143-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 143: وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 143: Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe...

 

 

 وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ ۚ وَإِن كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٣﴾

143. Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. Na Hatukukifanya Qiblah ambacho ulikuwa ukikielekea (Baytul-Maqdis) isipokuwa Tupate kumpambanulisha yule anayemfuata Rasuli miongoni mwa mwenye kugeuka akarudi nyuma. Na hakika ilikuwa ni jambo gumu isipokuwa kwa wale ambao Allaah Amewaongoza. Na Allaah Hakuwa Mwenye kupoteza iymaan (Swalaah) yenu, hakika Allaah kwa watu, bila shaka ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

عَنِ الْبَرَاءِ بن عازب، رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم صَلَّى إِلَى بَيْتِ الْمَقْدِسِ سِتَّةَ عَشَرَ شَهْرًا أَوْ سَبْعَةَ عَشَرَ شَهْرًا، وَكَانَ يُعْجِبُهُ أَنْ تَكُونَ قِبْلَتُهُ قِبَلَ الْبَيْتِ، وَإِنَّهُ صَلَّى أَوْ صَلاَّهَا صَلاَةَ الْعَصْرِ، وَصَلَّى مَعَهُ قَوْمٌ، فَخَرَجَ رَجُلٌ مِمَّنْ كَانَ صَلَّى مَعَهُ، فَمَرَّ عَلَى أَهْلِ الْمَسْجِدِ وَهُمْ رَاكِعُونَ قَالَ: أَشْهَدُ بِاللَّهِ لَقَدْ صَلَّيْتُ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قِبَلَ مَكَّةَ، فَدَارُوا كَمَا هُمْ قِبَلَ الْبَيْتِ، وَكَانَ الَّذِي مَاتَ عَلَى الْقِبْلَةِ قَبْلَ أَنْ تُحَوَّلَ قِبَلَ الْبَيْتِ رِجَالٌ قُتِلُوا لَمْ نَدْرِ مَا نَقُولُ فِيهِمْ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ إِنَّ اللَّهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَحِيمٌ ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه) kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali Swalaah zake akielekeza uso wake Baytul-Maqdis (Palestina) kwa muda wa miezi kumi na sita au miezi kumi na saba, lakini alipendezewa kuwa Qiblah chake kiwe ni Al-Ka’bah (Makkah).  [Ikateremshwa Aayah: Kwa yakini Tumeona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam…” (2:144)]. Akaswali pamoja na watu (akielekea Al-Ka’bah). Kisha mmoja wa aliyekuwa akiswali naye alitoka nje akapitia watu Msikitini wakiwa wako katika rukuu (wakielekea Baytul-Maqdis). Akasema kuwaambia: “Nashuhudia kwa Allaah, nimetoka (sasa hivi) kuswali pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa ameelekea Makkah (Al-Ka’bah).” Waliposikia hivyo, hapo hapo waligeuka kuelekea Al-Ka’bah wakati wakiwa katika hali hiyo hiyo ya  kurukuu. Baadhi ya Waislamu waliokuwa wakiswali kuelekea Qiblah (cha Baytul-Maqdis) kabla ya kubadilishwa kuelekea Nyumba (Al-Ka’bah Makkah) walifariki au walikufa kishahidi, nasi hatukujua tuseme nini kuhusu wao (na kuelekeza Swalaah zao Baytul-Maqdis). Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: Na Allaah Hakuwa Mwenye Kupoteza iymaan yenu (Swalaah), hakika Allaah kwa watu, bila shaka ni Mwenye huruma mno, Mwenye Kurehemu.” (2:143) [Al-Bukhaariy]

 

 

Share