060-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukarimu na Kutoa Katika Njia za Kheri na Kuwa na Imani Kwa Allaah Ta'aalaa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب الكرم والجود والإنفاق في وجوه الخير ثقةً بالله تعالى

060-Mlango Wa Ukarimu na Kutoa Katika Njia za Kheri na Kuwa na Imani Kwa Allaah Ta'aalaa

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ ۖ  ﴿٣٩﴾

Na kitu chochote mtoacho, basi Yeye Atakilipa,. [Sabaa: 39]

 

 

وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾

Na chochote cha khayr mtoacho basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika khayr mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa.

 

 لِلْفُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢٧٣﴾

Na chochote mtoacho katika khayr basi Allaah kwacho ni Mjuzi. [Al-Baqarah: 272-273]

 

 

 

 

Hadiyth – 1

وعن ابن مسعود رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  لا حَسَدَ إِلاَّ في اثْنَتَيْنِ : رَجُلٌ آتَاهُ اللهُ مَالاً ، فَسَلَّطَهُ عَلَى هَلَكَتِهِ في الحَقّ ، وَرَجُلٌ آتَاهُ اللهُ   حِكْمَةً ، فَهُوَ يَقْضِي بِهَا ويُعَلِّمُهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uuwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa; Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hapana husuda ila katika mawili: Mtu Allaah amempa mali, akamsalitisha katika kuimaliza katika haki. Na Allaah amempa mtu hekima, anahukumu nayo na anawaelimisha wengine." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  أيُّكُم مَالُ وَارِثِهِ أحبُّ إِلَيْهِ مِنْ    مَالِهِ ؟ )) قالوا : يَا رسول اللهِ ، مَا مِنَّا أحَدٌ إِلاَّ مَالُهُ أحَبُّ إِلَيْهِ . قَالَ : ((  فإنَّ مَالَهُ مَا قَدَّمَ وَمَالَ وَارِثِهِ مَا أخَّرَ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uuwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ni mtu gani miongoni mwenu ambaye anaipenda zaidi mali ya warithi wake kuliko mali yake mwenyewe?" Tukasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakuna miongoni mwetu isipokuwa anaipenda mali yake zaidi." Akasema: "Hakika mali yake ni ile aliyoitanguliza na mali aliyoibakisha ni ya warithi wake." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 3

وعن عَدِيِّ بن حَاتِمٍ رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  اتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Adiyy bin Haatim (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: "Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ""Ogopeni Moto ijapo kwa kipande cha tende moja." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن جابرٍ رضي الله عنه ، قَالَ : مَا سُئِلَ رسول الله صلى الله عليه وسلم  شَيْئاً قَطُّ ، فقالَ : لاَ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwahi kuombwa kitu chochote mara zote, akasema: hapana." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  مَا مِنْ يَوْمٍ يُصبحُ العِبَادُ فِيهِ إِلاَّ مَلَكَانِ يَنْزلانِ ، فَيَقُولُ أحَدُهُمَا : اللَّهُمَّ أعْطِ مُنْفِقاً خَلَفاً ، وَيَقُولُ الآخَرُ : اللَّهُمَّ أعْطِ مُمْسِكاً تَلَفاً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna siku yoyote inayopambazuka kwa waja isipokuwa Malaika wawili huteremka, mmoja wao anasema: 'Ee Mola! Mrudishie mwenye kutoa (kila anachotoa kwa wingi)'. Na mwengine naye anasema: 'Ee Mola! Mharibie mwenye kuzuia (vitu vyake)'. [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  قَالَ الله تَعَالَى : أنفِق يَا ابْنَ آدَمَ يُنْفَقْ عَلَيْكَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa tena kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Amesema Allaah Ta'aalaa: "Ee mwanadamu toa (katika njia ya Allaah) na Allaah atakupatia." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 7

وعن عبد اللهِ بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ رَجُلاً سَألَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : أيُّ الإسلامِ خَيْرٌ ؟ قَالَ : ((  تُطْعِمُ الطَّعَامَ ، وَتَقْرَأُ السَّلاَمَ عَلَى مَنْ عَرَفْتَ وَمَنْ لَمْ تَعْرِفْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba kuna mtu mmoja aliyemuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni Uislamu gani ulio bora?" Akasema: "Kulisha watu chakula na kuwatolea salamu unaowajua na usiowajua." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 8

وعن عبد اللهِ بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  أرْبَعُونَ خَصْلَةً : أعْلاهَا مَنِيحةُ العَنْزِ ، مَا مِنْ عَامِلٍ يَعْمَلُ بخَصْلَةٍ مِنْهَا ؛ رَجَاءَ ثَوَابهَا وَتَصْدِيقَ مَوْعُودِهَا ، إِلاَّ أدْخَلَهُ الله تَعَالَى بِهَا الجَنَّةَ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruu bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Sampuli arobaini za wema, ya juu kabisa ni kumwazima mtu ngamia (jike) wa maziwa ili apate maziwa (kisha amrudishie mwenyewe). Hakuna mfanyaji ambaye atafanya amali yeyote katika hizi akitarajia thawabu zake na kuswadikisha ile ahadi (aliyoahidiwa) isipokuwa Allaah humuingiza kwayo Peponi." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي أُمَامَة صُدّيِّ بن عَجْلانَ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم :  ((  يَا ابْنَ آدَمَ ، إنَّكَ أن تَبْذُلَ الفَضلَ خَيْرٌ لَكَ ، وَأن تُمْسِكَه شَرٌّ لَكَ ، وَلاَ تُلاَمُ عَلَى كَفَافٍ ، وَابْدَأْ بِمَنْ تَعُولُ ، وَاليَدُ الْعُلْيَا خَيْرٌ مِنَ الْيَدِ السُّفْلَى )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Umamah Sudayyi bin 'Ajlaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee mwanadamu! Hakika lau utatafutia fadhila (hela) za zaidi itakuwa bora kwako, na kuzuilia (kutotumia) ni shari kwako. Hutalaumiwa kuwa na hela kwa kadiri ya mahitaji yako. Na anza kuitumia kwa wale wenye haki kwako." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 10

وعن أنسٍ رضي الله عنه  ، قَالَ : مَا سُئِلَ رسول الله صلى الله عليه وسلم عَلَى الإسْلاَمِ شَيْئاً إِلاَّ أعْطَاهُ ، وَلَقَدْ جَاءهُ رَجُلٌ ، فَأعْطَاهُ غَنَماً بَيْنَ جَبَلَيْنِ ، فَرجَعَ إِلَى قَوْمِهِ ، فَقَالَ : يَا قَوْمِ ، أسْلِمُوا فإِنَّ مُحَمَّداً يُعطِي عَطَاءَ مَن لا يَخْشَى الفَقْر ، وَإنْ كَانَ الرَّجُلُ لَيُسْلِمُ مَا يُريدُ إِلاَّ الدُّنْيَا ، فَمَا يَلْبَثُ إِلاَّ يَسِيراً حَتَّى يَكُونَ الإسْلاَمُ أحَبَّ إِلَيْهِ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alikuwa katika Uislamu hakuombwa chochote Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa alimpatia. Na hakika alikuja mtu, naye akampatia mbuzi wengi sana waliojaa baina ya majabali mawili. Huyu mtu aliporudi kwa watu wake aliwaambia: "Enyi watu wangu kuweni Waislamu kwani Muhammad hutoa aina ya utoaji ambao haogopi ufakiri." Japokuwa mtu alikuwa akisilimu kwa sababu ya pato la kidunia, lakini baada ya muda mchache, Uislamu unakuwa ni mwenye kupendwa zaidi na yeye kuliko dunia na vilivyomo ndani yake." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 11

وعن عمر رضي الله عنه ، قَالَ : قسم رسول الله صلى الله عليه وسلم قَسْماً ، فَقُلْتُ :يَا رسولَ الله ، لَغَيْرُ هؤلاَءِ كَانُوا أحَقَّ بِهِ مِنْهُمْ ؟ فَقَالَ : ((  إنَّهُمْ خَيرُونِي أنْ يَسألُوني بالفُحْشِ ، أَوْ يُبَخِّلُونِي ، وَلَسْتُ بِبَاخِلٍ )) رواه مسلم

Imepokewa kutoka kwa 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aligawanya mali nami nikamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Mbali na hawa kuna watu wenye haki zaidi ya kupatiwa kuliko hawa." Akasema: "Hakika wao wamenipatia uchaguzi (kutumia uamuzi wangu). Hivyo, wanatakiwa ima waniombe waziwazi, nami nitawapatia au waninasibishe na ubakhili, na mimi si bakhili." [Muslim] 

 

 

Hadiyth – 12

وعن جبير بن مطعم رضي الله عنه  ، قَالَ : بَيْنَمَا هُوَ يَسِيرُ مَعَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم مَقْفَلَهُ مِنْ حُنَيْن ، فَعَلِقَهُ الأعْرَابُ يَسْألُونَهُ ، حَتَّى اضْطَرُّوهُ إِلَى سَمُرَة ، فَخَطِفَت رِدَاءهُ ، فَوَقَفَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم ، فقال : ((  أعْطُوني رِدَائي ، فَلَوْ كَانَ لِي عَدَدُ هذِهِ العِضَاهِ نَعَماً ، لَقَسَمْتُهُ بَينَكُمْ ، ثُمَّ لا تَجِدُونِي بَخِيلاً وَلاَ كَذّاباً وَلاَ جَبَاناً )) رواه البخاري

Imepokewa kutoka kwa Jubaiyr bin Mutw'im (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Baada ya vita vya Hunaiyn tulikuwa tunarudi na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), baadhi ya Mabedui walimzunguka alipokuwa chini ya mti wakitaka kupatiwa fungu lao (katika ngawira) na mmoja wao akachukua shuka yake. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama akasema: "Nipatieni shuka yangu; lau ningekuwa na neema nyingi sawa na idadi ya majani katika huu mchongoma ningewagawia baina yenu na hamungeniona mimi kuwa bakhili wala muongo wala mwoga?" [Al-Bukhaariy] 

 

 

Hadiyth – 13

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَال ، وَمَا زَادَ اللهُ عَبْداً بِعَفْوٍ إِلاَّ عِزّاً ، وَمَا تَواضَعَ أحَدٌ لله إِلاَّ رَفَعَهُ اللهُ عزوجل )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swadaqah haipunguzi mali; na Allaah anamuongezea utukufu mwenye kusamehe. Na hakuna anayenyenyekea kwa ajili ya Allaah Ta'aalaa isipokuwa humnyanyua daraja yake." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 14

وعن أَبي كبشة عمرو بن سعد الأنماري رضي الله عنه: أنّه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : ((  ثَلاَثَةٌ أُقْسمُ عَلَيْهِنَّ ، وَأُحَدِّثُكُمْ حَدِيثاً فَاحْفَظُوهُ : مَا نَقَصَ مَالُ عَبْدٍ مِنْ صَدَقَةٍ ، وَلاَ ظُلِمَ عَبْدٌ مَظْلَمَةً صَبَرَ عَلَيْهَا إِلاَّ زَادَهُ اللهُ عِزّاً ، وَلاَ فَتَحَ عَبْدٌ بَابَ مَسألَةٍ إِلاَّ فَتَحَ اللهُ عَلَيْهِ بَابَ فَقرٍ - أَوْ كَلِمَةً نَحْوَهَا - وَأُحَدِّثُكُمْ حَديثاً فَاحْفَظُوهُ، قَالَ : ((  إنَّمَا الدُّنْيَا لأرْبَعَةِ نَفَرٍ : عَبْدٍ رَزَقَهُ اللهُ مَالاً وَعِلماً ، فَهُوَ يَتَّقِي فِيهِ رَبَّهُ ، وَيَصِلُ فِيهِ رَحِمَهُ، وَيَعْلَمُ للهِ فِيهِ حَقَّاً ، فَهذا بأفضَلِ المَنَازِلِ . وَعَبْدٍ رَزَقهُ اللهُ عِلْماً، وَلَمْ يَرْزُقْهُ مَالاً ، فَهُوَ صَادِقُ النِّيَّةِ ، يَقُولُ : لَوْ أنَّ لِي مَالاً لَعَمِلتُ بِعَمَلِ فُلانٍ ، فَهُوَ بنيَّتِهِ ، فأجْرُهُمَا سَوَاءٌ . وَعَبْدٍ رَزَقَهُ الله مَالاً ، وَلَمَ يَرْزُقْهُ عِلْماً ، فَهُوَ يَخبطُ في مَالِهِ بغَيرِ عِلْمٍ ، لاَ يَتَّقِي فِيهِ رَبَّهُ ، وَلاَ يَصِلُ فِيهِ رَحِمَهُ ، وَلاَ يَعْلَمُ للهِ فِيهِ حَقّاً ، فَهذَا بأَخْبَثِ المَنَازِلِ . وَعَبْدٍ لَمْ يَرْزُقْهُ اللهُ مَالاً وَلاَ عِلْماً ، فَهُوَ يَقُولُ : لَوْ أنَّ لِي مَالاً لَعَمِلْتُ فِيهِ بعَمَلِ فُلاَنٍ ، فَهُوَ بنِيَّتِهِ ، فَوِزْرُهُمَا سَوَاءٌ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Kutoka kwa Abuu Kabshah 'Amar bin Sa'd Al-Anmaariy amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Matatu naapa juu yake na nakuwahadithieni hadiyth ihifadhini: Mali ya mja haipapungui kwa swadaqah, wala mja hakudhulumiwa chochote akasubiri ila Allaah humzidisha utukufu, na hatafungua mja mlango wa kuomba isipokuwa  Allaah humfungulia mlango wa ufukara, au neno mfano wake." na ninakuhadithieni hadiyth ihifadhini, akasema: "Hakika dunia ni kwa watu wanne: Mja Allaah amempa mali na elimu naye akamcha Mola ndani yake, akaunganisha ndani yake kizazi, na akajua ndani yake haki ya Allaah, huyu ni daraja bora, na cheo bora; na mja aliyepatiwa na Allaah elimu bila kupewa mali, naye akawa na nia ya kweli, akasema: 'Lau kama ningekuwa na mali ningefanya amali ya fulani', yeye atakuwa katika hiyo nia yake na ujira wa wote wawili ni sawa; na mja aliyepewa na Allaah mali lakini hakuruzukiwa elimu, nae anaifuja mali yake pasi na elimu. Yeye hamchi Rabb wake kwayo na wala haungi kizazi na wala hajui haki za Allaah juu yake, huyu atakuwa katika daraja ya chini kabisa; na mja ambaye hakuruzukiwa na Allaah mali wala elimu, naye akawa anasema: 'Kwa hakika lau kama ningekuwa na mali ningefanya amali ya fulani (amali ya mtu wa tatu).' Hiyo ianpokuwa ndio nia yake, wote watakuwa na madhambi sawa." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh] 

 

 

Hadiyth – 15

وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّهُمْ ذَبَحُوا شَاةً ، فَقَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم  :  ((  مَا بَقِيَ مِنْهَا ؟ )) قالت : مَا بَقِيَ مِنْهَا إِلاَّ كَتِفُها . قَالَ : ((  بَقِيَ كُلُّهَا غَيْرُ   كَتِفِهَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa wao walichinja mbuzi, (wakaigawa) kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuuliza: "Imebaki nyama kiasi gani?" Alijibu: "Haikubaki isipokuwa mkono wake." Akasema: "Imebaki nyama yote ila mkono." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 16

وعن أسماء بنت أَبي بكرٍ الصديق رضي الله عنهما ، قالت : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  لاَ تُوكِي فَيُوكى عَلَيْكِ )) .

وفي رواية : ((  أنفقي أَوِ انْفَحِي ، أَوْ انْضَحِي ، وَلاَ تُحصي فَيُحْصِي اللهُ عَلَيْكِ ، وَلاَ تُوعي فَيُوعي اللهُ عَلَيْكِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Asmaa bint Abuu Bakr As-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) Amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Usikusanye Allaah akakukatia riziki." 

Na katika riwaayah nyingine: "Toa swadaqah kwa mali yako au anfahiy (toa) au andhahiy (kutoa) wala usizuie mali yako kwa kuhesabu (kwa kuhofia itapungua), Allaah asije akakunyima rehma zake na wala usiwanyime watu kwa ile fadhila uliyopatiwa na hivyo Allaah akakunyima." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 17

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يَقولُ : ((  مَثَل البَخيل وَالمُنْفِقِ ، كَمَثَلِ رَجُلَيْنِ عَلَيْهِمَا جُنَّتَانِ مِنْ حَديد مِنْ ثُدِيِّهِمَا إِلَى تَرَاقِيهِمَا ، فَأَمَّا المُنْفِقُ فَلاَ يُنْفِقُ إِلاَّ سَبَغَتْ - أَوْ وَفَرَتْ - عَلَى جِلْدِهِ حَتَّى تُخْفِيَ بَنَانَهُ ، وَتَعْفُو أثرَهُ ، وأمَّا البَخِيلُ ، فَلاَ يُريدُ أنْ يُنْفِقَ شَيْئاً إِلاَّ لَزِقَتْ كُلُّ حَلْقَةٍ مَكَانَهَا ، فَهُوَ يُوسِّعُهَا فَلاَ تَتَّسِعُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amamsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mfano wa bakhili na yule anayetoa, ni kama mfano wa watu wawili waliovaa juba za chuma, mikono yao imelazimika kwenda kwenye maziwa na mitulinga yao. Ama yule mkarimu (mwenye kutoa swadaqah) akawa kila anapotoa swadaqah linatanuka mpaka linafunika vidole nyake, na linafunika alama zake zote. Na ama yule bakhili hataki kutoa kitu chochote ila zile kona hushikilia mahali pake na kuzidi kumbana, naye atakuwa anaitanua na wala haitanuki." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 18

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((  مَنْ تَصَدَّقَ بعَدلِ تَمْرَةٍ مِنْ كَسْبٍ طَيِّبٍ ، وَلاَ يَقْبَلُ اللهُ إِلاَّ الطَّيبَ ، فَإنَّ اللهَ يَقْبَلُهَا بِيَمِينِهِ ، ثُمَّ يُرَبِّيهَا لِصَاحِبِهَا كَمَا يُرَبِّي أحَدُكُمْ فَلُوَّهُ حَتَّى تَكُونَ مِثْلَ الجَبَلِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kutoa swadaqah kama tende moja, kwenye chumo zuri, Allaah hakubali isipokuwa kizuri, hakika Allaah Ataipokea kwa Mkono Wake wa kuume, kisha Atamletea (swadaqah hiyo), kama mmoja wenu anavyolea mtoto wa farasi wake, mpaka iwe kama mlima." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 19

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي بِفَلاَةٍ مِنَ الأَرْضِ ، فَسَمِعَ صَوْتاً في سَحَابَةٍ ، اسقِ حَدِيقَةَ فُلانٍ ، فَتَنَحَّى ذَلِكَ السَّحَابُ فَأفْرَغَ مَاءهُ في حَرَّةٍ ، فإِذَا شَرْجَةٌ مِنْ تِلْكَ الشِّرَاجِ قَدِ اسْتَوْعَبَت ذَلِكَ الماءَ كُلَّهُ ، فَتَتَبَّعَ المَاءَ ، فإذَا رَجُلٌ قَائمٌ في حَدِيقَتِهِ يُحَوِّلُ الماءَ بِمسحَاتِهِ، فَقَالَ لَهُ : يَا عَبْدَ اللهِ، ما اسمُكَ ؟ قال : فُلانٌ للاسم الذي سَمِعَ في السَّحابةِ ، فقال له : يا عبدَ الله ، لِمَ تَسْألُنِي عَنِ اسْمِي ؟ فَقَالَ : إنِّي سَمِعْتُ صَوتْاً في السَّحابِ الَّذِي هَذَا مَاؤُهُ ، يقولُ : اسْقِ حَدِيقَةَ فُلاَنٍ لاسمِكَ ، فَمَا تَصْنَعُ فِيهَا ، فَقَالَ : أمَا إذ قلتَ هَذَا ، فَإنِّي أنْظُرُ إِلَى مَا يَخْرُجُ مِنْهَا ، فَأتَصَدَّقُ بِثُلُثِهِ ، وَآكُلُ أنَا وَعِيَالِي ثُلُثاً ، وَأردُّ فِيهَا ثُلُثَهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu alipokuwa anatembea jangwani, alisikia sauti katika wingu: 'Nyweshea bustani la fulani.' Wingu hilo likakaribia na kumimina maji yake kwenye ardhi mawe. Maji hayo yakaenea katika kijito na kumiminika katika behewa kubwa. Akafuata maji akamuona mtu amesimama ndani ya bustanilake anagawa maji kwa jembe lake. Akaniambia: 'Ee mja wa Allaah, jina lako nani?' Akasema: 'fulani.' Akataja jina ambalo amelisikia katika wingu. Akamwambia: 'Ee mja wa Allaah! kwa nini unaniuliza jina langu?' Akasema: 'Nilisikia sauti katika wingu ambalo haya ndio maji yake ikisema: Nyweshea bustani la fulani kwa jina lako. Unafanya nini katika hili?' Akasema: 'Kwa sababu umeniuliza hili, Mimi naagalia kinachotoka humo, na kutoa swadaqah thuluthi, na narudisha humo (shambani) thuluthi yake." [Muslim]

 

 

 

 

Share