Zurubiani (Wali Wa Ki-Saudia)

Vipimo
Mchele 5 mugs (kikombe kikubwa)
Nyama (au kuku) 2 Ratili (LB)
Chumvi Kiasi
Mafuta 3/4 kikombe
Samli 1/2 kikombe
Vitunguu Vikubwa (kata virefu virefu) 6
Nyanya (iliyosagwa) 6 vijiko vya chakula
Thom 1 kijiko cha chakula
Pilipili mbichi ½ kijiko cha chai
Hiliki nzima 6 chembe
Mdalasini nzima 5 vijiti
Mtindi (yoghurt) ½ kikombe cha chai
Karoti 1
Mapilipili makubwa 2 kijani na jekundu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Sosi
1. Kwenye sufuria mimina mafuta na samli. Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown)
2. Mimina nyama, abdalasini, hiliki na chumvi kwenye hiyo sufuria ya vitunguu ikaange moto wa kiasi mpaka nyama iwive.
3. Saga ile Karoti pamoja na mtindi kwenye blender (mashine yakusagia) kisha imimine kwenye nyama
4. Tia nyanya iliyosagwa.
5. Ikichemka weka moto mdogo mdogo mpaka mafuta yake yaje juu.
6. Tia zile pilipili ulizo zikata kata rangi mbili.
7. Yatowe mafuta yote weka pembeni.
8. Acha sosi pee yake.
Wali
2. Chemsha maji kwenye sufuria kiasi cha magi 10
3. Yakishachemka unatia mchele, chemsha usiive
4. Unamimina ule mchele juu ya lile rojo (sosi)
5. Mafuta uliyoyatoa kwenye sosi yapashe moto halafu unayamimina juu ya mchele, unarudisha motoni. Unaweka motot mdogo mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
6. Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya nyama.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


