwingine, nikikhofia mwiba usije kunichoma.” ‘Ubay akamwambia: “Hiyo ndiyo taqwa!”

 

‘Aliy bin Abi Twaalib (رضي الله عنه)  amesema: “Taqwa ni kumkhofu Al-Jaliyl (Allaah) na kufanyia kazi Tanziyl (Qur-aan) na kuridhika na kidogo, na kujiandaa na Siku ya rahiyl (kuondoka duniani, kufariki).”

 

[5] Maana Ya Ghaibu:

 

Ghaibu ni kila ambayo yametambulishwa kwetu na Allaah (سبحانه وتعالى)  na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم). Ni mambo ambayo hayaonekani kwetu wala akili haidiriki utambuzi wake au kutambua uhalisi wake.  Mifano ya baadhi ya ghaibu ni kutomuona Allaah (سبحانه وتعالى) hapa duniani lakini tunamuamini. Pia kumuamini na kumpenda Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ingawa hatukumuona. Pia kuamini kwamba walikuweko Swahaba zake (رضي الله عنهم) na kuwapenda wote ingawa hatukuwaona, na kuamini yote yaliyokuja katika Siyrah ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hali kadhalika kuamini Manabii waliotangulia, kuamini Malaika na mambo yote mengineyo ya ghaibu yakiwemo alama za Qiyaamah, adhabu za kaburi na neema zake, Hayaatul-Barzakh (kipindi baina ya mtu kufariki hadi Siku ya Qiyaamah), Al-Ba’ath (kufufuliwa), Al-Hashr (mkusanyiko wa viumbe Siku ya Qiyaamah katika ardhi ya mkusanyiko), Al-Hisaab (kuhesabiwa matendo), Asw-Swiraatw (daraja watakalovuka watu Siku ya Qiyaamah ima kuingia Peponi au motoni), Miyzaan (Mizani itakayopima amali za watu), Jannah (Pepo) na An-Naar (moto), na mambo mengineyo ya ghaibu.  Na ghaibu ni sifa ambayo anaimiliki Muumini wa kweli na mwenye taqwa kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah hiyo tukufu ambayo Ameitanguliza mwanzo kabisa katika Qur-aan kwenye Suwrah hii ya pili, kutokana na umuhimu wake.

Rejea pia Al-An’aam (6:59), Luqmaan (31:34), An-Naml (27:65).

 

[6] Maana Ya Kusimamisha Swalaah: 

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Ni kuswali kwa kuzingatia nguzo na sharti zake.”  Adhw-Dhwahaak amesema kuwa Ibn ‘Abbaas alisema: “Iqaamat Asw-Swalaah maana yake ni kukamilisha rukuu, sujuwd, kusoma Qur-aan, kuwa na khushuu (unyenyekevu), na kuhudhurisha moyo katika Swalaah.” Qataadah alisema: “Iqaamat Asw-Swalaah maana yake ni kuchunga wakati, wudhuu, rukuu na sujuwd za Swalaah.” Muqaatil bin Hayyaan alisema: “Iqaamat Asw-Swalaah ina maana: Kuchunga wakati, kujitwaharisha kwa ajili yake, kukamilisha rukuu, sujuwd na kusoma Qur-aan, tashahhud na kumwombea Rehma Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hiyo ndiyo Iqaamat Asw-Swalaah.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr] Rejea An-Nisaa (4:108), Al-Muuminuwn (23:1).

 

[7]  Nyoyo Zenye Maradhi:

 

Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali kuhusu nyoyo zenye maradhi.

 

Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo kuhusu maana ya moyo uliopofuka.

Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.

 

 

[8] Allaah (سبحانه وتعالى) Hana Sifa Mbaya Isipokuwa Anarudisha Ubaya (Muqaabalah): Rejea Aal-‘Imraan (3:54).

 

[9] Changamoto Ya Kuleta Mfano Wa Qur-aan Wala Hakuna Awezaye Kamwe!

 

Rejea Yuwnus (10:38), Al-Israa (17:88), Huwd (11:13-14), Atw-Twuur (52:33-34), Rejea pia Al-An’aam (6:93) ambako kumetajwa waongo waliodai Unabii.

 

[10] Mifano Ya Kipekee Ya Allaah: Rejea Al-A’raaf (7:40).

 

[12] Kuunga Aliyoyaamrisha Allaah: Rejea Ar-Ra’d (13:21).

 

[13] Mauti Ya Mara Mbili Na Uhai Wa Mara Mbili

 

Mlikuwa wafu (kabla ya kuumbwa): Ni mauti ya kwanza.

 

Akakuhuisheni (kupulizwa roho tumboni mwa mama na kuzaliwa na kuishi uhai wa duniani): Ni uhai wa kwanza.

 

Kisha Atakufisheni (kukufisheni baada ya kumalizika muda wa kuishi duniani [kufariki dunia]): Ni mauti ya pili.

 

Kisha Atakuhuisheni (kurudishwa kuwa hai tena pindi mtakapofufuliwa kutoka makaburini Siku ya Qiyaamah): Ni uhai wa pili. (Na huku ndio kurudishwa Kwake Allaah (سبحانه وتعالى) ili kuhesabiwa na kulipwa mema na maovu).

 

Rejea Suwrah Ghaafir (40:11) kwenye Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) kama hii:

 

[14] اسْتَوَى إِلَى السَّمَاءِ" Amezikusudia (Kuziumba Mbingu):

 

Kwa hakika maana ya “Istawaa” ina unyeti katika kuielezea. Na katika Tarjama hii, maana ya “Istawaa” imeelezewa kwa bayana, maana zake zinazotofautiana, kwa mujibu wa maelezo ya ‘Ulamaa, katika Suwrah mbili: Katika Suwrah hii Al-Baqarah (2:29) na Al-A’raaf (7:54).

 

Hivyo basi, maana ya   "اسْتَوَى" katika Aayah hii ya Suwrat Al-Baqarah (2:29) na Suwrat Fusswilat (41:11), kwa mujibu wa kauli za ‘Ulamaa wa Ahlu As Sunnah wal Jama’ah na Mufassiruna, wanasema ina maana ya "قَصَدَ", yaani Amekusudia. Na ikiwa "اسْتَوَى إِلَى السَّمَاءِ" inakuwa kwa maana ya: قَصَدَ إِلَى خَلْقِهَا  yaani Amekusudia kuziumba. Kwa hiyo maana munaasib katika Suuwrah hizi mbili ni: Kisha Akazikusudia mbingu (Kuziumba).” 

 

[15]  Khalifa:

 

Katika Aayah hiyo imekusudiwa watu wanaokuja baada ya wengine, au wanaofuatana karne kwa karne, vizazi baada ya vizazi. Ama maana nyengine ya khalifa, ni Khalifa Walioongoka wanne wa Waumini baada ya kufariki (صلى الله عليه وآله وسلم) ambao walikuwa ni Abu Bakr Asw-Swiddiyq, ‘Umar bin Al-Khattwaab, ‘Uthmaan bin ‘Affaan na ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنهم).

 

[16]  Maasi Ya Kwanza Ya Kumuasi Allaah (سبحانه وتعالى):

 

Ibn ‘Atwiyyah amesema: Jambo la kwanza la kumuasi Allaah, lilikuwa ni uhasidi, nalo lilidhihirika kutoka kwa Ibliys. [Al-Muharrar Al-Wajiyz (3/469)]  Na sababu alizozitaja Ibliys za kukataa kwake kumsujudia Aadam ni kwamba, yeye alijiona ni mbora kuliko Aadam, hivyo akadhihirisha kibri. Rejea Al-A’raaf (7:11-12), Al-Hijr (15:28-33), Al-Israa (17:61-62), Swaad (38:71-76).

 

[18] Ummah Bora Kabisa Ni Ummah Wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم): 

 

Makusudio ya kufadhilishwa kwa Baniy Israaiyl juu ya walimwengu wote, ni kufadhilishwa kwao juu ya walimwengu wa zama zao, kwani inafahamika kuwa ummah ambao ni bora kuliko ummah zote ni ummah wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa dalili ya Kauli ya Allaah (تعالى):

 

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾

Mmekuwa ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Watu wa Kitabu ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wako wanaoamini na wengi wao ni mafasiki.” [Aal-‘Imraan (3:110)]

 

[19] Maana ya Al-Furqaan: Pambanuo: Rejea Al-Furqaan (25:1).

 

[20]  Al-Manna Na As-Salwaa:

 

Wafasiri wamekhitilafiana juu ya makusudio ya al-manna na as-salwaa. Lakini bila shaka ni aina ya chakula kama ilivyonukuliwa kutoka Tafsiyr ya Imaam Ibn Kathiyr kwamba: Al-manna ilikuwa ikiteremka kutoka mitini na walikuwa wakila kadiri walivyotaka kula. Na Qataadah amesema: “Al-manna ambayo ni nyeupe kuliko maziwa na tamu mno kulikoni asali ilikuwa ikiwanyeshea (kutoka mbinguni) kama vile barafu inavyoanguka kuanzia alfajiri hadi jua kuchomoza. Mmoja wao aliikusanya ya kutosha kwa ajili ya siku ile tu kwani ingebakia zaidi ya hivyo ingeharibika.” Imesimuliwa na Sa’iyd bin Zayd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Al-kama-ah (uyoga) ni aina ya manna na maji yake ni shifaa (ponyo) ya macho.”  [Al-Bukhaariy (4478)]

 

Ama as-salwaa, Ibn ‘Abbaas  (رضي الله عنهما)  amesema: As-salwaa ni aina ya ndege anayefanana na kware. Ama ‘Ikrimah na Qataadah  (رضي الله عنهما) wamesema: As-salwaa ni ndege wa Jannah (Peponi) anayefanana au ambaye ni kiasi cha ukubwa wa shomoro. [Tafisyr Ibn Kathiyr]

 

[21] Hittwah: Tuondolee Uzito Wa Madhambi: Mayahudi Kubadilisha Maana Ya Neno:

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wana wa Israaiyl waliamrishwa kuingia kupitia mlangoni huku wameinama na wanyenyekee na waseme ‘Hittwah’ (Tuondolee uzito wa madhambi). Lakini waliingia kinyumenyume wakipotosha maneno wakisema: Habbat fiy sha’arah (mbegu katika unywele).” [Al-Bukhaariy]

 

Rejea pia Al-Baqarah (2:104).

 

[22] Wasabai:

 

Wasabai ni nani, nini imaan na ‘aqiydah (itikadi) zao. Rejea Al-Hajj (22:17).

 

Nukuu nyengine zimetaja: “Wasabai ni watu waliobakia katika maumbile yao na maadili ya asili (au asili ya Uislamu), hawana dini maalumu wanayoifuata.” [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

“Hukmu hii inawahusu Watu wa Kitabu kwa sababu lilokuwa sahihi ni kwamba wao ni katika kundi la Manaswara.” [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[23] As-Sabt:

 

Maana yake asili ni mapumziko na hivyo Siku hiyo yao Mayahudi ya mapumziko (Jumamosi), waliwekewa sharia wasivue samaki. Lakini walikhalifu amri kwa kutumia njama na ujanja wakavua samaki kumuasi Allaah. Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaghadhibikia na kuwageuza manyani. Rejea An-Nisaa (4:47) na Al-A’raaf (7:163-166).

 

[24] Kisa Cha Al-Baqarah (Ng’ombe) Na Ndio Jina La Suwrah Hii:

 

Kisa chake kinaanzia Aayah hii ya (2:67) hadi Aayah (2:76). Kulikuweko na mtu aliyepooza (asiyekuwa wa kawaida) na alikuwa na mali nyingi. Hakuwa na mrithi isipokuwa jamaa yake mmoja. Mrithi huyo alimuua huyo bwana ili apate kurithi mali. Kisha akachukua mwili wake akautupa nje na nyumba ya mtu mmoja kumsingizia kuwa kamuua. Siku ya pili akadai kulipiza kisasi, pakatokea mzozano na watu walikaribia kuuana. Mwishowe wakasema “Mnaye Rasuli wa Allaah mwendeeni.” Walipomwendea Nabiy Muwsaa akawaambia:

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا بَقَرَةً ۖ

“Hakika Allaah Anakuamuruni mchinje ng’ombe.”

 

Wakafanya ugumu wa kutii amri hii kwa kubishana na wakazidi kufanyiwa ugumu kumtafuta ng’ombe mwenye sifa fulani. Wasingebishana basi ingewatosheleza kuchinja ng’ombe yoyote yule.  Ng’ombe mwenye sifa hizo akapatikana kwa mtu mmoja pekee naye akataka alipwe dhahabu iliyojaza ngozi ya ng’ombe. Wakamlipa na wakamchinja na kisha wakachukua sehemu ya ng’ombe kumpigia huyo mtu aliyeuliwa, akazindukana na wakamuuliza nani aliyemuua? Akamuashiria mrithi wake, basi hakuruhusiwa tena kumrithi. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

[25] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

[26] Maana Za Ruwh Katika Qur-aan:

 

Rejea An-Nahl (16:2).

 

Na Uthibitisho Kuwa Jibriyl ( (عليه السلام  Ndiye Ruwh Al-Qudus:

 

Amesimulia Ibn Mas‘uwd  (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ruwh Al-Qudus alinifahamisha kuwa hakuna roho itakayokufa mpaka imalizike rizki yake na muda wake, kwa hiyo mcheni Allaah na mtakeni rizki katika hali iliyo bora.” [As-Sunnah: (14/304), ameisahihisha Al-Albaaniy katika Mushkilat Al-Faqar (15), Swahiyh Al-Jaami’ (2085). Hadiyth kutoka Abuu Umaamah Al-Baahiliy (رضي الله عنه)]

 

[28] Maana Ya Baghyun/Baghaa Katika Qur-aan:

 

Rejea Ash-Shuwraa (42:14) kupata maana zake mbalimbali.

 

[30] Malaika Jibriyl Na Miykaail:

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapoamka usiku akisoma duaa ambayo  akiwataja Malaika hao wawili pamoja na Malaika Israafiyl; Hadiyth imethibiti:

 

Amesimulia Abuu Salamah bin ‘Abdir-Rahmaan bin ‘Awf (رضي الله عنه): Nilimuuliza ‘Aaishah (رضي الله عنها) : Je, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)   alikuwa akifungulia Swalaah yake kwa kitu gani alipoamka usiku? Akasema: alikuwa anapoamka usiku anafungulia Swalaah yake kwa:

 

اللَّهُمَّ رَبَّ جَبْرَائِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ. فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ. عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ. أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ. اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيم

Ee Allaah Rabb wa Jibraaiyl   na Miykaail na Israafiyl, Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Wewe Utahukumu baina ya waja Wako katika ambayo walikuwa wakikhitilafiana nayo. Niongoze mimi kwenye haki katika yale ambayo (watu) wamekhitilafiana kwa idhini Yako.  Hakika Wewe unamuongoza Umtakae kwenye njia ilionyoka.” [Muslim (1/534)]

 

Rejea Az-Zukhruf (43:77) kwenye maelezo bayana kuhusu baadhi ya Malaika; Majina yao, kazi zao, na idadi zao na faida nyenginezo.

 

[31] Haaruwt na Maaruwt:

 

Haaruwt na Maaruwt ni Malaika wawili katika Malaika wa mbinguni, ambao Allaah (عزّ وجلّ) Aliwateremsha ardhini kuwa ni fitnah (jaribio na mtihani) kwa watu.  Walikuwa wakiwafundisha watu sihri (uchawi) kwa amri ya Allaah (عزّ وجلّ).  Lakini kila walipotaka kuwafundisha  watu sihri, waliwatahadharisha kwanza wakiwaambia:

 

إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ    

“Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru.”

 

[32] Maana Ya: رَاعِنَا Na انظُرْنَا Na Tabia Ya Mayahudi Kubadilisha Maneno:

 

Swahaba  (رضي الله عنهم) walikuwa wakimwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Raa’inaa! Yaani: “Tega sikio lako utusikilize na utufahamu.” Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwakataza usemi huo kwa sababu usemi huo wa “raa’inaa” ulitumiwa na Mayahudi kukusudia neno ovu na ufidhuli kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Walipokuwa wakimtembelea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), walijaribu kutoa chuki zao kwa kutumia maneno ya kutatanisha katika maamkizi na maongezi yao. Walikuwa wakitumia maneno yenye maana mbili; moja yenye maana nzuri na nyengine ya tusi au ufidhuli. Na walipotamka maneno yafaayo walinong’ona maneno maovu. Walijifanya kudumisha adabu na heshima na huku wakiwa hawaachi njia yoyote ya kumtusi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Na kila walipotaka kumalizia chochote walichotaka kusema, walitumia usemi wa raa'inaa, ambao ulimaanisha “tafadhali tukubalie” au “tafadhali tutegee sikio utusikilize.”

 

Iliwezekana kwa usemi huo kutumiwa kwa maana tofauti kabisa katika lugha yao Mayahudi kwa mfano, kuna neno linalofanana nalo ambalo linamaanisha: “Sikiliza na uwe kiziwi!” Pia katika lugha hiyo hiyo ina maana ya ufidhuli, jahili, mjinga. Usemi huo pia ulitumiwa pindi mtu alitaka kusema: “Ukinisikiliza nitakusikiliza.” Na ilipotamkwa kwa kupindisha ulimi kidogo iligeuka kuwa “raa'inaa”, ikimaanisha “mchungaji wetu.” Ni kwa sababu ya uwezekano wa neno hilo kutumika katika maana hizi tofauti ndipo Waislamu wakaamriwa kuliepuka na badala yake watumie usemi ulionyooka na bayana kabisa usio na utata nao ni: انظُرْنَا “undhwurnaa,” yenye maana: “Tafadhali tuangalie kwa makini, au tafadhali tuangalie na tupe muhula tukufuate (unayotuambia au kutuamrisha).” Rejea pia An-Nisaa (4:46), Al-Baqarah (2:58).

 

[33] Hukmu Ya An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa):

 

Rejea pia An-Nahl (16:101).

 

Somo hili lina maelezo mapana na yanapatikana mtandaoni mwa Alhidaaya.com. Lakini kifupi ni: An-Naasikh ni Aayah Inayofuta. Al-Mansuwkh ni Aayah inayofutwa. Na katika Sunnah pia kuna Hadiyth inayofuta na inayofutwa, mfano hukmu ya ndoa ya mut’ah kuwa kwanza iliruhusika kisha ikafutwa ikaja haramisho lake. Rejea An-Nisaa (4:23). Pia hukmu ya kuzuru makaburi ilikuja kwanza makatazo ya kuzuru kisha ikaja ruhusa ya kuzuru kwa kauli yake Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):  “Nilikuwa nimewakataza kuzuru makaburi, sasa zuruni kwani hilo linawakumbusha nyinyi Aakhirah [Muslim na wengineo]

 

[35] Aqiydah Sahihi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Ni Kuthibisha Sifa Za Allaah.

 

Aayah tukufu imetaja Nafsi ya Allaah (سبحانه وتعالى). Na ‘Aqiydah sahihi ni kuithibitisha hivyo hivyo bila ya kuipa maana nyenginezo; Rejea Huwd (11:47) kwenye maelezo bayana.

 

[37] Kumsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwa Ana Mwana: 

 

Rejea An-Nisaa (4:171), Maryam (19:30-36), (At-Tawbah (9:30).

 

[38]  Maana Ya Neno Kun!

 

Ni neno Analotumia Allaah (سبحانه وتعالى) pindi Akitaka kufanya au kuamrisha jambo basi huliambia Kun! (Kuwa!) nalo hapo hapo jambo hilo huwa. Mfano katika Miujiza Yake ya kumuumba Nabiy ‘Aadam  (عليه السّلام)kwa udongo. Au katika kumfanya Maryam ashike mimba na amzae Nabiy ‘Iysaa  (عليه السّلام) bila ya baba.  Au Anapotaka kutoa Amri Yake yoyote ile basi hakuna jambo ambalo Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) linamshinda bali Husema tu Kun! (Kuwa!) na hapo hapo jambo huwa!  

 

[39] Maana Ya Kuisoma Qur-aan Ipasavyo Na Kuipa Haki Yake:

 

Ibn Mas‘uwd (رضي الله عنه) amesema maana yake ni: “Anahalalisha Aliyohalalisha Allaah, na Anaharamisha Aliyoyaharamisha Allaah, na anasoma kama Alivyoteremsha Allaah, na wala hapotoshi maneno sehemu zake, na wala hafanyii taawiyl lolote humo isiyokuwa taawiyl yake.” (Taawiyl: kukwepesha maana yake ya kihakika kwa kuipa maana ndogo au tofauti, ishara ambayo ni tofauti na maana ya juu, ni kukanusha maana).

 

Na Hudhayfah bin Al-Yamaan amehadithia kuhusu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba alipokuwa akiswali, pale anapopita Aayah ya Rehma aliomba Rehma, anapopita Aayah ya adhabu anajikinga nayo, anapopita Aayah ya kumsabihi Allaah anamsabihi (kumtukuza). [Swahiyh Ibn Maajah (1119)]

 

Na Al-Hasan Al-Baswriy amesema: “Wanaifanyia kazi sharia (hukmu) zake na wanaamini mutashaabih zake (mutashaabih: zilizofanana) na wanapeleka yanayowatatiza kufahamu kwa ‘Ulamaa wake.”

 

Pia, baadhi ya ‘Ulamaa wamesema kuwa: Ni kuisoma kwa hukmu zake za tajwiyd, kufahamu maana yake, kuyafanyia kazi maamrisho yake, kujiepusha na makatazo yake, kujifundisha na kuifundisha. Hali kadhaalika, kusabbih kila panapotajwa Tasbiyh, kumtukuza Allaah (عزّ وجلّ), kuomba rehma, kuomba maghfirah, kuomba kuingizwa Jannah (Peponi) na kuomba kinga ya moto kila panapotajwa moto.

 

[40] Imaam (Kiongozi). Neno La أُمَّةً Katika Qur-aan Lina Maana Kadhaa: Rejea An-Nahl (16:120) kwenye maana zake.

 

[41] Maqaam Ibraahiym: Ni jiwe ambalo Nabiy Ibraahiym (عَلَيْهِ السَّلاَمُ)  alisimama juu yake wakati wa ujenzi wa Al-Ka’bah.

 

[42] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

125-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 125: وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى

 

[43] Kujengwa Al-Ka’bah Na Duaa Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) Ukatoka Ummah Wa Mwisho Wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

Aayaat hizi kuanzia (127-129) zinatuthibitishia kuwa Nabiy Ibraahiym na mwanawe Nabiy Ismaa’iyl (عليهما السّلام) ndio walionyanyua misingi ya Al-Ka’bah na kuijenga. Wakaomba duaa wakati wa shughuli hiyo ya ujenzi Allaah Awataqabalie kazi yao hiyo, atokee Nabiy kuwaongoza watu katika Uislamu kutoka katika kizazi cha Nabiy Ismaa’iyl (عليه السّلام). Na katika kizazi hicho ndipo alipotoka Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa ni Nabiy wa Mwisho na ujumbe wake ni ujumbe wa mwisho kabisa. Nao ndio umekusudiwa kwa ummah huu wetu wa Kiislamu na Kitabu cha mwisho Al-Qur-aan.  Rejea Al-An’aam (6:92), Ibraahiym (14:35-41).

 

[44] Swalihina Na Tofauti Yao Na Manabii, Swiddiyqiyna, Shuhadaa Na Swahaba (رضي الله عنهم):

 

Rejea An-Nisaa (4:69) kwenye maelezo bayana.

 

[45] Dini Ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) Ni Dini Ya Kiislamu: Rejea Aal-‘Imraan (3:67).

 

[46] Al-Asbaatw:

 

Ni makabila kumi na mbili ya wana wa Ya’aquwb ((عليه السلام  waliyotokea Manabii.

 

[47] Maana Ya Swibghah Ya Allaah (عزّ وجلّ):

 

Swibghah kilugha maana yake ni rangi au kupaka rangi. Ama makusudio ya maana yake katika Aayah hii tukufu ni Dini ya Allaah. Wamesema hivyo Ibn ‘Abbaas, Qataadah na Al-Hasan  (رضي الله عنهم) na kwamba imeitwa Swibghah (rangi) kwa sababu athari ya Dini inaonekana wazi kwa mwenye kushikamana na Dini kama vile athari ya rangi inavyodhihirika kwenye nguo.

 

Imaam As-Sa’adiy  (رحمه الله) katika Tafsiyr yake amesema: Maana yake: Wamefaradhishiwa Swibghah ya Allaah, nayo ni Dini Yake, na isimamisheni kwa msimamo timilifu na njia sahihi kwa matendo yake yote ya nje na ya ndani. Na kwa ‘Aqiydah (itikadi) yake yote wakati wote, mpaka iwe kama Swibghah (rangi). Na Swibghah iwe ni moja ya sifa zenu. Kwa hivyo basi, inapokuwa ni moja ya sifa zenu, inakuwa imewajibika kwenu kutekeleza amri Zake kwa utiifu na kwa khiari, na kwa upendo. Hapo Dini huwa ni asasi na asili yao kama vile Swibghah ambayo imepaka rangi nguo kabisa kiasi kwamba ikachukua sifa hiyo (ya rangi yake). Na hii itawaletea furaha katika maisha ya dunia na Aakhirah kwa kuwa Dini inawaongoza katika khulqa (tabia) njema, amali njema, kutenda ihsaan na amali tukufu. Hivyo kwa sababu hii kama njia ya balagha ya kuthibitisha jambo hilo na kwa wale wenye akili safi ndio Akasema:

 

وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ صِبْغَةً ۖ  

“Na Swibghah (dini) gani yaweza kuwa bora zaidi kuliko Dini ya Allaah?”

 

Inamaanisha: Hakuna Swibghah (Dini) iliyo bora kuliko Swibghah (Dini) ya Allaah.

Na ukitaka kujua mfano, amekubainishieni tofauti ya Swibghah ya Allaah na Swibghah nyinginezo, kwani jambo linabainishwa kwa kinyume chake. Basi mtazame mja anayemuamini Rabb wake kwa imaan sahihi, ambayo athari zake ni moyo ulionyenyekea na viungo vilivyotiishwa kiasi kwamba anabakia kuwa na kila sifa njema, matendo mazuri, tabia njema kamilifu, sifa tukufu, na hivyo anakuwa ameepukana na kila sifa ovu za kuchukiza na za aibu. Basi mja huyo anasifika kwa asw-swidq (ukweli) katika kauli zake, matendo yake, subira na uvumilivu wake, upole, ushujaa, na kuwa na ihsaan kwa kauli na matendo, na   kumpenda Allaah na kumcha na kumkhofu, na kutaraji Kwake. Basi hii ndio hali yake ya ikhlaasw kwa Mwenye kustahiki kuabudiwa na kutenda ihsaan kwa Waja Wake.

 

Na haya yote kwa kinyume chake, yanatofautishwa na mja anayemkufuru Rabb wake na akamkimbia, na akawaelekea viumbe wengine badala Yake. Hivyo basi ndivyo anavyosifika kwa sifa ovu za kufr, shirk, kuongopa, khiyana, makri (kupanga njama), udanganyifu na ukosefu wa maadili mema, na kuwatendea uovu viumbe katika kauli zake, matendo yake, wala hana ikhlaasw kwa Mwenye Kustahiki Kuabudiwa, na wala hana ihsaan kwa Waja wa Allaah (سبحانه وتعالى).  

 

Kwa hivyo hii inadhihirisha tofauti kubwa kati ya viwili hivi kwako, na inakubainishia kwamba hakuna Swibghah bora kuliko Swibghah ya Allaah. Na katika hili ni kwamba hakuna Swibghah mbaya zaidi kuliko yule aliyetiwa rangi kwa dini isiyokuwa Dini Yake Allaah (سبحانه وتعالى).

 

[49]  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Atakuwa Shahidi Kwa Ummah Wake Wa Kiislamu Na Ummah Wa Kiislamu Watakuwa Mashahidi Kwa Rusuli Waliotangulia Kwamba Wamebalighisha Ujumbe.

 

Rejea pia Al-Hajj (22:78), An-Nisaa (4:41), Al-Jaathiyah (45:28), Al-Israa (17:71), Az-Zumar (39:69).

 

حَدَّثَنَا يُوسُفُ بْنُ رَاشِدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، وَأَبُو أُسَامَةَ ـ وَاللَّفْظُ لِجَرِيرٍ ـ عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، وَقَالَ أَبُو أُسَامَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو صَالِحٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ يُدْعَى نُوحٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَقُولُ لَبَّيْكَ وَسَعْدَيْكَ يَا رَبِّ‏.‏ فَيَقُولُ هَلْ بَلَّغْتَ فَيَقُولُ نَعَمْ‏.‏ فَيُقَالُ لأُمَّتِهِ هَلْ بَلَّغَكُمْ فَيَقُولُونَ مَا أَتَانَا مِنْ نَذِيرٍ‏.‏ فَيَقُولُ مَنْ يَشْهَدُ لَكَ فَيَقُولُ مُحَمَّدٌ وَأُمَّتُهُ‏.‏ فَتَشْهَدُونَ أَنَّهُ قَدْ بَلَّغَ ‏"‏‏.‏ ‏‏وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا‏ ‏ فَذَلِكَ قَوْلُهُ جَلَّ ذِكْرُهُ ‏وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ‏ وَالْوَسَطُ الْعَدْلُ‏.‏

Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nuwh ataitwa Siku ya Qiyaamah naye ataitikia: Labbayka wa Sa‘dayka, Ee Rabb!   Allaah Atasema: Je, ulibalighisha ujumbe? Nuwh atasema: Naam!   Ummah wake utaulizwa:  Je amewabalighishia ujumbe?  Watasema:  Hakutujia mwonyaji yeyote! Allaah Atasema: Ni nani atakayekushuhudia?  (Nuwh) atasema: Muhammad na Ummah wake.” Nanyi mtashuhudia kuwa yeye amebalighisha ujumbe. 

 

وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ  

“Na awe Rasuli shahidi juu yenu.”  [Al-Baqarah (2:143)]

 

Na ndio iliyokusudiwa Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ

“Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu.” [Al-Baqarah (2:143)]

 

Na Al-Wasatw ni Uadilifu. [Al-Bukhaariy]

 

[50] Sababu Ya Kuitwa Masjid Al-Qiblatayn (Msikiti Wa Vibla Viwili):

 

Waislamu kwanza walielekea Baytul-Maqdis kama ndio Qiblah chao. Kisha ilipoteremshwa Aayah (2:144) ambayo alipewa amri Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ageuze uso wake kuelekea Masjd Al-Haraam Makkah, khabari zikawafikia Swahaba wakiwa ndani ya Swalaah, ndipo nao wakageuza Qiblah chao hapo hapo ndani ya Swalaah kuelekea Al-Ka’bah iliyoko Masjid Al-Haraam. Na kuanzia hapo Msikiti huo ukapewa jina la Masjid Al-Qiblatayn (Msikiti wa Vibla Viwili) yaani, kuelekea kwao ndani ya Swalaah moja, kwanza Baytul-Maqdis (Palestina) kisha kuelekea kwao Al-Ka’bah baada ya kuteremshwa Aayah Al-Baqarah (2:144).

 

[51] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

143-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 143: وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ

 

[52] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

144-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 144: قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ

 

[53] La Kusema Na Kuomba Duaa Pindi Mtu Anapopatwa Msiba Au Janga Lolote Lile:

 

Muislamu apatapo msiba au janga lolote lile na si lazima liwe ni kufariki kwa mtu tu, bali ni kwa aina yoyote ile ya msiba, janga na balaa. Na pia ikiwa ni maradhi, au kupata khasara katika mali, au kupata mateso, au maafa ya aina yoyote, au mitihani, fitnah, n.k. Basi hapo hapo atamke kauli hii inayoitwa Istirjaa’ (kurejesha jambo kwa Allaah) kwani kutamka hivyo, atapata fadhila kadhaa zilizotajwa katika Aayah inayofuatia nazo ni Barakah na Rehma ya Allaah (سبحانه وتعالى):

إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ  

“Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.”

 

Kisha aombe duaa ifuatayo kwani pindi mtu akiiomba, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Humpa badala yake kilicho bora zaidi kuliko hicho alichopoteza au Humbadilishia hali ikawa bora kabisa. [Muslim (918) na Abu Daawuud (3115)]

 

اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا

Allaahumma Ajirniy fiy muswiybatiy wa-Akhlif-liy khayran minhaa.

Ee Allaah! Nilipe katika msiba wangu huu, na Unipe badali iliyo bora kuliko hiyo.

 

[54] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

158-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 158: إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ

 

[55] Jina Adhimu (Tukufu) Kabisa La Allaah (سبحانه وتعالى) Limo Katika Aayah Hii:

 

Amesimulia Asmaa bint Yaziyd (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jina Adhimu kabisa la Allaah limo katika Aayah zifuatazo:

 

وَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ لاَ إِلَهَ إلاَّ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ

 [Al-Baqarah: (163)] na za mwanzo wa ‘Aal-‘Imraan:

الم اللَّهُ لاَ إِلَهَ إلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّوم

[Aal-‘Imraan: (1-2) - Swahiyh At-Tirmidhiy (3478), Swahiyh Ibn Maajah (3123), Swahiyh Al-Jaami’ (980), Swahiyh Abiy Daawuwd (1496) na Swahiyh At-Targhiyb (1642)]

 

[56] Amrisho La Kula Vilivyo Vizuri Na Vya Halali Na Ni Sababu Ya Kutaqabaliwa Duaa: Rejea Al-Muuminuwn (23:51).

 

[57] Furqaan: Pambanuo: Rejea Al-Furqaan (25:1) kwenye maelezo bayana.

 

[58]  Ramadhwaan, Swiyaam Na Yanayohusu Duaa:

 

i-Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Duaa Na Duaa Ya Mwenye Swawm Inaitikiwa:

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله) amesema: “Faida zinapatikana kutokana na Aayah hii. Kwanza: Kwamba kuna uwezekano mkubwa katika Swiyaam (funga) kuitikiwa duaa, kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja Aayah hii baada ya kutaja Aayah za Swiyaam, khasa vile Anavotaja mwishoni mwa kutaja Aayaat za Swiyaam. Pili: Baadhi ya watu wa ilimu wamesema kwamba inaweza kupatikana katika humo faida nyengineyo, kwamba duaa iombwe mwisho wa Siku ya Swawm (kabla ya kufuturu). [Tafsiyr Imaan Ibn ‘Uthaymiyn]

 

Na Hadiyth kadhaa zimethibitisha kuitikiwa duaa ya mwenye Swawm, miongoni mwazo ni:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((ثَلاثَةٌ لا تُرَدُّ دَعْوَتُهُمْ الإِمَامُ الْعَادِلُ وَالصَّائِمُ حِينَ يُفْطِرُ وَدَعْوَةُ الْمَظْلُومِ  )) 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه):   Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watatu duaa zao hazirejeshwi: Imaam (kiongozi)  mtenda haki, mwenye Swawm wakati anapofungua, na duaa ya aliyedhulumiwa.” [Imesimuliwa na At-Tirmidhiy Hadiyth nambari (2525), na Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika Swahihy At-Tirmidhiy Hadiyth nambari (2050)]

 

ii-Kuomba Duaa Kwa Allaah (عزّ وجلّ) Pekee Bila Ya Kumshirikisha:

 

Swahaba walikuwa wanamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) maswali mbalimbali. Allaah (سبحانه وتعالى) Ameyataja katika Qur-aan na Akatoa majibu kwa kutanguliza kumwambia Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) aseme kuwajibu Swahaba “Sema!”. Mifano michache:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ ...  

“Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema…” [Al-Baqarah (2:219)]

 

يَسْأَلُكَ النَّاسُ عَنِ السَّاعَةِ ۖ قُلْ ...

“Watu wanakuuliza kuhusu Saa (Qiyaamah). Sema…” [Al-Ahzaab (33:63)]

 

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ ...  

“Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema…” [Al-Baqarah (2:222)]

 

Na maswali yote mengineyo katika Qur-aan, jibu la Allaah (سبحانه وتعالى) limeanzia hivyo hivyo: “Sema….” isipokuwa swali hili ambalo Allaah (عزّ وجلّ) Analijibu Mwenyewe moja kwa moja Anaposema: 

فَإِنِّي قَرِيبٌ

“Basi hakika Mimi ni Niko karibu.”

 

Hivyo ni kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Anadhihirisha kwamba Yuko karibu kabisa na hakuhitaji mtu kuomba duaa kupitia kwa mtu yeyote ili isije kuwa ni kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) katika kuabudiwa Kwake, kwa sababu duaa ni ibaada kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth aliyosimulia Nu’umaan bin Bashiyr  (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  katika kauli yake  Allaah (سبحانه وتعالى)

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ

“Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni.”  Amesema: “Duaa ni ibaada.” Kisha akasoma Aayah hiyo tukufu.   [Ghaafir (40:60)] [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, na Ahmad – Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Basi watanabahi na wazingatie na wamche Allaah wanaomshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) katika duaa zao kupitia viumbe kama wafanyavyo wenye kutufu makaburi kuwaomba wafu, jambo ambalo linaingia katika shirki kubwa ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Haisamehi pindi mtu akifariki bila ya kutubia.

 

Rejea Ghaafir (40:60).

 

[62] Tamattu’: Aina Mojawapo Ya Hajj Kati Ya Aina Tatu:

 

Tamattu’: Mwenye kuhiji ananuia ‘Umrah katika miezi ya Hajj, kisha anajivua Ihraam baada ya kumaliza ‘Umrah yake, kisha anasubiri hadi siku ya Tarwiyyah; tarehe nane Dhul-Hijjah aingie tena katika Ihraam atekeleze yote yanayompasa ya Hajj. Aina hii ya Hajj ni lazima mwenye kuhiji achinje mnyama.  Aina nyenginezo ni Ifraad na Qiraan na kila moja ina sifa na hukmu zake tofauti na hiyo ya Tamattu’.

 

 

[63]  Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

196-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 196: وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ

 

[64] Miezi Ya Hajj:

 

 Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) amesema: “Miezi ya Hajj ni Shawwaal, Dhul-Qa’dah na siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah. [Fat-hul-Baariy (3/491)]

 

[65] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

197-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 197: وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ

 

[68] Duaa Aliyokuwa Akiomba Sana Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ambayo Imejumuisha Kheri Za Dunia Na Aakhirah:

 

Amesimulia Anas (رضي الله عنه)  : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiomba sana duaa:

رَبَّنَا آتِنَا فِي اَلدُّنْيَا حَسَنَةً, وَفِي اَلْآخِرَةِ حَسَنَةً, وَقِنَا عَذَابَ اَلنَّارِ

“Rabb wetu Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na Tukinge na adhabu ya moto.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

[69] Kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) Katika Siku Za Kuhesabika:

Ni siku za tashriyq (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) kama alivyosema Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما). Na imetajwa kumdhukuru Allaah katika masiku maalumu katika Suwrah Al-Hajj (22:28).

 

[71] Kuteremka Allaah Na Malaika Siku Ya Qiyaamah:

 

 Rejea Al-An’aam (6:158), Al-Furqaan (25:25), Al-Haaqah (69:13-18).

 

[72] Tofauti Ya Ikabu Na Adhabu:

 

Rejea Al-Hashr (59:4).

 

[73] Maana Ya Baghyun/Baghaa Katika Qur-aan:

 

Rejea Ash-Shuwraa (42:14) kupata maana zake mbalimbali.

 

[74]  Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

219-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 219: يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ

 

Hatua Za Uharamisho Wa Pombe Na Kikomo Chake.

 

Rejea An-Nisaa (4:43), na pia Al-Maaidah (5:90-91) ambako kuna maelezo bayana ya Hatua Za Uharamisho Wa Pombe Na Kikomo Chake.

 

[76] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

222-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 222: وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ

 

[77] Haramisho La Kumuingilia Mwanamke Kupitia Dubur (Uchi Wa Nyuma): 

 

Hadiyth kadhaa zimethibiti za haramisho lake, baadhi yake ni hizi zifuatazo:

“Allaah Hatomtazama mwanamume mwenye kumuingilia mkewe kwa nyuma.” [An-Nasaaiy na Ibn Hibbaan kwa Isnaad nzuri]

 

"Amelaaniwa mwenye kumuingilia mwanamke kwa nyuma." [Ahmad, Abuu Daawuwd na Ibn 'Adiy]

 

"Mwenye kumuingilia mwenye hedhi, au mwanamke kwa nyuma, au kumwendea mchawi na kumuamini kwa anayosema, basi amekufuru aliyoteremshiwa Muhammad." [Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah, na Isnaad yake ni Sahihi]

 

[79] Kutimiza Au Kuvunja Viapo: Rejea An-Nahl (16:92).

 

[80] Imekatazwa Kuapa Ovyo Ovyo:

 

Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Aayah hii ya Al-Baqarah (2:225): “Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi.” Ni kutokana na kauli ya mtu (kusema kwake mara kwa mara): “Hapana wa-Allaahi, ndio wa-Allaahi.”  [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]

 

Rejea Al-Maaidah (5:89) na Al-Qalam (68:10). Pia An-Nahl (16:92) kwenye maelezo bayana kuhusu kutimiza au kuvunja viapo.

 

[82] Khul’u:

 

Ni mke kujivua katika ndoa kwa kurudisha mahari ya mume. Ina maelezo na hukumu zake.

 

[83] Uharamu Wa Kuhalalisha Ndoa Baaba Ya Talaka Tatu:

 

Ni haramu kabisa kufunga nikaah ya uongo kwa ajili ya kuhalalisha ndoa baada ya talaka tatu. Amelaaniwa afanyaye hivyo. Amesimulia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amemlaani anayefanya tahliyl (mhalalishaji ndoa) na mhalalishiwa, na wale wanaokula riba na wanaotoa riba.” [At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah na Ahmad]

 

[85] Hikma Ya Kufaridhiwa Eda Miezi Minne Na Siku Kumi: 

 

Sa’iyd bin Muswayyib, Abuu ‘Aaliyah na wengineo wamesema kuwa: Hikma ya kuifanya eda ya mjane kuwa miezi minne na siku kumi ni kuwa yawezekana kuwepo mimba. Mwanamke anaposubiri kwa kipindi hicho itathibitika kama ana mimba au la. Na dalili ni Hadiyth ifuatayo:  Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd  (رضي الله عنه) kwamba: Ametusimulia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho yake.”   [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

[86] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

238-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 238: حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ

 

[87]An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa): Hukmu Ya Kufutwa Eda Mwaka Mzima:

 

Hukumu ya eda hii ya mwaka mzima imefutwa na badala yake ni hukmu ya miezi minne na siku kumi. Rejea Aayah (2:234).

 

[88] Maana Za Ruwh Katika Qur-aan:

 

Rejea An-Nahl (16:2).

 

[89] Jina Tukufu Kabisa La Allaah (Al-Hayyu Al-Qayyuwm):

 

Aayah hii ina Jina Tukufu kabisa la Allaah katika Kauli Yake (تعالى):

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ

Na dalili ni Hadiyth ya Abuu Umaamah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  ”Jina Tukufu  kabisa la Allaah Ambalo likiombewa kwalo Anaitikia limo katika Suwrah tatu: Al-Baqarah, Aal-‘Imraan, na Twaaha’. [At-Tirmdhiy, Silsilah Asw-Swahiyhah (746)] Na mapokezi mengineyo yaliyothibitisha kuhusu Ismul-A’dhwam (Jina Tukufu kabisa).

 

[90] Hakuna Atakayemiliki Ash-Shafaa’ah (Uombezi) Isipokuwa Kwa Idhini Ya Allaah:

 

Rejea Twaahaa (20:109), An-Najm (53:26). Rejea pia Al-Israa (17:79) ambako kumetajwa kuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Nabii Pekee atakayeruhusiwa ash-shafaa’ah atakapokuwa katika Maqaaman Mahmuwdan (Cheo Cha Kuhimidiwa).

[91] Kursiyy Ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

Kuhusu Kauli ya Allaah (تعالى):

وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ

Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi.”

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Iwapo mbingu saba na ardhi saba zingekunjuliwa na kulazwa sambamba, basi zingefikia kipimo cha (udogo wa) pete katika jangwa, kulinganisha na ‘Arsh.” [Ibn Abiy Haatim (3/981)]  

 

[92] Al-‘Aliyyu Al-‘Adhwiym: Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Na Sifa Zake.

 

[93] Aayatul-Kursiyy Ni Aayah Tukufu Kabisa Katika Qur-aan

 

Aayah hii inayojulikana kwa Aayatul-Kursiyy, ni Aayah adhimu kabisa katika Qur-aan kwa dalili ya Hadiyth ya Muslim (810) kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Rabaah Al-Answaariy kutoka kwa Ubayy bin Ka’b ambaye amehadithia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yaa Abal-Mundhir! Hivi unajua ni Aayah gani ndani ya Kitabu cha Allaah ambayo ni adhimu kabisa?” Nikasema: Allaah na Rasuli Wake Ni Wajuzi zaidi. Akasema: “Yaa Abal-Mundhir! Hivi unajua ni Aayah gani ndani ya Kitabu cha Allaah ambayo ni adhimu kabisa?” Akasema: Nikasema:

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ

Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Al-Hayyu (Aliye Hai daima) Al-Qayyuwm (Msimamia kila kitu).” (mpaka mwisho wa Aayah).

 

Akasema Ubayy: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanipiga kifuani kisha akasema: “Wa-Allaahi upongezwe kwa ilimu yako yaa Abal-Mundir.” [Muslim] Na katika mapokezi ya Ahmad imeendelea: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, Aayah hii ina ulimi na midomo miwili ambayo inamtukuza Mfalme (Allaah) katika mguu wa ‘Arsh.” [Swahiyh Targhiyb (1471)]  

 

[94] Twaghuti:

 

Maana ya طَاغُوْتُ   kilugha: Asili ya neno hilo linatokana na  طغيان yenye kumaanisha uvukaji mipaka.

 

Na katika istilaahi, طُغْيَانُ  ni kuasi, uvukaji mipaka, kwenda kinyume na Sharia ya Allaah (عزّ وجلّ), kuabudu asiyekuwa Muumba (Allaah), kwa sababu asili ya kuumbwa ni kumwabudu Allaah (عزّ وجلّ) Pekee. Na kumwabudu ipasavyo ni kama vile inavyotaka sharia. Kinyume chake ni uvukaji mipaka ya sharia na hivyo atakua mtu ameasi na amevuka mipaka.

 

‘Ulamaa wamefafanua twaghuti kuwa ni kila kinachoabudiwa pasi na Allaah. Kadhaalika twaghuti ni kila anayelingania watu katika upotofu, au kuwaongoza watu katika kufru, shirki, au kumuasi Allaah (سبحانه وتعالى). Mifano ya twaghuti ni ibliys, shaytwaan, mizimu, mchawi, mganga, na kahini (mtabiri). Hali kadhaalika, twaghuti ni anayedai kuwa anajua ilimu ya ghaibu. Hayo yote ni uvukaji mipaka wa kutoka kwenye haki kuelekea ubatwilifu.

 

Aayah inayofuatia imetaja pia twaghuti. Na rejea An-Nisaa (4:51), (4:60), (4:76), Al-Maaidah (5:60), An-Nahl (16:36), Az-Zumar (39:17).

 

[96]  Nimruwdh Mfalme Dhalimu Aliyejifanya Ni Mwabudiwa Aliyebishana Na Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) Akafishwa Kwa Mbu Kuingia Sikioni Na Puani Mwake: 

 

Jina lake ni Nimruwdh bin Kina’aan, bin Rayb, bin Nimruwdh bin Kuwsh bin Nuwh (عليه السّلام).   

 

Alikuwa mfalme kafiri, dhalimu, mwenye kiburi, aliyejifanya jabari, aliyeitawala dunia kutoka katika ufalme wake Baabiyl huko Iraq katika zama za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). Nimruwdh alikuwa dhalimu wa kwanza katika ardhi aliyedai kuwa yeye ndiye apasaye kuabudiwa, ndipo Nabiy Ibraahiym  (عليه السّلام) alipobishana naye kuhusu kudai kwake hivyo, akampa changamoto hiyo iliyotajwa katika Aayah ya kumtaka alifanye jua lichomoze Magharibi badala ya kuchomza Mashariki, akashindwa na akahizika!

 

Kifo cha Nimruwdh kimesimuliwa katika Hadiyth za Israaiyliyyaat na hakuna kosa kusimulia ili tupate kupata mafunzo yake. Na katika kisa hiki tunapata funzo kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Alimfisha mfalme aliyejidai kuwa yeye ndiye anayepasa kuabudiwa, kwa kidudu dhalili na kidogo mno! [Hadiyth ya ‘Amr bin Al-Aasw (رضي الله عنه)  ameipokea Al-Bukhaariy]  

 

Imaam Atw-Twabariy ameitoa katika Jaami’u Al-Bayaan (14/204) kutoka kwa Zayd bin Aslam kwamba: “Nimruwdh hakika alikuwa dhalimu wa kwanza duniani. Allaah (سبحانه وتعالى) Akampelekea mbu, wakaingia masikioni na puani mwake.  Alibaki kujipiga kichwa chake kwa nyundo kwa miaka mia nne! Watu waliokuwa na huruma zaidi walikuwa ni wale waliounganisha mikono wakawa wanampiga kichwani (kutuliza mbu).  Alijifanya jabari na alikuwa dhalimu kwa muda wa miaka mia nne, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akamuadhibu miaka mia nne sawa na muda wa utawala wake. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akamfisha.”

 

[97] Mja Aliyefishwa Miaka Mia Ni ‘Uzayr?

 

Wafasiri wa Qur-aan wamekhitilafiana kama mja huyo aliyepita katika kijiji kilichoporomoka akafishwa miaka mia ni ‘Uzayr au la. Na kauli iliyo mashuhuri ni kwamba aliyekusudiwa hapo ni ‘Uzayr. [Imepokewa na Ibn Jariyr na Ibn Abiy Haatim kutoka kwa Ibn ‘Abbaas, Al-Hasan, Qataadah, As-Suddiy, na Sulaymaan Bin Buraydah [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Mayahudi wamesema kuwa yeye ni Nabiy miongoni mwa Manabii wa Bani Israa’iyl lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuthibitisha hilo. Rejea At-Tawbah (9:30).

 

[98] Riyaa-a (Kujionyesha Kwa Watu) Ni Shirki Inayobatwilisha Amali:

 

Hii ni riyaa-a ya kutoa mali katika njia ya Allaah. Rejea An-Nisaa (4:142). Rejea pia Az-Zumar (39:65) kwenye maelezo kuhusu aina za shirki.

 

[101] Adhabu Za Anayejihusisha Na Riba:

 

Hadiyth kadhaa za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zimethibiti kutahadharisha riba na adhabu zake, miongoni mwazo ni:

 

“Dirhamu ya riba anayokula mtu na huku anajua, ni mbaya zaidi kuliko kuzini mara thelathini na sita.” [Ahmad]

 

“Riba ina milango sabini na tatu (73). Iliyo nyepesi na sahali ni mtu kumuoa mamake.” [Al-Haakim]

 

“Jiepusheni na mambo saba yenye kuangamiza… kula riba.”  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

[102]  Anayejihusisha Na Riba Atangaze Vita Baina Yake Na Allaah Na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم)   

 

Ilipoteremka Aayah namba (2:275), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Yeyote asiyejizuia kufanya “mukhaabarah” (kukodisha shamba kwa malipo ya kugawana sehemu ya mazao), basi apokee tangazo la vita kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr] 

 

[103] Aayah Ya Mwisho Kuteremshwa:

 

‘Ulamaa wengi wamekubaliana kwamba hii ni Aayah ya mwisho kuteremshwa. Na miongoni mwa Salaf waliokiri ni Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), na Sa’iyd bin Jubayr (رحمه الله) kwa Riwayaah mbalimbali, kwamba baada ya kuteremshwa Aayah hii, yalipita masiku kadhaa kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akafariki. [An-Nasaaiy – Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Na Imaam As-Sa’dy (رحمه الله) amesema: “Hii ni Aayah ya mwisho iliyoteremshwa katika Qur-aan, na ikafanywa ni hatima ya hukmu hizi za maamrisho na makatazo kwa sababu humo mna ahadi za kutenda mema na kheri, na onyo kali la kutenda maovu. Na kwamba anayejua kwamba yeye atarejeshwa kwa Allaah, basi Allaah Atamlipa kwa dogo na kubwa (aliyoyatenda), na yaliyodhahiri na ya siri, na kwamba Allaah Hatomdhulumu uzito wa chembe ya hardali (au atomu). Hivyo basi itamwajibikia awe na raghbah (utashi, matumaini) na khofu. Na bila kuyajua hayo moyoni, kutakuwa hakuna sababu ya kuongozwa kuyatekeleza.”

 

[104] An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa):

 

Aayah hii imefutwa hukmu yake. Na badala yake ikateremshwa Aayah ya mwisho ya Suwrah hii:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ    

“Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake.” [Al-Baqarah: (286)]

 

 

[106] Mawlaa:  Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.  

 

[107]  Fadhila Za Aayah Mbili Za Mwisho Suwrah Al-Baqarah:

 

(i) Kutokuhesabiwa katika kusahau na kukosea. 

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ummah wangu umenyanyuliwa makosa na kusahau na wanayoshurutishwa.” [Ibn Maajah, Ibn Hibbaan, Ad-Daaraqutwniy, At-Twabaraaniy na Al-Haakim, Irwaa Al-Ghaliyl (1027)]

 

(ii) Atakayezisoma usiku zitamtosheleza:

 

Abuu Mas‘uwd Al-Answaariyy ‘Uqbah bin ‘Amr bin Tha’alabah (رضي الله عنه) amesimulia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesoma usiku Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah zitamtosheleza.” Yaani: zinamtosheleza kumkinga na kila baya na kila lenye kumdhuru. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

(iii) Hakuna Nabiy aliyepewa Aayah hizi isipokuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم): 

 

Ibn ‘Abbaas  (رضي الله عنهما) amesimulia:   Jibriyl  (عليه السّلام) alipokuwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisikia sauti kutoka juu. Jibriyl (عليه السّلام)  akatazama juu akasema: “Huu mlango wa mbinguni umefunguliwa na haujapatapo kamwe kufunguliwa isipokuwa leo! Malaika akateremka humo akasema: Huyu Malaika ameteremka ardhini, hajapatapo kuteremka kamwe isipokuwa leo! Akasalimia kisha   akasema: Pokea bishara ya Nuru mbili ulizopewa ambazo hakuna Nabiy aliyepewa kabla yako: Ufunguo wa Kitabu (Al-Faatihah), na Aayah (mbili) za mwisho wa Suwratul-Baqarah.  Hutosoma herufi humo ila utapewa barakah zake zilizomo.” [Muslim]

 

(iv) Aayah mbili hizi ni Aayah pekee ambazo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Amepewa Wahy mbinguni wakati alipofika mbingu ya saba katika tukio la Al-Israa Wal-Mi’raaj.

 

Hadiyth ya Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipopelekwa safari ya usiku mbinguni (Al-Israa Wal-Mi’raaj), aliishia Sidratul-Muntahaa (Mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa) katika mbingu ya sita ambapo huishia kila kitu (hakuna ajuaye ilimu ya baada ya hapo isipokuwa Allaah) ambapo pia kunaishia kila kinachopanda kutoka ardhini (amali za watu n.k) na kushikiliwa hapo, na kinapoishia kila kitu kinachoteremka kutoka juu yake na kushikiliwa hapo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ ﴿١٦﴾

“Ulipoufunika mkunazi huo unachokifunika.” [An-Najm: (16)]

 

(Msimulizi) akasema: (kilichofunika mkunazi) ni vipepeo vya dhahabu. Akasema: Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akapewa (mambo) matatu: Akapewa Swalaah tano za kila siku, na akapewa hitimisho la Suwrah Al-Baqarah, na kughufuriwa katika ummah wake ambaye hamshirikishi Allaah na chochote.  [Muslim]

 

 

 

Share