057 - Al-Hadiyd

 

  الْحَدِيد

 

057-Al-Hadiyd

 

 057-Al-Hadiyd: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١﴾

1. Vimemsabbih Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na ardhi,[1] Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[2]

 

 

 

 

لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢﴾

2. Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, Anahuisha na Anafisha, Naye juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

 

 

هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣﴾

3. Yeye Ndiye wa Awali hakuna kitu kabla Yake, na wa Mwisho hakuna kitu baada Yake, na Aliye juu hakuna kitu juu Yake, na Aliye karibu, hakuna kitu kilichokaribu kuliko Yeye, Naye kwa kila kitu Ni Mjuzi.

 

 

 

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٤﴾

4. Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Akawa juu[3]  ya ‘Arsh. Anajua yale yanayoingia ardhini, na yale yatokayo humo, na yale yanayoteremka kutoka mbinguni, na yale yanayopanda humo. Naye Yu Pamoja nanyi popote mlipo. Na Allaah Ni Mwenye Kuona yote myatendayo.

 

 

 

 

لَّهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٥﴾

5. Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, na kwa Allaah Pekee yanarejeshwa mambo yote.

 

 

 

 

يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۚ وَهُوَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٦﴾

6. Anauingiza usiku katika mchana, na Anaingiza mchana katika usiku, Naye Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.

 

 

 

 

آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَأَنفِقُوا مِمَّا جَعَلَكُم مُّسْتَخْلَفِينَ فِيهِ ۖ فَالَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَأَنفَقُوا لَهُمْ أَجْرٌ كَبِيرٌ ﴿٧﴾

7. Muaminini Allaah na Rasuli Wake, na toeni kutokana na yale Aliyokufanyieni kuwa warithi kwayo. Basi wale walioamini miongoni mwenu, na wakatoa, watapata ujira mkubwa.

 

 

 

 

وَمَا لَكُمْ لَا تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۙ وَالرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ لِتُؤْمِنُوا بِرَبِّكُمْ وَقَدْ أَخَذَ مِيثَاقَكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨﴾

8. Na mna nini nyinyi hata msimwamini Allaah, na hali Rasuli anakuiteni ili mumuamini Rabb wenu, Naye (Allaah) Amekwishachukua fungamano lenu mkiwa nyinyi ni Waumini!  

 

 

 

 

 

هُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ عَلَىٰ عَبْدِهِ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ بِكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٩﴾

9. Yeye Ndiye Anayemteremshia Mja Wake Aayaat bayana ili Akutoeni katika viza na kukuingizeni kwenye nuru. Na hakika Allaah kwenu Ni Mwenye Huruma mno, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

 

وَمَا لَكُمْ أَلَّا تُنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلِلَّـهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١٠﴾

10. Na mna nini hata hamtoi katika Njia ya Allaah, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Allaah Pekee! Hawi sawa miongoni mwenu aliyetoa kabla ya Ushindi (wa Makkah) na akapigana. Hao watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baadae na wakapigana.  Na wote Allaah Amewaahidi malipo mazuri kabisa. Na Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

 

 

مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ ﴿١١﴾

11. Nani ambaye atamkopesha Allaah karadha mzuri kisha (Allaah) Amuongezee maradufu na apate ujira mtukufu?[4]

 

 

 

 

 

يَوْمَ تَرَى الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ يَسْعَىٰ نُورُهُم بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِم بُشْرَاكُمُ الْيَوْمَ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾

12. Siku utakayowaona Waumini wa kiume na Waumini wa kike, nuru yao inakwenda mbele yao na kuliani kwao; (wataambiwa): Bishara njema kwenu leo! Jannaat zipitazo chini yake mito, mdumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa mno.[5]

 

 

 

 

يَوْمَ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ لِلَّذِينَ آمَنُوا انظُرُونَا نَقْتَبِسْ مِن نُّورِكُمْ قِيلَ ارْجِعُوا وَرَاءَكُمْ فَالْتَمِسُوا نُورًا فَضُرِبَ بَيْنَهُم بِسُورٍ لَّهُ بَابٌ بَاطِنُهُ فِيهِ الرَّحْمَةُ وَظَاهِرُهُ مِن قِبَلِهِ الْعَذَابُ ﴿١٣﴾

13. Siku wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike watakapowaambia wale walioamini: Tungojeeni, tupate mwangaza kutokana na nuru yenu! (Wataambiwa): Rudini nyuma yenu, mtafute huko nuru (yenu)! Kisha utawekwa ukuta baina yao wenye mlango, ndani mna rehma na nje kwa upande wake wa mbele mna adhabu.

 

 

 

 

يُنَادُونَهُمْ أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ وَلَـٰكِنَّكُمْ فَتَنتُمْ أَنفُسَكُمْ وَتَرَبَّصْتُمْ وَارْتَبْتُمْ وَغَرَّتْكُمُ الْأَمَانِيُّ حَتَّىٰ جَاءَ أَمْرُ اللَّـهِ وَغَرَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿١٤﴾

14. (Wanafiki) watawaita: Je, kwani hatukuwa pamoja nanyi? Watasema: Ndio (mlikuwa)! Lakini nyinyi mlizifitini nafsi zenu, na mkangojea itusibu misiba na mkatia shaka, na yakakughururini matumaini ya uongo mpaka ikaja Amri ya Allaah, na akakughuruni mdanganyifu (Ibliys) kuhusu Allaah.

 

 

 

 

فَالْيَوْمَ لَا يُؤْخَذُ مِنكُمْ فِدْيَةٌ وَلَا مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ مَأْوَاكُمُ النَّارُ ۖ هِيَ مَوْلَاكُمْ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٥﴾

15. Basi leo haitochukuliwa kutoka kwenu fidia wala kutoka kwa waliokufuru. Makazi yenu ni moto, huo ndio unaostahiki kwenu, na ubaya ulioje mahali pa kuishia!

 

 

 

 

أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿١٦﴾

16. Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah na yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawatawilikia muda, kisha zikasusuwaa nyoyo zao? Na wengi miongoni mwao ni mafasiki.[6]

 

 

 

 

اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٧﴾

17. Jueni kwamba Allaah Anahuisha ardhi baada ya kufa kwake. Hakika Tumekubainishieni Aayaat (Ishara, Dalili) ili mpate kutia akilini.

 

 

 

 

 

إِنَّ الْمُصَّدِّقِينَ وَالْمُصَّدِّقَاتِ وَأَقْرَضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعَفُ لَهُمْ وَلَهُمْ أَجْرٌ كَرِيمٌ ﴿١٨﴾

18. Hakika wanaume watoao swadaqa na wanawake watoao swadaqa na wakamkopesha Allaah karadha mzuri, watazidishiwa maradufu, na watapa ujira mtukufu.[7]

 

 

 

 

 

وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصِّدِّيقُونَ ۖ وَالشُّهَدَاءُ عِندَ رَبِّهِمْ لَهُمْ أَجْرُهُمْ وَنُورُهُمْ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿١٩﴾

19. Na wale waliomwamini Allaah na Rusuli Wake, hao ndio Asw-Swiddiyquwn (waliosadikisha kikweli) na Shuhadaa[8] mbele ya Rabb wao. Watapa ujira wao na nuru yao. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu, hao ni watu wa moto uwakao vikali mno.

 

 

 

 

اعْلَمُوا أَنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ ۖ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ الْكُفَّارَ نَبَاتُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَامًا ۖ وَفِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٌ ۚ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿٢٠﴾

20. Jueni kwamba hakika uhai wa dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu, na kushindana kwa wingi wa mali na Watoto. Ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha inanyweya, basi utaiona imepiga unjano, kisha inakuwa mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka.  Na Aakhirah kuna adhabu kali, na maghfirah kutoka kwa Allaah na radhi. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni starehe fupi za kughuri.[9]

 

 

 

 

سَابِقُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا كَعَرْضِ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أُعِدَّتْ لِلَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٢١﴾

21. Kimbilieni kuomba maghfirah[10] kwa Rabb wenu na Jannah (ambayo) upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, imeandaliwa kwa wale waliomwamini Allaah na Rusuli Wake. Hiyo ni Fadhila ya Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye Fadhila adhimu.

 

 

 

 

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٢٢﴾

22. Hausibu msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu kabla Hatujautokezesha. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.[11]

 

 

 

 

لِّكَيْلَا تَأْسَوْا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا تَفْرَحُوا بِمَا آتَاكُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ ﴿٢٣﴾

23. Ili msisononeke kwa yale yaliyokuondokeeni na wala msifurahie kwa yale Aliyokupeni (Allaah). Na Allaah Hapendi kila mwenye kujinata, anayejifakharisha.

 

 

 

 

الَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبُخْلِ ۗ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٢٤﴾

24. Ambao wanafanya ubakhili na wanaamrisha watu ubakhili. Na atakayekengeuka, basi hakika Allaah Ndiye Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.

 

 

 

 

لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ ۖ وَأَنزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٢٥﴾

25. Kwa yakini Tuliwapeleka Rusuli Wetu kwa hoja bayana, na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na miyzaan (hukumu) ili watu waamiliane kwa uadilifu. Na Tukateremsha chuma chenye nguvu shadidi na manufaa kwa watu, na ili Allaah Adhihirishe nani atakayeinusuru (Dini Yake) na Rusuli Wake hali ya kuwa amemtakasia niya bila kumwona. Hakika Allaah Ni Mwenye nguvu zote, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika.

 

 

 

 

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا وَإِبْرَاهِيمَ وَجَعَلْنَا فِي ذُرِّيَّتِهِمَا النُّبُوَّةَ وَالْكِتَابَ ۖ فَمِنْهُم مُّهْتَدٍ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٢٦﴾

26. Na kwa yakini Tulimtuma Nuwh, na Ibraahiym, na Tukaweka katika dhuriya wao Unabii na Kitabu. Basi miongoni mwao wako waongofu, na wengi wao ni mafasiki.

 

 

 

 

ثُمَّ قَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِرُسُلِنَا وَقَفَّيْنَا بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ وَجَعَلْنَا فِي قُلُوبِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ رَأْفَةً وَرَحْمَةً وَرَهْبَانِيَّةً ابْتَدَعُوهَا مَا كَتَبْنَاهَا عَلَيْهِمْ إِلَّا ابْتِغَاءَ رِضْوَانِ اللَّـهِ فَمَا رَعَوْهَا حَقَّ رِعَايَتِهَا ۖ فَآتَيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا مِنْهُمْ أَجْرَهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٢٧﴾

27. Kisha Tukafuatisha baada yao Rusuli Wetu, na Tukamfuatisha ‘Iysaa mwana wa Maryam, na Tukampa Injiyl. Na Tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na rehma na uruhubani (maisha ya utawa), wameuzusha wao wenyewe Hatukuwaandikia hayo juu yao isipokuwa kutafuta Radhi za Allaah. Lakini hawakuuchunga ipasavyo kuchungwa. Basi Tukawapa wale walioamini miongoni mwao ujira wao, na wengi wao ni mafasiki.

 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَآمِنُوا بِرَسُولِهِ يُؤْتِكُمْ كِفْلَيْنِ مِن رَّحْمَتِهِ وَيَجْعَل لَّكُمْ نُورًا تَمْشُونَ بِهِ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٨﴾

28. Enyi walioamini! Mcheni Allaah, na muaminini Rasuli Wake. (Allaah) Atakupeni sehemu mbili ya Rehma Zake,[12] na Atakuwekeeni Nuru mtembee nayo, na Atakughufurieni. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

 

لِّئَلَّا يَعْلَمَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَلَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّن فَضْلِ اللَّـهِ ۙ وَأَنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٢٩﴾

29. Ili wajue Watu wa Kitabu kwamba hawana uwezo wa chochote katika Fadhila za Allaah, na kwamba fadhila zimo Mkononi mwa Allaah Humpa Amtakaye, na Allaah Ni Mwenye Fadhila adhimu.

 

 

 

 

 

 

[1] Mbingu Na Ardhi Na Vilivyomo Humo Vinamsabbih Allaah (عزّ وجلّ):

 

Kutokana na taadhima ya Allaah (سبحانه وتعالى) Muumba wa kila kitu, vitu vyote vinamsabbih Yeye Allaah (سبحانه وتعالى).      

 

Rejea Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ﴿٤٤﴾

“Zinamsabihi mbingu saba na ardhi na waliomo humo. Na hakuna kitu chochote isipokuwa kinasabihi na kumhimidi Yeye, lakini hamzifahamu tasbihi zao. Hakika Yeye Ni Mvumilivu, Mwingi wa Kughufuria.” [Al-Israa (17:44)]

 

Na Aayah nyenginezo ambazo zinataja kwamba kila kitu Alichokiumba Allaah (عزّ وجلّ) kinamsabbih ni hizi zifuatazo:

 

Al-A’raaf (7:206), Ar-Ra’d (13:13), Al-Anbiyaa (21:79), An-Nuwr (24:41), Al-Hashr (59:1), Asw-Swaff (61:1), Al-Jumu’ah (62:1), At-Taghaabun (64:1).

 

Na miongoni mwa Hadiyth ni hizi zifuatazo:

 

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ يُونُسَ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيَّبِ، وَأَبِي، سَلَمَةَ أَنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏ "‏ قَرَصَتْ نَمْلَةٌ نَبِيًّا مِنَ الأَنْبِيَاءِ، فَأَمَرَ بِقَرْيَةِ النَّمْلِ فَأُحْرِقَتْ، فَأَوْحَى اللَّهُ إِلَيْهِ أَنْ قَرَصَتْكَ نَمْلَةٌ أَحْرَقْتَ أُمَّةً مِنَ الأُمَمِ تُسَبِّحُ اللَّهِ.‏"‏‏‏

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Sisimizi  alimuuma Nabii miongoni mwa Manabii, ambaye aliamuru kijiji hicho cha sisimizi kuchomwa. Hivyo, Allaah Alimteremshia Wahy: Je, kwa sababu sisimizi mmoja tu amekuuma, nawe ukaunguza Ummah mzima miongoni mwa Ummah unaomsabbih Allaah.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Jihaad (56), Muslim Kitabu Cha Salaam (39)]

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ كُنَّا نَعُدُّ الآيَاتِ بَرَكَةً وَأَنْتُمْ تَعُدُّونَهَا تَخْوِيفًا، كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي سَفَرٍ فَقَلَّ الْمَاءُ فَقَالَ ‏"‏ اطْلُبُوا فَضْلَةً مِنْ مَاءٍ ‏"‏‏.‏ فَجَاءُوا بِإِنَاءٍ فِيهِ مَاءٌ قَلِيلٌ، فَأَدْخَلَ يَدَهُ فِي الإِنَاءِ، ثُمَّ قَالَ ‏"‏ حَىَّ عَلَى الطَّهُورِ الْمُبَارَكِ، وَالْبَرَكَةُ مِنَ اللَّهِ ‏"‏ فَلَقَدْ رَأَيْتُ الْمَاءَ يَنْبُعُ مِنْ بَيْنِ أَصَابِعِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم، وَلَقَدْ كُنَّا نَسْمَعُ تَسْبِيحَ الطَّعَامِ وَهْوَ يُؤْكَلُ‏.

Amesimulia ‘Abdullaah (رضي الله عنه): Tulikuwa tukichukulia miujiza kuwa ni Baraka ya Allaah, lakini nyinyi mnachukulia kuwa ni onyo na tahadhari. Wakati mmoja tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) safarini, nasi tukapungukiwa na maji. Akasema: “Nileteeni maji mliyo nayo.” Watu walileta chombo kilichokuwa na maji kidogo. Alitia mkono wake ndani yake, akasema: “Njooni kwenye maji ya Baraka na Baraka inatoka kwa Allaah.” Niliyaona maji yakitoka kutoka kwenye vidole vya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Na kwa hakika tulikuwa tunasikia chakula kikileta Tasbiyh (Subhaana Allaah) kilipokuwa kinaliwa na yeye. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila Za Nabiy Na Ubora Wa Swahaba]

 

[2] Majina Na Sifa Za Allaah:

 

Suwrah hii tukufu imetaja baadhi ya Majina ya Allaah katika Aayah za mwanzo (1-6).

 

Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Na Sifa Za Allaah kupata maana zake.

 

[3] Istawaa اسْتَوَى

 

Yuko juu kwa namna inayolingana na Uadhama na Ujalali Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-A'raaf (7:54) kwenye maelezo bayana ya maana yake, yenye kutofautiana na maana ya katika Suwrah Al-Baqarah (2:29) na Suwrat Fusswilat (41:11).

 

[4] Fadhila Za Kutoa Mali Kwa Ajili Ya Allaah:

 

Kutoa mali kwa ajili ya Allaah iwe kwa ajili ya Jihaad katika Njia Yake, au swadaqa ya kuwasaidia wahitaji na kusaidia yanayohitajika katika jamii za Kiislamu, ina fadhila adhimu mno. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ametaja na kuamrisha kutoa mali katika Aayah nyingi. Ametaja katika Suwrah hii Al-Hadiyd (57:6), na Akaonya kutokutoa katika Aayah (57:10). Rejea pia Al-Baqarah (2:261) kwenye maudhui hii ya kutoa mali na maonyo yake. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amehimiza kutoa mali kwa ajili ya Allaah katika Hadiyth nyingi. Bonyeza viungo vifuatavyo vyenye faida tele kuhusu fadhila za kutoa mali kwa ajili ya Allaah na rejea zake mbalimbali:

03-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Zakaah: Mlango Wa Swadaqah Za Khiari

060-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukarimu na Kutoa Katika Njia za Kheri na Kuwa na Imani Kwa Allaah Ta'aalaa

265-Aayah Na Mafunzo: Mfano Wa Anayetoa Swadaqah Kwa Ikhlaasw Hulipwa Maradufu

271-Aayah Na Mafunzo: Anayetoa Swadaqah Kwa Kuficha Atakuwa Chini Ya Kivuli Cha Allaah

272-Aayah Na Mafunzo: Kutoa Swadaqah Kutaraji Wajihi Wa Allaah Ni Kupandishwa Daraja

274-Aayah Na Mafunzo: Kutoa Swadaqah Hata Riyali Moja Ni Kheri

092-Aayah Na Mafunzo: Mapendekezo Ya Kutoa Swadaqah Kitu Kilicho Kizuri

245-Aayah Na Mafunzo: Kutoa Kwa Ajili Ya Allaah Ni Kuzidishwa Mali Na Fadhila Tele Nyenginezo

Uzito Wa Thawabu Za Kutoa Mali Yako Kwa Ajili Ya Allaah (سبحانه وتعالى)

008-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Kukimbilia Kutoa Swadaqah Kabla Ya Mauti

 

[5] Waumini Watavuka Asw-Swiraatw Wakiwa Katika Nuru, Ama Wanafiki Watakuwa Kizani

 

Tafsiyr ya Aayah hii na zinazofuatia:

 

Hapa Allaah (سبحانه وتعالى) Anabainisha fadhila za imaan na jini gani Waumiini watakayokuwa furahani kwa imaan zao Siku ya Qiyaamah. Yaani Siku ambayo jua litakapokunjwakunjwa na kupotea mwanga wake, na mwezi utakapopatwa, na pindi watu watakapokuwa katika kiza, na Asw-swiraatw imewekwa juu ya moto wa Jahnnam. Hapo utawaona Waumini wa kiume na Waumini wa kike, nuru yao inatangulia mbele yao na kuliani kwao. Basi watatembea kwa fadhila za imaan na nuru zao katika hali hiyo ngumu mno na ya kutisha, kila mmoja (atavuka Asw-Swiraatw) kulingana na daraja ya imaan yake. Na hapo watabashiriwa bishara Adhimu kwa kuambiwa: 

 

بُشْرَاكُمُ الْيَوْمَ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾

“Bishara njema kwenu leo! Jannaat zipitazo chini yake mito, mdumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa mno.”

 

Basi Wa-Allaahi, bishara njema iliyoje hiyo na furaha iliyoje kwa bishara hiyo ambayo, watapata humo wanachokitaka, na kuokolewa na kila walilokhofia. Ama wanafiki watakapoona nuru za Waumini zinazowaongoza kutembea, ilhali nuru zao zimezimwa, na wamebakia wamechanganyikwa akili katika kiza, watawaambia Waumini: 

 

انظُرُونَا نَقْتَبِسْ مِن نُّورِكُمْ  

“Tungojeeni, tupate mwangaza kutokana na nuru yenu!”  

 

Yaani, nendeni polepole ili tuwadiriki na tupate mwanga wa nuru zenu ili tuweze kutembea na tuokolewe na adhabu. Lakini haiwezekani kamwe kwani

 

قِيلَ ارْجِعُوا وَرَاءَكُمْ فَالْتَمِسُوا نُورًا فَضُرِبَ بَيْنَهُم بِسُورٍ لَّهُ بَابٌ بَاطِنُهُ فِيهِ الرَّحْمَةُ وَظَاهِرُهُ مِن قِبَلِهِ الْعَذَابُ ﴿١٣﴾

 (Wataambiwa): “Rudini nyuma yenu, mtafute huko nuru (yenu)! Kisha utawekwa ukuta baina yao wenye mlango, ndani mna rehma na nje kwa upande wake wa mbele mna adhabu.”

 

[Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Na miongoni mwa Hadiyth kuhusu vukaji wa asw-swiraatw ni hii ifuatayo:

 

حَدَّثَنِي عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، وَإِسْحَاقُ بْنُ مَنْصُورٍ، كِلاَهُمَا عَنْ رَوْحٍ، قَالَ عُبَيْدُ اللَّهِ حَدَّثَنَا رَوْحُ بْنُ عُبَادَةَ الْقَيْسِيُّ، حَدَّثَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي أَبُو الزُّبَيْرِ، أَنَّهُ سَمِعَ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ، يُسْأَلُ عَنِ الْوُرُودِ، فَقَالَ نَجِيءُ نَحْنُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَنْ كَذَا، وَكَذَا، انْظُرْ أَىْ ذَلِكَ فَوْقَ النَّاسِ - قَالَ - فَتُدْعَى الأُمَمُ بِأَوْثَانِهَا وَمَا كَانَتْ تَعْبُدُ الأَوَّلُ فَالأَوَّلُ ثُمَّ يَأْتِينَا رَبُّنَا بَعْدَ ذَلِكَ فَيَقُولُ مَنْ تَنْظُرُونَ فَيَقُولُونَ نَنْظُرُ رَبَّنَا ‏.‏ فَيَقُولُ أَنَا رَبُّكُمْ ‏.‏ فَيَقُولُونَ حَتَّى نَنْظُرَ إِلَيْكَ ‏.‏ فَيَتَجَلَّى لَهُمْ يَضْحَكُ - قَالَ - فَيَنْطَلِقُ بِهِمْ وَيَتَّبِعُونَهُ وَيُعْطَى كُلُّ إِنْسَانٍ مِنْهُمْ - مُنَافِقٍ أَوْ مُؤْمِنٍ - نُورًا ثُمَّ يَتَّبِعُونَهُ وَعَلَى جِسْرِ جَهَنَّمَ كَلاَلِيبُ وَحَسَكٌ تَأْخُذُ مَنْ شَاءَ اللَّهُ ثُمَّ يَطْفَأُ نُورُ الْمُنَافِقِينَ ثُمَّ يَنْجُو الْمُؤْمِنُونَ فَتَنْجُو أَوَّلُ زُمْرَةٍ وُجُوهُهُمْ كَالْقَمَرِ لَيْلَةَ الْبَدْرِ سَبْعُونَ أَلْفًا لاَ يُحَاسَبُونَ ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ كَأَضْوَإِ نَجْمٍ فِي السَّمَاءِ ثُمَّ كَذَلِكَ ثُمَّ تَحِلُّ الشَّفَاعَةُ وَيَشْفَعُونَ حَتَّى يَخْرُجَ مِنَ النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَكَانَ فِي قَلْبِهِ مِنَ الْخَيْرِ مَا يَزِنُ شَعِيرَةً فَيُجْعَلُونَ بِفِنَاءِ الْجَنَّةِ وَيَجْعَلُ أَهْلُ الْجَنَّةِ يَرُشُّونَ عَلَيْهِمُ الْمَاءَ حَتَّى يَنْبُتُوا نَبَاتَ الشَّىْءِ فِي السَّيْلِ وَيَذْهَبُ حُرَاقُهُ ثُمَّ يَسْأَلُ حَتَّى تُجْعَلَ لَهُ الدُّنْيَا وَعَشَرَةُ أَمْثَالِهَا مَعَهَا ‏.‏

 

Amesimulia Jubayr (رضي الله عنه)  kwamba amemsikia Jaabir Bin ‘Abdillaah  (رضي الله عنهما) ambaye aliulizwa kuhusu (hali za) watu watakapofika  (Siku ya Qiyaamah) akasema: Tutafika Siku ya Qiyaamah kama hivi, kama hivi, na tazama! Yaani tutakuwa sisi (pamoja na Rasuli) mahala paliponyanyuka juu zaidi kuliko watu wote. (Kisha msimuliaji) akasema: Kisha watu wataitwa na masanamu yao waliyokuwa wakiyaabudu, mmoja baada ya mwengine. Kisha Rabb wetu Atakuja Atasema: “Mnamngojea nani?” Watasema: Tunamngojea Rabb wetu. Allaah Atasema: “Mimi Rabb wenu!” Watasema: (Hatuna uhakika) hadi tukuone. Kisha Allaah Atajidhihirisha huku Akicheka. Kisha Ataondoka nao watamfuata, na kila mtu akiwa mnafiki au Muumini, atapewa nuru. Kisha watamfuata (Allaah) katika daraja la Jahannam, na juu ya daraja kutakuweko miiba na kulabu ambazo zitawanyakua wale Atakao Allaah. Kisha nuru ya wanafiki itazimwa. Kundi la kwanza la Waumini watakaookolewa, ni watu sabiini elfu ambao nyuso zao zitakuwa na nuru kama ya mwezi mpevu, na hawataitwa kuhesabiwa. Kisha watafuatia ambao nyuso zao zitakuwa kama nyota angavu mbinguni. Hivyo ndivyo (makundi yatakavyofuatana kundi moja baada ya jengine). Kisha itafika hatua ya Ash-shafaa’ah (uombezi), na watakaopewa idhini ya kuombeza wataombeza mpaka atolewe kila aliyekiri

 

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ

Laa ilaaha illa-Allaah (Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah)

 

huku akiwa moyoni mwake kuna kheri (imaan) kiasi cha uzani wa punje. Kisha watahudhurishwa katika uwanja wa Jannah, na watu wa Jannah watawanyunyizia maji hadi wachipuke kama mchipuko wa kitu katika maji ya mafuriko, na kuungua kwao kutatoweka. Watamuomba Rabb wao mpaka wapewe (neema) za dunia na mara kumi zaidi ya hayo. [Muslim]

 

[6] Aayah Imewateremkia Swahaba Baada Ya Miaka Minne Tokea Kusilimu Kwao:

 

 

حَدَّثَنِي يُونُسُ بْنُ عَبْدِ الأَعْلَى الصَّدَفِيُّ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ وَهْبٍ، أَخْبَرَنِي عَمْرُو، بْنُ الْحَارِثِ عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي هِلاَلٍ، عَنْ عَوْنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّ ابْنَ مَسْعُودٍ، قَالَ مَا كَانَ بَيْنَ إِسْلاَمِنَا وَبَيْنَ أَنْ عَاتَبَنَا اللَّهُ بِهَذِهِ الآيَةِ ‏{أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ}‏ إِلاَّ أَرْبَعُ سِنِينَ ‏.‏

 

Amesimulia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه):  Kuanzia  kusilimu kwetu na kuteremka Aayah hii ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Ametuonya ndani yake:

 

أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ  

“Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah.”

 

Ilikuwa ni miaka minne. 

 

[Muslim]

 

[7] Fadhila Za Kutoa Mali Kwa Ajili Ya Allaah:

 

Rejea Aayah namba (11) ya Suwrah hii Al-Hadiyd.

 

[8] Tofauti Ya Manabii, Swiddiqiyn, Shuhadaa Na Swalihina.

 

Rejea Al-Baqarah (2:130) (An-Nisaa (5:69).

 

[9] Dunia Ni Starehe Fupi Tu, Kuipa Mgongo Dunia, Na Maonyo Ya Kupendelea Dunia Badala Ya Aakhirah:

 

Aayah hii ni sawa na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ۗ

“Na wapigie mfano wa uhai wa dunia. Ni kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, ikachanganyika nayo mimea ya ardhi (ikasitawi), kisha ikawa mikavu iliyovurugika, inapeperushwa na upepo. [Al-Kahf (18:45)]

 

Na Aayah kadhaa nyenginezo zimebainisha kuhusu uhai wa dunia kuwa ni mfupi na wenye kutoweka, na kwamba starehe za dunia si za kudumu, na kuna maamrisho ya kuipa mgongo dunia, na kuna maonyo ya kupendelea dunia badala ya Aakhirah au maonyo ya kupendelea uhai wa dunia badala ya uhai wa Aakhirah. Miongoni mwazo ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿١٦﴾ وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿١٧﴾

 

“Bali mnahiari zaidi uhai wa dunia. Na hali Aakhirah ni bora zaidi na ya kudumu zaidi.” [Al-A’laa (97:16-17)]

 

Rejea pia Aal-‘Imraan (3:14), (3:185), Al-An’aam (6:32), At-Tawbah (9:38), Yuwnus (10:24), Ar-Ra’d (13:26), Al-Qaswasw (28:60), Al-‘Ankabuwt (29:64), Luqmaan (31:33), Ash-Shuwraa (42:36), Muhammad (47:36).

 

Rejea pia Ash-Shuwraa (4:20) kwenye faida nyenginezo.

 

Na miongoni mwa Hadiyth ni hizi zifuatazo:

 

عن أنس رضي الله عنه : أن النبي صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( اللَّهُمَّ لاَ عَيْشَ إِلاَّ عَيْشَ الآخِرَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ee Allaah! Hakuna maisha isipokuwa maisha ya Aakhirah [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لَوْ كَانَتْ الدُّنْيَا تَعْدِلُ عِنْدَ اللَّهِ جَنَاحَ بَعُوضَةٍ مَا سَقَى كَافِرًا مِنْهَا شَرْبَةَ مَاءٍ)) رواه الترمذي وقال: حديث حسن صحيح

 

Amesimulia Sahl bin Sa'ad (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ingelikuwa (thamani ya) dunia ni sawasawa na bawa la mbu mbele ya Allaah, Asingelimnywesha kafiri hata tama moja la maji.” [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida tele na rejea mbalimbali:

 

01-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Kauli Zake Kuhusu Zuhd (Kuipa Mgongo Dunia)

055-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila na Ubora wa Kuupa Nyongo Ulimwengu wa Kukinai Kwa Kichache na Ubora wa Ufakiri

 

057-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Dunia Ni Jela Kwa Muumin, Kafiri Kwake Ni Kama Jannah

 

058-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Ishi Duniani Kama Mgeni Au Mpita Njia

 

059-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Kuipa Mgongo Dunia Kutampatia Mtu Mapenzi Ya Allaah Pamoja Na Ya Watu

 

 

060-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Ingelikuwa Dunia Sawa Na Bawa La Mbu, Allaah Asingelimnywesha kafiri maji.

 

061-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Dunia Ni Kama Kivuli Anachokitumia Msafiri Kwa Muda Tu

 

 

[10] Kuomba Maghfirah Na Tawbah:

 

Bonyeza viungo vifuatavyo kwenye faida tele:

01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuomba Maghfirah

Tawbah: Hukmu Na Fadhila Zake

 

[11] Subira Katika Mitihani, Maafa Na Misiba:

 

Mitihani, maafa na misiba ya kila aina anayojaaliwa mtu, anapaswa awe na subra ambayo ina fadhila zake tele. Rejea Al-Baqarah (2:155)

 

Na bonyeza viungo vifuatavyo vyenye Hadiyth na makala kuhusu subira na fadhila zake:

003-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Subira

Swabrun Jamiyl (Subira Njema)

 

[12] Kulipwa Thawabu Mara Mbili  

 

حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، حَدَّثَنَا صَالِحُ بْنُ حَىٍّ أَبُو حَسَنٍ، قَالَ سَمِعْتُ الشَّعْبِيَّ، يَقُولُ حَدَّثَنِي أَبُو بُرْدَةَ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَاهُ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ ثَلاَثَةٌ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُمْ مَرَّتَيْنِ الرَّجُلُ تَكُونُ لَهُ الأَمَةُ فَيُعَلِّمُهَا فَيُحْسِنُ تَعْلِيمَهَا، وَيُؤَدِّبُهَا فَيُحْسِنُ أَدَبَهَا، ثُمَّ يُعْتِقُهَا فَيَتَزَوَّجُهَا، فَلَهُ أَجْرَانِ، وَمُؤْمِنُ أَهْلِ الْكِتَابِ الَّذِي كَانَ مُؤْمِنًا، ثُمَّ آمَنَ بِالنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَلَهُ أَجْرَانِ، وَالْعَبْدُ الَّذِي يُؤَدِّي حَقَّ اللَّهِ وَيَنْصَحُ لِسَيِّدِهِ ‏"‏‏.‏ ثُمَّ قَالَ الشَّعْبِيُّ وَأَعْطَيْتُكَهَا بِغَيْرِ شَىْءٍ وَقَدْ كَانَ الرَّجُلُ يَرْحَلُ فِي أَهْوَنَ مِنْهَا إِلَى الْمَدِينَةِ‏.‏

 

Amesimulia babake Abuu Burdah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watu watatu watapewa ujira wao mara mbili: Mtu aliye na kijakazi, naye akamsomesha inavyotakiwa na akamfundisha adabu njema, kisha akamuacha huru na kumuoa. Mtu huyo atapata ujira mara mbili. Na Muumini miongoni mwa Ahlul-Kitaab, ambaye alikuwa Muumini, kisha akamuamini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), naye atakuwa na ujira mara mbili. Na mtumwa anayetekeleza haki za Allaah na akawa na ikhlaasw kwa bwanake.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Jihaad]

 

 

 

Share