B-Misamiati Yenye Asili Ya Lugha Ya Kiarabu

 

Misamiati Yenye Asili Ya Lugha Ya Kiarabu

Alhidaaya.com

 

 B

Neno

Maana

Kiarabu

baathi

kufufuliwa viumbe Siku ya Qiyaamah

بعث

 badhiri

kuzidisha kufanya israfu khasa kwa ajili ya kujionyesha au kujifakharisha.

بذر/ تبذير

 baghala

nyumbu

بغل

 bahaimu

mnyama mwenye miguu minne

بهيمة

 bahasa

bei ndogo, rahisi

بخس

 bai

chagua mtu na kumpa uongozi, unga mkono mtu kwa kitendo anachotaka kukifanya, kuahidi kumfuata kiongozi katika kuongoza kwake.

بيعة

baidika

kuweko mbali

بعد/بعيد

bairi

aina ya ngamia

بعير

baiti

nyumba

بيت

bakari

ng’ombe

بقرة

balagha

 

baleghe

1-kubalighisha jambo, kufikisha khabari, ujumbe.

2-kubaleghe, mvulana na msichanga kufikia umri wa upevu.

بلغ  - بلاغ

banati

wasichana

بنات

barasi

aina ya ugonjwa wa ngozi.

برص

barasi

ukoma

برص

barazahi

maisha ya baada ya kufariki; kaburini hadi Siku ya kufufuliwa Siku ya Qiyaamah.

برزخ

batili

kubatilisha, kulifanya jambo lisiwe lenye hukmu, kuliharibu jambo, kubatilisha ‘amali au ‘ibaadah.

باطل

bayana

waziwazi, kubainisha au kudhihirisha jambo.

بينات

biladi/baladi

nchi, mji.

بلد/بلاد

bishara

kutoa khabari, kubashiria khabari njema au mbaya.

بشير

burhani

Burhani: Muujiza, Ushahidi, Ishara, Dalili, Hoja za waziwazi kabisa zenye kuthibitisha kwa yakini na bila ya shaka na bila ya kupingika. 

برهان

buruji

mnara

بروج

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share