01-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah - كِتَابُ اَلطَّهَارَةِ

 

 

 

 

 

كِتابُ الطَّهارَة

Kitabu Cha Twahaarah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

 

Share

01-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah: Mlango Wa Maji

بُلُوغُ الْمَرام بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتابُ الطَّهارَة

Kitabu Cha Twahaarah

 

بَابُ الْمِياهِ

01-Mlango Wa Maji

 

 

 

 

1.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏فِي اَلْبَحْرِ:   ‏{ هُوَ اَلطُّهُورُ مَاؤُهُ، اَلْحِلُّ مَيْتَتُهُ } أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَابْنُ أَبِي شَيْبَةَ وَاللَّفْظُ لَهُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ وَاَلتِّرْمِذِيُّ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah[1] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema kuhusu bahari: “Maji yake yanatwaharisha, na maiti wake ni halaal (kuliwa).” [Imetolewa na Al-Arba’ah: Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah  na Ibn Abiy Shaybah na tamshi la Hadiyth hii ni lake Ibn Khuzaymah akaisahihisha na At-Tirmidhiy]

 

 

2.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم: {إِنَّ اَلْمَاءَ طَهُورٌ لَا يُنَجِّسُهُ شَيْءٌ)) أَخْرَجَهُ اَلثَّلَاثَةُ  ‏ وَصَحَّحَهُ أَحْمَدُ   ‏

Kutoka kwa Sa’iyd Al-Khudriyy[2] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  amesema: “Hakika maji ni masafi[3], hayanajisiwi na kitu.”  [Imetolewa na Ath-Thalaathah: Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy  na akaisahihisha Ahmad] 

 

 

3.

وَعَنْ أَبِي أُمَامَةَ اَلْبَاهِلِيِّ رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ صلى الله عليه وسلم: {إِنَّ اَلْمَاءَ لَا يُنَجِّسُهُ شَيْءٌ، إِلَّا مَا غَلَبَ عَلَى رِيحِهِ وَطَعْمِهِ، وَلَوْنِهِ} أَخْرَجَهُ اِبْنُ مَاجَهْ ‏ وَضَعَّفَهُ أَبُو حَاتِمٍ

Kutoka kwa Abuu Umaamah Al-Baahiliyy[4] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  amesema: “Hakika maji hayanajisiwi na chochote isipokuwa kinachozidi harufu yake, ladha yake na rangi.”   [Imetolewa na Ibn Maajah na Abuu Haatim akaidhoofisha]

Aliyepokea Al-Bayhaqiyy: “Maji ni yenye kutwahirisha isipokuwa yakiingia najsi na kuyabadilisha harufu, ladha au rangi[5] yake.”

 

 

4.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: {إِذَا كَانَ اَلْمَاءَ قُلَّتَيْنِ لَمْ يَحْمِلْ اَلْخَبَثَ}

 

 وَفِي لَفْظٍ: {لَمْ يَنْجُسْ}   أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ‏ وَابْنُ حِبَّانَ 

Kutoka kwa ‘Abdullaahi bin ‘Umar[6] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا)  amesema:  Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  amesema: “Pindi maji yakiwa qullatayn[7] (viriba au mitungi miwili) huwa hayachukui uchafu.”

 

Na katika tamshi: “Haifanyi kuwa najisi.” [Imetolewa na Al-Arba’ah na ameisahihisha Ibn Khuzaymah na Ibn Maajah]

 

 

5.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم:  { لَا يَغْتَسِلُ أَحَدُكُمْ فِي اَلْمَاءِ اَلدَّائِمِ وَهُوَ جُنُبٌ}  أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ 

وَلِلْبُخَارِيِّ: {لَا يَبُولَنَّ أَحَدُكُمْ فِي اَلْمَاءِ اَلدَّائِمِ اَلَّذِي لَا يَجْرِي، ثُمَّ يَغْتَسِلُ فِيه} ‏
وَلِمُسْلِمٍ: {مِنْهُ}‏
وَلِأَبِي دَاوُدَ: {وَلَا يَغْتَسِلُ فِيهِ مِنْ اَلْجَنَابَةِ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Asioge mmoja wenu katika maji yaliyotuwama ilhali ana janaba.” [Imetolewa na Muslim]

 

 Na katika Al-Bukhaariy: “Asikojoe mmoja wenu katika maji yaliyotuwama ambayo hayaendi kisha akaoga ndani yake[8].” 

 

Na katika riwaayah nyengine ya Muslim: “Kutoka humo” (yaani kutoka kwenye maji hayo).

 

Na kwa Abuu Daawuwd: “Mtu asioge humo janaba.”  

 

 

6.

وَعَنْ رَجُلٍ صَحِبَ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏"أَنْ تَغْتَسِلَ اَلْمَرْأَةُ بِفَضْلِ اَلرَّجُلِ، أَوْ اَلرَّجُلُ بِفَضْلِ اَلْمَرْأَةِ، وَلْيَغْتَرِفَا جَمِيعًا  .أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ.‏ وَالنَّسَائِيُّ، وَإِسْنَادُهُ صَحِيحٌ.‏

Mtu mmoja[9] aliyesuhubiana na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza mwanamke kuoga mabaki ya maji ya mwanamume  na mwanamume kuoga mabaki ya maji ya mwanamke, wachote pamoja.”

[Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na Isnaad yake ni Swahiyh]

 

 

 

7.

عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏كَانَ يَغْتَسِلُ بِفَضْلِ مَيْمُونَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا.   أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ .‏

 

وَلِأَصْحَابِ "اَلسُّنَنِ:  اِغْتَسَلَ بَعْضُ أَزْوَاجِ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏فِي جَفْنَةٍ، فَجَاءَ لِيَغْتَسِلَ مِنْهَا ، فَقَالَتْ لَهُ: إِنِّي كُنْتُ جُنُبًا، فَقَالَ: {إِنَّ اَلْمَاءَ لَا يُجْنِبُ} وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ خُزَيْمَةَ‏

 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas[10] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا)  kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  alikuwa akioga kwa maji yaliyoacha na Maymuwnah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا).” [Imetolewa na Muslim]

 

Na katika mapokezi ya Aswhaab As-Sunan]:

“Mmoja katika ya wake wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  alioga kwenye beseni kisha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaja kuoga katika chombo hicho, huyo mkewe[11] akamwambia: “Mimi nilikuwa na janaba.”  Akasema: “Hakika maji hayapati janaba.”  [Ameisahihisha At-Tirmidhiy na Ibn Khuzaymah]

 

 

8.

 وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم: {طَهُورُ إِنَاءِ أَحَدِكُمْ إِذْ وَلَغَ فِيهِ اَلْكَلْبُ أَنْ يَغْسِلَهُ سَبْعَ مَرَّاتٍ، أُولَاهُنَّ بِالتُّرَابِ}  أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ.‏

وَفِي لَفْظٍ لَهُ: { فَلْيُرِقْهُ }‏

وَلِلتِّرْمِذِيِّ: { أُخْرَاهُنَّ، أَوْ أُولَاهُنَّ بِالتُّرَابِ }‏ .‏

 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kutwaharisha chombo cha mmoja wenu ikiwa kimelambwa na mbwa, ni ki kukiosha mara saba[12].” 

[Imetolewa na Muslim].

 

Tamshi jengine la Muslim: “Basi amwage.”

Na katika riwaayah ya Imaam At-Tirmidhiy: “Kwanza au mwisho wake kwa mchanga.” 

 

 

9.

وَعَنْ أَبِي قَتَادَةَ ‏ رضى الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ ‏فِي اَلْهِرَّةِ‏: { إِنَّهَا لَيْسَتْ بِنَجَسٍ، إِنَّمَا هِيَ مِنْ اَلطَّوَّافِينَ عَلَيْكُمْ } أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ.‏ وَابْنُ خُزَيْمَةَ‏.‏

 

Kutoka kwa Abuu Qataadah[13] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema kuhusu paka: “Huyo si najsi bali ni mmoja wa wananchanganyika nanyi.”  [Imetolewa na Al-Arba’ah: Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah  na ameisahihisha At-Tirmidhiy na Ibn Khuzaymah]

 

 

10.

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: { جَاءَ أَعْرَابِيٌّ فَبَالَ فِي طَائِفَةِ اَلْمَسْجِدِ، فَزَجَرَهُ اَلنَّاسُ، فَنَهَاهُمْ اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏فَلَمَّا قَضَى بَوْلَهُ أَمَرَ اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏بِذَنُوبٍ مِنْ مَاءٍ، فَأُهْرِيقَ عَلَيْهِ}.‏  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.‏

 

Kutoka kwa Anas bin Maalik[14] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Bedui mmoja alikuja akakojoa katika pembe ya Msikiti, watu wakamkemea Lakini Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  akawakataza.  Alipomaliza mkojo wake, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  akaamrisha iletwe ndoo ya maji, ikamwagiwa[15] juu yake (huo mkojo). [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

11.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{ أُحِلَّتْ لَنَا مَيْتَتَانِ وَدَمَانِ، فَأَمَّا الْمَيْتَتَانِ: فَالْجَرَادُ وَالْحُوتُ، وَأَمَّا الدَّمَانُ: فَالطِّحَالُ وَالْكَبِدُ } أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَفِيهِ ضَعْفٌ

 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا)  kwamba Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  amesema: “Tumehalalishiwa maiti za aina bili na damu za aina mbili. Ama maiti mbili ni nzige na samaki ، na ama damu mbili  ni bandama na ini.” [Imetolewa na Ahmad na Ibn Maajah na Hadiyth hii ina yaliyo dhaifu]

 

 

12.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏} إِذَا وَقَعَ اَلذُّبَابُ فِي شَرَابِ أَحَدِكُمْ فَلْيَغْمِسْهُ، ثُمَّ لِيَنْزِعْهُ، فَإِنَّ فِي أَحَدِ جَنَاحَيْهِ دَاءً، وَفِي اَلْآخَرِ شِفَاءً } أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ.‏

 

وَأَبُو دَاوُدَ ، وَزَادَ: { وَإِنَّهُ يَتَّقِي بِجَنَاحِهِ اَلَّذِي فِيهِ اَلدَّاءُ }

 

Kutoka kwa Abuu  Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  amesema: “Pindi nzi akiangukia katika kinywaji cha mmoja wenu, basi amazmishe kisha amtoe , kwani kuna ugonjwa katika moja ya bawa lake na tiba katika bawa jengine[16].”  [Imetolewa na Al-Bukhaariy ]

 

Na Abuu Daawuwd ambaye aliongeza:

 

“Kwani yeye (inzi) huangulikia kwa bawa lake lenye ugonjwa.”

 

 

13.

عَنْ أَبِي وَاقِدٍ اَللَّيْثِيِّ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{ مَا قُطِعَ مِنْ اَلْبَهِيمَةِ ‏وَهِيَ حَيَّةٌ‏ فَهُوَ مَيِّتٌ } أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ، وَاللَّفْظُ لَهُ.‏

 

Kutoka kwa Abuu Waaqid Al-Laythiyy[17] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kilichokatwa kutoka kwa mnyama aliye hai basi hicho ni maiti.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy na ameipa daraja ya Hasan na tamashi hili ni lake]

 

 

 

 

[1] Abuu Hurayrah: Jina lake halisi ni ni ‘Abdullaah au ‘Abdur-Rahmaan bin Sakhr Ad-Daws, mmoja wa Swahaba wakubwa wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na alipokea Hadiyth nyingi kuliko wote. Zaidi ya watu 800 walipokea kutoka kwake. Alisilimu katika mwaka wa Khaybar (7H) na akawa karibu na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mpaka Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipofariki. Akateuliwa kuwa Mufti (Mwanazuoni wa hukumu za Kiislaam) wakati wa Ukhalifa wa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) na baadaye akawa gavana wa Madiynah wakati wa utawala wa Marwaan bin Al-Hakam. Alifariki mwaka 59 H na akazikwa Al-Baqi’.

 

[2] Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy: Jina lake ni Sa’d bin Maalik bin Sinan Al-Khazraj Al-Answaar. Alikuwa miongoni mwa Swahaba wasomi. Alipokea Hadiyth nyingi, na alitoa rai za kidini kwa muda fulani. Alifariki mwanzoni mwa mwaka wa 74H akiwa na umri wa miaka 86.

 

[3] Imepokewa na Ahmad, At-Tirmidhiy, na Abuu Daawud kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema maneno hayo katika kujibu swali kuhusu kisima cha Buda’a, kilicho karibu na Madiynah, na daima kilijaa uchafu. Kilikuwa kwenye eneo lililo chini, na maji ya mvua yalikuwa yanapeleka uchafu na takataka kisimani. Maneno haya bila shaka yanakihusu.

 

[4] Abuu Umaamah Al-Baahiliy: Jina lake halisi ni Suday bin Ajlaan akiwa ni mmoja wa Swahaba waliopokea Hadiyth nyingi. Aliishi Misri, kisha akahamia Hims (sasa iko Syria), na akafia kule akiwa na umri wa miaka 81 au 86.

 

[5] Baadhi ya watu wamehoji kwamba, maji yanaweza kupunguka au kuongezeka wingi wake ikiwa huo uchafu au taka zitabadili moja ya sifa zake hizo tatu (rangi, harufu na ladha), na hapo maji yatanajisika. Lakini maoni sahihi katika maudhui haya ni kuwa, iwapo maji yako chini ya kilo 227 (Qulla mbili), basi taka yoyote inayanajisi maji, iwe imebadilisha moja ya sifa zake au laa. Lakini ikiwa maji yana kilo 227, hayanajisiki mpaka ibadilike mojawapo kati ya sifa zake hizo tatu.

[6] ‘Abdullaah bin ‘Umar alikuwa miongoni mwa wenye kuipa nyongo dunia na mwenye elimu kubwa sana. Alisilimu Makkah wakati akingali kijana mdogo na akahamia Madiynah. Kwanza alishiriki katika vita vya Khandaq, na akafariki mnamo mwaka 73H, akazikwa kule Dhi-Twuwaa.

 

[7] Qulla ni mtungi mkubwa wa udongo unaoweza kuwa na maji yapatayo viriba viwili na nusu, yaani kilo 113.

 

[8] Hii inahusu maji kidogo. Iwapo maji ni mengi, yatahesabika kama maji yanayokwenda au kutiririka, ambayo si machafu na ni mazuri kwa kuogea. Imekatazwa kukojolea maji yaliyosimama ardhini, na kwamba mtu asifanye hivyo ili asizowee kuchafua maji. Maji yanayotiririka kila mara huwa masafi; na hayanajisiki kwa kutiwa takataka au uchafu.

 

[9] Huyu ni mmoja wa Swahaba, na kutokutajwa jina lake hakuiathiri Hadiyth kwa kuwa Swahaba wote walikuwa waaminifu kabisa.

 

[10] Ibn ‘Abbaas: Huyu ndiye ‘Abdullaah bin ‘Abbaas bin ‘Abdul-Mutwalib, binammi wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na Mwanazuoni wa Ummah wa Kiislaam, aliyezaliwa miaka 3 kabla ya Hijrah na akafariki mnamo mwaka 67 A.H.

 

[11] Hadiyth hii inaonekana kama inapingana na ya kwanza, lakini sivyo, kwani amri si ya kukataza moja kwa moja, bali ni mapendekezo ya kukataza ili kuepuka mabaki yoyote ya uchafu.

 

[12] Ieleweke kwamba, kukosha tu uchafu katika chombo, si lazima kuwe mara saba. Falsafa ya kukiosha kitu kikawaida ni tofauti na kukiosha uchafu mahsusi. Madaktari wa zama hizi wanasema kuwa aghalabu katika matumbo ya mbwa huwa kuna viini vya maradhi na minyoo ipatayo urefu wa milimita 4, na hivi hutoka pamoja na kinyesi na hujishikiza kwenye nywele zizungukazo duburi ya mbwa. Mbwa hujisafisha duburi kwa ndimi zao, huchukua viini na minyoo hiyo, na pindi anapolamba chombo au ukimbusu kinywa chake (kama wazungu wafanyavyo). Viini hivi huhamia kwenye chombo au kwenye mdomo wa mtu anayembusu mbwa, na hatimaye huingia tumboni mwa mwana Aadam, na huweza kupenya mpaka kwenye seli za damu na kusababisha magonjwa yanayoweza hata kuua. Kwa kuwa viini hivi havionekani bila darubini. Shariy’ah ya Kiislaam iliamuru kuwa mate ya mbwa kwa ujumla ni najsi, na chochote kinachonajisiwa na mate ya mbwa ni sharti kioshwe mara saba (7), moja ya mara hizi saba, iwe kwa udongo ili kuwa na hakika wa usafi wake. Ili uyajue vyema maudhui haya, tafadhali soma tanbihi chini ya ukurasa wa kitabu cha Ahkaamul-Ahsan, Sharh ’Umdatul Ahkaam.

 

[13] Huyu Abuu Qatada ndiye Al-Haarith bin Rib’I Al Answaar, mwangalizi wa farasi wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alipigana katika vita vya Uhud, na vita vingine vilivyofuatia. Inasemekana kuwa alifariki Madiynah au Kufa mnamo mwaka 54 A.H.

 

[14] Anas bin Maalik alikuwa mtumishi wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kutoka wakati alipokwenda Madiynah mpaka alipofariki. Anajulikana kwa jina la Abuu Hamzah na alikuwa Mkhazrajiy. Aliishi kule Basra wakati wa ukhalifa wa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), na akafariki kule akiwa na umri wa miaka 99 au 103, mnamo mwaka wa 91 au 92 au 93 A.H.

 

[15] Hadiyth hii inathibitisha kwamba, mchanga au udongo husafika ukikauka, kama Abuu Shaybah alivyopokea, hususan iwapo utamwagia maji na yatiririke juu ya mahali palipokojolewa.

 

[16] Ni wazi kutoka katika Hadiyth hii kwamba endapo inzi kadondokea katika maji au kinywaji, hakitafanywa kichafu, sawa na viumbe vya familia hii ambayo damu yake haitembei, kama mbu, dondola na buibui, hawakifanyi kinywaji kiwe kichafu wakidondokea au kufia humo.

 

[17] Jina halisi la Abuu Waqiyd ni Al-Haarith bin ‘Awf, na kizazi cha Banu ‘Aamir bin Layth. Alisilimu mapema sana na anahesabika kuwa ni mtu wa Madiynah. Inasemekana kwamba alipigana katika vita vya Badr, aliishi Makkah, na akafariki Makkah mnamo mwaka 65 au 68 A.H alipokuwa na miaka 57, na akazikwa Funj.

 

 

Share

02-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah: Mlango Wa Vyombo Vya Chakula, Kunywea Na Kutawadhia

بلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتابُ الطَّهارَة

Kitabu Cha Twahaarah

 

بَابُ الْآنِيَةِ

02-Mlango Wa Vyombo Vya Chakula, Kunywea Na Kutawadhia

 

 

 

 

14.

عَنْ حُذَيْفَةَ بْنِ الْيَمَانِ رَضِيَ الْلَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏{ لَا تَشْرَبُوا فِي آنِيَةِ الذَّهَبِ والْفِضَّةِ، وَلَا تَأْكُلُوا فِي صِحَافِهَا، فَإِنَّهَا لَهُمْ فِي الدُّنْيَا، وَلَكُمْ فِي الْآخِرَةِ } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Hudhayfah bin Al Yamaaniy[1] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msinywe katika vyombo vya fedha na vya dhahabu na wala msile katika sahani zake[2], kwani hivyo ni vya wasioamini humu duniani na ni vyenu Aakhirah.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

15.

وَعَنْ أُمِّ سَلَمَةَ رَضِيَ الْلَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ الْلَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{ الَّذِي يَشْرَبُ فِي إِنَاءِ الْفِضَّةِ إِنَّمَا يُجَرْجِرُ فِي بَطْنِهِ نَارَ جَهَنَّمَ } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Ummu Salamah[3] (رَضِيَ اللهُ عَنْهَا) amesema kuwa: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika anayekunywa katika vyombo vya fedha anameza moto wa Jahannam tumboni mwake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

16.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ الْلَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ الْلَّهِ  صلى الله عليه وسلم ‏{ إِذَا دُبِغَ الْإِهَابُ فَقَدْ طَهُرَ } أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ‏ .‏

 

وَعِنْدَ الْأَرْبَعَةِ: { أَيُّمَا إِهَابٍ دُبِغَ {

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُما) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ngozi ikitengezwa, imetoharika[4].”   [Imetolewa na Muslim]

 

Na kwa Al-Arba’ah: “Ngozi yoyote iliyotengenezwa.”

 

 

 

17.

وَعَنْ سَلَمَةَ بْنِ الْمُحَبِّقِ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ الْلَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{ دِبَاغُ جُلُودِ الْمَيْتَةِ طُهُورُهاَ } صَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ 

Kutoka kwa Salamah bin Al-Muhabbiq[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kuisafisha ngozi ya maiti ni kuitakasa kwake.” [Ameisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

18.

وَعَنْ مَيْمُونَةَ رَضِيَ الْلَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ: مَرَّ رَسُولُ الْلَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏بِشَاةٍ يَجُرُّونَهَا، فَقَالَ: {لَوْ أَخَذْتُمْ إِهَابَهَا؟} فَقَالُوا: إِنَّهَا مَيْتَةٌ، فَقَالَ: {يُطَهِّرُهَا الْمَاءُ وَالْقَرَظُ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ

Kutoka kwa Maymuwnah (رَضِيَ اللهُ عَنْهَا) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipita mbele ya watu wanaoburuza mbuzi akasema: “Lau mgelichukua ngozi yake.” Wakasema: “Huyo ni maiti.” Akasema: “Maji na qaradh huitakasa (ngozi hiyo).” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy]

 

 

19.

وَعَنْ أَبِي ثَعْلَبَةَ الْخُشَنِيِّ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ الْلَّهِ، إِنَّا بِأَرْضِ قَوْمٍ أَهْلِ كِتَابٍ، أَفَنَأْكُلُ فِي آنِيَتِهِمْ؟ فَقَالَ: {لَا تَأْكُلُوا فِيهَا، إِلَّا أَنْ لَا تَجِدُوا غَيْرَهَا، فَاغْسِلُوهَا، وَكُلُوا فِيهَا } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Tha’labah Al-Khushaniyyi[6] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Niliuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Tunaishi katika nchi inayokaliwa na Ahlul-Kitaab. Je tunaweza kula katika vyombo vyao? Akasema: “Msile katika vyombo vyao[7], isipokuwa msipopata vingine, hapo basi viosheni na mle katika vyombo hivyo.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

20.

وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ الْلَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ النَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏وَأَصْحَابَهُ تَوَضَّئُوا مِنْ مَزَادَةِ اِمْرَأَةٍ مُشْرِكَةٍ.‏ مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، فِي حَدِيثٍ طَوِيلٍ

Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn[8] (رضي الله عنهما)  amesema kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  na Swahaba zake walitawadha kutoka kwenye maji ya kiriba cha ngozi[9] cha mwanamke mshirikina.” [Al-Bukhaariy, Muslim] [Hii ni sehemu ya Hadiyth ndefu]

 

 

21.

وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ‏ رضى الله عنه ‏ أَنَّ قَدَحَ النَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏اِنْكَسَرَ، فَاتَّخَذَ مَكَانَ الشَّعْبِ سِلْسِلَةً مِنْ فِضَّةٍ.‏ أَخْرَجَهُ الْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba: “Jagi la Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  lilivunjika, akaziba penye mwanya kwa mnyororo wa fedha.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

 

[1] Hudhayfah alipewa jina la utani la Abuu ‘Abdillaah. Yeye na baba yake walikuwa Swahaba. Alikuja kuwa maarufu kwa kuwa msiri wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alifariki Midian (Madain) siku arubaini baada ya kuuliwa ‘Uthmaan katika mwaka wa 35 au 36.H.

 

[2] Hadiyth hii imetajwa hapa kwa madhumuni kuwa, iwapo imekatazwa kunywa au kula kwenye vifaa vya metali hizo, basi kutawadhia vyombo vya metali hizo kumekatazwa, vinginevyo Hadiyth hii ingewekwa katika Mlango wa Kula na Kunywa. Lakini kula na kunywa katika vifaa vilivyopambwa na almasi na rubi inaruhusiwa.

 

[3] Ummu Salamah ni Hindi bint Abiy ‘Umaiyyah. Aliolewa na Abuu Salamah, akahajiri naye hadi Uhabeshi (Ethiopia), na akaja naye hadi Madiynah. Abuu Salamah alipofariki kutokana na jeraha alilolipata katika vita vya Uhud, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuoa mnamo Shawwaal mwaka 4 A.H. Yasemekana kuwa alifariki mwaka 59 au 62 A.H akiwa na umri wa miaka 84, na akazikwa Al-Baqi’.

 

[4] Hadiyth hii inathibitisha kuwa ngozi ikishapitia kwa ufundi wa kiwandani (tasnia), huwa inakuwa safi na nadhifu, inaweza kuwa ni ngozi ya mnyama aliye haraam au halaal kuliwa, na kama mnyama huyo alichinjwa au amekufa mwenyewe. Lakini ngozi za wana Aadam na baadhi ya wanyama ni haraam na haziruhusiwi kutumika. Ngozi ya mwana Aadam ni haraam kwa sababu ya utukufu wake. Na ngozi za wanyama kama mbwa au nguruwe ni haraam kwa sababu wamezaliwa najisi na wachafu. Sharti ikumbukwe kwamba nywele, meno na pembe za wanyama walioruhusiwa pia ni halaal kutumika na kwa biashara.

 

[5] Salamah alipewa jina la utani la Abuu Sinaan wa kabila la Hudhayl. Alihesabika kuwa ni mkazi wa Basra, na Al-Hasan Al-Basr alipokea Hadiyth hii toka kwake.

 

[6] Abuu Tha’labah ni Swahaba aliyetokana na kizazi cha Khushayn bin An-Nimir wa kabila la Quda’a. Alikuwa mmoja wa Swahaba wa Asw-haab Ash-Shajarah waliombai Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) siku ya Al-Hudaibiyyah. Alitumwa kwa watu wake na wote wakasilimu. Aliishi Shaam na akafariki kule mwaka 75 A.H.

 

[7] Hadiyth hii inaweka wazi kuwa, endapo vipo vyombo vya Muislaam, basi visitumike vya asiye Muislaam kwa kula, kupikia chakula, wala kunywea vinywaji. Iwapo kuna uhakika kuwa asiye Muislaam havitumii vyombo vile kwa kula au kunywa vitu haraam, basi vyombo vyake hivyo vinaweza kutumika; lakini hata hivyo sharti kuwa na tahadhari.

 

[8] ‘Imraan alipewa jina la utani la Abuu Nujayd, na anatoka katika kabila la Khuza’a. alisilimu mnamo mwaka wa Khaybar. Alilelewa na kuishi Basra, na akafia hapo mnamo mwaka 52 au 53 A.H.

 

[9] Hadiyth hii inaweka wazi kuwa, vyombo kama hivyo vya waabuduo miungu wengi, vinaweza kutumika bila kusita, kukiwa hakuna uwezekano wa vyombo hivyo kuwa si visafi.

 

 

 

 

Share

03-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah:Mlango Wa Kuondosha Najisi Na Ubainifu Wake

بلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتابُ الطَّهارَة

Kitabu Cha Twahaarah

 

 

بَابُ إِزَالَةِ اَلنَّجَاسَةِ وَبَيَانِهَا

03-Mlango Wa Kuondosha Najisi Na Ubainifu Wake

 

 

 

 

22.

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: سُئِلَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏عَنْ اَلْخَمْرِ تُتَّخَذُ خَلًّا؟ قَالَ: { لَا} أَخْرَجَهُ مُسْلِم ٌ 

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliulizwa kuhusu kutengeneza siki kutokana na mvinyo. Akasema: “Hapana[1].” [Imetolewa na Muslim]

 

 

23.

وَعَنْهُ قَالَ: لَمَّا كَانَ يَوْمُ خَيْبَرَ، أَمَرَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏أَبَا طَلْحَةَ، فَنَادَى:  {إِنَّ اَللَّهَ وَرَسُولَهُ يَنْهَيَانِكُمْ عَنْ لُحُومِ اَلْحُمُرِ اَلْأَهْلِيَّةِ، فَإِنَّهَا رِجْسٌ } مُتَّفَقٌ عَلَيْه ِ

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Katika siku ya Khaybar, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuamrisha Abuu Twalhah[2] kutangaza: “Hakika Allaah na Rasuli Wake wamekukatazeni kula nyama ya punda vihongwe kwa kuwa ni najisi.[3][Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

24.

وَعَنْ عَمْرِو بْنِ خَارِجَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {خَطَبَنَا رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏بِمِنًى وَهُوَ عَلَى رَاحِلَتِهِ، وَلُعَابُهَا يَسِيلُ عَلَى كَتِفَيَّ }  أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ  وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَه ُ

Kutoka kwa ‘Amr bin Khaarijah[4] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitukhutubia kule Minna huku akiwa juu ya kipando chake, na mate yake yanachuruzika mabegani[5] mwangu.” [Imetolewa na Ahmad na ameisahihisha At-Tirmidhiy]

 

 

25.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: { كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَغْسِلُ اَلْمَنِيَّ، ثُمَّ يَخْرُجُ إِلَى اَلصَّلَاةِ فِي ذَلِكَ اَلثَّوْبِ وَأَنَا أَنْظُرُ إِلَى أَثَرِ اَلْغُسْلِ فِيهِ } مُتَّفَقٌ عَلَيْه ِ

وَلِمُسْلِمٍ: { لَقَدْ كُنْتُ أَفْرُكُهُ مِنْ ثَوْبٍ رَسُولِ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏فَرْكًا، فَيُصَلِّي فِيهِ }

وَفِي لَفْظٍ لَهُ: { لَقَدْ كُنْتُ أَحُكُّهُ يَابِسًا بِظُفُرِي مِنْ ثَوْبِهِ }

Kutoka kwa ‘Aaishah[6] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiosha manii[7], na kisha alikuwa akielekea katika Swalaah na nguo hiyo, nami nilikuwa naona mabaki ya athari za maosho ndani yake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na katika Muslim: “Nilikuwa nikikwangua (manii) kutoka kwenye nguo ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mkwanguo na huswali na nguo hiyo.”

Na katika riwaayah nyengine ya Muslim: “Mimi (‘Aaishah) nilikuwa nayakwangua kwa kucha yangu hali ya kuwa yamekauka.”

 

 

26.

وَعَنْ أَبِي اَلسَّمْحِ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{ يُغْسَلُ مِنْ بَوْلِ اَلْجَارِيَةِ، وَيُرَشُّ مِنْ بَوْلِ اَلْغُلَامِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ وَالنَّسَائِيُّ وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِم ُ

Kutoka kwa Abuu As-Samh[8] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mkojo wa mtoto mchanga wa kike uoshwe, na mkojo wa mtoto wa kiume unyunyiziwe maji[9].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na ameisahihisha Al-Haakim]

 

 

27.

وَعَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ أَبِي بَكْرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ ‏فِي دَمِ اَلْحَيْضِ يُصِيبُ اَلثَّوْبَ‏: { تَحُتُّهُ ثُمَّ تَقْرُصُهُ بِالْمَاءِ ثُمَّ تَنْضَحُهُ ثُمَّ تُصَلِّي فِيهِ } مُتَّفَقٌ عَلَيْه ِ

Kutoka kwa Asmaa’ bint Abiy Bakar[10] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema kuhusu damu ya hedhi inayodondokea nguo: “Aikwangue, aifikiche na maji, na kisha aioshe, na kisha aswali na nguo hiyo.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

28.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَتْ خَوْلَةُ: { يَا رَسُولَ اَللَّهِ، فَإِنْ لَمْ يَذْهَبْ اَلدَّمُ، قَالَ: "يَكْفِيكِ اَلْمَاءُ، وَلَا يَضُرُّكِ أَثَرُهُ" } أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَسَنَدُهُ ضَعِيف ٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Khawlah[11] aliuliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Je, endapo alama ya damu haitatoweka?” Akasema: “Maji yanakutosha, na athari yake haitokuathiri chochote.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy, na Isnaad yake ni dhaifu]

 

 

 

[1] Kutengeneza siki kwa kuongeza vitu kwenye mvinyo kumekatazwa.

 

[2] Abuu Twalhah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) ndiye Zayd bin Sahl bin Al-Aswad bin Haraam Al-Answaar An-Najaar, ambaye alikuwa ni mmoja wa Swahaba waandamizi. Alihudhuria Bay’atul-‘Aqabah na vita vyote.

Alipigana kishujaa wakati wa Vita Vya Uhud na akamhami Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mpaka mkono wake ukapooza. Pia aliua watu ishirini katika Vita Vya Hunayn. Akijulikana kwa Abuu Twalha Al-Answaawiry na alikuwa ni mume wa Ummu Sulaym ambaye alitaka mahari yake yawe ni kusilimu kwake. Wawili hawa walikuwa wakarimu mno na wenye iymaan za hali ya juu. Walikuwa na visa vizuri vyenye mafunzo na vya kusisimua, na hata kisa chake kimoja cha kupokea wageni kilikuwa ni sababu ya kuteremshwa kauli ya Allaah (عز وجل):

 وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ

 Na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji. [Al-Hashr: 9]

 

Alifariki mwaka 34 au 51 A.H.

 

[3] Hadiyth hii ni dalili kuwa nyama ya punda vihongwe ni haraam.

 

[4] ‘Amr ndiye ‘Amr bin Kharija bin Al-Muntafiq Al-Asad. Alikuwa rafiki wa Abuu Sufyaan. Anahesabika kuwa alitokana na ukoo wa Al-Ash’ar. Yeye ni miongoni mwa Swahaba waliolowea Sham, na Hadiyth yake iliripotiwa na watu wa Basra.

 

[5] Kutoka katika Hadiyth hii tunatambua kuwa mate ya mnyama ambaye ni halaal (kuliwa) ni masafi. Hadiyth hii iliafikiwa na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).

 

[6] ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) ni binti wa Abuu Bakar Asw-Swiddiyq (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) aliyeolewa na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) miaka miwili kabla ya Hijrah (kuhama) mnamo mwezi wa Shawwaal, lakini akaanza kuishi naye mnamo mwaka wa 1 A.H wakati akiwa na umri wa miaka 9. Alikuwa msomi sana na aliripoti Hadiyth nyingi. Alifariki mnamo tarehe 17 mwezi wa Ramadhwaan mwaka 57 au 58 A.H. Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimswalia Swalaah ya Janaazah, na akazikwa Al-Baq’.

 

[7] Kuna kutofautiana maoni kuhusu manii ya mwana Aadam, kama ni safi au siyo safi. Wanazuoni wengine wanayahesabu kama mate au makamasi, na kwa mujibu wa wengine ni lazima kuyaosha. Kundi hilo la kwanza linatoa sababu yake katika Hadiyth ya kuwa huwa yanakwanguliwa yakikauka, na kundi la pili linatoa sababu yake kutoka kwenye Hadiyth ya kuyaosha. Kwa hakika manii ni najsi, na lazima yasafishwe kwa kuyaosha, kuyakwangua au kuyapangusa. (Tazama kitabu cha Niyl Al-Awtwaar cha Imaam Shawkaaniy).

 

[8] Abuu As-Samh jina lake halisi ni Iyyaad. Alikuwa ni mtumwa aliyeachwa huru na akawa mtumishi wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Ibn Abdil-Barr alisema aliripotiwa kwamba alipotea na hakuna anayejua alifia wapi au lini.

 

[9] Hii inamaanisha kuwa ipo tofauti baina ya mkojo wa msichana na mvulana. Katika wakati wa kunyonya, mkojo wa mvulana ni msafi zaidi kuliko mkojo wa msichana.

 

[10] ‘Asmaa ni Mama wa ‘Abdullaah bin Az-Zubayr na ni dada mkubwa wa ‘Aaishah. Alisilimu mapema sana kule Makkah na akahamia Madiynah. Alifariki chini ya mwezi mmoja baada ya kuuliwa mwanawe Ibn Az-Zubayr mnamo mwaka 73 A.H akiwa na umri wa miaka 100, nab ado hakung’oa jino hata moja wala kuharibika akili kwa uzee.

 

[11] Khawlah bint Yaasir alikuwa Swahaba, na Abu Salamah bin ‘Abdir-Rahmaan alisimulia Hadiyth hiyo kutoka kwake.

 

Share

04-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah:Mlango Wa Wudhuu

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتابُ الطَّهارَة

Kitabu Cha Twahaarah

 

بَابُ اَلْوُضُوءِ

04-Mlango Wa Wudhuu

 

 

 

 

29.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: { لَوْلَا أَنْ أَشُقَّ عَلَى أُمَّتِي لَأَمَرْتُهُمْ بِالسِّوَاكِ مَعَ كُلِّ وُضُوءٍ } أَخْرَجَهُ مَالِكٌ، وأَحْمَدُ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة َ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Lau nisingeuogopea uzito ummah wangu, ningeliwaamrisha mswaki[1] kabla ya kila Swalaah.” [Imetolewa na Maalik, Ahmad na An-Nasaaiy. Akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

30.

وَعَنْ حُمْرَانَ; { أَنَّ عُثْمَانَ ‏ رضى الله عنه ‏ دَعَا بِوَضُوءٍ، فَغَسَلَ كَفَّيْهِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ مَضْمَضَ، وَاسْتَنْشَقَ، وَاسْتَنْثَرَ، ثُمَّ غَسَلَ وَجْهَهُ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ غَسَلَ يَدَهُ اَلْيُمْنَى إِلَى اَلْمِرْفَقِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ اَلْيُسْرَى مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ مَسَحَ بِرَأْسِهِ، ثُمَّ غَسَلَ رِجْلَهُ اَلْيُمْنَى إِلَى اَلْكَعْبَيْنِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ اَلْيُسْرَى مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ قَالَ: رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَوَضَّأَ نَحْوَ وُضُوئِي هَذَا‏ } مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa Humraan[2] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) mtumwa aliyeachwa huru na ‘’Uthmaan[3] amesema kuwa: “’Uthmaan alitaka maji ya kutawadhia. Akaosha viganja vyake mara tatu, kisha akasukutua na akatia maji puani, na kisha akapenga. Kisha akaosha uso wake mara tatu. Kisha akaosha mkono wake wa kuume hadi kwenye kiwiko cha mkono wake (fundo kati ya kiganja na bega) mara tatu[4], kisha akauosha hivyo hivyo mkono wake wa kushoto. Kisha akapaka maji kichwa chake. Kisha akauosha mguu wake wa kuume hadi kwenye vifundi viwili mara tatu, kisha akauosha mguu wake wa kushoto hivyo hivyo. Kisha akasema: Nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akitawadha mfano wa wudhuu wangu huu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

31.

وَعَنْ عَلِيٍّ ‏ رضى الله عنه ‏ ‏فِي صِفَةِ وُضُوءِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ‏ قَالَ: { وَمَسَحَ بِرَأْسِهِ وَاحِدَةً.‏ } أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُد

Kutoka kwa ‘Aliy[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuhusu wasifu wa wudhuu wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuwa: “Nabiy alipangusa kichwa chake kwa maji mara moja tu[6].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd]

 

 

 

32.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ زَيْدٍ بْنِ عَاصِمٍ ‏ رضى الله عنه ‏ ‏فِي صِفَةِ اَلْوُضُوءِ‏ قَالَ: { وَمَسَحَ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏بِرَأْسِهِ، فَأَقْبَلَ بِيَدَيْهِ وَأَدْبَرَ.‏ } مُتَّفَقٌ عَلَيْه

وَفِي لَفْظٍ: { بَدَأَ بِمُقَدَّمِ رَأْسِهِ، حَتَّى ذَهَبَ بِهِمَا إِلَى قَفَاهُ، ثُمَّ رَدَّهُمَا إِلَى اَلْمَكَانِ اَلَّذِي بَدَأَ مِنْهُ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Zayd bin ‘Aaswim[7] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema akielezea sifa ya wudhuu: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipangusa kichwa chake kutoka katika paji la uso mpaka kisogoni na kisha mpaka kwenye paji la uso[8].” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika riwaayah nyengine ya Al-Bukhaariy na Muslim: “Ameanza mwanzo wa kichwa chake kwa mikono yake hadi akaipeleka kisogoni mwake, kisha akairudisha mahali alipoanza.”

 

 

 

33.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا ‏فِي صِفَةِ اَلْوُضُوءِ‏ قَالَ: { ثُمَّ مَسَحَ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏بِرَأْسِهِ، وَأَدْخَلَ إِصْبَعَيْهِ اَلسَّبَّاحَتَيْنِ فِي أُذُنَيْهِ، وَمَسَحَ بِإِبْهَامَيْهِ ظَاهِرَ أُذُنَيْهِ‏ } أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr[9] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuhusu sifa za wudhuu: “Kisha Rasuli wa Alllaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipangusa kichwa chake, akaingiza vidole vyake vya Shahaadah katika masikio yake, na akapangusa nje ya masikio yake kwa vidole gumba.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na ameisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

34.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{ إِذَا اِسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ مَنَامِهِ فَلْيَسْتَنْثِرْ ثَلَاثًا، فَإِنَّ اَلشَّيْطَانَ يَبِيتُ عَلَى خَيْشُومِهِ } مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakapoamka mmoja wenu usingizini, apenge pua mara tatu, kwani  shaytwaan hulala kwenye mionzi ya pua[10] yake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

35.

وَعَنْهُ: { إِذَا اِسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ نَوْمِهِ فَلَا يَغْمِسُ يَدَهُ فِي اَلْإِنَاءِ حَتَّى يَغْسِلَهَا ثَلَاثًا فَإِنَّهُ لَا يَدْرِي أَيْنَ بَاتَتْ يَدَهُ } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.‏ وَهَذَا لَفْظُ مُسْلِم

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Rasuli wa Allah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Akiamka mmoja wenu usingizini, asizamishe mikono yake katika chombo chochote, hadi aioshe mara tatu[11], kwani hajui mkono wake ulilala wapi.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

36.

وَعَنْ لَقِيطِ بْنُ صَبْرَةَ، ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{أَسْبِغْ اَلْوُضُوءَ، وَخَلِّلْ بَيْنَ اَلْأَصَابِعِ، وَبَالِغْ فِي اَلِاسْتِنْشَاقِ، إِلَّا أَنْ تَكُونَ صَائِمًا } أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة

وَلِأَبِي دَاوُدَ فِي رِوَايَةٍ: { إِذَا تَوَضَّأْتَ فَمَضْمِضْ }

Kutoka kwa Laqiytw bin Swabrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Tawadha kikamilifu, na pitisha kati ya vidole vyako vya mikono na miguu[12], zidisha katika kuyapandisha maji puani isipokuwa utakapokuwa uko katika Swawm.” [Imetolewa na Al-Arba’ah; Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah na  ameisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

Na katika riwaayah ya Abuu Daawuwd: “Ukitawadha, sukutua mdomo wako.”

 

 

 

37.

وَعَنْ عُثْمَانَ ‏ رضى الله عنه ‏ { أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏كَانَ يُخَلِّلُ لِحْيَتَهُ فِي اَلْوُضُوءِ } أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة

Kutoka kwa ‘Uthmaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akitawadha, alikuwa akipitisha vidole kati ya ndevu[13] zake.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na ameisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

38.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ زَيْدٍ ‏ رضى الله عنه ‏ { أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏أَتَى بِثُلُثَيْ مُدٍّ، فَجَعَلَ يَدْلُكُ ذِرَاعَيْهِ } أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Zayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliletewa thuluthi mbili za Mudd[14] (kibaba cha maji), akawa anasugua mikono yake.” [Imetolewa na Ahmad na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

39.

وَعَنْهُ، { أَنَّهُ رَأَى اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَأْخُذُ لِأُذُنَيْهِ مَاءً غَيْرَ اَلَّذِي أَخَذَ لِرَأْسِهِ.‏ } أَخْرَجَهُ اَلْبَيْهَقِيّ

وَهُوَ عِنْدَ "مُسْلِمٍ" مِنْ هَذَا اَلْوَجْهِ بِلَفْظٍ: وَمَسَحَ بِرَأْسِهِ بِمَاءٍ غَيْرَ فَضْلِ يَدَيْهِ، وَهُوَ اَلْمَحْفُوظ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Zayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Alimuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akichukua maji kupangusa masikio, tofauti na maji aliyopangusia kichwa.” [Imetolewa na Bayhaqqiy]

Na katika riwaayah ya Muslim: “Alipangusa kichwa chake kwa kuchukua maji yasiyokuwa yaliyosalia kutoka katika maji ya kuoshea mikono.” [Hadithi hii ni Mahfuwdh]

 

 

 

40.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: سَمِعْتَ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَقُولُ: { "إِنَّ أُمَّتِي يَأْتُونَ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ غُرًّا مُحَجَّلِينَ، مِنْ أَثَرِ اَلْوُضُوءِ، فَمَنْ اِسْتَطَاعَ مِنْكُمْ أَنْ يُطِيلَ غُرَّتَهُ فَلْيَفْعَلْ.‏ } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِم

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Ummah wangu utakuja siku ya Qiyaamah na viungo vinavyong’aa (nyuso, mikono, miguu) kwa sababu ya alama za wudhuu, basi mwenye kuweza miongoni mwenu kuirefusha mng’aro wake[15], basi afanye hivyo.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

41.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: { كَانَ اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يُعْجِبُهُ اَلتَّيَمُّنُ فِي تَنَعُّلِهِ، وَتَرَجُّلِهِ، وَطُهُورِهُ، وَفِي شَأْنِهِ كُلِّهِ.‏ } مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anapendezwa sana na kuanza na upande wa kuume katika kuvaa kwake viatu; na katika kuchana nywele, na katika kujitwaharisha kwake, na katika mambo yote[16].” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

42.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{ إِذَا تَوَضَّأْتُمْ فابدأوا بِمَيَامِنِكُمْ } أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mnapotawadha, anzeni kulia kwenu.” [Imetolewa na Al-Arba’ah; Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah  na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

43.

وَعَنْ اَلْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةٍ ‏ رضى الله عنه ‏ { أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏تَوَضَّأَ، فَمَسَحَ بِنَاصِيَتِهِ، وَعَلَى اَلْعِمَامَةِ وَالْخُفَّيْنِ‏ } أَخْرَجَهُ مُسْلِم

Kutoka kwa Al-Mughiyrah bin Shu’bah[17] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitawadha na akawa ni mwenye kupangusa maji utosi wake na juu ya kilemba, na juu ya soksi (khofu) mbili za ngozi[18].” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

44.

وَعَنْ جَابِرٍ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا ‏فِي صِفَةِ حَجِّ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ‏ قَالَ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{ اِبْدَؤُوا بِمَا بَدَأَ اَللَّهُ بِهِ } أَخْرَجَهُ النَّسَائِيُّ، هَكَذَا بِلَفْظِ اَلْأَمْر ‏ وَهُوَ عِنْدَ مُسْلِمٍ بِلَفْظِ اَلْخَبَر

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah[19] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuhusu Hijjah ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anzeni kwa Alichoanza nacho Allaah[20].” [Imetolewa na An-Nasaaiy kwa tamshi hili la amri na imepokewa na Muslim kwa tamko la Al-Khabar[21]]

 

 

 

45.

وَعَنْهُ قَالَ: { كَانَ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏إِذَا تَوَضَّأَ أَدَارَ اَلْمَاءَ عَلَى مُرْفَقَيْهِ.‏ } أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ بِإِسْنَادِ ضَعِيف

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) anapotawadha hutiririsha maji hadi kwenye kiwiko.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

46.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{ لَا وُضُوءَ لِمَنْ لَمْ يَذْكُرِ اِسْمَ اَللَّهِ عَلَيْهِ } أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَابْنُ مَاجَهْ، بِإِسْنَادٍ ضَعِيف

وَلِلترْمِذِيِّ: عَنْ سَعِيدِ بْنِ زَيْد ٍ

وَأَبِي سَعِيدٍ نَحْوُه ُ

قَالَ أَحْمَدُ: لَا يَثْبُتُ فِيهِ شَيْء

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna wudhuu kwa asiyetaja Jina la Allaah wakati wa kutawadha[22].” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, na Ibn Maajah, kwa Isnaad dhaifu]

 

Na katika At-Tirmidhiy: “amepokea Hadiyth kama hiyo kutoka kwa Sa’iyd bin Zayd[23].”

Na Abuu Sa’iyd na Ahmad wamesema: “Hakujathibitika chochote ndani yake Hadiyth hiyo.”

 

 

 

47.

وَعَنْ طَلْحَةَ بْنِ مُصَرِّفٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ قَالَ: { رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَفْصِلُ بَيْنَ اَلْمَضْمَضَةِ وَالِاسْتِنْشَاقِ.‏ } أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادِ ضَعِيف

Kutoka kwa Twalhah bin Muswarrif[24] amemnukuu baba yake kwa upokezi wa babu yake[25] aliyesema: “Nimemuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akitenganisha kati ya kusukutua na kupandisha maji puani[26].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

48.

وَعَنْ عَلِيٍّ ‏ رضى الله عنه ‏ ‏فِي صِفَةِ اَلْوُضُوءِ‏ { ثُمَّ تَمَضْمَضَ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏وَاسْتَنْثَرَ ثَلَاثًا، يُمَضْمِضُ وَيَنْثِرُ مِنْ اَلْكَفِّ اَلَّذِي يَأْخُذُ مِنْهُ اَلْمَاءَ } أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ وَالنَّسَائِيّ

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuhusu wasifu wa kutawadha, “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisukutua kisha akavuta maji puani na kupenga mara tatu. Alisukutua na akapenga pua yake kwa kiganja kilekile alichochukulia maji.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nassaiy]

 

 

 

49.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ زَيْدٍ ‏ رضى الله عنه ‏ ‏فِي صِفَةِ اَلْوُضُوءِ‏ { ثُمَّ أَدْخَلَ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَدَهُ، فَمَضْمَضَ وَاسْتَنْشَقَ مِنْ كَفٍّ وَاحِدَةٍ، يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلَاثًا } مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Zayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuhusu wasifu wa kutawadha: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitumbukiza mkono wake (katika chombo), akasukutua na akapandisha maji puani kwa fumbo moja (maji). Alifanya hivyo mara tatu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

50.

وَعَنْ أَنَسٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: { رَأَى اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏رَجُلًا، وَفِي قَدَمِهِ مِثْلُ اَلظُّفْرِ لَمْ يُصِبْهُ اَلْمَاءُ.‏ فَقَالَ: "اِرْجِعْ فَأَحْسِنْ وُضُوءَكَ" } أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيّ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuona mtu katika unyayo wake kuna mfano wa kucha (baka) haikupata maji. Akamwambia: ‘Rejea vizuri wudhuu wako[27].’” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy]

 

 

 

51.

وَعَنْهُ قَالَ: { كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَتَوَضَّأُ بِالْمُدِّ، وَيَغْتَسِلُ بِالصَّاعِ إِلَى خَمْسَةِ أَمْدَادٍ } مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitawadha kwa kibaba[28] kimoja cha maji, na akikoga kwa pishi[29] moja hadi vibaba (Mudd) vitano.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

52.

وَعَنْ عُمَرَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{ مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ، فَيُسْبِغُ اَلْوُضُوءَ، ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ اَلْجَنَّةِ" } أَخْرَجَهُ مُسْلِم

وَاَلتِّرْمِذِيُّ، وَزَادَ: { اَللَّهُمَّ اِجْعَلْنِي مِنْ اَلتَّوَّابِينَ، وَاجْعَلْنِي مِنْ اَلْمُتَطَهِّرِينَ }

Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna yeyote miongoni mwenu anayetawadha vizuri, kisha akasema: “Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, wa ash-hadu anna Muhammad ‘Abduhuu wa Rasuwluhu” (Nashuhudia kuwa hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Peke Yake, hana mshirika, na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake) ila   atafunguliwa milango minane ya Jannah.” [Imetolewa na Muslim na At-Tirmidhiy]

At-Tirmidhiy aliongezea: “Allaahummaj-‘alniy minat-tawaabiyna Waj-‘alniy minal-mutatwahhiriyna (Ee Rabi! Nijaalie niwe miongoni mwa wenye kutubia na unijaalie niwe miongoni mwa wenye kujitwaharisha)”

 

 

 

[1] Hii inamaanisha kuwa matumizi ya mswaki kila mtu anapotawadha ni Sunnah, na Hadiyth hii iliyoripotiwa na Muslim inatuambia kwamba, ni sharti kutumia mswaki kabla ya kila Swalaah. Inamaanisha kuwa, haya tule anayekuenda kuswali na ‘udwuu ule ule aliotawadha safari iliyopita, hata hivyo sharti atumie mswaki. Ahadiyth hizi zinathibitisha mkazo mkubwa sana unaowekwa katika matumizi ya mswaki kila mara kwa ajili ya kusafisha meno. Hiyo ni Sunnah na siyo waajibu

 

[2] Humraan bin Aban alikamatwa na Khaalid bin Al-Waliyd katika vita wakati wa Ukhalifa wa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), naye akampeleka akamtumikie ‘Uthmaan ambaye alimuacha huru. Ni mwaminifu wa daraja la pili katika kuripoti Hadiyth. Alifariki mwano mwaka wa 75 A.H.

 

[3] ‘Uthmaan ni Khalifa wa tatu kati ya wanne walio wakuu au walioongozwa. Alisilimu mapema na akamuoa Ruqayyah bint wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na baada ya kufariki kwake akaozwa bint mwingine wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Ummu-Kulthum na hivyo anaitwa Dhun-Nurayn (yaani mwenye nuru mbili, maana yake mabinti wawili wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)). ‘Uthmaan aliuliwa shahidi siku ya Ijumaa tarehe 18 Dhul-Hijjah mwaka 35 A.H.

 

[4] Katika Hadiyth hii, kuosha uso, mikono na miguu, imetajwa kuwa vioshwe mara tatu kila kiuongo, lakini viungo vingine, inatosha kuviosha mara mbili au hata mara moja kila kiungo. Imaam Nawawi ameandika kuwa maafikiano ya pamoja ni kwamba kuosha mara moja ni faradhi yaani lazima.

 

[5] ‘Aliy ni Khalifa wa nne walioongozwa. Alipigana vita zote isipokuwa ya Tabuwk, kwa kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuacha akikaimu kule Madiynah. Mtu mmoja muovu aitwae ‘Abdur-Rahmaan bin Muljam, alimuua ‘Aliy akafa kama ni Shahidi asubuhi siku ya Ijumaa tarehe 17 mwezi Ramadhwaan mwaka 40 A.H huko Kufa.

 

[6] Hii maana yake ni kwamba kupangusa maji kichwa wakati wa kutawadha mara moja tu ndiyo faradha.

 

[7] ‘Abdullaah bin Zayd alikuwa Answaar (watu wa Madiynah waliowapokea Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na wenziwe wa Makkah waliohajiri Madiynah), aliyetoka kwa akina Bani Maazin kutoka katika ukoo wa An-Najaar. Alipigana katika vita vya Uhud alimuua Musailimah Al-Kadhdhaab na pia alimuua Wahshi mnamo Siku ya Al-Yamama. Aliuwawa mnamo siku ya Al-Harraah mnamo mwaka 63 A.H.

 

[8] Hadiyth hii inatuambia kupangusa maji (mas-h) kichwani sharti kuanzie mbele.

 

[9] ‘Abdullaah bin ‘Amr mwana wa ‘Amr bin Al-‘Aasw Al-Qurayshiy. Yeye alisilimu kabla ya babake ambaye alikuwa mkubwa kuliko yeye kwa miaka 13. Alikuwa ni ‘Aalim (msomi), alihifadhi Hadiyth na alikuwa mwenye taqwa sana. Alifariki mnamo mwaka 63 au 70 A.H.

 

[10] Kwa shaytwaan kulala ndani ya pua za mtu kunawezekana, lakini hali halisi inayotokea inajulikana na Mwenyewe Allaah (عز وجل)    na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Huenda huo ni usemi wa kimethali, kwa sababu kamasi mbaya hukusanyika puani na kusababisha uzembe, uvivu, kusahau au kupuuza. Hali hizi zote ni za kishaytwaan.

 

[11] Hii inamaanisha kuwa, mikono isitumbukizwe katika chombo cha maji ya kutawadhia, kwa kuwa neno “kutawadha” limo katika Hadiyth zilizoandikwa na Al-Bukhaariy. Ibn Hajar, katika kitabu chake cha Fat-h Al-Baariy amesema kuwa: “Ingawa Hadiyth hii inataja vyombo vya kutawadhia, lakini inajumuisha vyombo vyote vingine pamoja na vyombo vya kuogea. Lakini kukiweko bwawa kubwa au tanki la maji, basi inaruhusiwa kutumbukiza mkono humo.”

 

[12] Hii inamaanisha kuwa vidole vya mikononi na miguuni sharti vioshwe taratibu na kikamilifu.

 

[13] Wakati wa tendo la kutawadha, kuchanua ndevu zako kwa vidole vyako ni Sunnah na siyo lazima (wajibu).

 

[14] Katika Hadiyth zingine, Mudd kamili ni zaidi kidogo ya gram 600. Hii ndio idadi ndogo kuliko idadi zote zilizotajwa kwa ajili ya kutawadha, vinginevyo itakuwa tabu kubwa kutawadha kwa maji kidogo zaidi ya hivi. Hakijatajwa kiwango cha juu cha maji. Kiasi chochote cha maji kinaweza kutumika kwa kutawadha na kuoga, lakini inakatazwa kufanya israfu ya maji.

 

[15] Hii inaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Inaweza kumaanisha kuosha viungo zaidi ya kiwango cha chini, kwa mfano, kuosha mikono hadi mabegani, na kuosha miguu hadi magotini. Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) anaiafiki hii maana ya pili. Pia inaweza kumaanisha kuosha kila kiungo mara tatu, badala ya kuosha viungo kama vile viganja, mdomo na pua kwa uchache mara moja. Pia inaweza kumaanisha kutawadha tena na tena, au hata kubaki na wudhuu huo huo mmoja saa zote.

 

[16] Mtindo huu (wakuanzia kiungo cha kuume) wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), ulikuwa ni kwa matendo mema. Lakini kwa matendo mengine kama kuenda nje ya Msikiti, au kuingia chooni, ambapo mtu ni sharti atangulize mguu wa kushoto kwanza.

 

[17] Al-Mughiyrah ndiye Abuu ‘Abdillaah au Abuu Lisa. Al-Mughiyrah bin Shu’bah bin Mas-‘uwd Ath-Thaqaaf alikuwa Swahaba maarufu. Alisilimu mnamo mwaka wa vita ya Khandaq (Handaki), na akahajiri. Kwanza alishiriki katika vita ya Hudaybiyah. Alifariki mnamo mwaka 50 A.H. kule Kufa.

 

[18] Hadiyth hii inaweka wazi wazi kwamba, kupangusa maji kidogo juu ya kilemba (kofia) ni sahihi. Kuna aina mbili za tendo hili. Kwanza ni kupangusa kidogo juu ya kilemba na kidogo juu ya kichwa. Hakuna tofauti ya maoni juu ya tendo hili. Pili ni kupangusa juu ya kilemba peke yake. Kuna tofauti ya maoni kwa hili, lakini hii inathibitishwa pia na Hadiyth Swahiyh ya At-Tirmidhiy.

 

[19] Jaabir alikuwa Answaar aliyetoka katika ukoo wa Sulamiy, na alipewa jina la utani la Abuu ‘Abdillaah. Alikuwa mmoja wa Swahaba maarufu. Alipigana katika vita vya Badr, ingawa wengine wanasema kuwa hakuwahi kuishuhudia vita vya Badr wala ya Uhud, lakini alishiriki katika vita zilizofuata hizo. Pia alikuwako kule Siffin. Alikuwa mmoja wa watu waliohifadhi Hadiyth nyingi. Alipata upofu mnamo mwisho wa maisha yake, alifariki mnamo mwaka wa 74 A.H akiwa na umri wa miaka 94. Inasemekana kuwa yeye ndiye aliyekuwa Swahaba wa mwisho kufariki pale Madiynah.

 

[20] Qur-aan tukufu imetaja kwanza Asw-Swafaa katika kutaja Asw-Swafaa na Al-Marwaa. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliianza Saa’i (kutembea na kukimbia kati ya Asw-Swafaa na Al-Marwaa wakati wa kuhiji Hijjah kubwa (Hajj) na Hijjah ndogo (‘Umrah) kutokea upande wa Asw-Swafaa). Kwa hivyo anzeni kutawada kwa namna hiyo hiyo – kuanzia kuosha uso, kisha mikono mpaka katika kiwiko, kisha pangusa kichwa, na kisha osha miguu (kama alivyovifanya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)).

 

[21] Katika Hadiyth hii limetumika neno “bada-a” katika maandishi ya Kiarabu, kwa maana ya kutoa taarifa (kwa mfano naanza kwa) na siyo kwa kuamrisha (anza kwa).

 

[22] Kuhusu kadhia hii, zipo Ahaadiyth zinazopingana ambazo zinaashiria maoni yanayopishana kuhusu kuitamka “BismiLlaah” kabla ya kuanza kutawadha. Jibu sahihi la kadhia hii ni kusema kuwa, kutamka BismiLlaah ni Sunnah.

 

[23] Sa’iyd huyu ndiye Sa’iyd bin ‘Amr Al-Qurayshiy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), aliyepewa jina la utani la Abuu Al-A’war. Naye ni mmoja wa wale watu kumi waliyoahidiwa Al-Jannah. Alisilimu mapema sana, na akamuoa Faatwimah, dada wa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), na wote hawo (Faatwimah na Sa’iyd) walisababisha ‘Umar kujaaliwa na Allaah (عز وجل)    kusilimu. Alipigana vita vyote isipokuwa ya Badr, kwa sababu hakuwepo kwa kuwa alikuwa akiutafuta msafara. Alifariki mnamo mwaka 51 A.H na akazikwa Al-Baqi’.

[24] Huyu Twalhah ndiye Abuu Muhammad au Abuu ‘Abdillaah Twalhah bin Muswarrif. Alikuwa Taabi’ (mfuasi au mrithi ambaye alionana na au aliongozana na Swahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)) mtegemewa sana wa daraja la tano. Alikuwa ni mwenye taqwah na msomaji wa Qur-aan. Alifariki mnamo mwaka wa 112 A.H.  Baba yake Muswarrif, hajulikani na hilo limeifanya Hadiyth yake kuwa dhaifu.

 

[25] Babu wa Twalhah anaitwa Ka’b bin ‘Amr au ‘Amr bin Ka’b bin Juhdub Al-Yami anayetokana na kabila la Yemen linaloitwa Yam la Hamadan. Ibn ‘Abdil-Bar alisema kuwa, yeye (Ka’b) alilowea kule Kufa, naye ni Swahaba.

 

[26] Hii inamaanisha kwamba, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitwaa maji kwa mikupuo mbalimbali kwa kuosha pua na kusukutua mdomo. Kwa mujibu wa mwandishi, Hadiyth hii ni dhaifu. Kwa mujibu wa Al-Bukhaariy na Muslim, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitumia mkono mmoja tu wa maji kwa kuosha pua na kusukutua mdomo. Imaam Nawawi ameelezea aina zake tano, na akasema hiyo iliyotajwa na Al-Bukhaariy na Muslim ndiyo Swahiyh.

 

[27] Hadiyth hii inaweka wazi msimamo kwamba, kuuosha mguu mzima kikamilifu ni tendo la lazima. Katika Hadiyth iliyorikodiwa na Muslim inasema kuwa, ni moto kuacha eneo la mguu likiwa kavu. Katika Hadiyth hii kuna kukana kwa watu wanaosema kuwa kupangusa (mas-h) mguu pamoja na kuuosha vyote ni lazima; au watu wanaosema kuwa kupangusa na kuosha vyote vinaruhusiwa.

 

[28] Mudd moja ni sawa na takribani gram mia sita, na Sai’ moja ni sawa na zaidi kidogo ya kilo mbili unusu, na hiki ndicho kiasi cha chini kabisa cha kutumia. Hii inamaanisha kuwa kila mtu awe muangalifu sana katika matumizi ya maji (bila israaf).

 

[29] Sai’ moja ni sawa na mudd nne au gram 2660.

 

Share

05-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah:Mlango Wa Kupangusa Juu Ya Khuff Mbili (Soksi)

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتابُ الطَّهارَة

Kitabu Cha Twahaarah

 

بَابُ اَلْمَسْحِ عَلَى اَلْخُفَّيْنِ

05-Mlango Wa Kupangusa Juu Ya Khuff Mbili (Soksi Za Ngozi)

 

 

 

Tanbihi: Soksi za aina yoyote zinafaa ikiwa za sufi, pamba au katani na mifano hivyo.  

 

 

 

53.

عَنْ اَلْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {كُنْتُ مَعَ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏فَتَوَضَّأَ، فَأَهْوَيْتُ لِأَنْزِعَ خُفَّيْهِ، فَقَالَ: "دَعْهُمَا، فَإِنِّي أَدْخَلْتُهُمَا طَاهِرَتَيْنِ" فَمَسَحَ عَلَيْهِمَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْه

وَلِلْأَرْبَعَةِ عَنْهُ إِلَّا النَّسَائِيَّ: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏مَسَحَ أَعْلَى اَلْخُفِّ وَأَسْفَلَهُ} وَفِي إِسْنَادِهِ ضَعْف

Kutoka kwa Mughiyra bin Shu’bah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilikuwa na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akatawadha, nikaharakia kumvua soksi zake. Akasema: “Ziache, kwani nilizivaa zikiwa twahaara[1].” Akapungusa juu yake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na kutoka kwa Al-Arba’ah isipokuwa An-Nasaaiy: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipangusa sehemu ya juu na chini ya soksi za ngozi.” [Katika Isnaad yake kuna udhaifu].

 

 

 

54.

وَعَنْ عَلِيٍّ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {لَوْ كَانَ اَلدِّينُ بِالرَّأْيِ لَكَانَ أَسْفَلُ اَلْخُفِّ أَوْلَى بِالْمَسْحِ مِنْ أَعْلَاهُ، وَقَدْ رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَمْسَحُ عَلَى ظَاهِرِ خُفَّيْهِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادٍ حَسَن

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Lau Dini ingekuwa kwa rai[2], basi ingelikuwa kupangusa chini ya khuff ni bora zaidi kuliko juu yake. Na kwa yakini mimi nimemuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akipangusa juu ya khuff zake.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad Hasan]

 

 

 

55.

وَعَنْ صَفْوَانَ بْنِ عَسَّالٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَأْمُرُنَا إِذَا كُنَّا سَفْرًا أَنْ لَا نَنْزِعَ خِفَافَنَا ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ وَلَيَالِيَهُنَّ، إِلَّا مِنْ جَنَابَةٍ وَلَكِنْ مِنْ غَائِطٍ، وَبَوْلٍ، وَنَوْمٍ} أَخْرَجَهُ النَّسَائِيُّ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَاللَّفْظُ لَهُ، وَابْنُ خُزَيْمَةَ وَصَحَّحَاه ُ 

Kutoka kwa Swafwaan bin ‘Assaal (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akituamrisha pindi tukiwia safarini, tusivue khuff zetu siku tatu mfululizo mchana na usiku wak[3]e isipokuwa tukiwa katika janaba, lakini kwa haja kubwa, mkojo na usingizi (tulikuwa hatuvui).” [Imetolewa na An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy, na tamshi hili ni lake, na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

56.

وَعَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {جَعَلَ اَلنَّبِيُّ ‏صلى الله عليه وسلم ‏ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ وَلَيَالِيَهُنَّ لِلْمُسَافِرِ، وَيَوْمًا وَلَيْلَةً لِلْمُقِيمِ.‏ يَعْنِي: فِي اَلْمَسْحِ عَلَى اَلْخُفَّيْنِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِم

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alifanya kuwa siku tatu; mchana na usiku wake kwa msafiri, na siku moja; mchana na usiku wake kwa mkaazi yaani katika kufuta juu ya khuff.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

57.

وَعَنْ ثَوْبَانَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {بَعَثَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏سَرِيَّةً، فَأَمَرَهُمْ أَنْ يَمْسَحُوا عَلَى اَلْعَصَائِبِ ‏ يَعْنِي: اَلْعَمَائِمَ ‏وَالتَّسَاخِينِ‏ يَعْنِي: اَلْخِفَافَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِم

Kutoka kwa Thawbaan[4] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alituma kikosi cha jeshi na akawaamrisha wapanguse juu ya vilemba[5] na khuff.” [Imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd, na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

58.

وَعَنْ عُمَرَ ‏مَوْقُوفًا‏ وعَنْ أَنَسٍ ‏مَرْفُوعًا‏: {إِذَا تَوَضَّأَ أَحَدُكُمْ وَلَبِسَ خُفَّيْهِ فَلْيَمْسَحْ عَلَيْهِمَا، وَلْيُصَلِّ فِيهِمَا، وَلَا يَخْلَعْهُمَا إِنْ شَاءَ إِلَّا مِنْ جَنَابَةٍ"} أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَه

Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) katika Hadiyth Mawquwfaa na kutoka kwa Anas katika Hadiyth Marfuw’aa kuwa: “Pindi mmoja wenu akitawadha na akavaa khuff zake mbili, afanye mas-h (kupangusa kwa maji) juu yake na aswali nazo, na asizivue akipenda[6], isipokuwa kwa janaba.” [Imetolewa na Ad-Daarqutwniy na Al-Haakim, na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

59.

وَعَنْ أَبِي بَكْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ عَنْ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{أَنَّهُ رَخَّصَ لِلْمُسَافِرِ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ وَلَيَالِيَهُنَّ، وَلِلْمُقِيمِ يَوْمًا وَلَيْلَةً، إِذَا تَطَهَّرَ فَلَبِسَ خُفَّيْهِ: أَنْ يَمْسَحَ عَلَيْهِمَا} أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة

Kutoka kwa Abuu Bakrah[7] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ameruhusu msafiri kupangusa juu ya khuff siku tatu na usiku wake, na kwa mkaazi siku moja; mchana na usiku wake, atakapochukua wudhuu akavaa khuff zake mbili.” [Imetolewa na Ad-Daaruqutwniy na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

60.

وَعَنْ أُبَيِّ بْنِ عِمَارَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ أَنَّهُ قَالَ: {يَا رَسُولَ اَللَّهِ أَمْسَحُ عَلَى اَلْخُفَّيْنِ؟ قَالَ: "نَعَمْ" قَالَ: يَوْمًا؟ قَالَ: "نَعَمْ"، قَالَ: وَيَوْمَيْنِ؟ قَالَ: "نَعَمْ"، قَالَ: وَثَلَاثَةً؟ قَالَ: "نَعَمْ، وَمَا شِئْتَ" أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَقَالَ: لَيْسَ بِالْقَوِيِّ

Kutoka kwa Ubayy bin ‘Imaarah[8] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Ee Rasuli wa Allaah! Je, naweza kupangusa juu ya khuff mbili?” Akasema: “Ndiyo.” Akauliza tena: “Siku moja?” Akasema: “Ndiyo.” Akauliza tena: “Siku mbili je?” Akasema: “Ndiyo.” Akauliza tena: “Na siku tatu?: Akasema: “Ndiyo, na utakavyo[9].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, na akasema: “Hadiyth haina nguvu[10].”]

 

 

[1] Kupangusa (Mas-h) juu ya soksi kuna masharti. Hizo soksi lazima uwe ulizivaa ukiwa twahara. Ikiwa ulivaa soksi hizo hauko tohara, basi kupangusa juu yake hakuruhusiwi.

 

[2] Hadiyth hii inamaanisha kuwa amri za kidini (katika Uislaam) za maamrisho na makatazo hutegemea Wahyi. Mtu huwezi kukubali au kukataa amri kwa sababu ya kuzielewa au kutozielewa. Lakini hii haimaanishi kuwa maamrisho au makatazo hayo ya kidini huenda kinyume na akili na busara. Pia inathibitisha kuwa, pakiwepo Hadiyth Swahiyh, kutoa uamuzi kinyume na Hadiyth hiyo hairuhusiwi. Hili limebainishwa na Shariy’ah ya Kiislaam.

 

[3] Hadiyth hii inamaanisha kuwa, kupangusa (Mas-h) kunaruhusiwa kwa msafiri mpaka siku tatu, na kwa mkazi wa pale mpaka saa thelathini na nne. Kipindi cha Mas-h huhesabika tangu wudhuu unapobatilika na siyo tangu kuzivaa soksi. Njia ya kupangusa (Mas-h) ni kulowanisha mikono kwa maji, na kuanzia kwenye vidole kuupandisha mpaka chini ya magoti. Baada ya wakati unaoruhusiwa kwisha au ukijamba, ukikojoa, n.k., mas-h hubatilika. Na pia inabatilika kwa mambo yote yanayobatilisha wudhuu.

[4] Huyu Thawbaan ni Thawbaan bin Bujdud bin Jahdar, ambaye alipewa jina la utani la Abuu ‘Abdillaah. Alikuwa mkazi wa As-Surat, ambapo ni mahali kati ya Makkah na Al-Madiynah. Ilisemekana pia kuwa yeye alitoka Himyaar. Aliishi na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) maisha yake yote, baadaye akalowea Sham, na baadaye akahamia Hims alikofia mnamo mwaka 54 A.H.

 

[5] Katika maandishi ya Kiarabu neno ‘Aswaa-ib maana yake ni bendeji inayotumiwa kufungia vidonda, au ukivunjika mguu au mkono, kufungia juu ya vipande vya mbao viwekwavyo kuuzunguka mfupa uliovunjika.

 

[6]  “Akipenda” maana yake iwapo bado yumo katika wakati ulioruhusiwa kupangusa (Mas-h). Lakini mara wakati huo unapokwisha, lazima azivue soksi zake, akatawadhe upya pamoja na kuosha miguu yake, ndipo azivae tena hizo soksi zake, na kipindi cha kupangusa (Mas-h) kianze upya.

 

[7] Huyu Abuu Bakrah ndiye Nufai bin Al-Haarith au bin Al-Masruwh. Alishuka kutoka katika ngome ya Twaaif pamoja na kundi la watumwa na akasilimu, ndipo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuacha huru. Alikuwa mmoja wa Swahaba wenye taqwa na akafia Basra manmo mwaka 51 au 52 A.H.

 

[8] Ubay bin ‘Imaarah alikuwa Swahaba wa Kianswaar (wa kutoka Al-Madiynah). Alilowea Misr. Ibn Hibbaan alisema: “Aliswali kwa Qiblah mbili, lakini sichukulii ripoti yake kuwa ni mlolongo kamili wa wapokezi.”

 

[9] Isnaad ya Hadiyth hii si Swahiyh. Hadiyth ile inayotaja siku moja (saa 24) kwa mkazi, na siku tatu kwa msafiri ni Swahiyh.

 

[10] Hadiyth hii haikuchukuliwa kama ni ushahidi kwa udhaifu wake na kwa kuipinga Hadiyth Hasan na Swahiyh ambayo imetaja vipindi. An-Nawawi ametaja katika Sharh Al-Muhadhdhab kwamba, Imaam wamekubaliana juu ya udhaifu wa Hadiyth hii, na Ahmad alisema: “Wapokezi wake hawajulikani.”

 

Share

06-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah: Mlango Wa Kubatilika Wudhuu

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتابُ الطَّهارَة

Kitabu Cha Twahaarah

 

بَابُ نَوَاقِضِ اَلْوُضُوءِ

06-Mlango Wa Kubatilika[1] Wudhuu

 

 

 

 

61.

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {كَانَ أَصْحَابُ رَسُولِ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏‏عَلَى عَهْدِهِ‏ يَنْتَظِرُونَ اَلْعِشَاءَ حَتَّى تَخْفِقَ رُؤُوسُهُمْ، ثُمَّ يُصَلُّونَ وَلَا يَتَوَضَّئُونَ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ

وَأَصْلُهُ فِي مُسْلِمٍ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), katika zama zake (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) walikuwa wakingojea Swalaah ya ‘Ishaa hadi wanainamisha chini vichwa vyao (kwa kusinzia)[2], kisha wanaswali bila kutawadha upya[3].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ad-Daaruqutwniy]

[Chanzo chake ni Hadiyth ya Muslim]

 

 

 

62.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {جَاءَتْ فَاطِمَةُ بِنْتُ أَبِي حُبَيْشٍ إِلَى اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنِّي اِمْرَأَةٌ أُسْتَحَاضُ فَلَا أَطْهُرُ، أَفَأَدَعُ اَلصَّلَاةَ؟ قَالَ: "لَا.‏ إِنَّمَا ذَلِكَ عِرْقٌ، وَلَيْسَ بِحَيْضٍ، فَإِذَا أَقْبَلَتْ حَيْضَتُكِ فَدَعِي اَلصَّلَاةَ، وَإِذَا أَدْبَرَتْ فَاغْسِلِي عَنْكِ اَلدَّمَ، ثُمَّ صَلِّي} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَلِلْبُخَارِيِّ: {ثُمَّ تَوَضَّئِي لِكُلِّ صَلَاةٍ}

وَأَشَارَ مُسْلِمٌ إِلَى أَنَّهُ حَذَفَهَا عَمْدًا

Kutokwa kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: Faatwimah bint Abiy Hubaysh[4] alikuja kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akauliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Mimi ni mwanamke nakuwa na istihaadhwah (damu[5] ya haikatiki hata baada ya muda wa hedhi kumalizika) hivyo huwa sitohariki, je, niache kuswali?” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Hapana kwani huo ni mshipa wa damu, wala si hedhi, hivyo, ukiingia katika hedhi, sitisha kuswali, na hedhi ikiisha, osha damu huko iliko, kisha uswali.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na katika Riwaayah ya Al-Bukhaariy ameongezea: “Kisha tawadha kwa kila Swalaah[6].”

Na Muslim alitaja kuwa ameiondoa nyongeza hii kwa maksudi.

 

 

 

63.

وَعَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {كُنْتُ رَجُلاً مَذَّاءً، فَأَمَرْتُ اَلْمِقْدَادَ بْنَ اَلْأَسْوَدِ أَنْ يَسْأَلَ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏فَسَأَلَهُ  فَقَالَ: "فِيهِ اَلْوُضُوءُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa ‘Aliy bin Abuu Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilikuwa mtu wa kutokwa na madhiy[7] (majimaji yatokayo katika dhakari), nikamuamrisha Miqdaad bin Al-Aswad[8] amuulize Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), akamuuliza.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Anapaswa atawadhe.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

[Na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

 

64.

وَعَنْ عَائِشَةَ، رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَبَّلَ بَعْضَ نِسَائِهِ، ثُمَّ خَرَجَ إِلَى اَلصَّلَاةِ وَلَمْ يَتَوَضَّأْ} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَضَعَّفَهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimbusu[9] mmoja wa wake zake, na akaenda kuswali bila kutawadha upya.” [Imetolewa na Ahmad, na akaidhoofisha Al-Bukhaariy]

 

 

 

65.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{إِذَا وَجَدَ أَحَدُكُمْ فِي بَطْنِهِ شَيْئًا، فَأَشْكَلَ عَلَيْهِ: أَخَرَجَ مِنْهُ شَيْءٌ، أَمْ لَا؟ فَلَا يَخْرُجَنَّ مِنْ اَلْمَسْجِدِ حَتَّى يَسْمَعَ صَوْتًا، أَوْ يَجِدَ رِيحًا} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akipata kinachomtia shaka katika tumbo lake kuwa anatokwa kitu au la, basi asitoke Msikitini hadi amesikia sauti yake au ahisi harufu[10] yake.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

66.

وَعَنْ طَلْقِ بْنِ عَلِيٍّ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {قَالَ رَجُلٌ: مَسَسْتُ ذَكَرِي أَوْ قَالَ اَلرَّجُلُ يَمَسُّ ذَكَرَهُ فِي اَلصَّلَاةِ، أَعَلَيْهِ وُضُوءٍ ؟ فَقَالَ اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏"لَا، إِنَّمَا هُوَ بَضْعَةٌ مِنْكَ"} أَخْرَجَهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

وَقَالَ اِبْنُ اَلْمَدِينِيِّ: هُوَ أَحْسَنُ مِنْ حَدِيثِ بُسْرَةَ.‏

Kutoka kwa Twalq bin ‘Aliy[11] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mtu mmoja alisema: “Nimeigusa dhakari yangu” au aliuliza: “Mtu aliyegusa dhakari yake wakati wa Swalaah, Je ni lazima kutawadha?” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Hapana, hiyo ni sehemu ya mwili wako.” [Imetolewa na Al-Khamsah: Ahmad, Abuu Daawuwd, At-Tirmdhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah  na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

[Na Ibn Al-Madiyniyy amesema: “Hii ni bora kuliko Hadiyth ya Busrah.”]

 

 

 

67.

وَعَنْ بُسْرَةَ بِنْتِ صَفْوَانَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: "مَنْ مَسَّ ذَكَرَهُ فَلْيَتَوَضَّأْ"} أَخْرَجَهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ

وَقَالَ اَلْبُخَارِيُّ: هُوَ أَصَحُّ شَيْءٍ فِي هَذَا اَلْبَابِ.‏

Kutoka kwa Busrah bint Swafwaan[12] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakayegusa dhakari[13] yake basi na atawadhe.” [Imetolewa na Al-Khamsah, na akaisahihisha At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan]

 

[Na Al-Bukhaariy amesema: “Hadiyth hii ni sahihi zaidi kuliko zote katika mlango huu.”]

 

 

 

68.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: {مَنْ أَصَابَهُ قَيْءٌ أَوْ رُعَافٌ، أَوْ قَلَسٌ، أَوْ مَذْيٌ فَلْيَنْصَرِفْ فَلْيَتَوَضَّأْ، ثُمَّ لِيَبْنِ عَلَى صَلَاتِهِ، وَهُوَ فِي ذَلِكَ لَا يَتَكَلَّمُ} أَخْرَجَهُ اِبْنُ مَاجَه

وَضَعَّفَهُ أَحْمَدُ وَغَيْرُهُ.‏

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Yeyote atakayetapika au kutokwa na damu puani[14] kutokwa na madhiy, atoke atawadhe kisha aendelee na Swalaah yake[15] (kwa kuendelea kutokea pale alipoiachia hiyo Swalaah), kwa sharti kwamba  asizungumze katika wakati wa harakati hiyo.” [Imetolewa na Ibn Maajah]

 

Na akaidhoofisha Ahmad na wengine.

 

 

 

69.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {أَنَّ رَجُلاً سَأَلَ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏أَتَوَضَّأُ مِنْ لُحُومِ اَلْغَنَمِ ؟ قَالَ: إِنْ شِئْتَ قَالَ: أَتَوَضَّأُ مِنْ لُحُومِ اَلْإِبِلِ  ؟ قَالَ: نَعَمْ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Jaabir bin Samurah[16] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) anasema kuwa: “Mtu mmoja alimuuliza Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Je! Nitawadhe kwa kula nyama ya kondoo?” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ukipenda.” Akauliza: “Je nitawadhe kwa kula nyama ya ngamia[17]?” Akasema: “Ndiyo.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

70.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{مَنْ غَسَّلَ مَيْتًا فَلْيَغْتَسِلْ، وَمَنْ حَمَلَهُ فَلْيَتَوَضَّأْ} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَالنَّسَائِيُّ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ

وَقَالَ أَحْمَدُ: لَا يَصِحُّ فِي هَذَا اَلْبَابِ شَيْءٌ.

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Aliyemuosha maiti[18] na aoge na aliyembeba atawadhe.” [Imetolewa na Ahmad na An-Nassaiy, na ameifanya ‘Hasan’ At-Tirmidhiy]

 

[Na Ahmad amesema: “Hakuna Hadiyth yoyote iliyosihi katika mlango huu]

 

 

 

71.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ رَحِمَهُ اَللَّهُ، {أَنَّ فِي اَلْكِتَابِ اَلَّذِي كَتَبَهُ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏لِعَمْرِو بْنِ حَزْمٍ: أَنْ لَا يَمَسَّ اَلْقُرْآنَ إِلَّا طَاهِرٌ} رَوَاهُ مَالِكٌ مُرْسَلاً، وَوَصَلَهُ النَّسَائِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ، وَهُوَ مَعْلُولٌ.‏

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Abiy Bakr[19] (رَحِمَهُ اَللَّهُ) amesema kuwa: Katika barua ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliyomwandikia “’Amr bin Hazm[20]: “Asiiguse Qur-aan[21] isipokuwa aliyekuwa kwenye twahaarah.” [Imetolewa na Maalik Mursalaa, na Mawswul (wameiunganisha) An-Nasaaiy na Ibn Hibbaan, nayo ina dosari]

 

 

 

72.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يُذْكُرُ اَللَّهَ عَلَى كُلِّ أَحْيَانِهِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ، وَعَلَّقَهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akimdhukuru Allaah nyakati zake[22] zote.” [Imetolewa na Muslim, na Al-Bukhaariy akaipa daraja la Mu’alaq]

 

 

 

73.

وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ‏ رضى الله عنه ‏ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏اِحْتَجَمَ وَصَلَّى، وَلَمْ يَتَوَضَّأْ} أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَلَيَّنَهُ

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alifanya hijaamah[23] (kuumikwa au kupigwa chuku) akaswali wala hakutawadha.” [Imetolewa na Ad-Daaruqutwniy, aliyeipa daraja la Dhaifu]

 

 

 

74.

وَعَنْ مُعَاوِيَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{الْعَيْنُ وِكَاءُ السَّهِ، فَإِذَا نَامَتْ اَلْعَيْنَانِ اِسْتَطْلَقَ اَلْوِكَاءُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالطَّبَرَانِيُّ وَزَادَ {وَمَنْ نَامَ فَلْيَتَوَضَّأْ}

وَهَذِهِ اَلزِّيَادَةُ فِي هَذَا اَلْحَدِيثِ عِنْدَ أَبِي دَاوُدَ مِنْ حَدِيثِ عَلِيٍّ دُونَ قَوْلِهِ: {اِسْتَطْلَقَ اَلْوِكَاءُ} وَفِي كِلَا الْإِسْنَادَيْنِ ضَعْفٌ

وَلِأَبِي دَاوُدَ أَيْضًا، عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ مَرْفُوعًا: {إِنَّمَا اَلْوُضُوءُ عَلَى مَنْ نَامَ مُضْطَجِعًا} وَفِي إِسْنَادِهِ ضَعْفٌ أَيْضًا

Kutoka kwa Mu’aawiyah[24] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Jicho lililo macho ni kamba na kizuizi cha kutoka upepo, na macho yote mawili yakilala, hiyo kamba hufunguka (na upepo hutoka bila hisia[25]).” [Imetolewa na Ahmad na Atw-Twabaraaniy]

 

Na Atw-Twabaraaniy aliongezea: “Kila aliyelala atawadhe upya.”

 

Pia imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Hadiyth ya ‘Aliy bila maneno: “Kamba hufunguka” [Isnaad zote mbili ni dhaifu]

 

Na kutoka kwa Abuu Daawuwd vile vile kutoka kwa Ibn ‘Abbaas ikiwa ni Hadiyth Marfuw’aa: “Hakika wudhuu ungalipo kwa aliyelala kwa makalio yake.” [Katika Isnaad yake kuna udhaifu pia]

 

 

 

75.

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {يَأْتِي أَحَدَكُمُ الشَّيْطَانُ فِي صَلَاتِهِ، فَيَنْفُخُ فِي مَقْعَدَتِهِ فَيُخَيَّلُ إِلَيْهِ أَنَّهُ أَحْدَثَ، وَلَمْ يُحْدِثْ، فَإِذَا وَجَدَ ذَلِكَ فَلَا يَنْصَرِفُ حَتَّى يَسْمَعَ صَوْتًا أَوْ يَجِدَ رِيحًا} أَخْرَجَهُ اَلْبَزَّارُ

وَأَصْلُهُ فِي اَلصَّحِيحَيْنِ مِنْ حَدِيثِ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ زَيْدٍ

وَلِمُسْلِمٍ: عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ نَحْوُهُ.

وَلِلْحَاكِمِ.‏ عَنْ أَبِي سَعِيدٍ مَرْفُوعًا: {إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الشَّيْطَانُ، فَقَالَ: إِنَّكَ أَحْدَثْتَ، فَلْيَقُلْ: كَذَبْتَ}

وَأَخْرَجَهُ اِبْنُ حِبَّانَ بِلَفْظِ: {فَلْيَقُلْ فِي نَفْسِهِ}

Kutokwa kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesimulia kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Shaytwaan huja kwa mmoja wenu ndani ya Swalaah, na humpulizia upepo makalioni mwake naye hudhani amepata hadath nae hajapata hadath. Hivyo, akihisi hivyo asiondoke hadi asikie sauti au ahisi harufu[26].” [Imetolewa na Al Bazzaar]

 

[Asili yake ni katika Swahiyh mbili, Al-Bukhaariy na Muslim kuwa ilisimuliwa na ‘Abdullaah bin Zayd]

 

[Na Muslim amepokea Hadiyth ya Abuu Hurayrah vivyo hivyo]

 

Na Al-Haakim amemnukuu Abuu Sa’iyd katika Hadiyth Marfuw’aa (yenye upokezi wa wazi): “Endapo shaytwaan atamjia mmoja wenu na kumwambia: “Wewe umetengua wudhuu wako kwa kutoa upepo”, basi aseme: “Umesema uongo.”” [Imetolewa na Al-Haakim]

 

Na Ibn Hibbaan pia amepokea Hadiyth hiyo pamoja na tamshi: “Na aseme moyoni mwake.”

 

 

[1] Mazingira yote yanayobatilisha wudhuu na kutawadha kwa maji, pia hubatilisha wudhuu wa kutayammam (kutawadha kwa udongo safi itokeapo maji hakuna).

 

[2] Hii inathibitisha kwamba, kusinzia hakubatilishi au hakutangui wudhuu.

 

[3] Hili suala la iwapo usingizi unabatilisha wudhuu au laa, lina utata sana. Katika kadhia hii, maamuzi ya mwisho ni kuwa, endapo usingizi utakuwa ule mzito, basi wudhuu unabatilika, vinginevyo hautenguki.

 

[4] Faatwimah bint Abiy Hubaysh ni Swahabiyyah kutoka Quraysh na tena Asad. Babake ni Qays bin ‘Abdil-Mutwalib bin Asad bin ‘Abdil-‘Uzza bin Quswayy. Alikuwa Muhajira (mhamiaji kutoka Makkah) maarufu, na aliolewa na ‘Abdullaah bin Jahsh.

 

[5] Damu za mwanamke ziko za namna tatu:
a) Hedhi ni damu ya kila mwezi mmoja wa hedhi, ambayo huanza mwanamke akiwa baleghe. Damu ya aina hii husimama wakati mwanamke yu mjamzito.

b) Nifaas, yaani damu ya mwanamke imtokayo akisha kuzaa, ambayo haidumu zaidi ya siku 40.

c) Istihaadhwah, yaani damu inayoweza kutoka kwa sababu zisizokuwa hizo mbili. Hapa inamaanisha inayotajwa mwishoni.

 

[6] Hii inamaanisha kuwa, damu ya Istihaadhwah hubatilisha wudhuu, ndiyo maana Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaamuru kutawadha upya kabla ya kila Swalaah.

 

[7] Madhiy ni majimaji meupe kama mafuta ambayo hutoka bila kuzuilika wakati mtu ana ashki ya jimai. Ute huu hubatilisha wudhuu, lakini hauhitaji kuoga rasmi.

 

[8] Miqdaad bim ‘Amr bin Tha’labah Al-Bahraan alipewa jina la utani la Abul-Aswad au Abuu ‘Amr, na anajulikana kwa jina la Al-Miqdaad bin Al-Aswad. Al-Aswad bin Yaghuwth Az-Zuhr alimlea na wakafanya mkataba wa kujihami na Miqdaad zama za ujaahiliyyah (kabla ya ujio wa Uislaam). Alikuwa ni mmoja wa Swahaba wenye taqwah, wenye busara, na maarufu. Alikuwa wa sita kusilimu, alihama hijrah zote mbili, na alishiriki vita zote kuu. Alikuwa mpanda farasi katika vita vya Badr, na alishiriki katika kuiteka Misri. Alifariki akiwa na miaka 70 mnamo mwaka 33 A.H kule Al-Jawf, maili tatu kutoka Al-Madiynah. Kwa hivyo mwili wake ulipelekwa Al-Madiynah. ‘Uthmaan akasalisha Swalaah yake ya Janaazah, na kuzikwa Al-Baqi’.

 

[9] Hadiyth hii inathibitisha kwamba, wudhuu haubatiliki kwa kumgusa mwanamke, ukimtamani au usimtamani. Hii inaungwa mkono na ripoti ya Al-Bukhaariy iliyosimuliwa na ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) “Alikuwa akisali gizani, nami nilikuwa nimepumzika wakati miguu yangu ilining’inia hadi kule ambako Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikokuwa akisujudia juu ya msala wake. Kila anaposujudu alikuwa akigusa miguu yangu, nami nikawa naiondosha.”

 

[10] Hadiyth hii inataja msingi wa maana kwamba kila kitu hubaki katika amri ya awali, mpaka kitokee kitu dhahiri dhidi yake. Dhana peke yake si ya kuzingatia ukiwa umo ndani ya Swalaah au laa.

 

[11] Huyu Twalq ni Abuu ‘Aliy Twalq bin ‘Amr Al-Hanaf As-Siheim Al-Yamaam. Alimzuru Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mara alipofika Al-Madiynah, na akafanya naye kazi katika kuujenga Msikiti wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).

 

[12] Busrah bint Swafwaan bin Naefal bin Asad bin ‘Abdil-‘Uzza Al-Quraishiyyah Al-Asadiyyah alikuwa ni Swahaba miongoni mwa Waislaam wa kwanza, alihajiri (alihama) mapema, na akaishi hadi katika Ukhalifa wa Mu’aawiyah.

 

[13] Hadiyth hiyo hapo juu ya Twalq bin ‘Aliy inaelekea inapingana na hii, lakini sivyo hivyo. Kama kiungo hicho kitaguswa bila kufunikwa nguo au kwa nia ya matamanio hapo wudhuu utakuwa umebatilika; vinginevyo haubatiliki.

 

[14] Hadiyth hii ni dhaifu, na hakuna Hadiyth Swahiyh juu ya kadhia hii.

 

[15] Hii inamaanisha kwamba, iwapo mtu alishaswali rakaa  mbili na Imaam, na ikatokezea kwamba wudhuu wake umebatilika, ataicha Swalaah, na baada ya kutawadha upya, ajiunge na jamaa katika sehemu ile ile alipoachia, kisha amalizie Swalaah na Imaam.

 

[16] Jaabir ni Swahaba maarufu na ni mtoto wa dada wa Sa’d bin Abiy Waqqaas. Alilowea Kufa akajenga nyumba kule. Alifariki mnamo mwaka 66 au 74 A.H. Baba yake Samurah bin Junada As-Sawai Al-‘Aamir naye pia ni Swahaba.

 

[17] Watu wengine wanasema hii inamaanisha kutawadha kamili na wengine wanasema kusukutua mdomo tu. Fikra hii ya mwisho ni sahihi, kwa kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitaja sababu ya amri hii kuwa ni mafuta, na mafuta huganda mdomoni tu.

 

 

[18] Kuhusu kadhia hii, hakuna Hadiyth Swahiyh. Wengine wanasema kuwa kuoga ni lazima kwa yule anayeogesha maiti, wengine wanasema ni vizuri, na wengine wanasema kutawadha ni lazima, na wengine wanasema hata hii siyo lazma.

 

[19] Huyo ni ‘Abdullaah bin Abiy Bakr bin ‘Amr bin Hazm Al-Answaar Al-Madani Al-Qadi. Taabi’ wa daraja la 5. Alifariki mnamo mwaka 135 A.H akiwa na miaka 70.

 

[20] Huyu ‘Amr bin Hazm ni Mkhazraj, Mnajaar aliyepewa jina la utani la Abuu Ad-Dhwahhaak. Alishiriki kwanza katika vita ya Khandaq, na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtuma Najran kuwafundisha watu dini na kukusanya swadaqah. Aliwaandikia kitabu chenye matendo ya lazima na ya hiari, swadaqah na hiki ndicho kitabu kilichotajwa katika Hadiyth hii. Alifariki Madiynah akiwa na miaka hamsini na kitu.

 

[21] Hadath Akbar: (hadathi au najisi kubwa, yaani majimaji ya kijinsia yanayotoka kwenye sehemu za siri), na Hadath Aswghar: (Hadathi ndogo kutoa upepo, mkojo au kinyesi), vyote hivi vinahitaji kutawadha. Lakini ikiwa hiyo Hadath inatokana na kujamiiana, basi imeafikiwa na wote kuwa huna ruhusa kuigusa Qur-aan, lakini kuna maoni tofauti kuhusu kufanya hivyo bila kutawadha.

 

[22] Nyakati za kuenda haja kubwa, kukojoa na za kujamiiana, hazimo. Katika kunajisika kwa kujamiiana, dhikr au kutamka jina la Allaah kunaruhusiwa, lakini kuigusa au kuisoma Qur-aan hakuruhusiwi.

 

[23] Hadiyth hii inaweka wazi kwamba, kutokwa na damu nje ya sehemu mbili kama katika hali hii ya kufanyiwa hijaamah (ukeni na sehemu ya kutolea kinyesi) hakubatilishi wudhuu. Hadiyth za daraja hilo zimesimuliwa pia na Ibn ‘Umar Ibn ‘Abbaas na Abuu Aufa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).

 

[24] Mu’aawiyah huyu pamoja na babake, Abuu Sufyaan Sakhr bin Harb, walisilimu ilipotekwa Makkah. ‘Umar alimteuwa akawa Gavana wa Shaam, baada ya kifo cha kaka yake Yaziyd bin Abuu Sufyaan na alibakia hivyo hadi ‘Aliy alivyojitokeza ili apate kumuondosha kwa nguvu, na akaapishwa kuwa Khalifa wakati wa Al-Hasan alipojiuzulu kwa kumuachia yeye cheo mnamo mwaka wa 40 H. Alifariki mnamo mwezi wa Rajabu mwaka 60 A.H akiwa na miaka 78.

 

[25] Hii inamaanisha kuwa usingizi ni chanzo cha hadathi (uchafu), lakini siyo uchafu wenyewe.

 

[26] Hii maana yake ni kwamba, kulala na sambamba na kilalio hupelekea kubatilika kwa wudhuu, ambapo kwenye Hadiyth ya juu inaelezea kuwa usingizi peke yake wowote unabatilisha wudhuu. Kulala sambamba na kilalio ni ishara ya kulala usingizi mzito, wakati viungo vyote vya mwili vinapumzika na kunawezesha upepo kutoka bila kizuizi, ambapo katika usingizi mwepesi au kusinzia, mtu huwa hajapoteza fahamu zote.

 

Share

07-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah: Mlango Wa Kwenda Kujisaidia Haja Msalani

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتابُ الطَّهارَة

Kitabu Cha Twahaarah

 

بَابُ قَضَاءِ اَلْحَاجَةِ

07-Mlango Wa Kwenda Kujisaidia Haja Msalani

 

 

 

76.

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏إِذَا دَخَلَ اَلْخَلَاءَ وَضَعَ خَاتَمَهُ} أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَهُوَ مَعْلُولٌ

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anaivua pete[1] yake akiingia msalani.” [Imetolewa na Al-Arba’ah: Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah na ina dosari]

 

 

 

77.

وَعَنْهُ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏إِذَا دَخَلَ اَلْخَلَاءَ قَالَ: "اَللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ اَلْخُبُثِ وَالْخَبَائِثِ"} أَخْرَجَهُ اَلسَّبْعَةُ

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiingia msalani anasema[2]:

اَللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ اَلْخُبُثِ وَالْخَبَائِثِ

“Allaahumma inniy a’uwdhu ‘Bika minal khubuthi wal khabaaith.” (Ee Allaah, najikinga Kwako dhidi ya mashaytwani ya kiume na ya kike).” [Imetolewa na As-Sab’ah (Maimamu Saba Wa Hadiyth: Al-Bukhaariy, Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad)]

 

 

 

78.

وَعَنْهُ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏يَدْخُلُ اَلْخَلَاءَ، فَأَحْمِلُ أَنَا وَغُلَامٌ نَحْوِي إِدَاوَةً مِنْ مَاءٍ وَعَنَزَةً، فَيَسْتَنْجِي بِالْمَاءِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiingia msalani, mimi na ghulamu (mtoto mvulana) mwengine tukimchukulia viroba vya maji na mkuki, na anajisafisha kwa maji[3] yale.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

79.

وَعَنْ اَلْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {قَالَ لِي اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏ "خُذِ اَلْإِدَاوَةَ".‏ فَانْطَلَقَ حَتَّى تَوَارَى عَنِّي، فَقَضَى حَاجَتَهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Al-Mughiyrah bin Shu’bah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliniambia: “Chukua kiroba cha maji.” Kisha akaenda mbele hadi akanipotea[4], na ndipo akakidhi haja yake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

80.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{اِتَّقُوا اَللَّاعِنِينَ: اَلَّذِي يَتَخَلَّى فِي طَرِيقِ اَلنَّاسِ، أَوْ فِي ظِلِّهِمْ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

زَادَ أَبُو دَاوُدَ، عَنْ مُعَاذٍ: {وَالْمَوَارِدَ}

وَلِأَحْمَدَ; عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: {أَوْ نَقْعِ مَاءٍ} وَفِيهِمَا ضَعْفٌ

وَأَخْرَجَ اَلطَّبَرَانِيُّ اَلنَّهْيَ عَنْ ‏ تَحْتِ اَلْأَشْجَارِ اَلْمُثْمِرَةِ، وَضَفَّةِ اَلنَّهْرِ الْجَارِي.‏ مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ عُمَرَ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ogopeni viwili vyenye kusababisha laana; humpata ambaye hujisaidia (kukojoa au kunya) katika njia za watu[5], na chini ya vivuli vyao.” [Imetolewa na Muslim]

 

Ameongezea Abuu Daawuwd kuwa ilisimuliwa na Mu’aadh[6] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa: “Kujisaidia mahali pa kuchotea maji na hifadhi yake.”

 

Katika Riwaayah ya Ahmad (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alisimulia kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kuwa: “Kujisaidia palipokusanyika maji.” [Na Hadiyth zote mbili, zina udhaifu]

 

Atw-Twabaraaniy alitaja kuwa: “Imekatazwa kujisaidia chini ya miti ya matunda na kando kando ya mito inayotiririka[7].” [Imetolewa na Atw-Twabaraaniy kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Umar, kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

81.

وَعَنْ جَابِرٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{إِذَا تَغَوَّطَ اَلرَّجُلَانِ فَلْيَتَوَارَ كُلُّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا عَنْ صَاحِبِهِ، وَلَا يَتَحَدَّثَا.‏ فَإِنَّ اَللَّهَ يَمْقُتُ عَلَى ذَلِكَ} رَوَاهُ  أَحْمَدُ.‏ ‏ وَصَحَّحَهُ اِبْنُ اَلسَّكَنِ، وَابْنُ اَلْقَطَّانِ، وَهُوَ مَعْلُولٌ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Watu wawili wakijisaidia pamoja, kila mmoja ajifiche na mwenzie wala wasiongee, kwani Allaah anachukia hivyo.”” [Imetolewa na Ahmad na akaisahihisha Ibn As-Sakan na Ibn Al-Qatwaan, lakini ina dosari[8]]

 

 

 

82.

وَعَنْ أَبِي قَتَادَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{لَا يُمْسِكَنَّ أَحَدُكُمْ ذَكَرَهُ بِيَمِينِهِ، وَهُوَ يَبُولُ، وَلَا يَتَمَسَّحْ مِنْ اَلْخَلَاءِ بِيَمِينِهِ، وَلَا يَتَنَفَّسْ فِي اَلْإِنَاءِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ

Kutoka kwa Abuu Qataadah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mtu yeyote asishike dhakari[9] yake kwa kulia kwake wakati anakojoa, na asijisafishe (kutokana na haja kubwa au ndogo) kwa kulia kwake, wala asipumulie katika chombo (anachonywea).” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

83.

وَعَنْ سَلْمَانَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {لَقَدْ نَهَانَا رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏ "أَنْ نَسْتَقْبِلَ اَلْقِبْلَةَ بِغَائِطٍ أَوْ بَوْلٍ، أَوْ أَنْ نَسْتَنْجِيَ بِالْيَمِينِ، أَوْ أَنْ نَسْتَنْجِيَ بِأَقَلَّ مِنْ ثَلَاثَةِ أَحْجَارٍ، أَوْ أَنْ نَسْتَنْجِيَ بِرَجِيعٍ أَوْ عَظْمٍ"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَلِلسَّبْعَةِ مِنْ حَدِيثِ أَبِي أَيُّوبَ ‏ رضى الله عنه ‏ {لَا تَسْتَقْبِلُوا اَلْقِبْلَةَ بِغَائِطٍ وَلَا بَوْلٍ، وَلَكِنْ شَرِّقُوا أَوْ غَرِّبُوا}

Kutoka kwa Salmaan[10] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitukataza kuelekea Qiblah wakati wa kwenda haja kubwa au ndogo, wala tusijisafishe kwa mkono wa kulia, au kujisafisha kwa mawe yasiyotimia matatu, au kujisafisha kwa kinyesi cha wanyama au mfupa.” [Imetolewa na Muslim]

 

As-Sab’ah (Maimaam Saba wa Hadiyth) wamenukuu Hadiyth ya   Abuu Ayyuub[11] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Usielekee Qiblah[12] wakati unakwenda haja kubwa au ndogo, lakini geukia Mashariki au Mgharibi.”

 

 

 

84.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا; أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {مَنْ أَتَى اَلْغَائِطَ فَلْيَسْتَتِرْ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kwenda kujisaidia haja kubwa na ajisitiri.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd]

 

 

 

85.

وَعَنْهَا; {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏كَانَ إِذَا خَرَجَ مِنْ اَلْغَائِطِ قَالَ: "غُفْرَانَكَ"} أَخْرَجَهُ اَلْخَمْسَةُ.‏ وَصَحَّحَهُ أَبُو حَاتِمٍ، وَالْحَاكِمُ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema tena: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitoka msalani, anasema: “Ghufraanaka (Ee Allaah! Naomba Unighufurie).” [Imetolewa na Al-Khamsah: (Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, An-Nasaaiy, Ahmad, Ibn Hibbaan, Al-Haakim) Waliipa Hadiyth hii daraja la Swahiyh Abuu Haatim na Al Haakim]

 

 

 

86.

وَعَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {أَتَى اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏اَلْغَائِطَ، فَأَمَرَنِي أَنْ آتِيَهُ بِثَلَاثَةِ أَحْجَارٍ، فَوَجَدْتُ حَجَرَيْنِ، وَلَمْ أَجِدْ ثَالِثًا.‏ فَأَتَيْتُهُ بِرَوْثَةٍ.‏ فَأَخَذَهُمَا وَأَلْقَى اَلرَّوْثَةَ، وَقَالَ: "هَذَا رِكْسٌ"} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ

زَادَ أَحْمَدُ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ: {ائْتِنِي بِغَيْرِهَا}

Kutoka kwa Ibn Mas-’uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikwenda kujisaidia na akaniamrisha nimpelekee mawe matatu, nikapata mawe mawili na sikupata la tatu. Kwa hivyo nikampelekea kinyesi cha mnyama kilichokauka. Akakirushia mbali[13] kisha akasema: “Hii ni najisi.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

Katika nukuu ya Ahmad na Ad-Daaruqutwniy imeongezewa: “Niletee kisichokuwa hiki[14].”

 

 

 

87.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏نَهَى "أَنْ يُسْتَنْجَى بِعَظْمٍ، أَوْ رَوْثٍ" وَقَالَ: "إِنَّهُمَا لَا يُطَهِّرَانِ"} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ وَصَحَّحَهُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ametukataza kutumia mifupa au kinyesi kikavu cha mnyama kujisafisha, alisema: “Vitu hivi viwili havitwoharishi.”” [Imetolewa na Ad-Daaruqutwniy na akaisahihisha]

 

 

 

88.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{اِسْتَنْزِهُوا مِنْ اَلْبَوْلِ، فَإِنَّ عَامَّةَ عَذَابِ اَلْقَبْرِ مِنْهُ} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ

وَلِلْحَاكِمِ: {أَكْثَرُ عَذَابِ اَلْقَبْرِ مِنْ اَلْبَوْلِ} وَهُوَ صَحِيحُ اَلْإِسْنَادِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Jitakaseni kutoka na mkojo, kwani ni sababu kuu ya adhabu za kaburini.” [Imetolewa na Ad-Daaruqutwniy

Na kutoka kwa Al Haakim alisimulia kuwa: “Adhabu nyingi za kaburini ni kutokana na mkojo.” [Na Isnaad yake ni Swahiyh]

 

 

89.

وَعَنْ سُرَاقَةَ بْنِ مَالِكٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {عَلَّمْنَا رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏فِي اَلْخَلَاءِ: " أَنَّ نَقْعُدَ عَلَى اَلْيُسْرَى، وَنَنْصِبَ اَلْيُمْنَى"} رَوَاهُ اَلْبَيْهَقِيُّ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa Suraaqah bin Maalik[15] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitufundisha adabu za msalani: kuwa tukalie mguu wa kushoto[16] na tuusimamishe wima mguu wa kulia.” [Imetolewa na Al-Bayhaqiy kwa Isnaad dhaifu[17]]

 

 

 

90.

وَعَنْ عِيسَى بْنِ يَزْدَادَ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{إِذَا بَالَ أَحَدُكُمْ فَلْيَنْثُرْ ذَكَرَهُ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ} رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَه بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa ‘Iysaa bin Yazdaad[18] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kutoka kwa baba yake amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akikojoa, anapaswa akung’ute dhakari yake mara tatu.”  [Imetolewa na Ibn Maajah kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

91.

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا; {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏سَأَلَ أَهْلَ قُبَاءٍ،  فَقَالَ: "إنَّ اللهَ يُثْنِي عَلَيْكُمْ، فَقَالُوا: إِنَّا نُتْبِعُ اَلْحِجَارَةَ اَلْمَاءَ} رَوَاهُ اَلْبَزَّارُ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ

وَأَصْلُهُ فِي أَبِي دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيّ وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ مِنْ حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ بِدُونِ ذِكْرِ اَلْحِجَارَةِ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwauliza watu wa Qubaa akasema: “Allaah Anakusifuni.” Wakasema: “Sisi hufuatisha maji baada ya (kujisafisha kwa) mawe.” [Imetolewa na Al Bazzaar kwa Isnaad dhaifu]

Na chanzo chake ni Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy na akaisahihisha Ibn Khuzaymah Hadiyth hii kupitia kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) bila kutaja “mawe.”

 

 

 

 

[1] Pete ile ilikuwa imeandikwa mistari mitatu: “Muhammad Rasulu wa Allaah.” Hii inamaanisha kwamba, Majina ya Allaah (عز وجل) au Aayah za Qur-aan kamwe zisipelekwe chooni au unapokwenda haja yoyote.

 

[2] Kwa kawaida majini huishi sehemu chafu kama vyooni. Kwa sababu hiyo, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiomba hifadhi ya Allaah (عز وجل).   Mtu sharti aisome du’aa hii kabla ya kuingia chooni kwa sauti ya kusikika. Kwa mujibu wa usimulizi wa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) maporini na misituni, mtu sharti aisome du’aa hii kabla ya kuchuchumaa na kuenda haja. Wakati wa kuenda haja, mtu sharti aangalie mwili wake na nguo zake.

 

[3] Baadhi ya Wanazuoni hupendelea kujisafisha kwa dongo pamoja na maji.

 

[4] Tendo hili la Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) linatufundisha kuwa, wakati wa kuenda kujisaidia ni lazima kuandaa sitara (kificho) ili ufichike kwa watu wengine. Katika Hadiyth nyingine imesema kwamba, mahala palipo wazi, kijilima cha udongo au rundo la mchanga uandaliwe kwa ajili ya kujisitiri. Mtu akijisaidia mahali pa wazi kabisa, shaytwaani atayacheka matako yake na atachekwa na watu pia.

 

[5] Imekatazwa kuenda haja njiani au katika njia zilizo karibu na maeneo yenye watu wengi. Mahali penye barabara isiyotumika au magofu ya nyumba zilizohamwa zinaweza kutumika kuendea haja.

 

[6] Mu’aadh ni Answaar (wa kutoka Al-Madiynah) wa kabila la Al-Khazraj alikuwa mmoja wa Swahaba waadilifu, mtukufu na msomi mkubwa. Alishiriki katika vita za Aqabah, Badr na vita zingine kubwa. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimteuwa kuwa mwakilishi wake kule Yaman. Kisha ‘Umar akamteua kuwa Gavana wa Shaam baada ya Abuu ‘Ubaydah bin Al-Jarraah. Alifariki katika mji wa Amwaas mnamo mwaka 17 au 18 A.H akiwa na umri wa miaka 38.

 

[7] Sehemu zote zinazokatazwa ni sita. Imekatazwa katika Hadiyth kuenda haja kubwa au ndogo karibu na milango ya Misikiti.

 

[8] Hii inathibitishwa na Hadiyth zingine.

 

[9] Kuushika uume kwa mkono wa kuume wakati wa kuenda haja ndogo au kuuosha, na kupumulia kwenye chombo cha kunywea imekatazwa, kwa mujibu wa wengine, na kwa mujibu wa wengine wanasema haipendezi. Kutolea pumzi ndani ya chombo kuna madhara kwa sababu hiki ni chanzo cha kuambukiza viini kutoka kwa mtu mmoja mpaka kwa mwingine. Na Hadiyth inayoagiza kuwa na mapumziko matatu wakati wa kunywa, inamaanisha kuwa kinywaji sharti kinywewe taratibu na siyo kukimeza kwa mkupuo mmoja.

 

[10] Salmaan Al-Faarisiy: Alikuwa akijulikana kwa jina la “Salmaan mkarimu”, na akapewa jina la utani la Abuu ‘Abdillaah. Asili yake alitoka Uajemi (Persia). Alisafiri akitafuta dini, na akawa Mkristo. Kisha akahamia Al-Madiynah na akamuamini Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mara tu alipowasili Al-Madiynah. Salmaan Al-Faarisy ndiye aliyetoa fikra ya kuchimbwa mahandaki katika vita vya Al-Khandaq. Alikuwa kiongozi katika Uislaam, na alifariki Al-Madiynah mnamo mwaka 50 au 32 A.H. Imetaarifiwa kwamba aliishi muda mrefu sana, ama miaka 250 au 350.

 

[11] Abuu Ayuwb jina lake ni Khaalid bin Zayd bin Kulayb. Huyu ndiye aliyemkaribisha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipowasili Al-Madiynah mara ya kwanza. Alikuwa ni mmoja wa Swahaba wakubwa na waandamizi sana. Alishiriki katika vita vya Badr, na akafa shahidi wakati alipopigana vita dhidi ya Wabinzantina mnamo mwaka 50 A.H. Kaburi lake liko katika kuta za Istanbul linajulikana sana na watu wengi hulizuru.

 

[12] Katika kadhia hii, ‘Makatazo’ yako kwenye maeneo ya wazi. Haikatazwi ikiwa eneo hilo ni ndani ya jengo ambalo lina kuta zinazolizunguka. Kwani kuna Hadiyth ambayo ilisimuliwa na ‘Abdullaah bin ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kwamba: “Katika nyumba ya dadangu Hafswa (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) nilikuenda ghorofani kwenye paa, nikamuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) anakuenda haja, ameeleka Shaam.” Hadiyth hii ni ya Sahihi Muslim.

 

[13] Hadiyth hii inatujulisha kuwa, mtu asisafishe sehemu zake za siri kwa kinyesi au samadi ya mnyama; na pia imekatazwa kujisafisha kwa mifupa.

 

[14] Hiyo nyongeza inamaanisha kwamba, kwa ajili ya usafi, hutakiwa mabonge matatu ya udongo, ingawa mawili yangetosha, lakini sharti la matatu liko pale pale. Yanaweza kutumika mabonge zaidi ya matatu, ikilazimika, lakini namba iwe Witri. Hadiyth hii pia inathibitisha kuwa kinyesi cha Wanyama hakiwezi kutumika kusafishia sehemu za siri. Na pia kujisafisha kwa mifupa pia kumekatazwa.

 

[15] Suraaqah bin Maalik bin Ju’shum Al-Mudlaj Al-Kinaan aliyepewa jina la utani la Abuu Sufyaan alikuwa Swahaba maarufu. Huyu ndiye aliyemsaka Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akihama (kuenda zake Madiynah na Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) na mwishowe miguu ya mbele ya farasi wake ikazama ardhini mpaka magotini. Alifariki mnamo mwaka wa 24 A.H.

 

[16] Katika kila amri ya Uislaam kuna hikma, iwe tunaielewa au laa. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alituagiza sisi tuukalie mguu wa kushoto, ili kuweka uzito wa mwili upande wa kushoto kwani hata tumbo liko upande huo wa kushoto, kwa hivyo inalifanya tendo la kijisaidia liwe rahisi, na uyabisi wa tumbo, mama wa mgonjwa pia huondoshwa.

 

[17] Hadiyth hii ni dhaifu.

 

[18] ‘Iysaa na babake Yazdaad wote hawajulikani. Ibn ‘Iyn alisema kuwa: “’Iysaa na babake hawafahamiki.”

 

Share

08-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah: Mlango Wa Ghuslu (Kuoga) Na Hukumu Ya Janaba

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتابُ الطَّهارَة

Kitabu Cha Twahaarah

 

بَابُ اَلْغُسْلِ وَحُكْمِ اَلْجُنُبِ

Mlango Wa Ghuslu (Kuoga) Na Hukumu Ya Janaba

 

 

 

 

 

92.

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {اَلْمَاءُ مِنْ اَلْمَاءِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ وَأَصْلُهُ فِي اَلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Maji (ya ghuslu) ni kutokana na maji (ya kutoka manii)[1].”” [Imetolewa na Muslim, na chanzo chake ni Al-Bukhaariy]

 

 

 

93.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {إِذَا جَلَسَ بَيْنَ شُعَبِهَا اَلْأَرْبَعِ، ثُمَّ جَهَدَهَا، فَقَدْ وَجَبَ اَلْغُسْلُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

زَادَ مُسْلِمٌ: "وَإِنْ لَمْ يُنْزِلْ "

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “(Mwanamume) atakapokaa baina ya sehemu nne za mwanamke, kisha akamfanyia bidii kuingiza dhakari yake[2], itampasa ghuslu.”” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Na katika Muslim aliongeza yafuatayo: “Hata kama hakutokwa na manii.”

 

 

 

94.

وَعَنْ أُمِّ سَلَمَةَ; أَنَّ أُمَّ سُلَيْمٍ وَهِيَ اِمْرَأَةُ أَبِي طَلْحَةَ قَالَتْ: {يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنَّ اَللَّهَ لَا يَسْتَحِي مِنْ اَلْحَقِّ، فَهَلْ عَلَى اَلْمَرْأَةِ اَلْغُسْلُ إِذَا اِحْتَلَمَتْ؟ قَالَ: "نَعَمْ.‏ إِذَا رَأَتِ الْمَاءَ"} اَلْحَدِيثَ.‏ مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kuwa: “Ummu Sulaym[3], mke wa Abuu Twalhah amesema: “Ee Rasuli wa Allaah! Allaah Haionei haki aibu. Je mwanamke inamlazimu afanye ghuslu akiota ndoto ya kujimai[4]?” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ndiyo! Akiona maji maji.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

95.

وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ  رضى الله عنه  قَالَ: {قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم فِي اَلْمَرْأَةِ تَرَى فِي مَنَامِهَا مَا يَرَى اَلرَّجُلُ قَالَ: "تَغْتَسِلُ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

 

زَادَ مُسْلِمٌ: فَقَالَتْ أُمُّ سُلَيْمٍ  {وَهَلْ يَكُونُ هَذَا؟ قَالَ: "نَعَمْ فَمِنْ أَيْنَ يَكُونُ اَلشَّبَهُ؟ }

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema kuhusu mwanamke anayeota usingizini kujimai[5] kama aotavyo mwanamume: “Basi aoge.”” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Muslim aliongeza yafuatayo: “Ummu Salamah aliuliza: “Hii hutokea (kwa mwanamke pia)?”  Akasema:  “Ndiyo! Kwani inatoka wapi kushabihiana (kwa mtoto na mama yake)?”

 

 

 

96.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ اَلنَّبِيَّ  صلى الله عليه وسلم يَغْتَسِلُ مِنْ أَرْبَعٍ: مِنْ اَلْجَنَابَةِ، وَيَوْمَ اَلْجُمُعَةِ، وَمِنْ اَلْحِجَامَةِ، وَمِنْ غُسْلِ اَلْمَيِّتِ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akioga kutokana na mambo manne: Kutoka na janaba, siku ya Ijumaa, baada ya hijaamah (kuumika), na baada ya kuosha maiti[6].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

97.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رضى الله عنه  {فِي قِصَّةِ ثُمَامَةَ بْنِ أُثَالٍ، عِنْدَمَا أَسْلَم وَأَمَرَهُ اَلنَّبِيُّ  صلى الله عليه وسلم أَنْ يَغْتَسِلَ} رَوَاهُ عَبْدُ اَلرَّزَّاقِ

وَأَصْلُهُ مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuhusu kisa cha Thumaamah bin Uthaal[7] aliposilimu, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuamrisha aoge[8].” [Imetolewa na ‘Abdur-Razzaaq, na chanzo chake ni kutoka Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

98.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ  رضى الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم قَالَ: {غُسْلُ اَلْجُمُعَةِ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُحْتَلِمٍ} أَخْرَجَهُ اَلسَّبْعَةُ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ghuslu (kuoga) siku ya Ijumaa ni waajib kwa kila mtu aliyebaleghe.”” [Imetolewa na As-Sab’ah (Al-Bukhaariy, Muslim, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad, At-Tirmidhiy]

 

 

 

99.

وَعَنْ سَمُرَةَ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {مَنْ تَوَضَّأَ يَوْمَ اَلْجُمُعَةِ فَبِهَا وَنِعْمَتْ، وَمَنْ اِغْتَسَلَ فَالْغُسْلُ أَفْضَلُ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ

Kutoka kwa Samurah[9] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kutawadha siku ya Ijumaa anafanya jambo jema, na yule anayeoga, basi ghuslu (kuoga) ni bora zaidi.” [Imetolewa na Maimaam watano na akaipa daraja la Hasan At-Tirmidhiy]

 

 

 

100.

وَعَنْ عَلِيٍّ  رضى الله عنه  قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم يُقْرِئُنَا اَلْقُرْآنَ مَا لَمْ يَكُنْ جُنُبًا} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَهَذَا لَفْظُ اَلتِّرْمِذِيِّ وَحَسَّنَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitufundisha Qur-aan, isipokuwa alipokuwa katika janaba[10].” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, na Musnad Ahmad) na hili ni tamshi la At-Tirmidhiy aliyeipa daraja la Hasan na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

101.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {إِذَا أَتَى أَحَدُكُمْ أَهْلَهُ، ثُمَّ أَرَادَ أَنْ يَعُودَ فَلْيَتَوَضَّأْ بَيْنَهُمَا وُضُوءًا} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

زَادَ اَلْحَاكِمُ: { فَإِنَّهُ أَنْشَطُ لِلْعَوْدِ }

وَلِلْأَرْبَعَةِ عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم يَنَامُ وَهُوَ جُنُبٌ، مِنْ غَيْرِ أَنْ يَمَسَّ مَاءً} وَهُوَ مَعْلُولٌ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akijimai na mkewe, na akataka kurudia, basi na atawadhe[11] baina ya mara hizo mbili.” [Imetolewa na Muslim]

 

Na akaongezea Al Haakim: “Kwani huo (wudhuu) humchangamsha kwa ajili ya kurudia (jimai).”

 

Na Maimaam wanne wamepokea Hadiyth ya ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا): “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa analala na huku ana janaba bila ya kugusa maji[12].” [Imetolewa na Al-Arba’h, Hadiyth hii ina dosari]

 

 

 

102.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم إِذَا اِغْتَسَلَ مِنْ اَلْجَنَابَةِ يَبْدَأُ فَيَغْسِلُ يَدَيْهِ، ثُمَّ يُفْرِغُ بِيَمِينِهِ عَلَى شِمَالِهِ، فَيَغْسِلُ فَرْجَهُ، ثُمَّ يَتَوَضَّأُ، ثُمَّ يَأْخُذُ اَلْمَاءَ، فَيُدْخِلُ أَصَابِعَهُ فِي أُصُولِ اَلشَّعْرِ، ثُمَّ حَفَنَ عَلَى رَأْسِهِ ثَلَاثَ حَفَنَاتٍ، ثُمَّ أَفَاضَ عَلَى سَائِرِ جَسَدِهِ، ثُمَّ غَسَلَ رِجْلَيْهِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ

وَلَهُمَا فِي حَدِيثِ مَيْمُونَةَ: {ثُمَّ أَفْرَغَ عَلَى فَرْجِهِ، فَغَسَلَهُ بِشِمَالِهِ، ثُمَّ ضَرَبَ بِهَا اَلْأَرْضَ}

وَفِي رِوَايَةٍ: {فَمَسَحَهَا بِالتُّرَابِ}

وَفِي آخِرِهِ: {ثُمَّ أَتَيْتُهُ بِالْمِنْدِيلِ} فَرَدَّهُ، وَفِيهِ: { وَجَعَلَ يَنْفُضُ الْمَاءَ بِيَدِهِ }

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akioga janaba, akianza kuosha mikono, kisha anamimina kwa kulia kwake juu ya kushoto kwake na anaosha tupu yake, kisha anatawadha, kisha alichukua maji akapitisha vidole vyake kwenye mizizi ya nywele zake, kisha alitia mafumba matatu ya maji kichwani, kisha anamimina maji sehemu zingine za mwili wake, kisha anaosha miguu yake.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

Nao wawili (Al-Bukhaariy na Muslim) wamesimulia Hadiyth ya Maymuwnah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimwagia tupu yake na akaiosha kwa mkono wake wa kushoto. Kisha akapiga mkono wake ardhini.”

 

Katika Riwaayah nyengine: “Akaupangusa ardhini.”

 

Na mwisho inasema: “Kisha nikamletea kitambaa[13], akakirudisha, na akaendelea kujipangusa maji kwa mkono wake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

103.

وَعَنْ أُمِّ سَلَمَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {قُلْتُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ إِنِّي اِمْرَأَةٌ أَشُدُّ شَعْرَ رَأْسِي، أَفَأَنْقُضُهُ لِغُسْلِ اَلْجَنَابَةِ؟

 

وَفِي رِوَايَةٍ: وَالْحَيْضَةِ؟ فَقَالَ: "لَا، إِنَّمَا يَكْفِيكِ أَنْ تَحْثِي عَلَى رَأْسِكِ ثَلَاثَ حَثَيَاتٍ"} رَوَاهُ مُسْلِم

Kutoka kwa Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nilisema, Ee Rasuli wa Allaah! Mimi ni mwanamke nasuka nywele kichwa changu, Je! Nizifumue ili nipate kuoga janaba?”

 

Katika Riwaayah nyengine: “Na mwisho wa hedhi?” akasema: “Hapana, inatosha kumwagia mafumba matatuya maji kichwani kwako[14].” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

104.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {إِنِّي لَا أُحِلُّ اَلْمَسْجِدَ لِحَائِضٍ وَلَا جُنُبٌ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Siruhusu  Msikiti kwa mwenye hedhi[15] wala mwenye janaba[16].”” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

105.

وَعَنْهَا قَالَتْ: {كُنْتُ أَغْتَسِلُ أَنَا وَرَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم مِنْ إِنَاءٍ وَاحِدٍ، تَخْتَلِفُ أَيْدِينَا فِيهِ مِنَ اَلْجَنَابَةِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

زَادَ ابْنُ حِبَّانَ: وَتَلْتَقِي أَيْدِينَا

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema tena: “Mimi na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) tulikuwa tukioga (ghuslu ya) janaba katika chombo kimoja huku mikono yetu ikipishana.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na akaongezea Ibn Hibbaan: “Na (mikono yetu) ilikuwa inakutana.”

 

 

 

106.

 

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {إِنَّ تَحْتَ كُلِّ شَعْرَةٍ جَنَابَةً، فَاغْسِلُوا اَلشَّعْرَ، وَأَنْقُوا اَلْبَشَرَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَضَعَّفَاهُ

وَلِأَحْمَدَ عَنْ عَائِشَةَ نَحْوُهُ، وَفِيهِ رَاوٍ مَجْهُولٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kuna janaba chini ya kila unywele[17], kwa hivyo osheni nywele na osheni ngozi.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na wote waliidhoofisha]

 

Na katika Riwaayah ya Ahmad, Hadiyth sawa na hiyo imesimuliwa na ‘Aaishah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) na katika Isnaad yake kuna mpokezi mmoja Majhuwl (asiyejulikana).

 

 

[1] Inamaanisha baada ya kutokwa na manii, kuoga ni lazima na muhimu. Hadiyth hii inahusiana na “kutokwa kwa usiku” tu, siyo kwa kujamiiana. Wanazuoni wengi wanaamini hivyo. ‘Ubayy bin Ka’b alisema: “Katika siku za mwanzo za Uislaam, watu wakijamiiana, kuoga hakukuwa lazima hadi manii yawe yametoka; lakini baadaye amri hii ikabatilishwa. Baadhi ya watafiti wameripoti maafikiano ya Muslim juu ya kadhia hii, kwamba, mara kujamiiana kunapoanza, kuoga kunakuwa lazima, hata manii yasipotoka.”

 

[2] Hii inamaanisha kuwa kujamiiana kukianza tu, kuoga kunakuwa lazima. Hadiyth hii inaibatilisha hiyo iliyopita, ikihusiana na kujamiiana.

 

[3] Umm Sulaym ni Ar-Rumaysa au Al-Ghumaysa bint Milhaan, Mama wa Anas bin Maalik. Alikuwa miongoni mwa Swahabiyyah waadilifu. Aliolewa na Maalik bin An-Nasr. Kisha akasilimu, na akamualika aingie Uislaam. Lakini yeye alichukia na akaenda zake Shaam ambako alifia. Kisha akachumbiwa na Abuu Twalha Al-Anaswaariy wakati bado ni mshirikina, lakini yeye akampa sharti kuwa awe Muislaam kwanza, kwa hivyo akasilimu na akamuoa. Alifariki zama za Ukhalifa wa ‘Uthmaan.

 

[4] Kama walivyo wanaume, wanawake pia hupata “Ndoto za kulowana.”

 

[5] Inamaanisha kuwa wanawake pia hutokwa na maji maji kama manii ya mwanamme, ama sivyo watoto wangekuwa hawafanani na mama zao. Kufanana kwa watoto na wazazi wao kunategemea ukali wa hayo manii.

 

[6] Kati ya mambo hayo manne, kuoga baada ya kujamiiana ni fardhi (lazima), kuoga siku ya Ijumaa ni Sunnah (kufuata matendo ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)), na mawili yanayobaki ni Mustahab (yanapendeza). Ahaadiyth kuhusu ulazima wa kuoga siku ya Ijumaa ni sahihi zaidi, kwa hivyo zifuatwe hizo.

 

[7] Thumaamah bin Uthaal alikuwa anatoka kwa Banu Hanifa na Sultani wa watu wa Al-Yamaama. Alikuenda kuhiji Hijjah ndogo (‘Umrah) wakati akiwa bado mushrik na akakamatwa na wapanda farasi wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Walimpeleka Al-Madiynah na wakamfungia katika nguzo ya Msikiti. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuachia huru baada ya siku tatu. Basi akawa Muislaam muadilifu sana na imara sana, zama zile za ukanaji dini, dhidi ya watu wake ambao walighilibiwa na Musailima Al-Kadhdhaab.

 

[8] Mtu asiyekuwa Muislaam anaposilimu, sharti aoge. Abuu Daawuwd aliripoti kuwa, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuamuru Thumaamah aoge aliposilimu.

 

[9] Samurah bin Jundub ni Swahaba maarufu ambaye alipewa jina la utani la Abuu ‘Abdillaah. Alikuwa ni Fazari na alikuwa rafiki wa Answaar. Pia alikuwa mmoja wa mahaafidh waliohifadhi Ahaadiyth nyingi. Alilowea Basra, na alikuwa mkali sana dhidi ya Al-Haruriya. Alifariki mwishoni mwa mwaka 59 A.H.

 

[10] Kutokana na Hadiyth hii na zingine, inathibitika kwamba kusoma Qur-aan Tukufu kwa mtu anayepasa kuoga josho la baada ya kujamiiana, siyo sawa.

 

[11] Kutawadha huku kunapendeza lakini siyo lazima. Pia kunaleta raha na uchangamfu au upya katika hali ya tendo. Inasemekana kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akienda kulala na wakeze mbalimbali katika usiku mmoja, alikuwa akioga kabla ya kuenda kwa kila mmoja. Imeripotiwa pia kuwa mara nyingine alikuwa akitawadha baina yao na mara nyingine hakufanya hivyo. Kwa hivyo katika jambo hili, mtu aweza kuchagua mtindo wowote.

 

[12] Inamaanisha kwamba, kabla ya kuenda kulala, kuoga siyo lazima kwa mtu mwenye janaba. Kuna Hadiyth kutoka kwa Bukhaariy kuhusu kadhia hii kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitawadha kabla ya kula, kunywa au kulala. Kwa hiyo ni ubora kufuata njia za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), ingawa jambo hili linapendeza tu (lakini siyo lazima).

 

[13] Suala la kukausha viungo baada ya kutawadha ni la hiari, kwa hivyo ni hiari ya mtu kujikausha au laa.

 

[14] Hadiyth hii inaweka wazi kwamba, kwa mwanamke mwenye hedhi na kwa mwanamume mwenye janaba, siyo lazima kuzifumua nywele. Kuna Hadiyth nyingine kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) ambayo inataja kufumua nywele. Hadiyth zote mbili ni kwa mazingira au nyakati tofauti.

 

[15] Mwanamke mwenye hedhi haruhusiwi kuingia Msikiti wowote wala kutufu (kuizunguka) Ka’bah, na asiswali wala kufunga akiwa katika hedhi. Swalaah anazozikosa nyakati hizi anasamehewa, lakini ni sharti alipe Swawm baada ya hedhi. Wanazuoni wamekhitilafiana kuhusu mwanamke mwenye hedhi kusoma na kugusa Qur-aan, lakini rai iliyo na nguvu zaidi ni kuwa anaruhusika kuisoma kwani hawezi kuharamika kuihifadhi Qur-aan. Na wengineo wameona pia anaruhusika hata kuigusa wakatoa dalili kadhaa ikiwemo Hadiyth ya ‘Aaishah pindi alipokwenda Hajj ikamjia hedhi akaamrishwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) atekeleze yote wanayoyatekeleza Hujaji isipokuwa kutufu Ka'bah. Ama wengineo wamekubali aisome lakini asiiguse bali anaweza kuikamata kwa kushikia kitambaa au glavu. Kumdhukuru Allaah (عز وجل) imeruhusiwa kwake.   Anaruhusiwa kuenda mahali pa kuswalia ‘Iyd.

 

[16] Inamaanisha kuwa mwanamke mwenye hedhi na mwanamume mwenye janaba hawaruhusiwi kukaa Msikitini lakini kupita tu wanaruhusiwa. Mtu akiwa kalala Msikitini na akaota na akajikojolea huku bado yumo Msikitini, ni lazima atoke nje.

 

[17] Tunaelewa kuwa Hadiyth hii kwamba, ni lazima kuosha mwili mzima baada ya tendo la ndoa, isipokuwa kusukutua mdomo na kuweka maji puani kwa kuwa haya mawili yana ubishi.

 

Share

09-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah: Mlango Wa Tayammum (Kujitwaharisha Kwa Mchanga)

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتابُ الطَّهارَة

Kitabu Cha Twahaarah

 

بَابُ اَلتَّيَمُّمِ

09-Mlango Wa Tayammum (Kujitwaharisha Kwa Mchanga)

           

 

 

 

 

 

107.

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا; أَنَّ اَلنَّبِيَّ  صلى الله عليه وسلم قَالَ: {أُعْطِيتُ خَمْسًا لَمْ يُعْطَهُنَّ أَحَدٌ قَبْلِي: نُصِرْتُ بِالرُّعْبِ مَسِيرَةَ شَهْرٍ، وَجُعِلَتْ لِي اَلْأَرْضُ مَسْجِدًا وَطَهُورًا، فَأَيُّمَا رَجُلٍ أَدْرَكَتْهُ اَلصَّلَاةُ فَلْيُصَلِّ} وَذَكَرَ اَلْحَدِيثَ

وَفِي حَدِيثِ حُذَيْفَةَ عِنْدَ مُسْلِمٍ: {وَجُعِلَتْ تُرْبَتُهَا لَنَا طَهُورًا، إِذَا لَمْ نَجِدِ اَلْمَاءَ}

وَعَنْ عَلِيٍّ  رضى الله عنه  عِنْدَ أَحْمَدَ: {وَجُعِلَ اَلتُّرَابُ لِي طَهُورًا}

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Nimepewa mambo matano hakupewa yeyote kabla yangu: Nimenusuriwa na (kutiwa) kizaazaa (nyoyoni mwa maadui) kwa mwendo wa mwezi. Na nimefanyiwa ardhi kuwa sehemu ya kufanyia ‘ibaadah na kujitwaharishia[1], basi mtu mtu yeyote katika ummah wangu akifikiwa na Swalaah, aswali.”[2]

Katika Hadiyth ya Khudhayfah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) iliyoandikwa na Muslim inaeleza:

“Mchanga[3] wake (au udongo) umefanywa kitoharisho changu ikiwa hatukupata maji.”

 

Na Hadiyth ya ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) iliyoandikwa na Ahmad inasema: “Ardhi (mchanga) wake umefanywa kitoharisho kwa ajili yangu.”

 

 

 

108.

وَعَنْ عَمَّارِ بْنِ يَاسِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {بَعَثَنِي اَلنَّبِيُّ  صلى الله عليه وسلم فِي حَاجَةٍ، فَأَجْنَبْتُ، فَلَمْ أَجِدِ اَلْمَاءَ، فَتَمَرَّغْتُ فِي اَلصَّعِيدِ كَمَا تَمَرَّغُ اَلدَّابَّةُ، ثُمَّ أَتَيْتُ اَلنَّبِيَّ  صلى الله عليه وسلم فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لَهُ، فَقَالَ: "إِنَّمَا كَانَ يَكْفِيكَ أَنْ تَقُولَ بِيَدَيْكَ هَكَذَا" ثُمَّ ضَرَبَ بِيَدَيْهِ اَلْأَرْضَ ضَرْبَةً وَاحِدَةً، ثُمَّ مَسَحَ اَلشِّمَالَ عَلَى اَلْيَمِينِ، وَظَاهِرَ كَفَّيْهِ وَوَجْهَهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ

وَفِي رِوَايَةٍ لِلْبُخَارِيِّ: وَضَرَبَ بِكَفَّيْهِ اَلْأَرْضَ، وَنَفَخَ فِيهِمَا، ثُمَّ مَسَحَ بِهِمَا وَجْهَهُ وَكَفَّيْهِ

Kutoka kwa ‘Ammaar bin Yaasir[4] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alinituma katika haja fulani, kisha nikapata janaba na sikupata maji, nilijiviringisha kwenye mchanga kama mnyama, nikarejea kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) nikamtajia tukio hilo. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaniambia: “Inakutosha kufanya hivi kwa mikono.” Akapiga mikono yake mara moja juu ya mchanga, na akaupangusa mkono wa kushoto juu ya kiganja cha mkono wake wa kulia mbele na nyuma na uso wake.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi ni la Muslim]

 

Na katika Riwaayah ya Al-Bukhaariy: “Na (Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)) akapiga viganja vyake viwili ardhini[5], halafu akavipuliza, akapangusa navyo usoni na viganja vyake.”

 

 

 

109.

وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {التَّيَمُّمُ ضَرْبَتَانِ ضَرْبَةٌ لِلْوَجْهِ، وَضَرْبَةٌ لِلْيَدَيْنِ إِلَى اَلْمِرْفَقَيْنِ} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَصَحَّحَ اَلْأَئِمَّةُ وَقْفَهُ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Tayammum (kujitwaharisha kwa mchanga), ni mapigo mawili, pigo moja kwa ajili ya uso jingine kwa ajili ya mikono hadi kwenye viwiko viwili[6].”” [Imetolewa na Ad-Daaruqutwniy, na akaisahihisha Imaam kama Mawquwf]

 

 

 

110.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {اَلصَّعِيدُ وُضُوءُ اَلْمُسْلِمِ، وَإِنْ لَمْ يَجِدِ اَلْمَاءَ عَشْرَ سِنِينَ، فَإِذَا وَجَدَ اَلْمَاءَ فَلْيَتَّقِ اَللَّهَ، وَلْيُمِسَّهُ بَشَرَتَهُ} رَوَاهُ اَلْبَزَّارُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ اَلْقَطَّانِ، و لَكِنْ صَوَّبَ اَلدَّارَقُطْنِيُّ إِرْسَالَهُ

وَلِلتِّرْمِذِيِّ: عَنْ أَبِي ذَرٍّ نَحْوُهُ، وَصَحَّحَهُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mchanga ni wudhuu wa Muislamu hata kama hatapata maji kwa miaka kumi[7], akiyapata amche Allaah na ayagusishe ngozi yake.” [Imetolewa na Al-Bazzaar, na akaisahihisha Ibn Al-Qatwaan. Lakini aliidhinisha Ad-Daaruqutwniy kama Mursal]

 

Na katika Riwaayah ya At-Tirmidhiy amepokea Hadiyth inayofanana na hiyo kutoka kwa Abuu Dharr[8], ambayo aliisahihisha.

 

 

 

111.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ  رضى الله عنه  قَالَ: {خَرَجَ رَجُلَانِ فِي سَفَرٍ، فَحَضَرَتْ اَلصَّلَاةَ وَلَيْسَ مَعَهُمَا مَاءٌ فَتَيَمَّمَا صَعِيدًا طَيِّبًا، فَصَلَّيَا، ثُمَّ وَجَدَا اَلْمَاءَ فِي اَلْوَقْتِ.‏ فَأَعَادَ أَحَدُهُمَا اَلصَّلَاةَ وَالْوُضُوءَ، وَلَمْ يُعِدِ اَلْآخَرُ، ثُمَّ أَتَيَا رَسُولَ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم فَذَكَرَا ذَلِكَ لَهُ، فَقَالَ لِلَّذِي لَمْ يُعِدْ: "أَصَبْتَ اَلسُّنَّةَ وَأَجْزَأَتْكَ صَلَاتُكَ" وَقَالَ لِلْآخَرِ: "لَكَ اَلْأَجْرُ مَرَّتَيْنِ"} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، و النَّسَائِيُّ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al Khudriy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Watu wawili walikwenda safarini, Swalaah ikawadia, hawakuwa na maji. Walitayammam kwa mchanga safi na wakaswali. Baadaye wakapata maji wakati wa Swalaah. Mmoja wao akarudia Swalaah na kutawadha, mwenzie hakurudia. Walipofika kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wakamueleza hilo, akamgeukia yule ambaye hakurudia akamwambia kuwa: “Umefuata Sunnah, na Swalaah yako ya kwanza imekutosheleza[9].” Akamwambia yule aliyerudia kutawadha na kuswali akamwambia: “Wewe una malipo mara mbili[10].”” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy]

 

 

 

112.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا فِي قَوْلِهِ عَزَّ وَجَلَّ ﴿وَإِنْ كُنْتُمْ مَرْضَى أَوْ عَلَى سَفَرٍ﴾ ‏ قَالَ: "إِذَا كَانَتْ بِالرَّجُلِ اَلْجِرَاحَةُ فِي سَبِيلِ اَللَّهِ وَالْقُرُوحُ، فَيُجْنِبُ، فَيَخَافُ أَنْ يَمُوتَ إِنْ اِغْتَسَلَ: تَيَمَّمَ" .‏ رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ مَوْقُوفًا، وَرَفَعَهُ اَلْبَزَّارُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ، وَالْحَاكِم

Kutoka kwa Ibn “Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuhusu kauli yake Allaah (عَزَّ وَجَلَّ): “...Na mkiwa wagonjwa[11] au mko safarini…” [Al-Maaidah (5: 6)] kuwa: “Ikiwa mtu ana jeraha aloumia akiwa katika (jihaad) njia ya Allaah, kisha akapata janaba, na akaogopa kuwa atakufa endapo ataoga, basi atayammam.” [Imetolewa na Ad-Daaruqutwniy katika Hadiyth Mawquwf, na Al-Bazzaar katika Hadiyth Marfuw’aa, na wakaisahihisha Ibn Khuzaymah na Al Haakim]

 

 

 

113.

وَعَنْ عَلِيٍّ  رضى الله عنه  قَالَ: {اِنْكَسَرَتْ إِحْدَى زَنْدَيَّ فَسَأَلَتْ رَسُولَ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم فَأَمَرَنِي أَنْ أَمْسَحَ عَلَى اَلْجَبَائِرِ} رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَه بِسَنَدٍ وَاهٍ جِدًّا

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mkono wangu mmoja ulivunjika, nikamuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) nifanyeje, akaniamrisha nipanguse juu ya bendeji[12].” [Imetolewa na Ibn Maajah kwa Isnaad dhaifu sana]

 

 

 

114.

وَعَنْ جَابِرٍ بْنُ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا فِي اَلرَّجُلِ اَلَّذِي شُجَّ، فَاغْتَسَلَ فَمَاتَ :{"إِنَّمَا كَانَ يَكْفِيهِ أَنْ يَتَيَمَّمَ، وَيَعْصِبَ عَلَى جُرْحِهِ خِرْقَةً، ثُمَّ يَمْسَحَ عَلَيْهَا وَيَغْسِلَ سَائِرَ جَسَدِهِ"} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِسَنَدٍ فِيهِ ضَعْفٌ، وَفِيهِ اِخْتِلَافٌ عَلَى رُوَاتِهِ

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuhusu mtu aliyejeruhiwa kichwani akaoga na akafariki, kwamba Rasuli wa Allaah  (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ilikuwa inamtosha kutayammam, kisha afunge bendeji na apanguse maji juu yake, kisha aoshe sehemu nyingine za mwili wake.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, Isnaad yake ni dhaifu, na kuna kutofautiana wasimulizi wake]

 

 

 

115.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {مِنْ اَلسُّنَّةِ أَنْ لَا يُصَلِّيَ اَلرَّجُلُ بِالتَّيَمُّمِ إِلَّا صَلَاةً وَاحِدَةً، ثُمَّ يَتَيَمَّمُ لِلصَّلَاةِ اَلْأُخْرَى} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ جِدًّا

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Ni Sunnah mtu kutokuswali zaidi ya Swalaah moja[13] kwa Tayammum moja, kisha atayammam kwa ajili ya Swalaah nyingine.” [Imetolewa na Ad-Daaruqutwniy kwa Isnaad dhaifu sana[14]]

 

 

 

[1] Maana yake ni kwamba, kama maji hakuna, mtu asipoteze nusu ya wakati wa Swalaah kwa kutafuta maji.

 

[2] Vitu vingine hivi vitatu ni: (a) Ngawira amefanyiwa ziwe Halaal, (b) Shufaa siku ya Qiyaamah, (c) Unabii kwa ulimwengu wote.

 

[3] Mchanga au udongo na vitu vyote vingine vitokanavyo na udongo vinahesabika kuwa sawa, na Tayammam kwayo inaruhusiwa. Lakini siyo metali kama antimoni, arseniki, n.k. ambavyo havimo katika fungu la udongo.

 

 

[4]  ‘Ammaar alipewa jina la utani la Abul-Yaqzaan, na alikuwa miongoni mwa Swahaba waandamizi wa mwanzo, aliteswa kule Makkah kwa ajili ya Iymaan yake. Alishiriki katika Hijrah zote mbili, na katika vita vya Badr na vita vyote muhimu. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuambia kuwa: “Ee ‘Ammaar, kundi la wapotofu litakuua wewe.” Hiyo ilitokea Siffiyn mnamo mwaka wa 36 A.H wakati akiwa na ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), aliuawa na askari wa Mu’aawiya akiwa na umri wa miaka 73.

 

[5] Hadiyth hii inaongelea kuhusu Tayammam (kujitwaharisha kwa udongo). 'Ulamaa wa Fiqh wanasema kuwa pigo moja tu linatosha kwa uso na mikono yote miwili. Wengine wanasema kuwa mapigo mawili ni lazima, moja kwa uso na jingine kwa mikono, kama inavyotajwa katika Hadiyth hii inayofuata. Lakini Hadiyth zote zinazotaja mapigo mawili ni dhaifu.

 

[6] ‘Ulamaa wa Hadiyth wameihesabu Hadiyth hii kuwa ni dhaifu na milolongo yake yote ni dhaifu.

 

[7] Inamaanisha kwamba, wakati wa dharura, mchanga (udongo) ni badala kamili ya maji, na unakidhi shughuli zote za utwahirishaji, uwe ni kutawadha, au kuoga. Kwa kila Tayammam moja, matendo mengi ya faradhi yanaweza kufanywa, iwapo hakuna mazingira yanayoubatilisha.

 

[8] Jina la Abuu Dharr lilikuwa ni Jundub bin Junaadah, naye alikuwa miongoni mwa Swahaba maarufu na ni mtu aliyejinyima anasa za kimwili. Alisilimu mapema sana kule Makkah, kisha akaenda kwa watu wake. Alikuja kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Al-Madiynah, na baadaye akalowea na akafia Rabdha mnamo mwaka wa 32 A.H.

 

[9] Inamaanisha kwamba, ikiwa mtu amekwisha kuswali Swalaah moja kwa kutumia Tayammam, basi hakuna haja ya kurudia kuswali, hata kama maji yamepatikana baadaye tena kabla wakati wa Swalaah ile haujapita.

 

[10] Haikuwa lazima kurudia kuiswali Swalaah ile, kama Swalaah ile iliswaliwa kwa wudhuu wa kutayammam. Huyo mtu wa pili alipata malipo maradufu siyo kwa sababu kaswali mara mbili Swalaah moja, bali kwa sababu ya kufanya uamuzi kuhusu tatizo lililowakabili, hata kama uamuzi ule haukuwa sahihi, lakini kuna malipo zaidi kwa uamuzi usiyo sahihi. Sababu ya pili ya kupata malipo mara mbili, inawezekana ni kwamba aliswali mara mbili, mara moja kwa wudhuu wa Tayammam na mara ya pili kwa wudhuu wa maji.

 

[11] Inamaanisha kuwa ukiwa unataka kuswali lakini kuna kizuizi katika kutawadha au kuoga, Tayammam huwa ni lazima. Hapa ugonjwa ni ugonjwa kweli, siyo vipele au vijipu tu. (Kulingana na Maalik, Hanafi na moja katika maneno ya Imaam Shaafi’). Wengine kama (Ahmad na moja katika maneno ya Imaam shaafi’) kuwa Tayammam hairuhusiwi isipokuwa kwa mgonjwa anayehofia kuwa maji yatamsababishia kifo. Daawuwd anaona kuwa Tayammam inaruhusiwa kwa mgonjwa yoyote bila kujali kama anadhurika na maji au la.

 

[12] Neno la Kiarabu ni اَلْجَبَائِرِ ambalo hutumika kwa vile vipande vya mbao vinavyowekwa kuuzunguka mkono au mguu uliovunjika ili kuufanya ukae umenyooka saa zote.

 

[13] Kwa kuwa kutawadha kwa kutayammam ni badala ya kutawadha kwa maji, hufanya kazi namna ile ile. Swalaah nyingi zinaweza kuswaliwa kwa kutawadha kwa maji mara moja tu. Halikadhalika, Swalaah nyingi zinaweza kuswaliwa kwa kutayamamu mara moja tu. Watu wengine baada ya kutayamamu kwa kujamiiana au kwa kuota na kutoa manii husita kuingia Msikitini au kusoma Qur-aan. Hii ni kutia shaka kuovu na ni ushawishi wa shaytwaan tu, na wala usiujali. Hadiyth hii ya Hasan bin ‘Ammaar ni dhaifu katika mlolongo wa wapokezi. Kuna Hadiyth mbili zingine kuhusu kadhia hii hii na zote ni dhaifu.

 

[14]

  Hadiyth hii ni dhaifu kwa sababu ilisimuliwa na Hasan bin ‘Ammaar ambaye alikuwa dhaifu. Kwa sababu hii ‘Ulamaa walisema hawaitegemei lakini wakasema kwamba: “Allaah (عز وجل) Ameturuhusu tutumie udongo kukiwa hakuna maji. Na kwa kuwa kutawadha ni lazima baada ya kuenda haja ndogo au haja kubwa au kutoa upepo, basi halikadhalika kwa kutayammam.”

 

Share

10-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Twahaarah: Mlango Wa Hedhi

 

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتابُ الطَّهارَة

Kitabu Cha Twahaarah

 

بَابُ اَلْحَيْضِ

10-Mlango Wa Hedhi

 

 

 

 

116.

 

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {إِنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ أَبِي حُبَيْشٍ كَانَتْ تُسْتَحَاضُ، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم  "إِنَّ دَمَ اَلْحَيْضِ دَمٌ أَسْوَدُ يُعْرَفُ، فَإِذَا كَانَ ذَلِكَ فَأَمْسِكِي مِنَ اَلصَّلَاةِ، فَإِذَا كَانَ اَلْآخَرُ فَتَوَضَّئِي، وَصَلِّي"} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ، وَاسْتَنْكَرَهُ أَبُو حَاتِمٍ

وَفِي حَدِيثِ أَسْمَاءَ بِنْتِ عُمَيْسٍ عِنْدَ أَبِي دَاوُدَ: {لِتَجْلِسْ فِي مِرْكَنٍ، فَإِذَا رَأَتْ صُفْرَةً فَوْقَ اَلْمَاءِ، فَلْتَغْتَسِلْ لِلظُّهْرِ وَالْعَصْرِ غُسْلاً وَاحِدًا، وَتَغْتَسِلْ لِلْمَغْرِبِ وَالْعِشَاءِ غُسْلاً وَاحِدًا، وَتَغْتَسِلْ لِلْفَجْرِ غُسْلاً، وَتَتَوَضَّأْ فِيمَا بَيْنَ ذَلِكَ }

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: Fatwmah bint Abiy Hubaysh alikuwa na hedhi ya kudumu[1], Rasulu wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Damu ya hedhi ni nyeusi inatambulika, kwa hivyo ikiwa ndiyo hiyo, jizuie kuswali, na ikiwa ni nyingine (iliyopauka), basi tawadha na uswali.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy, wakaisahihisha Ibn Hibbaan na Al Haakim, na akaiita Munkar (si ya kawaida) Abuu Haatim]

Na katika Hadiyth ya Asmaa bint ‘Umays[2] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) iliyopokewa na Abuu Daawuwd, amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “(Mwanamke) Akae ndani ya bafu lenye maji, na akiona rangi ya njano hivi juu ya maji, basi afanye ghuslu moja kwa Swalaah ya Adhuhuri na Alasiri na afanye ghuslu moja tena kwa Swalaah ya Magharibi na ‘Ishaa, na afanye ghuslu kwa Swalaah ya Alfajiri, na baina ya nyakati hizi atawadhe.”

 

 

 

117.

 

وَعَنْ حَمْنَةَ بِنْتِ جَحْشٍ قَالَتْ: {كُنْتُ أُسْتَحَاضُ حَيْضَةً كَبِيرَةً شَدِيدَةً، فَأَتَيْتُ اَلنَّبِيَّ  صلى الله عليه وسلم أَسْتَفْتِيهِ، فَقَالَ: "إِنَّمَا هِيَ رَكْضَةٌ مِنَ اَلشَّيْطَانِ، فَتَحَيَّضِي سِتَّةَ أَيَّامٍ، أَوْ سَبْعَةً، ثُمَّ اِغْتَسِلِي، فَإِذَا اسْتَنْقَأْتِ فَصَلِّي أَرْبَعَةً وَعِشْرِينَ، أَوْ ثَلَاثَةً وَعِشْرِينَ، وَصُومِي وَصَلِّي، فَإِنَّ ذَلِكَ يُجْزِئُكَ، وَكَذَلِكَ فَافْعَلِي كَمَا تَحِيضُ اَلنِّسَاءُ، فَإِنْ قَوِيتِ عَلَى أَنْ تُؤَخِّرِي اَلظُّهْرَ وَتُعَجِّلِي اَلْعَصْرَ، ثُمَّ تَغْتَسِلِي حِينَ تَطْهُرِينَ وَتُصَلِّينَ اَلظُّهْرَ وَالْعَصْرِ جَمِيعًا، ثُمَّ تُؤَخِّرِينَ اَلْمَغْرِبَ وَتُعَجِّلِينَ اَلْعِشَاءِ، ثُمَّ تَغْتَسِلِينَ وَتَجْمَعِينَ بَيْنَ اَلصَّلَاتَيْنِ، فَافْعَلِي.‏ وَتَغْتَسِلِينَ مَعَ اَلصُّبْحِ وَتُصَلِّينَ.‏ قَالَ: وَهُوَ أَعْجَبُ اَلْأَمْرَيْنِ إِلَيَّ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَحَسَّنَهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Hamnah bint Jahsh[3] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: Nilikuwa na hedhi yangu ilikuwa nyingi mno na kali, kwa hivyo nilikwenda kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kumtaka fatwa, akasema: “Hii ni athari ya shaytwaan, kwa hivyo wewe zingatia hedhi yako kwa siku sita au saba, kisha fanya ghuslu na ukitwaharika, swali kwa siku ishirini na tatu au ishirini na nne, na ufunge na uswali, kwani hiyo itakutosheleza wewe, na ufanye hivyo hivyo kila mwezi kama wanavyopata hedhi wanawake wengine.  Lakini ukiwa na nguvu[4] unaweza kuakhirisha Swalaah ya Adhuhuri na kutanguliza Alasiri, kisha fanya ghuslu na uswali Adhuhuri na Alasiri pamoja kisha akhirisha Magharibi na kutanguliza ‘Ishaa, fanya hivyo, na ufanye ghuslu na ukusanye baina ya Swalaah mbili, fanya hivyo na fanya ghuslu asubuhi na uswali Alfajiri.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mimi hii ninaipendelea zaidi, (yaani kufanya ghuslu kwa kila Swalaah).” [Imetolewa na Al Khamsah (Maimaam watano wa Hadiyth) ila An-Nasaaiy. Na akaisahihisha At-Tirmidhiy, na akaipa daraja la Hasan, Al-Bukhaariy]

 

 

 

118.

 

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا; {أَنَّ أُمَّ حَبِيبَةَ بِنْتَ جَحْشٍ شَكَتْ إِلَى رَسُولِ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم اَلدَّمَ، فَقَالَ: "اُمْكُثِي قَدْرَ مَا كَانَتْ تَحْبِسُكِ حَيْضَتُكِ، ثُمَّ اِغْتَسِلِي" فَكَانَتْ تَغْتَسِلُ كُلَّ صَلَاةٍ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَفِي رِوَايَةٍ لِلْبُخَارِيِّ: {وَتَوَضَّئِي لِكُلِّ صَلَاةٍ} وَهِيَ لِأَبِي دَاوُدَ وَغَيْرِهِ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ.

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Ummu Habiybah bint Jahsh[5] alimshtakia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) damu (iliyokuwa ikitoka zaidi ya kipindi cha hedhi); akasema: “Kaa kadiri ilivyokuwa hedhi yako inakuzuia kuswali, kisha fanya ghuslu.” Akawa anafanya ghuslu kila Swalaah[6]. [Imetolewa na Muslim]

 

Na katika Riwaayah ya Al-Bukhaariy: “Tawadha kwa kila Swalaah.” [Pia ameipokea na Abuu Daawuwd na wengine kwa namna nyingine.]

 

 

 

119.

 

وَعَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كُنَّا لَا نَعُدُّ اَلْكُدْرَةَ وَالصُّفْرَةَ بَعْدَ اَلطُّهْرِ شَيْئًا} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ، وَأَبُو دَاوُدَ وَاللَّفْظُ لَهُ

Kutoka kwa Ummu ‘Aatwiyyah[7] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Hatukuwa tukihesabu unjano na ukahawia kuwa ni chochote (majimaji yanayotokea ukeni[8]) baada ya Twahaarah.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy na Abuu Daawuwd, na tamshi hili ni lake]

 

 

 

120.

 

وَعَنْ أَنَسٍ  رضى الله عنه  {أَنَّ اَلْيَهُودَ كَانُوا إِذَا حَاضَتْ اَلْمَرْأَةُ لَمْ يُؤَاكِلُوهَا، فَقَالَ اَلنَّبِيُّ  صلى الله عليه وسلم  "اِصْنَعُوا كُلَّ شَيْءٍ إِلَّا اَلنِّكَاحَ"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Mayahudi walikuwa hawali na mwanamke wakati ana hedhi, kwa hivyo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Fanyeni kila kitu (na wake zenu) isipokuwa kujamiiana.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

121.

 

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم يَأْمُرُنِي فَأَتَّزِرُ، فَيُبَاشِرُنِي وَأَنَا حَائِضٌ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiniamrisha kuvaa Izaar[9] (gagulo) kisha ananipapasa kwa mahaba[10] wakati nina hedhi.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

122.

 

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، عَنِ اَلنَّبِيِّ  صلى الله عليه وسلم فِي اَلَّذِي يَأْتِي اِمْرَأَتَهُ وَهِيَ حَائِضٌ قَالَ: {يَتَصَدَّقُ بِدِينَارٍ، أَوْ نِصْفِ دِينَارٍ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ وَابْنُ اَلْقَطَّانِ، وَرَجَّحَ غَيْرَهُمَا وَقْفَهُ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema kuhusu mume anayejamiiana na mkewe akiwa na hedhi: “Atoe dinari moja au nusu dinari kama Swadaqah.” [Imetolewa na Al-Khamsah (watano). Wakaisahihisha Al-Haakim na Ibn Al-Qatwaan, na wengine waliita kuwa Mawquwf[11]]

 

 

 

123.

 

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {أَلَيْسَ إِذَا حَاضَتْ لَمْ تُصَلِّ وَلَمْ تَصُمْ؟} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ فِي حَدِيثٍ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Je si kweli kuwa mwanamke aliye katika hedhi haswali wala hafungi[12]?” [Al-Bukhaariy, Muslim na ni sehemu ya Hadiyth ndefu]

 

 

 

124.

 

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {لَمَّا جِئْنَا سَرِفَ حِضْتُ، فَقَالَ اَلنَّبِيُّ  صلى الله عليه وسلم  "اِفْعَلِي مَا يَفْعَلُ اَلْحَاجُّ، غَيْرَ أَنْ لَا تَطُوفِي بِالْبَيْتِ حَتَّى تَطْهُرِي"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ فِي حَدِيثٍ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Tulipofika mahali paitwapo Sarif, mimi nilipata hedhi, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaniambia: “Wewe fanya analolifanya Haji isipokuwa usifanya twawaaf (kutufu Ka’bah) mpaka ukishatwahirika.” [Al-Bukhaariy, Muslim, na ni sehemu ya Hadiyth ndefu]

 

 

 

125.

 

وَعَنْ مُعَاذٍ  رضى الله عنه  {أَنَّهُ سَأَلَ اَلنَّبِيَّ  صلى الله عليه وسلم مَا يَحِلُّ لِلرَّجُلِ مِنِ اِمْرَأَتِهِ، وَهِيَ حَائِضٌ؟ قَالَ: "مَا فَوْقَ اَلْإِزَارِ"} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَضَعَّفَهُ

Kutoka kwa Mu’aadh (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuuliza Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kitu gani halali kwa mwanamume kwa mkewe wakati ana hedhi? Akasema: “Kilicho juu ya Izaar[13].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaidhoofisha]

 

 

 

126.

 

وَعَنْ أُمِّ سَلَمَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَتِ اَلنُّفَسَاءُ تَقْعُدُ فِي عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم بَعْدَ نِفَاسِهَا أَرْبَعِينَ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ، وَاللَّفْظُ لِأَبِي دَاوُدَ

وَفِي لَفْظٍ لَهُ: {وَلَمْ يَأْمُرْهَا اَلنَّبِيُّ  صلى الله عليه وسلم بِقَضَاءِ صَلَاةِ اَلنِّفَاسِ} وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Wanawake wenye nifaas zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) walikuwa wakikaa (bila kuswali) kwa siku arubaini[14].” [Imetolewa na Al Khamsah isipokuwa An-Nisaaiy, na tamshi hili ni la Abuu Daawuwd]

 

Na katika Riwaayah nyengine ya Abuu Daawuwd anasema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakumuamrisha (mzazi) alipe Swalaah alizoacha wakati wa nifaas yake.” [Aliisahihisha Al Haakim]

 

 

 

[1] Istihaadhwah (damu imtokayo mwanamke ukeni) ni damu inayodumu muda mrefu na inaweza kuwa ni damu ya uzazi au ya hedhi, na huhesabika kuwa ni kutokwa na damu kati kati ya vipindi. Kipindi cha hedhi, kwa mujibu wa ‘Ulamaa ni kutoka siku moja mpaka siku kumi na tano; na kwa mujibu wa wengine ni kutoka siku tatu mpaka siku kumi. Uzoefu unaonyesha kuwa huo usemi wa pili ni sahihi zaidi. Kila mwanamke huwa anafahamu vipindi vyake, na akitokwa damu zaidi ya wakati wake, basi hiyo ni Istihaadhwah.

 

 

[2] Asmaa alikuwa mke wa Ja’far bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Alihajiri pamoja naye hadi Habashah (Abyssinia   Ethiopia), na alimzalia watoto watatu, na kati ya hao ni ‘Abdullaah. Baada ya Ja’far (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kufa Shahidi katika vita vya Mut’a, Abuu Bakar Swiddiyq (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuoa Asmaa ambaye alimzalia mtoto mmoja Muhammad. Na baada ya kufariki Abuu Bakar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuoa Asmaa ambaye alimzalia Yahyaa. ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alizowea kumuuliza Asmaa tafsiri ya ndoto. Alikufa baada ya kifo cha ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).

 

 

 

[3] Hamnah bint Jahsh ni dada wa “Mama wa Waumini”, Zaynab bint Jahsh. Alioelewa na Musw’ab bin ‘Umayr ambaye alikufa Shahidi katika  vita vya Uhud, na baada ya hivyo akaolewa na Twalhah bin ‘Ubaydillaah.

 

 

[4] Katika Hadiyth hii Hamnah aliamriwa kuoga mara tatu kila siku. Aoge mara moja kwa ajili ya Swalaah za Adhuhuri na Alasiri, na aoge mara ya pili kwa Swalaah za Magharibi na ‘Ishaa, na aoge mara ya tatu kwa Swalaah ya Alfajiri. Katika Hadiyth iliyopita, Faatwimah binti Abiy Hubaysh aliamuriwa achukue wudhuu tu kabla ya kila Swalaah. Hii inamaanisha kuwa, kwa mwanamke anayekuwa na Istihaadhwah kuoga siyo lazima, lakini kuchukuwa wudhuu ni lazima kwa kila Swalaah. Kuoga ni bora ikiwa hali ya afya na ya hewa itaruhusu, vinginevyo hakuna haja ya kuoga.

 

 

[5] Habiybah bint Jahsh alikuwa dada mwingine wa “Mama wa Waumini” Zaynab bint Jahsh, naye aliolewa na ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf. Mulsim alisimulia kuwa alikuwa na damu iliyodumu miaka saba. Alifariki mnamo mwaka wa 44 A.H.

 

[6] Ilikuwa ni hatua ya hiari na ya tahadhari tu kwa Umm Habiybah kuoga kwa kila Swalaah. Uamuzi sahihi kuhusu kadhia hii ni kuoga baada ya hedhi na atawadhe. Kuhusu kutokwa damu kwa muda mrefu mno, ipo amri ya kuosha damu na kuchukua wudhuu katika kila Swalaah.

 

[7] Ummu ‘Atwiyyah ni jina la Nusaybah Ka’b bint Al-Haarith Al-Ansariyya. Alikuwa ni miongoni mwa Swahaba wa kike maarufu, na alikuwa akiongozana na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) vitani akiwauguza wagonjwa na kuwatibu majeruhi. Alipigana katika Vita vya Uhud kama shujaa. Alishuhudia kuoshwa kwa maiti ya binti wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ambako alieleza na alitusimulia, na Swahaba, Taabi’, ‘Ulamaa wa Basra walirikodi kutoka kwake. Hadiyth yake inahesabika kuwa ndiyo msingi wa kuosha maiti. Alikuwa mmoja wa Swahaba wa kike waliolowea kule Basra.

 

[8] Katika usimulizi wa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) majimaji ya rangi ya njano au na vumbi yanahesabika kuwa ni damu ya hedhi, lakini Hadiyth hii inasema: “Tuliyahesabu kuwa siyo kitu.” Hadiyth hizi mbili zaelekea kujipinga, lakini zote mbili ni sahihi katika muktadha wa kila moja. Ikiwa majimaji ya rangi ya njano au ya vumbi yatajitokeza wakati wa kipindi cha hedhi, yatahesabika kuwa ni “damu ya hedhi.” Lakini yakijitokeza baada ya kipindi cha hedhi basi si chochote kama maneno ya Kiarabu ya بَعْدَ اَلطُّهْرِ yanavyodokeza.

 

 

[9] Vazi linalovaliwa kutoka kiunoni kuenda chini kama gagulo au sketi.

 

[10] Wale ambao hawazisadiki Hadiyth, yaani wakanushaji wa Sunnah, wanaleta utata na mashaka hapa, na wanawafanya watu wazishuku Hadiyth. Wanasema kuwa tendo la ndoa katika kipindi cha hedhi limekatazwa na Qur-aan lakini kwa mujibu wa Hadiyth hii Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alifanya wakati ule, kwa hiyo Hadiyth hiyo siyo sahihi. Maana ya maneno ya ‘Mubaasharat’ ni kugusa na kuukanda mwili kwa mwili, na kwa kifumbo maana yake ni kufanya tendo la ndoa. Katika Hadiyth imewekwa wazi kwamba tendo la ndoa limekatazwa wakati ya hedhi ya mwanamke. Kwa hivyo ni udanganyifu tu kutafsiri neno hilo ‘mubashaarat’ kuwa ni ‘tendo la ndoa’ badala ya kulitafsiri kuwa ni ‘kushikashika kwa mahaba’ na kuleta mashaka.

 

[11] Hii ni Hadiyth dhaifu, kwa hivyo wengi wa ‘Ulamaa hawadhani kuwa ni lazima kufidia, ingawa baadhi ya ‘Ulamaa hudhani inafaa kufidia, lakini rai ya kwanza ni sahihi kwa kuwa amri hiyo ni kwa kuhamasisha Swadaqah.

 

[12] Hii ni sehemu ndogo tu ya Hadiyth ndefu. Alipokuwa akitoa khutbah kwa wanawake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaambia kuwa dini yao haijakamilika. Walipouliza kwa namna gani, kwa kusema maneno yanayomaanisha kuwa wanawake walio na hedhi wasiswali wala wasifunge Swawm.

 

[13] Kila kilicho juu ya Izaar (Nguo inayovaliwa chini ya kiuno) inaweza kuwa na maana mbili: kwanza inaweza kuwa na maana ya jimai. Kwa maneno mengine, kila kitu kinaruhusiwa isipokuwa jimai. Pili: ina maana ya ile sehemu inayovaliwa Izaar. Ila maana hii inaweza kupingana na Hadiyth isemayo: “Fanyeni kila kitu isipokuwa jimai.” Kwa hivyo basi ni vizuri kutumia maana ya kwanza.

 

[14] Hii inamaanisha ni kile kiwango cha juu cha siku za damu ya uzazi, na hakuna kiwango chake cha chini. Laiti ikiendelea zaidi ya siku arubaini, basi itakuwa ni Istihaadhwah (damu ya ugonjwa), ambayo siyo kizuizi kwa Swalaah, wala kufunga Swawm, wala kufanya tendo la ndoa. Kila amri kuhusu damu na uzazi ni sawa na ile ya damu ya hedhi.

 

 

 

Share