077 - Al-Mursalaat

 

   الْمُرْسَلاَت

 

077-Al-Mursalaat

 

077-Al-Mursalaat: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا﴿١﴾

1. Naapa kwa pepo zitumwazo kwa mfuatano.

 

 

 

فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفًا﴿٢﴾

2. Kisha Naapa kwa pepo zinazovuma kwa dhoruba.

 

 

 

وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرًا﴿٣﴾

3. Na Naapa kwa pepo zinazotawanya mawingu na mvua.

 

 

 

فَالْفَارِقَاتِ فَرْقًا﴿٤﴾

4. Kisha Naapa kwa (Malaika) wanaopambanua pambanuo la haki na batili.

 

 

 

فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرًا﴿٥﴾

5. Kisha Naapa kwa (Malaika) wanaopeleka Wahy kwa Rasuli.

 

 

عُذْرًا أَوْ نُذْرًا﴿٦﴾

6. Kwa ajili ya kuondosha udhuru au kwa ajili ya kuonya.

 

 

 

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِعٌ﴿٧﴾

7. Hakika yale mnayoahidiwa bila shaka yatatokea tu!

 

 

 

فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ﴿٨﴾

8. Basi pale nyota zitakapofutiliwa mbali mwanga wake.

 

 

 

وَإِذَا السَّمَاءُ فُرِجَتْ﴿٩﴾

9. Na pale mbingu zitakapofunguliwa.

 

 

 

وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ﴿١٠﴾

10. Na pale majabali yatakapopeperushiliwa mbali  

 

 

 

وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ﴿١١﴾

11. Na pale Rusuli watakapopangiwa wakati wao maalumu.

 

 

 

 

لِأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ﴿١٢﴾

12. Kwa Siku gani hiyo iliyoahirishwa?

 

 

 

لِيَوْمِ الْفَصْلِ﴿١٣﴾

13. Kwa ajili ya Siku ya hukumu na kutenganisha. 

 

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ﴿١٤﴾

14. Na nini kitakachokujulisha ni ipi Siku ya hukumu na kutenganisha?

 

 

 

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿١٥﴾

15. Ole[1] Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.

 

 

 

أَلَمْ نُهْلِكِ الْأَوَّلِينَ﴿١٦﴾

16. Je, kwani Hatukuangamiza watu wa awali?

 

 

 

ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الْآخِرِينَ﴿١٧﴾

17. Kisha Tukawafuatilishia wengineo?

 

 

 

كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ﴿١٨﴾

18. Hivyo ndivyo Tunavyowafanya wahalifu.

 

 

 

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿١٩﴾

19. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.

 

 

 

أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ﴿٢٠﴾

20. Je, kwani Hatukukuumbeni kutokana na maji dhalilifu (manii)?

 

 

 

 

فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ﴿٢١﴾

21. Kisha Tukayaweka katika mahali pa kutulia, thabiti?

 

 

 

إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ﴿٢٢﴾

22. Mpaka muda maalumu uliokadiriwa.

 

 

 

فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ﴿٢٣﴾

23. Tukakadiria. Basi ni wazuri walioje (Sisi) Wenye Kukadiria!

 

 

 

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٢٤﴾

24. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.

 

 

 

أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا﴿٢٥﴾

25. Je, kwani Hatukufanya ardhi kuwa ni chombo cha kukusanya?

 

 

 

 

أَحْيَاءً وَأَمْوَاتًا﴿٢٦﴾

26. Walio hai na wafu?

 

 

 

وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُم مَّاءً فُرَاتًا﴿٢٧﴾

27. Na Tukaweka humo milima thabiti mirefu iliyojikita na Tukakunywesheni maji matamu mno?

 

 

 

 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٢٨﴾

28. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.

 

 

 

 

انطَلِقُوا إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ﴿٢٩﴾

29. (Wataambiwa): Nendeni kwenye yale mliyokuwa mkiyakadhibisha.

 

 

 

 

انطَلِقُوا إِلَىٰ ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ﴿٣٠﴾

30.  Nendeni kwenye kivuli (cha Jahannam) chenye sehemu tatu.

 

 

 

لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّـهَبِ﴿٣١﴾

31.  Hakiwafuniki, na wala hakiwakingi na mwako wa moto.

 

 

 

إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ﴿٣٢﴾

32. Hakika huo (moto) hurusha macheche mfano wa makasri.

 

 

 

كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ﴿٣٣﴾

33. Kama kwamba ni ngamia wakubwa wa manjano.

 

 

 

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٣٤﴾

34. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.

 

 

 

هَـٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ﴿٣٥﴾

35. Siku hii hawatotamka.

 

 

 

وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ﴿٣٦﴾

36. Na wala hawatopewa idhini ili watoe nyudhuru.[2]

 

 

 

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٣٧﴾

37. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.

 

 

 

هَـٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ﴿٣٨﴾

38. Hii ni Siku ya hukumu na kutenganisha. Tumekukusanyeni pamoja na watu wa awali.

 

 

 

 

فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ﴿٣٩﴾

39. Ikiwa mnayo hila yoyote ile basi Nifanyieni (hizo) hila.

 

 

 

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٠﴾

40. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.

 

 

 

 

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ﴿٤١﴾

41. Hakika wenye taqwa watakuwa katika vivuli na chemchemu.

 

 

 

وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ﴿٤٢﴾

42. Na matunda katika yale wanayoyatamani.

 

 

 

كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٤٣﴾

43. (Wataambiwa): Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.

 

 

 

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿٤٤﴾

44. Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.

 

 

 

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٥﴾

45. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.

 

 

 

كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ﴿٤٦﴾

46. (Enyi makafiri): Kuleni na stareheni kidogo (duniani), hakika nyinyi ni wahalifu.

 

 

 

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٧﴾

47. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.

 

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ﴿٤٨﴾

48. Na wanapoambiwa rukuuni (mswali), hawarukuu.

 

 

 

 

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٩﴾

49. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.

 

 

 

فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ﴿٥٠﴾

50. Basi kauli gani baada ya hii (Qur-aan) wataiamini?

 

 

 

 

 

 

 

 

 

[1] Maana Ya ويل (Wayl)

Kauli ifuatayo ya Allaah (سبحانه وتعالى), yenye neno la ويل, imekariri mara kumi katika Suwrah hii.

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿١٥﴾

“Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.”

 

Na Kauli kama hii imetajwa pia katika Suwrah zifuatazo:  Atw-Twuur (52:11), Al-Mutwaffifiyn (83:10).

 

Na maana kadhaa za ويل zimetajwa na ‘Ulamaa kama ifuatavyo:

 

i- Bonde katika moto wa Jahannam.

 

ii- Neno linaloashiria tisho kali.

 

iii- Adhabu na maangamizi.

 

iv- Bonde linalotiririka kutoka usaha wa watu wa motoni.

 

v- Neno la kutokuridhia na lawama.

    

vi- Neno linalosemwa katika kupatwa masaibu kama vile walivyosema watu wa shamba baada ya kutambua kuwa Allaah (سبحانه وتعالى)  Ameliangamiza shamba lao kwa dhambi na udhalimu wao.

قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ﴿٣١﴾

“Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tumekuwa warukao mipaka.” [Al-Qalam (68:31).

 

vii- Neno linatumika katika kustaajabia jambo linaloonekana mustahili, kama alivyostaajabu Sara mke wa Nabiy Ibraahiym walipobashiriwa kumzaa Is-haaq wakiwa katika umri wa uzee:

قَالَتْ يَا وَيْلَتَىٰ أَأَلِدُ وَأَنَا عَجُوزٌ وَهَـٰذَا بَعْلِي شَيْخًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عَجِيبٌ﴿٧٢﴾

“Akasema: Yatakuwaje haya jamani! Je, nitazaa na hali mimi ni mkongwe na huyu mume wangu ni kizee? Hakika hili ni jambo la ajabu!” [Huwd (11:72)]

 

viii- Neno linatumika katika kushtuka, kustajaabu, kukhofu, katika jambo la aibu, mateso na katika hali ya kujuta jambo kama alivyojuta Qaabiyl mwana wa Aadam aliyemuua nduguye: 

 

فَبَعَثَ اللَّـهُ غُرَابًا يَبْحَثُ فِي الْأَرْضِ لِيُرِيَهُ كَيْفَ يُوَارِي سَوْءَةَ أَخِيهِ ۚ قَالَ يَا وَيْلَتَىٰ أَعَجَزْتُ أَنْ أَكُونَ مِثْلَ هَـٰذَا الْغُرَابِ فَأُوَارِيَ سَوْءَةَ أَخِي ۖ فَأَصْبَحَ مِنَ النَّادِمِينَ ﴿٣١﴾

“Kisha Allaah Akamleta kunguru akifukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi asitiri maiti ya ndugu yake. (Muuaji) akasema: Ole wangu! Hivi nimeshindwa kuwa mimi kama huyu kunguru nikamsitiri ndugu yangu? Akawa miongoni mwa wajutao.” [Al-Maaidah (5:31)]

 

  

[2] Watu Wa Motoni Hawatakubaliwa Nyudhuri Zao:

 

Rejea Al-Qiyaamah (75:15) kwenye faida.

 

 

 

Share