004-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa

Sababu Za Kuteremshwa

(Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Suwrah An-Nisaa

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

Share

003-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 003: وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa 003-Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima

وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا ﴿٣﴾

Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima; basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne. Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea kudhulumu [

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kumzungumzia Bwana mmoja alimuoa binti ambaye ni yatima aliyekuwa akimlea na kumsimamia, kwa sababu hakuwa na mtu wa kumsimamia. Huyo bwana hakumuoa kwa sababu ya kumpenda kwani alikuwa haamiliani naye vizuri. Akamuoa kwa sababu yatima huyo alikuwa ana (mali ya) shamba la mitende. Hapo ikateremka Aayah hii.” [Hadiyth ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) Al-Bukhaariy na Muslim]

Share

006-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 006: وَابْتَلُوا الْيَتَامَىٰ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغُوا النِّكَاحَ فَإِنْ آنَسْتُم مِّنْهُمْ رُشْدًا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa  006-Na wajaribuni mayatima (akili zao) mpaka wakifikia umri...

وَابْتَلُوا الْيَتَامَىٰ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغُوا النِّكَاحَ فَإِنْ آنَسْتُم مِّنْهُمْ رُشْدًا فَادْفَعُوا إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ ۖ وَلَا تَأْكُلُوهَا إِسْرَافًا وَبِدَارًا أَن يَكْبَرُوا ۚ وَمَن كَانَ غَنِيًّا فَلْيَسْتَعْفِفْ ۖ وَمَن كَانَ فَقِيرًا فَلْيَأْكُلْ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِذَا دَفَعْتُمْ إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ فَأَشْهِدُوا عَلَيْهِمْ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٦﴾

6. Na wajaribuni mayatima (akili zao) mpaka wakifikia umri wa kuoa. Na mkihisi kupevuka kwao, basi wapeni mali zao. Wala msiile kwa israfu na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliyekuwa tajiri basi ajizuilie (kuchukua ujira); na aliyekuwa fakiri basi ale kwa kadiri ya kukubalika ki-shariy’ah. Mtapowapa mali zao washuhudizeni. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mwenye Kuhisabu.

Sababun-Nuzuwl: 

Aayah hii imeteremka ikiwa inabainisha hukmu kuhusu mali ya yatima. Mlezi wa yatima huyo anapokuwa ni fakiri, basi anaweza kula katika mali hiyo kwa wema bila ya israaf. [Amehadithia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) na Al-Bukhaariy na Muslim wameipokea]

Share

011-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 011: يُوصِيكُمُ اللَّـهُ فِي أَوْلَادِكُمْ ۖ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa  011-Allaah Anakuamrisheni kuhusu watoto wenu. Mwanamume atastahiki

يُوصِيكُمُ اللَّـهُ فِي أَوْلَادِكُمْ ۖ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۚ فَإِن كُنَّ نِسَاءً فَوْقَ اثْنَتَيْنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَ ۖ وَإِن كَانَتْ وَاحِدَةً فَلَهَا النِّصْفُ ۚ وَلِأَبَوَيْهِ لِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُ وَلَدٌ ۚ فَإِن لَّمْ يَكُن لَّهُ وَلَدٌ وَوَرِثَهُ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ الثُّلُثُ ۚ فَإِن كَانَ لَهُ إِخْوَةٌ فَلِأُمِّهِ السُّدُسُ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِي بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ لَا تَدْرُونَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ لَكُمْ نَفْعًا ۚ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١١﴾ 

11. Allaah Anakuamrisheni kuhusu watoto wenu. Mwanamume atastahiki mfano wa fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake ni zaidi ya wawili basi watastahiki theluthi mbili za alichoacha (maiti). Lakini akiwa mtoto wa kike ni mmoja pekee basi atastahiki nusu, na wazazi wake wawili kila mmoja wao atastahiki sudusi katika alichoacha ikiwa anaye mtoto. Na ikiwa hakuwa na mtoto na wazazi wake wawili ndio warithi wake, basi mama yake atastahiki theluthi moja. Na ikiwa anao ndugu basi mama yake atastahiki sudusi, baada ya kutoa wasia aliousia (maiti) au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu hamjui ni yupi miongoni mwao aliye karibu zaidi kwenu kwa manufaa. Ni Shariy’ah kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii pamoja na Aayah ya mwisho katika Suwrah hii (3:176) imeteremka kuhusu Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) pale alipotembelewa na Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa na Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه) wakamkuta amezimia. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatawadha na akamrashia maji kutokana na wudhuu wake.  Kisha Jaabir (رضي الله عنه) akamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Niifanye vipi mali yangu?” Hapo ikateremka Aayah hii. [Amehadithia Jaabir (رضي الله عنه) na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]

Share

019-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 019: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا النِّسَاءَ كَرْهًا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa    019-Enyi walioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa kuwakirihisha

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا النِّسَاءَ كَرْهًا ۖ وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّـهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا ﴿١٩﴾

19. Enyi walioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa kuwalazimisha. Na wala msiwazuie kwa inda ili mpokonye baadhi ya vile mlivyowapa isipokuwa wakiwa wamefanya uchafu bayana. Na kaeni nao kwa wema. Na mkiwachukia, basi asaa ikiwa mnachukia jambo na Allaah Akalijaalia kuwa lenye khayr nyingi ndani yake.

Sababun-Nuzuwl:

Walikuwa Waarabu zama za Jaahiliyyah pindi anapokufa mwanaume na akaacha mke, basi wale ndugu wa mume wake wanakuwa na haki zaidi kwa mwanamke, na   baadhi yao wakitaka wanamuoa, na wakitaka wanamuozesha, na wakitaka hawamuozeshi, na wao wanakuwa wana haki naye zaidi kuliko hata ndugu zake mwanamke na wazazi wake. Ndipo Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha Aayah hii. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  na imepokelewa na Al-Bukhaary]  

Share

022-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 022: وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa     022-Na wala msiwaoe wanawake waliowaoa baba zenu isipokuwa

وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۚ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَمَقْتًا وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٢٢﴾

22. Na wala msiwaoe wanawake waliowaoa baba zenu isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika hayo yalikuwa ni uchafu na chukizo na njia ovu.

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kwa kuwa watu wa zama za Jaahiliyyah walikuwa wanaharamisha yaliyo ya haramu isipokuwa mke wa baba. Na walikuwa wanakusanya mabinti wawili ambao ni ndugu katika ndoa moja na kwa wakati mmoja, kisha ikateremka Aayah hii pamoja na Kauli ya Allaah Aliposema:

  وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمْ تَكُونُوا دَخَلْتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ

… na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu ambao mmewaingilia. Lakini ikiwa hamkuwaingilia basi hakuna dhambi (kuwaoa). Na (mmeharamishwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja, isipokuwa yaliyokwisha pita. [An-Nisaa (4:23)] [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  na imetajwa na Ibn Jariyr Atw-Twabariy katika Tafsiyr yake]  

Share

024-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 024: وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa     024-Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa...

وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُم بِهِ مِن بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٢٤﴾

24. Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni shariy’ah ya Allaah kwenu. Na mmehalalishiwa wengineo wasiokuwa hao, mtafute (kuwaoa) kwa mali zenu mkijistahi pasi na kuzini. Basi mliostarehe nao, wapeni mahari yao kuwa ni waajib. Na wala si dhambi kwenu katika mliyoridhiana baada ya yaliyowajibika. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kuhusu Maswahaba (رضي الله عنهم) , kwani wao siku ya Awtwaas (eneo lilipo baina ya Makkah na Twaaif ambapo walipatikana mateka baada ya vita vya Hunayn mwaka wa 8 Hijriyyah) walipata wanawake ambao ni mateka, basi wakaona uzito kuwaingilia kwa sababu waume zao ni washirikina. Allaah  (عزّ وجلّ) Akateremsha Aayah hii:

وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ  

24. Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume.

[Amehadithia Abuu Sa’iyd (رضي الله عنه)  na imepokelewa na Muslim]

Share

043-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 043: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa  043- Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa….

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا ﴿٤٣﴾

Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa mpaka mjue mnayoyasema, na wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho. Na mkiwa wagonjwa au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi ikusudieni ardhi safi ya mchanga (mtayammam), mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Kughufuria  [An-Nisaa (4:43)]

Sababun-Nuzuwl:

Sababu ya kuteremshwa hukmu ya tayammum:

Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها)  amehadithia: “Tulikwenda katika moja ya safari tukafika Al-Baydaa au Dhaatul-Jaysh ambako kidani changu kilivunjika (na kikapotea). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anakitafuta, kisha pia watu wengineo wakainuka kukitafuta. Hapakuweko na maji sehemu hiyo, basi watu wakamwendea Abuu Bakr Asw-Swiddiyq na kusema: Huoni alivyofanya ‘Aaishah? Kamfanya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na watu wakae sehemu ambayo hakuna maji! Abuu Bakr akaja wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amelala akiwa amelaza kichwa chake mapajani mwangu. Akaniambia: Umemzuia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na watu sehemu ambako hakuna maji na wala hawana (akiba ya) maji. Basi akanigombesha na akasema Aliyomjaalia (Allaah) kusema kuhusu mimi na akanipiga ubavuni kwa mkono wake. Hakuna kilichonizuia kusogea (kutokana na maumivu) isipokuwa kwa vile Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amelala mapajani mwangu. Hapo Allaah Akateremsha Aayah ya tayammum (4:43), basi wakatayammam. ‘Usayd bin Al-Hudhwayr akasema: Ee ahli ya Abuu Bakr! Hii si baraka ya kwanza kwenu. Kisha akaendeshwa ngamia ambaye nilikuwa nimempanda na tukakipata kidani chini yake.” [Al-Bukhaariy]

Sababun-Nuzuwl:

Uharamisho Wa Pombe:

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ

43. Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa

Ni kwamba, hatua ya kwanza kuhusu pombe imetahadharishwa katika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ

 Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake[Al-Baqarah (2:219)]

Hii ni hatua ya pili ya kukatazwa pombe katika nyakati za Swalaah kwa sababu Maswahaba walikosea kusoma Qur-aan katika Swalaah kutokana na kulewa. Baada ya hapo ikafutwa hukmu hii na ikabakia pombe kuwa ni haramu nyakati zote kwa Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) katika

Suwrat Al-Maaidah:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾

Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli, ni najisi na chukizo kutokana na kazi ya shaytwaan. Basi jiepusheni navyo mpate kufaulu. (5:90):

Share

051-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 051: أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa 051-Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na ...

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا ﴿٥١﴾

Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na wanasema juu ya wale waliokufuru kuwa: Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini.

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا ﴿٥٢﴾

Hao ndio wale Allaah Aliowalaani. Na ambaye Allaah Amemlaani basi hutamkuta kuwa na mtu wa kumsaidia. [An-Nisaa (4:51-52)

Sababun-Nuzwul:

Aayah hii imeteremshwa kama alivyohadithia ‘Ikrimah (رضي الله عنه) kwamba Huyay bin Akhtab na Ka’b Al-Ashraf (Wakuu wa ki-Yahudi) walikuja kwa watu wa Makkah (washirikina) wakawaambia: Nyinyi (Mayahudi) ni Ahlul-Kitaab na wenye ‘ilmu, hivyo basi tujulisheni (tofauti zetu) kuhusu sisi na kuhusu Muhammad. Wakasema: Jielezeni kuhusu nyinyi na kuhusu Muhammad. Wakasema: Sisi tunaunga ujamaa wa uhusiano wa damu, tunachinja ngamia (kwa ajili ya mafukara), tunasamehe madeni, tunawapa maji Mahujaji. Ama Muhammad, yeye hana watoto wa kiume, amekata ujamaa wa uhusiano wa damu, na wevi wa Mahujaji (kabila la) Ghifar wanamfuata. Basi je, sisi bora au yeye? Wakasema: Nyinyi bora zaidi na mlioongoka zaidi katika njia. Hapo Allaah Akateremsha:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا ﴿٥١﴾

Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini itikadi potofu na twaghuti na wanasema juu ya wale waliokufuru kuwa: Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini.

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا ﴿٥٢﴾

Hao ndio wale Allaah Aliowalaani. Na ambaye Allaah Amemlaani basi hutamkuta kuwa na mtu wa kumsaidia. [An-Nisaa (4:51-52)]

Share

058-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 058: إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa    058-Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe…

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿٥٨﴾

58. Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. Na mtakapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Ni uzuri ulioje wa Anayokuwaidhini kwayo Allaah! Hakika Allaah daima ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii ni ya pekee katika Suwrah hii ya An-Nisaa (4:58) ambayo imeteremka Makkah. Imeteremshwa Siku ya Fat-h Makkah (Ushindi). Ibn Jurayj amehadithia kwamba imeteremshwa kuhusu ‘Uthmaan bin Twalhah pale Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipochukua ufunguo wa Ka’bah kutoka kwake akaingia Ka’bah. Alipotoka nje ya Ka’bah, alitoka huku akiwa anasoma:

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا

Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe.”

Hapo akamwita ‘Uthmaan bin Twalhah na akampa funguo. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]. Funguo hizo zimeendelea kubakia katika ukoo huo, kizazi baada ya kizazi mpaka sasa, na mpaka Siku ya Qiyaamah ukoo huo umefadhilishwa kuwa ndio wenye amana ya kukamata funguo za Al-Ka’bah.

Share

059-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 059: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa    059- Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka...

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾

59. Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi.

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kuhusu ‘Abdullaah Ibn Hudhaafah (رضي الله عنه) pale alipotumwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwenye msafara wa Jihaad. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]

Pia Imeteremshwa pale Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotuma jeshi chini ya uongozi wa mtu mmoja wa Answaar. Walipoondoka, aliwaghadhibikia kwa sababu fulani akawaambia: Kwani Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakukuamrisheni mnitii? Wakasema: Ndio! Akasema: Okoteni kuni. Kisha akawasha moto akasema: Nakuamrisheni muingie motoni humu. Wakakaribia watu kuuingia lakini kijana mmoja miongoni mwao akasema: Nyinyi mmekimbia moto kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hivyo msikimbilie mpaka mrudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha akikuamrisheni kuingia hapo muuingie. Waliporudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamwelezea yaliyojiri, kisha yeye akasema: “Mngeliuingia, msingetoka kamwe humo. Hakika utiifu ni katika mema.” [Al-Bukhaariy na Muslim]  

Share

060-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 060: أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa 060-Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿٦٠﴾

60. Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako; wanataka wahukumiane kwa twaghuti (ubatilifu) na hali wameamrishwa wakanushe hayo. Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali.

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii pamoja na mbili zinazofuatia (4:60-62) zimeteremka kama alivyohadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kuwa Abuu Barzah Al-Aslamiyy alikuwa ni Kuhani akitoa hukumu kuhusu magomvi yanayotokea baina ya Mayahudi. Siku moja baadhi ya watu katika washirikina walileta magomvi kwake, kisha Allaah Akateremsha Aayah hii:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ  

60. Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)  

[Abuu Haatim Atw-Twabaraaniy, na Ibn Hajar Al-‘Asqalaaniy (4/19) ambaye amesema isnaad yake ni nzuri]  

Sababun-Nuzuwl:

Pia Sababun-Nuzuwl nyingine ya Aayah hii ni kwamba waligombana mtu kutoka Answaar na Myahudi kisha Myahudi akasema: “Twende kwa Muhammad akatuhukumu.” Na yule Answaar akasema: “Twende kwa Ka’ab bin Al-Ashraf.” Imesemwa pia kuwa miongoni mwa wanafiki waliokuwa wakijidai kuwa ni Waislamu, lakini huku wakitafuta hukmu za kijaahiliyyah. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

Pia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amesema: “Abuu Barzah Aslamiyy alikuwa mtabiri na akihukumu magomvi ya Mayahudi. Baadhi ya Waislamu walipomwendea kutaka awahukumu, Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿٦٠﴾

Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako; wanataka wahukumiane kwa twaghuti (ubatilifu) na hali wameamrishwa wakanushe hayo. Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali.

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا ﴿٦١﴾

Na wanapoambiwa: Njooni kwenye yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Rasuli, utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwa mkengeuko.

فَكَيْفَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ثُمَّ جَاءُوكَ يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا إِحْسَانًا وَتَوْفِيقًا ﴿٦٢﴾

Basi itakuwaje utakapowafika msiba kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao? Kisha wakakujia wakiapa Wa-Allaahi hatukutaka ila mazuri na mapatano.  [(4:60-62) - Atw-Twabaraaniy]  

Share

065-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 065: فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

065-Basi mambo si kama wanavyodai. Naapa kwa Rabb wako, hawatakuwa Waumini wa kweli mpaka

 فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

Basi mambo si kama wanavyodai. Naapa kwa Rabb wako, hawatakuwa Waumini wa kweli mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao ukakasi katika yale uliyohukumu na waikubali hukmu yako kwa moyo safi na maridhio [An-Nisaa: 65]

Aayah hii imeteremka kuhusu Az-Zubayr bin Al-‘Awwaam (رضي الله عنه)  na bwana mmoja katika Answaar, pale walipokhitilafiana kuhusu mfereji wa kupitisha maji ya mvua waliokuwa wakitumia maji yake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoa hukmu baina yao kwamba Az-Zubayr amwagilie maji ardhini mwake kisha ayaache yatiririke kwa Answaar. Akakasirika Answaar huyo na kumwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Umempendelea yeye kwa kuwa ni mtoto wa ‘ammat yako! Hapo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akabadilika uso rangi kwa hasira na akamwambia tena Az-Zubayr amwagie maji kwanza kisha ayaachie yatiririke kwa jirani yake huyo kwa kuwa hukumu hiyo ilikuwa kwa manufaa ya wote wawili. Hivyo akampatia Az-Zubayr haki yake. Ikateremka Aayah hii:

 فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

Basi mambo si kama wanavyodai. Naapa kwa Rabb wako, hawatakuwa Waumini wa kweli mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao ukakasi katika yale uliyohukumu na waikubali hukmu yako kwa moyo safi na maridhio [An-Nisaa: 65]

[Amehadithia Az-Zubayr (رضي الله عنه) na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]  

Share

069-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 069: وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa   069-Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja...

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾

69. Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiqiyna na Mashuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kuhusu Answaar mmoja ambaye alikuwa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa na huzuni. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza: “Mbona nakuona umehuzunika?” Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Nilikuwa natafakari jambo. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Jambo gani?” Akajibu: Kila siku tunakuja kwako asubuhi na usiku tukitazama uso wako na kukaa kitako nawe. Lakini kesho (Aakhirah), utakuja kufufuliwa pamoja na Manabii na hivyo sisi hatutoweza kukuona tena.  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakusema kitu, kisha Jibriyl (عليه السلام)  akamjia  kumteremshia Aayah hii:

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾

Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiqiyna na Mashuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao! (4:69)

 [Ibn Jariyr, Tafsiyr Ibn Kathiyr]

Sababun-Nuzuwl:

Pia Sababun-Nuzuwl ya Aayah hii, ni kama alivyohadithia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wewe ni kipenzi kwangu kuliko nafsi yangu, na kipenzi kwangu kuliko ahli yangu, na kipenzi kwangu kuliko wanangu. Na hakika ninapokuwa nyumbani kwangu nakukumbuka, basi huwa siwezi kusubiri mpaka nije kukutazama. Na ninapokumbuka mauti yangu na mauti yako, basi hutambua kwamba wewe utakapoingia Jannah utapanda pamoja na Manabii, lakini nitakapoingia mimi Jannah nakhofu kuwa sitokuona! Basi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumjibu mpaka hapo ikateremshwa:

وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾

Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiqiyna na Mashuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao! (4:69).

[At-Twabaraaniy katika Al-Mu’jamu Asw-Swaghiyr]

Share

077-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 077: أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوا أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa   077-Je, huoni wale walioambiwa: “Zuieni mikono yenu…

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوا أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَخْشَوْنَ النَّاسَ كَخَشْيَةِ اللَّـهِ أَوْ أَشَدَّ خَشْيَةً ۚ وَقَالُوا رَبَّنَا لِمَ كَتَبْتَ عَلَيْنَا الْقِتَالَ لَوْلَا أَخَّرْتَنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ ۗ قُلْ مَتَاعُ الدُّنْيَا قَلِيلٌ وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّمَنِ اتَّقَىٰ وَلَا تُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٧٧﴾

Je, huoni wale walioambiwa: Zuieni mikono yenu (msipigane) na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah. Basi walipoandikiwa amri kupigana, mara kundi miongoni mwao linawaogopa watu kama kumwogopa Allaah au woga zaidi. Na husema: Rabb wetu!  Kwa nini Umetuamrisha kupigana? Lau Ungelituakhirishia hadi muda kidogo hivi! Sema: Starehe za dunia ni chache; na Aakhirah ni bora zaidi kwa mwenye taqwa; wala hamtodhulumiwa kadiri ya uzi wa kokwa ya tende. [An-Nisaa (4:77)]

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremshwa kama alivyohadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kwamba: ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf na Swahaba wenzake  (رضي الله عنهم)  walipokuwa Makkah walimwendea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Tulipokuwa washirikina tulikuwa kwenye ‘izzah (hadhi na utukufu) lakini sasa tumeingia Uislamu tumekuwa madhalili. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika mimi nimeamrishwa kusamehe basi msifanye qitaal (vita).” Kisha Allaah Alipomuamrisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhajiri Madiynah, Alimuamrisha Jihaad na qitaal (dhidi ya washirikina), basi (wao Waislamu) wakasita. Hapo ikateremshwa Aayah hii. [An-Nasaaiy na Al-Haakim]  

Share

083-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 083: وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa    083-Na linapowafikia jambo lolote kuhusu amani au khofu hulitangaza...

وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٣﴾

Na linapowafikia jambo lolote kuhusu amani au khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Rasuli na kwa wenye madaraka kati yao, basi watakaolitafiti miongoni mwao wangelipatia jibu jambo hilo (kama linafaa kutangazwa au kufichwa). Na lau si Fadhila ya Allaah juu yenu na Rahmah Yake kwa yakini mngelimfuata shaytwaan ila wachache tu. (4:83)

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kuhusu kujitenga mbali  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na wakeze kwa muda mwezi na baadhi ya Swahaba wakadhani kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amewataliki wakeze:

Amehadithia  ‘Umar (رضي الله عنه) kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipojitenga mbali na wake zake, niliingia Masjid nikakuta watu wakipiga ardhi kwa changarawe wakisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewataliki wake zake! Na hivyo ni kabla ya kuamrishwa hijaab. ‘Umar akasema: Nitatambua hilo leo. Basi nikamwendea ‘Aaishah (رضي الله عنها) nikamwambia: Yaa bint Abiy Bakr! Je, hivi imekufikia kumuudhi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: Jambo langu halikuhusu wewe, na jambo lako halinihusu mimi yaa bin Al-Khattwaab, bali la wajibu kwako ni kumuwaidhi (bint yako)! Nikamwendea Hafswah bint ‘Umar nikamwambia: Yaa Hafswah! Imenifikia (khabari) kwamba umemuudhi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na nimetambua kuwa hakupendi! Na lau ningekuwa (si baba yako) angekutaliki! Hafswah akalia sana. Nikamwambia: Yuko wapi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: Yuko chumba cha darini. Nikaenda nikamkuta Rabaah, mtumishi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekaa kitako kingoni mwa dirisha akinin’giniza miguu yake juu katika ufumbi wa shina la mtende ambalo humsaidia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kupanda (chumba cha darini) na kuteremkia. Nikamwambia: Yaa Rabaah! Niombee idhini kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Rabaah akatazama chumbani kisha akanitazama mimi wala hakusema kitu. Kisha nikasema: Yaa Rabaah! Niombee idhini kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Rabaah akatazama chumbani kisha akanitazama mimi wala hakusema kitu. Kisha nikapandisha sauti yangu nikasema: Yaa Rabaah! Niombee idhini kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), mimi nadhani kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anadhania kuwa nimekuja kwa ajili ya Hafswah! Wa-Allaahi kama Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ataniamrisha nimpige (nimkate) shingo yake nitampiga! Nikapandisha sauti yangu akaniashiria nipande (kuingia chumba cha darini). Nikaingia kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikamkuta amelalia jamvi.

Nikakaa kitako, naye akaivuta shuka yake na hakuwa na nyingine (isipokuwa hiyo tu), na jamvi hilo lilimfanyia alama ubavuni mwake. Nikatazama kwa macho yangu hicho kijichumba cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikakuta shayiri kiasi kiasi cha kibaba kimoja na kiasi cha matawi ya mimosa yamewekwa pembeni mwa chumba na mkoba wa ngozi uliobadilishwa rangi. Nikatokwa na machozi (kuona maisha duni anayoishi).

Akasema: “Nini kinachokuliza yaa Ibn Al-Khattwaab?” Nikasema: Ee Nabiyy wa Allaah! Na kwa nini nisilie na hali jamvi limekufanyia alama ubavuni mwako na sioni kitu chumbani mwako humu (isipokuwa vitu vichache mno)?  (Mfalme) Qayswar na Kisraa wanaishi maisha ya kifakhari lakini wewe Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye Amekuteua (Allaah) hiki ndicho kijichumba chako? Akasema: “Ee Ibn Al-Khattwaab! Hivi huridhiki kuwa sisi tuna Aakhirah nao wana dunia?” Nikasema: Ndio. Kisha nilipoingia kwanza niliona usoni mwake alama za ghadhabu, basi nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Unatatizwa nini na wanawake? Ungeliwataliki basi hakika Allaah Yuko pamoja nawe, na Malaika Wake na Jibriyl, na Mikaaiyl na mimi, na Abuu Bakr, na Waumini (wote) tuko nawe. Na kichache nilichosema (siku ile) na namhimidi Allaah, nilitaraji kwamba Allaah Atasadikisha kauli yangu. Basi ikateremka Aayah hii ya At-Takhyiyr (kuchaguzwa):

إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ﴿٤﴾

Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah (basi ni kheri kwenu), kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (kwa yanayomchukiza Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mlinzi Msaidizi wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia.

عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا﴿٥﴾

Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Waislamu, Waumini, watiifu na wanyenyekevu, wanaotubia, wenye kufanya ‘ibaadah, wanaofunga Swiyaam au wanaohajiri kwa ajili ya Allaah, wajane, na walio bikra. [At-Tahriym (66:4-5)]

Na walikuwa ni ‘Aaishah bint wa Abuu Bakr na Hafswah ambao walishikilia na kusaidiana (kudai mali) kuliko wake wote wengine wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, umewataliki? Akasema: “Hapana.” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika niliingia Masjid nikakuta Waislamu wanacheza kwa vichangarawe (huku dhana zimewashughulisha) wakisema kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewataliki wake zake. Je, niende kuwajulisha kuwa hukuwataliki? Akasema: “Naam ukipenda.” Nikaendelea kuongea naye mpaka (nikatanabahi) alama za ghadhabu zimepotea usoni mwake na mpaka (huzuni yake ikageuka kuwa ni furaha na hivyo) uso wake ukarudi kuwa na bashasha kama kawaida yake, akacheka na meno yake yalikuwa ya kupendeza mno kuliko watu wote! Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akateremka, nami nikateremka huku nikikamata shina la mtende, naye Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akateremka (kwa wepesi kabisa) bila ya kukamata chochote mkononi mwake (kujizuilia). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Ulikuwa chumbani mwako siku ishirini na tisa. Akasema: (Mara nyingine) “Mwezi huwa ni siku ishirini na tisa.” Nikasimama mlangoni mwa Masjid nikaita kwa sauti yangu ya juu kabisa: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwataliki wake zake! Hapo ikateremka Aayah hii:

وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٣﴾

Na linapowafikia jambo lolote kuhusu amani au khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Rasuli na kwa wenye madaraka kati yao, basi watakaolitafiti miongoni mwao wangelipatia jibu jambo hilo (kama linafaa kutangazwa au kufichwa). Na lau si Fadhila ya Allaah juu yenu na Rahmah Yake kwa yakini mngelimfuata shaytwaan ila wachache tu. (4:83).

Ikawa ni mimi niliyetafiti jambo hilo. Na Allaah Akateremsha Aayah ya At-Takhyiyr [At-Tahriym (66:4-5)].  [Al-Bukhaariy na Muslim]  

Share

088-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 088: فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa     088-Basi mna nini mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki…

فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿٨٨﴾

Basi mna nini mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki; na Allaah Amewageuza (warudie ukafiri) kwa sababu ya waliyoyachuma. Je, mnataka kumwongoa ambaye Allaah Amempotoa? Na aliyepotozwa na Allaah basi hutompatia kamwe njia (ya kumwongoa).(4:88).   

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kuwazungumzia baadhi ya watu ambao walikuwa wametoka pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake kwenda katika vita vya Uhud. Wakarejea nyuma na hawakuungana na wenzao. Pakawa katika Swahaba, kuna makundi mawili; kundi moja likawa linasema tuwapige vita! Na kundi jingine likawa linasema hapana! Hapo ikateremka Aayah hii:

فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿٨٨﴾

Basi mna nini mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki; na Allaah Amewageuza (warudie ukafiri) kwa sababu ya waliyoyachuma. Je, mnataka kumwongoa ambaye Allaah Amempotoa? Na aliyepotozwa na Allaah basi hutompatia kamwe njia (ya kumwongoa).(4:88).   

 [Amehadithia Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه)   na kupokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]  

Sababun-Nuzuwl:

Pia Sababun-Nuzuwl: Al-‘Awf (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba Aayah hii imeteremshwa kuhusu baadhi ya watu wa Makkah ambao walisema wameingia Uislamu lakini huku wakiwaunga mkono washirikina. Walipokwenda Makkah kutimiza mahitaji yao wakaambizana: “Tutakapokutana na Maswahaba wa Muhammad hakutakuwa na madhara yoyote upande wetu.” Waumini walipopata khabari kwamba watu hao wameenda Makkah, wakasema baadhi yao: “Twendeni kwa waoga hao tuwaue kwa sababu wanawaunga mkono maadui zenu dhidi yenu!” Lakini kundi jingine la Waumini wakasema: “Subhaana Allaah! Mnataka kuua watu wanaosema kama mlivyosema kwa sababu tu hawakuhajiri au kuacha ardhi yao? Kwani inaruhusiwa kumwaga damu na kutaifisha mali yao katika hali hii?” Basi wakagawanyika makundi mawili, na wakati huo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa nao na hakukataza kundi lolote kuhusu mabishano yao. Hapo Allaah Akateremsha:

فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿٨٨﴾

Basi mna nini mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki; na Allaah Amewageuza (warudie ukafiri) kwa sababu ya waliyoyachuma. Je, mnataka kumwongoa ambaye Allaah Amempotoa? Na aliyepotozwa na Allaah basi hutompatia kamwe njia (ya kumwongoa.(4:88).   

[Ibn Abiy Haatim Tafsiyr Ibn Kathiyr]

Share

094-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 094: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa  094-Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo..

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٩٤﴾

Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo, na wala msimwambie anayekuamkieni kwa As-salaam: Wewe si Muumin kwa sababu ya kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan, basi fanyeni uhakiki. Hakika Allaah daima kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:94).

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kumzungumzia bwana mmoja ambaye alionekana kwenye vita akiwa ana msururu wa ghanima (ngawira) kisha Waislamu wakamfuata mbio. Yule bwana alipoona Waislamu wamemfikia aliwasalimia, lakini Waislamu walimuua na wakachukua ghanima zake. Na hapo ikateremka hii Aayah hii:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٩٤﴾

Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo, na wala msimwambie anayekuamkieni kwa As-salaam: Wewe si Muumin kwa sababu ya kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan, basi fanyeni uhakiki. Hakika Allaah daima kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:94).

[Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]  

Na At-Tirmidhiy na Imaam Ahmad wamerekodi kwamba:

Wakanong’onezana kwamba: “Anasema As-Salaam apate kujihami tu!” Wakamuua kisha wakaenda kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na kondoo hao, ndipo ikateremshwa Aayah hii

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٩٤﴾

Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo, na wala msimwambie anayekuamkieni kwa As-salaam: Wewe si Muumin kwa sababu ya kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan, basi fanyeni uhakiki. Hakika Allaah daima kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

(4:94).  

Na Imaam Ahmad amerekodi kwamba Al-Qa’qaa’ bin ‘Abdillaah bin Abiy Hadrad amehadithia kwamba baba yake ‘Abdullaah bin Abiy Hadrad alisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitutuma (maeneo ya) ‘Adhwam. Nikatoka pamoja na kundi la Waislamu ambamo alikuweko Abuu Qataadah, Al-Haarith bin Rab’iy na Muhallam bin Juthmaamah bin Qays. Tukaendelea mpaka tukafika eneo la ‘Adhwam ambako ‘Aamir Al-Ashja’iy alitupitia akiwa amepanda ngamia wake. Alipotupitia akatusalimia na hatukumhujumu. Lakini Muhallam bin Juthmaamah alimuua na kuchukua ngamia wake kwa sababu ya matatizo baina yao. Tuliporudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) tukamuhadithia yaliyotokea, hapo ikatuteremkia Qur-aan:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٩٤﴾

Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo, na wala msimwambie anayekuamkieni kwa As-salaam: Wewe si Muumin kwa sababu ya kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan, basi fanyeni uhakiki. Hakika Allaah daima kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:94).

Share

095-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 095: لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa   095-Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani)…

لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ وَالْمُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۚ فَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ عَلَى الْقَاعِدِينَ دَرَجَةً ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَفَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ عَلَى الْقَاعِدِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٩٥﴾

Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani), isipokuwa wale wenye udhuru, na kati ya wenye kupigana Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao. Allaah Amewafadhilisha kwa cheo wenye kupigana Jihaad kwa mali zao na nafsi zao kuliko waliokaa nyuma. Na wote Allaah Amewaahidi Al-Husnaa (Jannah). Na Allaah Amewafadhilisha wenye kupigana Jihaad kwa ujira mkubwa mno kuliko wanaokaa (nyuma) (4:95).

Sababun-Nuzuwl:

Ilipoteremka Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ   

Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani). (4:95)

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwamrisha Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه)  aiandike, na mara hapo akaja ‘Abdullaah bin Ummi Maktuwm(رضي الله عنه) akilalamika kuhusu upofu wa macho yake. Na hapo ikateremka Kauli ya Allaah kwa kuongezeka:

غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ

Isipokuwa wale wenye udhuru  (4:95).

[Amehadithia Al-Baraa bin ‘Aazib na Zayd bin Thaabit(رضي الله عنهما)  na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]

Sababun-Nuzuwl:  Katika riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy, Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy amehadithia kwamba: Nilimuona Marwaan bin Al-Hakam amekaa kitako Masjid. Nikamkabili na nikaketi karibu naye. Akatujulisha kwamba Zayd bin Thaabit amemwambia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesomea imla Aayah hii:

لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ   

Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani). (4:95)

Kisha Ibn Ummi Maktuwm akaja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati akinisomea Aayah ili niiandike. Ibn Ummi Maktuwm akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Ningekuwa na uwezo bila shaka ningeshiriki katika Jihaad. Alikuwa ni kipofu, basi hapo Allaah Akamteremshia Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati mapaja yake yakiwa juu yangu na yakawa mazito mno kwangu (kutokana na Wahyi kuteremka) mpaka nikakhofia kuwa mapaja yangu yatavunjika. Kisha Allaah Akateremsha:

غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ

Isipokuwa wale wenye udhuru

Pia Sababun-Nuzuwl:  At-Tirmidhiy amerekodi kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amehadithia kwamba:

لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ   

Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani). (4:95)

Inahusiana na wale wasiotoka kwenda kupigana vita vya Badr na wale waliokwenda Badr. Wakati vita vya Badr vilipokaribia kuanza, Abuu Ahmad bin Jahsh na Ibn Maktuwm walisema: Ee Rasuli wa Allaah! Sisi ni vipofu, je, tuna udhuru? Hapo ikateremshwa:

لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ  

Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani), isipokuwa wale wenye udhuru (4:95).

Share

097-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 097: إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa 097-Hakika wale ambao Malaika wanawafisha hali ya kuwa …

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٩٧﴾

Hakika wale ambao Malaika wanawafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao, (Malaika) watawaambia: Mlikuwa katika hali gani? Watasema: Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.  (Malaika) Watasema: Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni Jahannam, na uovu ulioje mahali pa kuishia!

إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا ﴿٩٨﴾

Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata hila yoyote wala hawawezi kuongoza njia. (4:97-98)

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Muhammad bin ‘Abdir-Rahmaan bin Al-Aswad (رضي الله عنه) kwamba: Watu wa Madiynah walilazimishwa kuandaa jeshi (kupigana na watu wa Ash-Shaam katika khilaafah ya Ibn Az-Zubayr Makkah) na nikawa nimeandikwa humo. Kisha nikakutana na ‘Ikrimah, mtumwa wa Ibn ‘Abbaas aliyekuwa huru, nikamjulisha (hayo), akanikataza mno (kuingia katika orodha ya jeshi), akasema: Ibn ‘Abbaas amenijulisha kwamba baadhi wa Waislamu walikuwa na washirikina hivyo wakikithiri idadi ya washirikina dhidi ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Mshale ulikuwa unarushwa ambao ulimpiga mmoja wao (Waislamu wakiwa pamoja na washirikina) na kumuua, au hupigwa na kuuliwa (kwa upanga).” Hapo Allaah Akateremsha:

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٩٧﴾

Hakika wale ambao Malaika wanawafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao, (Malaika) watawaambia: Mlikuwa katika hali gani? Watasema: Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.  (Malaika) Watasema: Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni Jahannam, na uovu ulioje mahali pa kuishia! (4:97)

Abuu Aswad akaongezea:

إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا ﴿٩٨﴾

Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata hila yoyote wala hawawezi kuongoza njia. (4:98) [Al-Bukhaariy]

Pia Adhw-Dhwahaak amesema kwamba Aayah hii imeteremshwa kuhusu baadhi ya wanafiki ambao hawakuungana na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), bali walibakia Makkah kisha wakatoka na washirikina katika vita vya Badr. Wakauawa pamoja na waliouawa. Hapo Aayah hii

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٩٧﴾

Hakika wale ambao Malaika wanawafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao, (Malaika) watawaambia: Mlikuwa katika hali gani? Watasema: Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.  (Malaika) Watasema: Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni Jahannam, na uovu ulioje mahali pa kuishia! (4:97)

Ikateremshwa kuhusu hao waliobakia pamoja na washirikina hali ya kuwa waliweza kufanya hijrah lakini hawakufanya na wakashindwa kuthibitisha Uislamu wao. Watu kama hao wamejidhulumu nafsi zao na wakaingia katika uharamisho kama ilivyokubalika na Ijmaa’ na kutokana na Kauli ya Allaah:

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٩٧﴾

Hakika wale ambao Malaika wanawafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao, (Malaika) watawaambia: Mlikuwa katika hali gani? Watasema: Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.  (Malaika) Watasema: Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni Jahannam, na uovu ulioje mahali pa kuishia! (4:97)

Share

100-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 100: وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa 100-Na anayehajiri katika Njia ya Allaah atapata katika ardhi…

وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٠﴾

Na anayehajiri katika Njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia kujihifadhi na wasaa (wa kila kitu). Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.  (4:100).

Sababun-Nuzuwl:

Ilipoteremka Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) :

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ  

Hakika wale ambao Malaika wanawafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao…(4:97),   

palikuwepo mtu mmoja Makkah akiitwa Dhwamrah. Yeye alikuwa ni mgonjwa na akaiambia familia yake: “Nitoeni Makkah kwani nahisi joto kali la maradhi.” Familia yake wakamuuliza: “Tukupeleke wapi?” Akaashiria kwa mkono wake kuwa wampeleke Madiynah. Hapo ikateremka Aayah hii:

وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٠﴾

Na anayehajiri katika Njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia kujihifadhi na wasaa (wa kila kitu). Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.  (4:100).

[Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  na imepokelewa na Ibn Jariyr]

Share

102-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 102: وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa  102-Na utapokuwa upo kati yao, ukawaswalisha, basi lisimame…

وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ وَلْيَأْخُذُوا أَسْلِحَتَهُمْ فَإِذَا سَجَدُوا فَلْيَكُونُوا مِن وَرَائِكُمْ وَلْتَأْتِ طَائِفَةٌ أُخْرَىٰ لَمْ يُصَلُّوا فَلْيُصَلُّوا مَعَكَ وَلْيَأْخُذُوا حِذْرَهُمْ وَأَسْلِحَتَهُمْ ۗ وَدَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ تَغْفُلُونَ عَنْ أَسْلِحَتِكُمْ وَأَمْتِعَتِكُمْ فَيَمِيلُونَ عَلَيْكُم مَّيْلَةً وَاحِدَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن كَانَ بِكُمْ أَذًى مِّن مَّطَرٍ أَوْ كُنتُم مَّرْضَىٰ أَن تَضَعُوا أَسْلِحَتَكُمْ ۖ وَخُذُوا حِذْرَكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٠٢﴾

Na utapokuwa upo kati yao, ukawaswalisha, basi lisimame kundi miongoni mwao pamoja nawe, na wachukue silaha zao. Watakaposujudu basi wawe nyuma yenu (kuwalinda). Na lije kundi jingine ambalo halikuswali, liswali pamoja nawe, nao washike hadhari na silaha zao. Wale waliokufuru wanatamani kama mtaghafilika na silaha zenu na vifaa vyenu wakuvamieni mvamio mmoja. Na wala si dhambi kwenu ikiwa mna maudhiko kutokana na mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu. Na mshike hadhari zenu. Hakika Allaah Amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.(4:102).

Sababun-Nuzuwl:

 ‘Abuu ‘Ayyaash Az-Zuraqiy amesema: “Tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) eneo la ‘Usfaan (sehemu maarufu karibu na Makkah) wakati washirikina walikutana na sisi wakiwa chini ya uongozi wa Khaalid bin Waliyd, nao walikuwa baina yetu na Qiblah. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akatuswalisha Swalaah ya Adhuhuri, basi washirikina wakasema: “Wameshughulishwa na jambo ambalo tulikuwa na fursa ya kuwahujumu.”  Kisha wakasema: “Inayofuatia ni Swalaah (ya ‘Alasiri) ambayo ni kipenzi zaidi kwao kuliko watoto wao na nafsi zao.” Hapo Jibriyl (عليه السلام)  aliteremka kuleta Aayah hizi wakati wa baina ya Adhuhuri na Alasiri:

وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ وَلْيَأْخُذُوا أَسْلِحَتَهُمْ فَإِذَا سَجَدُوا فَلْيَكُونُوا مِن وَرَائِكُمْ وَلْتَأْتِ طَائِفَةٌ أُخْرَىٰ لَمْ يُصَلُّوا فَلْيُصَلُّوا مَعَكَ وَلْيَأْخُذُوا حِذْرَهُمْ وَأَسْلِحَتَهُمْ ۗ وَدَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ تَغْفُلُونَ عَنْ أَسْلِحَتِكُمْ وَأَمْتِعَتِكُمْ فَيَمِيلُونَ عَلَيْكُم مَّيْلَةً وَاحِدَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن كَانَ بِكُمْ أَذًى مِّن مَّطَرٍ أَوْ كُنتُم مَّرْضَىٰ أَن تَضَعُوا أَسْلِحَتَكُمْ ۖ وَخُذُوا حِذْرَكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٠٢﴾

Na utapokuwa upo kati yao, ukawaswalisha, basi lisimame kundi miongoni mwao pamoja nawe, na wachukue silaha zao. Watakaposujudu basi wawe nyuma yenu (kuwalinda). Na lije kundi jingine ambalo halikuswali, liswali pamoja nawe, nao washike hadhari na silaha zao. Wale waliokufuru wanatamani kama mtaghafilika na silaha zenu na vifaa vyenu wakuvamieni mvamio mmoja. Na wala si dhambi kwenu ikiwa mna maudhiko kutokana na mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu. Na mshike hadhari zenu. Hakika Allaah Amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.(4:102).

[Imaam Ahmad, Tafsiyr Ibn Kathiyr]

Na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن كَانَ بِكُمْ أَذًى مِّن مَّطَرٍ أَوْ كُنتُم مَّرْضَىٰ أَن تَضَعُوا أَسْلِحَتَكُمْ ۖ وَخُذُوا حِذْرَكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٠٢﴾

Na wala si dhambi kwenu ikiwa mna maudhiko kutokana na mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu.  (4:102),

inahusiana na ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf ambaye alijeruhiwa. [Al-Bukhaariy]

Share

119-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 119: وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa   119-Na nitawaamrisha watabadili Uumbaji wa Allaah.

وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ﴿١١٩﴾

119. Na hakika nitawapoteza, na nitawashawishi matamanio ya kulaghai, na nitawaamrisha. Basi watakata masikio ya wanyama (wawatukuze), na nitawaamrisha watabadili Uumbaji wa Allaah. Na atakayemfanya shaytwaan kuwa rafiki mwandani badala ya Allaah basi kwa yakini amekhasirika khasara bayana. (4:119).

Sababun-Nuzuwl:

Sababu ya kuteremka Kauli ya Allaah:

وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ﴿١١٩﴾

Na nitawaamrisha watabadili Uumbaji wa Allaah. Na atakayemfanya shaytwaan kuwa rafiki mwandani badala ya Allaah basi kwa yakini amekhasirika khasara bayana. (4:119).

Imeteremka katika jambo la kuwahasi beberu kuwa ni katika njia ya kumtii shaytwaan. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) . Athar hii ameipokea Ibn Jariyr]

Share

123-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 123: لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa    123-Si kwa matamanio yenu wala si matamanio ya Watu wa Kitabu.

لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٢٣﴾

Si kwa matamanio yenu wala kwa matamanio ya Watu wa Kitabu. Atakayefanya uovu atalipwa kwalo, na wala hatopata mlinzi wala mwenye kumnusuru isipokuwa Allaah. (4:123)

Sababun-Nuzuwl:

Al-‘Awfiy amehadithia kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alisema kuhusu Aayah hii:

لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٢٣﴾

Si kwa matamanio yenu wala kwa matamanio ya Watu wa Kitabu. Atakayefanya uovu atalipwa kwalo, na wala hatopata mlinzi wala mwenye kumnusuru isipokuwa Allaah. (4:123)

Watu wa Dini mbali mbali walibishana. Watu wa Tawraat walisema: “Kitabu chetu ni Kitabu bora kabisa na Nabiy wetu (Muwsaa  عليه السلام) ni Nabiy bora kabisa.” Watu wa Injiyl wakasema kama hivyo. Waislamu wakasema: “Hakuna Dini isipokuwa ya Kiislamu, Kitabu chetu kimefuta vitabu vyote vingine na Nabiy wetu ni Nabiy wa mwisho na nyinyi mmeamrishwa katika vitabu vyenu kuamini na kufuata Kitabu chetu.” Hapo Allaah Akateremsha Aayah hii:

لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٢٣﴾

Si kwa matamanio yenu wala kwa matamanio ya Watu wa Kitabu. Atakayefanya uovu atalipwa kwalo, na wala hatopata mlinzi wala mwenye kumnusuru isipokuwa Allaah. (4:123)

 [Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

Share

127-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 127: وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa  127-Na wanakuuliza wewe hukmu ya kishariy’ah (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake.

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الْوِلْدَانِ وَأَن تَقُومُوا لِلْيَتَامَىٰ بِالْقِسْطِ ۚ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِهِ عَلِيمًا ﴿١٢٧﴾

Na wanakuuliza wewe hukmu ya kishariy’ah (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: Allaah Anakubainishieni hukmu ya kishariy’ah kuhusu wao na (hukmu ya) yale mnayosomewa katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa nanyi mna raghba ya kuwaoa, na kuhusu wanaokandamizwa miongoni mwa watoto, na wajibu ulio juu yenu wa kuwasimamia mayatima kwa uadilifu. Na lolote mlifanyalo katika la khayr basi hakika Allaah daima kwa hilo Ni Mjuzi. (4:127).

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii inamzungumzia bwana mmoja aliyekuwa anamlea bint yatima na alikuwa ni msimamizi na mrithi wake.  Amehadithia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها)

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ  

Na wanakuuliza wewe hukmu ya kishariy’ah (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: Allaah Anakubainishieni hukmu ya kishariy’ah kuhusu wao na (hukmu ya) yale mnayosomewa katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa nanyi mna raghba ya kuwaoa. (4:127),  

imeteremshwa kuhusu kesi ya bwana aliyekuwa anamlea bint yatima. Bwana huyo alikuwa ni msimamzi wake na mrithi wake. Yatima huyo alishirikiana naye katika mali ya huyo bwana mpaka katika (shamba la) mtende. Mlezi huyo akawa na raghba ya kumuoa yatima (juu ya kuwa hakumpenda) na hakupenda kumuozesha mtu mwengine asije kushirikiana naye mali yake (ya yatima) ambayo anashirikiana naye. Na kwa sababu hii, mlezi huyo alimzuia yatima huyo kuolewa, na hapo ikateremshwa Aayah hii (4:127) na inayofuatia (4:128):

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ  

Na wanakuuliza wewe hukmu ya kishariy’ah (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: Allaah Anakubainishieni hukmu ya kishariy’ah kuhusu wao na (hukmu ya) yale mnayosomewa katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa nanyi mna raghba ya kuwaoa.

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya kwao wawili wakisikilizana baina yao kwa suluhu. Na suluhu ni bora zaidi. Na nafsi zimeumbiwa tabia ya uchoyo na ubahili. Na mkifanya ihsaan (kwa wanawake) na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:127-128).

[Al-Bukhaariy]

Katika riwaayah nyengine, ‘Urwah alimuuliza ‘Aaishah (رضي الله عنها)  kuhusu Aayah:

 وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya kwao wawili wakisikilizana baina yao kwa suluhu. Na suluhu ni bora zaidi. Na nafsi zimeumbiwa tabia ya uchoyo na ubahili. Na mkifanya ihsaan (kwa wanawake) na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:128).

Aaishah (رضي الله عنها)   akahadithia kisa kama hicho cha bint yatima kwa nyongeza kuwa huyo bwana mlezi alitaka kumuoa kwa mahari kidogo kabisa kuliko walivyokuwa wakipewa wanawake wengine walio kama hali yake. Kisha watu wakaenda kutafuta fatwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), ndipo Allaah Akateremsha Aayah:

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ  

Na wanakuuliza wewe hukmu ya kishariy’ah (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: Allaah Anakubainishieni hukmu ya kishariy’ah kuhusu wao na (hukmu ya) yale mnayosomewa katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa nanyi mna raghba ya kuwaoa. (4:127).  

[Al-Bukhaariy na Muslim]

Dhulma Waliyokuwa Wakifanyiwa Mayatima Zama Za Jaahiliyyah:

‘Aliy bin Abiy Twalhah amesema: Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: Ilikuwa wakati wa  jaahiliyyah, mlezi wa yatima humfunga kamba binti yatima, hapo huwa hakuna ruhusa mtu kumuoa. Akiwa mzuri na akapenda kumuoa anamuoa na kudhibiti mali yake. Akiwa si mzuri, basi hamruhusu aolewe mpaka afariki, na akifariki yeye hurithi mali yake. Allaah Akaharamisha hili Akasema:

وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الْوِلْدَانِ وَأَن تَقُومُوا لِلْيَتَامَىٰ بِالْقِسْطِ ۚ  

Na kuhusu wanaokandamizwa miongoni mwa watoto, na wajibu ulio juu yenu wa kuwasimamia mayatima kwa uadilifu. (4:127).

Share

128-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 128: وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa  128-Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa...

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya kwao wawili wakisikilizana baina yao kwa suluhu. Na suluhu ni bora zaidi. Na nafsi zimeumbiwa tabia ya uchoyo na ubahili. Na mkifanya ihsaan (kwa wanawake) na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:128).

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremshwa kuhusu bwana mmoja aliyekuwa na mke lakini hakuwa akimuonyesha mahaba wala hamkithirishii katika mahaba na wala hamuonyeshi mwenendo uliokuwa mzuri. Huyo bwana hakutaka kuendelea (naye katika ndoa), na alishazaa naye mtoto, lakini huyo mke hakupenda apewe talaka. Basi akamwambia mumewe: “Nakuruhusu uishi na mke mwengine.” [Al-Bukhaariy na Muslim].

Katika riwaaya nyengine mwanamke huyo alisema: “Naachilia mbali haki zangu, lakini usinitaliki.” Hapo ikateremka Aayah hii:

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya kwao wawili wakisikilizana baina yao kwa suluhu. Na suluhu ni bora zaidi. Na nafsi zimeumbiwa tabia ya uchoyo na ubahili. Na mkifanya ihsaan (kwa wanawake) na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (4:128).

Share

176-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 176: يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

An-Nisaa 176-Wanakuuliza hukmu ya kishariy’ah. Sema: Allaah Anakubainishieni kuhusu Al-Kalaalah...

يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ ۚ إِنِ امْرُؤٌ هَلَكَ لَيْسَ لَهُ وَلَدٌ وَلَهُ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ ۚ وَهُوَ يَرِثُهَا إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَتَا اثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا الثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ ۚ وَإِن كَانُوا إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَاءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۗ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٧٦﴾

Wanakuuliza hukmu ya kishariy’ah. Sema: Allaah Anakubainishieni kuhusu Al-Kalaalah (asiye na wazazi wala watoto) Ikiwa mtu amefariki hana mtoto lakini ana dada; basi atastahiki nusu ya yale aliyoyaacha. Na yeye (huyo mtu) atamrithi huyo dada kama hana mtoto. Na ikiwa madada ni wawili; basi watastahiki thuluthi mbili ya yale aliyoyaacha (maiti). Na wakiwa ni ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamme atastahiki sehemu iliyo sawa na sehemu ya wanawake wawili. Allaah Anakubainishieni ili msipotee; na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi. (4:176).

Sababun-Nuzuwl:

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomtembelea Jaabir (رضي الله عنه) alipokuwa mgonjwa, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimkuta Jaabir akiwa amezimia. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akatawadha na akamrashia maji ya wudhuu, Jaabir akazindukana. Kisha Jaabir akamuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) namna gani ataigawa mali yake kwa sababu hali yake ni hali ya Al-Kalaalah (asiye na watoto, wala wazazi. Au asiye na mrithi wa kwenda juu wala kwenda chini) na hapo ikateremka Aayah hii:

يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ ۚ إِنِ امْرُؤٌ هَلَكَ لَيْسَ لَهُ وَلَدٌ وَلَهُ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ ۚ وَهُوَ يَرِثُهَا إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَتَا اثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا الثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ ۚ وَإِن كَانُوا إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَاءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۗ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٧٦﴾

Wanakuuliza hukmu ya kishariy’ah. Sema: Allaah Anakubainishieni kuhusu Al-Kalaalah (asiye na wazazi wala watoto) Ikiwa mtu amefariki hana mtoto lakini ana dada; basi atastahiki nusu ya yale aliyoyaacha. Na yeye (huyo mtu) atamrithi huyo dada kama hana mtoto. Na ikiwa madada ni wawili; basi watastahiki thuluthi mbili ya yale aliyoyaacha (maiti). Na wakiwa ni ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamme atastahiki sehemu iliyo sawa na sehemu ya wanawake wawili. Allaah Anakubainishieni ili msipotee; na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi. (4:176).

 [Amehadithia Jaabir (رضي الله عنه) na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]. Na katika riwaayah ya At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd: “(Jaabir) alikuwa na dada tisa.”

Share