Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 

Zimekusanywa Na:  Alhidaaya.com

 

 

 

 

Share

000-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Utangulizi

 

 

 Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Utangulizi

 

Utangulizi

 

Alhidaaya.com

 

 

Zifuatazo ni du’aa zilothibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ni busara kushikilia kusoma du’aa za Sunnah na kuacha nyinginezo zisizothibiti, kwani hizi za Sunnah ni nyingi mno zinazomtosheleza Muislamu kupata manufaa ya dunia na Aakhirah yake. Aghlabu ya du’aa za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  zilikuwa ni za mukhtasari lakini ni zenye hikma na maana nzito. Amesema katika usimulizi ufuatao:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ:  ((فُضِّلْتُ عَلَى الأَنْبِيَاءِ بِسِتٍّ:  أُعْطِيتُ جَوَامِعَ الْكَلِمِ، وَنُصِرْتُ بِالرُّعْبِ، وَأُحِلَّتْ لِيَ الْغَنَائِمُ، وَجُعِلَتْ لِيَ الأَرْضُ طَهُورًا وَمَسْجِدًا، وَأُرْسِلْتُ إِلَى الْخَلْقِ كَافَّةً، وَخُتِمَ بِيَ النَّبِيُّونَ))

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraryah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Nimefadhilishwa juu ya Manabii kwa mambo sita; nimepewa ‘Jawaami’al-Kalimi’  na nimenusuriwa kwa [kutiwa] hofu [katika nyoyo za maadui] na nimehalalishiwa ghanima  na nimefanyiwa ardhi kuwa kitoharishi na masjid [mahali pa kuswali], na nimetumwa kwa viumbe wote, na Manabii wamekhitimishwa kwangu))[Muslim]

 

‘Jawaami’al-Kalimi’: Mjumuisho wa maana nyingi katika maneno machache

 

Ghanima:  Mali inayopatikana baada ya kupigana katika vita.

 

 

 

 

 

Share

001-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Mema Ya Duniani Na Aakhirah Na Kinga Ya Adhabu Ya Moto

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Mema Ya Duniani Na Aakhirah Na Kinga Ya Adhabu Ya Moto

 

 

 

Alhidaaya.com

 

Hii ni miongoni mwa du'aa alizokuwa akiomba sana Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

  رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الأَخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ

Rabbaana aatinaa fid-dduniya hasanatan wafil Aakhirati hasanatan wa qinaa adhaaban-naari

 

Rabb wetu, tupe katika dunia mema na katika Akhera mema na Tukinge adhabu ya moto [Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu kwamba ilikuwa miongoni mwa du'aa alizokithirisha kuziomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Faida:  Du’aa hii ni ambayo imejumuisha maana nyingi ndani yake kwa kuwa imehusisha kuomba mema ya dunia na Aakhirah.   Na Du’aa hii inapatikana pia ndani ya Qur-aan Suwratul Baqarah (2: 201]

 

 

 

Share

002-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuthibitika Moyo Katika Dini

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kuthibitika Moyo Katika Dini

 

Alhidaaya.com

 

Du’aa Alizokuwa Akiomba Sana Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

 

 

يَا مُقَلِّبَ الْقُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِك

Yaa muqallibal quluwbi, thabbit qalbiy ‘alaa Diynika

Ee Mwenye kupindua nyoyo, Thibitisha moyo wangu katika Dini Yako [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad, Al-Haakim  na Taz Swahiyh Al-Jaami’ 7987]

 

 

 

 

 

Share

003-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kuelekezwa Moyo Katika Utiifu

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kuelekezwa Moyo Katika Utiifu

 

Alhidaaya.com

 

 

Du’aa Alizokuwa Akiomba Sana Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

 

  اللَّهُمَّ مُصَرِّفَ الْقُلُوبِ صَرِّفْ قُلُوبَنَا عَلَى طَاعَتِكَ

Allaahumma Muswarrifal quluwbi, swarrif quluwbanaa ‘alaa twaa’atika

Ee Allaah, Mwenye kuelekeza nyoyo, zielekeze nyoyo zetu katika utiifu Wako [Muslim]

 

 

 

Share

004-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Sayyid Al-Istighfaar: Du'aa Kubwa Kabisa Ya Kuomba Maghfirah Kuliko Zote

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 Sayyid Al-Istighfaar  Du'aa Kubwa Kabisa Ya Kuomba Maghfirah Kuliko Zote

 

Alhidaaya.com

 

 

 اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ

 

Allaahumma Rabbiy laa ilaaha illa Anta Khalaqtaniy wa-ana ‘abduka wa-anaa ‘alaa ‘ahdika wawa’dika mastatwa’tu, a’uwdhu bika minsharri maa swana’tu, abuu laka bini’matika ‘alayya waabuu bidhambiy, faghfirliy fainnahu laa yaghfirudh dhunuwba illaa Anta

 

Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana Muabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba nami ni mja Wako, nami niko juu ya  ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najikinga Kwako dhidi ya shari ya nilichokifanya, nakiri  Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unighufurie kwani hakuna anayeghufuria  madhambi ila Wewe  [Al-Bukhaariy, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad - Sayyidul-Istighfaar - Du’aa kuu ya kuomba Maghfirah. Atakayesema jioni akafariki ataingia Jannah, atakayesema asubuhi akafariki ataingia Jannah.

 

 

 

Share

005-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Du’aa Makhsusi Ya Laylatul-Qadr- Kuomba Al-'Afw (Msamaha)

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Du’aa Khasa Ya Laylatul-Qadr Kuomba Al-'Afw (Msamaha)

 

Alhidaaya.com

 

 اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي

Allaahumma Innaka ‘Afuwwun Tuhibbul-‘afwa fa’fu ‘anniy

 

Ee Allaah, hakika Wewe Mwingi wa kusamehe Unapenda kusamehe basi nisamehe.

[At-Tirmidhiy, Ahmad, Ibn Maajah, na Swahiyh At-Tirmidhiy (3/170)]

 

Pia kumwita Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Majina Yake Mazuri Yanayohusiana na kuomba msamaha na maghfirah. Unamwita Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Majina hayo kwa wingi bila ya kuwekea idadi maalumu au kuambatanisha na kitendo maalumu.

 

يــــــَــــاعَفُـــــــــــــوُّ   يَاغَفـــُــــــورُ

Yaa ‘Afuwwu Yaa Ghafuwru.

Ee Mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Kughufuria.

 

 

Share

006-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Maghfirah Na Rahmah Kutokana Na Kujidhulumu Nafsi

 

 

 Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم

 

Kuomba Maghfirah Na Rahmah Kutokana Na Kujidhulumu Nafsi

 

  Alhidaaya.com

 

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي ظُلْمًا كَثِيرًا وَلاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ فَاغْفِرْ لِي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ وَارْحَمْنِي إِنَّك أَنْتَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ

Allaahumma inniy dhwalamtu nafsiy dhwulman kathiyraw-walaa yaghfirudh-dhunuwba illa Anta faghfirliy maghfiratam-min ‘indika warhamniy innaka Antal-Ghafuwrur-Rahiym

 

Ee Allaah, hakika nimedhulumu nafsi yangu dhuluma nyingi wala hakuna wa kughufuria madhambi isipokuwa Wewe, basi Nighufurie maghfirah kutoka Kwako na Nirehemu, hakika Wewe ni Mwingi wa Kughufuria Mwenye Kurehemu daima [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad]

 

 

Share

007-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Maghfirah Na Tawbah

 

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Maghfirah Na Tawbah

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

اللَّهُمَّ أغْفِرْ لِي وَتُبْ عَلَيَّ إِنَّكَ أَنْتَ ألتَّوَابُ  الْغَفُورُ

Allaahumma-ghfirliy watub ‘alayya innaka Antat-Tawwaabul-Ghafuwr

Ee Allaah nighufurie na nipokelee tawbah yangu, hakika Wewe ni Mwingi wa Kupokea Tawba,  Mwingi wa Kughufuria [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah Taz Majma’ Az-Zawaaid (10/113)]

 

 

 

 

 

Share

008-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Maghfirah Na Tawbah Du'aa Ina Jina Tukufu La Allaah Ambalo Likiombwa Huitikiwa

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Maghfirah Na Tawbah Du'aa Ambayo Ina

Jina Tukufu La Allaah Ambalo Likiombwa Huitikiwa

 

 Alhidaaya.com

 

 

إِنِّي أَسْأَلُكَ يَا أَللَّهُ بِأَنَّكَ الْوَاحِدُ الاَحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أَحَدٌ أَنْ تَغْفِرَ لِي ذُنُوبِي إِنَّكَ أَنْتَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ

Allaahumma inniy as-aluka yaa Allaah, biannakal-Waahidusw-Swamadu ALladhiy lam yalid walam yuwlad walam yakullahu kufuwan ahad, an-Taghfiraliy dhunuwbiy innaka Antal-Ghafuwrur-Rahiym

Ee Allaah, hakika nakuomba ee Allaah kwamba hakika Wewe ni Mmoja Pekee Mtegemewa kwa haja zote, Hakuzaa wala Hakuzaliwa wala Hana anayefanana Naye hata mmoja, Unighufurie madhambi yangu, hakika Wewe ni Mwingi wa Kughufuria Mwenye Kurehemu daima.

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, kwa yakini Ameomba kwa Jina Lake Tukufu kabisa ambalo Anapoombwa kwalo [du’aa] Anaitikia na Anapotakwa kwalo [jambo] Hutoa)) [Hadiyth ya Buraydah bin Al-Haswiyb Al-Aslamiyy  kutoka kwa baba yake Radhwiya Allaahu ‘anhumaa – Swahiyh Ibn Maajah (3125) Swahiyh At-Tirmidhy  (3475), Swahiyh Abi Daawuwd (1493), Swahiyh At-Targhiyb  (1640)]

 

Share

009-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kutakaswa Madhambi Kama Inavyotakaswa Nguo Nyeupe Kutokana Na Uchafu

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba -Kutakaswa Madhambi Na Makosa Kama Inavyotakaswa

Nguo Nyeupe Kutokana Na Uchafu

 

 Alhidaaya.com

 

 

 اللَّهُمَّ طَهِّرْنِي مِنَ الذُّنُوبِ وَالْخَطَايَا، اللَّهُمَّ نَقِّنِي مِنْهَا كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الْأَبْيَضُ مِنَ الدَّنَسِ، اللَّهُمَّ طَهِّرْنِي بِالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ وَالْمَاءِ الْبَارِدِ

Allaahumma Twahhirniy minadh-dhunuwbi wal khatwaayaa, Allaahumma naqqiniy minhaa kamaa yunaqqath-thawabul-abyadhwu minad-ddanasi, Allaahumma Twahhirniy bith-thalji walbaradi walmaail-baridi

Ee Allaah, Nitakase madhambi na makosa. Ee Allaah, nitakase dhidi ya hayo kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu. Ee Allaah, nitwaharishe kwa theluji, na barafu na maji ya baridi [At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy]

 

Share

010-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Maghfirah, Hidaayah, Rizki, Msamaha, Dhiki Ya Kisimamo Cha Aakhirah

 (صلى الله عليه وآله وسلم) Du’aa Za Nabiy

 

Kuomba Maghfirah, Hidaayah, Rizki, Msamaha,

Dhiki Ya Kisimamo Cha Aakhirah

 

 Alhidaaya.com

 

 

  اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي، وَاهْدِنِي، وَارْزُقْنِي، وَعَافِنِي ، أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنْ ضِيقِ الْمَقَامِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ

Allaahumma-ghfirliy wahdiniy, warzuqniy, wa ‘aafiniy, a’uwdhu biLLaahi min dhwiyqil-maqaami Yawmal-Qiyaamah

 

Ee Allaah, nighufurie, nihidi, niruzuku, nisamehe, najikinga kwa Allaah dhidi ya dhiki ya kisimamo Siku ya Qiyaamah [Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah. -  Swahiyh An-Nasaaiy (1/356), Swahiyh Ibn Maajah (1/226)]

 

 

 

Share

011-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Maghfirah, Rahmah, Hidaaya, Kuungwa, Afya, Rizki, Kupandishwa Daraja

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Maghfirah, Rahmah, Hidaaya, Kuungwa,

Afya, Rizki, Kunyayuliwa Daraja

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللّهُـمَّ اغْفِـرْ لي، وَارْحَمْـني، وَاهْدِنـي، وَاجْبُرْنـي، وَعافِنـي وَارْزُقْنـي وَارْفَعْـني

Allaahummagh-fir-liy warhamniy, wahdiniy, wajburniy, wa ‘aafiniy, warzuqniy, warfa’-niy

 

Ee Allaah, nighufurie, na nirehemu, na nihidi na niunge kunitengenezea niliyoharamika nayo, na nipe afya, na niruzuku, na nipandishe [daraja].

 

[Aswhaabus-Sunan isipokuwa An-Nasaaiy. Nyiradi katika kikao baina ya Sajdah mbili]

 

 

Share

012-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Maghfirah, Kupanuliwa Neema Katika Nyumba, Kubarikiwa Katika Rizki

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Maghfirah, Kupanuliwa Neema Katika Nyumba,

Kubarikiwa Katika Rizki

 

 Alhidaaya.com

 

 

‏اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي، وَوَسِّعْ لِي فِي دَارِي، وَبَارِكْ لِي فِيمَا رَزَقْتَنِي

Allaahummagh-fir-liy dhambiy, wa wassi’ liy fiy daariy, wa Baarik liy fiymaa razaqtaniy

 

Ee Allaah nighufurie dhambi zangu, na nipanulie katika nyumba yangu, na nibarikie katika Uliyoniruzuku. [At-Tirmidhiy, Ahmad - Swahiyh Al-Jaami’ (1265) - Zaad-al-Ma’aad (2/354)]

 

 

Share

013-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Shari Ya Nafsi, Kuthibitika, Maghfirah Ya Dhambi Za Kila Aina

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Shari Ya Nafsi, Kuthibitika Katika Hidaaya,

Maghfirah Ya Dhambi Za Kila Aina

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ قِنِي شَرَّ نَفْسِي، وَاعْزِمْ لِي عَلَى أَرْشَدِ أَمْرِي، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي مَا أَسْرَرْتُ، وَمَا أَعْلَنْتُ، وَمَا أَخْطَأْتُ، وَمَا عَمَدْتُ، وَمَا عَلِمْتُ، وَمَا جَهِلْتُ

Allaahumma qiniy sharra nafsiy, wa a’-zim-liy ‘alaa arshadi amriy, Allaahummagh-fir-liy maa asrartu, wamaa a’-lantu, wamaa akh-twa-atu, wamaa ‘amadtu, wamaa ‘alimtu, wamaa jahiltu

 

Ee Allaah Nikinge shari ya nafsi yangu, na Nithibitishe katika uongofu bora kabisa wa mambo yangu, Ee Allaah, nighufurie niliyoyafanya kwa siri, na niliyoyafanya kwa dhahiri na niliyoyakosea, na niliyoyatenda kwa makusudi, na niliyoyafanya kwa kujua na niliyofanya kwa kutokujua. [Ahmad. Al-Haakim Adh-Dhahabiy amekubali na kuipa daraja ya Swahiyh. Tazama pia Majma’ Zawaaid (10/184)]

 

 

Share

014-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuhesabiwa Hesabu Nyepesi Siku Ya Qiyaamah

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kuhesabiwa Hesabu Nyepesi Siku Ya Qiyaamah

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ حَاسِبْنِي حِسَابًا يَسِيرًا

Allaahumma haasibniy hisaaban -yasiyraa

 

Ee Allaah nihesabie hisabu iliyo nyepesi  

 

Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) alimuuliza Rasuli wa Allaah (سبحانه وتعالى) alipomaliza kuisoma du’aa katika Swalaah: “Ipi hesabu iliyo nyepesi?” Akasema: ((Kwamba [Allaah] Atatazama kitabu chake [kilichorekodiwa ‘amali] kisha Amsamehe kwani hakika mwenye kuhojiwa hesabu siku hiyo ee ‘Aaishah ameangamia, na kila kinachomsibu Muumini Allaah عز وجل  Humfutia ([dhambi] japo ikiwa ni mwiba umchomao)) [Imaam Ahmad]

 

 

Share

015-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Kumshirikisha Allaah Ukiwa Unajua Na Kuomba Maghfirah Kwa Usiyoyajua

 Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kinga Ya Kumshirikisha Allaah Hali Ukijua Na Kuomba Maghfirah Kwa Usiyoyajua

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أُشْرِكَ بِكَ وَأَنَا أَعْلَمُ، وَأَسْتَغْفِرُكَ لِمَا لاَ أَعْلَمُ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika an-ushrika bika wa anaa a-’lamu, wa astaghfiruka limaa laa a’lamu

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kukushirikisha na hali najua, na nakuomba maghfirah kwa nisiyoyajua

[Ahmad - Swahiyh At-Targhiyb Wat-Tarhiyb (1/19)]

 

 

Share

016-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Jannah Na Kuepushwa Na Moto, Du'aa Yenye Jina Tukufu La Allaah

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 Kuomba Jannah Na Kuepushwa Na Moto

 

Du'aa Yenye Jina Tukufu La Allaah Ambalo Ukiomba Utakabaliwa

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ بِأَنَّ لَكَ الْحَمْدَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ وَحْدَكَ لاَ شَرِيكَ لَكَ الْمَنَّانُ يَا بَدِيعَ السَّمَوَاتِ وَالأرْضِ يَا ذَا الْجَلالِ وَالإكْرَامِ يَا حَيُّ يَا قَيُّومُ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ النَّارِ

 

Allaahumma inniy as-aluka bianna lakal-hamdu laa ilaaha illa Anta Wahdaka laa shariyka Laka, Al-Mannaanu  yaa  Badiy-’as-samaawati wal-ardhwi, yaa dhal-Jalaali wal-ikraami, yaa Hayyu yaa Qayyuwmu, inniy as-alukal-Jannata wa a’uwdhu bika minan-naari

 

Ee Allaah, nakuomba, hakika kuhimidiwa ni Kwako hapana muabudiwa wa haki ila Wewe, Peke Yako Huna mshirika, Mwenye Fadhila. Ee Mwanzishi wa mbingu na ardhi ee Mwenye Utukufu na Ukarimu, ee Aliye Hai [daima], ee Msimamizi wa yote, hakika mimi nakuomba Jannah na najikinga kwako na moto.

 

Du’aa hii tukufu ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo amesema: baada ya mtu kuomba du’aa hii:

 

“Kwa yakini amemuomba Allaah kwa Jina Lake Tukufu Ambalo Anapoombwa kwalo Anaitikia na Anapotakwa kwalo jambo hutoa:

 

[Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhiywa Allaahu ‘anhu) - Abuu Daawuwd [1495], An-Nasaaiy (3/52), Ibn Maajah [3858] na taz. Swahiyh Ibn Maajah (2/329)]

 

 

Share

017-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Jannah Na Kuepushwa Na Moto Mara Tatu Asubuhi Na Jioni

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Jannah Na Kuepushwa Na Moto Mara Tatu Asubuhi Na Jioni

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَأَسْتَجِيرُ بِكَ مِنَ النَّارِ (ثلاث مرات)

Allaahumma inniy as-alukal-Jannata wa astajiyru bika minan-naari [mara 3]

 

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba Jannah na najikinga Kwako dhidi ya Moto

 

Inapaswa kusomwa katika Swalaah baada ya Tashahhud kabla ya kutoa salaam.

[At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah – Swahiyh At-Tirmidhiy (2/319) na lafdhi yake ((Atakayemwomba Allaah Jannah mara tatu [asubuhi na jioni], Jannah itasema: Ee Allaah muingize Jannah, na atakayejilinda kwa Allaah na Moto mara tatu, Moto utasema: Ee Allaah mlinde na Moto))  

 

 

 

Share

019-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Adhabu Ya Moto Kaburi, Shari Za Utajiri Na Umasikini, Fitnah Za Masiyh Ad-Dajjaal

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kinga Ya Fitnah Na Adhabu Za Moto, Kaburi, Shari Za Utajiri Na Umasikini, Masiyh Ad-Dajjaal, Kutakaswa Na Madhambi

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ النَّارِ وَعَذَابِ النَّارِ وَفِتْنَةِ الْقَبْرِ وَعَذَابِ الْقَبْرِ وَشَرِّ فِتْنَةِ الْغِنَى وَشَرِّ فِتْنَةِ الْفَقْرِ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ فِتْنَةِ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ. اللَّهُمَّ اغْسِلْ قَلْبِي بِمَاءِ الثَّلْجِ وَالْبَرَدِ وَنَقِّ قَلْبِي مِنْ الْخَطَايَا كَمَا نَقَّيْتَ الثَّوْبَ الأَبْيَضَ مِنْ الدَّنَسِ. وَبَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْكَسَلِ وَالْمَأْثَمِ وَالْمَغْرَمِ.

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min fitnatin-naari wa ‘adhaabin-naari wa fitnatil-qabri, wa adhaabil-qabri, wa sharri fitnatil-ghinaa, wa sharri fitnatil-faqri. Allaahumma inniy a’uwdhu bika min sharri fitnatil-Masiyhid-dajjaal. Allaahummagh-sil qalbiy bimaaith-thalji walbaradi, wanaqqi qalbiy minal-khatwaayaa kamaa naqqaytath-thawbal-abyadhw minad-ddanasi, wa baa’id bayniy wa bayna khatwaayaaya kamaa baa’adta baynal-Mashriqi wal-Maghribi. Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-kasli wal-maa-thami wal-maghrami.

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako fitna za Moto na adhabu za Moto, na fitna za kaburi, na adhabu za kaburi, na shari za fitna za utajiri, na shari za fitna za ufakiri. Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako shari za fitna za Masiyh Ad-Dajjaal. Ee Allaah, Osha moyo wangu kwa theluji na barafu na Takasa moyo wangu madhambi kama Ulivyotakasa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na niweke mbali baina yangu na baina ya madhambi kama Ulivyoweka mbali baina ya Mashariki na Magharibi. Ee Allaah, hakika najikinga Kwako uvivu na madhambi na deni.

 

[Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

020-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kheri Alizoziomba Nabiy Na Shari Alizojikinga Nazo, Kuomba ...

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kheri, Kuomba Kinga Za Shari, Kheri Alizoziomba Nabiy Na Shari Alizojikinga Nazo Nabiy, Kuomba Yanayokaribisha Jannah Na Kujikinga Na Yanayokaribisha Na Moto

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

  ‏ اللَّهُمَّ إِني أسْأَلُكَ مِنْ الْخَيْرِ كُلِّهِ عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أعْلَمْ، وَأعُوذُ بِكَ مِنَ الشَّرِّ كُلِّهِ عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ ‏‏ أعْلَمْ،  اللَّهُمَّ إِنِّي أسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ مَا سَألَكَ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، وَأعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا استعَاذَ  بِكَ مَنْهُ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَمَا قَرَّبَ إلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أوْ عَمَلٍ وَأعُوذُ بِكَ مِنْ النَّارِ وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أوْ عَمَلٍ، وَأسْأَلُكَ أنْ تَجْعَلَ كُلَّ قَضَاءٍ قَضَيْتَهُ لِي خَيْرًا

 

Allaahumma inniy as-aluka minal-khayri kullihi ‘aajilihi wa aajilihi, maa ‘alimtu minhu wamaa lam a’lam. Wa a’uwdhu Bika min sharri kullihi ‘aajilihi wa aajilihi maa ‘alimtu minhu wamaa lam a’lam. Allaahumma inniy as-aluka min khayri maa saalaka ‘Abduka wa Nabiyyuka, wa a’uwdhu Bika min sharri masta’aadha Bika minhu ‘Abduka wa Nabiyyuka. Allaahumma inniy as-alukal-Jannata wamaa qarraba ilayhaa min qawlin aw ‘amal, wa a’uwdhu Bika minan-nnaari wamaa qarraba ilayhaa min qawlin aw ‘amal, wa as-aluka antaj-’ala kulla qadhwaai qadhwaytahu liy khayraa

 

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kheri zote zilizokaribu na mbali nizijuazo na nisizozijua. Najikinga Kwako shari zote za karibu na za mbali nizijuazo na nisizozijua. Ee Allaah, hakika nakuomba kheri alizokuomba mja Wako na Nabiy Wako, na najikinga Kwako shari alizojikinga nazo mja Wako na Nabiy wako. Ee Allaah, hakiki mimi nakuomba Jannah na yanayokaribisha kwayo katika kauli au amali, na najikinga Kwako Moto na yanayokaribisha kwayo katika kauli au amali, na nakuomba Ujaalie kila majaaliwa yangu [uliyonikidhia] yawe kheri

 

[Ibn Maajah – Ametaja katika mlango aliosimulia Hadiyth kwa anuani ya ‘Du’aa za  ‘Jawaami’ul-Kalimi’]

 

 

Share

021-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Hidaaya, Taqwa, Sitaha Na Kutosheka

 

 Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Hidaaya, Taqwa, Sitaha Na Kutosheka

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

‏ اللَّهُمَّ إِنِّي أسْألُكَ الْهُدَى وَالتُّقَى وَالْعَفَافَ وَالْغِنَى

Allaahumma inniy as-alukal-hudaa wat -ttuqaa wal ‘afaafa wal ghinaa

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba hidaaya na taqwa na sitaha (kujichunga) na kutosheka

 

[Muslim]

 

 

 

Share

022-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Hidaaya, Kunyooka Sawasawa Na Unyofu

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 

Kuomba Hidaaya Na Kunyooka Sawasawa Na Kuomba Hidaaya Na Unyofu

 

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

   اللَّهُمَّ اهْدِنِي وَسَدِّدْنِي، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْهُدَى وَالسَّدَادَ   

 

Allaahumma-hdiniy wasaddid-niy، Allaahumma inniy as-alukal-hudaa was-ssadaad

 

Ee Allaah, nihidi na nionyoshe sawasawa. Ee Allaah hakika mimi nakuomba hidaaya na unyofu

 

[Muslim]

 

Share

023-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Iymaan Isiyobadilika, Neema Zisizoisha, Kukaribiana Na Nabiy Janna

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 

Kuomba Iymaan Isiyobadilika, Neema Zisizoisha, Kukaribiana Na Nabiy Jannah

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

  اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ إِيمَانًا لاَ يَرْتَدُّ، وَنَعِيمًا لاَ يَنْفَدُ، وَمُرَافَقَةَ النَّبِيِّ  صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي أَعْلَى غُرَفِ الْجَنَّةِ جَنَّاتِ الْخُلْدِ

 

Allaahumma inniy as-aluka iymaanan laa yartaddu, wa na’iyman laa yanfaddu, wa muraafqatan-Nabiyyi Swalla-Allaahu ‘alayhi wa sallam fiy a’-laa ghurafil-Jannah, Jannaatil-khuldi

 

Ee Allaah, hakika nakuomba iymaan isiyobadilika, na neema zisizoisha na kukaribiana na Nabiy Swalla-Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam katika vyumba vya ghorofa za juu kabisa Jannah, Jannah ambazo ni za kudumu milele.

 

[Ahmad, na Ibn Hibbaan kwa njia nyingine. - As-Silsilah Asw-Swahiyhah (5/379)]

 

 

 

 

Share

024-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kusaidiwa Kumdhukuru Na Kumshukuru Allaah Na Kumwabudu Vizuri

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kusaidiwa Kumdhukuru Na Kumshukuru Allaah Na Kumuabudu Vizuri

 

 Alhidaaya.com

 

 

 اللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ وَشُكْرِكَ وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ

  

Allaahumma a’inniy ‘alaa dhikrika,  wa shukrika wa husni ‘ibaadatika

 

Ee Allaah nisaidie juu Kukudhukuru, na kukushukuru na kukuabudu kwa uzuri utakikanao

 

[Abuu Daawuwd, Ahmad na kwa usimilizi tofauti kidogo kutoka kwa An-Nasaaiy. Wasia wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliompa ‘Mu’aadh bin Jabal (رضي الله عنه)  aombe du’aa hii kila baada ya Swalaah].

 

 

Share

025-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Khofu Inayotenganisha Baina Maasi Na Utiifu Utakaofikisha Jannah...

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Khofu Inayotenganisha Baina Maasi

Na Kuomba Utiifu Utakaofikisha Jannah....

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ اقْسِمْ لَنَا مِنْ خَشْيَتِكَ مَا يَحُولُ بَيْنَنَا وَبَيْنَ مَعَاصِيكَ، وَمِنْ طَاعَتِكَ مَا ‏ ‏تُبَلِّغُنَا ‏بِهِ جَنَّتَكَ، وَمِنْ الْيَقِينِ مَا تُهَوِّنُ بِهِ عَلَيْنَا مُصِيبَاتِ الدُّنْيَا، وَمَتِّعْنَا بِأسْمَاعِنَا وَأبْصَارِنَا وَقُوَّتِنَا مَا أحْيَيْتَنَا، وَاجْعَلْهُ  ‏الْوَارِثَ مِنَّا، وَاجْعَلْ ثَأرَنَا عَلَى مَنْ ظَلَمَنَا وَانْصُرْنَا عَلَى مَنْ عَادَانَا، ولا تَجْعَلْ مُصِيبَتَنَا فِي دِينِنَا، وَلا تَجْعَلْ الدُّنْيَا أكْبَرَ هَمِّنَا وَلا مَبْلَغَ عِلْمِنَا، وَلا تُسَلِّطْ عَلَيْنَا مَنْ لا يَرْحَمُنَا

 

Allaahumma-qsim-lanaa min khash-yatika maa yahuwlu baynanaa wa bayna ma’aaswiyk, wamin twaa’atika maa tuballighunaa bihi Jannatak, wa minal-yaqiyni maa tuhawwinu bihi ‘alaynaa muswiybaatid-duniya, wa matti’-naa biasmaa’inaa wa abswaarinaa wa quwwaatinaa maa ahyaytanaa waj-’alhul-waaritha minnaa waj-’al tha-aranaa ‘alaa man dhwalamanaa wanswurnaa ‘alaa man ‘aadaana, walaa taj-’al muswiybatanaa fiy diyninaa, walaa taj-’alidduniya akbara hamminaa walaa mablagha ‘ilminaa, walaa tusallitw ‘alaynaa man-llaa yarhamunaa

 

Ee Allaah tugawanyie sisi khofu Yako itakayotenganisha baina yetu na baina ya maasi Yako, na  utiifu utakaotufikisha katika Jannah Yako na yaqini itakayotusahilishia misiba ya dunia, na tustareheshe kwa masikio yetu, na macho yetu, na nguvu zetu madamu Utatuweka hai, na yajaalie yawe ni urithi wetu na Jaalia iwe lipizo kwa anayetudhulumu, na tunusuru dhidi ya anayetufanyia uadui, na wala Usitufanyie msiba  wetu ni Dini yetu, wala Usifanye dunia kuwa ndio hima yetu kubwa kabisa, na wala upeo wa elimu yetu, wala Usitusaliti kwa asiyetuhurumia.

 

 

[Swahiyh At-Tirmidhiy 3502, Swahiyh Al-Jaami’ 1268]

 

 

Share

026-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Uhai Au Mauti Yakiwa Na Kheri, Kumkhofu Allaah Kisiri Na Dhahiri

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Uhai Au Mauti Yakiwa Na Khayr,

Kumkhofu Allaah Kwa  Siri Na Dhahiri...

 Alhidaaya.com

 

 026-Ee Allaah naomba kwa ujuzi Wako wa ghaibu na uwezo…

 

 

اللَّهُمَّ بِعِلْمِكَ الْغَيْبَ وَقُدْرَتِكَ عَلَى الْخَلْقِ أحْيِنِي مَا عَلِمْتَ الْحَيَاةَ خَيْرًا لِي، وَتَوَفَّنِي إِذَا عَلِمْتَ الْوَفَاةَ خَيْرًا ‏‏ لِي، ‏‏ اللَّهُمَّ إِنِّي أسْأَلُكَ خَشْيَتَكَ فِي الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ، وَأسْأَلُكَ كَلِمَةَ الْحَقِّ فِي الرِّضَا وَالْغَضَبِ، وَأسْأَلُكَ ‏الْقَصْدَ‏ ‏فِي الْغِنَى وَالْفَقْرِ، وَأسْألُكَ نَعِيمًا لا‏ ‏يَنْفَدُ،‏ ‏وَأسْألُكَ قُرَّةَ عَيْنٍ لا تَنْقَطِعُ وَأسْألُكَ الرِّضَاءَ بَعْدَ الْقَضَاءِ، وَأسْألُكَ بَرْدَ الْعَيْشِ بَعْدَ الْمَوْتِ وَأسْألُكَ لَذَّةَ النَّظَرِ ِإِلَى وَجْهِكَ وَالشَّوْقَ إِلَى لِقَائِكَ فِي غَيْرِ ضَرَّاءَ مُضِرَّةٍ وَلا فِتْنَةٍ مُضِلَّةٍ، اللَّهُمَّ ‏‏زَيِّنَّا بِزِينَةِ الإِيمَانِ وَاجْعَلْنَا هُدَاةً مُهْتَدِينَ

 

Allaahumma bi‘ilmikal-ghayba wa qudratika ‘alal-khalqi, ahyiniy maa ‘alimtal-hayaata khayral-liy, wa tawaffaniy idhaa ‘alimtal-wafaata khayral-liy. Allaahumma inniy as-aluka khash-yataka fil-ghaybi wash-shahaadah, wa as-aluka kalimatal-haqqi fir-ridhwaa wal-ghadhwabi, wa as-alukal-qaswda fil-ghinaa wal-faqri, wa as-aluka na’iyman-llaa yanfadu, wa as-aluka qurrata ‘aynin-llaa tanqatwi’u, wa as-alukar-ridhwaa ba’-dal-qadhwaai, wa as-aluka bardal-‘ayshi ba’-dal-mawti,  wa as-aluka laddhatan-nadhwari ilaa Wajhika, wash-shawqa ilaa liqaaika fiy ghayri dhwarraai mudhwirratin walaa fitnatin mudhwillatin. Allaahumma zayyinaa biziynatil-iymaani waj-’alnaa hudaatan muhtadiyna.

 

Ee Allaah naomba kwa ujuzi Wako wa ghaibu na uwezo Wako juu viumbe, nihuishe ikiwa Unajua uhai ni khayr kwangu, na nifishe ikiwa Unajua kufa ni khayr kwangu. Ee Allaah, nakuomba khofu Yako katika siri na dhahiri, na nakuomba Unifanye mkweli katika kauli wakati wa furaha na ghadhabu, na nakuomba unifanye wastani wakati wa utajiri na umasikini, na nakuomba neema isiyokoma, na kitulizo cha macho kisichokatika, na nakuomba niridhike Uliyonikidhia na nakuomba maisha mepesi baada ya mauti, na nakuomba ladha ya kuutazama Wajihi Wako na shauku ya kukutana Nawe, pasi na madhara yanayodhuru au fitna itakayosababisha upotofu. Ee Allaah, tupambie kwa pambo la iymaan na tujaalie wenye kuongoza na kuongoka.

 

[Swahiyh Sunan An-Nasaaiy (1/280/281), Ahmad (4/364) kwa isnaad nzuri]

 

Share

027-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kukithirishwa Mali Na Watoto Na Kubarikiwa

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kukithirishiwa Mali Na Watoto Na Kubarikiwa

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ أَكْثِرْ مَالِي وَوَلَدِي وَبَارِكْ لِي فِيمَا أَعْطَيْتَنِي وَأَطِلْ حَيَاتِي عَلىَ طَاعَتِكَ وَأَحْسِنْ عَمَلِي وَاغْفِرْلِي 

 

Allaahumma akhthir maaliy wa waladiy wa Baarikliy fiymaa a’twaytaniy.  Wa atwil hayaatiy ‘alaa twaa’atika wa ahsin ‘amaliy, waghfir-liy

 

Ee Allaah, ikithirishe mali yangu na watoto wangu, na nibarikie katika Uliyonipa

 

[Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, Ahmad – Du’aa ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله  وسلم ) kwa  Anas (رضي الله عنه) ]

 

Na nipe uhai mrefu niwe katika utiifu Wako, na boresha 'amali zangu na nighufurie

 

[Al-Bukhaariy katika Aadaab Al-Mufrad (653) na ameipa daraja Swahiyh Al-Albaaniy katika Silsilatul-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (2241)]

 

 

Share

028-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Al-'Aafiyaah: Afya, Hifadhi, Amani, Usalama Duniani Na Aakhirah

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Al-'Aafiyaah Duniani Na Aakhirah

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

  اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالأَخِرَةِ

 

Allaahumma inniy as-alukal-‘aafiyata fid-dunyaaa wal-Aakhirah

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba afya duniani na Aakhirah

 

 

[Swahiyh At-Tirmidhiy (3/180, 185, 170)]

 

Al-'Aafiyah : afya, hifadhi ya kila baya, amani, salama n.k.

 

 

Share

029-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Mwisho Mwema, Kuokoka Na Hizaya Duniani Na Adhabu Za Aakhirah

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Mwisho Mwema Na Kuokoka Na Hizaya Duniani Na Adhabu Za Aakhirah

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 أللَّهُمَّ أَحْسِنْ عَاقِبَتَنَا فِي الأًمُورِ كُلِّهَا وَأَجِرْنَا مِنْ خِزْيِ الدُّنْيَا وَعَذَابِ الأَخِرَةِ

 

Allaahumma ahsin ‘aaqibatanaa fil-umuwri kullihaa wa ajirnaa min khizyid-duniya wa adhaabil-Aakhirah

 

Ee Allaah fanya mwema mwisho wetu katika mambo yote, na tuokoe hizaya ya dunia na adhabu za Aakhirah

 

[Ahmad]

 

 

 

Share

030-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kusaidiwa, Kunusuriwa, Kupangiwa, Kumshukuru Na Kumdhukuru Allaah

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kusaidiwa, Kunusuriwa, Kupangiwa,

Kusahilishiwa Hidaaya, Kumshukuru  Na Kumdhukuru Allaah...

 

www.alhidaaya.com

 

 

 رَبِّ أَعِنِّي وَلاَ تُعِنْ عَلَيَّ، وَانْصُرْنِي وَلاَ تَنْصُرْ عَلَيَّ، وَامْكُرْ لِي وَلاَ تَمْكُرْ عَلَيَّ، وَاهْدِنِي وَيَسِّرْ الْهُدَى  إِلَيَّ ، وَانْصُرْنِي عَلَى مَنْ بَغَى عَلَيَّ، رَبِّ اجْعَلْنِي لَكَ شَكَّارًا، لَكَ ذَكَّارًا، لَكَ رَهَّابًا، لَكَ مُطِيعًا، إِلَيْكَ مُخْبِتًا أَوَّاهًا مُنِيبًا، رَبِّ تَقَبَّلْ تَوْبَتِي، وَاغْسِلْ حَوْبَتِي، وَأَجِبْ دَعْوَتِي، وَثَبِّتْ حُجَّتِي،  وَاهْدِ قَلْبِي، وَسَدِّدْ لِسَانِي، وَاسْلُلْ سَخِيمَةَ قَلْبِي  

 

Rabbi a’inniy walaa tu’in ‘alayya, wa-nswurniy walaa tanswur ‘alayya, wamkur-liy walaa tamkur ‘alayya, wahdiniy wa yassiril-hudaa ilayya, wa-nswurniy ‘alaa man baghaa ‘alayya. Rabbij-’alniy Laka shakkaaraa, Laka dhakkaaraa, Laka Rahhaabaa, Laka mutwi’y-aa, ilayka mukhbitan awwaaham-muniybaa. Rabbi taqabbal tawbatiy, waghsil hawbatiy, wa ajib da’-watiy, wa thabbit hujjatiy, wahdi qalbiy, wa saddid lisaaniy, waslul sakhiymata qalbiy.

 

Ee Rabb wangu nisaidie na Usisaidie dhidi yangu, na ninusuru wala Usinusuru dhidi yangu, na nipangie na Usipange dhidi yangu, na niongoze na usahilishe hidaaya kunijia na ninusuru dhidi ya atakayenifanyia uovu. Rabb wangu nijaalie niwe mwenye kukushukuru, mwenye kukudhukuru, mwenye kukuogopa, mwenye kukutii, mwenye kukukhofu, mwenye kunyenyekea na kurudia kuomba tawbah. Rabb wangu pokea tawbah yangu, na osha madhambi yangu, na Itikia du’aa zangu, na thibitisha hoja zangu, na Uhidi moyo wangu, na Nyosha ulimi wangu [useme kweli], na futa uovu wa moyo wangu.

 

[Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah – Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/178) na Ahmad (1/127)]

 

 

Share

031-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Azima Za Rahmah Za Allaah Na Maghfirah, Amani Na Kufuzu Jannah

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Azima Za Rahmah Za Allaah Na Maghfirah, Amani Katika Kila Dhambi Na Kufuzu  Jannah

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مُوجِبَاتِ رَحْمَتِكَ، وَعَزَائِمَ مَغْفِرَتِكَ، وَالسَّلامَةَ مِنْ كُلِّ إِثْمٍ، وَالْغَنِيمَةَ مِنْ كُلِّ بِرّ، وَالْفَوْزَ بِالْجَنَّةِ،  وَالنَّجَاةَ مِنَ النَّاَرِ

 

Allaahumma inniy as-aluka muwjibaati Rahmatik wa 'azaaima maghfiratik was salaamata min kulli ithm, wal ghaniymata minkulli birr, wal fawza bil Jannati, wan najaata minan-naari

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba azima za Rahmah Yako, na azimio la maghfirah Yako, na amani katika kila dhambi, na ghanima katika kila jema, na kufuzu Jannah na kuokoka na Moto.

 

[Al-Haakim (1/525) na ameipa daraja ya Swahiyh na ameiwafiki Adh-Dhahabiy]

 

 

Share

032-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ukunjufu Wa Rizki Katika Uzee Na Kukatika Umri

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Ukunjufu Wa Rizki Katika Uzee Na Kukatika Umri

 Alhidaaya.com

 

 

 

اللَّهُمَّ اجْعَلْ أَوْسَعَ رِزْقِكَ عَلَيَّ عِنْدَ كِبَرِ سِنَّي وَانْقِطَاعِ عُمُرِي

 

Allaahummaj-’al awsa’a rizqika ‘alayya ‘inda kibari sinniy wanqitwaa’i ‘umriy

 

Ee Allaah, Jaalia ukunjufu wa rizki Yako kwangu wakati wa uzee wangu, na kukatika umri wangu

 

[Al-Haakim, Swahiyh Al-Jaami’ (1/396), Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (1539)]

 

 

 

 

Share

033-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Fadhila Na Rahmah Za Allaah

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Fadhila Na Rahmah Za Allaah

 

 Alhidaaya.com

 

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ وَرَحْمَتِكَ  فَإِنَّهُ لاَ يَمْلِكُهاَ إِلاَّ أَنْتَ 

 

Allaahumma inniy as-aluka min-fadhwlika wa Rahmatika fainnahu laa yamlikuhaa illa Anta

 

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kutokana na fadhila Zako na Rahmah Zako, kwani hakuna anayezimiliki ila Wewe

 

[At-Twabaraaniy, Swahiyh Al-Jaami’ (1/404), As-Sisilatul-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (4/57)]

 

 

Share

034-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuunganishwa Nyoyo, Kusuluhishwa, Kuongozwa Njia Ya Amani, Kuokoka Kiza...

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kuunganishwa Nyoyo. Kusuluhishwa, Kuongozwa Njia Ya Amani, Kuokoka Na Kiza Na Kuingia Katika Nuru...

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ أَلِّفْ بَيْنَ قُلُوبِنَا، وَأَصْلِحْ ذَاتَ بَيْنِنَا، وَاهْدِنَا سُبُلَ السَّلاَمِ، وَنَجِّنَا مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّور، وَجَنِّبْنَا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ، وَبَارِكْ لَنَا فِي أَسْمَاعِنَا، وَأَبْصَارِنَا، وَقُلُوبِنَا، وَأَزْوَاجِنَا، وَذُرِّيَّاتِنَا، وَتُبْ عَلَيْنَا إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ، وَاجْعَلْنَا شَاكِرِينَ لِنِعْمَتِكَ مُثْنِينَ بِهَا قَابِلِيهَا وَأَتِمَّهَا عَلَيْنَا

 

Allaahumma allif bayna quluwbinaa, wa aswlih dhaata bayninaa, wahdinaa subulas-ssalaami, wanajjinaa minadhw-dhwulumaati ilan-nnuwri, wa jannibnal-fawaahisha maa dhwahara minhaa wamaa batwan, wa Baarik-lanaa fiy asmaa’inaa, wa abswaarinaa, wa quluwbinaa, wa azwaajinaa, wa dhurriyaatinaa, watub ‘alaynaa innaka Antat-Tawaabur-Rahiym, waj-’alnaa shaakiriyna lini’matika muthniyna bihaa qaabiliyhaa wa atimmahaa ‘alaynaa

 

Ee Allaah! Unganisha baina ya nyoyo zetu, na Suluhisha yaliyo baina yetu, na Tuongoze njia za amani, na Tuokoe kutokana na viza Utuingize katika Nuru, na Tuepushe machafu ya dhahiri na ya siri, na Tubarikie katika kusikia kwetu na kuona kwetu, nyoyo zetu, na wake zetu, na vizazi vyetu, na Tupokelee tawbah zetu, hakika Wewe ni At-Tawwaabur-Rahiym  (Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye Kurehemu), na Tujaalie kuwa wenye kushukuru neema Zako, wenye kuzielezea kwa uzuri, wenye kuzipokea (kwa shukrani), na Zitimize kwetu.

 

[Abuu Daawuwd, Al-Haakim akasema ‘Swahiyh kwa sharti ya Muslim, na ameikubali Adh-Dhahabiy (1/265)]

 

 

Share

035-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Maombi Bora, Duaa, Kufuzu, Amali, Thawabu, Uhai Mauti, Kuthibitishwa...

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Maombi Bora, Du'aa, Kufuzu, Amali, Thawabu,

Uhai, Mauti Bora, Kuthibitishwa, Mizani Nzito...

 

 Alhidaaya.com

 

 

 أللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ خَيْرَ الْمَسْأَلَةِ، وَخَيْرَ الدُّعَاءِ، وَخَيْرَ النَّجَاحِ، وَخَيْرَ الْعَمَلِ، وَخَيْرَ الثَّوَابِ، وَخَيْرَ الْحَيَاةِ، وَخَيْرَ الْمَمَاتِ، وَثَبِّتْنِي، وَثَقِّلْ مَوَازِينِي، وَحَقِّقْ إِيمَانِي، وَارْفَعْ دَرَجَاتِي، وَتَقَبَّلْ صَلاَتِي، وَاغْفِرْ خَطِيئَتِي، وَأَسْأَلُكَ الدَّرَجَاتِ الْعُلَى مِنَ الْجَنَّةِ آمِينْ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ فَوَاتِحَ اْلخَيْرِ، وَخَوَاتِمَهُ، وَجَوَامِعَهُ، وَأَوَّلَهُ، وَآَخِرَهُ،  وَظَاهِرَهُ، وَ بَاطِنَهُ،  وَالدَّرَجَاتِ الْعُلىَ مِنَ الْجَنَّةِ آمِينْ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ خَيْرَ مَا آتِي، وَخَيْرَ مَا أَفْعَلُ، وَخَيْرَ مَا أَعْمَلُ، وَخَيْرَ مَا بَطَنَ، وَخَيْرَ مَا ظَهَرَ، وَالدَّرَجَاتِ الْعُلىَ مِنَ الْجَنَّةِ آمِينْ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ أَنْ تَرْفَعَ ذِكْرِي ، وَتَضَعَ وِزْرِي، وَتُصْلِحَ أَمْرِي، وَتُطَهِّرَ قَلْبِي، وَتُحَصِّنَ فَرْجِي، وَتُنَوِّرَ قَلْبِي ، وَتَغْفِرَ لِي ذَنْبِي، وَاَسْأَلُكَ الدَّرَجَاتِ الْعُلىَ مِنَ الْجَنَّةِ آمِينْ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ أَنْ تُبَارِكَ فَي نَفْسِي، وَفِي سَمْعِي، وَفِي بَصَرِي، وَفِي رُوحِي، وَفِي خَلْقِي، وَفِي خُلُقِي، وَفِي أَهْلِي، وَفِي مَحْيَايَ، وفي مَمَاتِي، وَفِي عَمَلِي، فَتَقَبَّلْ حَسَنَاتِي، وَاَسْأَلُكَ الدَّرَجَاتِ الْعُلىَ مِنَ الْجَنَّةِ آمِينْ.    

 

Allaahumma inniy as-aluka khayral-mas-alah, wa khayrad-du’aai, wa khayran-najaah, wa khayral-‘amali, wa khayrath-thawaabi, wa khayral-hayaati, wa khayral-mamaati, wa thabbitniy, wa thaqqil mawaaziyniy, wa haqqiq iymaaniy, warfa’ darajaatiy, wa taqabbal Swalaatiy, waghfir khatwiy-atiy, wa as-alukad-darajaatil ‘ulaa minal-Jannah. Aamiyn. Allaahumma inniy as-aluka fawaatihal-khayri wa khawaatimahu, wa jawaami’ahu, wa awwalahu, wa- aakhirahu, wa dhwaahirahu, wa baatwinahu, wad-darajaatil ‘ulaa minal-Jannati. Aamiyn. Allaahumma inniy as-aluka khayra maa aatiy, wa khayra maa af-’alu, wa khayra maa a-’malu, wa khayra maa batwana, wa khayra maa dhwahara, wad-darajaatil ‘ulaa minal-Jannati. Aamiyn. Allaahumma inniy as-aluka an Tarfa’a dhikriy, wa tadhwa’a wizriy, wa tuswliha amriy, wa tutwahhira qalbiy, wa tuhaswina farjiy, wa tunawwira qalbiy, wa taghfiraliy dhambiy, wa as-alukad-darajaatil ‘ulaa minal-Jannati. Aamiyn. Allaahumma inniy as-aluka an Tubaarika fiy nafsiy, wafiy sam-’iy, wafiy baswariy, wafiy ruwhiy, wafiy khalqiy, wafiy khuluqiy, wafiy ahliy, wafiy mahyaaya, wafiy mamaatiy, wafiy ‘amaliy, fataqabbal hasanaatiy, wa as-alukaddarajaatil ‘ulaa minal-Jannah. Aamiyn

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba maombi bora kabisa na du’aa bora kabisa, na kufuzu bora kabisa, na ‘amali bora kabisa, thawabu bora kabisa, na uhai bora kabisa, na mauti bora kabisa, na nithibitishe, na fanya nzito Mizani yangu, na thibitisha iymaan yangu, na nyanyua daraja zangu, na Takabali Swalaah zangu, na Ghufuria madhambi yangu, na nakuomba daraja ya juu katika Jannah, Aamiyn. Ee Allaah hakika mimi nakuomba mwanzo mzuri, na khatima nzuri, na ujumla wa uzuri kutoka mwanzo mpaka mwisho wake, na dhahiri yake na undani wake, na daraja za juu katika Jannah, Aamiyn.

Ee Allaah hakika mimi nakuomba mazuri nnayoyaleta, na mazuri niyafanyayo, na mazuri niyatendayo, na mazuri yanayofichika, na mazuri yanayodhihiri, na daraja za juu katika Jannah, Aamiyn.

Ee Allaah hakika mimi nakuomba upandishe utajo wangu na uondoe dhambi zangu, na utengeneze mambo yangu, na utakase moyo wangu, na uhifadhi tupu zangu, na nawirisha moyo wangu, na unighufurie madhambi yangu, na nakuomba daraja za juu katika Jannah, Aamiyn.

Ee Allaah hakika mimi nakuomba unibariki katika nafsi yangu, na kusikia kwangu, na kuona kwangu, na roho yangu, na umbile langu, na tabia  yangu, na katika familia yangu, na katika uhai wangu, na katika mauti yangu, na katika ‘amali zangu, basi nitakabalie mazuri yangu, na nakuomba daraja za juu katika Jannah, Aamiyn.

 

[Ameitoa Al-Haakim kutoka kwa Umm Salamah marfuw’ na ameipa daraja ya Swahiyh na ameikubali Adh-Dhahabiy (1/520)]

 

 

Share

036-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kukinaishwa Ulivyoruzukiwa, Kubarikiwa Na Kubadilishiwa Maovu Kwa Khayr

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kukinaishwa Ulivyoruzukiwa, Kubarikiwa

Na Kubadilishiwa Maovu Kwa Ya Khayr

 

 Alhidaaya.com

 

 

 اللَّهُمَّ قَنِّعْنَي بِمَا رَزَقْتَنَي وَبَارِكْ لِي فِيهِ وَاخْلُفْ عَلَيَّ كُلَّ غَائِبَةٍ لِي بِخَيرٍ

 

Allaahumma qanni-’niy bimaa razaqtaniy, wa Baarikliy fiyhi, wakhluf ‘alayya kulla ghaaibatin-liy bikhayr

 

Ee Allaah, nikinaishe kwa Ulivyoniruzuku, na nibarikie ndani yake, na nibadilishie kila kilichofichika (kiovu) kwa khayr

 

[Al-Haakim na ameipa daraja ya Swahiyh na ameikubali Adh-Dhahabiy (1/510). Ibn Hajar Al-‘Asqalaaniy ameipa daraja ya Hasan katika Al-Futuhaat Ar-Rabbaaniyah (4/384)]

 

 

Share

037-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Maisha Ya Taqwa, Mauti Ya Wastani, Marejeo Kwa Allaah Bila Hizaya

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Maisha Ya Taqwa,  Mauti Ya Wastani, Marejeo Kwa Allaah Bila Hizaya

 

 Alhidaaya.com

 

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ عِيشَةً تَقِيَّةً وَمِيتَةً سَوِيَّةً وَمَرَدًّا غَيْرَ مُخْزٍ

 

Allaahumma inni as-aluka ‘iyshatan taqiyyatan wa miytatan sawiyyatan wa maraddan ghayra mukhzin

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba maisha ya taqwa na mauti ya wastani (yasiyo na madhara) na marejeo [Kwako] bila ya hizaya.

[Musnad Ahmad, Al-Haakim (1/541), Atw-Twabaraaniy katika Al-Mu’jam Al-Awsatw (7/306), kwa isnaad nzuri, na Taz. Majma’u Az-Zawaaid (10/179)].

 

 

Share

038-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kukunjuliwa Baraka, Rahmah, Fadhila, Rizki, Neema Ya Kudumu...

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kukunjuliwa Baraka, Rahmah, Fadhila, Rizki, Neema Ya Kudumu...

 

 Alhidaaya.com

 

 

038- Ee Allaah, Himdi ni Zako zote, Ee Allaah, hakuna mwenye kuzuia…  

 

 اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ كُلُّهُ . اللَّهُمَّ لاَ قَابِضَ لِمَا بَسَطْتَ ، وَلاَ بَاسِطَ لِمَا قَبَضْتَ ، وَلاَ هَادِيَ لِمَا أَضْلَلْتَ، وَلاَ مُضِلَّ لِمَنْ هَدَيْتَ ، وَلاَ مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ ، وَلاَ مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ، وَلاَ مُقَرِّبَ لِمَا بَاعَدْتَ، وَلاَ مُبَاعِدَ لِمَا قَرَّبْتَ. اللَّهُمَّ ابْسُطْ عَلَيْنَا مِنْ بَرَكَاتِكَ ، وَرَحْمَتِكَ، وَفَضْلِكَ، وَرِزْقِكَ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ النَّعِيمَ الْمُقِيمَ الَّذِي لاَ يَحُولُ وَلاَيَزُولُ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ النَّعِيمَ يَوْمَ الْعَيْلَةِ وَالأَمْنَ يَوْمَ الْخَوْفِ. اللَّهُمَّ إِنِّي عَائِذٌ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا أَعْطَيْتَنَا، وَشَرِّ مَا مَنَعْتَ. اللَّهُمَّ حَبِّبْ إِلَيْنَا الإِيمَانَ وَزَيِّنْهُ فِي قُلُوبِنَا وَكَرِّهْ إِلَيْنَا الْكُفْرَ وَالْفُسُوقَ وَالْعِصْيَانَ وَاجْعَلْنَا مِنَ الرَّاشِدِينَ. اللَّهُمَّ تَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ وَأَحْيِنَا مُسْلِمِينَ وَأَلْحِقْنَا بِالصَّالِحِينَ غَيْرَ خَزَايَا وَلاَ مَفْتُونِينَ. اللَّهُمَّ قَاتِلْ الْكَفَرَةَ الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ رُسُلَكَ وَيَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِكَ، وَاجْعَلْ عَلَيْهِمْ رِجْزَكَ وَعَذَابَكَ. اللَّهُمَّ قَاتِلْ الْكَفَرَةَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَهَ الْحَقِّ.

 

Allaahumma lakal-Hamdu kulluhu. Allaahumma laa qaabidhwa limaa basattwa, walaa baaswitwa limaa qabadhwta, walaa haadiya limaa adhw-lalta, walaa mudhwilla liman hadayta, walaa mu’-twiya limaa mana’-ta, walaa maani’a limaa a’-twayta, walaa muqarriba limaa baa’adta, walaa mubaa’idaa limaa qarrabta. Allaahumma absitw ‘alaynaa min Barakaatika, wa Rahmatika, wa fadhwlika, wa rizqika. Allaahumma inniy as-alukan-nna’iymal-muqiyma alladhiy laa yahuwlu walaa yazuwlu. Allaahumma inniy as-alukan-na’iyma yawmal-‘aylati wal amna yawmal-khawfi. Allaahumma inniy ‘aaidhum bika min sharri maa a’-twaytanaa, wa sharri maa mana’-ta. Allaahumma habbib ilaynaal-iymaana wa zayyanahu fiy quluwbina wa karrih ilaynal-kufra wal fusuwqa wal ‘iswyaana waj-‘alnaa minar-raashidiyna. Allaahumma tawaffanaa Muslimiyna wa ahyinaa Muslimiyna wa alhiqnaa bisw-Swaalihiyna ghayra khazaaya walaa maftuwniyna. Allaahumma qaatilil-kafarata alladhiyna yukadh-dhibuwna Rusulaka wa yaswudduwna ‘an Sabiylika, waj-’al ‘alayhim rijzika wa ‘adhaabika. Allaahumma qaatilil-kafarata alladhiyna uwtul-Kitaaba Ilaahal-haqq

 

Ee Allaah, Himdi ni Zako zote. Ee Allaah, hakuna mwenye kuzuia Ulivyovikunjua, wala mwenye kukunjua Ulivyozuia, wala mwenye kumhidi Uliyempotoa, wala kumpotoa  Uliyemhidi, wala mwenye kutoa Ulichokizuia, wala mwenye kuzuia Ulichokitoa, wala mwenye kukurubisha Ulichoweka mbali, wala mwenye kuweka mbali Ulichokiweka karibu. Ee Allaah tukunjulie katika baraka Zako, na Rahmah Zako, na fadhila Zako, na rizki Yako. Ee Allaah hakika mimi nakuomba neema ya kudumu isiyobadilika wala kutoweka. Ee Allaah, hakika mimi nakuomba neema siku ya shida na ufukara,  na amani Siku ya khofu. Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako shari Ulizotupa, na Ulizozizuwia. Ee Allaah, Ee Allaah, Pendezesha kwetu iymaan na Ipambe katika nyoyo zetu, na Chukiza kwetu kufru, ufasiki na uasi, na Tujaalie miongoni mwa waongofu. Ee Allaah, tufishe tukiwa Waislamu na tuhuishe tukiwa Waislamu na tukutanishe na waja wema bila hizaya wala kutahiniwa. Ee Allaah Wapige vita makafiri wanaokanusha Rusuli Wako na wanaozuia njia Yako, na wajaalie juu yao maangamizi Yako na adhabu Zako. Ee Allaah, Wapige vita makafiri waliopewa Kitabu. Ee Mwabudiwa wa haki [Aamiyn]

 

[Ahmad, na Al-Bukhaariy ameitoa katika Al-Adabul-Mufrad (699), na Al-Albaaniy ameipa daraja ya Swahiyh katika Takhriyj Fiqhus-Siyrah (348), Swahiyh Al-Adabil-Mufrad lil-Bukhaariy (538/259), na Majma’u Az-Zawaaid (6/124)].

 

 

Share

039-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuzidishiwa Bila Kupunguziwa, Hadhi Bila Kudunishwa...

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kuzidishiwa Bila Kupunguziwa, Hadhi Bila Kudunishwa...

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ زِدْنَا وَلاَ تَنْقُصْنَا، وَأَكْرِمْنَا وَلاَ تُهِنَّا، وَأَعْطِنَا وَلاَ تَحْرِمْنَا، وَآثِرْنَا وَلاَ تُؤْثِرْ عَلَيْنَا، وَارْضِنَا وَارْضَ عَنَّا

Allaahumma zidnaa walaa tanquswnaa, wa akrimnaa walaa tuhinnaa, wa a’-twinaa walaa tahrimnaa, wa aathirnaa walaa tu-uthir ‘alaynaa, wardhwinaa wardhwa ‘annaa.

 

Ee Allaah Tuzidishie wala usitupunguze, na tajaalie wenye hadhi, usitudunishe,  na tupe wala usitunyime, na tupendelee wala Usipendelee dhidi yetu, na Turidhishe, na Ridhike na sisi.

 

[At-Tirmidhiy, Ahmad Isnaad Swahiyh, Al-Haakim amepia daraja ya Swahiyh (2/98)]

 

 

Share

040-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Du'aa Ambayo Ni Hazina Kuliko Hazina Ya Dhahabu Na Fedha!

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Du'aa Ambayo Ni Hazina Kuliko Hazina Ya Dhahabu Na Fedha!

 

 Alhidaaya.com

 

 

 اللَّهُمَّ إِنَّي أَسْألُكَ الثَّباتَ فِي الأَمْرِ، والْعَزِيمَةَ عَلى الرُّشْدِ، وَأسْألُكَ مُوجِبَاتِ رَحْمَتِكَ، وَعَزَائِمَ مَغْفِرَتِكَ، وأسْألُكَ شُكْرِ نِعْمَتِكَ ، وحُسْنَ عِبَادَتِكَ، وأسْألُكَ قَلْبًا سَلِيمًا، ولِسَانًا صَادِقًا، وأسْألُكَ مِنْ خَيْرِ ما تَعْلَمُ، وأعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا تَعْلَمُ، وأسْتَغْفِرُكَ لِمَا تَعْلَمُ، إنَّكَ أنْتَ عَلاَمُ الغُيُوب

 

Allaahumma inniy as-alukath-thabaat fil-amri, wal-‘aziymata ‘alar-rushdi, wa as-aluka muwjibaati Rahmatika, wa ‘azaaima maghfiratika, wa as-aluka shukri ni’matika, wa husna ‘ibaadatika, wa as-aluka qalban saliyman, wa lisaanan swaadiqan, wa as-aluka min-khayri maa Ta’lamu wa a’uwdhu bika min sharri maa Ta’lamu, wa astaghfiruka limaa Ta’lamu innaka Anta ‘Allaamul-ghuyuwbi

 

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kuthibitika katika jambo (Dini na utiifu), na  azimio juu ya uongofu, na nakuomba haki yenye kuwajibisha Rahmah Zako, na azimio  la maghfirah Yako, na nakuomba kushukuru neema Zako, na uzuri wa kukuabudu, na nakuomba moyo uliosalimika, na ulimi usemao kweli, na nakuomba kheri Unazozijua na najikinga Kwako shari Unazozijua, na nakuomba maghfirah kwa Unayoyajua, hakika Wewe ni Mjuzi mno wa ya ghaibu.

 

Imepokelewa kutoka Shaddaad bin Aws (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Ee Shaddaad bin Aws, ukiona watu wanaweka hazina dhahabu na fedha, basi zidisha maneno haya)) [Atw-Twabaraaniy, Taz. As-Silsilatusw-Swahiyhah (3228]

 

Faida:  Moyo uliosalimika ni moyo uliosalimika na kufru, shirki, riyaa, bid’ah, unafiki, maovu, husda, chuki na kila ovu.

 

 

Share

041-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Taqwa Ya Nafsi Na Kuitakasa

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Taqwa Ya Nafsi Na Kuitakasa

 

 Alhidaaya.com

 

 

 041-Ee Allaah, Ipe nafsi yangu taqwa yake, Wewe ni Waliyy wake na…

 

 

 اللَّهُمَّ آتِ نَفْسِي تَقْوَاهَا، أَنْتَ وَلِيّهَا وَمَوْلاَهَا، وَخَيْر مَنْ زَكَّاهَا

 

Allaahumma aati nafsiy taqwaahaa, Anta Waliyyuhaa wa Mawlaahaa, wakhayru man zakkaahaa

 

Ee Allaah, Ipe nafsi yangu taqwa yake, Wewe ni Waliyy wake na Mlinzi wake na Mbora wa mwenye kuitakasa.

 

[Atw-Twabaraaniy (11:106) Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه و آله وسلم)  alikuwa akisita kila anapofikia Aayah: Na Naapa kwa nafsi na Aliyeisawazisha. Kisha Akaitambulisha uovu wake na taqwa yake.” [Ash-Shams 91: 7 -8] kisha huomba du’aa hiyo. Taz pia Majmau’ Az-Zawaaid (7/141) kwa isnaad Hasan]

 

Share

042-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Khulqa (Tabia) Njema

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Khulqa (Tabia) Njema

 

 Alhidaaya.com

 

 

 اللَّهُمَّ أَحْسَنْتَ خَلْقِي فَأَحْسِنْ خُلُقِي

 

Allaahumma ahsanta khalqiy, fa ahsin khuluqiy

 

Ee Allaah, Umeboresha umbo langu, basi boresha khulqa (tabia) zangu.

 

 

[Ahmad na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy katika Irwaa Al-Ghaliyl (1/115)]

 

 

Share

043-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Hikmah Kwani Atakayepewa Hikmah Amepewa Khayr Nyingi

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Hikmah Kwani Atakayepewa Hikmah Amepewa Khayr Nyingi

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ آتِنِي الْحِكْمَةَ الَّتِي مَنْ أُوتِيَهَا فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا

 

Allaahumma aatinil-hikmatallaty man uwtiyahaa faqad uwtiya khayran kathiyraa

 

Ee Allaah, Nipe Hikmah ambayo atakayepewa basi kwa yakini amepewa khayr nyingi.

 

Tanbihi:  Hii ni du’aa ambayo imenukuliwa kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Suwratul-Baqarah 2: 269.

 

Share

044-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Ilhamu Ya Uongofu Na Kuomba Kinga Ya Shari Za Nafsi

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Ilhamu Ya Uongofu Na Kuomba Kinga Ya Shari Za Nafsi

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 اللَّهُمَّ أَلْهِمْنِي رُشْدِي وَأَعِذْنِي مِنْ شَرِّ نَفْسِي

 

Allaahumma alhimniy rushdiy wa a’idhniy min sharri nafsiy

 

Ee Allaah, nitilie ilhamu uongofu wangu, na nikinge dhidi ya shari ya nafsi yangu

 

[At-Tirmidhiy, taz. Takhriyj Mishkaat Al-Miswbaah  Ibn Hajar Al-‘Asqalaani (3/24)]

 

 

Share

045-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Dhidi Ya Moyo Usionyenyekea, Du'aa Isiyosikizwa, Nafsi Isiyoshiba, Elimu...

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Dhidi Ya  Moyo Usionyenyekea, Du'aa Isiyosikizwa,

Nafsi Isiyoshiba, Elimu Isiyonufaisha

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ قَلْبٍ لاَ يَخْشَعُ وَمِنْ دُعَاءٍ لاَ يُسْمَعُ وَمِنْ نَفْسٍ لاَ تَشْبَعُ وَمِنْ عِلْمٍ لاَ يَنْفَعُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَؤُلآءِ الأَرْبَعِ

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min-qalbin-laa yakh-sha’u, wamin du’aain-laa yasma’u, wamin nafsin-laa tashba’u, wamin ilmin-laa yanfa’u, a’uwdhu bika min haaulail-arba’i

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga moyo usionyenyekea na du’aa isiyosikizwa na nafsi isiyoshiba na elimu isiyonufaisha, najikinga Kwako dhidi ya haya manne.

 

[Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Swahiyh An-Nasaaiy, Swahiyh Al-Jaami’ (1297)]

 

 

Share

046-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Mema Kuacha Maovu Kuwapenda Maskini, Mapenzi Ya Allaah

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Mema Kuacha Maovu Kuwapenda Maskini, Mapenzi Ya Allaah

 

 Alhidaaya.com

 

 

Du’aa hii inajumuisha pia kuomba kuwapenda masikini, kuacha maovu, kuomba maghfirah na Rahmah, kuomba mauti inapotokea fitnah katika Dini.  Du’aa hii amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Hakika hii ni haki basi jifunzeni kisha muifunze))

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَتَرْكَ الْمُنْكَرَاتِ وَحُبَّ الْمَسَاكِينِ وَأَنْ تَغْفِرَ لِي وَتَرْحَمَنِي وَإِذَا أَرَدْتَ فِتْنَةَ قَوْمٍ فَتَوَفَّنِي غَيْرَ مَفْتُونٍ أَسْأَلُكَ حُبَّكَ وَحُبَّ مَنْ يُحِبُّكَ وَحُبَّ عَمَلٍ يُقَرِّبُنِي إِلَى حُبِّكَ

 

Allaahumma inniy as-aluka fi’-lal khayraati wa tarakal-munkaraati, wa hubbal masaakiyni, wa antaghfiraliy wa tarhamniy waidhaa aradta fitnata qawmin fatawaffiny ghayra maftuwnin. As-aluka hubbaka, wa hubba man yyuhibbuka, wahubba ‘amaliyy yuqarribuniy ilaa hubbika

 

Ee Allah, hakika mimi nakuomba kutenda mema, na kuacha maovu na kuwapenda masikini, na Unighufurie na Unirehemu, na Unapowatakia watu fitnah, basi nifishe bila ya kufitinishwa. Nakuomba mapenzi Yako, na mapenzi ya anayekupenda, na mapenzi yatakayonikaribisha katika mapenzi Yako.

[At-Tirmidhiy, Ahmad - Hadiyth Hasan]

 

 

Share

047-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Mapenzi Ya Allaah Na Mapenzi Ya Watakaokunufaisha Kwa Allaah

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Mapenzi Ya Allaah Na Mapenzi Ya Watakaokunufaisha Kwa Allaah

 

 Alhidaaya.com

 

 

Du’aa kutafuta mapenzi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

 

اللَّهُمَّ ارْزُقْنِي حُبَّكَ وَحُبَّ مَنْ يَنْفَعُنِي حُبُّهُ عِنْدَكَ اللَّهُمَّ مَا رَزَقْتَنِي مِمَّا أُحِبُّ فَاجْعَلْهُ قُوَّةً لِي فِيمَا تُحِبُّ اللَّهُمَّ مَا زَوَيْتَ عَنِّي مِمَّا أُحِبُّ فَاجْعَلْهُ فَرَاغًا لِي فِيمَا تُحِبُّ

 

 

Allaahummar-zuqniy hubbaka wa hubba man yanfa’aniy hubbuhu ‘indaka. Allaahumma maa razaqtaniy mimmaa uhibbu faj-’alhu quwwatal-lliy fiymaa tuhibbu. Allaahumma maa zawayta ‘anniy mimmaa uhibbu faj-’alhu faraaghal-lliy fiymaa Tuhibbu

 

Ee Allaah, niruzuku mapenzi Yako, na mapenzi ya atakayeninufaisha mapenzi yake Kwako. Ee Allaah Uliyoniruzuku kati ya niyapendayo, basi yajaalie yawe ni nguvu kwangu kwa Uyapendayo. Ee Allaah, Uliyoniondoshea kati ya niyapendayo, basi yajaalie kuwa ni wasa’aa kwangu katika Uyapendayo

 

[At-Tirmidhiy  (5/523 ) na ameipa daraja ya Hasan]

 

 

 

Share

048-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Hifadhi Katika Uislamu Katika Hali, Kinga Na Bezo La Adui Na Hasidi ...

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Hifadhi Katika Uislamu Katika Hali; Kusimama, Kukakaa, Kulala

Kinga Na Bezo La Adui Na Hasidi Na Kheri Zote

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 اَللَّهُمَّ احْفَظْنِي بِالإِسْلاَمِ قَائِمًا  وَاحْفَظْنِي بِالإِسْلاَمِ قَاعِداً  وَاحْفَظْنِي بِالإِسْلاَمِ رَاقِداً  وَلاَ تُشْمِتْ بِي عَدُوًا وَلاَ حَاسِداً. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ كُلِّ خَيْرٍ خَزَائِنُهُ بِيَدِكَ  وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ كُلِّ شَرٍّ خَزَائِنُهُ بِيَدِك   

 

Allaahummah-fadhwniy bil Islaami qaaimaa, wahfadhwniy bil Islaami qaaidaa, wahfadhwniy bil Islaami raaqidaa, walaa tushmit biy ‘aduwwan walaa haasidaa. Allaahumma inniy as-aluka min kulli khayrin khazaainuhu Biyadika, wa a’uwdhu Bika min kulli sharrin khazaainuhu Biyadika

 

Ee Allaah, nihifadhi katika Uislamu nikiwa nimesimama, na nihifadhi katika Usilamu nikiwa nimekaa, na nihifadhi katika Uislamu nikiwa nimelala, wala Usinijaalie kuwa bezo la adui wala hasidi. Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kila kheri ambazo hazina zake zimo Mikononi Mwako, na najikinga Kwako shari zote ambazo hazina zake zimo Mikononi Mwako

 

[Al-Haakim, Taz., Swahiyh Al-Jaami’ (2/398) na Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (4/54 – 1540)]

 

 

 

Share

049-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Ya Kila Shari, Kulipiwa Madeni Na Kinga Ya Ufakiri

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Kila Shari, Kulipiwa Madeni Na Kinga Ya Ufakiri

 

 

 Alhidaaya.com

 

 

Du’aa hii ni miongoni mwa nyiradi za unaingia kitandani kulala.

 

 

اللَّهُمَّ رَبَّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ  وَرَبَّ الأَرْضِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ، رَبَّنَا وَرَبَّ كُلِّ شَيْءٍ، فَالِقَ الْحَبِّ وَالنَّوَى، وَمُنْزِلَ التَّوْرَاةِ وَالإِنْجِيلِ وَالْفُرْقَانِ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ كُلِّ شَيْءٍ أَنْتَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهِ، اللَّهُمَّ أَنْتَ الأَوَّلُ فَلَيْسَ قَبْلَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الآَخِرُ فَلَيْسَ بَعْدَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الظَّاهِرُ فَلَيْسَ فَوْقَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الْبَاطِنُ فَلَيْسَ دُونَكَ شَيْءٌ ، اقْضِ عَنَّا الدَّيْنَ وَأَغْنِنَا مِنَ الْفَقْر

 

Allaahumma Rabbas-samaawatis-sab-‘i wa Rabbal-ardhwi, wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwiym, Rabbanaa wa Rabba kulli shay-in, faaliqal-habbi wan-nnawaa, wa munzilat-Tawraati wal-Injiyli  wal-Furqaan. A’uwdhu bika min sharri kulli shay-in Anta aakhidhun binaaswiyatihi. Allaahumma Antal-Awwalu falaysa qablaka shay-un, wa Antal-Aakhiru falaysa ba’-daka shay-un wa Antadhw-Dhwaahiru falaysa fawqaka shay-un, wa Antal-Baatwinu falaysa duwnaka shay-un. Iqdhwi ‘annad-dayna wagh-ninaa minal-faqri  

 

Ee Allaah,  Rabb wa mbingu saba na Rabb wa ardhi, na Rabb wa ‘Arsh ‘Adhimu, Rabb wetu na Rabb wa kila kitu, Mpasuaji wa mbegu na kokwa na Aliyeiteremsha Tawraat na Injiyl na Qur-aan. Najikinga Kwako shari ya kila kitu, Wewe Ndiye Mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah, Wewe Ndiye Al-Awwalu (wa Awali hakuna kitu kabla Yako) na Al-Aakhiru (wa Mwisho hakuna kitu baada Yako) na Adhw-Dhwaahiru (Uliye juu hakuna kitu juu Yako), na Al-Baatwinu (Uliye karibu, hakuna kitu kilichokaribu kuliko Wewe), Nilipie madeni yangu na Niepushe na ufakiri.

 

[Muslim]

 

Share

050-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kujikinga Kushindwa Hila, Kutokuwa Na Uvivu, Uoga, Ubahili, Kutokudhoofika, Adhabu Za Kaburi Fitnah Za Uhai Na Mauti

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kujikinga Kutokana Na Kushindwa Hila, Kutokuwa Na Uvivu, Uoga,

Ubahili, Kutokudhoofika, Kinga Ya Adhabu Za Kaburi Na Fitnah Za Uhai Na Mauti

 

 Alhidaaya.com

 

 

050-Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na kushindwa hila, na uvivu...

 

  

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْعَجْزِ وَالْكَسَلِ وَالْجُبْنِ وَالْبُخْلِ وَالْهَرَمِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-‘ajzi wal-kasali, wal-jubni wal-bukhli, wal-harami wa a’uwdhu bika min ‘adhaabil-qabri, wamin fitnatil-mahyaa wal-mamaati

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na kushindwa hila, na kutokuwa na uvivu, na uoga, na ubahili, na kutokudhoofika [kutokana na uzee], na najikinga Kwako adhabu ya kaburi na najikinga Kwako fitnah za uhai na mauti

 

[Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

Share

051-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Kushindwa Hila, Kuomba Taqwa Ya Nafsi,Kinga Ya Elimu Isiyonufaisha, Moyo Usionyeyekea, Nafsi ...

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kinga Ya Kushindwa Hila, Kuomba Taqwa Ya Nafsi,  Kinga Ya Elimu Isiyonufaisha, Moyo Usionyeyekea, Nafsi Isiyoshiba, Du'aa Isiyoitikiwa.

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْعَجْزِ وَالْكَسَلِ، وَالْجُبْنِ وَالْبُخْلِ، وَالْهَرَمِ وَعَذَابِ الْقَبْرِ. اللَّهُمَّ آتِ نَفْسِي تَقْوَاهَا، وَزَكِّهَا أَنْتَ خَيْرُ مَنْ زَكَّاهَا، أَنْتَ وَلِيُّهَا وَمَوْلاَهَا. اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عِلْمٍ لاَ يَنْفَعُ، وَمِنْ قَلْبٍ لاَ يَخْشَعُ، وَمِنْ نَفْسٍ لاَ تَشْبَعُ، وَمِنْ دَعْوَةٍ  لاَ يُسْتَجَابُ لَهَا

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-‘ajzi wal-kasali, wal-jubni wal-bukhli, wal-harami, wa ‘adhaabil-qabri, Allaahumma aati nafsiy taqwaahaa, wa zakkihaa Anta khayru man zakkaahaa, Anta Waliyyuhaa wa Mawlaaha. Allaahumma inniy a’uwdhu bika min ’ilmin-laa yanfa’u, wamin qalbin-laa yakhsha’u, wamin-nafsil-laa tashba’u, wamin da’-watin-laa yustajaabu lahaa

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kushindwa hila, na uvivu, na uoga, na ubakhili, na kudhoofika [kutokana na uzee] na adhabu za kaburi. Ee Allaah, Ipe nafsi yangu taqwa yake, na Itakase kwani Wewe ni Mbora wa kuitakasa, Wewe ni Waliyyu wake na Mawlaa wake. Ee Allaah, hakika najikinga Kwako elimu isiyonufaisha, na moyo usionyeyekea na nafsi isiyoshiba, na du’aa isiyoitikiwa.

 

[Muslim, An-Nasaaiy , Ahmad]

 

 

Share

052-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Ya Shari Ulizotenda Na Shari Usizotenda

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Kutokana Na Shari Ulizotenda  Na Shari Usizotenda

 

 Alhidaaya.com

 

 

   اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَمِلْتُ وَمِنْ شَرِّ مَا لَمْ أَعْمَلْ

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min sharri maa ‘amiltu wamin sharri maa lam a’-amal

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na  shari nilizotenda na shari nisizotenda.

 

[Muslim,  Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy,  Ibn Maajah, Ahmad]

 

 

 

 

 

Share

053-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Ya Shari Ya Masikio, Macho, Ulimi, Moyo Na Manii

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Shari Ya Masikio, Macho, Ulimi, Moyo Na Manii

 Alhidaaya.com

 

 

أللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ سَمْعِي وَمِنْ شَرِّ بَصَرِي وَمِنْ شَرِّ لِسَانِي وَمِنْ شَرِّ قَلْبِي وَمِنْ شَرِّ مَنِيِّي   

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min sharri sam-’iy wamin sharri baswariy, wamin sharri lisaaniy wamin sharri qalbiy, wamin sharri maniyyi

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako shari ya masikio yangu na shari ya macho yangu, na shari ya ulimi wangu, na shari ya moyo wangu, na shari ya manii yangu

 

 

[Abuu Daawuwd , At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy –Swahiyh At-Tirmidhiy (3/166) na Swahiyh An-Nasaaiy (3/1108)]

 

 

 

 

 

Share

054-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Ya Tabia Ovu Za Kuchukiza Na Matendo Na Matamanio

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Tabia Ovu Za Kuchukiza Na Matendo Na Matamanio

 

 Alhidaaya.com

 

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ مُنْكَرَاتِ الاَخْلاَقِ وَالاَعْمَالِ وَالاَهْوَاءِ

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min munkaraatil-akhlaaqi wal a’-maali wal ahwaai

 

Ee Allaah, hakika najikinga Kwako tabia ovu za kuchukiza na matendo na matamanio

 

[At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Al-Haakim, At-Twabaraniy -  Swahiyh At-Tirmidhiy (3/184)]

 

 

Share

055-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Tabia Ovu Na Matamanio, Matendo Na Maradhi

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Tabia Ovu Za Kuchukiza Na Matamanio,

Matendo Na Maradhi

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 اللَّهُمَّ جَنِّبْنِي مُنْكَرَاتِ الاَخْلاَقِ وَالاَهْوَاءِ وَالاَعْمَالِ والأدْوَاءِ

 

Allaahumma jannibniy munkaraatil-akhlaaqi, wal ahwaahi, wal-a’maali, wal adwaai

 

Ee Allaah niepushe tabia ovu za kuchukiza na matamanio na na matendo, na maradhi

 

  

[Al-Haakim na kasema Swahiyh kwa sharti ya Muslim na ameikubali Adh-Dhahabiy.  Kitabus-Sunnah (13)  na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy]

 

 

 

Share

056-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Ya Njaa Na Khiyaana

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Njaa Na Khiyaana

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْجُوعِ فَإِنَّهُ بِئْسَ الضَّجِيعُ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الْخِيَانَةِ فَإِنَّهَا بِئْسَتِ الْبِطَانَةُ

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-juw’iy fainnahu biisadhw-dhwajiy’u wa a’uwdhu bika minal-khiyaanati fainnahaa bi-isatil-bitwaanatu.

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako na njaa kwani hiyo ni mbaya mno kulala nayo, na najikinga Kwako khiyana kwani hiyo ni dhamira ovu.

 

[Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah,  Swahiyh An-Nasaaiy (3/1112)]

 

 

 

Share

057-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Uoga, Ubakhili, Kurudishwa Katika Umri Wa Udhalili, Fitna Za...

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Uoga, Ubakhili, Kurudishwa Katika Umri Wa Udhalili,

Fitna Za Dunia Na Adhabu Za Kaburi

 

 www.alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْجُبْنِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الْبُخْلِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أُرَدَّ إِلَى أَرْذَلِ الْعُمُرِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الدُّنْيَا وَعَذَابِ الْقَبْرِ

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-jubni, wa a’uwdhu bika minal-bukhli, wa a’uwdhu bika min an uradda ilaa ardhalil ‘umuri, wa a’uwdhu bika min fitnatid-dunyaa wa adhaabil-qabri

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako uoga, na najikinga Kwako ubakhili, na najikinga Kwako kurudishwa katika umri wa kudhalilika [uzee], na najikinga Kwako fitnah za dunia na adhabu za kaburi. [Al-Bukhaariy]

 

 

Share

058-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Kudhoofika, Moyo Mgumu, Kughafilika, Kufedheheka, Kudhalilika Na...

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Kudhoofika, Moyo Mgumu, Kughafilika,

Kufedheheka, Kudhalilika Na Umasikini...

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْعَجْزِ وَالْكَسْلِ والْجُبْنِ وَالْبُخْلِ وَالْهَرَمِ وَالْقَسْوَةِ وَالْغَفْلَةِ وَالْعَيْلَةِ وَالذِّلَّةِ وَالْمَسْكَنَةِ  وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الْفَقْرِ وَالْكُفْرِ وَالْفُسُوقِ وَالشِّقَاقِ وَالنِّفَاقِ وَالسُّمْعَةِ وَالرِّياَءِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الصَّمَمِ  وَالْبُكَمِ والْجُنُونِ وَالْجُذَامِ والْبَرَصِ وَسَيِّءِ الاَسْقَامِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-‘ajzi, wal-kasli, wal-jubni, wal-bukhli, wal-harami, wal-qaswati, wal-ghaflati, wal-‘aylati, wadh-dhillati, wal-maskanati, wa a’uwdhu bika minal-faqri, wal-kufri, wal-fusuwqi, wash-shiqaaqi, wan-nifaaqi, wassum-’ati, warriyaai, wa a’uwdhu bika minasw-swamami, wal-bukami, wal-junuwni, wal-judhaami, walbaraswi, wasayyiil-asqaami

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutojiweza, na uvivu, na uoga, na ubakhili, na kudhoofika [kutokana na uzee], na  moyo mgumu, na kughafilika, na kufedheheka, na kudhalilika, na umasikini, na najikinga Kwako na ufakiri, na kufru, na ufasiki, na magomvi, na unafiki, na kupenda kusikika umaarufu, na riyaa, na najikinga Kwako dhidi ya uziwi na ububu na ukichaa na ukoma na mbalanga na maradhi mabaya. 

 

[Al-Haakim, Al-Bayhaqiy na Taz. Swahiyh Al-Jaami’ (1/406]

 

 

Share

059-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Kuangamia, Kuzama, Kuungua, Kughilibiwa Na Shaytwaan Wakati Wa .....

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kinga Ya Kuangamia, Kuvunjika, Kuzama, Kuungua Moto, Kughilibiwa Na Shaytwaan Wakati Wa Mauti...

 

 Alhidaaya.com

 

  

 

 

 

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ التَّرَدِّي ، وَالْهَدْمِ ، وَالْغَرَقِ ، وَالْحَرَقِ ،  وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ يَتَخَبَّطَنِي الشَّيْطَانُ عِنْدَ الْمَوْتِ ، وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ أَمُوتَ فِي سَبِيلِكَ مُدْبِرًا ، وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ أَمُوتَ لَدِيغًا

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minat-taraddiy, wal-hadmi, wal-gharaqi, wal-haraqi, wa a’uwdhu bika an yatakhabbatwniyash-shaytwaanu ‘indal-mawti, wa a’uwdhu bika an amuwta fiy sabiylika mudbiraa, wa a’uwdhu bika an amuwta ladiyghaa

 

Ee Allaah, hakika  mimi najikinga Kwako kuangamia na kuvunjika na kufa kwa kuzama na kuungua na Moto, na najikinga Kwako kughilibiwa na shaytwaan wakati wa mauti, na najikinga Kwako kufa  nikiwa  mwenye  kugeuka nyuma katika njia Yako [kukimbia vita] na najikinga Kwako kufa kwa kun’gatwa [na mdudu wa sumu]

 

 

[Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy  -  Swahiyh An-Nasaaiy (3/1123)]

 

 

Share

060-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Ufakiri, Uchache, Udhalili, Kudhulumu Au Kudhulumiwa

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Ufakiri, Uchahe, Udhalili

Na Kinga Ya Kudhulumu Au Kudhulumiwa

 Alhidaaya.com

 

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْفَقْرِ وَالْقِلَّةِ وَالذِّلَّةِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أَظْلِمَ أَوْ أُظْلَمَ

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-faqri wal-qillati, wadh-dhillati, wa a’uwdhu bika min an adhwlima aw udhwlama

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako ufakiri na uchache na udhalilifu na najikinga Kwako kudhulumu au kudhulumiwa.

 

[Abuu Daawuwd, Ahmad – Swahiyh Abiy Daawuwd (1544)]

 

 

Share

061-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Uoga, Ubakhili, Uovu Wa Umri, Fitna Za Moyo, Adhabu Za Kaburi

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Uoga, Ubakhili, Umri Wenye Uovu Fitnah Za Moyo, Adhabu Za Kaburi

 

 Alhidaaya.com

 

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْجُبْنِ، وَالْبُخْلِ، وَسُوءِ الْعُمُر، وَفِتْنَةِ الصَّدْر، وَعَذَابِ الْقَبْر

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-jubni, wal-bukhli, wa suuil-‘umri wa fitnatisw-swadri, wa ‘adhaabil-qabri

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako uoga na ubakhili na umri wenye uovu na fitnah za moyo na adhabu ya kaburi.

[An-Nasaaiy, Sunan Abiy Daawuwd kwa usimulizi kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijikinga nayo mambo hayo].

 

 

Share

062-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kinga Ya Balaa Kuu Kukumbwa Na Mateso Majaaliwa Mabaya Bezo La Maadui

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Balaa Kuu,  Kukumbwa Na Mateso, Majaaliwa Mabaya, Bezo La Maadui

 

www.alhidaaya.com

 

 

 أللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ جَهْدِ الْبَلاَءِ وَدَرَكِ الشَّقَاءِ وَسُوءِ الْقَضَاءِ وَشَمَاتَةِ الأَعْدَاءِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min jahdil-balaai wa darakish-shaqaai wa suw-il-qadhwaai, wa shamaatatil-a’daai

 

Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako na balaa kuu (misukosuko n.k.) na kukumbwa na mateso (mashaka n.k.) na majaaliwa mabaya na bezo la maadui.

[Al-Bukhaariy, Muslim]

Share

063-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Dhidi Ya Jirani Muovu

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Dhidi Ya Jirani Muovu

 

 Alhidaaya.com

 

  

063- Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako jirani muovu katika…

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ جَارِ السَّوْءِ فِي دَارِ الْمُقَامِ فَإِنَّ جَارَ الْبَادِيَةِ يَتَحَوَّلُ

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min jaaris-saw-i fiy daaril-muqaami fainna jaaral-baadiyati yatahawwalu.

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako na jirani muovu katika makazi ya kudumu kwani jirani wa jangwani hubadilika badilika kuhama.

 

[An-Nasaaiy kwa usimulizi ((Jikingeni na jirani muovu…)), As-Silsilatu Asw-Swahiyhah (3943), Swahiyh Al-Jaami’ (2967)]

 

Ufafanuzi: Makazi ya kudumu: Makazi ya kuthibitika hayabadiliki; watu hubakia hawaondoki kuhama kuhama.

 

 

Share

064-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Maovu Ya Mchana, Usiku, Saa, Rafiki Muovu, Jirani Muovu

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Kuomba Kinga Maovu Ya Mchana Na Usiku Na Saa,

Rafiki Muovu Na Jirani Muovu

 

 Alhidaaya.com

 

 

 أللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ  يَوْمِ السُّوءِ وَمِنْ لَيْلَةِ السُّوءِ وَمِنْ سَاعَةِ السُّوءِ وَمِنْ صَاحِبِ السُّوءِ وَمِنْ جَارِ السُّوءِ  فَي دَارِ الْمُقَامَةِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min yawmis-suw-i wamin laylatis-suw-I, wamin saa’atis-suw-i, wamin swaahibis-suw-i, wamin-jaaris suw-i fiy daaril-muqaamati

 

Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako kutokana na siku ovu, na usiku muovu, na saa ovu, na rafiki muovu, na jirani muovu katika makazi ya kudumu. 

 

[Atw-Twabaraaniy - Majma’ Az-Zawaaid (10/144), Swahiyh Al-Jaami’ (1/411)]

 

 

 

Share

065-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Ya Kushindwa Kulipa Deni, Kushindwa Na Adui Na Bezo La Maadui

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Kushindwa Kulipa Deni, Kushindwa Na Adui Na Bezo La Maadui

 

 Alhidaaya.com

 

 

  اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ غَلَبَةِ الدَّيْنِ وَغَلَبَةِ الْعَدُوِّ وَشَمَاتَةِ الأَعْدَاءِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min ghalabatid-dayni, wa ghalabatil-‘aduwwi wa shamaatatil-a’-daai

 

Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako kushindwa kulipa deni, na kushindwa na adui, na bezo la maadui.

 

[An-Nasaaiy, Ahmad -  Swahiyh An-Nasaaiy (3/1113)]

 

 

Share

066-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kutoshelezwa Vya Halali Dhidi Ya Haramu, Kutajirishwa Kwa Fadhila Za Allaah

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kutoshelezwa Kwa Vya Halali Dhidi Ya Haramu Na Kutajirishwa Kwa  Fadhila Za Allaah

 

 Alhidaaya.com

 

 

 066- Ee Allaah nitosheleze Vyako vya halali dhidi ya vyako ambavyo ni haramu

 

 

 اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلالِكَ عن حَرَامِكَ وَأغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِوَاكَ

 

Allaahumma akfiniy bi-halaalika ‘an-haraamika waghniniy bi-fadhwlika ‘an man siwaak

 

Ee Allaah nitosheleze na Vyako vya halali  dhidi ya Vyako ambavyo ni haramu, na nitajirishe kwa fadhila Zako kutokana na asiyekuwa Wewe.

 

[At-Tirmidhiy, taz. Swahiyh Sunan At-Tirmidhy (2822)]

 

 

Share

067-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kujisalimisha Kwa Allaah, Kumwamini, Kutawakali Kwake, Kutubia Kwake...

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kujisalimisha Kwa Allaah, Kumwamini,

Kutawakali Kwake, Kutubia Kwake...

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

 اللَّهُمَّ لَكَ أَسْلَمْتُ وَبِكَ آمَنْتُ وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْكَ أَنَبْتُ وَبِكَ خَاصَمْتُ.  اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِعِزَّتِكَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ أَنْ تُضِلَّنِي أَنْتَ الْحَيُّ الَّذِي لاَ يَمُوتُ وَالْجِنُّ وَالإِنْسُ يَمُوتُونَ

 

Allaahumma laka aslamtu, wa bika aamantu, wa ‘alayka tawakkaltu, wa ilayka anabtu, wa bika khaaswamtu. Allaahumma inniy a’uwdhu bika bi’izzatika laa ilaaha illa Anta an-tudhwillaniy Antal-Hayyu Alladhiy  laa yamuwtu wal-jinnu wal-insu yamuwtuwna.

 

Ee Allaah, Kwako najisalimisha na Kwako naamini na Kwako natawakali na Kwako narejea kutubu na Kwako nagombana [dhidi ya adui]. Ee Allaah, hakika mimi najikinga kwa Utukufu Wako, hapana muabudiwa wa haki ila Wewe Usije kunipotoa Wewe Uliye Hai daima Ambaye Hafi ilhali majini na watu wanakufa

 

[Muslim, Ahmad]

 

 

 

Share

068-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):Kinga Ya Kuondokewa Neema Za Allaah, Kubadilika 'Aafiyah, Adhabu Ya Ghafla...

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kinga Ya Kuondokewa Neema Za Allaah, Kubadilika 'Aafiyah,

Adhabu Ya Ghafla Na Hasira Za Allaah

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ زَوَالِ نِعْمَتِكَ وَتَحَوُّلِ عَافِيَتِكَ وَفُجَاءَةِ نِقْمَتِكَ وَجَمِيعِ سَخَطِكَ

 

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min-zawaali ni’matika, watahawwuli ‘aafiyatika, wafujaa-ati niqmatika, wajamiy’i   Sakhatwika.

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kuondoka na Neema Zako, na kubadilika 'Aafiyah  [afya, amani, salama, hifadhi ya kila baya.] na adhabu Yako ya ghafla na hasira Zako zote

 

[Muslim,  Abuu Daawuwd]

 

 

 

Share

069-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kunufaishwa Kwa Uliyojifunza, Elimu Ya Yatakayokufaa, Kuzidishiwa Elimu

 Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Kuomba Kunufaishwa Kwa Uliyojifunza

Na Yanayokufaa Na Kuzidishiwa Elimu

 Alhidaaya.com

 

  

069-Ee Allaah, ninufaishe kwa Uliyonifundisha, na nifundishe

 

 ‏‏ اللَّهُمَّ انْفَعْنِي بِمَا عَلَّمْتَنِي وَعَلِّمْنِي مَا يَنْفَعُنِي  وَزِدْنِي عِلْمًا

 

Allaahuuma anfa’-niy bimaa ‘allamtaniy wa-‘allimniy maa yanfa’uniy wazidniy ‘ilmaa

 

Ee Allaah, ninufaishe kwa Uliyonifundisha, na nifundishe yanayoyonifaa na Nizidishe elimu

 

[Ibn Maajah 1/92 ,  Swahiyh Ibn Maajah 3091]

 

Share

070-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Elimu Yenye Manufaa, Kuomba Kinga Dhidi Ya Elimu Isiyonufaisha

 

 Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Elimu Yenye Manufaa

Na Kuomba Kinga Dhidi Ya Elimu Isiyonufaisha

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ عِلْماً نَافِعًا وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ عِلْمٍ لاَ يَنْفَعُ

Allaahumma inniy as-aluka ‘ilman naafi’aa wa a’uwdhu bika min ‘ilmin-laa yanfa’u

 

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba elimu yenye manufaa, na najikinga Kwako elimu isiyonufaisha

 

[Swahiyh Ibn Maajah na Taz Majma’ Az-Zawaaid (10/185)]

 

 

 

 

 

Share

071-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kunufaishwa Kwa Masikio, Macho, Kunusuriwa Na Anayekudhulum, Allaah Kukulipizia...

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Kunufaishwa Kwa Masikio, Macho, Kunusuriwa Na Anayekudhulumu

Na Allaah Kukulipizia Dhidi Ya Maadui

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ مَتِّعْنِي بِسَمْعِي وَبَصَرِي  وَاجْعَلْهُمَا الْوَارِثَ مِنِّي وَانْصُرْنِي عَلَى مَنْ يَظْلِمُنِي وَخُذْ مِنْهُ بِثَأْرِي

 

Allaahumma matti’-niy bisam-’iy, wa baswariy, waj-’al-humal-waaritha minniy, wanswurniy ‘alaa man yadhwlimuniy, wa khudh minhu bitha-ariy

 

Ee Allaah, ninufaishe kwa masikio yangu, na macho yangu, na vijaalie viwili hivyo viwe wiratha wangu (viimarishe mpaka kufa kwangu) na ninusuru dhidi ya anayenidhulumu, na nilipizie dhidi yake.

 

[At-Tirmidhiy Taz Swahiyh At-Tirmidhiy (3/188)]

 

 

 

 

 

Share

072-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hasbuna Allaahu Wa Ni'mal-Wakiyl: Allaah Anatutosheleza Mzuri Alioje Mdhamini...

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Hasbuna Allaah Wa Ni'mal-Wakiyl

Allaah Anatutosheleza Na Mzuri Alioje Mdhamini Anayetegemmewa Kwa Yote

 

 Alhidaaya.com

 

  

 

 

حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

Hasbuna-Allaahu wa Ni’-mal-Wakiyl

 

Allaah Anatutosheleza, Na Mzuri Alioje Mdhamini Anayetegemewa kwa yote

 

[Al-Bukhaariy  kutoka kwa Ibn ‘Abaas: “Ameisema Ibraahiym  ('Alayhis-Salaam) alipotupwa Motoni na ameisema Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  waliposema (Suwrat A’Imraan 3: 173) “Hasbuna-Allaah! (Allaah Anatutosheleza) Na Mzuri Alioje Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.”

 

 

Share

073-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Maghfirah Kwa Makosa Uliyoyakusudia Na Ya Mzaha, Kinga Ya Kupinduka Mipaka...

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Maghfirah Kwa Makosa Uliyoyakusudia Na Ya Mzaha,

Kuomba Kinga Ya Ujahili Na Kupinduka Mipaka

 

 Alhidaaya.com

 

  

 

 اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي وَجَهْلِي وَإِسْرَافِي فِي أمْرِي وَمَا أنْتَ أعْلَمُ بِهِ مِنِّي، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي جِدِّي وَهَزْلِي وَخَطَئِي وَعَمْدِي وَكُلُّ ذَلِكَ عِنْدِي. اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ وَمَا أخَّرْتُ وَمَا أسْرَرْتُ وَمَا أعْلَنْتُ وَمَا أنْتَ أعْلَمُ بِهِ مِنِّي، أنْتَ الْمُقَدِّمُ وَأنْتَ الْمُؤَخِّرُ وَأنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

 

Allaahumma-ghfirliy khatwiy-atiy, wajahliy, waisraafiy fiy amriy, wamaa Anta A’lamu minniy. Allaahumma-ghfirliy jaddiy, wahazliy, wakhatwa-iy, wa-‘amdiy wa kullu dhaalika ‘indiy. Allaahumma-ghfirliy maa qaddamtu, wamaa akhkhartu, wamaa asrartu, wamaa a’lantu, wamaa Anta A’lamu bihi minniy, Antal-Muqaddimu wa-Antal-Muakhkhiru, wa-Anta ‘alaa kulli shay’in Qadiyr

 

Ee Allaah! Nighufurie makosa yangu, ujahili (ujinga) wangu, na israaf (upindukaji mipaka) katika mambo yangu, Unayoyajua Wewe kutoka kwangu. Ee Allaah! Nighufurie niliyoyafanya kwa kudhamiria, na niliyoyafanya kwa kukosea, na makosa yangu yote. Ee Allaah! Nighufurie niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha, na niliyoyadhihirisha, na ambayo Wewe Unayajua kuliko mimi, Wewe ni Mwenye kutanguliza, na Wewe ni mwenye kuchelewesha. Wewe ni Muweza juu ya kila kitu. 

[Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share

074-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kutengenezewa Dini, Dunia Na Aakhirah, Kuzidishiwa Kheri Za Uhai, Kuepushwa...

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Kuomba Kutengenezewa Dini, Dunia Na Aakhirah,

Kuzidishiwa Kheri Katika Uhai, Kuepushwa Na Shari Za Mauti

 Alhidaaya.com

 

 

 

اللَّهُمَّ أَصْلِحْ لِي دِينِي الَّذِي هُوَ عِصْمَةُ أَمْرِي، وَأَصْلِحْ لِي دُنْيَايَ الَّتِي فِيهَا مَعَاشِي، وَأَصْلِحْ لِي آخِرَتِي الَّتِي فِيهَا مَعَادِي، وَاجْعَلْ الْحَيَاةَ زِيَادَةً لِي فِي كُلِّ خَيْر، وَاجْعَلْ الْمَوْتَ رَاحَةً لِي مِنْ كُلِّ شَرٍّ

 

Allaahumma aswlih-liy diyni-lladhiy huwa ‘iswmatu amriy, wa aswlih-liy dunyaaya-llatiy fiyhaa ma’aashiy, wa aswlih-liy Aakhirati-llaty fiyhaa ma’aadiy, waj-’alil-hayaata ziyaadatan-lliy fiy kulli khayr, waj-’alil-mawta raahatan-lliy min kulli sharr.

 

Ee Allaah, nitengenezee Dini yangu ambayo ndio asasi ya mambo yangu, na nitengenezee dunia yangu ambayo humo ni maisha yangu, na nitengenezee Aakhirah yangu ambayo humo ni marejeo yangu, na Jaalia uhai wangu uwe wenye ziada ya kila kheri, na Jaalia mauti kwangu yawe ya raha kutokana na  kila shari

 

[Muslim]

 
Share

075-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Qur-aan Kuwa Ni Uhuisho Wa Moyo Na Nuru, Kuondokewa Huzuni,Wahka

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Kuomba Qur-aan Kuwa Ni Uhuisho Wa Moyo Na Na Nuru,

Ufumbuzi Wa Huzuni Na Kuondokewa Wahka

 

 Alhidaaya.com

 

 

  

 اللَّهُمَّ إِنِّي عَبْدُكَ، وَابْنُ عَبْدِكَ، وَابْنُ أَمَتِكَ، نَاصِيَتِي بِيَدِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤُكَ، أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيْتَ بِهِ نَفْسَكَ، أَوْ عَلَّمْتَهُ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ، أَوْ أَنْزَلْتَهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ اسْتَأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الْغَيْبِ عِنْدَكَ، أَنْ تَجْعَلَ الْقُرْآنَ رَبِيعَ قَلْبِي، وَنُورَ صَدْرِي، وَجَلَاءَ حُزْنِي، وَذَهَابَ هَمِّي

 

Allaahumma inniy ‘abduka, ibnu-‘abdika, ibnu-amatika, naaswiyatiy Biyadika, maadhwin fiyya hukmuka, ‘adlun fiyya qadhwaauka, as-aluka bikullismin huwa Laka, sammayta bihi Nafsaka aw Anzaltahu fiy Kitaabika, aw ‘Allamtahu ahadan min Khalqika, awis-staa-tharta bihi fiy ‘ilmil-ghaybi  ‘In-daka, an Taj-’alal-Qur-aana rabiy’a qalbiy, wanuwra swadriy, wajalaa-a huzniy, wa dhahaaba hammiy.

 

Ee Allaah hakika mimi ni mtumwa Wako, mtoto wa mtumwa Wako, mtoto wa kijakazi Chako, utosi wangu uko Mikononi Mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako, ni usawa kwangu kunihukumu Kwako, nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako Ulilojiita  Mwenyewe au Uliloliteremsha katika Kitabu Chako, au Ulilomfundisha yeyote yule kati ya viumbe Vyako, au Ulilolihifadhi Wewe mwenyewe (na kujihusisha kulijua) katika ’ilmu ya ghayb Kwako, nakuomba Ujaalie Qur-aan kuwa ni rabiy' (uhuisho, raha, furaha na ustawisho) wa moyo wangu na nuru ya kifua changu, na ufumbuzi wa  huzuni yangu, na sababu ya kuondoka wahka wangu.

 

 

[Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yeyote atakayefikiwa na dhiki na huzuni kisha akasema  (Du’aa hiyo) hakuna isipokuwa Allaah Atamuondoshea dhiki na huzuni na Atambadilisha badala yake faraja.” Ikasemwa: Ee Rasuli wa Allaah! Je tujifunze? Akasema: ”Ndio, inampasa kwa mwenye kuisikia kujifunza.” [Ameipokea Ahmad (1/391) [452], Al-Haakim (1/509) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (199) na Al-Kalimi Atw-Twayyib (124)]

 

Share

076-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kutaraji Rahmah Ya Allaah Kuomba Utengenezewe Mambo Yako Yote

 

Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

Kutaraji Rahmah Ya Allaah Kuomba Utengenezewe Mambo Yako Yote

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 اللّهُـمَّ رَحْمَتَـكَ أَرْجـو فَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـيْن، وَأَصْلِـحْ لي شَأْنـي كُلَّـه لَا إِلَهَ إِلَّا أنْـت

 

Allaahumma Rahmatika arjuw falaa takilniy ilaa nafsiy twarfata ‘aynin, wa aswlih liy sha-aniy kullahu, laa ilaaha illaa Anta

 

Ee Allaah, nataraji rahmah Zako, usinitegemeze  kwenye nafsi yangu japo kwa muda wa upepesa jicho, na Unitengenezee mambo yangu yote, hapana Muabudiwa wa haki ila Wewe

 

[Hadiyth ya Abu Bakr Nafiy’ bin Haarith Ath-Thaqafiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) - Abu Daawuwd (4/324) [5090], Ahmad (5/42),  ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy  katika Swahiyh Abi Daawuwd (3/959) ]

 

 

 

Share

077-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Rahmah Ya Allaah Itakayokutosheleza Usimtegemee Yeyote Ila Allaah

 

Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

Kuomba Rahmah Ya Allaah Itakayokutosheleza Usimtegemee Yeyote Ila Allaah

 

 Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ مَالِكُ الْمُلْكِ، تُؤْتِي الْمُلْكَ مَنْ تَشَاءُ، وَتَنْزِعُ الْمُلْكَ مِمَّنْ تَشَاءُ، وَتُعِزُّ مَنْ تَشَاءُ، وَتُذِلُّ مَنْ تَشَاءُ، بِيَدِكَ الْخَيْرِ إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، رَحْمَانُ الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، تُعْطِيهُمَا مَنْ تَشَاءُ، وَتَمْنَعُ مِنْهُمَا مَنْ تَشَاءُ، ارْحَمْنِي رَحْمَةً تُغْنِينِي بِهَا عَنْ رَحْمَةِ مَنْ سِوَاكَ

Allaahumma Maalikul-Mulki Tu-til-mulka man Tashaau wa Tanzi’ul-mulka mimman Tashaau, wa Tu’izzu man Tashaau, Biyadikal-khayri Innaka ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, Rahmaanud-duniyaa wal-Aakhirah, Tu’twiyhumaa man Tashaau wa Tamna’u minhumaa man Tashaau, Irhamniy Rahamatan tughniyniy bihaa ‘an Rahmatin man siwaaka.

 

Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, khayr imo Mkononi Mwako.  Hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza. Mwingi wa rahmah duniani na Aakhirah Mwenye kurehemu, Unampa rahmah mbili hizo Umtakaye na Unamnyima Umtakaye. Nirehemu rahmah itakayonitosheleza kwayo rahmah isiyotoka kwa mwengine isipokuwa Wewe

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Mu’aadh (Radhwiya Allaahu 'anhu): ((Je, nikufundishe duaa ambayo ukiiomba basi ikiwa una deni mfano wa mlima wa Uhud, Allaah Atakukidhia.  Sema ya Mu’aadh: “Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote……[Hadiyth Hasan - Swahiyh At-Targhiyb (1821)]

 

 

 

 

Share

078-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Msamaha, Al-'Aafiyah Duniani Na Aakhirah Kuhifadhiwa Kila Pande

 

Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

Kuomba Msamaha, Al-'Aafiyah Duniani Na Aakhirah

Kuhifadhiwa Kila Pande

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في الدُّنْـيا وَالآخِـرَة، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في ديني وَدُنْـيايَ وَأهْـلي وَمالـي، اللّهُـمَّ اسْتُـرْ عـوْراتي وَآمِـنْ رَوْعاتـي، اللّهُـمَّ احْفَظْـني مِن بَـينِ يَدَيَّ وَمِن خَلْفـي وَعَن يَمـيني وَعَن شِمـالي، وَمِن فَوْقـي، وَأَعـوذُ بِعَظَمَـتِكَ أَن أُغْـتالَ مِن تَحْتـي

 

Allaahumma inniy as-alukal ‘aafiyah fid-dun-yaa wal Aakhirah. Allaahumma inni as-alukal ‘afwa wal ‘aafiyata fiy Diyniy wa dun-yaaya, wa ahliy, wa maaliy. Allaahumma-stur ‘awraatiy, wa-aamin raw’aatiy. Allaahumma-hfadhwniy min bayni yadayya, wamin khalfiy, wa ‘an yamiyniy, wa ‘an shimaaliy, wamin fawqiy, wa a’uwdhu bi’adhwamatika an ughtaala min tahtiy

 

Ee Allaah, hakika nakuomba msamaha na Al’-Aafiyah (hifadhi ya kila shari, amani, salama) duniani na Aakhirah. Ee Allaah, hakika nakuomba msamaha na Al’-Aafiyah katika Dini na dunia yangu, na ahli wangu, na mali yangu. Ee Allaah nisitiri aibu zangu na nitulize khofu yangu. Ee Allaah, nihifadhi mbele yangu, na nyuma yangu, na kulia kwangu, na kushoto kwangu, na juu yangu, na najikinga kwa Uadhimu Wako kwa kutekwa chini yangu.

 

Miongoni mwa duu’aa alizokuwa akiomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika nyiradi za asubuhi na jioni. 

 

[Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ’anhu) Swahiyh Ibn Maajah (2/332), Swahiyh Abiy Daawuwd (5074)].  

 

 

Share

079-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Kinga Ya Jirani Na Mke Au Mume Muovu, Mwana Anayedhibiti, Rafiki Khaini

 

Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Kuomba Kinga Ya Jirani Na Mke Au Mume Muovu, Mwana Anayedhibiti, Rafiki Haini.

 

  Alhidaaya.com

 

 

اللَّهُمَّ إنِّي أّعُوذُ بِكَ مِنْ جَارِ السُّوءِ، وَمِنْ زَوْجٍ تُشَيِّبُنِي قَبْلَ المَشِيبِ، وَمِنْ وَلَدٍ يَكُونُ عَليَّ رَبّاً، وَمِنْ مَالٍ يَكُونُ عَلَيَّ عَذَابَاً، وَمِنْ خَلِيْلٍ مَاكِرٍ عَيْنُهُ تَرَانِي، وَقَلْبُهُ يَرْعَانِي؛ إِنْ رَأَى حَسَنَةً دَفَنَهَا، وَإِذَا رَأَى سَيِّئَةً أَذَاعَهَا 

 الطبراني في الدعاء، 3/ 1425، برقم 1339، وهناد في الزهد، برقم 1038، وقال الألباني في سلسلة الأحاديث الصحيحة، 7/ 377، برقم 3137 :  قلت: وهذا إسناد جيد، رجاله كلهم من رجال التهذيب

Allaahumma inniy a’uwdhu Bika min jaaris-suw-i, wa min zawjin tushayyibuniy qablal-mashiybi, wa min waladin yakuwnu ‘alayya rabban, wamin maalin yakuwnu ‘alayya ‘adhaaban, wamin khaliylin ‘aynuhuu taraaniy wa qalbuhu yar’aaniy, in raa hasanah dafanahaa, wa idhaa raa sayyiah adhaa’ahaa

 

Ee Allaah, najikinga Kwako kutokana na jirani muovu, na kutokana na mke au mume atakayenisababisha uzee kabla ya uzee, na kutokana mwana atakayekuwa ni bwana kwangu anayenidhibiti, na kutokana na mali itakayokuwa ni adhabu kwangu, na kutokana na rafiki mwandani khaini; ambaye macho yake yananitazama lakini huku moyo wake unaniangaza kwa hila kiasi kwamba anapoona zuri  hulificha, lakini  anapoliona baya hulitangaza.

 

 [Atw-Twabaraaniy katika Ad-Du’aa (3//1425) [1339] na Hunaad katika Az-Zuhd (1038) na Al-Albaaniy amesema katika As-Silsilat Asw-Swahiyhah (7/377) [3137]:  Nimesema hii ni Isnaad nzuri, watu wake wote ni katika watu wa kuaminika]

 

 

 

Share