096 - Al-'Alaq

 

  الْعَلَق

 

096-Al-‘Alaq

 

096-Al-‘Alaq: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾

1. Soma kwa Jina la Rabb wako Aliyeumba.

 

 

خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾

2. Amemuumba binaadamu kutokana na pande la damu linaloning’inia.

 

 

اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾

3. Soma. Kwani Rabb wako Ni Mkarimu kushinda wote.

 

 

الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾

4. Ambaye Amefunza kwa kalamu.

 

 

عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾

5. Amemfunza binaadamu asiyoyajua.

 

 

كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾

6. Laa hasha! Hakika binaadamu bila shaka hupindukia mipaka kuasi.

 

 

أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾

7. Anapojiona kuwa amejitosheleza. 

 

 

إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ﴿٨﴾

8. Hakika kwa Rabb wako ndio marejeo.

 

 

أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾

9. Je, umemuona yule anayemkataza?

 

 

عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾

10. Mja pale anaposwali?

 

 

أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ﴿١١﴾

11. Je umeona, ikiwa (huyu mwovu) atafuata uongofu.

 

 

أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ﴿١٢﴾

12. Au akalingania taqwa (si ingelikuwa bora zaidi kwake?)

 

 

أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٣﴾

13. Je umeona, kama ataendelea kukadhibisha na kukengeuka (si ataishilia pabaya?

 

 

أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ ﴿١٤﴾

14. Je, hajui kwamba hakika Allaah Anaona?

 

 

كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ ﴿١٥﴾

15. Laa hasha! Asipoacha, bila shaka Tutamburuta kwa shungi la nywele.

 

 

نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ﴿١٦﴾

16. Shungi la uwongo, lenye hatia.

 

 

فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾

17. Basi na aite timu yake.

 

 

سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾

18. Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyah (Malaika wa adhabu).

 

 

كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩﴿١٩﴾

19. Laa hasha! Usimtii. Na sujudu na kurubia (kwa Allaah). 

 

 

Share