002-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah

 

 

 

Sababu Za Kuteremshwa

(Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Suwrah Al-Baqarah

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

 

Share

026-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 026: إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 26-27: Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾

Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na ulio zaidi yake (kwa udogo). Basi wale walioamini wanajua kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wao; ama wale waliokufuru husema: “Anataka nini Allaah kwa mfano huu?” (Allaah) Huwapoteza kwayo (mfano huu) wengi na Huwaongoza kwayo wengi na wala Hawapotezi kwayo ila mafasiki.

 

الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٢٧﴾

Wale wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata Aliyoyaamrisha Allaah kuungwa, na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye khasara.  [Al-Baqarah: 26-27]

 

 

Sababun-Nuzuwl:  

 

Aayah hii imeteremshwa baada ya Allaah (سبحانه وتعالى) kupiga mifano kuhusu wanafiki katika kauli zifuatazo:

 

مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ ﴿١٧﴾

Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, ulipoyaangaza yaliyopo pembezoni mwake Allaah Akawaondoshea nuru yao na Akawaacha katika viza (hivyo) hawaoni.  [Al-Baqarah: 17]

 

أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾

Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni, ndani yake mna viza na radi na umeme, wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakikhofu mauti, na Allaah ni Mwenye kuwazunguka kwa ujuzi Wake makafiri. [Al-Baqarah 19]

 

Wanafiki wakasema: “Allaah Ametukuka na Jalali zaidi imekuwaje apige mifano kama hii?” Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Aayaat hizi (2:26-27) mpaka kauli Yake: “… hao ndio wenye khasara.”.

 

Na Sa’iyd amesema kuwa Qataadah amesema: “Allaah (سبحانه وتعالى) Alipotaja nzi na buibui katika Kitabu Chake (Qur-aan), wapotofu wakasema: “Kwanini Allaah Ametaja vitu hivi?” Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Aayah hiyo:

 

“Na Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na ulio zaidi yake (kwa udogo)…”   [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

 

Share

044-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 044: أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 44: Je, mnaamrisha watu watende mema na mnajisahu

 

 أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٤٤﴾ 

44. Je, mnaamrisha watu watende mema na mnajisahu nafsi zenu na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu; je hamtii akilini? 

 

Sababun-Nuzuwl: 

Imesimuliwa kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Aayah hii imeteremshwa kuhusu Mayahudi wa Madiynah. Alikuwa mtu miongoni mwao akimwambia mume wa mwanawe, jamaa zake na Waislamu ambao wamenyonya ziwa moja: “Thibitika katika Dini uliyo nayo na anayokuamrisha mtu huu -  yaani Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) - kwa sababu mambo yake ni ya haki.” Wakawa wanaamrisha watu kwa hayo lakini wao wenyewe hawatekelezi. [Asbaab Nuzuwl Al-Qur-aan – An-Naysaaburiy]

 

Ibn Jurayj amesema kuhusu Aayah: Je, mnaamrisha watu (watende) mema na mnajisahu nafsi zenu…” Ni kuhusu Ahlul-Ktaab na wanafiki. Walikuwa wakiamrisha watu kuswali na kufunga swawm. Lakini wao hawakuwa wakitekeleza waliyokuwa wakiamrisha wengine. Allaah Akawakumbusha tabia yao hii. Kwa hiyo yeyote anayeamrisha watu kutenda mema, basi na awe miongoni mwa wa mwanzo kutekeelza”.

 

Na pia Muhammad bin Is-haaq amesimulia kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuhusu:  “na mnajisahu nafsi zenu…” ina maana mnasahau kutekeleze nyinyi wenyewe.

Na kuhusu: “na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu; je hamtii akilini?”.

Nyinyi mnakataza watu wasikanushe Unabiy na  ahadi mliyoitaja iliyomo kwenu katika Tawraat na hali nyinyi wenyewe mmeisahau yaani: Mmesahau ahadi Niliyofungamana nanyi kwamba mtamkubali Rasuli Wangu. Mmevunja ahadi na mmekanusha mliyoyajua katika Kitabu Changu?  [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share

079-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 079: فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 79: Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa... 

 

 

فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ ﴿٧٩﴾

79. Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa mikono yao; kisha wakasema: ”Hiki ni kutoka kwa Allaah” ili wabadilishe kwa thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

 Aayah hii imeteremka ikiwazungumzia Mayahudi na Manaswara kama ilivyohadithiwa na Al-Bukhaary katika: Khalqu Af-’aal Al-‘Ibaad kutoka kwa Swahaba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)]

 

Na Hadiyth hiyo ameikusanya  Al-Bukhaariy katika: Kitaab Al-I’tiswaam bil-Kitaab wa Sunnah kama ifuatavyo:

 

عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، أَنَّ ابْنَ عَبَّاسٍ رضى الله عنهما قَالَ كَيْفَ تَسْأَلُونَ أَهْلَ الْكِتَابِ عَنْ شَىْءٍ، وَكِتَابُكُمُ الَّذِي أُنْزِلَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَحْدَثُ، تَقْرَءُونَهُ مَحْضًا لَمْ يُشَبْ وَقَدْ حَدَّثَكُمْ أَنَّ أَهْلَ الْكِتَابِ بَدَّلُوا كِتَابَ اللَّهِ وَغَيَّرُوهُ وَكَتَبُوا بِأَيْدِيهِمُ الْكِتَابَ وَقَالُوا هُوَ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ‏.‏ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلاً، أَلاَ يَنْهَاكُمْ مَا جَاءَكُمْ مِنَ الْعِلْمِ عَنْ مَسْأَلَتِهِمْ، لاَ وَاللَّهِ مَا رَأَيْنَا مِنْهُمْ رَجُلاً يَسْأَلُكُمْ عَنِ الَّذِي أُنْزِلَ عَلَيْكُمْ‏.‏

 

Imetoka kwa ‘Ubaydullaah kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Kwanini mnawauliza Ahlul-Kitaab kuhusu jambo lolote na hali Kitabu chenu (Qur-aan) ambacho kimeteremka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  ni cha mwisho? Mnakisoma kikiwa kimetakasika hakikubadilisha wala kupotoshwa na Allaah Amekujulisheni kuwa Ahlul-Kitaab wamebadili Kitabu cha Allaah na wakakibadilisha na wakaandika kwa mikono yao Kitabu kisha wakasema ni kutoka kwa Allaah ili wabadilishe kwa thamani ndogo.  Je kwani ilmu iliyokujieni haikukatazeni kuwauliza wao chochote? Hapana, wa-Allaahi hatukumuona mtu yeyote kati yao akikuulizeni yaliyoteremshwa kwenu.”  

 

Na akahadithia pia katika Kitaab Ash-Shahadaat, na Kitaab At-Tawhiyd.

 

Share

089-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 089: وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 89: Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho...

 

 

وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُم مَّا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ ۚ فَلَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾

89. Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao, na japokuwa kabla ya hapo walikuwa wakiomba ushindi dhidi ya wale waliokufuru; basi yalipowajia yale waliyokuwa wakiyatambua waliyakanusha, basi laana ya Allaah iwe juu ya makafiri.

 

 

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kuhusu Mayahudi kama alivyohadithia ‘Aaswim bin ‘Umar bin Qataadah kuhusu watu katika kaumu yake ambao walisema: Katika ambayo yaliyotuitia katika Uislaam kwa Rahmah ya Allaah (تعالى), na Akaiongoza kwetu, ni pale tulipokuwa tukisikia kutoka Mayahudi, wakati sisi tulikuwa washirikina waabudu masanamu, na Ahlul-Kitaab walikuwa ndio wenye ‘ilmu tusiyokuwa nayo sisi. Na ikawa inaendelea shari baina yetu na wao, basi ilikuwa pale tunapopata (matatizo) kutoka kwao kwa baadhi ya waliyoyachukia, walituambia: Hivi karibuni anakaribia kutumwa Nabiy, basi sasa tutawaua mauwaji ya ‘Aad na Iram, na yeye atakuwa pamoja nasi. Ikawa tunasikia sana hilo. Kisha Allaah Alipomtuma Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  tukamuitikia alipotuitia kwa Allaah  (تعالى)na tukatambua waliyokuwa wakituahidi. Tukawakimbilia na tukamwamini, lakini wao wakamkanusha. Na hapo zikateremshwa Aayaat za Al-Baqarah kuwazungumzia wao: Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao, na japokuwa kabla ya hapo walikuwa wakiomba ushindi dhidi ya wale waliokufuru; basi yalipowajia yale waliyokuwa wakiyatambua waliyakanusha, basi Laana ya Allaah iwe juu ya makafiri” (2: 89) [Amepokea Ibn Is-haaq katika Siyrah]

 

Sababun-Nuzuwl: Pia, Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amehadithia kwamba: Mayahudi walikuwa wakimuomba Allaah (kuletwa kwa Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili wapate ushindi juu ya (Qabila la) Aws na Khazraj kabla ya kutumwa kwake Nabiy. Kisha Allaah Alipomtuma kwa Waarabu, wakamkanusha na kukataa kwamba walikuwa wakimzungumza. Basi Mu’aadh bin Jabal na Bishr bin Al-Baraa bin Ma’ruwr kutoka Bani Salamah waliwaambia: Enyi Mayahudi! Mcheni Allaah na ingieni katika Uislamu, kwani mlikuwa mkimuomba Allaah kuja kwa Muhammad wakati sisi tulikuwa bado makafiri na nyinyi mlikuwa mkituambia kwamba atatumwa na mkatuelezea sifa zake kwetu. Salaam bin Mushkim kutoka Bani An-Nadhwiyr akajibu: Hakuleta lolote tunalolitambua, wala si yeye ambaye tulikuwa tukikutajieni. Hapo Allaah Akateremsha Aayah kuhusu kauli yao. Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao… (2:89) [Ameipokea Ibn Ishaaq- Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Share

097-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 097: قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah: 97 - 101: Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika

 

 

قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٩٧﴾

97. Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) kwa idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na mwongozo na bishara kwa Waumini

 

  مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ ﴿٩٨﴾

98. Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rasuli Wake, na Jibriyl, na Miykaala, basi hakika Allaah ni adui kwa makafiri.

 

وَلَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ وَمَا يَكْفُرُ بِهَا إِلَّا الْفَاسِقُونَ ﴿٩٩﴾

99. Na kwa yakini Tumeteremsha kwako Aayaat bayana, na hawazikanushi isipokuwa mafasiki.

 

أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْدًا نَّبَذَهُ فَرِيقٌ مِّنْهُم ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Je, ndio kila wanapochukua ahadi kundi miongoni mwao huivunja?  Bali wengi wao hawaamini.

 

 

وَلَمَّا جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ نَبَذَ فَرِيقٌ مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ كِتَابَ اللَّـهِ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ كَأَنَّهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٠١﴾ 

101. Na alipowajia Rasuli kutoka kwa Allaah mwenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao kundi miongoni mwa wale waliopewa Kitabu walikitupa Kitabu cha Allaah nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui (yaliyomo humo).

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

Aayah zimeteremka hali ya kuwa ni jawabu kwa Mayahudi miongoni mwa wana wa Israaiyl, pale walipodai kuwa Jibriyl ((عليه السلام ni adui yao. [Imaam Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)] kwamba:

 

حضرت عصابة من اليهود نبيّ الله صلى الله عليه وسلم

فقالوا:حدِّثنا عن خلال نسألك عنهن لا يعلمهن إلا نبي.

 قال : سَلُونِي عَمَّا شِئْتُمْ ، وَلَكِنْ اجْعَلُوا لِي ذِمَّةَ اللَّهِ، وَمَا أَخَذَ يَعْقُوبُ عَلَى بَنِيهِ لَئِنْ أنا حَدَّثْتُكُمْ شَيْئًا فَعَرَفْتُمُوهُ لَتُتَابِعُنِّي عَلَى الإسْلامِ

قَالُوا:فَذَلِكَ لَكَ.

 قَالَ : فَسَلُونِي عَمَّا شِئْتُمْ

 قالوا:أَخْبرْنَا عن أربع خلال:أَخْبرْنَا أَيُّ الطعام حَرَّمَ إسرائيل على نفسه ؟ وكيف ماء المرأة وماء الرجل؟ كيف هذا النبي الأمّي في النوم؟ ومن وَليّه من الملائكة؟

فأخذ عليهم العهد لئن أخبرهم ليتابعنه

وقال :  أَنْشُدُكُمْ بِالَّذِي أَنزلَ التَّوْرَاةَ عَلَى مُوسَى:هَلْ تَعْلَمُونَ أَنَّ إِسْرَائِيلَ مَرِضَ مَرَضًا شَدِيدًا وَطَالَ سُقْمُهُ ، فَنَذَرَ لِلَّهِ نَذْرًا لَئِنْ شَفَاهُ اللَّهُ مِنْ سُقْمِهِ لَيُحَرِّمَنَّ أَحَبَّ الشَّرَابِ إِلَيْهِ وَأَحَبَّ الطَّعَامِ إِلَيْهِ ، وَكَانَ أَحَبَّ الطَّعَامِ إِلَيْهِ لُحْمان الإبِلِ ، وَأَحَبَّ الشَّرَابِ إِلَيْهِ أَلْبَانُهَا

 فقالوا:اللهم نعم.

قال: اللَّهُمَّ اشْهَدْ عَلَيْهِمْ 

 وقال  : أَنْشُدُكُمْ بِاللَّهِ الَّذِي لا إِلَهَ إِلا هُوَ، الَّذِي أَنزلَ التَّوْرَاةَ عَلَى مُوسَى:هَلْ تَعْلَمُونَ أَنَّ مَاءَ الرَّجُلِ أَبْيَضُ غَلِيظٌ ، ومَاءَ الْمَرْأَةِ أَصْفَر رَقِيقٌ، فَأَيُّهُمَا عَلا كَانَ لَهُ الولد وَالشَّبَهُ بإذنِ اللَّهِ ، إِنْ عَلا مَاءُ الرَّجُلِ مَاءَ المرأة كَانَ ذَكَرًا بِإِذْنِ اللَّهِ وَإِنْ عَلا مَاءُ الْمَرْأَةِ مَاءَ الرَّجُلِ كَانَ أُنْثَى بِإِذْنِ اللَّهِ

 قالوا:نعم.

 قال: اللَّهُمَّ اشْهَدْ عَلَيْهِمْ

 وقال:  أَنْشُدُكُمْ بِالَّذِي أَنزلَ التَّوْرَاةَ عَلَى مُوسَى:هَلْ تَعْلَمُونَ أَنَّ هَذَا النَّبِيَّ الأمِّيَّ تَنَامُ عَيْنَاهُ وَلا يَنَامُ قَلْبُهُ  

 قالوا:اللهم نعمْ .

قَالَ:  اللَّهُمَّ اشْهَدْ  

 قالوا:وأنت الآن فحدثنا منْ وليُّك من الملائكة؟ فعندها نجامعك أو نفارقك

قال: إِنَّ وَلِيِّيَ جِبْرِيلُ، وَلَمْ يَبْعَث اللَّهُ نَبِيًّا قَطُّ إِلا وَهُوَ وَلِيُّهُ   

قالوا:فعندها نفارقك، ولو كان وليك غيره لتابعنَاك ، فعند ذلك قال الله تعالى: ((قُلْ مَنْ كَانَ عَدُوًّا لِجِبْرِيلَ ...))   

Kundi miongoni mwa Mayahudi lilihudhuria kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakasema: Yaa Abaa Qaasim! Tuelezee kuhusu tunayokuuliza kwani hayajui isipokuwa Nabiy. Akasema: “Niulizeni mnayotaka lakini niwekeeni ahadi kwa Allaah (kama ahadi) aliyofungamana Ya’quwb kwa wanawe, kuwa nikikuhadithieni jambo mkalijua, mtanifuata katika Uislamu.” Wakasema: Umelipata hilo! (tumekubali). Akasema: “Niulizeni mtakacho.” Wakasema: Tuelezee mambo manne tutakayokuuliza; Tueleze ni chakula gani alichojiharamishia Ya’quwb kabla ya kuteremshwa Tawraat? Na tueleze vipi yanakuwa maji (manii) ya mwanamme na mwanamke, na vipi anakuwa (mtoto) wa kiume anayetokana na maji hayo? Na tueleze vipi anakuwa usingizini huyu Nabiy ambaye hajui kusoma? Na nani anakuwa kipenzi chake katika Malaika? Akasema: “Je mnanipa ahadi kwa Allaah kuwa nikikuelezeni mtanifuata?” Ibn ‘Abbaas akasema: Mayahudi wakampa ahadi. Akasema: “Nakuapieni kwa Ambaye Ameteremsha Tawraat kwa Muwsaa (عليه السّلام).  Hivi mnajua kuwa Ya’quwb aliugua maradhi makali, yakakaa muda mrefu maradhi yake? Akaweka nadhiri kwa Allaah kuwa, endapo atapona maradhi yake, atajiharamishia vinywaji avipendavyo sana na vyakula avipendavyo sana? Na kilikuwa chakula akipendacho zaidi nyama ya ngamia na kinywaji akipendacho zaidi ni maziwa yake?” Wakasema: Allaahumma na’am! Akasema: “Yaa Allaah Washuhudie!  Na nakuapieni kwa Allaah Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, na Ambaye Ameteremsha Tawraat kwa Muwsaa ((عليه السلام, hivi mnajua kuwa maji ya mwanamme ni meupe mazito, na maji ya mwanamke ni ya njano mepesi? Basi moja ya maji hayo yakiwa juu ya mengine, anakuwa jinsia yake huyo mtoto na kufanana naye kwa Idhini ya Allaah.  Na endapo yakiwa maji ya mwanaume juu ya maji ya mwanamke, anakuwa (mtoto) wa kiume, na yakiwa maji ya mwanamke juu ya mwanamme, anakuwa wa kike kwa idhini ya (Allaah سبحانه وتعالى)?” Wakasema: Allaahumaa na’am! Akasema: “Yaa Allaah Washuhudie! Na nakuapieni kwa Allaah Ambaye Ameteremsha Tawraat kwa Muwsaa, hivi mnajua kuwa huyu Nabiy asiyejua kusoma (kuwa) yanalala macho yake wala haulali moyo wake?” Wakasema: Allaahumma na’am! Akasema: “Yaa Allaah Shuhudia!” Wakasema: Basi sasa wewe tuelezee ni nani kipenzi chako katika Malaika? Hapo ndio tutakuwa na wewe au tutafarikiana. Akasema: “Hakika kipenzi changu ni Jibriyl na wala Allaah Hakutuma Nabiy yeyote ila anakuwa kipenzi chake.” Wakasema: Hapo ndio tunafarikiana! Lau angekuwa kipenzi chako mwengine katika Malaika tungekufuata na tungekusadikisha. Akasema: “Kipi kinachokuzuieni kumsadikisha?” Wakasema: Hakika yeye ni adui yetu. Ibn ‘Abbaas akasema: Hapo ndipo Alipoteremsha Allaah Ta’aala: Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako...”  mpaka Kauli ya Allaah [Aayah (2:101)] “...Kitabu cha Allaah nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui.” Na hapo wakastahiki ghadhabu juu ya ghadhabu (2:90) Suwrah Al-Baqarah) [Musnad Ahmad (2384). Ni Hadiyth Swahiyh kwa mkusanyiko wa njia zake na imenukuliwa Ijmaa’ juu ya usahihi wake]  

 

Share

109-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 109: ‏وَدَّ كَثِيرٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُمْ مِنْ بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا

 

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah  109: Wengi katika Ahlil-Kitaab wametamani kama wangelikurudisheni...

 

 

وَدَّ كَثِيرٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُم مِّن بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِّنْ عِندِ أَنفُسِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْحَقُّ ۖ فَاعْفُوا وَاصْفَحُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٩﴾

Wengi katika Ahlil-Kitaab wametamani kama wangelikurudisheni baada ya kuamini kwenu mkawa makafiri kwa husuda iliyomo katika nafsi zao; baada ya kuwabainikia kwao haki. Basi sameheni na puuzeni; mpaka Allaah Alete amri Yake. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

عن أُسَامَةَ بْنَ زَيْدٍ رضى الله عنهما ـ أَخْبَرَهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم رَكِبَ عَلَى حِمَارٍ عَلَى قَطِيفَةٍ فَدَكِيَّةٍ، وَأَرْدَفَ أُسَامَةَ بْنَ زَيْدٍ وَرَاءَهُ، يَعُودُ سَعْدَ بْنَ عُبَادَةَ فِي بَنِي الْحَارِثِ بْنِ الْخَزْرَجِ قَبْلَ وَقْعَةِ بَدْرٍ ـ قَالَ ـ حَتَّى مَرَّ بِمَجْلِسٍ فِيهِ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ، ابْنُ سَلُولَ، وَذَلِكَ قَبْلَ أَنْ يُسْلِمَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ فَإِذَا فِي الْمَجْلِسِ أَخْلاَطٌ مِنَ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُشْرِكِينَ عَبَدَةِ الأَوْثَانِ وَالْيَهُودِ وَالْمُسْلِمِينَ، وَفِي الْمَجْلِسِ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ رَوَاحَةَ، فَلَمَّا غَشِيَتِ الْمَجْلِسَ عَجَاجَةُ الدَّابَّةِ خَمَّرَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ أَنْفَهُ بِرِدَائِهِ، ثُمَّ قَالَ لاَ تُغَبِّرُوا عَلَيْنَا‏.‏ فَسَلَّمَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَيْهِمْ ثُمَّ وَقَفَ فَنَزَلَ فَدَعَاهُمْ إِلَى اللَّهِ، وَقَرَأَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنَ، فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ ابْنُ سَلُولَ أَيُّهَا الْمَرْءُ، إِنَّهُ لاَ أَحْسَنَ مِمَّا تَقُولُ، إِنْ كَانَ حَقًّا، فَلاَ تُؤْذِينَا بِهِ فِي مَجْلِسِنَا، ارْجِعْ إِلَى رَحْلِكَ، فَمَنْ جَاءَكَ فَاقْصُصْ عَلَيْهِ‏.‏ فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ رَوَاحَةَ بَلَى يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَاغْشَنَا بِهِ فِي مَجَالِسِنَا، فَإِنَّا نُحِبُّ ذَلِكَ‏.‏ فَاسْتَبَّ الْمُسْلِمُونَ وَالْمُشْرِكُونَ وَالْيَهُودُ حَتَّى كَادُوا يَتَثَاوَرُونَ، فَلَمْ يَزَلِ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يُخَفِّضُهُمْ حَتَّى سَكَنُوا، ثُمَّ رَكِبَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم دَابَّتَهُ فَسَارَ حَتَّى دَخَلَ عَلَى سَعْدِ بْنِ عُبَادَةَ، فَقَالَ لَهُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ يَا سَعْدُ أَلَمْ تَسْمَعْ مَا قَالَ أَبُو حُبَابٍ ‏"‏‏.‏ يُرِيدُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ أُبَىٍّ ‏"‏ قَالَ كَذَا وَكَذَا ‏"‏‏.‏ قَالَ سَعْدُ بْنُ عُبَادَةَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، اعْفُ عَنْهُ وَاصْفَحْ عَنْهُ، فَوَالَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ، لَقَدْ جَاءَ اللَّهُ بِالْحَقِّ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ، لَقَدِ اصْطَلَحَ أَهْلُ هَذِهِ الْبُحَيْرَةِ عَلَى أَنْ يُتَوِّجُوهُ فَيُعَصِّبُونَهُ بِالْعِصَابَةِ، فَلَمَّا أَبَى اللَّهُ ذَلِكَ بِالْحَقِّ الَّذِي أَعْطَاكَ اللَّهُ شَرِقَ بِذَلِكَ، فَذَلِكَ فَعَلَ بِهِ ما رَأَيْتَ‏.‏ فَعَفَا عَنْهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَكَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم وَأَصْحَابُهُ يَعْفُونَ عَنِ الْمُشْرِكِينَ وَأَهْلِ الْكِتَابِ كَمَا أَمَرَهُمُ اللَّهُ، وَيَصْبِرُونَ عَلَى الأَذَى قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ‏{‏وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا أَذًى كَثِيرًا}‏ الآيَةَ، وَقَالَ اللَّهُ ‏{وَدَّ كَثِيرٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُمْ مِنْ بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِنْ عِنْدِ أَنْفُسِهِمْ}‏ إِلَى آخِرِ الآيَةِ، وَكَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَتَأَوَّلُ الْعَفْوَ مَا أَمَرَهُ اللَّهُ بِهِ، حَتَّى أَذِنَ اللَّهُ فِيهِمْ، فَلَمَّا غَزَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بَدْرًا، فَقَتَلَ اللَّهُ بِهِ صَنَادِيدَ كُفَّارِ قُرَيْشٍ قَالَ ابْنُ أُبَىٍّ ابْنُ سَلُولَ، وَمَنْ مَعَهُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ، وَعَبَدَةِ الأَوْثَانِ هَذَا أَمْرٌ قَدْ تَوَجَّهَ‏.‏ فَبَايَعُوا الرَّسُولَ صلى الله عليه وسلم عَلَى الإِسْلاَمِ فَأَسْلَمُوا‏.

 

Imehadithiwa na Usaamah bin Zayd (رضي الله عنهما) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipanda punda aliyefunikwa kitambaa kizito cha fadakiyyah na Usaamah alikuwa amepanda naye nyuma yake. Alikuwa anaenda kumtembelea Sa’ad bin ‘Ubaadah Al-Haarith bin Al-Khazraj kabla ya vita vya Badr.  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawapitia watu katika majlisi ambako alikuweko ‘Abdullaah bin ‘Ubay  bin Saluwl na hapo kabla ya ‘Abdullaah bin Ubay kuingia Uislaam (juu ya kuwa alibakia kuwa mnafiki). Katika kikao hicho walikuweko mchanganyiko wa Waislaam na washirikina, wanaoabudu masanamu na Mayahudi. Na katika majlisi hiyo alikuweko pia ‘Abdullaah bin Rawaahaa. Wingu la vumbi alolivurumisha punda huyo lilipowafunika watu hao, ‘Abdullaah bin ‘Ubay alisema: “Usitufunike na vumbi!” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawasalimia akasimama na kuteremka chini kisha akawalingania katika Uislaam na akawasomea Qur-aan. Hapo ‘Abdullaah bin Ubay bin Saluwl akasema: “Hakika hakuna unachosema isipokuwa ni mazuri. Ikiwa ni haki basi usituudhi kwayo katika majlisi yetu. Rudi katika kipando chako na atakapokujia mtu hapo msimulie (visa vyako).” Hapo ‘Abdullaah bin Rawaaha akasema: “Naam Ee Rasuli waAllaah, tuletee (uyesamayo) katika majlisi yetu, kwani hakika tunayapenda.” Hapo Waislaam, washirikina na Mayahudi wakaanza kutuhumiana mpaka wakakaribia kupigana. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anawanyamazisha mpaka wakabakia kimya, kisha hapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akampanda mnyama wake akaendelea mpaka akafika kwa Sa’d bin ‘Ubaadah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Je hukumsikia alivyosema Abuu Hubaab.” Alikusudia ‘Abdullaah bin ‘Ubay. “Amesema kadhaa wa kadhaa.” Sa’ad bin ‘Ubaadah akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Msamehe na mpuuze kwani naapa kwa Ambaye Amekuteremshia Kitaab, hakika Allaah Ameleta haki ambayo Amekuteremshia kipindi ambacho watu wa mji huu (Madiynah) wameamua kwa shauri moja kumvisha taji na kumfunga kilemba kichwani mwake (kumchagua kuwa kiongozi). Lakini Allaah Alipokataa hayo kwa haki Aliyokupa basi yeye (‘Abdullaah bin ‘Ubay) amesikitika kwa wivu na ndio ikamfanya afanye uliyoyaona.”  Basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamsamehe kwani Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake walikuwa wakisamehe washirikina na Ahlul-Kitaab kama Allaah Alivyowaamrisha na walikuwa wakivumilia maudhi. Allaah  (عزّ وجلّ)  Akasema:   “na bila shaka mtasikia kutoka kwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na kutoka kwa wale walioshirikisha udhia mwingi. Lakini mkisubiri na mkawa na taqwa basi hakika hayo ni mambo ya (thamani yapasayo) kuazimiwa (Aal-‘Imraan: 185) na Akasema Allaah: “Wengi katika Ahlil-Kitaab wametamani kama wangelikurudisheni baada ya kuamini kwenu mkawa makafiri kwa husuda iliyomo katika nafsi zao; (mpaka mwisho wa Aayah Al-Baqarah 2: 109). Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akishikilia kuwasemehe madamu Allaah Amemuamrisha mpaka Allaah Alipompa idhini ya kuwapiga vita.  Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipopigana vita vya Badr na Akawaua wakuu wa ki Quraysh kwa idhini ya Allaah, basi  ‘Abdullaah bin Ubay bin Saluwl na washirikina na waalioabudu masanamu wakasema: “Jambo hili (la Uislaam) limeelekea ushindi.” Hapo wakam baa’iy Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kiapo cha kuingia Uislaam wakawa Waislaam.” [Al-Bukhaariy katika Kitaab At-Tafsiyr]

 

 

Sababun-Nuzuwl: Kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Basi sameheni na puuzeni mpaka Allaah Alete Amri Yake…” (2:109). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipanda punda akamwambia Sa’d: “Je hukusikia alivyosema Abuu Hubaab?” (akikusudia ‘Abdullaah bin Ubayy. “Amesema kadhaa wa kadhaa.” Sa’d bin ‘Ubaadah akasema: “Msamehe na puuza, basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamsamehe. Na alikuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake wakiwasamehe Ahlul-Kitaab na Washirikina, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:Basi sameheni na puuzeni mpaka Allaah Alete Amri Yake…”   [Amehadithia ‘Urwah kutoka kwa Usaamah bin Zayd, amepokea Abuu Ash-Shaykh katika Al-Akhlaaq].

 

An-Naasikh Wal-Mansuwkh: Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amesema kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Basi sameheni na puuzeni mpaka Allaah Alete amri Yake” kuwa imefutwa hukmu yake kwa Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Basi waueni washirikina popote muwakutapo” (9:5) na “Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho” (9:29).

 

 

Share

115-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 115: وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 115: Na Mashariki na Magharibi ni ya Allaah; basi popote mnapogeuka...

 

 

وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿١١٥﴾

115. Na Mashariki na Magharibi ni ya Allaah; basi popote mnapogeuka kuna Wajihi wa Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka pale Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa akiswali akiwa juu ya mnyama wake. Alikuwa anarudi kutoka Makkah kuelekea Madiynah, na hapo ikateremshwa: “Basi popote mnapogeuka kuna Wajihi wa Allaah.” [Amehadithia Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) amepokea At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ahmad na Ibn Jariyj. Na amesema At-Tirmidhiy ni Hadiyth Hasan Swahiyh].

 

 

An-Naasikh Wal-Mansuwkh:

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amesema: “Sehemu ya kwanza ya Aayah imefutwa hukmu yake kuhusu Qiblah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipohamia Madiynah ambako walikuweko wakaazi Mayahudi, aliamrishwa kuelekeza uso wake Baytul-Maqdis (Palestina). Mayahudi wakafurahi na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaelekeza uso wake huko kiasi miezi kumi. Lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akipenda kuelekeza uso wake Qiblah cha Nabiy Ibraahiym (Al-Ka’bah Makkah) na alikuwa akitazama tazama mbingu kuomba, basi Allaah Akateremsha: “Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia…” (2: 144) [Tafsiyr Ibn Kathiyr na kwa riwaayah nyinginezo katika Al-Bukhaariy na wengineo]

 

Share

125-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 125: وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 125: na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia...

 

 

وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿١٢٥﴾ 

125. Na Tulipoifanya Nyumba (Al-Ka’bah) kuwa ni mahali pa kurejewa na watu na pa amani, na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia. Na Tulichukua ahadi kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl kwamba: “Itakaseni Nyumba Yangu kwa wanaotufu na wanaokaa i’tikaaf, na wanaorukuu na kusujudu.”

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii: “Na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia”, iliteremka pale ‘Umar (رضي الله عنه) alipomwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Lau tungelifanya sehemu aliyosimama Ibraahiym kuwa ni sehemu ya kuswalia.” Kisha baada ya hapo ikateremka Aayah hii. [Al-Bukhaariy kwa ufupi kutoka kwa ‘Umar] Na sehemu aliyosimama Ibraahiym ndiyo iitwayo Hijri.

 

 

Hadiyth kamili:

 

 عَنْ أَنَسٍ، قَالَ قَالَ عُمَرُ: وَافَقْتُ رَبِّي فِي ثَلاَثٍ، فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ لَوِ اتَّخَذْنَا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى فَنَزَلَتْ: ((‏وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى))‏ وَآيَةُ الْحِجَابِ،  قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، لَوْ أَمَرْتَ نِسَاءَكَ أَنْ يَحْتَجِبْنَ، فَإِنَّهُ يُكَلِّمُهُنَّ الْبَرُّ وَالْفَاجِرُ‏.‏ فَنَزَلَتْ آيَةُ الْحِجَابِ، وَاجْتَمَعَ نِسَاءُ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي الْغَيْرَةِ عَلَيْهِ فَقُلْتُ لَهُنَّ عَسَى رَبُّهُ إِنْ طَلَّقَكُنَّ أَنْ يُبَدِّلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِنْكُنَّ‏.‏ فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ‏

Kutoka kwa ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rabb Wangu Ameniwafikia mambo matatu: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Lau tungefanya sehemu aliyosimamia Ibraahiym kuwa sehemu ya kuswali. Ikateremka: “na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia.” (2: 125) Na Aayah ya hijaab nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Ungewaamrisha wake zako kujiwekea hijaab (kizuizi) kutokana na wanaume kwa sababu watu wema na waovu wanaongea nao. Basi ikateremka Aayah ya hijaab kwa wanawake. Na wakeze Nabiy walijiunga dhidi ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na wivu wao baina yao. Nikawaambia: Huenda akutalikini kisha Rabb wake Ambadilishie wake walio bora zaidi kuliko nyinyi” ikateremka Aayah (At-Tahriym  5)  [Al-Bukhaariy]

 

Share

142-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 142: سَيَقُولُ السُّفَهَاءُ مِنَ النَّاسِ مَا وَلَّاهُمْ عَن قِبْلَتِهِمُ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah  142:  Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: “Nini kilichowageuza...

 

 

سَيَقُولُ السُّفَهَاءُ مِنَ النَّاسِ مَا وَلَّاهُمْ عَن قِبْلَتِهِمُ الَّتِي كَانُوا عَلَيْهَا ۚ قُل لِّلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٤٢﴾

142. Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: “Nini kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea!” Sema: “Mashariki na Magharibi ni ya Allaah, Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii na zinazofuatia zimeteremka kama alivyohadithia Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anaposwali, huelekeza uso wake Baytul- Maqdis. Lakini kila mara alikuwa anatazama mbinguni akingojea Amri ya Allaah. Kisha Allaah Akateremsha: Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam…” (2:144). Kisha tukatamani kujua kuhusu hukmu ya waliofariki kabla ya kugeuzwa Qiblah. Hapo Allaah Akateremsha: “Na Allaah Hakuwa Mwenye Kupoteza iymaan yenu (Swalaah), hakika Allaah kwa watu, bila shaka ni Mwenye huruma mno, Mwenye Kurehemu.” (2:143) Kisha Mayahudi wakasema: Ni jambo lipi limewageuza na kuwatoa kwenye Qiblah chao? Hapo Allaah Akateremsha: Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: “Nini kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea…”  mpaka mwisho wa Aayah (2:142). [Hadiyth ameipokea Imaam Ibn Is-haaq katika Siyrah]

 

 

Na katika riwaaya nyengine:

 

عَنِ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم صَلَّى نَحْوَ بَيْتِ الْمَقْدِسِ سِتَّةَ عَشَرَ أَوْ سَبْعَةَ عَشَرَ شَهْرًا، وَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُحِبُّ أَنْ يُوَجَّهَ إِلَى الْكَعْبَةِ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ :((‏قَدْ نَرَى تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ)) ‏ فَتَوَجَّهَ نَحْوَ الْكَعْبَةِ، وَقَالَ السُّفَهَاءُ مِنَ النَّاسِ ـ وَهُمُ الْيَهُودُ ـ ((مَا وَلاَّهُمْ عَنْ قِبْلَتِهِمُ الَّتِي كَانُوا عَلَيْهَا ‏قُلْ لِلَّهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ))‏ فَصَلَّى مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم رَجُلٌ ثُمَّ خَرَجَ بَعْدَ مَا صَلَّى، فَمَرَّ عَلَى قَوْمٍ مِنَ الأَنْصَارِ فِي صَلاَةِ الْعَصْرِ نَحْوَ بَيْتِ الْمَقْدِسِ فَقَالَ هُوَ يَشْهَدُ أَنَّهُ صَلَّى مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم، وَأَنَّهُ تَوَجَّهَ نَحْوَ الْكَعْبَةِ‏.‏ فَتَحَرَّفَ الْقَوْمُ حَتَّى تَوَجَّهُوا نَحْوَ الْكَعْبَةِ‏.

Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنهما) amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali kuelekeza Baytul-Maqdis miezi kumi na sita au kumi na saba lakini alikuwa akipenda kuelekea Al-Ka’bah (Makkah). Basi Allaah Akateremsha: “Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni.” (2:144). Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaelekea Al-Ka’bah na masafihi miongoni mwa watu nao ni Mayahudi wakasema: “Nini kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea!” Allaah Akasema: “Sema: “Mashariki na Magharibi ni ya Allaah, Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka”.  Mtu mmoja akaswali na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha akatoka baada ya kuswali, akapita kwa  watu miongoni mwa Answaariy waliokuwa wakiswali Swalaah ya Alasiri wakielekea Baytul-Maqdis. Akasema kuwa anashuhudia kwamba ameswali na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa ameelekea Al-Ka’bah, basi watu wote wakageuka kuelekea Al-Ka’bah.  [Al-Bukhaariy Kitaab Asw-Swalaah- Baab At-Tawajjuh Nahwa Al-Qiblah Haythu Kaan]

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share

143-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 143: وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 143: Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe...

 

 

 وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ ۚ وَإِن كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٣﴾

143. Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. Na Hatukukifanya Qiblah ambacho ulikuwa ukikielekea (Baytul-Maqdis) isipokuwa Tupate kumpambanulisha yule anayemfuata Rasuli miongoni mwa mwenye kugeuka akarudi nyuma. Na hakika ilikuwa ni jambo gumu isipokuwa kwa wale ambao Allaah Amewaongoza. Na Allaah Hakuwa Mwenye kupoteza iymaan (Swalaah) yenu, hakika Allaah kwa watu, bila shaka ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

عَنِ الْبَرَاءِ بن عازب، رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم صَلَّى إِلَى بَيْتِ الْمَقْدِسِ سِتَّةَ عَشَرَ شَهْرًا أَوْ سَبْعَةَ عَشَرَ شَهْرًا، وَكَانَ يُعْجِبُهُ أَنْ تَكُونَ قِبْلَتُهُ قِبَلَ الْبَيْتِ، وَإِنَّهُ صَلَّى أَوْ صَلاَّهَا صَلاَةَ الْعَصْرِ، وَصَلَّى مَعَهُ قَوْمٌ، فَخَرَجَ رَجُلٌ مِمَّنْ كَانَ صَلَّى مَعَهُ، فَمَرَّ عَلَى أَهْلِ الْمَسْجِدِ وَهُمْ رَاكِعُونَ قَالَ: أَشْهَدُ بِاللَّهِ لَقَدْ صَلَّيْتُ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قِبَلَ مَكَّةَ، فَدَارُوا كَمَا هُمْ قِبَلَ الْبَيْتِ، وَكَانَ الَّذِي مَاتَ عَلَى الْقِبْلَةِ قَبْلَ أَنْ تُحَوَّلَ قِبَلَ الْبَيْتِ رِجَالٌ قُتِلُوا لَمْ نَدْرِ مَا نَقُولُ فِيهِمْ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ إِنَّ اللَّهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَحِيمٌ ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali Swalaah zake akielekeza uso wake Baytul-Maqdis (Palestina) kwa muda wa miezi kumi na sita au miezi kumi na saba, lakini alipendezewa kuwa Qiblah chake kiwe ni Al-Ka’bah (Makkah).  [Ikateremshwa Aayah: Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam…” (2:144)]. Akaswali pamoja na watu (akielekea Al-Ka’bah). Kisha mmoja wa aliyekuwa akiswali naye alitoka nje akapitia watu Msikitini wakiwa wako katika rukuu (wakielekea Baytul-Maqdis). Akasema kuwaambia: “Nashuhudia kwa Allaah, nimetoka (sasa hivi) kuswali pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa ameelekea Makkah (Al-Ka’bah).” Waliposikia hivyo, hapo hapo waligeuka kuelekea Al-Ka’bah wakati wakiwa katika hali hiyo hiyo ya  kurukuu. Baadhi ya Waislamu waliokuwa wakiswali kuelekea Qiblah (cha Baytul-Maqdis) kabla ya kubadilishwa kuelekea Nyumba (Al-Ka’bah Makkah) walifariki au walikufa kishahidi, nasi hatukujua tuseme nini kuhusu wao (na kuelekeza Swalaah zao Baytul-Maqdis). Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: Na Allaah Hakuwa Mwenye Kupoteza iymaan yenu (Swalaah), hakika Allaah kwa watu, bila shaka ni Mwenye huruma mno, Mwenye Kurehemu.” (2:143) [Al-Bukhaariy]

 

 

Share

144-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 144: قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 144: Kwa yakini Tumeona unavyogeuza geuza uso wako mbinguni....

 

 

قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ ۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا ۚ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٤﴾

144. Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. Na popote mtakapokuwepo (mkataka kuswali), basi elekezeni nyuso zenu upande wake. Na hakika wale waliopewa Kitabu bila shaka wanajua kwamba hivyo ni haki kutoka kwa Rabb wao. Na Allaah si Mwenye kughafilika kwa wayatendayo.

 

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali kwa kuelekeza uso wake Baytul-Maqdis (Palestina). lakini alikuwa akitazamatazama mbinguni akitegemea Amri ya Allaah (Ambadilishie Qiblah), ndipo ikateremka hii Aayah: Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia…” (2:144) [Al-Bukhaariy na wengineo kwa riwayaah nyenginezo, Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

 

Share

158-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 158: إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 158: Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika alama za Allaah...

 

 

 إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٥٨﴾

158. Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika alama za Allaah. Basi yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah basi hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya khayr basi hakika Allaah ni Mwenye kupokea shukurani, Mjuzi wa yote.

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Aayah hii imeteremka kuwazungumzia baadhi ya Swahaba (رضي الله عنهم) ambao walihisi uzito Kutufu baina ya Swafaa na Marwah, kwa sababu (Kutufu huko) kulikuwa ni katika ‘ibaadah za enzi ya jaahiliyyah. Washirikina walikuwa wameweka sanamu lao linaloitwa Manaat, wakiliabudu, wakilifanyia Hijjah ya kijahiliyyah na wakilizunguka. Ulipokuja Uislamu walimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hilo. Ndipo hapo Allaah Akateremsha Aayah hii (2:158) [Al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها)].  Rejea Utangulizi wa Tarjama, tanbihi katika Kufasiri Qur-aan kwa kauli za Swahaba  (رضي الله عنهم).

 

Pia, sababu nyingine ni pale iliposhuka Aayah inayoamrisha Kutufu Al-Ka’bah. Ilikuwa haikutajwa katika Qur-aan Kutufu Swafaa na Marwah. Swahaba wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Tulikuwa tunatufu Swafaa na Marwah, na Allaah Ameteremsha kuhusu Kutufu Nyumba (Al- Ka’bah). Basi je itakuwa dhambi kwetu Kutufu Swafaa na Marwah? Hapo Allaah Akateremsha Aayah hii: Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika Alama za Allaah…” (2:158) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Pia ‘Aaswim bin Sulaymaan (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba: Nilimuuliza Anas bin Maalik   (رضي الله عنه)  kuhusu Swafaa na Marwah, akasema: Tulikuwa tunaona kuwa hilo ni jambo la ujaahiliyyah. Kisha ulipokuja Uislamu tukazuia  Kutufu Vilima Viwili hivyo) ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika Alama za Allaah…” (2:158) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 

Share

187-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 187: أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 187: Mmehalalishiwa Usiku Wa Kufunga Swiyaam Kujamiiana na wake zenu...

 

 

 أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٨٧﴾

187. Mmehalalishiwa usiku wa kufunga Swiyaam kujamiiana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Allaah Anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkijifanyia khiyana nafsi zenu, hivyo Akapokea tawbah yenu na Akakusameheni. Basi sasa waingilieni na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). Kisha timizeni Asw-Swiyaam mpaka usiku. Na wala msiwaingilie hali ya kuwa nyinyi wenye kukaa i’tikaaf Misikitini. Hiyo ni mipaka ya Allaah basi msiikaribie. Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (na hukmu) Zake kwa watu wapate kuwa na taqwa.

 

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه)   kwamba: Swahaba wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) walipokuwa wakifunga Swawm kisha ikatokea kuwa walale bila ya kufuturu (Magharibi), walikuwa wakiendelea kufunga Swawm (usiku wote na mchana) mpaka kufike jioni tena (ya siku ya pili). Siku moja Swahaba Qays Ibn Swirmah alikuwa amefunga Swawm. Ulipofika wakati wa kufuturu, alimwendea mkewe akamuuliza: Je una chakula? Akajibu: Hapana, lakini nitajaribu kukupatia. Na (Qays) alikuwa akifanya kazi ngumu akaghilibiwa na usingizi. Mkewe alipokuja (na chakula) alimkuta ameshalala. Akasema: Ole wako, umelala! Ilipofika mchana wa siku ya pili, alizimia. Yakatajwa hayo kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na hapo Aayaah hii ikateremshwa: Mmehalalishiwa usiku wa kufunga Swiyaam kujamiiana na wake zenu…” wakafurahi mno! Na ikateremka: “Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). Kisha timizeni Swiyaam mpaka usiku.” [Al-Bukhaariy kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه)]  Na pia hukmu ya kufunga Swawm ilipotolewa, Waislamu walijizuia kujamiana na wake zao mwezi mzima, lakini baadhi ya watu walikuwa wakifanya khiyana (kuvunja Shariy’ah). Na kwa ajili hiyo, Allaah Akateremsha: Allaah Anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkijifanyia khiyana nafsi zenu, hivyo Akapokea tawbah yenu na Akakusameheni. Basi sasa waingilieni na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu…”

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Kuhusu Kauli ya Allaah: Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe…. ni kwa sababu baadhi ya Swahaba walikuwa wanaendelea tu kula huku wakiwa wamefunga nyuzi (kamba) mbili mguuni; mmoja mweusi na mmoja mweupe mpaka ibainike kuzitofautisha kwake nyuzi hizo. Allaah Akateremsha: (Ufafanuzi wa): mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku)”. [Al-Bukhaariy na Muslim; Hadiyth ya Sahl bin Sa’d  (رضي الله عنه)].

 

Faida: Swahaba walitatanishwa na kushindwa kuelewa maana ya neno uzi mweupe kutokana na uzi mweusi”.  ‘Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Ilipoteremshwa Aayah: mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku)”, nilichukua nyuzi moja nyeupe na moja nyeusi nikaziweka chini ya mto wangu, lakini haikunibainikia. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) asubuhi nikamwelezea. Akasema: “Hakika hiyo (imekusudiwa) ni kiza cha usiku na weupe wa Alfajiri.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share

189-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 189: يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah 189: Wanakuuliza kuhusu miandamo ya mwezi. Sema...

 

 

 يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَن تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٨٩﴾

189. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu miandamo ya mwezi. Sema: “Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa watu na Hajj.” Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake, lakini wema ni kuwa na taqwa. Na ingieni majumbani kupitia milango yake. Na mcheni Allaah mpate kufaulu

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Aayah hii imeteremka pale walipokuwa Answaar wa Madiynah wakienda Hajj na wakirejea wanapitia kwa nyuma ya majumba yao na hawakuwa wakiingia majumbani mwao kwa kupitia milango ya mbele ya majumba yao. Siku moja alikuja mtu mmoja akiwa ametoka Hajj akaingia kupitia mlango wa mbele wa nyumba yake akaaibishwa kwa ajili ya kitendo chake hicho. Hapo basi ikateremka Aayah hii. Hadiyth kama ilivyothibiti:

عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، قَالَ سَمِعْتُ الْبَرَاءَ ـ ر

ضى الله عنه ـ يَقُولُ نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ فِينَا، كَانَتِ الأَنْصَارُ إِذَا حَجُّوا فَجَاءُوا لَمْ يَدْخُلُوا مِنْ قِبَلِ أَبْوَابِ بُيُوتِهِمْ، وَلَكِنْ مِنْ ظُهُورِهَا، فَجَاءَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ، فَدَخَلَ مِنْ قِبَلِ بَابِهِ، فَكَأَنَّهُ عُيِّرَ بِذَلِكَ، فَنَزَلَتْ: ((‏وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَنْ تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ ظُهُورِهَا وَلَكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَى وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا‏))

Abuu Is-haaq amehadithia kwamba nilimsikia Al-Baraa akisema:  Aayah hii imeteremshwa kuhusu sisi, kwani Answaar walikuwa wanaporudi Hajj hawakuwa wakiingia majumbani mwao kupitia milango ya mbele bali wakiingia kwa milango ya nyuma. Akaja mtu katika Answaar akaingia kwa mbele, akatahayarishwa, ikateremka: Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake, lakini wema ni kuwa na taqwa. Na ingieni majumbani kupitia milango yake…”  [Al-Bukhaariy Kitaab Al-‘Umrah na Muslim Kitaab At-Tafsiyr]

 

 

Share

195-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 195: وَأَنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 195: Na toeni katika njia ya Allaah wala msijitupe katika maangamizi...

 

 

   وَأَنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٩٥﴾

195.

Na toeni katika njia ya Allaah wala msijitupe katika maangamizi kwa (kuzia) mikono yenu isitoe. Na fanyeni ihsaan Hakika Allaah Anapenda wafanyao ihsaan

 

 

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kuwazungumzia baadhi ya Swahaba ambao walikusudia kurudi ili kutengeneza mashamba yao na mali zao na waache Jihaad. [At-Tirmidhiy kutoka kwa Abuu Ayyuwb (رضي الله عنه)]

 

Pia, imeteremka kwa wale ambao walikuwa wakijitolea swadaqah (ambapo walikuwa) wanatoa vile ambavyo Allaah (سبحانه وتعالى) Ametaka. Lakini pindi walipopatwa na ukame, walijizuia kutoa. [Atw-Twabaraaniy kutoka kwa Abuu Jubayrah (رضي الله عنه)]  

 

Vile vile, mtu kati yao alipokuwa akifanya madhambi husema: “Allaah Hatonisamehe mimi.”  [Atw-Twabaraaniy kutoka kwa Nu’maan (رضي الله عنه)]

 

 

Hadiyth yake ni kama ifuatavyo:

 

عَنْ أَسْلَمَ أَبِي عِمْرَانَ التُّجِيبِيِّ، قَالَ كُنَّا بِمَدِينَةِ الرُّومِ فَأَخْرَجُوا إِلَيْنَا صَفًّا عَظِيمًا مِنَ الرُّومِ، فَخَرَجَ إِلَيْهِمْ مِنَ الْمُسْلِمِينَ مِثْلُهُمْ أَوْ أَكْثَرُ، وَعَلَى أَهْلِ مِصْرَ عُقْبَةُ بْنُ عَامِرٍ وَعَلَى الْجَمَاعَةِ فَضَالَةُ بْنُ عُبَيْدٍ، فَحَمَلَ رَجُلٌ مِنَ الْمُسْلِمِينَ عَلَى صَفِّ الرُّومِ حَتَّى دَخَلَ فِيهِمْ، فَصَاحَ النَّاسُ وَقَالُوا: سُبْحَانَ اللَّهِ يُلْقِي بِيَدَيْهِ إِلَى التَّهْلُكَةِ، فَقَامَ أَبُو أَيُّوبَ الأَنْصَارِيُّ فَقَالَ: يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّكُمْ تَتَأَوَّلُونَ هَذِهِ الآيَةَ هَذَا التَّأْوِيلَ وَإِنَّمَا نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ فِينَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ، لَمَّا أَعَزَّ اللَّهُ الإِسْلاَمَ وَكَثُرَ نَاصِرُوهُ فَقَالَ بَعْضُنَا لِبَعْضٍ سِرًّا دُونَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: إِنَّ أَمْوَالَنَا قَدْ ضَاعَتْ وَإِنَّ اللَّهَ قَدْ أَعَزَّ الإِسْلاَمَ وَكَثُرَ نَاصِرُوهُ فَلَوْ أَقَمْنَا فِي أَمْوَالِنَا فَأَصْلَحْنَا مَا ضَاعَ مِنْهَا.‏ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَلَى نَبِيِّهِ صلى الله عليه وسلم يَرُدُّ عَلَيْنَا مَا قُلْنَا‏:‏ ‏ ((وَأَنْفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلاَ تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ))‏ فَكَانَتِ التَّهْلُكَةُ الإِقَامَةَ عَلَى الأَمْوَالِ وَإِصْلاَحَهَا، وَتَرَكْنَا الْغَزْوَ فَمَا زَالَ أَبُو أَيُّوبَ شَاخِصًا فِي سَبِيلِ اللَّهِ حَتَّى دُفِنَ بِأَرْضِ الرُّومِ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ .

Imepokelewa kutoka kwa Aslam bin ‘Imraan At-Tujiybiyy (رضي الله عنه) kwamba: Tulikuwa mji wa Rumi, wakatujia safu kubwa ya Warumi. Basi Waislamu waliokaribia idadi yao au zaidi yake waliwaendea. ‘Uqbah bin ‘Aamir alikuwa ni Amiri wa Miswr,  na Amiri wetu alikuwa ni Fadhwaalah bin ‘Ubayd.  Mmoja miongoni mwa Waislamu alifikia safu ya Warumi mpaka akaingia kwao, watu wakapiga kelele: “Subhaana-Allaah! Amejitupa katika maangamizi!  Abuu Ayyuwb Al-Answaariy akasema: Enyi watu! Hakika nyinyi mnafasiri Aayah hii na hali Aayah hii imeteremshwa kuhusu sisi hadhara ya Answaariy pale Allaah Alipoupa nguvu Uislamu wakazidi wasaidizi wake.  Baadhi yetu wakaambizana siri bila ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba: Mali zenu zimepotea na kwamba Allaah Ameutia nguvu Uislamu na wamezidi wasaidizi wetu. Hivyo tungelitunza mali zetu, ingelikuwa ni mbadala wa mali tuliyopoteza. Hapo Allaah Akamteremshia Nabiy Wake  (صلى الله عليه وآله وسلم) kutukanya yale tuliyoyasema:  

Na toeni katika njia ya Allaah wala msijitupe katika maangamizi kwa (kuzia) mikono yenu isitoe…” Basi maangamizi yakawa ni vile kutunza mali  na kuzihifadhi.  Tukaondoka vitani basi Abuu Ayyuwb hakuacha lengo la kupigana kwa ajili ya Allaah mpaka akazikwa katika ardhi ya Warumi. [Abuu 'Iysaa At-Tirmidhiy, amesema hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh Ghariyb, Taz. Swahiyh At-Targhiyb (1388)]  

 

 

Share

196-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 196: وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 196: Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah.  Na kama mkizuilika…

 

 

 وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ ۚ فَإِنْ أُحْصِرْتُمْ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۖ وَلَا تَحْلِقُوا رُءُوسَكُمْ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِّن رَّأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِّن صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ ۚ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَمَن تَمَتَّعَ بِالْعُمْرَةِ إِلَى الْحَجِّ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۚ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ فِي الْحَجِّ وَسَبْعَةٍ إِذَا رَجَعْتُمْ ۗ تِلْكَ عَشَرَةٌ كَامِلَةٌ ۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمْ يَكُنْ أَهْلُهُ حَاضِرِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١٩٦﴾

196. Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah.  Na kama mkizuilika basi chinjeni wanyama walio wepesi kupatikana. Na wala msinyoe vichwa vyenu mpaka mnyama afikie machinjoni pake. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake (ikambidi anyoe); basi atoe fidia kwa kufunga Swiyaam au kutoa swadaqah au kuchinja mnyama. Na mtakapopata amani, basi mwenye kujistarehesha kwa kutekeleza ‘Umrah kwanza kisha Hajj, achinje mnyama aliye mwepesi. Na asiyepata afunge Swiyaam siku tatu katika Hajj na saba mtakaporejea. Hizo ni kumi kamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawaishi karibu na Al-Masjidil-Haraam. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Allaah ni Mkali wa kuakibu.

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

عن صفوان بن يعلى بن أمية عن أبيه قال: جاء إلى رسول صلى الله عليه وعلى آله وسلم وقال: كيف تأمرني في عمرتي، فأنزل الله عز وجل : ((وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّهِ)) فقال رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم: ((من السائل عن العمرة)) فقال: أنا. فقال:((ألق ثيابك واغتسل واستنشق ما استطعت وما كنت صانعا في حجتك فاصنع في عمرتك))

 

Imepokelewa kutoka kwa Swafwaan bin Ya’laa bin Umayyah kutoka kwa baba yake kwamba: Alikuja mtu kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Unaniamrishaje kuhusu ‘Umrah yangu? Hapo Allaah (عز وجلَّ)  Akateremsha: “Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah.” Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Nani aliyeuliza kuhusu ‘Umrah?”  Akajibu: Mimi. Akasema: “Toa nguo zako, uoge, usukutue uwezavyo na fanya katika ‘Umrah yako kama ulivyokuwa ukifanya katika Hajj yako.” [Atw-Twabaraaniy]

 

Na kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake….” mpaka mwisho wake, ni kuwa iliteremka kuhusu Swahaba Ka’ab Ibn ‘Ujrah kama alivyohadithia kwamba: 

 

رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَقَفَ عَلَيْهِ وَرَأْسُهُ يَتَهَافَتُ قَمْلاً فَقَالَ: ((أَيُؤْذِيكَ هَوَامُّكَ))‏.‏ قُلْتُ نَعَمْ.‏ قَالَ: ((‏فَاحْلِقْ رَأْسَكَ)) قَالَ فَفِيَّ نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: ((فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِنْ رَأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِنْ صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ)) ‏فَقَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((صُمْ ثَلاَثَةَ أَيَّامٍ أَوْ تَصَدَّقْ بِفَرَقٍ بَيْنَ سِتَّةِ مَسَاكِينَ أَوِ انْسُكْ مَا تَيَسَّرَ))‏

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama karibu yangu, na chawa walikuwa wakianguka kutoka kichwani mwangu. Akasema: “Je chawa wanakutatiza?” Nikasema ndio. Akaniamrisha kichwa kinyolewe. Ka’ab akasema: Aayah hii imeteremshwa kunihusu mimi. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake (ikambidi anyoe); basi atoe fidia kwa kufunga Swiyaam au kutoa swadaqah au kuchinja mnyama…” Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniamrisha nifunge Swawm siku tatu au nilishe masikini sita kwa faraq (Nusu ya pishi za tende au  chakula kinginecho kwa kila maskini mmoja; jumla ni pishi tatu kwa maskini sita) au nichinje mnyama au kilichopatikana kwa wepesi. [Al-Bukhaariy, Muslim kutoka kwa Ka’b (رضي الله عنه)]

 

 

Share

197-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 197: وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 197:  Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji ...

 

 

الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٧﴾

197. Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji (akahirimia), basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote mlifanyalo katika ya khayr Allaah Analijua. Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili!

 

 

Sababun-Nuzuwl:  

 

Sababu ya kuteremka Kauli ya Allaah: “Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa.” Watu wa Yemen walikuwa wanapokwenda Hajj hawachukui matumizi ya njiani na khatimae wanasema: “Sisi ni wenye kutawakali kwa Allaah.” Na wakiingia Makkah, wanaanza kuombaomba watu. Hapo ikateremka Aayah. [Al-Bukhaariy kutoka kwa ‘Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)]  

 

Hadiyth kama ilivyothibiti:

 

عنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضى الله عنهما قَالَ:  كَانَ أَهْلُ الْيَمَنِ يَحُجُّونَ وَلاَ يَتَزَوَّدُونَ وَيَقُولُونَ نَحْنُ الْمُتَوَكِّلُونَ، فَإِذَا قَدِمُوا مَكَّةَ سَأَلُوا النَّاسَ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: ((‏وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَى‏))

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba: Watu wa Yemen walikuwa wanapokwenda Hajj hawachukui matumizi ya njiani na khatimae wanasema: “Sisi ni wenye kutawakali kwa Allaah.” Na wakiingia Makkah, wanaanza kuombaomba watu.  Allaah تعالى Akateremsha: Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa.” [Al-Bukhaariy katika Kitaab Al-Hajj, na Sunan Abiy Daawuwd Kitaab Al-Manaasik]

 

Miezi ya Hajj:

 

Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) amesema: “Miezi ya Hajj ni Shawwaal, Dhul-Qa’dah na siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah. [Fat-hul-Baariy (3/491)]

 

 

 

 

 

 

 

Share

198-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 198: ‏لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَنْ تَبْتَغُوا فَضْلاً مِنْ رَبِّكُمْ‏

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 198: Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wen

 

 

 

لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ ۚ فَإِذَا أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ عِندَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ ۖ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّينَ ﴿١٩٨﴾ 

198. Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wenu. Basi mtakapomiminika kutoka ‘Arafaat mdhukuruni Allaah kwenye Mash’aril- Haraam (Muzdalifah) na mdhukuruni Yeye kama Alivyokuongozeni kwani hakika mlikuwa kabla ya hapo ni miongoni mwa waliopotea.

 

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii: Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wenu”, imeteremka kuhusu Maswahaba kuwa waliona uzito kufanya biashara kwenye masoko yaliyokuwa yakitumika zama za Jaahiliyyah. Ndipo ikateremka Aayah hii. [Al-Bukhaariy kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)] Hadiyth kamili:

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضى الله عنهما قَالَ : كَانَتْ عُكَاظٌ وَمَجَنَّةُ وَذُو الْمَجَازِ أَسْوَاقًا فِي الْجَاهِلِيَّةِ فَتَأَثَّمُوا أَنْ يَتَّجِرُوا فِي الْمَوَاسِمِ فَنَزَلَتْ: ((‏لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَنْ تَبْتَغُوا فَضْلاً مِنْ رَبِّكُمْ‏))  فِي مَوَاسِمِ الْحَجِّ‏.‏

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ambaye amesema: ‘Ukaadhw, na Majannah na Dhul-Majaaz yalikuwa masoko wakati wa Jaahiliyyah (kabla ya Uislamu). Basi (Waislamu) waliodhania ni dhambi kufanya biashara katika msimu (wa Hajj), ndipo ikateremka: Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wenu…”katika misimu ya Hajj [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr, Kitaab Al-Buyuw’, pia Sunan Abiy Daawuwd Kitaabu Al-Manaasik]

 

 

Share

199-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 199: ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 199: Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu;

 

 

  ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٩﴾

199. Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu; na ombeni maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii: “Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu;” imeteremka kuhusu Maquraysh kwa vile wao walikuwa wakimiminika kutokea Muzdalifah na hali ya kuwa watu wengineo wanamiminika kutokea ‘Arafah. Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaamrisha nao Maquraysh wamiminike kutokea ‘Arafah kama wafanyavyo wengineo. [Al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها)]

 

Hadiyth zimethibiti katika riwaayah kadhaa. Ama ifuAtayo ni kama ilivyokusanywa na Imaam Al-Bukhaariy katika Kitaab Al-Hajj iliyopokelewa kutoka kwa ‘Urwah (رضي الله عنه):

 

كَانَ النَّاسُ يَطُوفُونَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ عُرَاةً إِلاَّ الْحُمْسَ، وَالْحُمْسُ قُرَيْشٌ وَمَا وَلَدَتْ، وَكَانَتِ الْحُمْسُ يَحْتَسِبُونَ عَلَى النَّاسِ يُعْطِي الرَّجُلُ الرَّجُلَ الثِّيَابَ يَطُوفُ فِيهَا، وَتُعْطِي الْمَرْأَةُ الْمَرْأَةَ الثِّيَابَ تَطُوفُ فِيهَا، فَمَنْ لَمْ يُعْطِهِ الْحُمْسُ طَافَ بِالْبَيْتِ عُرْيَانًا، وَكَانَ يُفِيضُ جَمَاعَةُ النَّاسِ مِنْ عَرَفَاتٍ، وَيُفِيضُ الْحُمْسُ مِنْ جَمْعٍ‏.‏ قَالَ وَأَخْبَرَنِي أَبِي عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها أَنَّ هَذِهِ الآيَةَ نَزَلَتْ فِي الْحُمْسِ: ((‏ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ‏)) قَالَ كَانُوا يُفِيضُونَ مِنْ جَمْعٍ فَدُفِعُوا إِلَى عَرَفَاتٍ‏.‏

“Wakati wa kipindi cha Ujaahiliyyah, watu walikuwa wakitufu Al-Ka’bah wakiwa uchi isipokuwa Al-Hums. Na Al-Hums walikuwa ni (kabila la) Quraysh pamoja  na kizazi chao. Na Al-Hums walikuwa wakiwapa nguo watu wanaofanya twawaaf ili wazivae na wanawake (wa Al-Hums) walikuwa wakiwapa nguo wanawake waliokuwa wakifanya twawaaf wazivae. Wale ambao Al-Hums hawakuwapa nguo walifanya twawaaf wakiwa uchi. Wengi wa watu walikuwa wakimiminika kutoka ‘Arafah moja kwa moja lakini (Al-Hums) walikuwa wakimiminika kutoka baada ya kukaa Muzdalifah.” ‘Urwah akaendelea kusema: “Baba yangu amehadithia kwamba ‘Aaishah amesema: “Aayah ifuatayo imeteremshwa kuhusu Al-Hums. Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu” (2: 99) ‘Urwah akaendelea kusema: “Wao (Al-Hums) walikuwa wakibakia Muzdalifah na wakiondokea kutoka humo (kwenda Minaa), basi ndio wakageuzwa kuondokea ‘Arafah (kwa amri ya Allaah.”

 

Share

207-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 207: وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 207: Na miongoni mwa watu yupo anayeiuza nafsi yake kutafuta

 

 

   وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠٧﴾

207. Na miongoni mwa watu yupo anayeiuza nafsi yake kutafuta radhi za Allaah. Na Allaah ni Mwenye huruma mno kwa waja

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii: Na miongoni mwa watu yuko anayeiuza nafsi yake kutafuta Radhi za Allaah”, imeteremka kuhusu Suhayb (رضي الله عنه) pale alipotoka Makkah akiwa ni mwenye kuhamia Madiynah. Watu wa Makkah wakamfuata ili wamrejeshe. Alikuwa amewaacha vijakazi wawili Makkah, basi ili aachiwe kuhajiri kutoka Makkah kwenda Madiynah, aliwapatia hao waliomfuata vijakazi wawili hao. Hapo wakamuachia. [Imaam Al-Haakim kutoka kwa Anas (رضي الله عنه)]

 

 

 

 

 

Share

219-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 219: يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 219:  Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema:

 

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾

219. Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.” Na wanakuuliza nini watoe. Sema: “Yaliyokuzidieni.” Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na  shariy’ah) ili mpate kutafakari.

 

Sababun-Nuzuwl

 

Aayah hii imeteremshwa pale 'Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) ambaye alikuwa mmoja wa Swahaba wenye kulewa, siku moja alisema: Ee Rasuli wa Allaah, tupe hukmu kuhusu Al-khamr (pombe). Hapo ikateremka Aayah:

 

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ

Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake. [Al-Baqarah (2:219)]

 

Kisha ikafuatia Aayah (4:43) ya kutokukaribia Swalaah baada ya kulewa.

 

Kisha ikaharamishwa kabisa katika Suwratul-Maaidah (5:90). Rejea huko kupata maelezo bayana.

 

Hadiyth kama ilivyothibiti katika [Sunan Abiy Daawuwd Kitaab Al-Ashribah Baab Tahriym Al-Khamr]

 

عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ، قَالَ لَمَّا نَزَلَ تَحْرِيمُ الْخَمْرِ قَالَ عُمَرُ: اللَّهُمَّ بَيِّنْ لَنَا فِي الْخَمْرِ بَيَانًا شِفَاءً ، فَنَزَلَتِ الآيَةُ الَّتِي فِي الْبَقَرَةِ: ((‏يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ)) الآيَةَ قَالَ: فَدُعِيَ عُمَرُ فَقُرِئَتْ عَلَيْهِ، قَالَ: اللَّهُمَّ بَيِّنْ لَنَا فِي الْخَمْرِ بَيَانًا شِفَاءً، فَنَزَلَتِ الآيَةُ الَّتِي فِي النِّسَاءِ: ((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَقْرَبُوا الصَّلاَةَ وَأَنْتُمْ سُكَارَى))‏ فَكَانَ مُنَادِي رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا أُقِيمَتِ الصَّلاَةُ يُنَادِي: أَلاَ لاَ يَقْرَبَنَّ الصَّلاَةَ سَكْرَانُ، فَدُعِيَ عُمَرُ فَقُرِئَتْ عَلَيْهِ  فَقَالَ: اللَّهُمَّ بَيِّنْ لَنَا فِي الْخَمْرِ بَيَانًا شِفَاءً فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: ((‏فَهَلْ أَنْتُمْ مُنْتَهُونَ))‏ قَالَ عُمَرُ: انْتَهَيْنَا.‏

Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) kwamba ilipoharamishwa pombe alisema ‘Umar: Ee Allaah tubainishie kuhusu pombe bainisho la kuridhisha.” Hapo ikateremshwa Aayah katika Suwratul-Baqarah:

 

 ‏يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ

Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa.    

 

[Al-Baqarah 2: 219] Akaitwa ‘Umar akasomewa. Kisha akasema: “Ee Allaah tubainishie kuhusu pombe bainisho la kuridhisha.” Kisha ikateremshwa Aayah katika Suwratun-Nisaa:

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَقْرَبُوا الصَّلاَةَ وَأَنْتُمْ سُكَارَى

“Enyi waloamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa...” [An-Nisaa 4: 43]

 

Kisha muitaji wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitangaza  pale inapokimiwa Swalaah: “Tahadharini! Aliyelewa asikaribie Swalaah!” ‘Umar akaitwa tena na akasomewa akasema: “Ee Allaah tubainishie kuhusu pombe bainisho la kuridhisha.” Ikateremka Aayah:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾

Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli, ni najisi na chukizo kutokana na kazi ya shaytwaan. Basi jiepusheni navyo mpate kufaulu. [Al-Maaidah (5:90)]

 

إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾

Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na Swalaah; basi je mtakoma? [Al-Maaidah (5:90-91)]

‘Umar akasema: “Tumekoma.” [Imaam Al-Albaaniy ameisahihisha katika Swahiyh Abiy Daawuwd (3670)]

 

 

 

Share

220-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 220: وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 220: Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengeneza ni kheri.

 

 

فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۗ وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ ۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَأَعْنَتَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٠﴾

220. Katika dunia na Aakhirah. Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengeneza ni kheri. Na mkichanganya mambo yenu na yao basi hao ni ndugu zenu. Na Allaah Anamjua fisadi na mtengenezaji. Na lau Angetaka Allaah Angelikutieni katika shida.” Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: Ilipoteremka Aayah: Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya ihsaan”, na pia: “Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma… (4:10), watu wakajiepusha na mali na chakula cha yatima. Ikawa ni ngumu kwao, wakalalamika kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).  Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: “Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengenezea ni khayr…” (2:220) [Swahiyh An-Nasaaiy (3671), Fathul-Baariy (5/463)]

 

 

Hadiyth kama ilivyothibiti:

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ لَمَّا نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ ((‏وَلاَ تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلاَّ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ))‏ وَ‏((‏إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَى ظُلْمًا‏))‏ قَالَ: اجْتَنَبَ النَّاسُ مَالَ الْيَتِيمِ وَطَعَامَهُ فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَى الْمُسْلِمِينَ فَشَكَوْا ذَلِكَ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((‏وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَى قُلْ إِصْلاَحٌ لَهُمْ خَيْرٌ‏)) ‏ إِلَى قَوْلِهِ ‏((‏لأَعْنَتَكُمْ‏)).

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba pale Aayah hizi zilipoteremshwa:  Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya ihsaan…” [Al-Anaam 152] na, Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma…” [An-Nisaa: 10], akasema: Watu walijiepusha na mali ya yatima pamoja na chakula chake, ikawa ni mashaka kwa Waislamu wakashitaki kwa Nabiy   (صلى الله عليه وآله وسلم)  hapo ikataremka: “Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: “Kuwatengeneza ni kheri…” mpaka kauli Yake: “Angelikutieni katika shida.” [Sunan An-Nasaaiy katika Kitaab Al-Wiswaayaa, Baab maa lil-waswiyyi min maal al-yatiym idhaa qaama ‘alayhi].

 

 

Share

222-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 222: وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 222:Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema…  

 

 وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ ﴿٢٢٢﴾ 

222. Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara; basi waepukeni wanawake katika hedhi. Wala msiwakaribie (kujimai nao) mpaka watwaharike. Watakapotwaharika basi waendeeni kupitia pale Alipokuamrisheni Allaah.”  Hakika Allaah Anapenda wenye kutubia na Anapenda wenye kujitwaharisha.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii: Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara; basi waepukeni wanawake katika hedhi,” imeteremka kuwazungumzia Mayahudi ambao walikuwa mwanamke akipatwa na hedhi, hawali nae chakula wala hawajumuiki nae katika majumba. Maswahaba wakamuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu jambo hilo, na hapo ikateremka Aayah hii. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Fanyeni kila kitu isipokuwa jimai.”  [Muslim Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه)]

 

 

Hadiyth kama ilivyothibiti:

 

عَنْ أَنَسٍ، أَنَّ الْيَهُودَ، كَانُوا إِذَا حَاضَتِ الْمَرْأَةُ فِيهِمْ لَمْ يُؤَاكِلُوهَا وَلَمْ يُجَامِعُوهُنَّ فِي الْبُيُوتِ فَسَأَلَ أَصْحَابُ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: ((وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ‏))  إِلَى آخِرِ الآيَةِ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((اصْنَعُوا كُلَّ شَىْءٍ إِلاَّ النِّكَاحَ)) ‏ فَبَلَغَ ذَلِكَ الْيَهُودَ فَقَالُوا: مَا يُرِيدُ هَذَا الرَّجُلُ أَنْ يَدَعَ مِنْ أَمْرِنَا شَيْئًا إِلاَّ خَالَفَنَا فِيهِ. فَجَاءَ أُسَيْدُ بْنُ حُضَيْرٍ وَعَبَّادُ بْنُ بِشْرٍ فَقَالاَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ الْيَهُودَ تَقُولُ كَذَا وَكَذَا فَلاَ نُجَامِعُهُنَّ، فَتَغَيَّرَ وَجْهُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم حَتَّى ظَنَنَّا أَنْ قَدْ وَجَدَ عَلَيْهِمَا، فَخَرَجَا فَاسْتَقْبَلَهُمَا هَدِيَّةٌ مِنْ لَبَنٍ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَأَرْسَلَ فِي آثَارِهِمَا فَسَقَاهُمَا فَعَرَفَا أَنْ لَمْ يَجِدْ عَلَيْهِمَا ‏.‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba Mayahudi walikuwa pale mwanamke anapokuwa katika hedhi hawakuwa wakila naye wala hawajumuiki naye nyumbani mwao. Basi Maswahaba wakamuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Allaah (تعالى) Akateremsha: Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara; basi waepukeni wanawake katika hedhi.” Mpaka mwisho wa Aayah. Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Fanyeni kila kitu (nao) isipokuwa kujamiiana)). Yakawafikia Mayahudi hayo wakasema: “Mtu huyu hataki kuacha lolote ila tu akhitilafiane nasi kwalo.” Akaja Usayd bin Hudhwayr na ‘Abbaadu bin Bishr wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Hakika Mayahudi wamesema kadhaa wa kadhaa.  Hivyo basi tusijamiiane nao.” Hapo uso wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ukabadilika mpaka tukadhania kwamba amewakasirikia. Walipotoka nje walipokea hadiya ya maziwa aliyoletewa Nabiy. Akawaita akawagaia kinywaji hicho, hapo wakatambua kuwa kumbe hakukasirika nao. [Muslim katika Kitaab Al-Haydhw]

 

 

Share

223-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 223: نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 223: Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu…

 

 

نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُم مُّلَاقُوهُ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٢٣﴾

223. Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. Na kadimisheni (mema) kwa ajili ya nafsi zenu. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika nyinyi ni wenye kukutana Naye. Na wabashirie Waumini.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii: Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo.imeteremka kuwazungumiza Mayahudi waliokuwa wakisema kuwa mwanaume akimuingilia mke wake kupitia upande wa nyuma, basi anazaliwa mtoto akiwa ana makengeza. Ndipo ikateremka hii Aayah. [Al-Bukhaariy, Muslim kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه)]

 

 

Pia, Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alisema kuwa kauli hiyo; Wanawake zenu ni konde kwenu iliteremshwa kuwazungumzia baadhi ya watu wa Answaar ambao walikuja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamuuliza (kuhusu kumuingilia mwanamke kutokea upande wa nyuma). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawajibu: Muingilie vyovyote upendavyo madhali ni ukeni.” [Ahmad]  

 

 

Hadiyth kama ilivyothibiti :

 

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ يَهُودَ، كَانَتْ تَقُولُ إِذَا أُتِيَتِ الْمَرْأَةُ مِنْ دُبُرِهَا فِي قُبُلِهَا ثُمَّ حَمَلَتْ كَانَ وَلَدُهَا أَحْوَلَ ‏.‏ قَالَ فَأُنْزِلَتْ: ((نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ‏))

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah kwamba Mayahudi walikuwa wanasema pale mke anapoingiliwa mbele katika sehemu za siri, lakini akiwa amegeuka nyuma, na pindi anaposhika mimba husema kuwa mtoto atazaliwa kengeza. Hapo ikateremshwa Aayah: Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo.“  [Muslim Kitaab An-Nikaah]

 

 

Share

225-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 225: لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah225:

llaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi lakini..

 

 

لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٢٥﴾

225.

Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi lakini Atakuchukulieni kwa yaliyochuma nyoyo zenu. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mvumilivu

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii 

 

لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ

“Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi…” (2:225)  imeteremshwa kutokana na vile mtu kuapa: “Hapana wa-Allaahi, Ndio wa-Allaah.” (Yaani kuapa apa kila mara).   [Amehadithia  ‘Aaishah (رضي الله عنها)  na ameipokea Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth kama ilivyothibiti:

 

عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها أُنْزِلَتْ هَذِهِ الآيَةُ : ((لاَ يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ‏))‏ فِي قَوْلِ الرَّجُلِ: لاَ وَاللَّهِ، وَبَلَى وَاللَّهِ‏.‏

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah  (رضي الله عنها) kwamba Aayah hii

 

لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ

Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi” kuhusu kauli ya mtu (kusema kwake mara kwa mara): Hapana wa-Allaahi, ndio wa-Allaahi.   [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]

 

 

 

Share

232-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 232: وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 232:  Na mtakapowatalaki wanawake wakafikia muda wa...

 

 

 

 وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَن يَنكِحْنَ أَزْوَاجَهُنَّ إِذَا تَرَاضَوْا بَيْنَهُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ ذَٰلِكَ يُوعَظُ بِهِ مَن كَانَ مِنكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗ ذَٰلِكُمْ أَزْكَىٰ لَكُمْ وَأَطْهَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢٣٢﴾

232. Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao; basi msiwazuie kuolewa na waume zao (wa awali) ikiwa wameridhiana baina yao kwa mujibu wa ada. Hayo anawaidhiwa kwayo yeyote miongoni mwenu mwenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo kwenu ni wema zaidi na safi kabisa. Na Allaah Anajua nanyi hamjui.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao; basi msiwazuie kuolewa na waume zao (wa awali)…”, imeteremka kuhusu Ma’aqil bin Yasaar (رضي الله عنه) ambaye  alimuozesha dada yake kwa mwanaume kisha yule mwanaume akamtaliki, akakaa mpaka eda yake ikamalizika. Baada ya kumalizika eda, yule mwanaume akamchumbia tena huyo dada yake kwa Ma’aqil, lakini Ma’aqil alikataa. Ndipo hapo ikateremka Aayah hii. [Al-Bukhaariy kutoka kwa Ma’aqil (رضي الله عنه)]

 

 

Hadiyth kama ilivyothibiti:

 

عَنْ قَتَادَةَ، حَدَّثَنَا الْحَسَنُ، أَنَّ مَعْقِلَ بْنَ يَسَارٍ، كَانَتْ أُخْتُهُ تَحْتَ رَجُلٍ فَطَلَّقَهَا، ثُمَّ خَلَّى عَنْهَا حَتَّى انْقَضَتْ عِدَّتُهَا، ثُمَّ خَطَبَهَا فَحَمِيَ مَعْقِلٌ مِنَ ذَلِكَ أَنَفًا فَقَالَ: خَلَّى عَنْهَا وَهْوَ يَقْدِرُ عَلَيْهَا، ثُمَّ يَخْطُبُهَا فَحَالَ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا، فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((‏وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلاَ تَعْضُلُوهُنَّ))‏ إِلَى آخِرِ الآيَةِ، فَدَعَاهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَرَأَ عَلَيْهِ، فَتَرَكَ الْحَمِيَّةَ وَاسْتَقَادَ لأَمْرِ اللَّهِ‏.‏

Imepokelewa kutoka kwa Qataadah kwamba Al-Hasan ametuhadithia kuwa dada yake Ma’qil bin Yasaar aliolewa na mtu akamtaliki kisha akatengana naye mpaka muda wake wa eda ukamalizika. Kisha akarudi kutaka kumuoa lakini Ma’qil alikataa akasema kwa hamaki na kuringa: “Amemtenga hali angeliweza kukaa naye, sasa ndio anataka kumposa tena?” Basi Ma’qil akakataa kumuozesha tena hapo Allaah Akateremsha:Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao; basi msiwazuie …” mpaka mwisho wa Aayah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuita akamsomea akaacha tena hamaki na maringo akaelemea amri ya Allaah. [Al-Bukhaariy – Kitaab Atw-Talaaq]

 

 

Share

238-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 238: حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 238: Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati...

 

حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ﴿٢٣٨﴾

238. Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.

 

 

Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri)... imeteremka kuhusu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Alikuwa akiswali Swalaah ya Adhuhuri nusu ya mchana wakati jua linaposhtadi, na ilikuwa ni Swalaah ngumu zaidi kwa Swahaba (رضي الله عنهم). Mara nyingine ilikuwa haipatikani nyuma yake isipokuwa safu moja au mbili. Baada ya hali hiyo, ikateremka Aayah hii. [Ahmad kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه)]

 

 

Sababun-Nuzuwl: Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu” ni kwamba, Swahaba walikuwa wakizungumza ndani ya Swalaah; mtu anamsemesha ndugu yake katika haja zake akiwa ndani ya Swalaah. Basi hapo ikateremka Aayah hii. [Al-Bukhaariy, Muslim kutoka kwa Zayd bin Arqam (رضي الله عنه)]

 

 

 

 

 

 

 

 

Share

256-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 256: لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 256: Hapana kulazimisha katika Dini

 

 لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٥٦﴾

256. Hapana kulazimisha katika Dini, kwani imekwishabainika kati ya uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaghuti na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Aayah hii: “Hapana kulazimisha katika Dini…” imeteremka kumzungumiza mwanamke ambaye alikuwa kila anapozaa, mtoto wake hufariki. Basi mwanamke huyo akaweka nadhiri katika nafsi yake kwamba pindi akizaa na mtoto akaishi bila kufa, atamfanya kuwa Yahudi. Na walipotolewa Mayahudi wa Baniy An-Nadhwiyr, kulikuwa katika wao kuna watoto wa Answaar. Kisha wakasema: “Hatuwaachi watoto wetu!” (Wakikusudia na mtoto huyo?) Hapo ikateremeka Aayah hii. [Ibn Jariyr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)]

 

 

 

 

Share

267-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 267: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 267- Enyi walioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٢٦٧﴾

267. Enyi walioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma na katika ambavyo Tumekutoleeni kutoka katika ardhi. Na wala msikusudie vibaya kutoka humo mkavitoa na hali nyinyi wenyewe si wenye kuvichukuwa isipokuwa kuvifumbia macho. Na jueni kwamba hakika Allaah ni Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa.

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Aayah hii:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ

Enyi walioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma…” mpaka mwisho, imeteremka  kuwazungumzia baadhi ya Swahaba  ambao walikuwa wakileta chane au shada la tende kisha wanalitundika Msikitini. Na Swahabi yeyote katika Ahlus-Swufaa anapohitajia chakula, alikuwa anatungua tende iliyoiva na mbichi. Na hao Swahaba waliokuwa wakileta tende Msikitini, walikuwa ni wale wasiopenda kujitolea katika njia ya  khayr. Hivyo walikuwa wakileta chane au shada la tende ambalo lina mchanganyiko wa tende ambazo hazikuiva kutokana na matatizo ya ulimaji  wa tende, na nyinginezo zilikuwa mbovu. Na wengine huleta chane au shada ambalo limekatika katika. Hapo ndipo ikateremka hii Aayah. [At-Tirmidhiy kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه), na Taz. Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Kadhaali: Ibn Jariyr alinukuu kuwa Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) alisema kuhusu sababu ya kuteremshwa hiyo Aayah: “Iliteremeshwa kuwahusu Answaar. Kila ulipowadia msimu wa kuvuna tende, Answaar walikusanya tende mbivu katika bustani zao na kuzitundika kwenye kamba iliyofungwa kati ya nguzo mbili ndani ya Masjid ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Masikini katika Muhaajiruwn walikuwa wakila tende hizo. Hata hivyo, baadhi ya Answaar waliweka tende duni katika tende mbivu zilizokomaa, walidhani kwamba iliruhusiwa kufanya hivyo, ndipo Allaah (سبحانه وتعالى)  Alipowateremshia Aayah kwa  sababu ya kufanya hivyo. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Share

272-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 272: لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

Al-Baqarah Aayah  272-Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa, lakini Allaah Humwongoa Amtakaye

 

لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾

272. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa, lakini Allaah Humwongoa Amtakaye. Na chochote cha kheri mtoacho basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika kheri mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa.

 

 Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii:

لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ

Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa… imeteremka kuhusu Swahaba ambao walikuwa hawawapi msaada hata kidogo ndugu zao wa karibu katika Washirikina, basi hapo ikateremka:

 

الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٢٧﴾

Wale wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata Aliyoyaamrisha Allaah kuungwa, na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye khasara. (2:27)  [Ibn Jariyr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)]

 

 

Share

285-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 285: آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah 285- Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾

 285. Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rusuli Wake. (Nao husema): “Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rusuli Wake.” Na wakasema: “Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia.

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾  

286. Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata (thawabu) iliyoyachuma, na ni dhidi yake (kwa maovu) iliyojichumia. “Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabb wetu, Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu. Rabb wetu, Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mola Mlinzi wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii na inayofuatia imeteremka kwa sababu, pale ilipoteremka Aayah iliyotangulia;

 

لِّلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَإِن تُبْدُوا مَا فِي أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ اللَّـهُ ۖ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٨٤﴾

Ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha; basi Allaah Atakuhesabuni kwayo. Humghufuria Amtakaye na Humuadhibu Amtakaye. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muweza. [Al-Baqarah (2:284)]

 

Ilikuwa ngumu mno kwa Swahaba, wakaogopa mno kuhusu kuhesabiwa vinavyofichika moyoni. Wakakaa kitako wakiwa wameegemea magoti yao wakasema: Ee Rasuli wa Allaah!  Tumeamrishwa ‘amali tunazoziweza kama Swalaah, Swiyaam, Jihaad, swadaqah, lakini imeteremka kwako Aayah hii wala hatuiwezi! Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Je mnataka kusema kama walivyosema Ahlul-Kitaab walio kabla yenu waliosema: Tumesikia natumeasi? Bali semeni:

 

سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾

Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia. [Al-Baqarah (2:285)]

 

Na walipoizoea katika ndimi zao, hapo Allaah Akateremsha:

 

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾

Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rusuli Wake. (Nao husema): Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rusuli Wake. Na wakasema: Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia. [Al-Baqarah (2:285)]

 

Kisha walipofanya hivyo, Allaah (عزّ وجلّ)  Akateremsha:

 

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾  

Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata (thawabu) iliyoyachuma, na ni dhidi yake (kwa maovu) iliyojichumia. Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabb wetu, Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu. Rabb wetu, Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mola Mlinzi wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri. [Al-Baqarah (2:286)] [Muslim kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) na mfano wake kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)]

 

 

 

 

Share