234-Aayah Na Mafunzo: Hikma Ya Eda Ya Mjane Kuwa Miezi Minne Na Siku Kumi

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

 

Hikma Ya Eda Ya Mjane Kuwa Miezi Minne Na Siku Kumi

 

 www.alhidaaya.com

 

وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا ۖ فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٣٤﴾

234. Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao (eda) miezi minne na siku kumi. Watakapofikia muda wao, si dhambi kwao katika yale waliyoyafanya katika nafsi zao kwa ada ya shariy’ah. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

Mafunzo:

 

Hikma ya kufaridhiwa eda miezi minne na siku kumi:  Sa’iyd bin Muswayyib, Abuu ‘Aaliyah na wengineo wamesema kuwa: Hikma ya kuifanya eda ya mjane kuwa ni miezi minne na siku kumi ni kuwa yawezekana kuwepo mimba. Mwanamke anaposubiri kwa kipindi hicho itathibitika kama ana mimba. Na dalili ni Hadiyth ifuatayo:

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم -وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ: ((إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ،  رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: “Ametusimulia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho yake))   [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share