29-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ameharibu Mimba Mwaka Jana Akiwa Na Miezi Mitatu Hakuswali Mpaka Alipotoharika Je Alipaswa Kuswali Na Kama Hakujua Idadi Ya Siku Afanyeje?

 

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

29-Ameharibu Mimba  Mwaka Jana Akiwa Na Miezi Mitatu Hakuswali Mpaka Alipotoharika Je Alipaswa Kuswali Na Kama Hakujua Idadi Ya Siku Afanyeje?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Mimi ni mwanamke ambaye nimetoa mimba katika mwezi wa tatu yapata mwaka hivi, na sikuanza kuswali hadi nilipotoharika na niliambiwa kuwa ilikuwa juu yako kuswali. Je nifanye nini nami sijui idadi za siku haswa?

 

 

JIBU:

 

Kinachojulika kwa ‘Ulamaa ni kuwa mwanamke akiangusha mimba baada ya  miezi mitatu basi haswali; kwa kuwa mwanamke akidondosha mimba basi imeshabainika kuwa kichanga kimeshaumbwa kwani damu ambayo inatoka itakuwa ni damu ya nifaas, kwa hiyo hatakiwi kuswali.  ‘Ulamaa wamesema: “Inayumkinika kubaini uumbwaji wa kichanga ikitimia siku themanini na moja.”  Na hizi ni chini ya miezi mitatu.  Kwa hiyo akiwa na yakini kuwa  kichanga kimedondoka baada ya miezi mitatu,  basi ambayo itakuwa imemsibu itakuwa ni damu chafu. Lakini ikiwa kabla ya siku themanini, basi damu itakuwa ni kwa ajili ya ugonjwa na haachi kuswali.  Na huyu muulizaji akumbuke kuwa kama kichanga kimedondoka kabla ya siku themanini  basi itabidi alipe Swalaah na kama hajui ni ngapi ameacha basi na akadirie na alipe anayodhania hakuswali ndani yake.

 

Share