Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Tiba Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 

 

 

 

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

Share

000-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Utangulizi Wa Mwandishi

 

Swahiyh Twibbin-Nabawiy

 

 

000-Utangulizi:

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

Kwa hakika Himdi Anastahiki Allaah, tunamhimidi tunamtaka msaada, tunamuomba maghfirah, na tunajikinga kwa Allaah kutokana na shari za nafsi zetu, na kutokana na uovu wa matendo yetu.  Mwenye kuhidiwa na Allaah hakuna wa kumpotoa, na aliyeachwa kupotea hakuna wa kumhidi.

 

Na nashuhudia kuwa hapana muabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake Hana mshirika. Na nashuhudia kuwa Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake.

 

Ama baada ya utangulizi huo:  Mtazamo wa Uislamu kwenye Tiba Una pande mbili.

 

Kwanza: Mtazamo wa Uislamu kwa mwana Aadam; Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amejaalia kuwa mwana Aadam ni Khalifa katika ardhi.[1]

 

 

وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾

Na pindi Rabb wako Alipowaambia Malaika: “Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi khalifa.” [Al-Baqarah: 30]

 

Na kadhalika Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amemtukuza mwana Aadam. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

  

وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلًا ﴿٧٠﴾

Na kwa yakini Tumewakirimu wana wa Aadam, na Tukawabeba katika nchi kavu na baharini, na Tukawaruzuku katika vizuri na Tukawafadhilisha juu ya wengi miongoni mwa Tuliowaumba kwa ufadhilisho mkubwa. [Al-Israa: 70]

 

 

Na Amemdhalilishia vilivyomo duniani ili aiamarishe kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika Suwrat Al-Baqarah:

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا 

Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini [Al-Baqarah: 29]

 

Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

أَلَمْ تَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَسْبَغَ عَلَيْكُمْ نِعَمَهُ ظَاهِرَةً وَبَاطِنَةً ۗ وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَابٍ مُّنِيرٍ ﴿٢٠﴾

Je, hamuoni kwamba Allaah Amekuitishieni vile vilivyomo mbinguni na vile vilivyomo ardhini, na Akakutimizieni kitimilifu neema Zake kwa dhahiri na siri?  Na miongoni mwa watu wako wanaobishana kuhusu Allaah bila ya elimu yoyote ile, na bila ya mwongozo wowote ule, na bila ya kitabu chochote kile chenye nuru.  [Luqmaan: 20]

 

Na kauli yake Allaah (Ta’aalaa):  

 

اللَّـهُ الَّذِي سَخَّرَ لَكُمُ الْبَحْرَ لِتَجْرِيَ الْفُلْكُ فِيهِ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿١٢﴾

Allaah Ambaye Amekutiishieni bahari ili zipite merikebu humo kwa amri Yake, na ili mtafute katika fadhila Zake na ili mpate kushukuru.

 

وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مِّنْهُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿١٣﴾

Na Amekutiishieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini vyote humo. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayaat (hoja, dalili, ishara) kwa watu wanaotafakari. [Al-Jaathiyah 12-13]

 

 

Thamani hii kubwa ya mwana Aadam, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ameizungushia funiko madhubuti la dhamana na vizuizi vya kutendewa uadui isipokuwa kwa haki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Amefanya lile kosa la kumfanyia uadui mwana Aadam kama kwamba ni sawa na kufanya uadui kwa wana Aadam wote kama tusomavyo katika Suwrah Al-Maidah:

 

مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ۚ  

Kwa ajili ya hivyo, Tukawaandikia shariy’ah wana wa Israaiyl kwamba; atakayeiua nafsi bila ya nafsi (kuua), au kufanya ufisadi katika ardhi; basi ni kama ameua watu wote. Na atakayeiokoa kuihuisha, basi ni kama amewaokoa watu wote.  [Al-Maaidah: 32]

 

 

Na dhamana hizi, zimeelezwa na wanazuoni kuwa ni (Dharura Tano) na Ummah wote umeafikiana kuwa Shariy’ah imewekwa kwa ajili ya kuhifadhi mambo haya matano.

 

Al-Imaam Al-Shaatwiby (Rahimahu Allaah) amesema: “Kwa hakika Ummah umewafikiana, bali hata watu wa dini nyingine kuwa Shariy’ah imewekwa kwa lengo la kuhifadhi mambo hayo matano ‘Adh-Dhwaruriyyaat Al-Khamsah’ ambayo ni Dini, nafsi, kizazi, mali na akili, na ni lazima yajulikane kwa ummah wote kuwa ni mambo ya msingi…” [Al-Muwafaqaat (1/31)]

 

 

Na elimu ya Tiba ni katika njia kuu za kuhami nafsi, uzao, akili, na kulinda vitu hivyo ni haki ya kiwiliwili iliyo juu ya mtu. Kama walivyofahamu As-Salaf As-Swaalih (wema waliotangulia)

 

 

Imepokewa kutoka kwa Abuu Jahiyfah Wahab Ibn Abdillaah amesema:

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliunga udugu kati ya Salmaan Al-Farsiy na Abuu Dardaai. Siku moja Salmaan akamtembelea Abuu Dardaai akamkuta Ummu Dardaai na mavazi yasio maridadi (kama vile nguo za mfanyakazi). Salmaan akamuuliza: “Una nini”? (Ummu Dardaai) akasema: “Ndugu yako, huyu Abuu Dardaai hana haja na dunia.” (hamkurubii).  Alipokuja Abuu Dardaai akamtengenezea chakula Salmaan na akamwambia: “Kula, mimi nimefunga.” Salmaan akajibu: “Mimi sitokula mpaka wewe ule.” Basi akala, ilipokuwa usiku Abuu Dardaai akawa anasimama kufanya ‘ibaadah. Salmaan akamwambi: “Lala.” Akalala, kisha akawa anasimama tena kutaka kufanya ‘ibaadah, akamwambia: “Lala.”  Ilipokuwa mwishoni mwa usiku Salmaan alimwambia: “Sasa simama.” Wakaswali wote pamoja, Salmaan akamwambia Abuu Dardaai: “Rabb wako ana haki juu yako, na nafsi yako ina haki juu yako na mkeo ana haki juu yako, basi mpe kila mwenye haki haki yake”. Akamwendea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  na akamsimulia hayo,  kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akasema: “Amesema kweli Salmaan”  [Al-Bukhaariy 1968]

 

Waislamu wametambua umuhimu wa Tiba na thamani yake ukilinganisha na elimu mbali mbali; hivyo wakaiwekea umuhimu, wakasisitiza umuhimu wake, na ulazima wa kuifundisha na kujifundisha.

 

Imepokewa kutoka kwa ‘Urwah bin Az-Zubayr; kwamba alikuwa akimwambia Ummul-Muuminiyn ‘Aaishah bint As-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhaa). “Ee Mama yangu![2] Sishangai ufahamu wako; nasema: Mke wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na bint wa Abuu Bakr na sioni ajabu kutokana na ujuzi wako wa mashairi na masiku za watu; nasema: Bint wa Abuu Bakr na alikuwa katika wajuzi mno wa watu, lakini nastaajabu kutokana na elimu yako ya Tiba, vipi elimu hiyo, wapi umeipata?”

 

Kisha akasema huku akampiga kwenye mabega yake: “Ee ‘’Uryah!”[3]  “Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaugua mwishoni mwa umri wake ikawa makundi ya Waarabu kutoka pande mbali mbali yakimjia na kumpa aina mbalimbali za dawa, na nikawa ninamtibu kwa dawa hizo, basi ni kutokana na kisa hicho (ndipo nikajua Tiba)” [Hadiyth Hassan, imepokewa na Ahmad (6/67), na kutoka kwa Abuu Nu’aym katika ‘Al-Hilyah’ (2/50) na Adh-Dhahabi katika kitabu chake ‘As-Siyar’ (2/182) kwa isnaad yenye udhaifu ndani yake]

 

Ameeleza vema Imaam Al-Muttwalibiy Muhammad bin Idriys Ash-Shaafi’iy (Rahimahu Allaah) mlango huu wa Tiba, kwa namna ambayo imekuja kuwapa tabu sana waliokuja baada yake kwani Imaam Ash-Shaafi’iy alikuwa anajua vema elimu ya Tiba.

 

Imaam Adh-Dhahaby (Rahimahu Allaah) amesema, “Katika baadhi ya fani za Imaam huyu ni fani ya Tiba, kwani aliielewa vema’ [As-Siyar (10/56)]

 

Imaam Ash-Shaafi’iy (Rahimahu Allaah) alikuwa akisema: “Elimu ni aina mbili, elimu ya Fiqh kwa mambo ya Dini na elimu ya Tiba kwa ajili ya kiwiliwili. Na yasiyokuwa hayo ni ufasaha wa baraza” [Manaaqib Ash-Shafi’iy ya Al-Bayhaqiy (2/114)]

 

Na amesema: “Usikae kwenye mji usiokuwa na mwanazuoni anayeweza kufutu maswali ya Dini yako wala tabibu anayekuelimisha kuhusu mwili wako.” [Aadaab Ash-Shaafi’iy wa-Manaaqibihi cha Ibn Abiy Haatim (Uk. 323) na Manaaqib Ash-Shaafi’y (2/115)]

 

 

Na kwa ajili hii, Imaam Ash-Shaafi’iy aliwakosoa Waislamu wengi kwa kupuuzia elimu hii yenye manufaa.

 

Imepokewa kutoka kwa Harmalah, amesema nimemsikia Ash-Shaafi’iy akisema: “Mambo mawili wameghafilika nayo watu, elimu ya Tiba na Lugha ya Kiarabu.” [Manaaqib Ash-Shaafiy’ (2/116)]

 

Akasema tena: Ash-Shaafi’iy alikuwa anasikitikia Tiba walioipoteza Waislamu akisema, “Wamepoteza theluthi ya elimu, na wakaitelekeza kwa Mayahudi na Manaswara.” [Rejea iliyotangulia (2/116)]

 

Hivyo basi Tiba kwa Waislamu ni dharura ya ki mwana Aadam na hitajio la msingi na sio anasa ya kimawazo au jambo la ziada.

 

Imaam Ash-Shaafi’iy (Rahimahu Allaah) amesema: “Sijui elimu yeyote iliyo bora baada ya elimu ya halaal na haraam kuliko ta’aluma ya Tiba, isipokuwa watu wa kitabu wametushinda katika hilo.” [As-Siyar’ (10/57)]

 

Mwisho: Uislamu unatofautiana na dini zingine; Uislamu ni kwa ajili ya Aakhirah na dunia. Hivyo basi Uislamu haukuishia kuwafundisha watu yatakayowafaa na kuwaokoa wao Aakhirah tu, bali umewafundisha yatakayowafaa katika maisha yao ya dunia, pia ili kusimamisha jamii iliyo kamili duniani. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akateremsha elimu zote katika nyanja mbali mbali; kuna mfumo wa utawala na siasa, kuna mfumo wa kijamii na mfumo wa kiuchumi na mfumo wa siha na kadhalika.

 

Na atakayezingatia mwongozo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ataukuta ni mwongozo ulio bora kuliko yote na uliokamilika katika kuhifadhi siha. Kwani kulinda siha kunategemea katika kuzingatia vyema vinywaji, vyakula, mavazi, makazi, hewa, malazi, kuamka, harakati, na utulivu. Haya yakipatikana kwa namna iliyolingana sawa, inayoendana na mwili, basi hupelekea kuwa na afya ya kudumu na kuweza kuhifadhika.

 

Ilipokuwa daraja ya elimu ya Tiba ni kubwa katika Uislamu na ndio kauli sahihi ya kweli mno kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani msamiati ya Tiba ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) iko juu kileleni kabisa, ina sifa za pekee kuliko Tiba ya ki mwana Aadam kwani inatokana na chanzo cha Wahyi.  

 

Kwa kuwa Tiba ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) haijatiliwa mkazo, nikaamua kuhudumia maandiko ya ‘Ulamaa wetu, waliotangulia katika somo hili. Na nikaanza kuangalia kwa makini katika elimu waliyoiacha, na kuikuta katika kitabu bora kabisa; ‘Atw-twib An-Nabawiy’ (Tiba ya Nabiy)  cha Imaam  Ar-Rabbaany Shaykh Al-Islaam wa pili Ibn Al-Qayyim Al-Jawziyah (Rahimahu Allaah) ameng’ara katika misamiati ya Tiba ya Nabiy na kuitetea, na kuwajibu walioikana na kuipinga au kuona haina umuhimu mkubwa, kwa namna isiyo na kifani katika historia ya mwana Aadam, nikaanza kuiboresha na kuirekebisha na kuzihusisha mada zake nyingi na elimu ya “Tiba ya Kisasa” kwani pamoja na fadhila za Imaam Ibn Al-Qayyim Al-Jawziyah kama niliyotangulia kubainisha na pamoja na jitihada zake zote, alikuwa hakuvuka maarifa ya Tiba ya zama zake, ambapo tutaanzia hapo na kuendelea, na tutafanya marejeo kwake, na kinachojulikana haswa ni kuwa: Elimu hizi za Tiba hazina uwezo wa kuhifadhika kwa Tiba ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  wala ulinzi wake!

 

Hivyo basi hapana budi kusoma upya Milango ya Tiba za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam); usomaji unaotegemea taarifa za kitaalamu za kisasa ili kuweza kuelewa vema Tiba na maana yake mbali mbali, malengo, na kupangilia kwa utaratibu kutokea hatua ya awali hadi tamati yake. Lakini kwa kuchunga kiini na maneno aliyotumia Imaam Ar-Rabbaaniy pamoja na nususi za ki-Tiba za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ikawa kwa tawfiyq ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na fadhila zake. Ni chuo cha Tiba, na mambo ya kujivunia kisayansi ya Tiba na taaluma ya madawa ya Kinabii.

 

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa Majina Yake Mazuri na Sifa Zake Zilotukuka anitakabalie kwa kuinusuru Dini Yake, na kwa kuhudumia Sunnah ya Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuwanusuru ndugu zangu Waislamu, aniwekee akiba thawabu ya amali yote hii hadi siku ya kukutana Naye, siku mali haitafaa kitu wala watoto ila atakayemjia Allaah kwa moyo salama.

 

 

Mwandishi:

Saliym bin ‘Iyd El–Hilaaly Al-Athariy As-Salafy – Abuu Usaamah.

Asubuhi siku ya Jumamosi Tarehe 11 Rabiy’ul-Aakhir 1423 A.H.  ‘Ammaan, Al-Balqaa ‘Aaswimat Jundul-Jordan min Bilaad Ash-Shaam Al-Mahruwsah.

 

 

 

 

 

 

[1] Yaani: Wana Aadam wanafuatana baadhi yao kwa wao ardhini; kama ilivyo katika kauli ya Allaah (Ta’alaa):

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ الْأَرْضِ  

Naye (Allaah) Ndiye Aliyekufanyeni makhalifa wa duniani [Al-An’aam: 165]

 

Na kauli Yake:

ثُمَّ جَعَلْنَاكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ مِن بَعْدِهِمْ لِنَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ﴿١٤﴾

Kisha Tukakufanyeni warithi katika ardhi baada yao, ili Tutazame vipi mtatenda. [Yuwnus: 14]

 

Na kauli Yake:

أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ  

Au nani Anayemuitika mwenye dhiki mno anapomwomba, na Akamuondoshea ouvu na Akakufanyeni makhalifa wa ardhi?  [An-Naml: 62]

 

 

Wametofautiana katika ukweli wa msemo: “Mwana Aadam ni ni khalifa wa Allaah katika ardhi yake” kwa rai tatu: Wengine wamejuzisha, wamekataa na tafsili. Na kilicho sahihi kwangu: ni kile alichokichagua Imaam Ibn Qayyim Al-Jawziyyah (Rahimahu Allaah) katika ‘Miftah Daar As-Sa’aadah’ (1/472): “Nimesema: Kilichokusudiwa ni ziada kwa Allaah: Yeye ni khalifa Wake; na sahihi ni: Kauli ya waliokataa. Na kama imekusudiwa ni idhwaafah kuwa: Allaah kuwa Amemwakilisha (khalifa) kuliko wengine waliokuwa kabla yake; hili halikatazi ziada, na ukweli wake: Khalifa wa Allaah ambaye amemjaalia mwakilishi kwa wengine.”

 

[2] Alikuwa ni shangazi yake na shangazi anachukua nafasi ya mama, na anakuwa vile vile kuwa ni mama yake kwani mke wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa watu ni mama zao “Na wake zake ni mama zao” [Al-Ahzaab: 6]

 

[3] Kulidekeza jina au utukuzo wa jina Urwah.

Share

001-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Ufafanuzi

 

Swahiyh Twibbin-Nabawiy

 

001-Ufafanuzi

 

 

Kitabu cha “Atw-twib An-Nabawiy” ni baadhi ya sura zinazotokana na kitabu: ‘Zaad Al-Ma’ad Fiy Hady Khayril–‘Ibaad.’ cha Al-Imaam Al-Rabbaaniy Shaykh Al-Islaam Ath-Thaaniy Abi Abdillaah  Muhammad bin Abiy Bakr bin Ayyuwb bin Sa’ad Az-Zar’iyy aliyefariki mwaka (751 A.H. = 1350 AD).

 

 

Na mtu wa kwanza aliyechapa kitabu hiki ni Shaykh wa ma-Shaykh zetu[1] Al-‘Allaamah Muhammad Raaghib Atw-Twabaakh (Rahimahu Allaah), mwanazuoni wa Hadiyth na Taariykh wa mji Mtukufu wa Halab (Alepo) amefariki mwaka (1370 AH=1950 AD).

 

 

Katika aliyoyasema katika utangulizi wake: “Katika utafiti wangu kuhusu mabaki ya maandiko yenye thamani kubwa katika maktaba za mji wa Halab nimepata katika maktaba ya shule ya Al-Halawiyah kitabu cha zamani sana kimeandikwa tangu karne ya nane au ya tisa, kimeandikwa jina, ‘Kitaab Atw-Twibb An-Nabawiy’ cha Shaykh Al-Imaam Al-‘Aalim Al-‘Allaamah Abuu Abdillaah Muhammad bin Abiy Bakr bin Ayuwb maarufu kwa jina la: Ibn Qayyim Al-Jawziyyah ambaye amefariki mwaka mia saba na hamsini na moja (751).

 

 

Nilipofungua kitabu; nikakumbuka kuwa sura zake amezitaja mtunzi wa kitabu ndani ya kitabu chake: ‘Zaad Al-Ma’aad fiy Hadyi Khayril-‘Ibaad’ kilichochapwa nchini Misri mwaka 1324 AH katika vitabu viwili vikubwa.  Nilipolinganisha kati ya maandiko mawili sikuona tofauti katika juzuu ya pili nimekuta ndiyo yenyewe kabisa bila ziada au upungufu. Ikadhihirika wazi kuwa, baadhi ya watu walitoa sura hizo kwenye kitabu hiki na kuziweka kwenye kitabu pekee, kwani hakuna maelezo ya kitabu hicho katika wasifu wa mtunzi, kadhalika hakumtaja mtunzi wa kitabu ‘Kashf Adhwunuwn’. Katika maelezo yake juu ya elimu ya Tiba ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

   

Vitabu vya ki-Tiba vya Ibn Al-Qayyim ni:-

 

 

1. “Sharh Al-Arba’iyn Atw-Twibiyyah Al-Mustakhrajah min Sunan Ibn Maajah” cha Abdul-Latwiyf Al-Baghdady.

 

 

2. “Al-Ahkhaam An-Nabawiyyah fiy Asw-Swinaa’at Atw-Twibiyya” cha Al-Kahhaal Ibn Twarkhaan.

 

Imaam Ibn Al-Qayyim Al-Jawziyyah (Rahimahu Allaah) hakuvielezea hivyo ila haijifichi kwa mtu atakayechunguza kwa makini na kufanya malinganisho.

 

 

Kitabu cha Tiba “Atw-Twibb” kina pambanuka kwa yafuatayo:-

 

a. Kina maudhui zinazofanana, na wakati kwengine zinatofautiana.

 

b. Kuachwa yasiyohusiana na Tiba ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

c. Kuachwa kwa makusudi njia za kutibu zisizogongana na ‘Aqiydah ya Tawhiyd kwa mtazamo wa Salaf As-Swaalih.

 

d. Kitabu kinasifika na uslubu wa uandishi wenye kuvutia.

 

e. Tafiti nyingi zimeongezwa ambazo hazikuwemo kwenye kitabu kilichotangulia.

 

 

Kukosolewa Kwa Kitabu Atw-Twibb An-Nabawiy:

 

a. Kwamba Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah) hakuonesha rejea zake za ki-elimu na vyanzo vyake vya ki-Tiba, pengine udhuru wake ni kuwa maarifa haya yamezagaa katika vitabu vya Tiba.

 

 

b. Kuwepo kwa Hadiyth dhaifu bali hata mawdhwuw’ah pasina kuelezea daraja zake. Hivyo ameweza kuzitegemea katika Milango ya kitabu na kujengea hukumu mfano: ‘Mlango kuhusu mwongozo wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  katika kutibu Al-Khudraan’  na  ‘Mlango katika mwongozo wake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kutibu maradhi ya kuungua moto na kuuzima’.

 

 

Nilichofanya katika kitabu:-

 

a. Nimeondosha zile Hadiyth Mawdhwuw’ah na Dhwa’iy  na Milango yote na zile hukumu zilizojengewa kwa msingi wa Hadiyth hizo

 

 

b. Nikiona Hadiyth Swahiyh inaziba nafasi ya Mlango unastahiki kuondolewa, hapo nabakiza Mlango huo kama ulivyo, na kufuta kilicho dhaifu na badala yake naweka kilicho Swahiyh.

 

 

c. Ikiwa taarifa za ki-Tiba hazina uhusiano wa moja kwa moja na Hadiyth Dhwa’iyf, ninaziandika. Kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokea na kukubali yale waliyomsimulia Waarabu kwa ujumla, kama ilivyopokewa kwenye Athar ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa)  iliyotangulia.

 

 

d. Hadiyth zilizothibiti nimezifanyia uchambuzi mwepesi (Takhriyj) nimerejea vitabu vya Imaam Al-Muhaddith Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah), kwani watu wanaokuja baada yake ni wahitaji kwake katika fani hii.

 

 

e. Nimezielezea istilhai mbali mbali za kielimu na kubainisha maana zake.

 

 

f. Nimehusisha mas-ala yake na maarifa ya Tiba ya kisasa. Na kila maelezo ya kitabibu yanayoishia na (ع) ni ya Dr. ‘Aadil Al-Azhariy na kila maelezo yanaoishia na  (ق)basi hayo ni ya Al-Ustaadh Abdul-Ghaniyy Abdil-Khaaliq.

 

 

g.  Nimefanya faharisi zinazomwongoza msomaji kufanya marejeo kwa wepesi.

 

 

h. Nimebainisha umuhimu wa Tiba katika Uislamu na nimewajibu wale waliokosoa ‘Tiba ya Nabiy’ na kuihusisha kuwa katika daraja la Tiba ya ki mwana Aadam inayoweza kusibu na kukosea.

 

 

Hili ndilo ambalo nimeweza kulifanya, Allaah Ndiye Mwenye kufanikisha Naye Ndiye Mwenye kuongoza.

 

 

 

[1]Mwanazuoni mwanahistoria Raaghib At-Twabaakh (Allaah Amrehemu) kukutana na Shaykh wetu Al-Imaam Al-Albaaniy (Allaah Amrehemu) pindi aliposikia shughuli zake za Da’wah katika Kitaab na Sunnah na kupenda kwake elimu ya Hadiyth (hilo lilikuwa kwa wasita wa Ustaadh Muhammad Al-Mubaarak, hivyo akamhusisha kwa ijaazah yake na yaliyopokelewa kutoka kwake kama ni tuzo kwake na kutambua elimu yake na akafanya utangulizi wa kitabu chake: ‘Al-Anwaar Al-Jaliyyah fiy Mukhtasar Al-Athbaat Al-Halbiya’ ambayo amehitimisha kwa ijaazah ya ma- Shaykh  wake kwake.

 

Share

002-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Mfumo Wa Afya Katika Uislamu Athari Yake Kuhifadhi Nafsi Na Jamii

 

Swahiyh Twibbin-Nabawiy

 

002-Mfumo Wa Afya Katika Uislamu Na Athari Yake

Katika Kuhifadhi Nafsi Ya Mwana Aadam Na Jamii

 

 

 

 

Mafunzo ya kiafya yana kazi kubwa katika kulinda siha ya mtu mmoja mmoja na jamii. Ifuatayo ni baadhi ya mifano kwa ufupi:-

 

1. Binaadamu ni muungano kwa mwili na roho, na kila moja kina nguzo zake; nguzo za mwili ni chakula, vinywaji, makazi, mavazi, na matamanio ya kimaada ya kihisia.

 

Uislamu umeshughulikia mahitaji na maumbile kwa kuyaweka vema na kunyoosha ili kulinda siha ya mwili na kutimizia haki zake, katika hayo ni kama ifuatavyo:

 

a. Uislamu umeamrisha usafi wa mwili ikiwemo kutawadha, kunawa, kuosha au kuoga, kwa sababu nyingi, baadhi ni wajibu na sehemu zingine ni mustahab.

 

 

b. Uislamu umehimiza kuosha mikono baada ya kuamka, na kabla ya kuiweka kwenye vyombo.

 

c. Uislamu umehimiza usafi wa kichwa, nywele na viungo vyote.

 

d. Uislamu umefundisha usaji wa nyumba na viwanja vyake.

 

e. Uislamu umehadharisha uchafuzi wa maji, kama maji ya kisima na mito.

 

f. Uislamuu umefundisha unadhifu wa vyakula na vinywaji kwa kufunika vyombo kwa kutunza visichafuliwe kwa vumbi, nzi, au sumu.

 

g. Kadhalika Uislamu umekataza kutaabisha mwili kupita kiasi hata katika ‘ibaadah. Kwa mfano Uislamu umekataza kufunga mfululizo siku zote au kusimama usiku kucha kuswali.

 

h. Uislamu umebainisha tabia za maumbile na kuwahimiza Waislamu kusimamia tabia hizo na kuzifanya kuwa ni ‘ibaadah.

 

Kwa hiyo ni wazi kuwa:

 

Uislamu unatimiza nguvu za kiwiliwili na kuleta afya njema kwa mtazamo wa kisasa.

 

Kwa kuongezea kutilia mkazo Uislamu kwenye afya ya miili, kupendeza kwake na uzuri wake. Kwa sababu hiyo Uislamu umekataza kuhatarisha mwili katika hali za kuudhoofisha na kwa ajili hiyo umeweka shariy’ah za ruhusa za ki-shariy’ah ili mtu aweze kutekeleza wajibu wake wa ki-‘ibaadah katika hali za udhaifu unao tokezea katika mwili – kati ya hali hizo ni:-

 

a. Msafiri ameruhusiwa kadhalika mgonjwa, mama anayenyonyesha, mjamzito na kikongwe, hao wote wameruhusiwa kula mchana katika mwezi wa Ramadhwaan.

 

b. Uislamu umemharamishia Swawm mwenye hedhi kwani, Swawm  katika hali hiyo inaambatana na kudhoofu kwa mwili na damu ya mwenye hedhi hupungua kwa hali aliyonayo.

 

c. Kumuwekea vizuizi mtu anayekwenda Hijjah au ‘Umrah ambaye anaweza kupatwa na taabu na kwa ajili hiyo hupewa nafasi ya kuleta fidia, kufunga au kutoa swadaqah  au kuchinja.

 

d. Na katika hali ya kuwa maji yanaweza kumletea madhara mtu katika kiwiliwili cheke Uislamu umehalalisha kutayammam.

 

 

2. Kinga ya maradhi na kupambana na majanga:

 

a. Uislamu umefungamanisha baadhi ya ‘ibaadah na udhuu au kuoga kwa mfano Swalaah haiswihi bila udhuu au kukoga; na hapana shaka kudumu na udhuu kunapelekea kuwa na mwili msafi, hilo linaulinda mwili kutokana na maradhi.

 

b. Uislamu umeamuru kumtenganisha mgonjwa mwenye maradhi ya kuambukiza ili kuweza kuzuia maradhi hayo kuenea.

 

c. Uislamu umeelekeza kuweka karantini ya kiafya, ikizuka tauni au magonjwa kama hayo kama kipindupindu au ndui hakuna kutoka wala kuingia kwenye eneo lililowekewa karantini.

 

d. Uislamu umeamrisha mtu kujitibu kutokana na maradhi.

 

 

3. Elimu ya Vyakula.

 

Uislamu umetilia mkazo mambo ya lishe kwa namna mbalimbali:

 

a. Kubainisha vyakula haraam. Navyo ni mzoga, damu, nyama ya nguruwe na kila kimojawapo kati ya hivyo vilivyo haramishwa, kuna hekima kubwa ya kitaaluma katika kuviharamisha. Mwenye chembe ya akili hawezi kubisha juu ya hili.

 

b. Uislamu umeharamisha pombe, chache na nyingi, kwani ina madhara ya kiafya, akili, tabia, na jamii. Pombe ndio mama wa mambo maovu. Kinachofuata baada ya pombe ni madawa yote ya kulevya ambayo yanaondosha akili, mfano wa Bangi, Opium (Afyun), au yanayodhuru mwili, kama sigara.

 

Mtu akiona maradhi yanayowasumbua watu wa Magharibi, yanayoharibu viwiliwili vyao, maradhi yanayosababishwa na sigara na madawa ya kulevya, hapo atagundua kwa nini Uislamu uliharamisha uraibu huo mbaya.

 

 

c. Kubainisha vyakula halali:-

 

Uislamu haujaharamisha kitu ila kile kilicho na madhara na kwa ajili hiyo Uislamu umeshajiisha kula vyakula vyenye kuleta faida kwenye mwili, na kupinga dini ya matumizi ya mboga mboga peke yake inayokataza kula nyama kama ni ‘ibaadah kwao. Hilo ni kubainisha kuwa kiwiliwili cha mwana Aadam hakiwezi kuishi kwa mboga mboga peke yake; kwani utumbo wa mwana Aadam ni mfupi kuliko utumbo wa wanyama wanaokula majani na nyasi; kwani mwana Aadam hawezi kuchukua kiasi kinachowatosha cha protini kwa njia ya chakula. Uislamu pia umeshajiisha kutumia vyakula vilivyosheheni dawa na vyenye ponyo kama vile asali na maziwa.

 

d. Uislamu umepangilia chakula kiasi na wakati.

 

e. Uislamu umefundisha uharamu wa kufuja chakula na kunywa, na kuweka wazi kuwa hakuna chombo kibaya alichokijaza mwana Aadam kuliko kujaza tumbo lake.

 

f. Uislamu umeweka uhusiano kati ya chakula, vinywaji na hewa, kama ni lazima basi kila sehemu iwe theluthi moja.

 

g. Uislamu umefaradhisha mfumo wa ajabu wa Swawm kila mwaka mwezi mmoja. Nao ni mwezi wa Ramadhwaan, na kuhimiza mfumo wa kujitolea kufunga kwa hiari siku tatu kila mwezi nazo ni Ayyaamul-Biydhw (Masiku Meupe). Na siku mbili kwa wiki, nazo ni Jumatatu na Alkhamiys. Na hakuna yeyote anayebisha faida za Swawm  kiafya ya mwili, akili na nafsi.

 

 

4. Uislamu haukuacha kutatua mambo ya kujamiiana, yawe madogo au makubwa isipokuwa utaona Uislamu umeweka mpango thabiti na ufumbuzi makini:

 

a. Uislamu umetilia mkazo malezi ya kijinsia kwa namna bora kabisa: Uislamu unachambua mahusiano ya mwana Aadam na tendo la kujamiiana, namna mtoto anavyoumbwa katika tumbo la mamake ambapo Qudra ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) inadhihirika.

 

 

b. Uislamu umetilia mkazo ndoa na kujenga familia na kupangilia mahusiano yaliyopo kati ya mume na mke, watoto katika mazingira ya kuwa pamoja na kutengana.

 

c. Uislamu umesherehesha mahusiano ya kiafya yalio salama kati ya wanandoa, mume na mke. Na umebainisha namna ya mmoja kumshibisha kingono mwenzake kwa namna bora ya kulinda mahusiano ya kindoa kati ya mume na mke.

 

 

d. Uislamu umeharamisha starehe za haraam, umeharamisha zinaa, ushoga, na kumuendea mke kinyume na maumbile.

 

e. Uislamu umeamrisha kutahiri, ambako ni kukata govi ambalo linaficha uchafu. Tiba imebainisha kuwa, asilimia kubwa ya maradhi ya saratani ya kichwa cha uume hutokana na kubakia na govi bila kufanya tohara.

 

 

f. Uislamu umetilia mkazo usafi wa kijinsia, umeamrisha kuoga janaba, na kustanji baada ya kwenda chooni, na Uislamu umeharamisha kumwingilia mke akiwa kwenye hedhi.

 

 

5. Malezi ya kinafsi:

 

Miongoni mwa matatizo makubwa yanayowasibu watu katika zama hizi ni msongo wa mawazo, tatizo hili ni kubwa zaidi katika nchi zilizoendelea za viwanda, watu wengi huko wanajinyonga na wengi katika wazazi huko wamepatwa na hali ya kuvurugikiwa kwa ghafla, na hivyo kuwapelekea wao kuwauwa watoto na ndugu na familia zao na wengine hukimbilia katika vitulizo, na madawa ya kulaza usingizi, ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kila siku…. na yote haya yanatokana na kile kinachoitwa kuwa ni ‘msongo wa maendeleo’ na miongoni mwa sababu zake ni:

 

a. Kukosekana misingi ya kiroho na kiitikadi.

 

b. Kukosekana kwa dhamira ya ndani ya kimaadili.

 

c. Kupindukia kwa maisha ya kimaada.

 

d. Kutoweka kwa kuhurumiana, na kusaidiana katika jamii za kiviwanda na kimaada.

 

Mwenye akili yeyote hawezi kutia shaka kuwa matibabu ya kweli ya maradhi kama hayo ni Uislamu kwa sababu jamii ya Kiislamu ndiyo pekee ambayo hushikamana kwa pamoja katika mambo ya kidunia na akhera. Hivyo ndivyo Dini ifaayo kuweza kumaliza matatizo ya kiustaarabu wa kisasa na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

 

 

e. Uislamu unajikita katika msingi ya mapenzi, kusaidiana, usalama na amani, imani na kuhurumiana baina ya viumbe.

 

f. Uislamu hauna mianya ya ufisadi na msongo wa mawazo, kama ulevi, zinaa, kamari, na mihadarati.

 

g. Ni jamii inayokataa mtu kukata tama na kuruhusu mtu kujinyonga na kughadhibika.

 

Kwa mafunzo haya ya Kiislamu yanapotekelezwa vema basi haiwezekani kujitokeza sababu za msongo wa maendeleo ya kisasa ya kimaada.

 

 

6. Mtazamo wa Uislamu kuhusu maradhi na wagonjwa. 

 

Kuchukia maradhi ni jambo la kimaumbile, lakini Uislamu umegeuza jambo hilo kuwa ni jambo chanya:

 

a. Ni mtihani kutoka kwa Allaah lakini moja ya faida yake ni mtu kufutiwa madhambi, kuinua daraja za watu; hivyo basi yatakikana kwa Muumini kupokea maradhi bila kuwa na majonzi wala malalamiko au kuchukia.

 

 

b. Uislamu umemtendea mgonjwa na kumpa haki maalumu zaidi ya Waislamu wengine. Hivyo ukafanya kumzuru mgonjwa ni katika haki za Muislamu kumfanyia mgonjwa Muislamu.

 

c. Kumtakia kupona kwa kumuombea du’aa na kumhimiza kustahamili na kusubiri, ili aweze kuwa imara, na hizi ni hali za kinafsi zinazosaidia kukabiliana na maradhi.

 

d. Uislamu umemtendea mgonjwa kwa namna ya kipekee, hivyo Uislamu umedondosha na umesamehe baadhi ya faradhi kwa mgonjwa mfano, jihadi, na kumpunguzia zingine; kama, Swalaah, Swawm pale ambapo anapata shida kutekeleza faradhi hizo, na afya yake kuharibika zaidi, na kuchelewa kupona.

 

e. Uislamu umetoa ruhusa kwa mgonjwa na msamaha katika baadhi ya Shariy’ah kulingana na dharura itakavyo kuwa, ikahalalisha matumizi ya dhahabu katika Tiba mbadala na imeruhusu mwenye ugonjwa wa kuwashwa avae Hariri.

 

Katika hayo yaliyotangulia inadhihiri kwetu kuwa: Uislamu umetazama siha ya viwiliwili kama hitajio la msingi katika maisha ya watu, hivyo imeiunganisha na mambo ya ‘ibaadah mbali mbali. Hivyo basi Muislamu anatakiwa kutilia mkazo afya yake binafsi, na jamii kwa jumla ili jamii ya Kiislamu ibaki imara, yenye nguvu. Hayo hayawezi kutimia bila ya kupitia mafunzo ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  katika nyanja za ki-Tiba.

 

Ikiwa Waislamu hivi sasa, wanapitia hatua ya kuwa nyuma ki-Tiba, basi hivyo inatokana na wao kuwa kwao mbali na mafunzo ya Tiba ya Kiislamu kwani mara ya kwanza walipotekeleza mafunzo ya Tiba ya Kiislamu yaliweza kuleta matunda ya kupatikana kwa jamii yenye afya safi ya kupigiwa mfano. Wakati ambapo miji ya Ulaya Magharibi imetapakaa majalala na kuzalisha vijidudu na kuparaganywa kwa nguruwe.

 

Dr. Dr. Segrate Hookah amesema kwenye kitabu chake: “Jua la Arabuni lachomoza Ulaya’ kwamba msafiri Al-Tartusy wa Andalusia (Hispania) ameandika katika msafara wake kuelekea Ulaya, akisimulia hali ya wakazi wake huko: “Ndevu zao na nywele zao zimerefuka, hawafui nguo zao, hawakogi isipokuwa mara moja au mara mbili kwa mwaka.”

 

Zingatia pia kukiri kwa Tabibu wa Kiingereza (Bernard Shaw) katika kitabu chake, ‘Kubabaika kwa tabibu’ anaposema:  “Uingereza ilipotawala visiwa vya “Sandisk” vilijitahidi sana katika ukandamizaji na kushawishi watu wa visiwa hivyo na kuwageuza kutoka katika Uislamu na waingie katika Ukristo mpaka Uingereza ikafaulu katika jambo hilo, lakini matokeo yake ilikuwa ni kuenea kwa maradhi hatari, na hilo ni kwa sababu ya wao kuwa mbali na mafunzo ya Dini ya Kiislamu ambayo yanaweka shariy’ah ya kuwa nadhifu katika madogo na makubwa, kiasi cha kufikia kutoa malekezo ya kukata kucha na kusafisha uchafu ndani ya kucha na kufukia uchafu”.

 

Share

003-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Hoja MbaliMbali Kuhusu Mwongozo Wa Nabiy Katika Mambo Ya Kitiba

Swahiyh Twibbin-Nabawiy

 

003-Hoja MbaliMbali Kuhusu Mwongozo

 

Wa Nabiy Katika Mambo Ya Kitiba

 

 

 

 

‘Ulamaa wametofautiana katika maswala haya kwa kauli mbili:

 

 

Kauli ya kwanza: Wapo wanaosema kuwa maneno ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni hoja ya ki-Shariy’ah kwa waja kama itathibiti.

 

 

 Kauli ya Pili: Wapo wanaoona kuwa maelekezo ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni hoja tu katika upande wa Dini; kama kumwamini Allaah na Majina na Sifa Zake, na kuamini Malaika, Vitabu, Rusuli Wake, na Siku ya Mwisho, na zile Hadiyth zinazofafanua hukumu za halaal na haraam, faradhi na namna ya kuekeleza ‘ibaadah mbali mbali, na miamala mbali mbali na mambo mengine katika jumla ya mambo ya ki-Dini na ki-Shariy’ah.

 

 

Ama mambo ya kidunia; sio lazima kuwa kauli zake zilingane na hakika; kwani hakuna uhusiano wa mambo kama hayo na hadhi ya Unabii. Bali huenda ikatokea pia kukosewa kwa rai kuhusu hayo, kiasi kidogo au kingi, bali anaweza akasibu mtu mwingine asiyekuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye akakosea katika mambo kama hayo ya kidunia.

 

 

Na katika madai yao wamesema vile vile: Kuwa kusema hivi hakushushi hadhi au cheo cha Unabii ambacho Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alimkirimu, kwani cheo hicho kipo katika eneo la elimu ya mambo ya ki-Dini.

 

 

Ibn Khalduwn (Rahimahu Allaah) amesema katika kitabu chake kiitwacho ‘Al-Muqaddimah’ (Uk. 493): “Tiba iliyopokelewa katika mambo ya ki-Shariy’ah yapo katika mkabala huu (tiba ya ki-mila au ya kizamani na kutoka kwa mabedui yenye uzoefu mdogo), na hayamo kamwe katika Wahyi bali yalikuwa ni mambo yakifahamika na ada kwa Waarabu. Na imetokea kutajwa hali za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika hali zake ambazo ni tabia na silka na sio kwa sababu kuwa hilo limo kwenye Shariy’ah kulitimiza hivyo. Kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitumwa ila aje kutufundisha mambo ya ki-Shariy’ah na hakuja kwa ajili ya kufundisha tiba au mengine katika mambo ya kawaida. Na yaliyotokea katika habari ya kilimo cha mtende na akasema, “Ninyi ndiyo wajuzi zaidi wa mambo ya dunia yenu”.

 

 

Hivyo haipaswi kuchukulia kwamba tiba iliyonakiliwa kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka Hadiyth zake kuwa ndio Shariy’ah, kwani hakuna ushahidi wa hilo, isipokuwa ikiwa itatumika kwa namna ya kutabaruku na ukweli wa makusudio ya ki-iymaan. Hivyo patatokea manufaa makubwa na sio katika tiba ya hali ya kawaida.”

 

 

Al-Qaadhwiy ‘Iyaadhw amesema katika kitabu chake: “Ash-Shifaa Bita’riyf Huquwqil-Mustwafaa.” (2/183-185):

 

 

Faswl: “Ama hali zake katika mambo ya kidunia; sisi tunayaweka katika namna iliyotangulia, itikadi, kauli, na kitendo; ama kiitikadi ni, mtu anaweza kuwa anayaelewa mambo ya kidunia kwa upande mmoja lakini kikadhihiri kingine tofauti. Au akawa ana shaka ya jambo lenyewe au akadhania tofauti na mambo ya ki-Shariy’ah (kisha akataja Hadiyth ya mtende) na haya ndiyo tuliyothibitisha katika aliyoelezea kwa nafsi yake katika mambo ya kidunia na kudhani kwake katika hali zake na siyo kwa upande wa jitihada zake katika Shariy’ah au Sunnah alizoziweka mambo haya na mengine kama hayo ni katika mambo ya dunia yasio na uhusiano na elimu ya Dini wala itikadi yake au mafundisho yake kama yanajuzu kwa yale tuliyoyataja. Kwa haya hayapunguzi hadhi yake, haya ni mambo ya kimazowea mtu aliyefanya majaribio anayajua na kuweza kutilia hima na kuyashughulikia.”

 

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amejawa na mambo ya elimu za Ar-Rubuwbiyyah (Uola) na amesheheni elimu za Shariy’ah. Akili yake inazingatia maslahi ya ummah ya kidini na ya kidunia, lakini hii ni kwa baadhi ya mambo tu na inajuzu kwa mambo yaliyo nadra ambayo ili uweze kuyafikia ni kufanya ufuatiliaji wa makini katika kulinda dunia na kufanya uzalishaji na kuwekeza, sio katika mengi yanayoruhusu upuuzi wa kughafilika.

 

 

Imepokewa kwa wingi kwa njia ya ‘Tawaatur’ kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika ujuzi wa mambo ya dunia na undani wa maslahi yake ya kidunia na ya kisiasa ya makundi ya watu wake kwa namna ambayo ni muujiza kwa wana Aadam kama ilivyotanabahishwa kwetu kwenye mlango wa miujiza yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye kitabu hiki.”

Wote wanaokuja baada ya kauli hizo mbili huwa wanarudia kitu hicho hicho, na sio nje ya hayo waliyosema.

 

 

Yafuatayo ni majibu ya kauli hizo:

 

 

1. Tiba ya Nabiy inatokana na Wahyi na chimbuko la Unabiy na upevu wa akili, miongoni mwa hoja za mlango huu.

 

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾

Na wala hatamki kwa hawaa.

 

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa.

 

عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ ﴿٥﴾

Amemfunza (Jibriyl) mwenye nguvu shadidi. [An-Najm: 3-5]

 

 

Kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾

Na wala hatamki kwa hawaa. [An-Najm: 3]

 

 

Kwa mujibu wa lugha ni kila linalotokea kwenye kinywa cha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) miongoni mwa kauli. Ziwe ni kauli zote zinazohusiana na mambo ya Dini au kidunia, vyote hivyo ni Wahyi kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hakuna nafasi ya kukosea, au kuteleza kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 4]

 

 

Haya ndio madhhab ya watu wa Hadiyth.  Kwa mfano kwenye Swahiyh Al-Bukhaariy: ‘Baab As-Su’uwtw’, ‘Baab Ayyu Saa’ah Yuhtajam’, ‘Baab Al-Hijamah fis-Safar’, ‘Baab Al-Hijaamah Minash-Shaqiyqah wasw-Swudaa’ah’,   

 

 

Hii yote ni milango ya tiba na katika “As-Sunan” Utakuta sura mahsusi za tiba.

 

 

2. Ijtihaad ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) sio sawa na Ijtihaad ya wengine miongoni mwa Wanazuoni kwa sababu hakiri kufanyike kosa kamwe iwe kosa hilo ni katika mambo ya kidini au kidunia.

 

 

Huenda mtu atasema: Kwa kuwa Sunnah ni Wahy kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) basi inapingana na kusema kuwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni mujtahid, kwa mujibu wa wale wanaosema hivyo.

 

 

Jibu: Mas-ala ya Ijtihaad ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni mas-ala ya kiusuli yenye khilafu ndani yake. Lakini wanazuoni wengi wa elimu ya kiusuli wameshika kauli ya kwamba inajuzu kutokea ijtihaad kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kiakili na ki-Shariy’ah.[1]

 

 

Hapana kinachozuia kutokea hilo isipokuwa kwa uelewa wa watu wasiweze kufahamu haki, wameshindwa kuunganisha taarifa za ki-Shariy’ah zilizo sahihi. Kwani katika mas-ala haya kuna fumbo, wanaweza kulifungua waliozama kupekua katika fani hii nayo ni:

 

 

1. Ijtihaad yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inashika nafasi ya Wahy.

 

 

2. Ijtihaad yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) si sawa na ya mtu mwingine.

 

 

Al-‘Allaamah Ash-Shawkaaniy (Rahimahu Allaah) amesema katika “Irshaad Al-Fuhuwl” (uk 256) akijibu kauli ya waliosema kuwa: “Katika Ijtihaad kuna kusibu na kukosea.” Akajibu (Rahimahu Allaah): “Imekwishajibiwa suala hilo kwamba Ijtihaad yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) haihukumiwi sawa na Ijtihaad na mtu mwingine. Kwa mtu mwingine hayo ni sawa, kwani sio lazima kwake kumfuata.

 

 

Na akasema Al-‘Allaamah i bin Sultwaan Muhammad Al-Qaariy  katika ‘Mirqaat Al-Mafaatiyh Sharh Mishkaat Al-Maswaabiyh’  (1/237). “Kisha aliyesema kuwa (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) (Swala Allahu ‘Alayhi Wasallam) alikuwa mujtahid, Ijtihaad yake inachukua daraja ya Wahy, kwani hakosei, na akikosea husahihishwa na hii hali haipo kwa yeyote asiyekuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Na kabla ya wanazuoni hao wawili Al-Imaam Ash-Shaatwibiy amehakiki mas-ala haya kwa kina na kudhibiti vema akasema (Rahimahu Allaah) katika kitabu ‘Al-Muwafaqaat’ (4/21): “Kwani Hadiyth ima ni Wahyi kutoka Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) au ni Ijtihaad ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inazingatiwa kuwa inatokana na kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Sunnah zake. Na katika makadirio yote hayo ya aina mbili ni muhali kuwepo kwa mgongano na kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hazungumzi kwa matamanio ya nafsi yake, bali ni Wahyi anaoshushiwa, ikiwa itasemwa kuwa (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anaweza kukosea, basi kosa hilo kamwe hatalikiri, lazima atarejea katika njia yenye kusibu.”

 

 

Kauli yangu (mwandishi) Hii ndio kweli, na sahihi, kwani matukio sahihi yanathibitisha hili na udhibiti huu madhubuti. Jitihada za Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zilipatikana kama katika mateka wa vita vya Badri na katika kumpuuza kipofu, ‘Amru bn Ummi Makhtuwm (Radhwiya Allaahu 'anhu) na kuwapa ruhusa waliobaki nyumbani wasiende vitani. Basi ni haraka sana Wahy unashuka kumsahihisha na kumuonesha haki na kuwaongoza wafuasi wake.

 

 

Kwa hiyo khilafu kati ya pande mbili hizi ni ya lafudhi tu; kwani matokeo yake ni mamoja kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakiri yaani hadumu katika kufanya kosa, kwani yeye ameridhiwa kutokosea, yaani hatulii na kosa na hapitishi muda katika kosa. Kwa sababu anahifadhiwa na maasi. Hivyo ndivyo inayokuwa mambo ya Sunnah kama alivyosema Ash-Shaatwiby katika “Al-Muwafaqaat” (4/80) kuwa: “Yote aliyoyaeleza Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yapo kama alivyoeleza, ni kweli tupu. Kauli zake pia zilizoelezwa kuhusu yeye ni za kutegemewa iwe zina msingi wa kiutekelezaji wa Shariy’ah au hapana, kadhalika ikiwa akiweka hukumu ya Shariy’ah, ameamrisha, au kukataza basi huwa kama alivyosema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni sawa kati ya haya ikiwa ameelezwa na Malaika kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na yaliyopenyezwa moyoni mwake au njozi alizoziota ni kumulika mambo yaliyojificha kwa namna inayovunja kanuni za kawaida ni muujiza, au vyovyote iwavyo, vyote hivyo vitazingatiwa na kuwekewa msingi katika itikadi na matendo yote kwa sababu Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anaungwa mkono na sifa ya  “Iswmah” kuwa na hatamki kwa matashi ya nafsi yake.”

 

 

Kauli yangu: Katika masuala ya kuoanisha mitende kunajibu linaloleta mwanga basi usahihi wake ni huu:

 

 

Imaam Muslim, (15/116 Nawawiy) Ibn Maajah (2470) na Ahmad (1/162) kutoka kwa As-Simaak: Kwamba amemsikia Muwsaa bin Twalhah Ibn ‘Ubaydillaah akihadithia kutoka kwa Baba yake akisema: Nimepita pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa watu wakiwa juu ya mitende akasema: “Hawa wanafanya nini?” wakasema: “Wanaoanisha (wanaunganisha) dume na jike basi inazaa”. Akasema: “Sidhani kama inafaa kitu kufanya hivyo” Wakaeleza hivyo, wakaacha, akaelezwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hivyo akasema: “Ikiwa inawafaa, basi na wafanye, kwani mimi hakika nilidhani, msinichukulie kwa dhana, lakini nikiwahadithieni jambo kutoka kwa Allaah lichukueni, kwani mimi sitomsingizia urongo Allaah (‘Azza wa Jalla).”

 

 

Na imepokewa na Muslim (15/117) kutoka katika Hadiyth ya Raafi’ bin Khudayj amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia Madiynah wakiwa wanaunganisha mitende dume na jike. Na wanasema wanaweka uzazi katika tende, akawauliza kwa kusema: “Mnafanya nini?” Wakasema: “Tulikuwa tukifanya hivi mazowea yetu.” Akasema: “Msingefanya hivyo huenda ingekuwa bora.” Wakaacha ikapungua (kuzaa). Akasema: Wakaeleza hilo kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: “Hakika mimi ni mtu, nikikuamrisheni jambo katika Dini yenu lichukueni, na nikikwambieni jambo katika maoni yangu basi hakika mimi ni mtu.”

 

 

Ikrimah akasema: Au mfano wa hivi. Amesema Al-Ma’qiriy[2] “Yakapungua kuzaa hakutia shaka[3]

 

 

Imepokewa na Muslim (15/117 Nawawiy), Ibn Maajah (2471) na Ahmad (6/123) kutoka kwa Hammad kuwa Thaabit ametuhadithia kutoka kwa Maalik Ibn Anas na Hishaam Ibn ‘Urwah kutoka kwa baba yake kutoka kwa ‘Aaishah; kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amepita kwa watu wakiunganisha mitende dume na jike akasema: “Msingefanya, ingefaa.” Akatoka akawapitia akasema: “Mitende yenu ina hali gani.” Wakasema: “Ulisema hivi.” Akasema: “Ninyi ni wajuzi zaidi wa mambo ya dunia yenu.”

 

Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alielezea fikra yake na pia dhana yake, hivyo ndivyo ilivyokuwa kama ilivyobainishwa na riwaayah zilizo Swahiyh; hivyo basi taarifa hiyo sio katika mlango wa Ijtihaad yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo anaiona kuwa ni Shariy’ah ikiwa hivyo inapasa kuitimiza kwa kuifanyia kazi, hakuthibitisha kosa.

 

 

Imaam An-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema katika, “Sharh–Swahiyh Muslim: (15/116-117): “Wanazuoni wamesema kuhusu kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Katika maoni yangu” yaani: Katika mambo ya dunia na maisha yake na sio katika Shariy’ah. Ama aliyoyasema kwa Ijtihaad yake, na akayaona kuwa ni Shariy’ah hayo yanapasa kutendewa kazi na sio kuunganisha mitende katika fungu hilo bali ni katika aina ya yale yaliyotajwa kabla huko nyuma pamoja na kuwa lafudhi ya “Ar-Ra-yi” ameitamka Ikrimah katika maana, kwa kuwa alisema mwishoni mwa Hadiyth. Amesema Ikrimah: ‘Au maneno kama haya’, hakueleza tamko la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa hakika.

 

 

‘Ulamaa wamesema: Kauli hii haikuwa khabari bali ni dhana kama alivyoibainisha katika riwaayah hizi.

 

 

Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyah amesema katika Majmuw’ Al-Fataawa (18-12): “….yeye hakuwakataza kupandiliza uzazi wa mitende lakini wao walikosea katika dhana yao kuwa aliwakataza; kama alivyokosea aliyekosea kudhania kuwa uzi mweupe na uzi mweusi ni ile kamba nyeupe na nyeusi”.

 

 

3. Tiba ni katika matendo ya watu mukallafiyna (wenye kubebeshwa amri na makatazo ya Dini) ama Shariy’ah safi imekuja kudhibiti matendo ya mukallafiyna na kuyahukumu kwa kubainisha aliyowajibisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Shariy’ah na aliyoyakataza na anayopendelewa na yanayochukiwa au yanayojuzishwa kufanywa na hizi ndizo hukumu tano za Takliyf; matendo yote ya watu mukallafiyna hayatoki nje ya mambo hayo matano.

 

 

Kwa sababu hiyo zimekuja Hadiyth zinazoamrisha kujitibu, na Hadiyth zinazoelezea baadhi ya madawa, na zingine zinaharamisha fungu lingine n.k.

 

 

4. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameteremsha maradhi na dawa; waliojua wamejua na wasio jua hawakujua, na kuhusu mambo ya dawa yaliomo katika Sunnah ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni katika maelimisho ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ ﴿٥﴾

Amemfunza (Jibriyl) mwenye nguvu shadidi. [an-Najm: 5]

 

Na kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakupata elimu kwa mwengine asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwani wapinga haki wangetia shaka:

 

وَمَا كُنتَ تَتْلُو مِن قَبْلِهِ مِن كِتَابٍ وَلَا تَخُطُّهُ بِيَمِينِكَ ۖ إِذًا لَّارْتَابَ الْمُبْطِلُونَ ﴿٤٨﴾

Na wala hukuwa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ukisoma kabla yake kitabu chochote, na wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume, kwani basi hapo wangetilia shaka wabatilifu. [Al-‘Ankabuwt: 48]

 

 

5. Taarifa za kitaalamu na kitiba zinazokuja katika Sunnah zina dalili za nguvu zilizoungwa mkono na sayansi ya enzi hizi. Na tiba mpya imetilia mkazo na kuweka hoja ya wazi kabisa haina shaka yoyote. Wala haina kificho: kuwa Aliyemfunulia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni Rabb wa walimwengu (Subhaanahu wa Ta'aalaa).    

 

 

6. Zimepokewa Hadiyth zilizokata shauri kuwa Twibbun-Nabawiy ni Wahyi kutoka kwa Allaah; katika Swahiyh Al-Bukhaariy kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Kwamba mtu mmoja alimjia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ndugu yangu analalamika maumivu ya tumbo. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Mnyweshe asali.” Akamjia mara nyingine akamwambia: "Mnyweshe asali.” Kisha akamjia mara ya tatu akamwambia: "Mnyweshe asali.” Kisha akamjia akasema “Nimefanya.” Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Kasema kweli Allaah na tumbo la ndugu yako limeongopa! Mnyweshe asali!” Akamnywesha, akapona.

 

 

Imaam Ibn Al-Qayyim Al-Jawziyyah (Rahimahu Allaah) amesema: “Maelekezo ya dawa hiyo aliyomuelekeza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ni kusafisha tumbo lililojaa, hivyo akamuamuru kunywa asali ili kuondoa mabaki ya vyakula yaliyo jikusanya katika maeneo ya tumbo la chakula na utumbo. Kwa sababu asali hufanya kazi ya kutakasa na kuondosha mabaki ya chakula. Alikuwa ana tatizo la maada zenye kuteleza zinazozuia chakula kutulia tumboni kutokana na hali yake ya utelezi. Tumbo la chakula lina chamvaa kama ya taulo, hivyo basi ikishikamana na vitu vya kuteleza ambavyo vimeganda kwenye tumbo, huliharibu pia na huharibu chakula. Hivyo dawa yake ni kisafisho cha mchanganyo huo, na asali ni katika dawa bora sana ya kutibia maradhi hayo. Na hasa inapochanganywa na maji ya moto.

 

 

Na katika kuendelea kunywa asali kuna maana kubwa nzuri sana, nayo, ni kwamba dawa yoyote inabidi iwe na kiwango kulingana na hali ya ugonjwa wenyewe ulivyo, ikiwa chini ya kiwango haiwezi kutibu kabisa na ikivuka kiasi hudhoofisha nguvu, hapo basi husababisha madhara mengine. Alipomuamrisha kumpa asali alimnywesha kiasi kisichotosha kupambana na ule ugonjwa na wala lengo halikutimia, alipomjulisha akajua alichomnywesha hakikufikia kiwango kinachohitajika na lengo linakuwa halifikiwi. Alipoendelea kurudiarudia kwenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamsisitizia kurejea matumizi ya asali ili ifikie kiasi kinachoweza kupambana na maradhi. Alipokunywa asali tena na tena, kulingana na ugonjwa wake, akapona kwa idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

 

Kuzingatia viwango na aina ya dawa na matibabu yanayotolewa na nguvu ya ugonjwa ni katika misingi mikubwa ya tiba.

 

 

Kauli yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Allaah amesema kweli na tumbo la ndugu yako limeongopa.“ Ni ishara ya uhakika wa kufaa kwa dawa hii, na kwamba ugonjwa uliendelea kuwapo sio kwa dosari ya dawa, lakini kwa uongo wa tumbo na wingi wa maada mbovu ndani mwake, hapo ndipo alipomuamuru kurudia matibabu kulingana na hali ya tatizo lilivyo.

 

Tiba ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) sio sawa na tiba za matabibu wengine. Kwani tiba ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni yakini haina shaka, ni ya ki-Ilaah (Allaah), chanzo chake ni Wahyi na dirisha la Unabii na ukamilifu wa akili.

 

 

Na tiba nyingine sana huwa ni dhana, na kuthibitishwa dhana hizo kwa majaribio, na sio jambo la kukanusha kwamba Twibbun-Nabawiy haifai kwa baadhi ya watu kutonufaika nayo; bali wameweza kunufaika wengi, kwani hunufaika na tiba ya ki-Nabii yule anayeipokea kwa kuikubali na kuamini kuwa ataweza kupona kwa tiba hiyo.

 

Hii Qur-aan mathalan ambayo ni shifaa kwa maradhi ya nyoyo ikiwa haikupokelewa kwa namna inayostahiki kupokelewa, basi nyoyo hazitapona kamwe kwa dawa yake, bali maradhi ya wanafiki yanaongezeka juu ya maradhi yao, na tiba ya miili inaponya wapi? Basi Twibbnu-Nabawiy haiendani na miili isipokuwa iwe mizuri, kama ilivyokuwa tiba ya Qur-aan haiwiani isipokuwa na Roho nzuri safi na nyoyo zilizo hai. Watu kupuuza tiba ya ki-Nabii, ni sawa kwamba wamepuuza tiba ya Qur-aan ambayo ndio tiba yenye kufaa. Hiyo sio kwa sababu ya dosari katika dawa lakini ni kutokana na ubaya wa hali ya mazingira na ufisadi wa mahali, na kutoikubali tiba hiyo. WabiLLaah At-Tawfiyq .”

 

 

7. Kwa hiyo, Imaam Ibn Al-Qayyim Al-Jawaziyyah (Rahimahu Allaah) ameelezea sana kuhusu kadhia hii, na ameweza kuweka hoja madhubuti na kulifafanua kikamilifu. Na baadhi ya hayo aliyosema: - “Basi hizi ni fusuli zenye kufaa katika mwongozo wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika tiba aliyojitibia, na kuielekeza kwa wengine, tunaelezea hekima kubwa zinazohemeza akili za matabibu na kushindwa kuzifikia na mlinganisho wa tiba zao sawa na watu walioshindwa.” [ukurasa wa 35]

 

 

“Nasi tunasema: Kuna jambo lingine hapa. Kuwa mfano wa matabibu bingwa na wanaoshindwa kufikia mfano wao, hili wamekiri matabibu wao bora kabisa wenye ujuzi wa tiba, wapo wanaosema: “Ni majaribio” na wengine wanasema: “Ni il-hamu, njozi, na mabunio yenye kusibu.” Na kati yao wapo wanaosema: “Tiba nyingi zimechukuliwa kwa wanyama.” Kama tunavyoshuhudia paka anapokula wadudu wenye sumu, hukimbilia kwenye taa na kuramba mafuta kujitibia kama nyoka walivyoonekana anapotoka chini ya ardhi, na macho yao yana giza hivyo huelekea majani ya mmea uitwao, Ar-Raaziyanij na kupitisha macho yao kwenye majani hayo. Pia kama ilivyo kwa ndege wanapopatwa na hali ya kutatizika kiafya hujitibu kwa maji ya bahari na mifano ya hayo, mengi yametajwa katika taaluma ya tiba.

 

 

Ni umbali gani wa tiba ya namna hii na ile tiba itokanayo na Wahyi ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anamfunulia Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kumjulisha yanayofaa na yale yenye madhara mlingano wa tiba hizo kwa Wahyi huu, ni sawa na kulinganisha elimu mbali mbali walizokuja nazo Manabii.

 

 

Bali zipo dawa ziponyazo maradhi ambazo madaktari wakubwa wameshindwa kuzigundua. Kadhalika utaalamu wao haukuweza kufikia huko wala majaribio na vipimo vyao havikuweza kugundua. Ni maradhi ya nyoyo, ya kiroho, moyo madhubuti, imani na kutawakali kwa Allaah na kumkimbilia, kujitupa Kwake, kujivunjavunja, mbele yake, kujidhalilisha kabisa, na unyenyekevu wa hali ya juu, moyo wa utayari kutoa, kuomba, kutubia, kuomba maghfirah,  kuwafanyia ihsaan viumbe, kuwasaidia wenye mahitaji, kuwafariji wenye shida; kwani dawa hizi mataifa yamezijaribu, katika dini, mila na desturi zao mbalimbali wakaona dawa hizo zimetia fora kuliko ujuzi wa wataalamu bobezi wa tiba na kuliko hata majaribio na vipimo vyao.

 

 

Kwa kweli sisi tumefanyia majaribio jambo hili, katika mambo mengi. Tukaona linaleta matokeo ambayo dawa za kihisia haziwezi kuyaleta bali tiba hizo huwa sawa na tiba za atw-twarqiyyah (makuhani) mbele ya matabibu. Na jambo hili linakwenda kwa mujibu wa kanuni ya hekima ya ki-Ilaah (Allaah) na halitoki nje ya hapo, lakini sababu ziko tofauti, wakati moyo umeungana na Rabb wa walimwengu, Muumba wa maradhi na dawa, Mwendesha maumbile na kuyageuza Atakavyo, Allaah Ana dawa nyinginezo mbali na ambazo mtu mwenye moyo usioshikamana na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) huteseka. Inajulikana kuwa Roho zinapokuwa na nguvu, na nafsi na maumbile ya mtu yakawa na nguvu, husaidiana kuondosha na kushinda maradhi. Vipi isikubalike kwa mwenye hali na nafsi yenye nguvu, na moyo wake ukajawa na furaha kwa kuwa karibu na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Muumba wake na mtoa maliwazo, na kumpenda, kufurahia kumdhukuru na kuelekeza nguvu zake zote Kwake. Na kuzikusanya na kumtaka Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) msaada Wake. Pia kutawakali Kwake. Hayo kwa ajili hiyo ni dawa kubwa na kuwajibisha pia kuondosha maumivu, moja kwa moja. Hakanushi haya ila mjinga wa watu kupindukia. Asiyeona mbele, mwenye nafsi nzito aliye mbali na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na ukweli wa ki mwana Aadam. Tutataja In Shaa Allaah sababu ya Suwratul Al-Faatihah kuweza kuondosha ugonjwa wa kung’atwa, kwa yule aliyejitibu kwayo baada ya kung’atwa akasimama mzima kabisa” [Uk 41-43].

 

 

“Tutaongeza ufafanuzi wa hili wakati wa kuelezea matibabu kwa njia ya ruqyah na Al-‘Awdh (kinga) ya ki-Nabiy, dhikri na du’aa, na kufanya kheri mbali mbali. Na tutabainisha tiba ya matabibu mbele ya tiba ya ki-Nabiy ni sawa na tiba ya atw-tarqiyyah (makuhani) na wanaoshindwa kwenye tiba zao. Kama wabobezi na viongozi wao walivyokiri hivyo. Tutabainisha kuwa tabia ya mwana Aadam ni yenye kuathirika sana na Roho, na kwamba nguvu za Al-‘Awdh (kujinga), ruqyah na du’aa, ziko juu kuliko nguvu za madawa, hadi kufikia kubadilisha nguvu za sumu kali zenye uwezo wa kuuwa”  [Uk 77].

 

 

“Kwa ujumla: Tiba ya kawaida mbele ya tiba ya ki-Nabiy ni sawa tiba ya atw-twarqiyyah (makuhani) kulinganisha na tiba zao, bali chini ya hapo, na tofauti kati yake na Manabii ni kubwa na kubwa zaidi kuliko tofauti kati yake na atw-twarqiyyah (makuhani) kwa mtu asiyejua kipimo chake, imekudhihirikia mkataba wa udugu uliopo kati ya hikma na shariy’ah, na kuwa kimoja hakigongani na kingine, na Allaah Humhidi Amtakaye  katika lililo sahihi, na humfungulia kwa atakayedumu katika kugonga mlango kumpa taufiki ya kila mlango, na Yeye (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  ni Mwenye neema isiyo na ukomo na hoja yenye umbuji. [uk 238]”

 

 

“Na imetangulia kuwa: Tiba ya matabibu kulingana na tiba ya ki-Nabiy ipo chini kwa kiasi cha tiba ya atw-twarqiyyah (makuhani) na wasioweza kulinganisha na tiba ya Manabii; na ya kuwa kati ya yanayoshushwa katika Wahyi na yale ya majaribio na unaweza kupima tofauti iliyopo ni kubwa.

 

 

Walau kuwa wajinga wale wamepata dawa yenye andiko kutoka kwa baadhi ya Mayahudi na Manaswara na washirikina (miongoni mwa matabibu): ili waipokee kwa kukubali na kujisalimisha kwayo, wala wasisimame katika jaribio lake.

 

 

Naam: Sisi hatupingi kuwa ada, mazoea yana taathira yake katika kumfanya mtu anufaike na dawa au kutonufaika nayo; kwa Yule aliyezoea dawa pamoja na chakula: Basi itamnufaisha zaidi na itamfaa kuliko yule ambaye hajaizoea. Bali huenda hawezi kunufaika nayo yule ambaye hajaizoea.

 

 

Maneno ya madaktari bingwa ingawa katika hali zote bila ya upekee, basi ni kutokana na mazingira na nyakati, na mahali, na ada za watu na ikiwa maneno yao yanalenga hali maalum, maneno yao na ujuzi wao hauna dosari, basi vipi atiwe kasoro mkweli aliyesadikiwa (Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)? Lakini nafsi za wana Aadam zimeundwa kwa ujahili na dhulma, ila kwa yule atakayepata msaada wa Allaah kwa iymaan na kupata nuru ya mwongozo.” [Uk 442].

 

 

“Tumeleta kiasi cha kufaa kabisa katika jumla yenye kunufaisha miongoni mwa sehemu za za tiba ya kielimu na kimatendo, yamkini mtu hawezi kuona kwengine mambo haya ila ndani ya kitabu hiki. Na umekuonesha ukaribu wa tiba hiyo na Shariy’ah. Na kwamba Twibbun-Nabawiy uwiano wa tiba ya matibabu ya utaalamu wa kawaida ni kiwango cha chini kuliko uwiano wa kati yao na wale wanaowashinda.

 

 

Mambo hayo ni zaidi ya ulivyotaja ukubwa wake ni zaidi mno, na kiasi ulichokielezea ni kidogo tu. Na mtu ambaye hajapata busara ya upambanuzi wa mambo, hajaruzukiwa neema ya namna hiyo, waelewe tu, ile tofauti kubwa iliyopo kati ya nguvu inayoungwa mkono na Wahyi kutoka kwa Allaah, tofauti kabisa na elimu ya watu wasiokuwa Manabii.

 

 

Huenda msemaji akasema tu: “Kuna uhusiano gani wa mwongozo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na mlango huu wa tiba, na kutaja nguvu za madawa, na kanuni za tiba na uangalizi wa mambo ya afya?”

 

 

Hapo tatizo litakuwa kwa huyo msemaji ambaye ana upungufu wa kuelewa yale aliyokuja nayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani hayana mengine zaidi ya haya, kwa mwenye ujuzi sahihi wa ujumbe wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Kwa atakayefahamu yale aliyokuja nayo Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na mwongozo wake, na dalili kuhusu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na uelewa mzuri kuhusu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  Hii ni neema ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Humneemesha Amtakaye katika waja wake.

 

 

Tumekufahamisha misingi mitatu ya tiba katika Qur-a’an. Vipi ikanushwe kufaa kwa Shariy’ah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliyetumwa kwa maslahi ya kidunia na Aakhirah. Na hili ni jambo la maslahi ya miji pia ustawi wa viwiliwili kama vile inavyokusanya ustawi wa nyoyo bali pia mwongozo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) unaelekeza kutunza afya ya mwili, kwa namna zote. Ama upambanuzi wake unategemea akili sahhi, maumbile safi, kwa njia ya qiyasi, tanbihi, na ishara, kama ilivyo sana katika matawi ya ki-Fiqhi. Wala usiwe katika kundi la wale ambao hukifanyia uadui asichokijua.

 

Basi ambaye ataruzukiwa ufahamu wa kitabu cha Allaah na Sunnah ya Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mtu wa namna hiyo angeweza kutosheka kabisa, na akaacha maneno mengine yasiyokuwa hayo na angetoa elimu zote sahihi kutoka humo.

 

Elimu zote zimo katika kumjua Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na viumbe Wake. Na hili limeachwa kwa Rusuli (Swalaawatu Allaahi ‘alayhim wa salaam) kwani wao wana ujuzi zaidi. Hii linajulikana tu kwa mjuzi wa tiba sahihi na Shariy’ah ambaye anaweza kulinganisha kati ya pande mbili. Na kuona upande upi ulio bora.

 

 

Na tiba ya wafuasi wa Manabii: ni yenye kufaa zaidi kuliko tiba ya wengine.  Na tiba ya aliyewafuata ambaye ni mwisho wa Manabii na bwana wao na Imaam wao; Muhammad bin ‘Abdillaah (Swalawaatu-Allaahi Wa Salaamuhu ‘alayhi wa ‘alayhim) ni tiba kamili na sahihi na yenye manufaa zaidi.    

 

 

Na hayafahamu haya isipokuwa yule anayejua tiba ya watu wasiokuwa wao, kisha akapima kati yao, na hapo basi hudhihiri tofauti yao.  Nao ni ummah sahihi zaidi kwa maumbile ya fitwrah na akili, na wenye elimu kubwa zaidi na wa karibu zaidi katika haki; kwani wao ni wabora kwa Allaah katika watu wa ummah mbali mbali, kama ambavyo Rasuli wao ni bora zaidi kuliko Rusuli wengineo, na elimu ambayo amepewa, uvumilivu na hekima ni jambo ambalo hakuna mfano wake na kulinganisha na wengine.

 

Imaam Ahmad amepokea katika Musnad Hadiyth ya Bahz bin Hakiym, kutoka kwa Baba yake, kutoka kwa Babu yake (Radhwiya Allaahu) amesema: “Amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Nyinyi mnatoshea mataifa sabini, nyinyi ni wa bora wao na watukufu zaidi kwa Allaah.” 

 

Basi imejitokeza athari ya utukufu wake kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika elimu zao na akili zao na maumbile yao, hao wamedhihirishiwa elimu za ummah zilizotangulia na akili matendo na daraja zao.  Kwa hivyo wakazidi elimu upole na akili kuongeza katika ile elimu na upole na hekima alizowapa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa wingi mno. Kwa ajili hiyo ikawazidishia elimu, uvumilivu na utambuzi kwa yale ambayo Allaah Aliwapa katika elimu na uvumilivu.

 

Na hili lilipelekea tabia ya kidamu ni yao, ya umanjano ni ya Mayahudi, na kibalghamu kwa Manaswara na kwa ajili hiyo kwa Manaswara imezidi hali ya upumbavu, uchache wa kufahamu na utambuzi. Na kwa Mayahudi imezidi huzuni, majonzi na unyonge. Kwa Waislamu imezidi, akili, ushujaa, ufahamu kunusuru na furaha.

 

Na hizi ni siri na hakika ambazo atakayejua kiasi chake ni mwenye ufahamu mzuri na umakini wa ubongo, na wingi wa elimu yake, na kujua hali walizo nazo watu. WabiLLaah At-Tawfiyq.” [(Uk 499-501)]

 

Ama baada ya hayo. Basi yanayofuatia ni Fusuli zenye manufaa kutoka katika mwongozo wake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika tiba ambayo amejitibia akawaelekeza wengine na tutabainisha hekima ya kuwashangaza watu na kushindwa kuifikia, tiba zao mbele ya tiba ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni sawa na tiba ya wengine wenye kushindwa kufikia tiba zao (hao matabibu wa kawaida). Basi tunasema tukiwa tunamuomba msaada Allaah na kutafuta hila na nguvu kutoka Kwake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):   

 

 

 

 

[1] Angalia ‘Al-Musawwadah fiy Uswuwl Fiqhi cha Ibn Taymiyyah (uk 451-452) na Irshaad Al-Fuhuwl cha Ash-Shawkaany (uk 255-256).

 

[2]  Huyu Ahmad bin Ja’far Al-Ma’qiriy

[3] Kwa umakini huu wenye kushangaza Hadiyth nyingi za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zimenukuliwa, hivyo mpokezi akitia shaka, au akapokea kwa maana basi ataeleza hilo ili kile kinachonukuliwa kifahamike.

 

Share

004-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Aina Za Maradhi

 

Swahiyh Twibbin Nabawiy

 

004-Aina Za Maradhi

 

 

 

 بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

 

Kuna aina mbili za maradhi: Maradhi ya nyoyo na maradhi ya miili[1] Na aina mbili hizi zimetajwa ndani ya Qur-aan. Na maradhi ya nyoyo ni aina mbili:

 

a-Maradhi ya shubha na shaka

 

b-Maradhi ya matamanio na upotovu.

 

Na yote hayo yamo katika Qur-aan:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu maradhi ya shubha:

 

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ

Ndani ya nyoyo zao mna maradhi na Allaah Akawazidishia maradhi [Al-Baqarah: 10] 

 

Na Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa): 

 

 

   وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۚ

Na ili wale waliokuwa na maradhi nyoyoni mwao (ya unafiki, shaka) na makafiri waseme: “Allaah Amekusudia nini kwa mfano huu?”  [Al-Muddaththir: 31]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Allaah kuhusu wale walioitwa kuhukumu kwa Qur-aan na Sunnah wakakataa na kupuuza:

 

وَإِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٤٨﴾

Na wanapoitwa kwa Allaah na Rasuli Wake ili Awahukumu baina yao, mara hapo kundi miongoni mwao wanakengeuka.

وَإِن يَكُن لَّهُمُ الْحَقُّ يَأْتُوا إِلَيْهِ مُذْعِنِينَ ﴿٤٩﴾

Na inapokuwa haki ni yao, wanamjia (Rasuli) wakitii.

 

أَفِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَمِ ارْتَابُوا أَمْ يَخَافُونَ أَن يَحِيفَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَرَسُولُهُ ۚ بَلْ أُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٥٠﴾

Je, mna maradhi katika nyoyo zao, au wametia shaka, au wanakhofu kwamba Allaah na Rasuli Wake watawadhulumu katika kuwahukumu? Bali hao ndio madhalimu. [An-Nuwr: 48-50]

 

 

Haya ni maradhi ya shubha na shaka. Ama maradhi ya matamanio Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

 

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٣٢﴾

Enyi wake wa Nabiy!  Nyinyi si kama yeyote yule katika wanawake; mkiwa na taqwa, basi msilegeze kauli asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi na semeni kauli inayokubalika. [Al-Ahzaab: 32]

 

Haya ni maradhi ya matamanio ya zinaa. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.

 

 

 

 

 

[1]

 

 

Share

005-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Maradhi Ya Kiwiliwili Yanayoshambulia Mwili

Swahiyh Twibbin-Nabawiy

 

005-Maradhi Ya Kiwiliwili Yanayoshambulia Mwili

 

 

 

 

Ama maradhi ya viwiliwili Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

لَّيْسَ عَلَى الْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْمَرِيضِ حَرَجٌ  

Si vibaya kwa kipofu, na wala si vibaya kwa kilema, na wala si vibaya kwa mgonjwa,   [An-Nuwr: 61]

 

 

Na yametajwa maradhi ya mwili katika Hijjah, Swawm na udhu. Kwa siri kubwa ya ajabu, inayoweza kukubainishia utukufu wa Qur-aan vilivyo akatosheka na Qur-an tu. Nayo: Kwamba msingi ya tiba ya viwiliwili ni tatu:

 

 

1-Kuhifadhi siha

2-Kujilinda na madhara

3-Kutakasa na kuondosha maada mbovu na zenye madhara mwilini.

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema kuhusu misingi hii mitatu katika sehemu tatu tofauti:

 

  فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ  

Lakini atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. [Al-Baqarah 2: 184].

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akahalalisha kufuturu kwa mgonjwa, kwa udhuru wa maradhi na kadhalika msafiri anayo ruhusa kula ili kuhifadhi afya yake na nguvu isije ikaondoshwa nguvu hiyo kwenye safari, kwa kukutana na mazonge ya harakati, ambazo hupelekea kuyayuka kwa chakula wakati hakuna chakula cha badala ya kinachoyeyushwa tumboni ikiwa yuko katika Swawm. Matokeo yake nguvu hutoweka, na kudhoofu, kwa ajili hiyo msafiri ni halali kwake kufuturu. Kwa kuhifadhi afya yake na nguvu yake na kuepuka kinachodhoofisha afya.

 

Na katika Hajj Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِّن رَّأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِّن صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ ۚ

Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake (ikambidi anyoe); basi atoe fidia kwa kufunga Swiyaam au kutoa swadaqah au kuchinja mnyama. [Al-Baqarah: 196]

 

Akamhalalishia mgonjwa na mwenye udhia kichwani, kama chawa, au muwasho au mengineyo, huyo anayo ruhusa ya kunyoa nywele zake katika Ihraam ili kuondosha maada za mvuke mbaya ambao umemletea udhia ule kichwani chini ya nywele, basi atakaponyoa nywele zake, hufunguka tundu za ngozi, mvuke ule hutoweka, uondoshaji huu wa udhia hupimiwa kwa hali zote zenye kuleta udhia kwa kufungika tundu za mwili.

 

 

Kuna vitu kumi ambavyo huleta udhia kwa kufungika na kuleta nguvu kinzani: Damu inapopanda, manii yakizidi, mkojo, haja kubwa, upepo, matapishi, chafya, usingizi, njaa, na kiu.

 

 

Kila moja katika hayo kumi huleta maradhi endapo litazuiliwa na kuleta ugonjwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akazindusha kwa kuondosha udhia mdogo ulio chini ya hayo yote, ambao ni mvuke uliopenya kichwani, kwa kuondosha udhia mgumu kuliko huo, kama ilivyo njia ya Qur-aan; Kuzindua jambo la juu kupitia la chini kwa daraja. Ama kuhami nafsi na madhara Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

  وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا  

Na mkiwa wagonjwa au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi mtayammam (ikusudieni) ardhi safi ya mchanga. [An-Nisaa: 43]

 

 

Akamhalalishia mgonjwa kutumia udongo badala ya maji kwa ghera ya maslahi yake, kwamba isiwe mwili wake umesibu kinachoweza kudhuru, hii pia ni tanbihi ya ghera dhidi ya kila chenye kumdhuru kwa ndani na nje ya mwili. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amewaelekeza waja Wake katika misingi ya tiba. Nasi tunataja mwongozo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika hilo, na tunabainisha kuwa mwongozo wake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni mkamilifu mno.

 

Ama tiba ya nyoyo. Wamepewa Rusuli (‘Alayhim salaam) na hakuna njia ya kupata ila kutoka kwao[1], kwani uzima wa nyoyo, kutengenea kwa nyoyo ni pale nyoyo hizo zinapomjua Rabb wake, na Majina Yake na Sifa Zake, matendo Yake, na hukumu Zake na ziwe zinamridhisha katika kumpenda na kufanya yanayomridhisha. Na pia ziepuke makatazo na machukizo yake. Wala hapana siha kwa nyoyo bali hakuna maisha kamwe bila ya kufanya hivyo. Na hakuna namna ya kupata siha hiyo isipokuwa kupitia Rusuli (‘Alayhim salaam). Na ile dhana iliyopo kuwa yawezekana kupata siha ya nyoyo bila ya kuwafuata hao, basi wanaodhani hivyo wanakosea. Hayo ni maisha ya nafsi ya kihayawani yenye tabia ya kimatamanio, nguvu na afya ya nyoyo hizo ni mbali mbali na afya za kimwana Aadam kimoyo. Na mtu asiyetofautisha kati ya nyoyo hizi na zile, huyo ndie wa kusikitikia uhai wa moyo wake. Kwani huyo yumo miongoni mwa watu wafu, na kwa nuru yake kwani yumo kwenye mkondo wa bahari yenye giza.

 

 

 

 

 

 

[1] Kwa hakika kumwamini Allaah, Rusuli Wake, na ‘Aqiydah  iliyotua ni miongoni mwa tiba ya hali za wenye maradhi ya nyoyo, yaani maradhi ya nafsi.

Share

006-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Tiba Ya Kiwiliwili Imegawanyika Katika Sehemu Mbili

 

 

Swahiyh Twibbin Nabawiy

 

006- Tiba Ya Kiwiliwili Imegawanyika Katika Sehemu Mbili

 

 

 

 

Ya kwanza:

 

Aina ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amewaumbia wanyama wanaonena na wanyama wasionena; aina hii haihitajii matibabu ya tabibu; kama tiba ya njaa, kiu, baridi, uchovu, kwa kuelekea dhidi ya shida hizo na kuziondoa.

 

 

Aina ya pili inayohitajia kufikiria na kuzingatia kwa makini. Kama kutibu maradhi yanayoshabihiana yanayotokana na hali ya hisia ya nafsi inayomtoa mtu katika hali yake ya sawasawa, na kuelekea ima kwenye harara au baridi au yabisi, au unyevunyevu, au yanayokutana mawili katika hali hizo nazo ni aina mbili: Ima ni ya kimaada au ni hali isiyo maada. Yaani: Ima kuwa katika kumiminika maada, au kwa kuzuka, hali ya tofauti kati ya maradhi hayo ni maradhi ya kihali (kayfiyyah) hutokea baada ya kuondoka maada zilizozisababisha, hapo huondoka na maada yake na athari yake kubakia katika hisia.

 

 

Maradhi ya ki-maada zina sababu zake, na ikiwa sababu za maradhi pamoja nayo; basi atakayeangalia sababu hiyo inapasa kuanguka kwanza kisha pili huangalia maradhi, kisha la tatu kuangalia dawa.

 

 

Ama maradhi ya vifundo ni yale maradhi ambayo yanamuondosha mtu kiungo chake na kubadilsha umbo, ima katika umbo, au kwa kuminya, au kwa kupita, au kwa kuguswa au mfupa au kiunguo. Viungo vyote hivi, ikiwa vitaungana na kuitwa viwiliwili vitashikamana: Ama kuungana na kuachana kutoka katika hali ya kawaida huitwa: Kuachana, kukatika au maradhi ya jumla ambazo yanazikutanisha zilizoshabihiana na hizi za viungo.

 

Ama maradhi yanayoshabihiana, ni yale maradhi ambayo huondosha uchangamfu wa mtu wa kawaida (hali yake ya sawasawa). Nayo ni ambayo huondosha hali ya kawaida ya kiungo, ima katika umbo, au kuingiza uwazi, au mwendo, au ugumu, au kuwa laini, au idadi, au ukubwa, au muonekano, viungo hivi ikishikamana na kuunda kiwiliwii, huitwa muungano huo muungano wa mwili. Ama kutoka kwenye hali ya sawa sawa huitwa kukawanyika kwa muungano wa kimwili. Au maradhi ya jumla yanayo jumuisha yanayoshabihiana na ya viungo.

 

 

Maradhi yanayoshabihiana, ni yanayoitoa nafsi katika hisia ya sawasawa, kuitwa ugonjwa ni pale yatokapodhuru kwa dhahiri. Maradhi haya yako katika aina nane: Manne ni mepesi na manne ni muunganiko wa zaidi ya moja.

 

 

Mepesi (moja moja) ni: baridi, joto, rutuba, yabisi.

 

Muunganiko: Joto na rutuba, joto na yabisi, baridi na rutuba na baridi na yabisi.

 

Maradhi haya ima huwa kwa sababu ya kumiminika maada, au bila kumiminika maada, na kama hakuna madhara ya dhahiri huitwa, ni kutoweka katika hali ya afya iliyo sawa.

 

Mwili una hali tatu:

 

a-Hali ya kimaumbile

b-Hali iliyo nje ya kimaumbile

c-Hali ya kati na kati.

 

 

Ya Kwanza: Mwili huwa na afya.

 

Ya Pili: Mwili huugua.

 

Ya Tatu: Mwili huwa kati ya hali mbili hizo.

 

 

Hali hiyo ya tatu ni ya kati na kati; dhidi ya mbili hazigusi moja kwenda kwa mwengine, na mwili kutoka katika hali ya maumbile yake ya kawaida sababu yake ni ima ni kutokea ndani yake, kwani mwili ni muunganiko wa joto, baridi, rutuba, na yabisi, na ima kutokea nje kwani hukutana na kitu kinachoafikiana au kisichoafikiana, na madhara yanayomkuta mwana Aadam hutokana na hisia mbaya kutoka katika mstari wa sawa kiafya.

 

 

Au kutoka na uharibifu wa kiungo au kutokana na udhaifu wa nguvu, au roho zinazoibeba. Na hutokana na kuzidi, au kupungua au kufarikiana, au kuungana au kuendelea wakati mwili uko tofauti na hali hizo na kutoweka ulinganifu. Au kuwa nje ya umbo na kufanya kutoka katika ulinganifu wake ulio sawa.

 

 

Basi tabibu: Ni mtu anayetofautisha vitu ambavyo vikikutana humdhuru mwana Aadam.

 

 

Tabibu ni yule anayetenganisha vinavyomdhuru mwana Aadam ikiwa vitaunganishwa. Au anakusanya kwa mwana Aadam ile ambayo endapo vitatengana vitamdhuru mwana Aadam. Au humuongezea mtu ambayo humdhuru ikiwa vitapungua hapo huleta afya iliyokosekana, au kulinda kwa namna ilivyo au mfano wake na kuondosha shida iliyopo kwa kuleta hali tofauti, huiondosha shida hiyo kwa kizuizi cha kutoka hali hiyo kupitia  الحمية (himaya, kinga). Haya yote utayaona katika mwongozo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa namna ya kukidhi haja na kutosheleza kabisa yatatimia haya kwa hila, nguvu fadhila na msaada kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

 

Share

007-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Nabiy Amejitibu Na Akaamuru Dawa Kwa Maswahaba Zake Na Familia Yake

 

 

Swahiyh Twibbin-Nabawiy

 

007-Nabiy Amejitibu Mwenyewe Na Akaamuru Dawa

Kwa Maswahaba Zake Na Familia Yake

 

 

 

Ilikuwa katika mwongozo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kujiaguwa. Kadhalika aliwaamuru watu wake na Maswahaba wake waliopatwa na maradhi wajitibie. Haikuwa katika mwongozo wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba wake kutumia kinachoitwa أقرباذين (Aqrabaadhiyn – mchanganyiko wa madawa kadhaa ya kemikali); bali mara nyingi dawa zao zilikuwa ni aina moja kwa kila ugonjwa, mara nyingine huongezea nguvu kwa dawa nyingine au kupoza ukali wa dawa. Tiba hii sana ndio tiba ya mataifa mbalimbali, Waarabu, Waturuki, na watu wote wanaosihi majangwani, mataifa yaliyokazana na tiba ya michanganyo ni Warumi, Wagiriki, lakini mataifa ya Asia kama Wahindi sana walijitibu kwa dawa moja moja.

 

 

Matabibu wamekubaliana kwamba pale ambapo yamkinika kutumia chakula kama tiba, isitumike dawa badala yake. Na iwezekanapo kutia dawa moja tu, basi ni bora zaidi kuliko mchanganyiko wa aina nyingi.

 

 

Wakasema na kila shida inayowezekana kuondoshwa kwa chakula na kinga, watu wasijaribu kuiondosha kwa dawa. Haifai kwa tabibu kubobea kunywesha watu madawa bila kiasi.[1] Kwa sababu dawa huharibu mwili kama haijakuta ugonjwa humo mwilini, vile vile inadhuru mwili ikiwa ugonjwa upo, lakini hauafikiani na dawa ile, au hata dawa ikikutana na ugonjwa lakini imezidi kiwango kuliko ugonjwa huo au kuliko nguvu ya mwili kustahamilia dawa ile, au namna ilivyotumika hiyo dawa, yote hii huvuruga hali ya afya.

 

 

Wataalamu wanaofanya majaribio sana, tiba yao ni katika dawa moja moja. Kundi hili ni kati ya makundi matatu ya kitabibu.

 

Hakika ya hayo, ni kuwa tiba ni kutokana na jinsi ya vyakula vilivyo; taifa la watu ambao hula mno vyakula vya aina moja moja, huwa na maradhi machache sana. Basi na tiba yake ni kwa dawa za aina moja moja.  Ama watu wa mijini ambao ada yao ni kula vyakula vingi mbali mbali kwenye mlo mmoja tu hawa wanahitajia tiba mchanganyiko. Basi watu hawa huhitaji tiba kwa dawa zilizochanganywa pamoja kwa aina mbali mbali. Sababu ni kuwa maradhi yao zaidi huwa mchanganyiko huwa zinawafaa sana. Maradhi ya watu wa mashambani na majangwani huwa ni aina moja moja, hao hutosha kuwatibu kwa dawa zilizo moja-moja, hii ni hoja kulingana na taaluma ya tiba.

 

Sisi tunasema, “Kuna jambo lingine hapa, nali ni: Tiba ya Nabiy hailingani na tiba za matabibu wengine, na kama ilivyo tiba ya wataalamu wa tiba wanavyowazidi matabibu wasio mabingwa wa taaluma ya tiba. Hili wamekiri wataalamu mabingwa wa tiba, kati yao husema: “Tiba ni kiyasi (malinganisho ya pande mbili).” Na wapo wasemao: “Tiba ni majaribio.” Na wapo wasemao: “Tiba ni mawazo ya ki-ihamu, njozi, na dhana zenye kusibu.” Na wapo wasemao: “Elimu ya tiba kiasi kikubwa imechukuliwa kutoka kwa wanyama.” Kama tunavyoshuhudia wanyama mfano wa paka wanapokula vitu vyenye sumu, hukimbilia kwenye taa na kuramba mafuta kuweza kujitibia. Nyoka pia wanapotokea ardhini, macho yao yana kifuniko hawaoni vizuri. Basi nyoka hao huja katika majani ya الرازيانج )Ar-Raaziyaanij)[2] basi hupitisha macho yao kwenye dawa hiyo. Na kama mazowea ya ndege kuonekana wakijitibia kwa maji ya bahari baada ya kutatizika afya zao n.k. Mfano ya hayo yaliyotajwa katika msingi ya tiba.

 

            Majani Ya Ar-Raaziyanij                                         Shimaar (Bizari tamu)

                       

 

 

Hakika tiba zitokazo katika Wahyi ziko juu kuliko tiba za matabibu, kama zilivyo elimu za Manabii kuwa ziko juu kuliko elimu za watu wengine. Bali unapata dawa ambazo hutibu magonjwa kutoka katika maelekezo ya Kinabii; dawa ambazo hawakuzigundua matabibu wakubwa. Elimu zao zote na maarifa yao yote, majaribio na vipimo vyao hawavikugundua. Miongoni mwao ni madawa ya nyoyo na kiroho, nguvu ya moyo, kutawakali kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), kumuelekea na kujitupa, na kunyenyekea mbele Yake, kutoa swadaqah, kuomba du’aa, kuomba maghfirah na kutubia, kuwafanyia ihsaan watu na viumbe kwa ujumla, kuwapa msaada waliohemewa, kutatua matatizo ya wenye shida.  Dawa hizi zimejaribiwa na mataifa mbali mbali ya watu kwa dini mbali mbali na kuona matokeo makubwa kwenye kuponesha kwa namna ambayo matabibu wakubwa elimu zao zilikuwa hazijafikia huko.

 

 

Sisi pia tumefanya majaribio ya tiba nyingi kama hizi. Tumeziona zikitenda yasiyotendwa na tiba za kimaada, bali hizo huwa katika kiwango cha chini mbele ya tiba hizi za kimoyo, kiroho na kadhalika. Na haya yanakwenda na hekima ya Ki-Ilaah (Allaah) bila kutoka nje ya hapo, ila ifahamike kuwa sababu ziko aina kwa aina, pale moyo unapokuwa umeungana na Rabb wa walimwengu, Muumba wa maradhi na dawa Anayemiliki maumbile yote, na kuyaweka chini ya udhibiti Wake.

 

 

Moyo wa namna hii utakuwa na tiba tofauti na moyo ulio mbali na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni jambo linalojulikana kuwa nyoyo zikipata nguvu, nafsi na tabia ikapata nguvu pia huweza kusaidiana kuondoa maradhi na kuyashinda.

 

 

Kwa mwenye kuwa karibu na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) huwezi kukana haya, kwamba, kuwa karibu na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni katika tiba kubwa, kuna nguvu ya kuweza kuondosha maumivu jumla.

 

 

Hayakanushi haya ile asiyejua na aliye mbali na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na hakika ya ki mwana Aadam. Na tutaeleza In Shaa Allaah kwa nini Suwrah Al-Faatihah iliposomwa iliweza kuponyesha maradhi ya kung’atwa, aliyefanyiwa Ruqya kwa kisomo hicho akasimama kana kwamba hakuwa na shida.

 

 

Hizi ni aina mbili katika tiba ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa uwezo wa Allaah (Ta’aalaa) tutazungumzia kadri ya uwezo wetu, na upeo wa ujuzi wetu kiasi, lakini tutatoa hayo kwa kutegemea fadhila za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Mwenye ushindi, mpaji.

 

 

[1] Kama pana maradhi ya aina fulani; yapasa kutumia dawa fulani bila kuzidisha kipimo; kwani kila dawa ni silaha yenye ncha mbili, kwa upande mmoja humsaidia mgonjwa; kiwango kikizidi na muda wa kutumia kuwa mrefu; huenda ikapelekea katika maradhi na kuathiri kiungo kilichokuwa kizima. Kuna baadhi ya magonjwa ambayo tiba yake ni mapumziko kwa muda maalum na utaratibu maalum wa mlo.

[2] Neno la kifursi nalo ni Ansiyuwn ni mti wenye mauwa madogo na matunda yake ni mbegu zenye harufu nzuri hutumiliwa katika matibabu mbali mbali. Na katika nchi za Shaam na Miswr zinajulikana kama ‘shimaar’ au ‘shamuwr’. Na katika nchi za Magharibi zinaitwa ‘bisbaas’. Taz  Mu’jim Al-A’shaab wan-Nabaat Atwibiyyah (Uk. 208) (Mti huu Afrika Mashariki huitwa: ima aynisuni (au bizari shimari au bizari tamu). Kiingereza ni: Fennel Seeds.

 

 

 

Share

008-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Kila Maradhi Yana Dawa Yake

 

 

Swahiyh Twibbin-Nabawiy

 

008-Kila Maradhi Yana Dawa Yake

 

 

 

Amepokea Imaam Muslim katika sahihi yake. Hadiyth ya Jaabir bin Abdillaah kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amesema:

 

 

   ‏ ((لِكُلِّ دَاءٍ دَوَاءٌ فَإِذَا أُصِيبَ دَوَاءُ الدَّاءِ بَرَأَ بِإِذْنِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ)) ‏ ‏

 “Kila ugonjwa una dawa, ikipatiwa  dawa ya ugonjwa, hupona kwa idhini ya Allaah ‘Azza wa Jalla.”

 

Na Al-Bukhaariy (5678) kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

((مَا أَنْزَلَ اللَّهُ دَاءً إِلاَّ أَنْزَلَ لَهُ شِفَاءً)) ‏

“Allaah Hajateremsha ugonjwa wowote ila, ameteremsha na tiba yake.”

 

 

Na katika “Musnad Al-Imaam Ahmad” kutoka Hadiyth ya Usaamah bin Shariyk amesema:

 

كنتُ عندَ النبىِّ صلى الله عليه وسلم، وجاءت الأعرابُ، فقالوا: يا رسول الله؛ أَنَتَدَاوَى؟ فقال :((نَعَمْ يا عبادَ اللهِ تَدَاوَوْا، فإنَّ اللهَ عَزَّ وجَلَّ لم يضَعْ داءً إلا وَضَعَ لَهُ شِفاءً غيرَ داءٍ واحدٍ)) قالوا: ما هو ؟ قال: ((الهَرَمُ))

Nilikuwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakaja mabedui wakasema: Ee Rasuli wa Allaah, je, hujitibu? Akasema: “Naam, enyi waja wa Allaah jitibuni, kwani Allah ‘Azza wa Jalla Hajaweka ugonjwa ila pia Ameweka na tiba yake, isipokuwa ugonjwa mmoja tu”. Wakasema ni ugonjwa gani huo? Akasema: “Ukongwe”

 

na katika lafudhi nyingine,

 

 ((إنَّ اللهَ لم يُنْزِلْ دَاءً إلا أنزل له شِفَاءً، عَلِمَهُ مَنْ عَلِمَهُ، وَجَهِلَهُ مَنْ جَهِلَهُ))

“Hakika Allaah Hateremshi ugonjwa, ila Ameuteremshia tiba yake wameijua walioijua, na hawakuijua wasiyoijua.”

 

 

Hadiyth hizi ndani yake kuna kuthibitishia sababu na visababishi, na kubatilisha kauli ya anayekanusha. Yajuzu kuwa aliposema: “Kila ugonjwa una dawa.“ ni kwa ujumla wake inajumuisha pia hata magonjwa yanayoua na magonjwa ambao tabibu hawezi kuyatibu na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amejalia tiba ya kuyaponyesha, lakini Amefunika elimu yake kwa watu kuweza kuifikia. Kwani viumbe hawana ujuzi wowote isipokuwa ule waliofundishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Kwa ajili hii, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameweka sharti la kupona katika kusadifu kukubaliana kwa dawa na ugonjwa. Kwani hakuna chochote katika viumbe isipokuwa dhidi yake kipo vile vile. Hivyo kila ugonjwa una dhidi yake ya dawa inayoutibu huo ugonjwa. Hivyo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaambatanisha kupona kwa maradhi na kuafikiana kwa ugonjwa na dawa. Na hiki ni kiasi kilicho sawa na ugonjwa, dawa inapovuka kiwango cha ugonjwa katika namna ya kutibia, au kiasi cha kutibia, ikawa zaidi ya inavyotakiwa, dawa italeta ugonjwa mwingine. Pia dawa ikiwa pungufu, haitaweza kupambana na maradhi pia matibabu yatakuwa na kasoro. Na hapo matibabu hayatakuwapo kama dawa hailingani na mgonjwa, au dawa haijakutana na ugonjwa tiba haitapatikana, na pindi muda ukiwa sio muwafaka kwa dawa hiyo basi haitofaa, mwili kama haukubaliani na dawa, au hakuna nguvu ya kuhimili dawa. Au kuna kizuizi chochote, basi kupona hakutakuwepo, ikiwa hayajasadifu mambo hayo, na yakipatikana hayo kusadifu kukutana basi na ponya kwa idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) itatokea na hapana budi. Na maana hii ya Hadiyth ndio bora kati ya maana mbili.

 

Pili, Hadiyth ni katika kauli za jumla yenye muradi wa maana mahsusi hasa na hasa yanaoingia katika kauli, ni maradufu, maradufu ya maana iliyo nje.

Hii inatumika katika kila lugha na muradi unakuwa: kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Hajaweka ugonjwa unaotibika, ila Ameuwekea dawa. Hapa maradhi yale yasiyotibika hayaingii katika maana hiyo. Na hii kama kauli yake Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kuhusu upepo alioupeleka kwa kaumu ‘Aad.

 

تُدَمِّرُ كُلَّ شَيْءٍ بِأَمْرِ رَبِّهَا  

  Unadamirisha kila kitu kwa amri ya Rabb wake.  [al-Ahqaab: 25]

 

yaani, kila kitu kinachokubali kuteketea, ambacho kawaida upepo huweza kukiangamiza, na mifano ya hivyo ni mingi.

 

 

Na mwenye kuzingatia maumbile ya vitu vilivyo dhidi hapa Ulimwenguni, na kupingana, na vingine kuzuiana. Vingine kuishinda, mtu huyo atakumbuka hekima ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na ufundi Wake katika Ar-Rubuwbiyyah (Uola Wake) na Upekee Wake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika sifa Zake za ulezi, kuteza nguvu kila kitu. Yeye Ndiye Mmoja Pekee, lakini vingine vyote kila kimoja kina dhidi, na kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni Mkwasi kwa dhati Yake, na kila asiyekuwa Allaah anamuhitajia Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

 

Na katika Hadiyth zilizo sahihi ipo amri ya tiba. Na kwamba hilo halipingani na kutawakali kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

 

Kama ilivyokuwa kupambana na shida ya njaa, kifo, joto, baridi, na kuleta dhidi ya hiyo, yaani shibe kukata kiu, kuleta baridi, au joto, si kupingana na kutawakali kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Bali haitimii hakika ya Tawhiyd isipokuwa kwa kushikamana na sababu Alizoweka Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa makadirio na ki-Shariy’ah, na kuziacha. huharibu tawakkul, pia inatofautiana na amri na hekima, na kuzidhoofisha, wakati asiyeshikamana na sababu anadhani, kuwa kule kuziacha kunatia nguvu zaidi katika kutawakali kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).    Basi kumbe kuziacha kwa ajizi kunapingana na “Tawakkul” (Kumtegemea Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa) ambayo hakika yake moyo wa kutawakali kwa Allaah ni mjs kupata manufaa katika Dini yake na dunia yake na kuondosha madhara kwenye Dini yake na dunia yake, na katika kufanya hivyo hapana budi kushikamana na sababu kama sivyo itakuwa ameachilia kutofanya kazi, kwa hekima na shariy’ah, basi mja asifanye ile ajizi yake ndio, “Tawakkul” wala “Tawakkul” isiwe ni ajizi.

 

 

Katika haya, kuna radd kwa wale wanaokanusha kufaa kujitibia wakasema: “Kama kupona ni jambo limo katika Qadari ya Allaah basi kujitibu hakufai kitu, pia ikiwa haijakadiriwa kupona, vile vile hakuna maana ya kujitibia.”  Pia wanasema: “Maradhi yamepatikana kwa Qadari ya Allaah na Qadari ya Allaah haipangwi wala hairudishwi nyuma.”

 

 

Na swali hili ndilo ambalo wale mabedui walimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ama Maswahaba watukkufu (Radhwiya Allaahu ‘anhum) watukufu, ni wajuzi zaidi wa Allaah na hekima Zake na sifa Zake wasingeweza kuuuliza swali kama hilo. Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alishawajibu wale mabedui majibu kamili, yanayotosheleza. Akasema:  Madawa haya na ruqya na taqwa ni miongoni mwa Qadar za Allaah, basi haindoki kitu katika Qadar Yake, bali Qadar yake inarudisha Qadar nyingine. Na jibu hili ni katika Qadar Yake, na hili ni kama jibu la mwenye njaa, kiu, joto na baridi na kinyume chake, ni kama jibu la Qadar ya adui katika jihaad, na kila ambaye Allaah Anamuandikia ni Yule anayesukuma, anayesukumwa na kisukumo chenyewe.

 

 

Husemwa kwa mwenye kuuliza swali hili: Hii yakupasa kutofanya sababu yoyote katika sababu yenye kukuletea manufaaa na kukuondoshea madhara; kwa kuwa manufaaa na madhara ni makadirio yetu tuliyokadiriwa; hayakuwa na budi isipokuwa kutokea kwake, na hata kama hayajakadiriwa; basi yasingetokea, na hili ni kuharibu Dini na dunia kwa pamoja na kuharibu ulimwengu. Halisemi hili ila yule mpinga haki na mwenye inadi. Hutaja Qadar ili tu apinge hoja; kama vile washirikina walivyosema:

 

  لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكْنَا وَلَا آبَاؤُنَا

 “Lau Allaah Angetaka, tusingelifanya shirki, wala baba zetu” [Al-An’aam: 148]

 

 

Hili wamelisema kama kutetea hoja zao kwa Allaah juu ya Mitume.

 

 

Jibu la swali hili: Ni kusemwa: imebakia sehemu ya tatu ambayo hakutaja, nayo ni kuwa: “Allaah Amekadiria kadha wa kadha kwa sababu hii, ikija sababu basi itatokea kilichosababishwa, vinginevyo.” Hapana! Kwa mfano akisema: “Ikiwa nitakuwa nimekadiriwa sababu; nimefanya na kama haikukadiria kwangu; sitoweza kusema.” Je hoja hii itakubaliwa kwa mtumishi wako, na mtoto wako, na kukulipa ikiwa atatoa hoja kwako kwa kile ulichokiteremsha na kukikataza; na kuwa kinyume chako?

 

 

Utakapokutana nae; itakubaliwa vipi kwako katika kutetea haki za Allaah juu yako. Na katika kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema: “Kila ugonjwa una dawa.” Ni kumpa nguvu mgonjwa na tabibu, na akahimiza ili watu watafute hiyo dawa. Wafanye utafiti na kugundua dawa.

 

 

Mgonjwa anapohisi kuwa ule ugonjwa wake unayo dawa utakaouondosha; basi moyo wake utapata matumaini na kasi ya kukata tamaa itapoa, mlango wa matumaini utamfunukia nafsi yake inapopata nguvu, joto lake la kimaumbile huibuka na kwa hiyo huwa sababu ya kuibuka joto lake la kimaumbile na hiyo huwa ni sababu ya nguvu ya roho za kihayawani, kinafsi, na kitabia ya kimaumbile, na roho hizi zinapopata nguvu, basi huimarika nguvu zinazoibeba na kuyashinda maradhi na kuyaondoa kabisa.

 

 

Kadhalika tabibu anapojua kuwa ugonjwa huu unayo dawa hapo, ataweza kuitafuta na kuifanyia uchunguzi.

 

 

Maradhi ya viwiliwili yako katika vipimo vya maradhi ya nyoyo, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Hajafanya maradhi ya nyoyo ila pia Ameyafanyia “Shifaa” (ponya lake) kwa namna iliyo dhidi yake. Mgonjwa akijua hilo akatumia, na ikasadifu ugonjwa wa moyo wake itamponyesha kwa idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

 

 

 

Share

009-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Mwongozo Wa Nabiy Katika Kiasi Cha Kula Na Kunywa

 

Swahiyh Twibbin Nabawiy

 

009-Mwongozo Wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Katika Kiasi Cha Kula Na Kunywa

 

 

 

Imaam Ahmad katika “Al-Musnad”[1] na wengineo, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

((مَا مَلأَ آدَمِيٌّ وِعَاءً شَرًّا مِنْ بَطْنٍ حَسْبُ ابنِ آدمَ لُقَيْمَاتٌ يُقِمْنَ صُلْبَهُ فَإِنْ كانَ لاَ بُدَّ فاعِلاً فَثُلُثٌ لِطَعَامِهِ وَثُلُثٌ لِشَرَابِهِ وَثُلُثٌ لِنَفَسِهِ))  

“Mwanadamu hajapata kujaza chombo kibaya kuliko tumbo. Yamtosha mwanadamu vitonge vya kuunyoosha uti wake wa mgongo.[2] Na ikiwa yampasa kufanya hivyo; basi theluthi moja ni ya chakula chake, na theluthi moja ya kinywaji chake na theluthi ya nafsi yake.”[3]

 

 

 

 

 

[1] Imaam Ahmad (3/132), na At-Tirmidhiy amepokea (2380), na Ibn Maajah (3349) kutoka katika Hadiyth ya Al-Miqdaam bin Ma’ad Yakrib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ikiwa ni marfuw’an. Nimesema: Isnaad yake ni Swahiyh, na nimeweka fasli maalum katika kitabu changu: “Iyqaadhw Al-Himam Al-muntaqaa Min Jaami’ Al-‘Uluwm Wal-Hikam.” (uk 611-612)

 

[2]Yaani mgongo wake; na makusudio ni kiwiliwili kizima. Hadiyth hii tukufu inathibitisha kuwa mwana Aadam anakula ili apate kuishi, haishi ili apate kula; ikiwa lengo ni lile la kwanza; basi atakinaika kwa chakula kwa kitakachomtocheleza katika hilo; na hawezi kufikia katika hali ya kushiba, na mtu kama huyu hatonenepa kwa kuwa na mafuta mengi. Ama Yule aliye katika hali ya pili; huyu atakula na hatashiba; mfano wake ni kama vile hayawani:

يَتَمَتَّعُونَ وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ الْأَنْعَامُ  

Wanastarehe na wanakula kama walavyo wanyama wa mifugo. [Muhammad: 12]

 

[3] Hadiyth hii ni Hadiyth ya msingi katika tiba yote, na pindi tabibu Ibn Maaswiyyah alipoithibitisha alisema: “Lau watu wangetumia maneno haya basi wangesalimika na maradhi na maduka ya dawa yangefungwa.” Kwa hakika alisema hivyo; kwa sababu asili ya kila ugonjwa ni kuvimbiwa, na ndio iliyomfanya tabibu Al-Haarith bin Al-Kaladah: “Al-Himyah ni kichwa cha dawa na Al-Batwnah ni kichwa cha dawa.” Amesema vile vile, “Aliyeuwa mtu, na kumuangamiza samba porini; ni kule kuingiza chakula juu ya chakula kingine kabla hakijasagika.”

 

Haya ni baadhi ya manufaa ya kupunguza chakula, na kuacha kujaza chakula kwa lengo la ustawi wa kiwiliwili na afya yake. Ama manufaa yake kuhusu moyo na ustawi wake; kupunguza chakula kunatengeneza nyoyo na unaongeza ufahamu na kukata nafsi, kudhoofisha matamanio, ghadhabu, na wingi wa chakula hupelekea kinyume chake; amesema hilo Imaam Ibn Rajab Al-Hanbaliy (Rahimahu Allaah) katika: Jaami’ Al-‘Uluwm wal-Hikam  (2:525-526).

 

 

Share

010-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Maradhi Ya Kiwiliwili Kujikinga Na Kuvimbiwa Na Kula Kulingana Na Haja

Swahiyh Twibbin-Nabawiy

 

010-Maradhi Ya Kiwiliwili Kujikinga Na Kuvimbiwa

Na Kula Kulingana Na Haja.

 

 

 

Maradhi ni aina mbili: Maradhi ya kimaada, hutokana na kuongezeka kwa maada, imepitiliza kiwango kwenye mwili hadi ikadhuru utendaji wake wa kawaida na maradhi ya namna hii ni mengi yaliyokithiri na sababu yake: Kuingiza chakula mwilini kabla ya kuyeyushwa cha kwanza tumboni. Na kuzidisha kiasi kinachotakiwa na mwili. Pia kula vyakula vyenye virutubisho vichache. Vinavyosagwa polepole, na kula vyakula vingi kwa pamoja vyenye aina na mifumo mbali mbali. Binaadamu akijaza tumbo lake vyakula vya namna hii, akazowea kufanya hivyo, hiyo itamletea maradhi anuwai, kati ya hayo kupona kwake ni polepole, na mengine hupona haraka. Binaadamu akila ulaji wa wastani, akatumia kiwango kinachohitajia mwili kwa namna ya kiwango cha wastani na aina nzuri mwili huwa unafaidika zaidi kuliko kula sana.

 

Chakula kina ngazi tatu:

 Ya kwanza ni haja.

Ya pili ni kutosha.

Ya tatu yake ni ziada.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameeleza kuwa mtu vinamtosha vitonge vya kusaidia kunyoosha mgongo wake ili asiishiwe na nguvu, asidhoofike, akivuka kiasi hicho basi ale kiasi cha kujaza theluthi ya tumbo lake. Na theluthi nyingine aziache kwa maji na ya tatu, iwe kwa ajili ya kupumua vizuri. Na mwongozo huu una faida sana kwa mwili na moyo. Kwani tumbo linapojaa chakula huwa finyu katika kunywa maji na ikipata kinywaji basi hufinyika katika nafsi ya kupumua. Hapo huwa ni shida sana kama vile mtu aliyebeba mzigo mzito. Jambo hilo hufisidi moyo na viungo vyote kushindwa kuleta utiifu wa ‘ibaadah mbalimbali, na badala yake hujishughulisha na utashi wa matamanio unaotokana na kushiba mno.

 

Hivyo kujaza tumbo kwa chakula hudhuru moyo na mwili[1].  Hili likiwa linafanyika mara kwa mara (yaani mara nyingi), ama ikiwa mara moja moja basi haina madhara, kwani mara moja Swahaba Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikunywa maziwa mbele ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kiasi cha kusema: “Kwa hakika Yule aliyekutuma kwa haki simpatii njia.”[2]  Na mara nyingi Maswahaba walikula na kushiba na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yupo nao pamoja.

 

Kushiba kupindukia hudhoofisha nguvu na mwili, japo hurutubisha, kwani mwili hupata nguvu kulingana na anavyokula, na sio wingi wa chakula.

 

Kwa kuwa Mwanadamu sehemu yake moja ni ya ardhi, nyengine ya hewa, na nyingine ya maji. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amegawa chakula cha Mwana Aadam na kinywaji chake na nafsi yake mafungu matatu.

 

Pakisemwa iko wapi fungu la sehemu ya

kimoto?

 Jibu: Haya ni mambo ambayo wameyaongelea matabibu. Na kusema, “Kwenye mwili kuna sehemu ya kimoto hasa na ni mojawapo ya nguzo na asili yake”.  Wamepingwa na matabibu wengine. Na wengine wasio matabibu, kwa kusema kuwa: “Mwilini hakika hakuna sehemu ya kimoto” na wametegemea hoja mbali mbali kama ifuatavyo:

 

Ya Kwanza: Kwamba hiyo sehemu ya kimoto ima yaweza kusemwa kuwa imedondoka kutokana na “athiyr” na kuchanganyika na sehemu za kimaji na kiardhi, au itasemwa kwamba imefanya humo na ya kwanza katika namna mbili haikubaliki.  

 

Mojawapo ni kuwa moto daima kwa tabia yake ni wenye kupanda na kushuka basi ni kutokana na nguvu ya kulazimisha kutoka kwenye kutoka kwenye kituo chake na kuja Ulimwenguni.

 

Ya Pili kwamba ingebidi moto upite kwenye mzingo baridi mno kushuka chini, nasi tunaona kuwa hapa Ulimwenguni moto huzimika kwa maji kiasi kidogo tu, basi kiasi cha moto mdogo kupita katika mkusanyiko wa baridi kali mno, ni aula zaidi kuzimika.

 

Na ya Tatu, ni kusemwa kuwa:  Kuwa moto umefanyika hapa hapa, hilo ndio halikubaliki zaidi. Kwani mwili uliogeuka moto baada ya kutokuwa hivyo, hapo kabla ulikuwa ima, ardhi, na ima maji, au hewa. Kwani nguzo za asili ya vitu ni hizo nne tu. Na hiki kilichogeuka kuwa moto, kwanza, kilikuwa kimechanganyika na mojawapo ya vitu hivi, na kuungana pamoja kabisa. Na kitu ambalo sio moto, kikikutana na vitu vyenye maumbo makubwa visivyokuwa moto, hakiwezi kuwa katika uelekeo wa kuwa moto. Kwani chenyewe sio moto. Na maumbo ya vitu baridi mchanganyiko, vipi vitakuwa katika utayari wa kugeuka kuwa moto?

 

Mkisema: Kwa nini kusiwepo sehemu za tabia ya moto kuweza kugeuza maumbo ya kuyafanya kuwa ni moto, kwa kule kufanyika nayo.

 

Tunasema kuwa kuzungumzia kuwepo kwa hizo sehemu zenye tabia ya kimoto, kama kuzungumzia maelezo yaliyopita hapo awali. Kama mtasema: Tunaona kurashiza maji kwenye chokaa inayozima moto hujitenga na hiyo chokaa mwanga wa jua ukichoma kwenye maada ya kioo, moto hujitokea, tukipiga jiwe juu ya chuma moto hujitokeza, na tabia zote hizi za kimoto hutokea wakati wa kuchanganyika. Na hii linabatilisha mliyoyasema kwenye sehemu ya kwanza vile vile.

 

Wanaokanusha wanasema: Sisi hatukanushi kuwa kiponda kikubwa huzusha moto, kama vile kuponda mawe juu ya chuma, au nguvu ya kupasha moto kupitia jua huleta moto kama katika kioo, lakini tunasema haiwezekani kabisa hilo kutokea katika vitu vyenye maumbo ya mimea na wanyama hata kuleta moto. Pia hakuna ule usafi, na mng’aro unaofikia kiwango cha kioo. Vipi miali ya jua inamulika juu yake, na moto hautokei kabisa. Basi mwanga unaofika ndani yake utawezaje kuzua moto?

 

Namna ya pili: Katika hoja ya msingi: Matabibu wamekubaliana kwa pamoja maji ya kale yenye joto kali mno, kama vijisehemu vya tabia ya joto ndiyo sababu ya hilo joto linalopakaa kwenye maji ingekuwa ni muhali. Sababu sehemu za moto japo kidogo inaingiaje akilini kuwa itabakia ndani ya sehemu za maji mengi kitambo cha bahari, bila kuzimika, karne kwa karne wakati tunaona kitabia moto mkubwa huzimwa kwa maji machache.

 

Namna ya Tatu: Kama mnyama na mmea ni sehemu ya moto imo ndani yao hasa, ingezidiwa na sehemu ile ya maji iliyomo ndani yao, na kushinda chembe hufanya zile tabia za chembe iliyoshinda igeuze chembe iliyoshindwa, hivyo lazima vichembe vya moto vichache vingegeuka na kufuata tabia ya maji ambayo ni dhidi ya moto.

 

Namna ya Nne: Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametaja kuumbwa kwa mwana Aadam katika mahali pengi ndani ya Qur-aan.

 

Anamuelezea mwana Aadam kuwa ameumbwa kutokana na maji, na sehemu nyingine Anamulezea kutokana na udongo, na katika baadhi ya Aayah nyengine kuwa ameumbwa kwa mchanganyiko wa viwili hivyo ambao ni tope. Sehemu nyingine Anamuelezea kuwa Amemuumba kutokana na udongo mfinyanzi uliokauka, utoao sauti kama kigae; udongo huu umepigwa jua na upepo mpaka ukageuka kigae, na hakuna mahali popote ambapo Anapoelezea kuwa mwana Aadam aliumbwa kwa moto, bali amejaalia hiyo kuwa ni sifa mahsusi kwa iblisi.

 

Na imethibiti katika Swahiyh Muslim kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

خُلِقَتِ الْمَلاَئِكَةُ مِنْ نُورٍ وَخُلِقَ الْجَانُّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ وَخُلِقَ آدَمُ مِمَّا وُصِفَ لَكُمْ  

“Malaika wameumbwa kwa nuru, na majini wameumbwa kwa miali ya moto, na Aadam ameumbwa kutokana na mlivyoelezwa.” [Swahiyh Muslim (2996) kutokana na Hadiyth ya ‘Aaishah Radhwiya Allaahu ‘anhaa]

 

Na hili ni wazi kwamba Aadam  ameumbwa kwa kile kilivyoelezwa ndani ya Qur-aan tu na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)    Hajatuelezea kwamba Amemuumba kutokana na moto wala katika maada zake kuna chembe ya moto.

 

Namna ya Tano: Upeo wa dalili yao ni joto la miili ya wanyama, kwamba ni dalili ya kuwepo visehemu vya moto. Wakati hiyo sio dalili. Kwani sababu za joto ziko zaidi ya moto, wakati mwengine hutokana na moto, na mara nyingine hutokana na harakati na kutokana na kuakisi miali, na ujoto wa hewa, na kuwa jirani na moto, na hii ni kutokana na joto kali la hewa – vile vile –hutokea kutokana na sababu nyingine, hivyo sio lazima kuwa joto itokane tu na moto.

 

Watu wa moto (wenye kudai haya) wamesema kuwa: Inavyojulikana kuwa udongo na maji, vikichanganyika basi hapana budi kutokea joto ambalo hupelekea kupikika na kuchanganyika kwa viwili hivyo. Bila ya hivyo visingechanganyika, wala kuungana pamoja. Vile vile pindi unapotupa mbegu ardhini kiasi cha kutoifikia hewa wala jua haliifikii, huharibika mbegu hiyo. Basi lazima kutokea kitu cha kupika kuivisha kwanza katika umbo la mchanganyiko na ikitokea hivyo basi itakuwa ni chembe ya tabia ya kimoto. Kama haikutokea, basi umbo mchanganyiko halitapasha joto kwa tabia yake. Kama litapata joto, joto hilo likitoweka la mpito tu, na likipita joto hili la juu juu kitabaki sio cha joto chenyewe kwa tabia wala kwa namna yake nyingine kitakuwa baridi kabisa. Lakini baadhi ya vyakula na madawa kuna yaliyo ya joto kwa tabia yake hapo unapata kwamba joto la lake ni la asili ya moto. Vilevile, kama kwenye mwili kusingekuwa na chembe inayopasha joto, basi mwili ungefikia ukomo wa baridi.

 

Kwani tabia ikilazimu baridi, na kukakosekana kisaidizi au pingamizi, baridi lazima likomee upeo wake wa juu kabisa. Lau ingekuwa hivyo pasingetokea kuhisi baridi. Kwani baridi linalofika mwilini kama lina ukomo lingekuwa linafanana, na hakuna kuathiriwa kitu kutokana na mfano wake; yaani baridi haliwezi kuathiri baridi vile vile. Na kwa kuwa haliathiri, mtu asingehisi baridi. Na asingehisi baridi, asingepata maumivu yake. Na kama baridi litakuwa kiwango cha chini kuliko kilicho mwilini, basi kuathirika ndio zaidi. Kama kusingekuwako mwilini sehemu inayopasha moto, kimaumbile, basi mtu asingeathirika na baridi wala kupata maumivu kwa baridi.

 

Wanasema: Na dalili zenu hizo kusema kweli zinabatilisha yale wayasemayo kwamba: Chembe za kimoto husalia katika mchanganyiko wa maumbo kama zilivyo, na tabia yake ya kimoto, na sisi hatusemi hivyo bali twasema: Sura yake ilivyo katika asili huharibika pale inapochanganyika.

 

Wengine wamesema: Kwa nini isifae kusemwa: Kwamba ardhi na maji na hewa inapochanganyika: lile joto livishalo, lipikalo: Ni joto la jua, na nyota, sayari zingine. Kisha mchanganyiko ule, unapotimia kuiva huwa tayari kupokea umbo la mchanganyiko kupitia ujoto. Iwe mimea, wanyama, au madini, kizuizi kiko wapi kuwa joto hilo linalopatikana katika maumbo mchanganyiko ni kwa sababu ya sifa maalumu na nguvu ambazo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anazileta wakati wa kuwepo huo mchanganyiko na sio kwa kuwepo chembe za asili ya moto?[3]

 

Hamna njia yoyote kuweza kubadilisha uwezekano huu kabisa. Na kundi la matabibu bora kabisa wamekiri hilo.

 

Ama maelezo ya mwili kuhisi baridi, tunajibu kuwa: hiyo inajulisha kwamba kwenye mwili kuna joto, na kupasha joto. Kwani nani anakana hilo? Lakini nini dalili kuwa kinachopasha moto ni moto tu?  Kwani japo wajua kwamba kila moto huchemsha, kadhalika kwenye kadhia hii hili haijumuishi, bali kinyume chake ni kweli kuwa, baadhi ya inayochemsha ni moto.

 

Ama kauli yenu, mlipoelezea kuharibika sura ya moto wa asili; matabibu wengi wana msimamo kuwa sura ya asili ya moto ni yenye kusalia. Na kusema kuwa inaharibika ni kauli batili. Amekiri ubatili wa kauli hiyo, wa matabibu waliokuja nyuma katika kitabu chake kiitwaho “Ash-Shifaa”[4]. Ametoa hoja kuwa asili ya vitu hubaki kwenye tabia yake ndani ya maumbo mchanganyiko.  

 

 

[1]Amesema Imaam Shaafi’y (Rahimahu Allaah): “Sijashiba kwa muda wa miaka kumi na sita, isipokuwa nilishiba mara moja na kutoa (kutapika); kwani kushiba kunaupa uzito mwili na mashaka moyo na kuondosha utambuzi na kuleta usingizi na humdhoofisha mtu na ‘ibaadah.” [Imepokewa na Ibn Abiy Haatim katika ‘Aadab Ash-Shaafi’iy’ (uk 106)]

 

[2] Imepokewa na Al-Bukhari 6452

[3] Alichokiamua Imaam Ibn Al-Qayyim Al-Jawziyyah (Rahimahu Allaah) katika masuala haya ni yale yale waliyothibitisha wanazuoni wa elimu ya Hadiyth; viumbe hai vyote vinashirikiana katika mahitaji yake ya nguvu. Kadhalika suala la kupumua ni mtiririko wa silsila iliyoratibiwa katika katika maingiliano  (تفاعلات)za kibaolojia ambayo inakamilika kwa kuvunja vunja chembechembe (particles) za viungo vya kiwiliwili kuwa Carbon Dioxide na maji na nguvu, na kwa kuwa hizi  (تفاعلات) zinatimia na kutokea kwenye chembechembe hai, kwa hali hiyo imeitwa:  عملية التنفس الخلوي  )Cellular respiration(  Hili linatimia kwa   الميتوكندريا   (Al-Miytokandariyaa), hii ni sawa na kituo cha uzalishaji wa nguvu katika chembechembe hai, ambapo ndipo panapotokea mwingiliano (تفاعلات) wa ‘Cellular respiration.’

 

Kimefungwa na vifungo viwili, ambazo kwa pamoja na kifungo cha Plasma chenyewe ambacho ni:  Kifuniko cha nje ambayo ni nyeupe sana chenye kupenyeza mwanga (أملس), nayo imefungwa na mada nyingi za kikemia. Kifuniko cha ndani.

[4] Ni kitabu cha Shaykh Ar-Raiys: Abiy ‘Aliy Al-Husayn bin ‘Abdillaah bin Siynaa; anachukuliwa kuwa ni mwanafalsafa mkubwa katika hekima, mantiki, mazingira, ana baadhi ya makosa ambayo Uislamu hauridhiki na mfano wao. Miongoni mwa mwandishi. Kwa hivyo ikaoneshwa kwake kwa kauli yake: “Muta-aakhiriykum.” Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah na mwanafunzi wake Ibn Qayyim Al-Jawziyyah (Rahimahuma-Allaah) wanamtoa kasoro nyingi kwa kupotoka kwake kuliko kukubwa, alifariki mwaka 428 Hijriyyah.

 

 

Share

011-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Nabiy Alitumia Aina Tatu Za Tiba Kwa Magonjwa Mbalimbali

 

Swahiyh Twibbin Nabawiy

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Alitumia Aina Tatu Za Tiba Kwa Magonjwa Mbalimbali

 

 

Matibabu ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mgonjwa yalikuwa ya aina tatu.

 

Ya Kwanza:  Kutumia dawa za ki atw-twabiy’iyyah (natural)

 

Ya Pili:  Kutumia dawa za ki Ilaah (Allaah)

 

Ya Tatu: Kutumia mchanganyiko kati ya aina hizo mbili.

 

Tutataja aina hizo tatu katika mwongozo wake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo tunaanza kutaja dawa za atw-twabiy’iyyah alizoelekeza na kuzitumia (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kisha tutaje dawa za ki-Ilaah. Kisha mchanganyiko wa aina hizo za dawa.

 

Kumbuka kuwa, tunaashiria hapa kuwa ieleweke, hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  kazi iliyomleta, ametumwa kuwa ni mwongozaji, mlinganiaji, kwa Allaah na kwenye Jannah Yake,  na mtambulishaji wa Allaah na mbainishaji ummah maeneo ya kupata radhi Zake, na muamrishaji wao kufuata ardhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Pia yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni mbainishaji na mkatazaji wa mambo yanayomghadhibisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), na yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  ni msimuliaji wao habari za Manabii, hali zao na  Ummah zao. Habari za kuumbwa Ulimwengu, chanzo cha kuumbwa na marejeo ya viumbe, kupotea kwa nafsi na kutengenea, na sababu zake.

 

Ama tiba ya miili: Imekuja katika kukamilisha Shariy’ah yake, na imekusudiwa lengine, kwani hutumika tu pale inapohitajika kama itawezekana kuishi bila ya tiba, kama haihitajiki hapo hima zote, na nguvu zote zitaelekezwa katika kuagua nyoyo na Roho, kulinda siha yake, na kukinga magonjwa yake, na kuzihami zisiharibike na vitu vinavyoziharibu. Na hilo ndilo kusudio la awali. Na kutengeneza mwili bila kutengeneza moyo haifai. Kuharibika mwili pamoja na kutengenea kwa moyo madhara yake ni kidogo sana. Ni madhara yanayotoweka ambapo manufaa yake ya kudumu timilifu.  Wa biLLaahi At-Tawfiyq

 

 

Share

012-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Tiba Kwa Dawa Za Ki-Twabi’iyyah (Ki-Asilia): Tiba Ya Homa

 

 Swahiyh Twibbin-Nabawiy

 

Sehemu Ya Kwanza

 

Tiba Kwa Dawa Za Ki-Twabi’iyyah  (Asilia, Natural)

 

 

012-Tiba Ya Homa[1]

  

Imethibiti katika Asw-Swahiyhayn:

 

عَنْ ابْنِ عُمَرَ أَنّ النّبِيّ صَلّى اللّهُ عَلَيْهِ وَسَلّمَ قَالَ: ((إنّمَا الْحُمّى أَوْ شِدّةُ الْحُمّى مِنْ فَيْحِ جَهَنّمَ فَأَبْرِدُوهَا بِالْمَاءِ))

Kutoka kwa Ibn Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  “Hakika homa, au ukali wa homa unatokana na joto la Jahannam, ipozeni kwa maji.” [Imepokewa na Al-Bukhaariy (5723) na Muslim (2209)]

 

Hadiyth hii imewapa mushkeli matabibu wengi wasiojua, wakaona inapingana na dawa ya homa na tiba yake.  Sisi tunabainisha kwa uwezo wa Allaah na nguvu Zake - iliyo na fiqhi yake, basi tunasema: Maelezo ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni ya aina mbili. Kwa watu wote ardhini, na mahsusi kwa baadhi yao.

 

 

Ya kwanza, ni kama maelezo yake kwa ujumla na ya pili, ni kama pale aliposema:

 

لاَ تَسْتَقْبِلُوا الْقِبْلَةَ بِغَائِطٍ وَلاَ بِبَوْلٍ وَلاَ تَسْتَدْبِرُوهَا  وَلَكِنْ شَرِّقُوا أَوْ غَرِّبُوا

“Msielekee qibla kwa haja kubwa au ndogo, wala msikipe mgongo, lakini elekeeni Mashariki au Magharibi.” [Imepokewa na Al-Bukhaariy (144) na Muslim (264) kutoka katika Hadiyth ya Abuu Ayyuwb (Radhwiya Allaahu ‘anhu).

 

 

Maelezo haya hayawahusu watu wa Mashariki wala Magharibi, wala Iraq, lakini ni kwa watu wa mji wa Madiynah na walio katika uelekea wake, kama Shaam na miji kama hiyo[2] kadhalika aliposema:

 

مَا بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ قِبْلَةٌ

“Eneo kati ya Mashariki na Magharibi ndio qibla.”  [At-Tirmidhiy (344), Ibn Abiy Shaybah katika Al-Muswannaf (2363), na wengineo ni Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) marfuw’an kwake]

 

 

Hii likijulikana basi, maelezo yake katika Hadiyth hii yanawaelekea watu wa Hijaaz peke yao, na wanaowafuatia, kwani ilikuwa homa zao nyingi ni zile aina ya homa za kila siku zinazojitokeza zinazotokana na joto la jua. Homa ya namna hii inatosha maji baridi kunywa na kuoga. Homa ni joto la ajabu linafukuta kutoka moyoni na huko hutawanyika kupitia roho na damu kwenye mishipa ya mwili kusambaa mwili mzima, na hufukuta fukuto linalodhuru utendaji kazi wa mwili wa kawaida[3]. Nayo homa inagawika sehemu mbili.

 

i) Ya kupita: Ambayo huzuka kutokana na malengelenge au kushughulika, au kupatwa na joto la jua.

 

 

ii) Ya kimaradhi: Na hii haiwi isipokuwa katika kiungo cha awali kutokea hapo huchemsha mwili mzima. Ikiwa chanzo chake ni kuhusiana na roho, nafsi; basi huitwa: Homa ya Siku; kwani mara nyingi huondoka ndani ya siku moja na ukomo wake ni siku tatu.

 

 

Ikiwa chanzo chake ni kuhusiana na michanganyiko; huitwa: Homa ya kuambukiza (kama bakteria, virusi), nayo ina aina nne: Umanjano, weusi, balghami na kidamu.

 

 

Ikiwa chanzo chake ni kuhusiana na viungo vigumu ya asili huitwa ni homa ya  دق kushindika (kugandamiza, kushinikiza;  homa kuu) Chini ya aina hizi kuna vigawanyo vingi.

 

Mwili waweza kufaidika sana kwa kupata homa kuliko kufaidika kwa dawa.  Na mara nyingi hii huwa katika homa ya siku moja. Na homa ya kuambukiza, ni sababu ya kuivisha vitu vigumu bila ya joto hilo visingeweza kuiva, pia ni sababu ya kufunguka kwa tundu ambazo dawa bila ya hivyo isingeweza kufika dawa zenye kufungua.

 

 

Ugonjwa wa Ramad (kuvimba macho). Wa muda mfupi au wa zamani, aina zake nyingi hupona kwa haraka ya ajabu na husaidia kutokana na Al-Faalij (Hemiplegia) na Al-Laqwah (ugonjwa hufikia usoni na kupindisha shavu) na kufura, na maradhi  mengi yanayozuka yanayotokana na ziada nzito.

 

 

Baadhi ya matabibu bora wameniambia kuwa magonjwa mengi, baadhi yake huwa tunapata taarifa yake kupitia homa. Homa inaashiria kuja kwa maradhi mengine mwilini kama mgonjwa anapobashiri kupata nafuu. Basi homa kwake huwa na faida zaidi kuliko kunywa dawa kwa kiasi kikubwa tu.

 

 

Homa huiva kwa michanganyo na maada mbovu inayodhuru mwili inapoisha inasadifu dawa, hali tayari iko kwa ajili ya kutoka kwani imeiva hapo ikaitoa na kuwa ndio sababu ya kupona[4].

 

 

Iikijulikana hili, basi inajuzu kuwa muradi wa Hadiyth ni zile homa za mpito; kwani homa hizi mtu hupona kwa kuzama kwenye maji baridi. Na kunywa maji baridi yenye barafu. Mwenye homa hii hahitaji tiba nyengine. Hiyo ni hali ya ujoto tu iliyoambatana kwenye roho. Hivyo yatosha kuiondosha kwa maji baridi. Haihitaji kutoa maada, au kungojea kuiva. Pia inajuzu kuwa kusudio ni homa aina zote.

 

 

Bingwa wa matabibu Galenus[5] amekiri kuwa maji baridi yanafaa kutibu homa. Amesema katika makala ya kumi kutoka katika kitabu cha ‘Mbinu za Tiba’.  “Kama mtu ni kijana, mwenye mwili mzuri, nyakati za joto kali, akiwa katika homa kali sana, na hana uvimbe, malengelenge tumboni, akatoa maji baridi au akaogelea, ingemsaidia kutibu homa hiyo”. Akasema: “Nasi tunaamrisha kufanya hivyo mfululizo bila kuacha.”.

 

 

Amesema Ar-Raaziy[6] katika kitabu chake kikubwa[7]: “Ikiwa kuna nguvu kubwa na homa ni kali, na kuiva kuko waziwazi na hakuna vidonda tumboni, malenge malenge, uvimbe, maji baridi yanafaa kwa kunywa, mgonjwa akiwa na mwili mzuri, na kipindi cha joto, na amezowea kutumia maji baridi kutoka nje na aambiwe kutumia.”[8]. Kauli yake kuwa: “Homa ni kutokana na joto la moto wa Jehannamu” ni ukali wa miali yake na kuenea kwake, na mifano kama hiyo. Aliposema, “Ukali wa joto ni kutokana na joto la Jahannam.” [Al-Bukhaariy (533, 534) kutoka katika Hadiyth ya Abuu Hurayrah na Ibn Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuna sura mbili.

 

 

Kwanza, ni mfano tu unatokana na moto wa Jahannam, waja wapate kushuhudia kuwepo kwake, wapate mazingatio, kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amekadiria kudhihiri kwake kutokana na sababu zake, kama starehe, furaha, ladha ni katika neema za Jannah, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amevidhihirisha hapa duniani. Waja wapate kufaidika ni dalili kwao na imekadiriwa kutokea kwake kwa sababu zake.

 

 

Pili: Muradi wake ni kushabihisha akafananisha, ukali wa homa na moto wake na joto la Jahannam. Na kufananisha joto na homa kuwazindua watu wapate kuzingatia.

 

 

Hii nikuzindua nafsi za watu watambue ukali wa adhabu ya moto, kwamba joto hili kali limefananishwa na joto ya fukuto la miali ya moto wa Jahannam. Ni ile joto linalopatikana kwa kukaribia tu kabla hata ya kuingia motoni. Aliposema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Ipoozeni” imepokewa kwa namna mbili: kwa hamza mkato na kuipa fat-hah kitenzi chenye herufi nne. Kutokana na kama atakifanya kuwa baridi kitu, mfano: atakichemsha na kukifanya cha moto.

 

 

Ya Pili: Kutumia hamzah ya kuungia, yenye dhwammah “Hamzah Al-Waswli” kutokana na kitu kimekuwa baridi kwa kufanywa baridi. Na hii ndio lugha fasaha zaidi na yenye kutumiwa zaidi, na kitenzi chenye herufi nne “Ar-Rubaa’iy” ni lugha mbaya kwao.

 

 

Amesema: Al-Hamaasiy:

 

***

Nimeelekea yaliko maji ya jamii ya watu kutafuta burudisho

kupoza moyo uwakao kwa mapenzi…

 

Nipate baridi ya nje ya mwili,

ni yupi atakayesaidia mbele ya moto uwakao ndani ya mwili.[9]

 

***

 

Kauli yake: kwa maji hapo kuna kauli mbili:

 

Mojawapo ni kuwa kila maji, na hii ndio kauli sahihi.

 

Na ya pili ni:  Maji ya zamzam. Watu wanaoshika kauli hii wanatoa hoja kwa Hadiyth iliyopokelewa na Imaam Al-Bukhaariy katika Swahiyh Al-Bukhaariy (3261 kutoka kwa Abuu Jamrah Naswr bin ‘Imraan Adhw-Dhwuba’iy amesema: “Nilikaa na Ibn ‘Abbaas Makkah, nikashikwa na homa akasema: Ipoze ipate kukuondoka hiyo homa kwa maji ya zamzam kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: “Homa inatokana na fukuto la Jahannam, ipozeni kwa maji.” Au amesema: “Kwa maji ya Zamzam.”

 

 

Ametia shaka mpokezi huyu kama angesema bila shaka yoyote kwa kauli ya kukata shauri moja kwa moja, basi hiyo ingekuwa ni amri mahsusi kwa watu wa Makkah kutumia maji ya zamzam. Kwa sababu ni rahisi kwao kuyapata, na watu wengine watumie maji waliyokuwa nayo kwenye mazingira yao.

 

 

Wale wanaosema ni maji ya aina yote wamehitilafiana kuhusu muradi ni kutoa swadaqah ya maji, au kuyatumia maji?  Katika kauli mbili. Na iliyo sahihi, yaani kuyatumia. Nadhani waliopeleka kwenye maana ya swadaqah ya maji ni kwa sababu ameona mushkeli wa kuyatumia maji baridi katika homa, wala hakufahamu kusudio lake pamoja na kuwa ni zuri sana. Nayo ni kwamba malipo hulingana na jinsi kazi ilivyo. Kama maji baridi yanavyozima moto unaowaka kutokana na kiu, kwa hivyo pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atazima homa inayowaka kwa huyo mgonjwa kama malipo yaliyo muwafaka kabisa na hali yake. Yaani moto huzimwa kwa kutumia maji. Lakini uelewa huu unatokana na kuzingatia fiqh iliyomo kwenye Hadiyth na ishara yake, ama muradi hapo ni kuwa maji yatumike.

Imepokewa kutoka kwa Anas amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

إذَا حُمَّ أَحَدُكُمْ فَلْيُرَشَّ عَلَيْهِ الْمَاءُ الْبَارِدُ  ثَلاثَ لَيالٍ مِنَ السَّحَرِ   

“Mmoja Wenu akiugua homa, basi na arashiziwe maji baridi siku tatu kutokea usiku wa manane.”  [Imepokewa na Abuu Ya’-laa katika Musnad (379), Al-Hakam (4/200) na (401). Nimesema: Isnaad yake ni Swahiyh, imesahihishwa na Al-Hakam na Adh-Dhahabiy (Rahimahuma-Allaah) kwa sharti la Muslim, na imewafikiwa na Shaykh wetu Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) katika Asw-Swahiyhaa (1301).

 

 

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba  Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

لاَ تَسُبَّهَا فإنها تَنْفِى الذُّنُوبَ، كما تَنْفِى النَّارُ خَبَثَ الْحَدِيدِ

“Homa ni joto katika joto la Jahannam, basi liepusheni nanyi kwa maji baridi.” [Imepokewa na Ibn Maajah (3475). Nimesema: Isnaad yake ni Swahiy, na watu wake ni thiqah; kama alivyosema Al-Buwswariy (Rahimahu Allaah) katika Zawaid na kusahihishwa na Shaykh wetu Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)]

 

Na pia:

 

عَنْ جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ (رضي الله عنه)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ عَلَى أُمِّ السَّائِبِ أَوْ أُمِّ الْمُسَيَّبِ فَقَالَ:  ((مَا لَكِ يَا أُمَّ السَّائِبِ)) أَوْ ((يَا أُمَّ الْمُسَيَّبِ تُزَفْزِفِينَ؟)) قَالَتْ:  "الْحُمَّى لاَ بَارَكَ اللَّهُ فِيهَا"  فَقَالَ: ((لاَ تَسُبِّي الْحُمَّى فَإِنَّهَا تُذْهِبُ خَطَايَا بَنِي آدَمَ كَمَا يُذْهِبُ الْكِيرُ خَبَثَ الْحَدِيدِ)) مسلم

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa Ummu As-Saaib akasema: “Je, una nini ee Ummus-Saaib?” Akasema: Homa Allaah Asiibariki [ilaaniwe] Akasema: “Usiitukane homa kwani inaondosha dhambi za mwana Aadam kama tanuri la muhunzi linavyoodosha uchafu wa chuma.” [Muslim (2575)]

 

 

Kwa kuwa homa hufuatiwa na himaya ya vyakula vibaya, na kula vyakula na madawa yenye manufaa, na kufanya hivyo kuna faida katika kusafisha mwili, na kutowesha uchafu na ziada yake, kadhalika kuusafisha na maada mbaya, homa hufanya kile kinachofanywa na moto kwenye chuma kuondosha uchafu wake. Na kusafisha asili yake ya chuma: ndio maana ikafanana sana homa na moto wa kwenye tanuri la kuua vyuma ambao husafisha maada asili ya chuma kiasi hiki ndicho kinachojulikana na matabibu.

 

 

Ama homa kusafisha moyo hata ukasafika kutokana na taka zake jambo hili analijua matabibu wa nyoyo. Wanalikuta liko sawa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyowaelezea, lakini maradhi ya moyo ikiwa yamefikia kiwango cha kukatisha tamaa kupona katika tiba hii haifai.

 

 

Basi kwa maana hiyo, homa ina faida kwa mwili na moyo. Ikiwa homa ina nafasi hii basi kuilaani ni dhulma na ni uadui. Mara moja nilikumbuka, nikiwa naugua homa, kauli ya mshairi anayeitukana homa:

 

 

***

Amenitembelea anayekumbusha dhambi na ameaga.

Aangamie kabisa mgeni huyo ajaye na aagaye.

Ameniuliza wakati akiniaga,

Unataka nini?

Nikamjibu usirudi tena hapa!

 

***

 

Nikasema: Aangamie yeye; ameitukana kile Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekikataza kutukana kama angetaka angesema:

 

***

Anayefikirisha madhambi amenitembelea,

karibu mgeni ajaye na aagaye.

Ameuliza wakati akiniaga,

Wataka nini? Nikamwambia usiondoke.

 

***

 

Angesema hivyo, ilikuwa bora kwake, hapo homa, ikaniondoka haraka.

 

 

 

 

 

 

[1] Hali zote za homa ikipanda hutibiwa kwa njia ya maji katika hali mbili: a) Kutokea nje kwa njia ya مكمدات   (bendeji au taula, au kitambaa kinachowekwa juu ya sehemu iliyojeruhiwa) iliyokuwa ni baridi au yenye barafu, kwa ajili ya kushusha joto. b) Mwenye homa kunywa maji mengi, hili linasaidia viungo vya mwili na zaidi figo kufanya kazi zake sawasawa.

[2] Al-Baghwiy amesema: katika Sharh As-Sunnah (1/359) na kauli yake: “Elekeeni Mashariki au Magharibi” ni maelezo kwa watu wa Madiynah, na wale ambao Qiblah chao ni muelekeo huo. Ama wale ambao Qiblah chao ni muelekeo wa Mashariki ama Magharibi basi hawa wataelekee Kusini ama Kaskazini.”

 

[3] Imaam Ibn Muflih (Rahimahu Allaah) amesema: katika Al-Aadab Ash-Shar’iyyah’ (3/100):  Wamesema baadhi ya matabibu: “Hili ni bora kuliko tiba ya ugonjwa huu ikiwa imetokea Hijaaz, na huo ni mji wenye joto jingi na kavu, na joto kali ni dhaifu katika wakazi wake wa ndani, na kuwamwagia maji katika wakati ule uliotajwa (nao ni siku iliyo wazi kabisa) inapasa kukusanya joto kubwa lililosambaa lililotapakaa mwilini unaobebaa nguvu yote, na hivyo kuwa na nguvu yenye kusukuma na hukusanyika katika maeneo tofauti ya kiwiliwili kwenda ndani yake ambapo ndipo penye maradhi yale, na itadhihiri baki ya nguvu yake katika kuondosha maradhi yaliyotajwa, na hivyo kuyasukumu kwa idhinii ya Allaah (Ta’aalaa).

[4] Kwa hakika baadhi ya maradhi ya zama hizi, mfano maradhi ya Romatizim (rheumatism)  ambayo mishipa huwa inavimba, inamfanya mtu asiweze harakati yoyote, au maradhi ya Zuhri yaliyozidi katika ubongo hali huwa nzuri kwa kupanda joto la kiwiliwili; yaani katika hali mbali mbali za homa; na hiyo ni miongoni mwa mlolongo wa njia za matibabu katika hali hizi: Homa ya viwanda; yaani: Kutengeneza hali ya homa ya mgonjwa kwa sindano ya mada maalum.

 

[5] Tabibu wa kigiriki mwenye vumbuzi nyingi katika upasuaji. Ni miongoni mwa rejea nyingi za Waarabu, alifariki mwaka (201).

[6] Jina lake ni Abu Bakr Muhammad bin Zakariyyah, alizaliwa katika mji wa Ar-Ray, na akanasibishwa nao na akapewa jina la Galinus Al-‘Arab, kwa umaarufu wake.

 

[7]Jina la kitabu chenyewe ni ‘Al-Haawiy fiy Swinaa’ah Atw-Twibb’ yenye mijeledi thelathini.

 

[8] Nimesema: Vivyo hivyo tiba ya zama hizi maji hunufaisha katika kutibu homa. Dr. Mahmuwd An-Nusaimiy amesema katika: ‘Atw-Twibb An-Nabawiy wal-‘Ilm Al-Hadiyth’ (3/211): “Kwa hakika dawa anuwai zenye kutibu homa mbali mbali hazikuwa zinafahamika kabla ya karne ya tisa, na ya kuwa kushuka kwa joto maarufu katika tiba ya zama hizi, ambayo yalivumbuliwa mapema kama vile kwinini na asprini, hazikusambaa ulimwenguni kabla ya karne hiyo, na hivyo utumiaji wa dawa kwa kupunguza joto ni la mwanzo.

[9] Miongoni mwa mashairi ya ‘Urwah bin Adhiynah; kama ilivyo kwenye ‘Ash-Sha’r wash-Shu’araa’ (uk 580) na ‘Wafiyaat Al-A’yaan’ (2/394).

Share