08-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْمَلِكُ - الْمَالِكُ - الَّذِي لَهُ الْمُلْكُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْمَلِكُ  - الْمَالِكُ  -  الَّذِي لَهُ الْمُلْكُ

 

 

الْمَلِكُ

Al-Malik

Mfalme

 

 

 

الْمَالِكُ

Al-Maalik

Mwenye Kumiliki

 

 

 

الَّذِي لَهُ الْمُلْكُ

Alladhi Lahul-Mulk

Ambaye Ufalme Ni Wake

 

 

 

Allaah (عز وجل) Amesifika Sifa ya kuwa ni Mfalme, Mmiliki. Hizi ni Sifa zinazoeleza Utukufu, ‘Uluwa Zake na Usimamizi Wake na utaratibu wa mambo. Allaah (سبحانه وتعالى) Yeye Ndiye Pekee Anayeelekeza mambo yote ya uumbaji, amri na jaza. Ni Wake Yeye uumbaji wote, viumbe wote ni watiifu Kwake. Anaumiliki uumbaji nao unaendelea na utaendelea kuwa na haja Kwake.

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۗ وَلَا تَعْجَلْ بِالْقُرْآنِ مِن قَبْلِ أَن يُقْضَىٰ إِلَيْكَ وَحْيُهُ ۖ وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا ﴿١١٤﴾

Basi Ametukuka Allaah kwa ‘Uluwa, Mfalme wa haki. Na wala usiiharakize Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kabla haikumalizwa kufunuliwa Wahy kwako. Na sema: Rabb wangu! Nizidishie elimu. [Twahaa (20):114)]

 

 

Na Anasema pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٦﴾

Sema: Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, khayr imo Mkononi Mwako.  Hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۖ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ ۖ وَتَرْزُقُ مَن تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢٧﴾

Unauingiza usiku katika mchana na Unauingiza mchana katika usiku; na Unatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu na Unatoa kilicho mfu kutokana na kilicho hai na Unamruzuku Umtakaye bila ya hesabu. [Aal-‘Imraan  (3): 26, 27]

 

Na Anasema pia (سبحانه وتعالى):

 

الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٩﴾

Ambaye Pekee Ana ufalme wa mbingu na ardhi; na Allaah juu ya kila kitu ni Shahidi. [Al-Buruwj (85): 9]

 

 

 

Share