12-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْحَكِيمُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْحَكِيمُ

 

 

الْحَكِيمُ

Al-Hakiym

Mwenye Hikma Wa Yote Daima

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى), Yeye Ndiye Mwenye Hikma ya juu kabisa kuliko wote, Ambaye Ndiye Mwenye Hikma yote katika uumbaji Wake na kuamuru Kwake, Ambaye Alikifanya vyema kila Alichokiumba.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿٥٠﴾

Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini. [Al-Maa-idah (5): 50]

 

Kwa hivyo, Allaah (سبحانه وتعالى) Hakuumba kitu chochote kwa upuuzi tu na Hakutunga Shariy’ah yoyote bure tu au isiyokuwa ya maana na manufaa kwa viumbe Wake na uumbaji Wake.

 

  

Allaah (سبحانه وتعالى), Yeye Ndiye Pekee Mwenye kuhukumu mwanzoni na mwishoni. Ana sehemu tatu za kutawala ambazo hakuna kingine chochote chenye fungu humo. Anawatawala waja Wake kwa Shariy’ah Yake, Qadar Yake na jazaa Yake.

 

 

Maana ya hikma ni kukiweka kitu mahali pake.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ مَثَلُ السَّوْءِ ۖ وَلِلَّـهِ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٦٠﴾

Kwa wale wasioamini Aakhirah wana mfano mbaya (ya upungufu); na Allaah Ana Sifa kamilifu tukufu kabisa. Naye ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [An-Nahl (16): 60]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ﴿٨٤﴾

Na Yeye Ndiye Muabudiwa wa haki mbinguni na ardhini pia (Ndiye Huyo Huyo) Ilaah. Naye Ndiye Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote. [Az-Zukhruf [(43):84]

 

 

 

Share