031-Asbaabun-Nuzuwl: Al-A'raaf Aayah 031: يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

031: Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu (ya mavazi ya sitara na twahara) katika kila mahala pa ‘Ibaadah.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾

Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu (ya mavazi ya sitara na twahara) katika kila mahala pa ‘Ibaadah. Na kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu. [Al-A’raaf (7:31)]

 

Sababun-Nuzwul:

 

Sa’iyd bin Jubayr amehadithia kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kwamba Washirikina wanawake na wanaume walikuwa wakitufu Al-Ka’bah. Wanaume wakitufu mchana na wanawake wakitufu usiku. Wanawake wakisema wanapotufu: Leo baadhi yake (uchi) au wote uonekane na kitakachoonekana sikitolei ruhusa. Hapo ikateremka:

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ  

Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu (ya mavazi ya sitara na twahara) katika kila mahala pa ‘Ibaadah.   [Al-A’raaf (7:31)]

 

 

Share