14-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Al-Hadhwaanah Malezi

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلنِّكَاحِ

Kitabu cha Nikaah (Ndoa)

 

 

بَابُ اَلْحَضَانَةِ

14-Mlango Wa Al-Hadhwaanah Malezi[1]

 

 

 

 

 

986.

 

عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِوٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ اِمْرَأَةً قَالَتْ: {يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنَّ اِبْنِي هَذَا كَانَ بَطْنِي لَهُ وِعَاءً، وَثَدْيِي لَهُ سِقَاءً، وَحِجْرِي لَهُ حِوَاءً، وَإِنَّ أَبَاهُ طَلَّقَنِي، وَأَرَادَ أَنْ يَنْتَزِعَهُ مِنِّي. فَقَالَ لَهَا رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  "أَنْتِ أَحَقُّ بِهِ، مَا لَمْ تَنْكِحِي".}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa ‘Abdillaah bin ‘Amr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: Mwanamke mmoja alikuja akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Kwa hakika mwanangu huyu tumbo langu lilikuwa ndio mfuko wake, ziwa langu lilikuwa ni kiriba chake cha maji, na paja langu lilikuwa kitanda chake. Baba yake alinitaliki na anataka kunipokonya mtoto huyu!” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Wewe una haki zaidi kwake maadamu hujaolewa.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

987.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ اِمْرَأَةً قَالَتْ: {يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنَّ زَوْجِي يُرِيدُ أَنْ يَذْهَبَ بِابْنِي، وَقَدْ نَفَعَنِي، وَسَقَانِي مِنْ بِئْرِ أَبِي عِنَبَةَ  فَجَاءَ زَوْجُهَا، فَقَالَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  "يَا غُلَامُ! هَذَا أَبُوكَ وَهَذِهِ  أُمُّكَ، فَخُذْ بِيَدِ أَيُّهُمَا شِئْتَ" فَأَخَذَ بِيَدِ أُمِّهِ، فَانْطَلَقَتْ بِهِ.}  رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Mwanamke mmoja alikuja akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Mume wangu anataka kumchukua mwanangu na ananisaidia kuchotea maji katika kisima cha Abiy ‘Inabah, mumewe akaja, akasema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kumuambia yule kijana: “Ee mtoto, huyu ni baba yako na huyu ni mama yako, mshike mkono umtakae.”[2] Yule kijana akashika mkono wa mama yake na akaondoka naye.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha At-Tirmidhiy]

 

 

 

988.

وَعَنْ رَافِعِ بْنِ سِنَانٍ، {أَنَّهُ أَسْلَمَ، وَأَبَتِ اِمْرَأَتُهُ أَنْ تُسْلِمَ. فَأَقْعَدَ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  اَلْأُمَّ نَاحِيَةً، وَالْأَبَ نَاحِيَةً، وَأَقْعَدَ اَلصَّبِيَّ بَيْنَهُمَا. فَمَالَ إِلَى أُمِّهِ، فَقَالَ: "اَللَّهُمَّ اِهْدِهِ". فَمَالَ إِلَى أَبِيهِ، فَأَخَذَهُ.} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَالْحَاكِمُ

Kutoka kwa Raafi’ bin Sinaan[3] amesema kuwa: Yeye alisilimu, na mkewe akakataa kusilimu. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamkalisha mama upande mmoja na baba upande mwingine, na akamkalisha mtoto katikati yao, yule mtoto akawa ameegemea upande wa mama yake, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaomba: “Ee Allaah! Muongoze (mtoto huyu).” Yule mtoto akaegemea upande wa baba yake akamchukua.[4] [Imetolewa na Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Al-Haakim]

 

 

 

 

989.

وَعَنْ اَلْبَرَاءِ بْنِ عَازِبِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَضَى فِي اِبْنَةِ حَمْزَةَ لِخَالَتِهَا، وَقَالَ: اَلْخَالَةُ بِمَنْزِلَةِ اَلْأُمِّ.}  أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ

وَأَخْرَجَهُ أَحْمَدُ: مِنْ حَدِيثِ عَلَيٍّ فَقَالَ: {وَالْجَارِيَةُ عِنْدَ خَالَتِهَا، فَإِنَّ اَلْخَالَةَ وَالِدَةٌ}

Kutoka kwa Al-Baraai bin ‘Aazib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alihukumu kuhusu binti wa Hamza kwa mama yake mdogo na akasema: “Mama mdogo ni katika daraja yake mama.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

Na kutoka kwa Ahmad ameipokea hadiyth ya ‘Aliy alisema: “Binti mdogo anafaa kulelewa na mama yake mdogo kwani mama mdogo ni mama.”

 

 

 

990.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {إِذَا أَتَى أَحَدَكُمْ خَادِمُهُ بِطَعَامِهِ، فَإِنْ لَمْ يُجْلِسْهُ مَعَهُ، فَلْيُنَاوِلْهُ لُقْمَةً أَوْ لُقْمَتَيْنِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu atakapoletewa chakula na mtumishi wake iwapo hakumkalisha ale pamoja naye basi ampe tonge moja au matonge mawili.”[5] [Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Bukhaariy]

 

 

 

991.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {عُذِّبَتْ اِمْرَأَةٌ فِي هِرَّةٍ سَجَنَتْهَا حَتَّى مَاتَتْ، فَدَخَلْتِ اَلنَّارَ فِيهَا، لَا هِيَ أَطْعَمَتْهَا وَسَقَتْهَا إِذْ هِيَ حَبَسَتْهَا، وَلَا هِيَ تَرَكَتْهَا، تَأْكُلُ مِنْ خَشَاشِ اَلْأَرْضِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwanamke kaadhibiwa kwa sababu ya paka, alimfunga hadi akafa, akaingizwa motoni kwa ajili ya paka. Hakumlisha wala hakumpa maji, wala hakumuacha ale vidudu vya ardhini.” [Bukhaariy, Muslim]

 

[1] Al-Hadhwaanah kwa lugha ya kiarabu ina maana ya kuhifadhi na kulinda. Kulingana na Istilahi ya kishariy’ah ina maana ya malezi na maangalizi anayopewa mtoto. Ikiwa mtu kamuacha mkewe na wote ni Waislamu na wana watoto, katika hali hii mwanamke huwa ana haki zaidi ya malezi ya mtoto. Mwanamme hawezi kuwachukua na kuwaweka mbali na mama yao kwa nguvu. Ikiwa mtoto au watoto wapo katika hatua ya kunyonyeshwa ni haki ya baba kumgharimia mahitaji na matumizi ya yule mtoto kwa muda wote akiwa ni mtoto anayenyonya. Mtoto ataendelea kuhudumiwa na baba yake ikiwa anakaa naye au anakaa na mama yake. Akiwa anakaa na mama yake itaendelea kuwa hivyo maadamu mama yule atakuwa hajaolewa tena hadi atakapofikia baleghe. Ikiwa mama kaolewa ulezi wa mtoto utahamia kwa baba yake. Kulingana na madhehebu ya Hanafi ni kuwa, atakapoolewa na jamaa wa mtoto, malezi na uangalizi wake utabaki kwa mama yake.

 

[2] Hadiyth iliyotangulia, mama ametangulizwa zaidi kwa ulezi wa mwanawe, wakati katika Hadiyth hii mwana anapewa uhuru wa kuchagua baina ya wazazi wake wawili. Sababu ni kuwa katika Hadiyth hii mtoto ameshakuwa mkubwa na mwenye uwezo zaidi wa kuchagua wapi pa kumfaa zaidi. Kwa hali hii tunajifunza kuwa mtoto anapokuwa ameshakuwa na hana haja ya ulezi na ulinzi wa wazazi wake ana khiyari ya kuchagua pa kuenda kati ya kwa baba na kwa mama.

 

[3] Huyu ni Abul-Hakam Al-Answaar Al-Madaniy ambaye alikuwa Swahaba, Abul-Qaasim bin Salam amesema katika Al-Answaab kuwa walikuwa ni kizazi cha Al-‘Atbun ambaye ni ‘Aamir bin Tha’alabah.

 

[4] Hadiyth hii inathibitisha kuwa hata ikiwa mama ni kafiri hakumnyima haki ya mwanawe, ikiwa mtoto keshapambanukiwa, hatoendelea kukaa nae.

 

[5] Hadiyth hii inatuhimiza kuwa bwana mwenye nyumba ampe mfanyakazi wake chakula.

 

 

Share