03-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Akiomba Du’aa Ya Kujaaliwa Rizqi Ya Kumtosheleza Tu

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

03-Zuhd Yake:

Akiomba Du’aa Ya Kujaaliwa Rizqi Ya Kumtosheleza Tu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akimuomba Allaah (سبحانه وتعالى) rizki ya kumtosheleza tu basi akiomba du’aa:

 

 اللَّهُمَّ اجْعَلْ رِزْقَ آلِ مُحَمَّدٍ قُوتًا  

Ee Allaah ijaalie rizki ya Ahl wa Muhammad iwe ya kutosheleza tu.” [Muslim]

 

Na akataja katika Hadiyth yanayompasa bin Aadam kutosheka nayo:

 

عن أَبي عمرو ، ويقالُ : أَبو عبدِ الله ، ويقالُ : أَبو ليلى عثمان بن عفان رضي الله عنه  : أنَّ النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَيْسَ لاِبْنِ آدَمَ حَقٌّ في سِوَى هذِهِ الخِصَالِ : بَيْتٌ يَسْكُنُهُ ، وَثَوْبٌ يُوارِي عَوْرَتَهُ ، وَجِلْفُ الخُبز وَالماء )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu 'Amru (رضي الله عنه)  Inasemwa ni Abu 'Abdillaah, na inasemwa Abu Laylaa 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه) kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)    amesema: "Bin Aadam hana haki ya kuwa na zaidi ya vitu aina tatu: nyumba atakayoishi, na mavazi ya kusitiri uchi wake na kipande cha mkate na maji." [At-Tirmidhy, na akasema ni Hadiyth Swahiyh]

 

 

Share