004 - An-Nisaa

 

 

النِّسَاء

004-An-Nisaa

 

 

004-An-Nisaa: Utangulizi Wa Suwrah

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا ﴿١﴾ 

1. Enyi watu! Mcheni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Aadam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawwaa) na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume na wanawake wengi. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana (haki zenu kwa kuunga) undugu.[1] Hakika Allaah daima Ni Mwenye Kuwachungeni.

 

 

وَآتُوا الْيَتَامَىٰ أَمْوَالَهُمْ ۖ وَلَا تَتَبَدَّلُوا الْخَبِيثَ بِالطَّيِّبِ ۖ وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَهُمْ إِلَىٰ أَمْوَالِكُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ حُوبًا كَبِيرًا ﴿٢﴾ 

2. Na wapeni mayatima mali zao, wala msibadilishe kibaya (chenu) kwa kizuri (chao). Na wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika hilo limekuwa ni dhambi kubwa.  

 

 

 

وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا ﴿٣﴾

3. Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima, basi oeni waliokupendezeni katika wanawake (wengine); wawili au watatu au wanne. Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki.[2] Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea kudhulumu.

 

 

وَآتُوا النِّسَاءَ صَدُقَاتِهِنَّ نِحْلَةً ۚ فَإِن طِبْنَ لَكُمْ عَن شَيْءٍ مِّنْهُ نَفْسًا فَكُلُوهُ هَنِيئًا مَّرِيئًا ﴿٤﴾ 

4. Na wapeni wanawake mahari zao kwa maridhawa. Lakini wakitoa chochote wenyewe katika mahari yao kwa khiari zao, basi kuleni kwa kufurahia na kunufaika.

 

 

وَلَا تُؤْتُوا السُّفَهَاءَ أَمْوَالَكُمُ الَّتِي جَعَلَ اللَّـهُ لَكُمْ قِيَامًا وَارْزُقُوهُمْ فِيهَا وَاكْسُوهُمْ وَقُولُوا لَهُمْ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٥﴾ 

5. Wala msiwape wasiokomaa kiakili mali yenu ambayo Allaah Ameijaalia kuwa ni kisaidizi chenu cha maisha, na walisheni humo na wavisheni na waambieni maneno ya haki na kwa huruma.

 

 

وَابْتَلُوا الْيَتَامَىٰ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغُوا النِّكَاحَ فَإِنْ آنَسْتُم مِّنْهُمْ رُشْدًا فَادْفَعُوا إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ ۖ وَلَا تَأْكُلُوهَا إِسْرَافًا وَبِدَارًا أَن يَكْبَرُوا ۚ وَمَن كَانَ غَنِيًّا فَلْيَسْتَعْفِفْ ۖ وَمَن كَانَ فَقِيرًا فَلْيَأْكُلْ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِذَا دَفَعْتُمْ إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ فَأَشْهِدُوا عَلَيْهِمْ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٦﴾

6. Na wajaribuni mayatima (akili zao) mpaka wakifikia umri wa kuoa. Na mkihisi kupevuka kwao, basi wapeni mali zao. Wala msiile kwa israfu na pupa kwa (kuhofia) kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliyekuwa tajiri, ajizuilie (kuchukua ujira), na aliyekuwa fakiri basi ale kwa kadiri ya kukubalika kisharia. Mtapowapa mali zao washuhudizeni. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mwenye Kuhisabu.

 

 

لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنْهُ أَوْ كَثُرَ ۚ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿٧﴾

7. Wanaume wana fungu katika yale waliyoacha wazazi na jamaa wa karibu. Na wanawake wana fungu katika yale waliyoacha wazazi na jamaa wa karibu, ikiwa ni kidogo au kingi. Ni fungu la kisharia lilofaridhishwa.

 

 

 وَإِذَا حَضَرَ الْقِسْمَةَ أُولُو الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينُ فَارْزُقُوهُم مِّنْهُ وَقُولُوا لَهُمْ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٨﴾

8. Na wakati wa kugawa, wakihudhuria jamaa wa karibu na mayatima na masikini, basi wapeni kitu katika hayo na wasemezeni kauli njema ya haki na kwa huruma.

 

 

وَلْيَخْشَ الَّذِينَ لَوْ تَرَكُوا مِنْ خَلْفِهِمْ ذُرِّيَّةً ضِعَافًا خَافُوا عَلَيْهِمْ فَلْيَتَّقُوا اللَّـهَ وَلْيَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٩﴾ 

9. Na waogope (wasimamizi kukhini) wale ambao lau nao wangeliacha nyuma yao dhuriya dhaifu, wangeliwakhofia. Basi wamche Allaah na waseme kauli iliyo sawa ya haki.

 

 

 إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا ﴿١٠﴾

10. Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma hapana shaka kwamba wanakula katika matumbo yao moto, na watauingia moto uliowashwa vikali mno.

 

 

يُوصِيكُمُ اللَّـهُ فِي أَوْلَادِكُمْ ۖ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۚ فَإِن كُنَّ نِسَاءً فَوْقَ اثْنَتَيْنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَ ۖ وَإِن كَانَتْ وَاحِدَةً فَلَهَا النِّصْفُ ۚ وَلِأَبَوَيْهِ لِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُ وَلَدٌ ۚ فَإِن لَّمْ يَكُن لَّهُ وَلَدٌ وَوَرِثَهُ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ الثُّلُثُ ۚ فَإِن كَانَ لَهُ إِخْوَةٌ فَلِأُمِّهِ السُّدُسُ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِي بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ لَا تَدْرُونَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ لَكُمْ نَفْعًا ۚ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١١﴾ 

11. Allaah Anakuamrisheni kuhusu watoto wenu. Mwanamume atastahiki mfano wa fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake ni zaidi ya wawili basi watastahiki theluthi mbili za alichoacha (maiti). Lakini akiwa mtoto wa kike ni mmoja pekee basi atastahiki nusu, na wazazi wake wawili kila mmoja wao atastahiki sudusi katika alichoacha ikiwa anaye mtoto. Na ikiwa hakuwa na mtoto na wazazi wake wawili ndio warithi wake, basi mama yake atastahiki theluthi moja. Na ikiwa anao ndugu, basi mama yake atastahiki sudusi, baada ya kutoa wasia aliousia (maiti) au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu, hamjui ni yupi miongoni mwao aliye karibu zaidi kwenu kwa manufaa. Ni sharia kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

وَلَكُمْ نِصْفُ مَا تَرَكَ أَزْوَاجُكُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٌ فَلَكُمُ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْنَ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِينَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۚ وَلَهُنَّ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْتُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّكُمْ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَكُمْ وَلَدٌ فَلَهُنَّ الثُّمُنُ مِمَّا تَرَكْتُم ۚ مِّن بَعْدِ وَصِيَّةٍ تُوصُونَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ وَإِن كَانَ رَجُلٌ يُورَثُ كَلَالَةً أَوِ امْرَأَةٌ وَلَهُ أَخٌ أَوْ أُخْتٌ فَلِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ ۚ فَإِن كَانُوا أَكْثَرَ مِن ذَٰلِكَ فَهُمْ شُرَكَاءُ فِي الثُّلُثِ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصَىٰ بِهَا أَوْ دَيْنٍ غَيْرَ مُضَارٍّ ۚ وَصِيَّةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَلِيمٌ ﴿١٢﴾

12. Nanyi mtastahiki nusu katika walichoacha wake zenu ikiwa hawakuwa na mtoto. Na ikiwa wana mtoto, basi mtastahiki robo katika walichoacha, baada ya kutoa wasia waliyousia au kulipa deni. Nao wake zenu watastahiki robo katika mlichoacha ikiwa hamna mtoto. Na ikiwa mna mtoto, basi watastahiki thumni katika mlichoacha, baada ya kutoa wasia mliousia au kulipa deni. Na ikiwa mwanamume au mwanamke anayerithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye kaka au dada, basi kila mmoja kati yao atastahiki sudusi. Na wakiwa ni wengi ya hivyo, basi watashirikiana katika theluthi, baada ya kutoa wasia uliousiwa na kulipwa deni pasipo kuleta dhara.  Huu ni wasia kutoka kwa Allaah, na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mvumilivu.

 

 

تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۚ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٣﴾

13. Hiyo ni Mipaka ya Allaah. Na yeyote atakayemtii Allaah na Rasuli Wake Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, watadumu humo, na huko ndiko kufuzu kukubwa mno.

 

 

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٤﴾

14. Na yeyote atakayemuasi Allaah na Rasuli Wake na akataadi Mipaka Yake Atamuingiza motoni, atadumu humo na atapata adhabu ya kudhalilisha.

 

 

وَاللَّاتِي يَأْتِينَ الْفَاحِشَةَ مِن نِّسَائِكُمْ فَاسْتَشْهِدُوا عَلَيْهِنَّ أَرْبَعَةً مِّنكُمْ ۖ فَإِن شَهِدُوا فَأَمْسِكُوهُنَّ فِي الْبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّاهُنَّ الْمَوْتُ أَوْ يَجْعَلَ اللَّـهُ لَهُنَّ سَبِيلًا ﴿١٥﴾

15. Na wale wanaofanya uchafu miongoni mwa wanawake wenu, basi washuhudisheni mashahidi wanne kati yenu. Na wakishuhudia basi wazuieni majumbani mpaka mauti yawafishe au Allaah Awajaalie njia (nyingine).

 

 

 

وَاللَّذَانِ يَأْتِيَانِهَا مِنكُمْ فَآذُوهُمَا ۖ فَإِن تَابَا وَأَصْلَحَا فَأَعْرِضُوا عَنْهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ تَوَّابًا رَّحِيمًا ﴿١٦﴾ 

16. Na wale wawili wanaofanya huo (uchafu) waadhibuni. Wakitubu na wakajirekebisha basi waacheni. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.

 

 

 إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللَّـهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُولَـٰئِكَ يَتُوبُ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٧﴾

17. Hakika tawbah inayokubaliwa na Allaah ni ya wale wanaofanya uovu kwa ujahili kisha wakatubia haraka, basi hao Allaah Anapokea tawbah yao. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّىٰ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّي تُبْتُ الْآنَ وَلَا الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٨﴾ 

18. Lakini tawbah si kwa wale wanaofanya maovu mpaka mauti yanapomjia mmoja wao ndipo aseme: Hakika mimi sasa nimetubu. Na wala wale wanaokufa na hali wao ni makafiri. Hao Tumewaandalia adhabu iumizayo.

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا النِّسَاءَ كَرْهًا ۖ وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّـهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا ﴿١٩﴾

19. Enyi walioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa kuwalazimisha. Na wala msiwazuie kwa inda ili mpokonye baadhi ya vile mlivyowapa isipokuwa wakiwa wamefanya uchafu bayana. Na kaeni nao kwa wema. Na mkiwachukia, basi asaa mkachukia jambo na Allaah Akalijaalia kuwa lenye kheri nyingi ndani yake.

 

 

وَإِنْ أَرَدتُّمُ اسْتِبْدَالَ زَوْجٍ مَّكَانَ زَوْجٍ وَآتَيْتُمْ إِحْدَاهُنَّ قِنطَارًا فَلَا تَأْخُذُوا مِنْهُ شَيْئًا ۚ أَتَأْخُذُونَهُ بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٢٠﴾

20. Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na mmempa mmoja wao mirundi ya mali, basi msichukue humo chochote. Je, mnaichukua kwa dhulma na dhambi iliyo bayana?

 

 

وَكَيْفَ تَأْخُذُونَهُ وَقَدْ أَفْضَىٰ بَعْضُكُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ وَأَخَذْنَ مِنكُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿٢١﴾

21. Na mtaichukuaje na hali nyinyi kwa nyinyi mmeingiliana (kimwili na kustarehe), na wao wanawake wamechukua toka kwenu fungamano thabiti?

 

 

وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۚ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَمَقْتًا وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٢٢﴾

22. Na wala msiwaoe wanawake waliowaoa baba zenu isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika hayo yalikuwa ni uchafu na chukizo na njia ovu.

 

 

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمْ تَكُونُوا دَخَلْتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٢٣﴾

23. Mmeharamishiwa (kuwaoa) mama zenu, na mabinti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na makhalati zenu (mama wakubwa na wadogo), na mabinti wa kaka, na mabinti wa dada, na mama zenu ambao wamekunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu ambao mmewaingilia. Lakini ikiwa hamkuwaingilia basi hakuna dhambi (kuwaoa). Na (mmeharamishwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja, isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُم بِهِ مِن بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٢٤﴾

24. Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni sharia ya Allaah kwenu. Na mmehalalishiwa wengineo wasiokuwa hao, mtafute (kuwaoa) kwa mali zenu mkijistahi pasi na kuzini. Basi mliostarehe nao[3], wapeni mahari yao kwa kuwa ni waajib. Na wala si dhambi kwenu katika mliyoridhiana baada ya kukamilika ya waajib. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

وَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ مِنكُمْ طَوْلًا أَن يَنكِحَ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ فَمِن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُم مِّن فَتَيَاتِكُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ۚ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِكُم ۚ بَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ ۚ فَانكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ مُحْصَنَاتٍ غَيْرَ مُسَافِحَاتٍ وَلَا مُتَّخِذَاتِ أَخْدَانٍ ۚ فَإِذَا أُحْصِنَّ فَإِنْ أَتَيْنَ بِفَاحِشَةٍ فَعَلَيْهِنَّ نِصْفُ مَا عَلَى الْمُحْصَنَاتِ مِنَ الْعَذَابِ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ الْعَنَتَ مِنكُمْ ۚ وَأَن تَصْبِرُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٥﴾

25. Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake Waumini walio huru, basi (aoe) katika wale iliyomiliki mikono yenu ya kulia miongoni mwa wajakazi wenu Waumini. Na Allaah Anajua zaidi imaan yenu. Nyinyi (Waumini) mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao na wapeni mahari yao kwa ada inayokubalika, wawe wanawake wanaojistiri na machafu si makahaba na wala si wenye kuchukua hawara. Na watakapohifadhiwa katika ndoa, kisha wakafanya uchafu basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu ya waliyowekewa wanawake walio huru (wasioolewa). Hayo ni kwa yule anayeogopa dhambi ya zinaa miongoni mwenu. Na mkisubiri itakuwa ni kheri kwenu. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمْ وَيَهْدِيَكُمْ سُنَنَ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ وَيَتُوبَ عَلَيْكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٢٦﴾

26. Allaah Anataka kukubainishieni na kukuongozeni nyendo za wale walio kabla yenu, na Apokee tawbah kwenu. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

وَاللَّـهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيْكُمْ وَيُرِيدُ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الشَّهَوَاتِ أَن تَمِيلُوا مَيْلًا عَظِيمًا ﴿٢٧﴾

27. Na Allaah Anataka kupokea tawbah kwenu, na wale wanaofuata matamanio wanataka mkengeuke, mkengeuko mkubwa mno.

 

 

يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ ۚ وَخُلِقَ الْإِنسَانُ ضَعِيفًا ﴿٢٨﴾

28. Allaah Anataka kukukhafifishieni (tabu zenu), kwani binaadam ameumbwa dhaifu. 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ ۚ وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ﴿٢٩﴾

29. Enyi walioamini! Msiliane mali zenu kwa ubatwilifu, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana baina yenu. Wala msijiue. Hakika Allaah Ni Mwenye Kuwarehemuni.

 

 

وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ عُدْوَانًا وَظُلْمًا فَسَوْفَ نُصْلِيهِ نَارًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾

30. Na atakayefanya hivyo kwa uadui na dhulma, basi Tutamuingiza motoni. Na hilo kwa Allaah ni jepesi mno. 

 

 

 

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾

31. Mkijiepusha na madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu.[4]

 

 

وَلَا تَتَمَنَّوْا مَا فَضَّلَ اللَّـهُ بِهِ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبُوا ۖ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبْنَ ۚ وَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٣٢﴾

32. Wala msitamani ambayo Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wanayo sehemu katika waliyoyachuma, na wanawake wana sehemu katika waliyoyachuma. Na muombeni Allaah katika Fadhila Zake. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa kila kitu.

 

 

 

وَلِكُلٍّ جَعَلْنَا مَوَالِيَ مِمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ ۚ وَالَّذِينَ عَقَدَتْ أَيْمَانُكُمْ فَآتُوهُمْ نَصِيبَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدًا ﴿٣٣﴾

33. Na kila mmoja Tumemuwekea warithi katika yale waliyoyaacha wazazi wawili na jamaa wa karibu. Na wale mliofungamana nao viapo (vya undugu) basi wapeni fungu lao. Hakika Allaah daima Ni Shahidi juu ya kila kitu.  

 

 

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ ۚ وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا ﴿٣٤﴾

34. Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine, na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao. Basi wanawake wema ni wale watiifu, wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajihifadhi. Na wale ambao mnakhofu uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni[5] (kipigo kisichodhuru). Wakikutiini, basi msitafute njia dhidi yao (ya kuwaudhi). Hakika Allaah daima Ni Mwenye ‘Uluwa Uliotukuka, Mkubwa Kabisa.[6]

 

 

وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُوا حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَا إِن يُرِيدَا إِصْلَاحًا يُوَفِّقِ اللَّـهُ بَيْنَهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا ﴿٣٥﴾

35. Na mkikhofu mafarikiano baina yao wawili, basi pelekeni mwamuzi kutoka watu wa mume na mwamuzi kutoka watu wa mke. Wakitaka sulhu, basi Allaah Atawawafikisha baina yao.  Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Khabari za dhahiri na siri.

 

 

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا ﴿٣٦﴾

36. Na mwabuduni Allaah wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini, na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa, na rafiki wa karibu, na msafiri aliyeishiwa masurufu, na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. Hakika Allaah Hapendi mwenye majivuno na mwenye kujifakharisha.

 

 

الَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبُخْلِ وَيَكْتُمُونَ مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿٣٧﴾

37. (Pia Hawapendi) Wale wanaofanya ubakhili na wanawaamrisha watu ubakhili na wanaficha Aliyowapa Allaah katika Fadhila Zake. Na Tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha. 

 

 

وَالَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗ وَمَن يَكُنِ الشَّيْطَانُ لَهُ قَرِينًا فَسَاءَ قَرِينًا ﴿٣٨﴾

38. Na (Tumewaandalia pia adhabu hiyo) wale wanaotoa mali zao riyaa-a[7] (kujionyesha) kwa watu wala hawamwamini Allaah wala Siku ya Mwisho. Na yule ambaye shaytwaan amekuwa ni rafiki yake mwandani, basi mbaya alioje rafiki mwandani (huyo)!  

 

 

وَمَاذَا عَلَيْهِمْ لَوْ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقَهُمُ اللَّـهُ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِهِمْ عَلِيمًا ﴿٣٩﴾

39. Na ingeliwadhuru nini wao lau wangelimwamini Allaah na Siku ya Mwisho na wakatoa katika yale Aliyowaruzuku Allaah? Na Allaah Ni Mwenye Kuwajua vyema. 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٤٠﴾

40. Hakika Allaah Hadhulumu hata uzito au chembe (kama atomu). Na ikiwa ni amali njema Huizidisha na Hutoa kutoka Kwake ujira mkuu kabisa. 

 

 

فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا ﴿٤١﴾

41. Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa shahidi juu ya hawa?[8]

 

 

 

يَوْمَئِذٍ يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَعَصَوُا الرَّسُولَ لَوْ تُسَوَّىٰ بِهِمُ الْأَرْضُ وَلَا يَكْتُمُونَ اللَّـهَ حَدِيثًا ﴿٤٢﴾

42. Siku hiyo wale waliokufuru na wakamuasi Rasuli watatamani lau ardhi ingesawazishwa juu yao.  Na wala hawatoweza kumficha Allaah kauli hata moja. 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا ﴿٤٣﴾

43. Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa[9] mpaka mjue mnayoyasema, wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho. Na mkiwa wagonjwa au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi ikusudieni ardhi safi ya mchanga (mtayammam)[10]; mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Kughufuria.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يَشْتَرُونَ الضَّلَالَةَ وَيُرِيدُونَ أَن تَضِلُّوا السَّبِيلَ ﴿٤٤﴾

44. Je, huoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanakhiari upotofu na wanataka mpotee njia?

 

 

 

وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِأَعْدَائِكُمْ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَلِيًّا وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ نَصِيرًا ﴿٤٥﴾

45. Na Allaah Anawajua zaidi maadui zenu, na Allaah Anatosha kuwa Rafiki Mlinzi na Allaah Anatosha kuwa Mwenye Kunusuru. 

 

 

مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ وَيَقُولُونَ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَاسْمَعْ غَيْرَ مُسْمَعٍ وَرَاعِنَا لَيًّا بِأَلْسِنَتِهِمْ وَطَعْنًا فِي الدِّينِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ قَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَاسْمَعْ وَانظُرْنَا لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَقْوَمَ وَلَـٰكِن لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٤٦﴾

46. Katika Mayahudi wako wanaobadilisha maneno kuyatoa mahali pake, na husema (kumwambia Rasuli): Tumesikia (maneno yako) na tumeasi, na sikia bila ya kusikilizwa. Na (humwambia pia): Raa’inaa[11] kwa kuzipotoa ndimi zao na kutukana Dini. Na lau wangesema: Tumesikia na tumetii, na sikia na undhwurnaa, basi ingelikuwa kheri kwao na sawa zaidi. Lakini Allaah Amewalaani kwa kufru yao, basi hawaamini isipokuwa wachache tu.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ آمِنُوا بِمَا نَزَّلْنَا مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُم مِّن قَبْلِ أَن نَّطْمِسَ وُجُوهًا فَنَرُدَّهَا عَلَىٰ أَدْبَارِهَا أَوْ نَلْعَنَهُمْ كَمَا لَعَنَّا أَصْحَابَ السَّبْتِ ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ مَفْعُولًا ﴿٤٧﴾

47. Enyi mliopewa Kitabu! Aminini yale Tuliyoyateremsha (kwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) yanayosadikisha yale mliyonayo, kabla hatujabadilisha nyuso Tukazirudisha kisogoni, au Tukawalaani kama Tulivyowalaani watu wa As-Sabt.[12] Na Amri ya Allaah itafanyika tu.

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾

48. Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa, lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha[13] Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu kabisa.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُم ۚ بَلِ اللَّـهُ يُزَكِّي مَن يَشَاءُ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٤٩﴾

49. Je, hukuwaona wale wanaojitakasa nafsi zao? Bali Allaah Humtakasa Amtakaye, na wala hawatodhulumiwa hata kadiri ya uzi katika kokwa ya tende. 

 

 

انظُرْ كَيْفَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۖ وَكَفَىٰ بِهِ إِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٠﴾

50. Tazama vipi wanavyomtungia  uongo Allaah, na yatosha haya kuwa dhambi za dhahiri.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا ﴿٥١﴾

51. Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini Al-Jibt  (itikadi potofu) na twaghuti[14] na wanasema juu ya wale waliokufuru kuwa: Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini.

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا ﴿٥٢﴾

52. Hao ndio wale Allaah Aliowalaani. Na ambaye Allaah Amemlaani, kamwe hutamkuta kuwa na (mtu) wa kumsaidia.

 

 

أَمْ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّنَ الْمُلْكِ فَإِذًا لَّا يُؤْتُونَ النَّاسَ نَقِيرًا ﴿٥٣﴾

53. Au wanayo sehemu ya ufalme (wa Allaah?). Basi hapo wasingeliwapa watu kadiri ya kitone cha kokwa ya tende.

 

 

أَمْ يَحْسُدُونَ النَّاسَ عَلَىٰ مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۖ فَقَدْ آتَيْنَا آلَ إِبْرَاهِيمَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَآتَيْنَاهُم مُّلْكًا عَظِيمًا ﴿٥٤﴾

54. Au wanawahusudu watu (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم  na Waumini) kwa yale Aliyowapa Allaah katika Fadhila Zake? Basi kwa yakini Tuliwapa kizazi cha Ibraahiym Kitabu na Hikmah na Tukawapa ufalme mkubwa mno.

 

 

فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ بِهِ وَمِنْهُم مَّن صَدَّ عَنْهُ ۚ وَكَفَىٰ بِجَهَنَّمَ سَعِيرًا ﴿٥٥﴾

55. Basi miongoni mwao wako waliomuamini (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na miongoni mwao wako waliomkengeuka. Na Jahannam inatosheleza kuwa ni moto uliowashwa vikali mno.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا سَوْفَ نُصْلِيهِمْ نَارًا كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا الْعَذَابَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿٥٦﴾

56. Hakika wale waliokanusha Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu Tutawaingiza motoni. Kila ngozi zao zitakapobanikika zikaungua Tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje adhabu. Hakika Allaah daima Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ لَّهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَنُدْخِلُهُمْ ظِلًّا ظَلِيلًا ﴿٥٧﴾

57. Na wale walioamini na wakatenda mema Tutawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, watadumu humo abadi. Watapata humo wake waliotakasika na Tutawaingiza katika vivuli vizuri vya raha tele.

 

 

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿٥٨﴾

58. Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. Na mtakapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Ni uzuri ulioje wa Anayokuwaidhini kwayo Allaah! Hakika Allaah daima Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.[15]

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾

59. Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi.[16]  

 

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿٦٠﴾

60. Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa twaghuti (ubatwilifu) na hali wameamrishwa wakanushe hayo. Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali.

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا ﴿٦١﴾

61. Na wanapoambiwa: Njooni kwenye yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Rasuli, utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwa mkengeuko.

 

 

فَكَيْفَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ثُمَّ جَاءُوكَ يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا إِحْسَانًا وَتَوْفِيقًا ﴿٦٢﴾

62. Basi itakuwaje utakapowafika msiba kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao? Kisha wakakujia wakiapa: Wa-Allaahi hatukutaka ila mazuri na mapatano. 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَعْلَمُ اللَّـهُ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَعِظْهُمْ وَقُل لَّهُمْ فِي أَنفُسِهِمْ قَوْلًا بَلِيغًا ﴿٦٣﴾ 

63. Hao ndio ambao Allaah Anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi waachilie mbali na wape mawaidha (ya kuwaonya) na waambie kwa siri maneno mazito ya kuwatua na kuwagonga. 

 

 

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُوا أَنفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّـهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّـهَ تَوَّابًا رَّحِيمًا﴿٦٤﴾

64. Na Hatukutuma Rasuli yeyote ila atiiwe kwa Idhini ya Allaah. Na lau wao pale walipojidhulumu nafsi zao wangelikujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wakamwomba Allaah maghfirah na Rasuli akawaombea maghfirah, basi wangelimkuta Allaah Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu. 

 

 

 

 

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

65. Basi mambo si kama wanavyodai. Naapa kwa Rabb wako, hawatakuwa Waumini wa kweli mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao ukakasi katika yale uliyohukumu, na waikubali hukmu yako kwa moyo safi na maridhio.

 

 

 

وَلَوْ أَنَّا كَتَبْنَا عَلَيْهِمْ أَنِ اقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ أَوِ اخْرُجُوا مِن دِيَارِكُم مَّا فَعَلُوهُ إِلَّا قَلِيلٌ مِّنْهُمْ ۖ وَلَوْ أَنَّهُمْ فَعَلُوا مَا يُوعَظُونَ بِهِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَشَدَّ تَثْبِيتًا ﴿٦٦﴾

66. Na lau Tungeliwaandikia amri: Jiueni nafsi zenu na tokeni katika majumba yenu, wasingelifanya hayo ila wachache miongoni mwao. Na lau wangelifanya yale waliyowaidhiwa kwayo ingelikuwa kheri kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi (wa imaan zao).

 

 

وَإِذًا لَّآتَيْنَاهُم مِّن لَّدُنَّا أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٦٧﴾

67. Na hapo Tungeliwapa kutoka Kwetu ujira mkubwa mno.

 

 

وَلَهَدَيْنَاهُمْ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿٦٨﴾

68. Na Tungewaongoza njia iliyonyooka. 

 

 

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾

69. Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiqiyna na Shuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao![17]

 

ذَٰلِكَ الْفَضْلُ مِنَ اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ عَلِيمًا ﴿٧٠﴾

70. Hiyo ni fadhila kutoka kwa Allaah. Na inatosheleza Allaah kuwa Ni Mjuzi wa yote. 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا خُذُوا حِذْرَكُمْ فَانفِرُوا ثُبَاتٍ أَوِ انفِرُوا جَمِيعًا ﴿٧١﴾

71. Enyi walioamini! Chukueni tahadhari yenu! Na tokeni kwa vikosi vikosi au tokeni kwa pamoja. 

 

 

وَإِنَّ مِنكُمْ لَمَن لَّيُبَطِّئَنَّ فَإِنْ أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَالَ قَدْ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيَّ إِذْ لَمْ أَكُن مَّعَهُمْ شَهِيدًا ﴿٧٢﴾

72. Na katika nyinyi yuko anayejikokota abakie nyuma (asiende vitani). Na unapokusibuni msiba husema: Kwa yakini Allaah Kanipenda nilivyokuwa sikwenda nao vitani.

 

 

وَلَئِنْ أَصَابَكُمْ فَضْلٌ مِّنَ اللَّـهِ لَيَقُولَنَّ كَأَن لَّمْ تَكُن بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُ مَوَدَّةٌ يَا لَيْتَنِي كُنتُ مَعَهُمْ فَأَفُوزَ فَوْزًا عَظِيمًا ﴿٧٣﴾

73. Na ikikufikieni fadhila kutoka kwa Allaah husema (kwa majuto) kama kwamba hakukuwa baina yenu na yeye mapenzi: Laiti ningelikuwa pamoja nao nikapata kufuzu mafanikio makubwa mno. 

 

 

فَلْيُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يَشْرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ ۚ وَمَن يُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيُقْتَلْ أَوْ يَغْلِبْ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٧٤﴾

74. Basi wapigane katika Njia ya Allaah wale wanaouza uhai (wao) wa dunia kwa Aakhirah. Na atakayepigana katika Njia ya Allaah akauliwa au akashinda basi Tutampa ujira mkubwa mno.

 

 

 

وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا ﴿٧٥﴾

75. Na mna nini hata msipigane katika Njia ya Allaah, nailhali walio wanyonge kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao (kwa vile hawana wa kuwasaidia isipokuwa kuelekea kwa Rabb wao) husema: Rabb wetu! Tutoe kutoka katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na Tujaalie kutoka Kwako rafiki mlinzi na Tujaalie kutoka Kwako mwenye kunusuru.

 

 

الَّذِينَ آمَنُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ الطَّاغُوتِ فَقَاتِلُوا أَوْلِيَاءَ الشَّيْطَانِ ۖ إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا ﴿٧٦﴾

76. Wale walioamini hupigana katika Njia ya Allaah. Na wale waliokufuru hupigana katika njia ya twaghuti (kumtii shaytwaan). Basi wapigeni marafiki wandani na walinzi wa shaytwaan. Hakika hila za shaytwaan daima ni dhaifu.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوا أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَخْشَوْنَ النَّاسَ كَخَشْيَةِ اللَّـهِ أَوْ أَشَدَّ خَشْيَةً ۚ وَقَالُوا رَبَّنَا لِمَ كَتَبْتَ عَلَيْنَا الْقِتَالَ لَوْلَا أَخَّرْتَنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ ۗ قُلْ مَتَاعُ الدُّنْيَا قَلِيلٌ وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّمَنِ اتَّقَىٰ وَلَا تُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٧٧﴾

77. Je, huoni wale walioambiwa: Zuieni mikono yenu (msipigane) na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah. Basi walipoandikiwa amri kupigana, mara kundi miongoni mwao linawaogopa watu kama kumwogopa Allaah au woga zaidi. Na husema: Rabb wetu!  Kwa nini Umetuamrisha kupigana? Lau Ungelituakhirishia hadi muda kidogo hivi! Sema: Starehe za dunia ni chache, na Aakhirah ni bora zaidi kwa mwenye taqwa, wala hamtodhulumiwa kadiri ya uzi wa kokwa ya tende.

 

 

 

أَيْنَمَا تَكُونُوا يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ ۗ وَإِن تُصِبْهُمْ حَسَنَةٌ يَقُولُوا هَـٰذِهِ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَقُولُوا هَـٰذِهِ مِنْ عِندِكَ ۚ قُلْ كُلٌّ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ فَمَالِ هَـٰؤُلَاءِ الْقَوْمِ لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ حَدِيثًا ﴿٧٨﴾

78. Popote mtakapokuwa yatakufikieni mauti, japo mkiwa katika minara (au ngome) imara na madhubuti. Na likiwafikia jambo zuri husema: Hili linatoka kwa Allaah. Na likiwasibu ovu husema: Hili linatoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Sema: Yote ni yanatoka kwa Allaah. Basi wana nini hawa watu hawakaribii kufahamu maneno?

 

 

 

مَّا أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍ فَمِنَ اللَّـهِ ۖ وَمَا أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٍ فَمِن نَّفْسِكَ ۚ وَأَرْسَلْنَاكَ لِلنَّاسِ رَسُولًا ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿٧٩﴾

79. Zuri lililokufikia linatoka kwa Allaah. Na ubaya uliokusibu (ee mwanaadam) ni kutokana na nafsi yako. Na Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa watu uwe Rasuli na inatosheleza Allaah kuwa Ni Mwenye Kushuhudia yote. 

 

 

 

مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ﴿٨٠﴾

80. Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah.[18]  Na atakayekengeuka basi Hatukukutuma kuwa mlinzi juu yao.

 

 

وَيَقُولُونَ طَاعَةٌ فَإِذَا بَرَزُوا مِنْ عِندِكَ بَيَّتَ طَائِفَةٌ مِّنْهُمْ غَيْرَ الَّذِي تَقُولُ ۖ وَاللَّـهُ يَكْتُبُ مَا يُبَيِّتُونَ ۖ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٨١﴾

81. Na wanasema (wanafiki): Tunatii. Lakini wanapotoka kutoka kwako, kundi miongoni mwao hukesha kushauriana na kupanga kinyume na unayoyasema. Na Allaah Anayaandika yale wanayoyapanga usiku. Basi waachilie mbali na tawakali kwa Allaah. Na inatosheleza Allaah kuwa Ni Mtegemewa.[19]

 

 

أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ ۚ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللَّـهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلَافًا كَثِيرًا ﴿٨٢﴾

82. Je, hawaizingatii Qur-aan? Na lau ingelikuwa imetoka kwa asiyekuwa Allaah, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi.[20]

 

 

وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٣﴾

83. Na linapowafikia jambo lolote kuhusu amani au khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Rasuli na kwa wenye madaraka kati yao, basi watakaolitafiti miongoni mwao wangelipatia jibu jambo hilo (kama linafaa kutangazwa au kufichwa). Na lau si Fadhila ya Allaah juu yenu na Rehma Yake kwa yakini mngelimfuata shaytwaan ila wachache tu.[21]

 

 

 

فَقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا تُكَلَّفُ إِلَّا نَفْسَكَ ۚ وَحَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ عَسَى اللَّـهُ أَن يَكُفَّ بَأْسَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ وَاللَّـهُ أَشَدُّ بَأْسًا وَأَشَدُّ تَنكِيلًا ﴿٨٤﴾

84. Basi pigana (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika Njia ya Allaah, hukalifishwi ila nafsi yako. Na wahimize Waumini (wakuunge). Allaah kwa hakika Atazuia mashambulizi ya nguvu ya waliokufuru. Na Allaah Ni Mkali zaidi wa Kushambulia na Mkali zaidi wa Kuadhibu adhabu ya tahadharisho na fundisho. 

 

 

 

مَّن يَشْفَعْ شَفَاعَةً حَسَنَةً يَكُن لَّهُ نَصِيبٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن يَشْفَعْ شَفَاعَةً سَيِّئَةً يَكُن لَّهُ كِفْلٌ مِّنْهَا ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقِيتًا ﴿٨٥﴾

85. Atakayesaidia kufanikisha jambo la kheri atapata fungu lake katika hayo. Na atakayesaidia kuunganisha jambo la shari atapata sehemu yake katika hayo. Na Allaah daima Ni Mwenye Kudhibiti na Mwangalizi wa kila kitu. 

 

 

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَسِيبًا ﴿٨٦﴾

86. Na mtapoamkiwa kwa maamkiziyoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo.[22]  Hakika Allaah daima Ni Mwenye Kuhesabu kila kitu.

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۗ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا ﴿٨٧﴾

87. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Bila ya shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah, haina shaka   ndani yake. Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?

 

 

فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿٨٨﴾

88. Basi mna nini hata mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki, na hali Allaah Amewageuza (warudie ukafiri) kwa sababu ya waliyoyachuma? Je, mnataka kumhidi ambaye Allaah Amempotoa? Na aliyepotozwa na Allaah basi hutompatia kamwe njia (ya kumhidi).

 

 

وَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ كَمَا كَفَرُوا فَتَكُونُونَ سَوَاءً ۖ فَلَا تَتَّخِذُوا مِنْهُمْ أَوْلِيَاءَ حَتَّىٰ يُهَاجِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَخُذُوهُمْ وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ ۖ وَلَا تَتَّخِذُوا مِنْهُمْ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿٨٩﴾

89. Wanatamani kama mtakufuru kama walivyokufuru wao, ili muwe sawa sawa. Basi msiwafanye miongoni mwao marafiki wandani na walinzi mpaka wahajiri katika Njia ya Allaah. Wakikengeuka basi wakamateni na waueni popote muwapatapo. Wala msimfanye yeyote kati yao kuwa rafiki yenu wala msaidizi.  

 

 

إِلَّا الَّذِينَ يَصِلُونَ إِلَىٰ قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ أَوْ جَاءُوكُمْ حَصِرَتْ صُدُورُهُمْ أَن يُقَاتِلُوكُمْ أَوْ يُقَاتِلُوا قَوْمَهُمْ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَسَلَّطَهُمْ عَلَيْكُمْ فَلَقَاتَلُوكُمْ ۚ فَإِنِ اعْتَزَلُوكُمْ فَلَمْ يُقَاتِلُوكُمْ وَأَلْقَوْا إِلَيْكُمُ السَّلَمَ فَمَا جَعَلَ اللَّـهُ لَكُمْ عَلَيْهِمْ سَبِيلًا ﴿٩٠﴾

90. Isipokuwa wale waliokimbilia kupata hifadhi kwa watu ambao kuna mkataba kati yenu na wao, au wale waliokujieni vifua vyao vimedhikika kupigana nanyi au kupigana na watu wao (hao msiwapige). Na lau Allaah Angelitaka, Angeliwasalitisha juu yenu, wakapigana nanyi. Watakapojitenga nanyi na wasipigane nanyi, na wakakuwekeeni amani, basi Allaah Hakukufanyieni njia dhidi yao.

 

 

سَتَجِدُونَ آخَرِينَ يُرِيدُونَ أَن يَأْمَنُوكُمْ وَيَأْمَنُوا قَوْمَهُمْ كُلَّ مَا رُدُّوا إِلَى الْفِتْنَةِ أُرْكِسُوا فِيهَا ۚ فَإِن لَّمْ يَعْتَزِلُوكُمْ وَيُلْقُوا إِلَيْكُمُ السَّلَمَ وَيَكُفُّوا أَيْدِيَهُمْ فَخُذُوهُمْ وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ ۚ وَأُولَـٰئِكُمْ جَعَلْنَا لَكُمْ عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿٩١﴾

91. Mtawakuta wengine wanataka kupata amani kwenu na kupata amani kwa watu wao, kila wanaporudishwa katika fitnah huangushwa humo. Wasipojitenga nanyi au wasiweze kukuleteeni amani au kuizuia mikono yao (kukupigeni), basi wakamateni na waueni popote muwapatapo. Na hao Tumekufanyieni hoja bayana dhidi yao.

 

 

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ أَن يَقْتُلَ مُؤْمِنًا إِلَّا خَطَأً ۚ وَمَن قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَأً فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ وَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ إِلَّا أَن يَصَّدَّقُوا ۚ فَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ عَدُوٍّ لَّكُمْ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ وَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ فَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ وَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ تَوْبَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٩٢﴾

92. Na haiwi kwa Muumini amuue Muumini ila kwa kukosea tu. Na atakayemuua Muumini kwa kukosea, basi aachilie huru mtumwa Muumini na atoe diya kwa kuifikisha kwa ahli zake, isipokuwa kama wenyewe watasamehe. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu naye ni Muumini, basi (aliyeua) aachilie huru mtumwa Muumini. Na akiwa ni miongoni mwa watu ambao kuna mkataba baina yenu na baina yao, basi wapewe diya watu wake na aachiliwe huru mtumwa Muumini. Asiyepata, afunge (Swiyaam) miezi miwili mfululizo kuwa ni tawbah kwa Allaah.[23] Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote. 

 

 

 

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا ﴿٩٣﴾

93.  Na atakayemuua Muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni Jahannam, atadumu humo, na Allaah Atamghadhibikia, Atamlaani na Atamuandalia adhabu kubwa mno.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٩٤﴾

94. Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo, na wala msimwambie anayekuamkieni kwa As-salaam: Wewe si Muumini kwa sababu ya kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan, basi fanyeni uhakiki. Hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi daima wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ وَالْمُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۚ فَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ عَلَى الْقَاعِدِينَ دَرَجَةً ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَفَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ عَلَى الْقَاعِدِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٩٥﴾

95. Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani), isipokuwa wale wenye udhuru, na kati ya wenye kupigana Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao. Allaah Amewafadhilisha kwa cheo wenye kupigana Jihaad kwa mali zao na nafsi zao kuliko waliokaa nyuma. Na wote Allaah Amewaahidi Al-Husnaa (Jannah). Na Allaah Amewafadhilisha wenye kupigana Jihaad kwa ujira mkubwa mno kuliko wanaokaa (nyuma).

 

 

دَرَجَاتٍ مِّنْهُ وَمَغْفِرَةً وَرَحْمَةً ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٩٦﴾

96. Ni daraja za vyeo (vya juu) kutoka Kwake na maghfirah na rehma. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٩٧﴾

97. Hakika wale ambao Malaika wanawafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao, (Malaika) watawaambia: Mlikuwa katika hali gani? Watasema: Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.  (Malaika) Watasema: Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni Jahannam, na uovu ulioje mahali pa kuishia!

 

 

إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا ﴿٩٨﴾

98. Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata hila yoyote wala hawawezi kuongoza njia.  

 

 

فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا ﴿٩٩﴾

99. Basi hao bila shaka Allaah Atawasamehe. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Kughufuria. 

 

 

     

وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٠﴾

100. Na anayehajiri katika Njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia kujihifadhi na wasaa (wa kila kitu). Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

وَإِذَا ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَقْصُرُوا مِنَ الصَّلَاةِ إِنْ خِفْتُمْ أَن يَفْتِنَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُوا لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا ﴿١٠١﴾

101. Na mtakaposafiri katika ardhi basi si dhambi kwenu kufupisha Swalaah mkikhofu kwamba waliokufuru watakushambulieni. Hakika makafiri wamekuwa kwenu ni maadui dhahiri. 

                                       

 

 

وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ وَلْيَأْخُذُوا أَسْلِحَتَهُمْ فَإِذَا سَجَدُوا فَلْيَكُونُوا مِن وَرَائِكُمْ وَلْتَأْتِ طَائِفَةٌ أُخْرَىٰ لَمْ يُصَلُّوا فَلْيُصَلُّوا مَعَكَ وَلْيَأْخُذُوا حِذْرَهُمْ وَأَسْلِحَتَهُمْ ۗ وَدَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ تَغْفُلُونَ عَنْ أَسْلِحَتِكُمْ وَأَمْتِعَتِكُمْ فَيَمِيلُونَ عَلَيْكُم مَّيْلَةً وَاحِدَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن كَانَ بِكُمْ أَذًى مِّن مَّطَرٍ أَوْ كُنتُم مَّرْضَىٰ أَن تَضَعُوا أَسْلِحَتَكُمْ ۖ وَخُذُوا حِذْرَكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٠٢﴾

102. Na utapokuwa upo kati yao, ukawaswalisha, basi lisimame kundi miongoni mwao pamoja nawe, na wachukue silaha zao. Watakaposujudu, wawe nyuma yenu (kuwalinda). Na lije kundi jingine ambalo halikuswali, liswali pamoja nawe, nao washike hadhari na silaha zao. Wale waliokufuru wanatamani kama mtaghafilika na silaha zenu na vifaa vyenu wakuvamieni mvamio mmoja. Na wala si dhambi kwenu ikiwa mna maudhiko kutokana na mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu. Na mshike hadhari zenu. Hakika Allaah Amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.

 

 

فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا اطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا ﴿١٠٣﴾

103. Mtakapomaliza Swalaah, mdhukuruni Allaah mkiwa wima, mmeketi, au mmejinyoosha. Na mtakapopata utulivu, basi simamisheni Swalaah (kama desturi), hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekewa nyakati maalumu.[24]

 

 

وَلَا تَهِنُوا فِي ابْتِغَاءِ الْقَوْمِ ۖ إِن تَكُونُوا تَأْلَمُونَ فَإِنَّهُمْ يَأْلَمُونَ كَمَا تَأْلَمُونَ ۖ وَتَرْجُونَ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا يَرْجُونَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٠٤﴾

104. Wala msilegee katika kuwaandama watu (maadui). Mkiwa mnaumia basi nao pia wanaumia kama mnavyoumia. Lakini nyinyi mnataraji kutoka kwa Allaah wasiyoyataraji wao. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ بِمَا أَرَاكَ اللَّـهُ ۚ وَلَا تَكُن لِّلْخَائِنِينَ خَصِيمًا ﴿١٠٥﴾

105. Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki ili uhukumu baina ya watu kwa Aliyokuonyesha Allaah. Wala usiwe mtetezi kwa makhaini. 

 

 

وَاسْتَغْفِرِ اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٦﴾

106. Na muombe Allaah maghfirah. Hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

وَلَا تُجَادِلْ عَنِ الَّذِينَ يَخْتَانُونَ أَنفُسَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ خَوَّانًا أَثِيمًا ﴿١٠٧﴾

107. Wala usiwatetee wale wanaokhini nafsi zao. Hakika Allaah Hampendi aliye mwingi wa kukhini na kutenda dhambi. 

 

 

يَسْتَخْفُونَ مِنَ النَّاسِ وَلَا يَسْتَخْفُونَ مِنَ اللَّـهِ وَهُوَ مَعَهُمْ إِذْ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرْضَىٰ مِنَ الْقَوْلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطًا ﴿١٠٨﴾

108. Wanajificha watu wasiwaone (wakitenda machafu) na wala hawajifichi kwa Allaah (wakamwonea haya), Naye Yu pamoja nao (kwa Ujuzi Wake) pale wanapokesha kupanga makri kwa maneno Asiyoyaridhia. Na Allaah daima Ni Mwenye Kuyazunguka yale wayatendayo.

 

 

هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ جَادَلْتُمْ عَنْهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَمَن يُجَادِلُ اللَّـهَ عَنْهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَم مَّن يَكُونُ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا ﴿١٠٩﴾

109. Ha! Nyinyi ndio hawa mliowatetea katika uhai huu wa duniani. Basi nani atakayewatetea kwa Allaah Siku ya Qiyaamah? Au nani atakayekuwa mwakilishi wao wa kumtegemea? 

 

 

وَمَن يَعْمَلْ سُوءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ اللَّـهَ يَجِدِ اللَّـهَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١١٠﴾

110. Na atakayetenda ovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akamwomba Allaah maghfirah, basi atamkuta Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[25]

 

 

وَمَن يَكْسِبْ إِثْمًا فَإِنَّمَا يَكْسِبُهُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١١١﴾

111. Na atakayechuma dhambi, basi hakika anaichumia madhara nafsi yake. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote. 

 

 

وَمَن يَكْسِبْ خَطِيئَةً أَوْ إِثْمًا ثُمَّ يَرْمِ بِهِ بَرِيئًا فَقَدِ احْتَمَلَ بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿١١٢﴾

112. Na atakayechuma kosa au dhambi kisha akamtupia asiye na hatia, basi kwa yakini amejitweka (dhulma ya) usingiziaji na dhambi bayana.

 

 

وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ وَرَحْمَتُهُ لَهَمَّت طَّائِفَةٌ مِّنْهُمْ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ ۖ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَيْءٍ ۚ وَأَنزَلَ اللَّـهُ عَلَيْكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمْ تَكُن تَعْلَمُ ۚ وَكَانَ فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ عَظِيمًا ﴿١١٣﴾

113. Na lau kuwa si Fadhila ya Allaah na Rehma Yake juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), bila shaka kundi miongoni mwao lingefanya hima kudhamiria kukupoteza. Na hawazipotezi ila nafsi zao, na hawakudhuru kwa chochote. Na Allaah Amekuteremshia Kitabu na Hikmah na Akakufunza yale ambayo hukuwa unayajua. Na Fadhila za Allaah juu yako daima ni adhimu (na kubwa mno).

 

 

لَّا خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١١٤﴾

114. Hakuna kheri katika minong’ono yao mingi isipokuwa anayeamrisha kutoa swadaqa, au mema, au kusuluhisha baina ya watu. Na atakayefanya hivyo kutaka Radhi za Allaah, basi Tutampa ujira mkubwa kabisa.

 

 

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿١١٥﴾

115. Na atakayempinga Rasuli baada ya kuwa imeshambainikia hidaaya na akaifuata njia isiyokuwa ya Waumini, Tutamgeuza alikogeukia na Tutamuingiza Jahannam. Na uovu ulioje mahali pa kuishia! 

 

 

 إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١١٦﴾

116. Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa, lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha[26] Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali.

 

 

إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا ﴿١١٧﴾

117. Hawaombi badala Yake isipokuwa miungu ya kike na hawaombi isipokuwa shaytwaan muasi.

 

 

لَّعَنَهُ اللَّـهُ ۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿١١٨﴾

118. Allaah Amemlaani. Na (shaytwaan) akasema: Kwa hakika nitashika katika waja Wako sehemu maalumu!

 

 

وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ﴿١١٩﴾

119. Na hakika nitawapoteza, na nitawashawishi matamanio ya kulaghai, na nitawaamrisha. Basi watakata masikio ya wanyama (wawatukuze), na nitawaamrisha watabadili Uumbaji wa Allaah.[27] Na atakayemfanya shaytwaan kuwa rafiki mlinzi badala ya Allaah basi kwa yakini amekhasirika khasara bayana.

 

 

يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ ۖ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا ﴿١٢٠﴾

120. Anawaahidi na anawashawishi matamanio ya uongo. Na shaytwaan hawaahidi isipokuwa ulaghai tu.

 

 

أُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَلَا يَجِدُونَ عَنْهَا مَحِيصًا ﴿١٢١﴾

121. Hao makaazi yao ni Jahannam, wala hawatopata makimbilio ya kutoka humo. 

 

 

 

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا ۚ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا ﴿١٢٢﴾

122. Na wale walioamini na wakatenda mema Tutawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo abadi. Ahadi ya Allaah ni haki. Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah? 

 

 

لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٢٣﴾

123. Si kwa matamanio yenu wala kwa matamanio ya Watu wa Kitabu. Atakayefanya uovu atalipwa kwalo, na wala hatopata rafiki mlinzi wala mwenye kumnusuru isipokuwa Allaah.

 

 

وَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ مِن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ نَقِيرًا ﴿١٢٤﴾

124. Na atakayefanya mema akiwa mwanamume au mwanamke, hali ya kuwa ni Muumini, basi hao wataingia Jannah na wala hawatodhulumiwa kadiri ya kitone cha kokwa ya tende. 

 

 

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴿١٢٥﴾

125. Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Allaah naye anatekeleza maamrisho kwa uzuri unaotakikana, na akafuata mila ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki? Na Allaah Amemfanya Ibraahiym kuwa ni kipenzi.

 

 

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ مُّحِيطًا ﴿١٢٦﴾

126 Ni vya Allaah vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na Allaah daima Ni Mwenye Kuvizunguka kila kitu.

 

 

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الْوِلْدَانِ وَأَن تَقُومُوا لِلْيَتَامَىٰ بِالْقِسْطِ ۚ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِهِ عَلِيمًا ﴿١٢٧﴾

127. Na wanakuuliza wewe hukmu ya kisharia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: Allaah Anakubainishieni hukmu ya kisharia kuhusu wao na (hukmu ya) yale mnayosomewa katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa nanyi mna raghba ya kuwaoa, na kuhusu wanaokandamizwa miongoni mwa watoto, na wajibu ulio juu yenu wa kuwasimamia mayatima kwa uadilifu. Na lolote mlifanyalo katika la kheri basi hakika Allaah daima kwa hilo Ni Mjuzi.

 

 

 

 

 

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

128. Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya kwao wawili wakisikilizana baina yao kwa suluhu. Na suluhu ni bora zaidi. Na nafsi zimeumbiwa tabia ya uchoyo na ubahili. Na mkifanya ihsaan (kwa wanawake) na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi daima wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ وَإِن تُصْلِحُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٢٩﴾

129. Na wala hamtoweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msimili muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mwengine) kama aliyeachwa njia panda. Na mkiyaweka mambo vizuri na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغْنِ اللَّـهُ كُلًّا مِّن سَعَتِهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ وَاسِعًا حَكِيمًا ﴿١٣٠﴾

130. Na wakifarikiana basi Allaah Atamtosheleza kila mmoja kwa Wasaa Wake. Na Allaah daima Ni Mwenye Wasaa, Mwenye Hikmah wa yote. 

 

 

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ وَصَّيْنَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ اتَّقُوا اللَّـهَ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَنِيًّا حَمِيدًا ﴿١٣١﴾

131. Ni vya Allaah vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na kwa yakini Tumewausia wale waliopewa Kitabu kabla yenu na nyinyi kwamba: Mcheni Allaah. Na mkikufuru basi hakika ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na Allaah daima Ni Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa. 

 

 

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿١٣٢﴾

132. Na ni vya Allaah vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na inatosheleza Allaah kuwa Ni Mtegemewa.[28]  

 

 

إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ أَيُّهَا النَّاسُ وَيَأْتِ بِآخَرِينَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ قَدِيرًا ﴿١٣٣﴾

133. Akitaka, Atakuondoeni mbali enyi watu, na Ataleta wengine. Na Allaah kwa hayo daima Ni Muweza.

 

 

مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ ثَوَابُ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿١٣٤﴾

134. Anayetaka thawabu za dunia, basi kwa Allaah kuna thawabu za dunia na Aakhirah. Na Allaah daima Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote. 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّـهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ ۚ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَاللَّـهُ أَوْلَىٰ بِهِمَا ۖ فَلَا تَتَّبِعُوا الْهَوَىٰ أَن تَعْدِلُوا ۚ وَإِن تَلْوُوا أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٣٥﴾

135. Enyi walioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu kwa nguvu zote (na) wenye kutoa ushahidi kwa ajili ya Allaah tu japokuwa ni dhidi ya nafsi zenu, au wazazi wawili, au jamaa wa karibu. Akiwa tajiri au maskini, Allaah Anawastahikia zaidi. Basi msifuate hawaa mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkikanusha basi hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi daima wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي أَنزَلَ مِن قَبْلُ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١٣٦﴾

136. Enyi walioamini! Mwaminini Allaah na Rasuli Wake na Kitabu Alichokiteremsha kwa Rasuli Wake na Kitabu Alichokiteremsha kabla. Na atakayemkufuru Allaah na Malaika Wake, na Vitabu Vyake na Rusuli Wake na Siku ya Mwisho, basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali. 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا ثُمَّ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّمْ يَكُنِ اللَّـهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ سَبِيلًا ﴿١٣٧﴾

137. Hakika wale walioamini kisha wakakufuru, kisha wakaamini kisha wakakufuru, kisha wakazidi kufru, Allaah Hatowaghufiria na wala Hatowaongoza njia.

 

 

بَشِّرِ الْمُنَافِقِينَ بِأَنَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٣٨﴾

138. Wabashirie wanafiki kwamba watapata adhabu iumizayo. 

 

 

الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۚ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا ﴿١٣٩﴾

139. Wale wanaofanya makafiri kuwa ni marafiki wandani na walinzi badala ya Waumini. Je, wanatafuta utukufu kutoka kwao? Basi hakika utukufu wote ni wa Allaah Pekee. 

 

 

وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ جَامِعُ الْمُنَافِقِينَ وَالْكَافِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا ﴿١٤٠﴾

140. Na kwa yakini Amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayaat za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai,[29] basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Au sivyo mtakuwa kama wao. Hakika Allaah Atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannam.

 

 

الَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمْ فَإِن كَانَ لَكُمْ فَتْحٌ مِّنَ اللَّـهِ قَالُوا أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ وَإِن كَانَ لِلْكَافِرِينَ نَصِيبٌ قَالُوا أَلَمْ نَسْتَحْوِذْ عَلَيْكُمْ وَنَمْنَعْكُم مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ۚ فَاللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَلَن يَجْعَلَ اللَّـهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا ﴿١٤١﴾

141.  Wale wanaofuatilia khabari zenu wakisubiri nini kitawasibu; inapokuwa ni ushindi kwenu kutoka kwa Allaah husema: Je, hatukuwa pamoja nanyi? Na inapokuwa sehemu ya ushindi kwa makafiri husema: Je, hatukuwa wenye uwezo wa kukudhibitini nasi tukakuzuilieni na Waumini? Basi Allaah Atawahukumu baina yenu Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Hatojaalia kwa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.

 

 

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّـهَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٤٢﴾

142. Hakika wanafiki (wanadhani) wanamhadaa Allaah, na hali Yeye (Allaah) Ndiye Mwenye kuwahadaa. Na wanaposimama kuswali husimama kwa uvivu, wakijionyesha[30] kwa watu na wala hawamdhukuru Allaah isipokuwa kidogo tu.

 

 

مُّذَبْذَبِينَ بَيْنَ ذَٰلِكَ لَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ وَلَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿١٤٣﴾

143. Madhabidhabina baina ya hayo (imaan na kufru), hawako kwa hawa wala hawako kwa wale. Na ambaye Allaah Amempotoa huwezi kumpatia njia (ya kumhidi).

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجْعَلُوا لِلَّـهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿١٤٤﴾

144. Enyi walioamini! Msiwafanye makafiri kuwa marafiki wandani na walinzi badala ya Waumini. Je, mnataka Allaah Awe na hoja bayana dhidi yenu?

 

 

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا ﴿١٤٥﴾

145. Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika moto, na wala hutompata kwa ajili yao mwenye kunusuru.

 

 

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَاعْتَصَمُوا بِاللَّـهِ وَأَخْلَصُوا دِينَهُمْ لِلَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَسَوْفَ يُؤْتِ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٤٦﴾

146. Isipokuwa wale waliotubu, na wakarekebisha mwenendo wao, na wakashikamana na Allaah, na wakakhalisisha Dini yao kwa ajili ya Allaah, basi hao watakuwa pamoja na Waumini. Na Allaah Atawapa Waumini ujira mkubwa kabisa. 

 

 

مَّا يَفْعَلُ اللَّـهُ بِعَذَابِكُمْ إِن شَكَرْتُمْ وَآمَنتُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ شَاكِرًا عَلِيمًا ﴿١٤٧

147. Allaah Hatokuadhibuni ikiwa mtashukuru na mtaamini. Na Allaah daima Ni Mwenye Kupokea Shukurani, Mjuzi wa yote.

 

 

لَّا يُحِبُّ اللَّـهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا عَلِيمًا ﴿١٤٨﴾

148. Allaah Hapendi uovu utajwe hadharani isipokuwa kwa yule aliyedhulumiwa. Na Allaah daima Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

إِن تُبْدُوا خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا عَن سُوءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا قَدِيرًا ﴿١٤٩﴾

149. Mkidhihirisha kheri au mkiificha au mkisamehe uovu, basi hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kusamehe, Muweza wa yote.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُوا بَيْنَ اللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ وَنَكْفُرُ بِبَعْضٍ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُوا بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١٥٠﴾

150. Hakika wale wanaomkufuru Allaah na Rusuli Wake, na wanataka kufarikisha baina ya Allaah na Rusuli Wake, na wanasema: Tunaamini baadhi na tunawakanusha baadhi, na wanataka kuchukua njia iliyo baina ya hayo.

 

 

أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ حَقًّا ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٥١﴾

151. Hao ndio makafiri wa kweli. Na Tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.

 

 

وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَلَمْ يُفَرِّقُوا بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ أُولَـٰئِكَ سَوْفَ يُؤْتِيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٥٢﴾

152. Na wale waliomwamini Allaah na Rusuli Wake na hawakumfarikisha yeyote baina yao, hao Atawapa ujira wao. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

يَسْأَلُكَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَن تُنَزِّلَ عَلَيْهِمْ كِتَابًا مِّنَ السَّمَاءِ ۚ فَقَدْ سَأَلُوا مُوسَىٰ أَكْبَرَ مِن ذَٰلِكَ فَقَالُوا أَرِنَا اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ بِظُلْمِهِمْ ۚ ثُمَّ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ فَعَفَوْنَا عَن ذَٰلِكَ ۚ وَآتَيْنَا مُوسَىٰ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿١٥٣﴾

153. Wanakuuliza Watu wa Kitabu uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Kwa yakini walimuuliza Muwsaa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuonyeshe Allaah waziwazi. Basi iliwachukua radi na umeme angamizi kwa dhulma yao. Kisha wakamchukua ndama kumwabudu baada ya kwisha kuwajia hoja bayana. Tukawasamehe hayo, na Tukampa Muwsaa mamlaka bayana.

 

 

وَرَفَعْنَا فَوْقَهُمُ الطُّورَ بِمِيثَاقِهِمْ وَقُلْنَا لَهُمُ ادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُلْنَا لَهُمْ لَا تَعْدُوا فِي السَّبْتِ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا﴿١٥٤﴾

154. Na kwa (kuvunja) fungamano lao, Tuliunyanyua juu yao mlima, na Tukawaambia: Ingieni mlangoni hali mkiwa mmeinama kwa kunyenyekea, na Tukawaambia: Msitaadi mipaka ya As-Sabt[31] (Jumamosi). Na Tukachukua kutoka kwao fungamano madhubuti.

 

 

فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ وَكُفْرِهِم بِآيَاتِ اللَّـهِ وَقَتْلِهِمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَقَوْلِهِمْ قُلُوبُنَا غُلْفٌ ۚ بَلْ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَيْهَا بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٥٥﴾

155. Basi (Tuliwalaani) kwa kuvunja kwao fungamano lao, na kukanusha kwao Aayaat (na Ishara, Miujiza, Dalili, Hoja) za Allaah, na kuua kwao Manabii bila ya haki, na kusema kwao: Nyoyo zetu zimefumbwa; bali Allaah Amezipiga chapa juu yake kwa sababu ya kufuru zao, basi hawatoamini ila kidogo. 

 

 

وَبِكُفْرِهِمْ وَقَوْلِهِمْ عَلَىٰ مَرْيَمَ بُهْتَانًا عَظِيمًا ﴿١٥٦﴾

156. Na kwa kufuru yao (kumpinga Iysaa), na kumzushia kwao Maryam uongo mkubwa mno!

 

 

 

وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّـهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا ﴿١٥٧﴾

157. Na kusema kwao (kwa kujifaharisha): Hakika sisi tumemuua Al-Masiyh ‘Iysaa mwana wa Maryam, Rasuli wa Allaah. Na hawakumuua wala hawakumsulubu lakini walishabihishiwa tu. Na hakika wale waliokhitilafiana katika hayo, kwa hakika wamo katika shaka nayo. Hawana ujuzi nalo kabisa isipokuwa kufuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumuua.[32] 

 

 

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٥٨﴾

158. Bali Allaah Alimnyanyua Kwake. Na Allaah daima Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.  

 

 

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا ﴿١٥٩﴾

159. Na hakuna yeyote katika Watu wa Kitabu ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.[33]  

 

فَبِظُلْمٍ مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ طَيِّبَاتٍ أُحِلَّتْ لَهُمْ وَبِصَدِّهِمْ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ كَثِيرًا ﴿١٦٠﴾

160. Basi kwa dhulma ya Mayahudi, Tuliwaharamishia vizuri walivyohalalishiwa, na kwa sababu ya kuwazuilia kwao wengi Njia ya Allaah.  

 

 

وَأَخْذِهِمُ الرِّبَا وَقَدْ نُهُوا عَنْهُ وَأَكْلِهِمْ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٦١﴾

161. Na kuchukua kwao riba na hali wamekatazwa kuichukua, na kula kwao mali za watu kwa ubatwilifu. Na Tumewaandalia makafiri katika wao adhabu iumizayo. 

 

 

لَّـٰكِنِ الرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ مِنْهُمْ وَالْمُؤْمِنُونَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ ۚ وَالْمُقِيمِينَ الصَّلَاةَ ۚ وَالْمُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالْمُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ أُولَـٰئِكَ سَنُؤْتِيهِمْ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٦٢﴾

162. Lakini wenye msingi madhubuti katika ilimu miongoni mwao na Waumini (kati yao), wanaamini yale uliyoteremshiwa (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako. Na pia wasimamishao Swalaah, na watoao Zakaah na wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho, hao (wote) Tutawapa ujira mkubwa kabisa.

 

 

إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾

163. Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Manabii baada yake. Na Tumemfunulia Wahy Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw,[34] (kizazi chake) na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zabuwr.

 

 

وَرُسُلًا قَدْ قَصَصْنَاهُمْ عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَرُسُلًا لَّمْ نَقْصُصْهُمْ عَلَيْكَ ۚ وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا ﴿١٦٤﴾

164. Na Rusuli Tuliokwishakusimulia kabla, na Rusuli (wengine) Hatukukusimulia.[35] Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno moja kwa moja.[36]

 

 

رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٦٥﴾

165. Rusuli ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya (kuletwa) Rusuli. Na Allaah daima Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote. 

 

 

لَّـٰكِنِ اللَّـهُ يَشْهَدُ بِمَا أَنزَلَ إِلَيْكَ ۖ أَنزَلَهُ بِعِلْمِهِ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ يَشْهَدُونَ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿١٦٦﴾

166. Lakini Allaah Anayashuhudia Aliyoyateremsha kwako. Ameyateremsha kwa Ilimu Yake, na Malaika pia wanashuhudia. Na Anatosheleza Allaah kuwa Mwenye Kushuhudia yote.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ قَدْ ضَلُّوا ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١٦٧﴾

167. Hakika wale waliokufuru na wakazuia Njia ya Allaah, kwa yakini wamekwishapotea upotofu wa mbali. 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَظَلَمُوا لَمْ يَكُنِ اللَّـهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ طَرِيقًا ﴿١٦٨﴾

168. Hakika wale waliokufuru na wakadhulumu, haitokuwa kwa Allaah kuwaghufuria wala kuwaongoza njia. 

 

 

إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿١٦٩﴾

169. Isipokuwa njia ya Jahannam wadumu humo milele. Na hayo kwa Allaah ni mepesi.

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمُ الرَّسُولُ بِالْحَقِّ مِن رَّبِّكُمْ فَآمِنُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٧٠﴾

170. Enyi watu! Kwa yakini amekujieni Rasuli kwa haki kutoka kwa Rabb wenu. Basi aminini, ni bora kwenu. Na mkikufuru, basi hakika ni vya Allaah Pekee vilivyomo mbinguni na ardhini. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّـهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۖ وَلَا تَقُولُوا ثَلَاثَةٌ ۚ انتَهُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ إِنَّمَا اللَّـهُ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖسُبْحَانَهُ أَن يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ ۘ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿١٧١﴾

171. Enyi Watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msimzungumzie Allaah isipokuwa ukweli. Hakika Al-Masiyh ‘Iysaa mwana wa Maryam ni Rasuli wa Allaah na ni Neno Lake (la Kun!) Alompelekea Maryam na Ruwh (roho Aliyoumba kwa amrisho) kutoka Kwake. Basi mwaminini Allaah na Rusuli Wake. Wala msiseme: ‘watatu’. Komeni! Ni kheri kwenu. Hakika Allaah ni Mwabudiwa wa haki Mmoja Pekee, Ametakasika na kuwa na mwana![37] Ni Vyake vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Na Anatosheleza Allaah kuwa Ni Mtegemewa wa yote.

 

 

 

لَّن يَسْتَنكِفَ الْمَسِيحُ أَن يَكُونَ عَبْدًا لِّلَّـهِ وَلَا الْمَلَائِكَةُ الْمُقَرَّبُونَ ۚ وَمَن يَسْتَنكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيْهِ جَمِيعًا ﴿١٧٢﴾

172. Al-Masiyh kamwe hatojiona bora aje akatae kuwa ni mja kwa Allaah, wala Malaika waliokurubishwa. Na atakayejiona bora akakataa Kumwabudu (Allaah) na akatakabari, basi Atawakusanya wote Kwake.

 

 

فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضْلِهِ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ اسْتَنكَفُوا وَاسْتَكْبَرُوا فَيُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٧٣﴾

173. Ama wale walioamini na wakatenda mema, (Allaah) Atawalipa kwa ukamilifu ujira wao, na Atawazidishia katika Fadhila Zake. Ama waliojiona bora wakagoma na wakatakabari, basi hao Atawaadhibu adhabu iumizayo, na wala hawatopata asiyekuwa Allaah rafiki mlinzi wala mwenye kunusuru.

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا ﴿١٧٤﴾

174. Enyi watu! Kwa yakini imekujieni burhani[38] (hoja, dalili, muujiza) kutoka kwa Rabb wenu na Tumekuteremshieni Nuru bayana. 

 

 

فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَاعْتَصَمُوا بِهِ فَسَيُدْخِلُهُمْ فِي رَحْمَةٍ مِّنْهُ وَفَضْلٍ وَيَهْدِيهِمْ إِلَيْهِ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿١٧٥﴾

175. Ama wale waliomwamini Allaah, na wakashikamana Naye, hao Atawaingiza katika rehma itokayo Kwake na fadhila, na Atawaongoza njia iliyonyooka kuelekea Kwake. 

 

 

يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ ۚ إِنِ امْرُؤٌ هَلَكَ لَيْسَ لَهُ وَلَدٌ وَلَهُ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ ۚ وَهُوَ يَرِثُهَا إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَتَا اثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا الثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ ۚ وَإِن كَانُوا إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَاءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۗ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٧٦﴾

176. Wanakuuliza hukmu ya kisharia. Sema: Allaah Anakubainishieni kuhusu Al-Kalaalah (asiye na wazazi wala watoto). Ikiwa mtu amefariki hana mtoto lakini ana dada, basi atastahiki nusu ya yale aliyoyaacha. Na yeye (huyo mtu) atamrithi huyo dada kama hana mtoto. Na ikiwa madada ni wawili, basi watastahiki thuluthi mbili ya yale aliyoyaacha (maiti). Na wakiwa ni ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamme atastahiki sehemu iliyo sawa na sehemu ya wanawake wawili. Allaah Anakubainishieni ili msipotee, na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

 

 

 

 

 

 

 

[1] Amrisho La Kuunga Undugu Na Matahadharisho Ya Kukata Undugu:  

 

Rejea Ar-Ra’d (13:21), Muhammad (47:22-23).

 

[2] Iliowamiliki Mikono Yao Ya Kulia:

 

Inayomiliki mikono ya kuume ni wale watumwa wa kike waliotekwa na Waislamu katika vita vya Jihaad kisha ikaruhusika kuwaingilia kujamii nao. Uislamu ulipokuja,  ulikuja ili kusawazisha baina ya watu na kuwafanya wawe waadilifu. Na Uislamu ukahimiza kuwafanyia wema watumwa na kuwaacha huru. Na Uislamu ukafanya kafara ya matendo mengi kuwa ni kuacha huru watumwa, na ikawa kukomboa watumwa ni fadhila na thawabu nyingi mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) ili Waislamu wapendezewe kuacha huru na kuwakomboa watumwa. Uislamu ulikuja kuhifadhi heshima ya wanawake na sio kuwatiisha kwa wanaume, kama baadhi ya wanafiki wanaofasiri Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) kutokana na matamanio na upotofu wao.  Rejea pia An-Nisaa (5:25), Al-Muuminuwn (23:6), Al-Ma’aarij (70:30), Al-Ahzaab (33:50) (33:55).  

 

[3]  Uharamisho Wa Ndoa Ya Mut-’ah:  

 

Mut’ah: Maana yake kilugha ni kustarehe. Ama kisharia ni ndoa inayofungwa kwa muda maalumu na kiasi cha pesa maalumu kinachojulikana.

 

Imeitwa jina hilo kwa sababu mwanamume anapata faida na kustarehe kwa muda uliowekwa.

 

Aina hii ya ndoa ilikuwepo katika zama za Jaahiliyyah. Kuna wakati Uislamu ulikataza na wakati uliruhusu kwa masharti maalumu, lakini mwishowe ndoa hii iliharamishwa haramisho la wazi kabisa katika Hijjatul-Wada’ (Hijjah ya mwisho ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Hadiyth ifuatayo:

 

Sabrah bin Ma’abad Al-Juhniy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba baba yake aliandamana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika (ukombozi wa) Fat-h Makkah, akasema: “Enyi watu! Nilikuruhusuni ndoa ya mut-’ah hapo mwanzo. Leo Allaah Ameiharamisha mpaka Siku ya Qiyaamah! Basi ikiwa kuna yeyote ambaye ana mke wa ndoa ya mut-’ah amwache, na wala asichukue chochote katika alichompa.” [Muslim na wengineo]

 

[4] Al-Kabaair (Madhambi Makubwa):

 

Ni madhambi yaliyotajiwa ndani yake laana, au haddi (adhabu) hapa duniani, au yameahidiwa juu yake Ghadhabu za Allaah au moto. Na pia madhambi saba yanayoangamiza yaliyotajwa katika Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) :

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza!” Wakauliza: Ni yepi hayo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Ni kumshirikisha Allaah, sihri (uchawi), kuua nafsi Aliyoiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki, kula riba, kula mali ya yatima, kukimbia wakati wa kupambana na adui, na kuwatuhumu uzinifu wanawake Waumini waliohifadhika walioghafilika.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

[5] Jinsi Ya Kuwatia Adabu Wanawake Wenye Kuasi Katika Ndoa

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):    

 وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ

“Na wahameni katika malazi na wapigeni (kipigo kisichodhuru).”

 

Imekusudiwa kutokulala nao na kutokujimai nao, kwa ujumla ni kuwagomea. Ama kuhusu: “na wapigeni”, hii imekusudiwa kipigo kidogo kisichokuwa cha kuwadhuru, wala haipasi kupigwa usoni.

 

[6] Al-‘Aliyy (الْعَلِيُّ) Al-Kabiyr(الْكَبِيْرُ) : Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.

 

[7] Riyaa-a (Kujionyesha Kwa Watu) Ni Shirki Inayobatwilisha Amali: Rejea Az-Zumar (39:65).

 

[8] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alilia Kusikia Qiraa Cha Aayah Hii:

 

Amesimulia ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniambia: “Nisomee!” Nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Nikusomee na hali (Qur-aan) imeteremshwa kwako? Akasema: “Naam! Lakini mimi napenda kusikia wengine wakiisoma.” Nikasoma Suwratun-Nisaa mpaka nilipofikia Aayah:

 

فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا ﴿٤١﴾

“Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa shahidi juu ya hawa?”

Akasema: “Hasbuka! (Inatosha, simama hapo).” Nikaona machozi yamejaa machoni mwake. [Al-Bukhaariy]

 

Kila Ummah Utahudhurishwa Na Shahidi Wake:

 

Rejea Al-Baqarah (2:143), Al-Israa (17:71), Al-Hajj (22:78), An-Nahl (16:89), Az-Zumar (39:69), Al-Jaathiyah (45:28).

 

[9]  Hatua Za Uharamisho Wa Pombe Na Kikomo Chake:

 

Rejea Al-Baqarah (2:219), na pia Al-Maaidah (5:90-91) ambako kuna maelezo bayana ya Hatua Za Uharamisho Wa Pombe Na Kikomo Chake.

 

[10] Tayammum: Rejea Al-Maaidah (5:6).

 

[11] Maana Ya: رَاعِنَا (Raa’inaa) Na انْظُرْنَا  (Undhwurnaa):

Miongoni mwa ada za Mayahudi ni kuyapotosha Maneno ya Allaah (عزّ وجلّ) kwa kuyatoa kwenye makusudio yake, na pia wanayatafsiri kinyume na maana yake halisi. Na watu wa bid’ah wamejifananisha nao katika kupindisha na kupotosha maana ya Majina ya Allaah na Sifa Zake. Rejea Tanbihi ya Suwrat Al-Baqarah (2:104) ambako kuna maelezo bayana kuhusu maana mbili hizo.

 

[12] As-Sabt: Rejea Al-Baqarah (2:65), Al-A’raaf (7:163-166).

 

[13] Shirki Ni Dhambi Pekee Ambayo Allaah (سبحانه وتعالى)     Hamghufurii Mtu Akifariki

 

Rejea pia Suwrah hii An-Nisaa (4:116).

 

Muislamu anapotenda dhambi, anapaswa kukimbilia haraka kuomba maghfirah na kutubia kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Kwa sababu shirki ni dhambi pekee ambayo Allaah (سبحانه وتعالى)  Hamghufurii mtu pindi akifariki bila ya kutubia. Hivyo basi, hatima yake ni kuingizwa motoni! Makemeo mazito yametajwa katika Qur-aan na Sunnah. Kati ya Hadiyth zinazozungumzia hilo ni:  

 

Amesimulia Ibn Mas‘uwd  (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayefariki akiwa katika hali ya kumshirikisha Allaah kwa chochote, basi ataingia motoni.” [Al-Bukhaariy 1238, Muslim 92]

 

Shirki pia inawahusu makafiri wanaomshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) nao pia wametahadharishwa na kunasihiwa watubie kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah Al-Maaidah (5:72-74).

 

[14] Tofauti Ya Al-Jibt (الجِبْتُ) Na At-Twaaghuwt الطَّاغُوْتُ):

 

Al-Jibt inajumuisha sihri (uchawi), mchawi, kahini na kila aina ya shari na kila ambalo halina kheri. 

 

Ama twaghuti, ni uvukaji mipaka wa kumtoa Allaah (سبحانه وتعالى) kutoka nje ya Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Kumpwekesha katika Uola Wake), na Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (Kumpwekesha katika kumwabudu), au katika Sharia au Hukmu Yake.  Kwa hiyo kila anayemkosea Allaah (عزّ وجلّ) katika hayo, basi yeye ni twaghuti. Ndio maana ‘Ulamaa wamesema kuwa twaghuti ni wengi mno, lakini viongozi wao ni watano: (i) Ibliys laana ya Allaah iwe juu yake, naye ni wa kwanza wao. (ii) Kiumbe yeyote anayeabudiwa akiwa ameridhia hivyo. (iii) Anayelingania watu aabudiwe yeye. (iv) Anayedai kuwa anajua ilimu ya ghaibu. (v) Anayehukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah. [Fat-h Al-Majiyd Sharh Kitaab At-Tawhiyd]

 

Rejea pia Al-Baqarah (2:256).

 

[15] Aayah Pekee Katika Suwrah Hii Kuteremshwa Makkah Na Wasimamizi Wa Funguo Za Al-Ka’abah:

 

Aayah hii ni ya pekee katika Suwrah hii ya An-Nisaa (4:58) ambayo imeteremka Makkah. Imeteremshwa Siku ya Fat-h Makkah (Ukombozi). Ibn Jurayj amehadithia kwamba imeteremshwa kuhusu ‘Uthmaan bin Twalhah pale Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipochukua ufunguo wa Ka’bah kutoka kwake akaingia Ka’bah. Alipotoka nje ya Ka’bah, alitoka huku akiwa anasoma:

 

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا

“Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe.”

 

Hapo akamwita ‘Uthmaan bin Twalhah na akampa funguo. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

Funguo hizo zimeendelea kubakia katika ukoo huo, kizazi baada ya kizazi mpaka zama zetu hizi. Na mpaka Siku ya Qiyaamah ukoo huo umefadhilishwa kuwa ndio wenye amana ya kukamata funguo za Al-Ka’bah.

 

[16] Amri Na Masisitizo Ya Kuwatii Watawala Na Viongozi:

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameamrisha na kusisitiza katika Hadiyth kadhaa suala la kutii watawala na viongozi. Miongoni mwazo ni: “Muislamu anapaswa kusikia na kutii kwa anayoyapenda na anayoyachukia, madhali hakuamrishwa kuasi. Na pindi akiamrishwa katika maasi, basi hakuna kusikia wala kutii.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na amesema pia: “Sikieni na tiini (watawala na viongozi wenu) hata kama ni mtumwa wa Uhabeshi (Ethiopea) ambaye kichwa chake ni kama zabibu.” [Al-Bukhaariy]

 

Amri ya kuwatii kwa wema watawala na viongozi wa mambo ya Waislamu, ni jambo ambalo limenukuliwa na Ijmaa’ juu yake, bali ndiyo ‘Aqiydah sahihi ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah. Lakini kwa masikitiko makubwa jambo hili wamelipuuza wengi katika Waislamu na wale wasiofahamu mafunzo ya Dini yao. Na matokeo ya kwenda kinyume na jambo hilo na ‘Aqiydah hiyo, ni kuleta munkari mkubwa katika Ummah na ufisadi mpana. Kuna wanaofanya maandamano kupinga viongozi, kuna wanaojilipua kwa mabomu na kuua watu, kuna wanaoua watu kwa njia mbali mbali na kadhalika kumwaga damu za wanaadamu bure! Matokeo yake ni kuwa maadui wa Uislamu wametumia njia hiyo ili kuuchafua Uislamu na kuudidimiza.

 

[17] Tofauti Ya Manabii, Swiddiqiyn, Shuhadaa Na Swalihina. 

 

Manabii (الأَنْبِيَاءُ):

 

Manabii na Rusuli ni wengi mno. Baadhi yao wametajwa kwenye Qur-aan na Sunnah na wengineo hawakutajwa. Na baadhi yao visa vyao vimesimuliwa katika Qur-aan na baadhi yao havikusimuliwa. Rejea Ghaafir (40:78) na An-Nisaa (4:164).

Wa kwanza wao ni Nabiy Aadam (عليه السّلام) na wa mwisho wao ni Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). 

 

Tofauti Kati Ya Nabiy Na Rasuli:

 

‘Ulamaa wamezungumza mengi kuhusu tofauti baina ya Nabiy na Rasuli. Kimukhtasari ni kwamba Nabiy ni yule ambaye Ametumwa na Allaah (عزّ وجلّ) bila ya kuteremshiwa sharia au hukmu mpya. Ama Rasuli, ni yule ambaye ameteremshiwa sharia mpya na kuamriwa kufikisha Risala kwa watu wake. Hivyo, Nabiy hutumia sharia ya Rasuli aliyemtangulia.

 

Kwa msingi huu, kila Rasuli ni Nabiy, lakini si kila Nabiy ana sifa ya Rasuli. Na Rasuli ana daraja kubwa kuliko Nabiy kwa sababu Rasuli hubalighisha Risala (Ujumbe) kwa watu wake, huwaonya na huwabashiria. Na jukumu hili bila shaka linahitajia kuwa na subira ya hali ya juu kwa sababu watu wao waliwapinga vikali, wakawakadhibisha, wakawashutumu, wakawasingizia sifa mbaya, na wakawafanyia istihzai, dhihaka, kejeli na hata kuwapangia makri kutaka kuwaua. Kati ya hao ni Rusuli watano waliotajwa katika Suwrat Al-Ahzaab (33:7) ambao walitoa fungamano gumu kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Wanajulikana kuwa ni Ulul-‘Azmi; wenye azimio la nguvu. Rejea Al-Ahqaaf (46:35).

 

Imaam Ibn Baaz (رحمه الله) amesema: “Linalojulikana sana miongoni mwa ‘Ulamaa ni kwamba, Nabiy ni ambaye ameteremshiwa sharia, lakini hakuamrishwa kubalighisha Risala (Ujumbe) kwa watu. Huamrishwa afanye kadhaa na kadhaa, aswali namna kadhaa, afunge Swawm namna kadhaa, lakini haamrishwi kubalighisha Ujumbe kwa watu. Hivyo huyu ni Nabiy. Ama akiamrishwa kubalighisha (Ujumbe) kwa kuwabashiria na kuwaonya watu, huyo anakuwa ni Nabiy na Rasuli kama vile Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), Muwsaa, ‘Iysaa, Nuwh, Huwd, Swaalih (عليهم السلام) na wengineo”. [Mawqi' Ar-Rasmiy li-Samaahat Ash-Shaykh Ibn Baaz]

 

Swiddiyquwn(الصِّدِّيْقُوْنَ) :

 

Asw-Swiddiyq ni Muumini ambaye ni mkweli wa dhati, kwa kauli na matendo, katika Manabii na wafuasi wao, na akathibiti imara katika ukweli  kwa  imaan, na akaamini kila kinachomfikia kutoka kwa Rabb wake au Rasuli wake. Rejea (57:19).

 

Na Allaah (سبحانه وتعالى) Amewataja katika Qur-aan Manabii kwa sifa hii ya Asw-Swiddiyq Katika Yuwsuf (12:46), Maryam (19:41), (19:56) na kwengineko. Kwa hiyo Swiddiyquwn ni wengi. Nabiy Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم) Ametajwa na Allaah (سبحانه وتعالى)  kwa sifa hiyo katika Kauli Yake:

 

وَالَّذِي جَاءَ بِالصِّدْقِ وَصَدَّقَ بِهِ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ﴿٣٣﴾

“Na yule aliyekuja na ukweli na akausadikisha, hao ndio wenye taqwa.” [Az-Zumar: (39:33)]

 

Wafasiri wa Qur-aan wengi wamesema makusudio ya: “Aliyekuja na ukweli” ni Jibriyl   (عليه السلام)alipoteremsha Wahyi (Qur-aan). Na “aliyeusadikisha” ni Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). [Tafsiyr Ibn Kathiyr na Wafasiri wengineo]

 

Abu Bakr (رضي الله عنه) pia amepewa sifa ya Asw-Swiddiyq kwa sababu ya kumwamini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) baada ya safari ya muujiza ya Al-Israa Wal-Mi’raaj (kutoka Makkah hadi mbingu ya saba na kurudi Makkah kwa usiku mmoja). Yeye alimwamini Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na akamsadikisha yote aliyoyasema hapo hapo mbele ya watu, wakati ma-Quraysh wa Makkah walimkadhibisha na kudai kwamba ni uongo. Na bint yake Mama wa Waumin ‘Aaishah (رضي الله عنها), pia amepewa sifa hii kuwa ni Bint Asw-Swiddiyqah (binti wa Abu Bakr (رضي الله عنهما).  

 

Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام)  pia amepewa sifa hii kama Alivyomtaja Allaah (سبحانه وتعالى) katika Kauli Yake:

 

مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖ 

“Al-Masiyh mwana wa Maryam si chochote ila ni Rasuli tu, wamekwishapita kabla yake Rusuli (wengine). Na mama yake ni Muumini mkweli wa dhati.” [Al-Maaidah (5:75)]

 

Katika Hadiyth sifa ya Swiddiyqah imetajwa kuwa ni msema kweli:

 

Amesimulia ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika ukweli unaongoza katika wema, na hakika wema unaongoza katika Jannah, na mtu ataendelea kusema ukweli mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni Swiddiyqaa (mkweli wa dhati). Na hakika uongo unaongoza katika uovu, na hakika uovu unapelekea motoni, na mtu ataendelea kusema uongo mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni muongo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Shuhadaa(شُهَدَاءُ) :

 

Ni Waumini waliouwawa katika Vita Vitukufu vya Jihaad. Hawa sifa yao ni kwamba juu ya kuwa wamefariki duniani, lakini wako hai wanaendelea kuruzukiwa Jannah. Rejea Aal-‘Imraan (3:169-171).

 

Swalihina(صَالِحُوْنَ) :

 

Ni waja wema, Waumini walionyooka katika Dini ya Allaah (سبحانه وتعالى) wakatimiza haki ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kufuata Amri Zake. Pia ni wale wenye ikhlaasw (kutakasa amali zao), na ni wenye taqwa, na watiifu. Nao ni katika Manabii, Rusuli, Shuhadaa (waliofariki au kuuwawa katika vita vitukufu vya Jihaad), Swahaba, na waja wema wengineo wenye sifa hizo. Na pindi inapotajwa Swalihina kwa ujumla basi wote hao ni wenye sifa hizo. Ama inapotajwa Swalihina pamoja na Manabii, Swiddiyqiyna, Shuhadaa na wengineo kama katika Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):       

 

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾

“Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiyqiyna na Shuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao.” [An-Nisaa (4:69)]

 

basi hapo hubainisha kuwa kila mmoja katika hao anatofautiana na mwingine katika daraja na fadhila nyenginezo kama vile ilivyotajwa katika Hadiyth kwamba Shuhadaa (waliofariki katika vita vitukufu) wako hai Peponi. Au kuhusu Manabii kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ameiharamishia ardhi kuila miili yao. Hali kadhalika Swahaba nao wana daraja na fadhila tofauti tofauti.

 

[18] Kumtii Rasuli Ni Kumtii Allaah Na Kumuasi Ni Kumuasi Allaah:

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayenitii basi atakuwa amemtii Allaah, na atakayeniasi basi atakuwa amemuasi Allaah, na atakayemtii Amiri wangu (kiongozi niliyemteua), basi atakuwa amenitii mimi na atakayemuasi atakuwa ameniasi mimi.” [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]

 

Na pia: Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ummah wangu wote wataingia Jannah isipokuwa atakayekataa.” Akaulizwa: Ni yupi atakayekataa ee Rasuli wa Allaah? Akajibu: “Atakayenitii mimi ataingia Jannah, na atakayeniasi basi amekataa.” [Al-Bukhaariy]

 

[19] Al-Wakiyl (الوَكِيْلُ): Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.

 

[20] Radd Kwa Kundi La Al-Mufawwidhwah Wanaodai Kuwa Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى) Hazifahamiki:

 

Aayah hii ni miongoni mwa dalili na radd juu ya kundi la Al-Mufawwidhwah. Wafuasi wa kundi hili wanazikubali Sifa za Allaah, lakini wakati huo huo wanadai kuwa hazifahamiki. Wanasema kuwa Majina ya Allaah na Sifa Zake, maana Zake hazifahamiki, na kwa hivyo Allaah Kawaletea Waja Wake mafundisho ambayo hayaeleweki maana yake. Hii ni itikadi baatwil mno. Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (رحمه الله)  amesema alipolizungumzia pote hili la Mufawwidhwah kuwa ni katika mapote ya bid’ah. Kisha wakainasibisha kauli hii kuwa ni kauli ya Salaf! Huko ni kuwazulia wema waliotangulia (رحمهم الله). Imaam Ahmad anawaona Mufawwidhwah kuwa ni wabaya zaidi kuliko Jahmiyyah.

 

[21] Maonyo Ya Kutangaza Khabari Bila Kuhakikisha:

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Inamtosha mtu kuwa ni muongo kwa kusema kila anachokisikia.” [Amehadithia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) na Muslim kaipokea]

 

Na pia: Amesimulia Al-Mughiyrah bin Shu’bah (رضي الله عنه): Nimemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Hakika Allaah Anachukia kwenu “qiylaa wa qaala” (utesi, udaku n.k), kupoteza mali na kuuliza maswali mengi.” [Al-Bukhaariy na wengineo] “Qiylaa wa qaal” kwa maana: “imesemwa na amesema”, ni ibara inayokusudiwa uvumi, utesi, udaku, umbeya, usengenyaji n.k. Rejea pia Al-Hujuraat (49:6).

 

[22] Jinsi Ya Kuyaitikia Maamkizi Ya Kiislamu Na Baadhi Ya Fadhila Zake:

 

'Imraan bin Al-Huswayn (رضي الله عنهما) amehadithia: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuamkia: "Assalaamu 'alaykum." (Nabiy) akamrudishia salaam). Kisha yule mtu akakaa kitako. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: “Kumi.” (Kwa maana amepata thawabu kumi). Kisha akaja mtu mwengine, akasema: "Assalaamu 'alaykum wa RahmatuLLaah." Naye akamrudishia, kisha yule mtu akakaa kitako, na Nabiy akasema: “Ishirini.” Kisha akaja mtu mwengine akasema: "Assalaamu 'alaykum wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh.” Naye akamrudishia, kisha akasema: “Thelathini.” [Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth Hasan]

Na maamkizi ya Kiislamu ni funguo za Jannah: Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه):  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hamtoingia Jannah hadi muamini, na wala hamuwezi kuamini hadi mpendane. Je, nikujulisheni jambo ambalo mtakapolifanya mtapendana? Toleaneni Salaam baina yenu.” [Muslim]

 

Pia katika khutbah yake ya mwanzo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipohajiri Madiynah alisema: “Enyi watu! Enezeni salaam, na lisheni chakula, na swalini watu wakiwa wamelala (Qiyaam), mtaingia Jannah kwa amani.” [At-Tirmidhiy – Hadiyth Hasan]

 

[23] Haramisho La Kuua Bila Haki Na Adhabu Zake:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Ameharamisha mauaji bila ya haki, na Anatoa adhabu kali kabisa kwa kosa hili! Aayah hii na inayofuatia (4:92-93) ni miongoni mwa dalili za haramisho hilo. Hali kadhaalika dalili zimo katika Sunnah. Miongoni mwazo ni Hadiyth hii:

 

Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amru (رضي الله عنه) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Kutokomea dunia ni kwepesi zaidi kuliko kuua Muislamu.” [Swahiyh An-Nasaaiy (3998)]

 

Pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wangeshirikiana watu wa mbinguni na ardhini kumwaga damu ya Muumini, Allaah Angewaingiza (wote) motoni.” [Amehadithia Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه), na Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika Swahiyh At-Targhiyb]

 

Amesema pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Muumini hatoacha kuwa katika Dini yake madamu hajagusa damu ya haramu (hajamwaga damu).” [Al-Bukhaariy]

 

[24] Maamrisho Ya Kusimamisha Swalaah Kwa Nyakati Zake Na Makemeo Ya Kuipuuza:

 

Maamrisho ya kusimamisha Swalaah kwa nyakati zake yamesisitizwa katika Qur-aan na Sunnah. Na miongoni mwa Hadiyth za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zinazogusia hilo ni: Kitu cha kwanza atakachohesabiwa nacho mja Siku ya Qiyaamah katika amali zake ni Swalaah, ikitengenea atakuwa amefuzu na amefanikiwa, na ikiharibika atakuwa ameshapita patupu na amekhasirika…” [At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]

 

Pia Buraydah bin Al-Haswiyb (رضي الله عنه) amehadithia: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Mafungamano baina yetu na baina yao (wasio Waislamu) ni Swalaah, atakayeiacha atakuwa amekufuru.” [Ahmad, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

Imaam ibn Baaz (رحمه الله) amesema: “Yeyote atakayeweka makusudi kengele ya saa imuamshe baada ya kutoka jua akakosa Swalaah ya Alfajiri, basi mtu huyo amepuuza kuswali kwa wakati wake, na kufanya hivyo ni kufru kubwa kama walivyokubaliana ‘Ulamaa wengi, kwa sababu amekusudia kuswali baada ya jua kutoka. Ni sawa na mtu ambaye anachelewesha kuswali Alfajiri akaiswali karibu na Adhuhuri. [Fataawa Ibn Baaz, Kitaab As-Swalaah (10/374)]

 

Rejea pia Maana Ya Kusimamisha Swalaah katika Al-Baqarah (2:3). Rejea pia Al-Muuminuwn (23:1).

 

[25] Kuswali Rakaa Mbili Baada Ya Kutenda Dhambi Kwa Ajili Ya Maghfirah:  

 

Amesimulia ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه):  Kila niliposikia jambo kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), Allaah Huninufaisha kwa Apendayo kuninufaisha. Abuu Bakr amenihadithia, na Abuu Bakr amesadikisha, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna Muislamu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akatawadha akaswali rakaa mbili, kisha aombe maghfirah, basi hakuna isipokuwa Allaah Atamghufuria.” Kisha akasoma Aayah mbili hizi:

 

وَمَن يَعْمَلْ سُوءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ اللَّـهَ يَجِدِ اللَّـهَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١١٠﴾

“Na atakayetenda ovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akamwomba Allaah maghfirah, basi atamkuta Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.” [An-Nisaa (4:110)]

 

Na:

وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾

“Na ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na hali wanajua.” [Aal-‘Imraan (3:135)]

 

[Imepokelewa na Ahmad katika Musnad yake, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, na Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (406) na Swahiyh At-Targhiyb (680)]

 

[26] Shirk Ni Dhambi Pekee Ambayo Allaah Hamghufurii Mtu.  Rejea Suwrah hii (4:48).

 

[27]  Laana Ya Allaah Kwa Mwenye Kujibadilisha Maumbile: 

 

‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) alisema: “Allaah Anawalaani wanaopiga chale na wanaotaka kupigwa chale, na wanaochonga nyusi, na wanaochonga meno wakaacha mwanya kwa sababu ya uzuri, wanaobadilisha maumbile Aliyoyaumba Allaah.” Mwanamke mmoja akamlaumu juu ya jambo hilo (la kulaani). Akasema (‘Abdullaah): “Kwa nini nisimlaani aliyelaaniwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na ilhali iko ndani ya Kitabu cha Allaah? Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

 

وَمَا آتَاكُمْ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا

“Na lolote analokupeni Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na analokukatazeni, basi liepukeni.” [Al-Hashr (59:7)]  [Al-Bukhaariy na Muslim] 

 

Na katika riwaayah nyingine imetajwa: “Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amemlaani mwenye kuunga na mwenye kuungwa (nywele)…”

 

[28] Al-Wakiyl (الوَكِيْلُ): Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.

 

[29] Kufanya Istihzai Ni Miongoni Mwa Yanayomtoa Mtu Nje Ya Uislamu:

 

Miongoni mwa yanayomtoa mtu nje ya Uislamu ni kufanyia istihzai Maneno ya Allaah! Ni kama ilivyotajwa katika Nawaaqidhw Al-Islaam: “Mwenye kufanyia istihzai (shere, dhihaka, masikhara) kwa chochote katika Dini ya Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), au akafanya utani katika Thawabu au katika Adhabu za Allaah, basi amekufuru.” [Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab, Nawaaqidhw Al-Islaam]

 

Ni tahadharisho na onyo kubwa kwa Waislamu, kwani wengi katika mabaraza yao wanapoongea, hupenda kufanya istihzai kwa mambo ya Dini wakidhania kuwa ni jambo la kawaida ilhali hatari yake ni kubwa mno! Rejea At-Tawbah (9:64-66) ambapo Allaah (سبحانه وتعالى) Amehukumu kuwa kufanya istihzai katika Dini ni kufru!

 

Kuna wanaofanya istihzai na dhihaka kwa Aayah au maneno ya Qur-aan au Majina ya Suwrah za Qur-aan! Au kuhusu Manabii na Rusuli waliopita pamoja na kaumu zao. Wengine hufanya istihzai na dhihaka katika sharia za Dini kama vile kuwacheka Waumini kuhusu Isbaal (kanzu kutokuvuka mafundo ya miguu), au istihzai kuhusu ndevu n.k. Hayo yote na mengineyo yoyote ya istihzai na dhihaka katika Dini ni kukufuru!

   

[30] Riyaa-a (Kujionyesha Kwa Watu): Riyaa-a Inabatwilisha Amali:

 

Riyaa-a katika kuswali ni aina mojawapo ya riyaa-a. Rejea Al-Maa’uwn (107:4-6).  Rejea pia Az-Zumar (39:65) kwenye maelezo kuhusu aina za shirki.

 

[31] As-Sabt: Rejea Al-Baqarah (2:65), An-Nisaa (4:47), Al-A’raaf (7:165) na An-Nahl (16:124).

 

[32] Dalili Nyengineyo Kwamba Nabiy ‘Iysaa  (عليه السّلام) Hakufishwa Bali Yu Hai Mbinguni:

 

Aayah hii na zinazofuatia (155-157), ni dalili nyengineyo inayothibitisha kwamba Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) hakufishwa, bali amenyanyuliwa na Allaah mbinguni. Maelezo zaidi Rejea Aal-‘Imraan (3:55).  

 

[33] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Yu Hai Mbinguni Na Atateremka Duniani Kama Ni Alama Kubwa Za Qiyaamah: 

 

Ni hoja na dalili bayana kwa wanaokanusha kuteremka kwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) katika zama za mwisho kukaribia Qiyaamah. Rejea pia Az-Zukhruf (43:61). Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) atateremka kutoka mbinguni kuja duniani kama ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah, na atatekeleza mambo ambayo yametajwa katika Hadiyth ifuatayo ambayo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

 

 وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمْ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا  

“Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake! Hivi karibuni atateremka kwenu mwana wa Maryam ('Iysaa) akiwa ni kiongozi muadilifu. [Al-Bukhaariy, Muslim] 

 

Hali kadhaalika, kuna Hadiyth nyinginezo za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zenye kuthibitisha hilo kama hizi zifuatazo:   

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake! Hivi karibuni atateremka kwenu mwana wa Maryam ('Iysaa) akiwa ni kiongozi muadilifu, na atavunja misalaba na kuua nguruwe, na ataondosha jizyah (ushuru kutoka kwa wasio Waislamu ambao wamo katika himaya ya serikali ya Waislamu). Kisha kutakuwa na mali nyingi hadi itafikia kuwa hakuna mtu wa kupokea swadaqa. Wakati huu sijda moja itakuwa ni bora kwao kuliko maisha haya na yote yaliyomo (katika dunia).” Kisha Abuu Huraryah akasema: Someni mkipenda:

 

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا ﴿١٥٩﴾

“Na hakuna yeyote katika Watu wa Kitabu ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.”   (4:159) [Al-Bukhaariy]

 

Na pia: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mtakuwaje atakapoteremka Al-Masiyh, mwana wa Maryam (‘Iysaa) akiwa Imaam wenu miongoni mwenu wenyewe?” [Al-Bukhaariy]

 

Na pia amesema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Manabii ni bin-‘ammi; mama zao tofauti, lakini Dini yao moja. Mimi ndiye mwenye haki zaidi kwa ‘Iysaa mwana wa Maryam kuliko yeyote mwengine, kwani hapajakuwa na Nabiy baina yake na mimi. Atateremka, na mtakapomuona mtamtambua. Ni mtu aliyeumbika vizuri, rangi (ya ngozi) yake iko baina ya nyekundu na nyeupe. Atateremka akiwa amevaa nguo mbili ndefu, rangi ya njano isiyokoza. Kichwa chake kitakuwa kina michirizi ya matone ya maji, japokuwa umande haukugusa. Atavunja misalaba, ataua nguruwe, ataondosha jizyah na atawaita watu katika Uislamu. Wakati huu, Allaah Ataangamiza dini zote isipokuwa Uislamu, na Allaah Atamuangamiza Masiyh-Dajjaal. Usalama utajaa ardhini, hadi kwamba simba watachanganyika na ngamia, chui na ng'ombe, fisi na kondoo, na watoto watacheza na nyoka na hawatowadhuru. ‘Iysaa atabakia muda wa miaka arubaini kisha atafariki, na Waislamu watamswalia Swalaah ya janaazah.” [Abuu Daawuwd, Ahmad na Al-Albaaniy ameisahihisha katika Swahiyh Al-Jaami’ (2182)]

Rejea pia Aal-‘Imraan (3:55).

 

[34] Al-Asbaatw: Rejea Al-Baqarah (2:136).

 

[35]  Baadhi Ya Rusuli Vimesimuliwa Visa Vyao Na Baadhi Yao Havikusimuliwa:

 

Rejea Ghaafir (40:78). Al-‘An’aam (6:83), pia An-Nisaa (4:69) kupata maelezo kuhusu tofauti ya Manabii na Rusuli.

 

[36] Allaah (سبحانه وتعالى) Alimsemesha Nabiy Muwsaa  (عليه السّلام) Kwa Uhakika Wake Na Hii Ndio ‘Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Sifa Zake Allaah (سبحانه وتعالى).   

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Alimsemesha Muwsaa (عليه السلام) Maneno kwa uhakika wake na si kwa majazi kama wanavyosema watu wa bid’ah, bali ni maneno yaliyojengeka kwa herufi na sauti. Na Sifa ya Maneno ni Sifa iliyothibiti kwa Allaah kwa uhakika wake bila kuifanyia Ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala Tamthiyl (kumithilisha, kufafanisha, kulinganisha), wala Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah), wala Tahriyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutoa maana isiyo sahihi).

 

Na hii ndiyo kauli ya sawa ambayo wamepita kwayo Salaf na Imaam wa haki katika Uislamu katika Sifa zote zilizokuja ndani ya Qur-aan, rejea pia Al-A’raaf (7:143). Na katika Sunnah, Hadiyth zifuatazo:

 

Amesimulia ‘Adiy Bin Haatim (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna yeyote miongoni mwenu isipokuwa Allaah Atazungumza naye Siku ya Qiyaamah, kutakuwa hakuna mkalimani kati yake na Allaah. Kisha ataangalia na wala hatoona kitu alichokitanguliza, kisha ataangalia mbele yake ataona moto unampokea. Kwa hiyo, awezaye kuiokoa nafsi yake na moto kwa kutoa (swadaqa) kipande cha tende moja, na afanye hivyo.” [Al-Bukhaariy]

 

Na pia Hadiyth ndefu ya Ash-Shafaa’ah (uombezi) Siku ya Qiyaamah, ambayo amesimulia Anas (رضي الله عنه): …Watakwenda kwa Ibraahiym. Naye atawaambia: Siwezi kufanya mnaloomba! Nendeni kwa Muwsaa mja ambaye Allaah Alizungumza naye na Akampa Tawraat. [Al-Bukhaariy]

 

[37] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام)  Na Mama Yake Si Washirika Wa Allaah:

Allaah (سبحانه وتعالى) Amewakataza Watu Wa Kitabu (Mayahudi Na Manaswara) wasimfanye ‘Iysaa na Mama yake kuwa ni washirika wa Allaah, bali hao ni waja wawili katika waja wema wa Allaah, na si washirika Wake kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) Akimzungumzia Maryam na kumzaa kwake Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام)  katika Suwrat Maryam (19:16-36). Na pia katika Suwrah Al-Maaidah (5:17), (72-76), (116-118), Rejea pia At-Tawbah (9:30-31).

 

Pia ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه)  amehadithia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kushuhudia kuwa laa ilaaha illa Allaah (hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), Pekee, Hana mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wake na Rasuli Wake, na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah na Rasuli Wake, na Neno Lake (la Kun!) Aliloliweka kwa Maryam na roho ni kutoka Kwake (Ameiumba), na Jannah (Pepo) ni haki, na moto ni haki, Allaah Atamuingiza Jannah kwa ‘amali zozote alizonazo.” [Al-Bukhaariy] Na katika riwaayah nyingine: “Ataingizwa Jannah katika milango minane ataingia katika wowote aupendao.” [Muslim]

 

[38] Burhani: Muujiza, Ushahidi, Ishara, Dalili, Hoja za waziwazi kabisa zenye kuthibitisha kwa yakini na bila ya shaka na bila ya kupingika.

 

 

 

Share