imaam Al-Muzniy: Khofu Ya Imaam Ash-Shaafi’iyy Alipokuwa Katika Maradhi Aliyofia

 

Khofu Ya  Imaam Ash-Shaafi’iyy Alipokuwa Katika Maradhi Aliyofia

 

Imaam Al-Muzniy (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Imaam Al-Muzniy (Rahimahu-Allaah) amesema:  “Niliingia kwa  Ash-Shaafi’iyy katika maradhi yake aliyofia nikamwambia: Ee Abaa Abdillaah umeamkaje?” Akanyanyua kichwa chake na kusema: “Nimepambazukiwa kuondoka duniani na kufarikiana na ndugu zangu, na amali zangu mbaya kukutana nazo, na kwa Allaah nitafikia; Sijui roho yangu itakwenda Jannah (Peponi) niipongeze au motoni niipe rambirambi kwa msiba.” Kisha baada ya hapo akalia. [Siyar A’laam An-Nubalaa 10/76]

Share