050-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Hofu (Ya Allaah)

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب الخوف

050-Mlango Wa Hofu (Ya Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ ﴿٤٠﴾

Na Mimi Pekee niogopeni. [Al-Baqarah: 40]

 

إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ ﴿١٢﴾

Hakika mkamato wa kuadhibu wa Rabb wako bila shaka ni mkali. [Al-Buruj: 12]

 

وَكَذَٰلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَىٰ وَهِيَ ظَالِمَةٌ ۚ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ﴿١٠٢﴾

Na hivyo ndivyo mkamato wa Rabb wako unavyokuwa Anapokamata miji na huku ikifanya dhulma. Hakika mkamato Wake unaumiza vikali.

 

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّمَنْ خَافَ عَذَابَ الْآخِرَةِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّجْمُوعٌ لَّهُ النَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّشْهُودٌ﴿١٠٣﴾

Hakika katika hayo mna Aayah (funzo, zingatio, dalili) kwa anayekhofu adhabu ya Aakhirah. Hiyo ni Siku ya kujumuishwa watu, na hiyo ni Siku ya kushuhudiwa.

 

وَمَا نُؤَخِّرُهُ إِلَّا لِأَجَلٍ مَّعْدُودٍ﴿١٠٤﴾

Na hatuiakhirishi isipokuwa kwa muda maalumu unaohesabiwa.  

 

يَوْمَ يَأْتِ لَا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ فَمِنْهُمْ شَقِيٌّ وَسَعِيدٌ﴿١٠٥﴾

Siku itakapofika; haitosema nafsi yeyote isipokuwa kwa idhini Yake (Allaah). Basi miongoni mwao ni wenye mashaka wanaostahiki adhabu, na wenye furaha na neema.

 

فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ﴿١٠٦﴾

Basi ama wale walio mashakani, basi watakuwa motoni, lao humo ni upumuaji pumzi kwa mngurumo na uvutaji pumzi kwa mkoromo. [Huwd: 102-106]

 

وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ  ﴿٢٨﴾ 

Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi yake. [Aal-'Imraan: 28]

 

 

يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴿٣٤﴾ وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ ﴿٣٥﴾ وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ ﴿٣٦﴾ لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ ﴿٣٧﴾ 

Siku mtu atakapomkimbia ndugu yake. Na mama yake na baba yake. Na mkewe na wanawe.

Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na hali ya kumtosheleza. ['Abasa: 34-37]

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ ﴿١﴾

Enyi watu! Mcheni Rabb wenu. Hakika zilizala la Saa (Qiyaamah) ni jambo kuu.

 

يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَىٰ وَمَا هُم بِسُكَارَىٰ وَلَـٰكِنَّ عَذَابَ اللَّـهِ شَدِيدٌ ﴿٢﴾

Siku mtakapoiona kila mnyonyeshaji atamsahau anayemnyonyesha, na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake, na utawaona watu wamelewa, kumbe hawakulewa lakini ni adhabu ya Allaah kali. [Al-Hajj: 1-2]

 

وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ ﴿٤٦﴾

Na kwa mwenye kukhofu kisimamo mbele ya Rabb wake atapata bustani mbili. [Ar-Rahmaan: 46]

 

وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٥﴾

Na watakabiliana baadhi yao kwa wengineo wakiulizana.

 

قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ ﴿٢٦﴾

Watasema: Hakika sisi tulikuwa kabla kwenye ahli zetu wenye kuogopa

 

فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ ﴿٢٧﴾

Basi Allaah Akatufadhilisha, na Akatuokoa na adhabu ya moto unaobabua.

 

إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾

Hakika sisi tulikuwa kabla Tunamuomba Yeye Pekee, hakika yeye Ndiye Mwingi huruma na fadhila, Mwenye kurehemu. [Atw-Twuwr: 25-28]

 

 

 

Hadiyth – 1

عن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : حدثنا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَهُوَ الصادق المصدوق : (( إنَّ أحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّهِ أربَعِينَ يَوماً نُطْفَةً ، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذلِكَ ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذلِكَ ، ثُمَّ يُرْسَلُ المَلَكُ ، فَيَنْفُخُ فِيهِ    الرُّوحَ ، وَيُؤْمَرُ بِأرْبَعِ كَلِمَاتٍ : بِكَتْبِ رِزْقِهِ وَأجَلِهِ وَعَمَلِهِ وَشَقِيٌّ أَوْ سَعِيدٌ . فَوَالَّذِي لا إلهَ غَيْرُهُ إنَّ أحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ الجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وبيْنَهَا إلاَّ ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيهِ الكِتَابُ ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ النَّارِ فَيدْخُلُهَا ، وَإنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلاَّ ذراعٌ ، فَيَسْبِقُ عَلَيهِ الكِتَابُ فَيعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ الجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa na Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa: "Ametuhadithia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na yeye ni mkweli mswadikishwa: Hakika mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mamake siku arobaini; kisha kuwa pande la damu muda kama huo; kisha pande la nyama muda kama huo. Kisha hutumwa Malaika anapuliza roho ndani yake, na anaamrishwa maneno manne: Kuandika riziki yake, ajali yake, amali yake, mwema au muovu. Wa-Allaahi hakuna Rabb asiyekuwa Yeye, hakika mmoja wenu hufanya amali ya watu wa Peponi, mpaka haiwi baina yake na Pepo ila dhiraa, Basi kitabu kimtangulie akafanya amali ya watu wa Motoni. Na mmoja wenu hufanya amali ya watu wa Motoni mpaka haiwi baina yake na Moto ila dhiraa, kitabu kikamtangulia na hivyo akafanya amali za watu wa Pepono na kisha akaingia humo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

عن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يُؤتَى بِجَهَنَّمَ يَومَئذٍ لَهَا سَبْعُونَ ألفَ زِمَامٍ ، مَعَ كُلِّ زِمَامٍ سَبعُونَ ألْفَ مَلَكٍ يَجُرُّونَهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa na Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Siku ya Qiyaamah Jahanam italetwa ikiwa na hatamu elfu sabiini pamoja na kila hatamu kutakuwa na Malaika elfu sabiini  wanaoikokota." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إنَّ أهْوَنَ أهْلِ النَّارِ عَذَاباً يَوْمَ القِيَامَةِ لَرَجُلٌ يوضعُ في أخْمَصِ قَدَمَيْهِ جَمْرَتَانِ يَغْلِي مِنْهُمَا دِمَاغُهُ . مَا يَرَى أنَّ أَحَداً أشَدُّ مِنْهُ عَذَاباً ، وَأنَّهُ لأَهْوَنُهُمْ عَذَاباً )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa an-Nu'maan bin Bashiir (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) ambaye amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika watu wa Motoni watakaokuwa na adhabu duni kabisa Siku ya Qiyaamah ni mtu atakaye wekewa makaa mawili ya Moto chini ya miguu yake yatakayo lifanya bongo lake lichemke. Mtu huyo atajihisi kuwa yeye anapata adhabu kali zaidi kuliko wote, kumbe ndio amepewa adhabu ya chini kabisa." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

 

Hadiyth – 4

وعن سمرة بن جندب رضي الله عنه: أنَّ نبيَّ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مِنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ النَّارُ إِلَى كَعْبَيهِ ، وَمنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى رُكْبَتَيهِ ، وَمنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى حُجزَتِهِ ، وَمِنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى تَرْقُوَتِهِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Samurah bin Jundub (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Miongoni mwa watu wa Motoni ni wale ambao moto kwa ukali wake utawafika kwenye tindi za miguu, na wengine kwenye magoti, na wengine mpaka kiunoni, na madhambi yao." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يَقُومُ النَّاس لِرَبِّ العَالَمينَ حَتَّى يَغِيبَ أحَدُهُمْ في رَشْحِهِ إِلَى أنْصَافِ أُذُنَيهِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watasimama watu mbele ya Rabb wa walimwengu, (kwa amri Yake na kupatiwa malipo) hadi baadhi yao wapotee katika jasho lao hadi katika ya masikio yao." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : خطبنا رَسُول الله صلى الله عليه وسلمخطبة مَا سَمِعْتُ مِثلها قطّ ، فَقَالَ : (( لَوْ تَعْلَمُونَ مَا أعْلَمُ ، لَضحِكْتُمْ قَلِيلاً وَلَبَكَيتُمْ كَثِيراً )) فَغَطَّى أصْحَابُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَجُوهَهُمْ ، وَلَهُمْ خَنَينٌ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : بَلَغَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم عَنْ أَصْحَابِهِ شَيْءٌ فَخَطَبَ ، فَقَالَ : (( عُرِضَتْ عَلَيَّ الجَنَّةُ وَالنَّارُ ، فَلَمْ أرَ كَاليَومِ في الخَيرِ وَالشَّرِّ ، وَلَوْ تَعْلَمونَ مَا أعلَمُ لَضَحِكْتُمْ قَلِيلاً وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيراً )) فَمَا أتَى عَلَى أصْحَابِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَوْمٌ أَشَدُّ مِنْهُ ، غَطَّوْا رُؤُسَهُمْ وَلَهُمْ خَنِينٌ .

Na imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Alituhutubia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hotuba sijasikia mfano wake katu, akasema: 'Lau mngejua ninayoyajua, mngecheka kidogo na kulia sana.' Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakafunika nyuso zao na kulia kwa mayowe." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah: "Habari zilimfikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) toka kwa Swahaaba zake, basi akahutubia, akasema: 'Nime onyeshwa Pepo na Moto sijaona kama leo katika mazuri na shari. Lau mngejua ninayoyajua basi mngecheka kidogo na kulia sana.' Hii ilikuwa siku nzito zaidi kwa Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Walifunika nyuso zao wakaanza kulia kwa nguvu.

 

 

Hadiyth – 7

وعن المقداد رضي الله عنه، قَالَ : سمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( تُدْنَى الشَّمْسُ يَوْمَ القِيَامَةِ مِنَ الخَلْقِ حَتَّى تَكُونَ مِنْهُمْ كَمِقْدَارِ مِيلٍ )) قَالَ سُلَيْم بنُ عامِر الراوي عن المقداد : فَوَاللهِ مَا أدْرِي مَا يعني بالمِيلِ ، أمَسَافَةَ الأرضِ أَمِ المِيلَ الَّذِي تُكْتَحَلُ بِهِ العَيْنُ ؟ قَالَ : (( فَيكُونُ النَّاسُ عَلَى قَدْرِ أعْمَالِهِمْ في العَرَقِ ، فَمِنْهُمْ مَنْ يَكُونُ إِلَى كَعْبَيْهِ ، ومنهم من يكون إِلَى ركبتيه ، ومنهم مَنْ يَكُونُ إِلَى حِقْوَيْهِ ، وَمِنْهُمْ مَنْ يُلْجِمُهُ العَرَقُ إلْجَاماً )) . قَالَ : وَأَشَارَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بيدهِ إِلَى فِيهِ . رواه مسلم.

Toka kwa Al-Miqdaad (Radhwiyah Allahu 'anhu) Nilimsikia Rasuli wa Allaahu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Siku ya Qiyaamah jua litasongezwa kwa viumbe, litakuwa kiasi cha maili." Sulaym bin 'Aamir mpokezi kutoka kwa Al-Maqdaad alisema: "Naapa kwa Allaah! Sikujua alichokusudia kwa Maili - je, ni masafa ya ardhi au ni kijiti kinachopaka jicho wanja?, Watu watatokwa jasho kadiri ya matendo yao, kuna ambao jasho itawafika katika tindi mbili za miguu, na wengine magotini, na wengine kiunoni na wengine kufunikwa kabisa kwa mkono kwenye mdomo wake." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( يَعْرَقُ النَّاسُ يَومَ القِيَامَةِ حَتَّى يَذْهَبَ عَرَقُهُمْ في الأرضِ سَبْعِينَ ذِراعاً ، وَيُلْجِمُهُمْ حَتَّى يَبْلُغَ آذَانَهُمْ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaah 'anhu) amesema kuwa: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Watu watatoa jasho Siku ya Qiyaamah mpaka jasho yao ifike ardhini dhiraa sabini, naiwafunike, hadi ifike masikioni mwao." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : كُنَّا مَعَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم إذْ سمع وجبة، فَقَالَ : (( هَلْ تَدْرُونَ مَا هَذَا ؟ )) قُلْنَا : الله وَرَسُولُهُ أعْلَمُ . قَالَ : (( هذَا حَجَرٌ رُمِيَ بِهِ في النَّارِ مُنْذُ سَبْعينَ خَريفاً ، فَهُوَ يَهْوِي في النَّارِ الآنَ حَتَّى انْتَهَى إِلَى قَعْرِها فَسَمِعْتُمْ وَجْبَتَهَا )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye alisilimu: "Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na mara tukasikia sauti ya kitu kilichoanguka chini. Hapo akasema: "Je, mnajua hicho ni kitu gani?" Tukasema: "Allaah na Rasuli Wake wajua zaidi." Akasema: "Hilo ni jiwe liliorushwa Motoni miaka sabini iliyopita; lilikuwa likizunguka kwa kipindi mpaka leo ndilo limefika chini na ndio mmesikia kugusa chini." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 10

وعن عدي بن حاتم رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ إلاَّ سَيُكَلِّمُهُ رَبُّهُ لَيْسَ بَيْنَهُ وبَيْنَهُ تَرْجُمَانٌ ، فَيَنْظُرُ أيْمَنَ مِنْهُ فَلاَ يَرَى إلاَّ مَا قَدَّمَ ، وَيَنْظُرُ أشْأَمَ مِنْهُ فَلاَ يَرَى إلاَّ مَا قَدَّمَ ، وَيَنْظُرُ بَيْنَ يَدَيْهِ فَلاَ يَرَى إلاَّ النَّارَ تِلْقَاءَ وَجْهِهِ ، فَاتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa 'Adiy bin Haatim (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna yeyote miongoni mwenu isipokuwa Allaah Atazungumza naye Siku ya Qiyaamah, kutakuwa hakuna mkalimani kati yake na Allaah. Kisha ataangalia kuliani mwake na wala hatoona kitu alichokitanguliza, kisha ataagalia mbele yake ataona Moto unampokea, kwa hiyo awezaye kutoa kipande cha tende moja kama sadaqa, na afanye hivyo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 11

وعن أَبي ذر رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنِّي أَرَى مَا لا تَرَوْنَ ، أطَّتِ السَّمَاءُ وَحُقَّ لَهَا أنْ تَئِطَّ ، مَا فِيهَا مَوضِعُ أرْبَع أصَابعَ إلاَّ وَمَلَكٌ وَاضِعٌ جَبْهَتَهُ سَاجِداً للهِ تَعَالَى . والله لَوْ تَعْلَمُونَ مَا أعْلَمُ ، لَضَحِكْتُمْ قَلِيلاً وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيراً ، وَمَا تَلَذَّذْتُمْ بالنِّساءِ عَلَى الفُرُشِ ، وَلَخَرَجْتُمْ إِلَى الصُّعُدَاتِ تَجْأرُونَ إِلَى اللهِ تَعَالَى )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika mimi naona msiyoyaona, na ninasikia msiyosikia. Mbingu zinalia na ina haki kufanya hivyo (kulia). Hakuna nafasi yeyote hata ya vidole vinne isipokuwa yupo Malaaika ametandaza mbawa yake akimsujudia Allaah Ta'aalaa. Naapa kwa Allaah! Lau mngekuwa mnajua ninayoyajua basi mngecheka kidogo na kulia sana; hamngekuwa ni wenye kustarehe na wake zenu katika vitanda. Mngefanya haraka kutoka barabarani na njiani ili kutaka ulinzi wa Allaah." [At-Tirmidhiy, ambaye amesema hii ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 12

وعن أَبي برزة نَضْلَة بن عبيد الأسلمي رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لا تَزُولُ قَدَمَا عَبْدٍ يَومَ القِيَامَةِ حَتَّى يُسْأَلَ عَنْ عُمُرِهِ فِيمَ أفنَاهُ ؟ وَعَنْ عِلمِهِ فِيمَ فَعَلَ فِيهِ ؟ وَعَنْ مَالِهِ مِنْ أيْنَ اكْتَسَبَهُ ؟ وَفيمَ أنْفَقَهُ ؟ وَعَنْ جِسمِهِ فِيمَ أبلاهُ ؟ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Barzah Nadhlah bin 'Ubayd al-Aslamiy (Radhwiyah Allaah 'anhu) kuwa: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haitaondoka miguu ya mja Siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe kuhusu Umri wake ameumaliza vipi; na kuhusu elimu yake ametumia vipi; na kuhusu mali yake ameichuma vipi na ameitumia vipi; na kuhusu mwili wake ameuzeesha vipi? [At-Tirmidhiy, ambaye amesema ni Hadiyth Hasan]

 

 

 

Hadiyth – 13

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قرأ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ( يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا ) [ الزلزلة : 4 ] ثُمَّ قَالَ : (( أتَدْرونَ مَا أخْبَارهَا )) ؟ قالوا : الله وَرَسُولُهُ أعْلَمُ . قَالَ : (( فإنَّ أخْبَارَهَا أنْ تَشْهَدَ عَلَى كُلّ عَبْدٍ أَوْ أمَةٍ بما عَمِلَ عَلَى ظَهْرِهَا تَقُولُ : عَملْتَ كَذَا وكَذَا في يَومِ كَذَا وكَذَا فَهذِهِ أخْبَارُهَا )) رواه الترمذي ،  وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Alisoma Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Kauli ya Allaah: (Siku hiyo itahadithia khabari zake) [Al-Zalzalah: 4]. Kisha akasema: "Je, mnajua khabari yake?" Wakasema: "Allaah na Rasuli Wake Wajua zaidi." Akasema: Hakika khabari yake ni kumshuhudia kila mja mwanamume au mwanamke kwa aliyoyafanya juu ya mgongo wake. Itasema: 'Ulifanya kadha na kadha siku kadha na kadha, hii ndiyo hiyo khabari yake.' [At-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 14

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( كَيْفَ أنْعَمُ ! وَصَاحِبُ القَرْنِ قَدِ التَقَمَ القَرْنَ ، وَاسْتَمَعَ الإذْنَ مَتَى يُؤمَرُ بالنَّفْخِ فَيَنْفُخُ )) فَكَأنَّ ذلِكَ ثَقُلَ عَلَى أصْحَابِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم فَقَالَ لَهُمْ : (( قُولُوا : حَسْبُنَا الله وَنِعْمَ الوَكِيلُ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسنٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iid Al-Khudriy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Vipi nitakuwa na furaha na mwenye baragumu (Malaika Israfil) ametia mdomoni mwake hilo baragumu huku akisubiri idhini ni lini atapatiwa ili apulize." Kama kwamba hilo lilikuwa zito kwa Masahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hivyo akawaambia semeni: "Hasbuna Allaahu wa Ni'mal Wakiil yaani Allaah anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa." [At-Tirmidhiy, ambaye amesema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 15

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ خَافَ أدْلَجَ ، وَمَنْ أدْلَجَ بَلَغَ المَنْزِلَ . ألا إنَّ سِلْعَةَ اللهِ غَالِيَةٌ ، ألاَ إنَّ سِلْعَةَ الله الجَنَّةُ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumuogopa adui hutoks wakati wa mwanzo wa usiku; na mwenye kutoka mapema (usiku), hufika sehemu ya usalama (kutokana na adui). Jueni ya kwamba bidhaa za Allaah zina thamani kubwa. Jueni ya kwamba bidhaa za Allaah ni Pepo Yake." [At-Tirmidhiy, ambaye amesema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 16

وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَتْ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( يُحْشَرُ النَّاسُ يَوْمَ القِيَامَةِ حُفَاةً عُرَاةً غُرْلاً )) قُلْتُ : يَا رَسُول الله ، الرِّجَالُ وَالنِّساءُ جَمِيعاً يَنْظُرُ بَعضُهُمْ إِلَى بَعْض ؟! قَالَ : (( يَا عائِشَةُ ، الأمرُ أشَدُّ مِنْ أنْ يُهِمَّهُمْ ذلِكَ )) .

وفي رواية : (( الأَمْرُ أهمُّ مِنْ أنْ يَنْظُرَ بَعضُهُمْ إِلَى بَعض )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) ambaye amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Watu watafufuliwa Siku ya Qiyaamah wakiwa hawana viatu, uchi na wenye magovi." Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Wanaume na wanawake wote wakiwa pamoja, si wataangaliana wao kwa wao?" Akasema: "Ee 'Aaishah! Jambo hilo litakuwa zito (lenye kutisha) zaidi ya wao kutaka kuangaliana." Na katika riwaayah nyengine: "Jambo hilo litakuwa muhimu zaidi kuliko kuangaliana wao kwa wao (hawatakuwa na nafasi hiyo)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

 
Share