26-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Wanawake Bora Kuswali Nyumbani Au Miskitini Katika Nyusiku Za Ramadhwaan Kufaidika Na Mawaidha?

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

26-Wanawake Bora Kuswali Nyumbani Au Miskitini

Katika Nyusiku Za Ramadhwaan Kufaidika Na Mawaidha?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Lipi bora kwa mwanamke; kuswali usiku nyumbani kwake wakati wa Ramadhwaan au kuswali Msikitini na haswa ikiwa kuna mawaidha na kukumbushwa kuhusu Dini.  Na nini maelekezo yako kwa wanawake wanaoswali Misikitini?

 

JIBU:

 

Bora zaidi ni kuswali nyumbani kwa ujumla wa kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 وبيوتهن خير لهن

“Na nyumbani kwao ni bora zaidi.”

 

Na mwanamke kutoka nyumbani kwake wakati mwingine hasalimiki kwa fitnah. Hivyo mwanamke kubaki nyumbani mwake ni bora zaidi kwake kuliko kwenda Msikitini  kuswali. Ama Hadiyth na mawaidha mbali mbali anaweza kuyapata kwa njia ya kanda mbali mbali.

 

Ama maelekezo yangu kwa wale wanaokwenda kuswali Misikitini ni kuwa watoke majumbani mwao bila ya kujipamba na wasipake uturi.

 

 

 

 

Share