078 - An-Nabaa

 

  النَّبَاء

 

078-An-Nabaa 

 

078-An-Nabaa: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ ﴿١﴾

1. Kuhusu nini wanaulizana?

 

 

 

عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ ﴿٢﴾

2. Kuhusu khabari kubwa mno ya muhimu.[1]

 

 

 

الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ ﴿٣﴾

3. Ambayo wao wanakhitilafiana kwayo.

 

 

كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٤﴾

4. Laa hasha! Hivi karibuni watajua.

 

 

ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٥﴾

5. Kisha laa hasha! Hivi karibuni watajua.

 

 

 

أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا ﴿٦﴾

6. Je, kwani Hatukufanya ardhi kuwa tandiko?[2]

 

 

 

وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا ﴿٧﴾

7. Na milima kuwa kama vigingi?

 

 

 

وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا ﴿٨﴾

8. Na Tukakuumbeni kwa jozi; wanaume na wanawake!

 

 

 

وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا ﴿٩﴾

9. Na Tukafanya usingizi wenu mnono, kuwa mapumziko (kama kufa)!

 

 

 

وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا ﴿١٠﴾

10. Na Tukafanya usiku kuwa kama libasi la kufunika!

 

 

وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا ﴿١١﴾

11. Na Tukafanya mchana kuwa ni wa kutafutia maisha!

 

 

وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا ﴿١٢﴾

12. Na Tukajenga juu yenu (mbingu) saba imara!

 

 

وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا ﴿١٣﴾

13. Na Tukafanya siraji yenye mwanga mkali iwakayo kwa nguvu!

 

 

 

وَأَنزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا ﴿١٤﴾

14. Na Tukateremsha kutoka mawingu yaliyokurubia kunyesha, maji yenye kutiririka kwa kasi kubwa!

 

 

لِّنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا ﴿١٥﴾

15. Ili Tutoe kwayo nafaka na mimea. 

 

 

وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا ﴿١٦﴾

16. Na mabustani yanayosongomana na kuota teletele.

 

 

إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا ﴿١٧﴾

17. Hakika siku ya hukumu na kutenganisha ina wakati maalumu.

 

 

 

 

يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا ﴿١٨﴾

18. Siku litakapopulizwa baragumu, mtakuja makundi makundi.[3]

 

 

 

وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا ﴿١٩﴾

19. Na mbingu zitafunguliwa, zitakuwa milango ya njia.[4]

 

 

 

وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا ﴿٢٠﴾

20. Na milima itaendeshwa na itakuwa kama sarabi.

 

 

إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا ﴿٢١﴾

21. Hakika Jahannam itakuwa yenye kuvizia.[5]

 

 

لِّلطَّاغِينَ مَآبًا ﴿٢٢﴾

22. Kwa walioruka mipaka wakaasi, ndio mahali pao pa kurejea.

 

 

 

لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا ﴿٢٣﴾

23. Watabakia humo dahari nyingi.

 

 

 

لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا ﴿٢٤﴾

24. Hawatoonja humo cha baridi wala kinywaji.

 

 

 

إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا ﴿٢٥﴾

25. Isipokuwa maji yachemkayo mno na usaha.

 

 

 

جَزَاءً وِفَاقًا ﴿٢٦﴾

26. Jazaa inayowafikiana kabisa.

 

 

 

إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا ﴿٢٧﴾

27. Hakika wao walikuwa hawataraji kuhesabiwa.

 

 

وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا ﴿٢٨﴾

28. Na walikadhibisha Aayaat na Ishara Zetu kwa njia zote!

 

 

 

وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا ﴿٢٩﴾

29. Na kila kitu Tumekitia hesabuni barabara kwa kuandika.

 

 

 

فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا ﴿٣٠﴾

30. Basi onjeni, kwani Hatutokuzidishieni isipokuwa adhabu.

 

 

 

إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا ﴿٣١﴾

31. Hakika wenye taqwa watapata mafanikio.[6]

 

 

حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا ﴿٣٢﴾

32. Mabustani na mizabibu.

 

 

وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا ﴿٣٣﴾

33. Na wanawake wenye matiti ya kisichana, wa hirimu moja na waume zao.

 

 

وَكَأْسًا دِهَاقًا ﴿٣٤﴾

34. Na kombe lililojaa pomoni mvinyo.

 

 

لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا ﴿٣٥﴾

35. Hawatosikia humo upuuzi wala kukadhibisha ukadhibisho.

 

 

 

جَزَاءً مِّن رَّبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا ﴿٣٦﴾

36. Jazaa kutoka kwa Rabb wako, tunukio la kutosheleza.

 

 

 

رَّبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرَّحْمَـٰنِۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا ﴿٣٧﴾

37. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, Ar-Rahmaan. Hawatoweza kumsemesha.

 

 

 

يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا ﴿٣٨﴾

38. Siku atakayosimama Ruwh (Jibriyl) na Malaika safusafu. Hawatozungumza isipokuwa yule ambaye Ar-Rahmaan Amempa idhini na atasema yaliyo sahihi.

 

 

ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ مَآبًا ﴿٣٩﴾

39. Hiyo ni Siku ya haki. Basi atakaye, na ashike marudio kuelekea kwa Rabb wake.

 

 

 

إِنَّا أَنذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَا لَيْتَنِي كُنتُ تُرَابًا ﴿٤٠﴾

40. Hakika Sisi Tumekuonyeni adhabu ya karibu. Siku mtu atakapotazama yale iliyokadimisha mikono yake, na kafiri atasema: Laiti ningelikuwa mchanga.

 

 

 

 

[1] Khabari Kubwa Mno Ya Muhimu:

 

Khabari kubwa mno ya muhimu, ya kutisha na ya kustaajabisha. Qataadah na Ibn Zayd wamesema: “Ni kufufuliwa baada ya kufa.” Mujaahid amesema: “Ni Qur-aan.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

[2] Miongoni Mwa Neema Za Allaah Kwa Walimwengu:

 

Kuanzia Aayah hii namba (6) hadi Aayah namba (16) Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja baadhi ya Neema Zake kwa walimwengu. Rejea Ibraahiym (14:34) kwenye uchambuzi wa Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) pamoja na rejea mbali mbali. Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) ambazo hawezi mtu kuzihesabu.

 

[3] Kupulizwa Baragumu Kwa Ajili Ya Qiyaamah:

 

Rejea Az-Zumar (39:68) kwenye faida zake:

 

[4] Mbingu Kufunguliwa:

 

Mbingu zitafunguliwa Siku ya Qiyaamah kwa ajili ya Malaika kuteremka. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Rejea Al-Furqaan (25:25), Al-Haaqqah (69:13-18), Al-Fajr (89:21-22), Al-Baqarah (2:210), Al-An’aam (6:158).

 

Na mbingu zitapasuliwa na kuchanikachanika zitakuwa kama milango. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Rejea Al-Infitwaar (82:1), Al-Inshiqaaq (84:1).

 

[5] Mateso Na Adhabu za Watu Wa Motoni:

 

Kuanzia Aayah hii ya An-Nabaa (78:21) hadi namba (30), yanatajwa mateso na adhabu za watu wa motoni.

 

Adhabu za makafiri zinakuwa katika hali zifuatazo: 

 

(i) Wanapotolewa Roho:

 

Hali ya kafiri inapotolewa roho yake ikapelekwa juu imeelezewa katika Hadiyth ifuatayo ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  

 

فَإِذَا كَانَ الرَّجُلُ السُّوءُ قَالَ: اخْرُجِي أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْخَبِيثَةُ كَانَتْ فِي الْجَسَدِ الْخَبِيثِ اخْرُجِي ذَمِيمَةً وَأَبْشِرِي بِحَمِيمٍ وَغَسَّاقٍ وَآخَرَ مِنْ شَكْلِهِ أَزْوَاجٌ فَمَا تَزَالُ يُقَالُ لَهَا ذَلِكَ حَتَّى تَخْرُجَ ثُمَّ يُعْرَجُ بِهَا إِلَى السَّمَاءِ فَيُفْتَحُ لَهَا فَيُقَالُ: مَنْ هَذَا؟ فَيُقَالُ: فُلَانٌ فَيُقَالُ: لَا مَرْحَبًا بِالنَّفْسِ الْخَبِيثَةِ كَانَتْ فِي الْجَسَدِ الْخَبِيثِ ارْجِعِي ذَمِيمَةً فَإِنَّهَا لَا تفتح لَهُ أَبْوَابُ السَّمَاءِ فَتُرْسَلُ مِنَ السَّمَاءِ ثُمَّ تَصِيرُ إِلَى الْقَبْر ". رَوَاهُ ابْن مَاجَه

 

Lakini inapokuwa mtu ni mbaya kinachosemwa ni:  Toka ewe nafsi mbaya ambayo ilikuwa katika mwili mwovu! Toka ukiwa mwenye kulaumiwa na pokea habari mbaya ya maji yanayotokoka na usaha na mengineyo ya mfano wake na aina yake!  Ataendelea kuambiwa hivyo hadi roho itoke. Kisha itapandishwa juu mbinguni na itafunguliwa mlango. Itaulizwa: Ni nani huyu? Itajibiwa: Ni fulani. Itaambiwa: Hakuna ukaribisho kwa nafsi mbaya iliyokuwa ndani ya mwili mwovu! Rudi ukiwa mwenye kulaumiwa kwani milango ya mbinguni haitafunguliwa kwa ajili yake. Kisha itatupwa kutoka mbinguni hadi kufika kaburini.” [Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (3456)]

 

Rejea pia Al-A’raaf (7:40) kwenye maelezo kuhusu mbingu kutokufunguliwa kwa ajili ya roho ya kafiri.

 

Rejea pia Al-Baqarah (2:165), Al-An’aam (6:30), (6:93), Al-Anfaal (8:50-51), Qaaf (50:19-22), Al-Waaqi’ah (56:92-94) kwenye Aayah zinazotaja hali ya kafiri anapotolewa roho. 

 

Na pia rejea Qaaf (50:19) kwenye faida kadhaa.

 

(ii) Wataingizwa Motoni Na Kufungwa Minyororo Shingoni Mwao:

 

Rejea Ar-Ra’d (13:5), Ibraahiym (14:49-50), Sabaa (34:33), Ghaafir (40:70-72), Al-Haaqqah (69:30-32), Al-Muzzammil (73:11-12), Al-Insaan (74:4)

 

(iii) Watakuwa Kuni Za Moto Uzidi Kuwaunguza:

 

Rejea Al-Baqarah (2:24), Aal-‘Imraan (3:10), Al-Anbiyaa (21:98).

 

(iv) Mateso Na Adhabu Nyenginezo Pamoja Na Vyakula Vyao Na Vinywaji Vyao.

 

Kwanza rejea a Faatwir (33:36) kwenye faida kadhaa na rejea mbalimbali.

 

Kisha rejea Suwrah zifuatazo ambazo zimetaja kwa ujumla maudhui hii ya mateso na adhabu za watu wa motoni pamoja na vyakula vyao na vinywaji vyao.

 

An-Nisaa (4:56), Ibraahiym (14:15-17), (14:15-17), Asw-Swaaffaat (37:62-67), Swaad (38:55-64), Ad-Dukhaan (44:40-50), Al-Hajj (22:9-10), (22:19-22), Al-Kahf (18:29),  Ash-Shu’araa (26:91-102), Al-Baqarah (2:174-175), Al-Maaidah (5:35-37), Huwd (11:105-106), Ar-Rahmaan (55:43-44), Al-Qamar (54:46-48), Al-Waaqi’ah (56:41-56), Al-Mulk (67:6-11), Al-Haaqqah (69:25-37), Al-Ma’aarij (70:15-18), Al-Muddath-thir (74:26-30), Al-Muzzammil (73:11-12), Al-A’laa (87:11-13), Al-Ghaashiyah (88:1-7), Al-Humazah (104:4-9).

 

Na katika Suwrah Muhammad mwishoni mwa Aayah Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

كَمَنْ هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ﴿١٥﴾

“Ni kama yule mwenye kudumu motoni? Na watanyweshwa maji yachemkayo yakatekate machango yao?” [Muhammad (47:15)]

 

Na katika Hadiyth kadhaa za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pia adhabu za watu wa motoni, hali zao, vyakula vyao zimethibiti ambazo miongoni mwazo ni hizi zifuatazo:

 

عن سمرة بن جندب رضي الله عنه: أنَّ نبيَّ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مِنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ النَّارُ إِلَى كَعْبَيهِ ، وَمنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى رُكْبَتَيهِ ، وَمنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى حُجزَتِهِ ، وَمِنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى تَرْقُوَتِهِ )) رواه مسلم .

Amesimulia Samurah Bin Jundub (رضي الله عنه):  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Miongoni mwa watu wa motoni ni wale ambao moto kwa ukali wake utawafika kwenye vifundo vya miguu, na wengine kwenye magoti, na wengine mpaka kiunoni, na wengine hadi kwenye fupa la koo.” [Muslim]

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ إِنَّ غِلَظَ جِلْدِ الْكَافِرِ اثْنَانِ وَأَرْبَعُونَ ذِرَاعًا وَإِنَّ ضِرْسَهُ مِثْلُ أُحُدٍ وَإِنَّ مَجْلِسَهُ مِنْ جَهَنَّمَ كَمَا بَيْنَ مَكَّةَ وَالْمَدِينَةِ ‏"‏ ‏.‏ هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ مِنْ حَدِيثِ الأَعْمَشِ ‏.‏

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه):  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Unene wa ngozi ya kafiri ni dhiraa arobaini na mbili, na jino lake ni kama (mlima wa) Uhud, na makazi yake motoni ni kama baina ya Makkah na Madiynah. [At-Tirmidhiy]

 

 (v) Majina Ya Moto Na Aina Zake:

 

Rejea Al-Muddath-thir (74:26).

 

Bonyeza pia kiungo kifuatacho kwa faida ziyada:

An-Naar (Moto Wa Jahannam)

 

[6] Wenye Taqwa Na Neema Zao Za Jannah:

 

Rejea Faatwir (35:33) kwenye maelezo na rejea mbalimbali za maudhui.

Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo:

02-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kubainisha Yale Waliyoandaliwa Waumini na Allaah Peponi

Neema Za Jannah (Pepo) Tuliyoahidiwa

Al-Jannah (Pepo)

 

Share