033 - Al-Ahzaab

 

الأَحْزاب

 

033-Al-Ahzaab

 

  

033-Al-Ahzaab: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ اتَّقِ اللَّـهَ وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١﴾

1. Ee Nabiy! Mche Allaah, na wala usiwatii makafiri na wanafiki. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

وَاتَّبِعْ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٢﴾

2. Na fuata yale ulofunuliwa Wahy kutoka kwa Rabb wako. Hakika Allaah daima kwa yale myatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

 

وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٣﴾

3. Na tawakali kwa Allaah. Na Anatosheleza Allaah Kuwa Ni Mtegemewa.

 

 

 

مَّا جَعَلَ اللَّـهُ لِرَجُلٍ مِّن قَلْبَيْنِ فِي جَوْفِهِ ۚ وَمَا جَعَلَ أَزْوَاجَكُمُ اللَّائِي تُظَاهِرُونَ مِنْهُنَّ أُمَّهَاتِكُمْ ۚ وَمَا جَعَلَ أَدْعِيَاءَكُمْ أَبْنَاءَكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ قَوْلُكُم بِأَفْوَاهِكُمْ ۖ وَاللَّـهُ يَقُولُ الْحَقَّ وَهُوَ يَهْدِي السَّبِيلَ ﴿٤﴾

4. Allaah Hakufanya mtu yeyote kuwa na nyoyo mbili kifuani mwake. Na wala Hakufanya wake zenu ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu kuwa ni mama zenu. Na wala Hakufanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni watoto wenu khasa. Hizi ni kauli zenu za vinywa vyenu tu. Na Allaah Anasema ya haki, Naye Anaongoza njia (ya haki).

 

 

 

ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ ۚ فَإِن لَّمْ تَعْلَمُوا آبَاءَهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ وَمَوَالِيكُمْ ۚ وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُم بِهِ وَلَـٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥﴾

5. Waiteni kwa (majina ya) baba zao. Huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Allaah.[1] Na ikiwa hamuwajui baba zao, basi ni ndugu zenu katika Dini, na walio katika ulinzi wenu, na wala hakuna dhambi juu yenu katika yale mliyoyakosea, lakini isipokuwa katika yale iliyoyakusudia nyoyo zenu. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[2]

 

 

 

النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ ۖ وَأَزْوَاجُهُ أُمَّهَاتُهُمْ ۗ وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّـهِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُهَاجِرِينَ إِلَّا أَن تَفْعَلُوا إِلَىٰ أَوْلِيَائِكُم مَّعْرُوفًا ۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي الْكِتَابِ مَسْطُورًا ﴿٦﴾

6. Nabiy ana haki zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao.[3] Na wake zake ni mama zao.[4] Na wenye uhusiano wa damu wana haki zaidi (katika kurithiana) wao kwa wao katika Hukumu ya Allaah kuliko (undugu wa) Waumini na Muhaajiriyna, isipokuwa mkiwafanyia wema marafiki zenu wa karibu. Hayo yamekwishaandikwa Kitabuni.

 

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۖ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿٧﴾

7. Na pale Tulipochukua kutoka kwa Manabii fungamano lao, na kutoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na kutoka kwa Nuwh, na Ibraahiym, na Muwsaa, na ‘Iysaa mwana wa Maryam, na Tukachukua kutoka kwao fungamano gumu.[5]

 

 

 

لِّيَسْأَلَ الصَّادِقِينَ عَن صِدْقِهِمْ ۚ وَأَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿٨﴾

8. Ili Awaulize wakweli kuhusu ukweli wao, na Amewaandalia makafiri adhabu iumizayo.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَاءَتْكُمْ جُنُودٌ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا وَجُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا ﴿٩﴾

9. Enyi walioamini! Kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu, pale yalipokujieni majeshi Tukawapelekea upepo wa dhoruba na majeshi msiyoyaona (ya Malaika). Na Allaah daima Ni Mwenye Kuona myatendayo.[6]  

 

 

 

 

إِذْ جَاءُوكُم مِّن فَوْقِكُمْ وَمِنْ أَسْفَلَ مِنكُمْ وَإِذْ زَاغَتِ الْأَبْصَارُ وَبَلَغَتِ الْقُلُوبُ الْحَنَاجِرَ وَتَظُنُّونَ بِاللَّـهِ الظُّنُونَا ﴿١٠﴾

10. Walipokujieni kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu, na macho yalipokodoka, na nyoyo zikafika kooni (kwa kiwewe) na mkamdhania Allaah dhana nyingi.

 

 

هُنَالِكَ ابْتُلِيَ الْمُؤْمِنُونَ وَزُلْزِلُوا زِلْزَالًا شَدِيدًا ﴿١١﴾

11. Hapo ndipo Waumini walipojaribiwa na wakatetemeshwa mtetemesho mkali kabisa.

 

 

 

 

وَإِذْ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ مَّا وَعَدَنَا اللَّـهُ وَرَسُولُهُ إِلَّا غُرُورًا ﴿١٢﴾

12. Na pale waliposema wanafiki na wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi[7]: Allaah na Rasuli Wake Hawakutuahidi isipokuwa ghururi tu.

 

 

 

وَإِذْ قَالَت طَّائِفَةٌ مِّنْهُمْ يَا أَهْلَ يَثْرِبَ لَا مُقَامَ لَكُمْ فَارْجِعُوا ۚ وَيَسْتَأْذِنُ فَرِيقٌ مِّنْهُمُ النَّبِيَّ يَقُولُونَ إِنَّ بُيُوتَنَا عَوْرَةٌ وَمَا هِيَ بِعَوْرَةٍ ۖ إِن يُرِيدُونَ إِلَّا فِرَارًا ﴿١٣﴾

13. Na pale waliposema kundi miongoni mwao: Enyi watu wa Yathrib!  Hamna uimara, basi rudini (makwenu)! Na kundi miongoni mwao likamwomba idhini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) likasema: Hakika nyumba zetu ziko tupu! Na wala hazikuwa tupu! Hawakutaka ila kukimbia tu!

 

 

 

وَلَوْ دُخِلَتْ عَلَيْهِم مِّنْ أَقْطَارِهَا ثُمَّ سُئِلُوا الْفِتْنَةَ لَآتَوْهَا وَمَا تَلَبَّثُوا بِهَا إِلَّا يَسِيرًا ﴿١٤﴾

14. Na lau wangeliingiliwa kutoka pande zake zote (za mji), kisha wakatakwa kuritadi, basi wangeliifanya na wala wasingelisita kwayo isipokuwa kidogo tu.

 

 

 

وَلَقَدْ كَانُوا عَاهَدُوا اللَّـهَ مِن قَبْلُ لَا يُوَلُّونَ الْأَدْبَارَ ۚ وَكَانَ عَهْدُ اللَّـهِ مَسْئُولًا ﴿١٥﴾

15. Na kwa yakini walikwishamuahidi Allaah kabla, kwamba hawatogeuza migongo yao kukimbia. Na Ahadi ya Allaah ni yenye kuulizwa tu.  

 

 

 

قُل لَّن يَنفَعَكُمُ الْفِرَارُ إِن فَرَرْتُم مِّنَ الْمَوْتِ أَوِ الْقَتْلِ وَإِذًا لَّا تُمَتَّعُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٦﴾

16. Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kukimbia hakutakufaeni ikiwa mmeyakimbia mauti, au kuuawa, kwani hamtostareheshwa isipokuwa kidogo tu.

 

 

 

قُلْ مَن ذَا الَّذِي يَعْصِمُكُم مِّنَ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَ بِكُمْ سُوءًا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ رَحْمَةً ۚ وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٧﴾

17. Sema: Ni nani ambaye anaweza kukulindeni na Allaah, kama Akikutakieni uovu au Akikutakieni Rehma? Na wala hawatopata badala ya Allaah mlinzi wala mwenye kunusuru.

 

 

 

قَدْ يَعْلَمُ اللَّـهُ الْمُعَوِّقِينَ مِنكُمْ وَالْقَائِلِينَ لِإِخْوَانِهِمْ هَلُمَّ إِلَيْنَا ۖ وَلَا يَأْتُونَ الْبَأْسَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٨﴾

18. Allaah Amekwishawajua wanaozuia miongoni mwenu (watu wasiende vitani) na wale wanaowaambia ndugu zao: Njooni kwetu! Na hawaendi vitani isipokuwa kidogo tu.

 

 

 

أَشِحَّةً عَلَيْكُمْ ۖ فَإِذَا جَاءَ الْخَوْفُ رَأَيْتَهُمْ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ تَدُورُ أَعْيُنُهُمْ كَالَّذِي يُغْشَىٰ عَلَيْهِ مِنَ الْمَوْتِ ۖ فَإِذَا ذَهَبَ الْخَوْفُ سَلَقُوكُم بِأَلْسِنَةٍ حِدَادٍ أَشِحَّةً عَلَى الْخَيْرِ ۚ أُولَـٰئِكَ لَمْ يُؤْمِنُوا فَأَحْبَطَ اللَّـهُ أَعْمَالَهُمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿١٩﴾

19. Wachoyo sana juu yenu. Na inapokuja khofu utawaona wanakutazama macho yao yanazunguruka kama yule aliyefunikwa na mauti. Inapoondoka khofu wanakushutumuni kwa ndimi kali! Wachoyo wa kila kheri! Hao hawakuamini, na kwa hivyo Allaah Ameziporomosha amali zao. Na hayo kwa Allaah ni mepesi kabisa.

 

 

 

يَحْسَبُونَ الْأَحْزَابَ لَمْ يَذْهَبُوا ۖ وَإِن يَأْتِ الْأَحْزَابُ يَوَدُّوا لَوْ أَنَّهُم بَادُونَ فِي الْأَعْرَابِ يَسْأَلُونَ عَنْ أَنبَائِكُمْ ۖ وَلَوْ كَانُوا فِيكُم مَّا قَاتَلُوا إِلَّا قَلِيلًا ﴿٢٠﴾

20. Wanadhania kuwa makundi yaliyoshirikiana hayakuondoka bado. Na yanapokuja makundi yaliyoshirikiana, wanatamani lau kwamba wanaishi jangwani kwa mabedui, wanaulizia habari zenu. Na lau wangelikuwa wako pamoja nanyi, basi wasingelipigana isipokuwa kidogo tu.

 

 

 

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا ﴿٢١﴾

21. Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Rasuli wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho[8], na akamdhukuru Allaah kwa wingi.

 

 

 

وَلَمَّا رَأَى الْمُؤْمِنُونَ الْأَحْزَابَ قَالُوا هَـٰذَا مَا وَعَدَنَا اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَصَدَقَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ ۚ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا ﴿٢٢﴾

22. Basi Waumini walipoona makundi yaliyoshirikiana, walisema: Haya ndio yale Aliyotuahidi Allaah na Rasuli Wake, na Amesema kweli Allaah na Rasuli Wake. Na haikuwazidishia isipokuwa imaan na kujisalimisha.

 

 

 

مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّـهَ عَلَيْهِ ۖ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ ۖ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا ﴿٢٣﴾

23. Miongoni mwa Waumini, wapo wanaume waliotimiza kikweli waliyoahidiana na Allaah. Basi miongoni mwao wako waliotimiza nadhiri yao (wamekufa Shuhadaa), na miongoni mwao wako wanaongojea na hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.[9]

 

 

 

لِّيَجْزِيَ اللَّـهُ الصَّادِقِينَ بِصِدْقِهِمْ وَيُعَذِّبَ الْمُنَافِقِينَ إِن شَاءَ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٢٤﴾

24. Ili Allaah Awalipe wakweli kwa ukweli wao, na Awaadhibu wanafiki pindi Akitaka au Apokee tawbah yao. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. 

 

 

 

وَرَدَّ اللَّـهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا ۚ وَكَفَى اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ قَوِيًّا عَزِيزًا ﴿٢٥﴾

25. Na Allaah Akawarudisha nyuma wale waliokufuru kwa ghaidhi zao, hawakupata kheri yoyote. Na Allaah Amewatosheleza Waumini vitani. Na Allaah daima Ni Mwenye nguvu zote, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika.[10]

 

 

 

وَأَنزَلَ الَّذِينَ ظَاهَرُوهُم مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِن صَيَاصِيهِمْ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ فَرِيقًا تَقْتُلُونَ وَتَأْسِرُونَ فَرِيقًا ﴿٢٦﴾

26. Na Aliwateremsha wale waliowasaidia (maadui) miongoni mwa Watu wa Kitabu kutoka katika ngome zao, na Akavurumisha kizaazaa katika nyoyo zao; kundi mnaliua, na kundi jingine mnaliteka.

 

 

 

وَأَوْرَثَكُمْ أَرْضَهُمْ وَدِيَارَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ وَأَرْضًا لَّمْ تَطَئُوهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرًا ﴿٢٧﴾

27. Na Akakurithisheni ardhi yao, na majumba yao, na mali zao, na ardhi hamkuwahi kuzikanyaga. Na Allaah daima Ni Muweza juu ya kila kitu.

 

 

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ إِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَأُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا ﴿٢٨﴾

28. Ee Nabiy!  Waambie wake zako: Ikiwa mnataka uhai wa dunia na mapambo yake, basi njooni nikupeni kitoka nyumba na nikuacheni huru, mwachano mzuri.[11]

 

 

 

وَإِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ فَإِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِنَاتِ مِنكُنَّ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٢٩﴾

29. Na ikiwa mnamtaka Allaah na Rasuli Wake na Nyumba ya Aakhirah, basi hakika Allaah Amewaahidi wanawake watendao wema miongoni mwenu, ujira adhimu.

 

 

 

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ مَن يَأْتِ مِنكُنَّ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ يُضَاعَفْ لَهَا الْعَذَابُ ضِعْفَيْنِ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾

30. Enyi wake wa Nabiy! Yeyote yule miongoni mwenu atakayeleta uchafu bayana, atazidishiwa adhabu maradufu. Na hayo kwa Allaah ni mepesi.

 

 

 

وَمَن يَقْنُتْ مِنكُنَّ لِلَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتَعْمَلْ صَالِحًا نُّؤْتِهَا أَجْرَهَا مَرَّتَيْنِ وَأَعْتَدْنَا لَهَا رِزْقًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾

31. Na yeyote miongoni mwenu atakayemtii Allaah na Rasuli Wake, na akatenda mema, Tutampa ujira wake mara mbili, na Tumemuandalia riziki ya ukarimu.

 

 

 

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٣٢﴾

32. Enyi wake wa Nabiy!  Nyinyi si kama yeyote yule katika wanawake. Mkiwa na taqwa, basi msilegeze (sauti) katika kauli (zenu), asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi, na semeni kauli inayokubalika.[12]

 

 

 

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴿٣٣﴾

33. Na bakieni majumbani mwenu, na wala msionyeshe mapambo na uzuri kwa ajinabi kujishaua kama zama za ujahili. Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah na mtiini Allaah na Rasuli Wake. Hakika Allaah Anataka Akuondosheeni maovu enyi ahli wa nyumba (ya Nabiy) na Akutakaseni mtakaso barabara.

 

 

 

وَاذْكُرْنَ مَا يُتْلَىٰ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ وَالْحِكْمَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ لَطِيفًا خَبِيرًا ﴿٣٤﴾

34. Na kumbukeni yale yanayosomwa majumbani mwenu katika Aayaat za Allaah na Hikmah (Sunnah). Hakika Allaah daima Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

 

إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿٣٥﴾

35. Hakika Waislamu wanaume na wanawake, na Waumini wanaume na wanawake, na watiifu wanaume na wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao swadaqah wanaume na wanawake, na wafungao Swawm wanaume na wanawake, na wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanaomdhukuru Allaah kwa wingi wanaume na wanawake, Allaah Amewaandalia Maghfirah na ujira adhimu.[13]

 

 

 

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦﴾

36. Na haiwi kwa Muumini mwanamume wala kwa Muumini mwanamke, Anapohukumu Allaah na Rasuli Wake jambo lolote, iwe wana khiari katika jambo lao.  Na anayemuasi Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amepotoka upotofu bayana.

 

 

 

وَإِذْ تَقُولُ لِلَّذِي أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَأَنْعَمْتَ عَلَيْهِ أَمْسِكْ عَلَيْكَ زَوْجَكَ وَاتَّقِ اللَّـهَ وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّـهُ مُبْدِيهِ وَتَخْشَى النَّاسَ وَاللَّـهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَاهُ ۖ فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِّنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا لِكَيْ لَا يَكُونَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ حَرَجٌ فِي أَزْوَاجِ أَدْعِيَائِهِمْ إِذَا قَضَوْا مِنْهُنَّ وَطَرًا ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ مَفْعُولًا ﴿٣٧﴾

37. Na pale ulipomwambia yule ambaye Allaah Amemneemesha nawe ukamneemesha: Mshikilie mkeo, na mche Allaah! Na ukaficha katika nafsi yako ambayo Allaah Ametaka kuyafichua, na unakhofu watu, na hali Allaah Ana haki zaidi umkhofu. Basi Zayd alipomaliza haja kwake, Tukakuozesha ili isiwe dhambi juu ya Waumini kuhusu (kuoa) wake wa watoto wao wa kupanga wanapomaliza haja kwao. Na Amri ya Allaah daima ni yenye kutekelezwa.[14]

 

 

 

مَّا كَانَ عَلَى النَّبِيِّ مِنْ حَرَجٍ فِيمَا فَرَضَ اللَّـهُ لَهُ ۖ سُنَّةَ اللَّـهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلُ ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ قَدَرًا مَّقْدُورًا ﴿٣٨﴾

38. Hakuna lawama yoyote juu ya Nabiy katika (kufanya) yale Aliyomfaridhishia Allaah. Ni Desturi ya Allaah kwa wale waliopita kabla. Na Amri ya Allaah daima ni kudura iliyokwishakadiriwa vyema kabisa. 

 

 

 

الَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّـهِ وَيَخْشَوْنَهُ وَلَا يَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّـهَ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٣٩﴾

39. Wale wanaobalighisha Ujumbe wa Allaah na wanamkhofu Yeye na wala hawamkhofu yeyote isipokuwa Allaah. Na Allaah Anatosheleza Kuwa Mwenye Kuhesabu.

 

 

 

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٤٠﴾

40. Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baba wa yeyote katika wanaume wenu, lakini ni Rasuli wa Allaah na ni mwisho wa Manabii. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa kila kitu.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا ﴿٤١﴾

41. Enyi walioamini!  Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru.

 

 

 

وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿٤٢﴾

42. Na Msabbihini asubuhi na jioni.  

 

 

 

هُوَ الَّذِي يُصَلِّي عَلَيْكُمْ وَمَلَائِكَتُهُ لِيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا ﴿٤٣﴾

43. Yeye (Allaah) Ndiye Anakurehemuni, na Malaika Wake (wanakuombeeni maghfirah na rehma)[15] ili Akutoeni kutoka katika viza kuingia katika Nuru. Naye daima Ni Mwenye Kurehemu Waumini.

 

 

 

تَحِيَّتُهُمْ يَوْمَ يَلْقَوْنَهُ سَلَامٌ ۚ وَأَعَدَّ لَهُمْ أَجْرًا كَرِيمًا ﴿٤٤﴾

44. Maamkizi yao Siku watakayokutana Naye ni “Salaam.” Na Amewaandalia ujira wa ukarimu.[16]

 

 

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٤٥﴾

45. Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji.

 

 

 

وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا ﴿٤٦﴾

46. Na mlinganiaji kwa Allaah kwa Idhini Yake, na siraji kali yenye nuru.

 

 

 

وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ بِأَنَّ لَهُم مِّنَ اللَّـهِ فَضْلًا كَبِيرًا ﴿٤٧﴾

47. Na wabashirie Waumini kwamba watapata kutoka kwa Allaah fadhila kubwa.

 

 

 

وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ وَدَعْ أَذَاهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٤٨﴾

48. Na wala usiwatii makafiri na wanafiki, na achilia mbali maudhi yao, na tawakali kwa Allaah. Na Allaah Anatosheleza Kuwa Mtegemewa.  

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَكَحْتُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ فَمَا لَكُمْ عَلَيْهِنَّ مِنْ عِدَّةٍ تَعْتَدُّونَهَا ۖ فَمَتِّعُوهُنَّ وَسَرِّحُوهُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا ﴿٤٩﴾

49. Enyi walioamini! Mnapofunga nikaah na Waumini wa kike, kisha mkawataliki kabla ya kujimai nao, basi hamna juu yao eda yoyote mtakayohesabu. Basi wapeni kitoka nyumba na waacheni huru, kwa mwachano mzuri.

 

 

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَحْلَلْنَا لَكَ أَزْوَاجَكَ اللَّاتِي آتَيْتَ أُجُورَهُنَّ وَمَا مَلَكَتْ يَمِينُكَ مِمَّا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَيْكَ وَبَنَاتِ عَمِّكَ وَبَنَاتِ عَمَّاتِكَ وَبَنَاتِ خَالِكَ وَبَنَاتِ خَالَاتِكَ اللَّاتِي هَاجَرْنَ مَعَكَ وَامْرَأَةً مُّؤْمِنَةً إِن وَهَبَتْ نَفْسَهَا لِلنَّبِيِّ إِنْ أَرَادَ النَّبِيُّ أَن يَسْتَنكِحَهَا خَالِصَةً لَّكَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۗ قَدْ عَلِمْنَا مَا فَرَضْنَا عَلَيْهِمْ فِي أَزْوَاجِهِمْ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ لِكَيْلَا يَكُونَ عَلَيْكَ حَرَجٌ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥٠﴾

50. Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekuhalalishia wake zako ambao uliwapa mahari yao, na wale iliyomiliki mkono wako wa kuume katika wale (mateka) Aliokuruzuku Allaah, na mabinti wa ‘ammi zako, na mabinti wa mashangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa khalati zako ambao wamehajiri pamoja nawe, na mwanamke Muumini akijitunuku mwenyewe kwa Nabiy, ikiwa Nabiy anataka kumuoa. Ni makhsusi kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine. Tumekwishajua yale Tuliyowafaridhishia wao katika wake zao na wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume ili isijekuwa vigumu juu yako. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

تُرْجِي مَن تَشَاءُ مِنْهُنَّ وَتُؤْوِي إِلَيْكَ مَن تَشَاءُ ۖ وَمَنِ ابْتَغَيْتَ مِمَّنْ عَزَلْتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكَ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن تَقَرَّ أَعْيُنُهُنَّ وَلَا يَحْزَنَّ وَيَرْضَيْنَ بِمَا آتَيْتَهُنَّ كُلُّهُنَّ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَلِيمًا ﴿٥١﴾

51. Umuakhirishe umtakaye miongoni mwao na umsogeze kwako umtakaye. Na ukimtaka katika uliyemtenga basi hakuna dhambi juu yako. Hivyo ni karibu zaidi kupelekea kuburudika macho yao, na wala wasihuzunike, na waridhike kwa yale uliyowapa kila mmoja wao. Na Allaah Anajua yale yaliyomo nyoyoni mwao. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mvumilivu.[17]

 

 

 

لَّا يَحِلُّ لَكَ النِّسَاءُ مِن بَعْدُ وَلَا أَن تَبَدَّلَ بِهِنَّ مِنْ أَزْوَاجٍ وَلَوْ أَعْجَبَكَ حُسْنُهُنَّ إِلَّا مَا مَلَكَتْ يَمِينُكَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ رَّقِيبًا ﴿٥٢﴾

52. Si halali kwako wanawake wengine baada ya hao na wala kuwabadilisha kwa wake wengine japo kama uzuri wao umekupendeza, isipokuwa wale iliyomiliki mkono wako wa kuume. Na Allaah daima Ni Mwenye Kuchunga kila kitu.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتَ النَّبِيِّ إِلَّا أَن يُؤْذَنَ لَكُمْ إِلَىٰ طَعَامٍ غَيْرَ نَاظِرِينَ إِنَاهُ وَلَـٰكِنْ إِذَا دُعِيتُمْ فَادْخُلُوا فَإِذَا طَعِمْتُمْ فَانتَشِرُوا وَلَا مُسْتَأْنِسِينَ لِحَدِيثٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكُمْ كَانَ يُؤْذِي النَّبِيَّ فَيَسْتَحْيِي مِنكُمْ ۖ وَاللَّـهُ لَا يَسْتَحْيِي مِنَ الْحَقِّ ۚ وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ ۚ وَمَا كَانَ لَكُمْ أَن تُؤْذُوا رَسُولَ اللَّـهِ وَلَا أَن تَنكِحُوا أَزْوَاجَهُ مِن بَعْدِهِ أَبَدًا ۚ إِنَّ ذَٰلِكُمْ كَانَ عِندَ اللَّـهِ عَظِيمًا ﴿٥٣﴾

53. Enyi walioamini! Msiingie nyumba za Nabiy isipokuwa mkipewa idhini ya kwenda kula si kungojea kiive. Lakini mtakapoitwa, basi ingieni. Na mkimaliza kula, tawanyikeni, na wala msikae kujiliwaza kwa mazungumzo. Hakika hiyo ilikuwa inamuudhi Nabiy, naye anakustahini, lakini Allaah Hasitahi (kubainisha) haki. Na mnapowauliza wake zake haja, waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Na haipasi kwenu kumuudhi Rasuli wa Allaah. Na wala kuwaoa wake zake baada yake abadani. Hakika jambo hilo mbele ya Allaah ni kubwa mno.[18]

 

 

 

إِن تُبْدُوا شَيْئًا أَوْ تُخْفُوهُ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٥٤﴾

54. Mkidhihirisha kitu chochote au mkikificha, basi hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa kila kitu.

 

 

 

لَّا جُنَاحَ عَلَيْهِنَّ فِي آبَائِهِنَّ وَلَا أَبْنَائِهِنَّ وَلَا إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ أَخَوَاتِهِنَّ وَلَا نِسَائِهِنَّ وَلَا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ ۗ وَاتَّقِينَ اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدًا ﴿٥٥﴾

55. Hamna dhambi juu yao wanawake (kuonekana bila hijaab) mbele ya baba zao, wala watoto wao wa kiume, wala kaka zao, wala watoto wa kiume wa kaka zao, wala watoto wa kiume wa dada zao, wala wanawake wenzao (wa Kiislamu), wala iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah daima Ni Mwenye Kushuhudia kila kitu. 

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٥٦﴾

56. Hakika Allaah na Malaika Wake Wanamswalia Nabiy. Enyi walioamini! Mswalieni na msalimieni kwa maamkizi ya amani.[19]

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يُؤْذُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَأَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿٥٧﴾

57. Hakika wale wanaomuudhi Allaah na Rasuli Wake, Allaah Amewalaani duniani na Aakhirah, na Amewaandalia adhabu ya kudhalilisha. 

 

 

 

وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾

58. Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana.

 

 

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥٩﴾

59. Ee Nabiy! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jilbaab zao.[20] Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane (kwa heshima) wasiudhiwe. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

لَّئِن لَّمْ يَنتَهِ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْمُرْجِفُونَ فِي الْمَدِينَةِ لَنُغْرِيَنَّكَ بِهِمْ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَا إِلَّا قَلِيلًا ﴿٦٠﴾

60. Ikiwa wanafiki, na wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi , na waenezao fitnah katika (mji wa) Madiynah hawatokoma, bila shaka Tutakusalitisha juu yao, kisha hawatokaa humo kuwa jirani zako isipokuwa kidogo tu.

 

 

 

مَّلْعُونِينَ ۖ أَيْنَمَا ثُقِفُوا أُخِذُوا وَقُتِّلُوا تَقْتِيلًا ﴿٦١﴾

61. Maluuni hao!  Popote wanapopatikana, wachukuliwe, na wauliwe wote bila chembe ya huruma.  

 

 

 

سُنَّةَ اللَّـهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلُ ۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّةِ اللَّـهِ تَبْدِيلًا ﴿٦٢﴾

62.  Ni Desturi ya Allaah kwa wale waliopita kabla. Na wala hutopata mabadiliko katika Desturi ya Allaah.[21]

 

 

 

يَسْأَلُكَ النَّاسُ عَنِ السَّاعَةِ ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ اللَّـهِ ۚ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا ﴿٦٣﴾

63. Watu wanakuuliza kuhusu Saa. Sema: Ujuzi wake uko kwa Allaah. Na nini kitakujulisha? Huenda Saa itakuwa karibu.[22]

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَعَنَ الْكَافِرِينَ وَأَعَدَّ لَهُمْ سَعِيرًا ﴿٦٤﴾

64. Hakika Allaah Amewalaani makafiri, na Amewaandalia moto uliowashwa vikali mno.

 

 

 

خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ لَّا يَجِدُونَ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿٦٥﴾

65. Ni wenye kudumu humo abadi. Hawatopata mlinzi wala mwenye kunusuru.

 

 

 

يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّـهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا ﴿٦٦﴾

66. Siku zitakapopinduliwa nyuso zao motoni, watasema: Laiti tungelimtii Allaah, na tungelimtii Rasuli.

 

 

وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا ﴿٦٧﴾

67. Na watasema: Rabb wetu! Hakika sisi tuliwatii mabwana zetu na wakuu wetu, wakatupoteza njia.

 

 

 

رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا ﴿٦٨﴾

68. Rabb wetu! Wape adhabu maradufu, na Walaani laana kubwa.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ آذَوْا مُوسَىٰ فَبَرَّأَهُ اللَّـهُ مِمَّا قَالُوا ۚ وَكَانَ عِندَ اللَّـهِ وَجِيهًا ﴿٦٩﴾

69. Enyi walioamini! Msiwe kama wale waliomuudhi Muwsaa, lakini Allaah Alimtoa tuhumani kutokana na yale waliyoyasema. Na alikuwa mbele ya Allaah mwenye kuheshimika.[23]

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٧٠﴾

70. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na semeni kauli nyofu ya haki.

 

 

 

 

يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا ﴿٧١﴾

71. Atakutengenezeeni amali zenu, na Atakughufurieni madhambi yenu. Na anayemtii Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amefanikiwa mafanikio adhimu.

 

 

 

إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَن يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنسَانُ ۖ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا ﴿٧٢﴾

72. Hakika Sisi Tulihudhurisha amana[24] kwa mbingu na ardhi na majabali, vikakataa kuibeba na vikaiogopa, lakini binaadam aliibeba. Hakika yeye amekuwa dhalimu mno, jahili mno.

 

 

 

لِّيُعَذِّبَ اللَّـهُ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْمُشْرِكِينَ وَالْمُشْرِكَاتِ وَيَتُوبَ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٣﴾

73. Ili Allaah Awaadhibu wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike, na washirikina wa kiume na washirikina wa kike, na Allaah Apokee tawbah ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

 

[1] Amrisho La Kuwaita Watoto Wa Kupanga Kwa Majina Ya Baba Zao Na Sio Kwa Aliyemkafili Kumlea:

 

[2]  Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

033-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Ahzaab Aayah 05: ادْعُوهُمْ لآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِنْدَ اللَّهِ

 

[3] Kumpenda Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuliko Nafsi Yake Mtu

 

Mapenzi ya Waumini kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) yanapaswa kuwa makubwa zaidi kuliko mtu kujipenda mwenyewe. Na ndipo ikawa imaan ya Muislamu haitimii mpaka iwe kumpenda Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni zaidi kuliko anavyoipenda nafsi yake. Miongoni mwa Hadiyth zenye mada hii ni hizi zifuatazo

 

عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللّه عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قال: ((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكونَ أحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ وَوَلَدِه وَالنَّاسِ أَجْمَعينَ )) متفق عليه

Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه):  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hatoamini mmoja wenu mpaka niwe (mimi Muhammad) kipenzi chake kuliko mwanawe na wazazi wake na kuliko watu wote waliobakia.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na ‘Umar (رضي الله عنه) aliyathibitisha mapenzi ya kumpenda Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuliko nafsi yake:

 

عبد اللَّهِ بْنَ هِشَامٍ قَالَ، كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ آخِذٌ بِيَدِ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ فَقَالَ لَهُ عُمَرُ يَا رَسُولَ اللَّهِ لأَنْتَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنْ كُلِّ شَىْءٍ إِلاَّ مِنْ نَفْسِي‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((لاَ وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْكَ مِنْ نَفْسِكَ)) فَقَالَ لَهُ عُمَرُ فَإِنَّهُ الآنَ وَاللَّهِ لأَنْتَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنْ نَفْسِي‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((الآنَ يَا عُمَرُ))

Amesimulia ‘Abdullaah bin Hishaam (رضي الله عنه):  Tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) naye ameushika mkono wa ‘Umar bin Al-Khattwaab. ‘Umar akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, hakika wewe ni kipenzi zaidi kwangu kuliko kitu chochote isipokuwa nafsi yangu.  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hapana, (haiwezekani hivyo). Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, mpaka niwe kipenzi zaidi kwako kuliko nafsi yako.” ‘Umar (رضي الله عنه)  akamwambia:  Basi kwa sasa Wa-Allaahi wewe ni kipenzi zaidi kwangu kuliko nafsi yangu. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hivi sasa ee ‘Umar (umekuwa Muumini wa kweli).” [Al-Bukhaariy]

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رضى الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ‏ ((مَا مِنْ مُؤْمِنٍ إِلاَّ وَأَنَا أَوْلَى النَّاسِ بِهِ فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، اقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ‏: ((النَّبِيُّ أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنْفُسِهِمْ‏))‏ فَأَيُّمَا مُؤْمِنٍ تَرَكَ مَالاً فَلْيَرِثْهُ عَصَبَتُهُ مَنْ كَانُوا، فَإِنْ تَرَكَ دَيْنًا أَوْ ضِيَاعًا فَلْيَأْتِنِي وَأَنَا مَوْلاَهُ))  البخاري   

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna Muumini yeyote isipokuwa mimi nina haki zaidi kwake (ya kupendwa na kutiiwa) kuliko watu wote duniani na Aakhirah. Someni mkipenda:

 

النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ ۖ  

“Nabiy ana haki zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao.” [Al-Ahzaab (33:6)] 

 

Na Muumini yeyote aliyeacha mali basi na warithi jamaa zake waliopo. Na ikiwa ameacha deni au watoto masikini, basi na waje kwangu (niwalipie madeni yao na niwahudumie), mimi ni mlinzi wao.”  [Al-Bukhaariy] 

 

[4] Wake Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Mama Wa Waumini:

 

Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ndiye mwenye kupewa kipaumbele zaidi kwa Waumini, na ndiye aliye karibu na wao zaidi kuliko nafsi zao katika mambo ya Dini na dunia. Na heshima ya wake za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ummah wake, ni kama vile heshima ya mama zao, kwani haifai kuwaoa wake za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) milele baada yake. Na wenye ujamaa wa ukaribu, miongoni mwa Waislamu, baadhi yao wana haki zaidi ya kuwarithi wengine katika hukumu ya Allaah na Sharia Yake kuliko kurithi kwa misingi ya imaan na hijrah (uhamiaji). Waislamu hapo mwanzo wa Uislamu walikuwa wakirithiana kwa misingi ya hijrah na imaan au Dini, na si kwa kizazi, kisha hilo likaondolewa kwa Aayah ya Mirathi. [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

Hapa Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaambia Waumini jambo liwatambulishe daraja ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ili waweze kutaamali naye ipasavyo. Jambo la karibu zaidi kwa mtu yeyote ni nafsi yake, lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anatakiwa awe karibu naye zaidi kuliko nafsi yake, kwa sababu yeye aliwanasihi kidhati, na alikuwa na huruma mno kwao na wema.  Akathibitisha kuwa yeye ni mwenye zaidi na fadhila kuliko watu wote. Basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ndiye kiumbe mwenye fadhila kubwa zaidi kwao kuliko viumbe vyote, na ndiye mkarimu na mpole zaidi kwao kwani haikuwafikia uzito wa chembe ya kheri, wala hawakuepushwa uzito wa chembe ya madhara isipokuwa kwa sababu yake.

 

Kwa sababu hiyo, inawajibika kwao pindi utakapotofautiana muradi (makusudio) wa nafsi au muradi wa yeyote yule, ukatofautiana na muradi wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), basi utangulizwe wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na wala isipingwe kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kauli ya mtu yeyote yule, vyovyote atakavyokuwa. Watu wamtolee fidia nafsi zao, mali zao na watoto wao. Na watangulize mapenzi ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuliko mapenzi ya kiumbe chochote, na wasiongee mpaka aongee, na wasitangulie mbele yake (wasitangulize kauli ya yeyote). 

 

Na yeye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni baba wa Waumini, kama ilivyo katika Qiraa-a cha baadhi ya Swahaba, akiwa anawalea kama mzazi anavyomlea mtoto wake. Ndio ikapelekea kwa ubaba huu kuwa wake zake ni mama zao (Waumini), yaani, katika uharamu wa kuwaoa, kuwaheshimu na kuwakirimu, sio kwamba wakae nao faragha kama ni maharim zao (hapana). Haya maneno kama vile ni utangulizi wa maelezo yanayokuja yakihusu kisa cha Zayd bin Haarithah, ambae alikuwa kabla ya hapo akiitwa “Zayd Bin Muhammad” mpaka Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ  

“Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu.” [Al-Ahzaab (33:40)]

 

Ikakatwa nasaba yake, na kunasibishwa kwake, na Allaah Akahabarisha katika Aayah hii, ya kwamba, Waumini wote ni watoto wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hakuna yeyote atakayemzidi hadhi mwingine katika hili hata ikikatika nasaba ya kujinasibisha, kwani nasaba ya kiimani haikukatika, hivyo asihuzunike wala asisikitike.

 

Na kwa kuwa wake za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) washakuwa ni Mama wa Waumini wote, kwa msingi huu, hawahalaliki kuolewa na yeyote baada ya kuolewa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kama Alivyobainisha hilo Allaah (سبحانه وتعالى):

  وَلَا أَن تَنكِحُوا أَزْوَاجَهُ مِن بَعْدِهِ أَبَدًا ۚ  

“Na wala kuwaoa wake zake baada yake abadani.” [Al-Ahzaab (33:53)]

[Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[5] Rusuli Wa Ulul-‘Azmi (Wenye Azimio La Nguvu).

 

Rusuli hao watano waliotajwa wanajulikana kuwa ni Ulul-‘Azmi. Wameitwa hivi kwa sababu walikuwa ni wenye azimio la nguvu baada ya kuchukua ahadi  ngumu ya kubalighisha Risala na kufanya Jihaad katika Njia ya Allaah, kwa subira ya hali ya juu. Hivyo ni kutokana na kusumbuliwa na kukanushwa kwao na watu wao, wakapata mitihani na mashaka makubwa, hadi wengine kufukuzwa na watu wao na kutaka kudhuriwa na kuuliwa. Rejea Al-Ahqaaf (46:35). Rejea pia An-Nisaa (4:69) kwenye maelezo bayana kuhusu Rusuli kuwa na daraja la juu zaidi kulingana na Manabii kwa sababu ya subira zao katika kulingania Dini ya Allaah (سبحانه وتعالى).

 

[6] Ghazwat Al-Ahzaab (Vita Vya Makundi Yaliyoshirikiana) Au Al-Khandaq Handaki):

 

Vita vitukufu vya Al-Ahzaab au Al-Khandaq vimetajwa takriban kuanzia Aayah ya (9) hadi  ya (25) katika Suwrah hii ya Al-Ahzaab. 

 

Vita vya Al-Ahzaab au Al-Khandaq, ni vita vilivyopiganwa mwezi wa Shawwaal katika mwaka wa tano wa Hijriyyah. Vita vilikuwa kati ya Waislam wakiongozwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Ahzaab ambao ni mkusanyiko wa makabila mbalimbali ya Waarabu, wakiwemo Maquraysh wa Makkah ambao waliungana pamoja kwa lengo la kuipiga Madiynah na kuwamaliza Waislamu.

 

Baadhi ya matukio ya Vita vya Al-Ahzaab au Khandaq yametajwa katika Aayah hizo na maelezo ziyada ni kama yafuatayo:

 

Sababu ya Vita Kuitwa Khandaq (Handaki) ni kutokana na ushauri wa Swahaba mtukufu Salmaan Al-Faarisiy (رضي الله عنه) .

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na Swahaha zake walichimba handaki hilo kwa mikono yao kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

حَدَّثَنِي أَحْمَدُ بْنُ عُثْمَانَ، حَدَّثَنَا شُرَيْحُ بْنُ مَسْلَمَةَ، قَالَ حَدَّثَنِي إِبْرَاهِيمُ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبِي، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، قَالَ سَمِعْتُ الْبَرَاءَ، يُحَدِّثُ قَالَ لَمَّا كَانَ يَوْمُ الأَحْزَابِ، وَخَنْدَقَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم رَأَيْتُهُ يَنْقُلُ مِنْ تُرَابِ الْخَنْدَقِ حَتَّى وَارَى عَنِّي الْغُبَارُ جِلْدَةَ بَطْنِهِ، وَكَانَ كَثِيرَ الشَّعَرِ، فَسَمِعْتُهُ يَرْتَجِزُ بِكَلِمَاتِ ابْنِ رَوَاحَةَ، وَهْوَ يَنْقُلُ مِنَ التُّرَابِ يَقُولُ اللَّهُمَّ لَوْلاَ أَنْتَ مَا اهْتَدَيْنَا وَلاَ تَصَدَّقْنَا وَلاَ صَلَّيْنَا فَأَنْزِلَنْ سَكِينَةً عَلَيْنَا وَثَبِّتِ الأَقْدَامَ إِنْ لاَقَيْنَا إِنَّ الأُلَى قَدْ بَغَوْا عَلَيْنَا وَإِنْ أَرَادُوا فِتْنَةً أَبَيْنَا قَالَ ثُمَّ يَمُدُّ صَوْتَهُ بِآخِرِهَا‏.‏

Amesimulia Al-Baraa (رضي الله عنه):  Wakati wa siku ya (Vita vya) Al-Ahzaab (makundi yaliyoshirikiana), na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaingia katika kazi ya kuchimba handaki, nilikuwa namwona akiutoa nje udongo wa handaki mpaka vumbi lake likanifanya nisiweze kuona tena ngozi ya tumbo lake. Na alikuwa mwenye nywele nyingi. Nikamsikia akisoma maneno ya Ibn Rawaahah huku akiwa amebeba udongo, akisema: “Ee Allaah! Bila ya Wewe, tusingehidika, wala tusingetoa swadaqa, wala tusingeswali. Basi Tuteremshie utulivu na Imarishe miguu yetu kama tutakabiliana na adui. Hakika wao wametufanyia dhulma na kama watataka kutufanyia fitnah, basi hatutokubali.” Halafu akawa anavuta sauti yake mwishoni mwake. [Al-Bukhaariy].

 

Uchimbaji wa Khandaq kuizunguka Madiynah ndio ilikuwa sababu ya Ushindi kwa Waislamu, kutokana na kuwazuia maadui wasiweze kuingia. Baada ya Ahzaab (makundi yaliyoshirikiana) kufika kwenye mipaka ya Madiynah walishindwa kuingia, na hapo wakaamua kuuzingira mji. Na zingiro hili liliendelea kwa muda wa wiki tatu, na ilipelekea hali hii kwa Waislam kupata maudhi, mashaka, kiu na njaa. Lakini Waislamu hawakukata tamaa na wala hawakujisalimisha kwa maadui zao, bali walivuta subira mpaka Allaah (سبحانه وتعالى) Akawajaalia ushindi dhidi ya maadui wao.

 

Vita vya Khandaq vilimalizika kwa kujiondoa kwao Ahzaab (makundi yaliyoshirikiana), hali iliyosababishwa na kupigwa na upepo mkali wa baridi. Na Waislamu wanaamini kuwa ushindi wao katika Vita vya Khandaq ulikuwa kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى)

 

Aliitingisha miili na nyoyo za Ahzaab, Akasambaratisha muungano wao kwa kutofautiana wenyewe kwa wenyewe. Akatia khofu kwenye nyoyo zao, na Akateremsha jeshi kutoka Kwake wasioonekana ambao ni Malaika. Na baada ya kumalizika Vita, Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaamrisha Swahaba zake kuelekea kwa Baniy Quraydhwah. Wakaenda na wakawazingira mpaka wakajisalimisha. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasimama kwa kumteua mtu waliyemridhia atoe hukumu, naye alikuwa Sa’ad Bin Muaadh (رضي الله عنه)  ambae alikuwa mwenzao kabla ya Uislamu. Akatoa hukumu ya kuuwawa wapiganaji wao na kutawanywa wanawake na watoto wao, wakiwa watumwa kwa Waislamu. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), alitoa amri ya kupitishwa hukumu hiyo.

 

Sababu Ya Kutokea Vita Hivi:

 

Sababu ya Vita hivi ni kutolewa kwa Mayahudi wa Baniy An-Nadhwiyr katika mji wa Madiynah, kiasi kwamba hasadi na chuki zilitawala katika nyoyo zao. Nayo ni katika mambo ambayo yaliwafanya wawe wanadhamiria kufanya uadui kwa Waislamu.

 

Na pia sababu ya Vita vya Khandaq ni kwamba Mayahudi wa Baniy Nadhwiyr walivunja ahadi yao pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na walifanya hila ya kutaka kumuua. Akawapelekea jeshi lake, likawazingira mpaka wakajisalimisha. Matokeo ya jambo hilo ni kudhamiria Mayahudi wa Baniy An-Nadhwiyr kulipiza kisasi kwa Waislamu. Wakaanza kushawishi makabila ya Kiarabu kuipiga Vita Madiynah. Waliowakubalia katika Waarabu ni kabila la Maquraysh, na wale wenzao akina Kinaanah (Wahabeshi), Kabila ya Ghatwfaan (Fazaarah, na Baniy Murrah, na Ashja’a), na wenzao ambao ni Baniy Asad, na Sulaym na wengineo. Ndio maana wakaitwa Ahzaab (makundi yaliyoshirikiana), kisha wakajiunga nao Mayahudi wa Baniy Quraydhwah, ambao walikuwa na ahadi ya amani kati yao na Waislamu.

 

[7] Nyoyo Zenye Maradhi:

 

(i) Nyoyo Zenye Maradhi: Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali. Na rejea pia Suwrah hii Al-Ahzaab (33:32), (33:60).

 

(ii) Moyo Uliopofuka: Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo bayana.

 

(iii) Moyo Uliosalimika: Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye maelezo bayana.

 

[8] Kufuata Kigezo Cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

Kufuata kigezo cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kufuata Sunnah zake na hii ni waajib kwa Muislamu kama Anavyosema Allaah katika Aayah hii tukufu. 

 

Na Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: “Mwenye kufuata kigezo chake, amefuata njia ya kumfikisha katika Utukufu wa Allaah, na hiyo ndio Njia Iliyonyooka. Na kigezo hicho kizuri hukifuata na kupata tawfiyq kila yule mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho, kwa sababu ya kuwa kwake na iymaan, khofu ya Allaah, kutaraji thawabu na khofu ya adhabu Yake, huyu hujihimiza kufuata kigezo cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).” [Tafsiyr As-Sa’dy]

 

[11] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Aayah kuanzia hii namba (28) hadi (29), panaelezwa kuhusu wake wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na matukio yaliyotokea ambayo pia yanahusiana na Aayah za Suwrah At-Tahriym (66:1-5).

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

033-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Ahzaab Aayah 28-29: يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ إِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا

 

[12] Haramisho Kwa Wanawake Kulegeza Sauti Wanapoongea Na Wanaume:

 

Amrisho hili ni kwa wakeze Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na pia wanawake Waumini kuwa wanapoongea na wanaume, wasiwe wanaongea kwa sauti laini ya kupendezesha ili isije kusababisha fitnah kwa wanaume kuvutiwa na wanawake.

 

[15] Maana Ya Swalaah Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Waja Wake Na Swalaah Ya Malaika Kwa Waja:

 

Swalaah ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa waja Wake ni Rehma na kuwasifia kwa Malaika. Na Swalaah ya Malaika kwa wanaadam ni kuwaombea duaa na maghfirah. Pia Rejea Al-Faatihah (1:1) kupata tofauti ya Jina na Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym

 

[16] Maamkizi Jannah (Peponi) Ni “Salaam” (Amani!):

 

Rejea Yaasiyn (36:58), Ar-Ra’d (13:24), Yuwnus (10:10), Ibraahiym (14:23), An-Nahl (16:32).

 

[19] Maana Ya Allaah (سبحانه وتعالى)  Na Malaika Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):   

 

Maana ya Allaah (سبحانه وتعالى) kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), ni kumsifia kwa Malaika, kumteremshia Rehma na Baraka, Fadhila n.k. Ama Malaika Wake kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), ni kumuombea kwa Allaah (سبحانه وتعالى) duaa Amghufurie na Amteremshie baraka.  

 

Vipi Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

عن أَبي مسعودٍ البدري رضي الله عنه ، قَالَ : أتَانَا رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وَنَحنُ في مَجْلِسِ سَعدِ بن عُبَادَةَ رضي الله عنه ، فَقَالَ لَهُ بَشْيرُ بْنُ سَعدٍ : أمَرَنَا الله تَعَالَى أنْ نُصَلِّي عَلَيْكَ يَا رَسُولَ اللهِ ، فَكَيْفَ نُصَلِّي عَلَيْكَ ؟ فَسَكَتَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، حَتَّى تَمَنَّيْنَا أنَّهُ لَمْ يَسْأَلْهُ ، ثُمَّ قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( قُولُوا : اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ ، وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ ، كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى آلِ إبْرَاهِيمَ ، وَبَارِكْ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ ، كَمَا بَارَكْت عَلَى آلِ إبْرَاهِيمَ ، إنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ ، وَالسَّلاَمُ كَمَا قَدْ عَلِمْتُمْ )) . رواه مسلم .

Amesimulia Abuu Mas'uwd Al-Badriy (رضي الله عنه): Alitujia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na sisi tulikuwa katika majlisi ya Sa'ad bin 'Ubaadah (رضي الله عنه). Bashiyr bin Sa'ad akamwambia: Allaah Ametuamrisha tukuswalie ee Rasuli wa Allaah. Je, vipi tukuswalie? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanyamaza mpaka tukatamani kwamba asingelimuuliza. Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: Semeni:

 

اللَّهمَّ صلِّ عَلى مُحَمَّدٍ، وَعَلى آلِ مُحمَّدٍ، كما صليْتَ على آل إبْراهِيم، وَبارِكْ عَلى مُحَمَّد، وعَلى آلِ مُحمَّد، كما بَاركْتَ عَلى آل إبْراهِيم، إنكَ حمِيدٌ مجِيدٌ،

Allaahumma Swalli 'alaa Muhammadin wa 'alaa aali Muhammadin kamaa Swallayta 'alaa aali Ibraahiym, wa Baarik 'alaa Muhammadin wa 'alaa aali Muhammadin kama Baarakta 'alaa aali Ibraahiym Innaka Hamiydun-Majiyd. Na salaam kama mlivyofundishwa.” [Muslim]

 

Fadhila Za Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni katika ibaada tukufu yenye fadhila adhimu kwa kuwa ni ibaada Aliyojihusisha nayo Allaah (سبحانه وتعالى) na Malaika Wake. Na fadhila kadhaa zimethibiti za kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Mojawapo ya fadhila ni kwamba, ukimswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) mara moja, Allaah (سبحانه وتعالى) Anakuswalia mara kumi kwa Hadiyth ifuatayo:

 

عنْ عبد اللَّه بن عمرو بن العاص رضي اللَّه عنْهُمَا أنَّهُ سمِع رسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ: ((مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً، صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عشْراً))  رواهُ مسلم

Amesimulia 'Abdullaah bin 'Amru bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Atakayeniswalia mara moja, Allaah Atamswalia mara kumi.” [Muslim]

 

[20] Hijaab Na Masharti Yake:

 

(i) Jilbaab liwe refu la kukufunika mwili mzima mpaka miguu, na kama halikufunika miguu basi mwanamke avae soksi.  (ii) Jilbaab liwe pana na sio lenye kuonyesha umbo, yaani lisiwe lenye kubana popote mwilini. (iii) Jilbaab liwe zito na si jepesi la kuonyesha mwili. (iv)  Jilbaab lisiwe na marembo yoyote yale ya kuvutia. (v) Jilbaab halitakiwi lifanane na mavazi ya makafiri. (vi) Jilbaab halitakiwi liwe ni katika mavazi ya fakhari. (vii) Wanawake wasivae nguo zinazofanana na nguo za kiume. (viii) Nguo zote anazovaa mwanamke zisiwe na manukato.

 

Rejea An-Nuwr (24:31).

 

[21] Desturi Ya Allaah Ya Adhabu Kwa Makafiri Na Nusra Kwa Waumini: 

 

Rejea Aal-‘Imraan (3:137).

 

[22] Ada Ya Makafiri Kuuliza Qiyaamah Kitatokea Lini Na Kuhimiza Adhabu:

 

Rejea Al-An’aam (6:158), Al-A’raaf (7:187), An-Naazi’aat (79:42), Al-Mulk (67:25), Ash-Shuwraa (42:18).

 

Na wakihimiza adhabu: Rejea Al-Hajj (22:47), Swaad (38:16), Al-Anfaal (8:32-33).

 

[23] Tuhuma Alizopachikwa Nabiy Muwsaa :(عليه السّلام)

 

Maelezo yamethibiti katika Hadiyth:

 

حَدَّثَنِي إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا رَوْحُ بْنُ عُبَادَةَ، حَدَّثَنَا عَوْفٌ، عَنِ الْحَسَنِ، وَمُحَمَّدٍ، وَخِلاَسٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ إِنَّ مُوسَى كَانَ رَجُلاً حَيِيًّا سِتِّيرًا، لاَ يُرَى مِنْ جِلْدِهِ شَىْءٌ، اسْتِحْيَاءً مِنْهُ، فَآذَاهُ مَنْ آذَاهُ مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ، فَقَالُوا مَا يَسْتَتِرُ هَذَا التَّسَتُّرَ إِلاَّ مِنْ عَيْبٍ بِجِلْدِهِ، إِمَّا بَرَصٌ وَإِمَّا أُدْرَةٌ وَإِمَّا آفَةٌ‏.‏ وَإِنَّ اللَّهَ أَرَادَ أَنْ يُبَرِّئَهُ مِمَّا قَالُوا لِمُوسَى فَخَلاَ يَوْمًا وَحْدَهُ فَوَضَعَ ثِيَابَهُ عَلَى الْحَجَرِ ثُمَّ اغْتَسَلَ، فَلَمَّا فَرَغَ أَقْبَلَ إِلَى ثِيَابِهِ لِيَأْخُذَهَا، وَإِنَّ الْحَجَرَ عَدَا بِثَوْبِهِ، فَأَخَذَ مُوسَى عَصَاهُ وَطَلَبَ الْحَجَرَ، فَجَعَلَ يَقُولُ ثَوْبِي حَجَرُ، ثَوْبِي حَجَرُ، حَتَّى انْتَهَى إِلَى مَلإٍ مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ، فَرَأَوْهُ عُرْيَانًا أَحْسَنَ مَا خَلَقَ اللَّهُ، وَأَبْرَأَهُ مِمَّا يَقُولُونَ، وَقَامَ الْحَجَرُ فَأَخَذَ ثَوْبَهُ فَلَبِسَهُ، وَطَفِقَ بِالْحَجَرِ ضَرْبًا بِعَصَاهُ، فَوَاللَّهِ إِنَّ بِالْحَجَرِ لَنَدَبًا مِنْ أَثَرِ ضَرْبِهِ ثَلاَثًا أَوْ أَرْبَعًا أَوْ خَمْسًا، فَذَلِكَ قَوْلُهُ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَكُونُوا كَالَّذِينَ آذَوْا مُوسَى فَبَرَّأَهُ اللَّهُ مِمَّا قَالُوا وَكَانَ عِنْدَ اللَّهِ وَجِيهًا ‏‏"‏

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Muwsaa alikuwa ni mtu mwenye haya mno na anayejisitiri sana. Ngozi yake haionekani kabisa kwa ajili ya haya yake. Mmoja miongoni mwa Bani Israaiyl alimuudhi kwa kumwambia: Anajifinika hivi kwa sababu ya ila ya ngozi yake, ima ni kwa sababu ya ukoma au ngiri ya korodani au aibu nyenginezo. Allaah Alitaka kumtoa katika hayo waliyokuwa wakiyasema. Kwa hiyo, siku moja Muwsaa alipokuwa peke yake, alivua nguo zake, akaziweka juu ya jiwe na akaanza kuoga. Alipomaliza kuoga, alitembea kuzielekea nguo zake ili kuzichukua, lakini jiwe hilo lilichukua nguo zake na kukimbia nazo. Muwsaa alichukua fimbo yake na kulikimbiza hilo jiwe huku akisema: Ewe jiwe! Nipatie nguo zangu! Mpaka akafika kwenye kikundi cha Bani Israaiyl waliomuona akiwa uchi, na kumuona kuwa ni kiumbe mzuri mno miongoni mwa walioumbwa na Allaah. Hivyo, Allaah Akamtakasa kwa waliyokuwa wakimtuhumu nayo. Jiwe lilisimama hapo, na Muwsaa alichukua na kuvaa nguo zake na akaanza kulipiga kichapo hilo jiwe kwa fimbo yake. Naapa kwa Allaah! Jiwe hilo hadi sasa lina alama ya kichapo, alama tatu au nne au tano. Na hiyo ndiyo Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ آذَوْا مُوسَىٰ فَبَرَّأَهُ اللَّـهُ مِمَّا قَالُوا ۚ وَكَانَ عِندَ اللَّـهِ وَجِيهًا ﴿٦٩﴾

Enyi walioamini! Msiwe kama wale waliomuudhi Muwsaa, lakini Allaah Alimtoa tuhumani kutokana na yale waliyoyasema. Na alikuwa mbele ya Allaah mwenye kuheshimika.” [Al-Ahzaab (33:69)]

 

[24] Amana:

 

Kutimiza amana ni miongoni mwa sifa zitakazompatia Muislamu Jannah ya Firdaws kama zilivyotajwa katika Suwrah: Al-Muuminuwn (23: 1-11), Al-Ma’aarij (70:32).

 

Na maudhui hii ya amana ni pana mno, na kuna Hadiyth mbalimbali zinazotaja jambo hili la amana. Na ‘Ulamaa pia wametaja maana na tafsiri mbalimbali kuhusu maana yake. 

 

Rejea Alhidaaya.com katika viungo vifuatavo kupata faida tele:

025-Riyaadhw As-Swaalihiyn: Mlango Wa Amri Ya kurudisha Amana

Amana Katika Uislam

Na miongoni mwa amana ni kutekeleza ahadi, kurudisha kitu alichokabidhiwa mtu, kulipa alichokopa, kutokufanya khiyana na kadhaalika. Mfano ni Hadiyth:

 

Samurah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Rudisha amana kwa aliyekuaminisha na wala usimfanyie khiyana aliyekukhini.” [Ahmad, Swahiyh Abiy Daawuwd (3535), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (423)].

 

Na kutokutimiza amana ni miongoni mwa alama za Qiyaamah kwa kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mtu aliyemuuliza lini Qiyaamah kitasimama kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo:

 

عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : بَيْنَمَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم في مَجْلِسٍ يُحَدِّثُ القَومَ ، جَاءَ أَعْرَابِيٌّ فَقَالَ : مَتَى السَّاعَةُ ؟ فَمَضَى رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يُحَدِّثُ ، فَقالَ بَعْضُ القَومِ : سَمِعَ مَا قَالَ فَكَرِهَ مَا قَالَ ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ : بَلْ لَمْ يَسْمَعْ ، حَتَّى إذَا قَضَى حَدِيثَهُ قالَ : أيْنَ السَّائِلُ عَنِ السَّاعَةِ ؟ )) قال : هَا أنا يَا رسُولَ اللهِ . قال : (( إذَا ضُيِّعَتِ الأَمَانَةُ فَانْتَظِرِ السَّاعَةَ )) قال : كَيفَ إضَاعَتُهَا ؟ قال : (( إذَا وُسِّدَ الأَمْرُ إلى غَيْرِ أَهْلِهِ فَانْتَظِرِ السَّاعَةَ )) . رواه البخاري .

Amesimulia Abuu Huraiyrah (رضي الله عنه):  Alipokuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anahotubia kikao cha watu, mara akaja mbedui na kuuliza: Je, Qiyaamah kitakuwa lini?  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea na mazungumzo yake. Hapo wakasema baadhi ya watu: Amesikia alichoulizwa, lakini akachukia kukatizwa. Na wengine wakasema: Bali hajasikia. Mpaka alipomaliza mazungumzo yake, akasema: "Yu wapi muulizaji kuhusu Qiyaamah?" Akajibu: Nipo hapa, ee Rasuli wa Allaah. Akasema: "Inapopotezwa amana (kukawa na khiyana) basi ngojeeni Qiyaamah." Akaulizwa: Na itapotea vipi? Akasema: "Pindi uongozi unapopatiwa watu wasio stahiki basi ngojeeni Qiyaamah." [Al-Bukhaariy]

 

Na amana pia inaingia katika kutekeleza majukumu ya mtu aliyokabidhiwa, kama kuchunga kilichokuwa chini ya ulezi au jukumu lake. Hadiyth ifuatayo inaashiria hili: 

 

عَنْ ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قَالَ:  ((كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ،  وَالأمِيرُ رَاعٍ،  وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ، وَالْمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى بَيْتِ زَوْجِهَا وَوَلَدِهِ، فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ)) متفق  عليه

Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله  عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nyote ni wachunga na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga. Kiongozi ni mchunga, na mume ni mchunga juu ya mkewe na mke ni mchunga juu ya nyumba ya mumewe na watoto wake. Kwa hivyo nyote ni wachunga na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share