003-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan

 

 

 

Sababu Za Kuteremshwa

(Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Suwrah Aal-'Imraan

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

Share

077-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 077: إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

(Aina Tatu Ya Watu Ambao Allaah Hatowasemesha Siku Ya Qiyaamah)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan 077-Hakika wale wanaobadilisha ahadi ya Allaah

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٧﴾

77. Hakika wale wanaobadilisha ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo; hao hawana sehemu yoyote katika Aakhirah na wala Allaah Hatowasemesha na wala Hatowatazama Siku Ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa na watapata adhabu iumizayo.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia ’Abdullaah bin Mas’uwd(رضي الله عنه)  kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: ”Yeyote atakayeapa kiapo ili achukue mali ya Muislamu (bila ya haki) atakutana na Allaah Akiwa Amemghadhibikia.” Hapo Allaah Akateremsha kusadikisha kauli hii:

 

إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ

 

Hakika wale wanaobadilisha Ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo; hao hawana sehemu yoyote katika Aakhirah…

 

mpaka mwisho wa Aayah (3: 77). Akasema: Kisha akaingia Al-Ash’ath bin Qays akasema: Je, ’Abdur-Rahmaan anakuhadithieni nini? Tukasema: Kadhaa na kadhaa. Akasema: Aayah hii imeteremshiwa kuhusu mimi; nilikuwa na kisima katika ardhi ya bin-’ammi yangu (lakini alikanusha kuwa similiki). Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniambia: ”Ima ulete ushahidi au yeye (bin-’ammi yako) atatoa kiapo (kuthibitisha madai yake).” Nikasema:  Nina hakika atatoa kiapo (cha uongo) ee Rasuli wa Allaah. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ”Atakayeapa kwa ajili ya kuchukua ardhi ya Muislamu (bila haki) hali ya kuwa ni muongo katika kiapo chake, atakutana na Allaah Akiwa Amemghadhibikia.” [Al-Bukhaariy]  

 

Na pia imeteremka kwa mtu mmoja ambaye  aliisimamisha bidhaa yake sokoni,  kisha  akaapa juu ya bidhaa hiyo kuwa amekwishapewa thamani kubwa zaidi ya hiyo anayotaka kupewa,  hali ya kuwa hajapewa thamani hiy. Na aliapa kiapo hicho  ili amshawishi  mmoja katika Waislamu ainunue hiyo bidhaa, na hapo ikateremka Aayah hii.   [Amehadithia Ibn Abiy Awfaa (رضي الله عنه) ameipokea Al-Bukhaariy]

 

 

Share

086-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 086: كَيْفَ يَهْدِي اللَّـهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan 086-Vipi Allaah Atawaongoza watu waliokufuru baada ya kuamini

 

 

كَيْفَ يَهْدِي اللَّـهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٦﴾ 

Vipi Allaah Atawaongoza watu waliokufuru baada ya kuamini kwao na wakashuhudia kwamba Rasuli ni haki na zikawajia hoja bayana? Na Allaah Hawaongozi watu madhalimu.

 

 

 أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُمْ أَنَّ عَلَيْهِمْ لَعْنَةَ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿٨٧﴾

Hao jazaa yao ni kwamba juu yao ipo Laana ya Allaah na ya Malaika na ya watu wote.

 

 

خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٨٨﴾

Wadumu humo milele, hawatopunguziwa adhabu wala hawatopewa muda wa kuakhirishwa adhabu.

 

 

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٨٩﴾

Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengeneza, kwani hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu. [Aal-‘Imraan (3:86-89)]

 

 

 

Sababun-Nuzuwl

 

Aayah hizi (3:86-89) ziliteremka kumzungumzia mtu mmoja katika Answaar ambaye alisilimu kisha akaritadi na akaingia katika shirki. Halafu akajuta kwa tendo lake hilo la kuritadi. Akatuma watu wake ili wamfikishie swali lake kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa je, anaweza kuleta tawbah kwa tendo lake hilo? Baada ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuulizwa swali hilo, zikateremka Aayaat hizo, mtu huyo akatumiwa, na akasilimu. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما). Aathaar hii imepokelewa na Ibn Jariyr, na pia imesimuliwa na Ahmad, Ibn Hibbaan na wengineo. Adh-Dhahabiy ameiwafiki pamoja na Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah (3066)]

 

 

  

Share

090-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 090: إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan  090-Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru..

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ ﴿٩٠﴾ 

90. Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru; haitokubaliwa tawbah yao, na hao ndio waliopotoka.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremshwa kuhusu watu waliosilimu kisha wakaritadi kisha wakasilimu tena kisha wakaritadi. Wakatuma watu wao kwenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuulizia kuhusu jambo hilo. Na hapo ikateremka Aayah hii:

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ ﴿٩٠﴾ 

 

Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru; haitokubaliwa tawbah yao, na hao ndio waliopotoka. [(3:90). Amehadithia Ibn ‘Abbaas  (رضي الله عنهما) . Ameipokea Al-Haafidhw Abuu Bakr Al-Bazzaar – Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

 

 

Share

113-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 113: لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan   113-Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako

 

 

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾

113. Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba: (Siku moja) Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) aliichelewesha Swalaah ya ‘Ishaa, kisha akatoka kuja kuiswali Masjid na akawakuta Swahaba (رضي الله عنهم) bado wanamsubiri. Akasema: “Uhakika wa mambo ulivyo ni kuwa hakuna yoyote katika Watu wa Dini hizi anayemdhukuru Allaah katika wakati huu isipokuwa nyinyi tu.” Hapo ikateremka Aayah:

 

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ

Hawako sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu…  

 

 mpaka mwisho wa Aayah 115. [Hadiyth ya Ibn Mas’uwd ameipokea Al-Imaam Ahmad]  

 

 

 

Share

122-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 122: إِذْ هَمَّت طَّائِفَتَانِ مِنكُمْ أَن تَفْشَلَا وَاللَّـهُ وَلِيُّهُمَا ۗ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِذْ هَمَّت طَّائِفَتَانِ مِنكُمْ أَن تَفْشَلَا وَاللَّـهُ وَلِيُّهُمَا ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٢٢﴾

Pale makundi mawili miongoni mwenu walipofanya wasiwasi kwamba watashindwa nailhali Allaah Ndiye Mlinzi na Msaidizi wao.  Basi kwa Allaah Pekee Waumini watawakali. [Aal-‘Imraan (3:122)]

 

 

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka ikiwazungumzia Banuw Salamah na Banuw Haarithah kama alivyohadhithia Jaabir (رضي الله عنه) kwamba: Aayah hii imeteremshwa kuhusu sisi. Tulikuwa ni makabila mawili; Banuw Haarithah na Banuw Salamah. Tusingelipenda (kama isingeteremshwa). Sufyaan kasema: Tusingefurahi kama isingeteremshwa na hali Allaah Anasema:

 

وَاللَّـهُ وَلِيُّهُمَا

“Na Allaah Ndiye Mlinzi na Msaidizi wao.” [Amehadithia Jaabir (رضي الله عنه) na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share

128-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 128: لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan 128- Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au   

 

 

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

128. Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) kwamba: Alimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoinua kichwa chake kutoka rukuu’ ya mwisho ya Swalaah ya Alfajiri baada ya kusema:

سَمِعَ اَللَّهُ لِمَنْ حَمِدَه رَبَّنَا لَكَ اَلْحَمْدُ

“Sami’a-Allaahu liman hamidah Rabbanaa Lakal-Hamd.  

Allaah Amemsikia aliyemhimidi, Ee Rabb wetu, Himdi ni Zako Wewe

 

 

 Kisha akasema:

اللَّهُمَّ الْعَنْ فُلَانًا وفُلَانًا وفُلَانًا

“Allaahumma mlaani fulani na fulani na fulani.” Ikateremka:

 

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

 

Jambo hili halikuhusu wewe; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu. (3:128). [Al-Bukhaariy na wengineo kwa riwayaah nyenginezo]

 

 

Na Anas bin Maalik  (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Siku ya Uhud, jino la Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) lilivunjika na akachomwa mkuki begani mwake. Damu ikawa inamchirizika usoni mwake akawa anaifuta damu huku akisema: “Vipi watu watafaulu ikiwa wamerowanisha uso wa Nabiy wao kwa damu na hali yeye anawalingaia kwa Allaah?” Hapo ikateremka Aayah hii:

 

 لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

Jambo hili halikuhusu wewe; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu. (3:128). [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh]  

 

 

 

 

Share

154-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 154: ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan  154-Kisha Akakuteremshieni amani baada ya dhiki; usingizi unaofunika...

 

 

ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ ۖ وَطَائِفَةٌ قَدْ أَهَمَّتْهُمْ أَنفُسُهُمْ يَظُنُّونَ بِاللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ ۖ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ الْأَمْرِ مِن شَيْءٍ ۗ قُلْ إِنَّ الْأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّـهِ ۗ يُخْفُونَ فِي أَنفُسِهِم مَّا لَا يُبْدُونَ لَكَ ۖ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا ۗ قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ ۖ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّـهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٥٤﴾

154. Kisha Akakuteremshieni amani baada ya dhiki; usingizi unaofunika kundi miongoni mwenu na kundi likawashughulisha nafsi zao wakamdhania Allaah pasi na haki dhana ya kijahili; wanasema: “Je, tuna amri yoyote sisi katika jambo hili?” Sema: “Hakika amri yote ni ya Allaah.” Wanaficha katika nafsi zao yale wasiyokubainishia. Wanasema: “Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa.” Sema: “Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale walioandikiwa kuuawa kwenye mahali pa kuangukia wafe.” Ili Allaah Ayajaribu yale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyo zenu. Na Allaah ni Mjuzi kwa yaliyomo vifuani.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Abuu Twalhah (رضي الله عنه): “Niliinua kichwa changu siku ya Uhud nikawa ninatazama. Sikuona yeyote katika wao siku hiyo isipokuwa kila mtu alikuwa amesinzia, kila mmoja ameinama chini ya silaha yake ya kujilinda na kujihami katika vita. Na hiyo ndiyo Kauli ya Allaah:

 

 

ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ ۖ  

Kisha Akakuteremshieni amani baada ya dhiki; usingizi unaofunika kundi miongoni mwenu. [At-Tirmidhiy]  

 

Pia Az-Zubayr amehadithia kwamba: Nilikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati khofu ilizidi mno (katika vita vya Uhud) na Allaah Akatupa usingizi. Basi hapakuweko mtu ila alikuwa akisinzia (isipokuwa wanafiki). Wa-Allaahi! Kama kwenye ndoto nilisikia maneno ya Mu’attib bin Qushayr akisema:

 

لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا ۗ

Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa.

 

 Basi nikayahifadhi, kisha Allaah (تعالى)  Akateremsha:

 

ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ ۖ  

Kisha Akakuteremshieni amani baada ya dhiki; usingizi unaofunika kundi miongoni mwenu.

 

 mpaka Kauli Yake: tusingeliuliwa hapa.”

 

Kutokana na kauli ya Mu’attib bin Qushayr:

 

قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ ۖ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّـهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٥٤﴾

Sema: Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale walioandikiwa kuuawa kwenye mahali pa kuangukia wafe. Ili Allaah Ayajaribu yale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyo zenu. Na Allaah Anayajua vyema yaliyomo vifuani.

 

 [Ameipokea Ibn Raahwayh katika Al-Matwaalib Al-‘Aaliyah, (4/219)] 

 

 

 

 

Share

161-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 161: وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan   161-Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini

 

وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦١﴾

161. Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira). Na yeyote atakayekhini atakuja na kile alichokikhini Siku ya Qiyaamah. Kisha italipwa kamilifu kila nafsi yale iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituma jeshi, na jeshi hilo likarejeshewa bendera yake (yaani halikukubaliwa jeshi hilo ‘amali yake hiyo). Kisha akalituma tena likarejeshewa.  Halikukubaliwa ‘amali yake kwa sababu ya khiyaana iliyofanyika ya kutoweka kipande kikubwa cha dhahabu mfano wa kichwa cha mbuzi. Ndipo ikateremka:

 

 وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ  

Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira).

[Mu’jamu Atw-Twabaraaniy]

 

Pia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amehadithia kwamba Aayah hii:

 

 وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ

Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira).

 

Imeteremshwa kuhusiana na mahameli jekundu lilopotea siku ya Badr, kisha baadhi ya watu wakasema ameichukua Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Wakazidi kuendelea kusema hivyo, basi na hapo Allaah Akateremsha:

 

 وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦١﴾

Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira). Na yeyote atakayekhini atakuja na kile alichokikhini Siku ya Qiyaamah.  (3:161).  [Ameipokea Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema Hasan Ghariyb]

 

 

 

Share

165-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 165: أَوَلَمَّا أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُم مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّىٰ هَـٰذَا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan  165-Ulipokusibuni msiba ingawa mliwasibu (maadui) mara mbili yake

 

أَوَلَمَّا أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُم مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّىٰ هَـٰذَا ۖ قُلْ هُوَ مِنْ عِندِ أَنفُسِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٦٥﴾

165. Ulipokusibuni msiba ingawa mliwasibu (maadui) mara mbili yake mlisema: “Umetoka wapi huu?” Sema: “Huo ni kutoka kwenu wenyewe.” Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremshwa kuhusu makafiri kutokana na wao kulipiza kisasi cha yale yaliyowasibu katika vita vya Badr. Wakauawa Waislamu sabini siku ya Uhud, yakavunjwa meno ya mbele ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na likavunjwa yai juu ya kichwa chake, na damu zikachuruzika juu ya uso wake. Na hapo ikateremka Kauli ya Allaah:

 

أَوَلَمَّا أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُم مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّىٰ هَـٰذَا ۖ قُلْ هُوَ مِنْ عِندِ أَنفُسِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٦٥﴾

 

Ulipokusibuni msiba ingawa nyinyi mliwasibu (maadui) mara mbili yake mlisema: Umetoka wapi huu? Sema: Huo ni kutoka kwenu wenyewe. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) na imepokelewa na Ahmad].

 

 

 

Share

169-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 169: وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan  169-Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu….

 

 

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾ 

169. Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Rabb wao wanaruzukiwa.

 

فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١٧٠﴾ 

170. Wanafurahia kwa Aliyowapa Allaah kwa fadhila Zake na wanawashangilia ambao hawajaungana nao, walio nyuma yao, kwamba: “Hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.”

 

يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٧١﴾

171. Wanashangilia kwa neema za Allaah na fadhila na kwamba Allaah Hapotezi ujira wa Waumini.

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikutana nami siku moja akaniambia: “Ee Jaabir! Una nini nakuona una huzuni?” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Baba yangu amekufa shahidi na ameacha nyuma madeni na watoto. Akasema: “Je, nikujulishe kuwa Allaah Hajapata kuongea na mtu yeyote isipokuwa nyuma ya pazia? Lakini Amemhuisha baba yako na Akazungumza naye moja kwa moja. (Allaah) Akamwambia: Tamani (lolote) Nikupe!  Akasema: Yaa Rabb! Nihuishe (nirudi duniani) ili niuliwe tena kwa ajili Yako! Akasema Rabb (تبارك وتعالى): Nimeshatanguliza kauli kwamba wao hawatorudi tena (maisha ya dunia). Akasema: Yaa Rabb! Basi nifikishie khabari kwa niliowaacha nyuma. Kisha Allaah Akateremsha:

 

 وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾ 

Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika Njia ya Allaah kuwa ni wafu, bali wahai, wako kwa Rabb wao wanaruzukiwa.

 

فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١٧٠﴾ 

Wanafurahia kwa Aliyowapa Allaah kwa Fadhila Zake na wanawashangilia ambao bado hawajaungana nao, walio nyuma yao, kwamba: Hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.

 

يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٧١﴾

Wanashangilia Neema kutoka kwa Allaah na Fadhila na kwamba Allaah Hapotezi ujira wa Waumini. (3:169-171). [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Swahiyh At-Targhiyb (2276), Swahiyh At-Targhiyb (1361)]

 

 

 

 

Share

172-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 172: الَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ مِن بَعْدِ مَا أَصَابَهُمُ الْقَرْحُ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan 172-Wale waliomwitikia Allaah na Rasuli baada ya kuwasibu majeraha

 

 

الَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ مِن بَعْدِ مَا أَصَابَهُمُ الْقَرْحُ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا مِنْهُمْ وَاتَّقَوْا أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٢﴾

172. Wale waliomwitikia Allaah na Rasuli baada ya kuwasibu majeraha. Kwa wale waliofanya ihsaan miongoni mwao na wakawa na taqwa watapa ujira adhimu.

 

الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ ﴿١٧٣﴾

173. Wale walioambiwa na watu: “Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni.” Lakini hili liliwawazidishia iymaan wakasema: “Hasbuna-Allaah! Allaah Anatutosheleza, Mzuri Alioje Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.”

 

فَانقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ لَّمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ ﴿١٧٤﴾

174. Basi wakarudi na neema kutoka kwa Allaah na fadhila; halijawagusa ovu lolote; na wakafuatilia radhi za Allaah. Na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii mpaka Aayah 174 (3:172–174) zimeteremka pale washirikiana waliporudi Makkah kutoka Uhud.  Walipofika wakasema: “Hamjamuua Muhammad wala hamkuteka wanawake, ubaya ulioje mliofanya, rudini mkawamalize na kuwasagasaga! Ikamfikia khabari hii Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akaamrisha jeshi la Waislamu litoke (ili kuwaogopesha washirikina na kuwaonyesha kuwa Waislamu bado wako imara na wana uwezo mkubwa wa kukabiliana nao pamoja na kwamba wana majeraha ya vita). Wakatembea pamoja na maumivu na majeraha yao mpaka wakafikia (sehemu fulani ya) Hamraa Al-Asad au Bi-ir Abiy ‘Uyaynah.   Na hapo Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha:

 

الَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ مِن بَعْدِ مَا أَصَابَهُمُ الْقَرْحُ

Wale waliomwitikia Allaah na Rasuli baada ya kuwasibu majeraha.

 

Na Abu Sufyan alimwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Miadi yako ni msimu wa Badr ulipowauwa Swahaba wetu.” Basi waliokuwa waoga walirejea, ama walioshujaa  walijiandaa kwa vita  na biashara, wakamwendea lakini  hawakumkuta yeyote pamoja naye, wakafanya manunuzi, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

فَانقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ لَّمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ

Basi wakarudi na Neema kutoka kwa Allaah na Fadhila; halijawagusa ovu lolote. (3:174) [Atw-Twabaraaniy kwa Isnaa Swahiiyh].  

 

 

 

 

Share

186-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 186: لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan  186-Bila shaka mtajaribiwa katika mali zenu na nafsi zenu na bila shaka mtasikia

 

 

لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا أَذًى كَثِيرًا ۚ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ ﴿١٨٦﴾

186. Bila shaka mtajaribiwa katika mali zenu na nafsi zenu; na bila shaka mtasikia kutoka kwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na kutoka kwa wale walioshirikisha udhia mwingi. Lakini mkisubiri na mkawa na taqwa basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka ikibainisha mabaya aliyokuwa akiyafanya Myahudi Ka’b bin Al-Ashraf.    Alikuwa akimshambulia mno Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na anawashajiisha makafiri wa ki-Quraysh kumfanyia uadui Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).  Mayahudi wengine walikuwa pia wakimuudhi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na Swahaba zake.  Kisha Allaah Akamuamrisha Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) awasamehe na awapuuze Mayahudi hao. Ndipo hapo ikateremka Aayah hii. [Ka’b Ibn Maalik (رضي الله عنه)  ameipokea Abuu Daawuwd]

 

 

 

 

Share

188-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 188: لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوا وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan   188-Usiwadhanie kabisa wale wanaofurahia kwa waliyopewa

 

لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوا وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا فَلَا تَحْسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٍ مِّنَ الْعَذَابِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٨٨﴾ 

188. Usiwadhanie kabisa wale wanaofurahia kwa waliyopewa na wanapenda wasifiwe kwa wasiyoyatenda. Usiwadhanie kabisa kuwa watasalimika na adhabu. Nao watapata adhabu iumizayo.

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kuwazungumzia wanafiki kama alivyohadithia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) kwamba: “Katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), pale alipokuwa Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم) anatoka kwenda vitani, wanafiki walimkhalifu na kubakia nyuma wasiende vitani, na wakifurahi kwa kubakia kwao nyuma kinyume na (alivyofanya) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Kisha pale alipokuwa anarudi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) walitoa nyudhuru kwake na wakiapa na wakipenda wasifiwe kwa hayo waliyoyafanya, hapo ikateremka (hii Aayah…).” [Amehadithia Abuu Sai’yd (رضي الله عنه), ameipokea  Al-Bukhaariy na Muslim]  

 

 

Pia, Marwaan alimwambia mlinzi wake, Rafiy’ aende kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kumwambia: “Ingekuwa kila mtu miongoni mwetu anafurahia kwa aliyoyafanya na kupenda kusifiwa kwa ambayo hakuyatenda, basi ataadhibiwa na sisi tutaadhibiwa.” Ibn ‘Abbaas akasema: Mna nini na Aayah hii? Hakika Aayah hii imeteremshwa kuhusu Watu wa Kitabu. kisha akasoma Aayah:

 

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ ﴿١٨٧﴾

Na pale Alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu (Allaah Akawaambia): Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha. Lakini walikitupa nyuma ya migongo yao na wakakibadilisha kwa thamani ndogo. Basi ubaya ulioje kwa yale wanayoyanunua! [Aal-‘Imraan (3:187)]

 

 

Kisha Ibn ‘Abbaas akasoma:

 

لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوا وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا فَلَا تَحْسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٍ مِّنَ الْعَذَابِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٨٨﴾ 

Usiwadhanie kabisa wale wanaofurahia (mabaya) waliyoyafanya na wanapenda wasifiwe kwa (mazuri) wasiyoyatenda. Usiwadhanie kabisa kuwa watasalimika na adhabu. Nao watapata adhabu iumizayo. [Aal-‘Imraan (3:187)]

 

 Kisha akasema: “Waliulizwa jambo (waliokuwa na ujuzi nalo) na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) lakini walimficha kulijua na wakamuambia kinyume cha uhalisia wa jambo hilo, kisha wakaondoka wakifurahia kuwa wamemuongopea wakataka wasifiwe kwa hayo waliyoyaficha.” [Muslim]  

 

 

 

Share

199-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 199: وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَمَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan  199-Na miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo wanaomwamini Allaah  

 

وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَمَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِمْ خَاشِعِينَ لِلَّـهِ لَا يَشْتَرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩٩﴾

Na miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo ambao kwa hakika wanamwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwenu, na yaliyoteremshwa kwao, wananyenyekea kwa Allaah, na hawabadilishi Aayaat za Allaah kwa thamani ndogo. Hao watapata ujira wao kwa Rabb wao. Hakika Allaah Ni Mwepesi Mno wa Kuhesabu. [Aal-‘Imraan (3:199)]

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka alipofariki An-Najaashiy. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamrisha aswaliwe, wakatoka katika jangwa wakamswalia. [Al-Bukhaariy na Muslim] Imesemwa: Walipomswalia An-Najaashiy, baadhi ya watu walisema: “Unamswalia mtumwa wa kihabeshi?” Hapo ikateremka Aayah hii. [Imehadithiwa na Anas, Wahshiy na ‘Abdullaahi bin Az-Zubayr (رضي الله عنهم). Nayo imethibiti kwa irsaal kutoka kwa Hasan Al-Baswriy. “Watu wa Kitabu wamesema.”  Kwa mkusanyiko wa njia zake hizi inapanda daraja na kufanywa kuwa ni hoja]  

 

 

 

Share