48-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Imemtokea Hedhi Akiwa Katika Twawaaf Amekamilisha Kwa Ajili Ya Kusitahi Akarudi Nchini Kwake

 

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

48-Imemtokea Hedhi Akiwa Katika Twawaaf

Amekamilisha Kwa Ajili Ya Kusitahi Akarudi Nchini Kwake

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Mwanamke amesafiri kwenda Hajj ikamjia ada yake ya mwezi  siku tano tokea aanze safari yake na baada ya kufika kwake Miyqaat alikoga na kuingia katika ihraam yake hali ya kua hajatwaharika na ada yake. Pindi alipofika Makkah alibaki nje ya Haram (Masjid Al-Haraam) na hakufanya chochote kwenye ‘ibaadah ya Hajj wala ya ‘Umrah. Alikaa siku mbili Minaa kisha akatoharika na kukoga na kufanya ‘ibaadah zote za ‘Umrah akiwa ametoharika kisha damu ikamrejea akiwa katika Twawaaf Al-Ifaadhwah ya Hajj. Akaendelea kwa sababu alistahi (kusema) hivyo akakamilisha ‘ibaadah zote za Hajj bila kumwambia kiongozi wake isipokuwa alimjulisha hayo baada ya kurudi nchini mwao nini hukumu yake?

 

 

JIBU:

 

 

Hukumu yake ilikuwa damu iliyomtokea katika Twawaaf Al-Ifaadhwah ikiwa damu hiyo ya hedhi ambayo unaijua kwa tabia yake na maumivu yake basi Twawaaf Al-Ifaadhwah itakuwa haijaswihi na itamlazimu kurudi Makkah kufanya  Twawaaf Al-Ifaadhwah  na atahirimia kwa ajili ya ‘Umrah katika Miyqaat na kufanya ‘Umrah kwa kutufu na kufanya Sa’y na kupunguza nywele kisha hapo atafanya Twawaaf Al-Ifaadhwah.  Ama damu hii ikiwa siyo ya hedhi kwa wasifu ule tuliyoutaja mwanzoni (tabia yake na maumivu yake, rangi na kadhaalika) basi itakuwa ima imetokea kwa ajili ya msongamano au wasiwasi, khofu au unao fanana na hiyo,  basi Twawaaf yake inaswihi kwa yule ambaye hashurutishwi kufanya tohara kwa ajili ya Twawaaf. Na kama hawezi kurudi kama tulivyozungumza awali kwa sababu anakaa nchi ya mbali basi Hijjah yake inaswihi.

 

Share