Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

 

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

   

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

Share

01-Ruqyah Ya Shariy'ah Na Hukmu Zake

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Ruqyah Ya Kishariy’ah Na Hukmu Zake

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Maradhi  na  madhara yoyote yale hayamsibu mtu isipokuwa kwa majaaliwa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), lakini kwa rahmah Yake ‘Azza wa Jalla, Amejaalia shifaa (poza) kwa kila maradhi na kila dhara, kwa kutumia ruqyah pamoja na tiba ya Sunnah, na pia kutokana miti na majani kadhaa ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amejaalia kuwa ina tiba ndani yake kwa dalili:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَا أَنْزَلَ اللَّهُ دَاءً إِلاَّ أَنْزَلَ لَهُ شِفَاءً)) رواه البخاري   

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Hakuteremsha maradhi isipokuwa Ameyateremshia shifaa)) [Al-Bukhaariy]

 

Pia:

وعَنْ جَابِرٍعَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم؛ أَنَّهُ قَالَ: ((لِكُلِّ دَاءٍ دَوَاءٌ، فَإِذَا أُصِيبَ دَوَاءُ الدَّاءِ بَرَأَ بِإِذْنِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ)‏) رواه مسلم  

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kuna dawa kwa kila maradhi, na pindi dawa inapotumiliwa katika maradhi huponyesha kwa idhini ya Allaah ‘Azza wa Jalla)) [Muslim katika Kitaab As-Salaam]

 

Pia:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ابن مَسْعُدٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ لَمْ يُنْزِلْ دَاءً إلاَّ  أَنْزَلَ لَهُ شِفَاءً عَلِمَهُ مَنْ عَلِمَهُ، وَجَهِلَهُ مَنْ جَهِلَهُ))

Kutoka kwa Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah ‘Azza wa Jalla) Hakuteremsha maradhi ila Ameteremsha pamoja nayo shifaa, amejifunza aliyejifunza na amekuwa jahili aliyekuwa jahili kwayo)) [Musnad Ahmad (6/121) kwa isnaad Swahiyh. Taz. Majmuw’ Fataawa Ibn Baaz (1/171), (6/290)]

 

 

Imekatazwa kutumia dawa za haraam kwa dalili:

 

عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ (رضي الله عنه)  قَالَ:  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِنَّ اللَّهَ أَنْزَلَ الدَّاءَ وَالدَّوَاءَ، وَجَعَلَ لِكُلِّ دَاءٍ دَوَاءً، فَتَدَاوَوْا ولاَ تَدَاوَوْا بِحَرَامٍ))

Kutoka kwa Abuu Ad-Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Ameteremsha maradhi na dawa zake, Akajaalia kwa kila maradhi kuna dawa yake, basi jitibuni wala msijitibu kwa yaliyo haraam)) [Abuu Daawuwd, Ibn Hajar Al-‘Asqalaaniy ameipa daraja ya Hasan, Taz. Takhiryj Mishkaat Al-Maswaabiyh (4/272), Imaam Al-Albaaniy ameisahihisha katika Swahiyh Al-Jaami’ (1762) au (2390)]

 

Inafaa kusoma Suwrah au Aayah ambazo imepatikana dalili zake, lakini Qur-aan nzima ni shifaa kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ۙ وَلَا يَزِيدُ الظَّالِمِينَ إِلَّا خَسَارًا ﴿٨٢﴾

Na Tunateremsha katika Qur-aan ambayo ni shifaa na rahmah kwa Waumini; na wala haiwazidishii madhalimu isipokuwa khasara. [Al-Israa: 82]

 

Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٥٧﴾

Enyi watu! Kwa yakini yamekujieni mawaidha kutoka kwa Rabb wenu, na shifaa ya yale yaliyomo vifuani, na mwongozo na rahmah kwa Waumini. [Yuwnus: 57[

 

'Ulamaa wamejuzisha ruqya pindi ikipatikana masharti matatu ambayo ameyanukuu Al-Haafidhw Ibn Rajab (Rahimahu-Allaah):

  1. Iwe kwa maneno ya Allaah (Ta’aalaa) au kwa Majina Yake na Sifa Zake.
  2. Isomwe kwa lugha ya Kiarabu.
  3. Aitakidi kwamba si ruqya pekee ndiyo itakayomponyesha bali aitakidi kwa uwezo wa Allaah (Ta’aalaa).

Pia zifutazo ni nukta muhimu Muislamu azingatie kabla ya kufanya ruqyah:

 

1-Uitakidi moyoni mwako kwamba njia yoyote uitumiayo ikiwa ni ruqyah, au kutumia dawa, hakupatikani shifaa isipokuwa kwa uwezo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Kwa hiyo uanze kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee ili Akutakabalie ruqyah yako.

 

 

2-Unaweza kutumia Aayah na du’aa za Qur-aan na Sunnah madamu tu hutozitumia kwa kuziwekea idadi maalumu, au wakati maalumu ambavyo haikupatikana dalili, au kutumia njia nyinginezo kama kuweka kwenye hirizi, au kutundika mahali n.k. ambapo itakuingiza katika shirki. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya hayo aliposema:

 

عَنْ عَوْفِ بْنِ مَالِكٍ الأَشْجَعِيِّ قَالَ: كُنَّا نَرْقِي فِي الْجَاهِلِيَّةِ فَقُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ، كَيْفَ تَرَى فِي ذَلِكَ؟ فَقَالَ: ((اعْرِضُوا عَلَيَّ رُقَاكُمْ لاَ بَأْسَ بِالرُّقَى مَا لَمْ يَكُنْ فِيهِ شِرْكٌ))

Kutoka kwa ‘Awf bin Maalik Al-Ashja’iyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Tulikuwa tunafanya ruqyah katika zama za jahiliyyah, tukasema: Ee Rasuli wa Allaah,  unaonaje katika hayo (ruqyah yetu]? Akasema: ((Nionyesheni ruqyah yenu, hakuna ubaya katika ruqyah madamu tu haitokuwa na shirki)) [Muslim katika Kitaab As-Salaam, Abuu Daawuwd katika Kitaab Atw-Twibb]

 

3-Akipenda mtu, anaweza kubakia katika kutawakkal kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee bila ya kujizingua au kuomba kufanyiwa ruqyah kama ni mojawapo ya fadhila za kumuingiza mtu Jannah bila ya kuhesabiwa kama alivyosema  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ (رضي الله عنهما)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَدْخُلُ الْجَنَّةَ مِنْ أُمَّتِي سَبْعُونَ أَلْفًا بِغَيْرِ حِسَابٍ: هُمْ الَّذِينَ لاَ يَسْتَرْقُونَ ولاَ يَتَطَيَّرُونَ وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ))

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Wataingia Jannah kati ya Ummah wangu watu elfu sabini bila ya hesabu; hao ni wale ambao hawaombi kufanyiwa ruqyah, wala hawatabirii nuksi au mkosi, wala kujitibu kwa moto, bali wanatawakkal kwa Rabb wao tu.)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

​Tunaona kwenye Hadiyth hiyo kuwa, ni bora zaidi mtu kujizuia kuomba kufanyiwa ruqyah -  japo ni jambo lenye kuruhusiwa-, lakini ni bora zaidi kuacha kuomba kufanyiwa ruqyah na kuwa ni mwenye kutawakkal kwa Allaah, kwa sababu hiyo ni katika sababu ya kupata Pepo.

 

 

4-Ujiepushe  na kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kinyume chake ni kudumisha Tawhiyd ya Allaah (kumpwekesha) kwa Ar-Rubuwbiyyah (Uola), Al-Uluwhiyyah ('Ibaadah), na Asmaa wasw-Swifaat (Majina na Sifa Zake).

 

5- Ujiepushe na maasi na ubakie katika utiifu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

 

5-Udumishe Adhkaar za asubuhi na jioni, na Adhkaar za kulala kwa mfululizo bila ya kuacha  hata baada ya kupata tiba ili ujikinge kutokurudiwa tena kudhuriwa na viumbe viovu na shari zao.

 

 

6-Uvute subira na ukumbuke fadhila za kuvuta subira ili zikusaidie kuvumilia madhara yaliyokusibu.

 

 

7-Uanze kusoma ruqyah kwa thanaa - kumtukuza na kumsifu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kufuata adabu za kuomba du’aa  ili itakabaliwe ruqyah yako.

 

 

 

Share

02-Ruqyah: Suwrah, Aayah Na Mengineyo Yaliyothibiti Kutumia Kwa Ajili Ya Ruqyah

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

  Ruqya: Suwrah, Aayah Na Mengineyo Yaliyothibiti Kwa Ajili Ya Ruqyah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Japokuwa Suwrah kadhaa zimethibiti kusomwa kwa ajili ya kinga na shifaa kutokana na maradhi, au madhara mengineyo kama kupatwa na jicho baya, sihiri, kukumbwa na majini na mashaytwaan, lakini Qur-aan nzima ni shifaa kwa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ ۖ  

Sema: “Hiyo ni kwa walioamini ni mwongozo na shifaa.  [Fusw-swilat :44]

 

Ama Suwrah na Aayah zilizothibiti ni zifuatazo pamoja na dalili zake:

 

 

Suwratul-Faatihah:

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ (رضي الله عنه) قَالَ: كُنَّا فِي مَسِيرٍ لَنَا فَنَزَلْنَا فَجَاءَتْ جَارِيَةٌ فَقَالَتْ: "إِنَّ سَيِّدَ الْحَيِّ سَلِيمٌ وَإِنَّ نَفَرَنَا غَيْبٌ فَهَلْ مِنْكُمْ رَاقٍ؟" فَقَامَ مَعَهَا رَجُلٌ مَا كُنَّا نَأْبُنُهُ بِرُقْيَةٍ، فَرَقَاهُ فَبَرَأَ فَأَمَرَ لَهُ بِثَلاَثِينَ شَاةً وَسَقَانَا لَبَنًا فَلَمَّا رَجَعَ قُلْنَا لَهُ: "أَكُنْتَ تُحْسِنُ رُقْيَةً أَوْ كُنْتَ تَرْقِي؟" قَالَ: "لاَ مَا رَقَيْتُ إلاَّ بِأُمِّ الْكِتَابِ." قُلْنَا: "لاَ تُحْدِثُوا شَيْئًا حَتَّى نَأْتِيَ أَوْ نَسْأَلَ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)." فَلَمَّا قَدِمْنَا الْمَدِينَةَ ذَكَرْنَاهُ لِلنَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ: ((وَمَا كَانَ يُدْرِيهِ أَنَّهَا رُقْيَةٌ؟ اقْسِمُوا وَاضْرِبُوا لِي بِسَهْمٍ)).

 

Amesimulia Abuu Sa'iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Tulikuwa katika safari tukateremka mahali, akaja kijakazi akasema: Bwana wetu ametafunwa na nge na wanaume wetu hawapo, je, yupo kati yenu tabibu? Akasimama pamoja naye mtu mmoja ambaye hatukudhania kuwa anajua ruqyah (utabibu). Akamtibu kwa ruqyah akapona. Akampa kondoo thelathini na akatupa maziwa tunywe (kama ni malipo). Aliporudi tukamwambia: Je, ulikuwa kweli unajua kutibu kwa ruqyah, au ulikuwa unabahatisha tu? Akasema: Hapana, bali nimemsomea Ummul-Kitaab (Suwrah Al-Faatihah). Tukasema: Tusiseme kitu hadi tumfikie au tumuulize Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Tulipofika Madiynah, tulimwelezea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Alijuaje kuwa (Al-Faatihah) ni ruqyah? Gawaneni na mnitolee sehemu (ya kondoo.” [Al-Bukhaariy]

 

[Rejea:  Kutawassal Kwa Suwratul-Faatihah]

 

 

Suwratul-Baqarah:  

 

عن ‏ ‏أبي هريرة ‏ رضي الله عنه ‏أن رسول الله ‏ ‏صلى الله عليه وسلم ‏ ‏قال‏: ((لَا تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ مَقَابِرَ إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنْفِرُ مِنَ الْبَيْتِ الَّذِي تُقْرَأُ فِيهِ سُورَةُ الْبَقَرَةِ)) رواه مسلم  

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Msifanye nyumba zenu makaburi. Kwa hakika shaytwaan haingii nyumba ambayo husomwa humo Suwratul-Baqarah)).

[At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh] na katika Riwaayah ya Muslim, Hadiyth (780):

((Shaytwaan anakimbia nyumba inayosomwa ndani yake Suwratul-Baqarah)).

 

 

Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Kila kitu kina kipeo cha kudhibiti (na kuangaza yaliyo chini) na Al-Baqarah ndio kipeo cha Qur-aan. Atakayesoma Al-Baqarah usiku nyumbani kwake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba yake nyusiku tatu. Na atakayesoma mchana ndani ya nyumba yake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba hiyo kwa siku tatu)).

[Atw-Twabaraaniy (6/163), Ibn Hibbaan (2/78) na Ibn Mardawayh, Swahiyh At-Targhiyb (2/314)]

 

 

Aayatul-Kursiy:

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ وَكَّلَنِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِحِفْظِ زَكَاةِ رَمَضَانَ، فَأَتَانِي آتٍ، فَجَعَلَ يَحْثُو مِنَ الطَّعَامِ، فَأَخَذْتُهُ فَقُلْتُ: لأَرْفَعَنَّكَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم‏.‏ فَذَكَرَ الْحَدِيثَ فَقَالَ: إِذَا أَوَيْتَ إِلَى فِرَاشِكَ فَاقْرَأْ آيَةَ الْكُرْسِيِّ لَنْ يَزَالَ عَلَيْكَ مِنَ اللَّهِ حَافِظٌ، وَلاَ يَقْرَبُكَ شَيْطَانٌ حَتَّى تُصْبِحَ‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((صَدَقَكَ وَهْوَ كَذُوبٌ، ذَاكَ شَيْطَانٌ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniwakilisha kuhifadhi Zakaah ya Ramadhwaan (Zakaatul-Fitwr). Akaja mtu akaanza kuteka chakula (cha Zakaah) kwa mikono miwili. Nikamkamata na kumwambia: Nitakupeleka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kisha Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) akahadithia yote na akaongezea “Huyo (Mwizi) akasema kuniambia: “Utakapoingia kitandani kulala, soma Aayatul-Kursiy kwani mlinzi kutoka kwa Allaah atakulinda, na shaytwaan hatokukaribia mpaka asubuhi.”  Hapo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Amekwambia ukweli japokuwa yeye ni muongo, naye (huyo mwizi) ni shaytwaan)) [Al-Bukhaariy]

 

 

Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah:

 

 عن أَبِي مَسْعُودٍ الأَنْصَارِيِّ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((الآيَتَانِ مِنْ آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ مَنْ قَرَأَ بِهِمَا فِي لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ))

Abuu Mas‘uwd Al-Answaariyy  (Radhwiya Allaahu 'anhu)  amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayesoma usiku Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah zitamtosheleza)) Yaani: zinamtosheleza kumkinga na kila baya na lenye kumdhuru. [Al-Bukhaariy na  Muslim]

 

 

Suwratul-Ikhlaasw Na Al-Mu’awwidhataan (kinga mbili) na Suwratul-Kaafiruwn:

 

Kwanza, thawabu za kuisoma Suwratul-Ikhlaasw ni sawa na thawabu za thuluthi ya Qur-aan:

 

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لأَصْحَابِهِ: ((أَيَعْجِزُ أَحَدُكُمْ أَنْ يَقْرَأَ ثُلُثَ الْقُرْآنِ فِي لَيْلَةٍ؟)) فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَيْهِمْ وَقَالُوا: أَيُّنَا يُطِيقُ ذَلِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ فَقَالَ: ((اللَّهُ الْوَاحِدُ الصَّمَدُ ثُلُثُ الْقُرْآنِ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewaambia Maswahaba wake: ((Je, anaweza mmoja wenu asome thuluthi ya Qur-aan katika usiku mmoja?)) Likawa jambo gumu kwao wakasema: Tuwezeje sisi kufanya hivyo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: ((Allaah, Al-Waahidu (Mmoja Pekee, Asw-Swamadu (Mkusudiwa wa yote) ni thuluthi ya Qur-aan)) [Al-Bukhaariy  Na Muslim]

 

 

Kuisoma  Suwratul-Kaafiruwn thawabu zake ni kama thawabu za kusoma robo ya Qur-aan:

 

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم :((قُلْ هو اللَّهُ أحَدٌ تعدلُ ثلثَ القرآنِ. و قُلْ يَا أيُّهَا الْكَافِرُونَ تعدلُ ربعَ القرآنِ))

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sema: “Yeye ni Allaahu Mmoja Pekee)) [112] ni sawa na thuluthi ya Qur-aan na  ((Sema: “Enyi makafiri!)) [109] ni sawa na robo ya Qur-aan)) [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar, ameisahihisha Al-Albaaniy Taz. Swahiyh Al-Jaami’ (4405), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (586)]

 

Pia:

عَنْ مُعَاذِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ خُبَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: خَرَجْنَا فِي لَيْلَةٍ مَطِيرَةٍ وَظُلْمَةٍ شَدِيدَةٍ نَطْلُبُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي لَنَا. قَالَ: فَأَدْرَكْتُهُ فَقَالَ: ((قُلْ)).‏ فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا ثُمَّ قَالَ: ((قُلْ))‏ فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا.‏ قَالَ: ((قُلْ))‏ قُلْتُ: مَا أَقُولُ؟  قَالَ: ((قُلْ‏ هوَ اللَّهُ أَحَدٌ... ‏‏ وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ حِينَ تُمْسِي وَتُصْبِحُ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ تَكْفِيكَ مِنْ كُلِّ شَيْءٍ)).‏ قَالَ أَبُو عِيسَى وَهَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.

Imepokelewa kutoka kwa Mu’aadh bin ‘Abdillaah bin Khubayb (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kutoka kwa baba yake kwamba: “Tulitoka usiku mmoja wa kiza kinene na mvua tukimtafuta Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atuswalishe Swalaah.” Akasema: “Nikakutana naye, kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Sema)). Lakini sikusema kitu. Kisha akasema: ((Sema)). Lakini sikusema kitu. Kisha akasema ((Sema)). Nikasema: “Niseme nini?”  Akasema: ((Sema: “Yeye ni Allaahu Mmoja Pekee))  [112] … na Al-Mu’awwidhatayni [Al-Falaq na An-Naas 113-114] unapoingia jioni na unapoamka asubuhi mara tatu zitakutosheleza na kila kitu)) [Hadiyth Hasan Swahiyh, Taz. Swahiyh At-Tirmidhiyy (3575), Swahiyh Abiy Daawuwd (5082)]   

 

 

Al-Falaq na An-Naas:

 

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ قَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((أُنْزِلَ - أَوْ أُنْزِلَتْ - عَلَىَّ آيَاتٌ لَمْ يُرَ مِثْلُهُنَّ قَطُّ الْمُعَوِّذَتَيْنِ‏))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameniambia: ((Imeteremshwa (au) Nimeteremshiwa Aayaat ambazo hazijapatapo kuonekana kabla, Nazo ni Al-Mu’awwidhatayn)) [Muslim, Baab Fadhwl Qiraat Al-Mu’awwidhatyani]

 

Pia,

عن أَبِي سعيد الخدري: كان رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم يَتَعَوَّذُ من الجَانِّ، وعَيْنِ الإنسانِ، حتى نَزَلَتِ المعُوذَتَانِ، فلما نَزَلَتَا أَخَذَهُما، وتَرَكَ ما سِوَاهُما.

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba:  ‘Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijikinga kutokana na majini na jicho baya la bin Aadam mpaka zilipoteremshwa Al-Mu’awidhataan. Basi zilipoteremshwa, akazishika kujikingia akaacha isipokuwa hizo mbili.”  [At-Tirmidhiy, ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (2058)]

 

Pia,

عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ كُلَّ لَيْلَةٍ جَمَعَ كَفَّيْهِ ثُمَّ نَفَثَ فِيهِمَا فَقَرَأَ فِيهِمَا: ((‏قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ‏))‏ وَ‏ ((‏قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ‏))وَ‏ ((‏قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ‏))ثُمَّ يَمْسَحُ بِهِمَا مَا اسْتَطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ يَبْدَأُ بِهِمَا عَلَى رَأْسِهِ وَوَجْهِهِ وَمَا أَقْبَلَ مِنْ جَسَدِهِ يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ‏.‏

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anapanda kitandani kulala kila siku, alikuwa akikusanya viganja vyake vya mkono kisha akipulizia humo kisha akisoma: ((Sema: “Yeye ni Allaahu Mmoja Pekee)) [112] na ((Sema: “Najikinga na Rabb wa mapambazuko)) [113] na ((Sema: “Najikinga na Rabb wa watu)) [114], kisha hujifutia mwilini anapoweza, akianzia kichwani mwake, usoni na mbele, akifanya hivyo mara tatu)). [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Pia Muislamu asiache kusoma nyiradi za asubuhi na jioni kwani hizo ni kinga kubwa ya kila  madhara na balaa.

Kadhaalika, kusoma nyiradi za kulala na kuamka.

 

Kadhaalika kusema BismiLLaah kabla ya kula au kunywa, na mtu anapoingia na anapotoka katika nyumba, katika kujamiiana, anapoingia msalani pamoja na du’aa zake na kwa ujumla kabla ya kuanza lolote lile ni vizuri kusema BismiLLaah. Rejea: Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)

 

 

na Hiswnul Muumin.

 

 

Pia kutia wudhuu:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((يَعْقِدُ الشَّيْطَانُ عَلَى قَافِيَةِ رَأْسِ أَحَدِكُمْ إِذَا هُوَ نَامَ ثَلاَثَ عُقَدٍ، يَضْرِبُ كُلَّ عُقْدَةٍ عَلَيْكَ لَيْلٌ طَوِيلٌ فَارْقُدْ، فَإِنِ اسْتَيْقَظَ فَذَكَرَ اللَّهَ انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ، فَإِنْ تَوَضَّأَ انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ، فَإِنْ صَلَّى انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ فَأَصْبَحَ نَشِيطًا طَيِّبَ النَّفْسِ، وَإِلاَّ أَصْبَحَ خَبِيثَ النَّفْسِ كَسْلاَنَ)).

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anapolala mmoja wenu,  shaytwaan hufunga kisogoni mwake vifundo vitatu. Hupiga kila kifundo (kumwambia): Umebakiwa na usiku mrefu, basi lala. Anapoamka akamtaja Allaah, kifundo kimoja hufunguka. Anapotawadha, hufunguka kingine, na anaposwali cha tatu hufunguka. Hapo huwa mchangamfu na mwenye nafsi nzuri, na kama si hivyo, huwa na nafsi mbaya na mvivu)). [Al-Bukhaariy]

 

Share

03-Ruqyah: Du’aa Za Sunnah Kwa Ajili Ya Maradhi Na Mabaya Mengineyo

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Ruqya: Du’aa Za Sunnah Kujikinga Na Maradhi Na Mabaya Mengineyo

 

www.alhidaaya.com

 

 

Kupatwa maradhi ni miongoni mwa mitihani ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na inampasa Muumini awe na subra kwa ajili ya kupata radhi za Allaah (‘Azza wa Jalla), pamoja na fadhila zake tele, miongoni mwazo ni kufutiwa madhambi mpaka mtu atakasike nayo.

 عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ابن مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) قَالَ دَخَلْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يُوعَكُ، فَمَسِسْتُهُ بِيَدِي فَقُلْتُ: "يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّكَ لَتُوعَكُ وَعْكًا شَدِيدًا" فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَجَلْ، إِنِّي أُوعَكُ كَمَا يُوعَكُ رَجُلاَنِ مِنْكُمْ)) فَقُلْتُ: "ذَلِكَ أَنَّ لَكَ أَجْرَيْنِ؟"  فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَجَلْ)) ثُمَّ قَالَ: ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ يُصِيبُهُ أَذًى مِنْ مَرَضٍ فَمَا سِوَاهُ إلاَّ حَطَّ اللَّهُ بِهِ سَيِّئَاتِهِ كَمَا تَحُطُّ الشَّجَرَةُ وَرَقَهَا)) متفق عليه

Kutoka kwa Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Niliingia kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa anaugua homa. Nikamgusa kwa mkono wangu nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika una homa kali?  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ndio! Ninaugua kama wanavyougua wawili wenu)). Nikasema: “Je, ni kwa sababu utapata thawabu mara mbili?”  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ndio)) kisha akasema: ((Hakuna Muislamu yeyote anayefikwa na dhara kutokana na maradhi au vinginevyo isipokuwa Allaah Atamfutia madhambi yake mfano wa majani yanavyopuputika mtini)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida zaidi: 

 

04 - Subira Anaposibiwa Muislamu Na Maradhi

 

Du’aa alizokuwa akiomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kujikinga na maradhi pamoja na masaibu mengineyo:

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْبَرَصِ وَالْجُنُونِ وَالْجُذَامِ وَمِنْ سَيِّئْ الاَسْقَامِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-baraswi wal-junuwni wal-judhaami wamin sayyiil-asqaami

 

(Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na mambalanga na umajnuni, na ukoma na maradhi mabaya)) [Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ahmad. Swahiyh katika Swahiyh An-Nasaaiy (3/1116)]

 

 اللَّهُمَّ جَنِّبْنِي مُنْكَرَاتِ الاَخْلاَقِ، وَالاَهْوَاءِ، وَالاَعْمَالِ، والأدْوَاءِ

Allaahumma jannibniy munkaraatil-akhlaaqi, wal ahwaahi, wal-a’maali, wal adwaai

 

Ee Allaah niepushe machukizo ya tabia na matamanio, na matendo (maovu), na maradhi. [Al-Haakim na kasema Swahiyh kwa sharti ya Muslim na ameikubali Adh-Dhahabiy. Kitabus-Sunnah (13)  na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy]

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْعَجْزِ وَالْكَسْلِ والْجُبْنِ وَالْبُخْلِ وَالْهَرَمِ وَالْقَسْوَةِ وَالْغَفْلَةِ وَالْعَيْلَةِ وَالذِّلَّةِ وَالْمَسْكَنَةِ  وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الْفَقْرِ وَالْكُفْرِ وَالْفُسُوقِ وَالشِّقَاقِ وَالنِّفَاقِ وَالسُّمْعَةِ وَالرِّياَءِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الصَّمَمِ  وَالْبُكَمِ والْجُنُونِ وَالْجُذَامِ والْبَرَصِ وَسَيِّءِ الاَسْقَامِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-‘ajzi, wal-kasli, wal-jubni, wal-bukhli, wal-harami, wal-qaswati, wal-ghaflati, wal-‘aylati, wadh-dhillati, wal-maskanati, wa a’uwdhu bika minal-faqri, wal-kufri, wal-fusuwqi, wash-shiqaaqi, wan-nifaaqi, wassum-’ati, warriyaai, wa a’uwdhu bika minasw-swamami, wal-bukami, wal-junuwni, wal-judhaami, walbaraswi, wasayyiil-asqaami

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kushindwa nguvu [kutojiweza], na uvivu, na uoga, na ubakhili, na kudhoofika [kutokana na uzee], na  moyo mgumu, na kughafilika, na kufedheheka, na kudhalilika, na umasikini, na najikinga Kwako na ufakiri, na kufru, na ufasiki, na magomvi, na unafiki, na kupenda kusikika umaarufu, na riyaa, na najikinga Kwako dhidi ya uziwi na ububu na ukichaa na ukoma na mbalanga na maradhi mabaya. [Al-Haakim, Al-Bayhaqiy na Taz. Swahiyh Al-Jaami’ (1/406]

 

 

 

 

Share

04-Ruqyah: Du’aa Za Kujiombea Au Kumuombea Mgonjwa

 

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Ruqyah: Du’aa Za  Kujiombea Au Kumuombea Mgonjwa

 

www.alhidaaya.com

 

 

Du’aa zifuatazo, anaweza aliye mgonjwa kujiombea mwenyewe au kumsomea mgonjwa mwengine.

 

 

Unapopata maumivu mwilini

Kwanza: Weka mkono wako juu ya sehemu inayouma kisha useme mara tatu:

 

بِسْمِ الله  أَعُوذُ بِاللَّهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ

BismiLLaah, A’uwdhu biLLaahi wa-Qudratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru

((Kwa jina la Allaah, Najikinga kwa Allaah na kwa uwezo Wake kutokana na shari ya ninachokisikia na ninachokiogopa)) [Hadiyth ya ‘Uthmaan bin Abiy Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu)  - Muslim (4/1728) [2202],  Ibn Maajah na wengineo kwa usimulizi tofauti kidogo]

 

Pili: Unaweka vidole vyako katika ardhi kugusa au chovya mchanga, kisha upangusie sehemu ya mwili yenye maumivu au maradhi na useme:

 بِسْمِ اللَّهِ، تُرْبَةُ أَرْضِنَا، بِرِيقَةِ بَعْضِنَا، يُشْفَى سَقِيمُنَا بِإِذْنِ رَبِّنَا

BismiLlaahi turbatu ardhwinaa, biriyqati ba’dhwinaa, yushfaa saqiymunaa biidhni Rabbinaa

 

((Kwa Jina la Allaah, mchanga ya ardhi yetu, kwa mate ya baadhi yetu, yanaponyesha mgonjwa wetu, kwa idhini ya Rabb wetu)). [Al-Bukhaariy, Muslim, Abuu Daawuud, Ibn Maajah, Ahmad]

 

Du’aa nyenginezo za kusoma:

 

 اللَّهُمَّ أَذْهِبْ الْبَاسَ، رَبَّ النَّاسِ، اشْفِ وَأَنْتَ الشَّافِي، لاَ شِفَاءَ إلاَّ شِفَاؤُكَ، شِفَاءًلاَ يُغَادِرُ سَقَمًا

Allaahumma Adh-hibil-ba-asa, Rabban-naasi, Ishfi wa-Antash-Shaafiy, laa-shifaa illa Shifaauka, shifaa-llaa yughaadiru saqamaa

((Ee Allah, Ondosha maumivu, Rabb wa watu, Ponyesha Nawe ni Mponyeshaji, hakuna shifaa ila shifaa yako, shifaa isiyobakisha maradhi)) [Al-Bukhaariy, Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad]

 

Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoingia kumzuru mgonjwa akimwambia:

لا بأْسَ طَهـورٌ إِنْ شـاءَ الله

Laa ba-asa twahuwrun In Shaa Allaah

((Hakuna neno, (ugonjwa) ni kusafishwa (na madhambi) Akipenda Allaah)) [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas  (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa)  - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (10/118) [3616]

 

Na kumuombea mgonjwa uliye naye au unapomtembelea du’aa ifuatayo mara saba.

 أَسْـأَلُ اللهَ العَـظيـم، رَبَّ العَـرْشِ العَـظيـم أَنْ يَشْفِـيَكَ

As-alu-LLaahal-‘Adhwiym, Rabbal-‘Arshil-‘Adhwiym, an Yashfiyak  

Namuomba Allaah Mtukufu Rabb wa ‘Arshi Tukufu Akuponyeshe.  [Hadiyth ya ‘Abdullaahi bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ’anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hapana mja yeyote Muislamu anayemtembelea mgonjwa ambaye wakati wake wa kufa bado haujafika na akamuombea mara saba, isipokuwa  Allaah Humponyesha mgonjwa huyo)). [At-Tirmidhiy [2083], Abuu Daawuwd [3106], Tazama pia Swahiyh At-Tirmidhiy (2/210), Swahiyh Al-Jaami’ (5/180) [5766]

 

 

 

 

Share

05-Ruqyah Dhidi Ya Uhasidi Na Jicho Baya

 

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Ruqyah Dhidi Ya Uhasidi Na Jicho Baya

 

www.alhidaaya.com

 

 

Muumini hapaswi kuwa na sifa ya uhasidi kwa dalili kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لَا يَجْتَمِعُ الشُّحُّ وَالْإِيمَانُ فِي قَلْبِ عَبْدٍ أَبَدًا))   

وفي رواية أخرى قال: ((وَلا يَجْتَمِعُ فِي جَوْفِ عَبْدٍ مُؤْمِنٍ الإِيمَانُ وَالْحَسَدُ))   سنن النسائي كِتَاب الْجِهَادِ باب فَضْلِ مَنْ عَمِلَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ عَلَى قَدَمِهِ - المحدث الألباني خلاصة حكم المحدث صحيح في صحيح النسائي

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Uchoyo na iymaan haviwi  pamoja viwili hivi katika moyo wa mja)) na katika Riwaayah:  ((Iymaan na uhasidi haviwi pamoja viwili hivi katika moyo wa mja)) [Sunan An-Nasaaiy 3110 Kitaab Al-Jihaad Baab Fadhwl Man ‘Amila Fiy SabiyliLLaah ‘alaa Qadamihi - na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh An-Nasaaiy]

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatahadharisha:

 

عنْ أَنَسُ (رضي الله عنه) أنّ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لاَ تَبَاغَضُوا وَلاَ تَحَاسَدُوا وَلاَ تَدَابَرُوا وَلاَ تَقَاطَعوا  وَكُونُوا عِبَادَ اللَّهِ إِخْوَانًا  وَلاَ يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلاَثَةِ أَيَّامٍ)) متفق عليه

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Msibughudhiane [msichukiane], wala msihusudiane, wala msipeane mgongo, wala msikatane, kuweni ndugu enyi waja wa Allaah, wala haifai kwa Muislamu kumhama nduguye kwa zaidi ya siku tatu [asiseme naye])) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na jicho linaweza kuathiri mtu. Inalopasa kwa Muislamu anapomuona nduguye Muislamu amejaaliwa na neema basi ni kumuombea du’aa nzuri kwani imethibiti katika Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba unapomuombea mwenzako kwa siri Malaika huitikia ”Aamiyn” na hukuombea nawe pia kama hivyo unavyomuombea nduguyo au mwenzako. Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

إِذَا رَأَى أَحَدُكُمْ مِنْ أَخِيهِ أَوْ مِنْ نَفْسِهِ أَوْ مِنْ مَالِهِ مَا يُعْجِبُهُ فَلْيُبَرِّكْهُ فَإِنَّ الْعَيْنَ حَقٌّ

 

Mmoja wenu akiona kwa ndugu yake au kwake, au mali yake kinachomfurahisha akiombee baraka kwani kijicho ni haki. [Hadiyth ya ‘Aamir bin Rabiy’ah na Sahl bin Hunayf (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) - Ahmad (4/447), Ibn Maajah [3509], Maalik [1697, 1698] na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (1/212) na angalia: Tahqiyq Zaad Al-Ma’aad ya Al-Arnaawuwtw (4/170)]

 

Useme:

اللّهُـمَّ بارِك عَلَـيه أو اللَّهُمَّ بَارِك عَلَيْكَ

Allaahumma Baarik ’alayh  au Allaahumma Baarik ‘alayka

 

Ee Allaah, Mbariki kwa hicho  au Allaah Akubariki kwacho

 

Du’aa za kinga au tiba ya jicho baya na husda:

 

كَانَ النَّبِيُّ صلَّى اللّه عَلَيْهِ وسَلَّم يَعُوذُ الْحَسَنْ وَالْحُسَيْن

 

Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa  akiwakinga (wajukuu wake)  Al-Hasan na Al-Husayn akisema:

 

أُعيـذُكُمـا بِكَلِـماتِ اللهِ التّـامَّة مِنْ كُلِّ شَيْـطانٍ وَهـامَّة وَمِنْ كُـلِّ عَـيْنٍ لامَّـة

 

U’iydhukumaa bikalimaatiLLaahit-ttaammati min kulli shaytwaanin wa haammah, wa min kulli ’aynin laammah

Nawakinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia Awakinge kutokana na kila shaytwaan na uvamizi na kila jicho lenye kudhuru [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) Al-Bukhaariy (4/119) [3371]

 

Kwa hiyo unapotaja kujikinga mwenyewe useme:

 

 أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّةِ مِنْ كُلِّ شَيْطَانٍ وَهَامَّةٍ  وَمِنْ كُلِّ عَيْنٍ لاَمَّةٍ

 

A’uwdhu bikalimaatiLLaahit-ttaammati min kulli shaytwaanin wa haammah, wa min kulli ’aynin laammah

 

Na pia unaweza kumsomea ruqyah kwa du’aa zifuatazo mtu aliyepatwa na jicho au uhasidi:

 

بِاسْمِ اللَّهِ أَرْقِيكَ، مِنْ كُلِّ شَيْءٍ يُؤْذِيكَ، مِنْ شَرِّ كُلِّ نَفْسٍ أَوْ عَيْنِ حَاسِد، اللَّهُ يَشْفِيكَ بِاسْمِ اللَّهِ أَرْقِيكَ 

 

BismiLLaahi arqiyka, min kulli shay-in yu-udhiyka, min sharri kulli nafsin aw ‘aynin haasidin, Allaahu Yashfiyka BismiLLaahi arqiyka

 

((Kwa Jina la Allaah nakusomea ruqyah, kutokana na kila jambo linalokudhuuru, na kutokana na kila nafsi au jicho la hasidi, Allaah Akupe shifaa, kwa Jina la Allaah, nakusomea ruqyah)) [Muslim]

 

Jibriyl (’Alayhis-Salaam) alimsomea Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) du’aa ifuatayo pindi alipoumwa:

 

 بِاسْمِ اللَّهِ يُبْرِيكَ وَمِنْ كُلِّ دَاءٍ يَشْفِيكَ وَمِنْ شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ وَشَرِّ كُلِّ ذِي عَيْنٍ

 

BismiLlaahi Yubriyka, wa min kulli daain Yashfiyka, wa min sharri haasidin idhaa hasad, washarri kulli dhiy ‘aynin

 

((Kwa Jina la Allaah Akubariki, na kutokana kila ugonjwa Akuponyeshe, na kutokana na kila hasidi anapohusudu na kila shari ya jicho)) [Muslim]

   

Na bila shaka, kusomwe Suwrah na Aayah zilizothibiti za Ruqyah kama Suwratul-Faatihah, Aayatul-Kursiy, Aayah mbili za mwisho katika Suwratul-Baqrah, Suwratul-Ikhlaasw, Al-Mu’awwidhataan (Al-Falaq na An-Naas) na pia Qur-aan nzima ni shifaa ya kila madhara na magonjwa na masaibu.

 

 

Share

06-Ruqyah Dhidi Ya Sihri, Mashaytwaan, Majini Na Kila Aina Ya Uovu

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Ruqyah Sihri Mashaytwaan Majini Na Kila Aina Ya Uovu.

 

www.alhidaaya.com

 

Kujikinga au kujitibu na sihri (uchawi), kuvamiwa na mashaytwaan, majini na maovu yoyote yale ni kudumisha kuisoma Qur-aan kwa ujumla. Vile vile Suwrah na Aayah zilizothibiti kuwa zinafaa ruqyah, kama Suwratul-Faatihah, Suwratul-Baqarah, Aayatul-Kursiy, Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah, Suwratul-Ikhlaasw na Al-Mu’awwidhataan  (Al-Falaq na An-Naas), Suwratul-Kaafiruwn. Vile vile ni muhimu mno kudumisha nyiradi za asubuhi na jioni ambazo zina du’aa tele za kumkinga mtu anapozisoma na baadhi yake ni zifuatazo kama zilivyothibiti katika Hadiyth:

 

((مَنْ قالَ إذا أصْبَحَ : لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير كانَ لَهُ عَدْل رَقَبَة مِنْ وَلَدِ إسْماعِيل، وَكُتِبَ لَهُ عَشر حَسَناتِ وَحُطَّ عَنْهُ عَشر سَيِّئات، وَرُفِعَ لَهُ عَشر دَرَجات وَكانَ فَي حِرْزِ مِنَ الشَّيْطانِ حَتَّى يُمْسِي، وَإنْ قَالَها إذا أَمْسى كَانَ لَهُ مِثْل ذلِكَ حَتَّى يُصْبِحُ))

((Atakayesema atakapoamka:

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

”Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr”  

 

((Hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah  Peke Yake, Hana mshirika, ni Wake Ufalme, na Himdi ni Zake na Yeye juu ya kila kitu ni Mweza ...

Itakuwa ni kama kuacha huru mtumwa katika wana wa Ismaa’iyl, na ataandikiwa mema kumi, na atafutiwa makosa kumi, atapandishwa daraja kumi, na atakuwa katika kinga ya shaytwaan mpaka afike jioni na akisema jioni atapata kama hivyo mpaka afike asubuhi)).  [Hadiyth ya Abu ‘Ayyaash (Radhwiya Allaahu ’anhu) ameisahihisha Al-Albaaniy - Swahiyh Al-Jaami’ (6418) Swahiyh Abiy Daawuwd (5077), Swahiyh Ibn Maajah (3132)]

Pia:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ:  ((مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ ‏.‏ فِي يَوْمٍ مِائَةَ مَرَّةٍ ‏.‏ كَانَتْ لَهُ عَدْلَ عَشْرِ رِقَابٍ وَكُتِبَتْ لَهُ مِائَةُ حَسَنَةٍ وَمُحِيَتْ عَنْهُ مِائَةُ سَيِّئَةٍ وَكَانَتْ لَهُ حِرْزًا مِنَ الشَّيْطَانِ يَوْمَهُ ذَلِكَ حَتَّى يُمْسِيَ وَلَمْ يَأْتِ أَحَدٌ أَفْضَلَ مِمَّا جَاءَ بِهِ إِلاَّ أَحَدٌ عَمِلَ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ...))  

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ’anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Atakayesoma  kwa siku mara mia,

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

”Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr”

 

Basi atapata sawa na thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikiwa mema mia moja na atafutiwa makosa mia moja, na atakuwa na kinga ya Shaytwaan kwa siku hiyo yote hadi jioni na hatakuwa mtu yeyote mbora kumshinda ila yule aliyefanya zaidi yake)) [Al-Bukhaariy  pamoja na Al-Fat-h, (4/95) [3293], Muslim (4/2071) [2691].

Pia kuomba:

رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ ﴿٩٧﴾

 “Rabb wangu! Najikinga Kwako kutokana na udokezi wa mashaytwaan,”

وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ ﴿٩٨﴾

 “Na najikinga Kwako Rabb wasinihudhurie.”  [Al-Muuminuwn: 97-98]

Na,

أَعـوذُ بِكَلِـماتِ اللّهِ التّـامّاتِ مِنْ شَـرِّ ما خَلَـق

A’uwdhu Bikalimati-LLaahit-ttaammati min sharii maa Khalaq

 

Najikinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia na shari alichokiumba  [Hadiyth ya Khawlah bint Haakim kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((مَنْ نَزلَ مَنزِلاً ثُمَّ قال: أَعُوذُ بِكَلِمات اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ، لَمْ يضرَّه شَيْءٌ حتَّى يرْتَحِل مِنْ منزِلِهِ ذلكَ))

((Atakayeteremka katika kituo (au makazi) kisha akasema: 'Auwdhu bikalimati-LLaahit-taammati min sharri maa Khalaq' - Najilinda kwa maneno ya Allaah yaliyotimia na shari Alichokiumba - hakuna kitakachomdhuru hadi atakapoondoka katika kituo (au makazi) hicho)) [Muslim (4/2080) [2708].

 

Pia kusema ifuatavyo mara tatu asubuhi na jioni ambayo imo pia katika Adhkaar za asubuhi na jioni:

بِسـمِ اللهِ الذي لا يَضُـرُّ مَعَ اسمِـهِ شَيءٌ في الأرْضِ وَلا في السّمـاءِ وَهـوَ السّمـيعُ العَلـيم (ثلاثاً)

BismiLLaahiLLadhiy laa yadhwuru ma’a-Smihi shay-un fil-ardhwi walaa fissamaai wa Huwas-Samiy’ul ‘Aliym (mara 3)

 

Kwa jina la Allaah Ambaye hakidhuru kwa jina Lake kitu chochote kile kilicho ardhini, wala mbinguni, Naye ni Mwenye Kusikia yote daima Mjuzi wa yote daima.  [Hadiyth ya ‘Uthmaan bin ‘Afaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema:

((مَنْ قَالَها ثَلاثًا إذا أصْبَحَ وَثَلاثًا إذا أمْسَى لَمْ يَضُرُّهُ شَيْء))

((Atakayesema mara tatu asubuhi na jioni hatodhuriwa na chochote)) [Abu Daawuwd (4/323) [5089, 5088]. At-Tirmidhiy (5/465) [3388], Ibn Maajah [3869], Ahmad (1/72), Taz Swahiyh Ibn Maajah (2/332), Swahiyh Abi Daawuwd (5088), Swahiyh Al-Jaami’ (5745), Majmuw’ Fataawa ibn Baaz (8/108) na Isnaad yake imepewa daraja ya Hasan na Al-‘Allaamah Ibn Baaz katika Tuhfat Al-Akhyaar (Uk. 39)]

Pia kuomba unapopata mafazaiko ya shaytwaan usiku:

 

 أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ غَضَبِهِ وَعِقَابِهِ وَشَرِّ عِبَادِهِ وَمِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَنْ يَحْضُرُونِ

A’uwdhu bikalimati-LLaahit-ttaammati min ghadhwabihi wa-‘iqaabihi, wa sharri ‘ibaadihi, wa min hamazaatish-shayaatwiyni wa an-yahdhwuruwni

 

((Najikinga na maneno ya Allaah, yaliotimia kutokana na ghadhabu Zake na adhabu Yake na shari ya waja Wake na vioja vya mashaytwaan na kunijia kwao))

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Basi hawatomdhuru)) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ahmad, ameisahihisha Al-Albaaniy - Swahiyh Abi Daawuwd (3893), Swahiyh At-Tirmidhiy (3/171) Adhkaar ya kondosha wasiwasi usingizini au kusikia uoga na mfadhaiko]

Na unapohisi vitimbi vya mashaytwaan usome:

 

  أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ الَّتِي لاَ يُجَاوِزُهُنَّ بَرٌّ ولاَ فَاجِرٌ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ وَبَرَأَ وَذَرَأَ وَمِنْ شَرِّ مَا يَنْزِلُ مِنْ السَّمَاءِ وَمِنْ شَرِّ مَا يَعْرُجُ فِيهَا وَمِنْ شَرِّ مَا ذَرَأَ فِي الأَرْضِ وَمِنْ شَرِّ مَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمِنْ شَرِّ فِتَنِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمِنْ شَرِّ كُلِّ طَارِقٍ إلاَّ طَارِقًا يَطْرُقُ بِخَيْرٍ يَا رَحْمَنُ

A’uwdhu bikalimati-LLaahil-Ladhiy laa yujaawizuhunna barrun walaa faajirun min sharri maa khalaqa, wa baraa, wa dharaa, wa min sharri maa yanzilu minas-samaai, wa min sharri maa ya’ruju fiyhaa, wa min sharri maa dharaa fil-ardhwi, wa min sharri maa yakhruju minhaa, wa min sharri fitanil-layli wan-nnahaari wa min sharri kulli twaariqin illaa twaariqan yatwruqu bikhayri Yaa Rahmaan

 

((Najikinga kwa maneno ya Allaah yaliyokamilika ambayo hayapiti mwema wala muovu, na shari ya Alichokiumba, na Akakitengeneza na Akasambaza.  Na shari ya kinachoteremka kutoka mbinguni na shari ya kinachopanda huko, na shari ya kinachosambaa ardhini na shari ya inayotoka ndani yake na shari ya fitnah za usiku na za mchana na shari ya kila anayegonga usiku ila anayegonga kwa kheri Ee Rahmaan)) [Ahmad kwa Isnaad Swahiyh]

 

Itaendelea kutajwa Ruqya nyenginezo kujikinga na maovu hayo katika milango inayofutia.

 

 

 

Share

07-Ruqya: Kuomba Kinga Kwa Allaah Dhidi Ya Kila Aina Ya Shari

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Kuomba Kinga Kwa Allaah Dhidi Ya Kila Aina Ya Shari

 

www.alhidaaya.com

 

 

Zimethibiti katika Qur-aan na Sunnah du’aa tele za kujikinga na shari na dhidi ya maadui, mojawapo ni du'aa ifuatayo ya Sunnah ambayo ni mukhtasari wa kinga za aina zote za shari:

 

اللَّهُمَّ إِني أسْأَلُكَ مِنْ الْخَيْرِ كُلِّهِ عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أعْلَمْ، وَأعُوذُ بِكَ مِن الشَّرِّ كُلِّهِ عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ ‏‏ أعْلَمْ،  اللَّهُمَّ إِنِّي أسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ مَا سَألَكَ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، وَأعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا استعَاذَ  بِكَ مَنْهُ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَمَا قَرَّبَ إلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أوْ عَمَلٍ وَأعُوذُ بِكَ مِنْ النَّارِ وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أوْ عَمَلٍ، وَأسْأَلُكَ أنْ تَجْعَلَ كُلَّ قَضَاءٍ قَضَيْتَهُ لِي خَيْرًا

Allaahumma inniy as-aluka minal-khayri kullihi ‘aajilihi wa aajilihi, maa ‘alimtu minhu wamaa lam a’lam. Wa a’uwdhu Bika min sharri kullihi ‘aajilihi wa aajilihi maa ‘alimtu minhu wamaa lam a’lam. Allaahumma inniy as-aluka min khayri maa saalaka ‘Abduka wa Nabiyyuka, wa a’uwdhu Bika min sharri masta’aadha Bika minhu ‘Abduka wa Nabiyyuka. Allaahumma inniy as-alukal-Jannata wamaa qarraba ilayhaa min qawlin aw ‘amal, wa a’uwdhu Bika minan-nnaari wamaa qarraba ilayhaa min qawlin aw ‘amal, wa as-aluka antaj-’ala kulla qadhwaai qadhwaytahu liy khayraa

 

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba khayr zote zilizo karibu na mbali nizijuazo na nisizozijua. Najikinga Kwako na shari zote za karibu na za mbali nizijuazo na nisizozijua. Ee Allaah, hakika nakuomba khayr alizokuomba mja Wako na Nabiy Wako, na najikinga Kwako shari alizojikinga nazo mja Wako na Nabiy wako. Ee Allaah, hakika mimi nakuomba Jannah na yanayokaribisha kwayo katika kauli au 'amali, na najikinga Kwako Moto na yanayokaribisha kwayo katika kauli au 'amali, na nakuomba Ujaalie kila majaaliwa yangu [uliyonikidhia] yawe khayr.

[Ibn Maajah – Ametaja katika mlango aliosimulia Hadiyth kwa anuani ya ‘Du’aa za  ‘Jawaami’il-Kalimi’]

 

Du’aa nyinginezo:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَمِلْتُ وَمِنْ شَرِّ مَا لَمْ أَعْمَلْ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min sharri maa ‘amiltu wamin sharri maa lam a’-amal

 

 

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako shari niliyotenda na shari nisiyoitenda  [Muslim, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy,  Ibn Maajah na Ahmad]

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ التَّرَدِّي ، وَالْهَدْمِ ، وَالْغَرَقِ ، وَالْحَرَقِ ،  وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ يَتَخَبَّطَنِي الشَّيْطَانُ عِنْدَ الْمَوْتِ ، وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ أَمُوتَ فِي سَبِيلِكَ مُدْبِرًا ، وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ أَمُوتَ لَدِيغًا

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minat-taraddiy, wal-hadmi, wal-gharaqi, wal-haraqi, wa a’uwdhu bika an yatakhabbatwniyash-shaytwaanu ‘indal-mawti, wa a’uwdhu bika an amuwta fiy sabiylika mudbiraa, wa a’uwdhu bika an amuwta ladiyghaa

 

Ee Allaah, hakika  mimi najikinga Kwako kuangamia na kubomoka na kufa kwa kuzama na kuungua na Moto, na najikinga Kwako kughilibiwa na shaytwaan wakati wa mauti, na najikinga Kwako kufa nikiwa mwenye kugeuka nyuma katika njia Yako [kukimbia vita] na najikinga Kwako kufa kwa kung'atwa au kudungwa [na mdudu au mnyama wa sumu]. [Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy  - Swahiyh An-Nasaaiy (3/1123)]

 

Pia katika nyiradi miongoni mwa nyiradi za asubuhi kama alivyohadithia Abuu Ad-Dardaa (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

حَسْبِـيَ اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُوَ عَلَـيهِ تَوَكَّـلتُ وَهُوَ رَبُّ العَرْشِ العَظـيم

Hasbiya-Allaahu laa ilaaha illaa Huwa ‘Alayhi tawakkaltu wa Huwa Rabbul ’Arshil ‘Adhwiym (mara 7 asubuhi na jioni)

 

Ananitosheleza Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake Yeye nimetawakali na Yeye ni Rabb wa ‘Arsh Adhimu.

 

((من قالها حين يصبح وحين يمسي سبع مرات كفاه الله ما أهمه من أمر الدنيا والآخرة))

((Atakayesema asubuhi na jioni itamtosheleza katika mambo yake yanayomtia hamu ya dunia na Aakhirah)). [Fataawa Ibn Baaz, (9/294) Ibn As-Sunniy [71] Marfuw’ na Abuu Daawuwd Mawquwf (4/321), na isnadi yake ameisahihisha Shu’ayb na ‘Abdul-Qaadir Al-Arnaauwtw. Taz. Zaad Al-Ma’aad (2/376)]

 

Na du’aa ifuatayo kama ilivyotajwa katika Hadiyth na ambayo pia ni miongoni mwa nyiradi za asubuhi na jioni:

عن ابن عمر رضي الله عنهما، قَالَ: لَمْ يَكُنْ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يدع هؤلاء الكلمات إذا أصبح وَإذا أَمْسَى:

 

((اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ فِي دِينِي وَدُنْيَايَ وَأَهْلِي وَمَالِي، اللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَاتِي وَآمِنْ رَوْعَاتِي، اللَّهُمَّ احْفَظْنِي مِنْ بَيْنِ يَدَيَّ وَمِنْ خَلْفِي وَعَنْ يَمِينِي وَعَنْ شِمَالِي وَمِنْ فَوْقِي وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ مِنْ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتـي)) صحيح: أخرجه البخاري في ((الأدب المفرد)) (1200)، وأبو داود (5074)

 

Imepokelewa kutoka kwa ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa haachi kuomba mambo manne anapoamka asubuhi na jioni:

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في الدُّنْـيا وَالآخِـرَة، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في ديني وَدُنْـيايَ وَأهْـلي وَمالـي، اللّهُـمَّ اسْتُـرْ عـوْراتي وَآمِـنْ رَوْعاتـي، اللّهُـمَّ احْفَظْـني مِن بَـينِ يَدَيَّ وَمِن خَلْفـي وَعَن يَمـيني وَعَن شِمـالي، وَمِن فَوْقـي، وَأَعـوذُ بِعَظَمَـتِكَ أَن أُغْـتالَ مِن تَحْتـي

 

Allaahumma inniy as-alukal ‘aafiyah fid-dunyaa wal Aakhirah. Allaahumma inni as-alukal ‘afwa wal ‘aafiyata fiy Diyniy wa dunyaaya, wa ahliy, wa maaliy. Allaahumma-stur ‘awraatiy, wa-aamin raw’aatiy. Allaahumma-hfadhwniy min bayni yadayya, wamin khalfiy, wa ‘an yamiyniy, wa ‘an shimaaliy, wamin fawqiy, wa a’uwdhu bi’adhwmatika an ughtaala min tahtiy

 

Ee Allaah, hakika nakuomba msamaha na Al-'Aafiyah (hifadhi, amani, salama) duniani na Aakhirah. Ee Allaah, hakika nakuomba msamaha na Al-'Aafiyah katika Dini na dunia yangu, na ahli wangu, na mali yangu. Ee Allaah nisitiri aibu zangu na nitulize khofu yangu. Ee Allaah, nihifadhi mbele yangu, na nyuma yangu, na kulia kwangu, na kushoto kwangu, na juu yangu, na najikinga kwa Uadhimu Wako kwa kutekwa chini yangu. [Swahiyh Al-Bukhaariy katika Adab Al-Mufrad (1200), Abuu Daawuwd [5074], Ibn Maajah [3871]. Taz. Swahiyh ibn Maajah (2/332), Taz. Swahiyh Abiy Daawuwd [5074]  

 

Na kifupi yake unaweza kuomba:

  اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالأَخِرَةِ

Allaahumma inniy as-alukal-‘aafiyata fid-dunyaaa wal-Aakhirah

 

Ee Allaah hakika mimi nakuomba al’-aafiyah (hifadhi, amani, salama) duniani na Aakhirah   [Swahiyh At-Tirmidhiy (3/180, 185, 170)]

 

Na miongoni mwa Adhkaar za asubuhi pia ni zifuatazo:

 

أَصْبَـحْـنا وَأَصْبَـحْ المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذا الـيَوْم، فَـتْحَهُ، وَنَصْـرَهُ، وَنـورَهُ وَبَـرَكَتَـهُ، وَهُـداهُ، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَه.

Aswbahnaa wa aswbahal-Mulku liLLaahi Rabbil ‘Aalamiyn. Allaahumma inniy as-aluka khayra haadhal-yawmi fat-hahu, wanaswarahu, wanuwrahu, wabarakatahu, wahudaahu, wa a’uwdhu Bika min sharri maa fiyhi washarri maa ba’-dahu

 

Tumeingia asubuhi  na imefika asubuhi na Ufalme ni wa Allaah Rabb wa walimwengu, Ee Allaah, hakika mimi nakuomba khayr ya siku hii ya leo, ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najikinga Kwako kutokana na shari ya kilicho ndani ya siku hii, na shari ya baada ya siku hii. [Hadiyth ya Abuu Maalik Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ’anhu) ameikusanya Abuu Daawuwd (4/322) [5084], na isnadi yake ni Hasan kutoka kwa Shu’ayb na ‘Abdul-Qaadir Al-Arnaauwtw katika Tahqiyq Zaad Al-Ma’aad (2/273)].

 

Jioni useme:

 

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذهِ اللَّـيْلَة، فَتْحَهـا، وَنَصْـرَهـا، وَنـورَهـا، وَبَـرَكَتَـهـا، وَهُـداهـا، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهـاِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَهـا.

 

Amsaynaa wa amsal-Mulku liLLaah Rabbil ‘Aalamiyn. Allaahumma inniy as-aluka khayra haadhihil-laylati fat-hahaa, wanaswarahaa, wanuwrahaa, wabarakatahaa, wahudaahaa, wa a’uwudhu Bika min sharri maa fiyhaa washarri maa ba’dahaa

 

Tumeingia jioni na imefika jioni na Ufalme ni wa Allaah, Rabb wa walimwengu, Ee Allaah hakika mimi nakuomba khayr ya usiku huu, ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najikinga kwako kutokana na shari ya kilicho ndani ya usiku huu, na shari ya baada ya usiku huu.

 

Pia:

 

أَصْـبَحْنا وَأَصْـبَحَ المـلكُ لله وَالحَمدُ لله، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هَذا الْيَوْمِ  وَخَـيرَ ما بَعْـدَهُ، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هَذا الْيَوْمِ  وَشَرِّ ما بَعْـدَهُ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ  وَعَـذابٍ في القَـبْر  

 

Aswbahnaa wa aswbahal-Mulku liLLaah wal-HamduliLlaah. Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu, wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr. Rabbi as-aluka khayra maa fiy haadhal yawmi wakhayra maa ba’-daahu, wa a’uwdhu bika minsharri haadhal yawmi washarri maa ba’-dahuu, Rabbi a’uwdhu bika minal kasali wasuw-il kibari, Rabbi a’uwdhu bika min ‘adhaabin finnaari wa ‘adhaabin fil qabri

 

Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Allaah, na Himdi ni Zake Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah, hali yakuwa Peke Yake, Hana mshirika. Ni Wake Ufalme, na Himdi ni Zake, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. Rabb wangu, nakuomba khayr ya siku ya leo, na khayr ya baada ya siku hii, na ninajikinga Kwako kutokana na shari ya siku ya leo na shari ya baada ya siku hii.  Rabb wangu, najikinga Kwako kutokana na uvivu, na ubaya wa uzee ubaya. Rabb wangu, najikinga Kwako kutokana na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburi. [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas‘wud (Radhwiya Allaahu ‘anhu) - Muslim (4/2088) [2723]

 

 

Na ikiingia jioni useme:

 

 أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هـذهِ اللَّـيْلَةِ وَخَـيرَ ما بَعْـدَهـا، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هـذهِ اللَّـيْلةِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهـا، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ  وَعَـذابٍ في القَـبْر

 

Amsaynaa wa amsal-Mulku liLLaah wal-HamduliLLaahi. Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu, wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr. Rabbi as-aluka khayra maa fiy haadhihil-laylati wakhayra maa ba’dahaa, wa a’uwdhu bika minsharri haadhihil-laylati washarri maa ba’dahaa, Rabbi a’uwdhu bika minalkasli wasuw-il kibari, Rabbi a’uwdhu bika min ‘adhaabin finnaari wa ‘adhaabin filqabri

 

 

Nyinginezo ni du’aa ifuatayo ambayo ni miongoni mwa du’aa za usiku wakati wa kulala:

 

اللَّهُمَّ رَبَّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ وَرَبَّ الأَرْضِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ، رَبَّنَا وَرَبَّ كُلِّ شَيْءٍ، فَالِقَ الْحَبِّ وَالنَّوَى، وَمُنْزِلَ التَّوْرَاةِ وَالإِنْجِيلِ وَالْفُرْقَانِ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ كُلِّ شَيْءٍ أَنْتَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهِ، اللَّهُمَّ أَنْتَ الأَوَّلُ فَلَيْسَ قَبْلَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الآَخِرُ فَلَيْسَ بَعْدَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الظَّاهِرُ فَلَيْسَ فَوْقَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الْبَاطِنُ فَلَيْسَ دُونَكَ شَيْءٌ ، اقْضِ عَنَّا الدَّيْنَ وَأَغْنِنَا مِنَ الْفَقْر

 

Allaahumma Rabbas-samaawatis-sab-‘i wa Rabbal-ardhwi, wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwiym, Rabbanaa wa Rabba kulli shay-in, faaliqal-habbi wan-nnawaa, wa munzilat-Tawraati wal-Injiyli  wal-Furqaan. A’uwdhu bika min sharri kulli shay-in Anta aakhidhun binaaswiyatihi. Allaahumma Antal-Awwalu falaysa qablaka shay-un, wa Antal-Aakhiru falaysa ba’-daka shay-un wa Antadhw-Dhwaahiru falaysa fawqaka shay-un, wa Antal-Baatwinu falaysa duwnaka shay-un. Iqdhwi ‘annad-dayna wagh-ninaa minal-faqri  

 

Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba na Rabb wa ardhi, na Rabb wa ‘Arsh ‘Adhimu, Rabb wetu na Rabb wa kila kitu, Mpasuaji wa mbegu na kokwa na Aliyeiteremsha Tawraat na Injiyl na Qur-aan. Najikinga Kwako shari ya kila kitu, Wewe Ndiye Mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah, Wewe Ndiye Al-Awwalu (wa Awali hakuna kitu kabla Yako) na Al-Aakhiru (wa Mwisho hakuna kitu baada Yako) na Adhw-Dhwaahiru (Uliye juu hakuna kitu juu Yako), na Al-Baatwinu (Uliye karibu, hakuna kitu kilicho karibu kuliko Wewe), Nilipie madeni yangu na Niepushe na ufakiri.  [Muslim]

 

Tanbihi:

 

Tumezitaja humo baadhi ya adhkaar za asubuhi, jioni na usiku lakini hizo si zote, kwa hiyo nasaha ya dhati na muhimu kabisa ni kwamba Muislamu asiache kabisa kudumisha Nyiradi za asubuhi na jioni ambazo zimekusanya baadhi ya Suwrah na Aayah na du’aa mbali mbali za kumhifadhi dhidi ya kila aina ya maovu yakiwa ni shirki au shari za mashaytwaan na majini, au viumbe viovu na kila lenye shari.

Hali kadhaalika, kunapatikana kudumisha kuisoma Qur-aan na yaliyothibiti yote kama yalivyotangulia kutajwa.

 

 

 

 

Share

08-Ruqyah: Kuomba Kinga Kwa Allaah Kutokana Na Jirani Muovu

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Kuomba Kinga Kwa Allaah Kutokana Na Jirani Muovu

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Unapokuwa na jirani muovu huwa ni mtihani kwa sababu ya kukosa amani kutokana na shari zake. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba kinga dhidi ya jirani muovu na ameamrisha tujikinge naye:

  

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((تَعَوَّذُوا بِاللَّهِ مِنْ جَارِ السَّوْءِ فِي دَارِ الْمُقَامِ فَإِنَّ جَارَ الْبَادِيَةِ يَتَحَوَّلُ عَنْكَ))  رواه النسائي (5517) وأبو يعلى (6536) وابن حبان (1033) والحاكم (1951)

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ombeni kinga kwa Allaah kutokana na jirani muovu katika sehemu za makazi ya kudumu kwani jirani wa jangwani hubadilika badilika kuhama)) [An-Nasaaiy, Abuu Ya’laa (6536), Ibn Maajah (1033), Al-Haakim (1951) na ameisahihisha Imaam  Al-Albaaniy - Swahiyh An Nasaaiy (5517), As-Silsilatusw-Swahiyhah (3943),   Swahiyh Al-Jaami’ (2967)]

Ufafanuzi: Makazi ya kudumu: Makazi ya kuthibitika hayabadiliki; watu hubakia hawaondoki kuhama kuhama.

 

Hivyo basi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba:

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ جَارِ السَّوْءِ فِي دَارِ الْمُقَامِ فَإِنَّ جَارَ الْبَادِيَةِ يَتَحَوَّلُ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min jaaris-saw-i fiy daaril-muqaami fainna jaaral-baadiyati yatahawwalu.

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako na jirani muovu katika makazi ya kudumu kwani jirani wa jangwani hubadilika badilika kuhama)) [As-Silsilat Asw-Swahiyhah (3943), Swahiyh Al-Jaami’ (2967)]

 

Pia alikuwa akiomba:

أللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ  يَوْمِ السُّوءِ وَمِنْ لَيْلَةِ السُّوءِ وَمِنْ سَاعَةِ السُّوءِ وَمِنْ صَاحِبِ السُّوءِ وَمِنْ جَارِ السُّوءِ  فَي دَارِ الْمُقَامَةِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min yawmis-suw-i wamin laylatis-suw-I, wamin saa’atis-suw-i, wamin swaahibis-suw-i, wamin-jaaris suw-i fiy daaril-muqaamat

Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako kutokana na siku ovu, na usiku muovu, na saa ovu, na rafiki muovu, na jirani muovu katika makazi ya kudumu. [Atw-Twabaraaniy katika  Majma’ Az-Zawaaid (10/144), Swahiyh Al-Jaami’ (1/411)]

 

Pia:

 اللَّهُمَّ إنِّي أّعُوذُ بِكَ مِنْ جَارِ السُّوءِ، وَمِنْ زَوْجٍ تُشَيِّبُنِي قَبْلَ المَشِيبِ، وَمِنْ وَلَدٍ يَكُونُ عَليَّ رَبّاً، وَمِنْ مَالٍ يَكُونُ عَلَيَّ عَذَابَاً، وَمِنْ خَلِيْلٍ مَاكِرٍ عَيْنُهُ تَرَانِي، وَقَلْبُهُ يَرْعَانِي؛ إِنْ رَأَى حَسَنَةً دَفَنَهَا، وَإِذَا رَأَى سَيِّئَةً أَذَاعَهَا 

 الطبراني في الدعاء، 3/ 1425، برقم 1339، وهناد في الزهد، برقم 1038، وقال الألباني في سلسلة الأحاديث الصحيحة، 7/ 377، برقم 3137 :  قلت: وهذا إسناد جيد، رجاله كلهم من رجال التهذيب

Allaahumma inniy a’uwdhu Bika min jaaris-suw-i, wa min zawjin tushayyibuniy qablal-mashiybi, wa min waladin yakuwnu ‘alayya rabban, wamin maalin yakuwnu ‘alayya ‘adhaaban, wamin khaliylin ‘aynuhuu taraaniy wa qalbuhu yar’aaniy, in raa hasanah dafanahaa, wa idhaa raa sayyiah adhaa’ahaa

Ee Allaah, najikinga Kwako kutokana na jirani muovu, na kutokana na mke atakayenisababisha uzee kabla ya uzee na kutokana mwana atakayekuwa ni bwana kwangu anayenidhibiti, na kutokana na mali itakayokuwa ni adhabu kwangu, na kutokana na rafiki mwandani khaini; ambaye macho yake yananitazama lakini huku moyo wake unaniangaza kwa hila kiasi kwamba anapoona zuri  hulificha, lakini  anapoliona baya hulitangaza. [Atw-Twabaraaniy katika Ad-Du’aa (3//1425) [1339] na Hunaad katika Az-Zuhd (1038) na Al-Albaaniy amesema katika As-Silsilat Asw-Swahiyhah (7/377) [3137]:  Nimesema hii ni Isnaad nzuri, watu wake wote ni katika watu wa kuaminika]

 

Haipasi jirani kumfanyia jirani mwenzake uovu wowote ule, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameamrisha kumfanyia wema, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ

Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa. [An-Nisaa: 36]

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ ،  وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ ،  وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ!))  قِيلَ: مَنْ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟  قَالَ: الَّذِي لاَ يَأْمَنُ جَارُهُ بَوَائقَهُ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Wa-Allaahi hakuamini (hana Iymaan). Wa-Allaahi hakuamini, Wallaahi hakuamini!)) Akaulizwa: Nani ee Rasuli wa Allaah? Akasema: ((Ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

وَفِي رِوَايَة: ((لاَ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ مَنْ لاَ يَأْمَنُ جَارُهُ بَوَائِقَهُ)) مسلم

Na katika riwaaya nyengine: ((Hatoingia Peponi ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake)).[Muslim]

 

عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا زَالَ جِبْرِيلُ يُوصِينِي بِالْجَارِ حَتَّى ظَنَنْتُ أَنَّهُ سَيُوَرِّثُهُ)). متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jibriyl hakuacha kuniusia jirani mpaka nikadhani kuwa atawafanya warithi wangu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]  

 

 

Share

09-Ruqyah: Kuomba Kinga Kwa Allaah Dhidi Ya Adui, Dhulma, Na Ukandamizaji

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Kuomba Kinga Kwa Allaah Dhidi Ya Adui, Dhulma, Na Ukandamizaji

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Du’aa ifuatayo ni ya mwenye kuogopa dhulma ya anayetawala au ukandamizaji au dhidi ya yeyote unayekhofia dhulma zake. Unaisoma (hiyo du'aa) kisha unataja jina la mtu huyo.

 

أللَّهُمَّ رَبَّ السَّمواتِ السَّبْعِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيم، كُنْ لِي جاَراً مِنْ (فُلانِ بْنِ فُلاَنٍ) وَأَحْزَابِهِ مِنْ خَلاَئِقِكَ أَنْ يَفْرُطَ عَلَيَّ أحَدٌ مِنْهُمْ أَوْ يَطْغَى، عَزَّ جاَرُكَ وَجَلَّ ثَناَؤُكَ، وَلاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ

Allaahumma Rabbas-samaawatis-sab-’i wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwiym, kun liy jaaran min (fulaani bin fulaani – unamtaja jina lake) wa ahzaabihi min Khalaaiqika an yafrutwa ‘alayya ahadun minhum an yatw-ghaa. ‘Azza Jaaruka, wa Jalla Thanaauka, walaa ilaaha illaa Anta

 

Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba, na Rabb wa ‘Arshi Tukufu, kuwa Mlinzi wangu kutokana na (fulani bin fulani [taja mtu unayemhofu])  na vikosi vyake miongoni mwa viumbe Vyako, kwa kunisaliti mmoja miongoni  mwao, au kunifanyia uadui. Imeimarika madhubuti hifadhi Yako, na zimetukuka sifa Zako na hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe[Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) - Al-Bukhaariy fiy Al-Adab Al-Mufrad [707] na ameisahihisha Al-Albaaniy (  katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad [546].   

 

Du’aa nyingineyo ambayo pia unataja jina la mtu unayeogopa dhulma zake:

 

الله أكْبَر، الله أعَزُّ مِنْ خَلْقِهِ جَمِيْعاً، الله أعَزُّ مِمَّا أخَافُ وَأحْذَر، أعُوذُ بِاللهِ الَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ، الْمُمْسِكِ السَّمَوَا تِ السَّبْعِ أَنْ يَقَعْنَ عَلَى الأَرْضِ ِإلاَّ بِإِذْنِهِ، مِنْ شَرِّ عَبْدِكَ (فلان) وَجُنُوْدِهِ وَأَتْبَاعِهِ وَأَشْيَاعِهِ، مِنَ اْلجِنِّ والإِنْسِ، اَلَّلهُمَّ كُنْ لِيْ جَاراً مِنْ شَرِّهِمْ، جَلَّ ثَنَاؤُكَ وَعَزَّ جَارُكَ، وَتَبَارَكَ اسْمُكَ، وَلاَ إلَهَ غَيْرُكَ

Allaahu Akbar, Allaahu A’azzu min Khalqihi jamiy’aa. Allaahu A’azzu mimmaa akhaafu wa ahdharu. A’uwdhu biLLaahi Alladhiy laa ilaaha illaa Huwa. Al-Mumsikis-samawaatis-sab-’i an yaqa’-na ‘alal-ardhwi illaa biidhnihi, min sharri ‘abdika (fulani - mtaje mtu unayemkhofu) wa junuwdihi, wa atbaa’ihi, wa ash-yaa’ihii minal jinni wal insi. Allaahumma kun-liy jaaran min sharrihim, Jalla Thanaauka, wa ‘Azza Jaaruka, wa Tabaarakas-Smuka walaa ilaaha Ghayruka [mara 3].

 

Allaah ni Mkubwa, Allaah, ni Mwenye ni Mwenye nguvu Mshindi kuliko viumbe Vyake vyote. Allaah ni Mwenye nguvu Mshindi kuliko kila nikiogopacho na kujihadhari. Najikinga kwa Allaah Ambaye hapana muabudiwa wa haki ila Yeye tu, Ambaye Ameshikilia mbingu saba ili zisiangukie ardhi ila kwa idhini Yake, kutokana na shari ya mja (fulani - mtaje mtu unayemkhofu) na majeshi yake, na wanaomfuata, na wafuasi wake miongoni mwa majini na watu. Ee Allaah, kuwa Mlinzi wangu kutokana na shari yao. Zimetukuka Sifa Zako na Umetukuka ulinzi Wako na Limebarikika Jina Lako, na hapana muabudiwa wa haki ghairi Yako. [Du’aa ya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) Al-Bukhaariy fiy Adabil-Mufrad [708] na ameisahihisha Al-Albaaniy  katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad [546].]

 

 

Du’aa nyinginezo:

 

 اَللَّهُمَّ احْفَظْنِي بِالإِسْلاَمِ قَائِمًا  وَاحْفَظْنِي بِالإِسْلاَمِ قَاعِداً  وَاحْفَظْنِي بِالإِسْلاَمِ رَاقِداً  وَلاَ تُشْمِتْ بِي عَدُوًا وَلاَ حَاسِداً. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ كُلِّ خَيْرٍ خَزَائِنُهُ بِيَدِكَ  وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ كُلِّ شَرٍّ خَزَائِنُهُ بِيَدِك   

Allaahummah-fadhwniy bil Islaami qaaimaa, wahfadhwniy bil Islaami qaaidaa, wahfadhwniy bil Islaami raaqidaa, walaa tushmit biy ‘aduwwan walaa haasidaa. Allaahumma inniy as-aluka min kulli khayrin khazaainuhu Biyadika, wa a’uwdhu Bika min kulli sharrin khazaainuhu Biyadika

 

Ee Allaah, nihifadhi katika Uislamu nikiwa nimesimama, na nihifadhi katika Usilamu nikiwa nimekaa, na nihifadhi katika Uislamu nikiwa nimelala, wala Usinijaalie kuwa bezo la adui wala hasidi. Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kila khayr ambazo hazina zake zimo Mikononi Mwako, na najikinga Kwako shari zote ambazo hazina zake zimo Mikononi Mwako. [Al-Haakim, Taz., Swahiyh Al-Jaami’ (2/398) na Silsilat Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (4/54 – 1540)]

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ غَلَبَةِ الدَّيْنِ وَغَلَبَةِ الْعَدُوِّ وَشَمَاتَةِ الأَعْدَاءِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min ghalabatid-dayni, wa ghalabatil-‘aduwwi wa shamaatatil-a’-daai

 

Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako kushindwa deni, na kushindwa na adui, na bezo la maadui.  [An-Nasaaiy, Ahmad -  Swahiyh An-Nasaaiy (3/1113)]

 

أللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ جَهْدِ الْبَلاَءِ وَدَرَكِ الشَّقَاءِ وَسُوءِ الْقَضَاءِ وَشَمَاتَةِ الأَعْدَاءِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min jahdil-balaai wa darakish-shaqaai wa suw-il-qadhwaai, wa shamaatatil-a’daai

 

Ee Allaah hakika mimi najikinga Kwako shida ya balaa [mitihani n.k.] na kukumbwa na uovu na majaaliwa mabaya na bezo la maadui. [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْفَقْرِ وَالْقِلَّةِ وَالذِّلَّةِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أَظْلِمَ أَوْ أُظْلَمَ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika minal-faqri wal-qillati, wadh-dhillati, wa a’uwdhu bika min an adhwlima aw udhwlama

 

Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako ufakiri na uchache na udhalilifu na najikinga Kwako kudhulumu au kudhulumiwa. [Abuu Daawuwd, Ahmad – Swahiyh Abiy Daawuwd (1544)]

 

اللَّهُمَّ مَتِّعْنِي بِسَمْعِي وَبَصَرِي  وَاجْعَلْهُمَا الْوَارِثَ مِنِّي وَانْصُرْنِي عَلَى مَنْ يَظْلِمُنِي وَخُذْ مِنْهُ بِثَأْرِي

Allaahumma matti’-niy bisam-’iy, wa baswariy, waj-’al-humal-waaritha minniy, wanswurniy ‘alaa man yadhwlimuniy, wa khudh minhu bitha-ariy

 

Ee Allaah, ninufaishe kwa masikio yangu, na macho yangu, na vijaalie [viwili hivyo] viwe hivyo kwa warithi wangu na ninusuru dhidi ya anayenidhulumu, na nilipizie dhidi yake.[At-Tirmidhiy Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/188)]

 

حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

Hasbuna-Allaahu wa Ni’-mal-Wakiyl

 

Allaah Anatutosheleza, Mzuri Alioje Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.

[Al-Bukhaariy  kutoka kwa Ibn ‘Abbaas: “Ameisema Ibraahiym  ('Alayhis-Salaam) alipotupwa Motoni na ameisema Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) waliposema (Suwrat A’Imraan 3: 173) ((“Hasbuna-Allaah! Allaah Anatutosheleza, Mzuri Alioje Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.”)) 

 

اللَّهُمَّ لَكَ أَسْلَمْتُ وَبِكَ آمَنْتُ وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْكَ أَنَبْتُ وَبِكَ خَاصَمْتُ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِعِزَّتِكَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ أَنْ تُضِلَّنِي أَنْتَ الْحَيُّ الَّذِي لاَ يَمُوتُ وَالْجِنُّ وَالإِنْسُ يَمُوتُونَ

 

Allaahumma laka aslamtu, wa bika aamantu, wa ‘alayka tawakkaltu, wa ilayka anabtu, wa bika khaaswamtu. Allaahumma inniy a’uwdhu bika bi’izzatika laa ilaaha illa Anta an-tudhwillaniy Antal-Hayyu Alladhiy  laa Yamuwtu wal-jinnu wal-insu yamuwtuwna.

 

Ee Allaah, Kwako najisalimisha na Kwako naamini na Kwako natawakali na Kwako narejea kutubu na Kwako nagombana [dhidi ya adui]. Ee Allaah, hakika mimi najikinga kwa Utukufu Wako, hapana muabudiwa wa haki ila Wewe Usije kunipotoa Wewe Uliye Hai daima Ambaye Hafi ilhali majini na watu wanakufa.

[Muslim, Ahmad]

 

رَبِّ أَعِنِّي وَلاَ تُعِنْ عَلَيَّ، وَانْصُرْنِي وَلاَ تَنْصُرْ عَلَيَّ، وَامْكُرْ لِي وَلاَ تَمْكُرْ عَلَيَّ، وَاهْدِنِي وَيَسِّرْ الْهُدَى إِلَيَّ ، وَانْصُرْنِي عَلَى مَنْ بَغَى عَلَيَّ،  رَبِّ اجْعَلْنِي لَكَ شَكَّارًا، لَكَ ذَكَّارًا، لَكَ رَهَّابًا، لَكَ مُطِيعًا، إِلَيْكَ مُخْبِتًا أَوَّاهًا مُنِيبًا، رَبِّ تَقَبَّلْ تَوْبَتِي، وَاغْسِلْ حَوْبَتِي،  وَأَجِبْ دَعْوَتِي، وَثَبِّتْ حُجَّتِي، وَاهْدِ قَلْبِي، وَسَدِّدْ لِسَانِي، وَاسْلُلْ سَخِيمَةَ قَلْبِي  

 

Rabbi a’inniy walaa tu’in ‘alayya, wanswurniy walaa tanswur ‘alayya, wamkur-liy walaa tamkur ‘alayya, wahdiniy wa yassiril-hudaa ilayya, wanswurniy ‘alaa man baghaa ‘alayya. Rabbij-’alniy Laka shakkaaraa, Laka dhakkaaraa, Laka Rahhaaba, Laka mutwi’y-aa, ilayka mukhbitan awwaaham-muniybaa. Rabbi taqabbal tawbatiy, waghsil hawbatiy, wa ajib da’-watiy wahdi qalbiy, wa saddid lisaaniy, wa thabbit hujjatiy, waslul sakhiymata qalbiy.

 

Ee Rabb wangu nisaidie na Usisaidie dhidi yangu, na ninusuru wala Usinusuru dhidi yangu, na nipangie na Usipange dhidi yangu, na niongoze na usahilishe hidaaya kunijia na ninusuru dhidi ya atakayenifanyia uovu. Rabb wangu nijaalie niwe mwenye kukushukuru, mwenye kukudhukuru, mwenye kukuogopa, mwenye kukutii, mwenye kukukhofu, mwenye kunyenyekea na kurudia kuomba tawbah. Rabb wangu pokea tawbah yangu, na osha madhambi yangu, na Itikia du’aa zangu, na thibitisha hoja zangu, na Uhidi moyo wangu, na Nyoosha ulimi wangu [useme kweli], na futa uovu wa moyo wangu. [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah – Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/178) na Ahmad (1/127)]

 

 

Share

10-Ruqya: Kutafuta Shifaa: Poza Ya Maradhi, Sihri (Uchawi) Katika Baadhi Ya Vyakula

 

 Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Kutafuta Shifaa - Poza Ya Maradhi, Sihri (Uchawi) Katika Baadhi Ya Vyakula

 

www.alhidaaya.com 

 

 

Vifutavyo ni baadhi ya vyakula katika mwongozo wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) vyenye kusababisha kinga na shifaa ya kila aina ya maradhi ikiwemo sihri (uchawi).

 

 

1-Asali:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَأَوْحَىٰ رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا وَمِنَ الشَّجَرِ وَمِمَّا يَعْرِشُونَ ﴿٦٨﴾

68. Na Rabb wako Akamtia ilhamu nyuki kwamba: “Jitengenezee nyumba katika majabali, na katika miti, na katika wanavyojenga.”

 

ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ فَاسْلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا ۚ يَخْرُجُ مِن بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاءٌ لِّلنَّاسِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٦٩﴾

69. “Kisha kula katika kila matunda, na fuata njia za Rabb wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita). Kinatoka katika matumbo yao kinywaji cha rangi mbali mbali ndani yake mna shifaa (ya magonjwa) kwa watu. Hakika katika hayo, bila shaka ni Aayah (ishara, dalili, zingatio) kwa watu wanaotafakari.  [An-Nahl: 68-69]

 

 

2-Maji Ya Zamzam:

 

 عن جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ (رضي الله عنه) قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  يَقُولُ: ((مَاءُ زَمْزَمَ لِمَا شُرِبَ لَهُ))

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah  (Radhwiya Allaahu 'anhu)  amesema:  Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Maji ya zamzam kwa jambo linaloombewa wakati wa kunywa)) [Ibn Maajah, Ahmad. Taz, Swahiyh Ibn Maajah (2502), Swahiyh Al-Jaami’ (5502)]. Tanbihi: Ingawa kuna udhaifu katika Hadiyth hii lakini kutokana na Shawaahid imekuwa ni Hasan.

 

 

3-Habbat Sawdaa – Haba soda

 

عَنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) أَنَّهَا سَمِعَتْ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((إِنَّ هَذِهِ الْحَبَّةَ السَّوْدَاءَ شِفَاءٌ مِنْ كُلِّ دَاءٍ إلاَّ مِنْ السَّام))ِ قُلْتُ وَمَا السَّامُ؟  قَالَ: ((الْمَوْتُ))

Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika Habbat Sawdaa hii ni shifaa kwa kila maradhi isipokuwa sumu)) Nikasema: Nini sumu? Akasema: ((Mauti)) [Al-Bukhaariy, Muslim, Ibn Maajah, Ahmad]

 

 

4-Sannaa Na Sannuwt

 

Sannaa = Majani ya Sanamaki – yanachemshwa na kunywa kwa ajili ya kuendesha na kusafisha tumbo.

 

Sannuwt = Ima kotmiri mwitu (dill au parsley) au asali kama alivyosema ibn Maajah katika Kitaab Al-Twibb, Hadiyth (3457)

 

Wengineo wamesema Sannuwt ni aina ya binzari tamu (fennel), au habbat hamraa (sufa/dill seeds) wengine wamesema ni malai au asali inayopatikana katika mbegu. Na Allaah Anajua zaidi

 

عن أبي أُبَيِّ بْنَ أُمِّ حَرَامٍ رضي الله عنه قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: ((عَلَيْكُمْ بِالسَّنَى، وَالسَّنُّوتِ، فَإِنَّ فِيهِمَا شِفَاءً مِنْ كُلِّ دَاءٍ، إِلَّا السَّامَ)) قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا السَّامُ؟ قَالَ: ((الْمَوْتُ)) روى ابن ماجة (3457) ، والحاكم (7442) ، والطبراني في "مسند الشاميين" (14) ، وأبو نعيم في "الطب النبوي" (177) " وصححه الألباني في " سلسلة الأحاديث الصحيحة" (7442) .

 

Imepokelewa kutoka kwa Abiy Ubayy bin Ummi Haraam (Radhwiya Allaahu 'anhu) kasema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Tilieni hima kutumia sannah na sannuwt, kwani hivyo viwili ni  shifaa (poza) ya kila maradhi isipokuwa sumu)). Akaulizwa: Nini sumu? Akasema: ((Mauti)) [Ibn Maajah (3457), Al-Haakim (7442), Atw-Twabaraaniy katika Musnad Ash-Shaamiyiyn (14), Abuu Na’iym katika Twibb An-Nabawiy (177) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Silsilatul Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (7442)]

 

 

5-Tende:

 

Kula tende saba asubuhi kabla ya kula chochote ni kinga ya sihri (uchawi)

 

عن عَامِرُ بْنُ سَعْدٍ عَنْ أَبِيهِ (رضي الله عنهما) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَنْ تَصَبَّحَ كُلَّ يَوْمٍ سَبْعَ تَمَرَاتٍ عَجْوَةً لَمْ يَضُرَّهُ فِي ذَلِكَ الْيَوْمِ سُمٌّ وَلاَ سِحْرٌ))

Kutoka kwa ‘Aamir bin Sa’d  kutoka kwa baba yake (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Atakayeamka kila siku asubuhi [akala] tende saba za ‘ajwah haitomdhuru siku hiyo sumu wala sihri [uchawi])) [Al-Bukhaariy. Katika Riwaayah ya Muslim; Kitaab Al-Ashribah imetaja kuliwa asubuhi mapema kabla ya chochote -

 

 

Je, Ni Tende Za ‘Ajwah Pekee Zinazopatikana Faida Hiyo? 

 

‘Ajwah ni aina ya tende zinazopatikana mji wa Madiynah lakini ‘Ulamaa wamekubaliana kwamba aina yoyote ya tende zinafaa kupatikana faida iliyotajwa katika Hadiyth hizo.

 

Imaam bin Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Inatarajiwa kuwa Allaah Atanufaisha kwa aina zote za tende ila tu imenukuliwa kuwa ni za Madiynah kutoka na kufadhilishwa kwa tende zake na umakhsusi wake. Na inatarajiwa kuwa Allaah Atanufaisha kwa tende saba zozote zile zikiliwa asubuhi, na huenda Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja ametaja hizo kutokana na fadhila zake makhsusi, na utajo maalum kwa tende za Madiynah,  haizuii faida aliyoiashiria Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika aina nyinginezo za tende, na nadhani imekuja katika baadhi ya riwaaya "miongoni mwa tende" bila kufungamanisha."

[Majmuw’ Fataawaa bin Baaz (8/109)]

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Shaykh wetu Ibn Sa’diy (Rahimahu Allaah) alikuwa akiona kwamba hizo 'ajwah ni kwa kupigia mfano tu wa tende, na kwamba iliyokusudiwa ni tende kwa ujumla.” 

[Ash-Sharh Al-Mumti’ (5/123) na Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb]

 

 

6-Maziwa:

 

عَنْ طَارِقِ بْنِ شِهَابٍ الأَحْمَسِيِّ (رضي الله عنه) أَنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)) قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ لَمْ يَضَعْ دَاءً إِلاَّ وَضَعَ لَهُ شِفَاءً, فَعَلَيْكُمْ بِأَلْبَانِ الْبَقَرِ فَإِنَّهَا تَرُمُّ مِنْ كُلِّ الشَّجَرِ))

Kutoka kwa Twaariq bin Shihaab Al-Ahmasiyyi (Radhwiya Allaahu 'anhu)   kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah (‘Azza wa Jalla) Hakuteremsha maradhi ila Ameyawekea shifaa, basi juu yenu [kunyweni]  maziwa ya ng’ombe kwani hayo yanatokana na kila aina ya miti)) [Swahiyh Al-Jaami’ (1808). (1810)]

 

 

7-Talbiynah:

 

عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها أَنَّهَا كَانَتْ تَأْمُرُ بِالتَّلْبِينِ لِلْمَرِيضِ وَلِلْمَحْزُونِ عَلَى الْهَالِكِ، وَكَانَتْ تَقُولُ: إِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((إِنَّ التَّلْبِينَةَ تُجِمُّ فُؤَادَ الْمَرِيضِ، وَتَذْهَبُ بِبَعْضِ الْحُزْنِ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba alikuwa akiamrisha talbiynah kwa ajili ya mgonjwa na mtu aliyefikwa na huzuni kwa ajili ya kufariki mtu wake. Akawa anasema: “Nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika talbiynah inamtuliza moyo wa mgonjwa na kuufanya mchangamfu na inaondosha baadhi ya huzuni zake)) [Al-Bukhaariy, Kitaab Atw-Twibb, Baab At-Talbiynah Lil-Mariydhw]

 

 

عنْ عَائِشَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهَا كَانَتْ إِذَا مَاتَ الْمَيِّتُ مِنْ أَهْلِهَا فَاجْتَمَعَ لِذَلِكَ النِّسَاءُ، ثُمَّ تَفَرَّقْنَ إِلا أَهْلَهَا وَخَاصَّتَهَا، أَمَرَتْ بِبُرْمَةٍ مِنْ تَلْبِينَةٍ فَطُبِخَتْ، ثُمَّ صُنِعَ ثَرِيدٌ فَصُبَّتْ التَّلْبِينَةُ عَلَيْهَا، ثُمَّ قَالَتْ: كُلْنَ مِنْهَا، فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يقُول: ((التَّلْبِينَةُ مُجِمَّةٌ لِفُؤَادِ الْمَرِيضِ، تَذ هبُ بِبَعْضِ الْحُزْنِ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah mke wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba alikuwa pale mtu alipofariki  katika jamaa zake na wanawake wakakusanyika katika nyumba ya aliyefiwa kisha huondoka isipokuwa jamaa zake na rafiki wa karibu kabisa. Huamrisha ipikwe ‘talbiynah’ (uji wa unga wa shayiri). Kisha ‘thariyd’ (mikate katika supu ya nyama) hupikwa na ‘talbiynah’ humiminwa juu yake. Kisha ‘Aaishah huwaambia wanawake: “Kuleni kwani nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Talbiynah inapooza moyo wa mgonjwa na inaondosha baadhi ya huzuni.” [Al-Bukhaariy katika Kitaab Atw-Twa’aam, Muslim katika Baab As-Salaam]

 

عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها قَالَتْ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((عَلَيْكُمْ بِالْبَغِيضِ النَّافِعِ التَّلْبِينَةِ))‏‏.‏ يَعْنِي الْحَسَاءَ‏.‏ قَالَتْ وَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا اشْتَكَى أَحَدٌ مِنْ أَهْلِهِ لَمْ تَزَلِ الْبُرْمَةُ عَلَى النَّارِ حَتَّى يَنْتَهِيَ أَحَدُ طَرَفَيْهِ ‏.‏ يَعْنِي يَبْرَأُ أَوْ يَمُوتُ ‏.‏

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kuleni faida ya talbiynah inayochukizwa [asiyeipenda mgonjwa])) Yaani uji wa shayiri. Akasema: “Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa pindi anapolalamika mtu katika ahli yake, basi sufuria ya kupikia haindokani katika moto mpaka mawili yatokee.” Yaani: ima apone mtu huyo au afariki. [Swahiyh Sunan Ibn Maajah 3446)]

 

 

عَنْ عَائِشَة رضي الله عنها عن النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((عليكم بالبغيضِ النافعِ التلبينةِ والذي نفسي بيده إنها لتغسل بطن أحدكم كما يغسل أحدكم الوسخ عن وجهه بالما))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kuleni kitu chenye faida ambacho hakipendwi kuliwa (na mgonjwa); talbiynah. Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, hakika hiyo inasafisha tumbo la mmoja wenu kama anavyosafisha mmoja wenu uchafu wa usoni mwake kwa maji)) [Sunan An-Nasaaiy Al-Kubraa (7575) na Mustadrak ‘Alaa Asw-Swahiyhayn]

 

 

Anaweza pia mtu kutumia dawa za asilia zinazojulikana kuponyesha maradhi mfano kutokana na mitishamba, mbegu n.k. ambazo zimetajwa katika kitabu cha Twibbun-Nabawiy (Tiba ya Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) cha Imaam Ibnul-Qayyim (Rahimahu-Allaah) na ‘Ulamaa wengineo.

 

 

Tiba Makhsusi Ya Sihri (Uchawi) Kwa Kutumia Majani Ya Mkunazi:

 

a-Unaweza kufuata njii hii ya Imaam Ibn Hajar:

 

Amesema Al-Hafidhw bin Hajar (Rahimahu Allaah): (Mtu) Achukue majani saba ya Sidri (Kunazi) (yaliyo) mabichi kisha ayatwange kati ya mawe mawili, kisha ayachanganye na maji na (kisha) ayasomee Ayatul-Kursiyy na Al-Qawaaqil:  (Suwrah Al-Jinn, Al-Kaafiruwn, Al-Ikhlaasw, Al-Falaq, An-Naas)  kisha avivie (apulizie)  mara tatu na kisha ayaoge, basi,  itamuondoshea yote yaliyomsibu. Na ni nzuri pia kwa yule aliyezuiwa (ashindwaye kumuingilia) Ahli yake kwa uchawi." [Fat-hul Baariy (10/233)]

 

Al-Qawaaqil ni Suwrah zinazoanzia na  قُلْ nazo ni: Al-Jinn (72), Al-Kaafiruwn (109), Al-Ikhlaasw (112), Al-Falaq (113), An-Naas (114)

 

b-Na juu ya hivyo somea Suwrah na Aayah zifuatazo:

 

Al-Faatihah

Aayatul-Kursiyy

Aayah mbili za mwisho wa Suwrah Al-Baqarah

Aayah namba 117 - 122 Suwrah Al-A'raaf (7)

Aayah namba 79 - 82  Suwrah Yuwnus (10)

Aayah namba 65 - 70 Suwrah Twaahaa (20)

Adhkaar nyenginezo za kinga na du'aa za kuomba Shifaa na kwa ujumla Qur-aan kwa wingi.

 

Pia, kufanya hijaamah (kuumikwa au kupigwa chuku)

 

 

[Al-'Ilaaj Bir-Ruqaa Minal-Kitaabi Was-Sunnah - Sa'iyd Bin 'Aliy Bin Wahf Al-Qahtwaaniy]

 

 

                                Mkunazi                                                     Mawe Mawili

 

                              

 

 

 

 

 

Share

11-Ruqyah: Kutafuta Shifaa Kwa Hijaamah

Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Kutafuta Shifaa Kwa Hijaamah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Miongoni mwa mwongozo wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kutafuta shifaa ya maradhi mbali mbali, ni kufanya hijaamah kama alivyosema:

خَيرُ ما تَداوَيتُم به الحِجامةُ

((Lilokuwa bora kabisa kwa tiba zenu ni Hijaamah)) [Hadiyth ya Samurah bin Jundub – As-Silsilah Asw-Swahiyhah (1053)]

 

Hijaamah inajulikana kama ni chuku au kuumikwa; nayo ni kuvutwa damu chafu yenye madhara kutoka sehemu kadhaa za mwilini kwa kuchanjwa kisha kuvutwa hiyo damu kwa pembe au aina ya kikombe cha gilasi.

 

Hadiyth kadhaa zimetaja umuhimu wa kutafuta shifaa kwa hijaamah, baadhi yake zimetaja na mengineyo kama kayyah (tiba ya kuchomwa moto kwa chuma), na pia  asali ambayo imeshatangulia kutajwa, na, Qiswtw Al-Bahr (au Qiswtw Al-Hind) hinnah n.k.

 

Qistw Al-Bahr au Qistw Al-Hind ni aina ya vijiti ambavyo vinasagwa kutoa unga wake na kutumiwa kama dawa ya maradhi mbali mbali.

 

  

Zifautazo ni Hadiyth chache za kuhusu tiba kwa hijaamah:

 

Kila Malaika mbinguni alimuusia Rasuli wa  Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ummah wake wafanye hijaamah, pindi alipokuwa katika safari ya Al-Israa Wal-Mi’raaj. Na ikabainishwa kuwa tarehe za kupaswa kufanywa hijaamah ni tarehe kumi na saba, kumi na tisa, na ishirini na moja ya miezi ya Hijriy.

 

Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas na Ibn Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhumaa):

 

خَيرُ يومٍ تَحْتَجِمُونَ فيه سبعُ عَشْرةَ، و تِسعُ عشْرةَ، وإِحدَى و عِشرينَ. وما مَرَرْتُ بِمَلأٍ من الملائِكةِ لَيلةَ أُسْرِيَ بِي إِلَّا قالُوا : عليكَ بِالحِجامةِ يَا مُحمَّدُ

((Siku bora kabisa za kufanya hijaamah kwenu ni tarehe kumi na saba, kumi na tisa na ishirini na moja, na sijampitia Malaika yeyote yule usiku wa Israa isipokuwa walisema: Himiza kufanya hijaamah yaa Muhammad)) [Swahiyh Al-Jaami' (3332)]

 

 

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا) عَنْ النَبِيِّ (صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّم ) قَالَ: ((الشِّفَاءُ فِي ثَلاَثَةٍ:  شَرْبَةِ عَسَلٍ وَشَرْطَةِ مِحْجَمٍ وَكَيَّةِ نَارٍ وَأَنْهَى أُمَّتِي عَنْ الْكَيِّ ))

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Shifaa inapatikana kutokana na matatu; kinywaji cha asali, hijaamah [kuumikwa, chuku], na kayyah (tiba ya kuchomwa moto kwa chuma), lakini nakataza Ummah wangu na kayyah) [Al-Bukhaariy]

 

 

Tanbihi kuhusu kayyah (tiba ya kuchomwa moto kwa chuma).

 

Ingawa tiba hii ameitaja Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) lakini mwenyewe akasema kuwa anaikataza. ‘Ulamaa wameona kwamba imekusudiwia itumike tiba hii pale inapokuwa ni dharura tu, baada ya kushindwa kupata aina nyinginezo za matibabu. Na kwa sababu kuchomwa moto ni katika aina adhabu ya moto, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewasifu wenye kutawakali kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) (kuliko wale wenye kutafuta kinga). [Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (1445), Mawqi’  Ar-Rasmiy li-Imaam Ibn Baaz]

 

 

عَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه أَنَّهُ سُئِلَ عَنْ أَجْرِ الْحَجَّامِ، فَقَالَ احْتَجَمَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم حَجَمَهُ أَبُو طَيْبَةَ، وَأَعْطَاهُ صَاعَيْنِ مِنْ طَعَامٍ، وَكَلَّمَ مَوَالِيَهُ فَخَفَّفُوا عَنْهُ، وَقَالَ: ((إِنَّ أَمْثَلَ مَا تَدَاوَيْتُمْ بِهِ الْحِجَامَةُ وَالْقُسْطُ الْبَحْرِيُّ ‏))‏ وَقَالَ: ‏((لاَ تُعَذِّبُوا صِبْيَانَكُمْ بِالْغَمْزِ مِنَ الْعُذْرَةِ، وَعَلَيْكُمْ بِالْقُسْطِ))

Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba aliulizwa kuhusu ujira wa mtu anayewafanyia watu hijaamah. Akasema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifanyiwa hijaamah na Abuu Twayyibah akampa swaa’aah mbili (pishi mbili) za chakula, akazungumza na mabwana zake kuwaomba wampunguzie gharama au kodi waliyokuwa wakimtoza kila siku. Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Dawa bora kabisa yenu kutumia ni kufanya hijaamah, na Qistw Al-Bahr)). Akasema: ((Msiwatese watoto wenu kwa kutibu tezi za koo au kimio kwa kubinya kaakaa (sakafu) ya mdomo na tumieni Qistw))  [Al-Bukhaariy – Kitaab Atw-Twibb]

 

  

كان إذا اشْتَكَى أحدٌ رأسَهُ قال: ((اذْهَبْ فَاحْتَجِمْ))، و إذا اشْتَكَى رِجْلَهُ قال: ((اذْهَبْ فَأخْضِبْها بِالحِنَّاءِ))

Ilikuwa pindi mtu anapolalamika kuumwa kichwa, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: ((Nenda ukafanye hijaamah)) na alipolalamika mtu mguu wake alisema: ((Nenda kaupake hinnah)) [Hadiyth ya Salmah Umm Raafi’ Mtumishi wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) – Swahiyh Al-Jaami’ (4671), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (2059)]

 

 

Nyakati na siku bora za kufanya hijaamah:

 

 عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ يَا نَافِعُ قَدْ تَبَيَّغَ بِيَ الدَّمُ فَالْتَمِسْ لِي حَجَّامًا وَاجْعَلْهُ رَفِيقًا إِنِ اسْتَطَعْتَ وَلاَ تَجْعَلْهُ شَيْخًا كَبِيرًا وَلاَ صَبِيًّا صَغِيرًا فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((الْحِجَامَةُ عَلَى الرِّيقِ أَمْثَلُ وَفِيهِ شِفَاءٌ وَبَرَكَةٌ وَتَزِيدُ فِي الْعَقْلِ وَفِي الْحِفْظِ فَاحْتَجِمُوا عَلَى بَرَكَةِ اللَّهِ يَوْمَ الْخَمِيسِ وَاجْتَنِبُوا الْحِجَامَةَ يَوْمَ الأَرْبِعَاءِ وَالْجُمُعَةِ وَالسَّبْتِ وَيَوْمَ الأَحَدِ تَحَرِّيًا وَاحْتَجِمُوا يَوْمَ الاِثْنَيْنِ وَالثُّلاَثَاءِ فَإِنَّهُ الْيَوْمُ الَّذِي عَافَى اللَّهُ فِيهِ أَيُّوبَ مِنَ الْبَلاَءِ وَضَرَبَهُ بِالْبَلاَءِ يَوْمَ الأَرْبِعَاءِ فَإِنَّهُ لاَ يَبْدُو جُذَامٌ وَلاَ بَرَصٌ إِلاَّ يَوْمَ الأَرْبِعَاءِ أَوْ لَيْلَةَ الأَرْبِعَاءِ))

Ibn ‘Umar amesema: Ee Naafi’! Damu inanichemka, nitafutie mfanya hijaamah, lakini ukiweza tafuta mtu mpole na si mzee au kijana kwani nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hijaamah ni bora linapokuwa tumbo ni tupu kwani mna shifaa na barakah na inazidisha uwerevu na kuhifadhi kumbukumbu. Basi fanyeni hijaamah kwa barakah za Allaah siku za Alkhamiys, na epukeni hijaamah Jumatano, Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Fanyeni hijaamah Jumatatu na Jumanne kwani  hiyo ni siku ambao Allaah Alimpa afya (Nabiy) Ayyuwb kutokana na balaa (la maradhi), na alimsibu balaa la maradhi siku ya Jumatano, na ukoma na ubarasi hautokei isipokuwa Jumatano, au usiku wa Jumatano)) [Ibn Maajah – As-Silsilah Asw-Swahiyhah (766)]

 

 

 

 

 

 

 

Share