إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ - Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

 

 

 

 

 

   

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Share

00-Wewe Pekee Tunakuabudu: Utangulizi

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

00-Utangulizi:

           

 

 

 

Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Rahma na amani zimshukie kipenzi chetu Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na jamaa zake, na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum)  na wote waliotangulia kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Du’aa ni ‘ibaadah kwa dalili kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ﴿٦٠﴾

Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari katika kuniabudu wataingika Jahanam wadhalilike. [Ghaafir: 60]

 

Na kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي قَوْلِهِ ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ )) قَالَ: ((الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ)) وَقَرَأَ ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ )) إِلَى قَوْلِهِ: ((دَاخِرِينَ))

Amesimulia Nu’maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika kauli yake [Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa] ((Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni)) Amesema: ((Du’aa ni ‘ibaadah)) kisha akasoma: ((Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni)) mpaka kauli Yake: ((daakhiriyn)) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad – Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Na kwa kuwa lengo la kuumbwa kwa binaadamu ni kumwabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama Anavyosema:

 

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾

Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu. [Adh-Dhaariyaat: 56]

 

 

Ndio maana tunasoma Suwratul Faatihah katika Swalaah zetu zote, Suwrah ambayo imethibitisha kumwabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa aina zote za Tawhiyd na tunakiri humo:

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada. [Al-Faatihah: 5]

 

 

Basi hakuna budi kwamba tunamhitaji Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa haja zetu zote kila wakati, bali tunamhitaji Yeye kuliko tunavyohitaji chakula, hewa, maji au vyovyote vinginevyo Anavyoturuzuku. Pia tunamhitaji Atuongoze katika njia iliyonyooka ili tutimize lengo la kuumbwa kwetu kuwa ni kumwabudu Yeye Pekee bila ya kumshirikisha ili tutakapokutana Naye Aakhirah Aridhike nasi. Hali kadhaalika binaadamu hana budi imsibu mitihani mbali mbali; maafa, maradhi, shida, dhiki, maovu na kila aina za shari kutoka kwa binaadamu na majini; kwa hiyo binaadamu hatoacha kumhitaji Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa du’aa ili Amuondoeshee madhara hayo au amkinge nayo kwani hakuna Muweza ila Yeye. Lakini Ameonya kutokuelekeza du’aa kwa asiyekuwa Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٦﴾

Na wala usiombe badala ya Allaah visivyokufaa wala visivyokudhuru. Na ukifanya, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.

 

 

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ ۚ يُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚوَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿١٠٧﴾

Na Allaah Akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye. Na Akikutakia kheri, basi hakuna wa kurudisha fadhila Zake, Anasababisha kumfikia kwayo (fadhila Yake) Amtakaye katika waja Wake. Naye ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Yuwnus: 106-107]

 

Sababu za kukusanya makala za maudhui hii ya du’aa ni kutokana na kudhihirika makosa mengi yanayotendwa na ndugu zetu Waislamu katika kuomba du’aa ima kwa kumshirkisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) au kwa kuomba du’aa zisizothibiti katika mafunzo Swahiyh ya Dini, jambo ambalo ameonya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عَنْ عَائِشَةُ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ:  ((منْ أَحْدَثَ في أَمْرِنَا هذا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ))

Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayezusha [kitu] katika mambo yetu haya [katika Dini yetu] kitarudishwa)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Juu ya hivyo kumzulia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa uzushi ni dhambi kubwa itakayompeleka Muislamu katika makazi ya Moto:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم): ((مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ)) 

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeniongopea makusudi basi ajitayarishie makazi yake Motoni)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Pia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitanguliza khutbah zake kwa kutoa maonyo hayo:

 

 ((إِنَّ أَصْدَقَ الْحَدِيثِ كِتَابُ اللَّهِ وَأَحْسَنَ الْهَدْيِ هَدْيُ مُحَمَّدٍ وَشَرَّ الأُمُورِ مُحْدَثَاتُهَا وَكُلَّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ وَكُلَّ بِدْعَةٍ ضَلاَلَةٌ وَكُلَّ ضَلاَلَةٍ فِي النَّارِ))  

((Hakika mazungumzo bora ni kitabu cha Allaah [Qur-aan] na mwongozo mbora kabisa ni mwongozo wa Muhammad, na jambo la ovu kabisa ni uzushi, na kila jambo jipya [katika dini] ni bid'ah na kila bid'ah ni upotofu, na kila upotofu ni Motoni)) [An-Nasaaiy]

 

Tunatumai na kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ajaalie makala hizi ziwe zenye kuwanufaisha ndugu zetu Waislamu na ziwe ni sababu ya kuepukana na shirki pamoja na du’aa za uzushi na badala wabakie katika amani na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kutokumshirikisha na pia yafuatwe mafunzo Swahiyh ya Sunnah za Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika ‘ibaadah hii tukufu ya kuomba du’aa. Hatuna tawfiyq isipokuwa kutoka kwa Allaah, Kwake tunatawakali na Kwake tunarejea kutubia.

 

 

 

Share

01-Wewe Pekee Tunakuabudu: Maana Ya Du'aa Kilugha Na Ki-Iswtwilaah

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada.

 

01-Maana Ya Du’aa Kilugha Na Ki-Iswtwilaah

 

 

Maana Ya Du’aa Kilugha:

 

 

Neno du’aa asili yake ni kuita kwa sauti, mfano kumwita mtu, au kusema ameitwa ameitikia, au kuita wito fulani n.k. Mifano katika Kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

قَالَ رَبِّ السِّجْنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدْعُونَنِي إِلَيْهِ ۖ وَإِلَّا تَصْرِفْ عَنِّي كَيْدَهُنَّ أَصْبُ إِلَيْهِنَّ وَأَكُن مِّنَ الْجَاهِلِينَ﴿٣٣﴾

(Yuwsuf) Akasema: “Ee Rabb wangu! Nastahabu zaidi jela kuliko yale wanayoniitia. Na Usiponiepusha na vitimbi vyao nitaelemea kwao na nitakuwa miongoni mwa majahili.” [Yuwsuf: 33]

إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمْ عَدُوٌّ فَاتَّخِذُوهُ عَدُوًّا ۚ إِنَّمَا يَدْعُو حِزْبَهُ لِيَكُونُوا مِنْ أَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴿٦﴾

Hakika shaytwaan kwenu ni adui, basi mfanyeni kuwa ni adui. Hakika anaitia kikosi chake ili wawe miongoni mwa watu wa moto uliowashwa vikali mno. [Faatwir: 6] 

 

يَوْمَ يَدْعُوكُمْ فَتَسْتَجِيبُونَ بِحَمْدِهِ وَتَظُنُّونَ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٥٢﴾

 “Siku Atakayokuiteni, basi mtamuitika kwa Himidi Zake; na mtadhania kuwa hamkubakia (duniani) isipokuwa kidogo tu.” [Al-Israa: 52]

 

فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا ۚ فَلَمَّا جَاءَهُ وَقَصَّ عَلَيْهِ الْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ ۖ نَجَوْتَ مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥﴾

Basi akamjia mmoja kati ya wanawake wawili akitembea kwa kuona hayaa; akasema: “Baba yangu anakwita ili akulipe ujira wa kutunyweshea.” Basi alipomfikia na akamsimulia visa vyake; alisema: “Usikhofu, umeokoka na watu madhalimu.” [Al-Qaswasw: 25]

 

 

Maana Ya Du’aa ki Iswtwilaah:

 

Ni kitendo cha ‘ibaadah  kwa kumkabili Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kumuomba jambo kwa kuyakinisha kwamba Yeye Pekee Ndiye Anaepokea maombi kisha Ayaitikie kama Anavyosema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ﴿١٨٦﴾

Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah: 186]

 

Mifano michache kutoka katika Qur-aan:

 

هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٨﴾

Hapo hapo Zakariyyaa akamwomba Rabb wake, akasema: “Rabb wangu Nitunukie kutoka Kwako kizazi chema hakika Wewe ni Mwenye kusikia du’aa yangu.” [Aal-‘Imraan: 38]

 

 

رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ﴿٢٠٠﴾

“Rabb wetu Tupe katika dunia;” naye katika Aakhirah hana sehemu yoyote. [Al-Baqarah: 38]

 

 رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا ﴿١١٤﴾

“Rabb wangu! Nizidishie elimu.” [Twaahaa: 114]

 

 Mifano katika Sunnah:

 

 

اللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي ظُلْمًا كَثِيرًا وَلاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ فَاغْفِرْ لِي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ وَارْحَمْنِي إِنَّك أَنْتَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ

Ee Allaah, hakika nimedhulumu nafsi yangu dhuluma nyingi wala hakuna wa kughufuria madhambi isipokuwa Wewe, basi Nighufurie maghfirah kutoka Kwako na Nirehemu, hakika Wewe ni Mwingi wa Kughufuria Mwenye Kurehemu daima [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad]

 

  اَللَّهُمَّ يَا مُقَلِّبَ الْقُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِك

((Ee Mwenye kupindua nyoyo, Thibitisha moyo wangu katika Dini Yako [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad, Al-Haakim  na Taz Swahiyh Al-Jaami’ 7987]

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَأَسْتَجِيرُ بِكَ مِنَ النَّارِ

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba Pepo na najilinda Kwako dhidi ya Moto [At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah – Swahiyh At-Tirmidhiy (2/319]

 

  اللّهُـمَّ أَعِـنِّي عَلـى ذِكْـرِكَ وَشُكْـرِك ، وَحُسْـنِ عِبـادَتِـك

Ee Allaah nisaidie juu Kukudhukuru, na kukushukuru na kukuabudu kwa uzuri utakikanao. 

[Abu Daawuwd, An-Nasaaiy]

 

 

Share

02-Wewe Pekee Tunakuabudu: Hali Ya Du’aa Baada Ya Kuombwa

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada.

 

02- Hali Ya Du’aa Baada Ya Kuombwa

 

 

 

Kuomba du’aa wakati mwingine huwa ni mtihani wa kujaribiwa Iymaan ya Muislamu pale du’aa yake inapochelewa au isipotakabaliwa. Shaytwaan hapo humchochea binaadamu kwa kumkatisha tamaa na kumtia dhana mbaya kuhusu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Inapofika hali hii anapaswa Muislamu kujikinga na Shaytwaan na kuendelea kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) bila ya kuchoka na bila kukata tamaa kwa sababu hakuna shaka kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ameshaisikia du’aa ya mja Wake:

 

عَنْ سَلْمَانَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِنَّ رَبَّكُمْ تَبَارَكَ وَتَعَالَى حَيِيٌّ كَرِيمٌ يَسْتَحْيِي مِنْ عَبْدِهِ إِذَا رَفَعَ يَدَيْهِ إِلَيْهِ أَنْ يَرُدَّهُمَا صِفْرًا))

Kutoka kwa Salmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Rabb wenu Aliyebarikika na Aliyetukuka, Yuhai, Mkarimu, Anastahi kutoka kwa mja Wake anaponyanyua mikono yake kisha Airudishe sifuri)) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah]

 

 

Na Muislamu anapomkabili Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kumuomba jambo, du’aa yake huwa katika hali tatu kama iivyothibiti katika Hadiyth:

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ (رضي الله عنه)  أَنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَدْعُو بِدَعْوَةٍ لَيْسَ فِيهَا إِثْمٌ وَلاَ قَطِيعَةُ رَحِمٍ إِلاَّ أَعْطَاهُ اللَّهُ بِهَا إِحْدَى ثلاَثٍ:  إِمَّا أَنْ تُعَجَّلَ لَهُ دَعْوَتُهُ وَإِمَّا أَنْ يَدَّخِرَهَا لَهُ فِي الأَخِرَةِ وَإِمَّا أَنْ يَصْرِفَ عَنْهُ مِنْ السُّوءِ مِثْلَهَا))  قَالُوا إِذًا نُكْثِرُ قَالَ:  ((اللَّهُ أَكْثَرُ))

Kutoka kwa Abu Sa’iyd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna Muislamu atakayeomba du’aa ambayo haina dhambi wala kukata undugu wa uhusiano wa damu isipokuwa Allaah Atampa mojawapo ya matatu; ima Amharakishie du’aa yake, au Amuwekee akiba Aakhirah au ima Amuepushe nayo ovu kama hilo)) Wakasema: Basi tutazidisha (kuomba du’aa). Akasema: ((Allaah Mwingi zaidi [wa kuongeza])) [Ahmad]

 

Hali tatu hizo ni:

 

1-Kutakabaliwa du’aa yake; huenda akatakabaliwa hapo hapo, au baada ya muda mfupi au muda mrefu.

 

2-Kumwekea akiba Aakhirah ambako malipo yake huko ni bora zaidi na ya kudumu kuliko duniani.

 

3-Kutokutakabaliwa kwani huenda ikawa anachokiomba kina shari naye Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 

وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢١٦﴾

Na asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni kheri kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui. [Al-Baqarah: 216]

 

  

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) katika Fatwa ya: “Hukmu Ya Kusema Wazi (Au Kudhihirisha Wasiwasi) Kwa Kutokubaliwa Du'aa” kama ifuatavyo: 

 

Swali: 

 

Je inapokuwa haijahakiki kwangu jambo niloliomba huwa naghadhibika na husema maneno katika nafsi yangu na kuhusu Allaah mfano husema: “Kwanini Yaa Rabb Huitikii du'aa yangu?” Na husema mengineyo pia. Naomba tafadhali uniongoze kuhusu haya. Na je, binaadamu anapohisi kuwa du'aa yake haikutakabaliwa afanyeje?

 

Akajibu:

 

“Ni juu yako ee muulizaji na kila Muislamu mwanamme na mwanamke inapochelewa kutakabaliwa (du'aa yako) basi jirudie nafsi yako na ujipime kwani Allaah ni Hakiymun-‘Aliym (Mwenye hikma na Mjuzi) Huenda Anaichelewesha kutakabaliwa (hiyo du'aa) kwa hikma kubwa ili mja akithirishe du’aa kwa Muumba wake, na kujilazimisha Kwake, na  kujidhalilisha kwa Utukufu Wake na kungʼangʼania katika kuomba haja yake na kuzidisha kurudi Kwake na kunyenyekea Kwake. Ili kwa kufanya hivyo, (mja mwenye kuomba) apate kheri na manufaa mengi na aweze kuutengeneza moyo na kumridhia Rabb wake. Yote haya ni adhimu zaidi na yenye manufaa zaidi kuliko haja yake. 

 

Pia huenda Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akachelewesha (kujibu du'aa) kwa sababu nyinginezo kama vile (muombaji) kujichanganya katika maasi kama kula chumo la haraam au kuwaasi wazazi wawili na maasi mengineyo.

 

Basi inawajibika kwa muombaji du’aa ajihesabu nafsi yake na akimbilie kuomba tawbah huku awe na matumaini kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anamtakabalia tawbah yake na Atamuitikia du’aa yake.

 

Na huenda Akaichelewesha kwa hikma nyingine Anayoijua Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama vile ilivyo katika Hadiyth Swahiyh:

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ (رضي الله عنه)  أَنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَدْعُو بِدَعْوَةٍ لَيْسَ فِيهَا إِثْمٌ وَلاَ قَطِيعَةُ رَحِمٍ إِلاَّ أَعْطَاهُ اللَّهُ بِهَا إِحْدَى ثلاَثٍ:  إِمَّا أَنْ تُعَجَّلَ لَهُ دَعْوَتُهُ وَإِمَّا أَنْ يَدَّخِرَهَا لَهُ فِي الأَخِرَةِ وَإِمَّا أَنْ يَصْرِفَ عَنْهُ مِنْ السُّوءِ مِثْلَهَا))  قَالُوا إِذًا نُكْثِرُ قَالَ:  ((اللَّهُ أَكْثَرُ))

Kutoka kwa Abu Sa’iyd (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna Muislamu atakayeomba du’aa ambayo haina dhambi wala kukata undugu wa uhusiano wa damu isipokuwa Allaah Atampa mojawapo ya matatu; ima Amharakishie du’aa yake, au Amuwekee akiba Aakhirah au ima Amuepushe nayo ovu kama hilo)) Wakasema: Basi tutazidisha (kuomba du’aa). Akasema: ((Allaah Mwingi zaidi [wa kuongeza])) [Ahmad]

 

Basi itakapochelewa haja yako kutakabaliwa, usimlaumu Rabb wako wala usiseme: “kwanini, kwanini Yaa Rabb” bali ni juu yako kujirudi nafsi yako kwani Rabb wako ni Hakiymun-‘Aliym (Mwenye hikma, Mjuzi wa yote). Rudia nafsi yako na tazama kwani huenda una dhambi au maasi fulani ikawa ndio sababu ya kuchelewa kuitikiwa. Au huenda kuna jambo jengine lililosababisha kuchelewa kuitikiwa. Yote hayo huwa ni kheri kwako. Basi haijuzu kumlaumu Rabb wake yasiyomstahiki (Subhaanahu wa Ta’aalaa), lakini ni juu yako kujilaumu nafsi yako na utazame ‘amali zako na nyendo zako mpaka ujitengeneze nafsi yako ili uthibitike katika amri ya Rabb wako na uache kufanya Anayoyakataza na usimame (usivuke) katika mipaka Yake.

 

Pia inapasa kutambua kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) huenda Akachelewesha jibu kwa muda mrefu kama vile Alivyomcheleweshea kumtakabalia Nabiy Ya’quwb kuhusu kumrudisha kwake mwanawe Yuwsuf. Naye ni ni Nabiy mtukufu (‘Alayhis-ssalaam). Pia kama alivyochelewesha kumpa shifaa Nabiy Wake Ayyuwb (‘Alayhis-ssalaam).

 

Na huenda Allaah Akampa muombaji yaliyo kheri zaidi kuliko aliyoyaomba na huenda Akamuepusha na shari (ikawa kheri kwake) kuliko aliyoyaomba kama tulivyotaja katika Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (iliyotangulia...) Akabainisha (‘Alayhis-swalaatu was-salaam)) kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) huakhirisha jibu mpaka Aakhirah, au Huitakabali duniani, kutokana na hikma kubwa kwa sababu hivyo ina maslahi na manufaa zaidi kwa mja Wake, na Humuepusha na shari kubwa kabisa ikawa ni kheri kwake kuliko kutakabaliwa du’aa yake.

 

Basi kuwa na husnu-dhwann (dhana nzuri) kwa Allaah na endelea kuomba du’aa...”

[Fataawaa Ibn Baaz: Hukmu Al-Muswaarahah Bi ’Adami Qabuwl Ad-Du’aa, Juz. 5: 303].

 

 

 

Share

03-Wewe Pekee Tunakuabudu: Fadhila Za Du’aa

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada.

 

03-Fadhila Za Du’aa

 

 

 

Fadhila za du’aa ni nyingi mno, zifuatazo ni baadhi ya fadhila zake:

 

 

1- Du’aa Ni ‘Ibaadah:

 

Juu ya kuwa ‘ibaadah zetu hazimfai wala kumnufaisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) chochote, lakini Yeye (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anatuhimiza tumkabili kumuomba:

 

عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي قَوْلِهِ ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ)) قَالَ: ((الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ)) وَقَرَأَ ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ)) إِلَى قَوْلِهِ: ((دَاخِرِينَ))

Amesimulia Nu’maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika kauli yake [Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa] ((Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni. ) Amesema: ((Du’aa ni ‘ibaadah)) kisha akasoma: ((Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni. )) mpaka kauli Yake: ((daakhiriyn)) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad – Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

 

2- Du’aa Ni ‘Amali Tukufu Kabisa:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اللَّهِ تَعَالَى مِنْ الدُّعَاءِ))  

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna kitu kitukufu mbele ya Allaah kama du’aa))  [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad, na amesema At-Tirmidhiy: Hasan Ghariyb na ameisahihisha Ibn Hibbaan, Al-Haakim na ameipa muwafaka Adh-Dhahaabiy na ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy katika Swahiyh Adab Al-Mufrad] 

 

 

 

3- Du’aa Inadhihirisha Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

Mja anapomkabili Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kumuomba du’aa, huwa anamkabili kwa aina zote za Tawhiyd; kwani huwa ameamini kwamba Yeye Allaah ni Rabb, Mola, Muumbaji, Mtoaji rizki, Mwendeshaji na Msimamizi wa mambo, Mfishaji na Mwenye kuhuisha; nayo ni Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah. Na kwamba Yeye Pekee Ndiye Anayestahiki kuabudiwa kwa haki na kuombwa (Tawhiyd Al-Uluwhiyyah), na kwamba Yeye Ndiye Mwenye Majina Mazuri kabisa na Sifa Zake (Tawhiyd Al-Asmaa wasw-Swifaat).

 

 

 

4- Kuomba Du’aa Ni Kujikurubisha Na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama Anavyosema:

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ

Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi);  [Al-Baqarah: 186]

 

 

 

5- Kuomba Du’aa Ni Sifa mojawapo ya ‘Ibaadur-Rahmaan’ (Waja wa Mwingi wa Rahmah)   

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ametaja baadhi ya sifa ambazo Amezihusisha na waja Wake aliowaita ‘Ibaadur-Rahmaan katika Suwratul-Furqaan.  Miongoni mwa sifa hizo ni kuomba du’aa mbili zifuatazo:

وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ ۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿٦٥﴾

Na wale wanaosema: “Rabb wetu! Tuepushe adhabu ya Jahannam. Hakika adhabu yake ni yenye kugandamana daima; isiyomwacha mtu.” [Al-Furqaan: 65]

 

وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾

Na wale wanaosema: “Rabb wetu! Tutunukie katika wake zetu na dhuria wetu viburudisho vya macho yetu, na Tujaalie kuwa waongozi kwa wenye taqwa.  [Al-Furqaan: 74]

 

 

 

6- Kuomba Du’aa Ni Miongoni Mwa Sifa Za Watu Wa Jannah:

 

 

Waumini watakapokuwa Jannah hawatakuwa na la kuwashughulisha kama wanavyoshughulika duniani, bali ni starehe tupu na maombi yao na kauli zao zitakuwa ni kumtakasa, kumtukuza na kumhimidi Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama Anavyosema:

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُم بِإِيمَانِهِمْ ۖتَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ﴿٩﴾

Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Rabb wao Atawaongoza kwa iymaan zao. Zitapita chini yao mito katika Jannaat za neema.

 

 

دَعْوَاهُمْ فِيهَا سُبْحَانَكَ اللَّـهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ ۚ وَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿١٠﴾

Wito wao humo ni: “Utakasifu ni Wako ee Allaah.” Na maamkizi yao humo ni “Salaamun!” Na wito wao wa mwisho ni “AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah) Rabb wa walimwengu.” [Yuwnus: 9 -10]

 

 

 

7- Du’aa Ni Sababu Ya Kufunguliwa Milango Ya Rahmah Na Sababu Ya Kuondolewa Na Balaa Kabla Ya Kuteremka:

 

عَنْ ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَنْ فُتِحَ لَهُ مِنْكُمْ بَابُ الدُّعَاءِ فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الرَّحْمَةِ وَمَا سُئِلَ اللَّهُ شَيْئًا يَعْنِي أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ أَنْ يُسْأَلَ الْعَافِيَةَ)) وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِنَّ الدُّعَاءَ يَنْفَعُ مِمَّا نَزَلَ وَمِمَّا لَمْ يَنْزِلْ فَعَلَيْكُمْ عِبَادَ اللَّهِ بِالدُّعَاءِ))  

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayefunguliwa mmoja wenu mlango wa du’aa, amefunguliwa mlango wa Rahmah, na Akipendacho Allaah Zaidi kuombwa ni al-‘aafiyah (afya, siha, amani, hifadhi n.k))  Na akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hakika du’aa inanufaisha (misiba) inayoteremka na isiyoteremka, hivyo basi juu yenu waja wa Allaah kwa kuomba du’aa)) [At-Tirmidhiy na ameipa daraja ya Hasan Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’]

 

8- Du’aa Inaweza Kubadilisha Qadar (Majaaliwa):

 

Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عَنْ سَلْمَانَ (رضي الله عنه)  قَالَ:  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ):  ((لاَ يَرُدُّ الْقَضَاءَ إِلاَّ الدُّعَاءُ ولاَ يَزِيدُ فِي الْعُمْرِ إِلاَّ الْبِرُّ))  

Kutoka kwa Salmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hairudishi Qadhwaa ila du’aa na haizidishi umri ila wema)) [At-Tirmidhiy]

 

Kwa hiyo du’aa inabadilisha yaliyoandikwa katika Sahifa za Malaika wawili; wa kulia na kushoto kama vile ilivyothibiti katika kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

يَمْحُو اللَّـهُ مَا يَشَاءُ وَيُثْبِتُ ۖ وَعِندَهُ أُمُّ الْكِتَابِ﴿٣٩﴾

Allaah Anafuta yale Ayatakayo na Anathibitisha (Ayatakayo), na Kwake kiko Mama wa Kitabu. [Ar-Ra’d: 39]

 

Kwa maana mtu akifanya jema, basi jema hilo linafuta dhambi kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ﴿١١٤﴾

Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku; hakika mema yanaondosha maovu. Hivyo ni ukumbusho kwa wanaokumbuka. [Huwd: 114]

 

Au mtu akitubia na akaomba maghfirah basi maovu yake hubadilishwa kwa mema yake kama ilivyothibiti katika kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا ﴿٦٨﴾

Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na wala hawazini. Na atakayefanya hivyo atakutana na adhabu.

 

يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا ﴿٦٩﴾

Ataongezewa adhabu maradufu Siku ya Qiyaamah, na mwenye kudumu humo akiwa amedhalilika.

 

 

إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾

Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda ‘amali njema; basi hao Allaah Atawabadilishia maovu yao kuwa mema. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا ﴿٧١﴾

Na atakayetubu na akatenda mema, basi hakika yeye anatubia kwa Allaah tawbah ya kweli. [Al-Furqaan: 68-71]

 

Na katika kuhusiana na du’aa, mfano mtu amejiombea du’aa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amghufurie madhambi yake na kwa kutubia kwake, basi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) humghufuria madhambi yake. Au alimtendea wema fulani nduguye Muumini kisha huyu ndugu akamuombea du’aa njema kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) amghufurie dhambi zake au amjaalie kheri fulani. Basi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akaamrisha Malaika wayafute maovu na kuthibitisha mema. Lakini Allaah ('Azza wa Jalla) ni Mjuzi wa yote hayo kabla ya hapo, kwa kuwa imeshaandikwa katika Lawhum-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) kabla ya kuumbwa mbingu na ardhi na viliomo ndani yake pindi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alipoiamrisha kalamu iandike Qadhwaa na Qadar. Na hivyo basi yaliyoandikwa humo katika Lawhun-Mahfuwdhw hayafutiki kamwe, kwa sababu hiyo ni Ilmu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Kujua Kwake; kwamba mja atafanya wema fulani, siku kadhaa kisha Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atamuamrisha Malaika afute na athibitishe katika Sahifa za Malaika wawili.  Na hii ndio ‘Aqiydah Sahihi kuamini kuwa Allaah Ameandika katika Lawhun Mahfuwdhw yote yaliyotokea na yatakayotokea mpaka Siku ya Qiyaamah.

 

 

 

9- Kuomba Du’aa Ni Kuepushwa Na Moto  

 

Waumini wenye taqwa watakapoepushwa na Moto huko Aakhirah, watakabiliana na wenzao na kuulizana sababu za kuingizwa kwao Jannah, na kuomba du’aa ni mojawapo wa sababu hizo; Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٥﴾

Na watakabiliana baadhi yao kwa wengineo wakiulizana.

 

قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ ﴿٢٦﴾

Watasema: “Hakika sisi tulikuwa kabla kwenye ahli zetu wenye kuogopa

 

 

فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ ﴿٢٧﴾

Basi Allaah Akatufadhilisha, na Akatuokoa na adhabu ya moto unaobabua.

 

 

إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾

Hakika sisi tulikuwa kabla Tunamuomba Yeye Pekee, hakika yeye Ndiye Mwingi huruma na fadhila, Mwenye kurehemu.” [Atw-Twuwr: 25- 28]

 

 

Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) alipokuwa akisoma Aayah hizi, akiomba du’aa:

"اللَّهُمَّ مُنَّ عَلَيْنَا وَقِنَا عَذَاب السَّمُوم إِنَّك أَنْتَ الْبَرّ الرَّحِيم"

‘Ee Allaah, Tufanyie fadhila, na Tuepushe na adhabu Moto unaobabua, hakika Wewe ni Al-Barrur-Rahiym (Mwingi huruma na fadhila - Mwenye kurehemu).” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

 

10- Kuomba Du’aa Ni Kufuata Sunnah Za Manabiy, Na Nyendo Za Salaf.  

 

Kuhusu Manabiy, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwamba kuomba du’aa ilikuwa ni shani yao. Manabiy walipokosea walirudi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kuomba maghfirah na msamaha. Iliwasibu Manabiy balaa, maudhi, madhara na shari za kila aina kutoka kaumu zao baada ya kuwalingania Ujumbe wa Allaah. Walipotaka nusura, walitumia du’aa kuwa ni ufumbuzi, utatuzi wa mashakili yao wapate faraja.

Mfano kuhusu Nuhw (‘Alayhis-salaam) aliposhindwa kabisa baada na kaumu yake:

كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا عَبْدَنَا وَقَالُوا مَجْنُونٌ وَازْدُجِرَ ﴿٩﴾

Walikadhibisha kabla yao kaumu ya Nuwh, wakamkadhibisha mja Wetu, wakasema: “Majnuni.” Na akakaripiwa.

فَدَعَا رَبَّهُ أَنِّي مَغْلُوبٌ فَانتَصِرْ ﴿١٠﴾

Basi akamwita Rabb wake kwamba: “Hakika mimi nimeshindwa nguvu basi Nusuru.” [Al-Qamar: 9-10]

 

 

Mfano wa Nabiy Zakariyyah alipotamani mwana ili amrithi katika Unabiy:

 

 وَزَكَرِيَّا إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ ﴿٨٩﴾

Na Zakariyyaa alipomwita Rabb wake: “Rabb wangu! Usiniache pekee; Nawe Ndiye Mbora wa wenye kurithi.”

 

فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَوَهَبْنَا لَهُ يَحْيَىٰ وَأَصْلَحْنَا لَهُ زَوْجَهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ ﴿٩٠﴾

Basi Tukamuitikia na Tukamtunukia Yahyaa, na Tukamtengenezea mke wake. Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri, na wakituomba kwa raghba na khofu, na walikuwa wenye kutunyenyekea. [Al-Anbiyaa: 89-90]

 

Na mifano mingineyo mbali mbali ya du’aa za Manabiy katika katika Qur-aan. [Rejea mlango wa Du’aa katika Qur-aan]

 

Ilikuwa pia ni nyendo za Salafus-Swaalih ambao wakimuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa unyenyekevu nyakati za usiku:

 

إِنَّمَا يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا الَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِهَا خَرُّوا سُجَّدًا وَسَبَّحُوا بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ۩﴿١٥﴾

Hakika wanaamini Aayaat Zetu wale wanapokumbushwa nazo huporomoka kusujudu, na wakasabbih kwa Himidi za Rabb wao, nao hawatakabari.

 

تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿١٦﴾

Mbavu zao zinatengana na vitanda, wanamuomba Rabb wao kwa khofu na matumaini, na katika yale Tuliyowaruzuku wanatoa. [As-Sajdah: 15-16]

 

 

 

11- Kuomba Du’aa Ni Amali Mojawapo Itendwayo Na Malaika Kuwaombea Waumin:

 

الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ﴿٧﴾

 (Malaika) Ambao wanabeba ‘Arsh na walio pembezoni mwake, wanasabbih kwa Himidi za Rabb wao, na wanamwamini; na wanawaombea maghfirah wale walioamini: “Rabb wetu! Umekienea kila kitu kwa rahmah na ujuzi, basi waghufurie wale waliotubu, na wakafuata njia Yako, na wakinge na adhabu ya moto uwakao vikali mno.

 

رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدتَّهُمْ وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٨﴾

 “Rabb wetu! Waingize Jannaat za kudumu milele ambazo Umewaahidi, pamoja na waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na dhuria wao.  Hakika Wewe Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

وَقِهِمُ السَّيِّئَاتِ ۚ وَمَن تَقِ السَّيِّئَاتِ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمْتَهُ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٩﴾

 “Na wakinge maovu, kwani Unayemkinga na maovu Siku hiyo, basi kwa yakini Umemrehemu. Na huko ndiko kufuzu adhimu. [Ghaafir: 7-9]

 

 

12- Kuomba Du’aa Ni Dalili Ya Wenye Akili Wanaothibitisha Tawhiyd

 

Wenye akili hutafakari uumbaji wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Hutafakari pia jinsi Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anavyoendesha mambo yote ya ulimwengu kwa ajili ya walimwengu.  Hapo hutambua utukufu na uwezo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), kisha huomba du’aa. Basi hao Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amewasifu kuwa ni dalili ya ‘wenye akili’:

 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ 

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (ishara, zingatio) kwa wenye akili.

 

الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿١٩١﴾ 

Ambao wanamdhukuru Allaah kwa kusimama  na kwa kukaa na kwa kulala ubavuni mwao na wanatafakari katika kuumbwa mbingu na ardhi (wakisema): “Rabb wetu, Hukuumba haya bure, Subhaanak! (Utakasifu ni Wako) tukinge na adhabu ya moto.”

 

 

رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿١٩٢﴾

 “Rabb wetu, hakika Umuingizaye motoni, kwa yakini Umemhizi. Na madhalimu hawana yeyote mwenye kuwanusuru.”

 

 

رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلْإِيمَانِ أَنْ آمِنُوا بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا ۚ رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الْأَبْرَارِ ﴿١٩٣﴾

 “Rabb wetu, hakika sisi tumemsikia mwitaji anaita kwenye iymaan kwamba ‘mwaminini Rabb wenu’ basi tukaamini.  Rabb wetu, Tughufurie madhambi yetu na Tufutie makosa yetu na Tufishe pamoja na Waumini wema.”

 

 رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّكَ لَا تُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿١٩٤﴾

 “Rabb wetu na Tupe Uliyotuahidi kupitia Rusuli Wako, wala Usituhizi Siku ya Qiyaamah; hakika Wewe Huendi kinyume na miadi.” [Aal-‘Imraan: 190-194]

 

 

Fadhila zao Waumini hao wenye kuomba du’aa hizo, ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amewatakabalia du’aa zao, na Amewaghufuria maovu yao, na Amewaahidi mengi mazuri pamoja na kuwaingiza katika Jannah Yake yenye neema  [Aal-‘Imraan: 195-199]

 

 

 

Share

04-Wewe Pekee Tunakuabudu: Umuhimu Wa Kuomba Du’aa

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

04 -Umuhimu Wa Kuomba Du’aa

 

 

 

Muislamu mwenye akili, hathubutu kumkabili kiumbe yeyote mwingine kumuomba haja ambayo binaadamu hana uwezo nayo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), kwa sababu tofauti baina ya kumkabili Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kumuomba na kumkabili kiumbe ni:

 

Kumkabili Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

1-Kupata linaloombwa

 

2-Kupata manufaa kama thawabu kwa kutekeleza ‘ibaadah ya du’aa.

 

3-Kuepushwa na shari ya linaloombwa.

 

4-Kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa vile ni ‘amali Aipendayo Allaah.

 

5-Du’aa ni kitendo chepesi kabisa hakina masharti mazito kama sharti za fardhi au ‘amali nyinginezo. Popote ulipo; safarini bara au baharini, umesimama, umekaaa, umelala unaweza kutekeleza ‘ibaadah hii tukufu, hata moyoni mtu anaweza kuomba du’aa yake

 

 

Kumkabili kiumbe kwa ambalo hana uwezo nalo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

1-Anayekabiliwa hawezi kumiliki chochote ila kwa idhni ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)

 

2-Ni kujiingiza katika maasi makubwa ya kumshirkisha (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na hivyo ni kuchuma dhambi.     

 

3-Kujiingiza katika shari, balaa kwa sababu hakuna dhamana kwamba anayeombwa atakuwa ana ikhlaasw kwa muombaji yaani huenda hamtakii kheri, hivyo huenda akamdhuru badala ya kumnufaisha.

 

4-Kujidhalilisha kwa binaadamu kwa kudhihirisha shida, malalamiko n.k.

 

5-Ni kujitia katika taklifu ya nafsi na mali kumfuata anayeombwa. Aghlabu mahali pa anayefuatwa kuombwa huwa ni mahali mahsusi mfano wanaowaomba maiti kaburini, au kumwendea shekhe, mganga, mtabiri n.k.

 

 

Umuhimu mwengineo wa kuomba du’aa ni kama ifautavyo:

 

1- Kutokuomba du’aa ni kudhihirisha kibri:

 

Kuhusu Hadiyth:

 

عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي قَوْلِهِ ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ)) قَالَ: ((الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ)) وَقَرَأَ ((وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ)) إِلَى قَوْلِهِ: ((دَاخِرِينَ))

Amesimulia Nu’maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  katika kauli yake [Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa] ((Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni)) Amesema: ((Du’aa ni ‘ibaadah)) kisha akasoma: ((Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni)) mpaka kauli Yake: ((daakhiriyn)) [Ghaafir 40:60] [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad – Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Kauli hiyo tukufu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) inamalizika:

 

إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ﴿٦٠﴾

Hakika wale wanaotakabari katika kuniabudu wataingika Jahanam wadhalilike. [Ghaafir: 60]

 

Ash-Shawkaaniy (Rahimahu Allaah) amesema: “Aayah hii tukufu ni dalili kwamba du’aa ni kitendo cha ‘ibaadah kwa sababu Ameamrisha waja Wake wamwombe Yeye. Na kauli Yake: ((Hakika wale wanaotakabari katika kuniabudu)) inadhihirisha pia kuwa du’aa ni ‘ibaadah, na kuacha kuomba du’aa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni kudhihirisha kibri, bali hakika ni chukizo kubwa. Vipi mja atakabari kuomba du’aa kwa Ambaye Amemuumba na hali hakuwa chochote, Akampa rizki? Ambaye Ameumba ulimwengu na Akakipa kila kitu mahitaji yake, Akawapa maisha, Naye Ndiye Mwenye kufisha kisha Awalipe malipo mema au Awaadhibu? Bila ya shaka kibri kama hiki ni aina ya wazimu na ni dalili za wazi za kutokuwa na shukurani” [Tuhfat Adh-Dhaakiriyn]

 

 

 

2- Kuomba du’aa ni kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anatuamrisha katika kauli Zake mbali mbali tumuombe, Anasema:

قُلْ أَمَرَ رَبِّي بِالْقِسْطِ ۖ وَأَقِيمُوا وُجُوهَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

Sema: “Rabb wangu Ameniamrisha uadilifu; na muelekeze nyuso zenu kwenye kila mahali pa kusujudu na mumuombe Yeye, muwe wenye kumtakasia Yeye Dini [Al-A’raaf: 29]

 

Anasema pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):        

وَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ

Na muombeni Allaah fadhila Zake.     [An-Nisaa: 32]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):      

  

هُوَ الْحَيُّ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۗ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٦٥﴾

Yeye Ndiye Aliye hai daima hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye; basi muombeni Yeye wenye kumtakasia Dini. AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu. [Ghaafir: 65]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ﴿١٨٦﴾

186. Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah: 186]

 

 Pia rejea Aayah ilotangulia ya [Suwrat Ghaafir: 60]

 

 

 

 

 3- Asiyeomba du’aa, Allaah Humghadhibikia:

 

Kinyume na binaadamu ambaye huenda akachoshwa na kuchukizwa na maombi ya binaadamu mwenzake. Ama Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Humpenda mwenye kumuomba bali Hughadhibika na mja Wake asipomuomba: 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَنْ لَمْ يَسْأَل اللَّهَ يَغْضَب عَلَيْهِ)) حسنه الألباني في صحيح سنن الترمذي برقم 2686

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Asiyemuomba Allaah, Humghadhibikia)) [At-Tirmidhiy ameipa daraja ya Hasan Imaam Al-Albaaniy taz Swahiyh At-Tirmidhiy (2686)]

 

 

 

4- Kuomba du’aa ni kuepushwa na adhabu za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَمَا كَانَ اللَّـهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿٣٣﴾

Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu hali wao wanaomba maghfirah. [Al-Anfaal: 33]

 

 

 

 5- Majaaliwa Yaliyoandikwa Na Waandishi Wawili (Malaika) Hayabadilishwi Ila Kwa Du'aa:

 

عَنْ ثَوْبَانَ (رضي الله عنه)  أن النبي (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ:  ((لاَ يَرُدُّ الْقَدَرَ إلاَّ الدُّعَاءُ وَلاَ يَزِيدُ فِي الْعُمُرِ إلاَّ الْبِرُّ وَإِنَّ الْعَبْدَ لَيُحْرَمُ الرِّزْقَ بِالذَّنْبِ يُصِيبُهُ))

Kutoka kwa Thawbaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hairudishwi Qadar (majaaliwa) ila kwa du’aa, wala hauzidi umri ila kwa wema, na hakika mja anaharamishiwa rizki kutokana na dhambi aitendayo)) [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy ktk Swahiyh At-Targhiyb (638)]

 

 

 

6- Du’aa ni sababu kuu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kutujali:

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

قُلْ مَا يَعْبَأُ بِكُمْ رَبِّي لَوْلَا دُعَاؤُكُمْ ۖ فَقَدْ كَذَّبْتُمْ فَسَوْفَ يَكُونُ لِزَامًا ﴿٧٧﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Rabb wangu Asingekujalini lau kama si du’aa zenu; kwa yakini mmekadhibisha, basi adhabu itakuwa ya lazima kukugandeni tu! [Al-Furqaan: 77]

 

Aayah hii tukufu ni hitimisho baada ya kutaja Sifa za ‘Ibaadur-Rahmaan (Waja wa Rahmaan) ambazo humo zimo pia du’aa za kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).   

 

 

7- Du’aa ni silaha ya Muumini:

 

Du’aa ni silaha ya Muumini aliye dhaifu, aliyedhulumiwa, na pia kwa yeyote asiyekuwa na matumaini ya kupata faraja kutokana na shida na dhiki zake, au kupata ushindi dhidi ya adui yake. Manabiy wangapi walipata faraja baada ya madhara, mateso, na bughudha za watu wao hatimaye wakapata ushindi na wakainusuru Dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa sababu ya kuomba du’aa?

 

Nuwh (‘Alayhis-salaam) baada ya kulingania kaumu yake miaka 950 hatimaye alikata tamaa akamuelekea Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), Naye Akampa faraja na Akumnusuru na Akawaangamiza waovu katika kaumu yake: [Al-Qamar: 9-16, Al-‘Ankabuwt: 14-15]

 

Nabiy Ayyuwb (‘Alayhis-salaam) alipatwa na mitihani ya kila aina, alikumbwa na maradhi na ufakiri naye akavumilia mwishowe akamkabili Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Naye Akamuondoshea maradhi na kumpa yaliyo kheri zaidi. [Al-Anbiyaa: 83-84, Swaad: 41-44].

 

Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) alipatwa na mitihani wa baba yake na watu wake, na hadi kutumbukizwa kwenye moto lakini du’aa yake ya kumtegemea Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ndio iliyomuokoa na moto huo baada ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kuufanya moto uwe wenye amani na baridi. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akambariki kwa vizazi vyema naye akawa baba wa Manabiy wote baada yake. [Al-Anbiyaa: 51-73].

 

Nabiy Muwsaa (‘Alayhis-salaam) alikuwa kila inapomfika mtihani mkubwa au mdogo akimuelekea Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Naye Akamghufuria makosa yake, Akampa faraja baada ya kumuokoa kutokana na adui yake Fir’awn [Ash-Shu’araa: 63-67]

 

Nabiy Yuwnus (‘Alayhis-salaam) baada ya kufanya kosa kukimbia watu wake, akamezwa na nyangumi akawa katika kiza na dhiki, akamuelekea Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kumuomba maghfirah, akaokolewa na kupewa faraja kwa kuamrishwa nyangumi amcheuwe fukoni. [Al-Anbiyaa: 87-88] 

 

Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye mitihani yake ilikuwa ya aina mbali mbali zikiwemo njama za kuuliwa na watu wake. Lakini kila mara alikuwa akimuelekea Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ambaye Alimlinda na Akampa ushindi wa Dini ya Kiislamu. 

 

Basi Muumini hana budi kuithamini du’aa na kuitegemea kuwa ni silaha yake katika hali yoyote ya mitihani atakayoikabili ikiwa ni mitihani kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) au inayosababishwa na binaadamu.     

 

 

 

8- Kuomba du’aa ni kujiepusha na ubakhili na ukataji tamaa:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنِ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((إنَّ أَعْجَز النَّاس مَنْ عَجَزَ عَنْ الدُّعَاء وَأَبْخَل النَّاس مَنْ بَخِلَ بِالسَّلاَمِ))

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika aliye bakhili kabisa miongoni mwa wa watu ni mwenye kufanya ubakhili katika kutoa salaam, na mkataji tamaa kabisa miongoni mwa watu ni mwenye kukata tamaa na du’aa)) [Ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy Taz. As-Silsilah Asw-Swahiyhah (601)]

 

 

 

9- Takrima kwa muombaji du’aa na ni sababu ya kupata unyenyekevu:  

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا ﴿٢٨﴾

28. Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka Wajihi Wake. Na wala macho yako yasiwavuke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Na wala usimtii Tuliyemghafilisha moyo wake na Ukumbusho Wetu akakafuata hawaa zake, na jambo lake limekuwa la kuzidi kuvuka mipaka. [Al-Kahf: 28]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٢﴾

Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Rabb wao asubuhi na jioni wanataka Wajihi Wake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, na wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata ukawafukuza; utakuja kuwa miongoni mwa madhalimu. [Al-An’aam: 52]

 

 

 

10 – Du’aa inamtoa mja katika unyonge na ufidhuli:

 

Mafunzo kutoka kwa Manabiy watukufu; Nabiy Zakariyyah (‘Alayhis-salaam) alipoomba alisema:

 

رَبِّ إِنِّي وَهَنَ الْعَظْمُ مِنِّي وَاشْتَعَلَ الرَّأْسُ شَيْبًا وَلَمْ أَكُن بِدُعَائِكَ رَبِّ شَقِيًّا ﴿٤﴾

 

 “Rabb wangu! Hakika mimi mifupa imeninyong’onyea na kichwa kimeng’aa mvi, na wala sikuwa kwa kukuomba Rabb wangu, mwenye kukosa baraka.” [Maryam: 4]

 

Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) baada ya kufukuzwa na baba yake:

سَلَامٌ عَلَيْكَ ۖ سَأَسْتَغْفِرُ لَكَ رَبِّي ۖ إِنَّهُ كَانَ بِي حَفِيًّا ﴿٤٧﴾

 “Amani iwe juu yako. Nitakuombea maghfirah kwa Rabb wangu. Hakika Yeye daima kwangu ni Mwenye huruma sana.”

 

وَأَعْتَزِلُكُمْ وَمَا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَأَدْعُو رَبِّي عَسَىٰ أَلَّا أَكُونَ بِدُعَاءِ رَبِّي شَقِيًّا ﴿٤٨﴾

 “Na natengana nanyi na mnavyoviomba pasi na Allaah; na namuomba Rabb wangu asaa nisijekuwa kwa kumwomba Rabb wangu, mwenye kukosa baraka.” [Maryam: 47-48] 

 

 

 

11- Mwenye kuomba ana uhakika wa kutakabaliwa du’aa yake:

 

Licha ya umuhimu wote wa du’aa na fadhila zake, linalotia moyo zaidi ni kwamba lolote tumuombalo Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) tujue kwamba Analipokea na Atatutakabalia kwa njia moja au nyingine:

 

عَنْ جَابِرٍ (رضي الله عنه)  قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ يَقُولُ:  ((مَا مِنْ أَحَدٍ يَدْعُو بِدُعَاءٍ إلاَّ آتَاهُ اللَّهُ مَا سَأَلَ أَوْ كَفَّ عَنْهُ مِنْ السُّوءِ مِثْلَهُ مَا لَمْ يَدْعُ بِإِثْمٍ أَوْ قَطِيعَةِ رَحِمٍ))   

Kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakuna mtu aombaye du’aa ila Allaah Humpa Alichoomba au Akamupeusha kwayo shari kama hiyo, madamu haombi dhambi au kukata undugu)) [At-Tirmidhiy, Ahmad, Taz Swahiyh At-Tirimidhy (3381) na Swahiyh Al-Jaami’ (5678)

 

 

 

Share

05-Wewe Pekee Tunakuabudu: Adabu Za Kuomba Du'aa

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

05-Adabu Za Kuomba Du'aa

 

 

 Zifatazo ni adabu za kuomba du’aa na dalili zake:

 

 

1- Kutia Wudhuu  

 

Kutoka kwa Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba, wakati Abu ‘Aamir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliporushiwa mshale katika shingo yake alimuendea akamuomba amchopoe mshale. Akamchopoa kisha akamuomba amuendee Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili amuombee. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akachukua wudhuu, kisha akanyanyua mikono yake hadi zikaonekana kwapa zake, kisha akaomba:

((اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِعُبَيْدٍ أَبِي عَامِرٍ))

((Ee Allaah, Mghufurie ‘Ubayd Abiy ‘Aamir)) [Al-Bukhaariy (6383), Muslim (2498), Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake (7198)]

 

 

 

2- Kuelekea Qiblah

 

Imethibitika mara kadhaa kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  alikuwa akielekea Qiblah alipoomba du’aa; mfano alipoomba du’aa wakati wa Hajj; alipokuwa baina ya Swafaa na Marwah, baada ya kurusha vijiwe katika Jamaraat, katika Mash’aril-Haraam, au alipoomba dhidi ya makafiri katika vita vya Badr n.k.

 

 

 

3- Kuanza Kwa Kumtukuza Allaah Na Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

 

 

عن فَضَالَةَ بْنَ عُبَيْدٍ (رضي الله عنه) يَقُولُ: سَمِعَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) رَجُلاً يَدْعُو فِي صَلاَتِهِ فَلَمْ يُصَلِّ عَلَى النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ):  ((عَجِلَ هَذَا))  ثُمَّ دَعَاهُ فَقَالَ لَهُ أَوْ لِغَيْرِهِ: ((إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِتَحْمِيدِ اللَّهِ وَالثَّنَاءِ عَلَيْهِ ثُمَّ لْيُصَلِّ عَلَى النَّبِيِّ ثُمَّ لْيَدْعُ بَعْدُ بِمَا شَاءَ))  

Kutoka kwa Fadhwaalah bin ‘Ubayd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimsikia mtu akiomba katika du’aa yake bila ya kumswalia yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akasema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ameharakisha huyu)) kisha akamwita na kumwambia au kumwambia mwingine: ((Anapoomba mmoja wenu basi aanze kwa Kumhimidi Allaah, na kumtukuza kisha amswalie Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) halafu aombe anachotaka)) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ahmad]

 

Tunapoanza kuswali, tunaanza kusoma Suwratul-Faatihah ambayo ndani yake mna du’aa. Bila ya Suwrah hii tukufu Swalaah huwa haisihi. Tunaisoma mara kumi na saba kwa siku. Katika Suwrah hiyo, tunaanza kwanza kwa kumhimidi, kumsifu na kumtukuza Allaah Naye hutujibu hapo hapo, kisha tunaendelea kumuomba Atuongoze katika njia iliyonyooka. Imesimuliwa katika Hadiythul-Qudsiy:

 

 قال رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم): ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: قَسَمْتُ الصَّلاَةَ بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي نِصْفَيْنِ, وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ. فَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ: الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ,  قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: حَمِدَنِي عَبْدِي. وَإِذَا قَالَ: الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ, قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: أَثْنَى عَلَيَّ عَبْدِي. وَإِذَا قَالَ: مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ, قَالَ: مَجَّدَنِي عَبْدِي, فَإِذَا قَالَ: إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ, قَالَ: هَذَا بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ. فَإِذَا قَالَ: اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ ولاَ الضَّالِّينَ قَالَ: هَذَا لِعَبْدِي وَلِعَبْدِي مَا سَأَل))   

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Ta’aala Amesema:  Nimegawa Swalaah baina Yangu na mja Wangu sehemu mbili na mja Wangu atapata alichokiomba. Basi mja anaposema:  “Himidi zote Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu.”, Allaah Ta’aalaa Husema: “Mja Wangu amenisifu”. Mja akisema: " Mwingi wa Rahmah,  Mwenye kurehemu”, Allaah Husema: “Mja Wangu amenitukuza”. Mja akisema: "Mfalme wa siku ya malipo”, Allaah Husema: “Mja Wangu Ameniadhimisha". Mja akisema: "Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada”, [Husema]: "Hii ni baina Yangu na Mja Wangu, na Mja wangu atapata aliyoyaomba". Mja akisema: "Tuongoze njia iliyonyooka. Njia ya wale Uliowaneemesha, sio ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.”, [Husema] Yote haya ni ya Mja Wangu na Mja Wangu atapata aliyoyaomba)) [Muslim, Abu Daawuwd., At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy]

 

 

 

4- Kuinua Mikono

 

Hadiyth nyingi zimethibitisha kuwa Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  alipoomba du’aa alinyanyua mikono yake;, mfano alipoomba mvua alinyanyua mikono yake mpaka  kwapa zake zikaonekana, au alipoeleeka Qiblah na kuomba dhidi ya washirikina katika vita vya Badr mpaka joho lake likamuanguka kutoka mabegani mwake (Ar-Rahiyq Al-Makhtuwm). Pia alipokuwa akiomba du’aa katika ‘ibaadah za Hijjah mfano baina ya Swafaa na Marwah, au kila alipomaliza kurusha vijiwe katika Jamaraat na katika hali mbali mbali zilizothibiti katika Siyrah. Dalili nyingine ni Hadiyth ifuatayo:

 

عنْ سَلْمَانَ (رضي الله عنه) قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِنَّ رَبَّكُمْ تَبَارَكَ وَتَعَالَى حَيِيٌّ كَرِيمٌ يَسْتَحْيِي مِنْ عَبْدِهِ إِذَا رَفَعَ يَدَيْهِ إِلَيْهِ أَنْ يَرُدَّهُمَا صِفْرًا )) 

Kutoka kwa Salmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Rabb wenu Tabaaraka wa Ta’aalaa Yuhai na Mkarimu Anamstahi a mja Wake anapoinua mikono yake [kumuomba] Airudishe sifuri)) [bila ya kumjibu] [Abu Daawuwd na  ameipa daraja ya Swahiyh Shaykh Al-Albaaniy]   

 

Tanbihi: Haikuthibiti Katika Sunnah kunyanyua mikono kuomba du’aa baada ya Swalaah.

 

 

5- Kukiri Madhambi Na Kuomba Maghfirah:

 

Mfano wa Nabiy Yuwnus (‘alayhis-salaam) alipofanya kosa akamezwa na nyangumi alipomuomba Rabb wake kwa kukiri makosa yake kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَذَا النُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾

Na Dhan-Nuwn (Yuwnus) alipoondoka akiwa ameghadhibika, akadhani kwamba Hatutamdhikisha; akaita katika kiza kwamba: “Hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Subhaanak! Utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.”

 

فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُنجِي الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨٨﴾

Basi Tukamuitikia na Tukamuokoa kutokana na ghamu. Na hivyo ndivyo Tuwaokowavyo Waumini. [Al-Anbiyaa: 87-88]

 

Du’aa nyenginezo za kuomba maghfirah:   

 

 ‘Sayyidul-Istighfaar’ ni du’aa kuu ya kuomba maghfirah.

 

 عن شَدَّادُ بْنُ أَوْسٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((سَيِّدُ الإِسْتِغْفَارِ أَنْ تَقُولَ: اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي فَإِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ)) قَالَ:  ((وَمَنْ قَالَهَا مِنْ النَّهَارِ مُوقِنًا بِهَا فَمَاتَ مِنْ يَوْمِهِ قَبْلَ أَنْ يُمْسِيَ فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ وَمَنْ قَالَهَا مِنْ اللَّيْلِ وَهُوَ مُوقِنٌ بِهَا فَمَاتَ قَبْلَ أَنْ يُصْبِحَ فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ))

 

Kutoka kwa Shaddaad bin Aws (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sayyidul Istighfaar ni useme: “Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana ilahi (mungu apasaye kuabudiwa kwa haki) ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya  ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najikinga Kwako kutokana  na shari ya nilichokifanya, nakiri  Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unighufurie kwani hakuna mwingine wa kughufuria madhambi ila Wewe Akasema: ((Atakayesema mchana akiwa na yakini nayo, akafariki siku hiyo kabla kuingia jioni basi atakuwa mtu wa Jannah, na atakayesema usiku naye akiwa na yakini nayo akafariki kabla hajafika asubuhi basi yeye ni mtu wa Jannah))  [Al-Bukhaariy, Tirmidhy, An-Nasaaiy]

 

Pia:

 

عَنْ أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) أَنَّهُ قَالَ لِرَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:) "عَلِّمْنِي دُعَاءً أَدْعُو بِهِ فِي صَلاَتِي"  قَالَ: ((قُلْ اللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي ظُلْمًا كَثِيرًا وَلاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ فَاغْفِرْ لِي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ وَارْحَمْنِي إِنَّك أَنْتَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ))

Kutoka kwa Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Alimwambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “Nifunze du’aa niiombe katika Swalaah yangu.” Akasema: ((Sema, Ee Allaah hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu dhulma nyingi, na haghufurii madhambi ila Wewe, basi Nighufurie maghfira kutoka Kwako, na Unirehemu. Hakika Wewe ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu . [Al-Bukhaariy (8/168),  Muslim (4/2078) ]

 

 

 

6- Kukiri Neema Za Allaah

 

Kukumbuka neema za Allaah (Subhaanhu wa Ta’aalaa) kisha kuzikiri kwa moyo, ulimi na vitendo. Kufanya hivyo ni kujirudishia manufaa kwani kila mja anapomshukuru Rabb wake (’Azza wa Jalla) Humzidishia neema hizo. Anasema Allaah (Subhaanauu wa Ta’aalaa):

 

وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكُمْ لَئِن شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ

Na pindi Alipotangaza Rabb wenu: “Ikiwa mtashukuru, bila shaka Nitakuzidishieni (neema Zangu); [Ibraahiym: 7]

 

 

 

7- Kuomba Kwa Unyenyekevu, Khofu, Matumaini.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا ۚ إِنَّ رَحْمَتَ اللَّـهِ قَرِيبٌ مِّنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٦﴾

na muombeni kwa khofu na matumaini. Hakika rahmah ya Allaah iko karibu na wafanyao ihsaan. [Al-A’raaf: 56]

 

 

 

8- Kuomba Kwa Sauti Ndogo

 

Haipendekezi kuomba du’aa kwa sauti kubwa, kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni Mwenye Kusikia ya dhahiri na ya siri. Pia inazuia kufanya usumbufu na ghasia kwa wengine. Kuomba kwa siri pia kujiweka mbali na riyaa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ﴿٢٠٥﴾

Na mdhukuru Rabb wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu na si kwa jahara katika kauli asubuhi na jioni; na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika. [Al-A’raaf: 205]

 

 

Mafunzo kutoka Nabiy Zakariyyah (‘Alayhis-salaam) alipoomba kama ilivyotajwa katika Suwrat Maryam ambayo imeanza kwa:

كهيعص ﴿١﴾

Kaaf Haa Yaa ‘Ayyn Swaad. 

 

 

ذِكْرُ رَحْمَتِ رَبِّكَ عَبْدَهُ زَكَرِيَّا ﴿٢﴾

 (Huu ni) Ukumbusho wa rahmah ya Rabb wako kwa mja Wake Zakariyyaa.

 

 

إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ نِدَاءً خَفِيًّا ﴿٣﴾

Alipomwita Rabb wake mwito wa siri. [Maryam: 1-3]

 

 

 

Na dalili katika Hadiyth:

 

عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَكُنَّا إِذَا أَشْرَفْنَا عَلَى وَادٍ هَلَّلْنَا وَكَبَّرْنَا. ارْتَفَعَتْ أَصْوَاتُنَا فَقَالَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((يَا أَيُّهَا النَّاسُ ارْبَعُوا عَلَى أَنْفُسِكُمْ فَإِنَّكُمْ لاَ تَدْعُونَ أَصَمَّ ولاَ غَائِبًا إِنَّهُ مَعَكُمْ ، إِنَّهُ سَمِيعٌ قَرِيبٌ تَبَارَكَ اسْمُهُ وَتَعَالَى جَدُّهُ))

 

Amesimulia Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه): Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na tukawa kila tukipanda bonde, tunafanya tahliyl (Laa Ilaaha Illa-Allaah), na tunaleta takbiyr (Allaahu Akbar). Zikapanda sauti zetu, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Enyi watu, zihurumieni nafsi zenu, kwani hamumwombi kiziwi wala asiyekuwepo, hakika Yeye Yupo nanyi (kwa Ujuzi Wake), hakika Yeye Ni Mwenye Kusikia yote, Yupo Karibu, Limebarikika Jina Lake na Umetukuka Ujalali Wake.” [Al-Bukhaariy]

 

 

 

9- Kuomba Mara Tatu

 

Desturi iliyothibiti katika Sunnah kwenye du’aa mbali mbali na Adhkhaar ni kuomba mara tatu, na dalili mojawapo ni katika riwaya ndefu inayosema:

 

  “...وَكَانَ إِذَا دَعَا دَعَا ثَلاَثًا وَإِذَا سَأَلَ سَأَلَ ثَلاَثًا ثُمَّ قَالَ: ((اللَّهُمَّ عَلَيْكَ بِقُرَيْشٍ)) ثَلاَثَ مَرَّاتٍ...

“...na alikuwa anapoomba anaomba mara tatu, akiuliza anauliza mara tatu kisha akaomba: ((Ee Allaah, juu Yako Maquraysh)) mara tatu ...)) [Muslim]

 

 

 

10- Aanze Mtu Kujiombea Nafsi Yake Kwanza:

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amemuamrisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aanze kujiombea maghfirah.

 

وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ﴿١٩﴾

na omba maghfirah kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Allaah Anajua harakati zenu huku na kule na pahala penu pa kupumzikia. [Muhammad: 19]

 

Na katika Hadiyth:

 

عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ (رضي الله عنه)   أَنَّ "رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا ذَكَرَ أَحَدًا فَدَعَا لَهُ بَدَأَ بِنَفْسِهِ"

Kutoka kwa Ubayy bin Ka’b (Radhwiya Allaahu) kwamba “Alipotajwa mtu kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimuombea kwa kuanza  kujiombea mwenyewe kwanza” At-Tirmidhiy ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy [3385] na taz Swahiiyh Al-Jaami’ [4723]

 

Dalili kutoka kwa Manabii:

 

Nabiy Nuwh (‘Alayhis-salaam):

 

رَّبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًا﴿٢٨﴾

 “Rabb wangu! Nighufurie, na wazazi wangu wawili, na kila aliyeingia nyumbani mwangu mwenye kuamini, na Waumini wa kiume na Waumini wa kike, na wala Usiwazidishie madhalimu isipokuwa kuteketea kabisa. [Nuwh: 28]

 

 

Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam):

رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلَاةِ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاءِ﴿٤٠﴾

 “Rabb wangu! Nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swalaah na dhuria wangu. Rabb wetu! Nitakabalie du’aa yangu.”

رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾

 “Rabb wetu! Nighufurie na wazazi wangu wawili na Waumini Siku itakayosimama hesabu.” [Ibraahiym: 40-41]

 

Nabiy Muwsaa (‘Alayhis-salaam):

قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِأَخِي وَأَدْخِلْنَا فِي رَحْمَتِكَ ۖ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ﴿١٥١﴾

(Muwsaa) Akasema: “Rabb wangu! Nighufurie na kaka yangu, na Utuingize katika rahmah Yako. Nawe ni Mbora zaidi wa kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu.” [Al-A’raaf: 151]

 

 

Dalili kutoka Salafus-Swaalih (Wema waliotangulia)

 

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٠﴾

Na wale waliokuja baada yao wanasema: “Rabb wetu! Tughufurie na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini; Rabb wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu. [Al-Hashr:10]

 

 

 

11- Kuomba Jambo Likiwa Na Kheri 

 

Mfano mtu akiwa anaomba kupatiwa kazi aombe ile yenye kheri naye, au mwanamke akiomba kupatiwa mume, aombe mume wa kheri naye n.k. kwani mtu hawezi kujua lipi lenye kheri au shari naye. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢١٦﴾

Na asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni kheri kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui. [Al-Baqarah: 216]

 

 

 

12- Kusema "Aamiyn"

 

Anapomaliza mja du’aa yake, inapasa aseme ‘Aamiyn’ kwa maana: ‘Ee Rabb Nitakabalie’.  Kama vile tunavyomalizia Suwratul-Faatihah baada ya kuomba du’aa. Na kwa hivyo, imepokelewa kutoka kwa  ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

 ( إِنَّ الْيَهُودَ قَوْمٌ حُسَّدٌ ، وَهُمْ لَا يَحْسُدُونَا عَلَى شَيْءٍ كَمَا يَحْسُدُونَا عَلَى السَّلَامِ ، وَعَلَى آمِينَ  

 ((Hakika Mayahudi ni watu mahasid na hakuna jambo wanalotuhusudu kama kutuhusudu katika maamkizi na katika Aamiyn)) [Ibn Khuzaymah (574) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah (691)]

 

 

 

 

 

Share

06-Wewe Pekee Tunakuabudu: Yasiyopasa Katika Du’aa

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

06- Yasiyopasa Katika Du’aa

 

 

 

Baadhi ya yasiyopasa katika kuomba du’aa na dalili zake:

 

 

1- Kumwomba Asiyekuwa Allaah Ta’aalaa:

 

Haipasi kumkabili kiumbe kingine chochote kumuomba du’aa kwa kudhani kwamba kiumbe huyo ana uwezo wa kukidhi haja za mtu. Kufanya hivyo ni miongoni mwa shirki kubwa inayomtoa mtu nje ya Uislamu. Naye Ametuonya Anaposema:

 

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا﴿١٨﴾

Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah. [Al-Jinn: 18]

 

Pia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 

 

((إِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلْ اللَّهَ وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاللَّهِ))   

((Unapoomba basi muombe Allaah, na unapotaka msaada, basi taka msaada kwa Allaah))  [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]  

 

 

 

2- Kuharakiza Du’aa Itakabaliwe

 

Kwa maana mtu anapoona du’aa yake haikutakabaliwa akaanza kulalamika. Muislamu anapaswa kuwa na yaqiyn kuwa du’aa yake itatakabaliwa tu kwa njia moja au nyingine madamu amekwishamkabili Rabb wake kama alivyosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((يُسْتَجَابُ لإَحَدِكُمْ مَا لَمْ يَعْجَلْ يَقُولُ دَعَوْتُ فَلَمْ يُسْتَجَبْ لِي))

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli Wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atatakabaliwa mmoja wenu madamu hataharakiza akasema: “Nimeomba lakini sikutakabaliwa”)) [Al-Bukhaariy, Muslim,  Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy]

 

 Pia,

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) أَنَّهُ قَالَ: ((لاَ يَزَالُ يُسْتَجَابُ لِلْعَبْدِ مَا لَمْ يَدْعُ بِإِثْمٍ أَوْ قَطِيعَةِ رَحِمٍ مَا لَمْ يَسْتَعْجِلْ))  قِيلَ "يَا رَسُولَ اللَّهِ مَا الإِسْتِعْجَالُ؟" قَالَ: ((يَقُولُ قَدْ دَعَوْتُ وَقَدْ دَعَوْتُ فَلَمْ أَرَ يَسْتَجِيبُ لِي فَيَسْتَحْسِرُ عِنْدَ ذَلِكَ وَيَدَعُ الدُّعَاءَ))

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mja ataendelea kuitikiwa [du’aa yake] madamu hatoomba dhambi au kukata ukoo na madamu hatoharakiza)). Ikaulizwa: “Vipi kuharakiza”? Akasema: ((Aseme: “Nimeshaomba na kuomba lakini sikuona kuitikiwa”, akavunjikwa moyo akaacha kuomba)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

3- Kuomba Dhambi Au Kukata Undugu:

 

Hadiyth iliyotangulia juu inakataza jambo hili. Hali kadhaalika Hadiyth ifuatayo pia: 

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ (رضي الله عنه)  أَنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَدْعُو بِدَعْوَةٍ لَيْسَ فِيهَا إِثْمٌ وَلاَ قَطِيعَةُ رَحِمٍ إلاَّ أَعْطَاهُ اللَّهُ بِهَا إِحْدَى ثَلاَثٍ:  إِمَّا أَنْ تُعَجَّلَ لَهُ دَعْوَتُهُ وَإِمَّا أَنْ يَدَّخِرَهَا لَهُ فِي الأَخِرَةِ وَإِمَّا أَنْ يَصْرِفَ عَنْهُ مِنْ السُّوءِ مِثْلَهَا))  قَالُوا إِذًا نُكْثِرُ قَالَ: ((اللَّهُ أَكْثَرُ))

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna Muislamu atakayeoomba du’aa isiyokuwa ni dhambi wala kukata undugu isipokuwa Allaah Atampa mojawapo ya matatu: Ima Amharakizie du’aa yake, au Amuewekee akiba Akhera, au Amuepushe nayo ovu kama hilo)) Wakasema:  Basi tutazidisha [kuomba du’aa]. Akasema: ((Allaah Mwingi zaidi)) [wa kuongeza])). [Ahmad. Taz. Swahiyh At-Targhiyb (1633) na Swahiyh Al-Musnad (421)]

 

Mifano ya kuomba dhambi kusema: "Ee Allaah, nijaalie nichume mali nyingi japo ya haraam" au 'Ee Allaah, nijaalie nipende muziki na nihifadhi nyimbo nyingi” n.k. Ama kukata undugu,mfano kusema:  "Ee Allaah, mjaalie fulani awe muasi kwa wazazi wake na atengane nao" au "Ee Allaah, mjaalie fulani akhasimikiane na jamaa zake".

 

 

 

4- Kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Kwa Kumpa Khiari 

 

Hivyo haipasi kwani ni kuhusisha na majaaliwa na Qudra ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa mfano kusema: “Ee Allaah, Ukipenda nighufurie madhambi yangu” au: “Ee Allaah, Ukipenda nirehemu,” bali Muislamu anatakiwa awe na yaqiyn na yale anayoyaomba.

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لاَ يَقُولَنَّ أَحَدُكُمْ اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي إِنْ شِئْتَ, اللَّهُمَّ ارْحَمْنِي إِنْ شِئْتَ, لِيَعْزِمْ الْمَسْأَلَةَ فَإِنَّهُ لاَ مُكْرِهَ لَهُ))

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Asiseme mmoja wenu: “Ee Allaah, nighufurie Ukitaka, Ee Allaah, nirehemu Ukitaka”, bali awe na azma na  aliyoyaomba kwani hakuna wa kumlazimisha)) [Allaah kufanya Atakavyo] [Al-Bukhaariy, Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy]

 

 

 

 

5- Kuwekea Mipaka Rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

Haipasi kuwekea mipaka Rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwani Rahmah Yake ni pana, Anasema:

 وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ

Na rahmah Yangu imeenea kila kitu. [Al-A’raaf: 156]

 

na hakuna awezaye kuizuia kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

مَّا يَفْتَحِ اللَّـهُ لِلنَّاسِ مِن رَّحْمَةٍ فَلَا مُمْسِكَ لَهَا ۖ وَمَا يُمْسِكْ فَلَا مُرْسِلَ لَهُ مِن بَعْدِهِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢﴾

Rahmah yoyote Anayoifungua Allaah kwa watu, basi hakuna wa kuizuia, na Anayoizuia, basi hakuna wa kuipeleka baada Yake, Naye ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Faatwir: 2]

 

 

Mfano mtu asiombe "Ee Rabb! Niteremshie Rahmah Yako mimi na ahli yangu, lakini usimteremshie fulani”. Makatazo yamethibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

عن أبي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَامَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي صَلاَةٍ وَقُمْنَا مَعَهُ فَقَالَ أَعْرَابِيٌّ وَهُوَ فِي الصَّلاَةِ: "اللَّهُمَّ ارْحَمْنِي وَمُحَمَّدًا وَلاَ تَرْحَمْ مَعَنَا أَحَدًا" فَلَمَّا سَلَّمَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ لِلأَعْرَابِيِّ: (( لَقَدْ حَجَّرْتَ وَاسِعًا))  يُرِيدُ رَحْمَةَ اللَّهِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Alisimama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Swalaah, nasi tukasimama pamoja naye. Bedui mmoja akasema akiwa katika Swalaah: "Ee Allaah, nirehemu pamoja na Muhammad na wala Usimrehemu pamoja nasi yeyote mwengine”: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipotoa salaam kumaliza Swalaah akamwabia bedui: ((Kwa yakini umewekea mipaka jambo pana mno)) [akikusudia Rahmah ya Allaah] [Al-Bukhaariy, Abu Daawuwd, At-Tirmidhy, An-Nasaaiy]

 

 

 

6- Kupinduka Mipaka Katika Kuomba Du’aa

 

Amekataza Allaah (Subahaanu wa Ta’aalaa):

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٥٥﴾

Muombeni Rabb wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye Hapendi wenye kupindukia mipaka. [Al-A’raaf: 55]

 

Imaam As-Sa’diy (Rahimahu Allaah) amesema katika Tafsiyr yake inamanisha:

 

“Wapindukaji mipaka katika kila jambo, na mfano wa mja kumuomba Allaah mas-alah yasiyompasa, au kujikalifisha na kuzidisha kupita kiasi au kufikisha kupandisha sauti yake katika du’aa; haya yote yanaingia katika katakazo la uvukaji mipaka”.

 

Kuvuka mipaka kwa Mfano kuomba kubadilishwa shariy’ah za Allaah (Subhaanahuu wa Ta’aalaa) Alizozihukumu; kama yaliyoharamishwa kuwa yawe halali.  Au pia kuomba yasiyowezekana kama vile mfano wa walivyoomba Mayahudi kutaka kumwona Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) waziwazi, au Makafiri Quraysh walivyoomba kiteremshwe Kitabu kutoka mbinguni pamoja na Malaika wayaone hayo waziwazi.

 

Makatazo yamethibiti pia katika Hadiyth:

 

عن عبدَ اللَّهِ بنَ مُغفَّلٍ، سمعَ ابنَهُ يقولُ: اللَّهمَّ إنِّي أسألُكَ القَصرَ الأبيضَ، عن يمينِ الجنَّةِ إذا دخلتُها، فقالَ: أي بُنَيَّ، سلِ اللَّهَ الجنَّةَ، وتعوَّذ بِهِ منَ النَّارِ، فإنِّي سَمِعْتُ رسولَ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليهِ وسلَّمَ يقولُ: ((إنَّهُ سيَكونُ فيهذِهِ الأمَّةِ قومٌ يَعتدونَ في الطَّهورِ والدُّعاءِ))

Imetoka kwa ‘Abdullaah bin Mughaffal kwamba amemsikia mwanawe akiomba: “Ee Allaah, nakuomba qasri jeupe na kuliani mwa Jannah nitakapoingia”.  Akamwambia: “Ee mwanangu! Muombe Allaah Jannah na omba kinga Kwake ya Moto, kwani nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Watakuweko watu katika Ummah huu wakipinduka mipaka katika twahaarah na duaa)) [Abu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy, taz. Swahiyh Abiy Daawuwd (96) na Swahiyh Al-Jaami’ (2396)]

 

 

 

7- Kuomba Mauti

 

Muislamu anapofikwa na mitihani anapaswa kuwa mstahamilivu na kuridhika na majaaliwa ya Allaah hukuu aendelee kumuomba faraja. Haifai kutamani au kuomba mauti. Lakini pindi hali inapomfikisha kushindwa kuvumilia na kutamani mauti, aombe du’aa iliyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ:  ((لاَ يَتَمَنَّيَنَّ أَحَدُكُمْ الْمَوْتَ مِنْ ضُرٍّ أَصَابَهُ, فَإِنْ كَانَ لَا بُدَّ فَاعِلاً فَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ أَحْيِنِي مَا كَانَتْ الْحَيَاةُ خَيْرًا لِي وَتَوَفَّنِي إِذَا كَانَتْ الْوَفَاةُ خَيْرًا لِي))

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Asitamani mmoja wenu mauti kutokana na dhara ilomsibu. Akiwa hana budi kufanya, basi aseme: “Allaahumma Ahyiniy maa kaanat al-hayaatu khayran-liy, wa-tawaffaniy idhaa kaanat al-wafaatu khayran-liy - "Ee Allaah, nipe uhai ikiwa Unajua kwamba uhai ni bora kwangu, na nifishe ikiwa Unajua kuwa mauti ni bora kwangu "))[Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Pia mauti hayaombwi isipokuwa anapokhofia mtu fitnah ya kumharibia Dini yake kwa dalili ya du’aa ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

وَإِذَا أَرَدْتَ بِعِبَادِكَ فِتْنَةً فَاقْبِضْنِي إِلَيْكَ غَيْرَ مَفْتُون

((…Na Utakapokusudia kwa waja Wako fitnah, basi nifishe Kwako bila ya kufitiniwa)) [At-Tirmidhiy, taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3233)]

 

 

 

8- Kulaani Mtu Au Kitu

 

Muislamu haipasi kumuombea mwenzake laana hata akiwa ni mtendaji maasi: 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) أُتِيَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم) بِرَجُلٍ قَدْ شَرِبَ قَالَ: ((اضْرِبُوهُ)) قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ: فَمِنَّا الضَّارِبُ بِيَدِهِ وَالضَّارِبُ بِنَعْلِهِ وَالضَّارِبُ بِثَوْبِهِ, فَلَمَّا انْصَرَفَ قَالَ بَعْضُ الْقَوْمِ:  "أَخْزَاكَ اللَّهُ"  قَالَ: ((لاَ تَقُولُوا هَكَذَا لاَ تُعِينُوا عَلَيْهِ الشَّيْطَانَ))

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyekunywa pombe. Akasema ((Mpigeni)).Akasema Abuu Hurayrah: "Tukampiga kwa mikono yake, pigo kwa viatu vyake na pigo kwa nguo zake. Alipoondoka wakasema baadhi ya watu:  “Allaah Akuhizi [Akulaani]” Akasema: ((Msiseme hivi, msimsaidie shaytwaan dhidi yake)) [Al-Bukhaariy] na katika riwaaya ya Ahmad ameongeza kusema: ((lakini semeni: “Allaah Akurehemu.”))

 

Hali kadhalika haipasi kulaani wanyama hata wale wanaosumbua au kuleta madhara. Au pia kulaani wakati, mvua, upepo. Hadiyth kadhaa zimethibitisha katazo hili; mojawapo ni Hadiyth ifuatayo ambayo inatoa onyo kuwa mwenye kulaani kitu; laana humrudia mwenyewe:

 

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ ((رضي الله عنهما) أَنَّ رَجُلاً لَعَنَ الرِّيحَ عند رسول الله (صلى الله عليه وسلم) فَقَالَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لاَ تَلْعَنْهَا فَإِنَّهَا مَأْمُورَةٌ وَإِنَّهُ مَنْ لَعَنَ شَيْئًا لَيْسَ لَهُ بِأَهْلٍ رَجَعَتْ اللَّعْنَةُ عَلَيْهِ))

Kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba mtu alilaani upepo mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: ((Usiulaani kwani (huo upepo) umeamrishwa, na hakika mwenye kulaani kitu kisichostahiki inamrudia laana dhidi yake)) [At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd Swahiyh Abiy Daawuwd (4908)]

 

 

 

9- Kuwaombea Watoto Laana

 

Mzazi awe na tahadhari anapokuwa katika ghadhabu na mwanawe, asije kuteleza ulimi kwa kumuombea laana mwanawe, au kumuombea shari au kumtolea radhi kwa sababu; Kwanza: Du’aa ya mzazi hairudi kwa dalili ifuatayo:

 

عّنْ أَنسْ بِنْ ماَلِكْ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ): ((ثَلاَثُ دَعْواتِ لاَ تُرَدُّ: دَعْوَةُ الْوَالِدِ لِوَلَدِهِ، وَدَعْوَةُ الصَّائِم  وَدَعْوَةُ الْمُسَافَرَ))

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ((Du’aa za watatu hazirudishwi; du’aa ya mzazi kwa mwanawe, na du’aa ya mwenye kufunga swawm, na du’aa ya msafiri)) [Al-Bayhaqiy Swahiyh Al-Jaami’ (3032) na pia katika Silsilatu Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (1797)]

 

Pili: Ameonya wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  

 

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لاَ تَدْعُوا عَلَى أَنْفُسِكُمْ ولاَ تَدْعُوا عَلَى أَولاَدِكُمْ ))

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Msijiombee dhidi ya nafsi zenu wala msiombe dhidi ya watoto wenu)) [Muslim (3009), Abuu Daawuwd, taz. Swahiyh Abiy Daawuwd (1532) na Swahiyh Al-Jaami’ (7267)]

 

Inahitaji subira katika ghadhabu na kutokuazimia kulaani au kutoa radhi pindi mtoto anapovuka kumuasi mzazi. Ni bora kumchapa kuliko kumuombea laana kwani athari ya kumchapa itatoweka haraka kuliko athari ya kumlaani pindi du’aa itakapotakabaliwa na mtoto akadhurika na kisha yatabakia kuwa ni majuto!

 

Juu ya hivyo, kumuombea mtu laana ni kama kumuua. Amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

لَعْنُ المُؤْمِنِ كَقَتْلِه

((Kumlaani Muumini kama kumuua)) [Swahiyh Al-Jaami’y (710)]

 

 

 

10- Kuomba Yenye Manufaa Ya Dunia Pekee

 

Anapoomba Muislamu du’aa zake za manufaa ya kidunia daima aongoezee na du’aa za manufaa ya Aakhirah kwani hayo ndio yaliyo bora zaidi na ya kudumu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

فَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ﴿٢٠٠﴾

Kwani kuna baadhi ya watu wasemao: “Rabb wetu Tupe katika dunia;” naye katika Aakhirah hana sehemu yoyote.

 

  وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿٢٠١﴾

Na miongoni mwao kunawasemao: “Rabb wetu Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na Tukinge na adhabu ya moto.”

 

 أُولَـٰئِكَ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّمَّا كَسَبُوا ۚ وَاللَّـهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٢٠٢﴾

Hao watapata pato lao kutokana na waliyoyachuma, na Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu. [Al-Baqarah: 200-202]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ ۖ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ﴿٢٠﴾

Yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya Aakhirah Tunamzidishia katika mavuno yake; na yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya dunia, Tutampa humo, lakini Aakhirah hatokuwa na fungu lolote. [Ash-Shuwraa: 20]

 

 

 

11- Kutokujiombea Mwenyewe Na Badala Yake Kutegemea Watu Wengine Kukuombea Du’aa

 

Kutegemea watu wengine wakuombee du’aa kwa kujidharau mwenyewe kwa vile labda una kasoro fulani kama kukosa kuwa na ‘ilmu ya Dini au una madhambi kadhaa. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Hakutofautisha waja Wake kumuomba kati ya mtu aasi na mwenye taqwa Aliposema:

 

 وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ﴿١٨٦﴾

Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah: 186]

 

Inampasa hata mtu ambaye ni 'Aaswi (Mwenye kufanya maasi) ategemee Rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kuwa Atamtakabalia du’aa yake. Kwa hiyo haipasi kuitakidi kuwa du’aa ya mtu Swaalih (mwema) au Shaykh au Imaam au mtu mwenye hadhi fulani ndiyo itakayotakabaliwa. Hakuna ajuaye uhakika wa hayo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ ﴿٣٢﴾

Basi msizitakase nafsi zenu. Yeye Anamjua zaidi aliyekuwa na taqwa. [An-Najm: 32]

 

 

 

12- Kuomba Hadharani Kwa Sauti

 

Kuomba kwa sauti ni kinyume na miongoni mwa adabu za kuomba du’aa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٥٥﴾

Muombeni Rabb wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye Hapendi wenye kupindukia mipaka. [Al-A’raaf: 55]

 

 

 

13- Kuweka Nadhiri Kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Kutokumuomba Haja Nyingine 

 

Haipasi kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Atakabali haja kisha kuweka nadhiri kwamba pindi Akitakabali haja uliyoiomba, hutomkabili kumuomba jambo jingine kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ni Mkwasi wala hakipungui chochote katika ufalme Wake hata Akiitikia haja za viumbe Wake wote kama Anavyosema Mwenyewe (‘Azza wa Jalla) katika Hadiyth Al-Qudsiy:

 

 ...يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجنَّكُمْ قاموا في صَعِيدٍ وَاحِدٍ، فَسَأَلُوني، فأَعْطَيْتُ كلَّ واحدٍ مَسْأَلَتَهُ ما نَقَصَ ذلك مِمَّا عِنْدِي إلا كما يَنْقُصُ الْمِخْيَطُ إذا أُدْخِلَ الْبَحْرَ

((…Enyi waja Wangu ingelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi mkasimama pahala pamoja na mkaniomba, na Nikawapa kila mmoja alichoomba, haitonipunguzia katika nilicho Nacho zaidi kuliko sindano inavyopunguza bahari inapochovywa. [Muslim]

 

Na ni Mkarimu Humruzuku Amtakaye bila ya kipimo, Anasema:

 

وَاللَّـهُ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢١٢﴾

Na Allaah Humruzuku Amtakaye bila ya hesabu. [Al-Baqarah: 212]

 

 

 

 

 

Share

07-Wewe Pekee Tunakuabudu: Yanayokubalika Katika Du’aa

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

07- Yanayokubalika Katika Du’aa

 

 

Baadhi ya yanayokubalika katika kuomba du’aa na dalili zake:

 

 

1- Kuzidisha Du’aa

 

Inakubaliwa kuomba du’aa kwa wingi kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni Mkarimu mno na Mwingi vipawa, fadhila na kutunuku. Dalili ni Hadiyth ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘Anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

((إذَا سَألَ أحَدَكَمُ فَلْيُكْثِر، فَإنَّمَا يَسْألُ رَبَّهُ))

((Anapoomba mmoja wenu basi azidishe [du’aa] kwani anamuomba Rabb wake)) [Ibn Hibbaan - Swahiyh Al-Jaami’ (591)]

 

Pia katika riwaayah nyingine Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa):

 

(( إِذَا تَمَنَّى أحَدَكَمُ فَلْيُكْثِر، فَإنَّمَا يَسْألُ رَبَّهُ))

((Atakapotamani mmoja wenu basi azidishe [du’aa] kwani anamuomba Rabb wake)) [Atw-Twabaraaniy - Swahiyh Al-Jaami’ (437)]

 

 

 

2- Kuangaza Juu Wakati Wa Kuomba Du’aa

 

‘Ulamaa wamekubaliana kwamba inakubalika kuangaza juu wakati wa kuomba du’aa anapokuwa mtu nje ya Swalaah. Dalili mojawapo ni pale alipokuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiaga dunia akanyanyua macho yake kutazama juu na kusema:

 

((الرَّفِيقِ الأَعْلَى فِي الرَّفِيقِ الْأَعْلَى))

(([Niwe na ] Rafiki wa juu, kwa rafiki wa juu)) [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad katika riwaaya mbali mbali]

 

Pia katika kisa cha Miqdaad (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuhusu kinywaji cha maziwa alichokunywa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya kujua kwamba kinatoka kwake. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipofika Msikitini na kumaliza kuswali alikiendea kinywaji akanywa kisha akainua kichwa chake kuangaza juu na kuomba:

 

((اللَّهُمَّ أَطْعِمْ مَنْ أَطْعَمَنِي وَأَسْقِ مَنْ أَسْقَانِي))

((Ee Allaah, mlishe aliyenilisha, na mnywishe aliyeninywesha)) [Muslim na Swahiyh Muslim (2055)]

 

Pia,

 

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ (رضي الله عنهما) قَالَ: رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) جَالِسًا عِنْدَ الرُّكْنِ،  فَرَفَعَ بَصَرَهُ إِلَى السَّمَاءِ فَضَحِكَ، فَقَالَ: ((لَعَنَ اللَّهُ الْيَهُودَ ثَلاَثاً، إِنَّ اللَّهَ حَرَّمَ عَلَيْهِمْ الشُّحُومَ فَبَاعُوهَا، وَأَكَلُوا أَثْمَانَهَا، وَإِنَّ اللَّهَ إِذَا حَرَّمَ عَلَى قَوْمٍ أَكْلَ شَيْءٍ حَرَّمَ عَلَيْهِمْ ثَمَنَهُ))

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa ameketi pembeni akanyanyua macho yake mbinguni akacheka kisha akasema: ((Allaah Awalaani Mayahudi,  (mara tatu), hakika Allaah  Amewaharamishia shahamu  wakaiuza kisha wakala thamani yake. Na hakika Allaah Anapoharamisha kwa watu kula kitu Ameharamisha pia thamani yake)) [Abuu Daawuwd na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (3488)]

 

Lakini katika Swalaah imekatazwa kuangaza juu kwa dalili kadhaa mojawapo ifuatayo:  

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لَيَنْتَهِيَنَّ أَقْوَامٌ عَنْ رَفْعِهِمْ أَبْصَارَهُمْ عِنْدَ الدُّعَاءِ فِي الصّلاَةِ إِلَى السَّمَاءِ أَوْ لَتُخْطَفَنَّ أَبْصَارُهُمْ))

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Watu lazima waache kutazama juu mbinguni katika Swalah au macho yao yatanyofolewa)) [Muslim, An-Nasaaiy ameisahihisha Al-Albanaiy katika Swahiyh An-Nasaaiy (1275), Swahiyh Al-Jaami’ (5479)

 

 

3- Kuwaombea Wasio Waislamu 

 

Inafaa kuwaombea wasio Waislamu du’aa nzuri au mbaya kwa kutegemea na hali au sababu zake. Mfano inafaa kuwaombea wazazi hidaaya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Awaongoze katika Uislamu. Hadiyth kadhaa zimethibiti, mfano zifuatazo:

 

Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba alimuomba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amuombee mama yake hidaaya aingie Uislamu.

 

كُنْتُ أَدْعُو أُمِّي إِلَى الإسلام وَهِيَ مُشْرِكَةٌ، فَدَعَوْتُهَا يَوْمًا فَأَسْمَعَتْنِي فِي رَسُولِ اللَّهِ  صلى الله عليه وسلم مَا أَكْرَهُ، فَأَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَأَنَا أَبْكِى قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي كُنْتُ أَدْعُو أُمِّي إِلَى الإِسْلاَمِ فَتَأْبَى عَلَيَّ فَدَعَوْتُهَا الْيَوْمَ فَأَسْمَعَتْنِي فِيكَ مَا أَكْرَهُ، فَادْعُ اللَّهَ أَنْ يَهْدِىَ أُمَّ أَبِي هُرَيْرَةَ ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((اللَّهُمَّ اهْدِ أُمَّ أَبِي هُرَيْرَةَ)) فَخَرَجْتُ مُسْتَبْشِرًا بِدَعْوَةِ نَبِيِّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم، فَلَمَّا جِئْتُ فَصِرْتُ إِلَى الْبَابِ فَإِذَا هُوَ مُجَافٌ، فَسَمِعَتْ أُمِّي خَشْفَ قَدَمَيَّ فَقَالَتْ: مَكَانَكَ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ! وَسَمِعْتُ خَضْخَضَةَ الْمَاءِ قَالَ: فَاغْتَسَلَتْ وَلَبِسَتْ دِرْعَهَا وَعَجِلَتْ عَنْ خِمَارِهَا فَفَتَحَتِ الْبَابَ ثُمَّ قَالَتْ: يَا أَبَا هُرَيْرَةَ ، أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، قَالَ: فَرَجَعْتُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَأَتَيْتُهُ وَأَنَا أَبْكِي مِنَ الْفَرَحِ ، قَالَ: قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَبْشِرْ! قَدِ اسْتَجَابَ اللَّهُ دَعْوَتَكَ وَهَدَى أُمَّ أَبِى هُرَيْرَةَ! فَحَمِدَ اللَّهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ وَقَالَ خَيْرًا

“Nilikuwa namlingania mama yangu ambaye alikuwa mshirikina, ili aingie Uislamu. Siku moja nilipokuwa namlingania akanifanya nisikie (aliyotamka maovu) kuhusu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo nilichukia. Nikamwendea huku nikilia. Nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika nilikuwa namlingania mama yangu, lakini leo kanifanya nisikie aliyoyasema kuhusu wewe ambayo nimeyachukia, basi muombe Allaah Amhidi mama wa Abiy Hurayrah”. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuombea: ((Ee Allaah, Mhidi mama yake Abuu Hurayrah)). Nikatoka nikiwa na furaha kwa du’aa ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nilipofika mlangoni nilikuta umefungwa, na mama yangu aliposikia sauti za nyayo zangu, akasema: “Bakia hapo hapo ee Abuu Hurayrah!. Nikasikia mmwagiko wa maji, alipomaliza kuoga na kuvaa nguo yake, akaharakiza kuvaa khimaar yake, akaja kufungua mlango akasema: “Ash-hadu allaa ilaaha illa Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘abduhu wa Rasuwluhu – nashuhudia kwamba hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake”.  Hapo nikarudi kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huku nikilia kwa furaha”. “Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Nakubashiria, Allaah Ameshatakabali du’aa yako na Amemhidi Mama wa Abuu Hurayrah. Akamhimidi Allaah na akamtukuza kisha akasema ya khayr”. [Muslim (4/1938)] 

 

Vile vile pale Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipoomba mmoja kati ya Maquraysh wawili aingie Uislamu.

 

اللهم أَعِزَّ الإسلامَ بأَحَبِّ هذين الرجُلَيْنِ إليك بأبي جهلٍ أو بعمرَ بنِ الخطابِ قال وكان أَحَبَّهُما إليه عمرُ

((Ee Allaah, utie nguvu Uislamu kwa mmojawapo Umpendaye zaidi; Abuu Jahl au ‘Umar bin Al-Khatwaab. Akawa aliyependwa zaidi kati yao ni ‘Umar bin Al-Khattwaab)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3681)]

 

Pia Imaam Al-Bukhaariy katika mlango wa: “Kuwaombea du’aa washirikina”, Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

 

قدِم طُفَيلُ بنُ عمرٍو الدَّوسِيُّ وأصحابُه، على النبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم فقالوا: يا رسولَ اللهِ، إنَّ دَوسًا عصَتْ وأبَتْ، فادْعُ اللهَ عليها، فقيل: هلَكَتْ دَوسٌ، قال: ((اللهمَّ اهدِ دَوسًا وأَتِ بهم))

Atw-Twufayl ibn ‘Amr Ad-Dawsiyy na wenzake walimwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakasema: “(Kabila la) Daws wameasi na wamekanusha (Uislamu). Basi waombee dhidi yao kwa Allaah”. Ikasemwa: “Wameangamia Daws!”  (Lakini Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Akaomba: ((Ee Allaah wahidi Ad-Daws na walete hapa.)) [Al-Bukhaariy (2937), Muslim 2524)]

 

Ama kuhusu kuwaombea Rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) kauli iliyo na nguvu kabisa ya ‘Ulamaa ni kwamba haifai kuwaombea wasio Waislamu Rahmah, na dalili ni Hadiyth ifuatayo ya Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

 

كان اليهودُ يتعاطسون عندَ النبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ يرجونَ أنْ يقولَ لهم يرحَمُكم اللهُ فيقولُ يَهْدِيكم اللهُ ، ويُصْلِحُ بالَكُمْ

Mayahudi walikuwa wakipiga chafya (wakichemua) mbele ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakitaraji awaambie: Yarhamukumu-Allaah (Allaah Akurehemuni) lakini husema: ((Yahdiykumu-Allaahu wa Yuswlihu Baalakum (Akuongozeni Allaah na Akutengenezeeni mambo yenu)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (2739)]

 

Pia haifai kuwaombea maghfirah kwa kauli iliyo na nguvu kabisa baina ya ‘Ulamaa.

 

Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema: “Kuwaombea makafiri maghfirah hairuhusiwi kutokana na dalili za Qur-aan na Sunnah and Ijmaa’a ya Ulamaa” [Majmuw’ Al-Fataawaa (12/489)]

 

Na wakiwa wameshafariki haipasi kuwaombea jema lolote. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amekataza hayo:

 

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ﴿١١٣﴾

Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa moto uwakao vikali mno.

 

 

وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ ﴿١١٤﴾

Na haikuwa Ibraahiym kumuombea maghfirah baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allaah, alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym ni mwenye huruma mno na mvumilivu. [At-Tawbah: 113- 114]

 

 

Pia:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اسْتَأْذَنْتُ رَبِّي أَنْ أَسْتَغْفِرَ لأُمِّي فَلَمْ يَأْذَنْ لِي، وَاسْتَأْذَنْتُهُ أَنْ أَزُورَ قَبْرَهَا فَأَذِنَ لِي))

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nilimuomba idhini Rabb wangu nimuombee maghfirah mama yangu, Hakunipa idhini. Nikaomba idhini kuzuru kaburi lake Akanipa idhini.)) [Muslim (976)]

 

Imaam An-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema: “Kumswalia kafiri Swalaah ya janaazah au kumuombea maghfirah ni haram kutokana na nukuu za Qur-aan na Ijmaa’a ya ‘Ulamaa” [Al-Majmuw’ (5/19)]

 

 

 

4- Kuomba Du’aa Jambo Kubwa Na Dogo La Manufaa ya Dunia

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema: “Hakuna ubaya kuomba jambo linalohusiana na mambo ya kidunia mfano mtu aseme: “Ee Allaah niruzuku nyumba pana”. Au “Ee Allaah niruzuku mke mzuri”. Au, “Ee Allaah, niruzuku mali nyingi”. Au, “Ee Allaah niruzuku gari zuri”. Hivyo kwa sababu du’aa ni ‘ibaadah hata kama ni kuhusu mambo ya dunia, kwani binaadamu hana kimbilio isipokuwa kwa Allaah”. [Ash-Sharh Al-Mumti’ (3/284)] 

 

 

 

Share

08-Wewe Pekee Tunakuabudu: Sababu Za Kutakabaliwa Du’aa

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

08- Sababu Za Kutakabaliwa Du’aa

 

 

 

 

1- Kumwabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Pekee, Na Kumwomba Kwa Ikhlaasw

 

Sababu kuu ya mja kutakabaliwa du’aa ni kuwa na ikhlaasw na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kumtegemea Yeye Pekee, na kuamini kwamba hakuna mwengine atakayepokea du’aa. Kila inapozidi ikhlaasw ndipo huongezeka matumaini ya kutakabaliwa du’aa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

هُوَ الْحَيُّ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۗ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٦٥﴾

Yeye Ndiye Aliye hai daima hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye; basi muombeni Yeye wenye kumtakasia Dini. AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu. [Ghaafir: 65]

 

 

 

2- Kuanza Kwa Thanaa Mwanzo Na Mwisho wa Du’aa Na Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

Thanaa maana yake ni: kumtukuza, kumsifu na kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

Kufanya hivyo  ni sababu mojawapo ya sababu kuu ya kukubaliwa du’aa kwa sababu bila ya kufanya hivyo du’aa huwa haifiki mbinguni kwa dalili:

 

عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ (رضي الله عنه)  قَالَ: "إِنَّ الدُّعَاءَ مَوْقُوفٌ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ لاَ يَصْعَدُ مِنْهُ شَيْءٌ حَتَّى تُصَلِّيَ عَلَى نَبِيِّكَ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)"

Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu):  “Hakika du’aa inasimama baina ya mbingu na ardhi haipandi masafa yoyote mpaka umswalie Nabiy wako (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)." [Swahiyh At-Tirmidhiy (486), Swahiyh At-Targhiyb (1676)]

 

 

 

3- Kutumia Wasiylah

 

Kujikurubisha kwanza kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kabla ya kuanza kuomba haja, kwa tawassul zilizothibiti katika Shariy’ah. na si zile za shirki. (Mlango wake utafuatia)

 

 

 

4- Kuwa Na Matumaini, Unyenyekevu Na Kuuhudhurisha Moyo Kwa Allaah (‘Azza wa Jalla)

 

‘Ibaadah zote zinahitaji unyenyekevu wa mwili, akili na moyo ndipo ‘ibaadah hiyo inapokuwa imemridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

  

Vipi mtu amkabili Rabb kwa haja kisha mawazo na akili yake iwe kwingine? Unapomuomba binaadamu mwenzio unamkabili kwa adabu na heshima na upole, na akili yote imo katika kutegemea akupe unachokihitaji kwake, seuze unapomkabili Mwenye uwezo pekee wa kukidhi haja zako?  

 

Hivyo basi usiwe mwenye kughafilika katika kuomba du’aa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na dalili ni: 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ادْعُوا اللَّهَ وَأَنْتُمْ مُوقِنُونَ بِالإِجَابَةِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ لاَ يَسْتَجِيبُ دُعَاءً مِنْ قَلْبٍ غَافِلٍ لاَهٍ))

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muombeni Allaah huku mkiwa mna yakini kujibiwa, na jueni kwamba Allaah Hatakabali du’aa inayotoka katika moyo ulioghafilika au usiojali)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3479), Swahiyh Al-Jaami’ *245), Swahiyh At-Targhiyb (1653)]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٥٥﴾

Muombeni Rabb wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye Hapendi wenye kupindukia mipaka. [Al-A’raaf: 55]

 

 

 

5- Kuwa Na Dhana Nzuri Na Yakini Na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)

 

Inapasa kuwa na dhana nzuri kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ipate du’aa kutakabaliwa kama Anavyoahidi katika Hadiyth Al-Qudsiy:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم): ((إِنَّ اللَّهَ يَقُولُ أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي وَأَنَا مَعَهُ إِذَا دَعَانِي))

Imepokelewa kutoka  kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Anasema: Mimi Nipo pamoja na mja anaponidhania [dhana nzuri], Nami Nipo naye anaponiomba)) [Muslim]

 

Faida ziada za kuwa na dhana nzuri kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwamba mja anapotaka kufanya jambo basi Allaah (Subahanau wa Ta’aalaa) Humfanyia  wepesi kufikia atakacho kwa dalili:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ (( يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى: أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي وَأَنَا مَعَهُ إِذَا ذَكَرَنِي، فَإِنْ ذَكَرَنِي فِي نَفْسِهِ ذَكَرْتُهُ فِي نَفْسِي ، وَإِنْ ذَكَرَنِي فِي مَلَإٍ ذَكَرْتُهُ فِي مَلَإٍ خَيْرٍ مِنْهُمْ ، وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ بِشِبْرٍ تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعًا، وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ ذِرَاعًا تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ بَاعًا، وَإِنْ أَتَانِي يَمْشِي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً)) البخاري، مسلم، الترمذي وابن ماجه

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Allaah Ta’aalaa, Anasema: Mimi ni vile mja Wangu anavyonidhania. Niko pamoja naye Anaponikumbuka katika nafsi yake, Ninamkumbuka katika nafsi Yangu, anaponikumbuka katika hadhara, Ninamkumbuka katika hadhara bora zaidi. Na anaponikaribia shibiri Ninamkaribia dhiraa; anaponikaribia dhiraa, Ninamkaribia pima, anaponijia kwa mwendo (wa kawaida) ninamjia mbio)) [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]

 

Litakaloweza kumsaidia mja kuwa na dhanna nzuri na kuwa na yakini kwa Rabb wake ni kuzingatia Utukufu Wake, Ufalme Wake wa mbingu na ardhi, Ahadi Zake, Majina Yake Mazuri na Sifa Zake na zaidi katika du’aa kuzingatia Ukarimu na Fadhila Zake. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):     

 

لِيَجْزِيَهُمُ اللَّـهُ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۗ وَاللَّـهُ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٨﴾

Ili Allaah Awalipe mazuri zaidi kutokana na yale waliyoyatenda, na Awazidishie katika fadhila Zake. Na Allaah Humruzuku Amtakaye bila ya hesabu. [An-Nuwr: 38]

 

 

Kama vile Maswahaba watatu ambao Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwagomea kwa muda mrefu, wakawa katika dhiki kubwa lakini walimwekea dhana nzuri Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) wakatambua kuwa hakuna kimbilio ila kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Pekee ilivyothibiti katika Qur-aan Aliposema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١١٧﴾

Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Muhajirina na Answaar ambao wamemfuata (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki baada ya nyoyo za kundi miongoni mwao zilikaribia   kuelemea mbali na haki Akapokea tawbah yao. Hakika Yeye kwao ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.

 

 

وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّىٰ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوا أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ اللَّـهِ إِلَّا إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١١٨﴾

Na (Akapokea tawbah) ya wale watatu waliobaki nyuma (wakajuta mno) mpaka ardhi ikadhikika kwao juu ya kuwa ni pana na zikadhikika nafsi zao, na wakatambua kwamba hakuna pa kumkimbia Allaah isipokuwa kuelekea Kwake; kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao, ili watubie. Hakika Allaah Yeye Ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu. [At-Tawbah: 117-118]

 

Amesema Abul-‘Abbaas Al-Qurtwubi katika ‘Al-Mafham’: “Ina maana kuwa na dhana katika kutakabaliwa du’aa na dhana ya kutakabaliwa tawbah, na dhana ya maghfirah katika istighfaar, na dhana ya kutabaliwa 'amali wakati wa kuzitenda kwa sharti ya kuambatanisha kusadiki ahadi Zake na wingi wa fadhila Zake”.

 

 

 

6- Kuomba Du’aa Kila Mara Katika Hali Ya Raha Na Shida   

 

Hadiyth ya Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy, Abuu Hurayrah na Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhum)

 

تعرَّفْ إلى اللهِ في الرَّخاءِ يعرفُك في الشدَّةِ

((Mtambue [mkumbuke] Allaah wakati wa raha Akukumbuke katika shida))  [Swahiyh Al-Jaami’(2961)]

 

Hivyo ndivyo ipasavyo, kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika kila hali. Amewataja wafanyao kinyume chake; Anasema:

 

وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَىٰ بِجَانِبِهِ وَإِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ فَذُو دُعَاءٍ عَرِيضٍ﴿٥١﴾

Na Tunapomneemesha insani hukengeuka na kujitenga upande. Na inapomgusa shari, basi mara huwa mwenye du’aa refu refu. [Fusw-swilat: 51]

 

Na Anasema pia Allaah ('Azza wa Jalla):

وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ الضُّرُّ دَعَانَا لِجَنبِهِ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَائِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَا إِلَىٰ ضُرٍّ مَّسَّهُ ۚكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٢﴾

Na inapomgusa insani dhara hutuomba anapolala ubavu, au anapokaa au kusimama. Tunapomuondolea dhara, hupita kama kwamba hakutuomba dhara iliyomgusa. Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapindukao mipaka yale waliyokuwa wakiyatenda. [Yuwnus: 12]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ ضُرٌّ دَعَا رَبَّهُ مُنِيبًا إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا خَوَّلَهُ نِعْمَةً مِّنْهُ نَسِيَ مَا كَانَ يَدْعُو إِلَيْهِ مِن قَبْلُ

Na inapomgusa insani dhara, humwomba Rabb wake akirudiarudia kutubia Kwake, kisha Akimruzuku neema kutoka Kwake, husahau yale aliyokuwa akimwomba kabla, [Az-Zumar: 8]

 

 

 

7- Kuwa Na Iymaan na Taqwa

 

Kuwa na taqwa kwa maana; kumkumbuka Allaah na kumkhofu Allaah katika kila jambo atendalo binaadamu; ikiwa ni jambo ovu, basi kujiepusha nalo na ikiwa ni la khayr akimbilie kulitenda, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّـهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ ﴿٢٧﴾

Akasema: “Hakika Allaah Anatakabalia wenye taqwa.” [Al-Maaidah: 27]

 

Na Anasema Subhaanahu wa Ta’aalaa:

وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ

Na lau kama watu wa miji wangeliamimi na wakawa na taqwa, bila ya shaka Tungeliwafungulia baraka kutoka mbinguni na ardhini, [Al-A’raaf: 96]

 

 

 

8- Kutenda ‘Amali Nyingi Za Khayr

 

Nabiy Zakariyyaa (‘Alayhis-Salaam) alitakabaliwa du’aa yake kuomba mtoto akiwa na umri mkubwa kwa kuwa sababu mojawapo ilikuwa ni kuharakiza kutenda amali za khayr. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَزَكَرِيَّا إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ ﴿٨٩﴾

Na Zakariyyaa alipomwita Rabb wake: “Rabb wangu! Usiniache pekee; Nawe Ndiye Mbora wa wenye kurithi.”

 

 

فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَوَهَبْنَا لَهُ يَحْيَىٰ وَأَصْلَحْنَا لَهُ زَوْجَهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ ﴿٩٠﴾

Basi Tukamuitikia na Tukamtunukia Yahyaa, na Tukamtengenezea mke wake. Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri, na wakituomba kwa raghba na khofu, na walikuwa wenye kutunyenyekea. [Al-Anbiyaa: 89-90]

 

 

9- Kuzidisha ‘Amali Za Nawaafil (Sunnah Za Ziada)

 

Kila mja anapozidisha ‘amali za Sunnah baada ya kutimiza fardhi zake, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Humtakabalia du’aa zake:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِنَّ اللَّهَ قَالَ: مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ،  وَمَا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ ،  فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لأُعْطِيَنَّهُ ، وَلَئِنْ اسْتَعَاذَنِي لأُعِيذَنَّهُ، وَمَا تَرَدَّدْتُ عَنْ شَيْءٍ أَنَا فَاعِلُهُ تَرَدُّدِي عَنْ نَفْسِ الْمُؤْمِنِ يَكْرَهُ الْمَوْتَ وَأَنَا أَكْرَهُ مَسَاءَتَهُ))  

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Amesema: Yeyote yule atakayefanya uadui kwa walii Wangu (kipenzi changu) Nitatangaza vita dhidi yake. Mja Wangu hanikaribii na kitu chochote Ninachokipenda kama ‘amali nilizomfaridhishia, na mja Wangu huzidi kunikaribia kwa ‘amali njema za Sunnah ili nimpende. Ninapompenda, huwa masikio yake yanayosikilizia, macho yake anayoonea, mikono yake anayoshikia, miguu yake anayotembelea nayo. Na kama angeniomba kitu bila shaka ningempa. Na kama angeniomba himaya bila shaka ningelimkinga, na Sisiti juu ya kitu chochote kama ninavyosita [kuichukua] roho ya mja Wangu Muumin, anachukia mauti nami Nachukia kumfanyia ubaya)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

10- Kuwaombea Waislamu

 

Muislamu ampendelee nduguye Muislamu khayr kwa kumuombea. Na khasa pale mwenziwe anapokuwa ameneemeshwa kwa neema fulani, basi ni khayr kumuombea Allaah Ambariki. Kufanya hivi ni bora kuliko kumuonea wivu, kwa sababu kumuonea wivu hakutomfaa kitu bali kutazidi kumnyima yeye khayr, kwa sababu kumuombea Muislamu mwenziwe kwa siri, kuna faida ya kuwa Malaika huitikia du’aa na humuombea muombaji apate khayr na barakah kama hizo anazomuombea mwenziwe kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ صَفْوَانَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ صَفْوَانَ (رضي الله عنه)  قَالَ وَكَانَتْ تَحْتَهُ ابْنَةُ أَبِي الدَّرْدَاءِ فَأَتَاهَا فَوَجَدَ أُمَّ الدَّرْدَاءِ وَلَمْ يَجِدْ أَبَا الدَّرْدَاءِ, فَقَالَتْ لَهُ: "تُرِيدُ الْحَجَّ الْعَامَ؟" قَالَ" "نَعَمْ" قَالَتْ: "فَادْعُ اللَّهَ لَنَا بِخَيْرٍ فَإِنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) كَانَ يَقُولُ: ((دَعْوَةُ الْمَرْءِ مُسْتَجَابَةٌ لإَخِيهِ بِظَهْرِ الْغَيْبِ عِنْدَ رَأْسِهِ مَلَكٌ يُؤَمِّنُ عَلَى دُعَائِهِ كُلَّمَا دَعَا لَهُ بِخَيْرٍ قَالَ آمِينَ وَلَكَ بِمِثْلِهِ))  

Imepokelewa kutoka kwa Swafwaan bin ‘Abdillaah bin Swafwaan amesema:  alimwendea Abu Dardaa akawa hakumkuta bali alimkuta Ummu Dardaa ambaye alisema: “Je, unataka kuhiji mwaka huu?” Akasema: “Ndio”. Akasema: “Basi tuombee kwa Allaah khayr kwani Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema: ((Du’aa ya mtu anayomuombea nduguye kwa siri huweko Malaika juu ya kichwa chake akiitikia du’aa yake kila anapomuombea khayr, husema ‘Aamiyn nawe pia upate sawa nayo’)) [Ibn Maajah (2895), Asw-Swahiyhah (1339), Na riwayaah nyenginezo;  Swahiyh Al-Jaami’ (3381), Swahiyh Ibn Maajah (2358), Swahiyh Abiy Daawuwd (1534)]

 

 

 

11- Kuomba Maghfirah Kwa Wingi

 

Kuomba maghfirah kwa wingi kunampatia Muislamu faida kadhaa kwa dalili zifuatazo:

 

وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَاعًا حَسَنًا إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَهُ ۖ 

Na kwamba: “Mwombeni Rabb wenu maghfirah kisha tubuni Kwake, Atakustarehesheni starehe nzuri mpaka muda maalumu uliokadiriwa; na Atampa kila mwenye fadhila, fadhila Zake.  [Huwd: 3]

 

 وَيَا قَوْمِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمْ

 “Na enyi kaumu yangu!  Mwombeni maghfirah Rabb wenu, kisha tubieni Kwake, Atakuleteeni mbingu zenye kunyesha mvua tele ya kumiminika na Atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu [Huwd: 52]

 

فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُّجِيبٌ﴿٦١﴾

 basi mwombeni maghfirah, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu ni Yuko Karibu kwa ujuzi Wake, Mwenye kuitikia.” [Huwd: 61]

 

 

 Imaam Al-Qurtwuby katika Tafsiyr yake ya Suwrat Nuwh amesimulia:

 

“Katika Aayah hizi (za Suwrat Nuwh) na ambazo ziko katika (Huwd) ni dalili kwamba Istighfaar inateremsha kwayo rizki na mvua.

 

Ash-Sha‘biyy (Rahimahu Allaah) amesema:

 “Umar alitoka kuomba mvua, akawa hazidishi zaidi ya Istighfaar hadi aliporejea, kisha ikanyesha mvua. Walionyeshewa na mvua wakasema: “Hatukukuona ukiomba mvua!” Akasema: “Nimeomba mvua kwa ufunguo wake sahihi ambao unasababisha kuteremka mvua.” Kisha akasoma:

اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا﴿١٠﴾

 “Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu; hakika Yeye ni Mwingi mno wa kughufuria.

 

يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا﴿١١﴾

. “Atakutumieni mvua tele ya kuendelea.”

 

وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا﴿١٢﴾

“Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakupeni mito.” [Nuwh: 10-12]

 

Na Al-Awzaa’iy (Rahimahu Allaah) amesema: 

 

 “Walitoka watu kuomba mvua, wakasimama kati yao Bilaal bin Sa’d, akamhimidi Allaah na Akamtukuza, kisha akasema: “Ee Allaah hakika sisi Tumekusikia Unasema:

مَا عَلَى الْمُحْسِنِينَ مِن سَبِيلٍ

Hapana njia ya kuwalaumu wafanyao ihsaan [At-Tawbah: 51]

 “Na tumeshakiri makosa yetu, basi je, unaweza msamaha wako kuwa kwa watu mfano wetu? Ee Allaah! Tughufurie na Turehemu na Tunyweshee mvua”. Akanyanyua mikono yake, wakanyanyua watu mikono yao, wakanyweshewa mvua.”

 

Imaam Qurtwuby akaendelea kutaja kisa cha watu waliyemshitakia Hasan Al-Baswriy (Rahimahu Allaah) kwa shida mbali mbali:

 

 “Mtu mmoja alimjia Hasan Al-Baswriy kumshitakia ukame, Akamwambia: “Omba maghfirah kwa Allaah”.  Siku nyingine akaja wa pili kumshtakia ufakiri, Akamwambia: “Omba maghfirah kwa Allaah”. Akamjia mwengine kumwambia: “Niombee Allaah Aniruzuku mtoto” Akamwambia:  “Omba maghfirah kwa Allaah”. Akaja mwengine kumshtakia ukosefu wa maji shambani mwake. Akamwambia: “Omba maghfirah kwa Allaah” (Wakastajaabu watu kuwa mahitaji kadhaa tofauti lakini utambuzi ni mmoja tu!) Akasema:  “Sikusema lolote kutoka kwangu, bali hakika Allaah Ta’aalaa Anasema:

اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا﴿١٠﴾

 “Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu; hakika Yeye ni Mwingi mno wa kughufuria.

يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا﴿١١﴾

 “Atakutumieni mvua tele ya kuendelea.”

وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا﴿١٢﴾

 “Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakupeni mito.” [Nuwh: 10-12]

 

 

 

12- Kumshukuru Allaah Kwa Wingi Kuhusu Neema Zake

 

Neema za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni nyingi mno hakuna awezaye kuzihesabu kama Anavyosema:

 

وَآتَاكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ ۚ وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَتَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ إِنَّ الْإِنسَانَ لَظَلُومٌ كَفَّارٌ ﴿٣٤﴾

Na Akakupeni kila mnachomuomba. Na mkihesabu neema za Allaah hamtoweza kuziorodhesha hesabuni.  Hakika insani ni mwingi wa dhulma, mwingi wa kukufuru akosaye shukurani. [Ibraahiym: 3]

 

 

Na Amesema pia Allaah ('Azza wa Jalla):

وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَةَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ 

Na mkihesabu neema za Allaah hamtoweza kuziorodhesha hesabuni. [An-Nahl: 18]

 

 

Neema hizo ni aina mbili kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta''aalaa):

 

أَلَمْ تَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَسْبَغَ عَلَيْكُمْ نِعَمَهُ ظَاهِرَةً وَبَاطِنَةً ۗ 

Je, hamuoni kwamba Allaah Amekuitishieni vile vilivyomo mbinguni na vile vilivyomo ardhini, na Akakutimizieni kitimilifu neema Zake kwa dhahiri na siri?  [Luqmaan: 20]

 

 

Neema za dhahiri; kila kinachowezekana kuonekana katika Alivyoumba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) mfano; ardhi, bahari, jua, mwezi, nyota, maji, mwili, siha, mali, watoto, wanyama, miti, na neema nyingi nyinginezo zisizo hesabika).

 

Neema za siri; ni kila kilichofichika (mfano; iymaan, taqwa, ikhlaasw, akili, Malaika, Jannah na mazuri yaliyoko Aakhirah na neema nyingi mno nyenginezo tusizozijua au kuziona ambazo hazihesabiki).

 

Kwa hiyo imewajibika kwetu kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa wingi japokuwa shukurani zetu haziwezi kulingana uwingi wa neema Zake. Juu ya hivyo, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):  

وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكُمْ لَئِن شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ ۖ 

Na pindi Alipotangaza Rabb wenu: “Ikiwa mtashukuru, bila shaka Nitakuzidishieni (neema Zangu); [Ibraahiym: 7]

 

 

 

Share

09-Wewe Pekee Tunakuabudu: Kwanini Du’aa Hazitakabaliwi

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

09- Kwanini Du’aa Hazitakabaliwi

 

 

 

Muislamu huwa ni mtihani kwake pale anapoomba du’aa na ikawa haikukubaliwa, hasa anapopatwa na shida, dhiki na akahitaji faraja ya haraka. Ingawa kutokutakabaliwa du’aa huenda ikawa ni khayr kwa mwenye kuomba kama ilivyotangulia dalili yake, lakini pia huenda ikawa zipo sababu za kutokutakabaliwa du’aa. Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijinga dhidi ya kutokutakabaliwa du’aa kwa kuomba:  

 

 ((اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ قَلْبٍ لاَ يَخْشَعُ وَمِنْ دُعَاءٍ لاَ يُسْمَعُ وَمِنْ نَفْسٍ لاَ تَشْبَعُ وَمِنْ عِلْمٍ لاَ يَنْفَعُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَؤُلاَءِ الأَرْبَعِ))

 ((Ee, Allaah, hakika mimi najikinga Kwako dhidi ya moyo usionyenyekea, na dhidi ya du’aa isiyosikilizwa, na dhidi ya nafsi isiyoshiba, na dhidi ya elimu isiyonufaisha. Najikinga Kwako na haya manne)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3482), Swahiyh Al-Jaami’ (1297)]

 

Na katika Muslim na An-Nasaaiy Hadiyth ya Zayd bin Arqam (Radhwiya Allaahu ‘anhu)

 

وَمِنْ دَعْوَةٍ لَا يُسْتَجَابُ لَه

 ((Na kutokana na du’aa isiyoitikiwa))  [Muslim, Swahiyh An-Nasaaiy (5473)

 

Baadhi ya yanayosababisha du’aa kutokutakabaliwa na dalili zake:

 

 

1- Kutokufuata Yanayosababisha Du’aa Kutakabaliwa

 

Kama vile; adabu za du’aa, sababu za kutakabaliwa du’aa, nyakati na sehemu za kutakabaliwa du’aa, na kutokutumia Tawassul zinazokubalika ki-shariy’ah, na kadhaalika.    

 

 

02– Kuchuma Na Kula Vya Haraam

 

Mwenye kutaka du’aa yake ikubaliwe, ni muhimu ahakikishe kuwa chakula chake, mavazi yake na uchumi wake unapatikana kihalali, kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Hapokei isipokuwa yaliyo mema:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ اللَّهَ طَيِّبٌ لاَ يَقْبَلُ إِلاَّ طَيِّبًا, وَإِنَّ اللَّهَ أَمَرَ الْمُؤْمِنِينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ الْمُرْسَلِينَ فَقَالَ: ((يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ)) وَقَالَ: ((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ (( ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ يُطِيلُ السَّفَرَ أَشْعَثَ أَغْبَرَ يَمُدُّ يَدَيْهِ إِلَى السَّمَاءِ يَا رَبِّ يَا رَبِّ وَمَطْعَمُهُ حَرَامٌ وَمَشْرَبُهُ حَرَامٌ وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ وَغُذِيَ بِالْحَرَامِ فَأَنَّى يُسْتَجَابُ لِذَلِكَ  

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  “Enyi watu, hakika Allaah ni Mzuri na Hapokei ila kilicho kizuri. Na Allaah Amewaamrisha Waumini yale yale Aliyowaamrisha Rusuli (Mitume) Akasema:  

 

يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٥١﴾

“Enyi Rusuli! Kuleni katika vizuri na tendeni mema, hakika Mimi kwa yale myatendayo Ni Mjuzi.”  [Al-Muuminuwn (23:51)] 

 

Na Anasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ  

“Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni.” [Al-Baqarah (2:172)]. 

 

Kisha akamtaja mtu aliyekuwa safarini, nywele zimemsimama timtim na mwili umejaa vumbi, anainua mikono yake mbinguni akiomba: Ee Rabb! Ee Rabb! Na hali chakula chake ni haramu, kinywaji chake ni haramu na mavazi yake ni haramu, na amelishwa vya haramu, basi vipi ataitikiwa duaa yake?!” [Muslim]

 

03- Kutenda Madhambi

 

Muislamu anapoomba du’aa ukapita muda mrefu asitakabaliwe du’aa yake, arudie kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kuomba maghfirah na atubie sababu huenda akawa ametenda dhambi kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya ‘Uthmaan bin Abiy Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

 

(( تُفْتَحُ أَبْوَابُ السَّمَاءِ نِصْفَ اللَّيْلِ فَيُنَادِي مُنَادٍ: هَلْ مِنْ دَاعٍ فَيُسْتَجَابَ لَهُ؟ هَلْ مِنْ سَائِلٍ فَيُعْطَى؟ هَلْ مِنْ مَكْرُوبٍ فَيُفَرَّجَ عَنْهُ؟ فَلا يَبْقَى مُسْلِمٌ يَدْعُو بِدَعْوَةٍ إِلا اسْتَجَابَ اللَّهُ لَهُ إِلا زَانِيَةٌ تَسْعَى بِفَرْجِهَا أَوْ عَشَّارٌ))  

((Milango ya mbingu hufunguliwa inapofika nusu ya usiku, kisha hunadiwa na mwenye kunadi: “Je, yupo mwenye kuomba du’aa aitikwe? Je, yupo kwenye kutaka jambo apewe? Je, yupo mwenye dhiki afarijiwe? Basi habakii Muislamu yeyote anayeomba du’aa ila Allaah Anamtakabalia, isipokuwa mwanamke mzifinifu anayekimbia [kuuza] kwa uchi wake au mkusanyaji pesa kiharamu)) [Atw-Twabaraaniy katika Al-Mu’jam Al-Kabiyr  (9/59) na Al-Mu’jam Al-Awsatw (3/154) na amesema Al-Albaaniy Isnaad yake ni Swahiyh; Swahiyh At-Targhiyb (786), Swahiyh Al-Jaami’ (2971)]

 

 

04- Kutokuamrisha Mema Na Kutokukataza Maovu:

 

عَنْ حُذَيْفَةَ بْنِ الْيَمَانِ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم) قَالَ: ((والَّذي نَفسي بيدِهِ لتأمُرُنَّ بالمعروفِ ولتَنهوُنَّ عنِ المنكرِ أو ليوشِكَنَّ اللَّهُ أن يبعثَ عليكُم عقابًا منهُ ثمَّ تَدعونَهُ فلا يَستجيبُ لَكُم))

Kutoka kwa Hudhayfah bin Al-Yamaani (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake! Mtaamrisha mema na mtakataza maovu au sivyo Allaah Atakuleteeni adhabu kutoka Kwake, kisha mtamuomba wala Hatokuitikieni)) [Ahmad na At-Tirmidhy - Swahiyh At-Tirmdhiy (2169), Swahiyh Al-Jaami’ (7070)]

 

Na Al-Qurtwubiy ameleza kisa cha Ibraahiym bin Ad-ham kifuatacho:

Ibraahiym bin Ad-ham aliulizwa: “Kwa nini du’aa zetu hazitakabaliwi?” Alijibu: “Kwa sababu mnamjua Allaah lakini hamumtii. Mnaisoma Qur-aan lakini hamtekelezi yaliyomo. Mnajidai kumpenda Rasuli wa Allaah lakini hamfuati Sunnah zake. Mnamjua shaytwaan, lakini hampigani naye badala yake mnamtii. Mnadai mnaijua Jannah na kuitamani, lakini hamuikimbilii kwa juhudi. Mnadai mnaujua Moto lakini hamjiepushi nao. Mnasema mauti ni haki yatawafika tu, lakini hamtayarishi nafsi zenu kwayo. Mnashughulika na aibu za watu mnaacha zenu. Mnakula katika neema za Allaah, lakini hamshukuru. Mnazika maiti zenu lakini hamjifunzi kwayo. Basi vipi mtataitikiwa?”

[Tafsiyr Al-Qurtwubiy, mj. 2, uk.312]

 

Na ameelezkisa hicho vilevile Ibn 'Abdil-Barr katika "Jaami' Bayaan Al-'Ilm Wa Fadhwlih", isipokuwa yeye kataja mambo matano na si kumi kama aliyoyataja Al-Qurtwubiy.

 

 

 

Share

10-Wewe Pekee Tunakuabudu: Wanaotakabaliwa Du’aa Zao

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

10 - Wanaotakabaliwa Du’aa Zao

 

 

 

Baadhi ya waliotajwa kuwa du’aa zako zinatakabalilwa na dalili zake:

 

 

1-Du’aa Za Imaam Muadilifu, Mwenye Swawm Na Aliyedhulumiwa

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ثَلاَثَةٌ لاَ تُرَدُّ دَعْوَتُهُمْ، الإِمَامُ الْعَادِلُ، وَالصَّائِمُ حَتَّى يُفْطِرَ، وَدَعْوَةُ الْمَظْلُومِ يَرْفَعُهَا اللَّهُ دُونَ الْغَمَامِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَتُفْتَحُ لَهَا أَبْوَابُ السَّمَاء،وَيَقُولُ بِعِزَّتِي لأَنْصُرَنَّكِ وَلَوْ بَعْدَ حِينٍ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (([Watu] Watatu hazirudishwi du'aa zao; Imaam muadilifu, mwenye Swawm mpaka afuturu, na du'aa ya aliyedhulumiwa, Anainyanyua Allaah bila ya mawingu Siku ya Qiyaamah na inafunguliwa milango ya mbingu na Anasema: Kwa Utukufu Wangu, Nitakunusuru japo baada ya muda.))[Swahiyh At-Tirmidhiy (2526) Ibn Maajah, Ahmad]

 

Kuhusu mwenye Swawm ni kwamba ana fursa pana mno ya kuomba du'aa nyingi wakati wote tokea anapoanza kufunga Swawm asubuhi hadi Magharibi anapofuturu.  

 

Na kuhusu aliyedhulumiwa naye amepewa fadhila ya kukubaliwa du'aa zake dhidi ya aliyemdhulumu kwa aina yeyote ya dhulma; kudhulumiwa mali yake, kukandamizwa, kuteswa, kusengenywa, kuvunjiwa heshima yake na uovu wowote ule atakaofanyiwa. Hivyo basi ni khatari kwa anayedhulumu pindi mdhulumiwa akinyanyua mikono yake kumuombea mabaya kwani du’aa yake huitikiwa moja kwa moja bila ya kizuizi:

 

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا) أَنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) بَعَثَ مُعَاذًا إِلَى الْيَمَنِ فَقَالَ:  ((اتَّقِ دَعْوَةَ الْمَظْلُومِ فَإِنَّهَا لَيْسَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ اللَّهِ حِجَابٌ))

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpeleka Mu’aadh Yemen akasema: ((Iogope du’aa ya aliyedhulumiwa, kwani haina pazia baina yake na baina ya Allaah.)) [Al-Bukhaariy (2448), Swahiyh At-Tirmidhiy(2014), Swahiyh Al-Jaami’ (1037)]

 

Na pia Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

 

   اتَّقوا دعوةَ المظلومِ، فإنها تَصعدُ إلى السماءِ كأنها شرارةٌ

((Ogopeni du’aa ya aliyedhulumiwa kwani inapanda mbinguni kama cheche za moto.)) [Al-Haakim katika Al-Mustadrak ameisahihisha Al-Albaaniy; Swahiyh Al-Jaami’ (118), Swahiyh At-Targhiyb (2228)]

 

Hakuna tofauti ya aliyedhulumiwa akiwa ni Muislamu mwenye taqwa au muovu au hata Kafiri kama ilivyothibiti:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((دَعْوَةُ الْمَظْلُومِ مُسْتَجَابَةٌ وَإِنْ كَانَ فَاجِرًا فَفُجُورُهُ عَلَى نَفْسِهِ))

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Du’aa ya aliyedhulumiwa (dhidi ya aliyemdhulumu) ni yenye kuitikiwa japo akiwa ni mtendaji dhambi kwani dhambi zake ni dhidi ya nafsi yake.)) [Ahmad, Swahiyh At-Targhiyb (2229), Swahiyh Al-Jaami’ (3382)]

 

عَنْ أنس رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: اتَّقُوا دَعْوَةَ الْمَظْلُومِ وَإِنْ كَانَ كَافِرًا فَإِنَّهُ لَيْسَ دُونَهَا حِجَابٌ

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ogopeni du’aa ya aliyedhulumiwa hata akiwa ni Kafiri, kwani haina baina yake kizuizi.)) [Ameisahihisha Al-Albaaniyn katika Swahiyh At-Targhiyb (2231)

 

 

 

2- Du’aa Ya Mzazi Kwa Mwanawe

 

Du’aa ya mzazi kwa mwanawe hairudi:

 

عّنْ أَنسْ بِنْ ماَلِكْ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ): ((ثَلاَثُ دَعْواتِ لاَ تُرَدُّ: دَعْوَةُ الْوَالِدِ لِوَلَدِهِ، وَدَعْوَةُ الصَّائِم،  وَدَعْوَةُ الْمُسَافَرَ))

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu): ((Du’aa za watatu hazirudishwi; du’aa ya mzazi kwa mwanawe, na du’aa ya mwenye kufunga Swawm, na du’aa ya msafiri.))[Al-Bayhaqiy katika Swahiyh Al-Jaami’ (3032) na katika Asw-Swahiyhah (1797)]

 

Mzazi ana haki zaidi kutendewa wema na kutiiwa na mwanawe. Na ndipo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalih wa sallam) ameonya wazazi wasiwaombee watoto wao du’aa mbaya, kwani ni yenye kutakabaliwa:

 

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لاَ تَدْعُوا عَلَى أَنْفُسِكُمْ ولاَ تَدْعُوا عَلَى أَولاَدِكُمْ))

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Msijiombee dhidi ya nafsi zenu wala msiombe dhidi ya watoto wenu.)) [Muslim (3009), Abuu Daawuwd, taz. Swahiyh Abiy Daawuwd (1532) na Swahiyh Al-Jaami’ (7267)]

 

Hadiyth nyingine pia inayothibitisha kukubaliwa du’aa ya mzazi kwa mwanawe ni iliyotajwa pamoja na aliyedhulumiwa na msafiri.

 

 

 

3- Du’aa Ya Mtoto Mwema Kwa Wazazi Wake

 

Du’aa ya mtoto mwema kwa mzazi wake aliyefariki ni miongoni mwa ‘amali tatu ambazo aliyefariki anaendelea kunufaika nayo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((إِذَا مَاتَ الإِنْسَانُ انْقَطَعَ عَنْهُ عَمَلُهُ إلاَّ مِنْ ثلاَثَةٍ: صَدَقَةٍ جَارِيَةٍ، أَوْ عِلْمٍ يُنْتَفَعُ بِهِ، أَوْ وَلَدٍ صَالِحٍ يَدْعُو لَهُ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anapofariki mtu hukatika 'amali zake ila mambo matatu; swadaqah inayoendelea au elimu inayonufaisha au mtoto mwema anayemuombea.)) [Muslim, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ahmad]

 

Na pia

 

عن أبي هريرة عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إنَّ الرجل لتُرفع درجتُه في الجنَّة فيقول: أنَّى هذا فيقال: باستغفار ولدك لك ))  

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mtu hupandishwa daraja yake Jannah  basi husema: “Kutokana na nini?” Husemwa: “Kutokana na mwanao kukuombea maghfirah.”)) [Ibn Maajah (3660) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (1617)]

 

 

 

4- Du’aa Ya Msafiri

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ثلاثُ دَعَوَاتٍ مُسْتَجَابَاتٌ لاَ شَكَّ فِيهِنَّ، دَعْوَةُ الْمَظْلُومِ، وَدَعْوَةُ الْمُسَافِرِ، وَدَعْوَةُ الْوَالِدِ عَلَى وَلَدِهِ))

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Du’aa tatu ni zenye kuitikiwa, hazina shaka ndani yake; du’aa ya aliyedhulumiwa, du’aa ya msafiri, na du’aa ya mzazi kwa mwanawe.)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (1905), Swahiyh Ibn Maajah (3129) Swahiyh Al-Jaami’ (3033)

 

 

 

5- Du’aa Ya Mwenye Kumuombea Muislamu Mwenzake Kwa Siri

 

عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: مَا مِنْ عَبْدٍ مُسْلِمٍ يَدْعُو لأَخِيهِ بِظَهْرِ الْغَيْبِ، إِلاَّ قَالَ الْمَلَكُ: وَلَكَ بِمِثْلٍ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ad-Dardaai (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna mja Muislamu anayemuombea nduguye kwa ghayb (kwa siri) isipokuwa, Malaika husema: Nawe pia upate mfano wake.)) [Muslim (2732) na pia (2733)]

 

Na riwaayah nyingine pia katika Muslim:

 

 مَنْ دَعَا لأَخِيهِ بِظَهْرِ الْغَيْبِ، قَالَ الْمَلَكُ الْمُوَكَّلُ بِهِ: آمِينَ، وَلَكَ بِمِثْلٍ

((Atakayemuombea nduguye kwa ghayb (kwa siri), Malaika aliyewakilishwa kwake husema: “Aamiyn nawe upate kama hivyo.")) [Taz pia: Swahiyh Al-Jaami’ (6235), (5737), (3380), (3381), (3379), Swahiyh Ibn Maajah (2358) Abuu Daawuwd (1534)

 

 

 

6- Du’aa Ya Mwenye Dhiki

 

Muislamu aliye katika dhiki, shida, au kufikwa na janga, balaa amkabili Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kumuomba huku akiwa na matumaini na kutegemea Rahmah Yake. Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):   

 

أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾

Au nani Anayemuitika mwenye dhiki mno anapomwomba, na Akamuondoshea ouvu na Akakufanyeni makhalifa wa ardhi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Ni machache mno mnayokumbuka. [An-Naml: 62]

 

 

 

7- Du’aa Ya Mwenye Kufikwa Na Msiba

 

Muislamu anapopatwa na msiba, atambue kwamba amepewa fadhila badala yake ya kuomba du’aa, ili arudishiwe alichopoteza na ambacho kitakuwa cha khayr zaidi kuliko kilichomuondokea au kumsibu. Inapasa asichelewe kuomba du’aa yake bali hapo hapo akumbuke na aombe du’aa iliyothibiti katika Sunnah. Alifanya hivyo Mama wa Waumini Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) alipofiwa na mumewe Abuu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kama ilivyoelezwa katika Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ (رَضِيَ الله عَنْهَا) قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ تُصِيبُهُ مُصِيبَةٌ فَيَقُولُ مَا أَمَرَهُ اللَّهُ, إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ, اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا, إلاَّ أَخْلَفَ اللَّهُ لَهُ خَيْرًا مِنْهَا)) قَالَتْ: فَلَمَّا مَاتَ أَبُو سَلَمَةَ قُلْتُ أَيُّ الْمُسْلِمِينَ خَيْرٌ مِنْ أَبِي سَلَمَة أَوَّلُ بَيْتٍ هَاجَرَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم). ثُمَّ إِنِّي قُلْتُهَا فَأَخْلَفَ اللَّهُ لِي رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ). قَالَتْ: أَرْسَلَ إِلَيَّ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) حَاطِبَ بْنَ أَبِي بَلْتَعَةَ يَخْطُبُنِي لَهُ. فَقُلْتُ: إِنَّ لِي بِنْتًا وَأَنَا غَيُورٌ فَقَالَ: ((أَمَّا ابْنَتُهَا فَنَدْعُو اللَّهَ أَنْ يُغْنِيَهَا عَنْهَا وَأَدْعُو اللَّهَ أَنْ يَذْهَبَ بِالْغَيْرَةِ))

Imepokelewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakuna Muislamu anayefikwa na msiba akasema Alivyoamrishwa na Allaah: "Hakika sisi ni wa Allaah, na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea. Ee Allaah, nilipe kwa msiba wangu na nipe badala yake kilicho bora kuliko huo (msiba)", basi hapana isipokuwa Allaah Atampa kilicho bora kuliko [msiba] huo)). Alipofariki Abuu Salamah, alisema: “Muislamu gani ni bora kuliko Abuu Salamah ambaye familia yake ilikuwa ya kwanza kuhajiri kwa  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kisha nikaisoma [du’aa hiyo] na Allaah Akanipa badala yake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akaendelea kusema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamtuma Haatwib bin Abiy Balta’ah anipose kwake nikasema: “Mimi nina binti [anayenitegemea] nami nina tabia ya wivu. Akasema: ((Ama kuhusu binti yake tutamwomba Allaah Amtoshelezee [asiwe na jukumu naye], na namuomba Allaah Amuondoshee tabia ya wivu na hamaki.)) [Muslim]

 

 

 

Share

11-Wewe Pekee Tunakuabudu: Nyakati, Mahali Na Hali Za Kutakabaliwa Du'aa

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

11 - Nyakati, Mahali Na Hali Za Kutakabaliwa Du'aa

 

 

 

Neema za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) juu ya waja Wake kujaalia miezi bora kuliko miezi mingine, masiku bora kuliko mengineyo, masaa bora kuliko mengineyo, mahali bora kuliko pengineko. Vile vile kujaalia hali kadhaa kuwa ni hali zenye kutakabaliwa du’aa. Kwa hiyo Muislamu ajitahidi kuomba katika nyakati au hali zifuatazo:

 

 

1. Du’aa Wakati Wa Kuamka Usiku:

 

Unapoamka usiku, jambo la kwanza kufanya ni kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na kuomba utakacho:

 

عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ تَعَارَّ مِنْ اللَّيْلِ فَقَالَ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ، ثُمَّ قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي، أَوْ دَعَا اسْتُجِيبَ لَهُ، فَإِنْ عَزَمَ فَتَوَضَّأَ ثُمَّ صَلَّى قُبِلَتْ صَلَاتُهُ))

Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Swaamit (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeamka usiku akasema: Laa ilaaha illa-Allaah  Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa-Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, wa Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah walaa ilaaha illa-Allaah wa-Allaahu Akbar walaa hawla walaa quwwata illa biLlaah (Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Pekee Hana mshirika, Ufalme ni Wake na Himdi ni Zake Naye ni Mweza wa kila kitu. Ametakasika Allaah, na Himdi ni za Allaah, na hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, Allaah ni Mkubwa kabisa, na hapana uwezo wala nguvu ila za Allaah), kisha akasema Rabbigh-fir-liy [ee Allaah, nighufurie] au akaomba, ataitikiwa. Na akiazimia kutawadha na kuswali atatakabaliwa Swalaah yake)) [Al-Bukhaariy na wengineo] 

 

 

 

2. Du’aa Inapoadhiniwa Swalaah:

 

Hii ni fursa adhimu kwa Muislamu kupata mara tano kwa siku kuwa ni nyakati za kukubaliwa du’aa. Hadiyth mbali mbali za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zimethibiti baadhi yake zifuatazo:

 

عن أنس بن مالك (رضي الله عنه) عن النبي صلى الله عليه وسلم: ((إذا نودِي بالصلاةِ فُتحَتْ أبوابُ السماءِ، واستُجيبَ الدعاءُ))

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Inaponadiwa Swalaah, milango ya mbingu hufunguliwa na du’aa huitikiwa)) [Atw-Twayaalisiy, Abuu Ya’laa, Adhw-Dhwiyaa Al-Maqdasiy, na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (818), na As-Silsilah Asw-Swahiyhah (1413)]

 

 عَنْ أَبِي أُمَامَة الْبَاهِلِي (رَضِيَ اللَّه عَنْهُ) عَن النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّم) إِذَا نَادَى الْمُنَادِي فُتِحَتْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ، وَاسْتُجِيبَ الدَّعَاءِ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Umaamah Al-Baahiliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ((Anaponadi muadhini, milango ya mbingu inafunguliwa na du’aa zinaitikiwa)) [Abu Ya’laa, Al-Haakim na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (803)]

 

 عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ (رَضِيَ اللَّه عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((ثِنْتَانِ لاَ تُرَدَّان أَوْ قَلَّمَا تُرَدَّانِ: الدُّعَاءُ عِنْدَ النِّدَاءِ, وَعِنْدَ الْبَأْسِ حِينَ يُلْحِمُ بَعْضُهُمْ بَعْضًا))

Imepokelewa kutoka kwa Sahl bin Sa’d (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (([Du’aa] Mbili hazirudishwi au nadra kurudishwa; du’aa inapoadhiniwa na wakati wa vita majeshi wanapotekana)) [Abu Daawuwd imepewa daraja ya Swahiyh na Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (3079)]
 

 

 

3. Du’aa Baada Ya Kutawadha Kuomba Jannah:

 

Du’aa baada ya kutawadha iliyotajwa katika Hadiyth ifuatayo ya kuomba Pepo:

 

 عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ (رَضِيَ اللَّه عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَتَوَضَّأُ فَيُحْسِنُ الْوُضُوءَ ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إلاَّ اللَّهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، إلاَّ فُتِحَتْ لَهُ ثَمَانِيَةُ أَبْوَابِ الْجَنَّةِ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَا شَاءَ))

Kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna Muislamu yeyote anayetawadha akatia vizuri wudhuu wake, kisha akasema: “Ash-hadu anlaa ilaaha illa-Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu [Nashuhudia kwamba hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake] ila atafunguliwa milango minane ya Jannah ataingia wowote apendao)) [Ibn Maajah – Swahiyh Ibn Maajah (385)]

 

 

 

4. Du’aa Baina ya Adhaana Na Iqaamah:

 

Hii pia ni fursa nyingine kwa Muislamu kuwa katika mara tano kwa siku ana nyakati ya kuitikiwa du’aa zake:

 

 عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((الدُّعَاءُ لاَ يُرَدُّ بَيْنَ الأَذَانِ وَالإِقَامَةِ))  

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Du’aa hairudishwi baina ya adhana na iqaamah)) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ahmad – Hadiyth Hasan Swahiyh, ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (212), Irwaa-u Al-Ghaliyl (244), Swahiyh Al-Jaami’ (3408)]

 

 

 

5. Du’aa Kila Baada Ya Swalaah:

 

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قِيلَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَيُّ الدُّعَاءِ أَسْمَعُ؟ قَالَ: ((جَوْفَ اللَّيْلِ الآخِرِ وَدُبُرَ الصَّلَوَاتِ الْمَكْتُوبَاتِ))

Imepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema:  Ilisemwa: Ee Rasuli wa Allaah, du’aa ipi inayosikilizwa zaidi (inayotakabaliwa zaidi)? Akasema: ((Sehemu ya mwisho ya usiku na baada ya kila Swalaah ya faradhi))  [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan, Swahiyh At-Tirmidhiy (3499) Swahiyh At-Targhiyb (1648)]

 

Ufafanuzi wa ‘Baada ya Swalaah”:  Je ni kabla ya tasliym au baada ya tasliym?

 

‘Ulamaa wamekubaliana kwamba ikiwa ni adhkaar (nyiradi) zilizothibiti katika Sunnah kama tasbiyh, tahmiyd, takbiyr, na Aayatul-Kursiy, Suwratul-Ikhlaasw na Al-Mu’awwidhatayn, basi ilokusudiwa ‘baada ya Swalaah’ ni baada ya kutoa salaam. Ama ikiwa ni du’aa basi ilokusudiwa ni kabla ya kutoa salaam. Kauli zao ni kama zifuatazo:

 

Ibnul-Qayyim (Rahimahu-Allaah):

“Kila baada ya Swalaah, inajumuisha kabla ya salaam na baada ya salaam. Na Shaykh wetu Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema (kuhusu du’aa) ni kabla ya salaam kwa dalili ya mfano wa: ‘kila baada ya nyuma ya kitu kama vile nyuma ya mnyama.” [Zaad Al-Ma’aad(1/294)]

 

 

Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah):

“Kila baada ya Swalaah inaainisha kabla ya tasliym, na ina maana baada ya tasliym moja kwa moja. Na Hadiyth Swahiyh zimetajwa ambazo zinaonesha ilokusudiwa kwamba kama ni du’aa basi ni kabla ya tasliym. Ama adhkaar zilotajwa kuhusiana na hili, basi Hadiyth Swahiyh zimeashiria kwamba hizo ni baada ya Swalaah, kwa maana baada ya tasliym.” [Majmuw’ Fataawa Ibn Baaz (11/194)]

 

 

Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah):

“Yaliyotajwa makhsusi (ya Sunnah) kila baada ya Swalaah ikiwa ni adhkaar (nyiradi) basi hizo ni baada yake, na ikiwa ni du’aa basi ni mwisho wake (kabla ya salaam)." [Majmuu’ Fataawa Ibn ‘Uthaymiyn (13/268)]

 

 

 

6. Du’aa Katika Kusujudu:

 

Bin Aadam anapomsujudia Allaah (‘Azza wa Jalla) inadhihirisha unyenyekevu mbele Yake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwani anaweka kipaji cha uso wake ardhini kujidhalilisha kwa Aliyemuumba. Na kipaji cha uso ni sehemu bora kabisa katika mwili wa bin Aadam, ndipo hapo anapokuwa mja karibu kabisa na Rabb wake:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّه عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((أَقْرَبُ مَا يَكُونُ الْعَبْدُ مِنْ رَبِّهِ وَهُوَ سَاجِدٌ فَأَكْثِرُوا الدُّعَاءَ))

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mja huwa karibu kabisa na Rabb   wake anapokuwa anasujudu, kwa hiyo zidisheni du'aa)) [Muslim (482), Abu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ahmad]

 

 

 

7. Du’aa Katika Thulutuhi Ya Mwisho Ya Usiku:

 

Neema na fadhila kubwa kwa binaadam kwamba Allaah (‘Azza wa Jalla) Huteremka hadi mbingu ya dunia kututakabalia du’aa, kutukidhia haja na kutughufuria dhambi: 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْه)ُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ:  ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الآَخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ ، مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ ، مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Rabb wetu Tabaaraka wa Ta’aalaa) Huteremka [kwa namna inavyolingana na utukufu Wake] kila siku katika mbingu ya dunia [ya kwanza] inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba Nimtakabalie? Nani ananitaka jambo Nimpe? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad]

 

 

 

8. Du’aa Katika Saa Ya Usiku:

 

عَنْ جَابِرٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ)  قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ يَقُولُ: ((إِنَّ فِي اللَّيْلِ لَسَاعَةً لاَ يُوَافِقُهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ يَسْأَلُ اللَّهَ خَيْرًا مِنْ أَمْرِ الدُّنْيَا وَالآَخِرَةِ إِلاَّ أَعْطَاهُ إِيَّاهُ وَذَلِكَ كُلَّ لَيْلَةٍ))

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika katika usiku bila shaka kuna saa haimuwafikii mtu Muislamu anayemwomba Allaah khayr katika mambo ya dunia au Aakhirah ila Atampa, na hiyo ni kila usiku)) [Muslim (757), Swahiyh Al-Jaami’ (2130)]

 

 

 

9. Du’aa Katika Saa Ya Siku Ya Ijumaa:

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ذَكَرَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ فَقَالَ:  ((فِيهِ سَاعَةٌ لاَ يُوَافِقُهَا عَبْدٌ مُسْلِمٌ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي يَسْأَلُ اللَّهَ تَعَالَى شَيْئًا إلاَّ أَعْطَاهُ إِيَّاهُ)) وَأَشَارَ بِيَدِهِ يُقَلِّلُهَا

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja Siku ya Ijumaa akasema: ((Humo mna saa haimwafikii mja Muislamu akiwa amesimama anaswali anamwomba Allaah Ta’aalaa kitu ila Anampa)). Akaashiria kuonyesha ukaribu wake [Al-Bukhaariy (935), Muslim (852) na wengineo]

 

‘Ulamaa wamekubaliana kuwa ni nyakati mbili kwa dalili zifuatazo:

 

Kwanza: Anapopanda Imaam katika minbari na kukaa kwake hadi anapomaliza Swalaah:

 

عَنْ أَبِي بُرْدَةَ بْنِ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ (رضي الله عنهما) قَالَ: قَالَ لِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُمَرَ: أَسَمِعْتَ أَبَاكَ يُحَدِّثُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي شَأْنِ سَاعَةِ الْجُمُعَةِ؟ قَالَ: قُلْتُ: نَعَمْ سَمِعْتُهُ يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((هِيَ مَا بَيْنَ أَنْ يَجْلِسَ الإِمَامُ إِلَى أَنْ تُقْضَى الصّلاَةُ))

Kutoka kwa Abuu Burdah bin Abiy Muwsaa Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: ‘Abdullaahi bin ‘Umar ameniuliza: Je umemsikia baba yako akihadithia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu saa ya [kutakabaliwa du’aa) Ijumaa? Akasema: Nikasema:  Ndio, nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hiyo ni baina ya anapokaa Imaam hadi inapomalizika Swalaah)) [Muslim (853)]

 

Pili: Baada ya Swalaah ya Alasiri hadi kuzama jua. Hii ni kauli inayokubalika zaidi miongoni mwa ‘Ulamaa kwa dalili:

 

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ (رضي الله عنه) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((يَوْمُ الْجُمُعَةِ اثْنَتَا عَشْرَةَ سَاعَةً ،لاَ يُوجَدُ فِيهَا عَبْدٌ مُسْلِمٌ يَسْأَلُ اللَّهَ شَيْئًا إلاَّ آتَاهُ إِيَّاهُ ، فَالْتَمِسُوهَا آخِرَ سَاعَةٍ بَعْدَ الْعَصْر))

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Siku ya Ijumaa kuna masaa kumi na mbili ambayo hapatikani mja Muislamu anayemwomba Allaah kitu ila Anampa, basi itafuteni baada ya Swalaah ya Alasiri))  [Swahiyh Abiy Daawuwd (1048), Swahiyh An-Nasaaiy(1388), Swahiyh Al-Jaami’ (8190)]

 

Kauli za Baadhi Ya ‘Ulamaa:

 

Shaykh Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah):  

“Huu ndio wakati ambao ameupendekeza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ajili ya du’aa siku ya Ijumaa. Lakini hii haimaanishi kwamba Muislamu asimwombe Rabb wake siku ya Ijumaa ila wakati huu, bali ni Sunnah kuomba du’aa kila siku, na kila saa, na siku ya Ijumaa, isipokuwa tu saa iliyotajwa siku ya Ijumaa ni makhsusi.”

 

 

Al-Haafidhw Ibn Hajr (Rahimahu Allaah):

“Sa’iyd bin Manswuwr amesimulia katika Sunan yake kutoka kwa Abuu Salamah bin ‘Abdir-Rahmaan kwamba Maswahaba walijumuika wakataja kuhusu saa ya Ijumaa, kisha wakaachana, lakini hawakukhitilafiana kwamba ni saa ya mwisho ya siku ya Ijumaa.” [Fat-h Al-Baariy(2/421)]

 

 

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah):  

“Hadiyth nyingi kuhusu saa ambayo inatarajiwa kuitikiwa du’aa ni baada ya Swalaah ya Alasiri..." [At-Tirmidhiy (2/360)]

 

 

Hitimisho kuhusu rai hiyo ya pili ni kwamba, ‘Ulamaa wamekariri kutaja kwamba nyakati zote mbili hizo zihesabiwe kuwa ni saa iliyokusudiwa. Hata hivyo, anapaswa pia Muislamu ajitahidi kuomba du’aa siku nzima ya Ijumaa na haswa nyakati hizo zisikoswe kwa mwenye kutamani du’aa yake itakabliwe.

 

 

 

10. Du’aa Baada Ya Jua Kufikia Upeo Kabla Ya Adhuhuri:

 

Ni wakati mwengine ambao mbingu huwa wazi na du’aa hupaa juu moja kwa moja bila ya kizuzi:

 

 عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ السَّائِبِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) كَانَ يُصَلِّي أَرْبَعًا بَعْدَ أَنْ تَزُولَ الشَّمْسُ قَبْلَ الظُّهْرِ وَقَالَ: ((إِنَّهَا سَاعَةٌ تُفْتَحُ فِيهَا أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَأُحِبُّ أَنْ يَصْعَدَ لِي فِيهَا عَمَلٌ صَالِحٌ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin As-Saaib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaahh (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali [rakaa] nne baada ya jua kufikia upeo kabla ya Adhuhuri na akasema: ((Hakika hiyo ni saa inayofunguliwa milango ya mbingu na napenda zipande 'amali zangu njema)) [At-Tirmidhiy ameisahihisha Al-Albaaniy Swahiyh At-Tirmidhiy (478), Swahiyh At-Targhiyb (587)]

 

Swalaah hizo alizokuwa akiswali Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zilikuwa ni mbali na zile nne zinazoswaliwa kabla ya Adhuhuri zinazojulikana kuwa ni ‘rawaatib’ au ‘qabliyah’ Tofauti yake pia ni kwamba alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiziswali nne kwa pamoja badala ya mbili mbili kama kawaida.

 

 

 

11. Wakati Wa Kusubiri Swalaah:

 

Huu ni wakati wa baina ya Swalaah mbili pale mtu anaposwali kisha akabakia kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) mpaka ufikie wakati wa Swalaah inayofuatia:

 

 عنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو (رضي الله عنه)  قَالَ: صَلَّيْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) الْمَغْرِبَ فَرَجَعَ مَنْ رَجَعَ, وَعَقَّبَ مَنْ عَقَّبَ، فَجَاءَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) مُسْرِعًا قَدْ حَفَزَهُ النَّفَسُ وَقَدْ حَسَرَ عَنْ رُكْبَتَيْهِ فَقَالَ: ((أَبْشِرُوا هَذَا رَبُّكُمْ قَدْ فَتَحَ بَابًا مِنْ أَبْوَابِ السَّمَاءِ يُبَاهِي بِكُمْ الْمَلائِكَةَ يَقُولُ : انْظُرُوا إِلَى عِبَادِي قَدْ قَضَوْا فَرِيضَةً وَهُمْ يَنْتَظِرُونَ أُخْرَى))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Tuliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Magharibi, wakarudi walorudi, na wakabakia walobaki. Akaja Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiharakiza kutokana na kuhamasishwa na nafsi na likiwa vazi lake limepanda hadi magoti yake kuwa wazi akasema: ((Bashirieni! Huyo ni Rabb wenu Amefungua mlango kati ya milango ya mbingu Anajigamba kwa Malaika Akisema: Tazameni waja Wangu wamemaliza fardhi kisha wanangojea nyingine))  [Ibn Maajah 'Baab Luzuwm al-Masaajid Wa Intidhwaar Asw-Swalaah' (793), Ahmad. Taz. Swahiyh Ibn Maajah (660), Swahiyh Al-Jaami’ (36), Swahiyh At-Targhiyb (445)]

 

 

 

12. Du’aa Inaponyesha Mvua:

 

Inaponyesha mvua au barafu katika nchi za baridi, ni wakati wa du’aa kutakabaliwa. Wanaoishi katika nchi ambazo zinapatikana majira ya mvua watakuwa na fursa kubwa kuomba du’aa zao kila inaponyesha mvua. Dalili ya kuitikiwa du’aa inaponyesha mvua:

 

عَنْ مَكْحُول (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَن النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَال: ((اطْلُبُوا إجَابَةَ الدُّعَاءِ عِنْدَ الْتِقَاءِ الْجُيُوشِ، وَإِقَامَةِ الصَّلَاةِ، وَنُزُولِ الْمَطَر)

Kutoka kwa Mak-huwl (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ombeni kuitikiwa du’aa wakati wa kukutana majeshi, na inapokimiwa Swalaah na inapoteremka mvua)) [As-Silsilah Asw-Swahiyhah (1469)]

 

Pia:

ثنتان ما تردان الدعاء عند النداء وتحت المطر

(([Nyakati] mbili hazirudishwi du’aa; wakati inapoadhiniwa na wakati inaponyesha mvua)) [Al-Haakim katika Al-Mustadrak (2534) na Atw-Twabaraaniy katika Al-Mu’jam Al-Kabiyr (5756) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (3078)]

 

Linalopasa ni kwamba pale inapoanza tu kunyesha mvua Muislamu asome du’aa iliyothibiti ya kunyesha mvua kisha aombe haja zake. Na inapomalizika kunyesha mvua pia kuna du’aa iliyothibiti katika Sunnah. [Rejea 

 

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)

 

 

na Hiswnul-Muumin (kinapatikana madukani)]

 

 

 

13.  Du’aa Wakati Anapowika Jogoo:
 

Anapowika jogoo ni fursa ya mtu kuomba du’aa. Pia Hadiyth hii inatufunza pia kuomba du’aa ya kujikinga na shaytwaan na shari zake, jambo ambalo ni muhimu kwa Muislamu.

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((إِذَا سَمِعْتُمْ صِيَاحَ الدِّيَكَةِ فَاسْأَلُوا اللَّهَ مِنْ فَضْلِهِ فَإِنَّهَا رَأَتْ مَلَكًا، وَإِذَا سَمِعْتُمْ نَهِيقَ الْحِمَارِ فَتَعَوَّذُوا بِاللَّهِ مِنْ الشَّيْطَانِ فَإِنَّهُ رَأَى شَيْطَانًا))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mnaposikia mlio wa jogoo basi mwombeni Allaah kutokana na fadhila Zake kwani ameona Malaika. Na mnaposikia mlio wa punda, basi jikingeni kwa Allaah kutokana na shaytwaan, kwani ameona shaytwaan)) [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy]

 

 

 

14. Du’aa Wakati Wa Kunywa Maji Ya Zamzam:

 

Ni fursa nyingine za wenye kutekeleza ‘Umrah na Hajj kuomba du’aa zao kila mara wanapokunywa maji ya zamzam. Pia fursa kwa wengineo wenye kuyapata maji hayo. Ni maji ya ajabu ambayo yana shifaa kwa magonjwa ya kila aina, hivyo inapendekezwa kwa Muislamu anapokunywa aombe siha na afya pamoja na haja zake nyinginezo. 

 

عن جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((مَاءُ زَمْزَمَ لِمَا شُرِبَ لَهُ))

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Maji ya zamzam kwa [niyyah] inayonywewa)) [Swahiyh Ibn Maajah (2502), Ahmad, Swahiyh Al-Jaami’(5502)]. Hata hivyo, japo Hadiyth hii Wanachuoni wenngine wamesema inatiliwa nguvu na zingine na kuwa ni Hasan, lakini pia kuna wengine walioidhoofisha].

 

 

 

15. Du’aa Anapotembelewa Mgonjwa:

 

Kumtembelea mgonjwa kuna fadhila nyingi tukufu kama zilivyothibiti katika Hadiyth kadhaa mojawapo ni kwamba mwenye kumtembelea mgonjwa huswaliwa na Malaika elfu sabini. Hadiyth ya ‘Aliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

 

قَالَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِذَا عَادَ الرَّجُلُ أَخَاهُ المُسْلِمَ مَشَى فِي خِرَافَةِ الجَنَّةِ حَتَّى يَجْلِسَ فَإِذَا جَلَسَ غَمَرَتْهُ الرَّحْمَةُ، فَإِنْ كَانَ غُدْوَةً صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُوْنَ أَلْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُمْسِيَ، وَإِنْ كَانَ مَسَاءً صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُوْنَ أَلْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُصْبِحَ)).

Amesema (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) ((Mtu anapomtembelea ndugu yake Muislamu mgonjwa basi hutembelea katika bustani ya Jannah mpaka atakapoketi, na anapoketi hufunikwa na Rahmah ikiwa ni asubuhi wanamtakia Rahmah Malaika sabini elfu mpaka jioni. Na ikiwa ni jioni wanamtakia Rahmah Malaika sabini elfu mpaka asubuhi)) [Swahiyh Ibn Maajah (1/244), Swahiyh At-Tirmidhiy (1/286)]

 

Juu ya hivyo ni fursa kwa Muislamu kuomba du’aa yake itakabaliwe. Aanze kwanza kumwombea mgonjwa du’aa zilizothibiti katika Sunnah kisha ajiombee nafsi yake:

 

عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ (رضي الله عنها)  قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِذَا حَضَرْتُمْ الْمَرِيضَ أَوْ الْمَيِّتَ فَقُولُوا خَيْرًا فَإِنَّ الْملآئِكَةَ يُؤَمِّنُونَ عَلَى مَا تَقُولُونَ)) قَالَتْ: فَلَمَّا مَاتَ أَبُو سَلَمَةَ أَتَيْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقُلْتُ:  يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ أَبَا سَلَمَةَ قَدْ مَاتَ قَالَ:  ((قُولِي: اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وَلَهُ وَأَعْقِبْنِي مِنْهُ عُقْبَى حَسَنَةً)) قَالَتْ: فَقُلْتُ فَأَعْقَبَنِي اللَّهُ مَنْ هُوَ خَيْرٌ لِي مِنْهُ مُحَمَّدًا (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)

Imepokelewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mnapohudhuria mgonjwa au maiti basi semeni yaliyo mema kwani Malaika wanaitikia ‘Aamiyn’ msemayo)). Akasema: Alipofariki Abu Salamah nilimwendea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikasema:  Ee Rasuli wa Allaah! Abu Salamah amefariki. Akasema: ((Sema: ‘Allaahumma-ghfir-liy wa lahu wa a-’qibniy minhu ‘uqba hasanah’ [Ee Allaah, nighufurie pamoja naye na nilipie baada yake badali iliyo njema])). Akasema:  Akanilipa Allaah ambaye ni mbora zaidi kuliko yeye; (ambaye ni) Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  [Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]

 

 

 

16. Du’aa Za Watu Baada Ya Mja Kutolewa Roho:

 

Lilothibiti pale mtu anapotolewa roho ni kumuombea maiti du’aa na kujiombea kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:

 

  عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ (رضي الله عنها) قَالَتْ: دَخَلَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) عَلَى أَبِي سَلَمَةَ وَقَدْ شَقَّ بَصَرُهُ فَأَغْمَضَهُ ثُمَّ قَالَ: ((إِنَّ الرُّوحَ إِذَا قُبِضَ تَبِعَهُ الْبَصَرُ)) فَضَجَّ نَاسٌ مِنْ أَهْلِهِ فَقَالَ: ((لاَ تَدْعُوا عَلَى أَنْفُسِكُمْ إلاَّ بِخَيْرٍ فَإِنَّ الْمَلآئِكَةَ يُؤَمِّنُونَ عَلَى مَا تَقُولُونَ)) ثُمَّ قَالَ: ((اللَّهُمَّ اغْفِرْ  لإَبِي سَلَمَةَ وَارْفَعْ دَرَجَتَهُ فِي الْمَهْدِيِّينَ، وَاخْلُفْهُ فِي عَقِبِهِ فِي الْغَابِرِينَ، وَاغْفِرْ لَنَا وَلَهُ يَا رَبَّ الْعَالَمِينَ، وَافْسَحْ لَهُ فِي قَبْرِهِ وَنَوِّرْ لَهُ فِيهِ)) 

Imepokelewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa Abuu Salamah akiwa macho yake ya wazi kabisa. Akayafunga na akasema: ((Hakika roho inapotolewa, macho yanafuatia [kupoteza uoni)). Baadhi ya watu katika familia yake wakalia na kuomboleza [kwa sauti]. Akasema: ((Msijiombee nafsi zenu ila ya khayr kwani Malaika huitikia ‘Aamiyn’ kwa myasemayo)). Kisha akasema: ((Allaahumma-Ghfir-li abiy Salamah, warfa’ darajaatahu fil-Mahdiyyiyn, wakhluf-hu fiy ‘aqibihi fil-ghaabiriyn, wa Ghfir-lanaa walahu yaa Rabbal ‘Aalamiyn, wafsah lahu fiy qabrihi, wa Nawwir lahu fiyhi  [Ee Allaah, Mghufurie Abuu Salamah, mpandishe daraja yake pamoja na walioongoka, na mfuatilishie katika kizazi chake wanaobakia, na Tughufurie pamoja naye ee Rabb wa walimwengu, na mpanulie kaburi lake na mtilie mwanga humo]))  [Muslim]

 

 

 

17. Du’aa Mwezi Wa Ramadhwaan:

 

Mwezi wa Ramadhwaan unatambulikana pia kuwa ni mwezi wa du’aa kwa vile Aayah kuhusu kuomba du’aa imetanguliwa na Aayah za Swawm [Al-Baqarah: 183-186]. Vilevile ni mwezi ambao milango ya Jannah hufunguliwa, milango ya Moto hufungwa na mashaytwaan hufungwa minyororo:

 

عن أبي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قال: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِذَا دَخَلَ رَمَضَانُ فُتِّحَتْ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ جَهَنَّمَ وَسُلْسِلَتْ الشَّيَاطِينُ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Inapoingia Ramadhwaan, milango ya Jannah hufunguliwa, milango ya Moto wa Jahannam hufungwa na mashaytwaan hufungwa minyororo)) [Al-Bukhaariy, An-Nasaaiy]

 

Kwa hivyo, nyoyo za Waislamu hubakia katika taqwa na twaa’ah (utiifu), hali ambayo ina matumaini makubwa ya kutakabaliwa du’aa. Kwa hiyo Muislamu ajitahidi kuomba du’aa kwa wingi nyakati zote za Siku za Ramadhwaan khaswa kuomba aghufuriwe dhambi zake:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)) مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayefunga Ramadhwaan kwa iymaan na kutarajia malipo ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

18. Du’aa Laylatul-Qadr:

 

Masiku kumi ya mwisho katika mwezi wa Ramadhwaan kunapatika usiku mtukufu, wenye baraka wa Laylatul-Qadr ambao umejaa fadhila kama zilivyothibiti katika Qur-aan na Sunnah. Ni fursa ya Muislamu awe macho usiku wake kuomba aghufuriwe madhambi yake:

 

عن أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ قَامَ لَيْلَةَ الْقَدْرِ إيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ)) 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayesimama usiku wa Laylatul-Qadr kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy (1910) na Muslim (760)]  

 

Na du’aa muhimu usiku huo mtukufu ni kuomba msamaha:

 

  عَنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) أَنَّهَا قَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَرَأَيْتَ إِنْ وَافَقْتُ لَيْلَةَ الْقَدْرِ مَا أَدْعُو؟ قَالَ: ((تَقُولِينَ: اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, nitakapojaaliwa kuupata usiku wa Laylatul-Qadr niombe nini?   Akasema: ((Sema: Allaahumma Innaka 'Afuwwun Tuhibbul-'afwa fa'-fu 'anniy. [Ee Allaah Hakika Wewe Ndiye Mwenye kusamehe Unapenda kusamehe basi nisamehe))  [Swahiyh Ibn Maajah (3119)]

 

 

 

19. Du’aa Wakati Wa Kusoma Qur-aan:

 

Muislamu anaposoma Qur-aan, anapopitia Aayah zenye kubashiriwa Jannah, basi aiombe Jannah, na anapopitia Aayah za Moto, aombe kujikinga nao. Na anapopitia Aayah zenye maonyo ya adhabu za Allaah aombe kujikinga na adhabu za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) duniani na Aakhirah na aombe Rahmah za Allaah. Hivyo ni kufuata Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عن ‏حُذَيْفَةَ بِنْ اليمان (رضي الله عنه): أنَّ النَّبِيَّ‏ ‏(صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ‏) كَانَ ‏إِذَا مَرَّ بِآيَةِ رَحْمَةٍ سَألَ، وَإِذَا مَرَّ بِآيَةِ عَذَابٍاسْتَجَارَ، وَإِذَا مَـرَّ بِآيَةٍ فِيهَـا تنزيهٌ للَّهِ سبَّحَ

Imepokelewa kutoka kwa Hudhayfah bin Al-Yamaani (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapopitia Aayah ya Rahmah aliomba (Rahmah), na alipopitia Aayah ya adhabu aliomba kujikinga, na alipopitia Aayah zenye kumtakasa Allaah alimsabbih)) [Swahiyh Ibn Maajah (1119)]

 

Na katika riwaayah nyingine:

 

كان إذا مرَّ بآيةِ خوفٍ تعوَّذَ، و إذا مرَّ بآيةِ رَحمةٍ سألَ، و إذا مرَّ بآيةٍ فيها تَنزيهُ اللهِ سبَّحَ

Alikuwa anapopitia Aayah ya khofu, alijikinga, na alipopitia Aayah ya Rahmah aliomba (Rahmah), na alipopitia Aayah ya kumtakasa Allaah, alimsabbih)) [Swahiyh Al-Jaami’ (4782)]

 

Pia:

 

أَنَّهُ ‏صَلَّى إِلَى جَنْبِ النَّبِيِّ (‏صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ‏) ‏لَيْلَةً فَقَرَأ فَكَانَ إذَا مَرَّ بِآيَةِ عَذَابٍ وَقَفَ وَتَعَوَّذَ وَإذَا مَرَّ بِآيَةِ رَحْمَةٍ وَقَفَفَدَعَا

Kwamba ameswali pembeni na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku mmoja, akasoma akawa kila anapopitia Aayah ya adhabu alisita na akajikinga, na alipopitia Aayah ya Rahmah alisita akaomba. [Swahiyh An-Nasaaiy (1007)]

 

 

 

20. Du’aa Katika Masiku Kumi Ya Dhul-Hijjah:

 

Masiku kumi ya mwezi wa Dhul-Hijjah ni matukufu mno kwa sababu ‘amali yoyote ile inayotendwa humo ni kipenzi kabisa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ (رضي الله عنهما) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم): ((مَا مِنْ أَيَّامٍ الْعَمَلُ الصَّالِحُ فِيهِنَّ أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ مِنْ هَذِهِ الأَيَّامِ الْعَشْرِ)) فَقَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ: ولاَ الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((ولاَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ إلاَّ رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فَلَمْ يَرْجِعْ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْءٍ))

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna siku ambazo vitendo vyake vyema Anavipenda Allaah kama siku kumi hizi)) [siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah] Akaulizwa, je, hata Jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyekwenda na nafsi yake na mali yake ikawa hakurudi na kimojawapo)) [Al-Bukhaariy].

 

Na kwa vile kuomba du’aa ni ‘amali tukufu kabisa mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama ilivyothibiti:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اللَّهِ تَعَالَى مِنْ الدُّعَاءِ))  

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna kitu kitukufu mbele ya Allaah Ta’aalaa kama du’aa)) [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad, na amesema At-Tirmidhiy: Hasan Ghariyb na Ibn Hibbaan na Al-Haakim wameipa daraja ya Swahiyh, na ameiwafiki Adh-Dhahaabiy na Al-Albaaniy ameipa daraja ya Hasan katika Swahiyh Al-Adaab Al-Mufrad, na pia Swahiyh At-Tirmidhiy (3370), Swahiyh Al-Jaami’ (5392)]

 

Basi bila shaka kuomba du’aa itazidi kuwa ni kipenzi Kwake Allaah Ta'aalaa.

 

Zifuatazo ni nyakati nyiginezo na sehemu mbalimbali za kuomba du’aa kwa mukhtasari. Lakini Muislamu anaweza kuomba du’aa zake wakati wowote pale anapotaka, ila katika au sehemu, au hali hizi huwa ni makhsusi kutokana na dalili kuwa kuna uzito wa du’aa kutakabaliwa: [Taz. Ad-Du’aa wa yaliyhi Al-‘Ilaaj Bir-Ruqyaa Minal-Kitaabi was-Sunnah – Sa’iyd bin ‘Aliy Al-Qahtwaaniy]

 

 

21. Du’aa katika kusoma Suwratul-Faatihah.

 

22. Du’aa baada ya kusema ‘Laa ilaaha illa Anta Subhaanaka inniy kuntu minadhw-dhwaalimyn’.

 

23. Du’aa baada ya kutaja Jina Tukufu la Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

24. Du’aa ya mwenye kutekeleza Hajj.

 

25. Du’aa ya mwenye kutekeleza ‘Umrah.

 

26. Du’aa katika Twawaaf.

 

27. Du’aa katika jabali la Swafaa.

 

27. Du’aa katika jabali la Marwah.

 

28. Du’aa baina ya majabali ya Swafaa na Marwah.

 

29-Du’aa katika Mash-‘aril-Haraam  (Muzdalifah).

 

30. Du’aa siku ya ‘Arafah.

 

31. Du’aa katika kurusha vijiwe katika Jamarah ndogo.

 

32. Du’aa katika kurusha vijiwe Jamarah la wastani (katikati).

 

33. Du’aa katika kurusha vijiwe Jamarah kubwa.

 

34. Du’aa wanapojumuika Waislamu katika vikao vya kumdhukuru Allaah.

 

 

 

 

 

Share

12-Wewe Pekee Tunakuabudu: Wasiylah Na Tawassul

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

12 - Wasiylah Na Tawassul

 

 

 

Maana ya Wasiylah:

 

Kwanza:  Ni daraja au cheo cha juu kabisa atakachopewa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) huko Jannah kutokana na Hadiyth:

   

 عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ (رضي الله عنه)  أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((إِذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا, ثُمَّ سَلُوا اللَّهَ لِي الْوَسِيلَةَ فَإِنَّهَا مَنْزِلَةٌ فِي الْجَنَّةِ لاَ تَنْبَغِي إِلاَّ لِعَبْدٍ مِنْ عِبَادِ اللَّهِ وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُوَ فَمَنْ سَأَلَ لِي الْوَسِيلَةَ حَلَّتْ لَهُ الشَّفَاعَةُ))

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin 'Amr bin Al-'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mnapomsikia Muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni kwani atakayeniswalia Swalaah moja, Allaah Atamswalia mara kumi, kisha niombeeni kwa Allaah Al-Wasiylah  kwani hiyo ni daraja au cheo ambacho mja mmoja pekee wa Allaah  atakayefikia, na nataraji niwe mimi, basi atakayeniombea Wasiylah atastahiki kupata Shafaa-‘ah (uombezi)) [Muslim]

 

Pili:  Ni njia ya kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa twaa’ah na ‘ibaadah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣٥﴾

Enyi walioamini! Mcheni Allaah na tafuteni njia za kumkurubia; na fanyeni jihaad katika njia Yake ili mpate kufaulu. [Al-Maaidah: 35]

 

‘Ulamaa wamekubaliana kuhusu maana ya wasiylah kwamba ni kufuata maamrisho na kujiepusha na aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili kupata radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema kuhusu Aayah hiyo ya Al-Maaidah 35:

“Allaah Anawaamrisha waja Wake Waumini wamkhofu Yeye kwa taqwa ambayo inapotajwa na vitendo vya utiifu, inamaanisha kujiepusha na yaliyoharamishwa na kuacha yote yaliyokatazwa.

 

Kisha Akasema:

وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ

tafuteni njia za kumkurubia 

 

Sufyaan Ath-Thawriy amepokea kutoka kwa Twalhah, kutoka kwa ‘Atwaa, kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba ni: njia za kujikurubisha. Na akasema hivyo Mujaahid na Abu Waail na Al-Hasan na Qataadah na ‘Abdullaah bin Kathiyr na As-Sudiy na Ibn Zayd na wengineo wamesema maana hiyo hiyo ya Al-Wasiylah.  Qataadah amesema kuwa Aayah inamaanisha:  Tafuteni njia za kujikurubisha Kwake na mtiini Yeye na tendeni 'amali za kumridhisha. Na Ibn Zayd akasoma:

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا ﴿٥٧﴾

Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha, yupi miongoni mwao awe karibu zaidi na wanataraji rahmah Yake, na wanakhofu adhabu Yake. Hakika adhabu ya Rabb wako ni ya kutahadhariwa daima. [Al-Israa: 57]

 

Na hivi ndivyo ambavyo wamesema hawa Maimaam, hakuna khitilafu baina ya Mufassiriyn (wafasiri wa Qur-aan).” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema kuhusu maana ya:  

وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ

tafuteni njia za kumkurubia 

 

 “Na ombeni haja zenu kutoka kwa Allaah kwani Yeye Pekee Ambaye Anaweza kukupeni, na hii inabainisha kauli Yake Ta’aalaa:

 

إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ وَاعْبُدُوهُ

Hakika wale mnaowaabudu badala ya Allaah hawakumilikiini riziki; basi tafuteni riziki kwa Allaah, na mwabuduni Yeye [Al-‘Ankabuwt: 17]

 

Na kauli Yake:

وَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ ۗ

Na muombeni Allaah fadhila Zake [An-Nisaa: 32]

 

Na katika Hadiyth:

((وَإِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلْ اللَّهَ))

((Unapoomba basi muombe Allaah))  [Ahmad, Swahiyh At-Tirmidhiy (2516)]

 

Tawassul ni kuomba haja au du’aa kwa kutumia njia za kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Na tawassul ziko aina mbili; zinazokubalika katika shariy’ah ambazo zinatokana na mafundisho sahihi ya Qur-aan na Sunnah na zisizokubalika, ambazo ni zile zilizotoka nje ya mafundisho sahihi ya Qur-aan na Sunnah na hivyo hugeuka kuwa ni tawassul za shirki au bid’ah.

 

 

 

 

Share

13-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Thanaa Na Kumswalia Nabiy

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Zinazokubalika

 

13-Kutawassal Kwa Thanaa Ya Allaah 

Na kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

 

 

Thanaa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) maana yake ni kumtaja Allaah Ta'aalaa kwa majina Yake mazuri na Sifa Zake Zilizotukuka, na Matendo Yake adhimu  na kumsifu, kumhimidi, kumpwekesha na kumtukuza Allaah kwa maneno yenye kudhihirisha utukufu Wake ('Azza wa Jalla) na neema na fadhila Zake. Nayo yanapatikana katika Aayah nyingi za Qur-aan na katika Hadiyth za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Mifano michache katika Qur-aan ni kama kumwita Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kusema

“Yaa…

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

Mwanzilishi wa mbingu na ardhi [Aayaat kadhaa katika Suwraa kadhaa imetaja]

 

 عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْكَبِيرُ الْمُتَعَالِ ﴿٩﴾

Mjuzi wa ghayb na dhahiri, Mkubwa wa dhati vitendo na sifa, Mwenye Uluwa Aliyejitukuza kabisa. [Ar-Ra’d: 9]

 

 

اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ

“Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, [Aal-‘Imraan: 26]

 

رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ۩﴿٢٦﴾

Rabb wa Al-‘Arsh adhimu” [An-Naml: 26]

 

 

Inafaa pia mwombaji kuanza kwa thanaa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa mfano kusema:

 

‘Allahumma inniy as-aluka bianna Lakal-Hamdu laa ilaaha illa Anta Wahdaka laa shariyka Laka, (Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kwamba Himdi ni Zako, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Huna mshirika.” Na kadhaalika.

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoamka usiku akimhimidi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kumtukuza kwa kusema:

 

اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ نُورُ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ ، وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ قَيِّمُ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ ، وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ الْحَقُّ ، وَوَعْدُكَ حَقٌّ ، وَقَوْلُكَ حَقٌّ ، وَلِقَاؤُكَ حَقٌّ ، وَالْجَنَّةُ حَقٌّ ، وَالنَّارُ حَقٌّ ، وَالسَّاعَةُ حَقٌّ ، وَالنَّبِيُّونَ حَقٌّ ، وَمُحَمَّدٌ حَقٌّ ، اللَّهُمَّ لَكَ أَسْلَمْتُ ، وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ ، وَبِكَ آمَنْتُ ، وَإِلَيْكَ أَنَبْتُ ، وَبِكَ خَاصَمْتُ ، وَإِلَيْكَ حَاكَمْتُ : فَاغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ وَمَا أَخَّرْتُ ، وَمَا أَسْرَرْتُ وَمَا أَعْلَنْتُ ، أَنْتَ الْمُقَدِّمُ وَأَنْتَ الْمُؤَخِّرُ ، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ - أَوْ لَا إِلَهَ غَيْرُكَ  

Allaahumma Lakal-Hamdu Anta Nuwrus-samaawati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Anta Qayyimus-samaawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Antal-Haqqu, wa wa’dukal-haqqu, wa qawlukal-haqqu, wa liqaaukal-haqqu, wal-Jannata haqqun, wan-naaru haqqun, was-saa’atu haqqun,  wan-nabiyyuwna haqqun, wa Muhammadun  haqqun, Allaahumma Laka aslamtu, wa ’Alayka tawakkaltu, wabika aamantu, wa Ilayka anabtu, wabika khaaswamtu, wa Ilayka haakamtu, faghfir liy maa qaddamtu wamaa akh-khartu, wamaa asrartu, wamaa a’lantu, Antal-Muqaddimu wa Antal-Muakh-khiru laa ilaaha illa Anta. (Au) laa ilaaha ghayruka

 

Ee Allaah Himdi ni Zako  Wewe Ndiye Nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Himdi ni Zako Wewe Ndiye Wewe Ndiye Msimamizi wa  mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Himdi ni Zako Wewe ni Haki na ahadi Yako ni ya kweli, na neno Lako ni la kweli, na kukutana na Wewe ni kweli, na Jannah ni kweli, na moto ni kweli, na Manabii ni kweli, na Muhammad ni kweli, na Qiyaamah ni kweli.  Ee Allaah, Kwako nimejisalimisha, na kwako nimetawakali, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimerejea kutubia. Na kwa ajili Yako (au kwa hoja na dalili Zako) nimetetea (maadui Wako). Na nimeelekea Kwako kukufanya Wewe ni Hakimu Wangu (kuhukumu baina yetu). Basi nighufurie  niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza; Wewe Ndiye Al-Muqaddimu (Mwenye kutanguliza) na Al-Muakh-khiru (Mwenye kuchelewesha), hapana Muabudiwa wa haki ila Wewe; Wewe Ndiye Ilaah wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe (au) Hapana mwabudiwa wa haki ghairi Yako.” [Al-Bukhaariy (1120), Muslim (769) na wengineo]

 

Inafaa pia kumhimidi na kumtukuza kwa kauli au maneno mengineyo yenye kudhihirisha utukufu Wake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) lakini yawe maneno ambayo hayavuki mipaka yakatoka nje ya ’Aqiydah sahihi.

  

Kisha unamswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyothibiti katika Hadiyth zifuatazo:

 

 عن فَضَالَةَ بْنَ عُبَيْدٍ (رضي الله عنه) يَقُولُ: سَمِعَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) رَجُلاً يَدْعُو فِي صلاَتِهِ لَمْ يُمَجِّدْ اللَّهَ تَعَالَى وَلَمْ يُصَلِّ عَلَى النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((عَجِلَ هَذَا)) ثُمَّ دَعَاهُ فَقَالَ لَهُ أَوْ لِغَيْرِهِ: ((إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِتَمْجِيدِ رَبِّهِ جَلَّ وَعَزَّ وَالثَّنَاءِ عَلَيْهِ ثُمَّ  يُصَلِّي عَلَى النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ ثُمَّ يَدْعُو بَعْدُ بِمَا شَاءَ))

Kutoka kwa Fadhwaalah bin ‘Ubayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimsikia mtu akiomba katika Swalaah yake hamtukuzi Allaah (Ta’aalaa) wala hamswalii Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ameharakiza huyu)). Kisha akamwita akamwambia yeye au mwengine: ((Anaposwali mmoja wenu basi aanze kwa kumtukuza Rabb wake (‘Azza wa Jalla) amsifu kisha amswalie Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kisha aombe baadaye anachokitaka)) [Abuu Daawuwd, Ahmad na ameipa daraja ya Swahiyh Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (1481)]

 

Na katika riwaaya nyingine pia: 

 

عن فَضَالَةَ بْنَ عُبَيْدٍ (رضي الله عنه)  يَقُولُ: "سَمِعَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) رَجُلاً يَدْعُو فِي صَلاَتِهِ لَمْ يُمَجِّدْ اللَّهَ وَلَمْ يُصَلِّ عَلَى النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ), فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((عَجِلْتَ أَيُّهَا الْمُصَلِّي)) ثُمَّ عَلَّمَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ ( صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ).  وَسَمِعَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) رَجُلاً يُصَلِّي فَمَجَّدَ اللَّهَ وَحَمِدَهُ وَصَلَّى عَلَى النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ادْعُ تُجَبْ وَسَلْ تُعْطَ))

Kutoka kwa Fadhwaalah bin ‘Ubayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kamsikia mtu akiomba katika Swalaah yake hamtukuzi Allaah (Ta’aalaa) wala hamswalii Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Umeharakiza ee mwenye kuswali)). Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawafunza. Na akamsikia mtu anaswali akamtukuza Allaah na Akamsifu, na akamswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Omba du’aa utakaitikiwa, na omba utapewa)) [Swahiyh An-Nasaaiy (1283)]

 

 

 

 

Share

14-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Kutawassal Kwa Majina Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Zinazokubalika

 

14-Kutawassal Kwa Majina Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

 

 

 

Kutawassal kwa Majina Mazuri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama Anavyotuamrisha Mwenyewe:

 

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٨٠﴾

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanamili katika kukadhibisha Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A’raaf: 180]

 

Na kama alivyoomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika du’aa inayotaja:

 

  أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيْتَ بِهِ نَفْسَكَ، أَوْ عَلَّمْتَهُ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ، أَوْ أَنْزَلْتَهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ اسْتَأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الْغَيْبِ عِنْدَكَ،

As-aluka bikullismin huwa Laka, sammayta bihi Nafsaka aw Anzaltahu fiy Kitaabika, aw ‘Allamtahu ahadan min Khalqika, awis-staa-tharta bihi fiy ‘ilmil-ghaybi  ‘In-daka,

 

Nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako Ulilojiita Kwako Mwenyewe au Uliloliteremsha katika Kitabu Chako, au Ulilomfundisha yeyote yule kati ya viumbe Vyako, au Ulilolihifadhi Wewe mwenyewe (na kujihusisha kulijua) katika ’ilmu ya ghayb Kwako. [Ameipokea Ahmad (1/391) [452], Al-Haakim (1/509) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (199) na Al-Kalim Atw-Twayyib (124)]

 

Na pia anaweza mtu kusema: “Yaa Dhal-Jalaali wal-Ikraami” (Ee Mwenye Ujalali na ukarimu) kama alivyopokea Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

  ((‏‏ألِظُّوا بِيَا ذَا الْجَلالِ وَالإكْرَام ))

((Dumisheni kwa wingi: Yaa-Dhal-Jalaali wal-Ikraami)) [Swahiyh Sunan At-Tirmidhiy (2797)[

 

Na miongoni mwa Majina Yake (‘Azza wa Jalla) ni: “Ar-Rahmaan-Ar-Rahiym” (Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu). Anaweza kuanza mtu du’aa yake kwa kusema: 

 

Allaahumma inniy as-aluka biannaka Antar-Rahmaanu-Rahiym” (Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kwa kuwa Wewe ni Mwenye rahmah, Mwenye kurehemu)

 

Nitakabalie haja yangu kadhaa.”

 

Au kusema:

Yaa Arhamar-Raahimiyn”

(Ee Mbora zaidi wa kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu)

 

kama walivyoomba baadhi ya Manabiy wakatabaliwa du’aa zao:

 

وَأَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ أَنِّي مَسَّنِيَ الضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿٨٣﴾

Na Ayyuwb alipomwita Rabb wake: “Hakika mimi imenigusa dhara, Nawe Ndiye Mbora zaidi wa kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu”.

 

 

فَاسْتَجَبْنَا لَهُ فَكَشَفْنَا مَا بِهِ مِن ضُرٍّ ۖ وَآتَيْنَاهُ أَهْلَهُ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَذِكْرَىٰ لِلْعَابِدِينَ ﴿٨٤﴾

Tukamuitikia basi Tukamuondoshea dhara aliyokuwa nayo, na Tukampa ahli zake na mfano wao pamoja nao; ni rahmah kutoka Kwetu na ni ukumbusho kwa wanaoabudu (Allaah). [Al-Anbiyaa: 83-84]

 

 

Pia utumie Sifa za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kumuomba jambo makhsusi ulitakalo mfano:

Yaa Razzaqu, niruzuku kadhaa wa kadhaa.”

 

Yaa Ghafuwuru, nighufurie madhambi yangu.”

 

Yaa ‘Afuwwu, nisamehe.” Kama vile du’aa ya usiku wa Laylatul-Qadr:

 

اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي

Allaahumma Innaka ‘Afuwwun Tuhibbul-‘afwa fa’fu ‘anniy

Ee Allaah, hakika Wewe Mwingi wa kusamehe Unapenda kusamehe basi nisamehe [At-Tirmidhiy, Ahmad, Ibn Maajah, Swahiyh At-Tirmidhiy (3/170)]

 

Yaa Tawwaabu, nipokelee tawbah yangu.”

 

Yaa Hafiydhwu, nihifadhi kutokana na adui yangu, au kadhaa wa kadhaa.”

 

Yaa Wahhaabu, nitunukie (mke au mume mwema, au mwana…)

 

Yaa Fattaahu, nifungulie jambo langu kadhaa, au nihukumie jambo langu kadhaa.”

 

Yaa Shakuwru, nipokelee shukurani zangu Kwako…

 

Yaa Hamiydu, ee Mwenye kustahiki kuhimidiwa…

 

Yaa Shaafi’u, niponyeshe maradhi yangu.”

 

Yaa Qadiyru, niwezeshee jambo langu kadhaa.”

 

 

Na Sifa Zake nyinginezo utumie katika ile hali makhsusi inayohusiana na Sifa hiyo.

 

Pia unaweza kumwita kwa Sifa ambazo hakuna awezaye kuzimiliki mfano du’aa zifuatazo za Sunnah:

يَا مُقَلِّبَ الْقُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِك

Yaa muqallibal quluwbi, thabbit qalbiy ‘alaa Diynika

Ee Mwenye kupindua nyoyo, Thibitisha moyo wangu katika Dini Yako. [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad, Al-Haakim  na Swahiyh Al-Jaami’ 7987]

 

 

 اللَّهُمَّ مُصَرِّفَ الْقُلُوبِ صَرِّفْ قُلُوبَنَا عَلَى طَاعَتِك

Allaahumma Muswarrifal quluwbi, swarrif quluwbanaa ‘alaa twaa’atika

Ee Allaah, Mwenye kugeuza nyoyo, zigeuzi nyoyo zetu katika utiifu Wako  [Muslim]

 

Na pia unaweza kutumia Sifa kama zifuatazo:

 

Yaa Faarijal-hammi, nifarijie dhiki yangu kadhaa.”

 

Yaa Kaashifal-ghammi, niondoshee huzuni, au balaa, au janga kadhaa wa kadhaa.”

 

Yaa Qadhwiyal-hajaat, nikidhie, nitimizie haja zangu kadhaa wa kadhaa.”

 

Kisha unaweza kumalizia du’aa kwa kumwita Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

Yaa Kariymu, Ya Samiy’u, Yaa Qariybu, Ya Mujiybu

 (Ee Mkarimu, Ee Mwenye kusikia yote daima, Ee Uliye karibu kwa Ujuzi Wako, Ee Mwenye kuitikia)  Niitikie du’aa yangu kadhaa”.  

 

Na kadhaalika katika Majina na Sifa Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

 

 

 

Share

15-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Kutawassal Kwa Jina Adhimu Kabisa La Allaah

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Zinazokubalika

 

15-Kutawasal Kwa Jina Adhimu (Tukufu) Kabisa La Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

 

 

Hakuna ajuaye Jina Adhimu kabisa la Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Lakini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametudokezea kama ifuatavyo:  

 

 عَنْ الْقَاسِمِ عَنْ أَبِي أُمَامَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((اسْمُ اللَّهِ الأَعْظَمُ الَّذِي إِذَا دُعِيَ بِهِ أَجَابَ فِي سُوَرٍ ثَلاَثٍ: الْبَقَرَةِ، وَآلِ عِمْرَانَ، وَطه))

Kutoka kwa Al-Qaasim, kutoka kwa Abuu Umaamaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jina Adhimu kabisa la Allaah  ambalo likiombewa kwalo Anaitikia, limo katika Suwrah tatu; Al-Baqarah, Aal-‘Imraan, na Twaahaa)) [Swahiyh Ibn Maajah (3124), Swahiyh Al-Jaami’ (979)]

 

Katika Suwrah hizo Majina mawili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ambayo yamelingana kuweko kwa pamoja ni “Al-Hayyu”, “Al-Qayyuwm” na Akayataja tena hayo pamoja na  Majina ya Allaah, Ilaah, Al-Waahid, Ar-Rahmaan, Ar-Rahiym:

 

عَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ يَزِيدَ (رضي الله عنها) أَنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((اسْمُ اللَّهِ الأَعْظَمُ فِي هَاتَيْنِ الأَيَتَيْنِ ((وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ)) وَفَاتِحَةِ آلِ عِمْرَانَ ((الم  اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ))

Kutoka kwa Asmaa bint Yaziyd  (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jina Adhimu kabisa la Allaah limo katika Aayah zifuatazo: “Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.” (Al-Baqarah: 163) na na ufunguo (mwanzo) wa ‘Aal-‘Imraan: “Alif Laam Miym. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliye hai daima, Msimamia kila kitu. [Aal-‘Imraan: 1-2] [Swahiyh At-Tirmidhiy (3478), Swahiyh Ibn Majaah (3123), Swahiyh Al-Jaami’ (980),  Swahiyh Abiy Daawuwd (1496) Swahiyh At-Targhiyb (1642)]

 

Naye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba du’aa kwa kutaja baadhi ya Majina hayo mfano du’aa yake ambayo alikuwa anapopatwa dhiki au huzuni akiomba:

   يَا حَيُّ يَا قَيُّومُ بِرَحْمَتِكَ أَسْتَغِيثُ

 

Yaa Hayyu Yaa Qayyuwm bi-Rahmatika astaghiythu

 

(Ee Uliye Hai daima, Msimamia wa kila jambo, rahmah Zako naomba uokovu)  [At-Tirmidhiy (3524), An-Nasaaiy fiy As-Sunan Al-Kubraa(6/147), Al-Haakim (1/730) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy]

 

Pia akaashiria Majina ya Allaah (Subhaanahuu wa Ta’aala)  mengineyo katika Hadiyth:

 

‏‏عن ‏أنس بن مالك (رضي الله عنه) قال: ‏سَمِعَ النَّبِيُّ ‏(صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ‏رَجُلاً يَقُولُ: ((اللَّهُمَّ إنِّي أسْألُكَ بِأنَّ لَكَ الْحَمْدَلا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ وَحْدَكَ لا شَرِيكَ لَكَ،‏‏ الْمَنَّانُ،‏ ‏بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالأرْضِ ذُو الْجَلالِ وَالإِكْرَام)) فقال:‏ ((‏لَقَدْ سَألَ اللَّهَ بِاسْمِهِ الأعْظَمِ الَّذِي إذَا سُئِلَ بِهِ أعْطَى وَإذَا دُعِيَ بِهِ أجَابَ))

 

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimsikia mtu akiomba:

 

اللَّهُمَّ إنِّي أسْألُكَ بِأنَّ لَكَ الْحَمْدَلا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ وَحْدَكَ لا شَرِيكَ لَكَ،‏‏ الْمَنَّانُ،‏ ‏بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالأرْضِ ذُو الْجَلالِ وَالإِكْرَام)

 

Allaahumma inniy As-alauka bianna Lakal-Hamdu laa ilaaha illa Anta Wahdaka laa shariyka Laka. Al-Mannaanu, Badiy'us-samaawati wal-ardhwi, Dhul-Jalaali  wal-Ikraami

 

(Ee Allaah  hakika mimi nakuomba kwamba Himdi ni Zako, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, Huna  mshirika, Al-Mannaanu (Mwingi wa neema, Mwingi wa kutoa na  kutunuku, na kufadhili na kuwafanyia ihsaan waja Wake, Mwanzishi wa mbingu na ardhi, Mwenye Ujalali na Ukarimu”.

 

 Akasema: ((Kwa yakini amemuomba Allaah kwa Jina Lake Adhimu kabisa ambalo Akitakwa jambo kwalo Anatoa na Anapoombwa Huitikia))[Swahiyh Ibn Maajah (3126)]

 

 

Na pia akataja Majina mengineyo katika Hadiyth:

 

‏ ‏عن ‏عَبْدِ اللَّهِ بن بُرَيْدَةَ الأسْلَمِيِّ ‏عن‏ ‏أبِيهِ (رضي الله عنهما) ‏قال: ‏سَمِعَ النَّبِيُّ (‏صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ‏رَجُلاً يَدْعُو وَهُوَ يَقُولُ: "اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ‏ ‏كُفُوًا ‏‏أحَدٌ" فقال: ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَقَدْ سَألَ اللَّهَ بِاسْمِهِ الأعْظَمِ الَّذِي إذَا دُعِيَ بِهِ أجَابَ وَإذَا سُئِلَ بِهِ أعْطَى))   

 

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah Al-Aslamiyy, kutoka kwa baba yake (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimsikia mtu akiomba:

 

"اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ‏ ‏كُفُوًا ‏‏أحَدٌ" 

“Allaahumma inni as-aluka bianniy ash-hadu Annaka Anta-Allaahu laa ilaaha illa Anta Al-Ahadu Asw-Swamadu, Alladhiy lam Yalid walam Yuwlad walam Yakun Lahuu kufuwan ahad”.

 

(Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kwa kushuhudia kwamba hakika Wewe ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Mmoja, Aliyekamilika sifa za kila aina ya utukufu Wake, Mwenye kukusudiwa kwa haja zote, Ambaye Hakuzaa na wala Hakuzaliwa, Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye)

 

Akasema: ((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, amemuomba Allaah kwa Jina Lake Adhimu kabisa Ambalo Anapoombwa kwalo [du’aa] Anaitikia na Anapotakwa kwalo [jambo] Hutoa)) [Swahiyh Ibn Maajah (3125) Swahiyh At-Tirmidhy  (3475), Swahiyh Abi Daawuwd (1493), Swahiyh At-Targhiyb  (1640)]

 

 

 

Share

16-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Kutawassal Kwa Du'aa Ya Nabiy Yuwnus

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Zinazokubalika

 

16-Kutawassal Kwa Du'aa Ya Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam)

 

 

 

 

Du'aa ya Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam) ni sababu mojawapo kubwa ya kuitikiwa du’aa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam) baada ya kuwalingania watu wake katika Tawhiyd wakakanusha, aliwakimbia bila ya kupata idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hivyo akamkosea Rabb Wake. Baada ya kutupwa baharini kutoka katika jahazi aliyoipanda kwa ajili ya kukimbia mbali, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamuamrisha nyangumi ammeze bila ya kumla nyama yake au kumvunja mifupa yake. Akabakia tumboni mwa nyangumi kwa masiku kadhaa, akawa anaomba du’aa hiyo ya kujirudi kwa Rabb Wake.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

وَذَا النُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾

Na Dhan-Nuwn (Yuwnus) alipoondoka akiwa ameghadhibika, akadhani kwamba Hatutamdhikisha; akaita katika kiza kwamba: “Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Subhaanak! (Utakasifu ni Wako), hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.” [Al-Anbiyaa: 87]

 

Basi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamtakabalia:

فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُنجِي الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨٨﴾

Basi Tukamuitikia na Tukamuokoa kutokana na ghamu. Na hivyo ndivyo Tuwaokowavyo Waumini. [Al-Anbiyaa: 88]

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akathibitisha kwamba du’aa hiyo aliyoiomba Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam) ni du’aa inayosababisha kutakabaliwa du’aa:

 

عَنْ سَعْدٍ بن أبي وقاص (رضي الله عنه)  قَالَ:  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((دَعْوَةُ ذِي النُّونِ إِذْ دَعَا وَهُوَ فِي بَطْنِ الْحُوتِ: "لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنْ الظَّالِمِينَ" فَإِنَّهُ لَمْ يَدْعُ بِهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ فِي شَيْءٍ قَطُّ إِلاَّ اسْتَجَابَ اللَّهُ لَهُ))

Kutoka kwa Sa’d bin Abi Waqqaasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Du’aa ya Dhan-Nuwn (Nabiy Yuwnus 'Alayhis Salaam) alipoomba alipokuwa katika tumbo la nyangumi:

 

لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنْ الظَّالِمِينَ

“Laa ilaaha illa Anta Subhaanaka inniy kuntu minadhw-dhwaalimiyn”

 

basi hakika hakuna Muislamu aombaye kwayo kitu chochote kile ila Allaah Atamuitikia)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3505), Swahiyh Al-Jaami’ (3383), Takhriyj Al-Mishkaat Al-Maswaabiyh(2232), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (1744)]

 

Bila ya shaka du’aa ya Nabiy Yuwnus ('Alayhis-Salaam) inastahiki kuwa ni wasiylah ya kutakabaliwa du’aa kwa sababu du’aa hiyo imegawanyika katika sehemu tatu:

 

 

1. Kumpwekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ

Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe.

 

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema: “(Nabiy Yuwnus ‘Alayhis-Salaam) Amekiri Tawhiyd ya Uluwhiyyah ambayo inahusiana na aina mojawapo ya du’aa (Du’aa ya ‘ibaadah) kwa sababu ‘Ilaah’ Ndiye Mwenye kustahiki kuombwa aina zote mbili za du’aa; du’aa ya ‘ibaadah na du’aa ya mas-alah (jambo). Naye Ndiye Allaah Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye.” [Kuulizwa kwake Shaykh kuhusu du’aa ya Dhan-Nuwn]

 

 

2. Kumsabbih (kumtakasa) Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): Kwa maana kumtakasa Allaah ('Azza wa Jalla) kutokana na kila kasoro.

سُبْحَانَكَ

Subhaana! (Utakasifu ni Wako).

 

 

3. Mja kukiri madhambi:

إِنِّي كُنْتُ مِنْ الظَّالِمِينَ

 Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.

 

Akasema tena Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: “Kuhusu kauli yake: “Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu” Inahusiana na kukiri kwake dhambi, na hivyo ni kuomba maghfirah.”

 

Na Istighfaar (kuomba maghfirah) kuna faida tele kwa dalili kadhaa.

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا﴿١٠﴾

 “Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu; hakika Yeye ni Mwingi mno wa kughufuria.

 

يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا﴿١١﴾

 “Atakutumieni mvua tele ya kuendelea.”

 

 

وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا﴿١٢﴾

 “Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakupeni mito.” [Nuwh: 10-12]

 

 

 

 

Share

17-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Kutawassal Kwa Suwratul-Faatihah

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Zinazokubalika

 

17-Kutawassal Kwa Suwratul-Faatihah

 

 

 

 

Hii ni Suwrah tukufu kabisa katika Qur-aan, ina fadhila nyingi. Inaitwa Ummul-Kitaab (Mama wa Kitabu). Pia inaitwa Al-Faatihah (Ufunguo) kwa kuwa ni Suwrah ya mwanzo katika Muswhaf, na ni Suwrah inayopasa kusomwa katika kila rakaa ya Swalaah na bila kwayo, Swalaah haitimii. Inajulikana pia kwa majina yafuatayo: AlhamduliLLaah, Ummul-Qur-aan (Mama wa Qur-aan), Ash-Shifaa (Ponyo), Asw-Swalaah, Ar-Ruqya (tiba), Sab’ul-Mathaaniy (Aayah saba zinazokaririwa).

 

Na Allaah Ameigawa Suwrah hii sehemu mbili kama ilivyokuja maelezo yake katika Hadiyth Al-Qudsiy: 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ صَلَّى صَلاَةً لَمْ يَقْرَأْ فِيهَا بِأُمِّ الْقُرْآنِ فَهِيَ خِدَاجٌ)) ثَلاَثًا ((غَيْرُ تَمَامٍ)) فَقِيلَ لإِبِي هُرَيْرَةَ: إِنَّا نَكُونُ وَرَاءَ الإِمَامِ؟ فَقَالَ: اقْرَأْ بِهَا فِي نَفْسِكَ فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى قَسَمْتُ الصَّلاَةَ بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي نِصْفَيْنِ, وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ. فَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ (الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ) قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: حَمِدَنِي عَبْدِي, وَإِذَا قَالَ (الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ), قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: أَثْنَى عَلَيَّ عَبْدِي, وَإِذَا قَالَ (مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ) قَالَ: مَجَّدَنِي عَبْدِي, وَقَالَ مَرَّةً فَوَّضَ إِلَيَّ عَبْدِي, فَإِذَا قَالَ (إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ)  قَالَ: هَذَا بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ))  

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeswali Swalaah bila ya kusoma humo Mama wa Qur-aan, basi haijatimia)) (alikariri mara tatu “haijatimia”). Mtu mmoja akamwambia Abuu Hurayrah: Je, hata tukiwa nyuma ya Imaam? Akasema: Isome katika nafsi yako kwani nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Allaah Ta’aalaa Amesema: Nimeigawa Swalaah baina Yangu na mja Wangu nusu mbili, mja Wangu atapata yale aliyoyaomba. Mja anaposema “Al-HamduliLaah Rabb wa walimwengu.” Allaah Ta’aalaa Husema:  Mja Wangu amenihimidi. Na anaposema “Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu. ”Allaah Ta’aalaa Husema:  Mja wangu amenisifu na kunitukuza kwa wingi. Na anaposema “Mfalme wa Siku ya Malipo.” Allaah Ta’aalaa Husema: Mja wangu ameniadhimisha. Na mara moja alisema: Mja wangu ameniaminisha. Na anaposema “Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.” Husema: Hii ni baina Yangu na mja Wangu, na mja Wangu atapata kile alichokiomba. Na anaposema “Tuongoze njia iliyonyooka, njia ya wale Uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.”  Husema: Hii ni ya mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba)) [Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy,  An-Nasaaiy , Ibn Maajah, Maalik]    

  

 

Ibn Al-Qayyim amesema: “(Suwrah hii) imejumuisha baina Tawassul kwa Allaah (Ta’aalaa) kwa himdi na thanaa (kumsifu na kumtukuza kwa wingi) na kumuadhimisha, na kutawassal Kwake kwa kumfanyia Yeye ‘ibaadah na Tawhiyd (kumpwekesha Kwake). Kisha likaja ombi muhimu kabisa la kuombwa na la tamanio la kufaulu kabisa nalo ni hidaaya baada ya wasiylah mbili. Basi mwombaji kwayo ana uhakika wa wa kuitikiwa” [Madaarij As-Saalikiyn (1/24)]

 

 

Amesema pia: “Juu ya ufupi wake lakini inabeba aina zote tatu za Tawhiyd; Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Kumpwekesha Allaah katika Uola), Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (kumpwekesha Allaah katika ‘ibaadah), na Tawhiyd Al-Asmaa Wasw-Swifaat (Kumpwekesha Allaah katika Majina Na Sifa Zake).” [Madaarij As-Saalikiyn (1/24-27)]

 

 

Dalili ya Suwratul-Faatihah kuwa ni shifaa, ni kisa katika Hadiyth ifuatayo; kwa hiyo anaweza mtu kutawassal nayo ili aponyeshwe ugonjwa wake: 

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ (رضي الله عنه) قَالَ: كُنَّا فِي مَسِيرٍ لَنَا فَنَزَلْنَا فَجَاءَتْ جَارِيَةٌ فَقَالَتْ: "إِنَّ سَيِّدَ الْحَيِّ سَلِيمٌ وَإِنَّ نَفَرَنَا غَيْبٌ فَهَلْ مِنْكُمْ رَاقٍ؟" فَقَامَ مَعَهَا رَجُلٌ مَا كُنَّا نَأْبُنُهُ بِرُقْيَةٍ, فَرَقَاهُ فَبَرَأَ فَأَمَرَ لَهُ بِثَلاَثِينَ شَاةً وَسَقَانَا لَبَنًا فَلَمَّا رَجَعَ قُلْنَا لَهُ: "أَكُنْتَ تُحْسِنُ رُقْيَةً أَوْ كُنْتَ تَرْقِي؟" قَالَ: "لاَ مَا رَقَيْتُ إلاَّ بِأُمِّ الْكِتَابِ." قُلْنَا: "لاَ تُحْدِثُوا شَيْئًا حَتَّى نَأْتِيَ أَوْ نَسْأَلَ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)." فَلَمَّا قَدِمْنَا الْمَدِينَةَ ذَكَرْنَاهُ لِلنَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ: ((وَمَا كَانَ يُدْرِيهِ أَنَّهَا رُقْيَةٌ؟ اقْسِمُوا وَاضْرِبُوا لِي بِسَهْمٍ)) 

 

Amesimulia Abuu Sa'iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Tulikuwa katika safari tukateremka mahali, akaja kijakazi akasema: Bwana wetu ametafunwa na nge na wanaume wetu hawapo, je, yupo kati yenu tabibu? Akasimama pamoja naye mtu mmoja ambaye hatukudhania kuwa anajua ruqyah (utabibu). Akamtibu kwa ruqyah akapona. Akampa kondoo thelathini na akatupa maziwa tunywe (kama ni malipo). Aliporudi tukamwambia: Je, ulikuwa kweli unajua kutibu kwa ruqyah, au ulikuwa unabahatisha tu? Akasema: Hapana, bali nimemsomea Ummul-Kitaab (Suwrah Al-Faatihah). Tukasema: Tusiseme kitu hadi tumfikie au tumuulize Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Tulipofika Madiynah, tulimwelezea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Alijuaje kuwa (Al-Faatihah) ni ruqyah? Gawaneni na mnitolee sehemu (ya kondoo.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Ibn Al-Qayyim amesema: “(Suwrah Al-Faatihah) ni ufunguo wa Kitabu na Mama wa Kitabu na  Aayah saba zinazokaririwa, na shifaa kamili na dawa ya kunufaisha, na ruqya kamili, na ufungo wa utajiri na kufaulu, na hifadhi ya nguvu, na kinga ya dhiki na ghamu na khofu na huzuni kwa mwenye kuijua thamani yake na akaipa haki yake na akautumia vizuri uteremsho wake (Al-Faatihah) kwa ugonjwa wake na akajua njia ya kuiombea shifaa na kupata dawa kwayo na ni siri ambayo imekusudiwa kwa ajili yake….” [Zaad Al-Ma’aad (4/318)]

  

 

Amesema pia: “Nilikuwa na maumivu mabaya mno kiasi ilikaribia kunifanya nishindwe kutembea, na hivyo ilikuwa wakati wa twawaaf na kwengineko. Basi nikakimbilia kusoma Suwratul-Faatihah na kupangusa kwayo mahali pa maumivu. Ikawa kama kijiwe kinaanguka. Nikajaribu hiyvo mara kadhaa na nikawa nachukua gilasi ya maji ya zamzam nayasomea Al-Faatihah mara kwa mara kisha nakunywa. Nikapata nafuu na nguvu ambayo sijapatapo kuipata mfano wake katika dawa.” [Madaarij As-Saalikiyn (1/58)]

 

 

 

 

 

Share

18-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Kutawassal Kwa Aayah Katika Suwrah Az-Zumar

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Zinazokubalika

 

18-Kutawassa Kwa Aayah Katika Suwrah Az-Zumar

 

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 قُلِ اللَّـهُمَّ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ أَنتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِي مَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿٤٦﴾

Sema: “Ee Allaah Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghayb na dhahiri, Wewe Utahukumu baina ya waja Wako katika ambayo walikuwa wakikhitilafiana nayo.” [Az-Zumar: 46]

 

 

Dalili ni Hadiyth ifautayo pamoja na kauli ya  Sa’iyd bin Jubayr (Rahimahu Allaah) ambaye alikuwa ni miongoni mwa Taabi’uwn (waliofuatia baada ya Maswahaba):

 

عن أَبِي سَلَمَة بْن عَبْد الرَّحْمَن بْن عَوْف (رضي الله عنه) قَالَ: سَأَلْت عَائِشَة (رَضِيَ اللَّه عَنْهَا) بِأَيِّ شَيْء كَانَ النَّبِيّ (صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَسْتَفْتِح صَلاَته إِذَا قَامَ مِنْ اللَّيْل؟ قَالَتْ: كَانَ إِذَا قَامَ مِنْ اللَّيْل اِفْتَتَحَ صَلاَته ((اللَّهُمَّ رَبَّ جَبْرَائِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ. فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ. عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ. أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ. اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ).

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Salamah bin ‘Abdir-Rahmaan bin ‘Awf (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nilimuuliza ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Je, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifungulia Swalaah yake kwa kitu gani alipoamka usiku? Akasema: alikuwa anapoamka usiku anafungulia Swalaah yake kwa:

 

اللَّهُمَّ رَبَّ جَبْرَائِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ. فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ. عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ. أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ. اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيم

 

 ((Allaahumma Rabba Jibraaiyla wa Mikaaiyla wa Israafiyla, Faatwiras-samaawaati wal ardhw, ’Aalimal ghaybi wash-shahaadah, Anta Tahkmu bayna ’ibaadika fiymaa kaanuw fiyhi yakhtalifuwn. Ihdiniy limakhtulifa fiyhi minal haqqi biidhnika Innaka Tahdiy man Tashaau ilaa swiraatwil-mustaqiym – 

Ee Allaah  Rabb wa Jibraaiyl   na Miykaaila na Israafiyla, Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghayb na dhahiri, Wewe Utahukumu baina ya waja Wako katika ambayo walikuwa wakikhitilafiana nayo. Niongoze mimi kwenye haki katika yale ambayo (watu) wamekhitilafiana kwa idhini Yako.  Hakika Wewe unamuongoza Umtakae kwenye njia ilionyoka)). [Muslim (1/534)]

 

Na akasema Sa’iyd bin Jubayr:

 

 إِنِّي لأَعْرِفُ آيَة مَا قَرَأَهَا أَحَد قَطُّ فَسَأَلَ اللَّه شَيْئًا إلاَّ أَعْطَاهُ إِيَّاهُ, قَوْله تَعَالَى: (( قُلِ اللَّـهُمَّ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ أَنتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِي مَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ))

“Hakika mimi ninaijua Aayah, haisomi mtu yeyote akamwomba Allaah kitu ila Anampa. Nayo ni kauli ya Allaah (Ta’aalaa): Sema: “Ee Allaah Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghayb na dhahiri, Wewe Utahukumu baina ya waja Wako katika ambayo walikuwa wakikhitilafiana nayo.” [Tafsiyr Al-Qurtwuby]

 

 

 

 

Share

19-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Kutawassal Kwa ‘Iymaan na Tawhiyd na ‘Amali Za Kimatendo

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Zinazokubalika

 

19-Kutawassal Kwa ‘Iymaan na Tawhiyd na ‘Amali Za Kimatendo

 

 

 

 

Inafaa pia kutawassal kwa ‘amali za kimoyoni kama kumwamini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kumpwekesha (Tawhiyd) mfano kusema: “Ee Allaah!  Hakika mimi natawassal Kwako kwa iymaan yangu kwamba Wewe ni Mwabudiwa wa haki, Huna mshirika, nifarijie jambo langu kadhaa, au nijaalie kadhaa au nighufurie dhambi zangu.”

 

Au mfano kusema:

 

“Ee Allaah!  Hakika mimi natawassal Kwako kwa mapenzi yangu Kwako pamoja na kumpenda Nabiy Wako (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuamini yote aliyokuja nayo na kuwapenda Maswahaba wote, nijaalie kadhaa wa kadhaa.” Dalili ni kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) zifuatazo:

 

الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿١٦﴾ 

Wale wasemao: “Rabb wetu, hakika sisi tumeamini, basi Tughufurie madhambi yetu na Tukinge na adhabu ya moto.” [Aal-‘Imraan: 16]

 

Na kama walivyoomba Al-Hawaariyyuwn (wafuasi watiifu) wa Nabiy ‘Iysa ('Alayhis-Salaam):   

رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلْتَ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٥٣﴾

 “Rabb wetu, tumeamini Uliyoyateremsha na tumemfuata Rasuli basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (haki).” [Aal-‘Imraan: 53]

 

 

Au kama alivyotawassal Nabiy Yuwsuf ('Alayhis-salaam) akataja kwanza neema na fadhila za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) juu yake Alizomneemesha, kisha akamtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kisha ndio akaomba kufishwa akiwa katika hali ya Uislamu na kukutanishwa na waja wema, aliomba:

 

رَبِّ قَدْ آتَيْتَنِي مِنَ الْمُلْكِ وَعَلَّمْتَنِي مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَنتَ وَلِيِّي فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖتَوَفَّنِي مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ ﴿١٠١﴾

 “Rabb wangu kwa yakini Umenipa katika utawala, na Umenifunza katika tafsiri za masimulizi (ya ndoto na matukio). Muanzilishi wa mbingu na ardhi. Wewe ni Mlinzi, Msaidizi wangu duniani na Aakhirah. Nifishe hali ya kuwa Muislamu na Unikutanishe na Swalihina.” [Yuwsuf: 101]

 

 

Au kama walivyotawassal Maswahaba kwa Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika uumbaji Wake na kumwamini na kuamini Siku ya mwisho na kukhofu moto wa Aakhirah. 

 

الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿١٩١﴾ 

Ambao wanamdhukuru Allaah kwa kusimama  na kwa kukaa na kwa kulala ubavuni mwao na wanatafakari katika kuumbwa mbingu na ardhi (wakisema): “Rabb wetu, Hukuumba haya bure, Subhaanak! (Utakasifu ni Wako) tukinge na adhabu ya moto.”

 

 

رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿١٩٢﴾

 “Rabb wetu, hakika Umuingizaye motoni, kwa yakini Umemhizi. Na madhalimu hawana yeyote mwenye kuwanusuru.”

 

رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلْإِيمَانِ أَنْ آمِنُوا بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا ۚ رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الْأَبْرَارِ ﴿١٩٣﴾

 “Rabb wetu, hakika sisi tumemsikia mwitaji anaita kwenye iymaan kwamba ‘mwaminini Rabb wenu’ basi tukaamini.  Rabb wetu, Tughufurie madhambi yetu na Tufutie makosa yetu na Tufishe pamoja na Waumini wema.”

 

 رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّكَ لَا تُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿١٩٤﴾

 “Rabb wetu na Tupe Uliyotuahidi kupitia Rusuli Wako, wala Usituhizi Siku ya Qiyaamah; hakika Wewe Huendi kinyume na miadi.” [Aal-‘Imraan: 191-194]

 

Baada ya kauli zao na du’aa zao hizo, Allaah Akawaitikia na kuwaghufuria na kuwaruzuku mazuri zaidi:

 

فَاسْتَجَابَ لَهُمْ رَبُّهُمْ أَنِّي لَا أُضِيعُ عَمَلَ عَامِلٍ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ ۖ بَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ ۖ فَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَأُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأُوذُوا فِي سَبِيلِي وَقَاتَلُوا وَقُتِلُوا لَأُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأُدْخِلَنَّهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ثَوَابًا مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الثَّوَابِ ﴿١٩٥﴾

Basi Rabb wao Akawaitikia  “Hakika Mimi Sipotezi ‘amali za mtendaji yeyote yule miongoni mwenu akiwa mwanamume au mwanamke, nyinyi kwa nyinyi. Basi wale waliohajiri na wakatolewa majumbani mwao na wakaudhiwa katika njia Yangu, wakapigana na wakauliwa; bila shaka Nitawafutia makosa yao na bila shaka Nitawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, ni thawabu kutoka kwa Allaah.  Na kwa Allaah kuna thawabu nzuri kabisa.” [Aal-‘Imraan: 195]

 

 

Pia inafaa kutawassal kwa ‘amali njema yoyote ile. Mfano kusema:

 

“Ee Allaah hakika mimi natawassal kwako kwa kumsaidia jirani yangu katika hali yake ya shida kadhaa wa kadhaa Basi ee Allaah, nitakabalie haja yangu kadhaa, au niepushe na shari kadhaa.” 

 

Au mfano kusema:

"Ee Allaah, hakika mimi natawassal kwako kwa 'amali yangu ya kumsamehe deni ndugu yangu, au natawassal kwa swadaqah yangu niliyoitoa kwa masikini na wenye kuhitaji, unitakabalie haja yangu zangu kadhaa."

 

Au mfano kusema:

“Ee Allaah, hakika mimi natawassal kwako kwa kuwatendea wema wazazi wangu kuwafanyia kadhaa wa kadhaa unitakabalie haja zangu kadhaa au nijaalie kadhaa” Dalili ni Hadiyth swahiyh ifuatayo iliyotaja kisa cha watu watatu waliokwama pangoni wakakaribia kukata tamaa kuokoka:

 

عن عبدِ الله بنِ عمرَ بن الخطابِ رضيَ اللهُ عنهما، قَالَ: سمعتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، يقول: ((انطَلَقَ ثَلاثَةُ نَفَرٍ مِمَّنْ كَانَ قَبْلَكُمْ حَتَّى آوَاهُمُ المَبيتُ إِلى غَارٍ فَدَخلُوهُ، فانْحَدرَتْ صَخْرَةٌ مِنَ الجَبَلِ فَسَدَّتْ عَلَيْهِمُ الغَارَ، فَقالُوا: إِنَّهُ لا يُنْجِيكُمْ مِنْ هذِهِ الصَّخْرَةِ إِلا أنْ تَدْعُوا اللهَ بصَالِحِ أعْمَالِكُمْ. 
قَالَ رجلٌ مِنْهُمْ: اللَّهُمَّ كَانَ لِي أَبَوانِ شَيْخَانِ كبيرانِ، وكُنْتُ لا أغْبِقُ قَبْلَهُمَا أهْلًا ولا مالًا، فَنَأَى بِي طَلَب الشَّجَرِ يَوْمًا فلم أَرِحْ عَلَيْهمَا حَتَّى نَامَا، فَحَلَبْتُ لَهُمَا غَبُوقَهُمَا فَوَجَدْتُهُما نَائِمَينِ، فَكَرِهْتُ أنْ أُوقِظَهُمَا وَأَنْ أغْبِقَ قَبْلَهُمَا أهْلًا أو مالًا، فَلَبَثْتُ، والْقَدَحُ عَلَى يَدِي، أنتَظِرُ اسْتِيقَاظَهُما حَتَّى بَرِقَ الفَجْرُ والصِّبْيَةُ يَتَضَاغَوْنَ عِنْدَ قَدَميَّ، فاسْتَيْقَظَا فَشَرِبا غَبُوقَهُما.اللَّهُمَّ إنْ كُنْتُ فَعَلْتُ ذلِكَ ابِتِغَاء وَجْهِكَ فَفَرِّجْ عَنّا مَا نَحْنُ فِيهِ مِنْ هذِهِ الصَّخْرَةِ، فانْفَرَجَتْ شَيْئًا لا يَسْتَطيعُونَ الخُروجَ مِنْهُ. 

قَالَ الآخر: اللَّهُمَّ إنَّهُ كانَتْ لِيَ ابْنَةُ عَمّ، كَانَتْ أَحَبَّ النّاسِ إليَّ،

 وفي رواية:

 كُنْتُ أُحِبُّها كأَشَدِّ مَا يُحِبُّ الرِّجَالُ النساءَ، فأَرَدْتُهَا عَلَى نَفْسِهَا فامْتَنَعَتْ منِّي حَتَّى أَلَمَّتْ بها سَنَةٌ مِنَ السِّنِينَ فَجَاءتْنِي فَأَعْطَيْتُهَا عِشْرِينَ وَمائةَ دينَارٍ عَلَى أنْ تُخَلِّيَ بَيْني وَبَيْنَ نَفْسِهَا فَفعَلَتْ، حَتَّى إِذَا قَدَرْتُ عَلَيْهَا،

 وفي رواية:

فَلَمَّا قَعَدْتُ بَينَ رِجْلَيْهَا، قالتْ: اتَّقِ اللهَ وَلا تَفُضَّ الخَاتَمَ إلا بِحَقِّهِ، فَانصَرَفْتُ عَنْهَا وَهيَ أَحَبُّ النَّاسِ إليَّ وَتَرَكْتُ الذَّهَبَ الَّذِي أعْطَيتُها. اللَّهُمَّ إنْ كُنْتُ فَعَلْتُ ذلِكَ ابْتِغاءَ وَجْهِكَ فافْرُجْ عَنَّا مَا نَحْنُ فيهِ، فانْفَرَجَتِ الصَّخْرَةُ، غَيْرَ أَنَّهُمْ لا يَسْتَطِيعُونَ الخُرُوجَ مِنْهَا. 

وَقَالَ الثَّالِثُ: اللَّهُمَّ اسْتَأْجَرْتُ أُجَرَاءَ وأَعْطَيْتُهُمْ أجْرَهُمْ غيرَ رَجُل واحدٍ تَرَكَ الَّذِي لَهُ وَذَهبَ، فَثمَّرْتُ أجْرَهُ حَتَّى كَثُرَتْ مِنهُ الأمْوَالُ، فَجَاءنِي بَعدَ حِينٍ، فَقالَ: يَا عبدَ اللهِ، أَدِّ إِلَيَّ أجْرِي، فَقُلْتُ: كُلُّ مَا تَرَى مِنْ أجْرِكَ: مِنَ الإبلِ وَالبَقَرِ والْغَنَمِ والرَّقيقِ، فقالَ: يَا عبدَ اللهِ، لا تَسْتَهْزِئْ بي! فَقُلْتُ: لا أسْتَهْزِئ بِكَ، فَأَخَذَهُ كُلَّهُ فاسْتَاقَهُ فَلَمْ يتْرُكْ مِنهُ شَيئًا. الَّلهُمَّ إنْ كُنتُ فَعَلْتُ ذلِكَ ابِتِغَاءَ وَجْهِكَ فافْرُجْ عَنَّا مَا نَحنُ فِيهِ، فانْفَرَجَتِ الصَّخْرَةُ فَخَرَجُوا يَمْشُونَ))  مُتَّفَقٌ عليهِ

Imepokelewa kutoka kwa 'Abdullaah bin ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Nilimsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Waliondoka watu watatu, miongoni mwa watu waliokuwa kabla yenu waliosafiri hadi wakaingia pangoni ili walale.

 

Likaviringika jiwe kutoka juu ya jabali likawafungia pango. Wakasemezana: Hakuna kitakachowaokoa kutokana na jiwe hili isipokuwa mumuombe Allaah kwa ‘amali zenu njema.

 

Mmoja miongoni mwao akaanza kuomba: “Ee Allaah. Nilikuwa nina wazazi wawili wazee wakongwe, nilikuwa sitangulizi (kabla yao kunywa maziwa) familia wala watumwa. Siku moja haja ya kutafuta kuni ikanipeleka mbali, sikuweza kuwarudia (mapema) mpaka wakalala. Nikawakamulia maziwa yao, nikawakuta wameshalala. Nikachukia kuwaamsha na (nikachukia pia) kuwapa maziwa familia na watumwa kabla yao. Nikawa na (bilauri) imo mikononi mwangu mpaka waamke, hadi alfajiri ikatokeza huku watoto wakipiga kelele kwa njaa miguuni mwangu; wakaamka na wakanywa maziwa yao. Ee Allaah. Ikiwa nilifanya hivyo kwa kutaka radhi Zako, basi tufariji katika dhiki tuliyonayo ya jiwe hili.”

 

Kukafunguka kidogo kidogo kwa namna ambayo hawawezi kutoka.

 

Mwengine akasema: “Ee Allaah. Nilikuwa nina bint wa ‘ammi yangu, nilikuwa nikimpenda mno...”

 

Riwaayah nyingine imesema:

“Nilikuwa nikimpenda kama vile wanaume wanavyopenda mno wanawake. Nikamtaka (kuzini nae), akanikatalia. Mpaka alipokuja mwaka wa ukame, akanijia nikampa dinaar 120 ili niwe naye faragha. Akakubali. Nilipokuwa nimeshamuweza...”

 

Riwaayah nyingine inasema:

“Nilipoketi baina ya miguu yake akanambia: Mche Allaah, usiivunje pete ila kwa haki yake. Nikamuondokea nikiwa nampenda mno (wala sikumfanya chochote), na nikamuachia dhahabu niliyompa. Ee Allaah, Ikiwa nilifanya hivyo kwa ajili ya kupata radhi Zako, basi tufariji katika dhiki tuliyonayo.”

 

Jiwe likafunguka, lakini walikuwa hawawezi kutoka.

 

Mtu wa tatu akasema:

 

“Ee Allaah. Mimi niliwaajiri wafanyakazi, nikawapa ujira wao isipokuwa mtu mmoja, aliuacha ujira wake na akaenda. Nikauzalisha ujira wake mpaka ukawa ni mali nyingi. Baada ya muda akanijia na kuniambia: Ee mja wa Allaah, nipe ujira wangu! Nikamwambia: Kila unachokiona katika ngamia, ng’ombe, mbuzi na watumwa ni ujira wako! Akaniambia: Ee mja wa Allaah, usinifanyie istihzai (usinikebehi)!  Nikamwambia: Sikufanyii istihzai. Akachukua mali yote na akayachunga na wala hakubakisha mali yoyote. Ee Allaah. Ikiwa nilifanya hivyo kwa kutaka radhi Zako, basi tufariji katika dhiki tuliyonayo.”

 

Jiwe likafunguka wakatoka zao.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share

20-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Kutawassal Kwa Kutaja Hali Na Kutaja Sababu

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Zinazokubalika

 

20-Kutawasali Kwa Kutaja Hali Na Kutaja Sababu

 

 

 

 

Inafaa kutawassal kwa kutaja hali au sababu ya jambo unaloliombea du'aa. Ikiwa jambo unaloliomba ni kwa ajili ya manufaa ya dunia, basi  liwe ni jambo lenye kumridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na linalokubalika katika shariy’ah. 

 

Mifano mingi imo katika Qur-aan waliyoomba Manabii. Mifano michache ifuatayo:

 

Nabiy Nuwh ('Alayhis-Salaam):  

 

Aliomba nusra baada ya kushindwa kuwalingaia watu wake miaka mia tisa na khamsini. [Al-‘Ankabuwt 29: 14].

 

Katika Suwratul-Qamar Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:  

كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا عَبْدَنَا وَقَالُوا مَجْنُونٌ وَازْدُجِرَ ﴿٩﴾

Walikadhibisha kabla yao kaumu ya Nuwh, wakamkadhibisha mja Wetu, wakasema: “Majnuni.” Na akakaripiwa. [Al-Qamar: 9]

  

Nabiy Nuwh ('Alayhis-Salaam) akaomba:

فَدَعَا رَبَّهُ أَنِّي مَغْلُوبٌ فَانتَصِرْ ﴿١٠﴾

Basi akamwita Rabb wake kwamba: “Hakika mimi nimeshindwa nguvu basi Nusuru.” [Al-Qamar: 10]

 

Hapo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamtakabalia du’aa yake Akamuokoa Akawaangamiza madhalimu kama Anavyosema:

فَفَتَحْنَا أَبْوَابَ السَّمَاءِ بِمَاءٍ مُّنْهَمِرٍ ﴿١١﴾

Tukafungua milango ya mbingu kwa maji yanayofoka na kumiminika kwa nguvu.

 

وَفَجَّرْنَا الْأَرْضَ عُيُونًا فَالْتَقَى الْمَاءُ عَلَىٰ أَمْرٍ قَدْ قُدِرَ ﴿١٢﴾

Na Tukazibubujua ardhi chemchemu; basi yakakutana maji kwa amri iliyokwisha kadiriwa.

 

وَحَمَلْنَاهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلْوَاحٍ وَدُسُرٍ ﴿١٣﴾

Na Tukambeba kwenye ile (jahazi) yenye mbao na misumari.

 

تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا جَزَاءً لِّمَن كَانَ كُفِرَ ﴿١٤﴾

Inatembea chini ya Macho Yetu, ni jazaa kwa yule aliyekuwa amekanushwa.

 

وَلَقَد تَّرَكْنَاهَا آيَةً فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ ﴿١٥﴾

Na kwa yakini Tumeiacha iwe ni Aayah (ishara, zingatio) je, basi yuko yeyote mwenye kuwaidhika?

 

فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ ﴿١٦﴾

Basi vipi ilikuwa adhabu Yangu na maonyo Yangu? [Al-Qamar: 11-16]

 

 

Nabiy Ibraahiym ('Alayhis-Salaam):   

 

Alitaja hali yake ilivyo ya kuacha ahli yake baada ya kujenga Ka’bah, sehemu ambako kulikuwa bado hakuna mazao wala chochote. Akataja na sababu  ya kuomba Allaah Awaruzuku mazao ili watu waweze kuishi hapo na  kutekeleza ‘ibaadah na ili watu wapate kumshukuru Allaah (‘Azza wa Jalla). Akaomba:

 

رَّبَّنَا إِنِّي أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ ﴿٣٧﴾

 “Rabb wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria wangu katika bonde lisilokuwa na mmea wowote, kwenye Nyumba Yako Tukufu. Rabb wetu, ili wasimamishe Swalaah na Ujaalie nyoyo za watu zielekee kwao na Uwaruzuku mazao ili wapate kushukuru.” [Ibraahiym: 37]

 

Aayah zinazofuatia baada ya hiyo zinaendelea kutaja du’aa ya Ibraahiym ('Alayhis-Salaam). [Ibraahiym: 38-41]

 

 

Nabiy Zakariyyaa ('Alayhis-Salaam):

 

Aliomba mtoto akiwa katika hali ya uzee na mkewe pia alikuwa tasa. Akataja kwanza mifupa kuwa dhaifu na nywele kugeuka mvi. Kisha akataja sababu kwamba alikhofu baada ya kufariki kwake kubakia kizazi kiovu, hivyo aliomba mtoto ili awe Nabiy baada yake atakayeongoza watu katika Dini. Imetajwa katika Qur-aan:

ذِكْرُ رَحْمَتِ رَبِّكَ عَبْدَهُ زَكَرِيَّا ﴿٢﴾

 (Huu ni) Ukumbusho wa rahmah ya Rabb wako kwa mja Wake Zakariyyaa.

 

إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ نِدَاءً خَفِيًّا ﴿٣﴾

Alipomwita Rabb wake mwito wa siri.

 

 

قَالَ رَبِّ إِنِّي وَهَنَ الْعَظْمُ مِنِّي وَاشْتَعَلَ الرَّأْسُ شَيْبًا وَلَمْ أَكُن بِدُعَائِكَ رَبِّ شَقِيًّا ﴿٤﴾

Akasema: “Rabb wangu! Hakika mimi mifupa imeninyong’onyea na kichwa kimeng’aa mvi, na wala sikuwa mwenye kunyimwa katika kukuomba du’aa, ee Rabb wangu.

 

وَإِنِّي خِفْتُ الْمَوَالِيَ مِن وَرَائِي وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا فَهَبْ لِي مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا ﴿٥﴾

 “Nami nakhofia jamaa zangu nyuma yangu, na mke wangu ni tasa. Basi Nitunukie kutoka kwako mrithi.”

 

يَرِثُنِي وَيَرِثُ مِنْ آلِ يَعْقُوبَ ۖ وَاجْعَلْهُ رَبِّ رَضِيًّا ﴿٦﴾

Anirithi na arithi kizazi cha Ya’quwb, na Mjaalie Rabb wangu awe mwenye kuridhisha”. [Maryam: 2-6]

 

Hapo Jibriyl ('Alayhis-Salaam) akamjia na kumbashiria mtoto:  

 

يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُ مِن قَبْلُ سَمِيًّا ﴿٧﴾

 (Akaambiwa): “Ee Zakariyyaa! Hakika Sisi Tunakubashiria ghulamu jina lake Yahyaa, Hatukupata kabla kumpa jina hilo yeyote.” [Maryam: 7]

 

 

Nabiy Muwsaa ('Alayhis-Salaam):

 

Baada ya kumkimbia Fir’awn aliyetaka kumuua baada ya kufikwa na mtihani wa kumuua mtu bila ya kusudio mjini. Akakimbia hadi kufika mji wa Madyan akiwa amechoka, mwenye njaa hadi kufika kula majani njiani. Rejea Suwrah: Al-Qaswasw: (28: 15-21).

 

Alipofika mtoni ambako walikuweko watu wakichota maji, alikuta pembeni yake mabinti wawili wameakaa kando wakisubiri wachungaji Wanyama wachote maji kisha ndio wao wasogee kuchota. Endelea kurejea Al-Qaswasw (28: 22-23)

 

Nabiy Muwsaa ('Alayhis-Salaam) alipotambua kwamba mabinti hao hawakuwa na uwezo wa kuchota maji kwa sababu ya mzongano wa watu wanaochota maji,  aliwatekea maji kisha akakaa kivulini na akamwomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  kwa kumtajia hali yake kuwa ni  mhitaji wa neema Zake. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ ﴿٢٤﴾

Basi akawanyweshea, kisha akageuka kwenda kivulini, akasema: “Rabb wangu! Hakika mimi ni mhitajia wa kheri yoyote Utakayoniteremshia.” [Al-Qaswasw 28: 24]

 

Hapo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akampa faraja na akaruzukiwa mke katika mmoja wa hao mabinti kama Anavyosema:

 

فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا ۚ فَلَمَّا جَاءَهُ وَقَصَّ عَلَيْهِ الْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ ۖ نَجَوْتَ مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥﴾

Basi akamjia mmoja kati ya wanawake wawili akitembea kwa kuona hayaa; akasema: “Baba yangu anakwita ili akulipe ujira wa kutunyweshea.” Basi alipomfikia na akamsimulia visa vyake; alisema: “Usikhofu, umeokoka na watu madhalimu.”

 

قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ ۖ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ ﴿٢٦﴾

Mmoja wao akasema: “Ee baba yangu, muajiri! Hakika mbora uwezaye kumwajiri ni mwenye nguvu mwaminifu.”

 

 

قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَىٰ أَن تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ ۖ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِندِكَ ۖ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ ۚ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٢٧﴾

Akasema: “Mimi nataka nikuozeshe mmoja wapo wa binti zangu hawa wawili kwa sharti kuwa unitumikie miaka minane; ukitimiza kumi, basi ni kutoka kwako. Na wala sitaki kukutia mashakani; utanikuta In Shaa Allaah miongoni mwa Swalihina.”

 

قَالَ ذَٰلِكَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ ۖ أَيَّمَا الْأَجَلَيْنِ قَضَيْتُ فَلَا عُدْوَانَ عَلَيَّ ۖ وَاللَّـهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ ﴿٢٨﴾

 (Muwsaa) Akasema: “Hayo ni baina yangu na baina yako. Muda wowote kati ya miwili nitakaoutimiza basi hakuna uadui juu yangu. Na Allaah juu ya yale tunayoyasema ni Mdhamini.” [Al-Qaswasw: 25-28]

 

 

Na baada ya hapo ndipo alipofikia kuzungumza na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika bonde tukufu la Twuwaa, akajaaliwa kupewa Unabiy na kuwa Rasuli. Rejea Aayah zinazoendelea katika Suwrah hiyo ya Al-Qaswasw.

 

 

 

 

Share

21-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Kutawassal Kwa Maajabu ya Allaah Na Neema Zake

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Zinazokubalika

 

21-Kutawassal Kwa Maajabu ya Allaah Na Neema Zake

 

 

 

 

a) Kutawassal Kwa Neema Na Majabu Ya Allaah ('Azza wa Jalla):

 

 

Inafaa kutawassal uonapo maajabu au neema za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kutokana na mifano ifuatayo katika Qur-aan:  

 

Nabiy Zakariyyaa ('Alayhis Salaam) ambaye alikuwa ni mlezi wa Maryam, pale alipoingia katika mihraab ya Maryam akakuta maajabu ya rizqi kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): 

 

فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا ۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا ۖقَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا ۖ قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٧﴾ 

Basi Rabb wake Akampokea kwa kabuli njema na Akamkuza mkuzo mzuri na Akamfanya Zakariyyaa kuwa mlezi wake. Kila Zakariyyaa alipoingia kwake katika chumba cha kuswalia alikuta kwake kuna riziki Akasema: “Ee Maryam! Umepata wapi hivi? ”Akasema: “Hivi ni kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah Anamruzuku Amtakaye bila ya hesabu.” [Aal-‘Imraan: 37]

 

Maajabu zaidi ni kwamba yalikuwa ni matunda ya msimu wa baridi wakati wa msimu wa joto, na matunda ya msimu wa joto katika msimu wa baridi . [Tafsiyr Atw-Twabariy, Ibn Kathiyr]

 

Basi hapo hapo Nabiy Zakariyyaa ('Alayhis Salaam) aliomba naye du’aa ya kutaka mtoto japokuwa alikwishakata tamaa kutokana na uzee na vilevile mkewe akiwa ni tasa.

هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٨﴾

Hapo hapo Zakariyyaa akamwomba Rabb wake, akasema: “Rabb wangu Nitunukie kutoka Kwako kizazi chema hakika Wewe ni Mwenye kusikia du’aa yangu.” [Aal-‘Imraan: 38]

 

Kisha hapo hapo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akambashiria kumruzuku mwana aliyemtani, tena mwana mwema mwenye sifa njema:

 

فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًا بِكَلِمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٣٩﴾

Basi mara Malaika akamwita (Zakariyyaa) naye akiwa amesimama anaswali katika chumba kwamba: “Hakika Allaah Anakubashiria Yahyaa mwenye kusadikisha Neno (la Kun!) kutoka kwa Allaah na ni mwenye sharaf, busara na taqwa, na anayejitenga mbali na matamanio na Nabiy miongoni mwa Swalihina.” [Aal-‘Imraan: 39]

 

Imaam As-Sa’dy amesema: “Na katika Aayah hii:

هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ ۖ 

Hapo hapo Zakariyyaa akamwomba Rabb wake … [Aal-‘Imraan: 37]

 

ni dalili kuthibitika karama za awliyaa za kimiujiza, kinyume na wanaopinga hayo.

 

Basi Zakariyyaa ('Alayhis Salaam) alipoona yale ambayo Allaah Amemneemesha kwayo Maryam, na ambayo Amemkirimisha kwayo katika rizki Yake njema ya siha, ambayo Alimpa bila ya juhudi zake wala kuzihangaikia, nafsi yake ikapata tamaa ya kupata mtoto, ndio maana hapo Allaah (Ta’aalaa) Anasema… (Aayah za 38-41]" (mwisho wa kunukuu).

 

 

 

b) Kutawassal Kwa Neema Za Allaah ('Azza wa Jalla):

 

Malaika wanamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Awaghufurie Waumini dhambi zao na Awaepushe na maovu, wanaanza kwa kutawassal kwa kutaja neema ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kueneza rahmah Yake kama Anavyosema:

 

الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ﴿٧﴾

 (Malaika) Ambao wanabeba ‘Arsh na walio pembezoni mwake, wanasabbih kwa Himidi za Rabb wao, na wanamwamini; na wanawaombea maghfirah wale walioamini:  “Rabb wetu! Umekienea kila kitu kwa rahmah na ujuzi, basi waghufurie wale waliotubu, na wakafuata njia Yako, na wakinge na adhabu ya moto uwakao vikali mno.”

 

رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدتَّهُمْ وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٨﴾

 “Rabb wetu! Waingize Jannaat za kudumu milele ambazo Umewaahidi, pamoja na waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na dhuria wao.  Hakika Wewe Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

وَقِهِمُ السَّيِّئَاتِ ۚ وَمَن تَقِ السَّيِّئَاتِ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمْتَهُ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٩﴾

 “Na wakinge maovu, kwani Unayemkinga na maovu Siku hiyo, basi kwa yakini Umemrehemu. Na huko ndiko kufuzu adhimu. [Ghaafir: 7-9]

 

Mifano mingi mengineyo imo katika Qur-aan. Na hii ni fursa mojawapo kubwa kutawassal kwa neema za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa sababu neema Zake (Tabaaraka wa Ta’aalaa) ni nyingi mno hakuna awezaye kuzihesabu. Kwa hiyo Muislamu afuate kielekezo hiki cha kutafakari maajabu ya Allaah ('Azza wa Jalla), na Rahma Zake, na kukumbuka neema za Rabb wake na amshukuru kisha aombe anachotaka katika mas-alah ya dunia na Aakhirah.

 

 

 

 

Share

22-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Kutawassal Kwa Du'aa Ya Mja Mwema Aliye Hai

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee TunakuabuduNa Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Zinazokubalika

 

22-Kutawasali Kwa Du'aa Ya Mja  Mwema Aliye Hai

 

 

 

 

Inafaa Muislamu kumwomba nduguye Muumini aliye hai amkumbuke kwa du’aa. Maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) walikuwa wakimuomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) awaombee katika   mas-alah mbali mbali. Mfano pale mtu alipomwendea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) awaombee mvua baada ya kufikwa na ukame mkubwa uliosababisha balaa ya kuharibikiwa mali zao:

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّ رَجُلاً، دَخَلَ الْمَسْجِدَ يَوْمَ جُمُعَةٍ مِنْ بَابٍ كَانَ نَحْوَ دَارِ الْقَضَاءِ، وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَائِمٌ يَخْطُبُ، فَاسْتَقْبَلَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَائِمًا ثُمَّ قَالَ: "يَا رَسُولَ اللَّهِ هَلَكَتِ الأَمْوَالُ وَانْقَطَعَتِ السُّبُلُ، فَادْعُ اللَّهَ يُغِيثُنَا" فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَدَيْهِ ثُمَّ قَالَ: ((اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا)). قَالَ أَنَسٌ: وَلاَ وَاللَّهِ مَا نَرَى فِي السَّمَاءِ مِنْ سَحَابٍ، وَلاَ قَزَعَةً، وَمَا بَيْنَنَا وَبَيْنَ سَلْعٍ مِنْ بَيْتٍ وَلاَ دَارٍ‏.‏ قَالَ فَطَلَعَتْ مِنْ وَرَائِهِ سَحَابَةٌ مِثْلُالتُّرْسِ، فَلَمَّا تَوَسَّطَتِ السَّمَاءَ انْتَشَرَتْ ثُمَّ أَمْطَرَتْ، فَلاَ وَاللَّهِ مَا رَأَيْنَا الشَّمْسَ سِتًّا، ثُمَّ دَخَلَ رَجُلٌ مِنْ ذَلِكَ الْبَابِ فِي الْجُمُعَةِ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَائِمٌ يَخْطُبُ، فَاسْتَقْبَلَهُ قَائِمًا فَقَالَ: "يَا رَسُولَ اللَّهِ هَلَكَتِ الأَمْوَالُ وَانْقَطَعَتِ السُّبُلُ، فَادْعُ اللَّهَ يُمْسِكْهَا عَنَّا"‏.‏  قَالَ:  فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَدَيْهِ ثُمَّ قَالَ: ((اللَّهُمَّ حَوَالَيْنَا وَلاَ عَلَيْنَا، اللَّهُمَّ عَلَى الآكَامِ وَالظِّرَابِ وَبُطُونِ الأَوْدِيَةِ وَمَنَابِتِ الشَّجَرِ)) ‏ قَالَ: فَأَقْلَعَتْ وَخَرَجْنَا نَمْشِي فِي الشَّمْسِ‏.‏ قَالَ شَرِيكٌ: سَأَلْتُ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ أَهُوَ الرَّجُلُ الأَوَّلُ فَقَالَ مَا أَدْرِي‏.‏

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba mtu mmoja aliingia Masjid siku ya Ijumaa kupitia mlango ulioelekea Daar Al-Qadhwaa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa amesimama akikhutubia. Akasimama mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kisha akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Wanyama wameteketea na njia zimekatika, basi muombe Allaah Atuteremshie mvua.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akanyanyua mikono akaomba: ((Allaahumma Aghithnaa, Allaahumma Aghithnaa, Allaahumma Aghithanaa - Ee Allaah tubarikie kwa mvua))”. Anas amesema:  Wa-Allaahi hakukuwa na mawingu mbinguni na hakukuwa na nyumba au jengo baina yetu na baina ya mlima wa Sal’i.  Basi wingu kubwa kama ngao lilitokea nyuma yake.  Lilipofika katikati lilienea kisha ikanyesha mvua. Basi wa-Allaahi, hatukuona jua siku sita. Kisha Ijumaa iliyofuatia aliingia mtu kupitia mlango huo huo na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikhutubia khutbah ya Ijumaa, akasimama mbele yake akasema: “Ee Rasuli wa Allaah!  Mifugo ya nyama inateketea na njia zimekatika, muombe Allaah Atuzuilie mvua!” Anas akasema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akanyanyua mikono oyake akaomba: ((Allaahumma Hawaalaynaa walaa ‘alaynaa.” - Ee Allaah! Pembezoni mwetu na si juu yetu. Eee Allaah juu ya majabali, na vilimani, na ndani ya mabonde na juu ya sehemu zinazoota miti)) Anas akasema: Mvua ikasita na tukatoka tukitembea katika jua.  Shariyk alimuuliza Anas kama huyo mtu alikuwa ni yule yule wa kwanza? Akajibu kuwa hajui. [Al-Bukhaariy, Kitaab Al-Istisqaa]

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn ameeleza kama hayo, kisha akataja Hadiyth ya ‘Ukaashah kisha akasema: “Basi hii ni tawassuli inayojuzu nayo ni kumuomba mtu unayetaraji kutakabaliwa kwake amuombee kwa Allaah Ta’aalaa, lakini ambalo linalopasa ni kwamba muulizaji anakusudia hayo yamfanye yeye nafsi yake na yamfae pia nduguye ambaye anamuomba amuombeee na si kukusudia kujinufaisha yeye pekee kwa sababu unapotaka kumnufuisha nduguyo na kujinufaisha nafsi yako huwa ni kumfanyia ihsaan. Basi mtu anapomuombea nduguye du’aa kwa siri Malaika husema: “Aamiyn nawe upate mfano wake.” Kwa hiyo naye huwa katika wafanyao ihsaan kwa du’aa hii, na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.” [Fataawaa Imaam Ibn ‘Uthaymiyn, Hukmu At-Tawassul]  

 

 

 

Share

23-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Haijuzu Kutawassal Kwa Jaha Ya Nabiy

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Za Shirki, Kufru Na Bid-'ah

 

23-Haijuzu Kutawassal Kwa Jaha Ya

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

 

 

 

Haijuzu kutawassal kwa jaha ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kufariki kwake. Dalili ni Hadiyth ifuatayo ambayo Maswahaba hawakutawassal kwa jaha ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kufariki kwake:  

 

 عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ  (رضي الله عنه)  أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) كَانَ إِذَا قَحَطُوا اسْتَسْقَى بِالْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ فَقَالَ: "اللَّهُمَّ إِنَّا كُنَّا نَتَوَسَّلُ إِلَيْكَ بِنَبِيِّنَا فَتَسْقِينَا وَإِنَّا نَتَوَسَّلُ إِلَيْكَ بِعَمِّ نَبِيِّنَا فَاسْقِنَا"  قَالَ" فَيُسْقَوْنَ.

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliomba mvua kulipokuwa na ukame kwa kutawassal kwa ‘Abbaas bin ‘Abdil-Muttwalib akisema: “Ee Allaah, tulikuwa tunatawassal Kwako kupitia Nabiy wako, Ukatunyeshea mvua, na sasa tunatawassal Kwako kupitia ‘ami wa Nabiy Wako, basi tunyweshee mvua”. Akasema: Wakanyweshewa mvua. [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Istisqaa, na Kitaabu Fadhwaail Aswhaab An-Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam]

 

Baadhi ya Waislamu hukosea kwa kutawassal kwa jaha ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kufariki kwake.

Mfano kusema: “Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kwa jaha ya Nabiy Wako Unikidhie haja zangu kadhaa” au “Uniokoe na janga au balaa fulani” au “Unighufurie dhambi zangu n.k.”

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

“… Basi tunasema tawassul kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) imegawanyika sehemu tatu:

 

Kwanza: Atawassal mtu kwa iymaan yake kwake, na kwa kumfuata (Sunnah zake), na hii inakubalika katika uhai wake na baada ya kufariki kwake. 

 

Pili:  Atawassal kwa du’aa yake, yaani amwombe Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili amwombee mtu. Na hii inakubalika katika uhai wake wala si baada ya kufariki kwake, kwani baada ya kufariki kwake yeye ni mwenye udhuru (hayuko tena). 

 

Tatu:  Kutawassal kwa jaha yake na utukufu wake mbele ya Allaah. Hii haijuzu katika uhai wake wala si baada ya kufariki kwake, kwa sababu yeye siye wasiylah, hivyo hawezi kufikisha mtu katika lengo kwani si kazi yake.

Kwa hiyo akiuliza mtu: “Nimefika katika kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuomba anighufurie au anipe shifaa (aniombeleze) mbele ya Allaah; je, inajuzu au haijuzu?  Tunasema:  Haijuzu.”

 

[Fataawa Ibn ‘Uthaymiyn - Hukmu At-Tawassul Wa Ahkaamuhu (2/25 -380)]

 

 

 

Share

24-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Waja Wema Waliofariki

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee TunakuabuduNa Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Za Shirki, Kufru Na Bid’ah

 

24-Kutawassal Kwa Waja Wema Waliofariki

 

 

 

 

Haijuzu kutawassal kwa waja wema waliokwishafariki. Ingelikuwa inafaa kutawassal kwa waliofariki, basi ingelikuwa ni awlaa kutawassal kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na tumeshabainisha dalili yake katika makala iliyotangulia.

 

Kutawassal kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni shirki bali ni kufru inayomtoa mtu nje ya Uislamu kwa dalili ya kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿١١٧﴾

Na yeyote yule anayeomba du’aa (au kuabudu) pamoja na Allaah muabudiwa mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Rabb wake. Hakika hawafaulu makafiri. [Al-Muuminuwn: 11]

 

 

Miongoni mwa tawassul za shirki ya aina hii ni kuwaomba waja wema makaburini mwao kwa madai kuwa hawaabudiwi bali wanawakurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa sababu ya wema wao na hali Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anakusha hayo kama Anavyosema:

 

 وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّـهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١٨﴾

Na wanaabudu pasi na Allaah ambavyo haviwadhuru wala haviwanufaishi na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” Sema: “Je, mnamjulisha Allaah kwa yale Asiyoyajua katika mbingu na ardhini?” Subhaanah! (Utakasifu ni Wake) na Ametukuka kwa ‘Uluwa kwa yale yote wanayomshirikisha. [Yuwnus: 18]

 

Na Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

na wale waliojichukulia badala Yake walinzi (wakisema): “Hatuwaabudu isipokuwa ili wapate kutukurubisha kwa Allaah tumkaribie” [Az-Zumar 39: 3]

 

Kisha hao waliokwishariki wala hawawezi kusikia wito au ombi la mtu wala hawawezi kumnufaisha mtu kwa lolote lile wala wao wenyewe hawana uwezo wa kujisaidia lolote lile. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ ﴿١٤﴾

Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawatakuitikieni.  Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu, na wala hakuna atakayekujulisha vilivyo kamaMwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Faatwir: 14] 

 

Na pia Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):

 

إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ ۖ فَادْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا لَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٩٤﴾

Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah ni waja kama nyinyi. Hebu waiteni wakuitikieni ikiwa nyinyi ni wakweli. [Al-A’raaf: 194] 

 

Na Anasema pia Allaah ('Azza wa Jalla):

 

 إِنَّمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْثَانًا وَتَخْلُقُونَ إِفْكًا ۚ إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ وَاعْبُدُوهُ وَاشْكُرُوا لَهُ ۖ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿١٧﴾

 “Hakika mnaabudu badala ya Allaah masanamu, na mnaunda uzushi. Hakika wale mnaowaabudu badala ya Allaah hawakumilikiini riziki; basi tafuteni riziki kwa Allaah, na mwabuduni Yeye na mshukuruni, Kwake mtarejeshwa. [Al-‘Ankabuwt: 17]

 

Na Anasema pia Allaah ('Azza wa Jalla):

 

 وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَن دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ﴿٥﴾

 “Na nani aliyepotoka zaidi kuliko ambaye anayeomba asiyekuwa Allaah ambaye hamuitikii mpaka Siku ya Qiyaamah; nao wala hawatambui  maombi yao.” [Al-Ahqaaf: 5]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٦﴾

Na wala usiombe badala ya Allaah visivyokufaa wala visivyokudhuru. Na ukifanya, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.

 

 

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ ۚ يُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚوَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿١٠٧﴾

Na Allaah Akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye. Na Akikutakia kheri, basi hakuna wa kurudisha fadhila Zake, Anasababisha kumfikia kwayo (fadhila Yake) Amtakaye katika waja Wake. Naye ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Yuwnus: 106-107]

 

Kwa hiyo hata kama mtu aliyefariki alikuwa ni mwema mno haifai kutawassal kwake kwani juu ya kuwa ni kufru na shirki, pia ni upotofu mkubwa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُ وَمَا لَا يَنفَعُهُ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ ﴿١٢﴾

Humwomba badala ya Allaah ambavyo visivyomdhuru na wala visivyomnufaisha. Huo ndio upotofu wa mbali.

 

يَدْعُو لَمَن ضَرُّهُ أَقْرَبُ مِن نَّفْعِهِ ۚ لَبِئْسَ الْمَوْلَىٰ وَلَبِئْسَ الْعَشِيرُ ﴿١٣﴾

Humwomba yule ambaye dhara yake iko karibu kuliko manufaa yake. Bila shaka ni mlinzi muovu kabisa, na bila shaka ni rafiki muovu kabisa. [Al-Hajj: 12-13]

 

 

 

Share

25-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa 'Ahlul-Badr' Watu wa Badr

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah

 

25-Kutawassal Kwa Ahlul-Badr  Watu wa Badr

 

 

 

 Ahlul-Badr -   اهل البدر

 

Baadhi ya watu hutawassal kwa uradi unaojulikana katika jamii kama "albadiri" au "halalbadri" kama wanavyotamka watu wengi wa kawaida.

 

Jina lenyewe la tawassul hiyo laonesha wazi jinsi gani watu hawakufahamu maana yake halisi kama ilivyokusudiwa katika lugha ya Kiarabu kwamba maana yake ni: ‘Ahlul-Badr’ (Watu wa Badr).

 

Hao "Ahlul-Badr" ni Maswahaba waliopigana jihaad katika vita vya Badr Na Badr ni jina la mji ulio kiasi cha kilomita mia na khamsini mbali na mji wa Madiynah ambako Waislamu walipopigana vita vya kwanza na washirikina wa Makkah. Vita hivyo viliongozwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Baadhi ya mapokezi yanaeleza kuwa walikuwa Waislamu mia tatu na kumi na tatu au kumi na nne na riwaya zingine zinasema kuwa walikuwa mia tatu na kumi na saba.

 

Themanini na sita kati yao ni Muhaajiriyn (watu wa Makkah waliohamia Madiynah) na mia mbili thelathini na moja ni watu wa pale pale Madiynah.

 

Juu ya kuwa idadi ya Waislamu ni ndogo kulingana na jeshi la makafiri wa Makkah iliyofika takriban mara sita yao, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Aliwajaalia ushindi katika vita hivyo.

 

Baadhi ya Waislamu waliuawa katika vita hivyo wakafa wakiwa ni mashuhadaa.

 

Wazushi wakaandaa katika kijitabu kidogo, majina ya mashuhadaa na kufanya ni uradi wa kutawassal  ili mtu apate kukubaliwa du’aa yake.

 

Wengine hukusudia kwa kupitia du'aa hizo walizotunga, kumuombea laana au maangamizi mtu. Hutajwa majina yao mmoja baada ya mwengine. Na kila mmoja hutajwa kwa kumtambulisha kabila lake au asli ya eneo alilotokea; mfano ni ‘fulani Al-Answaariy’ au ‘fulani Al-Muhaajiriy’ au ‘fulani Al-Khazrajiyy’ au ‘fulani Al-Awsiy’ n.k.

 

‘Ulamaa wa Al-Lajnah Ad-Daaimah wamesema: “Akishafariki mwana Aadam, masikio yake hayafanyi kazi wala hadiriki kusikia sauti za duniani wala kusikia mongezi yao kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ ﴿٢٢﴾

nawe huwezi kuwasikilizisha walioko kaburini. [Faatwir: 22] 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (1/478-479)]

 

 

Na Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Na wanayoyafanya katika kuomba viumbe kama vile Malaika au Manabii na waja wema waliofariki mfano wa du’aa zao kwa Maryam na wengineo na kuwaomba shafaa'ah (uombezi) waliofariki kwa Allaah, hakutumwa Nabiy yeyote kuleta hilo (kufundisha hilo)."  [Al-Jawaab Asw-Swahiyh (5/187)]

 

 

Tawassul  kama hii ni baatwil; haijuzu kabisa kwa sababu ni shirki ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameiharamisha kwa dalili kadhaa zilizokwishatangulia; na  Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ ﴿١٣﴾

Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende.

 

إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ ﴿١٤﴾

Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawatakuitikieni.  Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu, na wala hakuna atakayekujulisha vilivyo kamaMwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Faatwir: 13-14]

 

 

 

 

Share

26-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Uradi "Swalaatun-Naariyah"

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah

 

26-Kutawassal Kwa Uradi Unaoitwa "Swalaatun-Naariyah"

 

 

 

 Swalaatun-Naariyah – صلاة النارية

 

Uradi wa Swalaatun-Naariyah ni uradi wa shirki kwa sababu anaombwa humo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa fadhila zake badala ya kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

Hata kama Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) angekuwa hai basi uradi huu ungebakia kuwa ni shirki kwa sababu ya kumuomba jambo ambalo hakuna mwenye uwezo nalo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee Naye Amemuamrisha Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿١٨٨﴾

188. Sema: “Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa Apendavyo Allaah. Na lau ningekuwa najua ya ghayb, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri, na wala lisingelinigusa ovu. Mimi si chochote isipokuwa ni mwonyaji na mbashiriaji kwa watu wanaoamini.” [Al-A’raaf: 188]

 

 

Na pia Anasema Allaah ('Azza wa Jalla) kumwambia Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا﴿٢١﴾

Sema: “Hakika mimi sikumilikieni dhara na wala uongofu.” [Al-Jinn: 21]   

 

Asili ya uradi huo ni kutoka Bara Hindi ukafika Afrika Mashariki. Husomwa pale mtu anapofikwa na matatizo, janga, dhiki au mtu anapotaka haja yake ikidhiwe. Husomwa mara elfu nne, mia nne na arubaini na nne (4444) kama ifuatavyo:

 

أللهم صلي صلاةً كاملة وسلم سلاما تاما على سيدنا محمد الذي تنحل به العقد، وتتفرج به الكرب، وتقضى به الحوائج ، وتنال به الرغائب، وحسن الخواتيم ويستسقى الغمام بوجهه الكريم وعلى آله وصحبه في كل لمحة ونفس بعدد معلوم لك

 

‘Allaahumma Swalli Swalaatan kaamilatan wa-sallim salaaman taamaa, ‘alaa Sayyidinaa Muhammad alladhiy tan-hallu bihil-‘uqadi, wa-tanfariju bihil-kurab, wa-tuqdhwaa bihil-hawaaij, wa-tunaalu bihir-raghaaib, wa-husnul-khawaatim, wa yustasqal-ghamaamu bi-wajhil-kariym, wa ‘alaa aalihi wa-swahbihi fiy kulli lamhatin wa nafsin, bi’adadi kulli ma’aluumin Lak’

 

(Ee Allaah, Mswalie  Swalaah iliyotimu bwana wetu Muhammad ambayo kwa fadhila zake, vizuizi vyote vinaondoka, mazonge (misukosuko) yanapoa, shida zote zinafarijika, na mahitaji yanakidhika, na inafikisha kwa yanayotamaniwa, na mwisho mwema wapatikana, na kwa fadhila zake yule mwenye uso mtukufu mawingu (mvua) huombwa kunyesha, na Swalah na Salaam ziwe juu ahli zake na Maswahaba wake kwa kila muda na kila pumzi kwa idadi ya kadiri ya Ujuzi Wako)

 

 

Sababu nyinginezo za kutokujuzu Uradi huo wa Swalaatun-Naariyah:

 

1. Nyiradi au du’aa za kuondosha matatizo, shida, dhiki zilizothibiti katika Qur-aan na Sunnah zimejaa tele, kwa hiyo kutafuta nyiradi za uzushi ni kujiingiza katika dhambi na upotofu.

 

 

2. Uradi huo husomwa idadi maalum, (mara 4444); ni uzushi kutaja idadi kadhaa katika aina yoyote ya ‘ibaadah bila ya dalili.

 

 

3. Husomwa kwa kukusanyana watu, nalo hili ni jambo la uzushi katika Dini. Na baya zaidi baadhi ya watu huusoma pale wanapokusanyika katika makhema Minaa katika katika kutekeleza 'ibaadah ya Hajj; wanaharibu Hajj zao kwa uzushi kama huu! 

 

 

4. Uradi huo umekusanya maneno ambayo yanavuka mpaka katika kumtukuza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumpachika Sifa ambazo zinamstahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee. Mfano wa sifa zilizohusishwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) uradi huu ni:

 

“Kwa fadhila zake shida za watu kufarijiwa, vizuizi kuondolewa, mazonge kupoozwa, mahitaji kukidhiwa, na mwisho mwema wupatikana, na kwa fadhila zake yule mwenye uso mtukufu mawingu (mvua) huombwa kunyesha.”

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuweza kujinufaisha nafsi yake wala mtu yeyote jambo ambalo hakuwa na uwezo nalo kama alivyoambiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) aseme:

قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ

Sema: “Siimilikii nafsi yangu dhara wala manufaa isipokuwa Aliyotaka Allaah. [Yuwnus: 49]

 

 

5. Kuusoma uradi huo ni kuufadhilisha uradi huo badala ya nyiradi au du’aa zilizothibiti katika Sunnah na hivyo kudharau mafundisho ya Sunnah na kumtuhumu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba amekasiri katika kuwafundisha yale wanayohitajia Waislamu katika hali za shida na dhiki; ilhali yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

((مَا تَرَكْتُ شَيْئًا يُقَرِّبُكُمْ إِلى اللهِ إِلاَّ وَأَمَرْتُكُمْ بِهِ، وَمَا تَرَكْتُ شَيْئًا يُبْعِدُكُمْ عَنِ اللهِ إِلاَّ وَقَدْ نَهَيْتُكُمْ عَنْهُ))

“Sikuacha jambo lolote linalokukurubisheni kwa Allaah isipokuwa nimeshakuamrisheni nalo. Na sikuacha jambo lolote linalokubaidisheni na Allaah ila nimeshakukatazeni nalo.” [Atw-Twabaraaniy Isnaad yake ni Swahiyh. Rejea Swiffatu-Swalatin-Nabiy (3/942) ya Imaam Al-Albaaniy].

 

 

Kwa hiyo, uradi huo unapelekea katika ushirikina na kuacha mafundisho ya Sunnah na badala yake kupelekea kwenye uzushi. Basi haifai kabisa kwa Muislam kuusoma wala kushiriki ndani yake. 

 

 

 

Share

27-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Bid’ah: Kutawassal Kwa Du'aa Kanzul-'Arsh (Ganjul-Arsh)

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah

 

27-Kutawassal Kwa Du'aa Ya Kanzul-‘Arsh  (Ganjul-‘Arsh)

 

 

 

 

 Kanzul-‘Arsh (Ganjul-‘Arsh) - كنز العرش

 

Du'aa au uradi huo wa “Kanzul-‘Arsh” (Hazina ya ‘Arsh ya Allaah) inajulikana  katika jamii yetu ya Kiswahili kama “Ganjul-‘Arsh” na hivyo kwa sababu  ndivyo inavyotamkwa katika jamii za Bara la Hindi.

 

Ndani yake kuna mkusanyiko wa du’aa na maneno ambayo yaliyokusanywa kwa wale ‘Muridu’ wa ki-Sufi wazisome na kuzirudia katika nyakati maalum na kwa muundo fulani na kwa idadi maalum inayojulikana kwao.

 

Kadhaalika, du'aa hiyo vilevile imo katika vitabu vya Kishia na wanachangia sana kuieneza.

 

 

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hapana shaka kwamba adkhaar na du’aa ni ‘ibaadah bora kabisa, na ‘ibaadah ni jambo mojawapo ambalo hakuna upenyo wa mtu kuleta rai zake. Inatupasa tufuate aliyotufunza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na si hawaa na matamanio yetu au uzushi. Du’aa na adhkaar za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni bora zaidi kuliko zozote nyinginezo. Na mwenye kuzifuata atabakia salama na kutenda yaliyo sahihi, na manufaa na matokeo mazuri atakayochuma ni mengi hata hayaelezeki.

 

Du’aa na adhkaar zozote nyinginezo zinakuwa ni haramu au makruhu kwani zinaweza kuhusiana na shirk japokuwa watu wengi hawatambui hilo. Maelezo yake ni marefu mno kuyaelezea hapa.

 

Mtu hana haki kufundisha watu du’aa au adhkaar zozote zisizokuwa katika Sunnah, au kuzifanya kuwa ni ‘ibaadah ya mazoea ambayo anategema watu kuifanya kama wafanyavyo Swalaah tano. Huu ni uzushi katika Dini ambao Allaah Hajautolea idhini. Ama kupanga uradi au kusoma kwa kudumisha adhkaar ambazo hazikuamrishwa katika shariy’ah, ni jambo lisiloruhusiwa.

 

Du’aa na adhkaar zilizoamrishwa katika shariy’ah, ni bora zaidi kwa yeyote kuzitaraji na kuzipata na hakuna anayezipuuza kwa kufadhilisha zilizo mpya za uzushi, au adhkaar za uzushi isipokuwa ambaye ni mjinga au mtendaji makosa.” [Majmuw’ Al-Fataawa (22/510/511)]

 

 

Uradi au du’aa hiyo ya Kanzul-‘Arsh imetangulia kutajwa katika kijitabu chake:   

 

الدعاء المكتوب حول عرش الرحمن ، اقرأ هذا الدعاء ولو مرة واحدة في حياتك  وياحبذا لو قرأته في حب الله وليس في حب الثواب، قيل أن جبريل عليه السلام أتى النبي صلى الله علية وسلم فقال: يا محمد، السلام يُقرئك السلام، ويخصك بالتحية والإكرام، وقد أوهبك هذا الدعاء الشريف!  يا محمد، ما من عبد يدعو وتكون خطاياه وذنوبه مثل أمواج البحار، وعدد أوراق الأشجار، وقطر الأمطار، وبوزن السموات والأرض، إلا غفر الله تعالى ذلك كله له -  يا محمد، هذا الدعاء مكتوب حول العرش، ومكتوب على حيطان الجنة وأبوابها، وجميع ما فيها...يا محمد أنزل بالوحي ببركة هذا الدعاء وأصعد به، وبهذا الدعاء تُفتح أبواب الجنة يوم القيامة، وما من ملك مقرب إلا تقرب إلى ربه ببركته!

 

Du’aa imeandikwa kuizunguka ‘Arshi ya Ar-Rahmaan. Soma du’aa hii japo mara moja katika uhai wako. Ee laiti ukaisoma kwa kupata mapenzi ya Allaah na si kwa mapenzi ya thawabu.

Inasemekana kwamba Jibriyl ('Alayhis-Salaam) alimwendea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Ee Muhammad! As-Salaam Anakutolea salaam, na Anakuamkia kwa maamkizi na heshima, na Amekutunukia du’aa hii tukufu.

Ee Muhammad, hakuna mja atakayeiomba hali yakuwa ana makosa yake na dhambi zake zinafikia mawimbi ya bahari, na yanafikia idadi ya majani katika miti yote, na matone ya mvua, na kwa uzito wa mbingu na ardhi isipokuwa Allaah Atamghufuria yote.

Ee Muhammad! Du’aa hii imeandikwa kuizunguka ‘Arshi na katika kuta za Jannah na milango yake, na yote yaliyomo humo.

Ee Muhammad (Allaah) Ameteremsha wahyi kwa baraka ya du’aa hii na Anapandisha kwa baraka ya du’aa hii, na kwa baraka ya du’aa, milango ya Jannah itafunguliwa Siku ya Qiyaamah, Na hakuna Malaika aliyekurubishwa isipokuwa atajikurubisha kwa Mola Wake kwa baraka ya du’aa hii."

 

ومن قرأ هذا الدعاء أمِن من عذاب القبر، ومن الطعن والطاعون، وينتصر ببركته على أعدائهـا يا محمد، من قرأ هذا الدعاء تكون يدك في يده يوم القيامة، ومن قرأ هذا الدعاء يكون وجهه كالقمر ليلة البدر عند تمامها، والحلق في عرسات القيامة ينظرون إليه كأنه نبي من الأنبياء

 

Na Atakayeisoma du’aa hii atasalimika na adhabu ya kaburi, na atasalimika na maradhi ya tauni na atanusurika na maadui wake kutokana na baraka yake (hii du'aa). Ee Muhammad! Atakayeisoma du’aa hii, basi mkono wako utakuwa katika mkono wake Siku ya Qiyaamah, na atakayeisoma du’aa hii uso wake utakuwa kama uso wa mwezi usiku wa mwezi kuwa kamilifu na mkusanyiko katika viwanja vya Qiyaamah wakimtazama kama kwamba yeye ni miongoni mwa Manabii. 

 

 

Haijuzu kuisoma du’aa au uradi huo wa Kanzul-‘Arsh  kwa sababu zifuatazo:

 

1. Ni uzushi na uzushi ni dhambi na unamuandalia makazi ya motoni mwenye kuzua na mwenye kuisambaza. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

((مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ)) البخاري

((Atakayenizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni.)) [Al-Bukhaariy]

 

 

2. Du’aa hiyo imevuka mipaka katika kuitukuza ‘Arshi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

 

3. Uradi huo ni uzushi wa Masufi na Mashia wa “Kanzul-‘Arsh” au “Ganjul-‘Arsh” kama wengine wanavyoiita na ambayo yamenukuliwa humo kuhusu fadhila zake; ni uzushi achilia mbali kuwa ina mambo yanayokwenda kinyume na matini (nuswuws) za Qur-aan na Sunnah.

 

4. Miongoni mwayo ni kumpa majina Allaah kwa majina yasiyothibiti katika Kitabu cha Allaah wala Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Mfano: Al-Burhaan (dalili). As-Swaafiy (halisi), Al-Mu’jiz (Wa Miujiza), Al-Qadiym (Wa Kale), Al-Mukhlis (Anayetakasa wengineo), Al-Faadhwil (Anayefadhilisha).  Majina yote haya si miongoni mwa Majina Mazuri ya Allaah na Sifa Zake.

 

 

5. Baada ya utafiti, imetambulika kuwa du’aa hiyo ya uzushi imenukuliwa kwa kauli mbali mbali tofauti na baadhi ya maneno yasiyofahamika maana yake na mengine makosa kataika uandishi wa Kiarabu, na hii ni dalili tosha kuwa kuwa ni uzushi wa kutupwa.

 

 

Mfano kuna wanaosema inaanza na:

 

لا إله إلا الله الملك الحق المبين،لا إله إلا الله العدل اليقين،لا إله إلا الله ربنا ورب آبائنا الأولين،سبحانك إني كنت من الظالمين،لا إله إلا الله  وحده لا شريك له،له الملك وله الحمد يُحيي ويُميت وهو حي لا يموت، بيده الخير وإليه المصير، وهو على كل شيء قدير.

 

Wengine wamenukuu:

 

لا إله إلا الله الحليم الكريم لا إله إلا الله العلي العظيم لا إله إلا الله الملك الحق المبين لا إله إلا الله الحق العدل اليقين لا إله إلا الله ربنا و رب آبائنا الأولين لا إله إلا أنت سبحانك إني كنت من الظالمين لا إله إلا الله وحده لا شريك له له الملك و له الحمد يحيي و يميت و يميت و يحيي و هو حي لا يموت بيده الخير و هو على كل شي‏ء قدير  

 

Wengine wamenukuu:

 

اللهم اني اسالك باسمك الذي اذا ذكرت به تزعزعت منه السماوات وانشقت منه الارضون وتقطعت منه السحاب وتصدعت منه الجبال وجرت منه الرياح وانتقصت منه البحار واضطربت منه الامواج وغارت منه النفوس ووجلت القلوب وزلت منه الاقدام وصمت منه النفوس ووجلت منه القلوب وزلت منه الاقدام وصمت منه الاذان وشخصت منه الابصار وخشعت منه الاصوات وخضعت له الرقاب وقامت له الارواح وسجدت له الملائكة

 

Wengine wamenukuu:

 

بسم الله الرحمنِ الرحيمِ ولا حول ولا قوة إلا بالله العلي العظيم لا إله إلا الله محمدٌ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم*  أستغفرُ اللهَ العظيمَ الذي لا إله إلا هو الحيَّ القيُّومَ بديعَ السماواتِ والأرضِ وما بينهما غفَّـارَ الذنوبِ سَتَّـارَ العيُوبِ مقلِّبَ القلُـوبِ كشَّافَ الكرُوبِ علاَّمَ الغيُوبِ * وأتوبُ إليهِ توبةَ عبدٍ صَاغِرٍ ظالِمٌ لنفسِهِ ذليـلٌ لا يملِكُ لنفسهِ ضَرَّاً ولا نفعاً ولا حياةً ولا موتاً ولا نُشوراً* يا عزيزُ يا غفَّارُ يا كريمُ يا ستَّارُ يا بارُّ يا رَبِّ يا ربّ يا رّبِّ أنا عَصَيْتُ وأنا جَنَيْتُ وأنا خالفتُ وأنا أخطأتُ ، يا مُنجِّـي موسى ، والخليلُ إبراهيم ، والمصطفى محمَّدٍ عليهُمُ الصلاة والسلام ، أسألُك يااللهُ ياحَيُّ يا قيُّومُ يا عليُّ يا عظيمُ يا رحمنُ يا رحيمُ * أنْ لا إلهَ إلا أنتَ سُبحانَك إنِّي كنتُ من الظَّالمينَ يا من لا يَخْفَى عليهِ

 

Basi tazama jinsi uongo na uzushi unavyodhihirika kwa wazushi kwa jinsi wanavyotofautiana katika kuzusha!

 

 

Tahadhari Muislamu!

 

Waislamu wanapaswa kujihadhari sana na uzushi mwingi unaotungwa na Mashia na Masufi haswa katika kupitia mlango wa du'aa. Katika mlango huo, kumepenyezwa mengi ya kumzulia Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuizulia Dini hii tukufu ya Kiislamu.

 

Tunawanasihi Waislamu wasio na maarifa ya kutosha kwenye Dini yao, wahakikishe jambo lolote linaloenezwa kuhusu Dini na haswa haswa haya mas-alah ya du'aa, wawaulize wajuzi kabla hawajaingia katika kusambaza haraka haraka wakidhania ni khayr na kuna kupata ujira na haswa zama hizi zenye njia nyepesi za usambazaji wa khabari kupitia Whatsapp, Telegram na mitandao mingine ya kijamii.

 

Na katika mambo ya kumfanya Muislamu atahadhari na azinduke haraka, ni pindi atakapoona ujumbe umeandikwa mwisho wake, "watumie watu 10 au 50", au "usibakishe ujumbe huu kwenye simu yako au inbox yako kama unampenda Mtume au kama unampenda Allaah", au "Katika saa moja hakikisha huu ujumbe unawafikia watu 500 au 1000", au "Tuma ujumbe huu na utaona maajabu au miujiza", au " Usipotuma ujumbe huu utapatwa na balaa kadhaa, na ukituma ujumbe huu utapata thawabu kadhaa"!!

 

Hizo zote ni katika alama za uzushi na ujumbe wa uzushi, tahadhari nazo jumbe kama hizo. Usiharakishe kueneza wala kutuma. Ukiwa huna uhakika, uliza wajuzi. Na ukiwa ni mwenye maarifa, wakanye wanaoeneza na waelimishe khatari ya kuzua na umuhimu wa kufuata mafundisho sahihi yaliyothibiti.

 

Kuna du'aa nyingi sana na adhkaar ambazo ni sahihi na zimethibiti katika Qur-aan na Sunnah na watu hawazijui wala hawawezi kuzimaliza kuzisoma au kuzihifadhi na wengi hawazijui, lakini wengi wanahangaika na du'a na adhkaar za uzushi zilizotungwa na wazushi wa Kishia na Kisufi! Na huu ndio katika moja ya mitihani iliyoikumba hii Dini yetu.

 

Tunamuomba Allaah afya na salama.

 

 

 

Share

28-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Du'aa Ya Al-Fawz Wal-Qabuwl

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah

 

28-Kutawassal Kwa Du’aa Ya  "Al-Fawz Wal-Qabuwl"

 

 

 

 

 Al-Fawz Wal-Qubuwl -  الفوز والقبول

 

Du’aa hiyo iliyopewa jina la "Al-Fawz wal-Qabuwl" (Kufuzu na kutakabaliwa) ni du’aa ya uzushi iliyoandaliwa katika kijitabu kidogo kabisa ambayo imeenea katika jamii mbali mbali ikiwemo jamii yetu ya Kiswahili.  

 

Imaam Ash-Shawkaaniy amesema katika ‘Al-Fawaaid Al-Majmuw’ah’: “Hadiyth isemayo: “Hakuna mja wa kike wala wa kiume amwombe Allaah au atake kitu usiku wa ‘Arafah kwa du’aa hii nayo ni maneno kumi, ila Allaah Atampa, isipokuwa kukata ukoo au dhambi…ikikusudiwa duaa inayosema - Subhaana-LLadhiy fis-Samaai ‘Arshuhuu…“

 

Inadaiwa imesimuliwa na Al-‘Uqayliy kutoka kwa Ibn Mas’uwd. Usimulizi unaodaiwa ni marfuw’ lakini katika isnaad yake kuna ‘Uzrah bin Qays Al-Yahmadiy, ambaye ni dhaifu.

 

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema: “Du’aa hii yenye maneno (kumi) isomwe mara elfu usiku wa ‘Arafah; ni katika bid’ah za ‘Arafah. Ametaja hivyo katika Kitabu chake cha Manaasik Al-Hajj wal-‘Umrah na kitabu chake ‘Hajjatun-Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)“ [Markaz Al-Fatwa namba 66019]

 

 

Du’aa hiyo ya uzushi ya Al-Fawza Wal-Qubuwl  inaanza kama ifuatavyo:

 

تعلموا هذا الدعاء فإنه تعلمه الأولياء والصالحون، فوالذي بعثني بالحق نبيا مادعا بهذا الدعاء أحد في عمره مرة واحده أو ساعه أو يوما أو شهرا إلا أدخله الله الجنه بلا حساب ولا عقاب وإن الملائكه يستغفرون له بأجمعهم ويصلون عليه، والذي بعثني بالحق بشيرا ونذيرا مادعا بهذا الدعاء مسلم في مفازه مخيفه إلا أمن ولا جائع إلا شبع ولا عريان إلاكساه الله ولا عطشان إلا رواه الله ولا مديون إلا قضى الله دينه ولا مكروب إلا فرج الله كربه ولا مغموم إلا أذهب الله غم.

 

"Jifunzeni du’aa hiyo kwani wamejifunza awliyaa na Swaalihiyna, kwani naapa kwa Ambaye Amenituma kuwa Nabiy, hakuna aombaye du’aa hii katika umri wake mara moja au saa moja, au siku moja au mwezi mmoja, isipokuwa Allaah Atamuingiza Jannah bila hesabu wala adhabu na Malaika wanamuombea maghfirah wote kwa umoja na wanamswalia. Naapa kwa Ambaye Amenituma kwa haki kuwa mbashiriaji na mwonyaji, hakuna Muislamu aliyekuwa katika khofu akaomba du’aa hii isipokuwa atakuwa katika amani, wala mwenye njaa isipokuwa atashiba, wala aliye uchi isipokuwa Allaah Atamvisha, wala mwenye kiu isipokuwa Allaah Atamnywesha, wala mwenye deni isipokuwa Allaah Atamkidhia deni lake, wala mwenye dhiki isipokuwa Allaah Atampa faraja kumtoa katika dhiki yake, wala mwenye ghamu (huzuni) isipokuwa Allaah Atamuondoshea ghamu yake…"

 

 

Du’aa hiyo ya uzushi ya Al-Fawz Wal-Qubuwl inaendelea mpaka inafikia kutaja:

 

 

من كتبه وجعله حرزا كفاه الله شر مايخافه ويحذره، ومن مات ثم جعله في عنقه كان له انيسا في قبره ووكل الله به ملائكه يحفظونه من كل سوء، ويكفيه الله شر منكر ونكير وما في يوم القيامه والملائكه عن يمينه وعن شماله ويجعله الله في أعلا عليين، ويبني له بيتا في الجنه من لؤلؤة بيضاء يرى باطنها من ظاهرها، ويفتح الله له مائة ألف باب في كل باب مائة ألف مدينه وفي كل مدينه مائة ألف قصر وفي كل قصر مائة ألف حجرة في كل حجرة مائة ألف زاويه في كل زاويه مائة ألف صفه في كل صفه مائة ألف سرير في كل سرير مائة ألف فراش في كل فراش مائة ألف حوريه لكل حوريه مائة ألف حلة معها كاس مملوء من شراب ، ثم ترفعه الملائكه على سرير من نور ويقبل الله عز وجل عليه من فوق العرش ثم يقول الله: ياعبدي أنا راض عليك بفضيلة هذا الدعاء.

"Atakayeiandika na kuifanya ni hirizi, Allaah Atamuondoshea shari anayokhofia na kuitahadhari, na atakayefariki kisha akaweka katika shingo yake, itakuwa ni kiliwazo katika kaburi lake, na Allaah Atamwakilishia Malaika wamhifadhi na kila ovu, na Allaah Atamtoshelezea shari za Munkar na Nakiyr (Malaika wawili watakaouliza wafu kaburini maswali matatu), na pia (Atamtosheleza) yale yaliyoko Siku ya Qiyaamah, na ambayo ya Malaika wa kuliani kwake na kushotoni kwake, na Allaah Atamjaalia awe miongoni mwa watu wa ‘Illiyyiyn (daraja ya juu kabisa ya watu wema), na Allaah Atamjengea nyumba huko Jannah ya lulu nyeupe ambayo inaonekana ndani yake kutoka nje yake, na Allaah Atamfungulia milango laki moja, kila mlango ataona miji laki moja na kila mji kuna maqasri (majumba ya fakhari) laki moja,  na kila qasri kuna vyumba laki moja na kila  chumba kuna kona laki moja, na kila kona kuna wanda (eneo, nafasi) laki moja na kila wanda kuna vitanda laki moja, na kila kitanda kina matandiko laki moja, na kila tandiko kuna mahuri (wanawake wazuri wa Jannah) laki moja, na kila huri ana mapambo ya thamani laki moja, na kila mmoja ana bilauri yenye kinywaji, kisha Malaika atamnyanyua kwenye kitanda kisha Allaah Atamkabili kutoka katika ‘Arshi Yake kisha Allaah Atasema: “Ee mja wangu, Mimi niko radhi nawe kwa fadhila ya du’aa hii..."

 

Du’aa yenyewe ya uzushi Al-Fawz Wal-Qubuwl  ni ifuatayo:

 

سبحان الذي في السماء عرشه، سبحان الذي في الأرض ملكه، سبحان الذي في الجنه رحمته، سبحان الذي في النار سلطانه، سبحان الذي في الهواء روحه، سبحان الذي في القبور قضاؤه، سبحان الذي لا منجا منه إلا إليه في الدنيا والآخره، سبحانك انت الله العزيز الحكيم، سبحانك انت الله رب العالمين، سبحانك انت الله الرحمن الرحيم، سبحانك انت الله الملك القدوس، سبحانك انت الله المؤمن المهيمن ، سبحانك انت الله الجبار المتكبر، سبحانك انت الله الخالق البارئ، سبحانك انت الله المصور الحكيم، سبحانك انت الله السميع العليم، سبحانك انت الله البصير الصادق، سبحانك انت الله اللطيف الواسع، سبحانك انت الله الولي الكبير، سبحانك انت الله البديع الاحد، سبحانك انت الله الغفور الودود، سبحانك انت الله الشكور الحميد، سبحانك انت الله الحميد المجيد، سبحانك انت الله المبدئ المعيد، سبحانك انت الله الأول الأخير، سبحانك انت الله الظاهر الباطن، سبحانك انت الله الوكيل الكافي، سبحانك انت الله الواحد الأحد، سبحانك انت الله الفرد الصمد، سبحانك انت الله القريب الدائم، سبحانك انت الله الحق المتعال، سبحانك انت الله الباعث الوارث، سبحانك انت الله الباقي الرزاق، سبحانك انت الله الحق المبين، سبحانك انت الله العزيز المجيب، سبحانك انت الله القابض الباسط، سبحانك انت الله الرزاق الفتاح، سبحانك انت الله الولي العلي، سبحانك انت الله البديع الصمد، سبحانك انت الله الحبيب البارئ، سبحانك انت الله ذو الجلال والإكرام، سبحانك انت الله الحي القيوم، سبحانك انت الله المحيي المميت، سبحانك انت الله الناظر الخالق، سبحانك انت الله العزيز الفتاح، سبحانك انت الله الحنان المنان ، سبحانك انت الله الشكور الديان، سبحانك انت الله القدير الغفار، سبحانك انت الله الصادق العدل، سبحانك انت الله الظاهر الباطن المتعال، سبحانك انت الله الرفيع الباقي سبحانك انت الله الوهاب المعطى، سبحانك انت الله الولي البصير، سبحانك انت الله الكفيل المستعان، سبحانك انت الله المنعم المتفضل، سبحانك انت الله أرحم الراحمين، سبحانك انت الله خير الفاصلين، سبحانك انت الله خير الناصرين، سبحانك انت الله خير القادرين، سبحانك انت الله خير الوارثين، سبحانك انت الله خير الزاهدين، سبحانك انت الله خير المعطين، سبحانك انت الله الرءوف الرحيم، سبحانك إني كنت من الظالمين .
فسيكفيكم الله وهو السميع العليم .

 

Basi tazama Muislamu jinsi uongo wa wazushi ulivyozidi hadi wanazusha katika mas-alah ya msingi ya ‘Aqiydah ya Muislamu; mas-alah ambayo yako wazi kuwa mwana Aadam hana uwezo wala madaraka nayo bali yako katika uwezo na mamlaka ya Allaah. Na mengineyo yaliyomo humo ndani wanayozusha ambayo ni katika mambo ya ghayb; hakuna mwenye ‘ilmu nayo isipokuwa Allaah pekee.

 

 

Tahadhari ee ndugu Muislmu ujiepushe na du’aa hiyo ya uzushi, kwa sababu:

 

1. Hapana shaka kwamba Hadiyth hiyo ni mawdhwuw’ (ya kutungwa) na makdhuwb (ya uongo).

 

 

2. Katika alama za uongo wake ni hayo malipo ya mwenye kusoma du’aa hiyo na kwamba Allaah Ataumba kadhaa wa kadhaa kwa ajili ya du’aa hii na idadi kubwa iliyotajwa ya hayo yatakayoumbwa na Allaah au Atakayoyatoa kama thawabu! Kama vile mahuril 'ayn laki moja!

 

 

3. Du’aa hiyo inaendelea kutajwa mengi ya uzushi kama kutajwa kwamba msomaji du’aa hiyo atapata thawabu za Malaika wanne na thawabu za Manabii wanne! Na pia inadaiwa kuwa atakayeibiwa kitu basi atakipata kitu alichoibiwa. Na baya zaidi ni kutaja ya kumshirikisha Allaah kuhusu kuandikwa kwake katika hirizi, jambo ambalo ni ubatilifu na shirki katika Uislamu na linafikia kumtoa mtu nje ya Uislamu! 

 

 

4. Kueneza Hadiyth za kumzulia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni khatari kwa Muislamu kuwa makazi yake yatakuwa ni motoni na kwamba ni dhambi kubwa, na kwamba atakayeeneza atabeba dhambi za kila atakayeisoma du’aa hiyo kwa dalili kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

((مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ)) البخاري

((Atakayenizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni [Al-Bukhaariy]

 

 

5. Hakuna shaka kwamba anayemuongopea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa ni mwenye kuwaongopea wenzake; amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

مَنْ حَدَّثَ عَنِّي حَدِيثًا وَهُوَ يَرَى أَنَّهُ كَذِبٌ، فَهُوَ أَحَدُ الْكَاذِبَيْنِ

(Atakayezua Hadiyth kutoka kwangu akijua kuwa  ni ya uongo basi yeye ni mmoja wa waongo wawili)) (Aliyeizua na anayeendelea kuizua) [Muslim katika Muqaddimah ya Swahiyh yake]

 

Basi haijuzu kuieneza Hadiyth hiyo, wala kuitaja fadhila zake, wala kuifanyia kazi wala haipasi kuitaja kabisa kuwa ni Hadiyth bali tunasema ni maneno ya uzushi kutoka kwa wazushi! 

 

 

 

Share

29-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Du’aa Ya "Al-Jawshan Al-Kabiyr"

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah

 

29-Kutawassal Kwa Du’aa Ya  "Al-Jawshan Al-Kabiyr"

 

 

 

 

Al-Jawshan Al-Kabiyr (Diraya Kubwa) الجوشن الكبير

 

 

Hii ni du’aa ya uzushi na iliyojaa uongo.  Inadai yafuatayo:

 

 

a)Jibriyl alimshukia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa katika vita akiwa na jawshan (diraya - vazi la kiaskari kama kizibao cha ngozi ngumu au chuma) akasema: Ee Muhammad, Rabb wako Anakupa salamu, Anakwambia vua hilo al-jawshan, na soma du’aa hii, kwani hiyo ni amani kwako na umma wako.”

 

 

b) “Atakayeiandika katika kafani yake, Allaah Atastahi kumuadhibu na moto. Na Atakayeiomba kwa nia safi mwanzo wa mwezi wa Ramadhwaan, Allaah Atamruzuku usiku wa Layalatul-Qadr, na Atamuumbia Malaika elfu sabiini wanamsabbih Allaah, na wanamtukuza, na Atajaalia thawabu zao kwake. Na atakayeomba katika mwezi wa Ramadhwaan mara tatu, Allaah Ataharamisha mwili wake dhidi ya moto, na atawajibika Pepo, na Allaah Atamwakilishia Malaika wawili wamhifadhi na maasi, na atakuwa katika amani ya Allaah uhai wake wote.”

 

 

c) “Al-Husayn amesema: ameniusia baba yangu ‘Aliy bin Abiy Twaalib kuhifadhi du’aa hii, na kuitukuza, na kuiandika katika kafani yake, na niwafundishe ahli yangu, na niwahimize nayo, nayo ni majina elfu na humo mna jina tukufu kabisa.”.

 

 

d) “Yeyote atakayeisoma na kuibeba (kuifanyia hirizi) anapotoka nyumbani kwake wakati wa Swalaah ya Alfajiri au Swalaah ya ‘Ishaa, itakuwa kama amefanya vitendo vikubwa vyema na kama kwamba amesoma Tawraat, Injiyl na Zabuwr na Qur-aan.”

 

 

Haya yamezidi uongo kwani hakuna kilicho sawa na vitabu vya Allaah! 

 

 

e) “Allaah Atampa kwa kila herufi asomayo, wake wawili wa huwrul’ayn (wanawake wa Peponi wenye macho mazuri) na Atamjengea kasri Peponi na Allaah Atampa thawabu kama hizo za Manabii wane; Ibraahiym, Muwsa, ‘Iysa na Muhammad.”

 

Huu ni uongo wa dhahiri kwani thawabu za Mitume hazipati yeyote ila wenyewe! 

 

 

f) “Allaah Atampa thawabu sawa na jini dume na jike la miongoni mwa majini walioamini tokea siku Aliyowaumba hadi siku ya kufufuliwa na Allaah Atampa thawabu za mashuhadaa 900,000.”.

 

 

g) “Du’aa hii ina manufaa kupata mapenzi na kufaulu kuondosha fundo za ndimi, kukabiliana na mahakimu, maamiri na wafalme na kuepusha mbali silaha zote za vyuma na risasi na kukidhia  haja n.k.”

 

 

Lililo dhahiri kwamba du’aa hiyo imejaa kauli za uongo za kila aina, na imejaa madai ya fadhila na mahadhi. Na la ajabu zaidi ni kwamba du’aa hiyo ni ndefu mno kupita kiasi kufikia idadi ya nukta mia (100) za hiyo duaa! 

 

Hili si jambo la kawaida abadani katika du’aa za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu aghlabu ya du’aa zake ni fupi zenye mkusanyiko wa maneno kwa dalili:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ:  ((فُضِّلْتُ عَلَى الأَنْبِيَاءِ بِسِتٍّ:  أُعْطِيتُ جَوَامِعَ الْكَلِمِ، وَنُصِرْتُ بِالرُّعْبِ، وَأُحِلَّتْ لِيَ الْغَنَائِمُ، وَجُعِلَتْ لِيَ الأَرْضُ طَهُورًا وَمَسْجِدًا، وَأُرْسِلْتُ إِلَى الْخَلْقِ كَافَّةً، وَخُتِمَ بِيَ النَّبِيُّونَ))

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraryah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nimefadhilishwa juu ya Manabii kwa mambo sita; nimepewa ‘Jawaami’ul-Kalimi’ (Mjumuisho wa maana nyingi katika maneno machache) na nimenusuriwa kwa [kutiwa] hofu [katika nyoyo za maadui] na nimehalalishiwa ghanima  na nimefanyiwa ardhi kuwa kitoharishi na masjid [mahali pa kuswali], na nimetumwa kwa viumbe wote, na Manabii wamekhitimishwa kwangu)) [Muslim]

 

Na pia kama alivyosimulia ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa):

 "كَانَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه وسلم) يَسْتَحِبُّ الْجَوَامِعَ مِنَ الدُّعَاءِ، وَيَدَعُ مَا سِوَى ذَلِكَ".

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akistahabu du’aa za ujumla na akiacha zisizokuwa kama hizo.” [Abu Daawuwd na Ameipa daraja ya Swahiyh Shaykh Al-Baaniy]

 

Kauli yake: “Akistahabu du’aa za ujumla.” Ina maana; zinazojumuisha malengo mema na makusudio sahihi au zinazojumuisha thanaa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na adabu za mas-ala. Na kauli yake. “Akiacha zisizokuwa kama hizo.” Amekusudia du’aa ndefu na ambazo hazijumuishi malengo sahihi.” [Sharh Sunan Abu Daawuwd 5/397-398 na katika ‘Awnil-Ma’buwd 4/249] 

 

Kauli yake: “Za ujumla.” Ina maana; kheri za dunia na Aakhirah na hiyo kwa lafdhi ya uchache. Maana yake, wingi, kama kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿٢٠١﴾

Na miongoni mwao kuna wasemao: “Rabb wetu Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na Tukinge na adhabu ya moto.” [Al-Baqarah: 201]

  

 

Na mfano wa du’aa za afya duniani na Akhera.” [Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuuth Al-‘Ilmiyyah wal-Iftaa (23/239)]  

 

 

Du’aa hiyo imo katika vitabu vya Mashia.  Imesimuliwa katika vitabu vyao kwa isnadi iliyotungwa na kubuniwa.    Miongoni mwa hivyo vitabu vya Mashia vyenye du’aa hiyo ni kile kiitwacho: ‘Mafaatiyhul Jinaan.’ Na katika mambo Mashia wanayoyafanya wanaposoma du’aa hiyo ni kuweka Misahafu vichwani mwao wanapofika maeneo fulani kwenye du’aa hiyo! Basi hebu tanabahi ee ndugu Muislamu ujahili kama huo na vituko kama hivyo kisha jiulize na fanya utafiti kama utakuta hayo kuwa ni katika mafunzo ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake. Hakika ni uvukaji mipaka wa uzushi!

 

 

Anasema Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah): “Huwezi kukuta mongoni mwa makundi yanayodai ni katika watu wa Qiblah (Waislam) walio na ujahili mkubwa kuliko Mashia (Raafidhwah), na hakuna waipendao dunia kama wao, na nimewatafiti na kuona kuwa aibu na kasoro zote wanazowasingizia nazo Maswahaba, basi wao ndio waliojawa nazo kuliko kiumbe chochote, na Maswahaba wametakasika kabisa na hayo. Hakuna shaka yoyote ile kuwa hakuna watu waongo kupita kiasi kama wao (Mashia). Ni kama yule Musaylamah al-Kadh-dhaab ambaye alidai: “Mimi ni Mtume mkweli, na Muhammad ni muongo!” Ndio kama Mashia wanaojisifu na kujitukuza kwa imani na wakiwatuhumu Maswahaba kuwa ni wanafiki, bali wao Mashia ndio katika kundi lenye unafiki mkubwa kuliko makundi yote. Na hakika Maswahaba ndio viumbe vyenye Iymaan kubwa kabisa” [Minhaajus Sunnah An-Nabawiyyah, mj. 2, uk. 87]

 

 

Tahadhari ee ndugu Muislamu na du’aa hiyo ambayo nukuu yake inaanza  kama ifuatavyo:

 

 

 

(1) اَللّـهُمَّ اِنّي اَسْأَلُكَ بِاسْمِكَ يا اَللهُ يا رَحْمنُ يا رَحيمُ يا كَريمُ يا مُقيمُ يا عَظيمُ يا قَديمُ يا عَليمُ يا حَليمُ يا حَكيمُ سُبْحانَكَ يا لا اِلـهَ إلاّ اَنْتَ الْغَوْثَ الْغَوْثَ خَلِّصْنا مِنَ النّارِ يا رَبِّ

 

(2) يا سَيِّدَ السّاداتِ يا مُجيبَ الدَّعَواتِ يا رافِعَ الدَّرَجاتِ يا وَلِيَّ الْحَسَناتِ يا غافِرَ الْخَطيئاتِ يا مُعْطِيَ الْمَسْأَلاتِ يا قابِلَ التَّوْباتِ يا سامِعَ الاْصْواتِ يا عالِمَ الْخَفِيّاتِ يا دافِعَ الْبَلِيّاتِ

 

(3) يا خَيْرَ الْغافِرينَ يا خَيْرَ الْفاتِحينَ يا خَيْرَ النّاصِرينَ يا خَيْرَ الْحاكِمينَ يا خَيْرَ الرّازِقينَ يا خَيْرَ الْوارِثينَ يا خَيْرَ الْحامِدينَ يا خَيْرَ الذّاكِرينَ يا خَيْرَ الْمُنْزِلينَ يا خَيْرَ الْمحْسِنينَ

 

(4) يا مَنْ لَهُ الْعِزَّةُ وَالْجَمالُ يا مَنْ لَهُ الْقُدْرَةُ وَالْكَمالُ يا مَنْ لَهُ الْمُلْكُ وَالْجَلالُ يا مَنْ هُوَ الْكَبيرُ الْمُتَعالُ يا مُنْشِىءَ الْسَّحابِ الثِّقالِ يا مَنْ هُوَ شَديدُ الْمحالِ يا مَنْ هُوَ سَريعُ الْحِسابِ يا مَنْ هُوَ شَديدُ الْعِقابِ يا مَنْ عِنْدَهُ حُسْنُ الثَّوابِ يا مَنْ عِنْدَهُ اُمُّ الْكِتابِ

 

(5) اَللّـهُمَّ اِنّي اَسْأَلُكَ بِاسْمِكَ يا حَنّانُ يا مَنّانُ يا دَيّانُ يا بُرْهانُ يا سُلْطانُ يا رِضْوانُ يا غُفْرانُ يا سُبْحانُ يا مُسْتَعانُ يا ذَا الْمَنِّ وَالْبَيانِ

 

(6) يا مَنْ تَواضَعَ كُلُّ شَيْءٍ لِعَظَمَتِهِ يا مَنِ اسْتَسْلَمَ كُلُّ شَيْءٍ لِقُدْرَتِهِ يا مَنْ ذَلَّ كُلُّ شَيْءٍ لِعِزَّتِهِ يا مَنْ خَضَعَ كُلُّ شَيْءٍ لِهَيْبَتِهِ يا مَنِ انْقادَ كُلُّ شَيْءٍ مِنْ خَشْيَتِهِ يا مَنْ تَشَقَّقَتِ الْجِبالُ مِنْ مَخافَتِهِ يا مَنْ قامَتِ السَّماواتُ بِاَمْرِهِ يا مَنِ اسْتَقَرَّتِ الاْرَضُونَ بِاِذْنِهِ يا مَنْ يُسَبِّحُ الرَّعْدُ بِحَمْدِهِ يا مَنْ لا يَعْتَدي عَلى اَهْلِ مَمْلَكَتِهِ

(7) يا غافِرَ الْخَطايا يا كاشِفَ الْبَلايا يا مُنْتَهَى الرَّجايا يا مُجْزِلَ الْعَطايا يا واهِبَ الْهَدايا يا رازِقَ الْبَرايا يا قاضِيَ الْمَنايا يا سامِعَ الشَّكايا يا باعِثَ الْبَرايا يا مُطْلِقَ الأُسارى

 

 

 

Share

30-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Uradi Wa: Wasiylatush-Shaafiy

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah

 

30-Kutawassal Kwa Uradi Wa: Wasiylatush-Shaafiy

 

 

 

 Wasiylatush-Shaafiy  وسيلة الشافي

Au:

Wasiylatun-Nabhaaniy  - وسيلة النبهاني

 

 

Uradi huu pia ni maarufu sana katika jamii. Umekusanya Majina na Sifa za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) nyingi, lakini ndani yake kuna makosa makubwa mno ya 'Aqiydah pale inaposema:

وحبذا محمد هادينا لولاه ما كنا ولا بقينا

Wahabadhaa Muhammadun haadiynaa lawlaahu maa kunnaa walaa baqaynaa.

“Na uzuri ulioje! Kwa Muhammad tumehidika, bila yeye tusingekuweko wala tusingebakia.”

 

 

Hivyo ni kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na uumbaji Wake kwani Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Al-Khaaliq (Muumbaji), Naye Ndiye Al-Qayyuwm (Mwenye kusimamia mambo ya waja Wake) na Naye Ndiye Mwenye kutoa tawfiyq ya Alhidaayah kwa waja Wake, Naye Ndiye Al-Wakiyl (Mdhamini Mwenye kutegemewa na waja Wake). Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amekariri katika Aayah kadhaa kwamba Yeye Ndiye Muumbaji wa kila kitu, mfano kauli Zake Allaah ('Azza wa Jalla):

 

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ﴿٦٢﴾

Allaah ni Muumbaji wa kila kitu, Naye juu ya kila kitu ni Mdhamini. [Az-Zumar: 62]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ﴿٨﴾

 Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Anahuisha na Anafisha; Rabb wenu na Rabb wa baba zenu wa awali. [Ad-Dukhaan: 8]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٥٤﴾

Tanabahi! Uumbaji ni Wake Pekee na kupitisha amri. Tabaaraka Allaah! (Amebarikika Allaah) Rabb wa walimwengu. [Al-A’raaf: 54]

 

‘Ulamaa wa Al-Lajnah Ad-Daaimah walipoulizwa kuhusu uradi huu wametoa Fatwa yao kwamba:

 

“Ama kuhusu Wasiylatush-Shaafiy wa An-Nabhaaniy yamedhihirika mambo mawili:

وحبذا محمد هادينا

Wahabadhaa Muhammadun haadiynaa

 

Kwamba Allaah Ametuhidi kupitia Nabiy wetu na Rasuli wetu  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), jambo ambalo lina aina ya sifa iliyopinduka mipaka.

 

La pili ni kauli:

 

اللهم اغفر لي ولعبدك المذنب الضعيف يوسف بن إسماعيل النبهاني مؤلف هذا الكتاب، وأدخلني وإياه الجنة من غير سابقة عذاب، وأوصل إلى روحه ثواب هذه الفاتحة. وبعد قراءتها يقول... إلخ

 Allaahumma-Ghfir-liy wa li’Abdika al-mudhnibi adhw-dhwa’iyfi Yuwsufa bni Ismaa’iyla An-Nabhaaniy muallifi haadhal-kitaabi, wa Adkhil-niy wa iyyaahu Al-Jannata min ghayri saabiqatin ‘adhaab, wa Awswil ilaa Ruwhihi thawaaba haadhihi Al-Faatihati!

 

“Ee Allaah, nighufurie pamoja na mja Wako mwenye dhambi, aliye dhaifu, Yuwsuf bin Ismaa’iyl An-Nabhaaniy, mwandishi wa kitabu hiki na niingize pamoja naye Jannah bila ya kutangulia adhabu na Mfikishie roho yake thawabu za hii Al-Faatihah! (inasomwa Suwratul Faatihah kisha inasemwa kadhaa wa kadhaa …)

 

Hakuna shariy’ah ya kuwasomea Qur-aan waliokufa na kuwaombea thawabu zake ziwafikie, kwa sababu hakuna dalili ya hilo. Na An-Nabhaaniy amefariki mwaka 1350H ana majanga katika ‘Aqiydah na ana uvukaji mipaka wa bid'ah na shirki katika vitu alivyoviandika vingine ambavyo ‘Ulamaa wametahadharisha. Na miongoni mwa ‘Ulamaa aliyemradi ni Shaykh Mahmuwd Shukriy Al-Aaluwsiy (Rahimahu-Allaah) katika kitabu chake: ‘Ghaayat Al-Amaaniy fiy ar-radd ‘alaa An-Nabhaaniy’. 

 

Basi inampasa Muislamu ailinde Dini yake, na ajiepushe na vitu vilivyotungwa kama hivi kwa sababu ya kuweko ndani yake shari kuu ya shirki na kuhusisha waliofariki, na yote haya yanaangamiza misingi ya Dini na asasi ya Tawhiyd.  [Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth wal-Iftaa, Fatwa namba (16863)]

 

 

Na jambo hilo la kusoma Suwratul-Faatihah kama kifungulizi cha du’aa ni miongoni mwa bid’ah zilizozushwa na Masufi na Mashia. Huvutwa hiyo Al-Faatihah “Al-Faaaaatihah!” kisha husemwa mfano: “Biniyyaatil-matwluwb ……” (kwa niyyah ya kuombwa jambo…) ikiwa kama ndio tawassul!

 

 

Tahadhari ee ndugu Muislamu!  Hakuna dalili ya kuthibitisha tawassul hii kamwe! 

 

 

 

Share

31-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Kuchinja Kukusudiwa Asiyekuwa Allaah

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah

 

31- Kutawassal Kwa Kuchinja Kukusudiwa Asiyekuwa Allaah

 

 

 

 

Kuchinja ni miongoni mwa ‘ibaadah tukufu ambayo inapaswa kumkusudia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake. [Al-Kawthar: 2]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika kauli Yake ambayo pia ni miongoni mwa du’aa ya kufungulia Swalaah: 

إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾

“Hakika Swalaah yangu, na kuchinja kafaara na ‘ibaadah zangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu.” [Al-An’aam: 162]

 

Mifano ya vichinjo vya shirki na bid’ah ni kuchinja kwa ajili ya majini au waliokufa makaburini.

 

Kadhalika, baadhi ya mila huchinja kwa ajili ya wanandoa na kuikanyaga damu wakiitakidi kuwa ni kinga ya husda au jicho baya. 

 

Wengine huchinja kwa ajili kumwaga damu katika nyumba mpya wanayohamia na hali kuna du’aa kutoka katika Sunnah iliyothibiti pindi mtu anapoteremka katika sehemu (makazi) mpya kama ifuatavyo:  

 

عن خَوْلَةَ بِنْتَ حَكِيمٍ السُّلَمِيَّةَ (رضي الله عنها) تَقُولُ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((مَنْ نَزَلَ مَنْزلاَ ثُمَّ قَالَ: "أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ" لَمْ يَضُرَّهُ شَيْءٌ حَتَّى يَرْتَحِلَ مِنْ مَنْزِلِهِ ذَلِكَ))

Kutoka kwa Khawlat bint Hakiym As-Sulamiyyah kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayeteremka katika kituo [makazi] kisha akasema:  A’uwdhu bikalimaati-LLaahit-ttaammati  min sharri maa Khalaq (Najikinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia na shari Alichokiumba), basi hakuna kitakachomdhuru hadi atakapoondoka katika kituo hicho)) [Muslim]

 

Tahadhari pia kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Humlaani mtu mwenye  kuchinja kwa kukusudia asiyekuwa Yeye.

 

عَنْ أَبِي الطُّفَيْلِ (رضي الله عنه) قَالَ: قُلْنَا لِعَلِيٍّ أَخْبِرْنَا بِشَيْءٍ أَسَرَّهُ إِلَيْكَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): فَقَالَ: مَا أَسَرَّ إِلَيَّ شَيْئًا كَتَمَهُ النَّاسَ وَلَكِنْ سَمِعْتُهُ يَقُولُ: ((لَعَنَ اللَّهُ مَنْ ذَبَحَ لِغَيْرِ اللَّهِ، وَلَعَنَ اللَّهُ، وَلَعَنَ اللَّهُ مَنْ لَعَنَ وَالِدَيْهِ وَلَعَنَ اللَّهُ مَنْ غَيَّرَ تُخُومَ الأَرْض))

Kutoka kwa Abuu Twufayl (Radhwiya Allaahu 'anhu)  kwamba tulimuuliza ‘Aliy: Tujulishe jambo alokutajia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni siri. Akasema: Hakunipa siri yoyote ambayo ameificha kwa watu, lakini nimemsikia akisema: ((Allaah Amelaani anayechinja pasi na Allaah, na Allaah Amelaani anayempa makazi (himaya) mzushi na Allaah Amelaani anayemlaani mzazi wake, na Allaah Amelaani anayebadilisha mistari ya mipaka ya ardhi [anayomiliki])) [Muslim, An-Nasaaiy, Ahmad]

 

Na maana ya laana ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kuepushwa na rahmah Zake.   

 

Kwa vile kuchinja ni ‘ibaadah ya kumkurubisha mja kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), basi inapasa kutahadhari kutokumshirikisha nayo kwa vyovyote vile na kwamba hata ikiwa kinachochinjwa ni kiasi kidogo vipi, basi huwa ni shirki na khatari yake ni kumuingiza mtu motoni kama ilivyonukuliwa katika Kitaab At-Tawhiyd Hadiyth: 

 

((دَخَلَ الْجَنَّةَ رَجُلٌ فِي ذُبَابc وَدَخَلَ النَّار رَجُلٌ فِي ذُبَاب)): قَالُوا: وَكَيْفَ ذَلِكَ يَا رَسُولَ الله؟ قَالَ: ((مَرَّ رَجُلانِ علَى قَوْمٍ لَهُمْ صَنَمٌ لاَ يَجُوزُهُ أحَدٌ حَتَّى يُقَرِّبَ لَهُ شَيْئاً، فَقَالُوا لإَحَدِهِمَا: قَرِّبْ، قَالَ: لَيْسَ عِنْدِي شَيْءٌ أُقَرِّبَهُ، قَالُوا بِه: قَرِّبْ وَلَوْ ذُباَبًا، فَقَرَّبَ ذُبَاباً، فَخَلُّوا سَبِيْلَهُ، فَدَخَلَ النَّارَ، وَقَالُوا لِلآخر: قَرِّبْ، فَقَالَ: مَا كُنْتُ لأُقَرِّبَ لأحَدٍ شَيْئًا دُونَ الله عَزَّ وَجَلَّ. فَضَرَبُوا عُنقَهُ، فَدَخَلَ الْجَنَّةَ)) 

((Mtu mmoja ameingia Jannah kwa nzi, na ameingia motoni mtu kwa ajili ya nzi)).  Wakasema: Vipi hivyo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: ((Watu wawili walipitia mbele ya watu walikuwa na sanamu lao, hapiti mtu hadi ajikurubishe kwa kuchinja. Wakamwambia mmoja wao: Jikurubishe! [Chinja!]  Akasema:  Sina kitu cha kujikurubisha. Wakasema: Jikurubishe japo kwa nzi.  Akajikurubisha kwa nzi. Wakamwachia apite njia akaingia motoni.  Wakawambia mwengine: Jikurubishe! Akasema: Sikuwa najikurubisha [nachinja] kwa yeyote pasi na Allaah ‘Azza wa Jalla. Wakampiga shingo [wakamuua] akaingia Jannah)). [Ahmad, Sharh Kitaab At-Tawhiyd li-Ibn  Baaz, na Majmuw’ Al-Fataawaa Ibn Baaz] 

 

Shaykh Fawzaan bin Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) akifafanua Hadiyth hiyo anasema:  

 

“[Mtu wa kwanza] Ametoa udhuru kutokuwa na kitu. Hakusema ‘hakika kuchinja pasi na Allaah haijuzu au ni munkari’ – Tunajikinga kwa Allaah.  Na hii inafahamika kwamba lau angelikuwa ana  mnyama wa kuchinja angelichinja. Wakamwambia: jikurubishe walau kwa nzi! Akajikurubisha kwa nzi, yaani akafanya hivyo kwa ajili ya sanamu wakamwachia apite njia, akaingia motoni kwa sababu ya shirki. Amejikurubisha pasi na Allaah, na 'ibra (zingatio) hapa ni niyyah na kusudio wala si kuhusu kinachochinjwa. Na kwamba hakuchukia jambo hili wala hakujiepusha nalo, bali ametoa udhuru kutokuwa na kitu na kwa hivyo amengia Motoni – Tunajikinga kwa Allaah. 

 

Na wakamwambia mwengine: Jikurubishe! Akasema: Sikuwa ni mwenye kuchinja chochote kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ‘Azza wa Jalla.

 

Amejiepusha na amechukia shirki. Wakampiga shingo yake, kwa maana wamemuua akaingia Jannah kwa sababu ya Tawhiyd. Hivyo basi, katika Hadiyth hii tukufu kuna mafunzo muhimu:

 

Kwanza: Hadiyth inaruhusu kuelezea habari za ummah zilizopita na kuelezea ilivyothibiti kwa ajili ya kuwaidhi na zingatio. 

 

Pili: Katika Hadiyth kuna dalili ya kuharamishwa kujikurubisha kwa kuchinja pasi na Allaah, na mwenye kujikurubisha pasi na Allaah, atakuwa ametenda shirki kwa sababu mtu aliyeua nzi ameingia motoni hata ikiwa ni kitu kichafu cha kutemwa (kidogo, duni mno). Na mtu wa pili amechukia shirki na amejiepusha japokuwa ilikuwa ni kitu cha kuchukizwa (duni) akaingia Jannah. 

 

Tatu: Kama alivyosema Shaykh (Rahimahu Allaah) kuhusu mas-alah ya niyyah ya 'amali za moyo, japokuwa ni kitu kichafu cha kutemwa (kidogo, duni mno) lakini itambulike kuwa niyyah ni 'amali ya moyo. 

 

Nne: Kama alivyosema Shaykh (Rahimahu Allaah) kuhusu wepesi wa bin Aadam kukaribia Jannah na moto ni kama alivyosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Jannah iko karibu zaidi kwa mmoja wenu kuliko nyuzi za viatu vyake, na moto kama hivyo)). [Al-Bukhaariy]

 

Huyu amepigwa shingo yake (ameuliwa) akaingia Jannah. Na yule wamemwachia njia akaingia motoni.  

 

Tano: Kwamba mtu aliyeua  nzi alikuwa Muumini, akaingia motoni kwa sababu ya kujikurubisha kwake kwa nzi, kwa sababu angelikua kafiri, angeliingia motoni kwa kufru yake si kwa kujikurubisha kwa nzi. Akadhihirisha kwamba alikuwa Muumini, na mas-alah haya ni khatari sana! Basi wako wapi wanaochinja kwa ajili ya makaburi, na majini, na mashaytwaan, na kwa ajili ya ardhi, na wachawi?

 

Akaonyesha kwamba shirki kubwa kabisa inamtoa mtu nje ya Dini japokuwa ikiwa ni kitu chepesi. Hivyo basi, suala la Tahwiyd na  ‘Aqiydah hayasamehewi hayo.” [Sharh Kitaab At-Tawhiyd – Baab maa jaa-a fiy adhdhab-h li-ghayri-LLaah]  

 

 

 

 

Share

32-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Vitu Vitukufu Vya Allaah

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah

 

32- Kutawassal Kwa Vitu Vitukufu Vya Allaah.

 

 

 

 

Kutawassal kwa kutafuta baraka katika vitu vitukufu vya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kuvifanya au kudhania kuwa ni sababu ya kutakabaliwa mtu du’aa yake haijuzu katika Shariy’ah kwa kuwa inaingia katika shirki.

 

Mfano ni kugusa Msahafu kisha kuomba du’aa au kugusa kuta za Misikiti mitukufu; Masjidul-Haraam au Masjidun-Nabawiy au Ka’bah, au Hajar Al-Aswad  au pia hata kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au kusugulia nguo katika kuta za vitukufu hivyo kisha kujipangusia navyo usoni au mwilini.  

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipofika Makkah kufanya twawaaf hakuashiria kuwa mtu akamate Ka’bah au Ruknul-Yamaani, au Hajar Al-Aswad (jiwe jeusi) kisha ajipangusie nalo kupata baraka zake.

 

Alilofanya ni kulibusu tu Hajar Al-Aswad, na ndio maana ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) alipolifikia na kulibusu alisema:

 

"إِنِّي أَعْلَمُ أَنَّكَ حَجَرٌ لاَ تَضُرُّ وَلاَ تَنْفَعُ وَلَوْلاَ أَنِّي رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُقَبِّلُكَ مَا قَبَّلْتُكَ"

“Hakika mimi natambua kwamba wewe ni jiwe tu, hudhuru wala hunufaishi. Na lau nisingelimuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  anakubusu, nisingelikubusu.” [ Al-Bukhaariy, Ibn Maajah na Ahmad]

 

Na ilipomfikia khabari kwamba watu wanapofika Hudaybiyah katika mti ambao tukio la bay’ah (fungamano) lilitokea chini yake, walikuwa wakiugusa na kuswali hapo n.k., basi aliukatilia mbali kukhofia watu wasiingie katika shirki. [Al-Haafidhw Ibn Hajar fiy Al-Fat-h (7/448)]

 

Pia, Maswahaba walipokuwa wanakwenda vitani, walitaka kuweka silaha zao katika mti kama kutawassal watakabaliwe kupata ushindi. Hawakujua kwamba ni jambo linalowaingiza katika kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).  Hadiyth ifuatayo inaeleza zaidi:    

 

عن أَبِي وَاقٍد اللَّيْثِيِّ (رضي الله عنه) قَالَ: خَرَجْنَا مَعَ النَّبِيِّ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) إِلَى حُنَيْنٍ وَنَحْنُ حُدَثَاءُ عَهْدٍ بِكُفْرٍ، وَلِلِمُشْرِكِينَ سِدْرَةٌ، يَعْكُفُونَ عِنْدَهَا وَيُنَوِّطُونَ بِهَا أَسْلِحَتَهُمْ، يُقَالَ لَهَا ذَاتُ أَنْوَاطٍ، فَمَرَرْنَا بِسِدْرَةٍ فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ اجْعَلْ لَنَا ذَاتَ أَنْوَاطٍ كَمَا لَهُمْ ذَاتُ أَنْوَاط. فَقَالَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم):َ((الله أكبر! هَذَا كَمَا قَالَ قَوْمُ مُوسَى "اجْعَلْ لَنَا إِلَهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ" وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَتَرْكَبُنَّ سُنَّةَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ))

Imepokewa kutoka kwa Abu Waaqid Al-Laythiyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tulitoka pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda (vitani) Hunayn nasi ndio kwanza tumetoka katika ukafiri, na washirikina walikuwa na mkunazi wanaufanyia ‘ibaadah na walikuwa wakitundika silaha zao (kupata baraka). Wakiuita ‘Dhaatu Anwaatw’. Tukapita mbele ya mkunazi tukasema: “Ee Rasuli wa Allaah, tufanyie nasi Dhaata Anwaatw kama walivyokuwa nao (makafiri) Dhaatu Anwaatw.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Allaahu Akbar!  (Allaah ni Mkubwa!) Hivi ni kama walivyosema watu wa Muwsaa “Tufanyie nasi muabudiwa kama walivyokuwa nao muabudiwa.” Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, mtafuata nyendo za walio kabla yenu [za ujahili na kufru].)) [At-Tirmidhiy; Swahiyh At-Tirmidhiy (2180)]

 

Kwa hiyo tawassul kama hizo hazijuzu kabisa.

 

 

 

Share

33-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutwassal Kwa Majini Na Mazimwi

 

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada

 

Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah

 

33-Kutwassal Kwa Majini Na Mazimwi

 

 

 

Baadhi ya Waislamu wanatafuta kujikinga na shari au kutaka poza ya maradhi na haja nyinginezo mbali mbali kwa kupitia majini, mazimwi au mashaytwaan.

 

Haumwi mtu au hahamii nyumba mpya au hafikiwi na dhara au mtihani wowote ila hukimbilia kwa wenye kupandisha mashaytwaan wamsikilize shaytwaan huyo anatabiria nini na anadai nini. 

 

Ada hiyo ya kutawassal kwa majini ilianza tokea zama za ujaahiliyyah, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا﴿٦﴾

 “Na kwamba walikuwa wanaume miongoni mwa wana Aadam wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia madhambi, uvukaji mipaka ya kuasi na khofu.” [Al-Jinn: 6]

 

 

Amesema Shaykh Swaalih bin ‘Abdil-‘Aziyz Aal Ash-Shaykh (Hafidhwahu Allaah): “Maana ya ‘rahaqa’ ni khofu na mpigo wa moyo. Wakawajaza khofu moyoni na mwilini na katika roho zao, na hivyo majini wakajitukuza na wakazidisha shari…. na washirikina walikuwa wanapotua katika bonde au mahali penye kutisha, waliitikadi kwamba kila mahali kuna jini au mkuu wa majini anahudumia sehemu hiyo na anatawala, ikawa wanapofikia bonde au mahali husema: ‘tunajikinga na bwana wa bonde hili kutokana na wajinga wa kaumu yao’ wakimaanisha majini. Hivyo wakajikinga kwa majini ili wawaepushe na shari ya muda wa makazi yao.” [Sharh Kitabit-Tawhiyd li ibn ‘Abdil-Wahhaab]

 

Wanaotawassal kwa viumbe hivyo watambue kwamba ni makhaini wenye kuhadaa wana Aadam, na Siku ya Qiyaamah watakanushana ushirikiano wao wa duniani: Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَقَالَ الشَّيْطَانُ لَمَّا قُضِيَ الْأَمْرُ إِنَّ اللَّـهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ الْحَقِّ وَوَعَدتُّكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ ۖ وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا أَن دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي ۖ فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنفُسَكُم ۖ مَّا أَنَا بِمُصْرِخِكُمْ وَمَا أَنتُم بِمُصْرِخِيَّ ۖ إِنِّي كَفَرْتُ بِمَا أَشْرَكْتُمُونِ مِن قَبْلُ ۗ إِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٢٢﴾

Na shaytwaan atasema itakapokidhiwa jambo: “Hakika Allaah Alikuahidini ahadi ya haki (na Ameitimiza); nami nilikuahidini kisha nikakukhalifuni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu isipokuwa nilikuiteni mkaniitikia. Basi msinilaumu, bali laumuni nafsi zenu. Mimi siwezi kukusaidieni kukuokeeni wala nyinyi hamuwezi kunisaidia kuniokoa. Hakika mimi nilikanusha yale mliyonishirikisha zamani. Hakika madhalimu watapa adhabu iumizayo.” [Ibraahiym: 22]

 

 Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ قَدِ اسْتَكْثَرْتُم مِّنَ الْإِنسِ ۖ وَقَالَ أَوْلِيَاؤُهُم مِّنَ الْإِنسِ رَبَّنَا اسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَا أَجَلَنَا الَّذِي أَجَّلْتَ لَنَا ۚ قَالَ النَّارُ مَثْوَاكُمْ خَالِدِينَ فِيهَا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ﴿١٢٨﴾

Na Siku Atakapowakusanya wote (Allaah Atasema):  Enyi hadhara ya majini! Kwa yakini mmetafuta kwa wingi (kuwapotoa) katika wana Aadam. Na watasema marafiki wao wandani katika wana Aadam: “Rabb wetu! Tulinufaishana baadhi yetu na wengineo, na tumefikia muda wetu ambao Umetupangia.” (Allaah) Atasema: Moto ndio makazi yenu, ni wenye kudumu humo, isipokuwa Atakavyo Allaah. Hakika Rabb wako ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote. [Al-An’aam: 128]

 

Maana ya “tulinufaishana” ni kwamba watu wamewatukuza majini na wakawanyenyekea na wakaomba, na majini wakawahudumia waliyoyataka, na wakawapatia wanayotaka. [Fataawa Al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth  Al-‘Ilmiyyah wal-Iftaa]

 

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametahadharisha kuwa mashaytwaan ni waongo:

 

هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ الشَّيَاطِينُ ﴿٢٢١﴾

Je, nikujulisheni wanaowateremkia mashaytwaan?

 

تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ ﴿٢٢٢﴾

Wanateremka juu ya kila mzushi mkubwa mwingi wa kutenda dhambi. 

 

يُلْقُونَ السَّمْعَ وَأَكْثَرُهُمْ كَاذِبُونَ ﴿٢٢٣﴾

Wanaotega sikio na wengi wao ni waongo. [Ash-Shu’araa 26: 221-223]

 

 WabiLLaahi At-Tawfiyq

 

 

 

  

 

 

 

Share