التِّين
095-At-Tiyn
095-At-Tiyn: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa tini na zaytuni.
وَطُورِ سِينِينَ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa Mlima wa Sinai.
وَهَـٰذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa mji huu wa amani (Makkah).
لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ﴿٤﴾
4. Kwa yakini Tumemuumba binaadamu katika umbile bora kabisa.
ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ ﴿٥﴾
5. Kisha Tukamrudisha chini kabisa ya walio chini.
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٦﴾
6. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema; hao watapata ujira usiokatika.
فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِالدِّينِ ﴿٧﴾
7. Basi lipi baada ya yote hayo linakufanya ukadhibishe (Siku ya) malipo?!
أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ ﴿٨﴾
8. Je, kwani Allaah Si Mwadilifu zaidi kuliko mahakimu wote?