099 - Al-Zalzalah

 

الزَّلْزَلَة

 

099-Al-Zalzalah

 

099-Az-Zalzalah: Utangulizi Wa Suwrah

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا ﴿١﴾

1. Itakapotetemeshwa ardhi zilzala yake (ya mwisho).[1]

 

 

وَأَخْرَجَتِ الْأَرْضُ أَثْقَالَهَا ﴿٢﴾

2. Na itakapotoa ardhi mizigo yake.

 

 

وَقَالَ الْإِنسَانُ مَا لَهَا ﴿٣﴾

3. Na binaadamu akasema: Ina nini?

 

 

يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا ﴿٤﴾

4. Siku hiyo itahadithia khabari zake.

 

 

بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَىٰ لَهَا ﴿٥﴾

5. Kwa kuwa Rabb wako Ameiamuru.

 

 

 

يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ ﴿٦﴾

6. Siku hiyo watatoka watu makundi mbalimbali wamefarakiana ili waonyeshwe ‘amali zao.

 

 

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾

7. Basi yule atakayetenda kheri uzito wa chembe (kama atomu) ataiona.

 

 

وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾

8. Na yule atakayetenda shari uzito wa chembe (kama atomu) ataiona.

 

  

Share