003-Aal-'Imraan: Aayah Na Mafunzo

 

 

 

 

003-Aal-'Imraan

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Share

000-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Suwratul-'Imraan

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Fadhila Za Suwratul-‘Imraan

 

 

Hadiyth Ya Kwanza:

 

عن النَّوَّاسَ بْنَ سَمْعَانَ قال: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((يُؤْتَى بِالْقُرْآنِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَهْلِهِ الَّذِينَ كَانُوا يَعْمَلُونَ بِهِ تَقْدُمُهُ سُورَةُ الْبَقَرَةِ وَآلُ عِمْرَانَ وَضَرَبَ لَهُمَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ثَلاثَةَ أَمْثَالٍ مَا نَسِيتُهُنَّ بَعْدُ قَالَ كَأَنَّهُمَا غَمَامَتَانِ أَوْ ظُلَّتَانِ سَوْدَاوَانِ بَيْنَهُمَا شَرْقٌ أَوْ كَأَنَّهُمَا حِزْقَانِ مِنْ طَيْرٍ صَوَافَّ تُحَاجَّانِ عَنْ صَاحِبِهِمَا)) 

Amesimulia An-Nawwaas bin Sam-‘aan (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Siku ya kufufuliwa, Qur-aan na watu waliokuwa wakiisoma na kutekeleza mafunzo yake, wataletwa mbele wakitangulizwa na Suwratul-Baqarah na Aal-‘Imraan.” Akasema An-Nawwaas: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoa mifano mitatu kwa Suwrah mbili hizi na sikusahau mifano hiyo tokea wakati huo. Alisema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Zitakuja kama mawingu mawili au vivuli viwili vyeusi kati yake kuna nuru, au makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao wakiruka. Zitawatetea watu wake (wanaoshikamana nazo).” [Muslim]

 

 

Hadiyth Ya Pili:

 

عن أبي أمامة رضي الله عنه  قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((اقْرَءُوا الْقُرْآنَ فَإِنَّهُ يَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ شَفِيعًا لِأَصْحَابِهِ ، اقْرَءُوا الزَّهْرَاوَيْنِ، الْبَقَرَةَ وَسُورَةَ آلِ عِمْرَانَ فَإِنَّهُمَا تَأْتِيَانِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كَأَنَّهُمَا غَمَامَتَانِ، أَوْ كَأَنَّهُمَا غَيَايَتَانِ، أَوْ كَأَنَّهُمَا فِرْقَانِ ، مِنْ طَيْرٍ صَوَافَّ، تُحَاجَّانِ عَنْ أَصْحَابِهِمَا، اقْرَءُوا سُورَةَ الْبَقَرَةِ فَإِنَّ أَخْذَهَا بَرَكَةٌ وَتَرْكَهَا حَسْرَةٌ وَلَا تَسْتَطِيعُهَا الْبَطَلَةُ)) مسلم

Amesimulia Abuu Umaamah Al-Baahiliy (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Someni Qur-aan kwani itakuja Siku ya Qiyaamah ikiwa ni shafaa’ah (kiombezi) kwa watu wake wanaoisoma na kutekeleza (amri zake). Someni taa mbili: Al-Baqarah na Aal-‘Imraan kwani zitakuja Siku ya Qiyaamah kama kwamba ni maumbile ya mawingu, au sehemu mbili za mawingu, au makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao wakiruka. Zitawatetea watu wake (walioshikamana nazo) siku hiyo. Someni Suwratul-Baqarah, kwani kushikamana nayo ni baraka, na kuiacha kwake ni khasara na majuto, na wachawi hawawezi kuihifadhi kwa moyo.” [Muslim (804)] 

 

 

Share

006-Aayah Na Mafunzo: Mambo Manne Huandikiwa Mwana Aadam Baada Ya Kutiwa Roho Tumboni

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Mambo Manne Huandikiwa Mwana Aadam Baada Ya Kutiwa Roho Tumboni

www.alhidaaya.com

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦﴾

6. Yeye Ndiye Aliyekusawirini umbo katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote

.

 

Mafunzo:

 

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم -وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ: ((إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَمْ سَعِيدٍ؛ فَوَاَللَّهِ الَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا. وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا)) رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: “Ametusimulia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake).  Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. Wa-Allaahi naapa kwa Yule Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye ‘amali za watu wa Jannah hadi ikawa baina yake na Jannah ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja wenu hufanya ‘amalii za watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

007-Aayah Na Mafunzo: Halaal Na Haraam Imebainika Baina Yake Ni Yenye Shubha

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Halaal Na Haraam Imebainika Baina Yake Ni Yenye Shubha

www.alhidaaya.com

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٧

7. Yeye Ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu humo mna Aayaat zenye maana wazi, hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo zisizokuwa wazi maana zake. Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu hufuata zile zisizokuwa wazi maana zake kutafuta fitnah (upotofu) na kutafuta maana zake zilofichika, na hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah. Na wenye msingi madhubuti katika elimu husema: “Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Rabb wetu.” Na hawakumbuki ila wenye akili

 

Mafunzo:

 

Aayaat Muhkamaat: Ni Aayaat ambazo maana zake zinafahamika kiwepesi, hazina mushkila wala utata, na dalili zake ziko wazi. 

 

Aayaat Mutashaabihaat: Ni Aayah ambazo ni ngumu kufahamika, na zinawatatanisha baadhi ya watu wasio na ‘ilmu ya kutosha

 

 

Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliisoma Aayah hii: “Yeye Ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu …” mpaka mwisho wa Aayah, kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Ee ‘Aaishah! Pindi utakapowaona wale ambao wanafuata zile Aayaat ambazo haziko wazi zaidi, basi fahamu kuwa hao ndio wale ambao Allaah Amewataja katika hii Aayah, basi tahadharini nao.” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Na pia,

 

عَن النُّعْمَانَ بْنَ بَشِيرٍ (رضي الله عنهما) قَال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:  ((الْحَلاَلُ بَيِّنٌ وَالْحَرَامُ بَيِّنٌ, وَبَيْنَهُمَا مُتَشَابِهَاتٌ لاَ يَعْلَمُهَا كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ, فَمَنْ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ اسْتَبْرَأَ  لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ,  وَمَنْ وَقَعَ فِي الشُّبُهَاتِ وَقَعَ فِي الْحَرَامِ,  كَالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الْحِمَى َيُوشِكُ أَنْ يَرْتَعْ فِيهِ, أَلاَ وَإِنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمًى,  أَلاَ وَإِنَّ حِمَى اللَّهِ مَحَارِمُهُ, أَلاَ وَإِنَّ فِي الْجَسَدِ مُضْغَةً إِذَا صَلَحَتْ صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّه, وَإِذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ أَلاَ وَهِيَ الْقَلْبُ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa An-Nu’maan bin Bashiyr (رضي الله عنهما) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Hakika halali iko wazi na haramu iko wazi. Baina ya mawili hayo mna yenye kutia shaka. Wengi miongoni mwa watu hawayajui. Basi atakayejiepusha yenye kutia shaka, atakuwa amejiepushia shaka katika Dini yake na heshima yake. Na Atakayetumbukia katika yenye kutia shaka, ataingia kwenye haramu. Kama mchunga anayechunga kando ya mipaka, ni haraka kulisha humo [mpaka mwingine wa watu]. Zindukeni!  Kila mfalme ana mipaka. Zindukeni! Kwa yakini mipaka ya Allaah ni haramu Alizoziharamisha. Zindukeni! Kwa yakini katika mwili mna kinofu [cha nyama], kinapokuwa sahihi, mwili wote unakuwa sahihi. Kinapoharibika, mwili wote unaharibika. Zindukeni! Kinofu hicho ni moyo)). [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Share

017-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Kuomba Maghfirah Kabla Ya Alfajiri

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Fadhila Za Kuomba Maghfirah Kabla Ya Alfajiri

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):

الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ﴿١٧﴾

17. Wenye kusubiri na wasemao kweli, na watiifu, na watoaji mali katika njia ya Allaah na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri. [Aal-'Imraan: 17]

 

Mafunzo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ، مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ، مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ)) البخاري و مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu)  kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Huteremka (kwa namna inavyolingana na utukufu Wake) kila siku katika mbingu ya dunia inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba du’aa Nimuitike? Nani Ananiomba jambo Nimpe? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na Allaah ('Azza wa Jalla) Anasema pia kuhusu fadhila za kuomba maghfirah kabla ya Alfajiri katika Suwrah ya Adh-Dhaariyaat:

 

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿١٥﴾

 Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na chemchemu. 

 

 

آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ﴿١٦﴾

Wakichukua yale Atakayowapa Rabb wao. Hakika wao walikuwa kabla ya hapo ni wahisani.

 

كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ﴿١٧﴾

Walikuwa kidogo tu katika usiku wakilala kwa raha. 

 

وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿١٨﴾

Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfirah.

[Adh-Dhaariyaat: 15-18]

 

 

Share

020-Aayah Na Mafunzo: Asiyemuamini Nabiy Katika Ahlil-Kitaabi Ataingia Motoni

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Asiyemuamini Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Ahlil-Kitaabi Ataingia Motoni

www.alhidaaya.com

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa);

 

فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّـهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ ۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْأُمِّيِّينَ أَأَسْلَمْتُمْ ۚ فَإِنْ أَسْلَمُوا فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠﴾

20. Na wakikuhoji, basi sema: “Nimejisalimisha kwa Allaah na ambao walionifuata” Na waambie waliopewa Kitabu na wasiojua kusoma na kuandika: “Je, mmesilimu?” Wakisilimu basi wameongoka, na wakikengeuka basi hakika juu yako ni kubalighisha. Na Allaah ni Mwenye kuwaona waja.

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi mwake, hatosikia yeyote yule kuhusu mimi katika Ummah huu; Yahudi wala Naswara, kisha akafariki bila ya kuamini kwa yale ambayo nimetumwa nayo, isipokuwa basi atakuwa miongoni mwa watu wa motoni.” [Al-Bukhaariy].

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema pia:  “Na alikuwa Nabiy akitumwa kwa watu wake pekee lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.”

 

 

Share

031-Aayah Na Mafunzo: Mkiwa Mnampenda Allaah Basi Mfuateni Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Mkiwa Mnampenda Allaah Basi Mfuateni Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): 

www.alhidaaya.com

 

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

Mafunzo:

 

Aayah hii tukufu inathibitisha kuwa mapenzi ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hayawezi kutimia isipokuwa kwa kufuta Sunnah zake. Ni hoja ya wazi pia kwa wanaodai kuwa wanampenda Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) lakini wakawa wanafanya bid’ah katika Dini kama kusoma Mawlid, Khitmah, Talqiyn, mikusanyiko ya kuomba Du’aa, kusheherekea maadhimisho na kumbukumbu za miaka, kusherehekea siku wanazosherehekea   wasiokuwa Waislamu, na yote mengineyo yasiyokuwemo katika Shariy’ah. Yeye mwenyewe Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameonya katika Hadiyth aliyosimulia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba: “Atakayetenda ‘amali isiyokuwa yetu (katika Dini yetu) basi itarudishwa.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Na katika Hadiyth iliyopokelewa na ‘Abdu-Rahmaan bin Quraad (رضي الله عنه) kuwa “Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anatawadha, na Swahaba wakaanza kukinga maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka katika wudhuu wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), wakijifutia katika miili yao kutafuta baraka za wudhuu ule wa Nabiy.  Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawauliza: “Kwa nini mnafanya hivi?” Wakasema; ni kwa ajili ya kumpenda Allaah na Rasuli Wake. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaambia: “Anayetaka kumpenda Allaah na Rasuli Wake, au kupendwa na Allaah na Rasuli Wake, basi aseme ukweli anapozungumza, na atekeleze amana yake anapoaminiwa, na awe jirani mwema kwa jirani yake.” [Mishkaatul Maswaabiyh – Imaam Al-Albaaniy]

 

Share

042-Aayah Na Mafunzo: Wanawake Wanne Walio Bora Kabisa

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Wanawake Wanne Walio Bora Kabisa

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَاكِ عَلَىٰ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ ﴿٤٢﴾

42. Na pale waliposema Malaika: “Ee Maryam! Hakika Allaah Amekuteua na Amekutakasa na Amekukhitari juu ya wanawake wa walimwengu.”

 

Mafunzo:

 

Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wanaume wengi wamekamilika, na hawakukamilika katika wanawake  ila  Aasiyah mke wa Fir’awn, na Maryam bint ‘Imraan. Na hakika ubora wa ‘Aaishah kwa wanawake ni kama ubora wa thariyd katika chakula.” [Aswhaabus-Sunan isipokuwa Abuu Daawuwd].

 

Thariyd ni mikate mikavu iliyokatwa katwa na kumwagiwa supu ya nyama chakula kimojawapo alichokuwa akikipenda sana Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).  

 

 

Kufadhilishwa ‘Aaishah (Radhwiya Alllaahu ‘anhaa) juu ya wanawake wengine

 

 

عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (( كَمَلَ مِنَ الرِّجَالِ كَثِيرٌ، وَلَمْ يَكْمُلْ مِنَ النِّسَاءِ إِلاَّ مَرْيَمُ بِنْتُ عِمْرَانَ، وَآسِيَةُ امْرَأَةُ فِرْعَوْنَ، وَفَضْلُ عَائِشَةَ عَلَى النِّسَاءِ كَفَضْلِ الثَّرِيدِ عَلَى سَائِرِ الطَّعَامِ ))‏

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wanaume wengi wamefikia daraja ya ukamilifu lakini hakuna mwanamke aliyefikia daraja hiyo isipokuwa Aasiyah mke wa Fir'awn, na Maryam bint 'Imraan. Na ubora wa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwa wanawake wengine ni kama mfano wa ubora wa thariydkwa vyakula vingine.” [Al-Bukhaariy na wengineo]

 

Share

046-Aayah Na Mafunzo: Watoto Watatu Ambao Waliongea Wakiwa Wachanga

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Watoto Watatu Ambao Waliongea Wakiwa Wachanga

www.alhidaaya.com

 

 

Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَيُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا وَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٤٦﴾

46. Na Atawasemesha watu katika utoto wake na utu uzima wake na ni miongoni mwa Swalihina.

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hawakuongea watoto wachanga isipokuwa watatu; ‘Iysaa na (kisa cha Jurayj katika Baniy Israaiyl, na kisha cha farisi mzuri ambaye mama wa mtoto aliyeongea utotoni alitamani mwanawe awe kama yeye, lakini mtoto akatamka kukataa…” [Al-Bukhaariy (3436)].

 

Share

054-Aayah Na Mafunzo: Allaah Hana Sifa Ya Makri Isipokuwa Ni Kulipiza

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Allaah Hana Sifa Ya Makri Isipokuwa Ni Kulipiza

www.alhidaaya.com

 

Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu makafiri: 

 

وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ ﴿٥٤﴾

54. Na wakapanga makri lakini Allaah Akapanga kulipiza makri. Na Allaah ni Mbora wa kulipiza mipango ya makri.

 

 

Mafunzo:

 

Sifa ya makri (njama) huthibitishwa kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa njia ya muqaabalah (yaani, ukipanga mabaya, Naye Ataamiliana nawe kwa ubaya, na ubaya utakurudia mwenyewe. Na ukipanga mazuri, Naye Ataamiliana nawe kwa uzuri, Atakusaidia na kukulipa mema). Na Sifa hii kama zilivyo zingine, huthibitishwa kwa Allaah kwa maana inayoendana na kulaikiana na Allaah (عزّ وجلّ). Kwa hiyo, Allaah Anamfanyia makri (njama) yule anayestahiki na pia yule ambaye anawafanyia makri waja Wake.

 

Hali kadhaalika kumfanyia Allaah (عزّ وجلّ) au waja Wake istihzai, kudhihaki na aina yoyote ya shutuma kama kudai kwamba Mkono wa Allaah umefumbwa (5:64) na mengineyo, basi Allaah Naye Huwarudishia shutuma zao.

 

 

Share

055-Aayah Na Mafunzo: Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam) Hakufa Na Atateremka Duniani Awe Katika Alama Kubwa Za Qiyaamah

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam) Hakufa

Na Atateremka Duniani Awe Katika Alama Kubwa Za Qiyaamah

www.alhidaaya.com

 

Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا وَجَاعِلُ الَّذِينَ اتَّبَعُوكَ فَوْقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۖ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأَحْكُمُ بَيْنَكُمْ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٥٥﴾ 

55.  Pale Allaah Aliposema: Ee ‘Iysaa! Hakika Mimi Nitakuchukua na Nitakupandisha Kwangu na Nitakutakasa na wale waliokufuru na Nitawafanya wale waliokufuata (kujisalimisha kwa Allaah) kuwa juu ya wale waliokufuru mpaka Siku ya Qiyaamah, kisha Kwangu ndio marejeo yenu Nitahukumu baina yenu katika yale mliyokuwa mkikhitilafiana[Aal-'Imraan: 55]

 

Mafunzo:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Alimnyanyua Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) kuelekea mbinguni akiwa hai, na wala hakuuliwa kabla ya hapo. Na atakuja kuteremka duniani zama za mwisho, na atamuua Masiyh Ad-Dajjaal, na atawaua nguruwe wote, na atavunja misalaba yote na ataondosha kodi, na hatokubali isipokuwa Uislamu, na atahukumu kwa shariy’ah ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). [Dalili katika Suwrat An-Nisaa (4:157-159)]

 

Aayah hii tukufu ni dalili ya wazi kwa wanaodai kwamba neno la مُتَوَفِّيكَ lina maana “kukufisha kikamilifu.”  Neno hilo hilo Amelitaja Allaah (سبحانه وتعالى) katika (Al-An’aam (6:60), Az-Zumar (39:42):

 

وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ

Naye Ndiye Anayekufisheni usiku (mnapolala) na Anajua yale yote mnayoyafanya mchana, kisha Anakufufueni humo ili utimizwe muda maalumu uliokadiriwa. [Al-An'aam (6:60)]

 

Na pia:

 

اللَّـهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا ۖ فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَىٰ عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَىٰ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ

Allaah Huzichukua roho wakati wa kufa kwake; na zile zisizokufa katika usingizi wake, kisha Huzizuia ambazo Amezikidhia mauti, na Huzirudisha nyingine mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Hakika katika hayo bila shaka kuna ishara kwa watu wanaotafakari. [Az-Zumar (39:42)]

 

Hapo tunafahamu kwamba, mtu anapolala anachukuliwa au anafishwa usingizini na kurudishwa katika uhai kwa kuwa roho yake inachukuliwa na ndio inayojulikana kuwa ni Al-Mawt As-Sughraa (mauti madogo). Kwa dalili pia kutoka katika mafunzo ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika nyiradi za kulala na kuamka tuwe tunasema:

 

بِاسْـمِكَ اللّهُـمَّ أَموتُ وَأَحْـيا

Kwa Jina Lako Ee Allaah ninakufa na ninakuwa hai.

 

الحَمْـدُ لِلّهِ الّذي أَحْـيانا بَعْـدَ ما أَماتَـنا وَإليه النُّـشور

Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Ametupa uhai baada ya kutufisha na Ni Kwake tu kufufuliwa.

 

Na Hadiyth zimethibitisha mojawapo ni:

 

Abuu Huraryah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, anakaribia kukuteremkieni Ibn Maryam hali ya kuwa hakimu muadilifu. Atavunja misalaba, ataua nguruwe, na hatopokea kodi, na mali zitazidi mpaka haikubali yoyote. Na itakuwa sijdah moja ni bora zaidi kuliko dunia nzima na vilivyomo ndani yake. Kisha Abuu Hurayrah akasema: Mkipenda someni:

 

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا ﴿١٥٩﴾

“Na hakuna yeyote katika Watu wa Kitabu ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.” [Al-Bukhaariy (3448), Aayah; Suwratun-Nisaa (4:159)].

 

 

 

 

 

Share

080-Aayah Na Mafunzo: Makatazo Ya Kupinduka Mipaka Kumtukuza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Makatazo Ya Kupinduka Mipaka Kumtukuza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُم بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨٠﴾ 

80. Na wala hakuamuruni kuwachukua Malaika na Manabii kuwafanya miola. Je, anakuamrisheni ukafiri baada ya nyinyi kuwa mmejisalimisha kwa Allaah? [Aal-'Imraan: 80]

 

Mafunzo:

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekataza kutukuzwa kupindukia kiasi amesema: “Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi na mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Rasuli Wake)) [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

Share

081-Aayah Na Mafunzo: Uthibitisho Kuwa Khidhr Hayuko Hai

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Uthibitisho Kuwa  Khidhr Hayuko Hai

www.alhidaaya.com

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨١﴾

81. Na pindi Alipochukua Allaah fungamano kwa Manabii (akawaambia) “Kwa yale niliyokupeni kutoka kitabu na hikmah, kisha akakujieni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi; ni juu yenu kumwamini na kumnusuru.” (Kisha Allaah): Akasema “Je, mmekiri na mmekubali kuchukua juu ya hayo fungamano zito Langu?” Wakasema: “Tumekiri.” (Allaah) Akasema: “Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia.”

 

Mafunzo:

 

Aayah hii ni miongoni mwa dalili za kufariki kwa Khidhwr (عليه السلام) na kuwa yeye amekwishakufa na si kama wanavyodai Masufi kuwa Khidhwr yupo hai,  na  lau kama angelikuwa yupo hai basi angesimama kumnusuru Nabiy Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kauli na matendo.

Share

085-Aayah Na Mafunzo: Jibriyl ('Alayhis-Salaam) Amekuja Kukufundisheni Dini Yenu

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Jibriyl ('Alayhis-Salaam) Amekuja Kukufundisheni Dini Yenu

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika. [Aal-'Imraan: 85]

 

 

 

Mafunzo:

 

Umar (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Siku moja tulikuwa tumekaa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hapo alitokea mtu ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaweka magoti yake karibu na magoti yake na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ee Muhammad! Niambie kuhusu Uislamu.  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Uislamu ni kukiri laa ilaaha illa Allaah na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah. Na kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kufunga Swiyaam Ramadhwaan na kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.” (Akasema yule mtu yaani Jibriyl) Umesema kweli. Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza kwake Rasuli na kumsadikisha.  Na akasema tena: Niambie kuhusu Iymaan.  Akasema “Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Rasuli Wake na Siku ya Qiyaamah, na kuamini ya kuwa kheri na shari zinatoka Kwake.” (Akasema Jibriyl): Umesema kweli. Akasema hebu nielezee kuhusu Ihsaan.  Akasema: “Ni kumuabudu Allaah kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona” Akasema (Jibriyl):  Niambie    kuhusu Qiyaamah.  Akajibu: “Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile Muulizaji.” Kisha akamwambia: Nijulishe alama zake: Akajibu: “Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga wenda miguu chini, wenda uchi (wasio na uwezo wa kumiliki hata mavazi), mafukara (wasiokuwa hata na sehemu ya kuishi kwa umaskini) wakishindana kujenga majumba ya fahari.” Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo (nikitafakari). Kisha akasema: “Ee 'Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza?” Nikasema: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi.  Akasema: “Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha Dini yenu.” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

Share

086-Aayah Na Mafunzo: Tawbah Baada Ya Kuritadi Inakubalika

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Tawbah Baada Ya Kuritadi Inakubalika

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa):

 

كَيْفَ يَهْدِي اللَّـهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٦﴾ 

86. Vipi Allaah Atawaongoza watu waliokufuru baada ya kuamini kwao na wakashuhudia kwamba Rasuli ni haki na zikawajia hoja bayana? Na Allaah Hawaongozi watu madhalimu.

 

 أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُمْ أَنَّ عَلَيْهِمْ لَعْنَةَ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿٨٧﴾

87. Hao jazaa yao ni kwamba juu yao ipo laana ya Allaah na ya Malaika na ya watu wote.

 

خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٨٨﴾

88. Wenye kudumu humo hawatopunguziwa adhabu wala hawatopewa muda wa kuakhirishwa adhabu.

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٨٩﴾

89. Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengenea, basi hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

Mafunzo:

 

Aayah hizi (3: 86-89) ziliteremka kuhusu mtu mmoja katika Answaar ambaye alisilimu kisha akaritadi na akaingia katika shirki kisha akajuta kwa hilo tendo lake la kuritadi. Akatuma watu wake ili wamtumie ujimbe wa swali kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa je, hivi anaweza kuleta tawbah kwa tendo lake hilo? Kisha baada ya swali hilo kuulizwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zikateremka hizo Aayaat, akatumiwa, akasilimu [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) imepokelewa aathaar hii na Ibn Jariyr, na pia imesimuliwa na Ahmad, Ibn Hibbaan na wengineo na ameiwafiki Adh-Dhahabiy na Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah (3066)].

 

 

 

Share

090-Aayah Na Mafunzo: Sababu Ya Kuteremshwa Aayah Kuhusu Walioritadi Na Kurudia Tena

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Sababu Ya Kuteremshwa Aayah Kuhusu Walioritadi Na Kurudia Tena

 

 

 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ ﴿٩٠﴾ 

90. Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru; haitokubaliwa tawbah yao, na hao ndio waliopotoka.

 

Mafunzo:

 

Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremshwa kuhusu watu waliosilimu kisha wakaritadi kisha wakasilimu tena kisha wakaritadi. Wakatuma watu wao kuuilizia kuhusu jambo hili wakamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha hapo ikateremka Aayah hii: “Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru; haitokubaliwa tawbah yao, na hao ndio waliopotoka.” (3: 90)  [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameipokea Al-Haafidhw Abuu Bakr Al-Bazzaar – Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

 

 

Share

091-Aayah Na Mafunzo: Mtu Wa Motoni Atatamani Kufidia Dhahabu Ya Ujazo Wa Duniani

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Mtu Wa Motoni Atatamani Kufidia Dhahabu Ya Ujazo Wa Duniani

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Taa'alaa):

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾

91. Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao dhahabu ya ujazo wa dunia nzima lau wakitaka kujifidia nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru.

 

 

Mafunzo:

 

Anas (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ataitwa mtu katika watu wa Jannah, kisha Allaah Atamuuliza: Ee mwana Aadam! Umeonaje makazi yako? Atasema: Yaa Rabb! Hakika ni makazi bora kabisa. Allaah Atasema: Omba na tamani (utakalo)! Atasema: Hakuna ninaloomba au kutamani isipokuwa Unirudishe duniani nipigane katika njia Yako mara kumi – kutokana fadhila anazoziona za waliokufa mashahidi. Kisha ataletwa mtu katika watu wa motoni Atasema: Ee mwana Aadam! Umeonaje makazi yako? Atasema: Yaa Rabb! Makazi maovu kabisa! Atasema: Je, unataka kufidia Kwangu dhahabu kwa ujazo wa dunia nzima? Atasema: Naam ee Rabbi! Atasema: Umeongopa! Kwani Nilikuomba la chini kuliko hilo na jepesi zaidi wala hukufanya! Atarudishwa motoni.” [Ahmad, As-Silsilah Asw-Swahiyhah (3008), Swahiyh Al-Jaami’ (7996)].

 

 

Share

092-Aayah Na Mafunzo: Mapendekezo Ya Kutoa Swadaqah Kitu Kilicho Kizuri

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Mapendekezo Ya Kutoa Swadaqah Kitu Kilicho Kizuri Na Mfano Wa Utoaji Wa Swahaba

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٩٢﴾

92. Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachotoa basi hakika Allaah kwacho ni Mjuzi.

 

Mafunzo:

 

 

Mapendekezo ya kutoa katika swadaqah kilicho kizuri, si kutoa kiichokuwa kibovu au kisichokuwa na thamani.  Anas bin Maalik (رضي الله عنه) kwamba: Abuu Twalhah alikuwa na mali kuliko yeyote miongoni mwa Answaar wa Madiynah na kilichokuwa kipenzi kabisa katika mali yake ni bustani ya Bayruhaa ambayo ilikuwa mbele ya Masjid Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Mara nyingine Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akienda katika bustani hiyo na kunywa maji yake baridi. Anas akaongeza kusema: Aayah hii ilipoteremka:

 

لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ

“Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda…” Abu Twalhah akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Allaah Anasema:

 

لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ

“Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda.” Na hakika bustani ya Bayruhaa ni kipenzi katika mali zangu. Kwa hiyo nataka kuitoa swadaqah kwa ajili ya Allaah nikitaraji wema wake na thawabu zake na malimbikizo kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Basi ee Rasuli wa Allaah! Itumie popote Anapokuonyesha Allaah kuwa ni bora kuitumia. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Umefanya vizuri, Ni mali yenye faida, ni mali yenye faida. Nimesikia ulivyosema na nafikiri itakuwa ni bora kuwapa walio karibu yako (jamaa zako).”  Abuu Twalhah akasema: Nitafanya hivyo ee Rasuli wa Allaah. Abuu Twalhah akagawa kwa jamaa zake na watoto wa ‘ammi yake. [Al-Bukhaariy, Muslim, Ahmad].

 

Share

096-Aayah Na Mafunzo: Masjid Al-Haraam Ni Ya Kwanza Kuanzishwa Duniani

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Masjid Al-Haraam Ni Ya Kwanza Kuanzishwa Duniani

Alhidaaya.com

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾ 

Hakika nyumba ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ‘ibaadah) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah), yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu. [Aal-'Imraan: 96]

 

Mafunzo:

 

Abuu Dharr (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Masjid gani ilijengwa ardhini mwanzo?  Akasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Masjid Al-Haraam (Makkah).” Kisha nikasema: Kishaupi? Akasema: “Masjid Al-Aqswaa (Palestina).” Nikasema: Kuna muda gani baina ya kuwepo Masjid mbili hizo? Akasema: “Miaka arubaini na popote itakapokudiriki Swalaah basi swali hapo pia ardhi ni mahala pa kuswali.” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

Share

102-Aayah Na Mafunzo: Hukmu Ya Kufutwa Enyi Walioamini Mcheni Allaah Kama Ipasavyo…

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan  

Hukmu Ya Kufutwa Enyi Walioamini Mcheni Allaah Kama Ipasavyo…

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٠٢﴾

 102. Enyi walioamini! Mcheni Allaah kama apasavyo kuogopwa na wala msife isipokuwa nyinyi (mmeshakuwa) ni Waislamu. [Aal-'Imraan: 102]

 

Mafunzo:

 

An-Naasikh Wal-Nasuwkh:  Aayah hii imefutwa hukmu yake kwa Aayah “Basi mcheni Allaah muwezavyo” [At-Taghaabun 64: 16]

 

Share

103-Aayah Na Mafunzo: Allaah Anaridhia Mshikamane Kwa Kamba Yake Msifarikiane

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Allaah Anaridhia Mshikamane Kwa Kamba Yake Msifarikiane

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٠٣﴾ 

103. Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Allaah juu yenu, pale mlipokuwa maadui (kati yenu); kisha Akaunganisha nyoyo zenu, mkawa kwa neema Yake ndugu; na mlikuwa ukingoni mwa shimo la moto Akakuokoeni humo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat Zake mpate kuongoka.

 

 

Mafunzo:

 

Maana Ya Kushikamana Na Kamba Ya Allaah Bila Kufarikiana.

 

Kushikamana na kamba ya Allaah bila ya kufarikiana   imekusudiwa kubakia katika Swiraatw Al-Mustaqiym [Rejea Al-Faatihah (1:6)] 

 

Na pia Kauli ya Allaah (عزّ وجلّ):

 

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٥٣﴾

Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa [Al-An’aam (6:153)]

 

Pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametahadharisho mno kuhusu kuthibitika katika Swiraatw Al-Mustaqiym ambayo inamaanisha kutokutoka nje na mafunzo ya Qur-aan na Sunnah. Miongoni mwa maonyo yake ni Hadiyth ifuatayo:

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Najiyh Al-‘Irbaadhw bin Saariyah (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitupa mawaidha mazito (yenye maana kubwa), nyoyo zikaogopa na macho yakabubujikwa machozi. Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Yanaonekana kama kwamba mawaidha ya kutuaga, basi tuusie.  Akasema: “Nakuusieni kuwa na taqwa ya Allaah na kusikiliza na kutii japokuwa mtaongozwa na mtumwa Mhabashi. Hakika atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona ikhtilaaf nyingi. Kwa hiyo, shikamaneni na Sunnah zangu na mwenendo wa Makhalifa waongofu, yashikilieni kwa magego [mambo yao]. Na tahadharini na mambo yenye kuzushwa, kwani kila uzushi ni upotovu.” [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh].

   

Na pia,

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Anawaridhia mambo matatu na Anachukia kwenu mambo matatu; Anawaridhia mumwabudu Yeye, wala msimshirikishe kwa chochote, na mshikamane nyote na kamba ya Allaah wala msifarikiane. Na anachukia kwenu uvumi, kuuliza sana na   kupoteza mali.” [Muslim, na katika riwayaah: “Na muwanasihi wenye kuwatawalia mambo yenu.” Swahiyh Adab Al-Mufrad (343)].

 

  

 

 

 

Share

104-Aayah Na Mafunzo: Umuhimu Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Umuhimu Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu

Alhidaaya.com

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفلِحُونَ ﴿١٠٤﴾

Na watokeze kutoka kwenu umati wa watu unaolingania kheri na unaoamrisha mema na unaokataza munkari. Na hao ndio waliofaulu. [Aal-'Imraan: 104]

 

Mafunzo:

 

Umuhimu Wa Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu:

 

Kuamrisha mema na kukataza maovu imesisitizwa katika Aayah kadhaa za Qur-aan na pia katika Sunnah imesisitzwa mno. Miongoni mwazo ni Hadiyth zifuatazo:

 

Hudhayfah bin Al-Yamaani (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake! Mtaamrisha mema na mtakataza maovu au sivyo Allaah Atakuleteeni adhabu kutoka Kwake, kisha mtamuomba wala Hatokuitikieni.” [Ahmad na At-Tirmidhy - Swahiyh At-Tirmdhiy (2169), Swahiyh Al-Jaami’ (7070)]

 

Pia: Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Atakayeona munkari (uovu) basi aubadilishe kwa mkono wake, na asipoweza basi kwa ulimi wake, na asipoweza basi kwa moyo wake (achukizwe) na huo ni udhaifu wa Iymaan.”  [Muslim]

 

 

 

Share

105-Aayah Na Mafunzo: Makundi Sabini Na Tatu Yataingia Motoni Isipokuwa Moja Tu.

 

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

 

Makundi Sabini Na Tatu Yataingia Motoni Isipokuwa Moja Tu

 

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٠٥﴾

Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na wakakhitilafiana baada ya kuwajia hoja bayana. Na hao watapata adhabu kuu. [Aal-'Imraan: 105]

 

Mafunzo:

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wamegawanyika Mayahudi katika mapote sabini na moja na wakagawanyika Manaswara katika mapote sabini na mbili na Ummah wangu utagawanyika mapote sabini na tatu. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu.” Maswahaba waliuliza: Ni lipi hilo ee Rasuli wa Allaah?  Akasema: “Ni lile nililokuwemo mimi na Maswahaba zangu.” [Ahmad, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ad-Daarimiy].

 

Share

110-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Ummah Wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

 Fadhila Za Ummah Wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):

 

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾

110. Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki.

 

Mafunzo:

 

Hadiyth kadhaa zimetajwa fadhila za Ummah huu wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi yake ni:

Mu’aawiyah bin Haydah Al-Qash-riyy  (رضي الله عنه) amehadithia kutoka kwa baba yake kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nyinyi mnakamilisha Ummah sabini. Nyinyi ndio mbora wao na ndio watukufu zaidi mbele ya Allaah (عزّ وجلّ).” [Ahmad, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Al-Haakim, na wengineo kwa riwaayah tofauti kidogo taz. Swahiyh Al-Jaami’ (2301), Swahiyh At-Tirmidhiy (3001)].

Pia rejea tanbihi (2: 213).

 

Na pia, Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Sisi (Waislamu) ni wa mwisho (kuja) na (tutakuwa) wa mwisho Siku ya Qiyaamah na wa mwanzo kuingia Jannah…” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

Share

113-Aayah Na Mafunzo: Sababu Ya Kuteremka Hawako Sawasawa Ahlil-Kitaab

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Sababu Ya Kuteremka Hawako Sawasawa Ahlil-Kitaab  

  

 

 

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾

113. Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).

 

يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٤﴾

114. Wanamwamini Allaah na Siku ya Mwisho na wanaamrisha mema na wanakataza munkari na wanakimbilia katika mambo ya kheri, na hao ni miongoni mwa Swalihina.

 

وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَن يُكْفَرُوهُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ ﴿١١٥﴾

115. Na kheri yoyote waifanyayo hawatokanushiwa (thawabu zake).  Na Allaah ni Mjuzi wa wenye taqwa.

Mafunzo:

 

 

Sababun-Nuzuwl: Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba: (Siku moja) Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) aliichelewesha Swalaah ya ‘Ishaa kisha akatoka kuja kuiswali Masjid akawakuta Maswahaba  (رضي الله عنهم)vado wamemsubiri akasema: “Uhakika wa mambo ulivyo hakuna yoyote katika Watu wa Dini hizi anayemdhukuru Allaah katika wakati huu asiyekuwa nyinyi.” Hapo ikateremka Aayah: Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi…” mpaka mwisho wa Aayah 115. [Hadiyth ya Ibn Mas’uwd ameipokea Al-Imaam Ahmad].

 

 

 

Share

118-Aayah Na Mafunzo: Kila Nabiy Au Khaliyfah Alikuwa Na Rafiki Mwandani Wawili

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Kila Nabiy Au Khaliyfah Alikuwa Na Rafiki Mwandani Wawili 

Alhidaaya.com

 

 

 Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١١٨﴾

118. Enyi walioamini! Msifanye rafiki mwandani na msiri (wenu) wasiokuwa nyinyi. Hawatoacha kukuharibieni. Wanatamani kama mngetaabika. Imekwishajitokeza bughudha kutoka midomoni mwao. Na yale yanayoficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Aayaat, (ishara, hoja, dalili) mkiwa mtatia akilini.

 

Mafunzo:

 

Abuu Sa’iyd (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Hakutuma Nabiy yeyote wala hakumweka Khaliyfah yeyote isipokuwa alikuwa na rafiki mwandani wawili; mmoja anayeamrisha ya kheri na kumsisitiza nayo, na mwengine akiamrisha maovu na kumchochea nayo. Na Al-Ma’swuwm (aliyehifahdiwa asikosee) ni ambaye ma’swuwm (amehifadhiwa asisokee) na Allaah.” [Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy].

Share

122-Aayah Na Mafunzo: Makabila Mawili Kufurahia Kuteremshwa Na Allaah Ni Mlinzi Wao

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Makabila Mawili Kufurahia Kuteremshwa Na Allaah Ni Mlinzi Wao

 

 

 

إِذْ هَمَّت طَّائِفَتَانِ مِنكُمْ أَن تَفْشَلَا وَاللَّـهُ وَلِيُّهُمَا ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٢٢﴾

122. Pale walipofanya wasiwasi makundi mawili miongoni mwenu kwamba watashindwa na Allaah ni Mlinzi na Msaidizi wao; basi kwa Allaah pekee na watawakali Waumini.

 

Mafunzo:

 

Sababun-Nuzuwl:: Aayah hii imeteremka ikiwazungumzia Banuw Salamah na Banuw Haarithah kama alivyohadhithia Jaabir (رضي الله عنه) kwamba: Aayah hii imeteremshwa kuhusu sisi nasi tulikuwa ni makabila mawili; Banuw Haarithah na Banuw Salamah tusingelipenda (kama isingeteremshwa) na Sufyaan kasema: Tusingefurahi kama isingeteremshwa na hali Allaah Anasema: “Na Allaah ni Mlinzi na Msaidizi wao.” [Amehadithia Jaabir (رضي الله عنه) ameipokea Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

Share

123-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya Badr

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

 Maana Ya Badr

Alhidaaya.com

Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):

 

وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ بِبَدْرٍ وَأَنتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢٣﴾

123. Kwa yakini Alikunusuruni Allaah katika Badr na hali nyinyi mlikuwa (kikosi) dhaifu. Basi mcheni Allaah mpate kushukuru.

 

Mafunzo:

 

Maana Ya Badr:

‘Ulamaa wametofautiana kuhusu maana ya jina hili ‘Badr’. Baadhi yao wamesema ni jina la mtu, na wengine wamesema ni jina la kisima. Sehemu hiyo iko baina ya Makkah na Madiynah, na umbali kati yake na Madiynah ni kilometa 150. Na Allaah ni Mjuzi zaidi

 

Share

128-Aayah Na Mafunzo: Tukio La Kuumizwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Vita Vya Uhud

 

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Tukio La Kuumizwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Vita Vya Uhud

Alhidaaya.com

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu. [Aal-'Imraan: 128]

 

 

Mafunzo:

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) kwamba: Alimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoinua kichwa chake kutoka rukuu’ ya mwisho ya Swalaah ya Alfajiri baada ya kusema:

سَمِعَ اَللَّهُ لِمَنْ حَمِدَه رَبَّنَا لَكَ اَلْحَمْدُ

“Sami’a-Allaahu liman hamidah Rabbanaa Lakal-Hamd.  

Allaah Amemsikia aliyemhimidi, Ee Rabb wetu, Himdi ni Zako Wewe

 

 

 Kisha akasema:

اللَّهُمَّ الْعَنْ فُلَانًا وفُلَانًا وفُلَانًا

“Allaahumma mlaani fulani na fulani na fulani.” Ikateremka:

 

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

 

Jambo hili halikuhusu wewe; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu. (3:128). [Al-Bukhaariy na wengineo kwa riwayaah nyenginezo]

 

 

Na Anas bin Maalik  (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Siku ya Uhud, jino la Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) lilivunjika na akachomwa mkuki begani mwake. Damu ikawa inamchirizika usoni mwake akawa anaifuta damu huku akisema: “Vipi watu watafaulu ikiwa wamerowanisha uso wa Nabiy wao kwa damu na hali yeye anawalingaia kwa Allaah?” Hapo ikateremka Aayah hii:

 

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

 

Jambo hili halikuhusu wewe; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu” (3: 128) [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh].

 

Share

133-Aayah Na Mafunzo: Unapoomba Jannah, Omba Jannatul-Firdaws

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Unapoomba Jannah Omba Jannatul-Firdaws

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ﴿١٣٣﴾ 

Na kimbilieni maghfirah kutoka kwa Rabb wenu na Jannah upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye taqwa.  [Aal-Imraan: 133]

 

Mafunzo:

 

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: إِنَّ فِي الْجَنَّةِ مِائَةَ دَرَجَةٍ أَعَدَّهَا اللَّهُ لِلْمُجَاهِدِينَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، مَا بَيْنَ الدَّرَجَتَيْنِ كَمَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ، فَإِذَا سَأَلْتُمُ اللَّهَ فَاسْأَلُوهُ الْفِرْدَوْسَ، فَإِنَّهُ أَوْسَطُ الْجَنَّةِ وَأَعْلَى الْجَنَّةِ، أُرَاهُ فَوْقَهُ عَرْشُ الرَّحْمَنِ، وَمِنْهُ تَفَجَّرُ أَنْهَارُ الْجَنَّةِ ‏"‏‏.‏  

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kuna daraja mia moja za Jannah ambazo Amezitayarisha Allaah kwa ajili ya Mujaahidiyn wanaopigana kwa ajili Yake. Baina ya sehemu moja na sehemu nyingine, ni masafa sawa ya baina ya ardhi na mbingu. Unapomuomba Allaah, muombe Al-Firdaws, kwa sababu ipo katikati ya Jannah na ni sehemu ya Juu kabisa (Msimuliajia amesema: Nadhani pia amesema: ”Juu yake kuna Arsh ya Ar-Rahmaan) na humo mnabubujika  mito ya Jannah.” [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share

134-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Anayezuia Ghadhabu

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Fadhila Za Anayezuia Ghadhabu

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa:)

 

الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾ 

Ambao wanatoa (kwa ajili ya Allaah) katika hali ya wasaa na katika hali ya shida, na wanazuia ghadhabu, na wenye kusamehe watu. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan. [Aal-'Imraan: 134]

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah  (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Aliye na nguvu si mwenye kushinda katika mieleka lakini mwenye nguvu ni ambaye anazuia nafsi yake kutokana na ghadhabu.” [Imaam Ahmad].

 

Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayezuia ghadhabu zake hali ya kuwa anaweza kuzidhihirisha, Allaah Atamwita huku wakishuhudia viumbe wote mpaka Ampe chaguo la Huwr (wanawake wazuri Jannah wenye macho mazuri) wowote awatakao.” [Ahmad].

 

 

 

Share

135-Aayah Na Mafunzo: Allaah Atakughufuria Madhambi Hata Kama Ukikariri Kumuasi

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Allaah Atakughufuria Madhambi Hata Kama Ukikariri Kumuasi

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾

135. Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua.

 

أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿١٣٦﴾

136. Hao jazaa yao ni maghfirah kutoka kwa Rabb wao na Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Na uzuri ulioje ujira wa watendaji (wema).  [Aal-'Imraan 135-136]

 

Mafunzo:

 

Hakika fadhila nyingi kabisa zimetajwa katika Qur-aan na Sunnah kuhusu kuomba tawbah, mojawapo: Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Mja alifanya dhambi akasema: Ee Allaah, nighufurie dhambi zangu. Allaah (عزّ وجلّ) Akasema: Mja wangu kafanya dhambi akajua kuwa anaye Rabb wa kumghufuria dhambi na kuziondosha. Kisha akarudia kufanya dhambi tena akasema: Ee Allaah nighufurie dhambi zangu. Allaah (Tabaaraka wa Ta’aala) Akasema: Mja wangu kafanya dhambi akajua kuwa anaye Rabb wa kumghufuria dhambi na kuziondosha. Kisha akarudia kufanya dhambi tena akasema: Ee Allaah nighufurie dhambi zangu. Allaah (عزّ وجلّ) Akasema: Mja wangu kafanya dhambi akajua kuwa anaye Rabb wa kumghufuria dhambi na kuziondosha. Nakushuhudisheni kwamba Nimemghufuria na afanye mja Wangu atakavyo.” [Ahmad].

 

 

Share

151-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Aliyopewa Nabiy Ni Kutiwa Kizaazaa Maadui Ili Waislamu Wapate Nusra

 

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

 

Miongoni Mwa Aliyopewa Nabiy Ni Kutiwa Kizaazaa Maadui Ili Waislamu Wapate Nusra

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

سَنُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ بِمَا أَشْرَكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا ۖ وَمَأْوَاهُمُ النَّارُ ۚ وَبِئْسَ مَثْوَى الظَّالِمِينَ ﴿١٥١﴾

151. Tutavurumisha kizaazaa katika nyoyo za waliokufuru kwa sababu ya kumshirikisha Allaah na ambayo Hakuyateremshia mamlaka. Na makazi yao ni moto, na ubaya ulioje maskani ya madhalimu

 

Mafunzo:

 

Pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipopigana vita pamoja na Swahaba zake dhidi ya makafiri, na idadi ya makafiri ilikuwa ni wengi mno kulikoni idadi ya Waislamu, Allaah (سبحانه وتعالى)  Aliwateremshia Waislamu miujiza kadhaa kuwasaidia waweze kupambana na makafiri na wapate ushindi. Mfano wa muujiza mmojawapo ni pale Allaah (سبحانه وتعالى) Alipowafanya makafiri wawaone Waislamu katika macho yao kuwa ni wa idadi kubwa ilhali ni wachache mno. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قَدْ كَانَ لَكُمْ آيَةٌ فِي فِئَتَيْنِ الْتَقَتَا ۖ فِئَةٌ تُقَاتِلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَأُخْرَىٰ كَافِرَةٌ يَرَوْنَهُم مِّثْلَيْهِمْ رَأْيَ الْعَيْنِ ۚ وَاللَّـهُ يُؤَيِّدُ بِنَصْرِهِ مَن يَشَاءُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّأُولِي الْأَبْصَارِ ﴿١٣﴾

Kwa hakika ilikuwa ni Aayah (ishara) kwenu katika makundi mawili; yalipokutana (vita vya Badr). Kundi linapigana katika njia ya Allaah na jingine ni makafiri ambao wanawaona (Waislamu) mara mbili yao kwa mtazamo wa macho. Na Allaah Humsaidia kwa nusura Yake Amtakaye. Hakika katika hayo bila shaka ni zingatio kwa wenye utambuzi. [Aal-‘Imraan: 13]

 

Hali kadhalika muujiza mwenginewe ni kutiwa kiwewe, kizaazaa, khofu kubwa nyoyoni mwa makafari, waogope na iwafanye wawe dhaifu na hivyo ushindi upatikane kwa Waislamu:

 

Abuu Huraryah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nimefadhilishwa juu ya Manabii kwa mambo sita: nimepewa; ‘Jawaami’al-Kalimi’ (mukhtasari unaojumuisha maneno mengi) na nimenusuriwa kwa (kutiwa) kizaazaa (katika nyoyo za maadui) na nimehalalishiwa ghanima na nimefanyiwa ardhi kuwa kitwaharishi na Masjid (mahali pa kuswali) na nimetumwa kwa viumbe wote, na Manabii wamekhitimishwa kwangu.” [Muslim].

 

 

 

 

 

 

 

Share

159-Aayah Na Mafunzo: Unyenyekevu Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kutaka Ushauri Kwa Swahaba

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Unyenyekevu Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kutaka Ushauri Kwa Swahaba

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾

Basi ni kwa rahmah kutoka kwa Allaah umekuwa mpole kwao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na lau ungelikuwa mjeuri mwenye moyo mgumu wangelitawanyika mbali nawe. Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali. [Aal-'Imraan: 159]

 

Mafunzo:

 

Upole na unyenyekevu wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) umetajwa mare tele katika Qur-aan na Sunnah, na rejea Aayah (9: 128).

 

Amri na pendekezo la kutafuta ushauri: Allaah  (سبحانه وتعالى) Amemuamrisha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) atake ushauri kwa Swahaba zake, naye (صلى الله عليه وآله وسلم) akawataka wamshauri katika hali kadhaa ili awatulize nyoyo zao. Na hili ni funzo kwamba ushauri ni jambo muhimu na pia mkubwa au mwenye cheo anaweza kutafuta ushauri kwa wadogo wake au walio duni yake.

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwataka ushauri Swahaba zake katika mambo mbali mbali, mfano;

 

  1. Aliwataka ushauri katika vita vya Badr kama kuteka msafara wa Abuu Sufyaan au kupigana vita wakamshauri kupigana vita.
  2. Aliwataka pia ushauri katika vita vya Uhud alipowauliza kama wanaona bora kuweka boma Madiynah au waende kupigana vita, basi wengi wao wakashauri kwenda vitani.
  3. Alichukua ushauri wao katika vita vya Khandaq kuhusu kufanya sulhu na makabila ya Al-Ahzaab (makundi ya washirikina wa Makkah), ili badala yake wawape thuluthi moja ya mazao ya Madiynah, lakini Sa’d bin ‘Ubaadah na Sa’d bin Mu’aadh (رضي الله عنهما) wakakataa bali wakakhitari na wakashauri vita.
  4. Aliwataka ushauri kama wawahujumu washirikina siku ya Hudaybiyah, lakini Abuu Bakr alikataa akasema: “Hatukuja kupigana bali tumekuja kutekeleza ‘Umrah.”
  5. Aliwataka ushauri katika tukio la Ifk (kusingiziwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها).
  6. Pia alimtaka ushauri Mama wa Waumini Ummu Salamah  (رضي الله عنها)  walipokuwa Hudaybiyah pindi makafiri wa Quraysh walipowazuia  kuingia Makkah. Ummu Salamah (رضي الله عنها)   Akamshauri Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wajivue Ihraam; wakachinja na wakanyoa nywele zao.

Na katika hali nyinginezo mbalimbali alikuwa akiwataka ushauri Swahaba zake (رضي الله عنهم).

 

Kwa faida ziyada tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho:

 

38-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):Unyenyekevu Wake: Akichukuwa Ushauri Kwa Maswahaba Zake

 

 

 

 

 

Share

161-Aayah Na Mafunzo: Tahadharisho La Kufanya Khiyana

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Tahadharisho La Kufanya Khiyana

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦١﴾

Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira). Na yeyote atakayekhini atakuja na kile alichokikhini Siku ya Qiyaamah. Kisha italipwa kamilifu kila nafsi yale iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa. [Aal-'Imraan: 161]

 

 

Mafunzo:

 

Abuu Maalik Al-Ashja’iy amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ghuluwl (khiyaana ya wizi) kubwa mbele ya Allaah ni kipande cha ardhi ambacho utakuta watu wawili majirani katika ardhi au katika nyumba kisha mmoja wapo akakata kipande cha ardhi ya mwenziwe (bila haki), basi akifanya hivyo, atafungwa nacho kutoka ardhi saba mpaka Siku ya Qiyaamah.” [Ahmad].

 

Pia,

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Alisimama mbele yetu Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akataja suala la kuiba ngawira, akalishadidia na kulitilia umuhimu jambo hilo, akasema: “Nisije kumkuta mmoja wenu siku ya Qiyaamah juu ya shingo yake kuna mbuzi anatoa sauti, juu yake kuna farasi anatoa sauti aseme: Ee Rasuli wa Allaah! Niokoe! Nitamwambia: Similiki kwako kitu chochote, hakika nilikubalighishia. Na juu ya shingo yake kuna ngamia anatoa sauti aseme: Ee Rasuli wa Allaah! Niokoe! Nitamwambia: Similiki kwako kitu chochote hakika nilikubalighishia. Na juu ya shingo yake kuna nguo zilizo chanikachanika zinapepea kisha aseme: Ee Rasuli wa Allaah! Niokoe! Nitamwambia: Similiki kwako kitu chochote hakika nilikubalighishia.[Al-Bukhaariy (2891)].

 

Na pia,

 

‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Siku ya vita vya Khaybar, Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) walimwendea na kusema: Fulani na fulani wamekufa shahidi, fulani na fulani wamekufa shahidi. Walipomtaja mmojawapo kuwa kafariki shahidi, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hapana! Nimemuona motoni kwa sababu ya kanzu aliyoiiba (katika ngawira).” [Ahmad na Muslim kwa riwaayah nyingine].

 

 

Share

169-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Mashuhadaa

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Fadhila Za Mashuhadaa

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾ 

Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Rabb wao wanaruzukiwa.

 

فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١٧٠﴾ 

Wanafurahia kwa Aliyowapa Allaah kwa fadhila Zake na wanawashangilia ambao hawajaungana nao, walio nyuma yao, kwamba: “Hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.”

يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٧١﴾

Wanashangilia kwa neema za Allaah na fadhila na kwamba Allaah Hapotezi ujira wa Waumini. [Aal-'Imraan: 169-171]

 

 

Mafunzo:

 

Fadhila za kufa shahidi: Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Pale walipopatwa msiba (walipofariki) ndugu zenu wa Uhud, Allaah Alijaalie roho zao kuwa katika maumbile ya ndege wa kijani ambao wanakunywa katika mito ya Jannah na wanakula katika matunda ya Jannah na hurukia na hustarehe kwenye kandili ya dhahabu chini ya kivuli cha ‘Arshi ya Allaah. Kisha roho hizo zilipopatwa na utamu wa kunywa na kula katika neema za humo ndani ya Jannah na uzuri wa makazi na marejeo yao wakasema: Laiti wangelifahamu ndugu zetu yale Allaah Aliyotufanyia sisi ili wasipuuze jambo la jihaad na wala wasirejee na kuogopa vita. Basi hapo Allaah Akasema: “Mimi ninayafikisha hayo kutoka kwenu!” Ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha: Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Rabb wao wanaruzukiwa… (mpaka Aayah (3: 169-171[Imaam Ahmad].

 

Pia ...

 

Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikutana nami siku moja akaniambia: “Ee Jaabir! Unanini nakuona una huzuni?” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Baba yangu amekufa shahidi na ameacha nyuma madeni na watoto. Akasema: “Je, nikujulishe kuwa Allaah Hajapata kuongea na mtu yeyote sipokuwa nyuma ya pazia? Lakini Amemhuisha baba yako na akazungumza naye moja kwa moja. Akasema: Tamani (lolote) Nikupe!  Akasema: Yaa Rabb! Nihuishe (nirudi duniani) ili niuliwe tena kwa ajili Yako! Akasema Rabb (تبارك وتعالى): Nimeshatanguliza kauli kwamba wao hawatorudi tena (maisha ya dunia). Akasema: Yaa Rabb! Basi nifikishie khabari kwa nilioawaacha nyuma. Kisha Allaah Akateremsha: Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Rabb wao wanaruzukiwa… (3: 169-171) [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Swahiyh At-Targhiyb (2276), Swahiyh At-Targhiyb (1361)].

 

 

Share

180-Aayah Na Mafunzo: Tahadharisho La Kutokutoa Zakaah

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Tahadharisho La Kutokutoa Zakaah

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَبْخَلُونَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ هُوَ خَيْرًا لَّهُم ۖ بَلْ هُوَ شَرٌّ لَّهُمْ ۖ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُوا بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَلِلَّـهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١٨٠﴾

Wala wasidhani kabisa wale wanaofanya ubakhili kwa yale Aliyowapa Allaah katika fadhila Zake kwamba hayo ni kheri kwao, bali ni shari kwao. Watafungwa kongwa yale waliyoyafanyia ubakhili Siku ya Qiyaamah. Na ni Wake Allaah Pekee urithi wa mbingu na ardhi. Na Allaah kwa myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Aal-'Imraan: 180]

 

 

Mafunzo:

 

 

Tahadharisho la kutokutoa Zakaah: Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yeyote yule ambaye Allaah Amemruzuku mali kisha asiitolee Zakaah yake, basi (Siku ya Qiyaamah) mali yake itakuwa kama nyoka dume kipara aliye na madoti mawili juu ya macho yake. Atamvingirita shingoni na kumuuma mashavu yake huku akisema: Mimi mali yako! Mimi hazina yako!” [Al-Bukhaariy]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٤﴾

Enyi walioamini! Hakika wengi katika Wanazuoni Marabai wa dini (zao) na Wamonaki wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuia njia ya Allaah. Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo. 

 

 

 

يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ﴿٣٥﴾

Siku zitakapopashwa katika Jahannam, na kwazo vikachomwa moto vipaji vyao, na mbavu zao, na migongo yao (wakiambiwa): Haya ndiyo mliyoyarundika kwa ajili ya nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkiyarundika. [At-Tawbah: 34-35]

 

 

Share

185-Aayah Na Mafunzo: Dunia Haina Thamani Kulingana Na Aakhirah

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Dunia Haina Thamani Kulingana Na Aakhirah

 

 

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿١٨٥﴾

185. Kila nafsi itaonja mauti. Na hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu Siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na moto na akaingizwa Jannah kwa yakini amefuzu. Na uhai wa dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu.

 

Mafunzo:

 

 

Dunia haina thamani kulingana na Aakhirah.

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Sehemu ndogo katika Jannah, kiasi cha ukubwa wa fimbo, ni bora kuliko dunia na yaliyokuwemo ndani yake. Someni mkipenda: “Basi atakayewekwa mbali na moto na akaingizwa Jannah kwa yakini amefuzu… (3: 185) [Ameinukuu Ibn Abi Haatim, At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh].

Anas (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Siku ya Qiyaamah ataletwa mtu wa motoni katika watu wa dunia aliyeneemeshwa neema nyingi mno, ataingizwa motoni kidogo kisha atatolewa: Ataulizwa: Ee mwana wa Aadam!  Je, umeona kheri yoyote? Ushawahi kuneemeka aslani? Atajibu: Hapana Wa-Allaahi Rabb wangu! Na ataletwa mtu aliyekuwa ana shida mno duniani katika watu wa Jannah. Ataingizwa Jannah kidogo kisha atatolewa. Ataulizwa: Ee mwana wa  Aadam! Je, umeona shida yoyote? Ushawahi kutaabika aslani? Atajibu: Hapana Wa-Allaahi Rabb wangu! Haikunipitia shida yoyote abadan, wala sikuona tabu yoyote Abadan.” [Muslim].

Sahl bin Sa'ad (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ingelikuwa (thamani ya) dunia ni sawasawa na bawa la mbu mbele ya Allaah, basi Asingelimnywesha kafiri hata tama moja la maji.” [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh].

Share

187-Aayah Na Mafunzo: Atakayeficha ‘Ilmu Atafungwa Lijamu La Moto Siku Ya Qiyaamah

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Atakayeficha ‘Ilmu Atafungwa Lijamu La Moto Siku Ya Qiyaamah

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ ﴿١٨٧﴾

187. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) pale Alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu (Allaah Akawaambia): “Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha.” Lakini walikitupa nyuma ya migongo yao na wakakibadilisha kwa thamani ndogo. Basi ubaya ulioje kwa yale wanayoyanunua

 

 

Mafunzo:

 

 

Tahadharisho kuficha elimu aliyojaaliwa nayo mtu: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayeulizwa jambo la kuhusiana na ‘ilmu (ya Dini) lakini alifiche, atafungwa lijamu la moto Siku ya Qiyaamah.” [At-Tirmidhy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Swahiyh At-Targhiyb (120)].

Share

190-Aayah Na Mafunzo: Unapoamka Tahajjud Sunnah Kusoma Aayah Za Mwisho Suwratul-‘Imraan

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Unapoamka Tahajjud Sunnah Kusoma Aayah Za Mwisho Suwratul-‘Imraan

Alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ 

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (ishara, zingatio n.k.) kwa wenye akili. [Aal-'Imraan:]

 

Mafunzo:

 

 

Ni Sunnah kuzisoma Aayah kuanzia hiyo mpaka mwisho wa Suwrah anapoamka mtu usiku kuswali (tahajjud). Pia Mama wa Waumini ‘Aaishah  (رضي الله عنها) aliulizwa kuhusu jambo la ajabu alilolishuhudia kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ‘Aaishah akalia kwanza kisha akasema: Mambo yake yote yalikuwa ya ajabu! Usiku mmoja alikuja karibu na mimi mpaka ngozi yake ikagusa ngozi yangu na akasema: “Huniachi nimuabudu Rabb wangu?” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Wa-Allaahi hakika mimi napenda ukaribu wako kwangu na pia napenda mahaba yako, na kwamba napenda usiwe mbali na mimi, na napenda yale yanayokufurahisha. Akasema ('Aaishah): Akainuka na kutumia kiroba cha maji na akafanya wudhuu wala hakutumia maji mengi., kisha akasimama akaswali 'Tahajjud' akalia mpaka ndevu zake zikawa zimerowa. Kisha akasujudu na kulia mpaka akaifanya ardhi irowe. Kisha akalala kwa upande wa kulia mpaka akaja Bilaal kumjulisha Adhaan ya Alfajiri, akamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Jambo gani linakuliza na hali Allaah (سبحانه وتعالى) Amekwishakufutia madhambi yako yaliyotangulia na yanayokuja? Nabiy(صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: “Ee Bilaal! Nini kinizuie mimi kulia wakati usiku huu Allaah (سبحانه وتعالى) Ameniteremshia Aayah hizi?

 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ 

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (ishara, zingatio) kwa wenye akili. (mpaka mwisho wa Suwrah hii ya Aal-'Imraan (190-200). Kisha akasema: “Ole wake, yule anayezisoma lakini hatafakari kwayo.” [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 

 

 

 

Share

200-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Ribaatw Fiy SabiliLLaah

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Fadhila Za Ribaatw  Fiy SabiliLLaah

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٢٠٠﴾

200. Enyi walioamini! Subirini na zidini kuvuta subira na bakieni imara na mcheni Allaah ili mpate kufaulu.

 

Mafunzo:

 

Baadhi Ya Maana Ya Ribaatw Na Fadhila Zake:

 

Kwanza:  Kubakia, kuthibitika kuchunga, kulinda mipaka katika Jihaad fiy SabiliLLaah

 

Pili:          Kubakia katika ‘Ibaadah baina ya Swalaah Na Swalaah ya pili.

 

Fadhila za Ribaatw:

 

Amesimulia Sahl bin Sa’ad (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ):  Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ) amesema: “Ar-Ribaatw (kusimama imara katika kulinda mipaka kwenye vita vya Jihaad) ya siku moja kwa ajili ya Allaah, ni bora kuliko dunia na vilivyomo. Na sehemu ndogo katika Jannah (Peponi), kiasi cha ukubwa wa fimbo ya mmoja wenu, ni bora kuliko dunia na yaliyomo ndani yake. Na safari ya asubuhi au ya jioni anayosafiri mja katika Njia ya Allaah, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Pia:  Amesimulia Salmaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ) amesema: “Ribaatw (kusimama imara katika kulinda mipaka kwenye vita vya Jihaad) ya siku moja na usiku wake, ni bora (katika malipo) kuliko Swiyaam ya mwezi mzima na Qiyaam (kisimamo cha kuswali usiku) chake. Na mtu akifariki (akiwa katika ribaatw), amali zake zitaendelea kuandikwa, na riziki yake ataendelea kuipata, na atasalimika na fitnah (za kaburi).”  [Muslim]

 

 

 

 

Share