007-Al-A'Raaf: Aayah Na Mafunzo

 

 

 

007-Al-A'raaf

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Share

031-Aayah Na Mafunzo: Pendekezo La Mavazi Mazuri Msikitini Na Kutokula Na Kunywa Mpaka Kushiba Sana

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf

 

031-Pendekezo La Mavazi Mazuri Msikitini

Na Kutokula Na Kunywa Mpaka Kushiba Sana

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾

Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu (ya mavazi ya sitara na twahara) katika kila mahala pa ‘Ibaadah. Na kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu. [Al-A’raaf (7:31)]

 

 

Mafunzo:

 

Amri Ya Kuvaa Mavazi Mazuri Masafi Ya Twahara Sehemu Za ‘Ibaadah:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anaamrisha waja Wake Waumini kuvaa nguo nzuri, safi, za twahara (na siwaak) anaposwali au katika sehemu zozote zile za ‘Ibaadah kama katika Manaasik ya ‘Umrah na Hajj; katika kutufu Al-Ka’baah na kwengineko.  Na nguo bora kabisa ni ya rangi nyeupe (kwa wanaume) kama alivyohadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Vaeni nguo nyeupe kwani ndio nguo zenu bora kabisa, na kafinini kwazo maiti wenu...” [Ahmad]

 

Katazo La Kufanya Israfu:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anakataza kufanya israfu; nayo ni israfu katika kula kunywa na hata katika mavazi na upotezaji wa neema nyenginezo. 

 

 

Katika kula, kuna nasaha ya kutokula kwa wingi mno mpaka mtu ashindwe kutekeleza ‘ibaadah zake: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Bin-Aadam hajijazii chombo vibaya kama anavyojaza tumbo lake. Inamtosheleza Bin-Aadam ale kidogo tu kiasi cha kumtia nguvu uti wa mgongo wake. Lakini akitaka kula zaidi, basi thuluthi ya chakula, na thuluthi ya maji na thuluthi aache kwa ajili ya hewa.” [Amehadithia Al-Miqdaam bin Ma’diykarib (رضي الله عنه)  na imepokelewa na  Ahmad, At-Tirmidhiy]

 

 

Share

033-Aayah Na Mafunzo: Allaah Anachukia Maasi Na Huwa Na Ghera Pindi Mja Wake Akitenda Maasi

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-‘Araaf 33

 

033-Allaah Anachukia Maasi Na Huwa Na Ghera Pindi Mja Wake Akitenda Maasi

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٣﴾

Sema: Hakika Rabb wangu Ameharamisha machafu ya wazi na ya siri, na dhambi, na ukandamizaji bila ya haki, na kumshirikisha Allaah kwa ambayo Hakuyateremshia mamlaka, na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui. [Al-Araaf: 33]

 

 

Mafunzo:

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ يَغَارُ وَغَيْرَةُ اللَّهِ أَنْ يَأْتِيَ الْمُؤْمِنُ مَا حَرَّمَ اللَّه)) متفق عليه

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه  وآله وسلم ) amesema: ((Hakika Allaah Ana hisia ya  ghera, na ghera  ya  Allaah [inachomoza] pale mtu anapofanya [maasi] Aliyoyaharamisha Allaah)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Na pia amesema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakuna mwenye ghera zaidi ya Allaah wakati anapozini mja wake au ummah Wake uzini.” [Al-Bukhaariy]

Faida: Kuhusu haramisho la kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) rejea tanbih (4: 48)

 

 

 

Share

040-Aayah Na Mafunzo: Anayemkadhibisha Allaah Na Aayaat Zake Hatofunguliwa Milango Ya Mbingu Mpaka Ngamia Aingie Katika Tundu Ya Sindao

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

 

Al-A’raaf 40

 

040-Anayemkadhibisha Allaah Na Aayaat Zake Hatofunguliwa Milango Ya Mbingu Mpaka Ngamia Aingie Katika Tundu Ya Sindao

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ ﴿٤٠﴾

Hakika wale waliokadhibisha Aayaat Zetu na wakazifanyia kiburi, hawatofunguliwa kamwe milango ya mbingu na wala hawatoingia Jannah mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wakhalifu.  (7:40).

 

Mafunzo:

 

 

Mustahili Kwa Waliokufuru Kuingia Janna (Peponi) Kama Vile Mustahili Ngamia Kuingia Katika Tundu Ya Sindano:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anatoa mifano mbali mbali katika Qur-aan; mifano yenye Hikmah, mafundisho na mazingatio kwa wenye kutafakari. Rejea Ibraahiym (14:24-25), Al-Kahf (18:54), Al-Hajj (22:73), Al-‘Ankabuwt (29:43), Ar-Ruwm (30:58) na kwengineko kwingi katika Qur-aan. Na katika Sunnah hali kadhaalika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amepiga mifano mingi mmojawapo ni kuhusu Swalaah tano jinsi zinavyomsafisha mtu na madhambi:

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:Mnaonaje kungekuwa na mto mlangoni mwa mmoja wenu na akaoga mara tano kwa siku, je, atabakiwa na tone la uchafu (mwilini mwake)?”  Wakasema: “Hatabakiwa na tone la uchafu.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ”Basi hivyo ni mfano wa Swalaah tano ambazo Allaah Anafuta madhambi kwazo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Sharh (Ufafanuzi) Ya Aayah:

 

Imaam Bin Baaz (رحمه الله)  amesema alipoulizwa kuhusu Aayah hii:

 

إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ ﴿٤٠﴾

Hakika wale waliokadhibisha Aayaat Zetu na wakazifanyia kiburi, hawatofunguliwa kamwe milango ya mbingu na wala hawatoingia Jannah mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wakhalifu.  (7:40).

 

“Ni dhahiri kuwa mwenye kukadhibisha Aayaat za Allaah akatakabari kufuata haki, hivyo ndivyo itakavyokuwa hali yake, haitopanda roho yake mbinguni, bali itarudishwa ardhini katika mwili wake aadhibishwe kaburini mwake. Kisha atahamishwa motoni, tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah. Kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu Fir’awn:

 

النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا ۖ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ﴿٤٦﴾

Wanadhihirishiwa moto asubuhi na jioni, na Siku itakayosimama Saa (itasemwa): Waingizeni watu wa Fir’awn katika adhabu kali kabisa.  [Ghaafir 40:46]

 

Hivyo ndivyo hali ya wengineo, kila atakayetakabari na haki na asifuate Mwongozo, haitofunguliwa milango ya mbingu wala hazirudishwi roho zao mbinguni wala kwa Allaah (عزّ وجلّ)  bali itarudi roho yake katika mwili wake muovu na ataadhibiwa kaburini mwake pamoja na adhabu ya moto Siku ya Qiyaamah. Tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah. Na pia hawatoingia Jannah kamwe. Ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Anabainisha kuwa hatoingia kamwe Jannah mpaka iwezekane ngamia aingie katika tundu ya sindano. Na inajulikana wazi kuwa ngamia hawezi kuingia kamwe katika tundu ya sindano! Na lilokusudiwa hapa ni jambo hili kuwa mustahili aingie Jannah kama vile ilivyokuwa mustahili ngamia aingie katika tundu ya sindano, kutokana na kufru zao na upotofu wao, ni mustahili kuingia Jannah bali wao wataingia motoni milele. Tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah.” [Fataawa Ibn Baaz]  

 

 

 

 

 

 

 

Share

043-Aayah Na Mafunzo: Waumini Kulipana Kisasi Na Kuondosheana Mafundo Ya Nyoyo Kabla Ya Kuingizwa Jannah Na Watashukuru Kuhidiwa Na Allaah

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-Araaf 43

 

043-Waumini Kulipana Kisasi Na Kuondosheana Mafundo Ya Nyoyo

Kabla Ya Kuingizwa Jannah

Na Watashukuru Kuhidiwa Na Allaah

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ ۖ وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي هَدَانَا لِهَـٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِيَ لَوْلَا أَنْ هَدَانَا اللَّـهُ ۖ لَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ ۖ وَنُودُوا أَن تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾

Na Tutaondosha mizizi ya mafundo ya kinyongo yaliyomo vifuani mwao itapita chini yao mito. Na watasema: AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Ametuongoza kwa haya, na tusingelikuwa wenye kuhidika kama Allaah Asingetuongoza. Kwa yakini wamekuja Rusuli wa Rabb wetu na haki. Na wataitwa (kuambiwa): Hii ndiyo Jannah mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mnayatenda. [Al-A'raaf: 43]
 

 

Mafunzo:

 

Qantwarah Daraja Baina Ya Jannah Na Moto Ambalo Waumini Watalipana Kisasi Na Kuondoshewa Mafundo Na Vinyongo Baina Yao.

 

Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) : Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Baada ya Waumini kuokolewa na moto, watazuiliwa wangojee katika Qantwarah (daraja) baina ya Jannah na moto. Kisha watahojiwa kuhusu dhulma zote walizotendeana duniani. Watakapotakaswa (madhambi yao kuhukumiwa) watapewa ruhusa kuingia Jannah. Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, kila mtu atatambua makazi yake Jannah kuliko anavyotambua makazi yake ya duniani.” [Al-Bukhaariy]  

 

 

Shukurani Za Watu Kuingia Jannah Na Majuto Kuingia Motoni:

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)   : Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kila mmoja katika watu wa Jannah ataona sehemu yake ya kikao chake cha motoni atasema: Ingekuwa Allaah Hakunihidi!  Basi itakuwa ndio shukurani yake. Na kila mtu wa motoni ataona sehemu yake ya kikao Jannah atasema: Ingekuwa Allaah Kanihidi! Basi huwa ndio majuto yake.” [An-Nasaaiy] 

 

 

 

Share

046-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya Al-A’raaf: Ukuta Wa Mwinuko

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf 46

 

046-Maana Ya Al-A’raaf: Ukuta Wa Mwinuko

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ ۚ وَعَلَى الْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّا بِسِيمَاهُمْ ۚ وَنَادَوْا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَن سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۚ لَمْ يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ ﴿٤٦﴾

Na baina yao kitakuwepo kizuizi. Na juu ya Al-A’raaf (ukuta wa mwinuko) patakuweko watu watakaowatambua wote (wabaya na wema) kwa alama zao. Na watawaita watu wa Jannah: Salaamun ‘Alaykum!  Hawakuingia humo lakini bado wanatumaini. 

 

وَإِذَا صُرِفَتْ أَبْصَارُهُمْ تِلْقَاءَ أَصْحَابِ النَّارِ قَالُوا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٤٧﴾

Na yatakapogeuzwa macho yao kuelekea watu wa motoni watasema: Rabb wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na watu madhalimu.

 

 

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ رِجَالًا يَعْرِفُونَهُم بِسِيمَاهُمْ قَالُوا مَا أَغْنَىٰ عَنكُمْ جَمْعُكُمْ وَمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٤٨﴾

Na watu wa Al-A’raaf watawaita watu (wa motoni) wanaowatambua kwa alama zao, watasema: Hakukufaeni kujumuika kwenu (duniani) na vile mlivyokuwa mkitakabari.

 

 أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللَّـهُ بِرَحْمَةٍ ۚ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ ﴿٤٩﴾

Je, hawa si wale ambao mliapa kwamba Allaah Hatowapa Rahmah yoyote ile? (Leo wanaambiwa) Ingieni Jannah! Hakuna khofu juu yenu na wala nyinyi hamtohuzunika. 

 

وَنَادَىٰ أَصْحَابُ النَّارِ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَنْ أَفِيضُوا عَلَيْنَا مِنَ الْمَاءِ أَوْ مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ ۚ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ حَرَّمَهُمَا عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٥٠﴾

Na watu wa motoni watawaita watu wa Jannah: Tumiminieni maji au katika ambavyo Amekuruzukuni Allaah. Watasema: Hakika Allaah Ameviharamisha kwa makafiri.  [Al-A’raaf: 46-50]

 

 

Mafunzo:

 

Al-A’raaf:

 

Al-A’raaf ni Jina la Suwrah hii. Na Ibn ‘Abbaas, Ibn Mas’uwd, Ibn Jariyr na Salaf wengineo wamesema: Al-A’raaf ni sehemu watakayosimama watu ambao ‘amali zao njema na mbaya zimelingana sawasawa. ‘Amali zao ovu zimewazuia kuingia Jannah, na ‘amali zao njema zimewastahiki waepukane na moto. Kwa hiyo watasimamishwa hapo katika mnyanyuko wa Al-A’raaf mpaka Allaah Awahukumu. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Share

054-Aayah Na Mafunzo: Kuumbwa Mbingu Na Ardhi Kwa Siku Sita Na Maana Ya Istiwaa

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf 54

 

054-Kuumbwa Mbingu Na Ardhi Kwa Siku Sita Na Maana Ya Istiwaa

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٥٤﴾

Hakika Rabb wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Akawa juu (Istawaa) ya ‘Arsh, Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesi upesi, na (Ameumba) jua na mwezi na nyota, (vyote) vimetiishwa kwa Amri Yake. Tanabahi! Uumbaji ni Wake Pekee na kupitisha amri. Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu. [Al-A’raaf: 54]

 

 

Mafunzo:

 

 

Masiku Yaliyoumbwa Dunia Na Viliyomo:

 

Amesimulia Abuu Hurayrah :(رضي الله عنه) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (عزّ وجلّ)  Ameumba mchana siku ya Jumamosi, Akaumba milima Jumapili, Akaumba miti Jumatatu, Akaumba yanayochukiza Jumanne, Akaumba nuru Jumatano, kisha Akaeneza humo viumbe vinavyotembea Alkhamiys. Kisha Akamuumba Aadam (عليه السلام)  Ijumaa baada ya Alasiri. Alikuwa ni wa mwisho kuumbwa katika saa ya mwisho katika saa za Ijumaa, baina ya Alasiri na usiku.” [Ahmad]  

 

 

Maana ya Istawaa: Yuko juu kabisa kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah. Pia rejea tanbihi (2:29).

 

 

Share

055-Aayah Na Mafunzo: Adabu Za Kuomba Du’aa: Kwa Unyenyekevu, Kwa Siri, Kwa Sauti Ndogo, Kwa Khofu Na Matumaini

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf  55 Na 56

 

055-Miongoni Mwa Adabu Za Kuomba Du’aa: Kwa Unyenyekevu, Kwa Siri, Kwa Sauti Ndogo, Kwa Khofu Na Matumaini

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٥٥﴾

Muombeni Rabb wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye Hapendi wenye kupindukia mipaka.

 

وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا ۚ إِنَّ رَحْمَتَ اللَّـهِ قَرِيبٌ مِّنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٦﴾

Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya (Allaah) kuitengeneza sawa, na muombeni kwa khofu na matumaini. Hakika Rahmah ya Allaah iko karibu na wafanyao ihsaan. [Al-A’raaf: 55-56]

 

 

Mafunzo:

 

Miongoni Mwa Adabu Za Kuomba Du’aa:  

 

Aayah hii Al-A’raaf (55) na inayofuatia (56) zimetajwa baadhi ya adabu za kuomba Du’aa nazo ni: Kuomba kwa unyenyekevu, kwa Siri, kwa sauti ndogo, kwa khofu na matumaini .

 

عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَكُنَّا إِذَا أَشْرَفْنَا عَلَى وَادٍ هَلَّلْنَا وَكَبَّرْنَا. ارْتَفَعَتْ أَصْوَاتُنَا فَقَالَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((يَا أَيُّهَا النَّاسُ ارْبَعُوا عَلَى أَنْفُسِكُمْ فَإِنَّكُمْ لاَ تَدْعُونَ أَصَمَّ ولاَ غَائِبًا إِنَّهُ مَعَكُمْ ، إِنَّهُ سَمِيعٌ قَرِيبٌ تَبَارَكَ اسْمُهُ وَتَعَالَى جَدُّهُ))

 

Amesimulia Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه): Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na tukawa kila tukipanda bonde, tunafanya tahliyl (Laa Ilaaha Illa-Allaah), na tunaleta takbiyr (Allaahu Akbar). Zikapanda sauti zetu, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Enyi watu, zihurumieni nafsi zenu, kwani hamumwombi kiziwi wala asiyekuwepo, hakika Yeye Yupo nanyi (kwa Ujuzi Wake), hakika Yeye Ni Mwenye Kusikia yote, Yupo Karibu, Limebarikika Jina Lake na Umetukuka Ujalali Wake.” [Al-Bukhaariy]

 

Rejea pia tanbihi (2:186).

 

Share

058-Aayah Na Mfunzo: Mfano Wa Uongofu Na ‘Ilmu Kulingana Na Ardhi Yenye Rutuba Na Isiyokuwa Na Rutuba

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf 58

 

058-

Mfano Wa Uongofu Na ‘Ilmu Kulingana Na Ardhi Yenye Rutuba

Na Isiyokuwa Na Rutuba

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَالْبَلَدُ الطَّيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُ بِإِذْنِ رَبِّهِ ۖ وَالَّذِي خَبُثَ لَا يَخْرُجُ إِلَّا نَكِدًا ۚ كَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَشْكُرُونَ ﴿٥٨﴾

Na nchi nzuri mimea yake hutoka kwa idhini ya Rabb wake. Na ile ambayo ni mbaya haitoki ila kwa uadimu. Hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna ishara na dalili kwa watu wanaoshukuru. [Al-A'raaf: 58]

 

 

Mafunzo:

 

Amesimulia Abuu Muwsaa Al-Ash-‘ariyy (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mfano wa uongofu na ‘Ilmu ambayo Allaah Amenituma kufikisha ni kama mvua kubwa inayoanguka juu ya ardhi, baadhi yake (hufikia) katika ardhi yenye rutuba ikanyonya maji ya mvua na ikaleta mimea na majani kwa wingi. Na baadhi yake (ardhi) ikawa nzito na ikazuia maji ya mvua (kupenya katika ardhi), na Allaah Akawanemeesha watu kutokana nayo, na wakaitumia kwa kunywa, kunyweshea wanyama wao na kwa ajili ya umwagiliaji na kilimo kwenye ardhi hiyo. Na baadhi yake ikawa si yenye rutuba ambayo haikuweza kukamata maji wala kutoa mimea (hivyo ardhi hiyo haikutoa faida yoyote). (Ardhi) Ya mwanzo ni mfano wa mtu anayetambua Dini ya Allaah na akapata faida (kutokana na ‘Ilmu) ambayo Allaah Ameishusha kupitia kwangu (Manabii na ‘Ulamaa) na akaisomesha kwa wengine. (Ardhi) Ya mwisho ni mfano wa yule mtu asiyejali na hafuati Uongofu wa Allaah Alioushusha kupitia kwangu (Ni mfano wa hiyo ardhi isiyo na rutuba).” [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share

156-Aayah Na Mafunzo: Rahmah Za Allaah Ni Mia: Moja Duniani, Tisini Na Tisa Aakhirah

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf 156

 

156-Rahmah Za Allaah Ni Mia: Moja Duniani, Tisini Na Tisa Aakhirah

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ ۚ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٦﴾

Na Tuandikie katika dunia hii mazuri na katika Aakhirah. Hakika sisi tumerudi kutubu Kwako. (Allaah) Akasema: Adhabu Yangu Nitamsibu nayo Nimtakaye. Na Rahmah Yangu imeenea kila kitu. Basi Nitawaandikia wale wenye taqwa na wanaotoa Zakaah na ambao wao wanaziamini Aayaat (ishara, dalili) Zetu. [Al-A'raaf: 156]

 

Mafunzo:

 

Rahmah Za Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Mia: Moja Duniani Na Rahmah Tisini Na Tisa Aakhirah:

 

Amesimulia Salmaan (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (عزّ وجلّ)   Ana Rahmah mia.  Katika hizo, Rahmah moja wanarehemiana viumbe baina yao, hata mnyama mwitu anakihurumia kizazi chake. Rahmah tisini na tisa Ameziweka kwa ajili ya Siku ya Qiyaamah.” [Ahmad]

 

Rejea Tanbihi Ya Al-Faatihah (1:1)

 

 

 

Share

172-Aayah Na Mafunzo: Ahadi Ya Alastu Waliyoahidiana Viumbe Na Allaah Katika Hali Ya Fitwrah Kumtii Na Kutokumshirikisha

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf 172

 

172-Ahadi Ya Alastu Walioahidi Viumbe Kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Kumtii

Na Kutokumshirikisha

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ ﴿١٧٢﴾

Na pindi Rabb wako Alipowaleta wana wa Aadam kutoka migongoni mwao kizazi chao, Akawashuhudisha juu ya nafsi zao, Je, Mimi siye Rabb wenu? Wakasema: Ndio bila shaka, tumeshuhudia! (Allaah Akawaambia): Msije kusema Siku ya Qiyaamah: hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya.

 

أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِن قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِّن بَعْدِهِمْ ۖ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ ﴿١٧٣﴾

Au mkasema: Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. Basi Utatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wabatilifu? [Al-A'raaf: 172-173]

 

 

Mafunzo:

 

Ahadi ya “Alastu” ni ile ambayo viumbe vyote viliahidi kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kutokumshirikisha na kumtii Amri Zake. Ahadi hiyo waliichukua viumbe kabla ya kuzaliwa kwao wakati roho zao zimeshaumbwa. Kwa kuwa kuna uhai miwili na mauti mawili kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Swurah Ghaafir 40:10-11) na (Al-Baqarah 2:28):

 

 

 كَيْفَ تَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَكُنتُمْ أَمْوَاتًا فَأَحْيَاكُمْ ۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٨﴾

Vipi mnamkufuru Allaah na hali mlikuwa wafu Akakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakuhuisheni, kisha Kwake mtarejeshwa [Al-Baqarah (2: 28)]

 

Na pia:

 

قَالُوا رَبَّنَا أَمَتَّنَا اثْنَتَيْنِ وَأَحْيَيْتَنَا اثْنَتَيْنِ فَاعْتَرَفْنَا بِذُنُوبِنَا فَهَلْ إِلَىٰ خُرُوجٍ مِّن سَبِيلٍ﴿١١﴾

Watasema: Rabb wetu! Umetufisha mara mbili na Umetuhuisha mara mbili, na tumekiri madhambi yetu. Basi je, kuna njia ya kutoka? [Ghaafir: 11]

 

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna kizazi kinachozaliwa (mtoto mchanga) isipokuwa anazaliwa katika 'fitwrah' kisha wazazi wake (humbadilisha na) humuingiza katika dini ya Uyahudi, au Unaswara au Umajusi, kama mfano mnyama mwenye pembe anavyomzaa mnyama mwenye pembe kama yeye, je, mtahisi kuwa hana pembe?”  Kisha Abuu Hurayrah akasema: Someni mkipenda: (Kauli ya Allaah): 

 

ۚ فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ

(Shikamana na) Umbile la asili la kumpwekesha Allaah Alilowaumbia watu. Hakuna kubadilisha Uumbaji wa Allaah.  (Ar-Ruwm 30:30). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Maana ya Fitwrah: Umbile la asili la Tawhiyd (Kumpwekesha Allaah bila ya kumshirikisha). Ahadi hiyo waliahidi viumbe kabla ya kuzalilwa kwao.

 

Rejea pia Ar-Ruwm (30:30)

 

 

Share

180-Aayah Na Mafunzo: ‘Aqiydah Sahihi Kuhusu Majina Mazuri Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Atakayehifadhi Ataingia Jannah

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf 180

 

180-‘Aqiydah Sahihi Kuhusu Majina Mazuri Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Atakayehifadhi Ataingia Jannah

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa na kuharibu Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A'raaf: 180]

 

 

Mafunzo:

 

Kumpwekesha Allaah Katika Majina Yake Na Kuthibitisha Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى) Na Ndio Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Na Sifa Zake:

 

Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah kuhusiana na Majina Mazuri kabisa ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Sifa Zake ni Tawqiyfiyyah;  Yanathibitishwa Aliyoyathibitisha Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى) katika Qur-aan na Sunnah bila kuzifanyia Ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala Tamthiyl (kumithilisha, kufafanisha, kulinganisha), wala Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah), wala Tahriyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutoa maana isiyo sahihi).

 

Rejea: An-Nisaa (4:164).

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ إِنَّ لِلَّهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ اسْمَا مِائَةً إِلاَّ وَاحِدًا مَنْ أَحْصَاهَا دَخَلَ الْجَنَّةَ ‏"‏‏.‏

Amesimulia Abuu Hurayrah(رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaaah  (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Ana Majina tisini na tisa,  atakayeyahifadhi ataingia Jannah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Maana ya أَحْصَاهَا ni: Kufahamu maana Zake, kuyahifadhi, kuyafanyia kazi, kuyatumia katika kuomba Du’aa. 

 

 

 

Share

181-Aayah Na Mafunzo: Kundi Katika Ummah Huu Watabakia Katika Haki Mpaka Siku Ya Qiyaamah

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-A’raaf 181

 

181-Kundi Katika Ummah Huu Watabakia Katika Haki Mpaka Siku Ya Qiyaamah

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمِمَّنْ خَلَقْنَا أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ ﴿١٨١﴾

Na katika Tuliowaumba, wako ummah wanaoongoza kwa haki na kwayo wanahukumu kiadilifu. [Al-A'raaf: 181]

 

 

Mafunzo:

Amesimulia Mu’aawiyah bin Abiy Sufyaan (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kutakuweko kundi katika Ummah wangu litaendelea kuwa juu ya haki likiwa na nguvu, hawezi kuwadhuru yeyote aliyekwenda nao kinyume au aliyesaliti mpaka Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share