16-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Alipomalizia Hedhi Kabla Ya Adhuhuri Hakuona Damu Je Afunge Siku Hiyo?

 

16-Alipomalizia Hedhi Kabla Ya Adhuhuri Hakuona Damu Je Afunge Siku Hiyo?

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Katika siku za mwisho za hedhi na kabla ya Swalaah ya Adhuhuri mwanamke hakuona athari yoyote ya damu je afunge siku ya leo ihali hakuona Qiswat baydhwaa (maji maji meupe ambayo ni dalili ya utohara yanayokuja baada ya kukatika damu) au afanye nini?

 

 

JIBU:

 

 

Ikiwa ni katika ada yake sio kuona Qiswat baydhwaa kama ilivyo kwa baadhi ya wanawake basi na afunge. Na ikiwa ni miongoni mwa ada yake kuona Qiswat baydhwaa basi asifunge hadi aone Qiswat baydhwaa.

 

 

 

 

Share