08-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akihisi Damu Au Maumivu Ya Hedhi Lakini Haikutoka Kabla Ya Magharibi Je, Swawm Itasihi?

 

08-Akihisi Damu Au Maumivu Ya Hedhi Lakini Haikutoka Kabla Ya Magharibi

Je, Swawm Yake Itasihi?

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Mwanamke akihisi damu na haikutoka kabla ya Magharibi au maumivu ya ada yake je, Swawm yake itasihi au itampasa alipe siku hiyo?

 

JIBU:

 

Mwanamke mwenye tohara akihisi damu hali ya kuwa yuko katika Swawm lakini damu yenyewe haikutoka ila baada ya kuzama jua (Magharibi) basi Swawm yake ni sahihi na hawajibishwi kuirejea ikiwa ni Swawm ya fardhi. Kadhalika haibatilishi thawabu yake ikiwa ni Swawm ya Sunnah.

 

 

Share