05-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Swiyaam: Kati Ya Fadhila Za Ramadhwaan Na Kufanya ‘Ibaadah Ndani Yake

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

Mlango Wa Swiyaam

 

05-Kati Ya Fadhila Za Ramadhwaan Na Kufanya ‘Ibaadah Ndani Yake

 

Alhidaaya.com

 

 

 

1- Toka kwa Abiy Bakrah (Radhwiya Allaahu Anhu) toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:

((شهران لا ينقصان، شهرا عيد: رمضان وذو الحجة))

((Miezi miwili haipungui, miezi miwili ya ‘Iyd: Ramadhwaan na Dhul Hijjah)). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1912) na Muslim (1089)]

 

Hadiyth hii inafidisha kuwa Ramadhwaan na Dhul Hijjah iko sawa katika fadhwiylah, na kwamba yote yaliyogusiwa kuhusu fadhwaail za miezi hii miwili, malipo yake na thawabu zake, yanapatikana kwa ukamilifu wake hata kama mwezi ni siku 29. [Fat-hul Baariy (4/150), Al-Majmuw’u (6/253) na Swahiyh Ibn Hibaan (8/218)]

 

2- Toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:

((إذا دخل شهر رمضان فتحت أبواب السماء، وغلقت أبواب جهنم، وسلسلت الشياطين))

((Unapoingia Mwezi wa Ramadhwaan milango ya mbingu hufunguliwa ikawa wazi, milango ya Jahannamu hufungwa ikakomewa, na Mashaytwaan hufungwa minyororo)). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1899) na Muslim (1079)]

 

3- Na toka tena kwa Abu Hurayrah kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:

((من صام رمضان إيمانا واحتسابا، غقر له ما تقدم من ذنبه))

((Atakayefunga Ramadhwaan kwa iymaan na kutarajia malipo [toka kwa Allaah], hughufiriwa dhambi zake zilizotangulia)). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (38), na (4/157) na Ibn Maajah (1641)]

 

Abu Haatim bin Hibaan amesema: "إيمانا" kwa kuamini ufaradhi wake, na "احتسابا" kwa kutakasia niya.

 

4- Na toka kwa huyo huyo Abu Hurayrah kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:

((الصلوات الخمس، والجمعة إلى الجمعة، ورمضان إلى رمضان، مكفرات لما بينهن إذا اجتنبت الكبائر))

((Swalaah Tano, na Ijumaa hadi Ijumaa, na Ramadhwaan hadi Ramadhwaan, ni zenye kufuta yaliyo baina yao ikiwa madhambi makubwa yataepukwa)). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (233)]

 

 

5- Ndani yake yapo Masiku Kumi ya Mwisho na Laylatul Qadr. Tutazielezea fadhiylah zake na kufanya ‘ibaadah ndani yake.

 

Share