02-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah - كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

 

 

 

 

كِتابُ الصَّلاة

Kitabu Cha Swalaah

 

 

 

 

 

Share

01-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Nyakati Za Swalaah

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

Kitabu cha Swalaah

 

بَابُ اَلْمَوَاقِيتِ

Mlango Nyakati Za Swalaah

 

 

 

127.

عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِوٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا‏ ، أَنَّ نَبِيَّ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {وَقْتُ اَلظُّهْرِ إِذَا زَالَتْ اَلشَّمْسُ‏،  وَكَانَ ظِلُّ اَلرَّجُلِ كَطُولِهِ  مَا لَمْ يَحْضُرْ اَلْعَصْرُ‏،  وَوَقْتُ اَلْعَصْرِ مَا لَمْ تَصْفَرَّ اَلشَّمْسُ‏،  وَوَقْتُ صَلَاةِ اَلْمَغْرِبِ مَا لَمْ يَغِبْ اَلشَّفَقُ‏،  وَوَقْتُ صَلَاةِ اَلْعِشَاءِ إِلَى نِصْفِ اَللَّيْلِ اَلْأَوْسَطِ‏،  وَوَقْتُ صَلَاةِ اَلصُّبْحِ مِنْ طُلُوعِ اَلْفَجْرِ مَا لَمْ تَطْلُعْ اَلشَّمْسُ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَلَهُ مِنْ حَدِيثِ بُرَيْدَةَ فِي اَلْعَصْرِ: {وَالشَّمْسُ بَيْضَاءُ نَقِيَّةٌ}

وَمِنْ حَدِيثِ أَبِي مُوسَى: {وَالشَّمْسُ مُرْتَفِعَةٌ}

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Wakati wa Swalaah ya Adhuhuri[1] ni jua linapopinduka (meridani) na kivuli cha mtu kuwa kama urefu wake, madamu haujaingia wakati wa Swalaah ya Alasiri. Wakati wa Swalaah ya Alasiri ni muda jua halijawa njano (machweo). Wakati wa Swalaah ya Magharibi (machweo)[2] ni katika wakati wa mawingu hayajapotea[3]. Wakati wa Swalaah ya ‘Ishaa hadi nusu ya usiku. Wakati wa Swalaah ya Alfajiri ni tangu kuchomoza Alfajiri mpaka wakati wa kuchomoza jua.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

Buraydah[4] amesema katika Hadiyth nyengine kuhusu Alasiri   kuwa: “Jua likiwa jeupe angavu[5].” [Imetolewa na Muslim]

 

 

Na Hadiyth ya Abuu Muwsaa[6] amesema kuhusu wakati wa Swalaah ya Alasiri: “Wakati jua liko juu.”[7] [Imetolewa na Muslim katika Hadiyth ndefu inayosema: “Kisha akamuamrisha akakimu Alasiri”]

 

 

 

128.

وَعَنْ أَبِي بَرْزَةَ الْأَسْلَمِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم  يُصَلِّيَ اَلْعَصْرَ‏، ثُمَّ يَرْجِعُ أَحَدُنَا إِلَى رَحْلِهِ  فِي أَقْصَى اَلْمَدِينَةِ  وَالشَّمْسُ حَيَّةٌ‏،  وَكَانَ يَسْتَحِبُّ أَنْ يُؤَخِّرَ مِنْ اَلْعِشَاءِ‏،  وَكَانَ يَكْرَهُ اَلنَّوْمَ قَبْلَهَا  وَالْحَدِيثَ بَعْدَهَا‏،  وَكَانَ يَنْفَتِلُ مِنْ صَلَاةِ اَلْغَدَاةِ حِينَ يَعْرِفُ اَلرَّجُلُ جَلِيسَهُ‏،  وَيَقْرَأُ بِالسِّتِّينَ إِلَى اَلْمِائَةِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَعِنْدَهُمَا مِنْ حَدِيثِ جَابِرٍ: {وَالْعِشَاءَ أَحْيَانًا وَأَحْيَانًا: إِذَا رَآهُمْ اِجْتَمَعُوا عَجَّلَ‏، وَإِذَا رَآهُمْ أَبْطَئُوا أَخَّرَ‏،  وَالصُّبْحَ: كَانَ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم  يُصَلِّيهَا بِغَلَسٍ}  

وَلِمُسْلِمٍ مِنْ حَدِيثِ أَبِي مُوسَى: {فَأَقَامَ اَلْفَجْرَ حِينَ اِنْشَقَّ اَلْفَجْرُ‏، وَالنَّاسُ لَا يَكَادُ يَعْرِفُ بَعْضُهُمْ بَعْضًا}

Kutoka kwa Abuu Barzah Al-Aslamiy[8] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Swalaah ya Alasiri na baada ya Swalaah, mmoja wetu alirejea nyumbani kwake mwisho kabisa wa Madiynah na kufika wakati jua bado linang’aa, na alipenda kuichelewesha Swalaah ya ‘Ishaa, na hakupenda kulala usingizi kabla yake na kuzungumza baada yake.[9] Na baada ya Swalaah ya Fajr alikuwa akitoka wakati mtu aliweza kumtambua mwenzie aliyekaa karibu naye, na alikuwa akisoma Aayah sitini hadi mia za Qur-aan katika Swalaah ya Fajr.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Kwao wawili (Al-Bukhaariy na Muslim) wamepokea Hadiyth ya Jaabir kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiiwahisha Swalaah ya ‘Ishaa na mara nyingine akiichelewesha, kila alipowaona watu wamekusanyika ili kuswali ‘Ishaa, aliiswali mapema, na watu wakiwa wamechelewa, naye aliichelewesha. Swalaah ya Fajr aliiswali wakati bado kungali kiza.”[10]

 

Muslim alimnukuu Abuu Muwsaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Fajr wakati wa kupambazuka ambapo watu hawakutambuana.”

 

 

 

129.

وَعَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ  رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {كُنَّا نُصَلِّي اَلْمَغْرِبَ مَعَ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم  فَيَنْصَرِفُ أَحَدُنَا وَإِنَّهُ لَيُبْصِرُ مَوَاقِعَ نَبْلِهِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Raafi’ bin Khadiyj[11] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Tulikuwa tukiswali Magharibi na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) halafu mmoja wetu alitoka nje ya Msikiti akaweza kuona mahali mshale ulipoangukia.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

130.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {أَعْتَمَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم  ذَاتَ لَيْلَةٍ بِالْعَشَاءِ‏،  حَتَّى ذَهَبَ عَامَّةُ اَللَّيْلِ‏،  ثُمَّ خَرَجَ‏، فَصَلَّى‏، وَقَالَ: "إِنَّهُ لَوَقْتُهَا لَوْلَا أَنْ أَشُقَّ عَلَى أُمَّتِي"}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alichelewesha Swalaah ya ‘Ishaa hadi sehemu kubwa ya usiku ilipopita, halafu akenda nje akaswali Swalaah ya ‘Ishaa akasema: “Huu ndio wakati wake[12] ingekuwa siyo kuogopea mashaka kwa Ummah wangu.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

131.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم   {إِذَا اِشْتَدَّ اَلْحَرُّ فَأَبْرِدُوا بِالصَّلَاةِ‏، فَإِنَّ شِدَّةَ اَلْحَرِّ مِنْ فَيْحِ جَهَنَّمَ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Joto likiwa kali lipoze kwa Swalaah[13] kwani ukali wa joto hutoka kwenye pumzi ya Jahannam.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

132.

وَعَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم   {أَصْبِحُوا بِالصُّبْحِ فَإِنَّهُ أَعْظَمُ لِأُجُورِكُمْ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ‏، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ‏، وَابْنُ حِبَّانَ

 

Kutoka kwa Raafi’ bin Khadiyj (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Pambazukeni kwa Swalaah ya Alfajiri[14] kwani hiyo ndio kubwa zaidi kwa ujira wenu.” [Imetolewa na Al-Khamsah na wakaipa daraja la Swahiyh At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan] 

 

 

 

133.

‏ وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {مَنْ أَدْرَكَ مِنْ اَلصُّبْحِ رَكْعَةً قَبْلِ أَنْ تَطْلُعَ اَلشَّمْسُ فَقَدْ أَدْرَكَ اَلصُّبْحَ‏، وَمَنْ أَدْرَكَ رَكْعَةً مِنْ اَلْعَصْرِ قَبْلَ أَنْ تَغْرُبَ اَلشَّمْسُ فَقَدْ أَدْرَكَ اَلْعَصْرَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَلِمُسْلِمٍ عَنْ عَائِشَةَ نَحْوَهُ‏، وَقَالَ: "سَجْدَةً" بَدَلَ "رَكْعَةً". ثُمَّ قَالَ: وَالسَّجْدَةُ إِنَّمَا هِيَ اَلرَّكْعَةُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuipata Rakaa moja ya Swalaah ya Alfajiri kabla jua halijachomoza, anakuwa ameipata Swalaah ya Alfajiri kwa wakati wake, na mtu anayeswali Rakaa ya Alasiri kabla ya jua halijatua anakuwa ameipata Swalaah ya Alasiri.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Muslim alipokea masimulizi kama hayo kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) na amesema: “Sajdah badala ya Rakaa.” Kisha amesema: “Sajdah inaashiria Rakaa.”

 

 

 

134.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: سَمِعْتَ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم  يَقُولُ: {لَا صَلَاةَ بَعْدَ اَلصُّبْحِ حَتَّى تَطْلُعَ اَلشَّمْسُ وَلَا صَلَاةَ بَعْدَ اَلْعَصْرِ حَتَّى تَغِيبَ اَلشَّمْسُ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَلَفْظُ مُسْلِمٍ: {لَا صَلَاةَ بَعْدَ صَلَاةِ اَلْفَجْرِ}  

وَلَهُ عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ: {ثَلَاثُ سَاعَاتٍ كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم  يَنْهَانَا أَنْ نُصَلِّي فِيهِنَّ‏، وَأَنْ  نَقْبُرَ فِيهِنَّ مَوْتَانَا: حِينَ تَطْلُعُ اَلشَّمْسُ بَازِغَةً حَتَّى تَرْتَفِعَ‏، وَحِينَ يَقُومُ قَائِمُ اَلظَّهِيرَةِ حَتَّى تَزُولَ   اَلشَّمْسُ‏، وَحِينَ تَتَضَيَّفُ  اَلشَّمْسُ لِلْغُرُوبِ}  

وَالْحُكْمُ اَلثَّانِي عِنْدَ "اَلشَّافِعِيِّ" مِنْ:

حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ. وَزَادَ: {إِلَّا يَوْمَ اَلْجُمْعَةِ} 

وَكَذَا لِأَبِي دَاوُدَ: عَنْ أَبِي قَتَادَةَ نَحْوُهُ 

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Hakuna Swalaah baada ya Swalaah ya Alfajiri hadi jua kuchomoza[15], wala hakuna Swalaah baada ya Swalaah ya Alasiri hadi jua lizame.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na tamshi la Muslim amesema: “Hakuna Swalaah baada ya Swalaah ya Alfajiri.”

 

Na Muslim amenukuu Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir[16] kuwa: “Nyakati tatu ambazo Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitukataza kuswali wala kuzika[17] wafu wetu: (a) Wakati wa kuchomoza jua mpaka lipae. (b) Wakati jua liko juu kati kati hadi lipinduke. (c) Wakati jua linakaribia kuzama (kuingia Magharibi).”

 

Hukmu ya pili kwa Ash-Shaafi’y[18] inatokana na Hadiyth ya Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwa Isnaad dhaifu, akaongezea: “Isipokuwa siku ya Ijumaa.” Kadhalika Abuu Daawuwd alisimulia hivyo kutoka kwa Abuu Qataadah.

 

 

 

135.

وَعَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم   {يَا بَنِي عَبْدِ مَنَافٍ‏، لَا تَمْنَعُوا أَحَدًا طَافَ بِهَذَا اَلْبَيْتِ وَصَلَّى أَيَّةَ سَاعَةٍ شَاءَ مِنْ لَيْلٍ أَوْ نَهَارٍ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ‏، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ‏، وَابْنُ حِبَّانَ 

Kutoka kwa Jubayr bin Mutw’im[19] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Enyi Baniy ‘Abdil-Manaaf, msimzuie yeyote kutufu Nyumba (Al-Ka’bah) hii na akaswali saa yoyote anayotaka, usiku au mchana.” [Imetolewa na Al-Khamsah, na wakaisahihisha At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan]

 

 

 

136.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا‏، عَنْ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {اَلشَّفَقُ اَلْحُمْرَةُ}  رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ وَصَحَّحَ اِبْنُ خُزَيْمَةَ وَغَيْرُهُ وَقْفَهُ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mawingu (ya machweo ya jua) ni wekundu.” [Imetolewa na Ad-Daaruqutwniy, na akaisahihisha Ibn Khuzaymah, na wengine waliipa daraja la Mawquwf]

 

 

 

137.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم  {اَلْفَجْرُ فَجْرَانِ: فَجْرٌ يُحَرِّمُ اَلطَّعَامَ وَتَحِلُّ فِيهِ اَلصَّلَاةُ‏، وَفَجْرٌ تَحْرُمُ فِيهِ اَلصَّلَاةُ ‏ أَيْ: صَلَاةُ اَلصُّبْحِ ‏ وَيَحِلَّ فِيهِ اَلطَّعَامُ}  رَوَاهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ‏، وَالْحَاكِمُ‏، وَصَحَّحَاهُ 

وَلِلْحَاكِمِ فِي حَدِيثِ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  نَحْوُهُ‏، وَزَادَ فِي اَلَّذِي يُحَرِّمُ اَلطَّعَامَ: {إِنَّهُ يَذْهَبُ مُسْتَطِيلاً فِي اَلْأُفُقِ}  وَفِي اَلْآخَرِ: {إِنَّهُ كَذَنَبِ اَلسِّرْحَان}

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Alfajiri ni Alfajiri mbili: Alfajiri moja inaharamisha chakula na inahalalisha Swalaah, na Alfajiri nyingine inaharamisha kuswali ndani yake: yaani Swalaah ya Alfajiri wakati huo chakula kinakuwa halali.” [Imetolewa na Ibn Khuzaymah na Al-Haakim aliyeisahihisha]

 

Na Al-Haakim alipokea Hadiyth ya Jaabir mfano wake, na ikaongeza katika ambayo inaharamisha kula: “Kumesambaa sana katika pambizo upeo.”

 

Na katika nyingine amesema: “Ni kama mkia wa mbwa.”

 

 

 

138.

وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم   {أَفْضَلُ اَلْأَعْمَالِ اَلصَّلَاةُ فِي أَوَّلِ وَقْتِهَا}  رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ‏، وَالْحَاكِمُ. وَصَحَّحَاهُ   .

وَأَصْلُهُ فِي "اَلصَّحِيحَيْنِ" 

Kutoka kwa Ibn Mas’uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Amali bora kabisa ni Swalaah mwanzo wa wakati wake[20].” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na Al-Haakim aliyeisahihisha] na chanzo chake ni katika Swahiyh mbili.

 

 

 

139.

وَعَنْ أَبِي مَحْذُورَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {أَوَّلُ اَلْوَقْتِ رِضْوَانُ اَللَّهُ‏، وَأَوْسَطُهُ رَحْمَةُ اَللَّهِ‏ ، وَآخِرُهُ عَفْوُ اَللَّهِ}  أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ جِدًّا 

وَلِلتِّرْمِذِيِّ مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ عُمَرَ نَحْوُهُ‏، دُونَ اَلْأَوْسَطِ‏، وَهُوَ ضَعِيفٌ أَيْضًا 

Kutoka kwa Abuu Mahdhuwrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Wakati wa mwanzo ni radhi ya Allaah, wa katikati yake ni wa Rahmah za Allaah, na wa mwisho wake ni msamaha wa Allaah.” [Imetolewa na Ad-Daaruqutwniy kwa Isnaad dhaifu sana]

 

Na At-Tirmidhiy alisimulia hivyo hivyo, na kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Umar, bila kutaja wakati wa kati na kati. [Hii Hadiyth pia ni dhaifu]

 

 

 

140.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {لَا صَلَاةَ بَعْدَ اَلْفَجْرِ إِلَّا سَجْدَتَيْنِ}  أَخْرَجَهُ اَلْخَمْسَةُ‏، إِلَّا النَّسَائِيُّ 

وَفِي رِوَايَةِ عَبْدِ اَلرَّزَّاقِ: {لَا صَلَاةَ بَعْدَ طُلُوعِ اَلْفَجْرِ إِلَّا رَكْعَتَيْ اَلْفَجْرِ}

وَمِثْلُهُ لِلدَّارَقُطْنِيّ عَنْ اِبْنِ عَمْرِوِ بْنِ اَلْعَاصِ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna Swalaah baada ya Alfajiri isipokuwa sajdah mbili (Rakaa mbili za Alfajr)[21].” [Imetolewa na Al-Khamsah isipokuwa An-Nasaaiy]

 

 

Katika Riwaayah nyingine ‘Abdur-Razzaaq pia alisimulia: “Hakuna Swalaah baada ya kupambazuka Alfajiri isipokuwa Rakaa mbili za Sunnah ya Alfajir[22]i.”

 

Mfano wa Hadiyth hiyo imepokewa na Ad-Daaruqutwniy kutoka kwa ‘Amr bin Al-‘Aasw.

 

 

 

141.

وَعَنْ أَمْ سَلَمَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {صَلَّى رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم اَلْعَصْرَ‏، ثُمَّ دَخَلَ بَيْتِي‏، فَصَلَّى رَكْعَتَيْنِ‏، فَسَأَلْتُهُ‏، فَقَالَ: "شُغِلْتُ عَنْ رَكْعَتَيْنِ بَعْدَ اَلظُّهْرِ‏، فَصَلَّيْتُهُمَا اَلْآنَ"‏، قُلْتُ: أَفَنَقْضِيهِمَا إِذَا فَاتَتْنَا‏ ؟ قَالَ: "لَا"} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ 

وَلِأَبِي دَاوُدَ عَنْ عَائِشَةَ بِمَعْنَاهُ

Kutoka kwa Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali Alasiri, kisha akaja nyumbani kwangu, akaswali Rakaa mbili, halafu nikamuuliza juu ya hizo, naye akasema: “Nilishughulishwa na Rakaa mbili za Sunnah baada ya Swalaah ya Adhuhuri, kwa hivyo nimeziswali sasa.” Nikasema: Tuzilipe tukizikosa? Akasema: “Hapana[23].” [metolewa na Ahmad]

Naye Abuu Daawuwd amepokea Hadiyth ya ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) yenye maana sawa na hiyo.

 

 

 

[1] Inamaanisha kuwa wakati wa Swalaah ya Adhuhuri ni hadi kivuli kiwe na ukubwa sawa (kutoka wakati jua linapanda mpaka wakati ukubwa wa mtu na wa kivuli chake viwe sawa), na baada ya pale, wakati wa Swalaah ya ‘Aswr huanza. Baadhi ya ‘Ulamaa wanahesabu wakati wa Swalaah ya Adhuhuri ni mpaka kivuli kiwe na ukubwa mara mbili, lakini hii haijathibitishwa na Hadiyth yoyote sahihi.

 

 

[2] Hadiyth hii inasema kuwa, Swalaah ya Maghrib pia ina nyakati mbili, mwanzo na mwisho. Katika Hadiyth ya Jibriyl wakati mmoja tu umetajwa kwa ajili ya Swalaah ya Maghribi mara zote mbili, lakini hii ilikuwa ni wakati wa mwanzo wa Uislaam. Baadaye kule Al-Madiynah, wakati wa Swalaah ya Maghribi ulirefushwa.

 

[3] اَلشَّفَقُ‏ Wakati wa mwanga wa jua unapofifia yaani ni ule wekundu katika upeo wa Maghribi wakati wa jioni jua linapotua, kama maelezo yanavyosimuliwa na Ad-Daaraqutniy.

 

[4] Huyu Buraydah ndiye Abuu ‘Abdillaah Buraydah bin Al-Husayb Al-Aslami. Alisilimu yeye pamoja na wenziwe themanini pale Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipompita yeye wakati akihama kwenda Al-Madiynah. Baadaye alikuja kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) baada ya Vita vya Uhud, na akashiriki katika Vita zingine. Na pia alihudhuria Al-Hudaybiyyah na pia Bay’atu Ar-Ridhwaan. Alilowea Basra, kisha akaenda na msafara hadi Khurasaan na akalowea Marwa alikofia na akazikwa mnamo mwaka 62 au 63 A.H.

 

 

[5] Inamaanisha kuwa Swalaah ya ‘Aswr ni sharti iswaliwe mapema. Baada ya kivuli chenye ukubwa sawa, wakati unatosheleza kuswali rakaah nne tu ambayo ndiyo kawaida kati ya Swalaah ya Dhuhuri na ya ‘Aswr. Baada ya hapo, wakati wa Swalaah ya ‘Aswr huanza.

 

[6] Abuu Muwsaa ndiye ‘Abdullaah bin Qays Al-Ash’ariyy aliyekuwa mmoja wa Swahaba maarufu kabisa. Alihamia Habasha (Abyssinia) na baadaye akaja kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kule Khaybar. Aliteuliwa kutawala Zabid na ‘Aden, na kisha akawa Gavana wa ‘Umar kule Kuwfah na Basra. Alisaidia kuikomboa Tastar na miji mingine kadhaa. Huenda alifariki mnamo mwaka 42 A.H

 

[7] Simulizi zote zilizotajwa zimethibitisha kuwa kila Swalaah ina “Wakati wa mwanzo” na “Wakati wa mwisho” kuiswali Swalaah ile; lakini kila Swalaah sharti iswaliwe katika wakati wake wa mwanzo.

 

[8] Abuu Barzah Al-Aslamiyy ndiye Nadla bin ‘Ubayd. Alisilimu mapema sana na akashuhudia kutekwa kwa Makkah na Vita zingine muhimu. Alilowea Basra, na baadaye Khurasaan, na akafia Marwa au Basra mnamo mwaka 60 au 64 A.H.

 

[9] Baada ya Swalaah ya ‘Ishaa imekatazwa kuongea. Sababu ya katazo hili ni kwamba dhambi za Muumini zimesamehewa baada ya kuswali, na bora kuenda kitandani kuliko kuongea na kushiriki katika mambo ya kidunia. Baada ya kuswali ‘Ishaa, mtu kuenda zake kulala kunampa faida maradufu; kwanza ni kujiepusha na dhambi, na pili ubora Swalaah ndiyo ihesabiwe kuwa ni tendo lake la mwisho kabla hajalala.

 

 

[10] Kuhusu wakati wa Swalaah ya Fajr, yapo maoni tofauti ya Swahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Katika Hadiyth hii, hilo neno la Kiarabu la   غَلَسٍ inamaanisha wakati ambao kupambazuka kunaonekana katika giza la usiku.

 

[11] Raafi’ bin Khadiyj ndiye Answari aliyeitwa Abuu ‘Abdillaah. Alikosa Vita ya Badr kwa sababu ya umri wake kuwa mdogo, lakini akashiriki katika Vita ya Uhud na Vita vilivyofuata. Alifariki mnamo mwaka wa 73 au 74 A.H akiwa na umri wa miaka 86.

 

[12] Ni ubora kuiswali Swalaah ya ‘Ishaa wakati wa mwisho kadiri iwezekanavyo. Amri hii ni maalumu kwa Swalaah ya ‘Ishaa tu, na siyo kwa Swalaah nyingine yoyote. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akingoja na kuichelewesha Swalaah hii.

 

 

[13] Kuna maoni tofauti kuhusu kuswali Dhuhuri mapema au mwishoni wakati wa majira ya joto. Lakini ni sawa kuichelewesha kidogo hadi mtu aweze kutembea katika vivuli vya kuta. Kwa mujibu wa Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiichelewesha Swalaah ya Dhuhuri hadi kivuli kilipokuwa na urefu wa hatua tatu au tano.”

 

[14] Hii inamaanisha kuwa mwanga wa Alfajiri sharti uonekane waziwazi na kusiweko shaka yoyote juu yake. Kwa hivyo Hadiyth hii haipingani na hiyo Hadiyth ya “Giza” hapo nyuma. Kipengele kingine ni kuwa Swalaah sharti ianze kuswaliwa wakati ikiwa giza, na visomo virefushwe mpaka mwanga wa Alfajiri uonekane waziwazi.

 

[15] . Maana yake hii ni kuwa, tangu kunapopambazuka mpaka kuchomoza jua, na tangu ‘Aswr hadi jua linapokuchwa, Swalaah za khiari (Nawaafil) zozote haziruhusiwi. Rakaah mbili kabla ya Swalaah ya faradhi ya Fajr hazimo katika amri hii, kama ilivyothibitishwa kutoka kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Ingawa Rakaah hizi mbili huswaliwa kabla ya Swalaah ya faradhi (Fajr), ukizikosa hizi unaweza kuziswali baada ya Swalaah ya fardhi kama ilivyoripotiwa katika At-Tirmidhiy.

 

 

[16] ‘Uqbah bin ‘Aamir alikuwa ni Junani aliyepewa jina la utani Abuu Hammad au Abu ‘Aamir. Alisilimu, akahama na kuandamana na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mwanzoni kabisa. Aliisoma sana Qur-aan na alikuwa mtaalamu wa Kanuni za Shariy’ah na mirathi, na alikuwa msomi na mshairi. Alipewa ardhi Basra, na alishiriki katika Siffin pamoja na Mu’aawiyah. Baadaye aliitawala Misri kwa niaba ya Mu’aawiyah kwa miaka mitatu, na akawa mkuu wa misafara ya baharini. Alifariki mwaka 58 A.H. kule Misri, na akazikwa Al-Muqtam.

 

[17] Hapa, “Kuzika” maana yake ni “Swalaah za maiti”. Swalaah za maiti zisiswaliwe katika nyakati hizo, lakini kumzika maiti inaruhusiwa. Lakini kwa mujibu wa Wanazuoni wengine, hata kuzika hakuruhusiwi. Kwa hivyo, katika hali hizo, inamaanisha kuwa hata maziko yasifanyike katika nyakati hizo. Lakini iwapo nyakati hizi zimewadia katikati ya shughuli za maziko, au hakuna njia nyingine, basi kuzika kunaruhusiwa.

 

[18] Amri ya pili maana yake wakati wa katikati ya siku, ambapo hakuna Swalaah inayoruhusiwa kuswaliwa wakati huu. Lakini Ijumaa haimo katika amri hii. Siku za Ijumaa inaruhusiwa kuswali wakati jua liko juu kabisa, kama inavyodhihirisha Hadiyth iliyoripotiwa na Abuu Hurayrah.

 

[19] Jubayr bin Mutw’im ndiye Abuu Muhammad au Abuu ‘Umayyah Jubayr bin Mutw’im bin ‘Aad bin Nawfal Al-Quraysh. Alikuwa mstahamilivu sana, mjuzi wa ukoo wa Maquraysh. Alisilimu kabla ya Fat-h (kutekwa kwa Makkah) na alilowea Al-Madiynah, na akafia huko mnamo mwaka 54 au 57 au 59 A.H.

 

[20] Katika Hadiyth hii, Swalaah inayoswaliwa katika nyakati zake za mwanzo huhesabika kuwa ni tendo bora sana. Katika Hadiyth zingine, Iymaan, Swadaqah na Jihaad huhesabika kuwa matendo bora sana. Hizi Hadiyth zinaonyesha Iymaan ni tendo la sifa, Swalaah ni tendo la mwili, Swadaqah ni tendo la mali, na Jihaad ni tendo la ujana na afya. Kwa hivyo haya yote ni matendo makubwa na bora kwa namna zake na mahala pake; na hakuna mapingano.

 

[21] Maana yake ni kwamba, baada ya kupambazuka, Swalaah za khiari (Nawaafil) haziruhusiwi, lakini Rakaa mbili za Sunnah zinakubaliwa, na zinaweza kuswaliwa baada ya Swalaah ya Fajr, kama rejeo la At-Tirmidhiy lilivyotaja hapo nyuma

 

[22] Hizo Rakaa mbili ni zile za Sunnah kabla ya Swalaah ya faradhi ya Fajr, ambayo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kamwe hakuwa anaikosa hata iwe baada ya kupambazuka, kama ilivyoonyeshwa na Hadiyth hii na Hadiyth zingine.

 

[23] Hadiyth hii inatuarifu kwamba, baada ya Swalaah ya ‘Aswr, kuswali Swalaah za ziada au za khiari tulizozikosa ni kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) tu, watu wengine hawaruhusiwi kulipa Swalaah za khiari. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliiswali Swalaah ile kwa sababu watu fulani wa kabila la Abdul-Qays walimzuru na walileta vitu vya Swadaqah, kwa hivyo ziara yao ile na ugawanyaji wa vitu walivyoleta ulimchelewesha.

 

 

Share

02-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Adhaan

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ اَلْأَذَانِ

02-Mlango Wa Adhaan[1]

 

 

 

 

 

142.

عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ زَيْدِ بْنِ عَبْدِ رَبِّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {طَافَ بِي وَأَنَا نَائِمٌ رَجُلٌ فَقَالَ: تَقُولُ: "اَللَّهُ أَكْبَرَ اَللَّهِ أَكْبَرُ،  فَذَكَرَ اَلْآذَانَ  بِتَرْبِيع اَلتَّكْبِيرِ بِغَيْرِ تَرْجِيعٍ،  وَالْإِقَامَةَ فُرَادَى،  إِلَّا قَدْ قَامَتِ اَلصَّلَاةُ  قَالَ: فَلَمَّا أَصْبَحْتُ أَتَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   فَقَالَ: "إِنَّهَا لَرُؤْيَا حَقٍّ..."}  اَلْحَدِيثَ. أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ،  وَأَبُو دَاوُدَ،  وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ،  وَابْنُ خُزَيْمَةَ 

وَزَادَ أَحْمَدُ فِي آخِرِهِ قِصَّةَ قَوْلِ بِلَالٍ فِي آذَانِ اَلْفَجْرِ: {اَلصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ اَلنَّوْمِ}  

وَلِابْنِ خُزَيْمَةَ: عَنْ أَنَسٍ قَالَ: {مِنْ اَلسُّنَّةِ إِذَا قَالَ اَلْمُؤَذِّنُ فِي اَلْفَجْرِ: حَيٌّ عَلَى اَلْفَلَاحِ،  قَالَ: اَلصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ اَلنَّوْمِ}

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Zayd bin ‘Abdi-Rabbih[2] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Mtu mmoja alinitembelea wakati nimelala[3], akaniambia: Sema:

اَللَّهُ أَكْبَرَ اَللَّهِ أَكْبَرُ

“Allaahu Akbar, Allaahu Akbar” (Allaah ni Mkubwa zaidi, Allaah ni Mkubwa zaidi). Akataja Adhaan kwa tamko la

اَللَّهُ أَكْبَر

Allaahu Akbar”

mara nne bila Tarjiy’[4] na Iqaamah mara moja, isipokuwa

قَدْ قَامَتِ اَلصَّلَاةُ 

Qad Qaamati Swalaah”[5]

(Swalaah imekwishakimiwa), ‘Abdullaah akasema: Asubuhi yake nilikwenda kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) naye akasema: “Hiyo ni ndoto ya kweli.” [Hadiyth hii imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd, na wakaisahihisha At-Tirmidhiy na Ibn Khuzaymah]

 

Ahmad aliongeza mwishoni wa Hadiyth hiyo, Hadiyth ya msemo wa Bilaal[6] katika Adhaan ya Alfajiri:

 

اَلصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ اَلنَّوْمِ

“Asw-Swalaatu khayrun minan-nawm (Swalaah ni bora kuliko usingizi).”

 

 

Ibn Khuzaymah alisimulia kuwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Ni Sunna Muadhini anaposema:

حَيٌّ عَلَى اَلْفَلَاحِ

Hayya ‘alal falaah” (Njooni kwenye kufaulu), aongeze:

 

اَلصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ اَلنَّوْمِ

Asw-Swalaatu khayrun minan-nawm”

 (Swalaah ni bora kuliko usingizi).”

 

 

 

143.

 عَنْ أَبِي مَحْذُورَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم {عَلَّمَهُ اَلْآذَانَ،  فَذَكَرَ فِيهِ اَلتَّرْجِيعَ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ. وَلَكِنْ ذَكَرَ اَلتَّكْبِيرَ فِي أَوَّلِهِ مَرَّتَيْنِ فَقَطْ 

وَرَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ فَذَكَرُوهُ مُرَبَّعًا 

Kutoka kwa Abuu Mahdhuwrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimfundisha Adhaan, na yeye (msimuliaji) akataja Tarjiy’ ndani yake.” [Imetolewa na Muslim, lakini alitaja Takbiyra, mwanzo wake mara mbili tu[7]]

[Imetolewa na Al-Khamsah, lakini wamesema Takbiyra hutajwa mara nne]

 

 

 

144.

وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {أُمِرَ بِلَالٌ أَنْ يَشْفَعَ اَلْآذَانَ،  وَيُوتِرَ اَلْإِقَامَةَ،  إِلَّا اَلْإِقَامَةَ،  يَعْنِي قَوْلَهُ: قَدْ قَامَتِ اَلصَّلَاةُ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ،  وَلَمْ يَذْكُرْ مُسْلِمٌ اَلِاسْتِثْنَاءَ  

وَلِلنَّسَائِيِّ: {أَمَرَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم   بِلَالاً}

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Bilaal aliamrishwa aitamke Adhaan kwa shufwa (mara mbili)[8], na Iqaamah kwa witri[9] isipokuwa “Qad Qaamati Swalaah” (yaani Swalaah imekwishakimiwa).” [Al-Bukhaariy, Muslim; lakini Muslim hakutaja huko kuvua]

 

 

Na An-Nasaaiy alipokea: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuamrisha Bilaal.”

 

 

 

145.

وَعَنْ أَبِي جُحَيْفَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {رَأَيْتُ بِلَالاً يُؤَذِّنُ وَأَتَتَبَّعُ فَاهُ،  هَاهُنَا وَهَاهُنَا،  وَإِصْبَعَاهُ فِي أُذُنَيْهِ}  رَوَاهُ أَحْمَدُ،  وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ 

وَلِابْنِ مَاجَهْ: وَجَعَلَ إِصْبَعَيْهِ فِي أُذُنَيْهِ 

وَلِأَبِي دَاوُدَ: {لَوَى عُنُقَهُ،  لَمَّا بَلَغَ "حَيَّ عَلَى اَلصَّلَاةِ " يَمِينًا وَشِمَالاً وَلَمْ يَسْتَدِرْ}

وَأَصْلِهِ فِي اَلصَّحِيحَيْنِ 

Kutoka kwa Abuu Juhayfah[10] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimemuona Bilaal akiadhini, nami nilikuwa nikifuatisha kwa kumtazama mdomo wake akiugeuza upande huu (kuume), na upande ule (kushoto)[11], kaweka vidole vyake masikioni.” [Imetolewa na Ahmad na At-Tirmidhiy aliyeipa daraja la Swahiyh]

 

Na katika mapokezi ya Ibn Maajah: “Na aliweka vidole vyake viwili kwenye masikio yake.”

 

Na mapokezi ya Abuu Daawuwd: “Aligeuza shingo yake kuumeni na kushotoni alipofika:  “Hayya ‘alasw-Swalaah” (njoo katika Swalaah), na hakugeuza mwili wake.” Na chanzo chake ni katika Swahiyh mbili.

 

 

 

146.

وَعَنْ أَبِي مَحْذُورَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   أَعْجَبَهُ صَوْتُهُ،  فَعَلَّمَهُ اَلْآذَانَ}  رَوَاهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ 

Kutoka kwa Abuu Mahdhuwrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipenda sauti yake[12] kwa hivyo akamfundisha Adhaan.” [Imetolewa na Ibn Khuzaymah]

 

 

 

147.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {صَلَّيْتُ مَعَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم   اَلْعِيدَيْنِ،  غَيْرَ مَرَّةٍ وَلَا مَرَّتَيْنِ،  بِغَيْرِ أَذَانٍ وَلَا إِقَامَةٍ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

وَنَحْوُهُ فِي اَلْمُتَّفَقِ: عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا،  وَغَيْرُهُ 

Kutoka kwa Jaabir bin Samurah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nimeswali na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ‘Iyd mbili, siyo mara moja au mara mbili tu[13], bila Adhaan wala Iqaamah.” [Imetolewa na Muslim]

 

Hadiyth kama hiyo imo katika Al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) na wengineo.

 

 

 

148.

وَعَنْ أَبِي قَتَادَةٌ فِي اَلْحَدِيثِ اَلطَّوِيلِ،  {فِي نَوْمهُمْ عَنْ اَلصَّلَاةِ  ثُمَّ أَذَّنَ بِلَالٌ،  فَصَلَّى رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   كَمَا كَانَ يَصْنَعُ كُلَّ يَوْمٍ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

وَلَهُ عَنْ جَابِرٍ: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   أَتَى اَلْمُزْدَلِفَةَ فَصَلَّى بِهَا اَلْمَغْرِبَ وَالْعِشَاءَ،  بِأَذَانٍ وَاحِدٍ وَإِقَامَتَيْنِ}

 وَلَهُ عَنْ اِبْنِ عُمَرَ: {جَمَعَ بَيْنَ اَلْمَغْرِبِ وَالْعِشَاءِ بِإِقَامَةٍ وَاحِدَةٍ}

زَادَ أَبُو دَاوُدَ: {لِكُلِّ صَلَاةٍ} 

وَفِي رِوَايَةِ لَهُ: {وَلَمْ يُنَادِ فِي وَاحِدَةٍ مِنْهُمَا}

Kutoka kwa Abuu Qataadah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) katika Hadiyth ndefu kuhusu: Maswahaba kulala kwao wakapitwa na Swalaah, kisha Bilaal akaadhini na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaswalisha kama alivyokuwa akifanya kila siku[14].” [Imetolewa na Muslim]

 

 Na Jaabir alihadithia: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipofika Muzdalifah[15] aliswali hapo Maghrib na ‘Ishaa kwa Adhaan moja na Iqaamah mbili.”

 

Alihadithia Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikusanya Swalaah ya Maghrib na ya ‘Ishaa kwa Iqaamah moja.”

 

Na Abuu Daawuwd akaongezea: “Kwa kila Swalaah[16].”

 

Na katika Riwaayah nyingine: “Adhaan haikuadhiniwa katika Swalaah yoyote kati ya hizo mbili.”

 

 

 

149.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ،  وَعَائِشَةَ قَالَا: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {إِنَّ بِلَالاً يُؤَذِّنُ بِلَيْلٍ،  فَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّى يُنَادِيَ اِبْنُ أُمِّ مَكْتُومٍ"،  وَكَانَ رَجُلاً أَعْمَى لَا يُنَادِي،  حَتَّى يُقَالَ لَهُ: أَصْبَحْتَ،  أَصْبَحْتَ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَفِي آخِرِهِ إِدْرَاجٌ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar na ‘Aaishah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) wamesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Bilaal huadhini usiku[17], kwa hivyo kuleni na kunyweni mpaka Ibn Ummi Maktuwm[18] aadhini.” Na Ibn Ummi Maktuwm alikuwa kipofu na kwa hivyo hakuadhini mpaka aambiwe: “Kumekucha, kumekucha.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika sehemu yake ya mwishoni mwake kuna Idraaj[19]

 

 

 

150.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ; {إِنَّ بِلَالاً أَذَّنَ قَبْلَ اَلْفَجْرِ،  فَأَمَرَهُ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم   أَنْ يَرْجِعَ،  فَيُنَادِيَ: "أَلَا إِنَّ اَلْعَبْدَ نَامَ}  رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَضَعَّفَهُ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Bilaal aliadhini kabla ya kupambazuka, na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamwambia arejee[20] na aadhini: Mja wa Allaah (Yaani Bilaal), amelala (na hiyo ndiyo sababu ya kosa lile).” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na ikapewa daraja la dhaifu]

 

 

 

151.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {إِذَا سَمِعْتُمْ اَلنِّدَاءَ،  فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ اَلْمُؤَذِّنُ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَلِلْبُخَارِيِّ: عَنْ مُعَاوِيَةَ 

 وَلِمُسْلِمٍ: {عَنْ عُمَرَ فِي فَضْلِ اَلْقَوْلِ كَمَا يَقُولُ اَلْمُؤَذِّنُ كَلِمَةً كَلِمَةً،  سِوَى اَلْحَيْعَلَتَيْنِ،  فَيَقُولُ: "لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاَللَّهِ"}

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mkisikia Adhaan semeni[21] kama anavyosema Muadhini.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na Al-Bukhaariy amepokea hivyo hivyo kutokana na uslimulizi wa Mu’aawiyah.

 

Na Muslim alipokea usimulizi wa ‘Umar kuhusu fadhila ya kusema kama anavyotamka Muadhini isipokuwa pale Muadhini anaposema: “Hayya ‘alasw-Swalaah” (Njoo katika Swalaah) na “Hayya ‘alal-falaah” (Njoo kwenye kufaulu) ambapo mtu hutakiwa aseme:  “Laa hawla wa laa quwwata illaa biLLaah” (Hakuna uwezo wala nguvu ila kwa msaada wa Allaah).”

 

 

 

152.

وَعَنْ عُثْمَانَ بْنِ أَبِي الْعَاصِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّهُ قَالَ : يَا رَسُولَ اَللَّهِ اِجْعَلْنِي إِمَامَ قَوْمِي . قَالَ : "أَنْتَ إِمَامُهُمْ،  وَاقْتَدِ بِأَضْعَفِهِمْ،  وَاِتَّخِذْ مُؤَذِّنًا لَا يَأْخُذُ عَلَى أَذَانِهِ أَجْرًا}  أَخْرَجَهُ اَلْخَمْسَةُ،  وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ،  وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa ‘Uthmaan bin Abiy Al-‘Aasw[22] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Ee Rasuli wa Allaah! Niteue niwe Imaam wa watu wangu. Akasema: “Wewe ni Imaam wao, zingatia wadhaifu wao zaidi[23], na uteue Muadhini asiyechukua ujira[24] kutokana na kuadhini.” [Imetolewa na Al-Khamsah, na aliipa daraja la Hasan At-Tirmidhiy, na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

153.

وَعَنْ مَالِكِ بْنِ الْحُوَيْرِثِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ لَنَا اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  {وَإِذَا حَضَرَتِ اَلصَّلَاةُ فَلْيُؤَذِّنْ لَكُمْ أَحَدُكُمْ . ..}  اَلْحَدِيثَ أَخْرَجَهُ اَلسَّبْعَةُ

Kutoka kwa Maalik bin Al-Huwayrith[25] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ametuambia: “Ukifika wakati wa Swalaah, mmoja wenu aadhini[26]….” [Imetolewa na Maimaam Saba]

 

 

 

154.

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ لِبِلَالٍ : {إِذَا أَذَّنْتَ فَتَرَسَّلْ ،  وَإِذَا أَقَمْتُ فَاحْدُرْ ،  وَاجْعَلْ بَيْنَ أَذَانِكَ وَإِقَامَتِكَ قَدْرَ مَا يَفْرُغُ اَلْآكِلُ مِنْ أَكْلِهِ}  اَلْحَدِيثَ . رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَضَعَّفَهُ .

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimwambia Bilaal: “Unapoadhini, tamka taratibu, na unapokimu kimu haraka, na acha muda baina ya Adhaan na Iqaamah kiasi cha mlaji amalize kula[27] kwake.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy, na akaidhoofisha]

 

 

 

155.

وَلَهُ : عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   قَالَ : {لَا يُؤَذِّنُ إِلَّا مُتَوَضِّئٌ}  وَضَعَّفَهُ أَيْضًا 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Asiadhini isipokuwa mwenye wudhuu[28].” [Pia ameidhoofisha]

 

 

 

156.

وَلَهُ : عَنْ زِيَادِ بْنِ اَلْحَارِثِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {وَمَنْ أَذَّنَ فَهُوَ يُقِيمُ}  وَضَعَّفَهُ أَيْضًا

Tena At-Tirmidhiy amepokea kuwa Ziyaad bin Al-Haarith[29] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuadhini ndiye mwenye kukimu[30].” [Pia ameidhoofisha]

 

 

 

157.

وَلِأَبِي دَاوُدَ: فِي حَدِيثِ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ زَيْدٍ أَنَّهُ قَالَ : أَنَا رَأَيْتُهُ  يَعْنِي : اَلْأَذَانُ  وَأَنَا كُنْتُ أُرِيدُهُ . قَالَ : "فَأَقِمْ أَنْتَ " وَفِيهِ ضَعْفٌ أَيْضًا 

 Abuu Daawuwd amepokea kutokana na Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Zayd kuwa amesema: “Niliiona (yaani Adhaan) ndotoni, nami nilikuwa naitaka (kuitumia), Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Kimu wewe (Swalaah).” [Hadiyth hii pia ni dhaifu]

 

 

 

158.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   {اَلْمُؤَذِّنُ أَمْلَكُ بِالْأَذَانِ ،  وَالْإِمَامُ أَمْلَكُ بِالْإِقَامَةِ}  رَوَاهُ اِبْنُ عَدِيٍّ وَضَعَّفَهُ

وَلِلْبَيْهَقِيِّ نَحْوُهُ : عَنْ عَلِيٍّ مِنْ قَوْلِهِ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muadhini ana haki zaidi ya kuadhini na Imaam ana haki zaidi ya kukimu.” [Imetolewa na Ibn ‘Adiy na akaidhoofisha]

 

Na Al-Bayhaqiy mfano wake: kutoka kwa ‘Aliy kutoka katika kauli yake.

 

 

 

159.

وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {لَا يُرَدُّ اَلدُّعَاءُ بَيْنَ اَلْأَذَانِ وَالْإِقَامَةِ}  رَوَاهُ النَّسَائِيُّ ،  وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Dua baina ya Adhaan na Iqaamah haikataliwi.” [Imetolewa na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

160.

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ : {مَنْ قَالَ حِينَ يَسْمَعُ اَلنِّدَاءَ : اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ،  وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ،  آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ،  وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ، حَلَّتْ لَهُ شَفَاعَتِي يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ}  أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kusema anaposikia Adhaan:

 اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ،  وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ،  آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ،  وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ

Allaahumma Rabba haadhihid-dda’watit- ttaamah, wasw-Swaalaatil qaaimah, aati Muhammada  al-wasiylata wal fadhwiylah, wab-‘ath-hu maqaaman mahmuwdan alladhiy wa’adtah[31].

 

(Ee Allaah, Rabb wa mwito huu uliotimia, na Swalaah iliyosimama, mpe (Nabiy) Muhammad al-Wasiylah (cheo, daraja), na fadhila[32], na mfikishe daraja yenye kuhimidiwa, ambayo Umemuahidi).

 

Ash-Shafaa’ah (Uombezi) wangu umehalalika kwake Siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na Al-Arba’ah]

 

 

 

 

[1] Maneno yanayounda “Adhaan” yamepangiliwa Kiilaahi. Hayaruhusiwi kuongezwa, kupunguzwa wala kubadilishwa. Maneno hayo alipewa ‘Abdullaah bin Zayd Answaariy na ‘Umar bin Khattwaab na Malaika ndotoni, na yakathibitishwa na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), yakakwezwa kufikia hadhi ya Wahyi. Kuna dalili pia katika Qur-aan juu ya hili.

 

[2] ‘Abdullaah bin Zayd ni Answaar Mkhariji (wa Al-Madiynah). Alipewa jina la utani, Abuu Muhammad. Alishuhudia Al-‘Aqaba, Badr na Vita vingine muhimu. Alionyeshwa ndotoni namna ya kuita watu kuenda kuswali katika mwaka wa kwanza wa Hijrah, baada ya kujengwa kwa Msikiti wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alifariki mwaka 32 A.H. akiwa na umri wa miaka 64.

 

[3] Waislaam walipoongezeka, tatizo la kuwaita watu waende kuswali likajitokeza. Mapendekezo mengi yalitolewa. Wengine wakapendekeza kupuliza kombe (gamba ya wanyama wa baharini) au pembe, na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema hiyo ilikuwa njia ya Mayahudi. Wengine wakapendekeza kuwasha moto, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema hiyo ilikuwa njia ya Majusi. Hawakufikia uamuzi wowote. Lakini usiku ule, ‘Abdullaah bin Zayd akamuota mtu amesimama na kombe mkononi mwake. ‘Abdullaah akamuuliza iwapo anaweza kumuuzia lile. Yule mtu akamuuliza ni kwa ajili gani? ‘Abdullaah akajibu kwa kuwaitia Waislaam kuja kuswali. Akamuuliza iwapo anataka amfunze njia nzuri kuliko hiyo; na akasoma maneno ya Adhaan. Asubuhi yake ‘Abdullaah akamuambia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), naye akasema ndoto ilikuwa ni ya kweli.

 

[4] تَرْجِيعٍ (Kurudia) Ni kutamka maneno ya Shahada mbili Yaani

 أشهد أن لا إله إلا الله وأشهد أن محمدا رسول الله

mara mbili kwa sauti ya chini, halafu utamke kwa sauti kubwa.

 

[5] Katika Iqaamah (mwito wa kuanza Swalaah), maneno yote ya Takbiyr (kumtukuza Allaah) lakini hapa ina maana ya Iqaamah hutamkwa mara moja isipokuwa maneno

 

 قد قامت الصلاة

 

(yaani Swalaah iko tayari kuanza) ambayo hutamkwa mara mbili.

 

[6] Bilaal bin Rabbaah, mtumwa aliyeachwa huru wa Banu Taym. Alisilimu mapema sana, na akateswa sana katika jihaad ya njia za Allaah (عز وجل). Alipigana katika Vita ya Badr na Vita vingine vikuu. Alikuwa muadhini wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na hakuadhini kwa ajili ya mtu yeyote mwingine isipokuwa mara moja aliporejea Madiynah kutoka Damascus alikolowea. Inasemekana hakuwahi kuimaliza Adhaan hiyo kwa sababu ya kelele za Swahaba waliokuwa wakilia waliposikia sauti ya Bilaal, kwa sababu ya mazowea na kumbukumbu. Bilaal alifia Shaam mnamo mwaka 17 au 18 au 20 A.H akiwa na umri wa miaka sitini hivi, na hakuacha watoto wowote.

 

[7] Mwanzo wa Adhaan, maneno haya

 اَللَّهُ أَكْبَرُ

Allaahu Akbar (Allaah ni Mkuu Zaidi kuliko wote)

hutakiwa yarudiwe mara nne. Kuyarudia mara mbili tu siyo sahihi kama walivyosimulia Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad)

 

[8] Adhaan iliyo na Tarji’ au hata isiwe na Tarji’ inaruhusiwa, na hali kadhalika Iqaamah nayo inaruhusiwa ikiwa mara moja au mara mbili. Lakini ni vizuri kuitangaza Adhaan pamoja na Tarji’ na kuitangaza Iqaamah bila marudio.

 

[9] Inamaanisha kwamba, maneno

 

 قد قامت الصلاة

(Yaani Swalaah iko tayari kuanza) yarudiwe mara mbili, na maneno mengine yatangazwe mara moja tu.

 

[10] Huyu Abuu Juhayfah ndiye Wahaab bin ‘Abdillaah As-Suwa’i Al-‘Aamir, ambaye alikuwa miongoni mwa Swahaba vijana. Alilowea Kufa. ‘Aliy alimfanya awe mkuu wa Baytul-Maal; na alishuhudia pamoja naye vita vyote. Alifia Kuwfah mnamo mwaka 74 A.H.

 

[11] Wakati anatamka maneno haya

 حَيَّ عَلَى اَلصَّلَاةِ

(njoo katika Swalaah) na

 حَيٌّ عَلَى اَلْفَلَاحِ

(njoo kwenye kufaulu),

kugeuza uso kuume na kisha kushoto ni Sunnah. Kugeuza mwili mzima hakuruhusiwi. Hadiyth zinazokataza kugeuka, zinamaanisha kugeuza mwili wote na siyo kugeuza uso tu.

 

 

[12] Inamaanisha kuwa awe anateuliwa Muadhini mwenye sauti nzuri.

 

[13] Hii ina maana kwamba, Swalaah za ‘Iyd zote mbili (ya Fitwr na ya Adhwhaa) huswaliwa bila Adhaan wala Iqaamah

 

[14] Ikiwa Swalaah ya Qadhwaa (Swalaah inayolipwa) inataka kuswaliwa kwa jamaa, basi ni Sunnah kutoa Adhaan kwa ajili yake. Siku moja Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na Swahaba zake walisafiri usiku sana. Waliposimama na wakataka kuenda kulala, walikuwa hawana hakika ya kuwahi kuamka Alfajiri iliyofuata ili kuiswali. Kwa hivyo wakamuomba Bilaal abakie macho, lakini naye akazidiwa na usingizi akalala. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa wa kwanza kuamka baada ya jua kuchomoza akawaamsha Swahaba. Walisogelea pembeni wakaswali baada ya kuadhini.

 

[15] Muzdalifah ni mahali kati ya Makkah na ‘Arafah. Usiku wa tarehe 9 kuamkia tarehe 10 ya mwezi wa Dhul-Hijjah, baada ya kurudi kutoka ‘Arafah, Mahujaji hubakia hapo. Swalaah za Maghribi na ‘Ishaa huswaliwa hapo kwa pamoja kwa Adhaan moja tu, bali hutolewa Iqaamah moja kwa kila Swalaah. Hii yamaanisha kuwa, kila panaposwaliwa Swalaah ya jamaa, lazima ikimiwe.

 

[16] Hadiyth hii inatofautiana na Hadiyth iliyosimuliwa na Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) ambapo imetajwa Adhaan moja na Iqaamah mbili.

 

[17]  Katika mwezi wa Ramadhwaan Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliteua Waadhini wawili, wa kwanza kuadhini ili kujulisha wakati wa kula daku, na Muadhini wa pili kuadhini ili kuwaita watu waende kuswali.

 

[18] Ibn Umm Maktuwm ndiye ‘Amr au ‘Abdullaah bin Qays Al-Qurayshiy Al-‘Aamir, yule mtu kipofu anayetajwa katika Suwrah ‘Abasa. Alisilimu zamani na akafanya Hijrah (kuhama). Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimteua yeye awe Mkuu wa Madiynah mara 13 akiwaswalisha watu. Alikufa shahidi kule Al-Qadisiya wakati akishika bendera siku ile.

 

[19] Neno إِدْرَاجٌ  Idraaj (kilichoongezwa) linamaanisha kwamba, maneno hayo: "Na alipokuwa kipofu." Hayakusemwa na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mwenyewe, bali msimulizi aliongeza maneno haya kwa utashi wake mwenyewe.

 

[20] Hii inamaanisha kuwa kama kumeadhiniwa kabla ya wakati, kuadhiniwe tena ukifika wakati wake sahihi.

 

[21] Ni amri kwamba, tunaposikia Adhaan, watu warudie yale maneno ya Adhaan kwa kujibu kila mara, kama mtu anao wudhuu au asiwe nao, awe msafi bila najsi au awe na najsi ya kijinsia; lakini wakati mtu anafanya tendo la ndoa au akiwa chooni, haifai kujibu.

 

[22] ‘Uthmaan bin Abiy Al-‘Aasw ndiye aliyepewa jina la utani la Abuu ‘Abdillaah. Alikuwa mdogo kuliko watu waliokuwa katika ujumbe wa Twaaif wa Banu Thaqif. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimteua awe mkuu wa Twaaif, na aliwazuia watu wake wasiasi, na kwa hivyo wabakie katika Uislaam. ‘Umar alimteua awe Gavana wa Bahrayn na Oman. Alifariki mnamo mwaka 51 A.H.

 

[23] Imaam (anayeswalisha) ni sharti awajali watu dhaifu na wazee kwa kutorefusha sana Swalaah, kiasi cha kuwafanya wafikirie kuacha jamaa.

 

[24] Inamaanisha kwamba, Muadhini sharti asiwe analipwa kwa kazi hiyo ya kuadhini. Lakini huku siyo kukataza, bali ni pendekezo linalopendeza.

 

[25] Maalik bin Al-Huwayrith alikuwa wa Banu Layth, na alipewa jina la utani la Abuu Salmaan. Alimzuru Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na akakaa naye kwa siku ishirini. Alilowea Basra na akafia huko mnamo mwaka wa 74 A.H.

 

[26] Inamaanisha kuwa, wakati wa safari pia, kuadhini na kukimu ni Sunnah.

 

[27] Mambo mengine yanajulikana kuhusu Hadiyth hii:

a) Adhaan sharti itolewe kwa sauti kubwa, pakiweko mapumziko kidogo kati ya maneno yake.

(b) Iqaamah itolewe haraka haraka.

(c) Sharti kuweko muda wa kutosha kati ya Adhaan na Swalaah, ili mtu aweze kuja kujiunga na jamaa baada ya kumaliza kula au baada ya kuenda na kutoka msalani na kutawadha. ‘Ulamaa wengine wamekisia wakati huo uwe sawa na muda wa Rakaa nne.

 

[28] Ni Sunnah kwa Muadhini kutoa Adhaan akiwa na wudhuu, lakini isipowezekana, Adhaan itolewe bila wudhuu. Hili ni pendekezo tu siyo lazima.

 

[29] Ziyaad bin Al-Haarith alikuwa Swahaba kutoka Yaman aliyekubaliana na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na akatoa Adhaan mbele yake. Inasemekana alilowea Basra.

 

[30] Ni Sunnah kwa mtu mmoja huyo huyo atoe Adhaan na Iqaamah; lakini akiruhusu, mtu mwingine anaweza kutoa Iqaamah.

 

[31] Du’aa kamili (اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ) maana yake ni ung’avu wa Umoja wa Allaah (عز وجل)  na Nuru ya Unabiy.

 

[32] Baki ya kumaanisha ‘uombezi na ukuu (wasiylah)’, hilo pia ni jina la mahali. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema kwamba, ni mtu mmoja tu miongoni mwa viumbe wa Allaah (عز وجل)   atakayefika kule, naye alitegemea, kwa Rahmah za Allaah (عز وجل), mtu huyo atakuwa yeye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).

 

 

Share

03-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Masharti Ya Swalaah

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

Kitabu Cha Swalaah

 

بَـــابُ شُــرُوطِ اَلصَّلَاةِ

03-Mlango Wa Masharti Ya Swalaah

 

 

 

 

 

161.

عَنْ عَلِيِّ بْنِ طَلْقٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {إِذَا فَسَا أَحَدُكُمْ فِي اَلصَّلَاةِ فَلْيَنْصَرِفْ ، وَلْيَتَوَضَّأْ ، وَلْيُعِدْ اَلصَّلَاةَ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa ‘Aliy bin Twalq[1] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akitoa upepo katika Swalaah aondoke akatawadhe, na arudie kuswali[2].” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

162.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  قَالَ : {لَا يَقْبَلُ اَللَّهُ صَلَاةَ حَائِضٍ إِلَّا بِخِمَارٍ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيُّ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah haikubali Swalaah ya mwanamke aliyebaleghe mpaka avae khimaar[3] (shungi la kufunika kichwa na mwili).” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy, na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

163.

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  قَالَ لَهُ : {إِنْ كَانَ اَلثَّوْبُ وَاسِعًا فَالْتَحِفْ بِهِ}   يَعْنِي : فِي اَلصَّلَاةِ  وَلِمُسْلِمٍ : {"فَخَالِفْ بَيْنَ طَرَفَيْهِ  وَإِنْ كَانَ ضَيِّقًا فَاتَّزِرْ بِهِ "}  . مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ .

وَلَهُمَا مِنْ حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  {لَا يُصَلِّي أَحَدُكُمْ فِي اَلثَّوْبِ اَلْوَاحِدِ لَيْسَ عَلَى عَاتِقِهِ مِنْهُ شَيْء}

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Iwapo nguo ni pana, jizungushie mwili wote (yaani wakati wa kuswali)

Na katika tamshi la Muslim: “Kutanisha ncha mbili, na ikiwa inabana, izungushie kiunoni.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Nao wawili (Al-Bukhaariy na Muslim) wamenukuu Hadiyth ya Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Asiswali mmoja wenu na vazi moja tu lisilofunika mabega.”

 

 

 

164.

وَعَنْ أُمِّ سَلَمَةَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا ; أَنَّهَا سَأَلَتْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم   {أَتُصَلِّي اَلْمَرْأَةُ فِي دِرْعٍ وَخِمَارٍ ، بِغَيْرِ إِزَارٍ  ؟ قَالَ : "إِذَا كَانَ اَلدِّرْعُ سَابِغًا يُغَطِّي ظُهُورَ قَدَمَيْهَا}  أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ وَصَحَّحَ اَلْأَئِمَّةُ وَقْفَهُ

Kutoka kwa Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa alimuuliza Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Je, mwanamke anaweza kuswali na vazi refu na ushungi bila kuvaa nguo ya chini? Akasema: “Ikiwa hilo vazi ni refu linalofunika miguu yake.[4][Imetolewa na Abuu Daawuwd, na wakaisahihisha Maimaam kuwa ni Mawquwf]

 

 

 

165.

وَعَنْ عَامِرِ بْنِ رَبِيعَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {كُنَّا مَعَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  فِي لَيْلَةٍ مَظْلَمَةٍ ، فَأَشْكَلَتْ عَلَيْنَا اَلْقِبْلَةُ ، فَصَلَّيْنَا . فَلَمَّا طَلَعَتِ اَلشَّمْسُ إِذَا نَحْنُ صَلَّيْنَا إِلَى غَيْرِ اَلْقِبْلَةِ ، فَنَزَلَتْ : (فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ)}  أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَضَعَّفَهُ

Kutoka kwa ‘Aamir bin Rabiy’ah[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulikwa na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika usiku wa giza na hatukuwa na hakika ya Qiblah, tukaswali, jua lilipochomoza tukagundua tulielekea upande usiokuwa Qiblah, ikateremka Aayah: (basi popote mnapogeuka kuna Wajihi wa Allaah) [Al-Baqarah: 115].” [Imetolewa na At-Tirmidhiy, na akaidhoofisha]

 

 

 

166.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   {مَا بَيْنَ اَلْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ قِبْلَةٌ}  رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ ، وَقَوَّاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Baina ya Mashariki na Magharibi ni Qiblah[6].” [Imetolewana At-Tirmidhiy, na akaipa daraja la Qawiy Al-Bukhaariy]

 

 

 

167.

وَعَنْ عَامِرِ بْنِ رَبِيعَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يُصَلِّي عَلَى رَاحِلَتِهِ حَيْثُ تَوَجَّهَتْ بِهِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

زَادَ اَلْبُخَارِيُّ : {يُومِئُ بِرَأْسِهِ ، وَلَمْ يَكُنْ يَصْنَعُهُ فِي اَلْمَكْتُوبَةِ}

وَلِأَبِي دَاوُدَ : مِنْ حَدِيثِ أَنَسٍ : {كَانَ إِذَا سَافَرَ فَأَرَادَ أَنْ يَتَطَوَّعَ اِسْتَقْبَلَ بِنَاقَتِهِ اَلْقِبْلَةِ ، فَكَبَّرَ ، ثُمَّ صَلَّى حَيْثُ كَانَ وَجْهَ رِكَابِهِ}  وَإِسْنَادُهُ حَسَنٌ

Kutoka kwa ‘Aamir bin Rabiy’ah[7] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimemuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiswali huku kapanda mnyama wake akielekea kokote alikoelekea mnyama wake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Al-Bukhaariy akaongeza: “Huku akiashiria kwa kichwa, hakufanya hivyo (kuswali huku kapanda mnyama) kwa Swalaah za faradhi.”

 

 

Na Abuu Daawuwd amepokea Hadiyth ya Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Aliposafiri na akataka kuswali Swalaah ya Sunnah, alikuwa akimuelekeza ngamia wake Qiblah[8], akapiga takbiyra na kuendelea kuswali huku akielekea kokote ngamia wake alikoelekea.” [Isnaad yake ni Hasan]

 

 

 

168.

 وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  {اَلْأَرْضُ كُلُّهَا مَسْجِدٌ إِلَّا اَلْمَقْبَرَةَ وَالْحَمَّامَ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَلَهُ عِلَّةٌ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ardhi yote ni Msikiti, isipokuwa makaburini na msalani.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy, na ina dosari]

 

 

 

169.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {نَهَى اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  أَنْ يُصَلَّى فِي سَبْعِ مَوَاطِنَ : اَلْمَزْبَلَةِ، وَالْمَجْزَرَةِ ، وَالْمَقْبَرَةِ، وَقَارِعَةِ اَلطَّرِيقِ، وَالْحَمَّامِ، وَمَعَاطِنِ اَلْإِبِلِ، وَفَوْقَ ظَهْرِ بَيْتِ اَللَّهِ}  رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَضَعَّفَهُ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikataza kuswali katika sehemu saba[9]: (a) jalalani (b) machinjioni (c) makaburini (d) katikati ya njia (e) msalani (bafuni, chooni) (f) wanapokaa ngamia, katika sehemu ya kunywea maji, na (g) juu ya paa la Ka’bah.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy, na akaidhoofisha]

 

 

 

170.

وَعَنْ أَبِي مَرْثَدٍ اَلْغَنَوِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : سَمِعْتَ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يَقُولُ: {لَا تُصَلُّوا إِلَى اَلْقُبُورِ ، وَلَا تَجْلِسُوا عَلَيْهَا}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Marthad Al-Ghanawiyy[10] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Msiswali kuelekea makaburi[11], wala msiyakalie[12].” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

171.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {إِذَا جَاءَ أَحَدُكُمْ اَلْمَسْجِدَ ، فَلْيَنْظُرْ، فَإِنْ رَأَى فِي نَعْلَيْهِ أَذًى أَوْ قَذَرًا فَلْيَمْسَحْهُ ، وَلْيُصَلِّ فِيهِمَا}  أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Mmoja wenu anapokuja Msikitini na atazame, na akiona uchafu katika viatu vyake, basi avipanguse na kisha aswali navyo.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

172.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   {إِذَا وَطِئَ أَحَدُكُمْ اَلْأَذَى بِخُفَّيْهِ فَطَهُورُهُمَا اَلتُّرَابُ}  أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akikanyaga uchafu kwa khofu yake (soksi zake za ngozi), basi kitakaso chake ni mchanga[13].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

173.

وَعَنْ مُعَاوِيَةَ بْنِ اَلْحَكَمِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم { إِنَّ هَذِهِ اَلصَّلَاةَ لَا يَصْلُحُ فِيهَا شَيْءٌ مِنْ كَلَامِ اَلنَّاسِ ، إِنَّمَا هُوَ اَلتَّسْبِيحُ ، وَالتَّكْبِيرُ ، وَقِرَاءَةُ اَلْقُرْآنِ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

Kutoka kwa Mu’aawiyah bin Al-Hakam[14] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika hii Swalaah ndani yake haifai chochote katika maneno ya watu, kwa kuwa hiyo ni Tasbiyh, Takbiyra na kusoma Qur-aan.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

174.

وَعَنْ زَيْدِ بْنِ أَرْقَمَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {إِنْ كُنَّا لَنَتَكَلَّمُ فِي اَلصَّلَاةِ عَلَى عَهْدِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  يُكَلِّمُ أَحَدُنَا صَاحِبَهُ بِحَاجَتِهِ، حَتَّى نَزَلَتْ : (حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ) ]اَلْبَقَرَة : 238] ، فَأُمِرْنَا بِالسُّكُوتِ، وَنُهِينَا عَنْ اَلْكَلَامِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ 

Kutoka kwa Zayd bin Arqama[15] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Sisi tulikuwa tukiongea ndani ya Swalaah zama za uhai wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na mtu alikuwa akiongea na mwenzake kuhusu mahitaji yake, ilipoteremka Aayah:

(حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ)

(Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu) [Al-Baqarah: 238] tukaamrishwa kunyamaza na tukakatazwa kuongea[16].” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

175.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {اَلتَّسْبِيحُ لِلرِّجَالِ، وَالتَّصْفِيقُ لِلنِّسَاءِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

زَادَ مُسْلِمٌ {فِي اَلصَّلَاةِ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Tasbiyh (Kusema Subhaana-Allaah) ni kwa mwanamume, na kupiga makofi[17] ni kwa wanawake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Muslim akaongezea: “Ndani ya Swalaah[18].”

 

 

 

176.

وَعَنْ مُطَرِّفِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ الشِّخِّيرِ ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ : {رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يُصَلِّي، وَفِي صَدْرِهِ أَزِيزٌ كَأَزِيزِ اَلْمِرْجَلِ، مِنْ اَلْبُكَاءِ}

أَخْرَجَهُ اَلْخَمْسَةُ ، إِلَّا اِبْنَ مَاجَهْ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Mutwarrif bin ‘Abdillaah bin Shikh-khiyr[19] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kutoka kwa baba yake[20] amesema: “Nimemuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiswali, na nikasikia sauti kifuani mwake kama kuchemka kwa chungu, kwa sababu ya kulia[21].” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ahmad) isipokuwa Ibn Maajah, na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

177.

وَعَنْ عَلَيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {كَانَ لِي مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  مَدْخَلَانِ ، فَكُنْتُ إِذَا أَتَيْتُهُ وَهُوَ يُصَلِّي تَنَحْنَحَ لِي}  رَوَاهُ النَّسَائِيُّ ، وَابْنُ مَاجَهْ

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilipata ruhusa ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kumwona nyumbani kwake mara mbili, na kila nilipokwenda na kumkuta anaswali, alikuwa anajikohoza kwa ajili yangu[22] (kuwa anaswali).” [Imetolewa na An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

 

 

178.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : {قُلْتُ لِبِلَالٍ : كَيْفَ رَأَيْتُ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  يَرُدَّ عَلَيْهِمْ حِينَ يُسَلِّمُونَ عَلَيْهِ ، وَهُوَ يُصَلِّي  ؟ قَالَ : يَقُولُ هَكَذَا ، وَبَسَطَ كَفَّهُ}  أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Nilimuuliza Bilaal hivi: “Ulimuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) anawajibu vipi Mswahaba zake pindi wanapomsalimia akiwa anaswali? Bilaal akasema: alikuwa akifanya hivi, naye Bilaal akaonyesha kwa kupanua kiganja chake[23].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy naye aliisahihisha]

 

 

 

179.

 

وَعَنْ أَبِي قَتَادَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يُصَلِّي وَهُوَ حَامِلٌ أُمَامَةَ بِنْتِ زَيْنَبَ، فَإِذَا سَجَدَ وَضَعَهَا ، وَإِذَا قَامَ حَمَلَهَا}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَلِمُسْلِمٍ : {وَهُوَ يَؤُمُّ اَلنَّاسَ فِي اَلْمَسْجِدِ}

Kutoka kwa Abuu Qataadah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anaswali huku kambeba Umaamah bint Zaynab[24], na aliposujudu[25] alimweka chini, na aliposimama alimnyanyua.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Muslim amesema: “Na yeye (Nabiy) anaswalisha watu.”

 

 

 

180.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   {اُقْتُلُوا اَلْأَسْوَدَيْنِ فِي اَلصَّلَاةِ : اَلْحَيَّةَ، وَالْعَقْرَبَ}  أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ueni vyeusi viwili mkiwa ndani ya Swalaah: nyoka na nge[26].” [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

[1] Aliy bin Twalq bin Al-Mundhir bin Qays Al-Hanafiy ni ambaye kutoka kwa Banu Hanifa, As-Sahimi, na Al-Yamami. Alikuwa ni Swahaba, na inasemekana kuwa ndiye aliyekuwa baba wa Twalq bin ‘Aliy, lakini ilisemekana kuwa majina hayo mawil ni ya mtu mmoja huyo huyo.

 

[2] Hii maana yake ni kwamba, ikiwa wudhuu umetanguka wakati wa Swalaah, lazima kuchukua wudhuu upya na Swalaah hiyo irudiwe. Hii ndiyo bora zaidi.

 

[3] Khimaar ni mtandio au kipande cha nguo ambacho kwacho mwanamke hujifunikia eneo la kichwa na la shingo lake. Hiyo inamaanisha kuwa mwili mzima wa mwanamke sharti ufunikwe pamoja na kichwa na nywele zake.

[4] Hii iko pamoja na masharti ya Swalaah kuwa, mwanamke sharti pia afunike miguu yake mpaka kwenye visigino, vinginevyo Swalaah yake haitokubaliwa.

 

[5] ‘Aamir bin Rabiy’ah bin Maalik Al-‘Inzy, na inasemekana ni Al-‘Adawy. Alisilimu na akafanya Hijrah mara mbili. Alihudhuria Vita vyote. Alifariki wakati alipokufa ‘Uthmaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).

 

[6] Kwa maneno hayo, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ameelezea upande iliko Qiblah (Ka’bah) kwa ulimwengu mzima. Watu wanaoishi Mashariki au Magharibi ya Qiblah, wachukue maana ya Hadiyth hii kwamba Qiblah iko kati ya kunakochomozea jua na kunakochwea jua mnamo majira ya baridi na joto. Na wale wanaoishi kaskazini na kusini ya Qiblah, wachukue maaana ya kuwa, wakisimama huku Mashariki na Magharibi iko upande wao wa kuume na kushoto, basi Qiblah yao iko katikati ya pande hizi mbili.

 

[7] ‘Aamir bin Rabiy’a alikuwa mmoja wa wana wa ‘Anz bin Wa’il, ambaye alikuwa ndugu ya Bakr na Taghlib, wana wa Wa’il. Alikuwa Swahaba aliyesilimu mapema sana na akafanya Hijrah (kuhama) zote mbili. Alishiriki katika Badr na vita zote nyingine, na akafariki mnamo mwaka 32 au 35 A.H

 

[8] Hii maana yake ni kwamba, Swalaah ya Sunnah (Nafl) ndiyo inayoweza kuswaliwa huku mtu kapanda mnyama au chombo, kwa sharti kuwa pale anapoanza kuswali, mnyama yule au chombo kile akielekeze Qiblah, na baada ya hapo badiliko lolote la mwelekeo haliathiri kitu. Lakini Swalaah za faradhi zisiswaliwe mtu akiwa kampanda mnyama, lakini meli, majahazi, mitumbwi, na ndege, vinaruhusiwa.

 

[9] Hadiyth hii ni ushahidi kuwa kuswali makaburini hairuhusiwi, uwe unaswali juu ya makaburi au katikati ya makaburi, na si hoja ikiwa makaburi hayo ni ya Waislaamu au wasiokuwa Waislaamu. Kuswalia makaburini kunatoa picha ya kuabudu asiyekuwa Allaah, ambalo ni kosa kubwa la ushirikina. Imekatazwa kuswali msalani kwa sababu ya najisi na uchafu uliyoko huko; na isitoshe Hadiyth zinasema kuwa msalani ni mahala pa shaytwaan.

 

[10] Jina la Abuu Marthad Al-Ghanawiyy ni Kannaz bin Hussayn bin Yarbu’ Al-Ghanawiyy kizazi cha Ghani bin Ya’sur, kabila la Ghatafan. Alikuwa ni Swahaba ambaye alishuhudia Badr na alikuwa sahibu wa Hamza bin ‘Abdil-Muttwalib, na alikuwa sawa naye ki umri. Alishiriki katika Vita vyote, na akafa mnamo mwaka 12 A.H. akiwa na umri wa miaka 66.

 

[11] Ina maana kuwa, imekatazwa kuswali huku ukielekea makaburi. Watu wengine wanajenga Misikiti karibu na makaburi ya watakatifu ili kupata fadhila za roho zilizokufa. Hii pia imekatazwa. Katika Hadiyth ya ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) imesemwa waziwazi kuwa: “Allaah (عز وجل) Awalaani Mayahudi na Wakristo, kwani walifanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kusalia.” Inaweza kumaanisha pia kwamba matendo yatakiwayo kuyafanya mbele ya Allaah (عز وجل) Misikitini kamwe yasitendwe katika makaburi. Au pia yaweza kumaanisha kuwa kamwe mtu asiswali mahala ambapo kuna makaburi mbele yake.

 

[12] Kukalia juu ya makaburi kuna maana mbili: moja ni kupumzika au kuegemea makaburi; na pili ni kuyamiliki makaburi kama Mujawwir (mwangalizi wa makaburi ambaye pia hukusanya pesa na vitu vingine kutoka kwa watu wanaozuru makaburi ili kupata radhi za roho zilizozikwa). Aina zote hizo mbili zimekatazwa, inaweza kuwa na maana nyingine kwamba mtu yoyote asikae juu ya kaburi au asijisaidie haja kubwa au ndogo. Hii pia imekatazwa.

 

[13] Hadiyth hizi mbili zinaonyesha kuwa kuswali huku mtu amevaa soksi na au viatu inaruhusiwa. Zinasema pia kuwa endapo viatu hivyo vitachafuliwa na uchafu wowote, vinyesi vya wanyama au bin Aadam, inatosha kusugua kwa vumbi na hakuna haja ya kuosha kwa maji.

 

[14] Huyu Mu’aawiyah bin Al-Hakam alikuwa Swahaba aliyehesabika miongoni mwa wakazi wa Hijaaz. Alikuwa akizuru Madiynah na akawa anakaa kwa akina Banu Sulaym. Alifariki mnamo mwaka 117 A.H.

 

[15] Zayd bin Arqam alipewa jina la utani la Abuu ‘Amr, na alikuwa Answaar Mkhazraj. Kwanza alishiriki katika Vita vya Al-Khandaq, na akaongozana na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika misafara 17. Alihudhuria Vita vya Siffin pamoja na ‘Aliy kwa kuwa alikuwa mmoja wa wafuasi wake. Alilowea kule Kuwfah, na akafia huko mnamo mwaka 66 A.H.

 

[16] Inamaanisha kuwa kuongea wakati wa Swalaah kumekatazwa. Mnamo siku za mwanzo mwanzo za Uislaam, watu walikuwa wakiongea tu ndani ya Swalaah, kisha likaja katazo.

 

[17] Inamaanisha kwamba, iwapo Imaam akitenda kosa kwa bahati mbaya ndani ya Swalaah, wanaume maamuma wake (wanaokuwa nyuma ya huyo Imaam) hutakiwa waseme hivi:

سبحان الله

(kumkumbusha Imaam alisahihishe kosa lake hilo), na wanawake wanatakiwa wapige makofi kidogo (kwa maana hiyo hiyo ya kumkumbusha Imaam), ili sauti (ya mwanamke) isisikike na wanaume.

 

[18] Yaani ikiwa mtu anataka kumkumbusha Imaam jambo alilolisahau, ndani ya Swalaah, sharti aseme:

 سبحان الله

Lakini ikiwa ni mwanamke anayetaka kumkumbusha Imaam, basi sharti mwanamke huyo apige makofi kwa kuvipiga pamoja na vidole vya kiganja chake cha kuume kwa cha kushoto.

 

[19] Huyu Mutwarrif ndiye Mutwarrif bin ‘Abdillaah bin Ash-Shikhkhir Al-Harashi Al-‘Aamir Al-Basr, miongoni mwa Taabi’iyna wa zamani. Aliaminika sana, alikua muadilifu, na alifanya matendo mengi ya sifa nzuri nzuri. Alikufa mnamo mwaka 95 A.H

 

[20] Baba yake Mutwarrif alikuwa ni ‘Abdullaah bin Ash-Shikhkhir bin ‘Awf bin Ka’b Al-Harashi Al-‘Aamir, huyo wa mwisho ni Swahaba. Alikuwa ni mjumbe wa ujumbe wa Banu ‘Aamir na anaaminiwa kuwa alilowea Basra.

 

[21] Kwa mujibu wa Hadiyth, kulia ndani ya Swalaah kwa kumuogopa Allaah kunaruhusiwa; lakini kulia kwa sababu ya ugonjwa au adha yoyote kunabatilisha Swalaah.

 

[22] Inamaanisha kuwa kutoa dalili ya kukohoa hasa mara moja moja au mbili, hakutangui Swalaah. Kitabu cha Musaffa cha ufafanuzi wa Mu’atta kinaelezea kuwa, kukohoa, kulia, au kucheka kwa mfululizo, ingawa huko siyo kusema, kunatangua Swalaah.

 

[23] Inamaanisha kuwa matendo madogo madogo hayabatilishi Swalaah.

 

[24] Umaamah ni mjukuu wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), binti wa Zaynab kwa Abdul-‘Aass bin Ar-Rabi’. Aliolewa na ‘Aliy baada ya kifo cha Faatwimah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kwa mujibu wa mapendekezo ya Faatwimah. Na ‘Aliy alipouliwa, aliolewa na Al-Mughiyrah bin Nawfal, na akafariki wakati akiwa kwa mume huyu.

 

[25] Shah Waliyu-Allaah wa Delhi aliandika katika kitabu chake  حجة الله البالغة kuwa, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alifanya vitendo vidogo vidogo kwa maksudi ili kuonyesha kuwa vitendo vidogo vidogo havitengui Swalaah. Hadiyth zinasema kuwa, kukiwa na dharura, yafuatayo hayaathiri wala kutangua Swalaah: (a) Tamko dogo, (b) Kuhama kidogo mahali ulipo, vitendo vidogo, (c) Badiliko dogo la mahala uliko kuenda mbele au nyuma, (d) Kutoa ishara au kuashiria kitu kwa mguu, (e) Kufungua mlango kwa kuhama kidogo tu, (f) Kusogea nyuma wakati mtu (wa tatu) anajiunga nanyi (kuswali jamaa), (g) Kulia kwa kumuogopa Allaah, (h) Kutoa ishara ili kuelewesha kitu fulani, (i) Kuua nge au nyoka, (j) Kutazama pembeni bila kugeuza shingo.

 

[26] Hadiyth hii inathibitisha vitu viwili: (a) Swalaah haitanguki kwa kuua nge na nyoka, (b) Mtu asiwaonee huruma. Sharti wauawe na wasiachwe kwani wao wana madhara.

 

Share

04-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Sutrah (Kizuzi) Ya Mwenye Kuswali

 

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

Kitabu Cha Swalaah

 

بَـــابُ سُــتْرَةِ اَلْمُصَــلِّي

04-Mlango Wa Sutrah[1] (Kizuzi) Ya Mwenye Kuswali

 

 

 

 

 

 

181.

عَنْ أَبِي جُهَيْمِ بْنِ اَلْحَارِثِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {لَوْ يَعْلَمُ اَلْمَارُّ بَيْنَ يَدَيِ اَلْمُصَلِّي مَاذَا عَلَيْهِ مِنْ اَلْإِثْمِ لَكَانَ أَنْ يَقِفَ أَرْبَعِينَ خَيْرًا لَهُ مِنْ أَنْ يَمُرَّ بَيْنَ يَدَيْهِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ

وَوَقَعَ فِي "اَلْبَزَّارِ" مِنْ وَجْهٍ آخَرَ : {أَرْبَعِينَ خَرِيفًا}

Kutoka kwa Abuu Juhaym bin Al-Haarith[2] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Lau angejua anayepita mbele ya anayeswali, dhambi kubwa aliyo nayo ingekuwa bora kwake kusimama (siku) arubaini, kuliko kupita mbele yake.[3][Al-Bukhaariy, Muslim, na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

Na imetajwa katika Al-Bazzaar kwa njia nyingine na imeongezwa: “Miaka arubaini.”

 

 

 

182.

وَعَنْ عَائِشَةَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ : {سُئِلَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   فِي غَزْوَةِ تَبُوكَ  عَنْ سُتْرَةِ اَلْمُصَلِّي . فَقَالَ : "مِثْلُ مُؤْخِرَةِ اَلرَّحْلِ"}  أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliulizwa katika vita vya Tabuwk kuhusu Sutrah (kizuizi) ya anayeswali, akasema: ni kama sehemu ya nyuma ya tandiko la mnyama[4].” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

183.

وَعَنْ سَبْرَةَ بْنِ مَعْبَدٍ اَلْجُهَنِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لِيَسْتَتِرْ أَحَدُكُمْ فِي صَلَاتِهِ وَلَوْ بِسَهْمٍ}  أَخْرَجَهُ اَلْحَاكِمُ 

Kutoka kwa Sabrah bin Ma’bad Al-Juhaniyy[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu aweke sutrah[6] katika Swalaah, japo kwa kuweka mshale.” [Imetolewa na Al-Haakim]

 

 

 

184.

وَعَنْ أَبِي ذَرٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {يَقْطَعُ صَلَاةَ اَلْمَرْءِ اَلْمُسْلِمِ  إِذَا لَمْ يَكُنْ بَيْنَ يَدَيْهِ مِثْلُ مُؤْخِرَةِ اَلرَّحْلِ  اَلْمَرْأَةُ ، وَالْحِمَارُ ، وَالْكَلْبُ اَلْأَسْوَدُ . . . " اَلْحَدِيثَ}  وَفِيهِ {اَلْكَلْبُ اَلْأَسْوَدِ شَيْطَانٌ}  . أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ 

وَلَهُ : عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   نَحْوُهُ دُونَ : "اَلْكَلْبِ

وَلِأَبِي دَاوُدَ ، وَالنَّسَائِيِّ : عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا نَحْوُهُ ، دُونَ آخِرِهِ . وَقَيَّدَ اَلْمَرْأَةَ بِالْحَائِضِ

 Kutoka kwa Abuu Dharr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Itakapokuwa hakuna mbele yake, (Sutrah) mfano wa sehemu ya nyuma ya tandiko la mnyama[7], basi Swalaah ya Muislamu itakatika ikiwa atapita mwanamke au punda na mbwa mweusi.” Na Hadiyth inasema pia: “Na mbwa mweusi ni shaytwaan.[8][Imetolewa na Muslim]

 

Naye amepokea Hadiyth ya Abuu Hurayrah kama hiyo pasi na kutaja “mbwa.”

 

Nao Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy wamepokea Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) pasi na mwisho wake, na akafungamanisha mwanamke na hedhi.

 

 

 

185.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ إِلَى شَيْءٍ يَسْتُرُهُ مِنْ اَلنَّاسِ ، فَأَرَادَ أَحَدٌ أَنْ يَجْتَازَ بَيْنَ يَدَيْهِ فَلْيَدْفَعْهُ ، فَإِنْ أَبَى فَلْيُقَاتِلْهُ ، فَإِنَّمَا هُوَ شَيْطَانٌ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ .

وَفِي رِوَايَةٍ : {فَإِنَّ مَعَهُ اَلْقَرِينَ}

 Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akiswali kuelekea kitu kinachomsitiri dhidi ya watu wengine, na mtu akataka kupita mbele yake, basi amzuie, akikataa, apigane naye[9], kwani huyo ni shaytwaan.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Riwaayah nyingine: “Kwani shaytwaan yuko pamoja naye.”

 

 

 

186.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَجْعَلْ تِلْقَاءَ وَجْهِهِ شَيْئًا ، فَإِنْ لَمْ يَجِدْ فَلْيَنْصِبْ عَصًا ، فَإِنْ لَمْ يَكُنْ فَلْيَخُطَّ خَطًّا ، ثُمَّ لَا يَضُرُّهُ مَنْ مَرَّ بَيْنَ يَدَيْهِ}  أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ وَابْنُ مَاجَهْ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ ، وَلَمْ يُصِبْ مَنْ زَعَمَ أَنَّهُ مُضْطَرِبٌ ، بَلْ هُوَ حَسَنٌ .

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Endapo mmoja wenu anaswali, basi aweke kitu mbele yake, na iwapo hana kitu cha kuweka, basi asimamishe fimbo, na akiwa hana fimbo basi achore msitari, ndipo hatadhuriwa na anayepita mbele yake[10].” [Imetolewa na Ahmad na Ibn Maajah, na akaisahihisha Ibn Hibbaan, wala hakupatia aliyesema ni Mudhw-twarib, bali hiyo ni Hasan]

 

 

 

187.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {لَا يَقْطَعُ اَلصَّلَاةَ شَيْءٌ ، وَادْرَأْ مَا اِسْتَطَعْتَ}  أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَفِي سَنَدِهِ ضَعْفٌ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna chochote kinachokatisha Swalaah, lakini epusha kadiri mnavyoweza (vitu vinavyokatisha Swalaah).” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, na katika Isnaad yake kuna udhaifu]

 

 

 

[1] Sutrah (kizuizi) ni kitu chochote ambacho mtu anayeswali hukiweka mbele yake iwe kama kizuizi kati yake yeye na wengine.

 

[2] Inasemekana kuwa huyu Abuu Juhaym jina lake ni ‘Abdullaah bin Al-Haarith bin As-Simma Al-Answaar Al-Khazraj. Alikuwa ni Swahaba anayejulikana sana, ambaye aliishi hadi wakati wa Ukhalifa wa Mu’aawiyah.

 

[3]  “Mpaka” wa mtu anayeswali ni mahala pale mahali anaposujudia. Kukatisha mbele zaidi ya mpaka huu siyo kosa. Onyo hili ni la mtu anayekatisha, siyo mtu aliyekwisha kukaa au anaswali mbele yake, na anayefanya vitendo vingine (visivyostahiki ndani ya Swalaah).

 

[4] Urefu wa Sutrah ni sharti uwe kwa uchache sawa sawa na sehemu ya nyuma ya tandiko. Hiyo ni sawa na takribani futi moja. Endapo hakuna kitu kingine, basi fimbo inaweza kufanya kazi badala ya Sutrah. Na iwapo hata fimbo hakuna, msitari waweza kuchorwa kama anavyoelezea Abuu Daawuwd.

 

[5] Sabrah bin Ma’yad Al-Juhaniyy alikuwa ni Swahaba kutoka Al-Madiynah aliyelowea kule Dhi Marwa. Alipewa jina la utani la Abuu Thuraiya. Kwanza alishiriki katika vita vya Al-Khandaq (Vita vya Handaki). Aliyekuwa ndiye mjumbe wa ‘Aliy kuenda kwa Mu’aawiyah, alipoteuliwa kuwa Khalifa, kumtaka athibitishe utii wa watu wa shaam kwa ‘Aliy. Alikufa mnamo mwish wa Ukhalifa wa Mu’aawiyah.

 

[6]  Wakati mtu anaposwali, Baraka za Allaah (عز وجل)  humuelekea yeye. Sutrah huwa kama ukingo, na Baraka za Allaah (عز وجل)  hubakia ndani ya eneo la ukingo huo. Mtu yoyote anayekatisha njia nje ya Sutrah hiyo, haikabili Baraka ya Allaah (عز وجل) na Swalaah haiathiriki. Kusipokuwepo Sutrah (kizuizi), basi huwa hakuna mpaka wa Baraka za Allaah (عز وجل), na mtu anayekatisha mbele ya mtu anayeswali hugongana na Baraka hiyo, na umakini kwa Allaah wa mtu wa anayeswali huvurugika. Kwa hivyo Sutrah ilifanywa iwe lazima.

 

[7] Inamaanisha kwamba inaathiri unyenyekevu kwa Allaah (عز وجل) tu, lakini hakuathiri Swalaah.

 

[8] Katika Hadiyth hii kuna ushahidi kuwa, bila kuwepo Sutrah viumbe vilivyotajwa hapo juu vikipita mbele ya mtu anayeswali, Swalaah yake hukatishwa. Lakini kuna Hadiyth iliyoafikiwa inayosema kuwa, Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) huku akiwa amempanda punda alipita mbele ya msururu wa Waumini wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anaswali, naye Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuirudia Swalaah yake wala hakuwaamuru Swahaba zake warudie Swalaah zao.

 

[9] Kupita mbele ya mtu anayeswali imeafikiwa kunahesabika ni kumtengeua. Iwapo mtu anaswali nyuma ya Sutrah (kizuizi), na mtu kukatisha njia apite ndani yake, asimamishwe kwa ishara, na aking’ang’ania kupita, azuiwe kwa nguvu. “Kupigana”. Endapo Muumini anaswali bila ya kuwa na Sutrah mbele yake, ni kosa na Muumini anayeswali na siyo kosa la mpitaji. Pia Hadiyth hii inaonyesha kuwa Swalaah ya Muumini huyo haikatishwi kwa kitendo hicho kidogo, lakini kitendo hicho kinaathiri umakinifu.

 

 

[10] Inaonyeshwa kuwa Swalaah haikatishwi kwa mtu kupita mbele, lakini huathiri umakinifu.

 

 

Share

05-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Sisitizo La Khushuw’ (Unyenyekevu) Katika Swalaah

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ اَلْحَثِّ عَلَى اَلْخُشُوعِ فِي اَلصَّلَاةِ

05-Mlango Sisitizo La Khushuw’[1] (Unyenyekevu) Katika Swalaah

 

 

 

 

188.

  عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ يُصَلِّيَ اَلرَّجُلُ مُخْتَصِرًا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ

وَمَعْنَاهُ: أَنْ يَجْعَلَ يَدَهُ عَلَى خَاصِرَتِهِ 

وَفِي اَلْبُخَارِيِّ : عَنْ عَائِشَةَ   رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا  أَنَّ ذَلِكَ فِعْلُ اَلْيَهُودِ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikataza mtu kuswali hali ya kuweka mikono kiunoni.[2] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

Na maana yake ni: “Mtu kuweka mikono yake kwenye kiuno.”

 

 

Na katika Al-Bukhaariy kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا): “Kuwa ni kitendo cha Mayahudi katika Swalaah zao.”

 

 

 

189.

وَعَنْ أَنَسٍ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ : {إِذَا قُدِّمَ اَلْعَشَاءُ فَابْدَءُوا بِهِ قَبْلَ أَنْ تُصَلُّوا اَلْمَغْرِبَ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kikiwadia chakula cha jioni (na huku Swalaah imewadia) kianzeni kabla hamjaswali[3]  Magharibi.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

190.

وَعَنْ أَبِي ذَرٍّ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   {إِذَا قَامَ أَحَدُكُمْ فِي اَلصَّلَاةِ فَلَا يَمْسَحِ اَلْحَصَى، فَإِنَّ اَلرَّحْمَةَ تُوَاجِهُهُ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ 

وَزَادَ أَحْمَدُ : "وَاحِدَةً أَوْ دَعْ"

وَفِي "اَلصَّحِيحِ" عَنْ مُعَيْقِيبٍ نَحْوُهُ بِغَيْرِ تَعْلِيلٍ

Kutoka kwa Abuu Dharr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anaposimama mmoja wenu katika Swalaah, asijipanguse vijiwe[4] kwani Rahmah inamuelekea yeye.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) kwa Isnaad swahiyh]

 

Na akaongezea Ahmad: “(Ondosha) mara moja tu, au acha.”

 

Na ndani ya Swahiyh (Al-Bukhaariy) kuna Hadiyth kama hiyo, kutoka kwa Mu’ayqib[5] bila kutajwa sababu.

 

 

 

191.

عَنْ عَائِشَةَ   رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا   قَالَتْ : {سَأَلْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  عَنْ اَلِالْتِفَاتِ فِي اَلصَّلَاةِ ؟  فَقَالَ : "هُوَ اِخْتِلَاسٌ يَخْتَلِسُهُ اَلشَّيْطَانُ مِنْ صَلَاةِ اَلْعَبْدِ}  رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

  وَلِلتِّرْمِذِيِّ: عَنْ أَنَسٍ  وَصَحَّحَهُ   {إِيَّاكَ وَالِالْتِفَاتَ فِي اَلصَّلَاةِ، فَإِنَّهُ هَلَكَةٌ، فَإِنْ كَانَ فَلَا بُدَّ فَفِي اَلتَّطَوُّعِ} 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) juu ya kugeuka geuka ndani ya Swalaah naye akasema: Huko ni kunyakua ambako shaytwaan hunyakua kutoka katika Swalaah ya mja.” [Imetolew na Al-Bukhaariy]

 

Na katika At-Tirmidhiy kutoka kwa Anas aliisahihisha ameandika: “Epuka kugeuka geuka ukiwa ndani ya Swalaah, kwani kutazama pembeni ni uharibifu, na ikiwa ni lazima[6] basi iwe katika Swalaah ya Sunnah.[7]

 

 

 

192.

وَعَنْ أَنَسٍ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {إِذَا كَانَ أَحَدُكُمْ فِي اَلصَّلَاةِ فَإِنَّهُ يُنَاجِي رَبَّهُ، فَلَا يَبْزُقَنَّ بَيْنَ يَدَيْهِ وَلَا عَنْ يَمِينِهِ، وَلَكِنْ عَنْ شِمَالِهِ تَحْتَ قَدَمِهِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَفِي رِوَايَةٍ : {أَوْ تَحْتَ قَدَمِهِ}  

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akiwa ndani ya Swalaah, anakuwa anamnong’oneza Allaah, kwa hivyo asiteme mate mbele yake[8], wala upande wa kuume, lakini kushotoni kwake na chini ya mguu wake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Riwaayah nyingine: “Au chini ya mguu wake.”

 

 

 

193.

وَعَنْهُ قَالَ : {كَانَ قِرَامٌ لِعَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا  سَتَرَتْ بِهِ جَانِبَ بَيْتِهَا فَقَالَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم   أَمِيطِي عَنَّا قِرَامَكِ هَذَا، فَإِنَّهُ لَا تَزَالُ تَصَاوِيرُهُ تَعْرِضُ لِي فِي صَلَاتِي}  رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ 

وَاتَّفَقَا عَلَى حَدِيثِهَا فِي قِصَّةِ أَنْبِجَانِيَّةِ أَبِي جَهْمٍ ، وَفِيهِ : {فَإِنَّهَا أَلْهَتْنِي عَنْ صَلَاتِي}

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “’Aaishah alikuwa na Qiraam[9] aliyoitumia kusitiri upande mmoja wa nyumba yake, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamwambia: “Ondoa[10] pazia lako, kwani picha zake hazijaacha kunitokea katika Swalaah yangu.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

Al-Bukhaariy na Muslim pia waliafikiana Hadiyth iliyosimuliwa naye (‘Aaishah) amabayo inataja kisa cha Anbijaaniyyah[11] Abiy Jahm[12], ikieleza pia: “Hiyo[13] imenivurugia umakinifu[14] wa Swalaah yangu.”

 

 

 

194.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةٍ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَيَنْتَهِيَنَّ قَوْمٌ يَرْفَعُونَ أَبْصَارَهُمْ إِلَى اَلسَّمَاءِ فِي اَلصَّلَاةِ أَوْ لَا تَرْجِعَ إِلَيْهِمْ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَلَهُ : عَنْ عَائِشَةَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا  قَالَتْ : سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   يَقُولُ : {لَا صَلَاةَ بِحَضْرَةِ طَعَامٍ ، وَلَا هُوَ يُدَافِعُهُ الْأَخْبَثَانِ}

  Kutoka kwa Jaabir bin Samurah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Watu wanaoelekeza macho yao mbinguni wanapokuwa ndani ya Swalaah, waache, au sivyo kuona kwao hakutawarudia[15].” [Imetolewa na Muslim]

 

 

Pia (Muslim) amenukuu Hadiyth ya ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kuwa amesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema hakuna Swalaah wakati wa kuhudhuria chakula, wala mtu anapojizuia haja mbili (kubwa na ndogo)[16].”

 

 

 

195.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   قَالَ : {اَلتَّثَاؤُبُ مِنْ اَلشَّيْطَانِ فَإِذَا تَثَاءَبَ أَحَدُكُمْ فَلْيَكْظِمْ مَا اِسْتَطَاعَ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

وَاَلتِّرْمِذِيُّ ، وَزَادَ : {فِي اَلصَّلَاةِ}  

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kupiga miayo hutokana na shaytwaan[17], kwa hivyo mmoja wenu anapopiga miayo ajizuie kadiri anavyoweza.” [Imetolewa na Muslim]

Na katika At-Tirmidhiy ameongeza: “Ndani ya Swalaah[18].”

 

 

[1] Khushuw’ maana yake ni unyenyekevu, utulivu, ushwari, na kumakinia mwili mzima na akili yote kwa Allaah (سبحانه وتعالى).

 

[2] Kuweka mikono pembeni au kiunoni ni kitendo cha kujiona, wakati unyenyekevu na upole ndio unaotakiwa katika Swalaah. Nukta nyingine iliyofafanuliwa katika Hadiyth inayofuata ni kuwa hii inafanana na desturi ya Mayahudi, na kuwaiga wao imekatazwa.

 

[3] Ikiwa chakula kimeandaliwa, kula chakula hicho ni afadhali hata kama huna njaa. Falsafa ya kufanya hivi ni kwamba, mtu anatakiwa asimame mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى)   huku akiwa karidhika kikamilifu na akiwa juu ya mahitaji yoyote ya kidunia. Lakini hairuhusiwi kuenda kula wakati wa Swalaah ilhali hicho chakula hakijaandaliwa.

 

[4] Kuondosha changarawe kutoka mahala pa kusujudia kumekatazwa ikiwa vijiwe vyenyewe ni vidogo na havina madhara. Ama ikiwa vijiwe ni vikubwa na vinaleta adha na vinazuia umakinifu, basi hakuna dhara kuviondosha.

 

[5] Mu’ayqiyb bin Abiy Faatwimah Ad-Daws alisilimu zamani sana kule Makkah, na akahama Abyssinia wakati wa Hijrah ya pili. Alishuhudia Badr. Alikuwa akiihifadhi lakiri ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na baadaye Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) na baadaye tena ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) walimfanya mkuu wa Baytul-Maal. Alikufa wakati wa Ukhalifa wa ‘Uthmaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).

 

[6] Iwapo ni lazima, waweza kugeuka katika Swalaah ya Sunnah (nafl) lakini siyo katika Swalaah ya fardhi. Kwa sababu kuna madhara kidogo zaidi kufanya kitendo hicho katika Swalaah ya Sunnah. Katika dharura muhimu sana, huruhusiwa, kama ilivyodhihirika katika ugonjwa wa mwisho wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipotoka nje ya nyumba yake ili akaswali Msikitini, Abuu Bakr Swiddiyq (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) aliyekuwa akiswalisha wakati huo alitaka arudi nyuma kumpisha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aswalishe, lakini aliashiriwa na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) asirudi nyuma akaendelea kuswalisha, naye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakumkosoa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).

 

[7] Hata katika Swalaah ya khiari, uso ukigeuka mbali na Qiblah, Swalaah inakatika.

 

[8] Sharti ikumbukwe kwamba mtu kamwe asiteme mate kuelekea Qiblah, au upande wa kuume, awe ndani ya Swalaah au nje ya Swalaah.

 

[9] Kipande cha nguo laini chenye nakhsi rangi.

 

[10] Inamaanisha kuwa kitu chochote kinachovuruga khushuw’ ni lazima kiondoshwe kutoka katika mahala pa kuswalia. Ikiwa hii haiwezekani, basi epuka mahala hapo na uende kwengine.

 

[11] Vazi la sufi lisilokuwa na nakshi wala picha au maandishi.

 

[12] Abuu Jahm ndiye Ibn Hudhayfah bin Ghaniym Al-‘Adawi. Jina lake ni ‘Aamir au ‘Ubayd. Alisilimu katika mwaka ule ilipotekwa Makkah. Alikuwa miongoni mwa Swahaba walioishi umri mrefu, kwani huyu alihudhuria ujenzi wa Ka’bah wa Maqurayshi kabla ya ujio wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na akashuhudia ujenzi wake upya wa ‘Abdullaah bin Az-Zubayr ambaye Abuu Jahm alifariki mwanzoni mwa Ukhalifa wake.

 

[13] Kipande cha nguo laini chenye nakshi na rangi.

 

[14] Inamaanisha kwamba Misikiti isipambwe kwa nakshi na urembo n.k. kwa kuwa vinazuwia umakinifu. Imaam Nawawi amenukuu maafikiano ya ‘Ulamaa wa Kiislamu kuwa katazo hili ni halisi.

 

[15] Imaam An-Nawawi ameripoti maafikiano ya ‘Ulamaa wa Kiislamu kwamba katazo hili ni halisi. Ibn Hazm anasema kuwa Swalaah inabatilika.

 

[16] Endapo mtu anahisi kutaka kuenda haja (choo), kukojoa au kutoa upepo, na akiwa anao muda wa kutosha, basi afanye hivyo kabla hajaanza kuswali, vinginevyo itakuwa karaha. Kwa mujibu wa wengine, hiyo haitahesabika kuwa ni Swalaah kabisa kwa sababu ya kutokuwepo umakinifu na unyenyekevu kwa Allaah (عز وجل). Iwapo muda ni mfupi sana na mtu ana haraka sana, basi aswali ile Swalaah kuliko kuchelewa.

 

 

[17] Kutoa mwayo ni matokeo ya kujaa tumbo ni uvivu. Shaytwaan hufurahi kumuona mwana Aadam yuko hivyo, kwa hivyo kupiga mwayo kunahesabika kuwa ni tabia ya kishaytwaan.

 

[18] Kuzuia mwayo ndani ya Swalaah au katika wakati wowote ni Sunnah

 

Share

06-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Misikiti

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ اَلْمَسَاجِدِ

06-Mlango Wa Misikiti

 

 

 

 

 

 

196.

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {أَمَرَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِبِنَاءِ اَلْمَسَاجِدِ فِي اَلدُّورِ، وَأَنْ تُنَظَّفَ، وَتُطَيَّبَ}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَ إِرْسَالَهُ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amsema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliamrisha Misikiti ijengwe katika maeneo ya makazi[1], na kwamba isafishwe na itiwe manukato.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, naye aliithibitisha kama Mursal]

 

 

 

197.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَاتَلَ اَللَّهُ اَلْيَهُودَ : اِتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْه

وَزَادَ مُسْلِمُ {وَالنَّصَارَى} 

وَلَهُمَا : مِنْ حَدِيثِ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا : {كَانُوا إِذَا مَاتَ فِيهِمْ اَلرَّجُلُ اَلصَّالِحُ بَنَوْا عَلَى قَبْرِهِ مَسْجِدًا}  وَفِيهِ : {أُولَئِكَ شِرَارُ اَلْخَلْقِ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah awalaani Mayahudi, wamefanya makaburi ya Manabii wao kuwa Misikiti.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na Muslim akaongeza: “Na Manaswara.”

 

Nao (Al-Bukhaariy, Muslim) wamepokea kuwa: “’Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: Walikuwa akifariki mtu mwema miongoni mwao (Mayahudi na Manaswara) wanajenga juu ya kaburi lake Msikiti.”

 

 

Katika Hadiyth hiyo hiyo iliongezwa: “Hao ni viumbe waovu kabisa katika viumbe[2].”

 

 

 

198.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {بَعَثَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم خَيْلاً، فَجَاءَتْ بِرَجُلٍ، فَرَبَطُوهُ بِسَارِيَةٍ مِنْ سَوَارِي اَلْمَسْجِدِ}  اَلْحَدِيثَ . مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alituma wapanda farasi ambao walirudi na mtu mmoja, kisha wakamfunga[3] katika moja ya nguzo za Msikiti.[4][Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

199.

وَعَنْهُ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   أَنَّ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  مُرَّ بِحَسَّانَ يَنْشُدُ فِي اَلْمَسْجِدِ ، فَلَحَظَ إِلَيْهِ ، فَقَالَ : "قَدْ كُنْتُ أَنْشُدُ ، وَفِيهِ مَنْ هُوَ خَيْرٌ مِنْكَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena: “’Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimkuta Hassan[5] akiimba mashairi Msikitini, akamtazama kwa jicho kali, akasema Nilikuwa naimba Msikitini[6] akiwemo mbora zaidi kuliko wewe (yaani Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)).” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

200.

وَعَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  مَنْ سَمِعَ رَجُلاً يَنْشُدُ ضَالَّةً فِي اَلْمَسْجِدِ فَلْيَقُلْ : لَا رَدَّهَا اَللَّهُ عَلَيْكَ، فَإِنَّ اَلْمَسَاجِدَ لَمْ تُبْنَ لِهَذَا}  رَوَاهُ مُسْلِم

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kumsikia mtu anatangaza Msikitini kupoteza kitu, aseme: Allaah Asikurejeshee[7] ulichopoteza, kwani Misikiti haikujengwa kwa ajili ya hilo.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

201.

وَعَنْهُ : أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  إِذَا رَأَيْتُمْ مَنْ يَبِيعُ ، أَوْ يَبْتَاعُ فِي اَلْمَسْجِدِ، فَقُولُوا: لَا أَرْبَحَ اَللَّهُ تِجَارَتَكَ}  رَوَاهُ النَّسَائِيُّ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mkimuona anayenunua au anauza[8] vitu Msikitini, semeni” “Allaah Asiipe faida biashara yako[9][Imetolewa na An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy, naye aliita Hasan]

 

 

 

202.

وَعَنْ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  لَا تُقَامُ اَلْحُدُودُ فِي اَلْمَسَاجِدِ ، وَلَا يُسْتَقَادُ فِيهَا}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ بِسَنَدٍ ضَعِيف

Kutoka kwa Hakiym bin Hizaam[10] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Adhabu hazitekelezwi Msikitini wala kisasi hakilipwi humo.” [Imetolewa na Ahmad, na Abuu Daawuwd, kupitia Isnaad dhaifu]

 

 

 

203.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ : {أُصِيبَ سَعْدٌ يَوْمَ اَلْخَنْدَقِ، فَضَرَبَ عَلَيْهِ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم خَيْمَةً فِي اَلْمَسْجِدِ، لِيَعُودَهُ مِنْ قَرِيبٍ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Katika siku ya Al-Khandaq (vita vya mahandaki), Sa’d[11] aliumia, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamwekea hema Msikitini ili awe karibu[12] kumzuru.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

204.

وَعَنْهَا قَالَتْ : {رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَسْتُرُنِي، وَأَنَا أَنْظُرُ إِلَى اَلْحَبَشَةِ يَلْعَبُونَ فِي اَلْمَسْجِدِ . . .}  اَلْحَدِيثَ . مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema tena: “Nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akinikinga wakati nikiangalia Wahabeshi[13] waliokuwa wanacheza Msikitini[14].” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

205.

وَعَنْهَا : {أَنَّ وَلِيدَةً سَوْدَاءَ كَانَ لَهَا خِبَاءٌ فِي اَلْمَسْجِدِ ، فَكَانَتْ تَأْتِينِي ، فَتَحَدَّثُ عِنْدِي . . .}  اَلْحَدِيثَ. مُتَّفِقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema tena: “Mjakazi mmoja mweusi alikuwa na hema Msikitini na alikuwa akinijia na kuongea nami[15].” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

206.

 وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلْبُزَاقُ فِي اَلْمَسْجِدِ خَطِيئَةٌ وَكَفَّارَتُهَا دَفْنُهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kutema mate Msikitini ni dhambi, na kafara yake ni kuyazika.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

207.

وَعَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{لَا تَقُومُ اَلسَّاعَةُ حَتَّى يَتَبَاهَى اَلنَّاسُ فِي اَلْمَسَاجِدِ}  أَخْرَجَهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Qiyaamah hakitasimama hadi watu wajifakharishe (kuhusiana na majengo na mapambo ya) Misikitini[16].” [Imetolewa na Al-Khamsah (An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa At-Tirmidhiy, na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

208.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{مَا أُمِرْتُ بِتَشْيِيدِ اَلْمَسَاجِدِ}  أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mimi sikuamrishwa kurefusha na kupamba Misikiti[17].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

209.

وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{عُرِضَتْ عَلَيَّ أُجُورُ أُمَّتِي ، حَتَّى اَلْقَذَاةُ يُخْرِجُهَا اَلرَّجُلُ مِنْ اَلْمَسْجِدِ}  رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَاسْتَغْرَبَهُ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Nilionyeshwa malipo ya Ummah wangu, hadi punje ya vumbi anayoiondoa mtu Msikitini.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, na At-Tirmidhiy aliyeipa daraja la Ghaarib (ngeni), na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

210.

وَعَنْ أَبِي قَتَادَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{إِذَا دَخَلَ أَحَدُكُمْ اَلْمَسْجِدَ فَلَا يَجْلِسْ حَتَّى يُصَلِّيَ رَكْعَتَيْنِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Qataadah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu anapoingia Msikitini, asiketi mpaka aswali Rakaa mbili[18].” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

 

[1] Ili mtu aswali karibu na nyumbani kwake.

 

 

[2] “Kugeuza makaburi kuwa Misikiti” kuna maana mbili. Kwanza, matendo ambayo yanatakiwa kufanywa mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى)    ndani ya Misikiti, yanafanywa karibu au juu ya makaburi kwa mfano kusujudu, kuinama, kukalia mapaja, au kusimama huku mikono imekunjwa kama ishara ya heshima. Pili, kujenga Misikiti karibu na makaburi kwa maana yoyote iwayo, kumekatazwa kabisa.

 

 

 

 

 

[3] Maana yake: kwa muda mfupi Msikiti unaweza kutumika kama mahabusu.

 

[4] Hadiyth hii inaonyesha kuwa mtu asiyekuwa Muislamu anaweza kuingia Msikitini kwa kuwa si msafi kiasili bali kidhahiri; lakini haruhusiwi kuingia ndani ya Ka’bah takatifu na hawezi kuhiji.

 

[5] Hassan huyu ndiye Hassan bin Thaabit Al-Answaar Al-Khazraj, aliyekuwa mshairi wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Abuu ‘Ubayda alisema kuwa: “Waarabu wameafiki kuwa Hassan bin Thaabit alikuwa mshairi mzuri kuliko wote.” Alikufa kabla ya mwaka 40 A.H zama za Ukhalifa wa ‘Aliy. Pia inasemekana kuwa alikufa mnamo mwaka 50 A.H. akiwa na umri wa miaka 120 ambayo miaka 60 ya hiyo alikuwa yumo bado katika ujahili, na miaka 60 alikuwa katika Uislaam.

 

[6] Huu ni ushahidi kuwa maadili mema na ushairi wa juu vyaweza kusomwa ndani ya Msikiti. Hassan bin Thaabit alikuwa akisoma mashairi muhimu kujibu mashairi ya makafiri yanayoudhihaki Uislaam, naye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) daima alikuwa akimsifu Hassan kwa kusema kuwa: “Jibriyl anakusaidia.”

 

[7] Hii ni kuwalaumu wanaosema upuuzi Msikitini. Kwa mfano, itokeapo ng’ombe wamepotea, mwenyewe asiulize ndani ya Msikiti kutoka kwa watu kwa kuwavurugia utulivu wao kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Akitaka, asimame kwenye lango la Msikiti aulize.

 

[8] Inamaanisha Misikiti isitumike kama masoko, kwa sababu itaathiri heshima ya Misikiti.

 

[9] Kufanya biashara Msikitini kumekatazwa. Yoyote anayefanya biashara mle, atahesabika kuwa ni mwenye dhambi, lakini mauziano yatakuwa Halaal.

 

[10] Huyu Hakiym bin Hizaam ndiye Abuu Khaalid Al-Qurashi Al-Asadi, kaka yake Khadiyjah “Mama wa Waumini”. Alikuwa miongoni mwa watu watukufu wa Maquraysh, na alizaliwa ndani ya Ka’bah miaka 13 kabla ya tukio la tembo. Alisilimu mnamo mwaka wa kutekwa Makkah, na alikufa Madiynah mnamo mwaka 54 A.H. akiwa na umri wa miaka 120.

 

[11] Sa’d bin Mu’aadh alikuwa kiongozi wa Al- Aws na mmoja wa Swahaba wakuu. Alisilimu kati ya ‘Aqaba ya kwanza na ya Bukhaariy na Muslim pili, na Banu ‘Abdul-Ashhar wakasilimu kwa athari ya Uislaam. Alikuwa anaheshimiwa na anatiiwa sana na watu wake. Alipigwa mshale katika Vita vya Handaki, na kafariki kwa jeraha lile baada ya Vita vya Banu Quraydha mnamo mwezi wa Dhul-Hijjah mwaka wa 5 A.H

 

[12] Hadiyth hii ni ushahidi kuwa kuweka hema ndani ya Msikiti la mtu mgonjwa au aliyejeruhiwa kukaa mle inaruhusiwa.

 

[13] Yaani mwanamke anaweza kumtazama mwanamume bila niyyah maalumu.

 

[14] Mazoezi yanayosaidia katika vita vya Jihaad yaruhusiwa kufanyiwa Msikitini, na wale Wahabeshi walikuwa wakicheza michezo ya kivita.

 

[15] Hadiyth kamili imesimuliwa katika Swahiyh Al-Bukhaariy. Lengo la kuisimulia hapa ni kufahamisha kuwa mwanamke pia anaweza kukaa Msikitini na kuweka hema Msikitini imeruhusiwa.

 

[16] Inamaanisha kuwa, watu watashindana kifahari, na watajivunia upambaji na uzuri wa Misikiti yao. Pia inaweza kumaanisha kuwa watajivunia uku una umaarufu wao ndani ya Misikiti.

 

[17] Inaonyesha kuwa, kwa kuwa ni desturi ya Kiyahudi, imekatazwa kuchora na kuiremba Misikiti.

 

[18] Hii ni wazi kuwa Rakaa hizi mbili ni za Tahiyyatul-Masjid (maamkizi ya Msikiti). Baadhi ya ‘Ulamaa wanazihesabu hizi ni za lazima, wakati wengine wengi wanazihesabu kuwa ni za hiari. Ukichunguza maana ya Hadiyth utaona kuwa ‘Ulamaa wengine wameiruhusu Swalaah hii iswaliwe hata nyakati za makruwh (zinazokatazwa kuswali), ambapo wengine wanakataza isiswaliwe nyakati hizo.

 

Share

07-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Sifa Ya Swalaah

 

بُلُوغُ الْمَرام

 

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

 

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ صِفَةِ اَلصَّلَاةِ

 

07-Mlango Wa Sifa Ya Swalaah

 

 

211.

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {إِذَا قُمْتُ إِلَى اَلصَّلَاةِ فَأَسْبِغِ اَلْوُضُوءَ ، ثُمَّ اِسْتَقْبِلِ اَلْقِبْلَةَ، فَكَبِّرْ، ثُمَّ اِقْرَأْ مَا تَيَسَّرَ مَعَكَ مِنْ اَلْقُرْآنِ ، ثُمَّ اِرْكَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ رَاكِعًا، ثُمَّ اِرْفَعْ حَتَّى تَعْتَدِلَ قَائِمًا، ثُمَّ اُسْجُدْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ سَاجِدًا، ثُمَّ اِرْفَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ جَالِسًا، ثُمَّ اُسْجُدْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ سَاجِدًا، ثُمَّ اِرْفَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ جَالِسًا، ثُمَّ اُسْجُدْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ سَاجِدًا، ثُمَّ اِفْعَلْ ذَلِكَ فِي صَلَاتِكَ كُلِّهَا}  أَخْرَجَهُ اَلسَّبْعَةُ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ 

وَلِابْنِ مَاجَهْ بِإِسْنَادِ مُسْلِمٍ :{حَتَّى تَطْمَئِنَّ قَائِمًا} 

وَمِثْلُهُ فِي حَدِيثِ رِفَاعَةَ عِنْدَ أَحْمَدَ وَابْنِ حِبَّانَ{حَتَّى تَطْمَئِنَّ قَائِمًا}    

وَفِي لَفْظٍ لِأَحْمَدَ :{فَأَقِمْ صُلْبَكَ حَتَّى تَرْجِعَ اَلْعِظَامُ} 

وَلِلنَّسَائِيِّ ، وَأَبِي دَاوُدَ مِنْ حَدِيثِ رِفَاعَةَ بْنِ رَافِعٍ :{إِنَّهَا لَنْ تَتِمُّ صَلَاةُ أَحَدِكُمْ حَتَّى يُسْبِغَ اَلْوُضُوءَ كَمَا أَمَرَهُ اَللَّهُ، ثُمَّ يُكَبِّرَ اَللَّهَ، وَيَحْمَدَهُ ، وَيُثْنِيَ عَلَيْهِ} 

وَفِيهَا {فَإِنْ كَانَ مَعَكَ قُرْآنٌ فَاقْرَأْ وَإِلَّا فَاحْمَدِ اَللَّهَ ، وَكَبِّرْهُ ، وهلِّلْهُ}

وَلِأَبِي دَاوُدَ :{ثُمَّ اِقْرَأْ بِأُمِّ اَلْقُرْآنِ وَبِمَا شَاءَ اَللَّهُ}  

وَلِابْنِ حِبَّانَ :{ثُمَّ بِمَا شِئْتَ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ukisimama kuswali, tawadha vizuri na kikamilifu, kisha elekea Qiblah, na piga takbiyra kisha soma unachoweza katika Qur-aan[1], kisha rukuu hadi utulie ukiwa katika rakaa, kisha inuka na usimame wima, kisha sujudu hadi utulie ukiwa katika sajdah, kisha inuka na utulie ukiwa umeketi[2], kisha sujudu tena na utulie katika sajdah, kisha ufanye vivyo hivyo katika Swalaah yako yote.” [Imetolewa na As-Sab’ah (Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

Pia ni tamshi la Ibn Maajah kwa Isnaad ya Muslim: “Mpaka utulie ukiwa umesimama wima.”

Hadiyth ya Rifaa’ah[3] iliyoko kwa Ahmad na Ibn Hibbaan: “Mpaka utulie hali ya kuwa umesimama.”

 

Naye Ahmad amesema: “Unyooshe mgongo wako hadi mifupa irejee nafasi zake.”

 

Nao An-Nasaaiy na Abuu Daawuwd wamepokea Hadiyth ya Rifaa’ah bin Raafi’ inasema: “Swalaah ya mmoja wenu haitatimia hadi atawadhe sawasawa kama Allaah Alivyoamrisha, kisha apige takbiyra na amhimidi na kumsifu Yeye.”

 

Pia inatajwa katika Hadiyth hiyo kuwa: “Ukiwa unajua sehemu yoyote ya Qur-aan, isome, vinginevyo mhimidi Allaah (AlhamduliLLaah), mpigie takbiyra (Allaahu Akbar) na mpwekeshe kwa tahliyl (laa ilaaha illa-Allaah).”

 

Na Abuu Daawuwd amesema: “Kisha soma Ummul-Qur-aan[4] (Suwrah Al-Faatihah) na kisha kila Atakacho Allaah.”

 

Na Ibn Hibbaan akasema: “na (usome) chochote unachotaka”

 

 

 

212.

وَعَنْ أَبِي حُمَيْدٍ اَلسَّاعِدِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {رَأَيْتُ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم إِذَا كَبَّرَ جَعَلَ يَدَيْهِ حَذْوَ مَنْكِبَيْهِ ، وَإِذَا رَكَعَ أَمْكَنَ يَدَيْهِ مِنْ رُكْبَتَيْهِ ، ثُمَّ هَصَرَ ظَهْرِهِ ، فَإِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ اِسْتَوَى حَتَّى يَعُودَ كُلُّ فَقَارٍ مَكَانَهُ ، فَإِذَا سَجَدَ وَضَعَ يَدَيْهِ غَيْرَ مُفْتَرِشٍ وَلَا قَابِضِهِمَا ، وَاسْتَقْبَلَ بِأَطْرَافِ أَصَابِعِ رِجْلَيْهِ اَلْقِبْلَةَ ، وَإِذَا جَلَسَ فِي اَلرَّكْعَتَيْنِ جَلَسَ عَلَى رِجْلِهِ اَلْيُسْرَى وَنَصَبَ اَلْيُمْنَى ، وَإِذَا جَلَسَ فِي اَلرَّكْعَةِ اَلْأَخِيرَةِ قَدَّمَ رِجْلَهُ اَلْيُسْرَى وَنَصَبَ اَلْأُخْرَى ، وَقَعَدَ عَلَى مَقْعَدَتِهِ}  أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ 

Kutoka kwa Abuu Humayd As-Saa’idiyy[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimemuona Nabiy[6] (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akipiga Takbiyra aliweka mikono yake sambamba na mabega yake[7], na aliporukuu aliweka mikono yake kwenye magoti, na alikunja mgongo wake, alipoinuka alisimama wima hadi mifupa ya uti wa mgongo ikarejea mahali pake, aliposujudu, aliiweka mikono yake bila kuisambaza wala kuifumba; na ncha za vidole vyake vya miguu vikawa vinaelekea Qiblah, alipoketi katika rakaa mbili, alikalia mguu wake wa kushoto na kusimamisha wa kuume, na alipoketi katika rakaa ya mwisho alitanguliza mbele mguu wake wa kushoto na akasimamisha wa kuume na akakalia makalio yake.“ [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

213.

وَعَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  أَنَّهُ كَانَ إِذَا قَامَ إِلَى اَلصَّلَاةِ قَالَ : "وَجَّهْتُ وَجْهِي لِلَّذِي فَطَّرَ اَلسَّمَوَاتِ " . . . إِلَى قَوْلِهِ : "مِنْ اَلْمُسْلِمِينَ ، اَللَّهُمَّ أَنْتَ اَلْمَلِكُ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ ، أَنْتَ رَبِّي وَأَنَا عَبْدُكَ . . .}  إِلَى آخِرِهِ . رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

وَفِي رِوَايَةٍ لَهُ : أَنَّ ذَلِكَ فِي صَلَاةِ اَللَّيْلِ

Kutoka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akisimama kuswali, alikuwa akisema[8]: “Wajjahtu wajhiya li-LLadhiy fatwaras-samaawaati…” mpaka: “minal muslimiyna. Allaahumma Antal-Maliku laa ilaaha illaa Anta, Anta Rabbiy wa anaa ‘abduka” mpaka mwisho wake. (Nimeelekeza uso wangu kwa Aliyeumba mbingu na ardhi”, hadi kauli yake: “miongoni mwa Waislamu. Ee Allaah, Wewe Ndiye Mfalme, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, Wewe ni Rabb wangu na mimi ni mja wako[9]).” [Imetolewa na Muslim]

 

Na katika mapokezi yake (Muslim) mengine: “Hayo ni katika Swalaah ya usiku.”

 

 

 

214.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا كَبَّرَ لِلصَّلَاةِ سَكَتَ هُنَيَّةً ، قَبْلِ أَنْ يَقْرَأَ ، فَسَأَلْتُهُ ، فَقَالَ : "أَقُولُ : اَللَّهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ اَلْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ، اَللَّهُمَّ نقِّنِي مِنْ خَطَايَايَ كَمَا يُنَقَّى اَلثَّوْبُ اَلْأَبْيَضُ مِنْ اَلدَّنَسِ ، اَللَّهُمَّ اِغْسِلْنِي مِنْ خَطَايَايَ بِالْمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akishasoma Takbiyra ya Swalaah alinyamaza kidogo kabla ya kusoma Qur-aan. Nikamuuliza juu ya hilo, akasema: Nasema:

 

 “Allaahumma baa’id bayniy wa bayna khatwaayaaya kamaa baa’adta baynal-Mashriqi wal-Maghrib. Allaahumma naqqiniy min khatwaayaaya kamaa yunaqqath-thawbul abyadhwu minad-danasi. Allaahumma-ghsiliniy min khatwaayaaya bil-maai wath-thalji wal-barad.”

 

(Ee Allaah niweke mbali na makosa yangu kama Ulivyoweka mbali baina ya Mashariki na Magharibi, Ee Allaah nisafishe makosa yangu kama vile inavyosafishwa nguo nyeupe kutokana na uchafu, Ee Allaah nisafishe makosa yangu kwa maji na theluji na  barafu). [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

215.

وَعَنْ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ : {سُبْحَانَكَ اَللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ ، تَبَارَكَ اِسْمُكَ ، وَتَعَالَى جَدُّكَ ، وَلَا إِلَه غَيْرُكَ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ بِسَنَدٍ مُنْقَطِعٍ ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ مَوْصُولاً وَهُوَ مَوْقُوفٌ 

وَنَحْوُهُ عَنْ أَبِي سَعِيدٍ مَرْفُوعًا عِنْدَ اَلْخَمْسَةِ 

وَفِيهِ : وَكَانَ يَقُولُ بَعْدَ اَلتَّكْبِيرِ : {أَعُوذُ بِاَللَّهِ اَلسَّمِيعِ اَلْعَلِيمِ مِنَ اَلشَّيْطَانِ اَلرَّجِيمِ ، مِنْ هَمْزِهِ ، وَنَفْخِهِ ، وَنَفْثِهِ }

Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisema:

 

”Subhaanaka-LLaahumma wabihamdika wa Tabaarakas-Smuka wa Ta’aalaa Jadduka walaa ilaaha Ghayruka.”

 

(Utakasifu ni Wako Ee Allaah, na Himdi ni Zako, na Limebarikika Jina Lako, na Utukufu Wako uko juu, na hapana mwabudiwa wa haki ghairi Yako)   [Imetolewa na Muslim kwa Isnaad iliyo Munqatwi’ (iliyokatika). Na katika Riwaayah ya Ad-Daaraqutwniy ina Isnaad Mawsuwl na Mawquwf]

 

Hadiyth kama hiyo ameisimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy ambayo ni Marfuw’ kwa Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) imesema: “(Nabiy) alikuwa akisema baada ya Takbiyra:

 

”‘Auwdhu biLLaahis-Samiy’il ‘Aliymi mina-sh-shaytwaanir-rajiym min hamzihi wa nafkhihi, wa nafthihi.”

(Najilindia na Allaah kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa na kulaaniwa, najilinda na kutokana na wazimu wake au ushauri wake muovu, na upulizaji wake, na kutabana kwake au uchawi wake).

 

 

 

216.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ :{كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَسْتَفْتِحُ اَلصَّلَاةَ بِالتَّكْبِيرِ ، وَالْقِرَاءَةَ : بِـ (اَلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ اَلْعَالَمِينَ ) وَكَانَ إِذَا رَكَعَ لَمْ يُشْخِصْ رَأْسَهُ ، وَلَمْ يُصَوِّبْهُ ، وَلَكِنْ بَيْنَ ذَلِكَ . وَكَانَ إِذَا رَفَعَ مِنْ اَلرُّكُوعِ لَمْ يَسْجُدْ حَتَّى يَسْتَوِيَ قَائِمًا . وَإِذَا رَفَعَ مِنْ اَلسُّجُودِ لَمْ يَسْجُدْ حَتَّى يَسْتَوِيَ جَالِسًا . وَكَانَ يَقُولُ فِي كُلِّ رَكْعَتَيْنِ اَلتَّحِيَّةَ . وَكَانَ يَفْرِشُ رِجْلَهُ اَلْيُسْرَى وَيَنْصِبُ اَلْيُمْنَى . وَكَانَ يَنْهَى عَنْ عُقْبَةِ اَلشَّيْطَانِ ، وَيَنْهَى أَنْ يَفْتَرِشَ اَلرَّجُلُ زِرَاعَيْهِ اِفْتِرَاشَ اَلسَّبُعِ . وَكَانَ يُخْتَمُ اَلصَّلَاةَ بِالتَّسْلِيمِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ ، وَلَهُ عِلَّةٌ 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akianza Swalaah kwa Takbiyra na kusoma:

 

AlhamduliLlaahi Rabbil ‘Aalamiyn[10]

 

Na aliporukuuu, hakuinua kichwa chake wala hakiinamishi, bali alikiweka baina ya sehemu hizi mbili. Alipoinua kichwa chake kutoka katika kurukuu, hakusujudu hadi aliposimama wima, na alipoinua kichwa chake baada ya kusujudu, hakurudia kusujudu mpaka alipoinuka na kuketi kitako, alikuwa akisoma katika Rakaa mbili At-Tahiyyah. Na alikuwa akitandika mguu wake wa kushoto na kuusimamisha wima wa kuume; na alikuwa alikataza mkao wa shaytwaan wa kukalia[11] makalio, na akakataza watu kutandika mikono yao kama wanyama, na alikuwa akikhitimisha Swalaah kwa tasliym (Assalaamu ‘alaykum).” [Imetolewa na Muslim, na ina dosari]

 

 

 

217.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَرْفَعُ يَدَيْهِ حَذْوَ مَنْكِبَيْهِ إِذَا اِفْتَتَحَ اَلصَّلَاةَ، وَإِذَا كَبَّرَ لِلرُّكُوعِ، وَإِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنْ اَلرُّكُوعِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

 

 وَفِي حَدِيثِ أَبِي حُمَيْدٍ، عِنْدَ أَبِي دَاوُدَ: {يَرْفَعُ يَدَيْهِ حَتَّى يُحَاذِيَ بِهِمَا مَنْكِبَيْهِ، ثُمَّ يُكَبِّرَ}

وَلِمُسْلِمٍ عَنْ مَالِكِ بْنِ الْحُوَيْرِثِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ نَحْوُ حَدِيثِ اِبْنِ عُمَرَ ، وَلَكِنْ قَالَ : {حَتَّى يُحَاذِيَ بِهِمَا فُرُوعَ أُذُنَيْهِ}  

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akinyanyua mikono yake usawa wa mabega[12] yake, anapoanza Swalaah, na anapopiga Takbiyra kwa ajili ya kurukuu, na aliponyanya kichwa chake baada ya kurukuu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Hadiyth aliyopokea Abuu Daawuwd kutoka kwa Abuu Humayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “(Nabiy) alikuwa akinyanyua mikono yake na kuiweka sambamba na mabega yake, kisha anapiga takbiyra.”

 

Katika Hadiyth ya Muslim iliyosimuliwa na Maalik bin Al-Huwayrith (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) ni sawa sawa kama Hadiyth iliyosimuliwa na Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) lakini yeye (Maalik bin Al-Huwayrith) alitaja kuwa: “Nabiy alikuwa akinyanyua mikono yake sambamba na mwisho wa masikio yake.”

 

 

 

218.

وَعَنْ وَائِلِ بْنِ حُجْرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {صَلَّيْتُ مَعَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَوَضَعَ يَدَهُ اَلْيُمْنَى عَلَى يَدِهِ اَلْيُسْرَى عَلَى صَدْرِهِ}  أَخْرَجَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ 

Kutoka kwa Waail bin Hujr[13] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mimi niliswali na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) naye aliweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto, na kisha akaiweka juu ya kifua[14] chake.” [Imetolewa na Ibn Khuzaymah]

 

 

 

219.

وَعَنْ عُبَادَةَ بْنِ اَلصَّامِتِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  لَا صَلَاةَ لِمَنْ لَمْ يَقْرَأْ بِأُمِّ اَلْقُرْآنِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَفِي رِوَايَةٍ ، لِابْنِ حِبَّانَ وَاَلدَّارَقُطْنِيِّ :{لَا تَجْزِي صَلَاةٌ لَا يُقْرَأُ فِيهَا بِفَاتِحَةِ اَلْكِتَابِ}  

وَفِي أُخْرَى ، لِأَحْمَدَ وَأَبِي دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيِّ ، وَابْنِ حِبَّانَ:{لَعَلَّكُمْ تَقْرَءُونَ خَلْفَ إِمَامِكُمْ  ؟ " قُلْنَا : نِعْمَ . قَالَ : "لَا تَفْعَلُوا إِلَّا بِفَاتِحَةِ اَلْكِتَابِ ، فَإِنَّهُ لَا صَلَاةِ لِمَنْ لَمْ يَقْرَأْ بِهَا} 

Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit[15] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna Swalaah kwa mtu asiyesoma Ummul-Qur-aan (Suwrah Al-Faatihah)[16].” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na katika Riwaayah ya Ibn Hibbaan na Ad-Daaraqutwniy: “Haijuzu Swalaah isiyosomwa ndani yake Suwrah Al-Faatihah.”

 

Na Riwaayah nyingine ya Ahmad, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan: “Huenda mnasoma nyuma ya Imaam wenu? Tukasema: “Ndiyo.” Akasema: “Msifanye hivyo, isipokuwa kwa Suwrah Al-Faatihah kwani hana Swalaah asiyeisoma.”

 

 

 

220.

 وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم وَأَبَا بَكْرٍ وَعُمَرَ كَانُوا يَفْتَتِحُونَ اَلصَّلَاةِ بِـ (اَلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ اَلْعَالَمِينَ)} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

زَادَ مُسْلِمٌ: {لَا يَذْكُرُونَ : (بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ ) فِي أَوَّلِ قِرَاءَةٍ وَلَا فِي آخِرِهَا}

وَفِي رِوَايَةٍ لِأَحْمَدَ ، وَالنَّسَائِيِّ وَابْنِ خُزَيْمَةَ :{لَا يَجْهَرُونَ ‏بِبِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ}  

وَفِي أُخْرَى لِابْنِ خُزَيْمَةَ :{كَانُوا يُسِرُّونَ}

وَعَلَى هَذَا يُحْمَلُ اَلنَّفْيُ فِي رِوَايَةِ مُسْلِمٍ ، خِلَافًا لِمَنْ أَعَلَّهَا

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Abuu Bakr na ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) walikuwa wakianza Swalaah kwa: “AlhamduliLLaahi Rabbil ‘Aalamiyn.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na Muslim aliongezea: “Walikuwa hawasomi “BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym” mwanzoni, wala mwishoni wake.[17]

 

Na katika Riwaayah ya Ahmad, An-Nasaaiy na Ibn Khuzaymah: “Hawadhihirishi BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym kwa sauti.”

 

Na katika Riwaayah ya Ibn Khuzaymah: “Walikuwa wanasoma (BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym)[18]

 

Na juu ya hili katika Riwaayah ya Muslim, tofauti na wenye kuitia dosari.

 

 

 

221.

 نُعَيْمٍ اَلْمُجَمِّرِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {صَلَّيْتُ وَرَاءَ أَبِي هُرَيْرَةَ فَقَرَأَ : (بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ) . ثُمَّ قَرَأَ بِأُمِّ اَلْقُرْآنِ ، حَتَّى إِذَا بَلَغَ : (وَلَا اَلضَّالِّينَ) ، قَالَ : "آمِينَ" وَيَقُولُ  كُلَّمَا سَجَدَ ، وَإِذَا قَامَ مِنْ اَلْجُلُوسِ : اَللَّهُ أَكْبَرُ . ثُمَّ يَقُولُ إِذَا سَلَّمَ : وَاَلَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنِّي لَأَشْبَهُكُمْ صَلَاةً بِرَسُولِ اَللَّهِ}  رَوَاهُ النَّسَائِيُّ وَابْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa Nu’aym Al-Mujammir[19] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Niliswali nyuma ya Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alisoma: “BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym”, kisha Ummul-Qur-aan (Al-Faatihah), alipofika: “Waladhw-dhwaalliyna” alisema: “Aamiyn.”[20] Akawa anasema: “Allaahu Akbar” kila aliposujudu na alipoinuka na kusimama kutoka katika Sijdah, na alipotoa salaam yaani kusema: “Assalaam ‘alaykum” alisema: “Ninaapa kwa Ambaye roho yangu iko Mkononi Mwake, Swalaah yangu inafanana sana na ile ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuliko yeyote miongoni mwenu.” [Imetolewa na An-Nasaaiy na Ibn Khuzaymah]

 

 

 

222.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  إِذَا قَرَأْتُمْ اَلْفَاتِحَةِ فَاقْرَءُوا : ( بِسْمِ اَللَّهِ اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ ) ، فَإِنَّهَا إِحْدَى آيَاتِهَا}  رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ ، وَصَوَّبَ وَقْفَهُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mnaposoma Suwrah Al-Faatihah someni “BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym”, kwani hiyo ni moja ya Aayah zake.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy, aliyeipa daraja la Mawquwf]

 

 

 

223.

 وَعَنْهُ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا فَرَغَ مِنْ قِرَاءَةِ أُمِّ اَلْقُرْآنِ رَفَعَ صَوْتَهُ وَقَالَ: "آمِينَ".}  رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ وَحَسَّنَهُ ، وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ

ـ وَلِأَبِي دَاوُدَ وَاَلتِّرْمِذِيِّ مِنْ حَدِيثِ وَائِلِ بْنِ حُجْرٍ نَحْوُهُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipomaliza kusoma Ummul-Qur-aan alipaza sauti yake na kusema “Aaamiyn.”[21] [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy, aliyeipa daraja la Hasan, na akaisahihisha Al-Haakim]

 

Na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy wamepokea masimulizi ya Waail bin Hujri mfano wake.

 

 

 

224.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ أَبِي أَوْفَى رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : {جَاءَ رَجُلٌ إِلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : إِنِّي لَا أَسْتَطِيعُ أَنْ آخُذَ مِنْ اَلْقُرْآنِ شَيْئًا ، فَعَلِّمْنِي مَا يُجْزِئُنِيٌ مِنْهُ . قَالَ : "سُبْحَانَ اَللَّهِ ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَاَللَّهُ أَكْبَرُ ، وَلَا حَوْلٌ وَلَا قُوَّةً إِلَّا بِاَللَّهِ اَلْعَلِيِّ اَلْعَظِيمِ . . .}  اَلْحَدِيثَ . رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَأَبُو دَاوُدَ ، وَالنَّسَائِيُّ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَالْحَاكِمُ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Abiy Awfaa[22] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Mtu mmoja alikuja kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Mimi siwezi kuhifadhi chochote katika Qur-aan, kwa hivyo nifundishe kitakachonitosha humo, akasema: Sema:

 

 “Subhaana-Allaah, (Utakasifu ni wa Allaah), “Wal-Hamdu liLLaah (Himdi ni za Allaah) wa laa ilaaha illa Allaah (na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah) wa-Allaahu Akbar (na Allaah   ni Mkubwa Zaidi), wa laa hawla wa laa quwwata illa biLLaahil-‘Aliyyil-‘Adhwiym (na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Allaah Aliyetukuka Aliye ‘Adhimu).[23][Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan, Ad-Daaraqutwniy na Al-Haakim]

 

 

 

225.

وَعَنْ أَبِي قَتَادَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي بِنَا ، فَيَقْرَأُ فِي اَلظُّهْرِ وَالْعَصْرِ  فِي اَلرَّكْعَتَيْنِ اَلْأُولَيَيْنِ  بِفَاتِحَةِ اَلْكِتَابِ وَسُورَتَيْنِ ، وَيُسْمِعُنَا اَلْآيَةَ أَحْيَانًا ، وَيُطَوِّلُ اَلرَّكْعَةَ اَلْأُولَى ، وَيَقْرَأُ فِي اَلْأُخْرَيَيْنِ بِفَاتِحَةِ اَلْكِتَابِ.}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Qataadah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akituswalisha anasoma katika Swalaah ya Adhuhuri na Alasiri, Suwrah Al-Faatihah katika Rakaa mbili za mwanzo, pamoja na Suwrah zingine mbili, na mara nyingine alitusikilizisha Aayah[24], alikuwa akiirefusha Rakaa ya mwanzo, na alikuwa akisoma Suwrah Al-Faatihah tu katika Rakaa mbili za mwisho.[25] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

226.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {كُنَّا نَحْزُرُ قِيَامَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي اَلظُّهْرِ وَالْعَصْرِ ، فَحَزَرْنَا قِيَامَهُ فِي اَلرَّكْعَتَيْنِ اَلْأُولَيَيْنِ مِنْ اَلظُّهْرِ قَدْرَ : (الم تَنْزِيلُ) اَلسَّجْدَةِ . وَفِي اَلْأُخْرَيَيْنِ قَدْرَ اَلنِّصْفِ مِنْ ذَلِكَ . وَفِي اَلْأُولَيَيْنِ مِنْ اَلْعَصْرِ عَلَى قَدْرِ اَلْأُخْرَيَيْنِ مِنْ اَلظُّهْرِ ، وَالْأُخْرَيَيْنِ عَلَى اَلنِّصْفِ مِنْ ذَلِكَ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulikuwa tukikisia urefu wa kisimamo cha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika Swalaah za Adhuhuri na Alasiri na tukapata ni kadiri ya kusoma Suwrah ya “Alif Laam Miym Tanziyl” (Suwrah As-Sajdah)[26], na katika Rakaa za mwisho mbili kadiri ya nusu ya hivyo, na katika Rakaa mbili za mwanzo za Swalaah ya Alasiri, alikuwa akisimama kwa muda kadiri ya Rakaa mbili za Swalaah ya Adhuhuri, na Rakaa mbili za mwisho kadiri ya nusu ya urefu wa Rakaa mbili za mwanzo.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

227.

وَعَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {كَانَ فُلَانٍ يُطِيلُ اَلْأُولَيَيْنِ مِنْ اَلظُّهْرِ، وَيُخَفِّفُ اَلْعَصْرَ، وَيَقْرَأُ فِي اَلْمَغْرِبِ بِقِصَارِ اَلْمُفَصَّلِ وَفِي اَلْعِشَاءِ بِوَسَطِهِ وَفِي اَلصُّبْحِ بِطُولِهِ . فَقَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ: "مَا صَلَّيْتُ وَرَاءِ أَحَدٍ أَشْبَهَ صَلَاةِ بِرَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنْ هَذَا} أَخْرَجَهُ النَّسَائِيُّ بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ

Kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar[27] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Fulani alikuwa akirefusha Rakaa mbili za mwanzo za Swalaah ya Adhuhuri, na akifupisha Alasiri na akisoma Suwrah fupi ya Mufasw-swal[28] wakati wa Swalaah ya Magharibi, na Suwrah za wastani kwa Swalaah ya ‘Ishaa, na Suwrah ndefu wakati wa Alfajiri.” Kisha Abuu Hurayrah akasema: “Sijaswali nyuma ya yeyote ambaye Swalaah yake inafanana zaidi na Swalaah ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuliko huyu.” [Imetolewa na An-Nasaaiy kwa Isnaad Swahiyh]

 

 

 

228.

 وَعَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: {سَمِعْتَ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي اَلْمَغْرِبِ بِالطُّورِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Jubayr bin Mutw’im (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisoma Suwrah “Atw-Twuwr” katika Swalaah ya Magharibi.[29][Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

229.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ فِي صَلَاةِ اَلْفَجْرِ يَوْمَ اَلْجُمْعَةِ : (الم تَنْزِيلُ ) اَلسَّجْدَةَ ، و (هَلْ أَتَى عَلَى اَلْإِنْسَانِ)}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَلِلطَّبَرَانِيِّ مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ مَسْعُودٍ :{يُدِيمُ ذَلِكَ} 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisoma katika Swalaah ya Alfajiri siku ya Ijumaa “Alif-Laam-Miym Tanziyl...” (As-Sajdah) na “Hal ataa ‘alal Insaani” (ambayo pia huitwa Suwrah Ad-Dahr)?[30][Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Riwaayah ya Atw-Twabaraaniyy imepokea Hadiyth ya Ibn Mas-‘uwd ikiwa na nyongeza kuwa: “Rasuli akidumisha hivyo.[31]

 

 

 

230.

وَعَنْ حُذَيْفَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {صَلَّيْتُ مَعَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَمَا مَرَّتْ بِهِ آيَةُ رَحْمَةٍ إِلَّا وَقَفَ عِنْدَهَا يَسْأَلُ، وَلَا آيَةُ عَذَابٍ إِلَّا تَعَوَّذَ مِنْهَا}  أَخْرَجَهُ اَلْخَمْسَةُ ، وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ 

Kutoka kwa Hudhayfah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimeswali pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na hakuipita Aayah ya Rahmah ila alisimama hapo na kuomba (Rahmah), wala Aayah ya adhabu ila aliomba kinga nayo (adhabu hiyo).” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaipa daraja la Hasan At-Tirmidhiy]

 

 

 

231.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  أَلَا وَإِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَقْرَأَ اَلْقُرْآنَ رَاكِعًا أَوْ سَاجِدًا ، فَأَمَّا اَلرُّكُوعُ فَعَظِّمُوا فِيهِ اَلرَّبَّ ، وَأَمَّا اَلسُّجُودُ فَاجْتَهِدُوا فِي اَلدُّعَاءِ ، فَقَمِنٌ أَنْ يُسْتَجَابَ لَكُمْ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Jueni nimekatazwa kusoma Qur-aan[32] nikiwa nimerukuu au nimesujudu, ama katika kurukuu Muadhimisheni humo Rabb, na wakati wa kusujudu jitahidini kuomba du’aa, kwani hakika mtajibiwa.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

232.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: فِي رُكُوعِهِ وَسُجُودِهِ : "سُبْحَانَكَ اَللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ ، اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anasema wakati wa kurukuu na kusujudu:

 

Subhaanaka-Allaahumma Rabbanaa wa bi-Hamdika, Allaahummagh-firliy

 

(Kutakasika ni Kwako, ee Allaah, Rabb wetu, na kuhimidiwa ni Kwako, ee Allaah nighufirie).” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

233.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا قَامَ إِلَى اَلصَّلَاةِ يُكَبِّرُ حِينَ يَقُومُ ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْكَعُ ، ثُمَّ يَقُولُ : "سَمِعَ اَللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ" حِينَ يَرْفَعُ صُلْبَهُ مِنْ اَلرُّكُوعِ ، ثُمَّ يَقُولُ وَهُوَ قَائِمٌ : "رَبَّنَا وَلَكَ اَلْحَمْدُ" ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَهْوِي سَاجِدًا ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْفَعُ رَأْسَهُ، ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَسْجُدُ  ثُمَّ يُكَبِّرُ حِينَ يَرْفَعُ ، ثُمَّ يَفْعَلُ ذَلِكَ فِي اَلصَّلَاةِ كُلِّهَا ، وَيُكَبِّرُ حِينَ يَقُومُ مِنْ اِثْنَتَيْنِ بَعْدَ اَلْجُلُوسِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) anaposimama kuswali, alikuwa anapiga Takbiyra[33] ilhali amesimama wima, kisha anatamka Takbiyra wakati akirukuu, kisha anasema:

 “Sami’a-Allaahu liman Hamidah.

(Allaah Amemsikia mwenye kumhimidi).

 

Wakati anainua mgongo wake kutoka katika rukuu akishasimama wima (I’tidaal) anasema:

Rabbanaa wa-Lakal Hamd.

(Rabb wetu kuhimidiwa ni kwako).

 

Kisha anapiga Takbiyra anapoinama kwa ajili ya kusujudu, kisha anapiga takbiyra anapoinua kichwa, kisha anapiga takbiyra anaposujudu mara ya pili, kisha anapiga takbiyra anapoinua kichwa mara nyingine. Na alifanya hivyo hivyo katika Swalaah yote. Na alipiga takbiyra aliposimama toka katika kikao, baada ya Rakaa mbili.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

234.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ :{كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنْ اَلرُّكُوعِ قَالَ : " اَللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ اَلْحَمْدُ مِلْءَ اَلسَّمَوَاتِ وَمِلْءَ اَلْأَرْضِ ، وَمِلْءَ مَا شِئْتَ مِنْ شَيْءٍ بَعْدُ ، أَهْلَ اَلثَّنَاءِ وَالْمَجْدِ ، أَحَقُّ مَا قَالَ اَلْعَبْدُ  وَكُلُّنَا لَكَ عَبْدٌ  اَللَّهُمَّ لَا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ ، وَلَا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ ، وَلَا يَنْفَعُ ذَا اَلْجَدِّ مِنْكَ اَلْجَدُّ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anapoinua kichwa chake baada ya rukuu alikuwa anasema:

 

Allaahumma Rabbanaa Lakal-Hamd, mil-as-samawaati wal-ardhwi, wa mil-a maa Shii-ta min shay-in ba’du, ahlath-thanaai wal-Majdi, ahaqqu maa qaalal-‘abdu, wa kullunaa Laka ‘abdu, Allaahumma laa maani’a limaa A’twayta, wa laa mu’twiya limaa Mana’ta, wa laa yanfa’u dhal-jaddi Minkal-jaddu.

 

(Ee Allaah! Rabb wetu, Himdi ni Zako, ujazo wa mbingu na ardhi, na ujazo wa chochote Ulichotaka (kuumba) baadaye. Ee Mwenye Sifa na Utukufu, Mwenye kustahiki kuliko vyote kwa kila alilolisema mja Wako, Ee Allaah hakuna mwenye kuzuia Ulichotoa, au kutoa Ulichozuia, wala mali[34] haziwezi kumnufaisha tajiri Kwako).[35] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

235.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {أُمِرْتُ أَنْ أَسْجُدَ عَلَى سَبْعَةِ أَعْظُمٍ : عَلَى اَلْجَبْهَةِ  وَأَشَارَ بِيَدِهِ إِلَى أَنْفِهِ  وَالْيَدَيْنِ ، وَالرُّكْبَتَيْنِ ، وَأَطْرَافِ اَلْقَدَمَيْنِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Nimeamrishwa kusujudu juu ya mifupa saba: paji la uso, akaashiria kwa mikono yake miwili juu ya pua yake[36], magoti mawili na vidole vya miguu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

236.

وَعَنْ اِبْنِ بُحَيْنَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم {كَانَ إِذَا صَلَّى فَرَّجَ بَيْنَ يَدَيْهِ ، حَتَّى يَبْدُوَ بَيَاضُ إِبِطَيْهِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn Buhaynah[37] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisujudu anaposwali, hupanua mikono yake hadi weupe wa kwapa zake ukaonekana.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

237.

وَعَنْ اَلْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا سَجَدْتَ فَضَعْ كَفَّيْكَ ، وَارْفَعْ مِرْفَقَيْكَ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Al-Baraai bin ‘Aazib[38] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Unaposujudu, weka viganja vya mikono yako juu ya ardhi na unyanyue viwiko vyako.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

238.

وَعَنْ وَائِلِ بْنِ حُجْرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم {كَانَ إِذَا رَكَعَ فَرَّجَ بَيْنَ أَصَابِعِهِ، وَإِذَا سَجَدَ ضَمَّ أَصَابِعَهُ}  رَوَاهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa Waail bin Hujr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alipokuwa akirukuu anapanua vidole vyake, anaposujudu alivikusanya.” [Imetolewa na Al-Haakim]

 

 

 

239.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ : {رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي مُتَرَبِّعًا}  رَوَاهُ النَّسَائِيُّ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiswali akiwa amekaa huku kakunja miguu.[39] [Imetolewa na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

240.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقُولُ بَيْنَ اَلسَّجْدَتَيْنِ : {اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي ، وَارْحَمْنِي ، وَاهْدِنِي، وَعَافِنِي، وَارْزُقْنِي} رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ إِلَّا النَّسَائِيُّ ، وَاللَّفْظُ لِأَبِي دَاوُدَ ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anasoma baina ya Sijda mbili:

 

“Allaahummagh-fir-liy Warhamniy, Wahdiniy, Wa’aafiniy, Warzuqniy.”

 

(Ee Allaah! Nighufirie, Nirehemu, Nihidi, Nijaalie ‘Aafiyah (siha, amani nk.) na Niruzuku).” [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa An-Nasaaiy, na tamshi hili ni la Abuu Daawuwd, na aliisahihisha Al-Haakim

 

 

 

241.

وَعَنْ مَالِكِ بْنِ الْحُوَيْرِثِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّهُ {رَأَى اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي ، فَإِذَا كَانَ فِي وِتْرٍ مِنْ صَلَاتِهِ لَمْ يَنْهَضْ حَتَّى يَسْتَوِيَ قَاعِدًا}  رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Maalik bin Al-Huwayrith (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Alimuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiswali, na alipokuwa katika Rakaa za Swalaah ya Witr, hakusimama wima hadi alipokaa chini sawasawa.”[40] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

242.

وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{ قَنَتَ شَهْرًا بَعْدَ اَلرُّكُوعِ ، يَدْعُو عَلَى أَحْيَاءٍ مِنْ أَحْيَاءِ اَلْعَرَبِ ، ثُمَّ تَرَكَهُ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَلِأَحْمَدَ وَاَلدَّارَقُطْنِيِّ نَحْوُهُ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ ، وَزَادَ :{فَأَمَّا فِي اَلصُّبْحِ فَلَمْ يَزَلْ يَقْنُتُ حَتَّى فَارَقَ اَلدُّنْيَا}

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisoma Qunuwt mwezi mmoja, baada ya kurukuu, akilaani makabila fulani ya Waarabu[41], kisha akaiacha.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Katika Riwaayah ya Ahmad na Ad-Daaraqutwniyy kuna Hadiyth kama hiyo kwa njia nyingine, na kuna ziada hii: “Ama katika Alfajiri aliendelea kusoma Qunuwt mpaka alipoaga dunia.”

 

 

 

243.

وَعَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم{ كَانَ لَا يَقْنُتُ إِلَّا إِذَا دَعَا لِقَوْمٍ ، أَوْ دَعَا عَلَى قَوْمٍ} صَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakutekeleza Qunuwt isipokuwa alipokuwa akiomba du’aa dhidi ya watu[42] baada ya kuinuka kutoka katika rukuu isipokuwa alipowaombea watu, au kuwalaani watu.” [Aliisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

244.

وَعَنْ سَعْدِ بْنِ طَارِقِ الْأَشْجَعِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ :{قُلْتُ لِأَبِي : يَا أَبَتِ ! إِنَّكَ قَدْ صَلَّيْتُ خَلْفَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَأَبِي بَكْرٍ ، وَعُمَرُ ، وَعُثْمَانُ ، وَعَلَيَّ ، أَفَكَانُوا يَقْنُتُونَ فِي اَلْفَجْرِ  ؟ قَالَ : أَيْ بُنَيَّ ، مُحْدَثٌ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ ، إِلَّا أَبَا دَاوُدَ

Kutoka kwa Sa’d[43] bin Twaariq[44] Al-Ashja’iyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nilimuuliza baba yangu: Ee baba yangu! Wewe umeswali nyuma ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Abuu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan na ‘Aliy, Je walikuwa wakifanya Qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri? Akasema: Ee mwanangu! Huo ni uzushi.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa Abuu Daawuwd]

 

 

 

245.

وَعَنْ اَلْحَسَنِ بْنِ عَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا ; قَالَ :{عَلَّمَنِي رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَلِمَاتٍ أَقُولُهُنَّ فِي قُنُوتِ اَلْوِتْرِ : "اَللَّهُمَّ اِهْدِنِي فِيمَنْ هَدَيْتَ ، وَعَافِنِي فِيمَنْ عَافَيْتَ ، وَتَوَلَّنِي فِيمَنْ تَوَلَّيْتَ ، وَبَارِكْ لِي فِيمَا أَعْطَيْتَ ، وَقِنِي شَرَّ مَا قَضَيْتَ ، فَإِنَّكَ تَقْضِي وَلَا يُقْضَى عَلَيْكَ ، إِنَّهُ لَا يَذِلُّ مَنْ وَالَيْتَ ، تَبَارَكْتَ رَبَّنَا وَتَعَالَيْتَ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ .  وَزَادَ اَلطَّبَرَانِيُّ وَالْبَيْهَقِيُّ :{وَلَا يَعِزُّ مَنْ عَادَيْتَ} زَادَ النَّسَائِيُّ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ فِي آخِرِهِ :{وَصَلَّى اَللَّهُ عَلَى اَلنَّبِيِّ}

وَلِلْبَيْهَقِيِّ عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا :{كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُعَلِّمُنَا دُعَاءً نَدْعُو بِهِ فِي اَلْقُنُوتِ مِنْ صَلَاةِ اَلصُّبْحِ}  وَفِي سَنَدِهِ ضَعْفٌ

Kutoka kwa Al-Hasan bin ‘Aliy[45] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alinifundisha maneno ya kusema katika Qunuwt ya Swalaah ya Witr:

 

“Allaahumma-hdniy fiyman Hadayta, wa-‘Aafiniy fiyman ‘Aafayta, wa-Tawallaniy fiyman Tawallayta, wa-Baarik liy fiymaa A’twayta, wa-Qiniy sharra maa Qadhwayta, fa-Innaka Taqdhwiy walaa yuqdhwaa ‘Alayka, innahu laa yadhillu man Waalayta, Tabaarakta Rabbanaa wa-Ta’aalayta.”

 

(Ee Allaah! Nihidi pamoja na Uliowahidi, na Unipe ’aafiyah pamoja na Uliowapa ’aafiyah, na Nifanye kuwa ni mpenzi Wako pamoja na Uliowafanya wapenzi Wako, na Nibariki katika Ulichonipa na Nikinge na shari ya Ulilolihukumu kwani Wewe Unahukumu wala Huhukumiwi. Hakika hadhaliliki Uliyemfanya mpenzi,  Umebarikika Ee Rabb wetu na Umetukuka)  [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad)]

 

Atw-Twabaraaniyy na Al-Bayhaqiyy wakaongeza:

 

Wa laa ya’izzu man ‘aadayta.”

(Wala hana ’izzah (hadhi) Unayemfanya adui).

 

Katika Riwaayah iliyopokewa na An-Nasaaiy aliongezea:

 

 Wa Swalla Allaahu ‘alan-Nabiyy.”

(na Allaah Amaswalie Nabiy).[46]

 

Na Bayhaqiyy amepokea kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anatufundisha du’aa tunaiomba katika Qunuwt ya Swalaah ya asubuhi.” Katika Isnaad yake kuna udhaifu.

 

 

 

246.

 وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا سَجَدَ أَحَدُكُمْ فَلَا يَبْرُكْ كَمَا يَبْرُكُ اَلْبَعِيرُ، وَلْيَضَعْ يَدَيْهِ قَبْلَ رُكْبَتَيْهِ} أَخْرَجَهُ اَلثَّلَاثَةُ

وَهُوَ أَقْوَى مِنْ حَدِيثِ وَائِلٍ :{رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا سَجَدَ وَضَعَ رُكْبَتَيْهِ قَبْلَ يَدَيْهِ} أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ

فَإِنْ لِلْأَوَّلِ شَاهِدًا مِنْ حَدِيثِ :اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا صَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ ، وَذَكَرَهُ اَلْبُخَارِيُّ مُعَلَّقًا مَوْقُوفًا

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu anaposujudu, asipige magoti kama afanyavyo ngamia, bali aweke viganja vyake chini kabla ya kuweka magoti yake.” [Imetolewa na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd)]

 

Nayo ina nguvu (kwa usahihi) zaidi[47] kuliko Hadiyth ya Waail bin Hujr: “Nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiweka magoti yake chini kabla ya kuweka viganja vyake akisujudu.” [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah)]

 

Hadiyth ya kwanza inashuhudiwa na Hadiyth ya Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) (inayofuata chini), ambayo Ibn Khuzaymah amesema ni Swahiyh, Al-Bukhaariy aliitaja kuwa ni Mu’allaq Mawquwf.

 

 

 

247.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا قَعَدَ لِلتَّشَهُّدِ وَضَعَ يَدَهُ اَلْيُسْرَى عَلَى رُكْبَتِهِ اَلْيُسْرَى ، وَالْيُمْنَى عَلَى اَلْيُمْنَى ، وَعَقَدَ ثَلَاثَةً وَخَمْسِينَ ، وَأَشَارَ بِإِصْبَعِهِ اَلسَّبَّابَةِ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَفِي رِوَايَةٍ لَهُ :{وَقَبَضَ أَصَابِعَهُ كُلَّهَا ، وَأَشَارَ بِاَلَّتِي تَلِي اَلْإِبْهَامَ}

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa anakaa kwa ajili ya Tashahhud aliweka kiganja chake cha kushoto juu ya goti lake la kushoto, na cha kuume juu ya goti lake la kuume, na akakunja vidole vyake[48] na akaashiria kwa kidole chake cha kulia cha Shahaadah.” [Imetolewa na Muslim]

 

Na katika mapokezi yake mengine tamshi la Muslim ilisema: “Na alikunja vidole vyake vyote vya mkono wa kuume, na akaashiria kwa kidole chake cha Shahaadah.”

 

 

 

248.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {اِلْتَفَتَ إِلَيْنَا رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : "إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَقُلْ : اَلتَّحِيَّاتُ لِلَّهِ ، وَالصَّلَوَاتُ ، وَالطَّيِّبَاتُ ، اَلسَّلَامُ عَلَيْكَ أَيُّهَا اَلنَّبِيُّ وَرَحْمَةَ اَللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ ، اَلسَّلَامُ عَلَيْنَا وَعَلَى عِبَادِ اَللَّهِ اَلصَّالِحِينَ ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ ، ثُمَّ لِيَتَخَيَّرْ مِنْ اَلدُّعَاءِ أَعْجَبُهُ إِلَيْهِ ، فَيَدْعُو}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ .

وَلِلنَّسَائِيِّ :{كُنَّا نَقُولُ قَبْلِ أَنْ يُفْرَضَ عَلَيْنَا اَلتَّشَهُّدُ}

وَلِأَحْمَدَ :{أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم عَلَّمَهُ اَلتَّشَهُّد ، وَأَمَرَهُ أَنْ يُعَلِّمَهُ اَلنَّاسَ}

وَلِمُسْلِمٍ : عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ يُعَلِّمُنَا اَلتَّشَهُّدَ: " اَلتَّحِيَّاتُ اَلْمُبَارَكَاتُ اَلصَّلَوَاتُ لِلَّهِ ...}  إِلَى آخِرِهِ

Kutoka kwa Abdullaah bin Mas- ‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Alitugeukia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mmoja wenu anaposwali aseme:

 

At-tahiyyaatu liLLaah, wasw-Swalawaatu, watw-Twayyibaatu. As-salaamu ‘alayka ayyuhan-Nabiy wa-RahmatuLLaahi wa Barakaatuh, As-salaamu ‘alaynaa wa ‘alaa ‘ibaadi-LLaahi-sw-Swaalihiyn. Ash-hadu an-laa ilaaha illaa Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu.”

 

(Maamkizi mema ni ya Allaah, na Swalaah na maneno mema yote. Amani iwe juu yako Ee Nabiy[49] na Rahmah za Allaah na Baraka Zake. Amani iwe juu yetu na juu ya waja Swalihina wa Allaah, Ninashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake).

Kisha achague dua yoyote[50] aipendayo aisome.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

Katika mapokezi ya An-Nassaiy: “Tulikuwa tukisema kabla ya kufaradhishwa (At-Tashahhud).[51]

Na katika mapokezi ya Ahmad: “Kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimfundisha At-Tashahhud na akamuamrisha kuwafundisha watu.”

 

Na katika Muslim kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitufundisha At-Tashahhud:

 

“At-Tahiyyaatu, Al-Mubaarakatu, Asw-Swalawaatu, Atw-Twayyibaatu liLLaah…”

 

(Maamkizi mema, maneno yenye baraka na mazuri yote, Swalaah ni kwa ajili ya Allaah).

Mpaka mwisho wake.

 

 

 

 

249.

وَعَنْ فَضَالَةَ بْنِ عُبَيْدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {سَمِعَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم رِجْلاً يَدْعُو فِي صَلَاتِهِ ، لَمْ يَحْمَدِ اَللَّهَ ، وَلَمْ يُصَلِّ عَلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : " عَجِلَ هَذَا " ثُمَّ دَعَاهُ ، فَقَالَ : " إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِتَحْمِيدِ  رَبِّهِ وَالثَّنَاءِ عَلَيْهِ ، ثُمَّ يُصَلِّي عَلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ يَدْعُو بِمَا شَاءَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَالثَّلَاثَةُ ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ ، وَالْحَاكِمُ

 

Kutoka kwa Fadhwaalah bin ‘Ubayd[52] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimsikia mtu akiomba du’aa ndani ya Swalaah na hakumhimidi Allaah wala hakumswalia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), akasema: “Huyu ameharakisha.” Kisha akamuita yule mtu na akasema: “Mmoja wenu anaposwali, aanze kwa kumhimidi Rabb wake na kumsifu, kisha amswalie Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kisha aombe anachotaka.” [Imetolewa na Ahmad na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd) na waliisahihisha At-Tirmidhiy, Ibn Hibbaan na Al-Haakim]

 

 

 

250.

وَعَنْ أَبِي مَسْعُودٍ اَلْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {قَالَ بَشِيرُ بْنُ سَعْدٍ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ ! أَمَرَنَا اَللَّهُ أَنْ نُصَلِّيَ عَلَيْكَ ، فَكَيْفَ نُصَلِّي عَلَيْكَ  ؟ فَسَكَتَ ، ثُمَّ قَالَ: " قُولُوا : اَللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ ، وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ ، كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ ، وَبَارِكْ عَلَى مُحَمَّدٍ ، وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ ، كَمَا بَارَكْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ فِي اَلْعَالَمِينَ إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ . وَالسَّلَامُ كَمَا عَلَّمْتُكُمْ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَزَادَ اِبْنُ خُزَيْمَةَ فِيهِ :{فَكَيْفَ نُصَلِّي عَلَيْكَ ، إِذَا نَحْنُ صَلَّيْنَا عَلَيْكَ فِي صَلَاتِنَا}

Kutoka kwa Abuu Mas-‘uwd Al-Answaariyy[53] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Bashiyr bin Sa’d[54] amesema Ee Rasuli wa Allaah! Allaah Ametuamrisha tukuswalie, sasa tukuswalie namna gani? (Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  akanyamaza, kisha akasema: Semeni[55]:

 

“Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Swallayta ‘alaa Ibraahiym, wa Baarik ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Baarakta ‘alaa Ibraahiym fil ‘Aalamiyna Innaka Hamiydun Majiyd.”

 

(Ee Allaah! Mswalie Muhammad na ahli wa Muhammad, kama ulivyomswalia Ibraahiym na Umbariki Muhammad na ahli wa Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym Ulimwenguni kote, hakika Wewe ni Mwenye Kuhimidiwa, Mtukufu)[56]

 

na kusalimiana ni kama mnavyojua.” [Imetolewa na Muslim]

 

Na akaongezea Ibn Khuzaymah: “Namna gani tukuswalie wakati tushakuswalia katika Swalaah zetu.”

 

 

 

251.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { إِذَا تَشَهَّدَ أَحَدُكُمْ فَلْيَسْتَعِذْ بِاَللَّهِ مِنْ أَرْبَعٍ ، يَقُولُ : اَللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ جَهَنَّمَ ، وَمِنْ عَذَابِ اَلْقَبْرِ ، وَمِنْ فِتْنَةِ اَلْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ ، وَمِنْ شَرِّ فِتْنَةِ اَلْمَسِيحِ اَلدَّجَّالِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ :{إِذَا فَرَغَ أَحَدُكُمْ مِنْ اَلتَّشَهُّدِ اَلْأَخِيرِ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu anapomaliza Tashahhud, aombe isti’aadhah (kinga) kwa Allaah dhidi ya mambo manne aseme:

 

“Allaahumma inniy a’uwdhubika min ‘adhaabi Jahannama, wamin ‘adhaabil qabri, wamin fitnatil-mahyaa wal-mamaati, wamin sharri fitnatil-masiyhid-dajjaal.”

 

(Ee Allaah, naomba kinga Kwako dhidi ya adhabu ya Jahannam na adhabu ya kaburi[57], na dhidi ya mitihani ya uhai na mauti, na dhidi ya mitihani ya Masiyh Ad-Dajjaal[58]).[59] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Akimaliza mmoja wenu Tahiyyaat ya mwisho.”

 

 

 

252.

وَعَنْ أَبِي بَكْرٍ اَلصِّدِّيقِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّهُ قَالَ لِرَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{ عَلِّمْنِي دُعَاءً أَدْعُو بِهِ فِي صَلَاتِي . قَالَ قُلْ : "اَللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي ظُلْمًا كَثِيرًا ، وَلَا يَغْفِرُ اَلذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ ، فَاغْفِرْ لِي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ ، وَارْحَمْنِي ، إِنَّكَ أَنْتَ اَلْغَفُورُ اَلرَّحِيمُ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amepokea[60] kuwa alimuambia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Nifundishe du’aa ya kuomba katika Swalaah yangu. Akasema: Sema:

 

“Allaahumma inniy dhwalamtu nafsiy dhwulman kathiyran, walaa yaghfirudh-dhunuwba illaa Anta, faghfir-liy maghfiratan min ‘Indika, war-hamniy, Innaka Antal-Ghafuwrur-Rahiym.”

 

 (Ee Allaah, hakika mimi nimedhulumu nafsi yangu dhulma nyingi, wala hapana wa kughufiria dhambi isipokuwa Wewe, kwa hivyo naomba unighufirie maghfirah Yako na unirehemu, Hakika Wewe ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu).[61] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

253.

وَعَنْ وَائِلِ بْنِ حُجْرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {صَلَّيْتُ مَعَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَكَانَ يُسَلِّمُ عَنْ يَمِينِهِ : " اَلسَّلَام عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اَللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ " وَعَنْ شِمَالِهِ : " اَلسَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اَللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ}   رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِسَنَدٍ صَحِيحٍ

Kutoka kwa Waail bin Hujr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimeswali pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitoa Salaam kulia kwake[62] akisema:

“Assalaam ‘alaykum wa-RahmatuLLaahi wa-Barakaatuh.

 (Amani iwe juu yenu na Rahmah za Allaah na Baraka Zake)

 

 na kushoto akisema:

“Assalaam ‘alaykum wa-RahmatuLLaahi wa-Barakaatuh.[Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]

 

 

 

254.

وَعَنْ اَلْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم { كَانَ يَقُولُ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلَاةِ مَكْتُوبَةٍ : " لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ ، لَهُ اَلْمُلْكُ ، وَلَهُ اَلْحَمْدُ ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، اَللَّهُمَّ لَا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ ، وَلَا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ ، وَلَا يَنْفَعُ ذَا اَلْجَدِّ مِنْكَ اَلْجَدُّ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Al-Mughiyrah bin Shu’bah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alikuwa akisema mwisho wa kila Swalaah ya faradhi:

 

“Laa ilaaha illaa Allaah Wahdahu laa shariyka Lah, Lahul-Mulk wa-Lahul-Hamd wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, Allaahumma laa maani’a limaa A’twayta, wa laa mu’twiya limaa Mana’ta, wa laa yanfa’u dhal-jaddi Minkal-jaddu.

 

(Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Peke Yake Hana mshirika, Ufalme ni Wake, Kuhimidiwa ni Kwake, Naye ni Mweza wa kila kitu. Ee Allaah, hakuna wa kuzuia Ulilotoa, wala wa kulitoa Ulilozuia, wala mwenye utajiri hatanufaishwa chochote Kwako na utajiri wake)[63]. [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

255.

وَعَنْ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {إِنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَتَعَوَّذُ بِهِنَّ دُبُرَ اَلصَّلَاةِ : " اَللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ اَلْبُخْلِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ اَلْجُبْنِ ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أُرَدَّ إِلَى أَرْذَلِ اَلْعُمُرِ ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ اَلدُّنْيَا ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ اَلْقَبْرِ}  رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Sa’d bin Abii Waqqaasw[64] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akijikinga (kwa Allaah) baada ya kila Swalaah:

 

Allaahumma inniy a’uwdhubika minal-bukhli, wa a’uwdhubika minal-jubni, wa a’uwdhubika min an uradda ilaa ardhalil-‘umuri, wa a’uwdhubika min fitnatid-dunyaa wa adhaabil-qabri.”

 

(Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na ubakhili, na najikinga Kwako kutokana na uoga, na najikinga Kwako kurudishwa katika umri wa kudhalilika [uzee][65], na najikinga Kwako fitnah za dunia na adhabu za kaburi). [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

256.

وَعَنْ ثَوْبَانَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا اِنْصَرَفَ مِنْ صَلَاتِهِ اِسْتَغْفَرَ اَللَّهَ ثَلَاثًا ، وَقَالَ : " اَللَّهُمَّ أَنْتَ اَلسَّلَامُ وَمِنْكَ اَلسَّلَامُ . تَبَارَكْتَ يَا ذَا اَلْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Thawbaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa alipomaliza Swalaah yake, anaomba maghfirah kwa Allaah mara tatu[66], na anasema:

 

“Allaahumma Antas-Salaam, wa Minkas-Salaam, Tabaarakta yaa Dhal Jalaali wal Ikraam.

 

 (Ee Allaah, Wewe Ndiye Amani, na Amani hutoka Kwako, Umebarikika ee Mwenye Ujalali na Utukufu).[67] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

257.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : {مَنْ سَبَّحَ اَللَّهَ دُبُرَ كُلِّ صَلَاةٍ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ ، وَحَمِدَ اَللَّهِ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ ، وَكَبَّرَ اَللَّهُ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ ، فَتِلْكَ تِسْعٌ وَتِسْعُونَ ، وَقَالَ تَمَامَ اَلْمِائَةِ : لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ ، لَهُ اَلْمُلْكُ ، وَلَهُ اَلْحَمْدُ ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، غُفِرَتْ لَهُ خَطَايَاهُ ، وَإِنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ اَلْبَحْرِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَفِي رِوَايَةٍ أُخْرَى: أَنَّ اَلتَّكْبِيرَ أَرْبَعٌ وَثَلَاثُونَ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema:  “Atakaye Sabbih (Subhaana Allaah) kila baada ya Swalaah mara thelathini na tatu[68], akaleta tahmiyd (AlhamduliLLaah) mara thelathini na tatu akaleta takbiyra (Allaahu Akbar) mara thelathini na tatu, akamalizia itimie mia kwa:

 

“Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah, Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa-Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr.”

 

(Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hana mshirika, ufalme wote ni Wake, na Himdi zote ni Zake, Naye ni Mweza wa kila kitu), ataghufuriwa makosa yake japokuwa ni mfano wa povu la bahari.”  [Imetolewa na Muslim]

 

Na katika mapokezi mengine: “Takbiyra ni mara thelathini na nne.”

 

 

 

258.

وَعَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{قَالَ لَهُ : " أُوصِيكَ يَا مُعَاذُ : لَا تَدَعَنَّ دُبُرَ كُلِّ صَلَاةٍ أَنْ تَقُولُ : اَللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ وَشُكْرِكَ وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَأَبُو دَاوُدَ ، وَالنَّسَائِيُّ بِسَنَدٍ قَوِيٍّ

Kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuambia: “Nakuusia ee Mu’aadh! Usiache abadani baada ya kila Swalaah kusema:

 

“Allaahumma a’inniy ‘alaa Dhikrika wa Shukrika, wa husni ‘ibaadatika.”

 

(Ee Allaah! Nisaidie kukudhukuru, na kukushukuru, na kukuabudu kwa uzuri upasao). [Imetolewa na Amad, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy kwa Isnaad yenye nguvu (Qawiyy)]

 

 

 

259.

وَعَنْ أَبِي أُمَامَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{مَنْ قَرَأَ آيَةَ اَلْكُرْسِيِّ دُبُرَ كُلِّ صَلَاةٍ مَكْتُوبَةٍ لَمْ يَمْنَعْهُ مِنْ دُخُولِ اَلْجَنَّةِ إِلَّا اَلْمَوْتُ} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

وَزَادَ فِيهِ اَلطَّبَرَانِيُّ :{وَقُلْ هُوَ اَللَّهُ أَحَدٌ} 

Kutoka kwa Abuu Umaamah[69] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kusoma Aayatul kursiyy[70] mwisho wa kila Swalaah ya faradhi, hakuna kitakachomzuia kuingia Jannah isipokuwa[71] mauti.”[72] [Imetolewa na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

At-Twabaraaniyy aliongezea: “Na Qul-Huwa-Allaahu Ahad.”[73]

 

 

 

260.

وَعَنْ مَالِكِ بْنِ الْحُوَيْرِثِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم{ صَلُّوا كَمَا رَأَيْتُمُونِي أُصَلِّي} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Maalik bin Al-Huwayrith (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”[74] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

261.

 وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {قَالَ لِيَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " صَلِّ قَائِمًا، فَإِنْ لَمْ تَسْتَطِعْ فَقَاعِدًا، فَإِنْ لَمْ تَسْتَطِعْ فَعَلَى جَنْبٍ وَإِلَّا فَأَوْمِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kwamba Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swali huku umesimama, na ukiwa huwezi swali kwa kukaa, na ukiwa huwezi, swali kwa ubavu, laa sivyo swali kwa ishara.”[75] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

262.

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم {قَالَ لِمَرِيضٍ  صَلَّى عَلَى وِسَادَةٍ ، فَرَمَى بِهَا  وَقَالَ : " صَلِّ عَلَى اَلْأَرْضِ إِنْ اِسْتَطَعْتَ ، وَإِلَّا فَأَوْمِئْ إِيمَاءً ، وَاجْعَلْ سُجُودَكَ أَخْفَضَ مِنْ رُكُوعِكَ} رَوَاهُ اَلْبَيْهَقِيُّ بِسَنَدٍ قَوِيٍّ وَلَكِنْ صَحَّحَ أَبُو حَاتِمٍ وَقْفَهُ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuambia mgonjwa aliyekuwa anaswali juu ya mto (tandiko) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliutupa, akasema: “Swali juu ya ardhi ukiweza, vinginevyo swali kwa ishara na uzifanye Sijdah zako ziwe chini zaidi kuliko rukuu zako.” [Imetolewa na Al-Bayhaq kwa Isnaad yenye nguvu, lakini Abuu Haatim aliisahihisha iliyo Mawquwf]

 

 

 


 

[1] Ni wazi kwamba kuisoma Qur-aan ni lazima. Kuna Hadiyth inayosema:

 

((ثُمَّ اِقْرَأ بِأمِّ الْقُرْآن))

 ((Kisha soma kwa Mama wa Qur-aan))

 

Ni wazi kuwa inamaanisha Suwrah Al-Faatihah.

 

[2] Wale watu ambao hawarukuu vizuri, hawasujudu vizuri, na hawakai vizuri, n.k katika Swalaah zao, waizingatie Hadiyth hii. Vitendo vinavyofanywa ovyo-ovyo, na harakaharaka siyo sahihi. Hivi vitendo vya ovyo-ovyo huharibu Swalaah zao. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema Swalaah kama hiyo ni “Swalaah ya mnafiki” na wanaotenda hivyo ni “Wezi wa aina mbaya kabisa.”

 

[3] Huyu Rifaa’ah alipewa jina la utani la Abuu Mu’aadh na alikuwa Az-Zurqi Al-Answaar Al-Madaniy, Swahaba mkubwa ambaye alishiriki katika Al-‘Aqabah pamoja na babake ambaye alikuwa Answaar wa kwanza kusilimu. Rifaa’ah alishiriki katika vita vya Badr na vita vyote vilivyofuata; na pia alikuwa pamoja na ‘Aliy katika vita vya Al-Jamal na Siffiyn. Alikufa mwanzoni mwa Ukhalifa wa Mu’aawiyah mnamo mwaka 41 A.H.

 

[4] Ummul-Qur-aan ni jina lingine la Suwrah Al-Faatihah. Hadiyth hii ya kusoma Al-Faatihah na Suwrah au Aayah zingine za Qur-aan ni muhimu. Kwa mujibu wa ‘Ulamaa wengine, baada ya kuisoma Al-Faatihah ni muhimu kusoma zaidi, na wengine wanasema inapendeza. Ukitaka kujua zaidi soma vitabu vya Hadiyth.

 

[5] Abuu Humayd anaitwa ‘Amr au Mundhir bin Sa’d bin Al-Mundir au Maalik Al-Answaar Al-Khazraj Al-Madaniy. Ametoka katika kizazi cha Saa’idah ambaye ndiye baba wa Al-Khazraj. Alishiriki katika Uhud na vita vilivyofuatia, na akafariki ima mwishoni mwa Ukhalifa wa Mu’aawiyah au mwanzoni mwa utawala wa Yaziyd mnamo mwaka 61 A.H.

 

[6] Ummah wote wa kiislamu unatakiwa uswali kama alivyokuwa akiswali mwenyewe Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alikuwa akiswali kwa amani na utulivu wa akili na ukamilifu. Kuswali kwa papara, harakaharaka kunakatazwa.

 

[7] Katika Hadiyth hii, “Raf’u yadayni” (kunyanyua mikono) imetajwa kuwa ifike hadi mabegani. Usimulizi wa Waail bin Hujr, umetaja hadi masikioni.

 

[8] Katika mwisho wa Hadiyth hii, inatajwa kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisoma du’aa hii wakati wa kuswali Tahajjud iswaliwayo katikati ya usiku. Mtunzi, katika kitabu chake cha Talkhiys, ameripoti kutoka kwa Imaam Shaafi’iy na Ibn Khuzaymah kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliisoma du’aa hiyo katika Swalaah zote za faradhi. Katika usimulizi wa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) anasema uwezekano wa kusoma du’aa hii katika Swalaah zote mbili upo.

 

[9] Katika maneno haya matukufu, Muislamu anaagizwa aombe maghfirah kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى)  juu ya dhambi zake, anazozijua na asizozijua, hata awe mtiifu sana kuliko wote.

 

[10] Suwrah Al-Faatihah:

 

[11] “’Uqbat ash-shaywaan” (mkao wa shaytwaan) ni kuweka matako ardhini na kunyanyua magoti na mguu uliyoko chini ya goti na viganja vikiwa ardhini pande zote mbili. “Iftiraash As-Sab’i” (kutandaza mikono kama mnyama mwitu) ni kukalia sehemu za nyuma za mguu wa chini na sehemu ya nyuma ya paja na kisha kuinamia mbele huku ukinyoosha viganja mbele yako juu ya ardhi.

 

[12] Simulizi hii ya ‘Abdullaah bin ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) ni dhahiri kabisa kuthibitisha kwa kila mwanzo wa Swalaah, wakati wa kurukuu, kuinuka baada ya kurukuu, kunyanyua mikono mpaka kwenye masikio ni Sunnah. Hayo maneno:

 كانَ يَرْفَعُ

“alikuwa akinyanyua…”

 

Yanaonyesha udumishaji. Inathibitisha unyanyuaji wa mikono haukuwahi kufutwa wala kuachwa. Ahaadiyth zote zinazopinga “kunyanyua mikono” ni dhaifu au mawdhwu’ (zimetungwa). Miongoni mwa Hadiyth dhaifu, udhaifu wa zingine umeafikiwa na wengi, na zingine zina kukhitilafiana. Katika zote hizo, usimulizi wa ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd huhesabika kuwa bora zaidi. Imaam Al-Bukhaariy alinukuu maoni ya kishariy’ah ya mwalimu wake ‘Ali bin Al-Madiniy kwa msingi wa simulizi za ‘Abdullaa bin ‘Umar ni lazima kwa kila Muislamu kunyanyua mikono. Ikhtilaaf kuhusu kadhia hii ni pana mno kujadaliwa hapa.

 

[13] Waail bin Hujr au Abuu Hunayda au Abuu Hinda, alikuwa Swahaba mkubwa, na babake alikuwa mmoja wa wafalme wa Hadhramaut. Alimzuru Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ambaye alitandika shali (nguo ya juu) yake ili akalie, na akamuombea Baraka yeye na wanawe, na kisha akamteua awe mkuu wa Aqyal ya Hadhramaut. Alilowea mji wa Kufa, na akafariki wakati wa Ukhalifa wa Mu’aawiyah.

 

[14] Hadiyth hii inaweka wazi mambo mawili: Kwanza kuikunja mikono ndani ya Swalaah ni Sunnah, na kutokuikunja ni kuipinga Sunnah. Watu wengine wameipokea Hadiyth hii kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) lakini siyo sahihi. Pili, mkono ikunjwe juu ya kifua, siyo chini ya kitovu, kama wanavyofanya watu wengine. Usimulizi wanaotegemeza ubishani wao pia siyo sahihi.

 

[15] ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit alikuwa mmoja wa viongozi wa ki-Answaar katika ‘Aqabah (Maktaba) wa kwanza na wa pili wa Aqaba. Pia alihudhuria katika vita vya Badr na vita vilivyofuata. ‘Umar alimpeleka Shaam awe Kadhi na mwalimu. Kwa hivyo alilowea Hims na baadaye alikwenda Palestina na akafia Ramlah au Bayt Al-Maqdis mnamo mwaka 34 A.H. akiwa na miaka 72.

 

[16] Hadiyth iliyotajwa hapo juu ni ushahidi tosha kuwa bila kusoma Suwrah Al-Faatihah Swalaah haiswihi. Maswahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na wafuasi wa Maswahaba na wengi wa ‘Ulamaa waliiamini desturi hii. Katika Hadiyth ijulikanayo kama (مسء الصلاة)  - maneno yenyewe ni:

إِقْراْ بِاُمِّ الْكِتاب

(Soma kwa Ummul-Kitaab)

 

Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliamrisha kuswali kwa kusoma Al-Faatihah katika kila Rakaa. Imaam na Maqtadi (Maamuma) wote sharti waisome Al-Faatihah. Hakuna mtu yoyote aliyeepushiwa kusoma, na yatakiwa isomwe katika kila Swalaah, kimyakimya (Sirran) au kwa sauti (Jahran), ni lazima kuisoma Al-Faatihah. Muslim amesimulia Hadiyth aliyoipokea Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), aliulizwa juu ya kuisoma Al-Faatihah, endapo Swalaah inaswaliwa nyuma ya Imaam. Abuu Hurayrah alijibu kuwa: ni lazima isomwe kwa siri kwa sauti ya chini. At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy wameripoti Hadiyth kutoka kwa ‘Ubaadah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwahi kuwauliza: “Je mnasoma chochote mkiwa nyuma ya Imaam?” Maswahaba wakajibu: ‘Ndiyo,” Ndipo Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaambia: Someni Al-Faatihah na siyo nyingine yoyote, kwa kuwa bila kuisoma Suwrah hiyo Swalaah haiswihi. Kuna Hadiyth nyingine nyingi tu ambazo zinathibitisha kuwa kuisoma Al-Faatihah ni lazima hata ukiwa nyuma ya Imaam pia. Ama kuhusu Hadiyth inayosema kuwa kusoma kwa Imaam kunatosheleza kwa Maamuma pia, ni dhaifu. Miongoni mwa wale wanaoamini maoni haya (kuisoma Al-Faatihah), kwengine wanaona kuwa Al-Faatihah isomwe katikati ya mapumziko ya visomo vya Imaam, na wengine wanasema kuwa isomwe baada ya kumaliza Imaam kusoma Al-Faatihah.

 

 

[17] Inamaanisha kuwa walikuwa hawaisomi kwa sauti, bali waliisoma kimyakimya kama ilivyosema Hadiyth iliyofuatia.

 

[18] Mtu anaweza kufanya yoyote kati ya hizo njia, ni sahihi.

 

[19]Nu’aym huyu ndiye Abuu ‘Abdillaah Nu’aym ‘Abdillaah Al-Mujmir, ambaye ni mtumwa aliyeachwa huru na ‘Umar bin Al-Khatwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Alikuwa akifukiza manukato katika Msikiti wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kila siku ya Ijumaa saa sita mchana, kwa hivyo alipewa jina la utani la Al-Mujmir. Alikuwa Taabi’i na Abuu Haatim, Ibn Ma’iyn, Ibn Sa’d na An-Nasaaiy walimthibitisha kuwa ni wa kutegemewa.

 

[20] Baada ya kuisoma Suwrah Al-Faatihah ni Sunnah kusema “Aamiyn”.  Ikiwa ni Imaam au Maamuma, kila mtu ni wajibu kusema “Aamiyn” ambayo maana yake ni: “Ee Allaah Ikubali du’aa hii au kisomo hiki.”

 

[21] “Aamiyn” inajuzu kwa sauti au kimyakimya. Kuna kutofautiana maoni juu ya kadhia hii. Hanafiyah wanaisoma kimyakimya.  Shaafi’i na Ahlul-Hadiyth huisoma kwa sauti kubwa. Sauti kubwa (Jahr) maana yake, ni sauti ya mtu wa pili kuweza kuisikia. Kusoma “Aamiyn” kwa sauti kubwa kumethibitishwa na Ahaadiyth nyingi zingine. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisoma kwa sauti na alikuwa akiirefusha. At-Tirmidhiy aliipa Hadiyth hii kuwa ni Hasan, na Ad-Daaraqutwniy aliipa daraja la Swahiyh. Maulana Abdul-Hayy Lucknowi alisema kuwa, kwa mujibu wa kutopendela upande wowote, kuisoma Aamiyn kwa sauti kubwa ni sahihi zaidi. Ama kuhusu kuisoma Aamiyn kimya kimya, Imaam At-Tirmidhiy amesimulia Hadiyth ambayo kwayo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliisoma Aamiyn na akatumia sauti ya chini. Kwa hivyo baadhi ya Wahanafi wanahoji matumizi ya Hadiyth hii, ingawa At-Tirmidhiy mwenyewe ameikanusha Hadiyth hii kwa nukta nne za maoni. Hata hivyo, kila mtu ana uhuru na anawajibika kwa desturi na matendo yake mwenyewe.

 

[22] ‘Abdullaah bin Abiy Awfaa ndiye aliyepewa jina la utani la Abuu Mu’aawiyah, na jina la babake ilikuwa ‘Alqamah bin Al-Haarith Al-Aslamiy. Yeye na babake wote walikuwa Maswahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alihudhuria Al-Hudaybiyyah, Khaybar, na vita vilivyofuata. Aliishi katika mji wa Kufa nchini ‘Iraaq na alifariki huko katika mwaka 87H. Alipofuka macho na alikuwa Swahaba wa mwisho kufariki katika mji wa Kufa huko ‘Iraaq.

 

[23] Watu wengine hutumia Hadiyth hii kudai kuwa kusioma Suwrah Al-Faatihah ndani ya Swalaah siyo lazima kwa sababu Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakusema kuwa alilazimika kujifunza Al-Faatihah. Hii na ikumbukwe kwamba kuna kuwahurumia walemavu katika Shariy’ah. Makatazo na amri huwa hazibadili Shariy’ah za kuhurumia kama hizo. Iwapo mtu anasema kuwa hawezi kutawadha kwa sababu asizoweza kuzizuia, basi huambiwa ajitwahirishe kwa kutayammam (kwa mchanga); na hii haimaanishi kuwa kuchukua wudhuu siyo lazima.

 

[24] Hii imeafikiwa na wengi kuwa kuisoma Al-Faatihah kwa Swalaah za Adhuhuri na Alasiri huwa kwa sauti ya chini au kimyakimya.

 

[25] Inaelekea kutoka katika Hadiyth hii kuwa, hakuisoma Suwrah yoyote baada ya Al-Faatihah katika Rakaa mbili za mwisho. Lakini Hadiyth ya Abuu Sa’iyd katika Swahiyh Muslim inaripoti kwamba, walikisia urefu wa Rakaa ya mwisho ni kama Aayah 15 wakati wa Aayah za Al-Faathah ni Aayah 7 tu. Kwa hivyo, yaelekea kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alizisoma Aayah zingine na wakati mwingine hakuzisoma. Yaani, kusoma katika Rakaa za mwisho ni Sunnah.

 

[26] Suwrah As-Sajdah (32: 1-30) ambayo ina Aayah thelathini (30).

 

[27] Sulaymaan bin Yasaar alikuwa ni mmoja wa ‘Ulamaa saba wa Fiqh na miongoni mwa Taabi’iyn maarufu. Alikuwa ni wa kutegemewa, mwenye taqwa, msomi, na alihifadhi Hadiyth nyingi. Alipewa jina la utani la Abuu Ayyuwb, na alikuwa mtumwa alieachwa huru na Maymuwnah, (Mama wa Waumini). Alifariki mnamo mwaka wa 107A.H. akiwa na umri wa miaka 73.

 

[28] Kutoka Suwrah ya Al-Hujuraat mpaka mwisho, Suwrah zote zinaitwa “Mufasw-swal” (zilizopambanuliwa), kwa sababu ya nafasi ndefu kati ya BismiLLaahi mbili. Na kutoka Suwrah ya Al-Hujuraat hadi Al-Buruwj zinaitwa “Twiwaal Mufasw-swal” (ndefu zilizopambanuliwa) na kutoka Al-Buruwj mpaka Al-Bayyinah mpaka mwisho zinaitwa “Awsaatw Mufasw-swal” (zenye urefu wa wastani). Na kutoka Al-Bayyinah mpaka mwisho zinaitwa “Qiswaar Mufasw-swal” (Fupi zilizopambanuliwa). Kuisoma Twiwaal katika Swalaah za Alfajiri, Awsaatw katika Swalaah za ‘Ishaa, na Qiswaar katika Swalaah ya Magharibi ni Sunnah. Mara nyingine hutokea kinyume chake kama inavyoelezewa katika Hadiyth ifuatayo.

 

[29] Hadiyth zingine zinaripoti kwamba, Suwrah Al-A’raaf, Asw-Swaffaat, na Ad-Dukhaan pia zilizomwa kwenye Swalaah ya Magharibi. Inamaanisha kuwa Suwrah ndefu pia zimewahi kusomwa katika Swalaah ya Magharibi; na Mu’awwidhatayn (Suwrah Al-Falaq na An-Naas) zilizosomwa katika Swalaah ya Alfajiri. Lakini kawaida ilikuwa ni kusoma kama ilivyoelezwa hapo juu.

 

[30] Katika Suwrah hizi yametajwa mambo ya kuumbwa kwa Aadam, maajabu ya uumbaji, na Siku ya Mkusanyiko, na Siku ya kufufuliwa itatokea siku ya Ijumaa. Kwa sababu hii, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akizisoma Suwrah hizi mnamo siku ya Ijumaa, ili watu waweze kufikiri kuwa kitu chaweza kutokea leo na wamuogope Allaah (سبحانه وتعالى).  

 

[31] Inamaanisha kuwa, Suwrah hizi zisomwe kila siku ya Ijumaa katika Swalaah ya Alfajiri, Suwrah zozote maalumu ambazo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akizisoma katika Swalaah yoyote maalumu kwa mpangilio maalumu na kila mara, ni vizuri kuzisoma hizo kwa namna ile ile kwa kila Swalaah kwa kuwa hiyo ndiyo Sunnah. Kuzisoma Suwrah nyingine pia inaruhusiwa.

 

[32] Katika Rukuu na Sijdah, kusoma Qur-aan ni haraam na inachukiza. Kuna sehemu nyingi za Qur-aan, na kila sehemu ina namna yake, na kwa kila sehemu imeelezwa du’aa na maombi maalumu. Katika Rukuu yatakiwa kusomwa:

سُبْـحانَ رَبِّـيَ الْعَظـيم

 

 na katika Sijdah isomwe:

سُبْـحانَ رَبِّـيَ الأَعْلـى  

Katika Sijdah inaruhusiwa kuomba du’aa.

 

[33] Takbiyra ya kwanza inaitwa Takbiyraatul-Ihraam (ya kukataza kufanya lolote liwalo isipokuwa Swalaah tu), au huitwa Takbiyratul-Iftitaah (ya kufungulia), au Takbiyratul-Uwlaa (ya mwanzo), na Takbiyra zingine zote zinaitwa Takbiyratul-Intiqaal, maana yake ni ya kuhamia ndani ya Swalaah kwa mfano kutoka katika kisimamo hadi kwenda Rukuu, na kutoka Rukuu kwenda Sijdah, n.k. Ile Takbiyra ya mwanzo (Takbiyratul-Ihraam) imeshurutishwa  kuwajibika, na Takbiyra zinazobakia ni za Sunnah, na kwa mujibu wa wengine ni waajib (lazima).  

 

[34] Neno hilo   جد linatumika katika lugha ya Kiarabu kwa maana mbili; Kwanza babu na mababu, na pili utukufu na hadhi. Maana zote mbili ni sahihi katika muktadha huu kwa sababu mali au utajiri, utukufu wa kuzaliwa na taadhima, vyote havina thamani mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى). ‘Amali njema pekee ndiyo dira ya kuepukia adhabu. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuambia binti yake Faatwimah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kutenda ‘amali njema ili kujiokoa yeye mwenyewe kutokana na adhabu ya Allaah (سبحانه وتعالى), na wala asimtegemee babake (Yeye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wala unasaba wake. Kuokoka kunategemea ‘amali njema tu, sasa iwapo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kamuambia hivyo binti wa kumzaa yeye mwenyewe namna hii, basi nani mwingine tena anaweza kujivunia hadhi ya kuzaliwa?

 

[35] Du’aa hii ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni ushahidi tosha wa kukanusha dhana ya wale wanaosimama wima moja kwa moja baada ya kurukuu, na kuchukulia kwamba ucheleweshaji wa kutamka Tasbiyh tatu (yaani kusema سبحان الله) utaifanya Sijdah ya kulipia ni lazima. Inapokuwa imethibitishwa na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) basi tena hakuna nafasi ya maoni ya mtu mwingine binafsi.

 

[36] Hadiyth hii inaweka wazi kuwa paji la uso na pua, vyote vinahesabika kuwa ni kiungo kimoja. Ukihesabu paji la uso mbali na pua, utapata viungo vinane.

 

[37] Huyu Ibn Buhaynah ni Abuu Muhammad ‘Abdillaah bin Maalik bin Al-Qishb Al-Azdi, na hilo Buhaynah ni jina la mamake. Alisilimu zamani na akawa mtawa, mwenye taqwa, na alikuwa akifunga (Swawm) siku zote. Alifariki chini ya bonde la Rim, maili tatu kutoka Al-Madiynah, mnamo mwaka wa 54 au 58 A.H.

 

[38] Huyu Al-Baraa ndiye Abuu ‘Ammaara Al-Baraa bin ‘Aazib bin Al-Haarith bin ‘Adiy Al-Answaariy Al-Aws, ambaye alikuwa Swahaba na pia mwana wa Swahaba. Aliachwa kwenye vita vya Badr kwa sababu ya umri wake ulikuwa mdogo, na kushiriki kwake mara ya kwanza kulikuwa katika vita vya Uhud au Al-Khandaaq. Aliteka Ar-Ray na alishiriki katika vita vya Al-Jamaal, Siffiyn, na Naharwaan pamoja na ‘Aliy. Alifia Kufa mnamo mwaka wa 72 A.H.

 

[39] Hii ilikuwa kwa ajili ya kutojiweza kwa sababu alianguka kutoka juu ya farasi wake, na akateguka kiunganishi cha mguu wake.

 

[40] Inamaanisha katika Rakaa ya kwanza na ya tatu. Na hii inaitwa Jalsatul-Istiraahah (mkao wa kupumzika). Kwa mujibu wa usimulizi, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akikaa katika mkao huu kwa muda mrefu kiasi kwamba watu walifikiri ni kwa ajili ya kusahau kwake. Haikuwa kwa sababu ya umri wake, kwani yeye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kamwe hakurahisisha wajibu wake wowote kwa ajili ya udhaifu utokanao na uzee.

 

[41] Makabila haya yalikuwa ya رعل  (Ri’il),  ذكوان  (Dhakwaan) na عصية (‘Uswayyah). Haya yalifanya bay’ah (mkataba) na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) lakini yakavunja ahadi yao na yakawaua Wahubiri sabiini wa Kiislamu baada ya kuwategea kwa kuwaalika. Tukio hili linajulikana kama Bi’r Ma’uwnah.

 

[42] Inaelekea kuwa kuna ikhtilaaf miongoni mwa Hadiyth hizi. Ya kwanza inasema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) daima alikuwa akisoma Qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri kisha akaacha. Hadiyth nyengine inasema kuwa aliisoma Qunuwt kila alipokuwa akiomba ustawi wa kijamii wa taifa au kuwalaani watu fulani kwa ufisadi wao. Hadiyth ya tatu inasema kuwa, kusoma Qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri ni uzushi. Lakini iliyo sahihi ni kwamba haikuwa ni waajib zama hizo kuisoma Qunuwt kama wafanyavyo baadhi ya watu sasa kuidumisha Qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri, bali lililo sahihi ni kuwa Qunuwt inasomwa pale inapotokea shida fulani kwa Waislamu, kisha inapomalizika huachwa kutekelezwa Qunuwt kama ilivyotajwa katika Hadiyth namba (242) ya Al-Bukhaariy na Muslim.

 

[43] Sa’d huyu ndiye Abuu Maalik Sa’d bin Twaariq bin Ashyaam bin Mas-‘uwd Al-Ashja’iy Al-Kuwfi. Alikuwa miongoni mwa Taabi’iyn waliotegemewa. Alifariki mnamo mwaka 140 A.H.

 

[44] Twaariq ni Swahaba aliyesimulia Hadiyth chache. Hadiyth kumi nne tu ndizo zilizosimuliwa kutoka kwake, na zote zilisimuliwa na mwanae huyo aliyetajwa hapo juu, Sa’d. Alistakir kule Kufa.

 

[45] Al-Hasan ni mjukuu kipenzi wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na ni mmoja wa vijana wa Jannah. Alizaliwa mnamo mwezi wa Ramadhwaan mwaka wa 3 A.H; na aliapishwa kuwa Khalifa baada ya kuuliwa baba yeke ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), lakini alimkabidhi Mu’aawiyah Ukhalifa mnamo mwezi wa Jumaadal-Uwlaa mwaka 41 baada ya miezi saba tu kwa kuchukia kumwaga damu ya Waislamu. Alikufa mnamo mwaka 49 A.H., na akazikwa Al-Baqiy’.

 

[46] Ifahamike kuwa baadhi ya watu husoma Qunuwt mikono yao ikiwa wazi kabla ya kurukuu. Lakini sahihi yake ni kusoma kwanza Qunuwt huku mikono imeinuliwa juu baada ya kusimama wima kutoka katika Rukuu. Watu wengine husoma Qunuwt kila wanaposwali Witr, wakati wengine husoma Qunuwt katika wiki mbili za mwisho za mwezi wa Ramadhwaan tu. Watu wengine huhesabu Qunuwt kama ni Waajib (lazima), na wengine huihesabu kuwa ni Sunnah. Ukweli ni kwamba hiyo ni Sunnah.

 

[47]Kitabu cha Fathul-‘Uluwm kinasema kuwa, Hadiyth zote mbili ni imara, na zinatumika sawasawa. Hata hivyo tendo la Muhaddithiyn (‘Ulmaa Wasimulizi wa Hadiyth) na Hanaabilah (wafuasi wa Hanbali) imeegemezwa kwenye Hadiyth ya Abuu Hurayrah. Msimamo wa Shafi’iyya, Hanafiyya na Malikiyya ummegemezea katika rejea ya Waail.

 

[48] Sharti ikunjwe kwa njia ambayo mtu aweke kidole gumba chake chini (kifunikwe na) kidole chake cha Shahaadah huku akiwa kavifumba vidole vitatu vilivyobaki. Kisha ainue kidole chake cha Shahaadah wakati akisoma sehemu ya Tahiyyaat inayosema:

أَشْـهَدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ الله

“Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaah”

 

Na wakati anapokishusha asome hivyo hivyo.

 

[49] Mwanzoni, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitufundisha tumswalie yeye, kwa sababu haki yake kwa Ummah wake ni zaidi kuliko mtu yoyote awaye, zaidi kuliko Muumini mwenyewe.

 

 

[50] Hadiyth hii inaelezea kuwa, du’aa yoyote ndani ya Swalaah ni kufuata mwendo wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), hii pia inaweka wazi kuwa hakuna jambo lolote makhsusi ambalo mja anaweza kuomba ndani ya Swalaah. Mtu anaweza kuomba chochote akitakacho, iwe cha hapahapa duniani au cha Aakhirah.

 

[51] Yale maneno ambayo watu walikuwa wakiyasoma kabla ya kufaradhishwa At-Tashahhud hayajatajwa na msimulizi. Lakini kwa mujibu wa Hadiyth zingine, walikuwa wakisema hivi:

 

السَّلاَمُ عَلَى جِبْرِيلَ، السَّلاَمُ عَلَى مِيكَائِيلَ ...

Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwazuia kusema hivyo, ndipo akawafundisha At-Tashahhud.

[52] Fadhwaalah bin ‘Ubayd bin Naafidh bin Qays alipewa jina la utani la Abuu Muhammad Al-Answaar Al-Aws. Mwanzo alipigana vita vya Uhud na vita vingine vilivyofuata. Alichukua Bay’atur-Ridhwaan. Alilowea Damascus, Shaam na akawa Kadhi wake akiwa aliteuliwa na Mu’aawiyah wakati alipokuwa akienda kwenye vita vya As-Siffiyn. Alifariki mnamo mwaka wa 56 A.H.

 

[53] Abuu Mas-‘uwd ndiye ‘Uqbah bin ‘Amr bin Tha’alabah Al-Answaar Al-Badri, alikuwa ni mmoja wa Maswahaba maarufu. Alishiriki ‘Aqabah ya pili wakati angali kijana. Alilowea Kufa na akafia huko au Al-Madiynah baada ya miaka ya arubaini ya Hijrah.

 

[54] Bashiyr Ibn Sa’d huyu ndiye Abuu An-Nu’maan Bashiyr bin Sa’d bin Tha’alabah bin Al-Jullaas au Al-Khallaas Al-Answaar Al-Khazraj. Alipigana vita vya Badr, na alihudhuria Bay’atul-‘Aqabah. Pia alishiriki katika vita vya Uhud, Al-Khandaq, na vita vingine vilivyofuata. Aliuwawa kule ‘Ayn At-Tamr mnamo mwaka wa 13 A.H.

 

[55] Maneno ya kumswalia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) yametajwa namna tofauti katika Hadiyth mbalimbali. Kwenye Hadiyth moja huweko neno au maneno zaidi kuliko kwenye Hadiyth nyingine.

 

[56] Hii inaweka wazi kuwa hiyo kumswalia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) yatakiwa isomwe baada ya kusoma At-Tashahhud ndani ya Swalaah, na kuomba du’aa sharti iwe katika Tashahhud ya mwisho tu. Tuna arifiwa zaidi kwamba, kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Swalaah ndani ya Swalaah ni Waajib (lazima).

 

[57] Hadiyth hii inatuarifu kwamba, mtu akishafariki hukumbana na adhabu kaburini, halikadhalika inatuarifu kuwa Muumin wa kweli huwa hana khofu yoyote kaburini. Hii inatibitishwa na Hadiyth nyingi tu.

 

[58] Al-Masiyh Ad-Dajjaal atakuwa ni kafiri atakayezuka kabla ya Siku ya Qiyaamah ili kuijaribu Iymaan za Waumini. Waumini wakweli watabakia wameishikilia Iymaan yao kwa dhati kabisa juu ya madhila makubwa, ambapo watu wenye Iymaan dhaifu na yenye kuyumba, na makafiri na wanafiki, watafuata amri zake huyo Masiyh Ad-Dajjaal. Huyo ataitwa Masiyh na Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) pia anaitwa Masiyh. Ingawa matamshi ya haya majina mawili ni sawa, lakini maana zake hapo ni tofauti. Nabiy ‘Iysaa  (عليه السلام) anaitwa Masiyh kwa sababu aliwaponya wagonjwa kwa kuwagusa. Maana ya Masiyh ni kugusa. Lakini Ad-Dajjaal ataitwa Masiyh kwa sababu jicho lake moja limeguswa au limeharibiwa na kwa hivyo limegeuka umbo.

 

[59] Katika Ahaadiyth zingine maneno yafuatayo yameongezwa:

 

مِنَ المْغْـرَم وَالْمأْثَمِ

“Minal maghrami wal ma-athami” (dhidi ya madeni na mwenye dhambi). Imeripotiwa katika Al-Bukhaariy kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliulizwa kwamba kwa nini alikuwa anaomba hifadhi dhidi ya kuwa na madeni kwa namna hiyo? Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema kwamba: “Mtu mwenye deni siyo tu huwa anaongopa, bali pia huwa anavunja ahadi zake. Maafa ya maisha yapo kwenye mwisho wa maisha (huku mtu ukiwa huna Iymaan), na maafa ya kifo yapo katika ukali wa maswali aulizwayo mtu kaburini.”

 

[60] Huyu ndiye ‘Abdullaah bin ‘Uthmaan Abuu Quhaafah bin ‘Aamir bin At-Taymiy, ambaye ndiye Khalifa wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na mwenzi wake aliyekuwa naye pamoja pangoni, na ndiye mzuri kuliko watu wote wa Ummah huu baki ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mweyewe. Alikuwa mweupe na nywele za singa, mzuri na mwembamba. Anajulikana sana, na hahitaji kujulishwa. Alikufa mnamo Jumaada Al-Aakhir mwaka wa 13 A.H.

 

[61] Hadiyth hii inafahamisha kuwa, mwana Aadam anapaswa awe muombaji wa maghfirah hata kama amepata daraja la juu kabisa la taqwa, ukweli na ikhlasi.

 

[62] Kuna simulizi kutoka kwa Maswahaba kumi na tano wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuhusu Tasliym (kumalizia kwa Salaam). Baadhi ya hizo ni Swahiyh, zingine ni Hasan, na zingine ni dhaifu. Hakuna hata moja ya hizo zilikuwa na maneno ya

وَبَرَكاتُه

 “wa Barakaatuh.”

 

Kuna usimulizi mmoja tu kati ya hizi unaohesabika kuwa ni wa kuaminika na unakubalika.

[63] Maneno ya

ذَا اَلْجَدِّ مِنْكَ اَلْجَدُّ

Ina maana: “Endapo Kuridhia Kwako Allaah, hakupo, basi ukuu wote, ufakhari, na mali za kidunia zote, huwa hazina maana, yaani vitu vyovyote vya kidunia utakavyokuwa navyo (mali, vizazi, hadhi na uwezo), haisaidii katika uokovu. Uokovu utapatikana kutokana na Rahmah na Baraka Zako Wewe tu.”

 

[64] Sa’d bin Abiy Waqqaasw ndiye aliyepewa jina la utani la Abuu Is-haaq bin Maalik, na alikuwa ni Zuhri na Quraysh. Alikuwa ni Muislamu wa tano au wa saba, na ni mmoja wa wale watu kumi ambao waliahidiwa kuingia Jannah. Yeye ni mtu wa kwanza kupiga silaha katika njia ya Allaah, na alishiriki katika vita vyote muhimu. Alikomboa ‘Iraaq kwa ajili ya Uislamu, na du’aa zake zilitakabaliwa. Alikuwa mfupi, mnene, na mwenye nywele nyingi. Alifia Al-‘Aqiyq ambayo iko maili kumi kutoka Al-Madiynah, na alibebwa juu ya mabega ya watu hadi Al-Madiynah, na akazikwa Al-Baqi’y mnamo mwaka 55 H.

 

[65] Maana ya

أَرْذَلِ اَلْعُمُرِ

Ni pale uzee unamfikia mtu anapokuwa uwezo wa ndani ya mwili wake au nje yake, na akili, unadhoofika ima wote au baadhi yake.   

[66] Kuonyesha kutubu na kuomba maghfirah kwa Allaah (سبحانه وتعالى) baada ya kumaliza Swalaah, ni dalili ya kuwa Swalaah ya mtu anayoswali haina hadhi ya kuiwakilisha mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى), khasa kwa vile mja huwa amekwisha kutenda makosa, ukhalifu na dosari katika Swalaah yake.

 

[67] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alionyesha kutubu na aliomba maghfirah kwa Allaa (سبحانه وتعالى) kama njia ya kutoa shukrani kwa Allaah (سبحانه وتعالى), pamoja na kuwafundisha watu maadili mema. Basi na Muumini wa kawaida naye hufanya vivyo hivyo kutubia kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kutokana na utovu wa khushuw’ (unyenyekevu) kwa kumjia fikra na mawazo yanayomtoa nje ya Swalaah na kumweka mbali wakati anaswali.

 

[68] Adkhaar hizi zinawakilisha mambo yote mazuri ya dunia hii na Aakhirah. Inaelekea kuwa mtu sharti atamke Adhkaar baada ya kila Swalaah ya fardhi na Swalaah ya Sunnah. Lakini baadhi ya Wanachuoni wamependekeza kusoma Adkhaar hizi katika Swalaah za fardhi tu. Kwa hivyo umuhimu wa du’aa baada ya Swalaah za fardhi umethibitishiwa, lakini Ahaadiyth hazithibitishi kuwepo kwa kusoma Adhkaar hizi au du’aa zozote zile kwa pamoja (kwa jamaa) wala kwa kuinua mikono juu. Bali kila mtu anatakiwa asome Adhkaar hizi na du’aa zake binafi peke yake na bila ya kuinua mikono.

[69] Abuu Umaamah ndiye Iyaas bin Tha’labah Al-Balawiyy na Swahibu wa Banu Haarithah wa wa Answaar. Yeye ni Swahaba, na alisimulia Hadiyth nyingi. Hakushiriki katika vita vya Badr kwa kuwa alikuwa akimuuguza Mama yake.

 

[70] Aayatul-Kursiyy ni ya katika Suwrah Al-Baqarah (2: 255).

  

[71] Hii inamanisha kuwa ataingia Jannah mara atakapofariki.  Yaani, kinachomzuia kuingia Jannah ni kuweko kwake duniani. 

 

[72] Umuhimu wa Aayatul-Kursiyy ni kutokana na Aayah hii kuweko Majina ‘Adhimu kabisa na Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) na pia yanaelezea Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) ambayo Yeye Anapenda zaidi Apwekeshwe. Suwrah Ikhlaasw pia ina Majina na Sifa kama hizo.

 

[73] Suwrah Ikhlaasw ni Suwrah namba (112).

 

[74] Hadiyth hii Swahiyh na ‘adhimu inatuambia kuwa kauli zote na matendo yote ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni maelezo ya kutulengea, kutuongoza na kutuamrisha kutekeleza Swalaah kama ilivyoamrishwa katika Qur-aan na Sunnah.  Juu ya hivyo, ni dalili kwamba Muislamu anapaswa lazima afuate Sunnah za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika ‘ibaadah zake zote katika kila kitendo na kauli. Hivyo basi matendo yote aliyoyatenda Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kauli zote alizotamka katika Swalaah ni waajib kwetu isipokuwa zile ambazo zimethibitishwa vinginevyo kwa dalili ya wazi kabisa.

 

[75] Endapo mtu yoyote, kwa sababu zisizokuwa za maradhi, hawezi kusimama wima, anaruhusiwa yeye kuswali huku amekaa, kama ambavyo mtu hufanya akiwa katika safari ya treni, ilimradi awe akikamilisha vizuri vitendo vya kurukuu na kusujudu. Akiwa hawezi kufanya hivyo kwa sababu ya maradhi, lazima afanye hivyo kwa kuashiria na kuinama. Akiwa anataka kusujudu mathalani, ni lazima ainamishe kichwa chake mbali zaidi kuliko kuinamisha kwa ajili ya kurukuu. Hii imeripotiwa katika Hadiyth iliyosimuliwa na Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).

Share

08-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Sajdatus-Sahw Na Nyingine

 

بُلُوغُ الْمَرام

 

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

 

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ سُجُودِ اَلسَّهْوِ وَغَيْرِهِ

 

08-Mlango Wa Sajdatus-Sahw[1] Na Nyingine

 

 

 

 

263.

عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ بُحَيْنَةَ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  صَلَّى بِهِمُ الظُّهْرَ ، فَقَامَ فِي اَلرَّكْعَتَيْنِ اَلْأُولَيَيْنِ ، وَلَمْ يَجْلِسْ ، فَقَامَ اَلنَّاسُ مَعَهُ ، حَتَّى إِذَا قَضَى اَلصَّلَاةَ ، وَانْتَظَرَ اَلنَّاسُ تَسْلِيمَهُ ، كَبَّرَ وَهُوَ جَالِسٌ . وَسَجَدَ سَجْدَتَيْنِ ، قَبْلَ أَنْ يُسَلِّمَ ، ثُمَّ سَلَّمَ}  أَخْرَجَهُ اَلسَّبْعَةُ ، وَهَذَا لَفْظُ اَلْبُخَارِيِّ

وَفِي رِوَايَةٍ لمُسْلِمٍ :{يُكَبِّرُ فِي كُلِّ سَجْدَةٍ وَهُوَ جَالِسٌ وَسَجَدَ اَلنَّاسُ مَعَهُ ، مَكَانَ مَا نَسِىَ مِنَ الْجُلُوسِ} 

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buhaynah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaswalisha Adhuhuri, akasimama mwisho wa Rakaa mbili za mwanzo na hakuketi chini.[2] Watu walimfuata wakasimama pamoja naye. Swalaah ilipomalizika, watu wakangojea atoe salaam. Akapiga Takbiyra hali akiwa ameketi. Huku akiwa amekaa, akasujudu Sajdah mbili kabla hajatoa salaam,[3], kisha akatoa salaam.” [Imetolewa na As-Sab’ah (Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad), na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipiga Takbiyra kwa kila Sajdah alipiga akiwa amekaa. Kisha alisujudu na Maamuma wote walisujudu pamoja naye kwa kufidia kule kuketi alikosahau.”

 

 

 

264.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ قَالَ :{صَلَّى اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  إِحْدَى صَلَاتِي اَلْعَشِيِّ  رَكْعَتَيْنِ ، ثُمَّ سَلَّمَ ، ثُمَّ قَامَ إِلَى خَشَبَةٍ فِي مُقَدَّمِ اَلْمَسْجِدِ ، فَوَضَعَ يَدَهُ عَلَيْهَا ، وَفِي اَلْقَوْمِ أَبُو بَكْرٍ وَعُمَرُ ، فَهَابَا أَنْ يُكَلِّمَاهُ ، وَخَرَجَ سَرَعَانُ اَلنَّاسِ ، فَقَالُوا : أَقُصِرَتْ . الصَّلَاةُ ، وَرَجُلٌ يَدْعُوهُ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  ذَا اَلْيَدَيْنِ ، فَقَالَ : يَا رَسُولَ اَللَّهِ ، أَنَسِيتَ أَمْ قُصِرَتْ ؟ فَقَالَ : " لَمْ أَنْسَ وَلَمْ تُقْصَرْ " فَقَالَ : بَلَى ، قَدْ نَسِيتُ ، فَصَلَّى رَكْعَتَيْنِ ثُمَّ سَلَّمَ ، ثُمَّ كَبَّرَ ، فَسَجَدَ مِثْلَ سُجُودِهِ ، أَوْ أَطْوَلَ ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ فَكَبَّرَ ، ثُمَّ وَضَعَ رَأْسَهُ ، فَكَبَّرَ ، فَسَجَدَ مِثْلَ سُجُودِهِ ، أَوْ أَطْوَلَ .  ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ وَكَبَّرَ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ

وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ :{صَلَاةُ اَلْعَصْرِ}

وَلِأَبِي دَاوُدَ ، فَقَالَ :{أَصَدَقَ ذُو اَلْيَدَيْنِ ؟ " فَأَوْمَئُوا : أَيْ نَعَمْ}

وَهِيَ فِي " اَلصَّحِيحَيْنِ " لَكِنْ بِلَفْظِ : فَقَالُوا  وَهِيَ فِي رِوَايَةٍ لَهُ :{وَلَمْ يَسْجُدْ حَتَّى يَقَّنَهُ اَللَّهُ تَعَالَى ذَلِكَ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalisha Rakaa mbili za Swalaah mojawapo kati ya mbili za Al-‘Ashiyy (yaani Adhuhuri au Alasiri), kisha akatoa salaam. Akasimama karibu na kipande kimoja cha ubao kilichokuwa mbele ya Msikiti akaweka mkono wake juu yake. Abuu Bakr na ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) walikuwa miongoni mwa watu waliokuwepo pale, wakaogopa kumsemesha lolote Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Wenye haraka wakatoka na wakasema Swalaah imefupishwa. Miongoni mwa watu hao alikuwepo mtu ambaye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akimwita Dhul-Yadayn[4] (mtu mwenye mikono mirefu), akauliza: Ee Rasuli wa Allaah! Umesahau au Swalaah imefupishwa? Akasema: “Sijasahau[5] wala haijafupishwa.” Akasema: “Bali umesahau.”[6], Kisha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaswali Rakaa mbili zilizobakia, kisha akatoa salaam. Akapiga Takbiyra, akasujudu kama anavyosujudu Sajdah yake kawaida au ndefu zaidi. Kisha akainua kichwa chake na akatamka Takbiyra[7], akasujudu, akapiga Takbiyra, akasujudu kama Sajdah yake ya kawaida au ndefu zaidi. Akainua kichwa chake na akapiga Takbiyra.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Swalaah ya Alasiri.”

 

Na katika upokezi wa Abuu Daawuwd: “Je Dhul-Yadayn amesema kweli? Nao wakasema “Ndio” kwa kuashiria.   

Na hiyo imo katika Swahiyhayn lakini kwa neno  فَقالوا(wakasema). Na katika mapokezi yake (Abuu Daawuwd) mengine: “Hakusujudu hadi Allaah (تعالى) alipompa uhakika wa hilo.”

 

 

 

265.

وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  صَلَّى بِهِمْ ، فَسَهَا فَسَجَدَ سَجْدَتَيْنِ ، ثُمَّ تَشَهَّدَ ، ثُمَّ سَلَّمَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ ، وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ

Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaswalisha wao, akasahau kitu. Akasujudu Sajdah mbili, akasoma, kisha akatoa Tashahhud na salaam.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy aliipa daraja la Hasan, na Al-Haakim akaipa daraja la Swahiyh]

 

 

 

266.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {إِذَا شَكَّ أَحَدُكُمْ فِي صَلَاتِهِ ، فَلَمْ يَدْرِ كَمْ صَلَّى أَثْلَاثًا أَوْ أَرْبَعًا ؟ فَلْيَطْرَحِ الشَّكَّ وَلْيَبْنِ عَلَى مَا اسْتَيْقَنَ ، ثُمَّ يَسْجُدُ سَجْدَتَيْنِ قَبْلَ أَنْ يُسَلِّمَ ، فَإِنْ كَانَ صَلَّى خَمْساً شَفَعْنَ لَهُ صَلَاتَهُ ، وَإِنْ كَانَ صَلَّى تَمَامًا  كَانَتَا تَرْغِيمًا لِلشَّيْطَانِ"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akitia shaka katika Swalaah yake, hajui Rakaa ngapi ameswali, ni tatu au nne, basi aache mashaka na ajengee idadi aliyo na yakini nayo[8]. Kisha asujudu Sajdah mbili kabla hajatoa salaam. Ikiwa aliswali Rakaa tano, basi Swalaah yake itamuombea[9], na ikiwa aliswali Rakaa nne kamili zitakuwa zimemtahayarisha shaytwaan.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

267.

وَعَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  قَالَ:{صَلَّى رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  فَلَمَّا سَلَّمَ قِيلَ لَهُ : يَا رَسُولَ اَللَّهِ ، أَحَدَثَ فِي اَلصَّلَاةِ شَيْءٌ ؟ قَالَ : " وَمَا ذَلِكَ ؟ " .  قَالُوا : صَلَّيْتَ كَذَا ، قَالَ : فَثَنَى رِجْلَيْهِ وَاسْتَقْبَلَ اَلْقِبْلَةَ ، فَسَجَدَ سَجْدَتَيْنِ ، ثُمَّ سَلَّمَ ، ثُمَّ أَقْبَلَ عَلَيْنَا بِوَجْهِهِ فَقَالَ: " إِنَّهُ لَوْ حَدَثَ فِي اَلصَّلَاةِ شَيْءٌ أَنْبَأْتُكُمْ بِهِ ، وَلَكِنْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِثْلُكُم، أَنْسَى كَمَا تَنْسَوْنَ ، فَإِذَا نَسِيتُ فَذَكِّرُونِي ، وَإِذَا شَكَّ أَحَدُكُمْ فِي صَلَاتِهِ فَلْيَتَحَرَّ اَلصَّوَابَ ، فلْيُتِمَّ عَلَيْهِ ، ثُمَّ لِيَسْجُدْ سَجْدَتَيْنِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَفِي رِوَايَةٍ لِلْبُخَارِيِّ:{ فَلْيُتِمَّ ، ثُمَّ يُسَلِّمْ ، ثُمَّ يَسْجُدْ} 

وَلِمُسْلِمٍ :{أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  سَجَدَ سَجْدَتَيْ اَلسَّهْوِ بَعْدَ اَلسَّلَامِ وَالْكَلَامِ}

وَلِأَحْمَدَ ، وَأَبِي دَاوُدَ ، وَالنَّسَائِيِّ ; مِنْ حَدِيثِ عَبْدِ بْنِ جَعْفَرٍ مَرْفُوعاً:{مَنْ شَكَّ فِي صَلَاتِهِ ، فَلْيَسْجُدْ سَجْدَتَيْنِ بَعْدَمَا يُسَلِّمُ} وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa Ibn Mas‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalisha, na alipotoa salaam aliulizwa: Ee Rasuli wa Allaah! Kuna jambo jipya limetokea katika Swalaah? Akasema: “Kitu gani?” Wakasema: “Umeswali Rakaa kadhaa.” Hapo akakunja miguu yake akaeleka Qiblah na akasujudu Sajdah mbili, akatoa salaam. Akaelekea watu akasema: “Endapo kitu kipya kingeletwa katika Swalaah, ningekujulisheni, lakini mimi ni mwana Aadam kama nyinyi,[10] ninasahau kama nyinyi mnavyosahau. Kwa hivyo nikisahau mnikumbushe. Na ikiwa yeyote kati yenu ana mashaka katika Swalaah yake, basi afuate lililo sawa na aikamilishe, kisha alete Sajdah mbili.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika mapokezi ya Al-Bukhaariy: “Akamilishe (Swalaah yake) kisha atoe salaam, kisha asujudu.”

 

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisujudu Sajdah mbili za Sahw baada ya kutoa salaam na kuongea.”

 

Na katika mapokezi ya Ahmad, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy kutokana Hadiyth Marfuw’ ya ‘Abdullaah bin Ja’far[11] ilisema: “Mwenye kutia shaka katika Swalaah yake, basi asujudu sijda mbili baada ya salaam.” [Akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

268.

وَعَنِ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  قَالَ {إِذَا شَكَّ أَحَدُكُمْ ، فَقَامَ فِي اَلرَّكْعَتَيْنِ ، فَاسْتَتَمَّ قَائِمًا ، فَلْيَمْضِ ، وَلْيَسْجُدْ سَجْدَتَيْنِ ، وَإِنْ لَمْ يَسْتَتِمْ قَائِمًا فَلْيَجْلِسْ وَلَا سَهْوَ عَلَيْهِ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَابْنُ مَاجَهْ ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ ، وَاللَّفْظُ لَهُ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa Al-Mughiyrah bin Shu’bah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Endapo mmoja wenu atapata mashaka akasimama katika Rakaa mbili, akikumbuka wakati ameshasimama basi aendelee[12] na asirejee kwenye kukaa, na asujudu katika Sajdah mbili. Lakini endapo hakuwahi kusimama wima kabisa basi akae na hana Sajdah mbili za kusahau.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, Ibn Maajah na Ad-Daaraqutwniy na tamshi ni lake, kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

269.

وَعَنْ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  قَالَ :{لَيْسَ عَلَى مَنْ خَلَفَ اَلْإِمَامَ سَهْوٌ فَإِنْ سَهَا اَلْإِمَامُ فَعَلَيْهِ وَعَلَى مَنْ خَلْفَهُ"} رَوَاهُ اَلْبَزَّارُ وَالْبَيْهَقِيُّ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna Sijdatus-sahw kwa anayeswali[13] nyuma ya Imaam, Imaam akisahau, ni juu yake na juu ya Imaam na wanaomfuata kuileta.” [Imetolewa na Al-Bazzaar na Al-Bayhaqiyy kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

270.

وَعَنْ ثَوْبَانَ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {لِكُلِّ سَهْوٍ سَجْدَتَانِ بَعْدَمَا يُسَلِّمُ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَابْنُ مَاجَهْ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa Thawbaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kila sahau ni Sajdah mbili baada ya salaam.[14][Imetolewa na Abuu Daawuwd, na Ibn Maajah kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

271.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  قَالَ: {سَجَدْنَا مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  فِي : ( إِذَا اَلسَّمَاءُ اِنْشَقَّتْ ) ، و : ( اِقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ )} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulisujudu pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akisoma Suwrah:[15]

إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾[16],

na

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ[17]

 .” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

272.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {( ص ) لَيْسَتْ مِنْ عَزَائِمِ اَلسُّجُودِ ، وَقَدْ رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يَسْجُدُ فِيهَا} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutokwa kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Kusujudu wakati inaposomwa Suwrah Swaad[18] si katika ‘azaaaim (zilizoamrishwa kusujudu)[19], lakini nilimuona Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisujudu katika Suwrah hiyo.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

273.

وَعَنْهُ: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  سَجَدَ بِالنَّجْمِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) tena amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisujudu kwa kusoma Suwrah An-Najm.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

274.

وَعَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  قَالَ: {قَرَأْتُ عَلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  اَلنَّجْمَ ، فَلَمْ يَسْجُدْ فِيهَا}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Zayd bin Thaabit[20] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilisoma mbele ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Suwrah An-Najm[21], na hakusujudu ndani yake.[22][Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

275.

وَعَنْ خَالِدِ بْنِ مَعْدَانَ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  قَالَ: {فُضِّلَتْ سُورَةُ اَلْحَجِّ بِسَجْدَتَيْنِ}  . رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ فِي " اَلْمَرَاسِيلِ "

وَرَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ مَوْصُولًا مِنْ حَدِيثِ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ ، وَزَادَ: {فَمَنْ لَمْ يَسْجُدْهُمَا ، فَلَا يَقْرَأْهَا} وَسَنَدُهُ ضَعِيفٌ

Kutoka kwa Khaalid bin Ma’daan[23] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Suwrah Al-Hajj[24] imefadhilishwa kwa kuwa na Sajdah mbili.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd katika Al-Maraasiyl]

 

Na waliipokea Ahmad na At-Tirmidhiy katika Hadiyth Mawsuwl kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir, akaongezea: “Asiyesujudu Sajdah hizo mbili (za Suwrah Al-Hajj), basi asiisome.” [Isnaad yake ni dhaifu]

 

 

 

276.

وَعَنْ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  قَالَ: {يَا أَيُّهَا اَلنَّاسُ إِنَّا نَمُرُّ بِالسُّجُودِ فَمَنْ سَجَدَ فَقَدْ أَصَابَ ، وَمَنْ لَمْ يَسْجُدْ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ}  . رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ . وَفِيهِ: {إِنَّ اَللَّهَ تَعَالَى لَمْ يَفْرِضْ اَلسُّجُودَ إِلَّا أَنْ نَشَاءَ} . وَهُوَ فِي " اَلْمُوَطَّأِ

Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Enyi watu, katika visomo vyetu tunapita Aayah za kusujudu. Hivyo, anayesujudu amefanya sawa na asiyesujudu hana dhambi.[25][Imetolewa na Al-Bukhaariy] na ndani yake kuna: “Allaah (تعالى)    Hakufaradhisha kusujudu, ila tukipenda.” [Ipo katika kitabu Al-Muwatwa’ cha Imaam Maalik]

 

 

 

277.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {كَانَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  يَقْرَأُ عَلَيْنَا اَلْقُرْآنَ ، فَإِذَا مَرَّ بِالسَّجْدَةِ ، كَبَّرَ ، وَسَجَدَ ، وَسَجَدْنَا مَعَهُ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِسَنَدٍ فِيهِ لِيِنٌ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitusomea Qur-aan, na kila alipofika mahali pa kusujudu alipiga Takbiyra na akasujudu, nasi tukasujudu pamoja naye.[26][Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad laini]

 

 

 

278.

وَعَنْ أَبِي بَكْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   كَانَ إِذَا جَاءَهُ أَمْرٌ يَسُرُّهُ خَرَّ سَاجِداً لِلَّهِ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ

Kutoka kwa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa likimjia jambo lililomfurahisha anaporomoka, akisujudu.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy]

 

 

 

279.

وَعَنْ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  قَالَ: {سَجَدَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  فَأَطَالَ اَلسُّجُودَ ، ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ وَقَالَ: " إِنَّ جِبْرِيلَ آتَانِي ، فَبَشَّرَنِي ، فَسَجَدْت لِلَّهِ شُكْرًا"} رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf[27] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisujudu na akarefusha Sajdah, kisha akainua kichwa chake akasema: “Jibriyl amekuja na akanibashiria habari nzuri, kwa hiyo nimesujudu kumshukuru Allaah.” [Imetolewa na Ahmad, na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

280.

وَعَنْ اَلْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  بَعَثَ عَلِيًّا إِلَى اَلْيَمَنِ  فَذَكَرَ اَلْحَدِيثَ  قَالَ : فَكَتَبَ عَلِيٌّ رَضِيَ اَللَّهُ  عَنْهُ  بِإِسْلَامِهِمْ ، فَلَمَّا قَرَأَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  اَلْكِتَابَ خَرَّ سَاجِدًا}  رَوَاهُ اَلْبَيْهَقِيُّ  وَأَصْلُهُ فِي اَلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtuma ‘Aliy kwenda Yaman. Msimuliaji akaitaja Hadiyth.[28] Alisema: “’Aliy akaandika barua kuhusu kusilimu kwao. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasoma barua hiyo akasujudu kumshukuru[29] Allaah (تعالى)    kwa ajili ya hilo.” [Imetolewa na Al-Bayhaqiyy na chanzo chake kimo katika Al-Bukhaariy]

 

[1] Sijdatus-sahw (Sajdah ya kusahau) huwa ni waajib iwapo mtu anayeswali anaongeza au anapunguza tendo fulani ndani ya Swalaah kwa makosa.

 

[2] Yapasa tuelewe kwamba tafsiri ya maneno ya kiarabu “Sahw” na “Nisyaan” ni “Kusahau”. Lakini “Sahw” inamaanisha kutenda mambo zaidi, na “Nisyaan” kwa kawaida inamaanisha sehemu ndogo ya taarifa. Lakini maneno yote haya mawili yanahesabika kuwa ni visawe, yaani moja ni sawasawa na jingine. Miongoni mwa ‘Ulamaa, hakuna hata mmoja anayelitumia neno “Nisyaan” kwa ajili ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Kwa hivyo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kamwe hakuwahi kuugua maradhi ya kuchanganyikiwa katika mambo yahusuyo kulingania Risala ya Uislamu. Angewezaje kuugua maradhi kama hayo wakati Allaah, Anasema katika Suwrah Al-A’laa:

سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰ ﴿٦﴾

Tutakusomesha (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi hutoisahau

 [Al-A’laa: 6].

 

‘Ulamaa waadilifu wanasema kuwa, matumizi ya neno ‘Sahw’ kwa ajili ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) inaruhusiwa kwa kuwa zipo rejea nyingi kutoka katika Hadiyth nyingi kuhusu kadhia hii. Maimaamu wote wane wanaafiki kwamba, mazingira yanayohusu kusahau (Sahw) kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) yamethibitishwa. Hakuna ubaya katika hili; bali kuna niyyah njema (inamaanisha, usahau wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)).

 

[3] Hadiyth hii inatufunza kuwa, mtu anaweza kufidia katika kuacha Tashahhud ya kwanza kwa kuleta Sijdatus-Sahw. Wengine wanasema iletwe kabla ya Salaam, na wengine wanasema iletwe baada ya Salaam. Hali zote hizi mbili zina ushahidi kutoka kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ambaye hakuweka kanuni thabiti kuhusu hili. Katika kitabu cha Niyl Al-Awtwaar kuwa endapo kumeondoshwa jambo ndani ya Swalaah basi Sajdah iletwe baada ya Salaam. Wanazuoni wengine wanasema kuwa, ushahidi wa Sajdah kabla ya Salaam ni sahihi na sawa zaidi.

 

[4] Huyu Dhul-Yadayn ndiye Al-Khirbaq bin ‘Amr As-Sulaymiy wa kabila la Baniy Sulaym. Alifariki zama za Ukhalifa wa Mu’aawiyah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Inasemekana pia kuwa alifia kule Dhi Khashab zama za Ukhalifa wa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Alikuwa na mikono mirefu mno; ndiyo maana akaitwa kiutani Dhul-Yadayn

 

[5] Kwa mujibu wa ufahamu wangu, sijaugua usahaulifu wala haikuja amri la Shariy’ah kwa Swalaah kufupishwa.

 

[6] Usahaulifu wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiwa ndani ya Swalaah, juu ya ukweli kwamba alikuwa kazama sana katika tafakuri wakati akiomba Du’aa kwa Allaah (سبحانه وتعالى) inaweza kueleweka kikweli kuwa ilikuwa tendo la haki na lilikuwa kwa niyyah njema. Kwanza tendo lile lilikuwa la kuuelimisha Ummah kimatendo juu ya mambo yanayohusu kusahau (Sahw) na ni yapi maagizo yake na jinsi ya kuyarekebisha pindi mtu yeyote atakabiliwa na hali kama ile. Pili, alitaka kuufundisha Ummah kwamba, juu ya heshima zake, hadhi, na nafasi ya juu sana ya kuwa zaidi kuliko viumbe wote, na yeye ni mwana Aadam, na amerithi hisia zote za kibinadamu kwa mfano kula, kunywa, kulala, kuamka, kutembea tembea, kwenda haja, kupata magonjwa na kuponywa, n.k. sifa zote zilizotajwa hapo juu zimedhihirishwa kwa nafsi yake. Yeye mwenyewe alilitaja jambo hili la busara na kama hilo litakalotajwa katika Hadiyth iliyosimuliwa na Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).

 

[7] Hadiyth hii inaweka wazi kwamba, pindi mtu akifikiri ana hakika amekamilisha Swalaah yake, anatoa Salaam, anaanza hata kuzungumza, na kisha ghafla anatambua kosa lake kwa kukumbuka yeye mwenyewe au mtu mwingine anamkumbusha kosa lake, Swalaah yake inabakia kuwa sahihi ilimradi tu aikamilishe mara moja.

 

[8] Hii ina maana mbili: Kwanza, kukiweko mashaka, mtu achukue namba ndogo zaidi. Kwa mfano, akiwa hana hakika ameshaziswali Rakaa tatu au nne, basi achukulie kuwa ni Rakaa tatu, kwani hii ni karibu zaidi na ukweli. Pili afanye lile ambalo ana hakika zaidi kuwa ndiyo sawa.

 

[9] Inamaanisha kuwa iwapo mtu kaziswali Rakaa tano, zitakuwa sita kwa kujumlisha na Sijdatus-Sahw. Inaonekana kutoka katika Hadiyth hii kuwa mtu sharti awe akichukulia namba ya Rakaa ya chini zaidi, kwani hiyo ndiyo huwa karibu zaidi na ukweli.

 

[10] Kwa mujibu wa rejea hii, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitumia maneno ya:

" إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِثْلُكُم "

 

((Mimi ni mwanadamu kama nyinyi).”

 

Hii huenda itawashangaza sana watu wasiomchukulia yeye  kama mwana Aadam, na wanadai kuwa kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى)  katika Qur-aan:

إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ

 

 “Hakika mimi ni mtu kama nyinyi;” [Fusw-Swilat: 6],

 

Unawania kuwanyamazisha tu washirikina wengi, ambapo ukweli ni kwamba watu wanaohusika hapa ni Waumini na wala sio washirikina.

 

[11] ‘Abdullaah bin Ja’far ndiye Abuu Ja’far ‘Abdullaah bin Ja’far bin Abiy Twaalib, na mama yake ni Asmaa’ bint ‘Umays. Huyu ni Mwislamu wa mwanzo kuzaliwa kule Abyssinia, na baba yake alitoka Al-Madiynah mnamo mwaka wa 7 A.H. alikuwa mcheshi sana, mwenye taqwa, na mkarimu sana. Alikuwa mkarimu kuliko wote miongoni mwa Waislamu. Alifariki Al-Madiynah mnamo mwaka 80 A.H. akiwa na umri wa miaka 80.

 

[12] Endapo mtu amesahau kusoma Tashahhud ya kati na akasimama wima kabisa, lazima aendelee na Swalaah yake. Lakini akiwa hakuwahi kusimama wima kikamilifu, achunguze kama yuko karibu na kusimama au karibu na kukaa. Akiwa karibu zaidi na kusimama, lazima asimame na alete Sijdatus-Sahw. Akiwa karibu na kukaa basi lazima akae chini kabisa, asome Tashahhud, na hana haja ya kuleta zile Sajdah mbili za Sahw.

 

[13] Hadiyth hii inatufunza kwamba, kuleta Sijdatus-Sahw huwa ni lazima kwa Muqtadi (mtu anayeswalishwa yaani Maamuma) pale tu ambapo Imaam kasahau, na wala siyo ikiwa yeye mtu mwenyewe kasahau.

 

[14] Hadiyth hii haina maana ya kuwa endapo mtu kafanya makosa mawili au manne, basi lazima alete Sijdatus-Sahw mbili kwa kila kosa. Inamaanisha tu kwamba, bila kujali aina na wingi wa makosa ambayo mtu kayafanya, Sajdah mbili tu zinatosheleza kufidia makosa yote. (Baadhi ya Wanazuoni wanaona kuwa Hadiyth hii inakubalika. Tazama Subulus-Salaam, (1/418-419), namba (319) na Irwaa’ Al-Ghaliyl, (2/47- 48) namba (339).

 

[15] Kama Sijdatut-Tilaawa (Sajdah ya kusoma baada ya Aayah maalumu za Qur-aan) itahesabika kama Mashruw’ (ya kuamrishwa), Sunnah (ya khiayri), au Waajib (ya kuwajibika), Wanazuoni wengi wanahesabu ile ni Sunnah, lakini Imaam Abuu Haniyfah amesema kuwa ni Waajib. Pia kuna kutofautiana maoni mtu sharti awe na wudhuu au hata akiwa hana wudhuu, anaweza kuleta Sajdah hii.

 

[16] Al-Inshiqaaq (84: 21)

 

[17]Al-‘Alaq (96: 19)

 

 

[18] Swaad  (38: 88)

 

[19] Kwa mujibu wa Imaam wengine, Sajdah hii ni lazima kama Sajdah zingine. Hadiyth hii inaashiria tu kwamba hii haikuamriwa kuwa iwe ni tendo la ‘Ibaadah; lakini Sajdah hii inatekelezwa mpaka sasa ikiwa kama ukumbusho wa mwenendo wa Nabiy Daawuwd  (عليه السلام) .

 

[20] Zayd bin Thaabit ni Answaar na Najjaar, alipewa jina la utani la Abuu Sa’iyd au Abuu Khaarijah. Alikuwa muandishi mzuri wa Qur-aan, na alijua sana elimu ya Mirathi. Alipigana kwanza katika vita vya Al-Khandaq. Alikusanya Qur-aan zama za Ukhalifa wa Abuu Bakr, na aliinakili katika Ukhalifa wa ‘Uthmaan. Alijifunza maandishi ya Kiyahudi kwa nusu mwezi. Kwa amri ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na alikuwa akimuandikia na kumsomea maandishi hayo. Alifia Al-Madiynah mnamo mwaka wa 45 A.H. Imesemekana pia kuwa alikufa katika mwaka mwingine.

 

[21] An-Najm (53: 62).

 

[22] Hii ndiyo maana Wanazuoni wameihesabu Sijdatut-Tilaawah inayofanywa wakati wa kusoma Aayah maalumu za Qur-aan kuwa ni Sunnah, kwa sababu Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuitekeleza hii mara zote. Wakati mwingine alisujudu, na wakati mwingine hakuisujudu kabisa.

 

[23] Khaalid bin Ma’daan ndiye Abuu ‘Abdillaah Al-Kalaa’i kutoka Hims, Syria. Alikuwa miongoni mwa kizazi cha Taabi’iy (watu waliokuja baada ya Maswahaba) maarufu na wenye elimu na ujuzi sana. Alisema kuwa aliwahi kukutana na Maswahaba sabini wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alifariki mwaka 103 au 104 au 108 A.H

 

[24] Al-Hajj (22:  18 , 77).

 

[25] Hadiyth hii ni ushahidi wa wazi kuwa Sijdatut-Tilaawah siyo tendo la lazima. ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alisema hivyo alipokuwa akiwahutubia Maswahaba waliokusanyika kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na hakuna hata mmoja kati yao aliyenena neno juu yake, hiyo ilithibitisha kuwa wote walibaki kimya kuhusu jambo hili.

 

[26] Hii inatufahamisha kuwa kusujudu ni waajib wa msomaji na hata msikilizaji, kwa sharti kwamba watu wawe ndani ya Swalaah. Na vivyo hivyo huwa kwa Sijdatut-Tilaawah (Sajdah ndani ya kisomo) na Sajdah Ash-Shukr.

 

[27] ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf (رضي الله عنه) ndiye aitwaye Abuu Muhammad Az-Zuhriy Al-Qarayshiy. Alisilimu mapema, akahamia Abyssinia mara mbili. Alishiriki katika vita vya Badr na vita vingine vikubwa. Huyu ni mmoja katika wale watu kumi walioahidiwa Jannah, na ni mmoja wa watu sita ambao ‘Umar (رضي الله عنه)  aliwateua kuwa Makhalifa baada yake. Alitoa dinari elfu nne, kisha elfu arubaini, na kisha farasi mia tano na ngamia mia tano waliobebeshwa kama Swadaqah wakati Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akingali hai. Aliacha wasia wa bustani la thamani ya elfu mia nne kwa “Akina Mama wa Waumini.” Alikufa mnamo mwaka wa 34 A.H. na akazikwa Al-Baqi’.

 

[28] Imeripotiwa kuwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikwenda Yemen na watu wake mia tatu. Akawaita Wayemeni kusilimu. Jibu la Wayemeni lilikuwa kuwashambulia akina ‘Aliy kwa mishale, ‘Aliy alijibu mashambulizi yale, na wanaharakati wake maarufu 20 wakauliwa. Kukazuka mfarakano katika kambi ya ‘Aliy, na wengine wakakimbia kutoka uwanja wa vita. Wakaitwa kusilimu mara ya pili, nao wakakubali. ‘Aliy alikutana na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kule Makkah wakati wa Hijjah, mwaka ule ule, baada ya kurejea salama toka katika ujumbe huo.

 

[29] Hii inatoa jibu watu wale wasioamini usahihi uliothibitishwa wa Sajdah Ash-Shukr

 

 

Share

09-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Swalaah Za Sunnah

 

بُلُوغُ الْمَرام

 

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

 

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ صَلَاةِ اَلتَّطَوُّعِ

 

09-Mlango Wa Swalaah Za Sunnah

 

 

 

 

 

281.

  عَنْ رَبِيعَةَ بْنِ كَعْبٍ الْأَسْلَمِيِّ  رِضَى اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: {قَالَ لِي اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم   سَلْ . فَقُلْتُ : أَسْأَلُكَ مُرَافَقَتَكَ فِي اَلْجَنَّةِ . فَقَالَ: أَوَغَيْرَ ذَلِكَ  ؟ ، قُلْتُ: هُوَ ذَاكَ ، قَالَ: " فَأَعِنِّي عَلَى نَفْسِكَ بِكَثْرَةِ اَلسُّجُودِ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Rabiy’ah bin Ka’b Al-Aslamiyy[1] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliniambia: “Omba.” Nikasema: “Ninakuomba niwe pamoja nawe Jannah.” Aksema: “Hakuna zaidi ya hilo?” Nikasema: “Hilo tu basi.” Akasema: “Basi nisaidie mimi juu ya nafsi yako[2] kwa kukithirisha kusujudu.” (Yaani Swalaah)[3] [Imetolewa na Muslim][4]

 

 

 

282.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا  قَالَ : {حَفِظْتُ مِنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم   عَشْرَ رَكَعَاتٍ : رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ اَلظُّهْرِ ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَهَا ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ اَلْمَغْرِبِ فِي بَيْتِهِ ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ اَلْعِشَاءِ فِي بَيْتِهِ ، وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ اَلصُّبْحِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَفِي رِوَايَةٍ لَهُمَا: {وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ اَلْجُمْعَةِ فِي بَيْتِهِ}

وَلِمُسْلِمٍ: {كَانَ إِذَا طَلَعَ اَلْفَجْرُ لَا يُصَلِّي إِلَّا رَكْعَتَيْنِ خَفِيفَتَيْنِ} 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nimehifadhi kutoka kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Rakaa kumi (za Sunnah): Rakaa mbili kabla ya Adhuhuri, na mbili baada yake; Rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na Rakaa mbili baada ya ‘Ishaa nyumbani kwake; na Rakaa mbili kabla ya Alfajiri.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika mapokezi yao (Al-Bukhaariy, Muslim) mengine: “Rakaa mbili baada ya Ijumaa nyumbani kwake.”

 

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Haswali baada ya kutoka jua ila Rakaa mbili khafifu.”

 

 

 

283.

وَعَنْ عَائِشَةَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا : أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  { كَانَ لَا يَدَعُ أَرْبَعًا قَبْلَ اَلظُّهْرِ وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ اَلْغَدَاةِ}  رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Hakuacha Rakaa nne kabla ya Swalaah ya Adhuhuri, na Rakaa mbili kabla ya Swalaah ya Alfajiri.[5][Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

284.

وَعَنْهَا قَالَتْ: {لَمْ يَكُنْ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم   عَلَى شَيْءٍ مِنْ اَلنَّوَافِلِ أَشَدَّ تَعَاهُدًا مِنْهُ عَلَى رَكْعَتَيْ اَلْفَجْرِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَلِمُسْلِمٍ: {رَكْعَتَا اَلْفَجْرِ خَيْرٌ مِنْ اَلدُّنْيَا وَمَا فِيهَا}

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuwahi kukaza niyyah ya kuswali Rakaa mbili za Swalaah yoyote ya khiari kuliko Rakaa mbili kabla ya Alfajiri. [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Rakaa mbili za Alfajiri ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake.”

 

 

 

285.

وَعَنْ أُمِّ حَبِيبَةَ أُمِّ اَلْمُؤْمِنِينَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا  قَالَتْ : سَمِعْتَ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   يَقُولُ: {مَنْ صَلَّى اِثْنَتَا عَشْرَةَ رَكْعَةً فِي يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ بُنِيَ لَهُ بِهِنَّ بَيْتٌ فِي اَلْجَنَّةِ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ . وَفِي رِوَايَةٍ " تَطَوُّعًا"

وَلِلتِّرْمِذِيِّ نَحْوُهُ ، وَزَادَ: {أَرْبَعًا قَبْلَ اَلظُّهْرِ وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَهَا ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ اَلْمَغْرِبِ ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ اَلْعِشَاءِ ، وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ صَلَاةِ اَلْفَجْرِ}

وَلِلْخَمْسَةِ عَنْهَا: {مَنْ حَافَظَ عَلَى أَرْبَعٍ قَبْلَ اَلظُّهْرِ وَأَرْبَعٍ بَعْدَهَا حَرَّمَهُ اَللَّهُ عَلَى اَلنَّارِ}

Kutoka kwa Ummu Habiybah[6] Mama wa Waumini (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nimemsikia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Mwenye kuswali Rakaa kumi na mbili mchana na usiku atajengewa nyumba Jannah kwa sababu ya hizo Rakaa.” [Imetolewa na Muslim]

 

Katika mapokezi mengine: “…Za Sunnah….”

 

Na At-Tirmidhiy alisimulia hivyo hivyo ila akaongezea: “Rakaa nne kabla ya adhuhuri na mbili baada yake; na Rakaa mbili baada ya Magharibi, na Rakaa mbili baada ya ‘Ishaa, na Rakaa mbili kabla ya Swalaah ya Alfajiri.”

 

Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) wamepokea toka kwake (Ummu Habiybah): “Mwenye kuhifadhi (kuswali) Rakaa nne kabla ya Adhuhuri na nne baada yake, Allaah (تعالى)  Atamharamishia Moto.”

 

 

 

286.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {رَحِمَ اَللَّهُ اِمْرَأً صَلَّى أَرْبَعًا قَبْلَ اَلْعَصْرِ}  رَوَاهُ أَحْمَدُ ، وَأَبُو دَاوُدَ وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ ، وَابْنُ خُزَيْمَةَ وَصَحَّحَهُ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Anamrehemu mtu anayeswali Rakaa nne kabla ya Alasiri.[7][Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, na At-Tirmidhiy naye aliipa daraja la Hasan. Na Ibn Khuzaymah aliipa daraja la Swahiyh]

 

 

 

287.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ مُغَفَّلٍ الْمُزَنِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم   قَالَ: {صَلُّوا قَبْلَ اَلْمَغْرِبِ ، صَلُّوا قَبْلَ اَلْمَغْرِبِ" ثُمَّ قَالَ فِي اَلثَّالِثَةِ : " لِمَنْ شَاءَ"  كَرَاهِيَةَ أَنْ يَتَّخِذَهَا اَلنَّاسُ سُنَّةً}  رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

وَفِي رِوَايَةِ اِبْنِ حِبَّانَ: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   صَلَّى قَبْلَ اَلْمَغْرِبِ رَكْعَتَيْنِ}

وَلِمُسْلِمٍ عَنْ أَنَسٍ قَالَ: {كُنَّا نُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ بَعْدَ غُرُوبِ اَلشَّمْسِ ، فَكَانَ صلى الله عليه وسلم   يَرَانَا ، فَلَمْ يَأْمُرْنَا وَلَمْ يَنْهَانَا}

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mughaffal Al-Muzaniyy[8] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalini kabla ya Magharibi, swalini kabla ya Magharibi.”[9] Na mara ya tatu amesema: “Kwa anayetaka.” Kwa kuchelea watu wasiifanye kuwa ni Sunnah.[10] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

Na katika Riwaayah ya Ibn Hibbaan: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali Rakaa mbili kabla ya Magharibi.”

 

Na Muslim kupitia kwa Anas (رضي الله عنه)  amesema: “Tulikuwa tukiswali Rakaa mbili baada ya kuchwa jua, na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akituona naye hakutuamrisha wala hakutukataza.”

 

 

 

288.

وَعَنْ عَائِشَةَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا  قَالَتْ: {كَانَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم   يُخَفِّفُ اَلرَّكْعَتَيْنِ اَللَّتَيْنِ قَبْلَ صَلَاةِ اَلصُّبْحِ ، حَتَّى إِنِّي أَقُولُ : أَقَرَأَ بِأُمِّ اَلْكِتَابِ ؟}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akihafifisha Rakaa mbili kabla ya Alfajiri hadi mimi ninasema: Amesoma Ummul-Kitaab? (Al-Faatihah).” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

289.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ : {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   قَرَأَ فِي رَكْعَتَيْ اَلْفَجْرِ: ( قُلْ يَا أَيُّهَا اَلْكَافِرُونَ ) و ( قُلْ هُوَ اَللَّهُ أَحَدٌ )رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisoma:

قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ ﴿١﴾

Sema: “Enyi makafiri!”[11]

Na:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾

“Sema: “Yeye ni Allaahu Mmoja Pekee.”[12] katika Rakaa mbili za Alfajiri.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

290.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم   إِذَا صَلَّى رَكْعَتَيْ اَلْفَجْرِ اِضْطَجَعَ عَلَى شِقِّهِ اَلْأَيْمَنِ}  رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Pindi Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Rakaa mbili za Alfajiri analalia ubavu wake wa kulia.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

291.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  { إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ اَلرَّكْعَتَيْنِ قَبْلَ صَلَاةِ اَلصُّبْحِ ، فَلْيَضْطَجِعْ عَلَى جَنْبِهِ اَلْأَيْمَنِ}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakaposwali mmoja wenu Rakaa mbili kabla ya Swalaah ya Alfajiri, basi alalie upande wake wa kuume.”[13] [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, na At-Tirmidhiy naye aliipa daraja la Swahiyh]

 

 

 

292.

  وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  { صَلَاةُ اَللَّيْلِ مَثْنَى مَثْنَى ، فَإِذَا خَشِيَ أَحَدُكُمْ اَلصُّبْحِ صَلَّى رَكْعَةً وَاحِدَةً ، تُوتِرُ لَهُ مَا قَدْ صَلَّى}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَلِلْخَمْسَةِ   وَصَحَّحَهُ اِبْنِ حِبَّانَ: {صَلَاةُ اَللَّيْلِ وَالنَّهَارِ مَثْنَى مَثْنَى"}  وَقَالَ النَّسَائِيُّ : "هَذَا خَطَأٌ"

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah za usiku ni Rakaa mbili mbili, na mmoja wenu akikhofia Swalaah ya Alfajiri, basi aswali Rakaa moja ambayo itakuwa ni Witr ya Rakaa alizoswali.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Imepokewa Hadiyth na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad), ambayo Ibn Hibbaan aliipa daraja la Swahiyh: “Swalaah za (Sunnah za) usiku na mchana ni Rakaa mbili mbili.”

An-Nasaaiy amesema: “Hili ni kosa.[14][15]

 

 

 

293.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { أَفْضَلُ اَلصَّلَاةِ بَعْدَ اَلْفَرِيضَةِ صَلَاةُ اَللَّيْلِ}  أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah bora zaidi baada ya Swalaah ya faradhi ni Swalaah ya usiku.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

294.

وَعَنْ أَبِي أَيُّوبَ اَلْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ: {اَلْوِتْرُ حَقٌّ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ ، مَنْ أَحَبَّ أَنْ يُوتِرَ بِخَمْسٍ فَلْيَفْعَلْ ، وَمَنْ أَحَبَّ أَنْ يُوتِرَ بِثَلَاثٍ فَلْيَفْعَلْ ، وَمَنْ أَحَبَّ أَنْ يُوتِرَ بِوَاحِدَةٍ فَلْيَفْعَلْ}  رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ إِلَّا اَلتِّرْمِذِيَّ ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ ، وَرَجَّحَ النَّسَائِيُّ وَقْفَهُ

Kutoka kwa Abuu Ayyuwb Al-Anaswaariy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah ya Witr ni haki juu ya kila Muislamu.[16] Anayependa kuswali kwa Rakaa tano, na afanye hivyo, na anayetaka kuiswali kwa Witr ya Rakaa tatu na afanye hivyo, na anayetaka kuiswali kwa Rakaa moja na afanye hivyo.[17][Imetolewa na Al-Arba’ah (An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa At-Tirmidhiy, na akaisahihisha Ibn Hibbaan, na An-Nasaaiy aliipa daraja la Mawquwf]

 

 

 

295.

وَعَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {لَيْسَ اَلْوِتْرُ بِحَتْمٍ كَهَيْئَةِ اَلْمَكْتُوبَةِ ، وَلَكِنْ سُنَّةٌ سَنَّهَا رَسُولُ اَللَّهِ}  رَوَاهُ النَّسَائِيُّ وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ

Kutoka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Swalaah ya Witr siyo lazima kama Swalaah ya faradhi, lakini ni Sunnah iliyowekwa na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).” [Imetolewa na An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy naye aliipa daraja la Hasan, na Al-Haakim akaisahihisha]

 

 

 

296.

وَعَنْ جَابِرٍ {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَامَ فِي شَهْرِ رَمَضَانَ، ثُمَّ اِنْتَظَرُوهُ مِنْ اَلْقَابِلَةِ فَلَمَّا يَخْرُجْ ، وَقَالَ: " إِنِّي خَشِيتُ أَنْ يُكْتَبَ عَلَيْكُمْ اَلْوِتْرُ}  رَوَاهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali katika mwezi wa Ramadhwaan kisha Maswahaba zake wakamngojea usiku wa pili, lakini hakutoka (nyumbani kwake) akasema: Niliogopa isije[18] Witr ikafaradhishwa kwenu[19].” [Imetolewa na Ibn Hibbaan]

 

 

 

297.

وَعَنْ خَارِجَةَ بْنِ حُذَافَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { إِنَّ اَللَّهَ أَمَدَّكُمْ بِصَلَاةٍ هِيَ خَيْرٌ لَكُمْ مِنْ حُمُرِ اَلنَّعَمِ " قُلْنَا : وَمَا هِيَ يَا رَسُولَ اَللَّهِ  ؟ قَالَ: " اَلْوِتْرُ ، مَا بَيْنَ صَلَاةِ اَلْعِشَاءِ إِلَى طُلُوعِ اَلْفَجْرِ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

وَرَوَى أَحْمَدُ: عَنْ عَمْرِوِ بْنِ شُعَيْبٍ ، عَنْ أَبِيهِ ، عَنْ جَدِّهِ نَحْوَهُ

Kutoka kwa Khaarijah bin Hudhaafah[20] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Amekupeni Swalaah ya ziada iliyo bora kwenu kuliko ngamia wekundu.” Tukasema: “Ni ipi Ee Rasuli wa Allaah?” Akasema: “Ni Witr iliyo baina ya Swalaah ya ‘Ishaa na Alfajiri.[21] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy, na akaisahihisha Al-Haakim]

 

Na Ahmad amepokea Hadiyth inayofanana na hiyo kutoka kwa ‘Amr[22] bin Shu’ayb[23] kwa usimulizi wa baba yake aliyeipokea kutoka kwa babu yake ‘Amr.

 

 

 

298.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ بُرَيْدَةَ ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  { اَلْوِتْرُ حَقٌّ، فَمَنْ لَمْ يُوتِرْ فَلَيْسَ مِنَّا}  أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ بِسَنَد لَيِّنٍ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

وَلَهُ شَاهِدٌ ضَعِيفٌ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عِنْدَ أَحْمَدَ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah[24] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amepokea kutoka kwa baba yake kuwa, Rasuli wa Allaa (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Witr ni haki kwa hivyo asiyeiswali si miongoni mwetu.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad laini, na akaisahihisha Al-Haakim]

Na ina ushahidi dhaifu kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) uliopokewa na Ahmad.

 

 

 

299.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {مَا كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   يَزِيدُ فِي رَمَضَانَ وَلَا فِي غَيْرِهِ عَلَى إِحْدَى عَشْرَةَ رَكْعَةً، يُصَلِّي أَرْبَعًا، فَلَا تَسْأَلْ عَنْ حُسْنِهِنَّ وَطُولِهِنَّ، ثُمَّ يُصَلِّي أَرْبَعًا، فَلَا تَسْأَلْ عَنْ حُسْنِهِنَّ وَطُولِهِنَّ، ثُمَّ يُصَلِّي ثَلَاثًا. قَالَتْ عَائِشَةُ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ، أَتَنَامُ قَبْلَ أَنْ تُوتِرَ ؟ قَالَ: "يَا عَائِشَةُ، إِنَّ عَيْنَيَّ تَنَامَانِ وَلَا يَنَامُ قَلْبِي".}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَفِي رِوَايَةٍ لَهُمَا عَنْهَا: {كَانَ يُصَلِّي مِنْ اَللَّيْلِ عَشْرَ رَكَعَاتٍ، وَيُوتِرُ بِسَجْدَةٍ، وَيَرْكَعُ رَكْعَتَيْ اَلْفَجْرِ، فَتِلْكَ ثَلَاثُ عَشْرَةَ}

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuzidisha Rakaa kumi na moja za Sunnah katika mwezi wa Ramadhwaan wala katika miezi mingine, Aliswali Rakaa nne, usiulize uzuri wake wala urefu wake. Kisha Rakaa nne usiulize uzuri na urefu wake. Kisha akswali Rakaa tatu za Witr.” ‘Aaishah akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Utalala usingizi kabla ya kuswali Witr?” Akasema: “Ee ‘Aaishah macho yangu hulala, lakini moyo wangu haulali.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Na katika mapokezi ya Al-Bukhaariy na Muslim: “Alikuwa akiswali usiku Rakaa kumi, na anamalizia Witr kwa kuswali Rakaa moja, na alikuwa akiswali Rakaa mbili za Alfajiri, kwa hiyo hizo ni Rakaa kumi na tatu.[25]

 

 

 

300.

وَعَنْهَا قَالَتْ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   يُصَلِّي مِنْ اَللَّيْلِ ثَلَاثَ عَشْرَةَ رَكْعَةً، يُوتِرُ مِنْ ذَلِكَ بِخَمْسٍ، لَا يَجْلِسُ فِي شَيْءٍ إِلَّا فِي آخِرِهَا}

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema tena: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Rakaa kumi na tatu usiku, akiswali Witr Rakaa tano kati ya hizo, na hakai popote isipokuwa katika Rakaa ya mwisho.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

301.

وَعَنْهَا قَالَتْ: {مِنْ كُلِّ اَللَّيْلِ قَدْ أَوْتَرَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  فَانْتَهَى وِتْرُهُ إِلَى اَلسَّحَرِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِمَا

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Katika usiku mzima Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ameswali Witr, na Witr yake iliishia wakati wa suhuwr.” (Saa ya mwisho kabla ya Alfajiri)[26]  [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

302.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ اَلْعَاصِ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {يَا عَبْدَ اَللَّهِ! لَا تَكُنْ مِثْلَ فُلَانٍ، كَانَ يَقُومُ مِنْ اَللَّيْلِ، فَتَرَكَ قِيَامَ اَللَّيْلِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amri bin Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliniambia: “Ee ‘Abdullaah! Usiwe kama fulani alikuwa akiswali usiku akaacha kuswali usiku.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

303.

وَعَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  { أَوْتِرُوا يَا أَهْلُ اَلْقُرْآنَ، فَإِنَّ اَللَّهَ وِتْرٌ يُحِبُّ اَلْوِتْرَ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Enyi watu wa Qur-aan! Swalini Swalaah ya Witr kwa sababu Allaah ni Witr (Mmoja)[27] na Anapenda Witr.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha Ibn Khuzayma]

 

 

 

304.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا; عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم   قَالَ: {اِجْعَلُوا آخِرَ صَلَاتِكُمْ بِاللَّيْلِ وِتْرًا}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Fanyeni mwisho wa Swalaah zenu usiku ni Witr.”[28] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

305.

وَعَنْ طَلْقٍ بْنِ عَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتَ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   يَقُولُ: {لَا وِتْرَانِ فِي لَيْلَةٍ}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالثَّلَاثَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Twalq bin ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Hakuna Witr mbili katika usiku mmoja.” [Imetolewa na Ahmad, na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd), na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

306.

وَعَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   يُوتِرُ بِـ "سَبِّحِ اِسْمَ رَبِّكَ اَلْأَعْلَى"، و: "قُلْ يَا أَيُّهَا اَلْكَافِرُونَ"، و: "قُلْ هُوَ اَللَّهُ أَحَدٌ"}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ. وَزَادَ: {وَلَا يُسَلِّمُ إِلَّا فِي آخِرِهِنَّ}  

وَلِأَبِي دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيِّ نَحْوُهُ عَنْ عَائِشَةَ وَفِيهِ: {كُلَّ سُورَةٍ فِي رَكْعَةٍ، وَفِي اَلْأَخِيرَةِ: "قُلْ هُوَ اَللَّهُ أَحَدٌ"، وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ}

Kutoka kwa Ubayy bin Ka’b[29] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akiswali Witr anasoma Suwrah Al-A’laa[30] katika Rakaa ya kwanza, na Suwrah Al-Kaafiruwn katika Rakaa ya pili na Suwrah Al-Ikhlaasw katika Rakaa ya tatu.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy] Naye akaongeza: “Wala hatoi Salaam isipokuwa mwishoni.”

 

Na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy wamepokea Hadiyth kama hiyo kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisoma kila Suwrah moja katika kila Rakaa, na katika Rakaa ya mwisho alikuwa akisoma Al-Ikhlaasw pamoja na Al-Mu’awwidhatayn.[31]

 

 

 

307.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   قَالَ: {أَوْتِرُوا قَبْلَ أَنْ تُصْبِحُوا}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَلِابْنِ حِبَّانَ: {مَنْ أَدْرَكَ اَلصُّبْحَ وَلَمْ يُوتِرْ فَلَا وِتْرَ لَهُ }

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalini Witr kabla ya Alfajiri.” [Imetolewa na Muslim]

 

Na Ibn Hibbaan amepokea: “Mwenye kudiriki Alfajiri na hakuiswali Witr, basi hana Witr.”[32]

 

 

 

308.

وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   { مَنْ نَامَ عَنْ اَلْوِتْرِ أَوْ نَسِيَهُ فَلْيُصَلِّ إِذَا أَصْبَحَ أَوْ ذَكَرَ}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kulala akakosa Witr au akaisahau, basi na aiswali asubuhi[33] au hapo atakapokumbuka.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy]

 

 

 

309.

وَعَنْ جَابِرٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  { مَنْ خَافَ أَنْ لَا يَقُومَ مِنْ آخِرِ اَللَّيْلِ فَلْيُوتِرْ أَوَّلَهُ، وَمَنْ طَمِعَ أَنْ يَقُومَ آخِرَهُ فَلْيُوتِرْ آخِرَ اَللَّيْلِ، فَإِنَّ صَلَاةَ آخِرِ اَللَّيْلِ مَشْهُودَةٌ، وَذَلِكَ أَفْضَلُ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuchelea kuamka mwishoni mwa usiku, basi aswali Witr mwanzoni mwa usiku, na mwenye azma ya kuamka mwisho mwa usiku basi aiswali Witr mwishoni mwa usiku, kwani Swalaah iswaliwayo mwishoni mwa usiku hushuhudiwa (Na Malaika) nayo ni bora zaidi.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

310.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا ، عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم   قَالَ: {إِذَا طَلَعَ اَلْفَجْرُ فَقَدْ ذَهَبَ كُلُّ صَلَاةِ اَللَّيْلِ وَالْوَتْرُ، فَأَوْتِرُوا قَبْلَ طُلُوعِ اَلْفَجْرِ}  رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Alfajiri ikichomoza Swalaah zote za usiku pamoja na Witr zimeondoka, basi swalini Witr kabla ya kuchomoza Alfajiri.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy]

 

 

 

311.

وَعَنْ عَائِشَةَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا  قَالَتْ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   يُصَلِّي اَلضُّحَى أَرْبَعًا، وَيَزِيدُ مَا شَاءَ اَللَّهُ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَلَهُ عَنْهَا: {أَنَّهَا سُئِلَتْ: هَلْ كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   يُصَلِّي اَلضُّحَى ؟ قَالَتْ: لَا، إِلَّا أَنْ يَجِيءَ مِنْ مَغِيبِهِ} 

وَلَهُ عَنْهَا: {مَا رَأَيْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   يُصَلِّي سُبْحَةَ اَلضُّحَى قَطُّ، وَإِنِّي لَأُسَبِّحُهَا}

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Dhwuhaa Rakaa nne[34] na akizidisha kiasi apendacho Allaah.” [Imetolewa na Muslim]

 

Katika upokezi wake (Muslim) mwingine: “’Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) aliulizwa: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Dhwuhaa? Akasema: “Laa isipokuwa awe kutoka safarini.”

 

Na katika upokezi wake (Muslim) mwingine: ’Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Sikumuona kamwe Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiswali Dhwuhaa, lakini mimi ninaiswali.”[35]

 

 

 

312.

وَعَنْ زَيْدِ بْنِ أَرْقَمَ; أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ: {صَلَاةُ اَلْأَوَّابِينَ حِينَ تَرْمَضُ اَلْفِصَالُ}  رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ

Kutoka kwa Zayd bin Arqam (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimuliwa kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah ya Al-Awwaabiyn (wanaotubia) huswaliwa wakati ndama wa ngamia wanapochomwa na jua.”[36] [Imetolewa na At-Tirmidhiy]

 

 

 

313.

وَعَنْ أَنَسٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { مَنْ صَلَّى اَلضُّحَى ثِنْتَيْ عَشْرَةَ رَكْعَةً بَنَى اَللَّهُ لَهُ قَصْرًا فِي اَلْجَنَّةِ}  رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَاسْتَغْرَبَهُ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuswali Rakaa kumi na mbili za Dhwuhaa, Allaah atamjengea nyumba Jannah.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy, na aliipa daraja la Ghaarib (ngeni)]

 

 

 

314.

وَعَنْ عَائِشَةَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا  قَالَتْ: {دَخَلَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم   بَيْتِي، فَصَلَّى اَلضُّحَى ثَمَانِيَ رَكَعَاتٍ}  رَوَاهُ اِبْنُ حِبَّانَ فِي "صَحِيحِهِ"

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliingia nyumbani kwangu akaswali Rakaa nane za Dhwuhaa.” [Imetolewa na Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]

 

[1] Jina la utani la Rabiy’ah bin Ka’b Al-Aslamiyy ni Abuu Firaas Al-Madaniy. Alikuwa Swahaba alitoka katika Maswahaba wa Suffa. Alikuwa mtumishi wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na alikuwa akimhudumia na kuongozana naye katika safari na nyumbani. Alifariki mnamo mwaka wa 3 A.H.

[2] Hii inatufunza kuwa, iwapo mtu anataka kumkurubia sana Allaah (سبحانه وتعالى) na Nabiy wake (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), ni lazima aswali Swalaah za khiari (Nawaafil) kwa wingi.

[3] Hadiyth hii ina ushahidi kwa watu wale wanaohesabu kwamba kusujudu ni bora kabisa kuliko vitendo vingine vya Swalaah.

 

[4] Maana ya Hadiyth hii ni kwamba: “Mimi ninaomba kwa Allaah ili Akupe wewe kile unachokitaka, na nitamuomba Yeye Akupe wewe, lakini kwa kuwa ni kitu kikubwa sana kuomba hicho, basi ni sharti uswali Swalaah nyingi sana za khiari ili du’aa zangu zipate kukubalika.”

[5] Hadiyth hii inatuarifu kuhusu Rakaa nne za Sunnah kabla ya Swalaah ya faradhi wakati wa Adhuhuri. Imetajwa kupitia katika rejea ya ‘Abdullaah bin ‘Umar kuwa kuna Rakaa mbili za kuswaliwa kabla ya Swalaah ya faradhi. Kama ufafanuzi kuhusu hali hii, inasemwa kwamba Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Rakaa nne kama tendo la kuonyesha unyenyekevu na kufunguliwa kwa milango ya  Jannah, na Rakaa mbili za Sunnah Msikitini. Wengine wanasema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Rakaa nne nyumbani, na kuhusu Rakaa mbili ambazo alikuwa akiziswali Msikitini, hazikuwa zingine ila ni ile Swalaah ya Tahiyyatul-Masjid (Maamkizi ya Msikiti). Wengine wanasema kwamba, zote mbili zilikuwa ni Sunnah za Swalaah ya Adhuhuri, na kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mara nyingine alikuwa akiziswali Rakaa nne na mara nyingine mbili tu. Zote mbili ni sawa, lakini nne ni bora zaidi kuliko mbili. Hakuna tofauti ya maoni juu ya Rakaa mbili za Swalaah ya Alfajiri, kwa kuwa zinahesabika kuwa ni Sunnah Muakkadah (Sunnah iliyosisitizwa iliyoswaliwa mara kwa mara na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)). Imeripotiwa kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa haziachi hizo hata akiwa safarini, na kwa hivyo ni Waajib kwa msafiri kutoiacha Swalaah ya Witr ya usiku na pia Sunnah ya Swalaah ya Alfajiri.

[6] Ummu Habiybah anaitwa Ramla bint Abuu Sufyaan ni dada wa Mu’aawiyah. Alisilimu zamani, akahamia Abyssinia, na mumewe ‘Ubaydullaah bin Jahsh alirtadi na akawa Mkristo akafia huko. Kisha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuoa mnamo mwaka wa 7A.H. wakati yeye Ramla yuko kule, kisha akaja Al-Madiynah pamoja na wahamiaji wa Abyssinia. Alifariki mnamo mwaka wa 42, au 44 au 50 A.H.

[7] Hadiyth hii inatuarifu kuwa, desturi ya Rakaa nne kuswaliwa kabla ya Swalaah ya Alasiri pia ilikuwepo. Endapo mtu yeyote ataziswali hizo, atapata thawabu, lakini asipozswali hana lawama.

[8] ‘Abdullaah bin Mughaffal alikuwa miongoni mwa Aswhaab Ash-Shajara (Waliofanya bay’ah yaaani kula kiapo kuutetea Uislamu dhidi ya Maquraysh kule Hudaybiyah). Aliishi Al-Madiynah na baadae Basra. Alikuwa ni mmoja wa wale watu kumi waliopelekwa na ‘Umar Basra kuwafundisha watu Dini. Alikufa mnamo mwaka wa 60 A.H

[9] Kuna tofauti ya maoni miongoni mwa Wanazuoni kuhusu ubora wa kuswali Rakaa mbili kabla ya Swalaah ya Magharibi. Wale wanaokubali kusihi kwake wanachukua ushahidi kutoka katika Swahiyhayn (Al-Bukhaariy na Muslim). Na wale wanaokanusha wanalinganisha na Hadiyth ya Abuu Daawuwd kuwa, alipoulizwa ‘Abdullaah bin ‘Umar juu ya hizo Rakaa mbili za kabla ya Swalaah ya Magharibi alisema hakuwahi kumuona yeyote akiziswali Rakaa hizo wakati Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa bado yu hai. Ukweli ni kuwa, usahihi unathibitishwa, lakini zisihesabike kuwa ni Sunnah Muakkadah (Zilosisitizwa), kwa sababu Anas, msimuliaji wa Hadiyth za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema kuwa: “Kila Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipotuona sisi tunaswali Rakaa hizo, hakutuamrisha sisi kuwa lazima tuwe tukiziswali, wala hakutuamrisha sisi tuache tusiziswali.” Kwa hivyo inaonekana kuwa mtu anaweza kuziswali iwapo tu bado upo muda kabla ya Swalaah ya Jamaa lakini si sawa kuichelewesha Swalaah ya faradhi kwa ajili yake.

[10] Hadiyth hii inatuambia sisi kuwa, kujuzu na usahihi wa Rakaa hizo mbili kabla ya Swalaah ya Magharibi umethibitishwa.

[11] Suwrah Al-Kaafiruwn (109)

[12] Suwrah Al-Ikhlaasw (113) 

[13] Kuna tofauti ya maoni juu ya tatizo hili ambalo ni la kipekee. Wengine wanakuhesabu kule kulala chini kuwa ni Waajib (Lazima); wengine wanasema ni Sunnah (khiari), na wapo wanaosema hiyo ni Mustahab (iliyopendekezwa). Kwa mujibu wa maoni ya Imaam Nawawi, ni Sunnah ambayo inaingia akilini pia. Ama ripoti ya Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kutokuafiki, ni sababu ya kuhusiana na Msikiti. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alilala chini hivyo nyumbani kwake tu. Vitendo vyote viwili vya kuswalia hizo Rakaa mbili Msikitini na akalala chini mle, havijathibitishwa.

[14] An-Nasaaiy anasema kuwa yale maneno ya

صَلَاةُ اَللَّيْلِ مَثْنَى مَثْنَى

 (Swalaah za usiku ni Rakaa mbili, mbili)

ni sawa, lakini maneno ya

صَلَاةُ اَللَّيْلِ وَالنَّهَارِ مَثْنَى مَثْنَى

(Swalaah za usiku na za mchana ni Rakaa mbili, mbili) siyo sawa. Yaani kule kuongezwa kwa neno “Wan-nahaar” kunahisabika kuwa ni kwingi mno na kwa hivyo ni makosa, kwa mujibu wa maoni ya Imaam An-Nasaaiy.

[15] Maoni ya Imaam An-Nasaaiy kuhusu usimulizi huo na kukiri kuwa sio sahihi haukubaliki na hauna uthibitisho kwa kuwa Bayhaqiy amekiri kuwa ni sahihi. Tena Imaam Muslim, kwa kunukuu usimulizi wa ‘Aliy bin ‘Abdullaah Bariqi, msimuliaji wa Ahaadiyth za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliidhinisha kwa hiyo akauthibitisha usahihi wake.  Imaam Al-Bukhaariy ameripoti Hadiyth nane kuhusu kadhia hii, na zote zinaiunga mkono. Hata hivyo, bila kujali kuwa Rakaa hizo zitaswaliwa mchana au usiku, ni ubora kuziswali hizo Nawaafil (Swala za khiari, yaani Sunnah) kwa Swalaah za Rakaa mbili mbili, na inaruhusika pia kuziswali kwa Swalaah za Rakaa nne.

[16] Hadiyth hii inatuarifu kwamba kuswali Witr ni lazima. Wale Ahnaaf (Wafuasi wa Imaam Abuu Haniyfah yaani Wahanafi) wanafuata fikra hizo hizo. Maimaam waliobaki na Wanazuoni wengi wengine wanaihesabu Witr kuwa ni Sunnah. Kwa hivyo Hadiyth inayofuata, ambayo ni imara zaidi katika mlolongo wa wapokezi, nayo inaunga mkono.

[17] Kwa mujibu wa ripoti, namba ya Rakaa za Swalaah ya Witr ni kati ya moja na kumi na moja. Wanazuoni wengine hupendelea kuswali Rakaa tatu. Wengi wa Maswahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), wafuasi wao, Imaam Shaafi’, Imaam Ahmad, na Imaam Maalik, wanatambua na wanapendelea Rakaa moja.

[18] Kwa mujibu wa Hadiyth hii, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalisha Swalaah ya Taraawiyh katika Jamaa kwa mausiku matatu tu katika maisha yake yote, na kuiswali Swalaah hii kila siku katika mwezi wa Ramadhwaan, kulianzishwa baadaye na Khalifa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)

[19] Hadiyth hii inaelezea Swalaah ya Taraawiyh ambayo wingi wa Rakaa zake ni kumi na moja, na Witr nayo wingi wa Rakaa zake ni kumi na moja pia. ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) aliripoti kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuswali zaidi ya Rakaa kumi na moja za Witr mnamo mwezi wa Ramadhwaan na katika miezi mingine. ‘Umar (رضي الله عنه)  alimuamrisha ‘Ubay bin Ka’b (رضي الله عنه) kuswalisha Rakaa nane za Taraawiyh. Kwa hivyo inaweza kusemwa kuwa watu walikuwa wakiswali kwa uwingi Rakaa ishirini (20) pia mnamo zama za ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) (ilimradi hii pia ilithibitishwa na mlolongo wa wapokezi). Lakini hakuna Hadiyth Swahiyh inayojulikana chanzo inayothibitisha Rakaa ishirini za Taraawiyh.

[20] Khaarijah bin Hudhaafah ni Qurayshi na ni ‘Adawi ambaye alifananishwa na wapanda farasi elfu moja. ‘Amr bin Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuomba ‘Umar bin Al-Khatwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), ampelekee wapanda farasi elfu tatu, lakini yeye akampelekea watu watatu tu, nao ni Az-Zubayr bin Al-‘Awwaam, Al-Miqdaad bin Al-Aswad, na Khaarijah. Alikuwa Qadhi kule Misri kwa ‘Amr bin Al-‘Aasw na akauliwa kule mnamo Ramadhwaan mwaka 40 A.H, na mmoja wa Khawaarij aliyemdhania kuwa yeye ndiye ‘Amr bin Al-‘Aasw. Hii ilikuwa wakati ule wale Makhawaarij walipokula njama ya kuwaua ‘Amr, ‘Aliy na Mu’aawiyah.

[21] Kwa mujibu wa Hadiyth hii, wakati wa ‘Ishaa ni kutokea wakati wa Swalaah ya ‘Ishaa mpaka wakati wa dalili za kwanza za Alfajiri. Wakati wake mzuri ni usiku zaidi; lakini iwapo mtu hatokuwa na hakika kuwa atawahi kuamka toka usingizini, basi ni ubora aiswali Witr mara baada ya kuiswali ‘Ishaa.

[22] ‘Amr huyu ndiye Abuu Ibraahiym ‘Amr bin Shu’ayb bin ‘Abdillaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw As-Sahmiy Al-Qurayshiy Al-Madaniy, aliyelowea Twaaif. An-Nasaaiy alimthibitisha kuwa ni wa kutegemewa. Alikufa mnamo mwaka 118 A.H.

[23] Shu’ayb alikuwa mmoja wa Taabi’iyn wa kutegemewa. Inasemekana kuwa babake Muhammad alikufa zama za utoto wake; kwa hivyo babu yake ‘Abdullaah bin ‘Amr yule Swahaba maarufu ndiye alimlea. Na imethibitika kuwa yeye aliisikia hasa hii Hadiyth kutoka kwake. Kwa hiyo hii siyo Munqatwi’ wala siyo Mursal, bali ni Mutwassil ambayo haiendi chini ya daraja la Hassan.

[24] ‘Abdullaah bin Buraydah ndiye Abuu Sahl, Qadhi wa Marw, ambaye alikuwa ni mmoja wa Taabi’iyn wa daraja la tatu wa kutegemewa sana na maarufu kabisa. Alifia Marw mnamo mwaka wa 115 A.H.

[25] Kuna tofauti ya maoni iwapo Swalaah ya Tahajjud (Swalaah ya usiku wa manane) ina Rakaa kumi na moja au kumi na tatu. Kumi na moja zimeafikiwa, lakini kumi na tatu zina mtafaruku. Ukweli ni kwamba, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wakati mwingine aliswali kumi na moja za Tahajjud kujumlisha na Witr na wakati mwingine kumi na tatu.

[26] Suwhur inajulikana pia ni kula daku.

[27] Inamaanisha Sifa za Allaah, yaani Yeye ni wa Kipekee, na “Hakuna chochote kinachofanana na Yeye”

[28] Kwa mujibu wa simulizi zingine, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiswali Rakaa mbili za Sunnah (Naafil) baada ya Swalaah ya Witr kwa hivyo amesamehewa. Wengine wanasema kuwa mtu ni bora aswali Rakaa mbili za Swalaah ya Sunnah katika sehemu ya mwisho ya usiku, akiwa ameshaswali Swalaah ya Witr sehemu ya mwanzo ya usiku. Endapo ataswali Witr katika sehemu ya mwisho ya usiku, basi hana haja ya kuswali hiyo Swalaah ya Sunnah.

[29] Ubayy bin Ka’b ni Answaar, na ni Khazraj, alipewa jina la utani la Abu Al-Mundhir. Alikuwa ndiye Sayyid wa Wanazuoni wa Qur-aan na alikuwa mmoja wa waandishi wa Wahy. Na alikuwa pia mmoja wa watu walioikusanya Qur-aan na alitoa Fatwa (uamuzi wa kisheria) zama za uhai wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alishiriki katika vita vya ‘Aqabah, Badr na vita vilivyofuatia hivi. Mwaka wa kufa kwake kumetofautiana; wengine wakisema alikufa mnamo mwaka wa 19, au 20, au 22, au 30, au 32, au 33 A.H

[30] Suwrah Al-A’laa (87).

[31] Suwrah za Al-Mu’awwidhatayn ni: Al-Falaq (113) na An-Naas (114).

 

[32] Hadiyth hii inatuambia kuwa wakati wa Witr unakwisha kunapopambazuka; na Hadiyth hii inamaanisha kuwa Witr anayoiswali mtu huku wakati huo umepita basi inakuwa haikuswaliwa kwa mujibu wa Sunnah ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Haimaanishi kuwa iwapo mtu hakuwahi kuswali Witr kabla ya Alfajiri basi asiiswali kabisa. Tukio moja linalowahusu Maswahaba linasimuliwa na Hadiyth isemayo kwamba, wakati fulani alilala na akachelewa kuamka. Akamtuma Mtumwa wake akaone kama Swalaah ya Jamaa imekwisha kuswaliwa; na Mtumwa akarejea na kumjibu kuwa imekwisha kuswaliwa. Baada ya kuambiwa hivi, aliswali hiyo Witr kwanza, kisha Sunnah na kisha akaiswali Swalaah ya faradhi ya Alfajiri. Kwa hivyo inaeleweka kwamba, mtu asipowahi kuswali Witr katika wakati wake, ni lazima aiswali kama kadhaa baadaye. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisisitiza kuwa Witr ni lazima iswaliwe katika wakati wake bila kukosa. Na aliagiza kuwa kwa wale waliokuwa na shaka ya kuwahi kuamka kuiswali, basi waiswali usiku (kabla hawajalala). Kwa hivyo akamuamrisha Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) aswali Witr usiku.

[33] Ieleweke kwamba, mtu akiikosa Swalaah kwa sababu ya kusahau au usingizi, hatotiwa hatiani na atapata thawabu na kama aliiswali Swalaah ile kwa wakati wake; lakini imekatazwa kwenda kulala wakati ambao unakaribia Swalaah fulani. Itokeapo kwamba hili linatokea kwa bahati mbaya na kwa hali ambayo yeye hawezi kuiepuka, basi hatolaumiwa.

[34] Ifahamike kwamba Ishraaq, Swalaatul-Awwaabiyn, na Dhwuhaa ni majina tofauti yanayomaanisha Swalaah zile zile za kabla ya Swalaah ya Adhuhuri. Wakati wa Swalaah hiyo ni mara baada ya kuchomoza jua na huendelea hadi robo moja ya mchana. Idadi ya chini kabisa ya Rakaa za Dhwuhaa ni Rakaa mbili, na idadi ya juu kabisa ni Rakaa kumi na mbili. Inayopendelewa ni Rakaa nne, ambayo inaungwa mkono na Hadiyth za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Ikumbukwe pia kuwa Swalaah hii ni Sunnah ya Manabiy waliotangulia kwa vile walikuwa wakiziswali hizo katika zama zao. Kwa hivyo Swalaah hii ni Sunnah na Mustahabb (inayopendekezwa). Ama ‘Umar (رضي الله عنه) kuiita Swalaah hii ni Bid’ah (uzushi), inamaanisha tu kuwa ikiwa mtu atazowea kuiswali hiyo kila siku zote, yaweza kuhesabika ni Bid’ah kwa kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuiswali siku zote.

[35] Ingawa Hadiyth hii na hizo mbili zilizoitangulia zinaonekana kupingana, zinaonyesha tu kuwa Swalaah ya Dhwuhaa ni Swalaah ya khiari kama inavyothibitishwa na Wanazuoni wa Hadiyth.

[36] Hadiyth hii inaonyesha kuwa wakati mzuri kuliko wote wa Swalaah ya Dhwuhaa ni kabla tu ya saa sita mchana.

Share

10-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Swalaah Ya Jamaa Na Uimaamu

 

بُلُوغُ الْمَرام

 

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

 

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ صَلَاةِ اَلْجَمَاعَةِ وَالْإِمَامَةِ

 

10- Mlango Wa Swalaah Ya Jamaa Na Uimaamu1

 

 

 

 

 

 

315.

عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا; أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {صَلَاةُ اَلْجَمَاعَةِ أَفْضَلُ مِنْ صَلَاةِ اَلْفَذِّ بِسَبْعٍ وَعِشْرِينَ دَرَجَةً}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَلَهُمَا عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: {بِخَمْسٍ وَعِشْرِينَ جُزْءًا} 

وَكَذَا لِلْبُخَارِيِّ: عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، وَقَالَ: "دَرَجَةً

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah ya Jamaa ina fadhila zaidi kuliko ya peke yake kwa daraja ishirini na saba[1].” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Nao (Al-Bukhaariy na Muslim) tena wamepokea Hadiyth ya Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Kwa mafungu ishirini na tano.”

 

Kadhalika Al-Bukhaariy amepokea Hadiyth ya Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy, amesema: “...daraja…”

 

 

 

 

316.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ: {وَاَلَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَقَدْ هَمَمْتُ أَنْ آمُرَ بِحَطَبٍ فَيُحْتَطَبَ، ثُمَّ آمُرَ بِالصَّلَاةِ فَيُؤَذَّنَ لَهَا، ثُمَّ آمُرَ رَجُلًا فَيَؤُمَّ اَلنَّاسَ، ثُمَّ أُخَالِفُ إِلَى رِجَالٍ لَا يَشْهَدُونَ اَلصَّلَاةَ، فَأُحَرِّقَ عَلَيْهِمْ بُيُوتَهُمْ، وَاَلَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَوْ يَعْلَمُ أَحَدُهُمْ أَنَّهُ يَجِدُ عَرْقًا سَمِينًا أَوْ مِرْمَاتَيْنِ حَسَنَتَيْنِ لَشَهِدَ اَلْعِشَاءَ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, nimetamani kuamuru kukusanywa kuni, kisha kuamrisha kwa Swalaah kuadhiniwe, kisha nimuamrishe mtu mmoja aongoze watu, kisha niwaendee watu wasiohudhuria Swalaah nichome[2] nyumba zao. Naapa kwa Ambaye Nafsi yangu ipo Mikononi Mwake, angejua mmoja wao atapata mfupa ulionona au miguu mizuri ya kondoo angehudhuria Swalaah ya ‘Ishaa.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

 

 

 

317.

وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  { أَثْقَلُ اَلصَّلَاةِ عَلَى اَلْمُنَافِقِينَ: صَلَاةُ اَلْعِشَاءِ، وَصَلَاةُ اَلْفَجْرِ، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِيهِمَا لَأَتَوْهُمَا وَلَوْ حَبْوًا}  مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) tena amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah nzito zaidi kwa wanafiki[3] ni ‘Ishaa na Alfajiri, na laiti wangalijua yaliyomo humo, wangeziendea, hata kwa kutambaa kwa magoti.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

 

 

318.

وَعَنْهُ قَالَ: {أَتَى اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   رَجُلٌ أَعْمَى فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! لَيْسَ لِي قَائِدٌ يَقُودُنِي إِلَى اَلْمَسْجِدِ، فَرَخَّصَ لَهُ، فَلَمَّا وَلَّى دَعَاهُ، فَقَالَ: "هَلْ تَسْمَعُ اَلنِّدَاءَ بِالصَّلَاةِ؟" قَالَ: نَعَمْ. قَالَ: "فَأَجِبْ"}  رَوَاهُ مُسْلِم

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena: “Mtu kipofu[4] alikuja kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Mimi sina mwongozaji anayeniongoza Msikitini. Na Nabiy  (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamruhusu (kuswali nyumbani). Kisha mtu yule alipogeuka kwenda zake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuuliza: “Je, unaisikia Adhana?” Akasema: “Ndiyo.”  Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Basi itikia.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

319.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {مَنْ سَمِعَ اَلنِّدَاءَ فَلَمْ يَأْتِ فَلَا صَلَاةَ لَهُ إِلَّا مِنْ عُذْرٍ}  رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَهْ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ، وَإِسْنَادُهُ عَلَى شَرْطِ مُسْلِمٍ، لَكِنْ رَجَّحَ بَعْضُهُمْ وَقْفَه

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kusikia[5] Adhana asije, hana Swalaah isipokuwa kwa udhuru.” [Imetolewa na Ibn Maajah, Ad-Daaraqutwniy, Ibn Hibbaan na Al-Haakim. Isnaad yake ni kwa sharti la Muslim, lakini baadhi ya wapokezi wa Hadiyth waliipa daraja la Mawquwf]

 

 

 

320.

وَعَنْ يَزِيدَ بْنِ اَلْأَسْوَدِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  {أَنَّهُ صَلَّى مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم    صَلَاةَ اَلصُّبْحِ، فَلَمَّا صَلَّى رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  إِذَا هُوَ بِرَجُلَيْنِ لَمْ يُصَلِّيَا، فَدَعَا بِهِمَا، فَجِيءَ بِهِمَا تَرْعَدُ فَرَائِصُهُمَا، فَقَالَ لَهُمَا: "مَا مَنَعَكُمَا أَنْ تُصَلِّيَا مَعَنَا؟" قَالَا: قَدْ صَلَّيْنَا فِي رِحَالِنَا. قَالَ: "فَلَا تَفْعَلَا، إِذَا صَلَّيْتُمَا فِي رِحَالِكُمْ، ثُمَّ أَدْرَكْتُمْ اَلْإِمَامَ وَلَمْ يُصَلِّ، فَصَلِّيَا مَعَهُ، فَإِنَّهَا لَكُمْ نَافِلَةٌ"}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَاللَّفْظُ لَهُ، وَالثَّلَاثَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ حِبَّان

Kutoka kwa Yaziyd bin Al-Aswad[6] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alisema kuwa: “Yeye aliswali Swalaah ya Fajr pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipomaliza kuswali, aliwaona watu wawili ambao hawakuswali pamoja naye. Akaamrisha waletwe, na wakaletwa huku wakitetemeka[7] (kwa uoga). Akawauliza: “Jambo gani  lilowazuia msiswali pamoja nasi?” Wakasema: “Tumeswali majumbani mwetu.” Akasema: “Msifanye hivyo, mkiswali majumbani mwenu, kisha mkaja Msikitini wakati Imaam hajamaliza kuswalisha watu, swalini pamoja naye, na hiyo itakuwa ni Swalaah ya Sunnah kwenu.” [Imetolewa na Ahmad, na tamshi hili ni lake, na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd) na akaisahihisha At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan]

 

 

 

321.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {إِنَّمَا جُعِلَ اَلْإِمَامُ لِيُؤْتَمَّ بِهِ، فَإِذَا كَبَّرَ فَكَبِّرُوا، وَلَا تُكَبِّرُوا حَتَّى يُكَبِّرَ، وَإِذَا رَكَعَ فَارْكَعُوا، وَلَا تَرْكَعُوا حَتَّى يَرْكَعَ، وَإِذَا قَالَ سَمِعَ اَللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، فَقُولُوا: اَللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ اَلْحَمْدُ، وَإِذَا سَجَدَ فَاسْجُدُوا، وَلَا تَسْجُدُوا حَتَّى يَسْجُدَ، وَإِذَا صَلَّى قَائِمًا فَصَلُّوا قِيَامًا، وَإِذَا صَلَّى قَاعِدًا فَصَلُّوا قُعُودًا أَجْمَعِينَ}  رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَهَذَا لَفْظُهُ   وَأَصْلُهُ فِي اَلصَّحِيحَيْن

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika Imaam amefanywa ili afuatwe, kwa hivyo akipiga Takbiyra nanyi pigeni, lakini nyie msipige Takbiyra hadi yeye apige. Na akirukuu nanyi mrukuu, wala msirukuu hadi amerukuu. Imaam akisema:

سَمِعَ اَللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ

 

“Sami’a-Allaahu liman hamidah” (Allaah Amemsikia aliyemhimidi),

 

Semeni:

 

اَللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ اَلْحَمْدُ

“Allaahumma Rabbanaa Lakal-Hamd.” (Ee Allaah! Rabb wetu, ni Zako Wewe Himd).

 

Na akisujudu, nanyi msujudu, wala msisujudu hadi amesujudu. Akiswali akiwa amesimama nanyi simameni, na akiswali huku amekaa, nanyi swalini huku mmekaa.[8][Imetolewa na Abuu Daawuwd, na hili ni tamshi lake, na chanzo chake kimo katika Swahiyhayn (Al-Bukhaariy na Muslim)]

 

 

 

322.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {رَأَى فِي أَصْحَابِهِ تَأَخُّرًا. فَقَالَ: "تَقَدَّمُوا فَائْتَمُّوا بِي، وَلْيَأْتَمَّ بِكُمْ مَنْ بَعْدَكُمْ"}  رَوَاهُ مُسْلِم

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipoona Maswahaba zake wanachelewa, alisema: “Njooni mbele na mnifuate, na wale wa nyuma wawafuate nyinyi.”[9] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

323.

وَعَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {اِحْتَجَرَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم حُجْرَةً بِخَصَفَةٍ، فَصَلَّى فِيهَا، فَتَتَبَّعَ إِلَيْهِ رِجَالٌ، وَجَاءُوا يُصَلُّونَ بِصَلَاتِهِ...}  اَلْحَدِيثَ، وَفِيهِ: {أَفْضَلُ صَلَاةِ اَلْمَرْءِ فِي بَيْتِهِ إِلَّا اَلْمَكْتُوبَةَ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitengeneza mswala akaswali ndani yake. Watu wakamfuata na wakawa wanaswali nyuma yake…”[10] Msimuliaji aliitaja Hadiyth yote na ina maneno: “Swalaah bora ya mtu ni (anayoiswali) nyumbani kwake isipokuwa Swalaah ya faradhi.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

324.

وَعَنْ جَابِرٍ قَالَ: {صَلَّى مُعَاذٌ بِأَصْحَابِهِ اَلْعِشَاءَ، فَطَوَّلَ عَلَيْهِمْ، فَقَالَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم:   "أَتُرِيدُ أَنْ تَكُونَ يَا مُعَاذُ فَتَّانًا؟ إِذَا أَمَمْتَ اَلنَّاسَ فَاقْرَأْ: بِالشَّمْسِ وَضُحَاهَا، وَ: سَبِّحْ اِسْمَ رَبِّكَ اَلْأَعْلَى، وَ: اِقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ، وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَى"}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mu’aadh aliwaswalisha Maswahaba wenziwe Swalaah ya ‘Ishaa na akawarefushia Swalaah. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Ee Mu’aadh! Unataka uwe Fattaan[11]? Ukiswalisha watu[12] soma:

 وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا[13]

na

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى[14]  

na

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ[15]

na

وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ[16]

 

[Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim[17]]

 

 

 

325.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا فِي قِصَّةِ صَلَاةِ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  بِالنَّاسِ، وَهُوَ مَرِيضٌ  قَالَتْ: {فَجَاءَ حَتَّى جَلَسَ عَنْ يَسَارِ أَبِي بَكْرٍ، فَكَانَ يُصَلِّي بِالنَّاسِ جَالِسًا وَأَبُو بَكْرٍ قَائِمًا، يَقْتَدِي أَبُو بَكْرٍ بِصَلَاةِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم    وَيَقْتَدِي اَلنَّاسُ بِصَلَاةِ أَبِي بَكْرٍ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuhusu Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuswalisha watu wakati akiwa mgonjwa. Amesema: “Alikuja na akaketi upande wa kushoto wa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Akawa anaswalisha watu huku amekaa na Abuu Bakr amesimama. Abuu Bakr alikuwa anamfuata Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na watu wanafuata Swalaah ya Abuu Bakr.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

326.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {إِذَا أَمَّ أَحَدُكُمْ اَلنَّاسَ فَلْيُخَفِّفْ، فَإِنَّ فِيهِمْ اَلصَّغِيرَ وَالْكَبِيرَ وَالضَّعِيفَ وَذَا اَلْحَاجَةِ، فَإِذَا صَلَّى وَحْدَهُ فَلْيُصَلِّ كَيْفَ شَاءَ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu atakaposwalisha watu, afupishe, kwani miongoni mwao wapo watoto, wazee, wadhoofu, na wenye shida. Lakini akiwa anaswali peke yake, na aswali kadiri anavyotaka.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

327.

 وَعَنْ عَمْرِو بْنِ سَلَمَةَ قَالَ: قَالَ أَبِي: {جِئْتُكُمْ مِنْ عِنْدِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  حَقًّا. قَالَ: "فَإِذَا حَضَرَتْ اَلصَّلَاةُ فَلْيُؤَذِّنْ أَحَدُكُمْ، وَلْيَؤُمَّكُمْ أَكْثَرُكُمْ قُرْآنًا"، قَالَ: فَنَظَرُوا فَلَمْ يَكُنْ أَحَدٌ أَكْثَرَ قُرْآنًا مِنِّي، فَقَدَّمُونِي، وَأَنَا اِبْنُ سِتٍّ أَوْ سَبْعِ سِنِينَ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيّ

Kutoka kwa ‘Amr bin Salamah[18] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Baba yangu amesema: “Nimekuleteeni haki kutoka kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kwa hivyo wakati wa Swalaah ukiwadia, mmoja wenu aadhini, na mmoja wenu na aliyehifadhi Qur-aan kuliko wote awe Imaam.” ‘Amr akaendelea kusema: Wakaangalia lakini hakuwepo mtu aliyejua Qur-aan kuliko mimi.[19]. Wakanitanguliza nami nikiwa na umri wa miaka sita au saba tu. ”[20] [Imetolewa na Al-Bukhaariy, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy]

 

 

 

328.

وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  {يَؤُمُّ اَلْقَوْمَ أَقْرَؤُهُمْ لِكِتَابِ اَللَّهِ، فَإِنْ كَانُوا فِي اَلْقِرَاءَةِ سَوَاءً فَأَعْلَمُهُمْ بِالسُّنَّةِ، فَإِنْ كَانُوا فِي اَلسُّنَّةِ سَوَاءً فَأَقْدَمُهُمْ هِجْرَةً، فَإِنْ كَانُوا فِي اَلْهِجْرَةِ سَوَاءً فَأَقْدَمُهُمْ سِلْمًا وَفِي رِوَايَةٍ: سِنًّا وَلَا يَؤُمَّنَّ اَلرَّجُلُ اَلرَّجُلَ فِي سُلْطَانِهِ، وَلَا يَقْعُدْ فِي بَيْتِهِ عَلَى تَكْرِمَتِهِ إِلَّا بِإِذْنِهِ".}  رَوَاهُ مُسْلِم

وَلِابْنِ مَاجَهْ: مِنْ حَدِيثِ جَابِرٍ: {وَلَا تَؤُمَّنَّ اِمْرَأَةٌ رَجُلًا، وَلَا أَعْرَابِيٌّ مُهَاجِرًا، وَلَا فَاجِرٌ مُؤْمِنًا.}  وَإِسْنَادُهُ وَاه

Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema kuwa: “Anaswalisha watu msomaji wao zaidi wa Qur-aan. Ikiwa wako sawa katika usomaji, basi anayejua Sunnah zaidi, na ikiwa wako sawa katika Sunnah basi mtu aliyetangulia Hijrah[21], na kama wako sawa katika uhamiaji basi aliyetangulia kusilimu.”

 

Na katika mapokezi mengine: “Kwa umri.” Na mtu asiswalishe mtu aliyekaa katika milki yake au asikae nyumbani kwa mwenyeji wake penye nafasi ya heshima isipokuwa kwa ruhusa yake.” [Imetolewa na Muslim]

 

Na Ibn Maajah amepokea kutokana na Hadiyth ya Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Mwanamke asimswalishe kamwe mwanamume, wala Bedui (Mwarabu wa jangwani) asimswalishe mhamiaji, na muovu asimswalishe Muumini.” [Isnaad yake ni Waahin (Dhaifu sana)]

 

 

 

329.

وَعَنْ أَنَسٍ، عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {رُصُّوا صُفُوفَكُمْ، وَقَارِبُوا بَيْنَهَا، وَحَاذُوا بِالْأَعْنَاقِ.}  رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Pangeni safu zenu na karibieni baina yake[22], na muwe shingo kwa shingo.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy, na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

330.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { خَيْرُ صُفُوفِ اَلرِّجَالِ أَوَّلُهَا، وَشَرُّهَا آخِرُهَا، وَخَيْرُ صُفُوفِ اَلنِّسَاءِ آخِرُهَا، وَشَرُّهَا أَوَّلُهَا}  رَوَاهُ مُسْلِم

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Safu bora kwa wanaume ni ya kwanza, na mbaya zaidi ni ya mwisho; na kwa mwanamke safu bora zaidi ni ya mwisho na mbaya zaidi ni ya mwanzo.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

331.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {صَلَّيْتُ مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم    ذَاتَ لَيْلَةٍ، فَقُمْتُ عَنْ يَسَارِهِ، فَأَخَذَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  بِرَأْسِي مِنْ وَرَائِي، فَجَعَلَنِي عَنْ يَمِينِهِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) usiku mmoja, nikasimama kushoto kwake, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akanishika kisogoni[23] na akaniweka upande wake wa kulia.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

332.

وَعَنْ أَنَسٍ قَالَ: {صَلَّى رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  فَقُمْتُ وَيَتِيمٌ خَلْفَهُ، وَأُمُّ سُلَيْمٍ خَلْفَنَا}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيّ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali nikasimama mimi na yatima[24] nyuma yake, na Ummu Sulaym nyuma yetu[25].” [Al-Bukhaariy, Muslim, na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

 

333.

وَعَنْ أَبِي بَكْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ{ أَنَّهُ اِنْتَهَى إِلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  وَهُوَ رَاكِعٌ، فَرَكَعَ قَبْلَ أَنْ يَصِلَ إِلَى اَلصَّفِّ، فَقَالَ لَهُ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم زَادَكَ اَللَّهُ حِرْصًا وَلَا تَعُدْ}  رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

وَزَادَ أَبُو دَاوُدَ فِيهِ: {فَرَكَعَ دُونَ اَلصَّفِّ، ثُمَّ مَشَى إِلَى اَلصَّفِّ}

Kutoka kwa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba alikwenda kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiwa anarukuu. Akarukuu kabla hajakuta safu.  Akamtajia hayo Nabiy , (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hapo akamuambia: “Allaah Akuongezee himma,  lakini usirudie.[26] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

Na Abuu Daawuwd akaongezea: “Alirukuu kabla hata ya kuifikia safu, kisha akatembea hadi kwenye safu.”

 

 

 

334.

وَعَنْ وَابِصَةَ بْنِ مَعْبَدٍ اَلْجُهَنِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { رَأَى رَجُلًا يُصَلِّي خَلْفَ اَلصَّفِّ وَحْدَهُ، فَأَمَرَهُ أَنْ يُعِيدَ اَلصَّلَاةَ}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

وَلَهُ عَنْ طَلْقٍ  {لَا صَلَاةَ لِمُنْفَرِدٍ خَلْفَ اَلصَّفِّ}

وَزَادَ اَلطَّبَرَانِيُّ مِنْ حَدِيثِ وَابِصَةَ: {أَلَا دَخَلْتَ مَعَهُمْ أَوْ اِجْتَرَرْتَ رَجُلًا؟ }

Kutoka kwa Waabiswah bin Ma’bad[27] Al-Juhaniyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuona mtu mmoja anaswali peke yake nyuma ya safu, na akamuamrisha arudie kuswali.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd, na At-Tirmidhiy naye akaipa daraja la Hasan, Ibn Hibbaan akaipa daraja la Swahiyh]

 

Naye (Ibn Hibbaan) amepokea Hadiyth ya Twalq bin ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Hakuna Swalaah ya mtu peke yake nyuma ya safu.[28]

Na akaongezea Atw-Twabaraaniyy kwenye usimulizi wa Waabiswah: “Kwa nini hukujiunga nao au kumvuta mtu (ajiunge nawe?).”

 

 

 

335.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {إِذَا سَمِعْتُمْ اَلْإِقَامَةَ فَامْشُوا إِلَى اَلصَّلَاةِ، وَعَلَيْكُمْ اَلسَّكِينَةُ وَالْوَقَارُ، وَلَا تُسْرِعُوا، فَمَا أَدْرَكْتُمْ فَصَلُّوا، وَمَا فَاتَكُمْ فَأَتِمُّوا}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mkisikia Iqaamah, nendeni kuswali kwa utulivu na taadhima, na msifanye haraka, na swalini sehemu yoyote ya Swalaah mtakayoiwahi[29], kisha timizeni sehemu iliyokupiteni." [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

 

336.

وَعَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { صَلَاةُ اَلرَّجُلِ مَعَ اَلرَّجُلِ أَزْكَى مِنْ صَلَاتِهِ وَحْدَهُ، وَصَلَاتُهُ مَعَ اَلرَّجُلَيْنِ أَزْكَى مِنْ صَلَاتِهِ مَعَ اَلرَّجُلِ، وَمَا كَانَ أَكْثَرَ فَهُوَ أَحَبُّ إِلَى اَللَّهِ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّان

Kutoka kwa ‘Ubayy bin Ka’b (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah ya mtu anayoiswali pamoja na mtu mwingine ni bora zaidi kuliko anayoswali peke yake. Na Swalaah ya mtu anaiswali pamoja na watu wawili ni bora zaidi kuliko anayoswali na mtu mmoja; na Swalaah inapokuwa na watu wengi zaidi humpendeza zaidi Allaah (عزّ وجلّ).” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

337.

وَعَنْ أُمِّ وَرَقَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  أَمَرَهَا أَنْ تَؤُمَّ أَهْلَ دَارِهَا}  رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa Ummu Waraqah[30] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuamrisha Ummu Waraqah awaswalishe watu wa nyumba yake.”[31] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

338.

وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ; {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  اِسْتَخْلَفَ اِبْنَ أُمِّ مَكْتُومٍ، يَؤُمُّ اَلنَّاسَ، وَهُوَ أَعْمَى}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُد

وَنَحْوُهُ لِابْنِ حِبَّانَ: عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimteua Ibn Ummu Maktuwm (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) aswalishe, alipokuwa hayupo, naye (Ibn Ummu Maktuwm) alikuwa kipofu.[32][Imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd]

 

Ibn Hibbaan pia amepokea Hadiyth kama hiyo, kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا)

 

 

339.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { صَلُّوا عَلَى مَنْ قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ، وَصَلُّوا خَلْفَ مَنْ قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ}  رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mswalieni mtu aliyetamka (aliyesilimu) Laa ilaaha illa Allaah (hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah) na swalini nyuma ya mtu aliyesema: Laa ilaaha illa Allaah.”[33] [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniyy kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

340.

وَعَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم { إِذَا أَتَى أَحَدُكُمْ اَلصَّلَاةَ وَالْإِمَامُ عَلَى حَالٍ، فَلْيَصْنَعْ كَمَا يَصْنَعُ اَلْإِمَامُ}  رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akiingia katika Swalaah, na Imaam yuko katika kitendo fulani, basi afanye anavyofanya Imaam.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

[1] Katika simulizi zinazofuata, thawabu zimeripotiwa kuwa ni kubwa mara ishirini na tano. Inategemeana na hali ya huyo anayeswali. Mtu mwenye hadhi ya juu hupata mara ishirini na saba zaidi, na yule mwenye hadhi ya chini hupata mara ishirini na tano tu zaidi.

[2] Tunaarifiwa katika Hadiyth hii kwamba, kuswali katika jamaa ni Fardhw ‘Ayn (wajibu wa binafsi). Ingelikuwa ni Fardhw Kifaaya (wajibu wa wengi) au Sunnah Muakkadah (iliyosisitizwa), Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) asingetumia maneno makali vile kwa watu wasiohudhuria Swalaah za Jamaa.

[3] Neno hilo “unafiki” hapa limetumika kuhusu unafiki wa matendo na siyo unafiki wa uaminifu, kwani mnafiki ni mtu asiyeamini moyoni mwake, na huenda Msikitini kwa ajili ya kujionyesha tu kwa watu.

[4] Mtu huyo asiyeona hakuwa mwengine bali ni ‘Abdullaah bin Ummi Maktuwm. Baada ya amri hiyo ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akienda kuswali Msikitini kila mara hadi akateuliwa kuwa Muadhini. Kwa kuwa hata walemavu wanaamrishwa wahudhurie Swalaah ya Jamaa Msikitini, je wale wasiohudhuria Swalaah za jamaa bila kisingizio chochote? Swalaah ya mlemavu inakubalika iswaliwe nyumbani, lakini yeye pia hazipati thawabu za jamaa.

[5] Hadiyth hii inadhihirisha kwamba, ni waajib kwa kwa anayesikia Adhana kuitikia kwa kuwenda kuswali Jamaa Msikitini. Hakuna kisingizio cha kutokwenda kuswali jamaa madamu tu kasikia Adhana.   Miongoni mwa nyudhuru zinazokubalika mtu asiende Msikitini kuswali Jamaaa, ni kimbunga, mvua, njaa kali sana, kwenda haja kubwa, kukojoa, kuugua maradhi n.k.  

[6] Yaziyd bin Al-Aswad ndiye Jaabir As-Sawaaiy Al-‘Aamiriy, ambaye alikuwa sahiba wa Maquraysh. Alikuwa ni Swahaba aliyeishi Twaaif, na hii ndiyo Hadiyth pekee kutoka kwake kupitia kwa mwanawe Jaabir.

[7] Miili yao ilianza kusisimka kwa sababu ya  woga kutokana na haiba ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), kama ambavyo hutokea kwa sababu ya mshituko wa woga.

[8] Shariy’ah hii sasa imefutwa. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalisha watu huku kaketi chini kwa sababu ya maradhi yake (ambayo ndiyo yaliyomuua), ambapo Maamuma (wafuasi) wake waliswali huku wamesimama wima kama ilivyo kawaida.

[9] Hadiyth hii inaweza kunukuliwa kuwa ndiyo ushahidi wa Maamuma ambao wanaweza kumuona Imaam lakini hawawezi kumsikia. Maamuma kama hao lazima wafuate Maamuma mwengine walio mbele yao. Pia inatufundisha kuwa msitari wa mbele kabisa ndiyo mbora, na mtu sharti afuate kuujaza huo kwanza ikiwezekana, na kwamba msitari wa pili usiwe mbali na msitari wa kwanza, na halikadhalika msitari wa kwanza usiwe mbali na Imaam.

[10] Hadiyth hii inaonyesha kuwa, ikiwa upo ukuta au kitenganisho au umbali fulani kati ya Imaam na Maamuma, Swalaah itabakia kuwa halali. Watu wengine hawaafiki maneno yote ya Hadiyth hii, lakini usahihi wake unatosha kuwashawishi watu hao.

[11] Inamaanisha: “Kwa kukirefusha kisomo unataka kuwatesa watu unaowaswalisha, na kwa hivyo unawakatisha tamaa wasiwe wanahudhuria Swalaah za Jamaa?”

[12] Hadiyth hii inatufundisha kwamba, Imaam asirefushe kisomo chake ndani ya Swalaah asiwakere Maamuma wake, wasije kuiepuka Swalaah ya Jamaa. Hadiyth nyingine inayoifuatia hii inatoa sababu za kutorefusha kisomo, lakini pia kisifupishwe kwa kiasi cha Maamuma kushindwa hata kukamilisha kisomo chake au Swalaah yake. Njia iliyo sahihi ni kuswalisha kwa namna ya wastani kwa mujibu wa Sunnah ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)

[13] [Ash-Sams (91)]

 

[14] [Al-A’laa (87)]

 

[15] [Al-‘Alaq (96)]

 

[16] [Al-Layl: (92)]

[17] Hadiyth nyingine inaripoti kwamba, Mu’aadh alikuwa kwanza anaswali nyuma ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), kisha anaswali Nafl (Swalaah ya khiari, ya Sunnah), na kisha alikuwa anakwenda kuswalisha katika Msikiti mwingine. Hii inaonyesha kuwa, mtu anaweza kuswali Swalaah yake ya faradhi nyuma ya Imaam anayeswali Swalaah yake ya Nafl.

[18] ‘Amr bin Salamah ndiye Abu Yaziyd au Abuu Burayd. Alikuja na baba yake kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Inasemekana pia kuwa hakuja na baba yake. Alikuwa katika kabila la Jarum, na akawa anaishi Basra.

[19] Hadiyth hii inaeleza kuwa, mtu anayestahili zaidi kuliko wengine wote kuwa Imaam ni yule anayejua Shari’a zaidi kuliko wote. Ikiwa watu wawili wana ujuzi sawa, yule ambaye ni mwenye taqwa zaidi ndiye awe Imaam. Vigezo hivyo pia vimetajwa katika usimulizi wa Ibn Mas-‘uwd.

[20] Hadiyth hii inaonyesha kuwa mtoto ambaye bado hajabaleghe anaweza kumswalisha mtu mkubwa au kundi la watu wakubwa iwapo anatokezea kuwa mjuzi zaidi kuliko wale wakubwa kwenye mambo ya Shariy’ah.

[21] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba walipohamia Madiynah kutoka Makkah.

[22] Imeripotiwa katika Swahiyh mbili kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwakhutubia watu huku uso wake umewaelekea wao, na akawaamrisha wanyooshe safu (misitari) zao vinginevyo Allaah (عزّ وجلّ) Atafanya kutopatana ndani ya nyoyo zenu. Msimuliaji anasema aliwaona watu wanaoswali jamaa walikuwa wakisogezeana vifundo vya miguu na mikono yao karibu karibu. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema huku akimuapia Allaah (عزّ وجلّ)  kuwa iwapo safu za ndani ya Swalaah zinaacha mapengo, anaweza kumuona shaytwaan mle. Pamoja na hii, zipo Hadiyth nyingi zinazozungumzia mpangilio wa safu katika Swalaah.

[23] Safu ya mwisho ya wanaume ni mbaya kwa sababu kwa kuwa imenyimwa fadhila za kuwa katika safu ya kwanza. Safu ya mwisho kuliko zote kwa mwanamke ndio bora zaidi kwa sababu iko mbali zaidi kuweza kuchanganyika na wanaume. Lakini iwapo jamaa ni  ya wanawake watupu na Swalaah hiyo ya jamaa inaswalishwa na mwanamke, basi kanuni hiyo hiyo inahusika kwa wanawake pia, yaani safu ya kwanza ya wanawake hao ni bora zaidi kuliko safu ya mwisho sawa sawa na wanaume.

[24] Hukmu ni kwamba, wanaume sharti wapange safu kwanza, kisha watoto na kisha wanawake. Endapo yupo mwanamme mmoja na mtoto mmoja, basi wote wawili wasimame safu moja.

[25] Mwanamke mmoja tu anaruhusiwa aswali nyuma ya safu ya mwisho ya wanaume kukiwa hakuna mwanamke mwingine wa kuungana naye.

[26] Maana yake ni kuwa: “Allaah (عزّ وجلّ)  na Aongeze shauku au himma yako ya kufanya matendo ya uadilifu, lakini tendo hilo lisikiuke mipaka.”

[27] Waabiswah bin Ma’bad ndiye Answaar kutoka katika ukoo wa Asad bin Khuzaymah. Alipewa jina la utani la Abuu Qirswaafah. Kwanza aliishi Kufa, kisha akahamia Al-Hira na akafariki mnamo mwaka 90 A.H.

[28] Kama Swalaah ya mtu anayeswali peke yake nyuma ya safu inakubalika au laa ni suala lenye kutofautiana na linalohitaji majadiliano zaidi. Ukweli ni kuwa mtu asiswali kwa kusimama peke yake wakati Swalaah ya Jamaa inaendelea.

[29] Nukta nyingine yenye kutofautiana ni kama sehemu ya Swalaah iliyobakia anayoiswali mtu nyuma ya Imaam katika Swalaah ya jamaa, ihesabike kuwa ni sehemu ya mwanzo ya Swalaah au kama ihesabike kuwa ni sehemu ya mwisho.

[30] Umm Waraqah huyu ndiye Bint Nawfal, au Bint ‘Abdillaah bin Al-Haarith bin ‘Uwaymr Al-Answaariyyah. Alikusanya Qur-aan na akamuomba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amruhusu ashiriki katika vita vya Badr. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akimzuru na akimwita “Shahidi”. Aliuliwa na watumwa wake wa kiume na wa kike kwa kumziba pumzi na nguo. Kisha wakakimbia, lakini walikamatwa na wakauliwa kwa amri ya ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)

[31] Hadiyth hii inaeleza kuwa inaruhusiwa kwa mwanamke kuswalisha. Ni ukweli uliothibitishwa kuwa ‘Aaishah na Ummu Salamah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) waliwahi kuswalisha. Imaam Shawkaan alisema kuwa, mwanamke akiswalisha, asisimame peke yake mbele ya safu, bali naye asimame ndani ya safu. Iwapo katika Maamuma wake wamo wanaume pia, basi ni sharti wawe Mahaarim (wasioweza kuwaoa). Mwanamke hawezi hadhara ya watu ambao kuna watu wageni au watu wasio mahaarim wake.

[32] Hadiyth hii inaweka wazi kabisa kuwa kipofu asiyeona anafaa kuswalisha. Wanazuoni wengine huafiki hili, lakini hiyo ni kinyume cha desturi. Wanazuoni wengine husema kuwa, pakiwepo Mwanazuoni mwenye uwezo kamili wa kuona, si sahihi kumuomba Mwanazuoni asiyeona kuswalisha na oni hili ni batili pia. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuamuamrisha  ‘Abdallaah bin Umm Maktwum (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) pamoja na kutoona kwake aswalishe kiasi cha mara kumi na tatu.

[33] Nukta inayodhihirishwa hapa ni kuwa, inaruhusiwa kuswali nyuma ya mtu anayepuuza kutekeleza mambo ya waajib. Lakini mtu kama huyo asiteuliwe kamwe kuwa Imaam, yaani asipewe kazi ya kuswalisha.

 

Share

11-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Swalaah Ya Msafiri Na Mgonjwa

 

بُلُوغُ الْمَرام

 

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

 

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ صَلَاةِ اَلْمُسَافِرِ وَالْمَرِيضِ

 

11-Mlango Wa Swalaah Ya Msafiri Na Mgonjwa

 

 

 

 

 

341.

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {أَوَّلُ مَا فُرِضَتْ اَلصَّلَاةُ رَكْعَتَيْنِ ،  فَأُقِرَّتْ صَلَاةُ اَلسَّفَرِ وَأُتِمَّتْ صَلَاةُ اَلْحَضَرِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْه

وَلِلْبُخَارِيِّ: {ثُمَّ هَاجَرَ،  فَفُرِضَتْ أَرْبَعًا،  وَأُقِرَّتْ صَلَاةُ اَلسَّفَرِ عَلَى اَلْأَوَّلِ} 

زَادَ أَحْمَدُ: {إِلَّا اَلْمَغْرِبَ فَإِنَّهَا وِتْرُ اَلنَّهَارِ،  وَإِلَّا اَلصُّبْحَ،  فَإِنَّهَا تَطُولُ فِيهَا اَلْقِرَاءَةُ } 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Mwanzo kufaradhishwa Swalaah ni Rakaa mbili[1], baadaye zikabakishwa (Hizo Rakaa mbili) kuwa Swalaah ya safari. Na Swalaah ya mkazi ikatimizwa (kwa kuongezwa Rakaa mbili nyingine).” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na katika mapokezi ya Al-Bukhaariy: “Kisha (Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akahajiri kwa hiyo Rakaa zikafaradhishwa nne, na Swalaah ya safari ikaachwa juu ya hali yake ya mwanzo.”

 

Na Ahmad aliongezea: “Isipokuwa Swalaah ya Magharibi kwani hiyo ni (Swalaah ya) Witr ya mchana, na isipokuwa Swalaah ya Alfajiri kwani hurefushwa ndani yake kisomo.”

 

 

 

 

342.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  كَانَ يَقْصُرُ فِي اَلسَّفَرِ وَيُتِمُّ،  وَيَصُومُ وَيُفْطِرُ.}  رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ،  وَرُوَاتُهُ ثِقَاتٌ. إِلَّا أَنَّهُ مَعْلُول

وَالْمَحْفُوظُ عَنْ عَائِشَةَ مِنْ فِعْلِهَا،  وَقَالَتْ: {إِنَّهُ لَا يَشُقُّ عَلَيَّ}  أَخْرَجَهُ اَلْبَيْهَقِيّ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akifupisha Swalaah safarini, na pia alikuwa akitimiza (Rakaa)[2], na alikua akifunga Swawm na akifuturu.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniyy, na wapokezi wake ni waaminifu, isipokuwa ni Hadiyth yenye ila]

 

Na imehifadhiwa kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) na ndivyo alivyokuwa anafanya na amesema (‘Aaishah): “Hakika (kufanya) hivyo si mashaka kwangu.” [Imetolewa na Al-Bayhqayy[3]]

 

 

 

343.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { إِنَّ اَللَّهَ يُحِبُّ أَنْ تُؤْتَى رُخَصُهُ كَمَا يَكْرَهُ أَنْ تُؤْتَى مَعْصِيَتُهُ}  رَوَاهُ أَحْمَدُ،  وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ،  وَابْنُ حِبَّانَ .

وَفِي رِوَايَةٍ: {كَمَا يُحِبُّ أَنْ تُؤْتَى عَزَائِمُهُ}

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika Allaah Anapenda rukhusa Zake zitumiwe, kama Anavyochukia kufanywa maasi Yake[4].” [Imetolewa na Ahmad, na akaisahihisha Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan]

Katika mapokezi mengine: “Kama Anavyopenda utekelezwe wajibu Wake.”

 

 

 

344.

وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  إِذَا خَرَجَ مَسِيرَةَ ثَلَاثَةِ أَمْيَالٍ أَوْ فَرَاسِخَ،  صَلَّى رَكْعَتَيْنِ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Pindi Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akisafiri safari ya maili tatu[5] au faraasikh[6] tatu, anaswali Rakaa mbili.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

345.

وَعَنْهُ قَالَ: {خَرَجْنَا مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  مِنْ اَلْمَدِينَةِ إِلَى مَكَّةَ، فَكَانَ يُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ رَكْعَتَيْنِ حَتَّى رَجَعْنَا إِلَى اَلْمَدِينَةِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ،  وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) tena amesema: “Tulitoka pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) toka Madiynah kwenda Makkah, akawa anaswali Rakaa mbili mbili mpaka tuliporejea Madiynah.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

 

346.

 وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {أَقَامَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم تِسْعَةَ عَشَرَ يَقْصُرُ} وَفِي لَفْظٍ: {بِمَكَّةَ تِسْعَةَ عَشَرَ يَوْمًا} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيّ

وَفِي رِوَايَةٍ لِأَبِي دَاوُدَ: {سَبْعَ عَشْرَةَ}

وَفِي أُخْرَى: {خَمْسَ عَشْرَةَ}

وَلَهُ عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ: {ثَمَانِيَ عَشْرَةَ}

وَلَهُ عَنْ جَابِرٍ: {أَقَامَ بِتَبُوكَ عِشْرِينَ يَوْمًا يَقْصُرُ اَلصَّلَاةَ}  وَرُوَاتُهُ ثِقَاتٌ،  إِلَّا أَنَّهُ اُخْتُلِفَ فِي وَصْلِه

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikaa siku kumi na tisa (safarini ambapo alikuwa) akifupisha (Swalaah zake).” Katika tamshi lingine: “Alikaa siku kumi na tisa Makkah.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

Na katika Riwaayah ya Abuu Daawuwd: “…Siku kumi na saba...[7]

 

Na katika mapokezi mengine tena: “…Siku kumi na tano…”

 

Yeye (Abuu Daawuwd) tena amepokea kutokana na masimulizi ya ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “…Siku kumi na nane…”

 

(Abuu Daawuwd) tena amepokea Hadiyth ya Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikaa Tabuwk siku ishirini, akifupisha Swalaah.” [Wapokezi wake wanategemewa, isipokuwa wamekhitilafiana kuhusu muunganiko wake]

 

 

 

347.

وَعَنْ أَنَسٍ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  إِذَا اِرْتَحَلَ قَبْلَ أَنْ تَزِيغَ اَلشَّمْسُ أَخَّرَ اَلظُّهْرَ إِلَى وَقْتِ اَلْعَصْرِ،  ثُمَّ نَزَلَ فَجَمَعَ بَيْنَهُمَا،  فَإِنْ زَاغَتْ اَلشَّمْسُ قَبْلَ أَنْ يَرْتَحِلَ صَلَّى اَلظُّهْرَ،  ثُمَّ رَكِبَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَفِي رِوَايَةِ اَلْحَاكِمِ فِي "اَلْأَرْبَعِينَ" بِإِسْنَادِ اَلصَّحِيحِ: {صَلَّى اَلظُّهْرَ وَالْعَصْرَ،  ثُمَّ رَكِبَ}.

وَلِأَبِي نُعَيْمٍ فِي "مُسْتَخْرَجِ مُسْلِمٍ": {كَانَ إِذَا كَانَ فِي سَفَرٍ،  فَزَالَتْ اَلشَّمْسُ صَلَّى اَلظُّهْرَ وَالْعَصْرَ جَمِيعًا،  ثُمَّ اِرْتَحَلَ}  

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa safarini na akaendelea safari kabla jua halijapinduka, aliakhirisha Swalaah ya Adhuhuri hadi wakati wa Alasiri. Kisha alishuka na akaziunganisha Swalaah zote mbili. Jua likipinduka kabla hajaondoka anaswali Adhuhuri kisha anapanda mnyama wake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Katika mapokezi ya Al-Haakim iliyonukuliwa katika Al-Arba’iyn kwa Isnaad Swahiyh: “Aliswali Adhuhuri na Alasiri kisha akapanda mnyama wake na akaendelea na safari yake.”

 

Na Abuu Nu’aym (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alisimulia katika matoleo ya Muslim: “Akiwa safarini, kama jua limevuka, alikuwa akiswali Dhuhuri na Alasiri pamoja, kisha aliendelea na safari yake.”

 

 

 

348.

وَعَنْ مُعَاذٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: {خَرَجْنَا مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  فِي غَزْوَةِ تَبُوكَ، فَكَانَ يُصَلِّي اَلظُّهْرَ وَالْعَصْرَ جَمِيعًا،  وَالْمَغْرِبَ وَالْعِشَاءَ جَمِيعًا}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Mu’aadh (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tuliondoka pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika vita vya Tabuwk akawa anaswali Adhuhuri na Alasiri pamoja[8], na Swalaah ya Magharibi na ‘Ishaa pamoja.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

349.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  : { لَا تَقْصُرُوا اَلصَّلَاةَ فِي أَقَلَّ مِنْ أَرْبَعَةِ بُرُدٍ; مِنْ مَكَّةَ إِلَى عُسْفَانَ}  رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ  وَالصَّحِيحُ أَنَّهُ مَوْقُوفٌ، كَذَا أَخْرَجَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ

Kutoka kwa Ibn ‘Abaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema:  Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msifupishe Swalaah katika umbali usiozidi burud nne;[9] kutoka Makkah mpaka ‘Usfaan.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniyy kwa Isnaad dhaifu, lililo sahihi ni kuwa hiyo ni Mawquwf, kadhalika ameipokea Ibn Khuzaymah]

 

 

 

350.

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {خَيْرُ أُمَّتِي اَلَّذِينَ إِذَا أَسَاءُوا اِسْتَغْفَرُوا،  وَإِذَا سَافَرُوا قَصَرُوا وَأَفْطَرُوا}  أَخْرَجَهُ اَلطَّبَرَانِيُّ فِي "اَلْأَوْسَطِ" بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ.

وَهُوَ فِي مُرْسَلِ سَعِيدِ بْنِ اَلْمُسَيَّبِ عِنْدَ اَلْبَيْهَقِيِّ مُخْتَصَر

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Walio bora katika Ummah wangu ni wale ambao wakitenda dhambi huomba maghfirah kwa Allaah, na wakiwa safarini, wanafupisha Swalaah na kuacha kufunga Swawm.” [Imetolewa na Atw-Twabaraaniyy ameiandika katika Al-Aswatw kwa Isnaad dhaifu]

 

Al-Bayhaqiyy ameipokea kwa ufupi kuwa ni Mursal kutoka kwa Sa’iyd bin Al-Musayyib.

 

 

 

351.

 وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {كَانَتْ بِي بَوَاسِيرُ،  فَسَأَلْتُ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم عَنْ اَلصَّلَاةِ؟ فَقَالَ: "صَلِّ قَائِمًا،  فَإِنْ لَمْ تَسْتَطِعْ فَقَاعِدًا،  فَإِنْ لَمْ تَسْتَطِعْ فَعَلَى جَنْبٍ"} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ.

Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nilikuwa na maradhi ya bawasiri, nikamuuliza Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) juu ya Swalaah. Akasema: “Swali kwa kusimama, na ukiwa huwezi hivyo swali kwa kukaa, na ukiwa huwezi hivyo, swali kwa kulalia ubavu.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

352.

 وَعَنْ جَابِرٍ قَالَ: {عَادَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم مَرِيضًا،  فَرَآهُ يُصَلِّي عَلَى وِسَادَةٍ،  فَرَمَى بِهَا،  وَقَالَ: "صَلِّ عَلَى اَلْأَرْضِ إِنْ اِسْتَطَعْتَ،  وَإِلَّا فَأَوْمِ إِيمَاءً،  وَاجْعَلْ سُجُودَكَ أَخْفَضَ مِنْ رُكُوعِكَ"} رَوَاهُ اَلْبَيْهَقِيُّ. وَصَحَّحَ أَبُو حَاتِمٍ وَقْفَهُ.

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alizuru mgonjwa, akamkuta anaswali juu ya mto (tandiko). Akalitupa na akamuambia: “Swalia juu ya ardhi ukiweza, laa sivyo swali kwa ishara[10], na zifanye Sijdah zako kuwa chini zaidi kuliko rukuu zako.” [Imetolewa na Al-Bayhaqiyy, na Abuu Haatim akaipa daraja Mawquwf]

 

 

 

353.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {رَأَيْتُ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  يُصَلِّي مُتَرَبِّعًا}  رَوَاهُ النَّسَائِيُّ. وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nilimuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) anaswali huku ameketi chini kwa kuikunja miguu yake.[11] [Imetolewa na An-Nasaaiy na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

 


[1] Hii inajulisha kwamba hapo mwanzoni, Swalaah ya fardhi ilikuwa inaswaliwa kwa Rakaa mbili tu (kama Swalaah ya safari). Baadaye urefu wa Swalaah za wakazi wa kudumu uliongezwa na urefu wa Swalaah ya safari ukabakia Rakaa mbili,   Haijathibitishwa na mlolongo wa wapokezi kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali Swalaah kamili wakati wa safari.

[2] Mlolongo wa wapokezi kuhusu Hadiyth hii ni pamoja na ‘Alaa bin Zuhayr ambaye juu ya kujulikana kwake kuwa haifai, anajulikana kuwa si mkweli. Imaam Ibn Taymiyyah anasema kuwa anayosingiziwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni ‘Uongo’. Katika Swahiyh mbili kupitia kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuswali kamwe zaidi ya Rakaa mbili alipokuwa safarini.

[3] Hadiyth hii haiwezi kutumika kama ushahidi kwa sababu katika mlolongo wa wapokezi yupo ‘Alaa bin Zuhayr ambaye si wa kutegemewa. Pia inaipinga Hadiyth iliyosimuliwa na Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) na iliripotiwa na Al-Bukhaariy na Muslim kwamba, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kamwe hakuswali Rakaa zaidi ya mbili ya Swalaah za Rakaa nne.

[4] Hadiyth hii inadhihirisha kuwa, ni bora zaidi kuswali Swalaah ya Rakaa mbili, na kuswali kamili ni kukosa kutumiza Sunnah.

[5] Kuna mashaka katika Hadiyth hii kama ilitajwa maili tatu au farsakh tatu. Hadiyth ya awali haikutaja hili, lakini ni mashaka ya msimuliaji wa mlolongo wa wapokeaji kama Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alitumia maneno: “Maili tatu” au “farsakh tatu”. Ni lazima tujue hilo ili tuweze “kuswali Swalaah ya Rakaa mbili.” Hakuna umbali uliotajwa katika Hadiyth yoyote, kama ile ruhusa ya kuchukua wudhuu kwa Tayammum (kutwawadha kwa mchanga) wakati mtu yumo safarini, umbali wakati wa safari umeachwa wazi sana kiasi kwamba imeruhusiwa kuswali Rakaa mbili wakati wa safari yoyote ile. Inaelekea Hadiyth hii inaonyesha kuwa “Safari ya maili tatu” ni safari khasa, lakini kwa kuwa Shu’ba anaitilia shaka, Wanazuoni wengine wameamua kuwa umbali uwe farsakh tatu (yaani maili tisa). Wanazuoni wengine wamependekea maili 36, wengine maili 48, na wengine maili 52. Rejea ya kuhusu maili 48 ni imara zaidi, kwa kuwa Ahnaf na Wanazuoni wa Hadiyth wanapendekeza hiyo. Lakini hizi zote ni makisio ya kubahatisha tu, na hayajatolewa ushahidi wowote.

[6] Faraasikh (uwingi wa farsakh) ni kipimo cha Kiajemi cha umbali ambacho ni sawa na takribani maili tatu.

[8] Hadiyth hii inadhirisha kuwa inaruhusiwa kuunganisha Adhuhuri na Alasiri pamoja na Magharibi na ‘Ishaa wakati wa safari, bila kujali kuwa Swalaah hizo zinaswaliwa wakati mahususi wa Swalaah ya mwanzo au wakati wa Swalaah ya pili. Hali zote hizi mbili zinathibitishwa kwa mfano au desturi za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Wafuasi wa Kihanafi hawaafiki desturi hii, ambayo inamaanisha kuwa wao hawaiafiki Hadiyth hii.

[9] Burud ni wingi wa barid, ambayo inamaanisha farsakh tatu, na farsakh moja ni sawa na maili tatu.

[10] Endapo mtu hawezi hata kutoa ishara, basi husamehewa kwa muda wajibu wa kuswali. Lakini mara atakavyopona na kurejesha afya na nguvu zake, lazima aziswali zote kama deni. Ikiwa mtu amezirai na amepotewa na fahamu kabisa, husamehewa Swalaah zake kadiri anavyokuwa hana fahamu.

[11] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliketi chini vile kwa sababu maalumu. Hadiyth nyingine inasema kwamba, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliugua jipu pajani, na kadiri mtu anavyougua maradhi, anaweza kuswali kwa mkao wowote anaouweza bila kushurutishwa vyovyote. Hiyo ni zawadi kutoka kwa Allaah (عزّ وجلّ).   

Share

12-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Swalaatul-Jumu'ah (Swalaah Ya Ijumaa)

 

بُلُوغُ الْمَرام

 

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

 

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ صَلَاةُ اَلْجُمُعَةِ

 

12-Mlango Wa Swalaatul-Jumu'ah [1]

 

 

 

 

354.

عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عُمَرَ، وَأَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمْ، {أَنَّهُمَا سَمِعَا رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يَقُولُ عَلَى أَعْوَادِ مِنْبَرِهِ "لَيَنْتَهِيَنَّ أَقْوَامٌ عَنْ وَدْعِهِمُ اَلْجُمُعَاتِ، أَوْ لَيَخْتِمَنَّ اَللَّهُ عَلَى قُلُوبِهِمْ، ثُمَّ لَيَكُونُنَّ مِنَ اَلْغَافِلِينَ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar na Abuu Hurayrah (رضيَ اللهُ عَنْهُمْ) wamesema: “Walimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema huku akiwa juu ya Minbar: “Watu lazima waache kupuuza Swalaah za Ijumaa, vinginevyo Allaah Atapiga muhuri nyoyo zao, na kisha watakuwa miongoni mwa walioghafilika.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

355.

 وَعَنْ سَلَمَةَ بْنِ اَلْأَكْوَعِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: {كُنَّا نُصَلِّي مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  اَلْجُمُعَةَ، ثُمَّ نَنْصَرِفُ وَلَيْسَ لِلْحِيطَانِ ظِلٌّ نَسْتَظِلُّ بِهِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيّ

وَفِي لَفْظٍ لِمُسْلِمٍ: {كُنَّا نَجْمَعُ مَعَهُ إِذَا زَالَتِ اَلشَّمْسُ، ثُمَّ نَرْجِعُ، نَتَتَبَّعُ اَلْفَيْءَ }

Kutoka kwa Salamah[2] bin Al-Akwa’ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulikuwa tukiswali Swalaah ya Ijumaa pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kisha tunaondoka wakati kuta hazijawa na kivuli[3] tunachojihifadhi[4].” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Tulikuwa tukikusanyika pamoja naye jua linapoondoka halafu tunarejea tunatafuta vivuli.”

 

 

 

356.

وَعَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {مَا كُنَّا نَقِيلُ وَلَا نَتَغَدَّى إِلَّا بَعْدَ اَلْجُمُعَةِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ

وَفِي رِوَايَةٍ: {فِي عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم}

Kutoka kwa Sahl bin Sa’d[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Tulikuwa hatulali mchana wala hatuli chakula cha mchana isipokuwa baada ya kuswali Ijumaa.”[6] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

Katika Riwaayah nyingine: “…zama za uhai wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).”

 

 

 

357.

وَعَنْ جَابِرٍ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  كَانَ يَخْطُبُ قَائِمًا، فَجَاءَتْ عِيرٌ مِنَ اَلشَّامِ، فَانْفَتَلَ اَلنَّاسُ إِلَيْهَا، حَتَّى لَمْ يَبْقَ إِلَّا اثْنَا عَشَرَ رَجُلًا}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anatoa khutuba kwa kusimama siku ya Ijumaa. Ukaja msafara kutoka Sham (Syria, Palestina, Lebanon na Jordan). Watu wakaukimbilia hadi hakuna aliyebakia na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) isipokuwa watu kumi na wawili.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

358.

وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   مَنْ أَدْرَكَ رَكْعَةً مِنْ صَلَاةِ اَلْجُمُعَةِ وَغَيْرِهَا فَلْيُضِفْ إِلَيْهَا أُخْرَى، وَقَدْ تَمَّتْ صَلَاتُهُ}  رَوَاهُ النَّسَائِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَاللَّفْظُ لَهُ، وَإِسْنَادُهُ صَحِيحٌ، لَكِنْ قَوَّى أَبُو حَاتِمٍ إِرْسَالَهُ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Endapo mtu yeyote kawahi Rakaa ya Swalaah ya Ijumaa au Swalaah yoyote nyingine[7], basi aongeze kuswali Rakaa ingine ndipo Swalaah yake itakamilika.[8][Imetolewa na An-Nasaaiy, Ibn Maajah na Ad-Daaraqutwniy na tamshi hili ni lake. Isnaad yake ni sahihi; lakini Al-Haatim aliipa nguvu kama Mursal]

 

 

 

359.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ ، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  كَانَ يَخْطُبُ قَائِمًا، ثُمَّ يَجْلِسُ، ثُمَّ يَقُومُ فَيَخْطُبُ قَائِمًا، فَمَنْ أَنْبَأَكَ  أَنَّهُ كَانَ يَخْطُبُ جَالِسًا، فَقَدْ كَذَبَ}  أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Jaabir bin Samurah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitoa Khutbah akiwa amesimama[9], kisha anaketi, halafu anasimama tena. Na yeyote anayekuarifu kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitoa khutbah huku amekaa chini, amedanganya.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

360.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  إِذَا خَطَبَ، احْمَرَّتْ عَيْنَاهُ، وَعَلَا صَوْتُهُ، وَاشْتَدَّ غَضَبُهُ، حَتَّى كَأَنَّهُ مُنْذِرُ جَيْشٍ يَقُولُ: صَبَّحَكُمْ وَمَسَّاكُمْ، وَيَقُولُ: "أَمَّا بَعْدُ، فَإِنَّ خَيْرَ اَلْحَدِيثِ كِتَابُ اَللَّهِ، وَخَيْرَ اَلْهَدْيِ هَدْيُ  مُحَمَّدٍ، وَشَرَّ اَلْأُمُورِ مُحْدَثَاتُهَا، وَكُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَفِي رِوَايَةٍ لَهُ كَانَتْ خُطْبَةُ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  يَوْمَ اَلْجُمُعَةِ: {يَحْمَدُ اَللَّهَ وَيُثْنِي عَلَيْهِ، ثُمَّ يَقُولُ عَلَى إِثْرِ ذَلِكَ، وَقَدْ عَلَا صَوْتُهُ}

وَفِي رِوَايَةٍ لَهُ: {مَنْ يَهْدِهِ اَللَّهُ فَلَا مُضِلَّ لَهُ، وَمَنْ يُضْلِلْ فَلَا هَادِيَ لَهُ }

وَلِلنَّسَائِيِّ: {وَكُلَّ ضَلَالَةٍ فِي اَلنَّارِ }

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdullaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa akitoa khutbah, macho yake huwa mekundu, na sauti yake hupanda[10], na ghadhabu yake huwa kali, kama vile mtu anayelionya jeshi akiwaambia: “(Adui) atakushambulieni asubuhi na jioni.” Na anasema: Ammaa Ba’du[11], Hakika mazungumzo bora ni Kitabu cha Allaah, na uongozi bora kabisa ni wa Muhammad, na mambo maovu ni ya uzushi (Bid’ah) na kila Bid’ah ni upotevu.[12][Imetolewa na Muslim]

 

Na katika Riwaayah yake nyingine: “Khutbah ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) siku ya Ijumaa ilikuwa hivi: Anamhimidi Allaah na anamsifu. Kisha anakhutubiu baada ya hayo na sauti yake inapanda.”

 

Na katika Riwaayah yake (Muslim) nyingine: “Na ambaye Allaah Amemhidi, basi hapana wa kumpotoa.” [Az-Zumar: 37], “Ambao Allaah Amewapotoa, basi hakuna wa kuwahidi” [Al-A’raaf: 186] na Ambaye Allaah Anampotosha hakuna yeyote anayeweza kumhidi.”

 

Na tamshi la An-Nasaaiy: “…na kila upotovu ni Motoni.”

 

 

 

361.

وَعَنْ عَمَّارِ بْنِ يَاسِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يَقُولُ: {إِنَّ طُولَ صَلَاةِ اَلرَّجُلِ، وَقِصَرَ خُطْبَتِهِ مَئِنَّةٌ مِنْ فِقْهِهِ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Ammaar bin Yaasir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) anasema: “Urefu wa Swalaah ya mtu, na ufupi wa khutbah yake ni alama ya Fiqhi yake (uelewa)[13] katika Dini.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

362.

وَعَنْ أُمِّ هِشَامٍ بِنْتِ حَارِثَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {مَا أَخَذْتُ: "ق وَالْقُرْآنِ اَلْمَجِيدِ"، إِلَّا عَنْ لِسَانِ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يَقْرَؤُهَا كُلَّ جُمُعَةٍ عَلَى اَلْمِنْبَرِ إِذَا خَطَبَ اَلنَّاسَ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ .

Kutoka kwa Umm Hishaam[14] bint Haarithah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Sikuihifadhi Suwrah Qaaf[15] isipokuwa kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliyekuwa akiisoma kila siku ya Ijumaa juu ya Minbar[16] anapowakhutubia watu.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

363.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { مَنْ تَكَلَّمَ يَوْمَ اَلْجُمُعَةِ وَالْإِمَامُ يَخْطُبُ فَهُوَ كَمَثَلِ اَلْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا، وَاَلَّذِي يَقُولُ لَهُ: أَنْصِتْ، لَيْسَتْ لَهُ جُمُعَةٌ}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، بِإِسْنَادٍ لَا بَأْسَ بِهِ

 وَهُوَ يُفَسِّرُ حَدِيثَ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  فِي "اَلصَّحِيحَيْنِ" مَرْفُوعًا: {إِذَا قُلْتَ لِصَاحِبِكَ: أَنْصِتْ يَوْمَ اَلْجُمُعَةِ وَالْإِمَامِ يَخْطُبُ، فَقَدْ لَغَوْتَ} 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuzungumza siku ya Ijumaa wakati Imaam anakhutubia yeye ni kama punda aliyebeba vitabu[17], na anayemuambia: “Nyamaza!” basi hana Ijumaa.[18] [Imetolewa na Ahmad, kwa Isnaad isiyo na ubaya wowote]

 

Hadiyth hii inafanana na Hadiyth Marfuw’ ya Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) iliyopokewa katika Swahiyh mbili: “Utakapomuambia mwenzako: “Nyamaza!” wakati Imaam anakhutubia, basi umefanya upuuzi.”

 

 

 

364.

 وَعَنْ جَابِرٍ قَالَ: {دَخَلَ رَجُلٌ يَوْمَ اَلْجُمُعَةِ، وَالنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  يَخْطُبُ. فَقَالَ: "صَلَّيْتَ ؟" قَالَ: لَا. قَالَ: "قُمْ فَصَلِّ رَكْعَتَيْنِ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mtu mmoja aliingia Msikitini siku ya Ijumaa wakati Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akikhutubia. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Umeswali?” Akajibu: “Hapana.” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Simama uswali Rakaa mbili.”[19] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

365.

 وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ; {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقْرَأُ فِي صَلَاةِ الْجُمُعَةِ سُورَةَ الْجُمُعَةِ، وَالْمُنَافِقِينَ} رَوَاهُ مُسْلِم

وَلَهُ: عَنِ اَلنُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ: {كَانَ يَقْرَأُ فِي اَلْعِيدَيْنِ وَفِي الْجُمُعَةِ: بِـ "سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ اَلْأَعْلَى"، وَ: "هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ اَلْغَاشِيَةِ" }

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anasoma katika Swalaah ya Ijumaa Suwrah Al-Jumu’ah na Al-Munaafiquwn.

Suwrah Al-Jumua’ah[20] na Al-Munaafiquwn[21].” [Imetolewa na Muslim]

Naye (Muslim) amenukuu Hadiyth ya Nu’maan bin Bashiyr[22] amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anasoma katika Swalaah ya ‘Iyd mbili na Swalaah ya Ijumaa[23]

 

 

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى[24]  

na

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ[25]

 

 

 

 

 

 

366.

وَعَنْ زَيْدِ بْنِ أَرْقَمَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: {صَلَّى النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  اَلْعِيدَ، ثُمَّ رَخَّصَ فِي الْجُمُعَةِ، فَقَالَ: "مَنْ شَاءَ أَنْ يُصَلِّيَ فَلْيُصَلِّ"}  رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا اَلتِّرْمِذِيَّ، وَصَحَّحَهُ ابْنُ خُزَيْمَة

Kutoka kwa Zayd bin Arqam (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali ‘Iyd (Siku ya Ijumaa), na akaruhusu iswaliwe Swalaah ya Ijumaa akasema: Anaetaka kuiswali aswali.”[26] [Imetolewa na Al-Khamsah (An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa At-Tirmidhiy. Na akaisahihisha Ibn Khuzaymah]

 

 

 

367.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمُ الْجُمُعَةَ فَلْيُصَلِّ بَعْدَهَا أَرْبَعًا}  رَوَاهُ مُسْلِم

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Yeyote kati yenu ataswali Swalaah ya Jumua’ah basi na aswali Rakaa nne baadaye.”[27] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

368.

وَعَنِ السَّائِبِ بْنِ يَزِيدَ، أَنَّ مُعَاوِيَةَ قَالَ لَهُ: {إِذَا صَلَّيْتَ الْجُمُعَةَ فَلَا تَصِلْهَا بِصَلَاةٍ، حَتَّى تُكَلَّمَ أَوْ تَخْرُجَ، فَإِنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  أَمَرَنَا بِذَلِكَ: أَنْ لَا نُوصِلَ صَلَاةً بِصَلَاةٍ حَتَّى نَتَكَلَّمَ أَوْ نَخْرُجَ}  رَوَاهُ مُسْلِم

Kutoka kwa As-Saaib bin Yaziyd[28] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Mu’aawiyah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuambia: “Unaposwali Ijumaa usiiunganishe na Swalaah nyingine hadi umeongea au umekwenda nje. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alituamrisha hivyo, kuwa tusiunganishe Swalaah moja na Swalaah nyingine, mpaka mtu tumeongea au tumetoka nje.”[29] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

369.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { مَنِ اغْتَسَلَ، ثُمَّ أَتَى الْجُمُعَةَ، فَصَلَّى مَا قُدِّرَ لَهُ، ثُمَّ أَنْصَتَ، حَتَّى يَفْرُغَ اَلْإِمَامُ مِنْ خُطْبَتِهِ، ثُمَّ يُصَلِّي مَعَهُ: غُفِرَ لَهُ مَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجُمُعَةِ اَلْأُخْرَى، وَفَضْلُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ}  رَوَاهُ مُسْلِم

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuoga, kisha akaja kuswali Ijumaa na akaswali alichopangiwa[30], halafu akanyamaza mpaka Imaam amemaliza khutbah, halafu akaswali pamoja naye, ataghufiriwa (madhambi) kati ya Ijumaa hiyo na inayofuatia na kwa siku tatu zaidi.”[31] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

370.

وَعَنْهُ; أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  ذَكَرَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ فَقَالَ: {فِيهِ سَاعَةٌ لَا يُوَافِقُهَا عَبْدٌ مُسْلِمٌ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي، يَسْأَلُ اَللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ شَيْئًا إِلَّا أَعْطَاهُ إِيَّاهُ، وَأَشَارَ بِيَدِهِ يُقَلِّلُهَا}  مُتَّفَقٌ عَلَيْه

وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ: {وَهِيَ سَاعَةٌ خَفِيفَةٌ}  

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliitaja siku ya Ijumaa akasema: “Katika siku hii kuna muda ambapo hakuna mja Muislamu atakayesimama kuswali na anamuomba lolote isipokuwa Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Atampa hilo jambo”[32] Akaashiria kwa mkono wake kuwa muda huo ni mdogo sana.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Na muda huo ni hafifu.”

 

 

 

371.

وَعَنْ أَبِي بُرْدَةَ عَنْ أَبِيهِ سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يَقُولُ: {هِيَ مَا بَيْنَ أَنْ يَجْلِسَ اَلْإِمَامُ إِلَى أَنْ تُقْضَى اَلصَّلَاةُ}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ،

 وَرَجَّحَ اَلدَّارَقُطْنِيُّ أَنَّهُ مِنْ قَوْلِ أَبِي بُرْدَةَ

وَفِي حَدِيثِ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ سَلَامٍ عِنْدَ ابْنِ مَاجَه

وَجَابِرِ عِنْدَ أَبِي دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيِّ  : {أَنَّهَا مَا بَيْنَ صَلَاةِ اَلْعَصْرِ إِلَى غُرُوبِ اَلشَّمْسِ}

وَقَدْ اِخْتُلَفَ فِيهَا عَلَى أَكْثَرَ مِنْ أَرْبَعِينَ قَوْلًا، أَمْلَيْتُهَا فِي "شَرْحِ اَلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa Abuu Burdah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa baba yake amesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Muda huo ni baina ya Imaam anapokaa mpaka mwisho wa Swalaah.” [Imetolewa na Muslim]

 

Na Ad-Daaraqutwniyy ana kauli kama ya Abuu Burdah.

 

Katika Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Salaam iliyopokewa na Ibn Maajah

Pia Hadiyth ya Jaabir iliyopokewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy: “Muda huo ni baina ya Swalaah ya Alasiri na kukuchwa kwa jua (Magharibi).”

 

Kuna kauli zaidi ya arubaini kuhusu muda huo, na nimezinukuu katika “Sharh Al-Bukhaariy”

 

 

 

372.

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: {مَضَتِ السُّنَّةُ أَنَّ فِي كُلِّ أَرْبَعِينَ فَصَاعِدًا جُمُعَةً} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيف

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Sunnah[33] imekuwa ni kuwa katika kila watu arubaini au zaidi ni Ijumaa.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy kwa Isnaad dhaifu[34]]

 

 

 

373.

وَعَنْ سَمُرَةَ بنِ جُنْدُبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَسْتَغْفِرُ لِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ كُلَّ جُمُعَةٍ}  رَوَاهُ اَلْبَزَّارُ بِإِسْنَادٍ لَيِّن

Kutoka kwa Samurah bin Jundub (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiombea maghufirah Waumini wanaume na Waumini wanawake katika kila Ijumaa.” [Imetolewa na Al-Bazzaar kwa Isnaad laini]

 

 

 

374.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  كَانَ فِي اَلْخُطْبَةِ يَقْرَأُ آيَاتٍ مِنَ اَلْقُرْآنِ، وَيُذَكِّرُ اَلنَّاسَ}  رَوَاهُ أَبُو دَاوُد وَأَصْلُهُ فِي مُسْلِم

Kutoka kwa Jaabir bin Samurah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa anakhutubia alisoma Aayah kadhaa za Qur-aan, na anawakumbusha watu[35].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, na chanzo chake ni katika Swahiyh Muslim]

 

 

 

375.

وَعَنْ طَارِقِ بْنِ شِهَابٍ; أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {الْجُمُعَةُ حَقٌّ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ فِي جَمَاعَةٍ إِلَّا أَرْبَعَةً: مَمْلُوكٌ، وَاِمْرَأَةٌ، وَصَبِيٌّ، وَمَرِيضٌ}  رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَقَالَ: لَمْ يَسْمَعْ طَارِقٌ مِنَ اَلنَّبِيِّ

وَأَخْرَجَهُ اَلْحَاكِمُ مِنْ رِوَايَةِ طَارِقٍ اَلْمَذْكُورِ عَنْ أَبِي مُوسَى 

Kutoka kwa Twaariq bin Shihaab[36] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah ya Ijumaa kwa jamaa ni waajibu kwa kila Muislamu isipokuwa wane: mtumwa, mwanamke, mtoto na mgonjwa.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akasema: Twaariq hakusikia (haya) kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)]

 

Al-Haakim ameyapokea haya kutoka kwa Twaariq aliyetajwa hapa, naye kutoka kwa Abuu Muwsaa.

 

 

 

376.

وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَيْسَ عَلَى مُسَافِرٍ جُمُعَةٌ}  رَوَاهُ اَلطَّبَرَانِيُّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيف

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaah ya Ijumaa si lazima kwa msafiri.”[37] [Imetolewa na Atw-Twabaraaniyy kwa Isnaad dhaifu]

 

 

 

377

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  إِذَا اسْتَوَى عَلَى الْمِنْبَرِ اسْتَقْبَلْنَاهُ بِوُجُوهِنَا}  رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ

وَلَهُ شَاهِدٌ مِنْ حَدِيثِ الْبَرَاءِ عِنْدَ اِبْنِ خُزَيْمَة

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa sawasawa juu ya minbar, sisi tunamuelekea kwa nyuso zetu.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy kwa Isnaad dhaifu]

 

Nayo ina ushahidi wa Hadiyth ya Al-Baraa iliyopokelewa na Ibn Khuzaymah.

 

 

 

378.

وَعَنِ اَلْحَكَمِ بْنِ حَزْنٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: {شَهِدْنَا الْجُمُعَةَ مَعَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  فَقَامَ مُتَوَكِّئًا عَلَى عَصًا أَوْ قَوْسٍ}  رَوَاهُ أَبُو دَاوُد

Kutoka kwa Al-Hakam bin Hazn[38] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulihudhuria Swalaah ya Ijumaa pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), naye akasimama wima akiegemea fimbo au upinde.”[39] [Imetolewa na Abuu Daawuwd]

 

 

 

 

 


[1] Siku ya Ijumaa ilikuwa ikijulikana kama Al-‘Aruwbah zama za Jaahiliyyah (kipindi kabla ya Uislamu kuja). Uislamu ukaita Jumua’ah kwa kuwa Waislamu wa mji hukusanyika (Jamaa) ili kuswali na kumwabudu Allaah (عزّ وجلّ). Zaidi ya hizi, zipo sababu zingine pia.

[2] Salamah bin Al-Akwa’ ndiye Abuu Muslim, Salamah bin ‘Amr bin Al-Akwa’ Sinaan bin ‘Abdillaah Al-Aslamiy Al-Madaniy. Alikuwa mmoja wa Maswahaba mashujaa, na alikuwa akikimbia kwa kasi zaidi kuliko farasi kwa miguu yake. Alikuwa ni mtu mzuri, Mwenye taqwa, na mkarimu sana. Alifia Al-Madiynah mnamo mwaka wa 74 A.H.

[3] Hadiyth hii inasema wazi kwamba, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akimaliza Swalaah yake ya Ijumaa katika wakati ambao vivuli vya kuta vilikuwa havitoshi kuwafunika watu. Yaani Swalaah ya Ijumaa ni sharti iswaliwe mapema.

[4] Kwa mujibu wa Imaam Ahmad bin Hambal, inaruhusiwa kuanza kuswali Swalaah ya Ijumaa kabla ya Zawaal (jua halijageuka). Maimaamu waliobaki na Wanazuoni wengi wanasema kwamba Swalaah ya Ijumaa sharti ianze kuswaliwa mara baada ya zawaal. Siku hizi imekuwa desturi kuiahirisha Swalaah ya Ijumaa mbele zaidi, hata baada ya Adhuhuri yenyewe, ambaye ni kinyume na mwenendo wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).

[5] Sahl bin Sa’d ndiye Abdul-‘Abbaas Al-Khazraji As-Sa’d Al-Answaariy. Aliripoti Hadiyth mia moja, na alifariki mnamo mwaka 91 A.H. akiwa na umri wa takribani miaka mia moja. Inasemekana kuwa alikuwa Swahaba wa mwisho kufariki Al-Madiynah.

[6] Haimaanishi kuwa alikuwa akiswali Swalaah ya Ijumaa hata kabla ya wakati wa zawaal (kugeuka kwa jua). Swalaah ya Ijumaa huitangulia Swalaah ya Adhuhuri. Na kadri inavyohitaji kusomwa khutbah, ni waajibu kuswali haraka, ili Swalaah imalizike ndani ya wakati wa mwanzo wa Adhuhuri.

[7] Usimulizi ambao unanasibishwa na Abuu Hurayrah katika Swahiyh mbili, haikusudii Swalaah ya Ijumaa peke yake, bali umejumuisha Swalaah zote. Madhali mtu kawahi Rakaa kamili na Imaam, anapata thawabu za Swalaah ya jamaa. Hii inahusu Swalaah ya Ijumaa pia. Kisha mtu huyo asimame na kukamilisha sehemu ya Swalaah iliyobakia.

[8] Hadiyth hii inakanusha maoni ya wale wanaodai kuwa Swalaah ya Ijumaa haikubaliki hadi mtu awe kasikiliza sehemu ya khutbah.

[9] Hadiyth hii inadhihirisha kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiwakhutubia watu Msikitini huku amesimama wima. Pia inadhihirisha kwamba, katika Swalaah ya Ijumaa, kutoa khutbah kwa sehemu mbili kunafuata Sunnah, na kwamba ni Sunnah pia kuketi chini kwa muda mfupi katika sehemu mbili hizo za khutbah; na kuikhalifu Sunnah hii ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kunahesabika kuwa ni bid’ah (iuzushi).

[10] Hadiyth hii inatufunza kwamba, khutbah ni sharti itolewe kwa sauti kubwa, na itolewe kwa njia mbayo itatoa athari ya kutosha kwa wanaosikiliza.

[11] Hayo ni maneno ya ufunguzi wa khutbah ya Kiislamu inayomaanisha: “Baada ya huo utangulizi.”

[12] Kwa mujibu wa Shariy’ah, bid’ah ni tendo lolote ambalo halijatajwa au kuthibitishwa na Qur-aan wala Sunnah, wala haitokani na hizo. Maneno yale yasemayo “Kullu bid’ah (kila uzushi)” inaashiria kuwa bid’ah zote ni mbaya au hakuna uzushi (bid’ah) uliokuwa na uzuri wowote, kwa taarifa za kina, rejea kitabu cha Al-I’tiswaam cha Imaam Ash-Shaatwibiyy.

[13] Hii inadhihirisha kwamba, mtu sharti arefushe Swalaah yake na aifupishe khutbah. Baadhi ya Makhatibu   siku hizi hurefusha mno khutbah, kiasi kwamba huuingilia muda wa Swalaah, na kisha hujaribu kuimaliza Swalaah kwa haraka. Hii ni kinyume na mwenendo wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)

[14] Umm Hishaam ndiye Umm Hishaam bint Haarithah bin Nu’umaan, dada (kwa upande wa Mama) wa ‘Umrah bint ‘Abdir-Rahmaan. Yeye ni Answaariyyah kutoka katika ukoo wa Najjaar. Inasemekana kuwa alishiriki katika Bay’atur-Ridhwaan.

[15] Qaaf (50)

[16] Hii ndiyo Shariy’ah kwetu kuwa, wakati tunawakhutubia watu kabla ya kuwaswalisha Swalaah.

[17] Mtu kama huyo anafanana na punda (mnyama wa kubeba mizigo), kwa vile hapati faida yoyote kwa kule kubeba vitabu vingi mgongoni kwake. Halikadhalika mtu huyo hapati faida yoyote kwa kuswali Swalaah ya Ijumaa.

[18] Zingatia kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakusema Swalaah ya mtu huyo haitakubaliwa, bali atanyimwa fadhila za Swalaah ya Ijumaa. Kwa hivyo Wanazuoni wamebainisha kutoka katika hilo kuwa mtu yeyote atakayeshiriki mazungumzo bila shaka atapata thawabu za Swalaah, lakini atanyimwa thawabu zinazonasibishwa na Swalaah ya Ijumaa.

[19] Usimulizi wa Al-Bukhaariy unao neno: “Khafiyfatayn (Khafifu mbili)” baada ya neno “Raka’tayn (Rakaa mbili)”, yaani inamaanisha kuwa yule mtu aliagizwa aswali Rakaa mbili lakini ziwe nyepesi ili ahifadhi muda mrefu zaidi wa kusikiliza khutbah.

[20] Al-Jumua’ah  (62)

[21] Al-Munaafiquwn (63)

[22] Nu’umaan bin Bashiyr ndiye Abuu ‘Abdullaah Al-Answaariyy Al-Madaniy, na alikuwa mtoto wa kwanza wa Kianswaar kuzaliwa baada ya Hijrah (kuhama) ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alizaliwa mnamo mwezi wa kumi na tatu wa Hijrah. Alilowea Sham na baadaye akawa gavana wa Kufa na kisha Hims. Khaalid bin Khali Al-Kilaa’i alimuua yeye Abuu ‘Abdullaah Al-Answaariyy katika siku ya Rahit mnamo mwaka 64 A.H.

[23] Miongoni mwa Suwrah hizi alikuwa akisoma Suwrah tofauti nyakati mbalimbali.

[24] [Al-A’laa (87)]

 

[25] Al-Ghaashiyah (88)

[26] Hii inaleta ushahidi kwamba, iwapo siku kuu ya ‘Iyd inaangukia siku ya Ijumaa, siyo lazima kuswali Swalaah ya Ijumaa, lakini ni bora kuswali Ijumaa.

[27] Kuna tofauti ya maoni ya Rakaa ngapi ziswaliwe kama Sunnah baada ya Swalaah ya Ijumaa. Wengine wanatambua Rakaa mbili tu, wakati wengine hupendelea kuswali Rakaa nne. Imaam Shaafi’y na Imaam Ahmad na wengi wa Wanazuoni wameshikilia maoni hayo hayo ambayo ndiyo bora zaidi. Hadiyth ya Rakaa nne ni usemi wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mwenyewe, kwa hivyo watu wautekeleze.

[28] As-Saaib bin Yaziyd ndiye Abuu Yaziyd Al-Kindiy. Alizaliwa mnamo mwaka wa 2 A.H. na alihudhuria ile Hijjatul Wadaa’i pamoja na baba yake. Alikufa mnamo mwaka 80 A.H.

[29] Hadiyth hii inadhihirisha kwamba, endapo mtu ataiswali Swalaah fulani mahali fulani, basi asiswali Swalaah nyingine mahali palepale katika wakati uleule. Lazima uwepo umbali kati ya Swalaah hizo mbali ama kwa kubadilisha mahali au kwa njia ya Adhkaar (Kumdhukuru Allaah). Lengo la niyyah njema la kutenda hivi ni kwamba, rikodi ya matendo yake ipate kuonyeshe kuwa aliswali mahali pengi mbalimbali kadiri iwezekanavyo, au ionyeshe kuwa ameswali mara nyingi.

[30] Hakuna kikomo cha Swalaah za Sunnah (Nawaafil) mtu anazoweza kuziswali wakati akingojea Swalaah ya Ijumaa, na hakuna kikomo cha wakati. Lakini kama Hadiyth nyingine inavyosema kuwa hakukatazwi kuswali Swalaah za khiari siku ya Ijumaa hata iwe ni wakati wa zawaal.

[31] Ni ghuslu (Kuoga josho) mnamo siku ya Ijumaa ni tendo la Sunnah  kwa mujibu wa Wanazuoni wengi, ambayo ndiyo sahihi. Wengine wanaitambua kuwa ni waajib.

[32] Kuna wakati unaopatikana kila siku ya Ijumaa ambapo du’aa ya Muislamu hutakabaliwa bila shaka. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْه وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuuutaja wakati huu maalumu. Wakati huo umefichwa kama ulivyofichwa Laylatul-Qadr   ili watu watumie muda mwingi zaidi kuutafuta, na kwa hivyo wapate thawabu nyingi zaidi. Kuna nukuu mbili juu ya wakati huu. Ya kwanza inasema wakati huo ni kati ya Alasiri na machweo ya jua. Ya pili inasema wakati huo umo ndani ya wakati Imaam anapowasomea watu khutbah yake. Waislamu wajitahidi kuutafuta  wakati huu nyakati zote za siku ya Ijumaa na khasa nyakati mbili hizo.

[33] Suala kuhusu watu wangapi wakusanyike pahala ili liswihi sharti la kuswali Swalaah ya Ijumaa nalo bado lina khitilafu miongoni mwa Wanazuoni. Tarakimu tofauti zimetolewa na watu mbalimbali watu watatu, wane, tisa, kumi na mbili, ishirini, arubaini, khamsini na sabiini. Ukweli ni kwamba hakuna tarakimu iliyotolewa na Hadiyth. Swalaah zote mbili, Swalaah ya Ijumaa hata kama kuna watu wawili tu wanaoziswali. Hadiyth hii inayotaja tarakimu ni dhaifu. Imeripotiwa katika Hadiyth kwamba, Swalaah ya kwanza kabisa ya Ijumaa katika Usilamu iliswaliwa katika kijiji cha Juwaathaa.

[34] Ameipokea ‘Abdul Aziyz bin ‘Abdir-Rahmaan ambaye Hadiyth zake zimeelezewa na Wanazuoni kuwa ni za “uongo”, za ‘kughush’ na yeye mwenyewe ahisabika kuwa “si wa kutegemewa.” Kwa hivyo sharti hilo kwa Swalaah ya Ijumaa siyo sahihi.  

[35] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiwapa mawaidha watu juu ya misingi ya Uislamu, mambo ya msingi ya lazima ya Dini, na alikuwa akiwaonya watu wasighurike na anasa na starehe za dunia hii bali akiwavutia watu waelekee katika maisha ya Aakhirah.

[36] Twaariq bin Shihaab ni wa Ahmusi, Bajali, na wa Kufi, na aliishi muda mrefu katika zama za Jaahiliyyah na zama za Uislamu. Alimuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) lakini hakuwahi kusikia Hadiyth kutoka kwake. Alishiriki katika misafara ya kivita wakati wa Ukhalifa wa Abuu Bakr na ‘Umar. Alikufa mnamo mwaka 82 A.H.

[37] Hadiyth zote hizi zinaelezea kuwa, kuna aina sita za watu ambao kwao wao Swalaah ya Ijumaa siyo lazima. Hao ni watumwa, wanawake, watoto, wasafiri, wagonjwa na wanaohamahama, aina zingine mbili zaidi, yaani vipofu na walemavu wametajwa ndani ya Qur-aan. Hao wakiswali Swalaah ya Ijumaa basi hawatawajibika tena  Swalaah ya Adhuhuri.

[38] Al-Hakam bin Hazn ndiye Al-Hakam bin Hazn bin Abdil-Waahaab Al-Makhzuwm. Alisilimu katika mwaka ilipokombolewa Makkah. Na kwa hivyo akahudhuria Swalaah ya Ijumaa pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).

[39] Hii inathibitisha kwamba, Khatiyb anapotoa khutbah anaweza kuegemea kitu ili kuepusha uchovu kutokana na kisimamo cha muda mrefu.

 

 

 

Share

13-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Swalaatul-Khawf (Swalaah Kipindi Cha Ya Khofu)

 

بُلُوغُ الْمَرام

 

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

 

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ صَلَاةِ اَلْخَوْفِ

 

13-Mlango Wa Swalaatul-Khawf (Swalaah Ya Kipindi Cha Khofu)

 

 

 

 

 

379.

عَنْ صَالِحِ بْنِ خَوَّاتٍ، {عَمَّنْ صَلَّى مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يَوْمَ ذَاتِ اَلرِّقَاعِ صَلَاةَ اَلْخَوْفِ: أَنَّ طَائِفَةً صَلَّتْ مَعَهُ وَطَائِفَةٌ وِجَاهَ اَلْعَدُوِّ، فَصَلَّى بِاَلَّذِينَ مَعَهُ رَكْعَةً، ثُمَّ ثَبَتَ قَائِمًا وَأَتَمُّوا لِأَنْفُسِهِمْ، ثُمَّ اِنْصَرَفُوا فَصَفُّوا وِجَاهَ اَلْعَدُوِّ، وَجَاءَتِ اَلطَّائِفَةُ اَلْأُخْرَى، فَصَلَّى بِهِمْ اَلرَّكْعَةَ اَلَّتِي بَقِيَتْ، ثُمَّ ثَبَتَ جَالِسًا وَأَتَمُّوا لِأَنْفُسِهِمْ، ثُمَّ سَلَّمَ بِهِمْ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَهَذَا لَفْظُ مُسْلِمٍ 

وَوَقَعَ فِي "اَلْمَعْرِفَةِ" لِابْنِ مَنْدَهْ، عَنْ صَالِحِ بْنِ خَوَّاتٍ، عَنْ أَبِيهِ 

Kutoka kwa Swaalih bin Khawwaat[1] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kwa upokezi wa mtu aliyeswali pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Swalaatul-Khawf (Swalaah ya Khofu) katika vita vya Dhaat Ar-Riqaa’i[2]: “Kuwa kundi la jeshi lilijipanga safu moja pamoja naye, na kundi jingine mkabala na maadui. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaswalisha kundi lililokuwa pamoja naye Rakaa moja, kisha akabaki amesimama wima wakati wanamalizia Swalaah yao wenyewe. Wakaondoka na wakapanga safu mkabala na maadui, na kundi jingine la jeshi likaja. Akawaswalisha Rakaa iliyobaki ya Swalaah yake, kisha akabakia ameketi wakati wao wakimalizia Swalaah yao kisha akatoa nao Salaam.”[3] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

Na katika mapokezi ya Al Ma’rifah ya Ibn Mandah kutoka kwa Swaalih bin Khawwaat kutoka kwa babaake.

 

 

 

380.

وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ قَالَ: {غَزَوْتُ مَعَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  قِبَلَ نَجْدٍ، فَوَازَيْنَا اَلْعَدُوَّ، فَصَافَفْنَاهُمْ، فَقَامَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يُصَلِّي بِنَا، فَقَامَتْ طَائِفَةٌ مَعَهُ، وَأَقْبَلَتْ طَائِفَةٌ عَلَى اَلْعَدُوِّ، وَرَكَعَ بِمَنْ مَعَهُ، وَسَجَدَ سَجْدَتَيْنِ، ثُمَّ انْصَرَفُوا مَكَانَ اَلطَّائِفَةِ الَّتِي لَمْ تُصَلِّ فَجَاءُوا، فَرَكَعَ بِهِمْ رَكْعَةً، وَسَجَدَ سَجْدَتَيْنِ، ثُمَّ سَلَّمَ، فَقَامَ كُلُّ وَاحِدٍ مِنْهُمْ، فَرَكَعَ لِنَفْسِهِ رَكْعَةً، وَسَجَدَ سَجْدَتَيْنِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَهَذَا لَفْظُ اَلْبُخَارِيِّ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nilikwenda vitani pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) huko Najd[4], tulipofika mbele ya adui tulijipanga msitari tukiwakabili, akasimama Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akatuswalisha. Kundi moja likasimama pamoja naye kundi jingine limesimama mkabala na adui. Akawaswalisha Rakaa moja waliokuwa pamoja naye na akasujudu Sijdah mbili. Kisha wakaondoka wakaenda mahali pa kundi lililokuwa bado halijaswali. Wakaja na akawaswalisha Rakaa moja na akasujudu Sijdah mbili. Kisha akatoa Salaam. Kila mmoja akasimama na kuswali peke yake Rakaa moja na kusujudu Sijdah mbili.[5] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

 

381.

وَعَنْ جَابِرٍ قَالَ: {شَهِدْتُ مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  صَلَاةَ اَلْخَوْفِ، فَصَفَّنَا صَفَّيْنِ: صَفٌّ خَلْفَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  وَالْعَدُوُّ بَيْنَنَا وَبَيْنَ اَلْقِبْلَةِ، فَكَبَّرَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  وَكَبَّرْنَا جَمِيعًا، ثُمَّ رَكَعَ وَرَكَعْنَا جَمِيعًا، ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ اَلرُّكُوعِ وَرَفَعْنَا جَمِيعًا، ثُمَّ اِنْحَدَرَ بِالسُّجُودِ وَالصَّفُّ اَلَّذِي يَلِيهِ، وَقَامَ اَلصَّفُّ اَلْمُؤَخَّرُ فِي نَحْرِ اَلْعَدُوِّ، فَلَمَّا قَضَى اَلسُّجُودَ، قَامَ اَلصَّفُّ اَلَّذِي يَلِيهِ...}  فَذَكَرَ اَلْحَدِيثَ

وَفِي رِوَايَةٍ: {ثُمَّ سَجَدَ وَسَجَدَ مَعَهُ اَلصَّفُّ اَلْأَوَّلُ، فَلَمَّا قَامُوا سَجَدَ اَلصَّفُّ اَلثَّانِي، ثُمَّ تَأَخَّرَ اَلصَّفُّ اَلْأَوَّلِ وَتَقَدَّمَ اَلصَّفُّ اَلثَّانِي...}  فَذَكَرَ مِثْلَهُ

وَفِي آخِرِهِ: {ثُمَّ سَلَّمَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  وَسَلَّمْنَا جَمِيعًا}  رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

وَلِأَبِي دَاوُدَ: عَنْ أَبِي عَيَّاشٍ الزُّرَقِيِّ مِثْلُهُ، وَزَادَ: {أَنَّهَا كَانَتْ بِعُسْفَانَ}  

وَلِلنَّسَائِيِّ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ عَنْ جَابِرٍ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  صَلَّى بِطَائِفَةٍ مِنْ أَصْحَابِهِ رَكْعَتَيْنِ، ثُمَّ سَلَّمَ، ثُمَّ صَلَّى بِآخَرِينَ أَيْضًا رَكْعَتَيْنِ، ثُمَّ سَلَّمَ}

وَمِثْلُهُ لِأَبِي دَاوُدَ، عَنْ أَبِي بَكْرَةَ 

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilihudhuria Swalaatul-Khawf (Swalaah ya Khofu) pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Tulijipanga safu mbili. Safu nyuma yake na maadui wakiwa baina yetu na Qiblah. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akapiga Takbiyr nasi sote tukaitamka, kisha akarukuu na sisi sote tukarukuu, kisha akanyanyua kichwa chake baada ya kurukuu na sisi sote tukanyanyua vichwa vyetu, kisha akateremka kusujudu pamoja na safu iliyokuwa karibu yake wakati safu ya nyuma imesimama mkabala na adui. (Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)) alipomaliza kusujudu ikasimama safu iliyo karibu yake...” akaitaja Hadiyth yote mfano wake.”[6] [Imetolewa na Muslim]

 

Na katika mapokezi mengine: “...kisha safu ya kwanza ikasujudu pamoja naye, waliposimama, ikasujudu safu ya pili, halafu safu ya kwanza ikaenda nyuma na safu ya pili ikaenda mbele.” Hadiyth ikatajwa kama hiyo iliyotangulia.

 

Na mwisho wake inaeleza: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akatoa Salaam, kisha nasi sote tukatoa Salaam.” [Imetolewa na Muslim]

 

Abuu Daawuwd amepokea Hadiyth kama hiyo kutoka kwa Abuu ‘Ayyaash Az-Zuraqiyy[7] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) akaongezea: “Ilikuwa Usfaan.[8]

 

An-Nasaaiy amepokea kwa njia nyingine kutoka Hadiyth ya Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalisha kundi la Maswahaba wake Rakaa mbili, kisha akatoa Salaam, kisha akaswalisha kundi jingine Rakaa mbili, kisha akatoa Salaam.”

 

Hadiyth kama hiyo imepokewa na Abuu Daawuwd kutoka kwa Abuu Bakr.

 

 

 

382.

 وَعَنْ حُذَيْفَةَ: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  صَلَّى صَلَاةَ اَلْخَوْفِ بِهَؤُلَاءِ رَكْعَةً، وَبِهَؤُلَاءِ رَكْعَةً، وَلَمْ يَقْضُوا} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ 

وَمِثْلُهُ عِنْدَ ابْنِ خُزَيْمَةَ: عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ 

Kutoka kwa Khudhayfah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali Swalaatul-Khawf (Swalaah ya Khofu) kwa kuswalisha hawa Rakaa moja na hawa (kundi jingine) Rakaa moja, na hawakukidhi (kulipa).” [Imetolewa na Ahmad, Abu Daawuwd na An-Nasaaiy, na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

Mfano wa Hadiyth hiyo ameipokea Ibn Khuzaymah kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا)

 

 

 

383.

وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { صَلَاةُ اَلْخَوْفِ رَكْعَةٌ عَلَى أَيِّ وَجْهٍ كَانَ}  رَوَاهُ اَلْبَزَّارُ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swalaatul-Khawf (Swalaah  ya Khofu) ni Rakaa moja, kwa njia yoyote iwayo.” [Imetolewa na Al-Bazzaar kwa Isnaad dhaifu[9]]

 

 

 

384.

وَعَنْهُ مَرْفُوعًا: {لَيْسَ فِي صَلَاةِ اَلْخَوْفِ سَهْوٌ} أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) tena katika Hadiyth Marfuw’ amesema: “Katika Swalaatul-Khawf (Swalaah ya Khofu) hakuna (Sijdah ya) kusahau.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniyy kwa Isnaad dhaifu]

 

[1] Swaalih bin Khawwaat ndiye Swaalih bin Khawwaat bin Jaabir bin An-Nu’maan Al-Answaariyy Al-Madaniy. Alikuwa ni mmoja wa Maswahaba maarufu, na Ahaadiyth zake zina usahihi wa hali ya juu.

[2] Dhaati Ar-Riqaa’ inaweza kutafsiriwa kuwa ni “iliyo na misitari au milia”. Waislamu walikuwa wana ufukara wa hali ya juu sana, na walikuwa wanatembea pekupeku, bila kuvaa viatu. Miguu yao ikipata malengelenge, walikuwa wakiifungiliza kwa marapurapu ya nguo chakavu. Kwa hivyo vita hivi vikaja kujulikana kama ni vita vya Dhaati Ar-Riqaa’.

[3] Hadiyth hii inaeleza kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalisha Swalaah moja yenye Rakaa mbili, na Hadiyth ya pili inasema aliswalisha Swalaah mbili za Rakaa mbili kila moja kwa makundi mawili tofauti. Kwa kuwa kuswalisha Swalaah mbili kumetajwa, hakuna tofauti ya maoni juu yake. Uhakika wa mambo ni kwamba, katika Swalaatul-Khawf  (Swalaah ya Khofu) kama mbinu za vita zimezingatiwa. Imethibitishwa kwamba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akitumia aina mbalimbali za kuswali wakati wa vita. Ibn Hazam alirejea au alizitaja namna kumi na nne mbalimbali za kuswali, kulingana na mahitaji au mazingira ya wakati ule. Wakati mwingine Swalaah ilikuwa ndefu, na wakati mwingine inakuwa fupi. Mara nyingine mtindo mmoja, na mara nyingine mtindo mwingine. Jina la Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) huyo lilitajwa kuwa ni Sahl bin Abuu Hathmah.

[4] Najd ni jina la sehemu ya Rasi ya Arabuni ambako kuna nyanda za juu za milima.

[5] Kutokana na Hadiyth hii, inaelekea kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswalisha Rakaa moja kwa kila moja ya makundi mawili tofauti, wakati kila kundi liliswali Rakaa nyingine moja peke yake. Inaelekea kuwa hali hii inaafikiana na Aayah za Qur-aan [An-Nisaa (4: 102-103)]

[6] Sehemu iliyobaki ya Hadiyth inaeleza: “...safu ya nyuma ikaenda chini kusujudu kisha wakasimama. Halafu safu ya nyuma ikaenda mbele na safu ya mbele ikarudi nyuma. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akarukuu nasi sote tukarukuu, akanyanyua kichwa chake baada ya kurukuu na sisi sote tukanyanyua vichwa vyetu. Kisha yeye na safu ya karibu yake lakini ilikuwa nyuma katika Rakaa ya kwanza wakasujudu, wakati safu ya nyuma imesimama mkabala na adui. Kisha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na safu iliyokuwa karibu naye walipomaliza kusujudu, safu ya nyuma nao wakaenda chini kusujudu. Kisha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akatoa Salaam, nasi sote tukafanya hivyo.” Mwisho wa Hadiyth.

[7] Abuu ‘Ayyaash ndiye Zayd bin Thaabit, ambaye ni Answaariyy na Zuraqiyy. Kundi la Waislamu limeripoti Hadiyth kutoka kwake na alikufa baada ya mwaka 40 A.H.

[8] ‘Usfaan ni pahala ambapo pako Nanzil (takribani sawa na safari ya siku mbili) kutoka Makkah.

[9] Hadiyth hii imewafanya wengine waamue kwamba ipo Rakaa moja tu kwa wote Maamuma na Imaam pia. Kwa hivyo Sufyaan anafuata vivyo hivyo.

 

 

Share

14-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Swalaatul-'Iydayni (Swalaah Za ‘Iyd Mbili)

بُلُوغُ الْمَرام

 

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

 

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ صَلَاةِ اَلْعِيدَيْنِ

14-Mlango Wa Swalaatul-‘Iydayni (Swalaah Za ‘IydMbili)[1]

 

 

 

385.

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { الْفِطْرُ يَوْمَ يُفْطِرُ اَلنَّاسُ، وَالْأَضْحَى يَوْمَ يُضَحِّي اَلنَّاسُ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Al-Fitwr ni siku ambapo watu wanakula. Na Al-Adhwhaa ni siku ambapo watu wanachinja.”[2] [Imetolewa na At-Tirmidhiy]

 

 

 

386.

وَعَنْ أَبِي عُمَيْرِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ عُمُومَةٍ لَهُ مِنَ اَلصَّحَابَةِ، {أَنَّ رَكْبًا جَاءُوا، فَشَهِدُوا أَنَّهُمْ رَأَوُا الْهِلَالَ بِالْأَمْسِ، فَأَمَرَهُمْ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  أَنْ يُفْطِرُوا، وَإِذَا أَصْبَحُوا يَغْدُوا إِلَى مُصَلَّاهُمْ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ وَهَذَا لَفْظُهُ وَإِسْنَادُهُ صَحِيحٌ 

Kutoka kwa Abuu ‘Umayr bin Anas[3] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kwa upokezi wa maami zake miongoni mwa Maswahaba: “Msafara ulikuja wakashuhudia kuwa wao wameona mwezi mwandamo jana. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaamrisha kula (waache Swawm) na asubuhi waende mahali pa kuswalia.”[4] [Imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd, na tamshi hili ni la Abuu Daawuwd, na Isnaad zake ni Swahiyh]

 

 

 

387.

وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ:{كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  لَا يَغْدُو يَوْمَ اَلْفِطْرِ حَتَّى يَأْكُلَ تَمَرَاتٍ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ

وَفِي رِوَايَةٍ مُعَلَّقَةٍ وَوَصَلَهَا أَحْمَدُ: وَيَأْكُلُهُنَّ أَفْرَادًا 

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa hatoki siku ya ‘Iyd Al-Fitwr isipokuwa mpaka ale tende.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

Na katika mapokezi mengine ni Mu’allaq lakini imeunganishwa na Ahmad: “...Na alikuwa akila moja moja Witr.”

 

 

 

388.

وَعَنِ ابْنِ بُرَيْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ:{كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  لَا يَخْرُجُ يَوْمَ اَلْفِطْرِ حَتَّى يَطْعَمَ، وَلَا يَطْعَمُ يَوْمَ اَلْأَضْحَى حَتَّى يُصَلِّيَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ 

Kutoka kwa Ibn Buraydah amesema kutoka kwa baba yake kuwa amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa hatoki siku ya ‘Iyd isipokuwa mpaka ale, wala hali kitu siku ya ‘Iyd ya kuchinja[5] mpaka aswali.” [Imetolewa na Ahmad na At-Tirmidhiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

389.

وَعَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ قَالَتْ:{أُمِرْنَا أَنْ نُخْرِجَ اَلْعَوَاتِقَ، وَالْحُيَّضَ فِي الْعِيدَيْنِ; يَشْهَدْنَ الْخَيْرَ وَدَعْوَةَ اَلْمُسْلِمِينَ، وَيَعْتَزِلُ اَلْحُيَّضُ اَلْمُصَلَّى} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Ummu ‘Atwiyyah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Tumeamrishwa[6] siku za ‘Iyd mbili (‘Iydul Fitwr na ‘Iydul Adhwhaa) tuwatoe wasichana na wenye hedhi ili wahudhuriye kheri na du’aa ya Waislamu, isipokuwa wanawake wenye hedhi waepuke mahala pa kuswalia.”[7] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

390.

وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ:{كَانَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  وَأَبُو بَكْرٍ، وَعُمَرُ: يُصَلُّونَ الْعِيدَيْنِ قَبْلَ اَلْخُطْبَةِ}  مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Abuu Bakr na ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) walikuwa wakiswali ‘Iyd kabla ya Khutbah.”[8] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

391.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  صَلَّى يَوْمَ اَلْعِيدِ رَكْعَتَيْنِ، لَمْ يُصَلِّ قَبْلَهَا وَلَا بَعْدَهَا}  أَخْرَجَهُ اَلسَّبْعَةُ 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali Rakaa mbili[9] siku ya ‘Iyd na hakuswali kabla wala baada yake.”[10] [Imetolewa na As-Sab’ah (Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad)]

 

 

 

392.

وَعَنْهُ: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  صَلَّى اَلْعِيدَ بِلَا أَذَانٍ، وَلَا إِقَامَةٍ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ  . وَأَصْلُهُ فِي اَلْبُخَارِيِّ 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema tena: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali ‘Iyd bila Adhana wala Iqaamah.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na chanzo chake ni katika Al-Bukhaariy]

 

 

 

393.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  لَا يُصَلِّي قَبْلَ اَلْعِيدِ شَيْئًا، فَإِذَا رَجَعَ إِلَى مَنْزِلِهِ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ}  رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَهْ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ 

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuswali kamwe Swalaah yoyote kabla ya Swalaah ya ‘Iyd, lakini aliporejea nyumbani alikuwa anaswali Rakaa mbili.” [Imetolewa na Ibn Maajah kupitia mlolongo mzuri wa wapokezi]

 

 

 

394.

وَعَنْهُ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يَخْرُجُ يَوْمَ اَلْفِطْرِ وَالْأَضْحَى إِلَى اَلْمُصَلَّى، وَأَوَّلُ شَيْءٍ يَبْدَأُ بِهِ اَلصَّلَاةُ، ثُمَّ يَنْصَرِفُ فَيَقُومُ مُقَابِلَ اَلنَّاسِ وَالنَّاسُ عَلَى صُفُوفِهِمْ فَيَعِظُهُمْ وَيَأْمُرُهُمْ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anatokea siku ya Fitwr na siku ya Al-Adhwhaa, mpaka mahala pa kuswalia, na jambo la mwanzo alilofanya ni kuswali. Alipomaliza, alisimama wima kuwakabili watu walioketi chini katika safu zao. Kisha aliwakhutubia na kuwaamrisha.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

395.

وَعَنْ عَمْرِوِ بْنِ شُعَيْبٍ عَنْ أَبِيهِ عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قَالَ نَبِيُّ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلتَّكْبِيرُ فِي اَلْفِطْرِ سَبْعٌ فِي اَلْأُولَى وَخَمْسٌ فِي اَلْآخِرَةِ، وَالْقِرَاءَةُ بَعْدَهُمَا كِلْتَيْهِمَا} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ  وَنَقَلَ اَلتِّرْمِذِيُّ عَنِ اَلْبُخَارِيِّ تَصْحِيحَهُ 

Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb amesema kutoka kwa baba yake, naye kutoka kwa babu yake, amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Takbiyr katika Swalaah ya ‘Iydul Fitwr ni saba katika Rakaa ya kwanza[11], na tano katika Rakaa ya pili. Na kisomo (cha Qur-aan) katika zote mbili ni baada yake (Takbiyra).” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, na At-Tirmidhiy aliisahihisha kutoka kwa Al-Bukhaariy]

 

 

 

396.

وَعَنْ أَبِي وَاقِدٍ اللَّيْثِيِّ قَالَ: {كَانَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  يَقْرَأُ فِي اَلْأَضْحَى وَالْفِطْرِ بِـ (ق)، وَ (اقْتَرَبَتْ) } أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ 

Kutoka kwa Abuu Waaqid Al-Laythiyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anasoma katika ‘Iydul Adhwhaa na ‘Iyd Al-Fitwr

ق[12]

na,

اقْتَرَبَتِ[13]

  [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

397.

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  إِذَا كَانَ يَوْمُ اَلْعِيدِ خَالَفَ اَلطَّرِيقَ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ

وَلِأَبِي دَاوُدَ: عَنِ ابْنِ عُمَرَ، نَحْوُهُ 

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Ilipofika siku ya ‘Iyd, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akibadilisha njia[14]”. [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

Naye Abuu Daawuwd amepokea Hadiyth kama hiyo kutoka kwa ‘Umar.

 

 

 

398.

وَعَنْ أَنَسٍ قَالَ: {قَدِمَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  اَلْمَدِينَةَ، وَلَهُمْ يَوْمَانِ يَلْعَبُونَ فِيهِمَا. فَقَالَ: "قَدْ أَبْدَلَكُمُ اَللَّهُ بِهِمَا خَيْرًا مِنْهُمَا: يَوْمَ اَلْأَضْحَى، وَيَوْمَ اَلْفِطْرِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ 

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuja Al-Madiynah, watu wakiwa na siku mbili wacheza michezo ndani yake (kusherehekea). Akasema: “Allaah Amewabadilishieni kilicho bora zaidi, siku ya Al-Adhwhaa (kuchinja) na siku ya Al-Fitwr (kufungua Swawm).” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy kwa Isnaad Swahiyh]

 

 

 

399.

وَعَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {مِنَ اَلسُّنَّةِ أَنْ يَخْرُجَ إِلَى اَلْعِيدِ مَاشِيًا} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَحَسَّنَهُ

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Ni miongoni mwa Sunnah kwenda kwa kuswali ‘Iyd kwa miguu.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaopa daraja la Hasan]

 

 

 

400.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ{  أَنَّهُمْ أَصَابَهُمْ مَطَرٌ فِي يَوْمِ عِيدٍ. فَصَلَّى بِهِمْ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  صَلَاةَ اَلْعِيدِ فِي اَلْمَسْجِدِ}  رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادٍ لَيِّنٍ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Mvua ilinyesha siku ya ‘Iyd, kwa hivyo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akawaswalisha watu ‘Iyd ndani ya Msikiti.”[15] [Imetolewa na Abuu Daawuwd kwa Isnaad layyin (dhaifu)]

 

[1] Swalaah za Iyd mbili ni Sunnah Muakkadah (Sunnah iliyosisitizwa). Wanazuoni wengine huzitekeleza hizo kama Fardwh Kifaayah (Faradhi ya kutoshelezana). Na wengine wanasema hizo ni Fardhw ‘Ayn (wajibu wa binafsi ambayo ni sharti utekelezwe na kila mtu). Rai ya  mwanzo ndio inaonekana ni ya nguvu.

 

[2] Hadiyth hii inadhihirisha kuwa, ili kuiadhimisha ‘Iydul-Fitwr na ‘Iydul-Adhwhaa kwa Swalaah inahitajika kuswaliwa na ummati wa watu kwa amri ya kiongozi Muislamu. Kama mtu anauona mwezi mchanga wa Shawwaal na watu hawamuamini, basi mtu huyo hawezi kuacha Swawm wala kuswali ‘Iyd hiyo pekee. Anaweza kufanya hivyo pale tu ambapo Waislamu wengine wameshiriki.

 

[3] Jina la Abuu ‘Umayr ni ‘Abdullaah bin Anas bin Maalik Al-Answaariyy, naye alikuwa ndiye mtoto mkubwa kuliko wote. Alikuwa wa kutegemewa wa daraja la nne, na alikuwa mmoja wa Taabi’iyn. Aliishi muda mrefu baada ya babake.

 

[4] Hii inathibitisha kuwa ikiwa mwezi haujaonekana mnamo tarehe 29 ya mwezi wa Ramadhwaan, lakini siku inayofuata taarifa za kuthibitisha kuona mwezi zikifika, Swawm sharti isitishwe pale pale. Iwapo uthibitisho huo utafika kabla ya wakati wa Zawaal (Jua linapogeuka), Swalaah ya ‘Iyd ni sharti iswaliwe siku ile ile. Lakini ikiwa uthibitisho umefika baada ya wakati wa Zawaal basi ‘Iyd sharti iswaliwe asubuhi siku inayofuata.

 

[5] Hadiyth hii inatufunza kuwa ni Sunnah watu kula kitu fulani kabla ya kuswali ‘Iydul-Fitwr na kula baada ya ‘Iydul-Adhwhaa. Hakijapendekezwa chakula chochote maalumu, lakini kwa kuzingatia mwenendo wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), bora kula tende.

 

[6] Hadiyth hii inatufunza kuwa ni ubora wanawake waende kwenye Muswalla wa ‘Iyd na wakaswali kule pamoja na wanaume. Upendeleo huo wanapewa wanawake ili nao pia washiriki katika du’aa pamoja na Baraka za siku kuu hiyo.

 

[7] Watu wengine wanaifasiri Hadiyth hii kwamba upendeleo huu ulikuwa kwa siku zile za mwanzo mwanzo tu ili uwingi wa Ummah wa Waislam uonekane mkubwa sana, lakini wanadai kuwa, rukhsa ile kwa wanawake kuja nje ilifutwa baadaye. Lakini kuijibu hoja yao uzuri, yatosheleza kunukuu Hadiyth iliyosimuliwa na ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) ambayo inasema, hata baada ya kuiteka Makkah yeye aliwaona wanawake wakienda katika Muswalla wa ‘Iyd.

 

[8] Kwa mujibu wa Sunnah, Khutbah hutolewa baada ya kuswali, na hakuna kutofautiana maoni juu ya hili. Katika enzi za Baniy Umayyah, Marwaan alileta uzushi kwamba Khutbah itolewe kabla ya kuswali, lakini desturi hiyo haina nafasi katika Uislam.

 

[9] Iwapo mtu atashindwa kuunga nyuma ya Imaam katika Swalaah ya ‘Iyd, akaswali pekee, basi Imaam Ahmad na Ath-Thawriy wana rai kwamba aswali Rakaa nne. Wanazuoni wengine wanaona kwamba aswali Rakkaa mbili. Ama Imaam Abuu Haniyfah ana rai kwamba mtu anaweza kuchagua kati ya kuswali Swalaah ya ‘Iyd iliyompita kama ni Rakaa mbili au nne [Rejea Fathul-‘Allaam (2/521)] 

 

 

[10] Kusiswaliwe Naafil (Swalaah ya Sunnah, ya khiari) kabla wala baada ya Swalaah ya ‘Iyd katika mahala pa kuswalia ‘Iyd. Lakini mtu anaweza kuswali Sunnah nyumbani.

 

[11] Kuna tofauti ya maoni miongoni mwa Wanazuoni juu ya ripoti kumi kuhusu hizi Takbiyra zaidi mbili. Mchakato sahihi ni huo uliosimuliwa katika Hadiyth hii. Watu wengine wanaegemea katika Hadiyth iliyosimuliwa na Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa baki ya Takbiyratul-Iftitaah (ya kufungulia Swalaah),  na Takbiyratur-Rukuwu’ (ya kurukuu) zipo Takbiyra nyenginezo sita; tatu za kutamka ndani ya Rakaa ya kwanza kabla ya kisomo, na tatu zingine za kutamka ndani ya Rakaa ya pili baada ya kisomo. Kwa usahihi, Hadiyth iliyosimuliwa na Ibn Mas-‘uwd si ya kutegemewa.

 

[12] Qaaf (50)

 

[13] Al-Qamar: (54)

 

[14] Yaani kama alipokua akienda kuswali ‘Iyd alifuata njia hii, basi aliporudi kutoka huko alirudi kwa njia nyingine, kwa sababu mahala mbalimbali hizo zitashuhudia  upitaji njia kuenda kuswali, na hadhi ya Uislam itakuwa juu.

 

[15] Hadiyth hii inathibitisha kuwa itokeapo ugumu kuswalia Muswalla wa ‘Iyd (Pahala pa kuswalia ‘Iyd), ni rukhsa kuswali ‘Iyd ndani ya Msikiti.

 

 

Share

15-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Swalaatul-Kusuwf (Swalaah Ya Kupatwa Jua Au Mwezi)

 بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ صَلَاةِ اَلْكُسُوفِ

15-Mlango Wa Swalaatul-Kusuwf [1] (Swalaah Ya Kupatwa Jua Au Mwezi)

 

 

 

401.

 عَنِ اَلْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  قَالَ: {اِنْكَسَفَتِ اَلشَّمْسُ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   يَوْمَ مَاتَ إِبْرَاهِيمُ، فَقَالَ اَلنَّاسُ: اِنْكَسَفَتِ اَلشَّمْسُ لِمَوْتِ إِبْرَاهِيمَ، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   "إِنَّ اَلشَّمْسَ وَالْقَمَرَ آيَتَانِ مِنْ آيَاتِ اَللَّهِ لَا يَنْكَسِفَانِ لِمَوْتِ أَحَدٍ وَلَا لِحَيَاتِهِ، فَإِذَا رَأَيْتُمُوهُمَا، فَادْعُوا اَللَّهَ وَصَلُّوا، حَتَّى تَنْكَشِفَ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

وَفِي رِوَايَةٍ لِلْبُخَارِيِّ: «حَتَّى تَنْجَلِيَ»

وَلِلْبُخَارِيِّ مِنْ حَدِيثِ أَبِي بَكْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  {فَصَلُّوا وَادْعُوا حَتَّى يُكْشَفَ مَا بِكُمْ}

Kutoka kwa Al-Mughiyrah bin Shu’bah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Jua lilipatwa wakati wa uhai wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), siku alipofariki (mwanae) Ibraahiym,[2] watu wakasema: Jua limepatwa kwa sababu ya kifo cha Ibraahiym. Akasema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): Jua na mwezi ni Aayaat (ishara) mbili kati ya Aayaat za Allaah. Havipatwi kwa sababu ya kufa yeyote wala kwa uhai wake.[3] Kwa hivyo munapoona kupatwa kwake, muombeni Allaah na mswali hadi kupatwa huko kuondoke.”[4] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Na katika Riwaayah ya Al-Bukhaariy: “Mpaka pawe paangavu.”

 

 

Na katika upokezi wa Al-Bukhaariy kutoka kwa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Swalini na ombeni hadi kuondoke kilichokufikeni.”

 

 

 

402.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم  جَهَرَ فِي صَلَاةِ اَلْكُسُوفِ  بِقِرَاءَتِهِ، فَصَلَّى أَرْبَعَ رَكَعَاتٍ فِي رَكْعَتَيْنِ، وَأَرْبَعَ سَجَدَاتٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَهَذَا لَفْظُ مُسْلِمٍ 

وَفِي رِوَايَةٍ لَهُ: {فَبَعَثَ مُنَادِيًا يُنَادِي: اَلصَّلَاةُ جَامِعَةٌ}

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisoma kwa sauti[5] kisomo chake cha Swalaatul-Kusuwf (Swalaah ya kupatwa jua au mwezi), akaswali Rakaa mbili ambamo alirukuu mara nne[6] na alisujudu mara nne.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

Na katika mapokezi mengine: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akatuma mtu akaenda kutangaza: “Njooni kwenye Swalaah ya Jamaa.”[7]

 

 

 

403.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {اِنْخَسَفَتِ الشَّمْسُ عَلَى عَهْدِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم   فَصَلَّى، فَقَامَ قِيَامًا طَوِيلًا، نَحْوًا مِنْ قِرَاءَةِ سُورَةِ اَلْبَقَرَةِ، ثُمَّ رَكَعَ رُكُوعًا طَوِيلًا، ثُمَّ رَفَعَ فَقَامَ قِيَامًا طَوِيلًا وَهُوَ دُونَ اَلْقِيَامِ اَلْأَوَّلِ، ثُمَّ رَكَعَ رُكُوعًا طَوِيلًا، وَهُوَ دُونَ اَلرُّكُوعِ اَلْأَوَّلِ، ثُمَّ سَجَدَ، ثُمَّ قَامَ قِيَامًا طَوِيلاً، وَهُوَ دُونَ اَلْقِيَامِ اَلْأَوَّلِ، ثُمَّ رَكَعَ رُكُوعًا طَوِيلًا، وَهُوَ دُونَ اَلرُّكُوعِ اَلْأَوَّلِ، ثُمَّ رَفَعَ، فَقَامَ قِيَامًا طَوِيلًا، وَهُوَ دُونَ اَلْقِيَامِ اَلْأَوَّلِ، ثُمَّ رَكَعَ رُكُوعًا طَوِيلاً، وَهُوَ دُونَ اَلرُّكُوعِ اَلْأَوَّلِ، ثُمَّ سَجَدَ، ثُمَّ انْصَرَفَ وَقَدْ تَجَلَّتِ اَلشَّمْسُ. فَخَطَبَ اَلنَّاسَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ 

وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ: {صَلَّى حِينَ كَسَفَتِ اَلشَّمْسُ ثَمَانَ رَكَعَاتٍ فِي أَرْبَعِ سَجَدَاتٍ}

وَعَنْ عَلِيٍّ مِثْلُ ذَلِكَ 

وَلَهُ: عَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ {صَلَّى سِتَّ رَكَعَاتٍ بِأَرْبَعِ سَجَدَاتٍ}  

وَلِأَبِي دَاوُدَ: عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ: {صَلَّى، فَرَكَعَ خَمْسَ رَكَعَاتٍ وَسَجَدَ سَجْدَتَيْنِ، وَفَعَلَ فِي اَلثَّانِيَةِ مِثْلَ ذَلِكَ} 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Jua lilipatwa wakati wa uhai wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), akaswali na akasimama kisomo kirefu, kadiri ya kuweza kusoma Suwratul-Baqarah, kisha akarukuu Rukuu ndefu, akainua kichwa na kusimama kisimamo kirefu, chini ya kisimamo cha kwanza, kisha akarukuu Rukuu ndefu chini ya Rukuu ya kwanza, akasujudu na akasimama kisimamo kirefu chini ya kisimamo cha kwanza, kisha akarukuu Rukuu ndefu chini ya Rukuu ya kwanza, kisha akainua kichwa, kisha akasujudu, kisha akaondoka, na jua lilishafunguka. Akatoa Khutbah.”[8] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

Na katika Riwaayah ya Muslim: “Jua lilipopatwa, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliswali Rakaa nane katika Sijdah nne.” Na ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alisimulia Hadiyth nyingine kama hiyo.

Yeye (Muslim) tena amemnukuu Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa: “(Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)) aliswali kwa Rakaa sita na Sijdah nne.”

 

 

Na Abuu Daawuwd amepokea masimulizi ya Ubayy bin Ka’b (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa: “(Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)) aliswali na akarukuu mara tano na akasujudu mara mbili, na katika Rakaa ya pili alifanya hivyo hivyo.”

 

 

 

404.

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {مَا هَبَّتْ رِيحٌ قَطُّ إِلَّا جَثَا اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم   عَلَى رُكْبَتَيْهِ، وَقَالَ: "اَللَّهُمَّ اجْعَلْهَا رَحْمَةً، وَلَا تَجْعَلَهَا عَذَابًا"} رَوَاهُ اَلشَّافِعِيُّ وَالطَّبَرَانِيُّ 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Upepo haukuvuma kamwe, isipokuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipiga magoti na kusema: Ee Allaah! Ujaalie uwe Rahmah wala Usiujaalie uwe adhabu.” [Imetolewa na Ash-Shaafi’iyy na Atw-Twabaraaniyy]

 

 

 

405.

وَعَنْهُ: أَنَّهُ صَلَّى فِي زَلْزَلَةٍ سِتَّ رَكَعَاتٍ، وَأَرْبَعَ سَجَدَاتٍ، وَقَالَ: هَكَذَا صَلَاةُ اَلْآيَاتِ  رَوَاهُ اَلْبَيْهَقِيُّ 

وَذَكَرَ اَلشَّافِعِيُّ عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  مِثْلَهُ دُونَ آخِرِهِ 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema tena: “(Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)) aliswali pindi ilipotokea tetemeko la ardhi Rakaa sita na Sijdah nne, na akasema: Hivi ndivyo namna ya kuswali Swalaatul-Aayaat (Swalaah ya ishara  (ya Maafa).”[9] [Imetolewa na Al-Bayhaqiyy]

 

Na Ash-Shaafi’iyy ametaja Hadiyth ya ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kama hiyo pasi na kutaja mwisho wake.

 


[1] Maana ya neno hilo ‘Kusuwf’ na ‘Khusuwf’ (kushikwa kwa jua na kushikwa kwa mwezi) ni “kubadilika”. Maneno haya yaweza kuwa kinyume cha hivi.

 

[2] Mama yake Ibraahiym alikuwa Maria, Mmisri aliyewahi kuwa mtumwa ambaye Al-Muqawqis mtwawala wa Alexandria na Misri alimpa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kama zawadi amuoe. Ibraahiym alizaliwa mnamo mwezi wa Jumaadal-Uwlaa mwaka wa 9A.H., na akafariki mnamo tarehe 29 Shawwaal mwaka 11 A.H. akiwa na umri wa miezi kumi na nane. Alizikwa Al-Baqi’, na yeye (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema kuwa: “Anaye wa kumkamilishia kunyonya kwake huko Jannah.”

 

[3] Siku za Jaahiliyya (kipindi kabla ya ujio wa Uislamu), watu walikuwa wakiamini kuwa kila mtu mashuhuri anapozaliwa au anapokufa, jua au mwezi hupatwa. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikanusha itikadi hii.

 

[4] Al-Bukhaariy na Muslim.

 

[5] Hoja ya kama Swalaatul-Kusuwf (Swalaah ya kupatwa kwa jua au mwezi) bora iswaliwe kwa sauti kubwa au sauti ndogo, nayo imetofautiana. Lakini kuswali kwa sauti kubwa ndiko kumethibitishwa kwa Hadiyth Marfuw’.

 

[6] Kinyume na Swalaah zingine, Swalaah hii ina kurukuu mara mbili kila Rakaa.

 

[7] Kwa mujibu wa Hadiyth Swahiyh kutangaza au kuita watu kwa ajili ya Swalaah yoyote hairuhusiwi isipokuwa Swalaatul-Kusuwf (Swalaah ya kupatwa kwa jua au mwezi).

 

[8] Inaeleweka kutokana na Hadiyth kuwa Khutbah hutolewa pia katika Swalaatul-Kusuwf (Swalaah ya kupatwa jua au mwezi).

 

[9] Hadiyth hii inatufunza kuwa, kukizuka balaa, liwe ni janga la ardhini kama tetemeko la ardhi, au kuporomoka kwa milima ya theluji na barafu, n.k; au maangamizi ya kutoka angani tufani, kimbunga cha mchanga, au kimbunga cha theluji, vinavyoathiri viumbe kwa maumivu na huzuni, watu sharti wajitume wenyewe kuswali Swalaah hii inayoitwa Swalaatul-Aayaat (Swalaah ya ishara za Allaah (عزّ وجلّ).

 

Share

16-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Swalaatul-Istisqaa (Swalaah Ya Mvua)

 

بُلُوغُ الْمَرام

 

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

 

Kitabu Cha Swalaah

 

 

بَابُ صَلَاةِ اَلِاسْتِسْقَاءِ

16-Mlango Wa Swalaatul-Istisqaa[1] (Swalaah Ya Mvua)

 

 

 

 

 

406.

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {خَرَجَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  مُتَوَاضِعًا، مُتَبَذِّلًا، مُتَخَشِّعًا، مُتَرَسِّلًا، مُتَضَرِّعًا، فَصَلَّى رَكْعَتَيْنِ، كَمَا يُصَلِّي فِي اَلْعِيدِ، لَمْ يَخْطُبْ خُطْبَتَكُمْ هَذِهِ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَأَبُو عَوَانَةَ، وَابْنُ حِبَّانَ 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alitoka (kwenda kuswali Swalaah ya kuomba mvua) huku akiwa mnyonge, amevaa nguo duni na katika hali ya udhalili na mnyenyekevu, anaomba du’aa. Akaswali Rakaa mbili kama za Swalaah ya ‘Iyd,[2] lakini hakukhutubu kama khutbah yenu hii.”[3] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na wakaisahihisha At-Tirmidhiy, Abuu ‘Awaanah na Ibn Hibbaan]

 

 

 

407.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {شَكَا اَلنَّاسُ إِلَى رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  قُحُوطَ الْمَطَرِ، فَأَمَرَ بِمِنْبَرٍ، فَوُضِعَ لَهُ فِي اَلْمُصَلَّى، وَوَعَدَ اَلنَّاسَ يَوْمًا يَخْرُجُونَ فِيهِ، فَخَرَجَ حِينَ بَدَا حَاجِبُ اَلشَّمْسِ، فَقَعَدَ عَلَى اَلْمِنْبَرِ، فَكَبَّرَ وَحَمِدَ اَللَّهَ، ثُمَّ قَالَ: "إِنَّكُمْ شَكَوْتُمْ جَدَبَ دِيَارِكُمْ، وَقَدْ أَمَرَكُمْ اَللَّهُ أَنْ تَدْعُوَهُ، وَوَعَدَكُمْ أَنْ يَسْتَجِيبَ لَكُمْ، ثُمَّ قَالَ: اَلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ اَلْعَالَمِينَ، اَلرَّحْمَنِ اَلرَّحِيمِ، مَالِكِ يَوْمِ اَلدِّينِ، لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ، اَللَّهُمَّ أَنْتَ اَللَّهُ، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، أَنْتَ اَلْغَنِيُّ وَنَحْنُ اَلْفُقَرَاءُ، أَنْزِلْ عَلَيْنَا الْغَيْثَ، وَاجْعَلْ مَا أَنْزَلْتَ قُوَّةً وَبَلَاغًا إِلَى حِينٍ" ثُمَّ رَفَعَ يَدَيْهِ، فَلَمْ يَزَلْ حَتَّى رُئِيَ بَيَاضُ إِبِطَيْهِ، ثُمَّ حَوَّلَ إِلَى اَلنَّاسِ ظَهْرَهُ، وَقَلَبَ رِدَاءَهُ، وَهُوَ رَافِعٌ يَدَيْهِ، ثُمَّ أَقْبِلَ عَلَى اَلنَّاسِ وَنَزَلَ، وَصَلَّى رَكْعَتَيْنِ، فَأَنْشَأَ اَللَّهُ سَحَابَةً، فَرَعَدَتْ، وَبَرَقَتْ، ثُمَّ أَمْطَرَتْ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَقَالَ: "غَرِيبٌ، وَإِسْنَادُهُ جَيِّدٌ"

وَقِصَّةُ اَلتَّحْوِيلِ فِي "اَلصَّحِيحِ" مِنْ: حَدِيثِ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ زَيْدٍ، وَفِيهِ: {فَتَوَجَّهَ إِلَى اَلْقِبْلَةِ، يَدْعُو، ثُمَّ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ، جَهَرَ فِيهِمَا بِالْقِرَاءَةِ}

وَلِلدَّارَقُطْنِيِّ مِنْ مُرْسَلِ أَبِي جَعْفَرٍ اَلْبَاقِرِ: وَحَوَّلَ رِدَاءَهُ؛ لِيَتَحَوَّلَ اَلْقَحْطُ 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Watu walimlalamikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) uhaba wa mvua. Kwa hivyo akaamrisha ijengwe Mimbar, akawekewa hapo Al-Muswallaa, na akaagana na watu siku watakayotoka watu kuja hapo. Akatoka jua lilipoanza kudhihiri. Akakaa juu ya Mimbar, akapiga Takbiyra na akamhimidi Allaah, akasema: Hakika nyinyi mmelalamikia ukame wa maskani zenu, Allaah Amekuamrisheni mumuombe Yeye na Amekuahidini kuwa Atakujibuni. Kisha akasema:  “AlhamduliLLaah, Rabb wa ulimwengu, Ar-Rahmaan,  Mwenye kurehemu, Mfalme wa siku ya malipo, hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hufanya Alitakalo. Ee Allaah! Wewe ni Allaah hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, Wewe ni Mkwasi, nasi ni mafukara. Tuteremshie mvua na Ukifanye Utakachotuteremshia kiwe nguvu na chenye kutufikisha mpaka muda (wa mwisho).” Akanyanyua mikono,[4] na akawa anazidi kuinyanyua hadi weupe wa kwapa zake unaonekana. Kisha akawapa mgongo watu, na akageuza ridaa (juba) yake ya juu huku mikono yake kainyanyua juu. Akawageukia watu, akashuka akawaswalisha Rakaa mbili. Kisha Allaah Akaanzisha wingu, radi na umeme, kisha ikanyesha mvua.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, ambaye aliipa daraja la Ghaarib, na Isnaad yake ni nzuri]

Kisa cha kugeuza nguo kimetajwa katika Swahiyh Al-Bukhaariy kutokana na usimulizi wa ‘Abdullaah bin Zayd, na kinasema: “(Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)) alielekea Qiblah huku akiomba du’aa, akaswalisha Rakaa mbili na akasoma kwa sauti.”

 

Na Ad-Daaraqutwniyy alisimulia vivyo hivyo katika Hadiyth Mursal iliyosimuliwa na Abuu Ja’far Al-Baaqir[5]: “(Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)) aligeuza ridaa (juba) yake ili ukame ugeuke.”

 

 

 

408.

 وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  {أَنَّ رَجُلًا دَخَلَ اَلْمَسْجِدَ يَوْمَ اَلْجُمُعَةِ، وَالنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم   قَائِمٌ يَخْطُبُ. فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ، هَلَكَتِ اَلْأَمْوَالُ، وَانْقَطَعَتِ اَلسُّبُلُ، فَادْعُ اَللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يُغِيثُنَا، فَرَفَعَ يَدَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: "اَللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اَللَّهُمَّ أَغِثْنَا..." فَذَكَرَ اَلْحَدِيثَ، وَفِيهِ اَلدُّعَاءُ بِإِمْسَاكِهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mtu aliingia Msikitini katika siku ya Ijumaa huku Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiwa amesimama akikhutubia. Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Mali imeangamia na njia zimekatika, basi muombe Allaah (عزّ وجلّ)  Atuletee mvua. (Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)) akainua mikono yake, akasema: Ee Allaah! (Tuteremshie mvua), Ee Allaah! Tuteremshie mvua.” Msimulizi akataja Hadiyth yote, ndani yake kuna du’aa za kuzuia mvua.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

409.

وَعَنْ أَنَسٍ; {أَنَّ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  كَانَ إِذَا قَحِطُوا يَسْتَسْقِي بِالْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ اَلْمُطَّلِبِ. وَقَالَ: اَللَّهُمَّ إِنَّا كُنَّا نَسْتَسْقِي إِلَيْكَ بِنَبِيِّنَا فَتَسْقِينَا، وَإِنَّا نَتَوَسَّلُ إِلَيْكَ بِعَمِّ نَبِيِّنَا فَاسْقِنَا، فَيُسْقَوْنَ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) tena amesema: “Walikuwa walipofikwa na ukame, ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikuwa akiomba mvua[6] kwa Al-‘Abbaas bin ‘Abd Al-Mutwallib[7] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ), naye akasema: Ee Allaah! Tulikuwa tukikuomba kwa Nabiy wetu, na Ukatuteremshia maji. Sasa tunakuomba kwa Ammi wa Nabiy wetu. Kwa hivyo tunakuomba mvua. Wakawa wanateremshiwa mvua.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

410.

وَعَنْ أَنَسٍ قَالَ: {أَصَابَنَا وَنَحْنُ مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   مَطَرٌ قَالَ: فَحَسَرَ ثَوْبَهُ، حَتَّى أَصَابَهُ مِنَ اَلْمَطَرِ، وَقَالَ: "إِنَّهُ حَدِيثُ عَهْدٍ بِرَبِّهِ"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Tulipata mvua wakati tulipokuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), akafunua nguo yake hadi akapata mvua ikamnyeshea na akasema: Imetoka sasa hivi kutoka kwa Rabb wake.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

411.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا; أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   كَانَ إِذَا رَأَى اَلْمَطَرَ قَالَ: {اَللَّهُمَّ صَيِّبًا نَافِعًا} أَخْرَجَاهُ 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipoona mvua alikuwa akisema: Ee Allah! Tumiminie mvua yenye manufaa.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

412.

وَعَنْ سَعْدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   دَعَا فِي اَلِاسْتِسْقَاءِ: {اَللَّهُمَّ جَلِّلْنَا سَحَابًا، كَثِيفًا، قَصِيفًا، دَلُوقًا، ضَحُوكًا، تُمْطِرُنَا مِنْهُ رَذَاذًا، قِطْقِطًا، سَجْلًا، يَا ذَا اَلْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ} رَوَاهُ أَبُو عَوَانَةَ فِي "صَحِيحِهِ

Kutoka kwa Sa’d (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliomba mvua inyeshe[8]: Ee Allaah! Tufunike kwa mawingu mazito mengi, yenye ngurumo, ya kuteleza, na yenye umeme na kutokea humo Utushushie mvua ya kumwagika na ya manyunyu. Ee Mwenye Ujalali na Utukufu.” [Imetolewa na Abuu ‘Awaanah katika Swahiyh yake]

 

 

 

413.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ: {خَرَجَ سُلَيْمَانُ عَلَيْهِ اَلسَّلَامُ يَسْتَسْقِي، فَرَأَى نَمْلَةً مُسْتَلْقِيَةً عَلَى ظَهْرِهَا رَافِعَةً قَوَائِمَهَا إِلَى اَلسَّمَاءِ تَقُولُ: اَللَّهُمَّ إِنَّا خَلْقٌ مِنْ خَلْقِكَ، لَيْسَ بِنَا غِنًى عَنْ سُقْيَاكَ، فَقَالَ: ارْجِعُوا لَقَدْ سُقِيتُمْ بِدَعْوَةِ غَيْرِكُمْ} رَوَاهُ أَحْمَدُ وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Sulaymaan (عَلَيْهِ اَلسَّلَامُ) alitoka kuenda kuomba mvua, akamuona sisimizi amelala chali huku amenyanyua miguu yake mbinguni akisema:[9] “Ee Allaah! Sisi ni miongoni mwa viumbe Wako, na hatuwezi kuishi bila mvua Yako.” Akasema (kuwaambia Maswahaba): “Rudini, kwani mumenyeshewewa kwa du’aa za wengine.” [Imetolewa na Ahmad na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

414.

وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم   اسْتَسْقَى فَأَشَارَ بِظَهْرِ كَفَّيْهِ إِلَى اَلسَّمَاءِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ 

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliomba mvua, akaashiria kwa nyuma ya viganja[10] vyake kuelekea angani.” [Imetolewa na Muslim]

 

[1] Maana ya kifasihi ya Istisqaa ni “Kutafuta au kuomba maji.” Katika lugha ya ki Shariy’ah, hutumika kuuswalisha mkusanyiko maalumu ambamo du’aa huombwa ya kuomba mvua.  Ziko aina tatu za Istisqaa: (a) Adnaa (ndogo kuliko zote), (b) Awsatw (ya kati), (c) A’alaa (kubwa kuliko zote). Adnaa inamaanisha maombi ya mdomo tu. Awsatw ni maombi ya mdomo katika jamaa baada ya kuswali Swalaah ya Faradhi.   A’alaa inahitaji Swalaah maalumu ya jamaa kuomba mvua. Mchakato sahihi wa kuswali Istisqaa ni kuswali Rakaa mbili. Kisomo kiwe kwa sauti kubwa, kikifuatiwa na Khutbah mbili, na mwishowe du’aa iombwe kwa kuelekea Qiblah.

[2] Kuna tofauti ya idadi na mfululizo wa kutamka Takbiyra kati ya Swalaah ya ‘Iyd na Swalaah ya Istisqaa. Khutbah ni sharti ifuatie Swalaah ya Istisqaa, kwa namna ile ile kama katika Swalaah ya ‘Iyd.

[3] Maneno yale yasemayo, “Hakutoa aina yako ya Khutbah” inaashiria kuwa haikuwa Khutbah yake ndefu na ya kuchosha. Shah Waliyullaah katika kitabu chake ‘Hujjatullaahil-Baalighah’ amesema kuwa ziko njia nyingi za Istisqaa ambazo zimehusishwa na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Njia nzuri kuliko zote ambazo watu wanaweza kuzifuata ni kuwa watu wote wakusanyike msituni na Imaam; wawe wamevaa nguo za marapurapu, na wamuombe Allaah (عزّ وجلّ) huku wakilia machozi na nyoyo zilizojaa huzuni. Kisha Imaam aswalishe Swalaah yenye Rakaa mbili kwa kisomo cha sauti kubwa. Baada ya Swalaah, Imaam atoe Khutbah, kwa kumuomba Allaah (عزّ وجلّ) wakati uso wake umeelekea Qiblah, na kisha ageuze ridaa (juba) lake ndani nje.

[4] Kwa hivyo tunafahamishwa kuwa, katika Swalaah ya Istisqaa, du’aa zisomwe huku mikono imenyanyuliwa juu. Imaam An-Nawawi amekusanya Hadiyth ishirini juu ya jambo hili. Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia kuwa hakuwahi kamwe kumuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akinyanyua mikono yake katika du’aa zozote isipokuwa hizo za Istisqaa. Hii inadhihirisha ukweli kwamba hakuwahi kumuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akinyanyua mikono yake juu sana katika Swalaah yoyote ile isipokuwa hiyo ya Istisqaa.

[5] Abuu Ja’far Al-Baaqir ndiye Muhamaad Al-Baaqir bin ‘Aliy Zainul-‘Aabidiyn bin Husayn bin ‘Aliy bin Abiy Twaalib, Aliitwa Baaqir kwa ajili ya ‘Ilmu au ujuzi wake mpana. Alizaliwa mnamo mwaka 56 A.H. na akafa mnamo mwaka 117 A.H. akiwa na umri wa miaka 63, na akazikwa Al-Baqi’.

[6] Hadiyth hii inadhihirisha  kwamba, inafaa kuwataka watu wenye taqwa walio hai watuombee du’aa za Istisqaa, na wala siyo watu waliokwisha kufa. Watu wengi wanaamini kuwa du’aa zinaweza kuombwa kupitia kwa wafu, kwa kuwafanya wao wawe mapitio. Hivi ni kumshirikisha Allaah (عزّ وجلّ). Ingekuwa ni sahihi kuomba kwa kupitia wafu, ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) asingemuomba ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwaombea du’aa badala ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).

[7] Al-‘Abbaas bin Abd Al-Mutwallib ndiye Ammi yake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na alipewa jina la Abul-Fadhwl. Alikuwa ndiye anayewapa maji mahujaji Makkah na ujenzi wa Ka’bah. Alihudhuria Bay’atul-‘Aqabah (mkataba ‘Aqabah) kuhakikisha Maanswaar walikuwa waaminifu na wakweli katika ahadi zao, alikuwa hajawa Muislam hadi wakati ule. Alikamatwa pamoja na makafiri katika vita vya Badr, akasilimu kabla ya kuiteka Makkah, naye alishiriki kuiteka, alisimama imara katika vita vya Hunayn. Alikufa mwezi wa Rajab au Ramadhwaan mwaka 32 A.H. na akazikwa Al-Baqi’.

 

[8] Du’aa nyingi kuhusu Istisqaa zimeripotiwa kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na hii ni mojawapo.

[9] Mtindo wa kuwachukua wanyama katika Swalaah ya Istisqaa imethibitishwa kupitia Hadiyth hii. Kwa kuwa Allaah pengine Anaweza kuzikubali du’aa zao.

[10] Wanazuoni wanasema, iwapo du’aa itaombwa ili kupata Baraka za Allaah, mtu sharti anyanyue mikono yake kuomba du’aa kama kawaida (viganja viwe vinamwelekea huyo muombaji du’aa katika Swalaah hiyo). Lakini ikiwa du’aa inaombwa kuliepusha jambo ovu, mnyanyuo wa mikono sharti ugeuzwe (mikono inyanyuliwe, na viganja vikielekea nje). Inaelekea kuwa Allaah Ageuze ile hali. Kule kugeuza ridaa (juba) ndani kuwe nje pia kunamaanisha hivyo hivyo; na hali kadhalika tendo la kuelekeza nyuma ya viganja nje inaashiria ni kuomba Allaah Ayasogeze mawingu chini (yakiwa yamejaa maji).

 

 

Share

17-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Swalaah: Mlango Wa Adabu Za Mavazi

 

بُلُوغُ الْمَرام

 

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلصَّلَاةِ

 

Kitabu Cha Swalaah

 

بَابُ اَللِّبَاسِ

 

17-Mlango Wa Adabu Za Mavazi

 

 

 

 

415.

عَنْ أَبِي عَامِرٍ اَلْأَشْعَرِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم    {لَيَكُونَنَّ مِنْ أُمَّتِي أَقْوَامٌ يَسْتَحِلُّونَ اَلْحِرَ وَالْحَرِيرَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَأَصْلُهُ فِي اَلْبُخَارِيِّ 

Kutoka kwa Abuu ‘Aamir Al-Ash’ariyy[1] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kutakuwepo miongoni mwa ummah wangu watu watakaohalalisha zinaa pamoja na hariri.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na chanzo chake[2] kimo katika Al-Bukhaariy]

 

 

 

416.

وَعَنْ حُذَيْفَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   قَالَ: {نَهَى اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  أَنْ نَشْرَبَ فِي آنِيَةِ اَلذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ، وَأَنْ نَأْكُلَ فِيهَا، وَعَنْ لُبْسِ اَلْحَرِيرِ وَالدِّيبَاجِ، وَأَنْ نَجْلِسَ عَلَيْهِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ 

Kutoka kwa Khudhayfah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ametukataza kunywa katika vyombo vya dhahabu na fedha, na kula humo na kuvaa hariri na ad-diybaaj (vitambaa vya hariri vya vito na vilotariziwa kwa dhahabu na fedha) na kukaa juu yake.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

417.

وَعَنْ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   قَالَ: {نَهَى اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  عَنْ لُبْسِ اَلْحَرِيرِ إِلَّا مَوْضِعَ إِصْبَعَيْنِ، أَوْ ثَلَاثٍ، أَوْ أَرْبَعٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ 

Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kuvaa hariri isipokuwa sehemu ya vidole viwili, vitatu au vinne.”[3] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

418.

وَعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ  أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم {رَخَّصَ لِعَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ، وَالزُّبَيْرِ فِي قَمِيصِ اَلْحَرِيرِ، فِي سَفَرٍ، مِنْ حَكَّةٍ كَانَتْ بِهِمَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaruhusu ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf na Az-Zubayr[4] wavae kanzu za hariri katika safari kwa sababu ya upele wa kuwashwa ngozi waliokuwa nao.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

419.

وَعَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ:{كَسَانِي اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  حُلَّةً سِيَرَاءَ، فَخَرَجْتُ فِيهَا، فَرَأَيْتُ اَلْغَضَبَ فِي وَجْهِهِ، فَشَقَقْتُهَا بَيْنَ نِسَائِي} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَهَذَا لَفْظُ مُسْلِمٍ 

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alinipa mie juba lenye mistari[5] yenye hariri, halafu nikalivaa, nikaona ghadhabu usoni mwake, nililikatakata (na kuligawa) baina ya ahli zangu wanawake.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

420.

وَعَنْ أَبِي مُوسَى رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ: {أُحِلَّ اَلذَّهَبُ وَالْحَرِيرُ لِإِنَاثِ أُمَّتِي، وَحُرِّمَ عَلَى ذُكُورِهِمْ.} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالنَّسَائِيُّ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ 

Kutoka kwa Abuu Muwsaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Dhahabu na hariri vimeruhusiwa kwa wanawake wa Ummah wangu, na vimekatazwa kwa wanaume wao.” [Imetolewa na Ahmad, An-Nisaaiy na At-Tirmidhiy, naye aliisahihisha]

 

 

 

421.

وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا; أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: {إِنَّ اَللَّهَ يُحِبُّ إِذَا أَنْعَمَ عَلَى عَبْدٍ أَنْ يَرَى  أَثَرَ نِعْمَتِهِ عَلَيْهِ} رَوَاهُ اَلْبَيْهَقِيُّ 

Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Anapomneemesha mja Wake hupenda kuona athari ya neema yake juu yake.”[6] [Imetolewa na Al-Bayhaqiyy]

 

 

 

422.

وَعَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ   أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { نَهَى عَنْ لُبْسِ الْقَسِيِّ وَالْمُعَصْفَرِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kuvaa hariri na nguo zenye rangi ya zaafarani. [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

423.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِوٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: {رَأَى عَلَيَّ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  ثَوْبَيْنِ مُعَصْفَرَيْنِ، فَقَالَ: "أُمُّكَ أَمَرَتْكَ بِهَذَا؟"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliniona mimi nikiwa nimevaa nguo mbili za rangi ya zaafarani, akasema: “Mama yako ndiye aliyekuamrisha ufanye hivi?”[7] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

424.

وَعَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ أَبِي بَكْرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّهَا أَخْرَجَتْ جُبَّةَ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم  مَكْفُوفَةَ اَلْجَيْبِ وَالْكُمَّيْنِ وَالْفَرْجَيْنِ، بِالدِّيبَاجِ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ 

وَأَصْلُهُ فِي "مُسْلِمٍ"، وَزَادَ: {كَانَتْ عِنْدَ عَائِشَةَ حَتَّى قُبِضَتْ، فَقَبَضْتُهَا، وَكَانَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم  يَلْبَسُهَا، فَنَحْنُ نَغْسِلُهَا لِلْمَرْضَى نَسْتَشْفِي بِهَا}

وَزَادَ اَلْبُخَارِيُّ فِي "اَلْأَدَبِ اَلْمُفْرَدِ". {وَكَانَ يَلْبَسُهَا لِلْوَفْدِ وَالْجُمُعَةِ}

Kutoka kwa Asmaa bint Abiy Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Yeye alilitoa joho la Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) lililokuwa limedariziwa kwa hariri nzito mifukoni, mikononi na sehemu mbili zilizo wazi.”[8] [Imetolewa na Abuu Daawuwd]

 

Na chanzo chake kimo katika Swahiyh Muslim na kina nyongeza: “Lilikuwa kwa ‘Aaishah hadi alipokufa, nikalichukua mimi. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akilivaa, nasi tulikuwa tukiliosha kwa ajili ya wagonjwa waliokuwa wakilitumia kwa kuponywa nalo.”

 

Na Al-Bukhaariy aliongezea katika kitabu Adab Al-Mufrad[9]: “Alikuwa akilivaa kwa ajili ya wageni[10] na siku za Ijumaa.” [Imetolewa na Muslim]

 

[1] Abuu ‘Aamir Al-Ash’ariyy ndiye anayeitwa ‘Abdullaah bin Haaniy au ‘Ubayd bin Wahaab. Alikuwa ni Swahaba aliyelowea Sham, na alikuwa wakati wa utawala wa ‘Abdul Maalik bin Marwaan.

[2] Inamaanisha kwamba, watakuwa wakivaa mavazi ya hariri na watakuwa wanatenda zinaa kwa wingi sana ikiwa vitu hivi havitaharamishwa.

[3] Uvaaji wa mavazi ya hariri umekatazwa kwa wanaume. Hata hivyo inaruhusiwa kwa wanaume kuvaa vazi lenye msitari usiozidi sentimita tano hadi kumi. Lakini inaruhusiwa kwa mwanaume kuvaa vazi la hariri iwapo ana maradhi ya kuwashwa ngozi yaani eczema, n.k., au iwapo anashambuliwa na chawa. Kwa kuwa mavazi ya hariri humsaidia mtu anayeumwa magonjwa kama hayo, wanaruhusiwa kuendelea kuyatumia mpaka wapone.

[4] Az-Zubayr hyu ndiye Az-Zubayr bin Al-‘Awwaam bin Khuwaylid bin Asad Al-Qurayshiy Al-Asad, ambaye Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwita mwenyewe kuwa ni mfuasi mtiifu wake. Ni mtoto wa Swafiyyah bint Abdil-Muttwalib shangazi yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).  Zubayr ni miongoni mwa Maswahaba kumi waliobashiriwa Jannah. Alikuwa ni miongoni mwa mashujaa katika vita vya Kiislamu. Alifariki mwaka 36H baada ya kurejea kutoka vita vya Al-Jamal.  

[5] Vazi hili alipewa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na Mfalme wa jimbo la Aila. Lilikuwa na taraza (nakshi) za nyuzi za dhahabu na hariri.

[6] Hii inaweka wazi kwamba, kula chakula kizuri na kuvaa nguo nzuri sio dhidi ya taqwa. Kwa mujibu wa Hadiyth kwamba Allaah (عزّ وجلّ) Anapenda uzuri na usafi. Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hatoingia Jannah ambaye moyoni mwake mna kiburi uzito wa chembe (au sisimizi)). Mtu mmoja akauliza: “Mtu hupenda nguo yake iwe nzuri na viatu vyake viwe vizuri [itakuwaje?]” Akasema: ((Hakika Allaah ni Mzuri Anapenda Uzuri. Kiburi ni kukataa haki na kudharau watu)).  [Muslim]

 

[7] Hadiyth yote inasema hivi: “’Abdullaah bin ‘Amr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuomba ruhusa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuenda kuliosha lile vazi. Jibu lake (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikanusha, na akamuamrisha alichome, ambayo bila shaka ni adhabu.”

[8] Diybaaj ni hariri nzito iliyotariziwa kwa dhahabu.

[9] Hili ndilo jina la kitabu kilichoandikwa na Imaam Al-Bukhaariy.

[10] Hii inathibitisha kuwa, kuvaa mavazi mazuri inaruhusiwa siku za Ijumaa, na katika ‘Iyd zote mbili, na katika hadhara za watu. 

 

 

Share