Mukhtasari Wa 'Aqiydah Ya Muislamu: Maswali Na Majibu

 

 

 

 

 

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na  Sunnah

 

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

Share

01-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Kwa nini Allaah Katuumba?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

01-Kwa nini Allaah Katuumba?

 

Allaah Ametuumba ili tumuabudu na tusimshirikishe Naye kwa chochote.

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾

Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu. [Adh-Dhaariyaat: 56]

 

((حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ أَنْيَعْبُدُوهُ، وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا))متّفق عَلَيهِ

((Haki ya Allaah kwa waja wake ni kwamba wamwabudu na wasimshirikishe na chochote)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share

02-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Vipi tumuabudu Allaah?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 02-Vipi tumuabudu Allaah?

 

Tumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa ikhlaasw kama Alivyotuamrisha Allaah na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini [Al-Bayyinah: 5]

 

((مَن عمِلَ عمَلاً لَيْسَ عَلَيهِ أمْرُنا فَهُوَ رَدٌّ)) رواه مسلم .

((Atakayetenda kitendo kisichokuwa katika jambo letu kitarudishwa)) [Muslim]

 

Yaani: Hakitapokelewa.

 

 

Share

03-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Tumuabudu Allaah kwa kumuogopa na kutumaini?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

03- Je, Tumuabudu Allaah kwa kumuogopa na kutumaini?

 

Naam! Tumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kumukhofu na kuwa na matumaini

وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا ۚ

Na muombeni kwa khofu na matumaini.  [Al-A’raaf: 56]

 

Yaani: Kukhofu moto na kutumaini Jannah.

 

((أسألُ اللهَ الجنّة وأعوذ بِهِ مِن النّار)) صحيح رواه أبو داود .

((Namuomba Allaah Jannah na najikinga Kwake kutokana na moto)) [Swahiyh ameipokea Abuu Daawuwd]

 

 

Share

04-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini Ihsaan katika ‘Ibaadah?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 04-Nini Ihsaan katika ‘ibaadah?

 

Maana ya Ihsaan katika i’baadah ni kujichunga kuwa makini katika ‘ibaadah kwa ajili Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee.

إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا ﴿١﴾ 

Hakika Allaah daima Amekuwa juu yenu Mwenye kuchunga [An-Nisaa: 1]

الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ ﴿٢١٨﴾

Ambaye Anakuona wakati unaposimama. [Ash-Shu’araa: 218]

 

((الإحسانُ أَنْ تعبُدَ اللهَ كأنّك تراه فإن لَمْ تكن تراهُ فإنَّه يراك))  رواه مسلم

 ((Ihsaan ni kumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama vile unamuona, na kama humuoni basi Yeye Anakuona)). [Muslim]

 

 

 

Share

05-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Kwanini Allaah Ametuma Rusuli?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 05-Kwanini Allaah Ametuma Rusuli?

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewatuma Rusuli ili walinganie watu kumwabudu na kuepukana na kumshirikisha.

 

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ

Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (alinganie) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaghuti.  [An-Nahl: 36]

 

((الأنبياء إخوةٌ ودينُهُم واحد)) متّفق عَلَيهِ

أَيْ كلُّ الرسل دعوا إِلَى التّوحيد

((Manabiy ni ndugu na Dini yao ni moja)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Yaani: Rusuli wote wamelingania Tawhiyd

 

 

 

Share

06-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini Tawhiyd ya Ilaah?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

06-Nini Tawhiyd ya Ilaah?

 

Tawhiyd ya Ilaah ni kumfanyia ‘ibaadah Pekee Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama du’aa, kuchinja, kuweka nadhiri na kadhaalika.

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ

Basi jua kwamba laa ilaaha illa-Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah [Muhammad: 19]

Yaani: Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah.

 

((فَلْيَكُنْ أَوَّلَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ شَهَادَةَ أَنلاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ))  متّفق عليه  

أَيْ إِلَى أَنْ يوحّدوا الله

((Basi liwe jambo la kwanza la kuwalingania wao Kwake ni "Shahaadah kwamba hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Yaani; Wampwekeshe Allaah.

 

 

 

Share

07-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini maana ya Laa Ilaaha illa Allaah?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

07-Nini maana ya Laa Ilaaha illa Allaah.

 

Maana ya laa ilaaha illa-Allaah ni: Hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الْبَاطِلُ

Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ndiye wa Haki na kwamba wale wanaowaomba badala Yake, ni batili; [Luqmaan: 30]

 

((من قَالَ لآ إله إِلاَّ الله وكَفَرَ بِمَا يُعبدُ مِن دون الله حَرُمَ مالُه ودمُه)) مسلم

((Atakayesema 'Laa ilaaha illa Allaah na akakanusha wanaoabudiwa wasio Allaah italindwa (itakuwa haramu mtu kuchukua) mali yake na damu yake (uhai wake)) [Muslim]

 

Share

08-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini maana ya Tawhiyd katika Sifa za Allaah?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

08-Nini maana ya Tawhiyd katika Sifa za Allaah?

 

Tawhiyd katika Sifa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kuthibitisha vile vile Alivyojiwekea Sifa Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) au Rasuli Wake.

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿١١﴾

Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Ash-Shuwraa: 11]

 

((ينزِلُ ربُّنا تبارك وتعالى فِي كلّ ليلةٍ إِلَى السّمَاء الدُّنْيَا)) متّفق عليه

نزولاً يليق بجلاله

((Rabb wetu Huteremka kila usiku katika mbingu ya dunia)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Kuteremka kunakolaikiana na Ujalali Wake.

 

Share

09-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini faida ya Tawhiyd kwa Muislamu?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

09-Nini faida ya Tawhiyd kwa Muislamu?

 

Faida ya Tawhiyd kwa Muislamu ni kupata Hidaaya duniani na kuwa katika amani  Aakhirah.

الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢﴾

Wale walioamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma; hao ndio watakaopata amani nao ndio walioongoka. [Al-An’aam: 82]

 

((وَحَقُّ الْعِبَادِ عَلى اللهِ أَنْ لاَ يُعَذِّبَ مَنْ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا)) متّفق عَلَيهِ

((Haki ya waja kwa Allaah ni kwamba Hatomwadhibu yeyote ambaye hamshirikishi na chochote kile)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share

10-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Allaah Yuko wapi?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

10-Je, Allaah Yuko wapi?

 

Allaah Yuko mbinguni juu ya ‘Arsh.

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

Ar-Rahmaan juu ya ‘Arshi Istawaa [Twaahaa: 5]

 

Maana ya Istawaa: Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah.

 

((إِنَّ اللَّهَ كَتَبَ كِتَابًا : إِنَّ رَحْمَتِي سَبَقَتْ غَضَبِي، فَهُوَمكتوبٌ عِنْدَهُ فَوْقَ الْعَرْشِ))   البخاري

((Hakika Allaah Ameandika maandishi kwamba: “Rahmah yangu imeshinda ghadhabu yangu, nayo yameandikwa kumhusu Yeye juu ya 'Arsh)) [Al-Bukhaariy]

 

 

Share

11-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Allaah Yuko na sisi kwa dhati Yake au kwa ujuzi Wake?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

11-Je, Allaah Yuko na sisi kwa dhati Yake au kwa ujuzi Wake?

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Yuko na sisi kwa ujuzi Wake Anatuona na Anatusikia. Hayuko na sisi kwa dhati Yake.

 

قَالَ لَا تَخَافَا ۖ إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ ﴿٤٦﴾

(Allaah) Akasema: “Msikhofu; hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona. [Twaahaa: 46]

 

((إنَّكُمْ تَدْعونَ سَميعاً قَريباً وَهُوَ مَعَكُم)) رواه مسلم.

((Hakika nyinyi mnamuomba Mwenye kusikia, Aliye karibu, na Yeye Yuko pamoja nanyi)) [Muslim]

 

 

 

Share

12-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Dhambi gani kubwa zaidi?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

 12-Dhambi gani kubwa zaidi?

 

Dhambi kubwa kabisa ni kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

 يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ﴿١٣﴾

 “Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah, hakika shirki ni dhulma kubwa mno!” [Luqmaan: 13]

 

سُئِلَ صلى الله عليه وسلم أيُّ الذَّنب أعظم؟ قَالَ: ((أَنْ تدعو للهِ ندّاً وَهُوَ خَلَقَك))   رواه مسلم

Aliulizwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) dhambi gani kubwa? Akasema: ((Ni kumuomba Allaah pamoja na mshirika Na hali Yeye Ndiye Aliyekuumba)) [Muslim]

 

 

Share

13-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Shirki gani iliyokuwa kubwa?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

13-Shirki gani iliyokuwa kubwa?

 

Shirkii kubwa ni kufanya ‘ibaadah kwa kumuelekea asiye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama du'aa.

 

قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا﴿٢٠﴾

Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi namuomba Rabb wangu na wala simshirikishi na yeyote.” [Al-Jinn: 20]

 

 ((أَكْبرَرُ الْكَبآئِر الإشراكُ باللهِ))  رواه البخاري

((Dhambi kubwa ni kumshirikisha Allaah)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 

 

 

Share

14-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Ni yapi madhara ya kumshirikisha Allaah?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

14-Ni yapi madhara ya kumshirikisha Allaah?

 

Madhara ya kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) husababisha kudumu milele motoni.

 

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ

Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni.  [Al-Maaidah: 72]

 

((من ماتَ يُشرِك باللهِ شيئاً دخل النّار))   رواه مسلم

((Atakayekufa na huku amemshirikisha Allaah kwa chochote, ataingia motoni)) [Muslim]

 

 

 

 

 

 

Share

15-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Kitendo chema kinafaa kikiwa kimemshirikisha Allaah?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

15-Je, Kitendo chema kinafaa kikiwa kimemshirikisha Allaah?

 

Hapana! Kitendo chema ambacho kina kumshirikisha Allaah hakifai kitu mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾

Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda. [Al-An’aam: 88]

 

((من عمِلَ عملاً أشرك معيَ فِيهِ غيري تركتُه وشِرْكَه)) حديث قدسي رواه مسلم.

((Atakayefanya kitendo na huku kanishirikisha Mimi na mwengine, namwacha yeye na mshirika wake)) [Hadiyth Qudsiy ameipokea Muslim]

 

 

Share

16-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Shirki ipo kwa Waislamu?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

16-Je, Shirki ipo kwa Waislamu?

 

Naam! Shirki ipo kwa Waislamuna masikitiko kuwa ipo tena wanamshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa wingi!

 

وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُم بِاللَّـهِ إِلَّا وَهُم مُّشْرِكُونَ ﴿١٠٦﴾

106. Na wengi kati yao hawamwamini Allaah isipokuwa wao ni wenye kufanya shirki. [Yuwsuf: 106]

 

((لاَ تقوم السّاعة حتّى تلحق قبائل مِن أُمّتي بالمشركين وحتى تُعبَد الأوثان)) صحيح رواه الترمذي.

((Qiyaamah hakitosimama mpaka kutafika wakati watu wa baadhi ya makabila katika ummah wangu wataungana na washirikina na hadi watakapoabudu asiye Allaah! [Swahiyh ameipokea At-Tirmidhiy]

 

 

 

 

 

 

 

Share

17-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini hukumu ya kumuomba asiye Allaah kama Mawalii?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

17-Nini hukumu ya kumuomba asiye Allaah kama Mawalii?

 

 

Hukmu ya kuwaomba ‘Mawalii’ ni shirki yenye kumpeleka mtu motoni.

 

فَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَكُونَ مِنَ الْمُعَذَّبِينَ ﴿٢١٣﴾

Basi usiombe pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine ukaja kuwa miongoni mwa watakaoadhibiwa. [Ash-Shu’araa: 213]

 

((من ماتَ وَهُوَ يدعو مِن دون الله نِدّاً دخل النّار)) رواه البخاري

((Atakayefariki katika hali ya kumuomba asiye Allaah ataingia motoni)) [Al-Bukhaariy]

 

 

Mawalii:  Waliokusudiwa hapa ni watu wema waliofariki wakaombwa wao makubirini badala ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) au wakatumiliwa kama ni tawassul ya kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). 

 

 

 

 

Share

18-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Kuomba du'aa ni ‘ibaadah ya Allaah?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

18-Je, Kuomba du'aa ni ‘ibaadah ya Allaah?

 

 

Naam! Kuomba du'aa ni ‘ibaadah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ

Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni.  [Ghaafir: 60]

 

((الدّعاء هُوَ العبادة)) رواه الترمذي وقال حديث صحيح

((Du’aa ndio ‘ibaadah)) [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Swahiyh]

 

 

 

Share

19-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, waliokufa wanasikia wito?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

19- Je, waliokufa wanasikia wito?

 

Hapana! Waliokufa hawasikii wito.

 

إِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ

Hakika wewe huwezi kusikilizisha wafu [An-Naml: 80]. 

 

 وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ ﴿٢٢﴾

Nawe huwezi kuwasikilizisha walioko kaburini. [Faatwir: 22]

 

((إنَّ لِلَّهِ ملائكةً سَيّاحِين فِي الأرْضِ يُبَلّغوني عَنْ أُمّتي السَّلام)) رواه أحمد

((Hakika Allaah Anao Malaika wanaozunguka katika ardhi wakinifikishia salaam kutoka kwa ummah wangu)) [Ahmad]

 

 

 

 

Share

20-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kustaghithi (kuomba uokovu) maiti na wasiokuwepo?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

20-Je, Inajuzu kustaghithi (kuomba uokovu) maiti na wasiokuwepo?

 

Hapana! Haijuzu kustaghithi kwa maiti na wasiokuwepo, bali tustaghithi (tuombe uokovu) kwa Allaah.

 

إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ

Na (kumbukeni) pale mlipomuomba uokovu Rabb wenu Naye Akakuitikieni [Al-Anfaal: 9] 

 

((كَانَ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا أصابه هَمٌّ أَوْ غَمٌّ قَالَ: ((يَا حيُّ يَا قيّوم برحمتك أستغيث))    رواه الترمذي

Alikuwa (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapofikwa na wahka au dhiki husema: ((Yaa Hayyu Yaa Qayyuwm bi Rahmatika astaghiythu - Ee Uliye hai daima, Msimamia wa kila kitu, kwa rahmah Zako naomba uokozi)) [At-Tirmidhy Hadiyth Hasan]

 

 

 

 

Share

21-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzukuomba Isti’aanah kwa asiyekuwa Allaah?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 21-Je, Inajuzukuomba Isti’aanah kwa asiyekuwa Allaah?

 

 

Hapana! Haijuzu kuomba Isti’aanah kwa mwengine asiye Allaah.

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada. [Al-Faatihah: 5]

 

((إِذَا سَأَلْتَ فاسْألِ الله وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فاسْتَعِنْ بالله))  رواه الترمذي

((Unapoomba muombe Allaah na unapotaka Isti’aanah (msaada) taka isti’aanah kwa Allaah)) [At-Tirmidhiy]

 

 

 

 

 

 

Share

22-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kuomba msaada kwa walio hai?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

22-Je, Inajuzu kuomba msaada kwa walio hai?

 

Naam, inajuzu kuomba msaada kwa walio hai katika mambo ambayo wana uwezo nayo. 

 

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ

Shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui [Al-Maaidah: 2]

((واللهُ فِي عَوْنِ الْعَبْد مَا دام الْعَبْدُ فِي عَوْنِ أخِيه)) رواه مسلم

((Allaah Yuko katika kumsaidia mja Wake maadam mja huyo yuko katika kumsaidia nduguye)) [Muslim]

 

 

 

Share

23-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

23 Je, Inajuzu kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah?

 

Hapana! Haijuzu kuweka nadhiri isipokuwa kwa sababu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي ۖ   

 “Rabb wangu, hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kilichomo katika tumbo langu kuwa ni wakfu kukutumikia, basi nitakabalie. [Aal-‘Imraan: 35]

 

((مَنْ نَذَرَ أَنْ يُطِيعَ اللَّهَ فَلْيُطِعْهُ ، وَمَنْ نَذَرَ أَنْ يَعْصِيَهُ فَلَا يَعْصِهِ))رواه البخاري

((Anayeweka nadhiri kumtii Allaah basi amtii, na aliyeweka nadhiri kumuasi Allaah basi asimuasi)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 

Share

24-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kuchinja bila kumkusudia Allaah?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

24-Je, Inajuzu kuchinja bila kumkusudia Allaah?

 

Hapana! Haijuzu kuchinja kwa malengo yasiyo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa sababu ni shirki kubwa.

 

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake. [Al-Kawthar: 2]

 

((لَعَنَ الله مَنْ ذبح لِغير الله))  رواه مسلم

((Allaah Humlaani anayechinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah)) [Muslim]

 

 

 

Share

25-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kutufu makaburi?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

25-Je, Inajuzu kutufu makaburi?

 

Hapana! Haijuzukutufu (kuzunguka) makaburi, bali kutufu ni kwa ajili ya Ka'abah pekee.

 

 وَلْيَطَّوَّفُوا بِالْبَيْتِ الْعَتِيقِ ﴿٢٩﴾

Na watufu kwenye Nyumba ya Kale. (Al-Ka’bah) [Al-Hajj: 29]

 

((مَنْ طافَ بِالْبَيْتِ سَبْعاً وَصَلّى رَكَعَتينِ كَانَ كَعتق رَقَبة))  رواه ابن ماجه و صححه الألباني 

((Atakayezunguka Ka'bah mara saba kisha akaswali rakaa mbili ni kama mfano kamwacha huru mtumwa mmoja)) [Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (6379)]

 

 

 

Share

26-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kuswali na kaburi liko mbele yako?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

26-Je, Inajuzu kuswali na kaburi liko mbele yako?

 

Hapana! Haijuzu kuswali kulielekea kaburi.

 

فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِۚ

Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam [Al-Baqarah: 144]

 

Yaani: Qiblah

((لا تَجْلِسُوا عَلَى الْقُبُورِ وَلا تُصَلُّوا إِلَيْهَا)) رواه مسلم

((Msikalie makaburi wala msiswali kuyaelekea)) [Muslim]

 

 

 

 

 

 

Share

27-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini hukumu ya mwenye kufanya sihri (uchawi)?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

27-Nini hukumu ya mwenye kufanya sihri (uchawi)?

 

Mwenye kufanya sihri ni kukufuru.

 

وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ

lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri [Al-Baqaarah: 102]

 

((اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ:الشِّرْكُ بِاللَّهِ وَالسِّحْرُ))  متّفق عليه

 ((Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza; kumshirikisha Allaah, sihri (uchawi)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share

28-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kumwendea kahini na mpiga ramli?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

28-Je, Inajuzu kumwendea kahini na mpiga ramli?

 

Hapana! Haijuzu kumwendea kahini wala mpiga ramli.

 

هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ الشَّيَاطِينُ ﴿٢٢١﴾

Je, nikujulisheni wanaowateremkia mashaytwaan?

تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ ﴿٢٢٢﴾

Wanateremka juu ya kila mzushi mkubwa mwingi wa kutenda dhambi.  [Ash-Shu’araa: 221-222]

 

((مَنْ أَتَى عَرَّافًا فَسَأَلَهُ عَنْ شَيْءٍ لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلَاةٌ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً)) مسلم

((Atakayekwenda kwa mtabiri akamuuliza kitu haitokubaliwa Swalaah yake siku arubaini)) [Muslim]

 

 

 

 

 

Share

29-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kuwaamini wanaopiga ramli na makahini?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

29-Je, Inajuzu kuwaamini wanaopiga ramli na makahini?

 

Hapana! Haijuzu kuwaamini wala kuamini wayasemayo ya ghayb. (yaliyofichika ambayo hakuna mwenye ujuzi nao isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

 

قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ﴿٦٥﴾

Sema: “Hakuna aliyoko katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah. Na wala hawatambui lini watafufuliwa.” [An-Naml: 65]

 

((مَنْ أَتَى كَاهِنًا، أَوْ عَرَّافًا، فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ، فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم)) صحيح رواه أحمد

 ((Atakayemwendea kahini au mpigaji ramli akamuamini asemayo, basi atakuwa ameshakufuru yale aliyoteremshiwa nayo Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)). [Ahmad, na Aswhaabus-Sunan wanne, na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb (3047)]

 

 

 

 

Share

30-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Mtu anaweza kuyajua mambo ya ghayb?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

30-Je, Mtu anaweza kuyajua mambo ya ghayb?

 

Hakuna awezaye kuyajua ya ghayb isipokuwa Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ

Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu. [Al-An’aam: 59]

 

((لاَ يَعْلَمُ الْغَيْبَ إِلاَّ الله)) حسن رواه الطّبراني

((Hakuna ajuaye mambo ya ghayb isipokuwa Allaah. [Hadiyth Hasan ameipokea Atw-Twabaraaniy]

 

Share

31-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Waumini watamuona Rabb wao watakapoingia Jannah?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 31-Je, Waumini watamuona Rabb wao watakapoingia Jannah?

 

Naam. Waumini watamuona Rabb wao watakapoingia Jannah.

 

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ ﴿٢٢﴾

 

Nyuso siku hiyo zitanawiri.

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ﴿٢٣﴾

Zikimtazama Rabb wake. [Al-Qiyaamah: 22-23]

 (إنَّكُمْ سَتَرون رَبكُم) رواه البخاري ومسلم

((Hakika nyinyi mtamuona Rabb wemu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share

32-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Waislamu wanapaswa wawe wanahukumu mambo yao kwa kufuata nini?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

32-Waislamu wanapaswa wawe wanahukumu mambo yao kwa kufuata nini?

 

Waislamu wanapaswa wahukumu kufuata Qur-aan na Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ

Na wahukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah [Al-Maaidah: 49]

 

((الله هُوَ الْحكم وَإلَيْهِ المَصِير))  حسن رواه أبو داود

((Allaah ndiye mwenye kuhukumu na Kwake ndio marejeo)) [Hadiyth Hasan ameipokea Abuu Daawuwd]

 

 

 

Share

33-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini hukumu ya kufuata shariy’ah zisizo za Kiislam?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

33-Nini hukumu ya kufuata shariy’ah zisizo za Kiislam?

 

Kuzifuata shariy’ah zisizo za Kiislamu na kuzifanyia kazi na kuziacha shariy’ah za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kufuru kubwa.

 

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ﴿٤٤﴾

Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri. [Al-Maaidah 44]

 

((وَمَا لَمْ تَحْكُمْ أَئِمَّتُهُمْ بِكِتَابِ اللَّهِ وَيَتَخَيَّرُوا مِمَّا أَنْزَلَ اللَّهُ إِلَّا جَعَلَ اللَّهُ بَأْسَهُمْ بَيْنَهُمْ))  حسن رواه ابن ماجه

((Na wasipohukumu viongozi wao kwa Kitabu cha Allaah na wakawa wanachagua katika Aliyoyateremsha Allaah, basi Allaah Atawajaalia kutoelewana (migongano) baina yao [Hadiyth Hasan ameipokea Ibn Maajah]

 

 

 

Share

34-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kuapa kwa mwengine asiye Allaah?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

34-Je, Inajuzu kuapa kwa mwengine asiye Allaah?

 

Hapana! Haijuzuu kuapa kiapo kisicho cha Allaah.

قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ

Bali hapana! Naapa kwa Rabb wangu, bila shaka mtafufuliwa [At-Taghaabun: 7]

 

((مَنْ حَلَفَ  بِغَيْرِ اللَّهِ فَقَدْ كَفَرَ أَوْ أَشْرَكَ))  رواه الترمذي   وأبو داود  وصححه الألباني في صحيح الترمذي .

 ((Atakayeapa pasi na Allaah, atakuwa amekufuru au amemshirikisha Allaah])) [At-Tirmidhiy, Abu Daawuwd na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy]

 

 

Share

35-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kutundika au kuvaa hirizi?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

35-Je, Inajuzu kutundika au kuvaa hirizi?

 

Hapana! Haijuzu kutundika au kuvaa hirzi kwa sababu ni shirki.

 

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ

Na Allaah Akikugusisha kwa dhara, basi hakuna yeyote wa kukuondolea hiyo isipokuwa Yeye [Al-An’aam: 17]

 

((من علّق تميمةً فَقَدْ اشرك)) صحيح رواه أحمد

((Atakayetundika hirizi, atakuwa ameshirikisha Allaah)) [Hadiyth Swahiyh ameipokea Ahmad]

 

 

Share

36-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Tunatakiwa tutawassal kwa Allaah kwa vipi?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

36-Je, Tunatakiwa tutawassal kwa Allaah kwa vipi?

 

Tunapaswa kutawassal kujikurubisha Kwake kwa kutaja majina Yake Mazuri, na Sifa Zake, na ‘amali njema zetu.

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ

 

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo.  [Al-A’raaf: 180]

 

((أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيْتَ بِهِ نَفْسَكَ)) صحيح رواه أحمد  - صححه الألباني في السلسلة الصحيحة (199)

 ((Nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako Ulilojiita Mwenyewe)) [Hadiyth Swahiyh ameipokea Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Silsilah Asw-Swahiyhah (199)]

 

 

Share

37-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Unahitaji kumuomba Allaah kumtegemea kiumbe yeyote?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

37-Je, Unahitaji kumuomba Allaah kumtegemea kiumbe yeyote?

 

Hapana! Huhitaji kumtegemea kiumbe mwengine unapomuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ

Na watakapokuuliza waja Wangu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba.  [Al-Baqarah: 186]

 

((إِنَّكُمْ تَدْعُونَ سَمِيعًا قَرِيبًا وَهُوَ مَعَكُمْ))  رواه مسلم

((Hakika nyinyi mnamuomba Mwenye kusikia, Aliye karibu (nanyi) Naye Yuko na pamoja nanyi [kwa ujuzi Wake])) [Muslim]

 

 

 

Share

38-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini jukumu la Rasuli

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

38-Nini jukumu la Rasuli?

 

Jukumu la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kubalighisha ujumbe.

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako.  [Al-Maaidah: 67]

 

((أللّهم هَلْ بلّغت؟ اللّهم اشهد))  مسلم 

جواباً لقول الصحابة نشهد أنّك قد بلّغت

((Ee Allaah! Je nimebalighisha? Ee Allaah Shuhudia)) [Muslim]

 

Jibu la Maswahaba walosema kuwa: Tunashuhudia kuwa umebalighisha.

 

 

 

Share

39-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nani tumuombe tukitaka kuombewa shafaa'ah na Nabiy?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

39-Nani tumuombe tukitaka kuombewa shafaa'ah na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?

 

Tukitaka kuombewa shafaa’ah na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inapasa tumuombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).  

 

قُل لِّلَّـهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا ۖ

Sema: “Uombezi wote ni wa Allaah Pekee.  [Az-Zumar: 44]

 

((اللّهم شفّعه فيّ)) رواه الترمذي وقال حديث حسن.

((Ee Allaah! Ikubali shafaa’ah (maombezi) yake kwangu))

 

 

 

Share

40-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Vipi tumpende Allaah Na Rasuli Wake?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

40-Vipi tumpende Allaah Na Rasuli Wake?

 

Mapenzi ya Allaah na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kutii na kufuata amri ya Allaah.

 

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ...

31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah  [Aal-‘Imraan: 31]

 

((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكونَ أحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ وَوَلَدِه وَالنَّاسِ أَجْمَعينَ)) متفق عليه

((Hatoamini mmoja wenu mpaka niwe (mimi Muhammad) kipenzi chake kuliko mwanawe na wazazi wake na kuliko watu wote waliobakia)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share

41-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kupinduka mipaka kumsifu Nabiy kwa kumpandisha cheo kama cha Allaah?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

41-Je, Inajuzu kupinduka mipaka kumsifu Nabiy kwa kumpandisha cheo kama cha Allaah?

 

 Hapana! Haijuzu kupinduka mipaka kumsifu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka kumfikisha cheo cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni mtu kama nyinyi, nafunuliwa Wahy kwamba: Hakika Muabudiwa wa haki wenu ni Ilaah Mmoja Pekee [Al-Kahf: 111]

 

((لا تُطْرُونِي كَمَا أَطْرَتْ النَّصَارَى ابْنَ مَرْيَمَ فَإِنَّمَا أَنَا عَبْدُهُ فَقُولُوا عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ)) متفق عليه

((Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi ni mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Rasuli Wake)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share

42-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nani kiumbe cha mwanzo na kipi kilichoumbwa mwanzo?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

42-Nani kiumbe cha mwanzo na kipi kilichoumbwa mwanzo?

 

Kiumbe cha mwanzo kabisa ni Aadam ('Alayhis-Salaam) na kitu cha mwanzo kuumbwa ni kalamu.

إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن طِينٍ ﴿٧١﴾

Pale Rabb wako Alipowaambia Malaika: “Hakika Mimi Namuumba mtu kutokana na udongo. [Swaad: 71]

 

((إنّ أوّلَ مَا خَلَقَ اللهُ الْقَلَم))  رواه أبو داود والترمذي، وقال: حسن صحيح

((Kitu cha kwanza Alichoumba Allaah ni kalamu)) [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy amesema Hasan Swahiyh]

 

 

 

Share

43-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ameumbwa kutokana na nini?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

43-Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameumbwa kutokana na nini?

 

Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameumbwa kutokana na manii (kwa sababu yeye ni mwana Aadam kama sisi).

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ

Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na mchanga, kisha kutokana na tone la manii. [Ghaafir: 67]

 

((إنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّه فِي أرْبعينَ يوْماً نُطْفَةً)) متفق عليه

((Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa manii)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Manii ni mbegu za uzazi za mama na baba.

 

Share

44-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini hukumu ya jihaad kwa Muislamu?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

44-Nini hukumu ya jihaad kwa Muislamu?

 

Kufanya jihaad ni waajib kwa Muislamu kwa kutumia mali, nafsi, na ulimi.

 

انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ

Tokeni mwende (vitani) mkiwa wepesi na (mkiwa) wazito, na fanyeni jihaad kwa mali zenu na nafsi zenu katika njia ya Allaah.  [At-Tawbah: 41]

 

((جَاهِدُوا الْمُشْرِكِينَ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنْفُسِكُمْ وَأَلْسِنَتِكُمْ)) صحيح أبي داود

((Piganeni Jihaad na washirikina kwa mali zenu, nafsi zenu na ndimi zenu)) [Swahiyh Abiy Daawuwd: (2186)]

 

 

 

Share

45-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Vipi kuwafanyia urafiki Waumini?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

45-Vipi kuwafanyia urafiki Waumini?

 

Kuwafanyia urafiki Waumini ni kuwaandama kwa mapenzi na kuwanusuru Waumini walioshikamana na Tawhiyd.

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ

71. Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki wandani wao kwa wao, [At-Twabah: 71]

 

 

((الْمُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِ كَالْبُنْيَانِ يَشُدُّ بَعْضُهُ بَعْضًا)) متفق عليه.

((Muumini kwa Muumini mwenzake ni kama mfano wa jengo (matofali) hushikamana pamoja. [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share

46-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inafaa kufanya urafiki na makafiri na kuwasaidia?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

46-Je, Inafaa kufanya urafiki na makafiri na kuwasaidia?

 

Hapana! Haifai kufanya urafiki na kuwaandama makafiri na kuwasaidia.

 

 وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ

 Na yeyote atakayewafanya marafiki wao wandani; basi hakika yeye ni miongoni mwao.  [Al-Maaidah: 51]

 

((إنَّ آلَ أَبِي فُلَانٍ لَيْسُوا لِي بأولياء))  متّفق عَلَيهِ

لأنّهم من الكفّار

((Hakika watu wa kabila fulani si vipenzi vyangu))[Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Kwa sababu wao ni makafiri.

 

 

Share

47-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nani Waliyy wa Allaah?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

47-Nani Waliyy wa Allaah? 

 

Waliyy wa Allaah ni Muumini mwenye taqwa mno na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٦٢﴾

Tanabahi!  Hakika vipenzi wa Allaah hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika

 

الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿٦٣﴾

Ambao wameamini na wakawa wana taqwa. [Yuwnus: 63]

 

((إِنَّمَا وَلِيِّيَ اللهُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ)) متّفق عَلَيهِ

((Bali yeye ni kipenzi cha Allaah na Muumini mwema)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share

48-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Kwanini Allaah Ameteremsha Qur-aan?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

48-Kwanini Allaah Ameteremsha Qur-aan?

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameteremsha Qur-aan ili tufuate yaliyomo.

 

اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٣﴾

Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Rabb wenu na wala msifuate badala Yake walinzi. Ni machache mnayoyakumbuka. [Al-A’raaf: 3]

 

((اقْرَءُوا الْقُرْآنَ وَاعْمَلُوا بِهِ وَلَا تَغْلُوا فِيه وَلَا تَجْفُوا عَنْهُ وَلَا تَأْكُلُوا بِهِ وَلَا تَسْتَكْثِرُوا بِهِ)) رواه أحمد

((Someni Qur-aan na muifanyie kazi, na wala msipokee ujira kwa kuisoma)) [Ahmad]

 

 

Share

49-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, tutosheke na Qur-aan bila Hadiyth?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

49-Je, tutosheke na Qur-aan bila Hadiyth?

 

 

Hapana! Tunapaswa tuifuate Qur-aan na pia Hadiyth bila kutosheka na Qur-aan pekee.

 

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ

(Tumewatuma) Kwa hoja bayana na vitabu. Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao. [An-Nahl: 44]

 

((أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ مَعَهُ)) صحيح رواه أبو داود

((Hakika mimi nimepewa Qur-aan na mfano wake)) [Hadiyth Swahiyh, Abuu Daawuwd]

 

 

Share

50-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je? Tunaweza kutanguliza maneno yetu mbele ya kauli ya Allaah Na Rasuli Wake?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

50-Je? Tunaweza kutanguliza maneno yetu mbele ya kauli ya Allaah Na Rasuli Wake?

 

 

Hapana! Haifai kutanguliza maneno yetu mbele ya kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

Yaani: Msilete rai zenu wala msifanye kinyume na Aliyoamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١﴾

Enyi walioamini! Msikadimishe (lolote) mbele ya Allaah na Rasuli Wake [Al-Hujuraat: 1]

 

((لَا طَاعَة لأحدَ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوفِ)) متّفق عَلَيهِ

((Hakuna kumtii mtu yeyote katika kumuasi Allaah, Bali Utiifu ni katika mambo mema)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share

51-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Tufanye nini pale tunapokhitilafiana?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

51-Tufanye nini pale tunapokhitilafiana?

 

Pale tunapokhitilafiana, inatupasa turejee katika Qur-aan na Sunnah Sahihi?

 

 فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli [An-Nisaa: 59]

 

((تَرَكْتُ فِيكُمْ أَمْرَيْنِ لَنْ تَضِلُّوا مَا تَمَسَّكْتُمْ بِهِمَا: كِتَابَ اللهِ وَسُنَّةَ نَبِيِّهِ)) صحيح لغيره رواه مالك

((Nimekuachieni viwili ambavyo mkikamatana navyo hamtopotea abadan baada yangu; Kitabu cha Allaah na Sunnah zangu)) [Swahiyh lighayrihi – ameipokea Maalik]

 

 

Share

52-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini Bid'ah katika Dini?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

52-Nini Bid'ah katika Dini?

 

Bid’ah katika Dini ni kila kilichokuwa hakina dalili katika Shariy’ah ya Dini.

 

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ ۚ

Je, wanao washirika waliowaamuru Dini yale ambayo Allaah Hakuyatolea idhini? [Ash-Shuwraa: 21]

 

((مَنْ أَحْدَثَ فِيْ أَمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ)) متّفق عَلَيهِ

Atakayezusha katika mambo yetu haya (Dini yetu) yasiyokuwemo basi kitarudishwa)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Yaani: Hakitokubaliwa kitendo chake

 

 

Share

53-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Ipo bid'ah inayoitwa bid-‘atun-hasanah’ katika Dini?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

53-Je, Ipo bid'ah inayoitwa bid-‘atun-hasanah’ katika Dini?

 

Hapana! Hakuna bid’atun-hasanah (uzushi mzuri) katika Dini.

 

 

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ

Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislaam uwe Dini yenu. [Al-Maaidah: 3]

 

 

((إِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الْأُمُورِ، فَإِنَّ كُلَّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ، وَكُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ)) صحيح رواه أبو داود

((Jitahadharini na uzushi wa mambo, kwani kila uzushi ni bid'ah na kila bid'ah ni upotofu)) [Swahiyh - Abuu Daawuwd]

 

Share

54-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Ipo Sunnatun-hasanah katika Uislamu?

 

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

54-Je, Ipo Sunnatun-hasanah katika Uislamu?

 

Naam, ipo Sunnatun-hasanah (Sunnah nzuri) katika Uislamuu kama vile anayeanza kufanya kitendo chema cha kheri akafuatwa.

 

 وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾

Na Tujaalie kuwa waongozi kwa wenye taqwa.  [Al-Furqaan: 74]

 

((مَنْ سَنَّ فِي الإِسْلامِ سُنَّةً حَسَنَةً فَلَهُ أَجْرُهَا وَأَجْرُ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ بَعْدِه )) مسلم

"Atakayeanzisha mwenendo mwema " سُنَّةً حَسَنَةً katika Uislamu atapata ujira wake na ujira wa atakayetenda wema huo." [Muslim]

 

 

Share

55-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, inamtosheleza mtu kuwa ajichunge na kujilinda dhidi ya maasi peke yake tu?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

55-Je, inamtosheleza mtu kuwa ajichunge na kujilinda dhidi ya maasi peke yake tu?  

 

Hapana! Bali inamapsa ajichunge na ajilinde nafsi yake na pia familia yake.

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَاراً

Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na moto)) [At-Tahriym: 6]

 

((إِنَّ اللهَ سَائِلٌ كُلَّ رَاعٍ عَمَّا اسْتَرْعَاهُ، أَحَفِظَ أَمْ ضَيَّعَه)) حسن رواه النسائي

((Hakika Allaah Atamuuliza kila mchungaji kile alichokichunga kama alikilinda au alikiacha kikapotea)) [Hadiyth Hasan – An-Nasaaiy]

 

 

Share

56-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Lini watapata nusra Waumini?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

56-Lini watapata nusra Waumini?

 

Waumini watapata nusura pale watakapofuata Kitabu cha Rabb wao na Sunnah za Nabiy wao.

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّـهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ﴿٧﴾

Enyi mloamini! Mkisaidia kunusuru Dini ya Allaah, (Allaah) Atakunusuruni na Ataithibitisha miguu yenu. [Muhammad: 7]

 

((لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي مَنْصُورِينَ)) صحيح رواه ابن ماجه

((Litabakie kundi miongoni mwa Umma wangu kuwa ni lenye kunusuriwa)) [Hadiyth Swahiyh Ibn Maajah]

 

 

 

Share

57-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nani watu bora kabisa baada ya Rusuli?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

57-Nani watu bora kabisa baada ya Rusuli?

 

 

Watu bora kabisa baada ya Rusuli, ni Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٠٠﴾

Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhajirina na Answaar na wale waliowafuata kwa ihsaan; Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye)) [At-Tawbah: 110]

 

((خَيْرُ النَّاسِ قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ)) متَّفق عليه

((Watu bora kabisa ni karne yangu, kisha wanaowafuatia kisha wanawafuatia)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

Share

58-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Wepi ni Maswahaba bora kabisa?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

58-Wepi ni Maswahaba bora kabisa?

 

Maswahaba bora kabisa ni Makhulafaa Ar-Raashiduwn nao ni: Abuu Bakr, kisha ‘Umar, kisha ‘Uthmaan, kisha ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhum)

 

إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّـهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا ۖ

Msipomnusuru (Rasuli), basi Allaah Amekwishamnusuru, pale walipomtoa (Makkah) wale waliokufuru akiwa wa pili katika wawili; walipokuwa katika pango, alipomwambia swahibu yake: ““Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.”[At-Tawbah: 40]

 

((فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الْمَهْدِيِّينَ الرَّاشِدِينَ، تَمَسَّكُوا بِهَا وَعَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ)) رواه أبو داوود والترمذي وقال حديث حسن صحيح

((Kwa hiyo, shikamaneni na mwenendo wangu na mwenendo wa Makhalifa waongofu, yashikilieni na yakamateni barabara kwa magego)) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Share

59-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini hukmu ya anayesema kuwa Qur-aan imepotoshwa?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

59-Nini hukmu ya anayesema kuwa Qur-aan imepotoshwa?

 

Anayesema kuwa Qur-aan impotoshwa ni kafiri.

 

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾

Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka ndio Wenye kuihifadhi. [Al-Hijr: 9]

 

((وَأَنْزَلْتُ عَلَيْكَ كِتَابًا لاَ يَغْسِلُهُ الْمَاءُ تَقْرَؤُهُ نَائِمًا وَيَقْظَانَ)) مسلم - كتاب الجنة وصفة نعيمها وأهلها

((Na Nimekuturemshia Kitabu ambacho hakioshelewi mbali na maji ili ukisome katika hali ya kulala na kuwa macho)) [Muslim – Kitabu cha Jannah, wasifu wake, neema zake na watu wake]

 

 

 

Share

60-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Nabiy ‘Iysaa atateremka duniani kuwa ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

60-Je, Nabiy ‘Iysaa atateremka duniani kuwa ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah?

 

Naam! Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam) atateremka kutoka mbinguni kuja duniani kama ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah.

 

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا﴿١٥٩﴾

Na hakuna yeyote katika Ahlil-Kitaabi ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao [An-Nisaa: 159]

 

((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمْ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا)) 

((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, hivi karibuni atateremka kwenu mwana wa Maryam ('Iysaa) akiwa ni kiongozi muadilifu)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share