34-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwenye Hedhi Kuweko Msikitini Kwa Ajili Ya Kusikiliza Hadiyth Na Khutbah

 

 Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

34-Mwenye Hedhi Kuweko Msikitini Kwa Ajili Ya Kusikiliza Hadiyth Na Khutbah

  

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Nini hukumu ya kuwepo mwanamke katika Masjid Al-Harama naye ni mwenye hedhi kwa ajili ya kusikiliza khutbah au Hadiyth?  

 

 

JIBU:

 

Haijuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kukaa Masjid Al-Haraam au katika Msikiti mwingine wowote, bali inapasa kupita Msikitini na kuchukua haja yake  na mfano wake kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  kumwambia ‘Aaishah alipomwambia alete kilemba naye ‘Aaishah akasema: “Kipo Msikitini nami ni mwenye hedhi.” Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akasema: “Hedhi yako haipo mikononi mwako.”

 

Ikiwa mwenye hedhi atapita Msikitini na akaaminisha kutokuteremka kwa damu ya hedhi pale Msikitini sio tatizo.

 

Ama akitaka kuingia na kukaa, basi hii haijuzu,  na dalili juu ya hilo ni kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alipowaamrisha wanawake watoke kwenda kwenye Mswalla wa ‘Iyd isipokuwa wenye hedhi waliambiwa wasikae kwenye Muswalla.

 

Hii ni dalili kuwa mwenye hedhi hatakiwa kukaa Msikitini kwa kusikiliza khutbah  au darsa au Hadiyth.

 

 

Share