045-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwazuru Watu wa Kheri, Kukaa Nao, Kuhusubiana Nao na Kuwapenda

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب زيارة أهل الخير ومجالستهم وصحبتهم ومحبتهم وطلب زيارتهم والدعاء منهم وزيارة المواضع الفاضلة

045-Mlango Wa Kuwazuru Watu wa Kheri, Kukaa Nao, Kuhusubiana Nao na Kuwapenda

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَاهُ لَا أَبْرَحُ حَتَّىٰ أَبْلُغَ مَجْمَعَ الْبَحْرَيْنِ أَوْ أَمْضِيَ حُقُبًا ﴿٦٠﴾ إِلَى قوله تَعَالَى : قَالَ لَهُ مُوسَىٰ هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا ﴿٦٦﴾

Na pindi Muwsaa alipomwambia kijana wake: Sitoacha kuendelea mpaka nifikie zinapokutana bahari mbili, na nitaendelea muda mrefu. Hadi Kauli Yake T'aalaa: ...Basi walipofika zinapoungana bahari mbili, walimsahau samaki wao; naye akachukua njia yake baharini akiponyoka chini kwa chini. [Al-Kahf: 60-66]

 

وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ  ﴿٢٨﴾

Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka Wajihi Wake. [Al-Kahf: 28]

 

 

 

Hadiyth – 1

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ أَبُو بكر لِعُمَرَ رضي الله عنهما بَعْدَ وَفَاةِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم: انْطَلِقْ بِنَا إِلَى أُمِّ أيْمَنَ رضي الله عنها نَزُورُهَا كَمَا كَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَزُورُهَا ، فَلَمَّا انْتَهَيَا إِلَيْهَا ، بَكَتْ ، فَقَالاَ لَهَا : مَا يُبْكِيكِ ؟ أمَا تَعْلَمِينَ أنَّ مَا عِنْدَ اللهِ خَيْرٌ لرَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَتْ : مَا أبْكِي أَنْ لاَ أَكُونَ أَعْلَم أنَّ مَا عِنْدَ الله تَعَالَى خَيْرٌ لرسول الله صلى الله عليه وسلم، ولَكِنْ أبكي أنَّ الوَحْيَ قدِ انْقَطَعَ مِنَ السَّماءِ ، فَهَيَّجَتْهُمَا عَلَى البُكَاءِ ، فَجَعَلا يَبْكِيَانِ مَعَهَا . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Abu Bakr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) alimwambia 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) baada ya kuanga dunia kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Twende tukamzuru Ummu Ayman (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) kama alivyokuwa akimzuru Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." Walipofika kwake akalia. Wakamwambia: "Nini kinachokuliza? "Kwani hujui Allaah Aliyomwandalia Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni bora?" Akasema: "Mimi nami silii kwa kuwa sijui yalio kwa Allaah ni bora kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), bali nalia kwa sababu wahyi umekatika toka mbinguni." Wakawa wanalia pamoja naye." [Muslim]

 

 

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم: (( أنَّ رَجُلاً زَارَ أَخَاً لَهُ في قَريَة أُخْرَى ، فَأرْصَدَ الله تَعَالَى عَلَى مَدْرَجَتِهِ مَلَكاً ، فَلَمَّا أتَى عَلَيهِ ، قَالَ : أيْنَ تُريدُ ؟ قَالَ : أُريدُ أخاً لي في هذِهِ القَريَةِ . قَالَ : هَلْ لَكَ عَلَيهِ مِنْ نِعْمَة تَرُبُّهَا عَلَيهِ ؟   قَالَ : لا ، غَيْرَ أنِّي أحْبَبْتُهُ في الله تَعَالَى ، قَالَ : فإنِّي رَسُول الله إلَيْكَ بَأنَّ الله قَدْ أَحَبَّكَ كَمَا أحْبَبْتَهُ فِيهِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: " Mtu mmoja alimzuru nduguye katika kijiji kingine. Allaah akamwakilishia Malaika njiani. Alipomfikia alisema: "Unaelekea wapi?" Akasema: "Namtaka ndugu yangu katika kijiji hiki." Akasema: "Una neema yeyote unaipata kwake?" Akasema: "La, isipokuwa mimi nampenda kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa)." Akasema: "Mimi ni mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwako; kuwa Allaah anakupenda kama ulivyompenda ndugu yako kwa ajili Yake." [Muslim]

 

 

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ عَادَ مَرِيضاً أَوْ زَارَ أخاً لَهُ في الله ، نَادَاهُ مُنَادٍ : بِأنْ طِبْتَ ، وَطَابَ مَمْشَاكَ ، وَتَبَوَّأتَ مِنَ الجَنَّةِ مَنْزِلاً )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) ، وفي بعض النسخ : (( غريب )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote mwenye kumtembelea mgonjwa au akamzuru ndugu yake kwa ajili ya Allaah, anaita mwenye kuita: Uwe na furaha, na kwenda kwako kubarikiwe na utunukiwe cheo Peponi." [At-Tirmidhy], ambaye amesema hii ni Hadiyth Hassan, na katika baadhi ya nuskha ni Hadiyth Ghariib (Ngeni)

 

 

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِنَّمَا مَثلُ الجَلِيسِ الصَّالِحِ وَجَلِيسِ السُّوءِ ، كَحَامِلِ المِسْكِ ، وَنَافِخِ الْكِيرِ ، فَحَامِلُ الْمِسْكِ : إمَّا أنْ يُحْذِيَكَ ، وَإمَّا أنْ تَبْتَاعَ مِنْهُ ، وَإمَّا أنْ تَجِدَ مِنْهُ ريحاً طَيِّبَةً ، وَنَافِخُ الكِيرِ : إمَّا أنْ يُحْرِقَ ثِيَابَكَ ، وَإمَّا أنْ تَجِدَ مِنْهُ رِيحاً مُنْتِنَةً )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika mfano wa kikao kizuri na kikao kiovu ni kama mfano wa mchukuaji (mwuzaji) manukato na mfuaji vyuma. Ama mbebaji manukato ima atakupatia (hidaya) au utanunua kutoka kwake au utapata harufu nzuri. Na kwa mfuaji chuma, ima atakuunguzia nguo yako au utapata harufu mbaya kutoka kwake." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( تُنْكَحُ المَرْأَةُ لأَرْبَعٍ : لِمَالِهَا ، وَلِحَسَبِهَا ، وَلِجَمَالِهَا ، وَلِدِينِهَا ، فَاظْفَرْ بِذاتِ الدِّينِ تَربَتْ يَدَاك )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke huolewa kwa sababu nne: Mali yake, nasaba yake, uzuri wake na Dini yake. Tafuta yule mwenye Dini, isije ikafukarika mikono yako (yaani ili upate kubarikiwa)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Hadiyth – 6

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم لِجبريل : (( مَا يَمْنَعُكَ أنْ تَزُورنَا أكثَر مِمَّا تَزُورَنَا ؟ )) فَنَزَلَتْ : ( وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلاَّ بِأَمْرِ رَبِّكَ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَلِكَ ) [ مريم : 64 ] رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Jibriyl: "Ni kitu gani kinachokuzuilia kutuzuru kwa wingi zaidi kuliko unavyoturuzuku sasa." Hapo ikateremka ayah inayosema: (Na (sisi Malaika) hatuteremki ila kwa amri ya Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Ni Yake Yeye yaliyoko mbele yetu, na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyoko baina ya hayo). [Maryam: 64] [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لا تُصَاحِبْ إلاَّ مُؤْمِناً ، وَلاَ يَأْكُلْ طَعَامَكَ إلاَّ تَقِيٌّ )) . رواه أَبُو داود والترمذي بإسناد لا بأس بِهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msiwe pamoja isipokuwa na Muumini na wala asile chakula chako isipokuwa mcha Mungu." [Abu Daawuud na At-Tirmidhy, kwa Isnaad ambayo si mbaya]

 

 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( الرَّجُلُ عَلَى دِينِ خَلِيلِهِ ، فَليَنْظُرْ أَحَدُكُمْ مَنْ يُخَالِلُ )) رواه أَبُو داود والترمذي بإسناد صحيح ، وَقالَ الترمذي : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu  'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu anakuwa katika Dini ya rafiki yake, basi atizame mmoja wenu anayefanya urafiki naye." [Abu Daawuud na At-Tirmidhy na amesema kuwa hii ni Hadiyth Hasan]

 

 

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( المَرْءُ مَعَ مَنْ أَحَبَّ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : قيل للنبي صلى الله عليه وسلم: الرَّجُلُ يُحبُّ القَومَ وَلَمَّا يَلْحَقْ بِهِمْ ؟ قَالَ : (( المَرْءُ مَعَ مَنْ أَحَبَّ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu anakuwa pamoja na wale anaowapenda." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah nyengine amesema: aliambiwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mtu anawapenda watu lakini hatangamani nao?" Akasema: "Mtu anakuwa pamoja na wale aanowapenda."

 

 

 

Hadiyth – 10

وعن أنس رضي الله عنه: أنَّ أعرابياً قَالَ لرسول الله صلى الله عليه وسلم: مَتَى السَّاعَةُ ؟ قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا أعْدَدْتَ لَهَا ؟ )) قَالَ : حُبَّ الله ورسولهِ ، قَالَ : (( أنْتَ مَعَ مَنْ أحْبَبْتَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ ، وهذا لفظ مسلم .

وفي رواية لهما : مَا أعْدَدْتُ لَهَا مِنْ كَثيرِ صَوْمٍ ، وَلاَ صَلاَةٍ ، وَلاَ صَدَقَةٍ ، وَلَكِنِّي أُحِبُّ الله وَرَسُولَهُ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ya kwamba Mbedui mmoja alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Lini Qiyaamah?" Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Je, umejiandalia nini?" Akasema: "Mapenzi ya Allaah na Rasuli Wake." Akasema: "Wewe uko pamoja na unaowapenda." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud na At-Tirmidhiy]. Na hii ni lafdhi ya Muslim.

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy na Muslim: "Sijajiandaa kwa kwa hicho Qiyaamah kwa funga nyingi wala Swalaah na Swadaqah nyingi lakini mimi nampenda Allaah na Rasuli Wake."

 

 

 

Hadiyth – 11

وعن ابن مسعود  رضي الله عنه، قَالَ : جاء رجلٌ إلى رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ: يَا رَسُول الله ، كَيْفَ تَقُولُ في رَجُلٍ أَحَبَّ قَوْماً وَلَمْ يَلْحَقْ بِهِمْ ؟ فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( المَرْءُ مَعَ مَنْ أحَبَّ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Alikuja mtu kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: "Ee Rasuli wa Allaah unasemaje kuhusu mtu ambaye anawapenda watu lakini hajatangamana nao? Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mtu anakuwa pamoja na wale anaowapenda." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 12

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( النَّاسُ مَعَادِنٌ كَمَعَادِنِ الذَّهَبِ وَالفِضَّةِ ، خِيَارُهُمْ في الجَاهِلِيَّةِ خِيَارُهُمْ في الإسْلاَمِ إِذَا فَقهُوا ، وَالأرْوَاحُ جُنُودٌ مُجَنَّدَةٌ ، فَمَا تَعَارَفَ مِنْهَا ائْتَلَفَ ، ومَا تَنَاكَرَ مِنْهَا اخْتَلَفَ )) رواه مسلم .

وروى البخاري قوله: (( الأَرْوَاحُ … )) إلخ مِنْ رواية عائشة رضي الله عنها .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watu ni kama madini ya dhahabu na fedha, mbora wao katika ujahiliya (zama za ujinga) anakuwa mbora katika Uislamu anapokuwa na ufahamu (wa Dini). Na roho zao zinakuwa kama kundi la jeshi, miongoni mwao ni wale wenye sifa zilizosawa, hivyo kuchanganyika na kuwa pamoja na wale wenye sifa tofauti wanatengana na wenziwao." [Muslim] .

Al-Bukhaariy amepokea kauli: "Roho" mpaka mwisho kuwa hii ni riwaayah ya 'Aaishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa).

 

 

 

Hadiyth – 13

وعن أُسَيْر بن عمرو ، ويقال : ابن جابر وَهُوَ - بضم الهمزة وفتح السين المهملة - قَالَ : كَانَ عُمَرُ بْنُ الخَطَّابِ رضي الله عنه إِذَا أتَى عَلَيهِ أمْدَادُ أهْلِ اليَمَنِ سَألَهُمْ : أفِيكُمْ أُوَيْسُ بْنُ عَامِرٍ ؟ حَتَّى أتَى عَلَى أُوَيْسٍ رضي الله عنه ، فَقَالَ لَهُ : أنْتَ أُوَيْسُ ابْنُ عَامِر ؟ قَالَ : نَعَمْ ، قَالَ : مِنْ مُرَادٍ ثُمَّ مِنْ قَرَنٍ ؟ قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : فَكَانَ بِكَ بَرَصٌ ، فَبَرَأْتَ مِنْهُ إلاَّ مَوْضِعَ دِرْهَمٍ ؟ قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : لَكَ وَالِدةٌ ؟ قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( يَأتِي عَلَيْكُمْ أُويْسُ بْنُ عَامِرٍ مَعَ أمْدَادِ أهْلِ اليَمَنِ مِنْ مُرَادٍ ، ثُمَّ مِنْ قَرَنٍ كَانَ بِهِ بَرَصٌ ، فَبَرَأَ مِنْهُ إلاَّ موْضِعَ دِرْهَمٍ ، لَهُ وَالدةٌ هُوَ بِهَا بَرٌّ لَوْ أقْسَمَ عَلَى الله لأَبَرَّهُ ، فإنِ اسْتَطَعْتَ أنْ يَسْتَغْفِرَ لَكَ فَافْعَل )) فَاسْتَغْفِرْ لي فَاسْتَغْفَرَ لَهُ ، فَقَالَ لَهُ عُمَرُ : أيْنَ تُريدُ ؟ قَالَ : الكُوفَةَ ، قَالَ : ألاَ أكْتُبُ لَكَ إِلَى عَامِلِهَا ؟ قَالَ : أكُونُ في غَبْرَاءِ النَّاسِ أَحَبُّ إِلَيَّ ، فَلَمَّا كَانَ مِنَ العَامِ المُقْبِلِ حَجَّ رَجُلٌ مِنْ أشْرَافِهِمْ ، فَوافَقَ عُمَرَ ، فَسَألَهُ عَنْ أُوَيْسٍ ، فَقَالَ : تَرَكْتُهُ رَثَّ البَيْتِ قَليلَ المَتَاع ، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقولُ : (( يَأتِي عَلَيْكُمْ أُوَيْسُ بْنُ عَامِرٍ مَعَ أمْدَادٍ مِنْ أهْلِ اليَمَنِ مِنْ مُرَادٍ ، ثُمَّ مِنْ قَرَنٍ ، كَانَ بِهِ بَرَصٌ فَبَرَأَ مِنْهُ إلاَّ مَوضِعَ دِرْهَمٍ ، لَهُ وَالِدَةٌ هُوَ بِهَا بَرٌّ لَوْ أقْسَمَ عَلَى اللهِ لأَبَرَّهُ ، فَإنِ اسْتَطْعتَ أنْ يَسْتَغْفِرَ لَكَ ، فَافْعَلْ )) فَأتَى أُوَيْساً ، فَقَالَ : اسْتَغْفِرْ لِي . قَالَ : أنْتَ أحْدَثُ عَهْداً بسَفَرٍ صَالِحٍ ، فَاسْتَغْفِرْ لي . قَالَ : لَقِيتَ عُمَرَ ؟ قَالَ : نَعَمْ ، فاسْتَغْفَرَ لَهُ ، فَفَطِنَ لَهُ النَّاسُ ، فَانْطَلَقَ عَلَى وَجْهِهِ . رواه مسلم .

وفي رواية لمسلم أيضاً عن أُسَيْر بن جابر رضي الله عنه: أنَّ أهْلَ الكُوفَةِ وَفَدُوا عَلَى عُمَرَ رضي الله عنه، وَفِيهمْ رَجُلٌ مِمَّنْ كَانَ يَسْخَرُ بِأُوَيْسٍ ، فَقَالَ عُمَرُ : هَلْ هاهُنَا أَحَدٌ مِنَ القَرَنِيِّينَ ؟ فَجَاءَ ذلِكَ الرَّجُلُ ، فَقَالَ عمرُ : إنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَدْ قَالَ : (( إنَّ رَجُلاً يَأتِيكُمْ مِنَ اليَمَنِ يُقَالُ لَهُ : أُوَيْسٌ ، لاَ يَدَعُ باليَمَنِ غَيْرَ أُمٍّ لَهُ ، قَدْ كَانَ بِهِ بَيَاضٌ فَدَعَا الله تَعَالَى ، فَأذْهَبَهُ إلاَّ مَوضِعَ الدِّينَارِ أَو الدِّرْهَمِ ، فَمَنْ لَقِيَهُ مِنْكُمْ ، فَلْيَسْتَغْفِرْ لَكُمْ )) . 

وفي رواية لَهُ : عن عمر رضي الله عنه، قَالَ : إنِّي سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول :(( إنَّ خَيْرَ التَّابِعِينَ رَجُلٌ يُقَالُ لَهُ : أُوَيْسٌ ، وَلَهُ وَالِدَةٌ وَكَانَ بِهِ بَيَاضٌ ، فَمُرُوهُ ، فَلْيَسْتَغْفِرْ لَكُمْ )) .

Imepokewa kutoka kwa Usayr bin 'Amru (Radhwiyah Allaahu 'anhu), Imesemwa ni Ibn Jaabir (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "'Umar bin Al-Khataab (Radhwiyah Allaahu 'anhu) anapojiwa na kundi kutoka Yemen huwauliza: "Ndani yenu yupo Uways bin 'Aamir?" Mpaka siku hiyo akamkuta Uways, akamwambia: "Wewe ni Uways bin 'Aamir?" Akasema: "Ndio." Akasema: "Kutoka kabila la Muraad, kutoka ukoo wa Qaran?" akasema: "Ndio." Akasema: "Ulikuwa na mbalanga ukapona isipokuwa sehemu kiasi cha dirhamu?" Akasema: "Ndio'" Akasema: "Una mama?" Akasema: "Ndio." Akasema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akisema: "Atakujieni Uways pamoja na kundi la watu wa Yemen kabila la Muraad, kisha kwa Qaran. Alikuwa na mbalanga akapona isipokuwa sehemu ndogo mfano wa dirhamu. Ana mama anayemtendea wema, lau ataapa kwa Allaah atamtimizia. Ukiweza kumpata ili akuombee maghfira fanya." Hivyo niombee msamaha kwa Allaah, naye akamuombea. 'Umar akamwambia: "Unakwenda wapi?" Akasema; "Kufah." Akasema: "Je, nikuandikie kwa gavana wake? Akasema; "Kuwa katika watu maskini ni bora kwangu. Ulipofika mwaka uliofuata walihiji watu watukufu kutoka Kufah nao walikutana na 'Umar, akawauliza kuhusu Uways. Akasema: "Nimemuacha katika nyumba mbaya, samani chache." Akasema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akisema: "Atakujieni Uways pamoja na kundi la watu wa Yemen kabila la Muraad, kisha kwa Qaran. Alikuwa na mbalanga akapona isipokuwa sehemu ndogo mfano wa dirhamu. Ana mama anayemtendea wema, lau ataapa kwa Allaah atamtimizia. Ukiweza kumpata ili akuombee maghfira fanya." Akamjia Uways akamwambia: "Niombee msamaha kwa Allaah." Akasema: 'Wewe umerudi punde safarini niombee msamaha."Akamuuliza: "Je, umekutana na 'Umar?" Akasema: "Ndio." Akamuombea maghfira, watu wakamgundua." [Muslim]

Na riwaayah ya Muslim toka kwa Usayr bin Jaabir (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa watu wa Kufah walipeleka wawakilishi wao kwa 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu), Miongoni mwao alikuwepo mtu aliyekuwa akimdhihaki Uways. Akasema 'Umar: "Hapa yupo yeyote kutoka ukoo wa Qaran?" Yule mtu akaja mbele. Akasema 'Umar: "Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika atakujieni mtu kutoka Yemen anaitwa Uways. Amemuacha mamake peke yake, ana weupe (mbalanga) akamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa). Allaah akauondoa isipokuwa sehemu ndogo mfano wa dinari au dirhamu. Atakayekutana naye miongoni mwenu amtake amuombee maghfira kwa Allaah." 

Katika riwaayah yake kutoka kwa 'Umar amesema: "Hakika nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mbora wa Tabi'in ni mtu anayeitwa Uways. Ana mama yake na weupe katika mwili wake. Nendeni kwake na mumuombe awaombee maghfira."

 

 

 

Hadiyth – 14

وعن عمر بن الخطاب رضي الله عنه، قَالَ : اسْتَأذَنْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم في العُمْرَةِ ، فَأذِنَ لِي ، وَقالَ : (( لاَ تَنْسَنا يَا أُخَيَّ مِنْ دُعَائِكَ )) فَقَالَ كَلِمَةً مَا يَسُرُّنِي أنَّ لِي بِهَا الدُّنْيَا

وفي رواية : وَقالَ : (( أشْرِكْنَا يَا أُخَيَّ في دُعَائِكَ )) .

حديث صحيح رواه أَبُو داود والترمذي، وَقالَ: (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Al-Khattaab (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye alisema: "Nilimuomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)ruhusa ya kwenda kufanya Umrah, naye alinipatia idhini. Na akasema: "Ee ndugu yangu! Usitusahau katika dua'a zako." Akasema (Radhwiyah Allaahu 'anhu):"Hili ni neno ambalo sitataka kubadilishana hata na dunia yote."

Na katika riwaayah nyingine, alisema: "Ee ndugu yangu! Tushirikishe katika dua yako."

Hadiyth Swahiyh iliyonukuliwa na Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa hii ni Hadiyth Swahiyh.

 

 

 

Hadiyth – 15

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يزور قُبَاءَ رَاكِباً وَمَاشِياً ، فَيُصَلِّي فِيهِ رَكْعَتَيْنِ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : كَانَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يَأتي مَسْجِد قُبَاءَ كُلَّ سَبْتٍ رَاكباً ، وَمَاشِياً وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ يَفْعَلُهُ .

Imepokewa kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) ambaye amesema: "Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akizuru Qubaa (Msikiti wa sehemu hiyo) akiwa amepanda (mnyama) na kwa miguu. Na alikuwa akiswali katika Msikiti huo rakaa mbili." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad].

Katika riwaayah nyingine: "Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiuzuru Msikiti wa Qubaa kila siku ya Jumamosi kwa kupanda mnyama na kwa miguu (wakatika mwengine). Na Ibn 'Umar alikuwa akifanya hivyo."

 

 

 

 

 

Share