101-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Maaidah Aayah 101: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

Al-Maaidah 101-Enyi walioamini! Msiulizie mambo ambayo mkifichuliwa yatakuchukizeni

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهَا ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٠١﴾

Enyi walioamini! Msiulizie mambo ambayo mkifichuliwa yatakuchukizeni. Na mkiyaulizia pale inapoteremshwa Qur-aan mtafichuliwa. Allaah Ameyasamehe hayo. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mvumilivu. [Al-Maaidah (5:101)]

Sababun-Nuzuwl: 

Aayah hii imeteremshwa kwa sababu ya wingi wa maswali waliyokuwa wakiuliza watu katika hali tofauti na wakati nyakati mbali mbali; ima kwa istihzaa au mitihani iliyowasibu au kwa talbiys (kufunika haki na kuipotosha). Mfano pale ilipoteremka Aayah ya kuwajibika Hajj:

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾ 

Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba (Al-Ka’bah) hiyyo kwa mwenye uwezo.  (3:97)

akashikilia mtu kuuliza kuhusu kuwajibika Hajj kama inawajibikia kila mwaka, jambo ambalo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) angejibu kuwa “Naam”, basi ingewajibikia, kisha hapo ingekuwa ni amri na jambo gumu mno kulitekeleza. [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]  

Pia Sababun-Nuzuwl:

Ni  kama alivyohadithia Anas bin Maalik (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoa khutbah ambayo sijapatapo kuisikia kama hiyo kisha akasema: “Mngelikuwa mnayajua yale ninayoyajua, basi mngelicheka kidogo na mngelia sana.” Waliposikia hivyo, Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) walijifunika nyuso zao wakalia mpaka sauti za vilio vyao vikasikika. Kisha mtu mmoja hapo akamuuliza: Nani baba yangu? Akamjibu: “Fulani.” Hapo ikateremka Aayah hii:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهَا ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٠١﴾

Enyi walioamini! Msiulizie mambo ambayo mkifichuliwa yatakuchukizeni. Na mkiyaulizia pale inapoteremshwa Qur-aan mtafichuliwa. Allaah Ameyasamehe hayo. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mvumilivu. [Al-Maaidah (5:101)] [Al-Bukhaariy]

Pia Sababun-Nuzuwl:

Anas (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba: Siku moja walianza kumuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) maswali mengi mpaka akaghadhibika. Akapanda mimbar akasema: “Hamtaniuliza lolote leo ila nitawajibu tu.” Nikatazama kuliani na kushotoni nikaona kila mtu amejifunika uso wake kwa nguo akilia. Hapo alikuweko mtu mmoja ambaye kila alipogombana na wenziwe aliitwa ‘mwana wa fulani asiyekuwa ni baba yake’. Akamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah, nani baba yangu? Akasema: “Hudhaafah.” Hapo ‘Umar akainuka akasema: Tumeridhika na Allaah kuwa ni Rabb, na Uislamu kuwa Dini, na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa ni Rasuli. Tunajikinga kwa Allaah na fitnah! Hapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Sijapatapo kuona kheri au shari kama siku ya leo, kwani imedhihirishwa mbele yangu Jannah (Pepo) na moto hadi kwamba nimeviona viwili hivi nyuma ya ukuta.”  Qataadah alipokuwa akihadithia Hadiyth hii alikuwa akitaja Aayah hii:

Share