Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Na Tarjuma Ya Kiswahili Na Sikiliza Hadiyth

 

 

 

 

Imaam An-Nawawiy

 

Na Tarjuma Ya Kiswahili

 

 Na Sikiliza Hadiyth

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Share

01-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: 'Amali Zinategemea Niyyah

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 1

 

إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ

 

Kila ‘Amali Zinategemea Niyyah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

 

عن أَمِيرِ المُؤمِنِينَ أَبي حَفْصٍ عُمَرَ بنِ الخطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى، فَمَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ فَهِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ، ومَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيا يُصِيبُها أو امْرأةٍ يَنْكِحُها فَهِجْرَتُهُ إلى ما هَاجَرَ إليه)). رَوَاهُ إِمَامَا الْمُحَدِّثِينَ أَبُو عَبْدِ اللهِ مُحَمَّدُ بنُ إِسْمَاعِيل بن إِبْرَاهِيم بن الْمُغِيرَة بن بَرْدِزبَه الْبُخَارِيُّ وَأَبُو الْحُسَيْنِ مُسْلِمٌ بنُ الْحَجَّاج بن مُسْلِم الْقُشَيْرِيُّ النَّيْسَابُورِيُّ   رحمهما الله  فِي "صَحِيحَيْهِمَا" اللذينِ هُمَا أَصَحُّ الْكُتُبِ الْمُصَنَّفَةِ.

Kutoka kwa Amiri wa Waumuni, Abu Hafs 'Umar Ibn Al Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hakika (kusihi kwa) ‘amali kunategemea niyyah, na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokinuia. Kwa hiyo ambaye hijrah yake ni kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, basi hijrah yake ni kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake. Na ambaye hijrah yake ni kwa ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya kumuoa mwanamke (fulani), basi hijrah yake ni kwa lile aliloliendea.”   [Hadiyth hii imepokelewa na Maimaam wawili ‘Ulamaa wa Hadiyth, Abuu ‘Abdillaah Muhammad bin Ismaa’iyl bin Ibraahiym bin Al-Mughiyrah bin Bar-dizbah Al-Ju’fiyy Al-Bukhaariy, na Abul-Husayn Muslim bin Al-Hajjaaj bin Muslim Al-Qushayriyy An-Naysaaburiyy (Rahimahuma-Allaah) Wameipokea katika vitabu vyao ambavyo ndio Swahiyh katika vitabu vya Hadiyth vilivyosanifiwa] 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share

02-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Kuja Kwa Jibriyl Kuwafundisha Waislamu Mambo Ya Dini Yao

 

 

 

 

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 2

 

مجىء جبريل ليعلم المسلمين أمر دينهم

 

 Kuja Kwa Jibriyl ('Alayhis-Salaam) Kuwafundisha

Waislamu Mambo Ya Dini Yao

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

 

 عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قَالَ: بَيْنَما نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْدَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَومٍ، إذْ طَلَعَ عَلَينا رَجُلٌ شَديدُ بَياضِ الثِّيابِ، شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عَلَيهِ أثَرُ السَّفَرِ، وَلا يَعْرِفُهُ مِنَّا أحَدٌ، حَتَّى جَلَسَ إِلَى النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيهِ إِلَى رُكْبتَيهِ، وَوَضعَ كَفَّيهِ عَلَى فَخِذَيهِ.

وَقالَ: يَا مُحَمَّدُ، أخْبرني عَنِ الإسلامِ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((الإسلامُ: أنْ تَشْهدَ أنْ لاَّ إلهَ إلاَّ الله وَأنَّ مُحمَّدًا رسولُ الله، وتُقيمَ الصَّلاةَ، وَتُؤتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ البَيتَ إن اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبيلًا)). قَالَ: صَدَقْتَ. فَعَجِبْنَا لَهُ يَسْأَلُهُ وَيُصَدِّقهُ!

قَالَ: فَأَخْبرنِي عَنِ الإِيمَانِ. قَالَ: ((أنْ تُؤمِنَ باللهِ، وَمَلائِكَتِهِ، وَكُتُبهِ، وَرُسُلِهِ، وَاليَوْمِ الآخِر، وتُؤْمِنَ بالقَدَرِ خَيرِهِ وَشَرِّهِ)). قَالَ: صَدقت. قَالَ: فأَخْبرني عَنِ الإحْسَانِ. قَالَ: ((أنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاكَ)).

قَالَ: فَأَخْبِرني عَنِ السَّاعَةِ. قَالَ: ((مَا المَسْؤُولُ عَنْهَا بأعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ)). قَالَ: فأخبِرني عَنْ أمَاراتِهَا. قَالَ: ((أنْ تَلِدَ الأَمَةُ رَبَّتَهَا، وأنْ تَرَى الحُفَاةَ العُرَاةَ العَالَةَ رِعَاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ في البُنْيَانِ)).

ثُمَّ انْطَلقَ فَلَبِثْتُ مَلِيًّا، ثُمَّ قَالَ: ((يَا عُمَرُ، أَتَدْري مَنِ السَّائِلُ؟)) قُلْتُ: اللهُ ورسُولُهُ أعْلَمُ. قَالَ: ((فإنَّهُ جِبْريلُ أَتَاكُمْ يعْلِّمُكُمْ دِينَكُمْ)). رواه مسلم

‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa mbele ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa ghafla akatutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaweka magoti yake karibu na magoti yake (Rasuli) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ee Muhammad! Niambie kuhusu Uislaamu.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:  “Uislamu ni kukiri kuwa hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa  Allaah, na Muhammad ni Rasuli wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kufunga swawm Ramadhwaan na kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.” (Akasema yule mtu yaani Jibriyl): “Umesema kweli.” Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza  kwake Rasuli na kumsadikisha.  Na akasema tena: Niambie kuhusu Iymaan.  Akasema: “Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Rasuli Wake na siku ya Qiyaamah, na  kuamini Qadar  (majaaliwa ya Allaah) ya kheri zake na shari zake.” (Akasema Jibriyl): “Umesema kweli.”. Akasema: “Hebu nielezee kuhusu Ihsaan.”  Akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni kumuabudu Allaah kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona.”  Akasema (Jibriyl): “Niambie    kuhusu Qiyaamah.”  Akajibu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile Muulizaji.” Kisha akamwambia: “Nijulishe alama zake.”: Akajibu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga wenda miguu chini, wenda uchi (wasio na uwezo wa kumiliki hata mavazi), mafukara (wasiokuwa hata na sehemu ya kuishi kwa umaskini) wakishindana kujenga majumba ya fahari.” Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo (nikitafakari). Kisha akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee 'Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? Nikasema: Allaah na Rasuli wake wanajua zaidi.  Akasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha dini yenu.” [Muslim]

 

 

 

 

Share

03-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Nguzo Za Kiislamu Ni Tano

 

 

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 3

 

بني الإسلام على خمس

 

Nguzo Za Kiislamu Ni Tano

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي عَبْدِ الرَّحْمنِ عَبْدِ اللهِ بنِ عُمَرَ بنِ الخَطابِ رَضيَ اللهُ عنهُما قال: سَمِعْتُ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ: ((بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ: شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ )) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Abuu Abdir-Rahmaan Abdillaah Ibn 'Umar Ibn  Al-Khattwaab  (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema:  Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akisema: “Uislamu umejengwa kwa nguzo tano: Kukiri na kushuhudia kwamba hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli Wake,  kusimamisha Swalaah, kutoa Zaka na kuhiji Al-Bayt (Makkah) na kufunga swawm Ramadhwaan.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share

04-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Hakika Kila Mmoja Wenu Hukusanywa Umbo Lake Katika Tumbo La Mama Yake

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

 

Hadiyth Ya 4

 

إنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّه

 

Hakika Kila Mmoja Wenu Hukusanywa Umbo Lake

Katika Tumbo La Mama Yake

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي عبْدِ الرَّحْمن عبدِ الله بنِ مسعودٍ رضي الله عنه قال: حدَّثَنا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وهُوَ الصَّادقُ المَصْدوق: ((إنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّه فِي أرْبعينَ يوْماً نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يُرْسَلُ إليه المَلكُ فَيَنْفخُ فيه الرُّوحَ ويُؤمَرُ بأرْبَعِ كلماتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ وأَجَلِهِ وعَمَلِهِ وشَقيٌّ أو سَعيدٌ، فَوَاللهِ الَّذي لا إله غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ ليَعْمَلُ بعَمَلِ أهْلِ الجَنَّةِ حتى ما يكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَليْه الكِتابُ فَيَعْمَلُ بعَملِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُها. وإنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهل النَّارِ حتى ما يَكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكتابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهل الجنَّةِ فَيَدْخُلُها)) رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: “Ametusimulia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake).  Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. Wa-Allaahi naapa kwa Yule Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye ‘amali za watu wa Jannah hadi ikawa baina yake na Jannah ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja wenu hufanya ‘amalii za watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

 

Share

05-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Atakayezusha Katika Jambo Letu Hili (la Dini) Ambalo Halimo Humu Basi Litakataliwa

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 5

 

مَنْ أَحْدَثَ في أَمْرِنا هذا ما لَيْسَ منهُ فَهُوَ رَد

 

Atakayezusha Katika Jambo Letu hili (la Dini)

Ambalo Halimo Humo Litarudishwa

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أُمِّ المُؤمِنينَ أُمِّ عَبْدِ الله عائِشَةَ رَضي اللهُ عنها قالَتْ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ أَحْدَثَ في أَمْرِنا هذا ما لَيْسَ منهُ فَهُوَ رَد)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ  وَمُسْلِمٌ 

 وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ :     ((مَن عَمِلَ عَمَلاً لَيْسَ عَلَيْهِ أَمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ ))

Imepokelewa kutoka kwa Mama wa Waumini Ummu Abdillaah ‘Aishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ambaye amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayezusha katika jambo letu hili (la Dini) lolote ambalo halimo humo litarudishwa.”  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na katika riwaayah ya Muslim:  ”Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika Dini) basi kitarudishwa.”

 

 

 

 

 

Share

06-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Hakika Halaal Imebainika Na Haraam Imebainika

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 6

 

إن الْحَلالَ بَيِّنٌ وَإنَّ الْحَرَامَ بَيِّنٌ

 

Hakika Halaal Imebainika Na Haraam Imebainika

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

عَنْ أبي عَبْدِ اللهِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُما قَالَ : سمعتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:  ((إن الْحَلالَ بَيِّنٌ وَإنَّ الْحَرَامَ بَيِّنٌ وَبَيْنَهُما أمورٌ مُشْتَبِهَاتٌ لا يَعْلَمُهُنَّ كَثيِرٌ مِنَ الناسِ، فَمَنِ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ فَقَد اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ، وَمَنْ وَقَعَ في الشَّبُهاتِ وَقَعَ في الْحَرَامِ، كالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الْحِمَى يُوشِكُ أَنْ يَرْتَعَ فِيهِ، أَلا وَإنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمىً أَلا وَإنَّ حِمَى الله مَحَارِمُه، أَلا وَإنَّ في الجَسَدِ مُضْغَةً إذَا صَلَحَتْ صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّهُ وإذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، أَلا وَهِيَ الْقَلْبُ))  رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ  وَمُسْلِمٌ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu  ‘Abdillaah An-Nu’umaan bin  Bashiyr  (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye alisema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hakika halaal imebainika na haraam imebainika na baina ya mawili hayo mna yenye kutia shaka. Wengi miongoni mwa watu hawayajui. Basi atakayejiepusha yenye kutia shaka, atakuwa amejiepushia shaka katika Dini yake na heshima yake. Na Atakayetumbukia katika yenye kutia shaka, ataingia kwenye haraam. Kama mchunga anayechunga kando ya mipaka, ni haraka kulisha humo (mpaka mwingine wa watu). Zindukeni!  Kila mfalme ana mipaka. Zindukeni! Kwa yakini mipaka ya Allaah ni haraam Alizoziharamisha. Zindukeni! Kwa yakini katika mwili mna kinofu cha nyama, kinapokuwa salama, mwili wote unakuwa salama. Kinapoharibika, mwili wote unaharibika. Zindukeni! Kinofu hicho ni moyo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share

07-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Dini Ni Nasiha

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 7

 

الدِّينُ النَّصِيحَةُ

 

Dini Ni Nasiha

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بنِ أوْسٍ الدَّارِيِّ رضي اللهُ عنه: أَنَّ النَّبي صلى الله عليه وسلم قالَ:((الدِّينُ النَّصِيحَةُ)). قُلْنَا: لِمَنْ ؟ قالَ: ((للهِ، ولِكِتَابِهِ، ولِرَسُولِهِ، ولِلأَئِمةِ المُسْلِمِينَ، وعامَّتِهِمْ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ    

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ruqayyah Tamiymi Ibn Aws Addaarriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Dini ni nasiha.”  Tukauliza: Kwa nani? Akasema: “Kwa Allaah na Kitabu Chake, na Rasuli Wake, na kwa viongozi wa Waislamu na watu wa kawaida.” [Muslim]

 

Share

08-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Nimeamrishwa Nipigane Vita Na Watu

 

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 8

 

أُمِرْتُ أَنْ أُقاتِلَ النَّاسَ

 

Nimeamrishwa Nipigane Vita Na Watu

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

 عن ابنِ عُمَرَ رضي الله عنهما أنَّ رسُوَل الله صلى الله عليه وسلم قال: ((أُمِرْتُ أَنْ أُقاتِلَ النَّاسَ حتَّى يَشْهَدُوا أنْ لا إلَهَ إلاَّ اللهُ وأنَّ محمداً رسوُل اللهِ، ويُقِيمُوا الصَّلاَةَ، ويُؤتُوا الزَّكاةَ، فإذا فَعَلوا ذَلِكَ عَصَموا منِّي دِماءَهُمْ وأمْوَالَهُمْ إلا بِحَقِّ الإِسْلامِ، وحِسابُهُم على اللهِ تعالى)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ   وَمُسْلِمٌ   

 Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa)  kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Nimeamrishwa nipigane vita na watu mpaka washahidie kwamba hakuna Muabudiwa wa haki ila Allaah  na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah.  Watakapofanya hivyo, watakuwa wamepata himaya Kwangu ya damu zao, na mali zao isipokuwa  kwa haki ya Uislamu, na hesabu yao itakuwa kwa Allaah Ta’aalaa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

09-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Nilichokukatazeni Kiepukeni

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 9

 

ما نَهَيْتُكُمْ عَنْهُ فَاجتَنبوهُ

 

Nilichokukatazeni Kiepukeni

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي هُرَيْرةَ عَبْدِ الرَّحمنِ بنِ صَخْرٍ رضي الله عنه قال : سمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((ما نَهَيْتُكُمْ عَنْهُ فَاجتَنبوهُ، وَمَا أَمَرْتُكُمْ بِهِ فأتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ، فإنَّما أَهْلَكَ الَّذينَ مِنْ قَبْلِكُمْ كَثْرَةُ مَسَائِلِهِمْ واخْتلاُفُهُمْ على أَنْبِيَائِهِمْ)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ   

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah ‘Abdir-Rahmaan bin Swakhr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Kile nilichokukatazeni kiepukeni, na kile nilichokuamrisheni fanyeni kwa wingi kadiri muwezavyo. Hakika kilichowaangamiza wale waliokuwa kabla yenu ni masuala (mahojiano) mengi na kukhitilafiana kwao na Manabii wao.”  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

10-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Allaah Ni Twayyib Hapokei Isipokuwa Kilichokuwa Ni Twayyib (Kizuri)

 

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 10

 

إنَ الله تعالى طَيِّبٌ لا يَقْبَلُ إلا طَيِّباً

 

Hakika Allaah Ni Twayyib Hapokei Isipokuwa

Kilichokuwa Twayyib (Kizuri)

 

Alhidaaya.com

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 عن أبي هُرَيْرَةَ رَضي اللهُ عنه قال: قاَل رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَ الله تعالى طَيِّبٌ لا يَقْبَلُ إلا طَيِّباً، وإنَّ الله أَمَرَ المُؤمِنينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ المُرْسَلينَ فقال تعالى: ((يا أَيُّها الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيَّباتِ واعمَلُوا صالحاً)) [المؤمنون: 51] وقال تعالى: ((يا أَيُّها الَّذِينَ آمَنُوا كلُوا مِنْ طَيِّباتِ ما رَزَقْناكُمْ)) [البقرة: 172] ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ يُطِيلُ السَّفَرَ أشْعَثَ أَغْبَرَ يَمُدُّ يَدَيْهِ إلى السَّماءِ يا رَبُّ يا رَبُّ، ومَطْعَمُهُ حَرَامٌ، ومَشْربُهُ حَرَامٌ، وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ وغُذِّيَ بالحَرَامِ، فأَنَّى يُسْتَجَابُ لهُ!)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ    

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allaah ni Twayyib Hapokei isipokuwa kilichokuwa twayyib (kizuri). Na hakika Allaah Amewaamrisha Waumini yale ambayo Amewaamrisha Rasuli Akasema:

 

((يا أَيُّها الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيَّباتِ واعمَلُوا صالحاً))

 

“Enyi Rasuli! Kuleni katika vizuri na tendeni mema.” [Al-Muuminuwn: 51]  Na Akasema Ta’aalaa:

 

((يا أَيُّها الَّذِينَ آمَنُوا كلُوا مِنْ طَيِّباتِ ما رَزَقْناكُمْ))

 

Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni” [Al-Baqarah: 172] Kisha akamtaja mtu  aliyesafiri safari ndefu, kachafuka na kajaa mavumbi na huku anayanyua mikono yake mbinguni akisema: “Ee Rabb!  Ee Rabb! Na hali chakula chake ni haraam, na kinywaji chake ni haraam, na mavazi yake ni haraam   na  anashibishwa na haraam, je, vipi atajibiwa (du’aa zake?)” [Muslim]

 

 

Share

11-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Acha Kinachokutia Shaka Ufuate Kisichokutia Shaka

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 11

 

دَعْ ما يَرِيبُكَ إلى مَا لاَ يَرِيُبكَ

 

Acha Kinachokutia Shaka Ufuate Kisichokutia Shaka

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 عَنْ أَبي مُحمَّدٍ الحسَنِ بْنِ عليّ بْنِ أبي طَالِب، سِبْطِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم وَرَيْحَانَتِهِ رضيَ اللهُ عنهُما، قالَ: حَفِظْتُ مِنْ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ ما يَرِيبُكَ إلى مَا لاَ يَرِيُبكَ)) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ   وَالنَّسَائِيُّ    وَقَالَ التِّرْمِذِيُّ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ. 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muhammad Al-Hasan Ibn ‘Aliyy Ibn Abi Twaalib mjukuu wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kipenzi chake (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amesema: Nilihifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Wacha kile kinachokutia shaka ufuate kile kisichokutia shaka”. [At-Tirmidhiy na An-Nasaai, At-Tirmidhiy amesema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Share

12-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Miongoni Mwa Uzuri Wa Uislamu Wa Mtu

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 12

 

مِنْ حُسْنِ إسْلاَمِ الْمَرْءِ

 

Miongoni Mwa Uzuri Wa Uislamu Wa Mtu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 عن أبي هُرَيْرَةَ رضي اللهُ عنه قالَ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مِنْ حُسْنِ إسْلاَمِ الْمَرْءِ تَرْكُهُ مَا لاَ يَعْنِيهِ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ، وَغَيره هكذا      

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Miongoni mwa uzuri wa Uislamu wa mtu, ni  kuacha yale yasiyomuhusu.” [Hadiyth Hasan, Imesimuliwa na At-Tirmidhiy na wengineo]

 

 

Share

13-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Hatoamini Mmoja Wenu Mpaka Ampendelee Nduguye Anachokipendelea Nafsi Yake

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 13

 

لا يُؤمِنُ أحَدُكُمْ حتى يُحِبَّ لأخِيهِ ما يُحِبُّ لِنَفْسِهِ

 

Hatoamini Mmoja Wenu Mpaka Ampendelee Nduguye

Anachokipendelea Nafsi Yake

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي حَمْزَةَ أَنسِ بنِ مالكٍ رضي اللهُ عنه خادِمِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم , عَنِ النَّبِي  صلى الله عليه وسلم قال : ((لا يُؤمِنُ أحَدُكُمْ حتى يُحِبَّ لأخِيهِ ما يُحِبُّ لِنَفْسِهِ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hamzah Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu), mtumishi wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hatoamini mmoja wenu mpaka atakapompendelea ndugu yake kile anachojipendelea nafsi yake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share

14-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Haipasi Kumwagwa Damu Ya Muislamu Isipokuwa Kwa Sababu Tatu

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 14

 

 لاَ يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ إلاّ بإحْدَى ثَلاَثٍ

 

Haipasi Kumwagwa Damu Ya Muislamu Isipokuwa Kwa Sababu Tatu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

 

 

 

عن ابْنِ مَسْعُودٍ رضي اللهُ عنه قالَ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لاَ يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ   إلاّ بإحْدَى ثَلاَثٍ: الثَّيِّبُ الزَّاني، وَالنَّفْسُ بالنّفْسِ، وَالتَّارِكُ لِدِيِنِهِ الْمُفَارِقُ لِلْجَماعَةِ))  رَوَاهُ الْبُخَارِيّ وَمُسْلِمٌ    

Imepokelewa kutoka kwa Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Haipasi kumwagwa damu ya Muislamu isipokuwa kwa sababu tatu:  Mzinifu aliyeolewa, uhai kwa uhai, na anayeacha Dini  na akajifarikisha na  jamaa-‘ah.”  [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

 

Share

15-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Anayemuamini Allaah Na Siku Ya Mwisho Basi Aseme Ya Khayr Au Anyamaze...

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 15

 

مَنْ كانَ يُؤمِنُ باللهِ والْيَوْمِ الآخِرِ فَلْيَقُل خَيْراً

 

Anayemuamini Allaah Na Siku Ya Mwisho Basi

Aseme Ya Khayr Au Anyamaze

 

Alhidaaya.com

 

Sikiliza Hadiyth:

 

عن أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنهُ: أنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : ((مَنْ كانَ يُؤمِنُ باللهِ والْيَوْمِ الآخِرِ فَلْيَقُل خَيْراً أَوْ لِيَصْمُتْ، ومَنْ كانَ يُؤمِنُ باللهِ والْيَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ جارَهُ، ومَنْ كانَ يُؤمِنُ باللهِ والْيوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ )) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ  وَمُسْلِمٌ    

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Anayemuamini Allaah na Siku ya mwisho basi aseme ya khayr au anyamaze. Na Anayemuamini Allaah na Siku ya mwisho basi amkirimu jirani yake. Na anayemuamini Allaah na Siku ya mwisho basi amkirimu mgeni wake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share

16-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Usighadhibike

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 16

 

لا تَغْضَبْ

 

Usighadhibike

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي هُرَيْرَةَ رضي اللهُ عنه أنَّ رَجُلاً قال لِلنَّبِّي صلى الله عليه وسلم: أَوصِني، قالَ: ((لا تَغْضَبْ))، فَرَدَّدَ مِرَاراً، قال: ((لا تَغْضَبْ)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ   

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba mtu alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Niusie. Akasema: “Usighadhibike.” Yule mtu akakariri tena (ombi lake na kuusiwa) mara kadhaa (Na kila mara Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: “Usighadhibike.” [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share

17-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Hakika Allaah Ameandika Ihsani Katika Kila Kitu

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

 

Hadiyth Ya 17

 

إنَّ اللهَ كَتَبَ الإِحْسانَ على كلِّ شَيءٍ

 

Hakika Allaah Ameandika Ihsani Katika Kila Kitu

 

Alhidaaya.com

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عَنْ أبي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رضي اللهُ عنه، عن رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال: ((إنَّ اللهَ كَتَبَ الإِحْسانَ على كلِّ شَيءٍ، فإذا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذِّبْحَةَ، ولْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ ولْيُرِحْ ذَبيحَتَهُ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ   

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ya’laa Shaddaad bin Aws (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allaah Ameandika ihsaan katika kila kitu. Kwa hiyo mnapoua (mnyama), ueni vizuri  na unapochinja chinjeni vizuri.  Basi kila mmoja wenu anoe kisu chake barabara (anapotaka kuchinja) na amuondoshee mateso mnyama anayemchinja.” [Muslim]

 

 

 

Share

18-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Mche Allaah Popote Ulipo

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 18

 

اتَّقِ اللهَ حَيْثُما كنْتَ

 

Mche Allaah Popote Ulipo

 

Alhidaaya.com

 

Sikiliza Hadiyth:

 

عن أبي ذَرٍّ جُنْدُب بِن جُنَادَة، وأبي عبد الرحمن مُعَاذ بِن جَبَلٍ رضي الله عنهما، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((اتَّقِ اللهَ حَيْثُما كنْتَ، وأَتْبِعِ السَّيئةَ الحسنةَ تَمْحُها، وخالقِ الناسَ بخُلُقٍ حسنٍ)) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ   وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ، وَفِي بَعْضِ النُّسَخِ: حَسَنٌ صَحِيحٌ. 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr Jundub bin Junaadah Na Abuu ‘Abdir-Rahmaan Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ““Mche Allaah popote pale ulipo. Na fuatisha kitendo kiovu kwa kitendo kizuri ili kikifute (kilicho kiovu), na ishi na watu kwa tabia nzuri.” [At-Tirmidhiy na kasema ni Hadiyth Hasan. Na katika  baadhi ya nukuu: Hasan Swahiyh]

 

 

Share

19-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Mhifadhi Allaah Atakuhifadhi

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

 

Hadiyth Ya 19

 

احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ

 

Mhifadhi Allaah Atakuhifadhi

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

عن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما، قَالَ: كنت خلف النَّبيّ صلى الله عليه وسلم يومًا، فَقَالَ: ((يَا غُلامُ، إنِّي أعلّمُكَ كَلِمَاتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إِذَا سَألْتَ فَاسأَلِ الله، وإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ باللهِ. وَاعْلَمْ: أنَّ الأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ لَكَ، وَإِن اجتَمَعُوا عَلَى أنْ يَضُرُّوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأَقْلاَمُ وَجَفَّتِ الصُّحفُ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن صحيح)).

وفي رواية غيرِ الترمذي: ((احْفَظِ الله تَجِدْهُ أَمَامَكَ، تَعرَّفْ إِلَى اللهِ في الرَّخَاءِ يَعْرِفكَ في الشِّدَّةِ، وَاعْلَمْ: أنَّ مَا أَخْطَأكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبكَ، وَمَا أصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَاعْلَمْ: أنَّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ، وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ، وَأَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرًا))

‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (juu ya mnyama). Akaniambia: “Ee kijana, mimi nitakufundisha maneno: Mhifadhi Allaah Naye Atakuhifadhi. Mhifadhi Allaah utamkuta yupo mbele yako. Unapoomba, muombe Allaah. Unapotaka msaada, mtake Allaah. Fahamu kuwa, lau ummah (wote) utajikusanya ili wakunufaishe kwa jambo, basi hawataweza kukunufaisha ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah; na wakijumuika ili wakudhuru kwa jambo, hawataweza kukudhuru ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah. Kalamu zimeshasimama na karatasi zimeshakauka.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Riwaayah nyingine isiyokuwa ya At-Tirmidhiy imesema:

 

“Mhifadhi Allaah utamkuta Yupo mbele yako. Mjue Allaah katika raha Naye Atakujua katika shida. Ujue kuwa, lililokukosa halikuwa ni lenye kukupata, na lililokusibu halikuwa ni lenye kukukosa. Ujue kuwa nusura ipo pamoja na subira, faraja ipo pamoja na dhiki, na kwenye uzito kuna wepesi.”

 

 

 

Share

20-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Ikiwa Huna Hayaa Basi Fanya Utakavyo

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 20

 

إِذا لمْ تَسْتَحِ فاصْنَعْ ما شِئْتَ

 

Ukiwa Huna Hayaa Basi Fanya Utakavyo

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي مَسْعُودٍ عُقْبَةَ بن عمرو الأَنْصَارِيّ البَدْرِيّ رضي اللهُ عنه قال : قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((إِنَّ مما أَدْرَكَ النَّاسُ مِنْ كَلامِ النُّبُوَّةِ الأولَى: إِذا لمْ تَسْتَحِ فاصْنَعْ ما شِئْتَ)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ  

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Mas’uwd ‘Uqbah bin ‘Amruw Al-Answaariyy Al-Badriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: “Katika maneno ambayo watu waliyapata kutoka kwa Manabii wa mwanzo (waliotangulia) ni:  Ikiwa huna hayaa basi fanya utakavyo.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Share

21-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Sema Namuamini Allaah Kisha Thibitika Imara

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 21

 

قُلْ: آمَنْتُ بِاللهِ، ثُمَّ استَقِمْ

 

Sema Namuamini Allaah Kisha Thibitika Imara

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي عمر، وقيل: أبي عَمرة سفيان بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُول الله، قُلْ لي في الإسْلامِ قَولًا لا أسْأَلُ عَنْهُ أَحَدًا غَيْرَكَ. قَالَ: ((قُلْ: آمَنْتُ بِاللهِ، ثُمَّ استَقِمْ)). رواه مسلم

Abuu 'Umar, na pia imesemwa anajulikana kama: Abuu ‘Amrah Sufyaan bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimwambia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); niambie neno katika Uislamu ambalo sitamuuliza yoyote zaidi yako. Akasema: “Sema: Nimemuamini Allaah, kisha uthibitike imara.” [Muslim]

 

 

Share

22-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Je, Nikiswali Swalaah Za Fardhi, Nikafunga Swawm Ramadhwaan…

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

 

Hadiyth Ya 22

 

أَرَأَيْتَ إذَا صَلَّيْتُ  الْمكْتُوباتِ، وَصُمْتُ رَمَضانَ

 

Je, Nikiswali Swalaah Za Fardhi, Nikafunga Swawm Ramadhwaan

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عَنْ أبي عَبْدِ اللهِ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ الأنْصَارِيِّ رَضي اللهُ عَنْهُما أَنَّ رَجُلاً سَأَلَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَقال: أَرَأَيْتَ إذَا صَلَّيْتُ  الْمكْتُوباتِ، وَصُمْتُ رَمَضانَ، وَأَحْلَلْتُ الْحَلاَلَ، وَحَرَّمْتُ الْحَرَامَ، وَلَمْ أَزِدْ على ذِلكَ شَيْئاً، أَأَدْخُلُ الْجَنَّةَ ؟ قال: ((نَعَمْ))  رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu ‘Abdillaah Jaabir bin ‘Abdillaah Al-Answaariy (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba mtu alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Je nikiswali Swalaah za fardhi, nikafunga Swawm Ramadhwaan, na nikafanya halaal yaliyo halaal, na nikaharamisha kile kilichoharimishwa, na nisizdishe juu yake chochote, je nitaingia Jannah? Akamjibu: “Ndio.” [Muslim]

 

 

 

 

 

Share

23-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Twahaarah Ni Nusu Ya Iymaan

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 23

 

الطُّهُورُ شَطْرُ الإِيَمانِ

 

Twahaarah Ni Nusu Ya Iymaan

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي مالكٍ الحارِثِ بنِ عاصِمٍ الأَشْعَرِيِّ رضي اللهُ عنهُ قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((الطُّهُورُ شَطْرُ الإِيَمانِ، والحمدُ لِلهِ تَمْلأُ الْمِيزَانَ، وسُبْحانَ اللهِ والحمدُ لِلهِ تَمْلآنِ - أو تَمْلأُ - ما بَيْنَ السَّمآءِ والأرضِ، والصَّلاةُ نورٌ، والصَّدَقَةُ بُرْهانٌ، والصَّبْرُ ضِيَاءٌ، والْقُرآنُ حُجَّةٌ لَكَ أو عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدو، فَبائعٌ نَفْسَهُ، فَمُعْتِقُها أَو مُوبِقُها))  رَوَاهُ مُسْلِمٌ   

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Maalik Al-Haarith bin ‘Aaswim Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Twahaara ni nusu ya iymaan, na AlhamduliLLaah inajaza mizani, na Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah inajaza baina  ya mbingu na ardhi.  Na Swalaah ni nuru, na swadaqah ni burhani na subira ni mwangaza, na Qur'aan ni hoja yako au dhidi yako. Kila mtu anaianza siku yake akiichuuza nafsi yake, aidha huiacha huru au anaisambaratisha.” [Muslim]

 

 

 

 

 

Share

24-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Enyi Waja Wangu Hakiki Mimi Nimeiharamisha Nafsi Yangu Dhulma

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 24

 

إنِّي حَرَّمْتُ الظُلْمَ على نَفْسِي

 

Hakika Mimi Nimeiharamisha Nafsi Yangu Dhulma

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

عن أبي ذَرٍّ الْغِفاريِّ رضي الله عنه، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم فيما يَرْويهِ عن رَبِّهِ عَزَّ وجَلَّ أَنَّهُ قال: 

 

((يا عِبادي إنِّي حَرَّمْتُ الظُلْمَ على نَفْسِي وَ جعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّماً فلا تَظَالَمُوا.

 

يا عِبادي كُلُّكُمْ ضالٌّ إلا مَنْ هَدَيْتُهُ، فاسْتَهدُوني أهْدِكُمْ.

 

يا عِبادِي كُلُّكُمْ جائعٌ إلا مَنْ أطْعَمْتُهُ، فاسْتَطْعِمُوني أُطْعِمْكُم.

 

يا عِبادِي كُلُّكُمْ عَارٍ إلا مَنْ كَسَوْتُهُ، فاسْتكْسوني أَكسُكُم.

 

يا عِبادِي إِنَّكُمْ تُخْطِئُونَ بالليْلِ والنَّهارِ، وأنا أَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَميعاً، فاسْتَغْفِرُوني أُغْفِر لكُمْ.

 

يا عِبادِي إِنَّكُمْ لنْ تبْلغُوا ضُرِّي فتَضُرُّوني، ولن تبْلُغُوا نفْعي فَتَنْفعُوني.

 

يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَتْقَى قَلْبِ رَجُلٍ واحدٍ مِنْكُمْ ما زادَ ذلك في مُلْكي شَيئاً.

 

يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَفْجَرِ قَلْبِ رَجُلٍ وَاحدٍ مِنْكُمْ ما نَقَصَ ذَلِكَ مِنْ مُلْكي شَيئاً.

 

يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجنَّكُمْ قاموا في صَعِيدٍ وَاحِدٍ، فَسَأَلُوني، فأَعْطَيْتُ كلَّ واحدٍ مَسْأَلَتَهُ ما نَقَصَ ذلك مِمَّا عِنْدِي إلا كما يَنْقُصُ الْمِخْيَطُ إذا أُدْخِلَ الْبَحْرَ.

 

يا عِبادِي إنَّما هي أعمَالُكُمْ أُحْصِيها لَكُمْ ثُمَّ أُوَفِّيكُمْ إيَّاها، فَمَنْ وَجَدَ خيْراً فَلْيَحْمَدِ اللهَ، ومَنْ وَجَدَ غَيْرَ ذلك فَلا يَلومَنَّ إلا نَفْسَه)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ     

 

Imepokelewa kutoka kwa Abu Dharr Al-Ghifaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisimulia yale aliyopokea kutoka kwa  Rabb wake (Aliyetukuka na Jalaali) :

 

“Enyi waja Wangu, Nimeikataza nafsi Yangu dhulma na Nimeiharamisha kwenu (hiyo dhulma), kwa hivyo msidhulumiane.

 

Enyi waja Wangu, nyote mumepotea isipokuwa wale Niliowaongoza, kwa hivyo tafuteni muongozo kutoka Kwangu Nitakuongozeni. 

 

Enyi waja Wangu nyote mna njaa isipokuwa wale Niliowalisha, kwa hivyo tafuteni chakula kutoka Kwangu na Nitakulisheni.

 

Enyi waja Wangu, nyote mko uchi isipokuwa wale niliowavika nguo, kwa hivyo tafuteni vazi kutoka Kwangu Nitakuvisheni.

 

Enyi waja Wangu, mnafanya makosa usiku na mchana, na Ninaghufuria dhambi zote, kwa hivyo ombeni maghfirah kutoka Kwangu Nitakughufurieni.

 

Enyi waja Wangu hamuwezi kunidhuru Mimi wala kuninufaisha.  

 

Enyi waja Wangu, ingekuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mwenye taqwa kama moyo wa mwenye taqwa katika nyinyi, haitaongeza chochote katika ufalme Wangu.

 

Enyi waja Wangu, angelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadam katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mbaya kama moyo mbaya wa mtu miongoni mwenu (mtu mbaya kupita kiasi) haitonipunguzia chochote katika ufalme Wangu.

 

Enyi waja Wangu ingelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadam katika nyinyi na majini katika nyinyi mkasimama pahala pamoja na mkaniomba, na Nikawapa kila mmoja alichoomba, haitonipunguzia katika nilicho Nacho zaidi kuliko sindano inavyopunguza bahari inapochovywa.

 

Enyi waja Wangu, ni vitendo vyenu ninavyovihesabu, kwa ajili yenu Nikakulipeni. Kwa hivyo anayekuta kheri amhimidi Allaah na yule anayekuta kinyume chake basi ajilaumu mwenyewe.” [Muslim]

 

 

 

 

Share

25-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Wenye Mali Wameondoka Na Thawabu Nyingi

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 25

 

ذَهَب أَهْلُ الدُّثورِ بالأُجورِ

 

Wenye Mali Wameondoka Na Fungu Kubwa (La Thawabu)

 

Alhidaaya.com

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

عن أبي ذَرٍّ رضي اللهُ عنه:  أَنَّ ناساً من أَصْحابِ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قالوا لِلنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم: يا رسولَ اللهِ، ذَهَب أَهْلُ الدُّثورِ بالأُجورِ، يُصَلُّونَ كما نُصَلِّي، ويَصُومُونَ كما نَصُومُ، وَيَتَصَدَّقُونَ بِفُضُولِ أَمْوَالِهِمْ. قَالَ: ((أوَ لَيْسَ قَدْ جَعَلَ اللهُ لَكُمْ مَا تَصَدَّقُونَ ؟ إنَّ  بكلِّ تَسْبيحَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَكْبِيرَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَحْمِيدَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةً، وَأَمْرٍ بِالْمَعرُوفِ صَدَقَةً، وَنَهْيٍ عَنْ مُنْكَرٍ صَدَقَةً، وفي بُضْعِ أحَدِكُمْ صَدَقَةً)). قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، أَيَأْتي أحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أجرٌ ؟ قَالَ:

((أَرَأَيْتُمْ لَوْ وَضَعَها في حَرَامٍ، أَكَانَ عَليْهِ وزْرٌ ؟ فَكَذلِكَ إذَا وَضَعَها في الْحَلاَلِ كانَ لَهُ أَجْرٌ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ   

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Watu katika Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Ee Rasuli wa Allaah! Watu wenye mali wameondoka na thawabu nyingi; wanaswali kama tunavyoswali, na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa swadaqah kwa fadhila za mali zao. Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Je, kwani Allaah Hakukujaalieni njia ya kutolea swadaqah? Hakika kila (kutamka) Tasbiyh (Subhaana Allaah) ni swadaqah. Na kila Takbiyr (Allaahu Akbar) ni swadaqah. Na kila Tahmiyd (AlhamduliLLaah) ni swadaqah, na kila Tahliyl (Laa ilaaha illa Allaah) ni swadaqah. Na kuamarisha mema ni swadaqah. Na kukataza munkari ni swadaqah. Na mmoja wenu kujimai (na mkewe) ni swadaqah.”  Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah. Hivi mmoja wetu kujitoshelezea kwa shahawa yake atakuwa anapata thawabu? Akasema: “Mnaonaje kama atajitosheleza kwa njia ya haraam angelipata dhambi? Hivyo basi ikiwa atafanya kwa njia ya halaal, atapata thawabu.”  [Muslim]

 

 

 

 

    

 

Share

26-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Kila Kiungo Cha Mtu Lazima Kitolewe Swadaqah

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 26

 

كُلُّ سُلامَى مِنَ النَّاسِ عليه صَدَقَةٌ

 

Kila Kiungo Cha Mtu Lazima Kitolewe Swadaqah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أَبي هُرَيْرَةَ رَضي اللهُ عنه قال: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((كُلُّ سُلامَى مِنَ النَّاسِ عليه صَدَقَةٌ، كُلُّ يَوْمٍ تَطْلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ: تَعْدِلُ بَيْنَ اثْنَيْنِ صَدَقَةٌ، وتُعينُ الرَّجُلَ في دَابَّتِهِ فَتَحْمِلُهُ عَلَيْها أو تَرْفَعُ لهُ عَلَيْها متَاَعَهُ صَدَقَةٌ، والْكَلِمةُ الطَّيِّبةُ صَدَقَةٌ، وبكُلِّ خَطْوَةٍ تَمشِيها إلى الصَّلاةِ صَدَقَةٌ، وتُمِيطُ الأَذَى عنِ الطَّرِيِق صَدَقَةٌ)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ   

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kila kiungo cha mtu lazima akitolee swadaqah kila siku linapochomoza jua. Kufanya uadilifu baina ya wawili ni swadaqah. Kumsaidia mtu kupanda mnyama wake kwa kumsaidia  kumnyanyua  au kumnyanyulia  mizigo ni swadaqah. Neno zuri ni swadaqah. Na kila hatua unayotembea kuelekea Swalaah ni swadaqah, na kuondosha udhia katika njia ni swadaqah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share

27-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Wema Ni Katika Tabia Nzuri

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 27

 

الْبِرُّ حُسْنُ الْخُلُقِ

 

Wema Ni Katika Tabia Nzuri

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن النّوَّاسِ بْنِ سَمْعَانَ رضيَ اللهُ عَنْهُ عن النَّبي صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((الْبِرُّ حُسْنُ الْخُلُقِ، وَالإِثْمُ مَا حاكَ في نَفْسِكَ وَكَرِهْتَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِ النَّاسُ))  رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

 

وعن وَابصَةَ بْنِ مَعْبَدٍ رضي اللهُ عَنْهُ قالَ: أَتَيْت رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم فَقَالَ: ((جِئْتَ تَسأَلُ عَنِ الْبِرِّ؟)). قُلْتُ: نَعَمْ. قَالَ: ((اسْتَفْتِ قَلْبَكَ، الْبِرُّ مَا اطْمَأَنَّتْ إلَيْهِ النَّفْسُ وَاطْمَأَنَّ إلَيْهِ الْقَلْبُ، وَالإِثْمُ مَا حاكَ في النَّفْسِ وَتَردَّدَ في الصَّدْرِ وَإنْ أَفْتَاكَ النّاسُ وَأَفْتَوْكَ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَيْنَاهُ في مُسْنَدَي الْإِمَامَيْنِ أَحْمَدَ بْنِ حَنْبَلٍ وَالدَّارِمِيّ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ. 

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu An-Nawaas bin Sam-‘aan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wema ni tabia nzuri, na dhambi ni kile kinachositasita katika nafsi yako na unachukia watu kukitambua. [Muslim]

 

Na kutoka kwa Waaswibah bin Ma’bad (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilimwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Je, umekuja kuuliza kuhusu wema?” Nikasema: Ndio. Akasema:  Ushauri  moyo wako. Wema ni kile ambacho nafsi yako inatumainika kwacho na moyo wako pia unatumainika. Na dhambi ni kile kinachositasita katika nafsi na kifua kinataradadi japokuwa watu wamekariri kukupa shauri lao la kishariy'ah (kukipendelea).” [Hadiyth Hasan, imenukuliwa katika Musnad za Imaam wawili Ahmad bin Hanbal na Ad-Daarimiyy kwa isnaad Hasan]  

 

 

 

 

Share

28-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Nakuusieni Taqwa Ya Allaah Na Usikivu Na Utiifu

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 28

 

أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللهِ والسَّمْعِ والطَّاعَةِ

 

Nakuusieni Kumcha Allaah Na Usikivu Na Utiifu

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي نَجيحٍ الْعِرْباضِ بنِ سارِيَةَ رضي اللهِ عنه قال: وَعَظَنَا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنها الْقُلُوبُ، وذَرَفَتْ منها الْعُيُونُ، فَقُلْنا: يا رسول اللهِ، كأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ، فأَوْصِنا. قال: ((أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللهِ عَزَّ وَجَلَّ، والسَّمْعِ والطَّاعَةِ، وإن تَأَمَّرَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ، فإنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اخْتِلافاً كَثِيراً، فَعَليْكُمْ بِسُنَّتي وسُنَّةِ الخُلفَاءِ الرَّاشِدِينَ المَهْدِيِّينَ، عَضُّوا عَلَيْها بالنَّواجِذِ، وإيَّاكُمْ ومُحْدَثاتِ الأُمُورِ، فإنَّ كلَّ مُحْدَثَةٍ  بِدْعَةٌ وَ كُلَّ  بِدْعَةٍ ضَلاَلَةٌ  وَكُلَّ ضَلاَلَةٍ فِي النَّارِ))  رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ. 

Imepokelewa kutoka kwa Abu Najiyh Al-‘Irbaadhw bin Saariyah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitupa mawaidha mazito (yenye maana kubwa), nyoyo zikaogopa na macho yakabubujikwa machozi. Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Yanaonekana kama kwamba mawaidha ya kutuaga, basi tuusie.  Akasema: “Nakuusieni kuwa na taqwa ya Allaah na usikivu na utiifu japokuwa mtaongozwa na mtumwa. Hakika atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona ikhtilaaf nyingi. Kwa hiyo, shikamaneni na Sunnah zangu na mwenendo wa  Makhalifa waongofu, yashikilieni kwa magego (mambo yao). Na tahadharini na mambo yenye kuzushwa, kwani kila uzushi ni bid’ah, na kila bid-ah ni upotofu, na kila upotofu ni motoni.” [Abuu Daawuwd, AT-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

 

Share

29-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Muabudu Allaah Na Usimshirikishe Na Chochote

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 29

 

تَعْبُدُ اللهَ لا تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً

 

Muabudu Allaah Na Usimshirikishe Na Chochote

 

Alhidaaya.com

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

عن معاذِ بن جبلٍ رضي الله عنه قال: قلت: يا رسول الله، أخْبِرني بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجنَةَ ويُبَاعِدُني عَنِ النارِ. قال: ((لَقَدْ سألْتَ عَنْ عَظيمٍ، وإنَهُ لَيَسيرٌ عَلى من يَسَّرَهُ اللهُ تعالى عَلَيْهِ: تَعْبُدُ اللهَ لا تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً، وتُقيمُ الصَّلاةَ، وتُؤتي الزكاةَ، وتصومُ رمضانَ، وتَحُجُّ البيتَ))

ثم قال:  ((ألا أَدُلُّكَ على أبْوَابِ الخيرِ؟: الصَّومُ جُنَّةٌ، والصَّدقةُ تُطْفِىءُ الخَطِيئةَ كما يُطْفىءُ الماءُ النارَ، وصَلاةَ الرَّجُلِ في جَوْفِ الَّليْلِ، ثم تلا: ((تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنْ الْمَضَاجِعِ)) حتى بلغ : ((يَعْمَلُونَ))  السجدة: 16-17 .

ثم قال:  ((ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأمْرِ وَعَمودِهِ وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ؟)) قلتُ: بَلىَ يا رسول الله. قال:  ((رَأْسُ الأمْرِ الإسلامُ، وعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الجِهادُ))

ثم قال: ((ألا أخْبِرُكَ بِمِلاكَ ذَلِكَ  كلِّهِ ؟)) فَقُلْتُ بَلَى يا رَسول الله، فأخَذَ بِلِسانِهِ وقال: ((كُفَّ عَلَيْكَ هذا)) قلت: يا نبيَّ الله، وإنَّا لمؤاخَذُونَ بِما نَتَكَلَّمُ بِه ؟)) فقال: (( ثَكِلَتْكَ أمُّكَ يَا مُعَاذُ،  وَهَلْ يَكُبُّ الناسَ في النارِ على وُجُوهِهِمْ))  أو قال: ((على مناخِرِهِم - إلاَّ حَصَائدُ  ألسِنَتهم))  رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ   وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ. 

 

Imepokelewa kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah, nijulishe ‘amali itakayoniingiza Jannah na itanibaidisha na moto. Akasema: “Umeniuliza jambo kubwa mno nalo ni jepesi kwa ambaye Allaah Ta’aalaa Amemwepesishia.  Muabudu Allaah usimshirikishe na chochote, na usimamishe Swalaah, na utoe Zakkaah, na ufunge swawm Ramadhwaan, na uhiji Nyumba (Makkah).” 

 

Kisha akasema: “Je nikuelekeze milango ya kheri? Swawm ni ngao, na swadaqah inazima madhambi kama vile maji yanavyozima moto, na Swalaah ya mtu katika nyakati za usiku.” Kisha akasoma:

((تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنْ الْمَضَاجِعِ))

 

 

Mbavu zao zinatengana na vitandaa..”

 

mpaka akafikia:

((يَعْمَلُونَ))

 

“wakiyatenda” [As-Sajdah: 16-17]

 

Kisha akasema: “Je, nikujulishe  kilele cha hilo jambo na nguzo yake na sehemu yake ya juu kabisa?”  Nikasema: Ndio ee Rasuli wa Allaah! Akasema:  “Kilele chake ni Uislamu, nguzo yake ni Swalaah na sehemu yake ya juu kabisa ni jihaad.”

Kisha akasema: “Je, nikujulishe muhimili wa yote haya?”  Nikasema:  Ndio ee Rasuli wa Allaah!  Akaukamata ulimi wake na akasema: “Uzuie huu!” Nikasema: Ee Nabiy wa Allaah! Kwani hivi sisi tutahukumiwa yale tunayoyasema?  Akasema: “Akukose mama yako ee Mu'aadh! 

Kuna kitu zaidi kinachowaangusha watu kifudifudi motoni?” 

Au kasema: “Juu ya  pua zao – isipokuwa ni ni mavuno ya ndimi zao?” [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]

Maana ya:

ثَكِلَتْكَ أمُّكَ

“Akukose mama yako”: Ni Neno linalotamkwa na Waarabu katika hali ya kukemea bila ya kukusudiwa maana yake.

 

 

 

 

Share

30-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Allaah Amefaridhisha Mambo Ya Kuwajibika Basi Msiyapoteze

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 30

 

إنّ اللهَ تَعَالى فَرَضَ فَرَائِضَ فَلاَ تُضَيّعوها

 

Hakika Allaah Amefaridhisha Faraaidhw

 

(Mambo Ya Kuwajibika Katika Dini) Basi Msiyapoteze

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عَنْ أَبيِ ثَعْلَبَةَ الخُشَنِيِّ جُرْثُومِ بْن نَاشرٍ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنّ اللهَ تَعَالى فَرَضَ فَرَائِضَ فَلاَ تُضَيّعوهاَ وَحَدَّ حُدُودَاً فَلاتَعْتَدُوهَا وَحَرّمَ أَشْياءَ فَلاَتَنْتَهِكُوهَا وَسَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ رَحْمَةً لَكُمْ غَيْرَ نِسْيانٍ فَلا تَبْحَثُوا عَنْهَا)) حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ الدَّارَقُطْنِيّ وَغَيْرُهُ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Tha'alabah Al-Khushaniyy Jurthuwm bin Naashir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ”Hakika Allaah Amefaridhisha faraaidhw (Mambo ya kuwajibika katika Dini) hivyo msiyapoteze. Na Akaweka mipaka basi msiivuke. Na Ameharamisha mambo kwa hivyo msiyahalifu. Na Amenyamazia mambo kutokana na rahmah (Yake) kwenu wala hakusahau kwa hivyo msiyadadisi.”  [Hadiyth Hasan Ad-Daaraqutwniy na wengineo]

 

 

 

Share

31-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Ipe Mgongo Dunia Allaah Atakupenda

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 31

 

ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ

 

Ipe Mgongo Dunia Allaah Atakupenda

 

Alhidaaya.com

 

 

 Sikiliza Hadiyth:

 

 

عَنْ أَبِي العَبّاسِ سَهلِ بْن سَعْدٍ السّاعِدِيِّ رضي الله عنه  قَالَ : جَاءَ رَجُلُ إِلى النَبِي صلى الله عليه وسلم  فَقَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أَحَبَّنِي اللَّهُ وَأَحَبَّنِي النَّاسُ . فَقَالَ: (( ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبُّكَ النّاسُ)) رَوَاهُ ابْنُ مَاجَهْ  وَغَيْرُهُ بِأَسَانِيدَ حَسَنَةٍ. 

 

Imepokelewa kutoka kwa Sahl bin Sa'ad As-Saa’idiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: “Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Nijulishe ‘amali ambayo nikiifanya Allaah Atanipenda na watu pia watanipenda.  Akasema: “Ipe mgongo dunia Allaah Atakupenda, na vipe mgongo vilivyomo kwa watu, watu watakupenda.” [Ibn Maajah na wengineo kwa mtiririko mzuri wa isnaad]*

 

*Hata hivyo Wanavyuoni wa Hadiyth wameeleza kuwa Hadiyth hii ni dhaifu kutokana na udhaifu wa sanad yake japo An-Nawawiy kaitumia na kasema ina sanad nzuri.

 

 

 

 

Share

32-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Kusiwe Na Kudhuriana Wala Kulipizana Madhara

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 32

 

لاَ ضَرَرَ وَلاَ ضِرَارَ

 

Kusiwe Na Kudhuriana Wala Kulipizana Madhara

 

Alhidaaya.com

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عنْ أَبىِ سَعيدٍ سَعْدِ بْن مَالكِ بْن سِنَانٍ الْخُدريِّ رضي الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم  قَالَ :(( لاَ ضَرَرَ وَلاَ ضِرَارَ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ ابْنُ مَاجَهْ وَالدَّارَقُطْنِيّ، وَغَيْرُهُمَا مُسْنَدًا. وَرَوَاهُ مَالِكٌ فِي  الْمُوَطَّإِ مُرْسَلاً عَنْ عَمْرِو بْنِ يَحْيَى عَنْ أَبِيهِ عَنْ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  مُرْسَلًا، فَأَسْقَطَ أَبَا سَعِيدٍ، وَلَهُ طُرُقٌ يُقَوِّي بَعْضُهَا بَعْضًا. 

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Sa’d bin Maalik bin Sinaan Alkhudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kusiwe na kudhuriana wala kulipizana madhara.” [Imesimuliwa na Ibn Maajah, Ad-Daaraqutwniy na wengineo na ina kiwango cha 'Musnad'. Vile vile imesimuliwa na Maalik katika Al-Muwatwaa kama 'Mursal'. Inayo mtiririko wa mapokezi kutoka kwa 'Amr bin Yahyaa, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hata ukimuacha Abuu Sa'iyd bado inayo mtiririko wa mapokezi unayoiunga mkono.]

 

 

 

 

Share

33-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Jukumu La Ushahidi Liko Kwa Yule Anayedai Na Kula Kiapo Kunamuwajibikia Yule Anayekanusha

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 33

 

البَيِّنَةُ على المُدَّعِى والْيَمينُ على من أَنْكَرَ

 

Jukumu La Ushahidi Liko Kwa Yule Anayedai

 

Na Kula Kiapo Kunamuwajibikia Yule Anayekanusha

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن ابن عَبَّاسٍ رضي اللُه عنهما: أن رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قال: ((لَو يُعْطَى النَّاسُ بِدَعْوَاهُمْ لادَّعَى رِجَالٌ أموالَ قَوْمٍ ودِماءَهُمْ لَكِنِ البَيِّنَةُ على المُدَّعِى والْيَمينُ على من أَنْكَرَ))  حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ الْبَيْهَقِيّ وَغَيْرُهُ هَكَذَا، وَبَعْضُهُ فِي  الصَّحِيحَيْنِ

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kama watu wangelipewa kwa mujibu  wa madai yao, watu wangelidai mali na damu za wenzao (uhai) lakini jukumu la ushahidi liko kwa yule anayedai na kula kiapo kunawajibika kwa yule anayekanusha (kuwa hakutenda)”  [Al-Bayhaqiy na wengineo. Ni Hadiyth Hasan na baadhi yake imo katika Asw-Swahiyhayni]

 

 

 

Share

34-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Atakayeona Munkari Aondoe Kwa Mkono Wake

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 34

 

مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَراً فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ

 

Atakayeona Munkari Aondoe Kwa Mkono Wake

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي سعيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قال: سمعتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقوُل: ((مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَراً فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإنْ لمَ يَسْتَطِعْ فَبلِسانِهِ، فَإنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أضْعَفُ اْلإِيمَانِ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ  

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Atakayeona munkari basi aondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake (akataze), na ikiwa hawezi basi kwa moyo wake (achukie) na huo (yaani kutokukataza) ni udhaifu wa iymaan.”  [Muslim]

 

 

 

Share

35-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Msihusudiane Msizidishiane Bei Msibughudhiane

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 35

 

لا تَحَاسَدُوا، ولا تَنَاجَشُوا، ولا تَباغَضُوا

 

Msihusudiane Msizidishiane Bei Msibughudhiane

 

 

Alhidaaya.com

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أبي هُريرةَ رضي اللهُ عنه قال: قال رسوُل الله صلى الله عليه وسلم: ((لا تَحَاسَدُوا، ولا تَنَاجَشُوا، ولا تَباغَضُوا، ولا تَدَابَرُوا، ولا يَبعْ بَعْضُكُمْ على بَيْعِ بَعْضٍ، وكُونُوا عِبادَ اللهِ إخْوَاناً، المُسْلمُ أَخُو المُسْلمِ: لا يَظْلِمُهُ، وَلَا يَخْذُلُهُ، ولا يَكْذِبُهُ، ولا يَحْقِرُهُ، التَّقْوَى هاهُنا - ويُشِيرُ إلى صَدْرِه ثَلاثَ مَرَّاتٍ، بِحَسْبِ امْرِىءٍ مِنَ الشَّرِّ أن يَحْقِرَ أخاهُ المُسْلِمَ، كُلُّ المُسْلِمِ على الْمسْلِم حَرَامٌ: دَمُهُ ومالُهُ وعِرْضُهُ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ  

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Msihusudiane, wala msizidishiane bei (biashara), wala msibughudhiane, wala msitengane, wala msishindane kwa kupunguza bei.  Lakini enyi waja wa Allaah kuweni ndugu. Muislamu ni ndugu wa Muislamu mwenzake, hamdhulumu wala hamtelekezi, wala hamuongopei, wala hamdharau.  Taqwa iko hapa.” (huku akiashiria kifuani kwake kwa vidole vyake) mara tatu. “Ni uovu wa kutosha kwa mtu kumdharau ndugu yake Muislamu. Muislamu ameharamishiwa kwa Muislamu mwenzake: damu yake, mali yake na heshima yake.” [Muslim]

 

 

Share

36-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Atakayemuondoshea Muumini Dhiki Za Dunia, Allaah Atamuondoshea Dhiki Katika Dhiki Za Siku Ya Qiyaamah

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 36

 

مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيا نَفَّسَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً من كُرَبِ يوْمِ القيامَةِ

 

Atakayemuondoshea Muumini Dhiki Za Dunia,

Allaah Atamuondoshea Dhiki Katika Dhiki Za Siku Ya Qiyaamah

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

عن أبي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه، عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قال: ((مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيا نَفَّسَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً من كُرَبِ يوْمِ القيامَةِ، ومَنْ يَسَّرَ على مُعْسِرٍ يَسَّرَ اللهُ عليه في الدنْيا والآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ الله في الدُّنْيا والآخِرَةِ  واللهُ في عَوْنِ الْعَبْدِ ما كانَ الْعَبْدُ في عَونِ أخيهِ. ومَنْ سلك طَريقاً يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْماً سَهَّلَ اللهُ له بِهِ طَرِيقاً إلى الجنَّةِ.

وَمَا اجتَمَعَ قَوْمٌ في بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ ويَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ، إلا نَزَلَتْ عليهمُ السَّكِينَةُ، وغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وحَفَّتهُمُ المَلائِكَةُ، وذَكَرَهُمُ اللهُ فيمَنْ عِنْدَه. وَمَنْ بَطَّأ بِه عَمَلُهُ لمْ يُسْرِعْ به نَسَبُهُ))  رَوَاهُ مُسْلِمٌ بهذا اللفظ

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayemuondoshea Muumini dhiki katika dhiki za dunia, Allaah Atamuondoshea dhiki katika dhiki za Siku ya Qiyaamah. Na Atakayemsahilishia mwenye ugumu wa jambo, Allaah Atamsahilishia duniani na Aakhirah. Na Atakayemsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri duniani na Aakhirah. Na Allaah Humsaidia mja madamu mja yuko katika kumsaidia nduguye. Na Atakayetafuta njia ya kujipatia elimu, Allaah Atamsahilishia njia ya Jannah.

 

Na hawajumuiki watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma Kitabu cha Allaah na wakasomeshana baina yao ila watateremkiwa na sakiynah (utulivu) na itawafunika rahmah, na Malaika watawazunguka, na Allaah Atawataja kwa walio Naye.  Yeyote yule anayeakhirishwa na ‘amali zake (kwenda Jannah) hatoharakishwa na nasaba yake.” [Muslim kwa tamshi hili]

 

 

 

 

Share

37-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Hakika Allaah Kaandika Hasanaat Na Maovu

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 37

 

إِنَّ الله كَتَبَ الحَسَنَاتِ وَالسَّيئَاتِ

 

Hakika Allaah Kaandika Hasanaat Na Maovu

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

'

 

 

عَن ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا عَنِ النبي صلى الله عليه وسلم فِيْمَا يَرْوِيْهِ عَنْ رَبِّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالى أَنَّهُ قَالَ: (إِنَّ الله كَتَبَ الحَسَنَاتِ وَالسَّيئَاتِ ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ؛ فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إِلَى سَبْعِمائَةِ ضِعْفٍ إِلىَ أَضْعَاف كَثِيْرَةٍ. وَإِنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً،وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً)) رَوَاهُ البُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ في صَحِيْحَيْهِمَا بِهَذِهِ الحُرُوْفِ

 

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kutokana na yale aliyoyapokea kwa Rabb wake Tabaaraka Wa Ta’aalaa kwamba amesema: “Hakika Allaah Ameandika hasanaat (mazuri) na maovu kisha Akayabainisha. Basi atakayetilia hima kufanya hasanah (zuri) moja, kisha asiweze kuifanya, basi Allaah Atamwandikia (thawabu za) hasanah moja kamilifu. Na ikiwa ametilia hima kuifanya kisha akaifanya, basi Allaah Atamwandikia hasanaat kumi hadi mara mia saba maradufu zaidi ya hayo. Na akitilia hima kufanya ovu moja kisha asifanye, basi Allaah Atamuandikia hasanah moja kamilifu. Na ikiwa akitilia hima akalifanya, basi Allaah Atamuandikia ovu moja.” [Al-Bukhaariy na Muslim kwa matamshi hayo]

 

 

 

 

Share

38-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Atakayemfanyia Uadui Kipenzi Changu Ninatangaza Vita Dhidi Yake

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 38

 

مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ

 

Atakayemfanyia Uadui Kipenzi Changu Ninatangaza Vita Dhidi Yake

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ قَال:َ مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ،  وَمَا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنْ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ)) البخاري

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: “Atakayemfanyia uadui kipenzi changu Ninatangaza vita dhidi yake. Mja Wangu hanikaribii na kitu chochote Ninachokipenda kama ‘amali nilizomfaridhishia. Na mja Wangu huzidi kunikaribia kwa ‘amali za Sunnah ili nimpende. Ninapompenda, huwa masikio yake yanayosikilizia, macho yake anayoonea, mikono yake anayonyoshea, miguu yake anayotembelea nayo, lau angeniomba kitu bila shaka ningempa, lau angeniomba himaya bila shaka ningelimkinga.” [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 

Share

39-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Allaah Amesamehe Kwa Ajili Yangu Ummah Wangu Kukosea Na Kusahau

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 39

 

إنَّ الله تَجاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتي الْخَطَأَ والنِّسْياَنَ

 

Allaah Amesamehe Kwa Ajili Yangu Ummah Wangu Kukosea Na Kusahau

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

عَن ابْنِ عَبَّاسِ رَضِيَ الله عَنْهُما: أن رَسُوَل اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّ الله تَجاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتي: الْخَطَأَ، والنِّسْياَنَ، وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ ابْنُ مَاجَهْ وَالْبَيْهَقِيّ وَغيرهما 

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Amewasamehe (au ameachilia mbali kuwatia hesabuni) kwa ajili yangu ummah wangu kwa kukosea, kusahau, na yale wanayoyafanya kwa kulazimishwa kwa nguvu.” [Ibn Maajah, Al-Bayhaqiy na wasiokuwa hao wawili]

 

 

 

 

Share

40-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Kuwa Duniani Kama Vile Mgeni Au Mpita Njia

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 40

 

كُنْ في الدُّنْيا كأنَّكَ غَرِيبٌ أو عابرُ سبِيلٍ

 

Kuwa Duniani Kama Vile Mgeni Au Mpita Njia

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

عن ابنِ عُمَرَ رضي اللهُ عنهما قال: أَخَذَ رسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم بِمَنْكِبيَّ فقال: ((كُنْ في الدُّنْيا كأنَّكَ غَرِيبٌ، أو عابرُ سبِيلٍ))

 

وكانَ ابنُ عُمَرَ رَضي اللهُ عنهما يقولُ: إذا أمْسَيْتَ فلا تَنْتظِرِ الصبَّاحَ، وإذا أصْبَحْتَ فلا تَنْتَظِرِ الَمسَاءَ، وخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرضِكَ، ومِنْ حَياتِكَ لِمَوْتِكَ. رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ    

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alinishika bega akasema: “Kuwa (ishi) duniani kama vile mgeni au mpita njia.”

 

Na Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) alikuwa akisema: Utakapoamka basi usingojee (kutegemea kuishi mpaka) asubuhi. Na utakapoamka asubuhi basi usingojee (kutegemea kuishi mpaka) jioni. Na chukua (mafao ya) siha yako kwa maradhi yako, na (mafao ya) uhai wao kwa mauti yako.  [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share

41-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Hatoamini Mmoja Wenu Mpaka Matamanio Yake Yatakapomili Yale Niliyokuja Nayo

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

 

Hadiyth Ya 41

 

لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعَاً لِمَا جِئْتُ بِهِ

 

Hatoamini Mmoja Wenu Mpaka Matamanio Yake Yatakapomili Yale Niliyokuja Nayo

 

Alhidaaya.com

 

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عَنْ أَبِي مُحَمَّدٍ عَبْدِ اللَّهِ بِنْ عَمْرُو بِنْ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم: ((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعَاً لِمَا جِئْتُ بِهِ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ، رَوَيْنَاهُ فِي كِتَابِ  الْحُجَّةِ  بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ.

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muhammad ‘Abdillaah bin ‘Amru bin Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hatoamini mmoja wenu mpaka hawaa (matamanio) zake yatakapomili kutii yale niliyokuja nayo.” [Hadiyth Hasan Swahiyh, katika Kitabu “Al-Hujjah” kwa Isnaad Swahiyh]

 

 

 

Share

42-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Ee Bin Aadam! Madamu Utaniomba Na Kutaraji Kwangu Nitakughufuria

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 42

 

يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ

 

Ee Bin Aadam! Madamu Utaniomba

Na Kutaraji Kwangu Nitakughufuria

 

Alhidaaya.com

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

عن أنس رضي الله عنه  قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم   يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ مِنْكَ وَلاَ أُبَالِي. يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ . يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لاَ تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لاَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً)) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah Ta’aalaa Amesema: Ee bin-Aadam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakughufuria yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee bin-Aadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfirah, Ningekughufuria (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee bin-Aadam! Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na maghfirah yanayolinga nayo.” [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

 

 

 

 

 

Share