063-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kushindana Katika Mambo Yanayohusu Aakhera na Kutaka Vitu vya Baraka

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب التنافس في أمور الآخرة والاستكثار مما يتبرك بِهِ

063-Mlango Wa Kushindana Katika Mambo Yanayohusu Aakhera na Kutaka Vitu vya Baraka

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ ﴿٢٦﴾

Mwisho wake ni miski. Na katika hayo basi washindane wenye kushindana …[Al-Mutwaffifiyn: 26]

 

 

 

 

Hadiyth – 1

وعن سَهْلِ بن سَعدٍ رضي الله عنه  : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أُتِيَ بِشَرابٍ ، فَشَرِبَ مِنْهُ وَعَنْ يَمِينِهِ غُلاَمٌ ، وَعَنْ يَسَارِهِ الأشْيَاخُ ، فَقَالَ لِلغُلاَمِ : ((  أتَأذَنُ لِي أنْ أُعْطِيَ هؤُلاء ؟ )) فَقَالَ الغُلامُ : لاَ وَاللهِ يَا رسولَ الله ، لا أُوْثِرُ بِنَصِيبـي مِنْكَ أحَداً . فَتَلَّهُ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم في يَدِهِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kutoka kwa Sahl bin Sa'd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa kinywaji, naye akanywa kidogo. Kulikuwa na kijana upande wake wa kulia na wazee upande wake wa kushoto.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia yule kijana: "Je, utanipatia idhini niwapatie hawa (yaani wazee)?' Akasema yule kijana: "Ee Rasuli wa Allaah! Naapa kwa Allaah kuwa simpatii nafasi hiyo yeyeote baada yako." Hivyo, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimpatia kinywaji kilichobaki." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  بَيْنَا أيُّوبُ عَلَيْهِ السَّلام يَغْتَسِلُ عُرْيَاناً ، فَخَرَّ عَلَيْهِ جَرَادٌ مِنْ ذَهَبٍ ، فَجَعَلَ أيُّوبُ يَحْثِي في ثَوْبِهِ ، فَنَادَاهُ رَبُّهُ عز وجل : يَا أيُّوبُ ، ألَمْ أكُنْ أغْنَيتكَ عَمَّا تَرَى ؟! قَالَ : بَلَى وَعِزَّتِكَ وَلَكِنْ لاَ غِنى بي عن بَرَكَتِكَ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wakati Nabiy Ayyub ('Alayhis Salaam) alikuwa akioga uchi, mara nzige wa dhahabu akadondoka juu yake. Alijaribu kumshika kwa nguo yake, Allaah ('Azza wa Jalla) akamwita: 'Ee Ayyuwb!, Je sikuwa mwenye kukutosha wewe kama uonavyo?' Akasema: Ndio! lakini mimi sitosheki na baraka zako." [Al-Bukhaariy]  

 

 

 

 

Share