Fataawaa
Swalaah Ya Ijumaa
Swalaah Ya Ijumaa Ni Fardhi Kwa Kila Mwanamume
Haijuzu Kuiacha Kwa Sababu Ya Kazi Au Masomo Na Kadhaalika
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Swalaah ya Ijumaa ni Fardhw ‘Ayn (Fardhi kwa kila mtu mwanamme) wala haijuzu kuiacha kwa sababu ya kazi au masomo na sababu kama hizo.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
“Na yeyote anayemcha Allaah; Atamjaalia njia ya kutoka (shidani).”
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/184)]
Swalaah Ya Ijumaa Ni Fardhi Kwa Kila Mwanamme
Haijuzu Kuikhalifu Hata Ukikatazwa Na Mwajiri Wako
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Swalaah ya Ijumaa ni fardhi kwa kila mwanamme mwenye kukafilika katika ‘Ibaadah, mkazi, wala haikupasi kuikhalifu kwa sababu ya kazi hata kama mwajiri wako atakukataza.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/185)]
Wanaume Kuswali Ijumaa Misikitini Wanawake Nyumbani
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Ni wajibu kwa wanaume kuswali Ijumaa pamoja na ndugu zao Waislamu katika nyumba za Allaah (Misikitini). Ama wanawake wao hawana Ijumaa na ni wajibu kwao kuswali Adhuhuri.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/196)]
Haifai Kuzungumza Kamwe Pindi Khutba Ya Ijumaa Inapotolewa
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Haifai kwa mtu anayekuweko Masjid kuongea na yeyote yule pindi khutbah ya Ijumaa inatolewa.
Ama Imaam, yeye anaweza kuongea inapombidi kwa lile analoliona lina maslahi.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/201, 202)]
Kujuzu Swalaah Ya Ijumaa Hata Kama Idadi Ya Watu Ni Chini Ya Arubaini
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Inajuzu kusimamisha Swalaah ya Ijumaa hata kama idadi imepunguka chini ya watu arubaini kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ
“Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Swalaah siku ya Ijumaa, kimbilieni kumdhukuru Allaah.” [Al-Jumu’ah: 9]
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/215)]
Vipi Kuitikia Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Khatwiyb (wa Ijumaa) anapomswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), waitikie wanaomsikiliza (Maamuma) bila ya kupandisha sauti.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/217)]
Hukmu Ya Anayepitwa Na Rakaa Ya Swalaah Ya Ijumaa
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Anayepitwa na Rakaa katika Swalaah ya Ijumaa, na akaipata Rakaa nyingine, basi aiswali ile Rakaa (iliyompita) na hivyo atakuwa amepata Ijumaa kwa sababu limesihi kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hilo.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/225)]
Wajibu Kwa Imaam Kuwasalimia Maamuma Baada Ya Kupanda Minbari
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Ni Sunnah kwa Khatwiyb (wa Ijumaa) kuwasalimia maamuma anapopanda minbari kabla ya kukaa kitako (kusubiri Adhana).
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/234)]
Kuzungumza Wakati Khutbah Inapotolewa Ni Haramu
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Maongezi ya watu wakati Imaam anatoa khutbah siku ya Ijumaa ni haramu.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/240)]
Hukmu Ya Kumuombea Rahmah Anayepiga Chafya
Au Kurudisha Salaam Wakati Imaam Anakhutubia
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Kauli iliyo sahihi ya ‘Ulamaa ni kwamba, haijuzu kumuombea rahmah anayepiga chafya wala kurudisha salaam wakati Imaam (Khatwiyb) anakhutubia.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/242)]
Hakuna Sunnah Rawaatib Katika Swalaah Ya Ijumaa
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Hakuna Sunnah za Rawaatib za qabliyyah (kabla ya Swalaah) katika Swalaah ya Ijumaa. Lakini anaweza kuswali Sunnah atakazo kabla ya kuingia Imaam.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/249)]
Suwrah Za Kusomwa Katika Swalaah Ya Ijumaa
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Iliyo katika Shariy’ah kusomwa katika Swalaah ya Ijumaa ni Suwrat “Al-A’laa” na “Al-Ghaashiyah” au “Al-Jumu’ah” na “Al-Munaafiquwn”, au “Al-Jumu’ah” na “Al-Ghaashiyah”.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/279)]
Hukmu Ya Anayeswalisha Ahli Zake Nyumbani Swalaah Ya Ijumaa
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Atakayeswalisha ahli zake Swalaah ya Ijumaa nyumbani, anapaswa airudie kwa kuiswali Swalaah ya Adhuhuri, wala Swalaah (hiyo) ya Ijumaa (walioiswali nyumbani) haisihi kwao.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/196)]