Kauli Za Salaf Kuthibitisha Adhabu Ya Kaburi Kuwajibu Hizbut-Tahriyr

 

 

 

1.   Sufyan bin 'Uyaynah (f.197H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"Sunnah ni kumi. Yeyote mwenye kuzikubali amekamilisha Sunnah na mwenye kukataa chochote katika hizo ameiwacha Sunnah; kukubali Qadr (uwezo wa Allaah), kuwatambua Abu Bakr na 'Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma), mto ulioko peponi, shafa'ah, Mizani, Sirat, Emaan ni maneno na vitendo, Quran ni maneno ya Allaah, Adhabu ndani ya kaburi, kufufuliwa siku ya hisabu na kutokubali yakuwa muislamu yeyote bila ya shaka atakuwa peponi au motoni" (15)

2.   Imaam ash-Shafi'iy (f.204H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"Twaba'an al-Qadr (uwezo wa Allaah): yote ya kheri na shari ni kutoka kwake Allaah-Mwenye Uwezo na Nguvu. Bila shaka adhabu ya kaburi ni jambo la kweli, kuulizwa kwa wale walioko makaburini ni kweli, kufufuliwa ni kweli, kufanyiwa hesabu ni kweli, pepo na moto ni kweli. Jambo lolote linalohusiana ndani ya Sunnah na kutajwa na Maulamaa na wafuasi wao kote katika ardhi za waislamu ni kweli"(16)

3.   Imaam Ahmad (f.241H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"Kutoka katika Sunnah (Muakkadah) ambayo mtu yeyote akiiacha au kutoikubali na kutokua na imani nayo basi hatokua katika sisi watu wake! (kisha akataja) imani katika adhabu ya kaburi ni jambo la kweli. Mja ataulizwa maswali kuhusu Dini yake na Mola wake. Munkar na Nakiyr na Pepo na Moto vilevile ni mambo ya kweli (18)

4.   Abu Dawuud (d.275H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"Sura: Maswali ndani ya kaburi na adhabu ndani ya kaburi" (19)

5.   Ibn Qutaybah (d.278H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"Watu wa hadiyth wameungana juu ya ukweli ya kwamba chochote Mola Akadiriacho kiwe, huwa na chochote akadiriacho kisiwe hakiwi; ya kwamba Yeye ni Muumbaji wa uzuri na uovu; ya kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah, haikuumbwa, ya kwamba Allaah ataonekana siku ya malipo, kuwafadhilisha Abu Bakr na 'Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu), kuwa na imani ya adhabu ya kaburi. Hawakhitalifiani katika mambo haya. Yeyote mwenye kupinga mambo haya basi wao humkataa, humchukia na kumtangaza mtu kama huyo kuwa ni mzushi na hujiweka mbali nae" (20).

6.   Imaam at-Tahaawee (f.321H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"Huu ni ufafanuzi wa ‘Aqiydah ya Alhus-Sunnah wal-Jama'ah juu ya njia ya Maulamaa wa dini hii; Abu Haniyfa an-Nu'maan ibn Thaabit al-Kuufiy, Abu Yusuf Ya’quub ibn Ibrahim al-Ansariy na Abu Abdullah Muhammad ibn al-Hasan-ash-Shaybaniy- Allaah Awarehemu na awe na furaha na wote-na imaani yao juu ya misingi ya dini na 'Aqiydah yao juu ya Allaah.'Mpaka akafikia aliposema': walisema tuna imani na Malaika wa mauti ambaye kazi yake ni kutoa roho za watu wote ulimwenguni; na katika adhabu ya kaburi kwa wale wanaostahili.(21)

7.   Abul-Hassan al-Ash'ariy (f.324H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"Mu'tazilah walikataa adhabu ndani ya kaburi.Imepokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwa njia nyingi na Maswahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum). Hakuna kitu kilichopokewa kutoka kwa hata mmoja wao kuhusu kupinga au kukataa jambo hili (adhabu ya kaburi), kufikia kiwango ambapo kumepatikana ijmaa' (makubaliano) kutoka kwa Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)" (22). Pia akaendelea kusema "kumepatikana makubaliano yakwamba adhabu ya kaburi ni jambo la kweli, na kwamba watu watatahiniwa na kuulizwa maswali ndani ya makaburi yao. Kwahivyo, Allaah Atuthibitishe sisi na kile akipendacho." (23)

8.   Imaam al-Aajuriy (f.360H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"Sura: tasdiyq (kuthibitisha) na kuamini adhabu ya kaburi "ambapo ameleta ahaadiyth zilizopokewa na al-Bukhaariy na Muslim na amemalizia sura kwa kusema: "Wale watu wanaokataa ahaadiyth hizi, hapana usalama kwao isipokua wako kwenye upotofu ulio mbali na wamo katika hasara kubwa."(24)

9.   Ibn Abi Haatim (f.327H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
Njia tuliyochagua ni kumfuata Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), Maswahaba, Tabi'een na wale wote waliowafuata wao kwa wema, yakiandamana na kujiepusha na mambo ya uzushi, kushikamana na njia ya Ahlul-Athar (wapokezi wa riwaya) kama vile Abu Abdullah Ahmad Ibn Hanbal, Is'haaq ibn Ibrahim, Abu 'Ubayd al-Qaasim ibn salaam na ash-Shaafi'iy, kushikamana na kitabu (Qur'aan) Sunnah na njia za Maimamu wenye kufuata riwaya za Salaf, kuchukua yaliochukuliwa na Ahlus-Sunnah katika miji tafauti mpaka aliposema: "Imani yaongezeka na yapungua na tuna imani katika adhabu ya kaburi."(25)

 

10.   Imaam al-Barbahaariy (f.329H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"Imani katika adhabu ya kaburi na Munkar na Nakiyr."(26)

11.   AL-Ismaeeliy (f.371H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"Jua na kutanabahi- Allaah Awe na huruma juu yetu na wewe – ya kwamba njia ya ahlul-Hadiyth, Ahlus-Sunnah wal-Jama'ah ni kukubali kidhati Imani kuhusu Allaah, Malaika Wake, Mitume Yake na kukubali chochote kilichoandikwa ndani ya kitabu cha Allaah Alie juu - na mambo swahihi yalioyopokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) mpaka akasema; "Adhabu ndani ya kaburi ni jambo la kweli."

 

12.   AL-Qayrawaaniy (f.386H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
Katika Sura: Yale yaliotajwa katika Sunnah kuhusu ‘Aqiydah ya moyo kutokana na mambo ya waajib katika Dini. Miongoni mwa hayo ni: Imani ndani ya moyo na kutamka kwa ulimi ya kwamba Allaah peke Yake ndiye apasaye kuabudiwa kwa haki, na mwengine yeyote asiyekua Allaah hana haki ya kuabudiwa" kisha akaendelea mpaka alipofikia kusema: "Na adhabu ndani ya kaburi ni jambo la kweli na waumini watatahiniwa ndani ya makaburi yao."(28)

13.   Ibn Abee Aamniyn (f.399H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"Ahlus-Sunnah wana imani kuhusu adhabu ya kaburi, Allaah Atukinge nayo sote"(29)

14.   Imaam al-Laalikaaiy (f.418H) (Rahimahu Allaah) Amesema:
"SURA: Riwaya kuhusu yaliopokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuhusiana na ukweli ya kwamba wakati Waislamu wakiteremshwa ndani ya makaburi yao, wataulizwa na Munkar na Nakiyr, na kwamba adhabu ndani ya kaburi ni kweli na kuiamini ni wajib." (30)

15.   Imaam al-Bayhaqiy (f.458H) (Rahimahu Allaah) Amesema.
"SURA: Imani katika adhabu ya kaburi" (31)

REJEA:

(15)   Sharh Usuul I'tiqaad Ahlus-Sunnah wal Jama'ah (namba 312) ya al-Laalikaiy.
(16)   Manaaqibush-Shafi'iy (1/415) cha al-Bayhaqiy.

 
(17)   Usuulus-Sunnah (namba 8) cha Imaam Ahmad.

 
(18)   Risaalatus-Sunnah (ukurasa 72) cha Imaam Ahmad.

 
(19)   Kitaabus-Sunnah (ukurasa 900) sehemu ya Sunan Abi Dawuud.

 
(20) Ta'wiyl Mukhtaliful-Hadith (uk.18)

(21)   Aqiydatut-Tahaawiyyah (namba 79-80)

(22)   Al-Ibaanah'an Usuulid-Diyaanah (uk.201)

 
(23)   Risaalah ilaa Ahlith-Thaghr (ukurasa 279) cha Abul-Hasan al-Ash'ariy.

 
(24)   Ash-Shariy’ah (ukurasa 358-364) cha al-Aajurriy.

 
(25)   Ahlus-Sunnah wal I'tiqaadud- Diyn (namba 14).

 
(26)   Sharhus-Sunnah (namba 18).

 
(27)   I'tiqaad A'immatul-Hadiyth (namba 22).

(28)   Imepokewa na Ibn al Qayyim katika Ijtimaa 'ul-Juyuushil-Islaamiyyah (ukurasa 152)

(29)   Usuulus-Sunnah (Q.7)

(30)    Sharh usuul I'tiqaad Ahlus-Sunnah wal-Jamaah (6/1127) cha al-Laalikaaiy.

(31)    Al-I'tiqaad (ukurasa 107) cha al-Bayhaqiy.

 

 

Share